_id
stringlengths
15
22
url
stringlengths
31
150
title
stringlengths
1
86
text
stringlengths
100
23.8k
20231101.sw_174621_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/Fortunato%20wa%20Fano
Fortunato wa Fano
Alijitahidi kukomboa watumwa hata kwa kuingia madeni ambayo Papa Gregori I alimruhusu kuyalipa hata kwa kuuza vyombo vya ibada.
20231101.sw_174624_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ukristo%20wa%20Kisiria
Ukristo wa Kisiria
Ukristo wa Kisiria (kwa Kiingereza Syriac Christianity; kwa Kisyria ܡܫܝܚܝܘܬܐ ܣܘܪܝܝܬܐ / Mšiḥoyuṯo Suryoyto au Mšiḥāyūṯā Suryāytā) ni aina ya Ukristo wa Mashariki ambayo imestawi kwanza katika lugha ya Kiaramu na matawi yake mbalimbali.
20231101.sw_174624_1
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ukristo%20wa%20Kisiria
Ukristo wa Kisiria
Lugha hiyo, pamoja na Kigiriki na Kilatini, ni lugha muhimu zaidi ya Ukristo wa karne za kwanza, ikiheshimika pia kwa sababu ndiyo lugha mama ya Yesu na ya mitume wake wengi, kama si wote. Lugha hiyo ilienea na kutawala mawasiliano kutoka Antiokia upande wa magharibi hadi Seleucia-Ctesiphon, mji mkuu wa Milki ya Wasasani upande wa mashariki. Eneo hilo, lililojumlisha Syria, Lebanoni, Israeli/Palestina, Iraq na sehemu za Uturuki na Iran za leo, lilikuwa linagombaniwa kwa muda mrefu na Dola la Roma Mashariki na hiyo milki ya Wasasani.
20231101.sw_174624_2
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ukristo%20wa%20Kisiria
Ukristo wa Kisiria
Maandishi muhimu zaidi ya mababu wa Kanisa kwa lugha hiyo yanapatikana katika mkusanyo Patrologia Orientalis.
20231101.sw_174624_3
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ukristo%20wa%20Kisiria
Ukristo wa Kisiria
Tangu wakati wa Mitume Ukristo ulienezwa kwa lugha ya Kiaramu na jamii yake kutoka Yerusalemu hadi sehemu nyingi zilizoitumia, ingawa ushahidi wa hakika ni mdogo hadi karne ya 3. Katika mtaguso wa kwanza wa Nisea (325) walishiriki maaskofu 20 kutoka Syria na 1 kutoka Uajemi, nje ya Dola la Roma.
20231101.sw_174624_4
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ukristo%20wa%20Kisiria
Ukristo wa Kisiria
Katika karne ya 5 Ukristo wa Kisiria ulijitenga na umoja wa Kanisa. Hawakuwa tena waamini binafsi walioshika msimamo tofauti na ule rasmi, bali Wakristo karibu wote wa nchi fulani chini ya maaskofu wao ndio waliojitenga.
20231101.sw_174624_5
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ukristo%20wa%20Kisiria
Ukristo wa Kisiria
1. Kufuatana na mtaguso wa Efeso (431), Wakristo wa nje ya Dola la Roma upande wa mashariki (Mesopotamia, Uajemi n.k.) walijitenga na kuendeleza maisha ya Kikristo chini ya dhuluma za Dola la Uajemi, huku wakieneza habari njema mbali zaidi na zaidi, hadi China na Indonesia.
20231101.sw_174624_6
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ukristo%20wa%20Kisiria
Ukristo wa Kisiria
Hadi leo, warithi wa Ukristo huo wanafuata liturujia ya Mesopotamia. Ni kama milioni 5, wengi wakiwa Kerala (India Kusini).
20231101.sw_174624_7
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ukristo%20wa%20Kisiria
Ukristo wa Kisiria
2. Kwa sababu ya matatizo ya ndani ya dola la Roma la Mashariki mafarakano yalitokea hata katika nchi ya Siria na nyinginezo zilizokuwa chini ya Kaisari wa Bizanti. Katika nchi hizo, baada ya mtaguso wa Kalsedonia (451), sehemu kubwa ya Wakristo walijitenga na kuendelea kama Kanisa la kitaifa.
20231101.sw_174624_8
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ukristo%20wa%20Kisiria
Ukristo wa Kisiria
Katika hali hiyo ya mafarakano, mbali ya dhuluma kutoka kwa Dola la Uajemi, ilitokea kwamba Muhammad aliunganisha makabila yote ya Waarabu kwa jina la Mungu mmoja, (kwa Kiarabu: Allah). Alipofariki mwaka 632 Waarabu walishambulia maeneo jirani ya Waroma wa Bizanti na ya Waajemi. Miaka mia moja baada ya kifo cha Muhamad sehemu kubwa ya dunia kati ya Moroko na Bonde la Indus (leo Pakistan) ilikuwa chini ya Uislamu.
20231101.sw_174624_9
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ukristo%20wa%20Kisiria
Ukristo wa Kisiria
Uislamu ulienea haraka sana kwa nguvu ya kijeshi katika nchi hizo, ambazo baadhi, kama Syria, zilikuwa na Wakristo wengi. Mwanzoni walikuja Waarabu kadhaa tu: walichukua madaraka ya serikali kuu na kujenga makambi ya kijeshi katika kila nchi. Vijana wa Kiarabu walifuata baba zao wakiitikia wito wa dini uliokuja pamoja na nafasi ya kupata maisha nafuu. Mbali ya nguzo tano za Uislamu, walifundishwa kwamba ikiwa watakufa katika vita vitakatifu watapokewa na Mungu kama mashahidi wa imani na kuingia Paradiso moja kwa moja. Lakini wasipokufa vitani watakuwa matajiri wakitawala nchi mpya na kupokea kodi za wenyeji wasio Waislamu. Imani ya aina hii iliwapa nguvu kweli na iliendelea kuvuta Waarabu wengi kutoka kwao kuhamia hadi Asia ya Kati.
20231101.sw_174624_10
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ukristo%20wa%20Kisiria
Ukristo wa Kisiria
Kwa kawaida Wakristo hawakulazimishwa kuacha imani yao. Viongozi wa Waarabu washindi walifanya mikataba na maaskofu wa Kikristo katika maeneo waliyoyateka. Wakristo waliahidiwa ulinzi wa makanisa yao wakiambiwa wanaweza kuendelea na mila na desturi walivyozoea. Lakini hawakuwa na haki zote za uraia. Wasio Waislamu walijiona wanabaguliwa mbele ya Waislamu. Walitozwa kodi kubwa ya pekee. Mahakamani hawakuweza kushuhudia dhidi ya Mwislamu, walilazimishwa kuvaa nguo za pekee tofauti na Waislamu, walikataliwa kupanda farasi, kujenga makanisa mapya, au kutumia kengele makanisani. Waislamu walipata kipaumbele katika mambo yote. Hivyo polepole wenyeji walianza kutumia lugha ya Kiarabu pamoja na kujiunga na Uislamu. Aliyejiunga na Uislamu na kujifunza Kiarabu alikubaliwa lakini Wakristo wenyeji waliotunza urithi wao walibaguliwa. Bila shaka wazazi wengine walitumaini kuwasaidia watoto wao wapate maendeleo maishani wakifuata dini ya watawala.
20231101.sw_174624_11
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ukristo%20wa%20Kisiria
Ukristo wa Kisiria
Masharti ya kujiunga na Uislamu ni rahisi. Hakuna mafundisho magumu, mwanzoni inatosha kutamka "shahada" ya Kiislamu ambayo ni fupi sana: As-haddu inna la ilaha ila allah, wa Muhamad rasul ullah. (Nakiri ya kwamba Mungu ndiye mmoja tu, na Mohamad ni mtume wa Mungu). Lakini baadaye haiwezekani kurudi katika Ukristo maana sheria ya Kiislamu inaruhusu Mkristo kugeuka Mwislamu lakini inakataza kwa adhabu ya kifo Mwislamu asitoke katika imani hiyo na kufuata dini nyingine.
20231101.sw_174624_12
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ukristo%20wa%20Kisiria
Ukristo wa Kisiria
Mara kwa mara upande wa watawala na wakubwa yalijitokeza matendo mabaya, kama makanisa kubomolewa au kugeuzwa misikiti, n.k. Kwa mfano msikiti mkuu wa Dameski (Siria) ulikuwa zamani Kanisa la Mt. Yohane Mbatizaji. Mwanzoni Waarabu waliahidi kuliheshimu, lakini mtawala aliyefuata alitaka jengo kubwa lililopatikana mjini kwa ajili ya ibada yake.
20231101.sw_174624_13
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ukristo%20wa%20Kisiria
Ukristo wa Kisiria
Vipindi vya kulazimisha vilitokea tena na tena, hasa baada ya mataifa mapya kuwa Waislamu. Waarabu wenyewe walionyesha ustahimilivu zaidi kwa wenye imani nyingine (Wakristo, Wayahudi n.k.). Lakini Waturuki, Waajemi na Wamongolia baada ya kuwa Waislamu walikuwa wakali. Hasa vipindi vya vita vya msalaba kati ya Wakristo kutoka Ulaya na Waturuki viliongeza uchungu kwa Wakristo waliokuwa chini ya utawala wa Kiarabu. Katika vipindi hivyo Wakristo chini ya Waislamu waliweza kuangaliwa kama wasaliti na kuteswa, makanisa yao kubomolewa n.k. Majaribio yote ya kupigania uhuru yaligandamizwa vikali.
20231101.sw_174624_14
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ukristo%20wa%20Kisiria
Ukristo wa Kisiria
Pamoja na Wakristo wengi kugeuka Waislamu, umisionari kwa mataifa mengine ya Asia ulizuiwa na dola la Kiislamu lililozunguka karibu pande zote nchi za Kikristo. Hata hivyo wamisionari wa Kanisa la Mesopotamia na Uajemi walikuwa wameshahubiri kote Asia ya Kati hadi China na Indonesia.
20231101.sw_174624_15
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ukristo%20wa%20Kisiria
Ukristo wa Kisiria
Lakini huko Asia makabila na mataifa mapya walipokea Uislamu, mara nyingi kwa njia ya vita. Makabila hayo ya Waturuki na Wamongolia yalifuata imani ya Kiislamu kwa ukali kuliko Waarabu wenyewe. Walilazimisha wote waliokuwa na imani tofauti (Wakristo, Wabuddha au wafuasi wa dini za jadi) wawe Waislamu. Mtawala Mwislamu wa Wamongolia, Timur, aliua Wakristo lukuki na kubomoa makanisa elfu kadhaa alipofanya vita vyake Asia ya Kati. Katika vita hivyo Ukristo wa Asia ya Kati uliharibika kabisa. Maeneo makubwa yalichomwa moto, watu walilazimishwa kwa upanga kuwa Waislamu au kuuawa. Mnamo mwaka 1400 Ukristo wa Asia ulibaki katika Mashariki ya Kati tu (Asia ya Magharibi) pamoja na India Kusini (jimbo la Kerala).
20231101.sw_174624_16
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ukristo%20wa%20Kisiria
Ukristo wa Kisiria
Qambel Maran- Syriac chants from South India- a review and liturgical music tradition of Syriac Christians revisited
20231101.sw_174628_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/Funguvisiwa%20la%20Bismarck
Funguvisiwa la Bismarck
Funguvisiwa la Bismarck (kwa Kiingereza: Bismarck Archipelago) ni funguvisiwa la kaskazini mwa Papua Guinea Mpya. Vingi vina asili ya volikano.
20231101.sw_174628_1
https://sw.wikipedia.org/wiki/Funguvisiwa%20la%20Bismarck
Funguvisiwa la Bismarck
Firth, Stewart (1983). New Guinea Under the Germans. Carlton, Australia: Melbourne University Press. .
20231101.sw_174628_2
https://sw.wikipedia.org/wiki/Funguvisiwa%20la%20Bismarck
Funguvisiwa la Bismarck
Howe, K. R., Robert C. Kiste, Brij V. Lal, eds. (1994). Tides of History: The Pacific Islands in the Twentieth Century. Honolulu: University of Hawaii Press. .
20231101.sw_174628_3
https://sw.wikipedia.org/wiki/Funguvisiwa%20la%20Bismarck
Funguvisiwa la Bismarck
King, David et al. (1982). Papua New Guinea Atlas: A Nation in Transition. Bathurst, Australia: R. Brown and the University of Papua New Guinea. .
20231101.sw_174628_4
https://sw.wikipedia.org/wiki/Funguvisiwa%20la%20Bismarck
Funguvisiwa la Bismarck
Moore, Clive (2003). New Guinea: Crossing Boundaries and History. Honolulu: University of Hawaii Press. .
20231101.sw_174628_5
https://sw.wikipedia.org/wiki/Funguvisiwa%20la%20Bismarck
Funguvisiwa la Bismarck
Ryan, Peter, ed. (1972). Encyclopedia of Papua New Guinea. 3 volumes; Vol I: A – K, maps, black and white illustrations, xv + 588pp. Vol II: l – Z, maps, black and white illustrations, 589–1231pp. Vol III: Index, folding colour map in rear pocket, map, colour illustration, v + 83pp. Carlton, Australia: Melbourne University Press. .
20231101.sw_174629_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/Funguvisiwa%20la%20Karolini
Funguvisiwa la Karolini
Funguvisiwa la Karolini (kwa Kiingereza: Caroline Islands) ni funguvisiwa la Mikronesia lililosambaa sana katika Bahari ya Pasifiki hadi umbali wa kilomita 3,540. Ni visiwa vidogo 500 hivi vyenye asili ya matumbawe.
20231101.sw_174629_1
https://sw.wikipedia.org/wiki/Funguvisiwa%20la%20Karolini
Funguvisiwa la Karolini
Visiwa vimekaliwa na watu tangu miaka 4,000 iliyopita, hasa kutoka Rasi ya Malay na visiwa vya Indonesia. Wengine wametokea visiwa vya Polinesia.
20231101.sw_174629_2
https://sw.wikipedia.org/wiki/Funguvisiwa%20la%20Karolini
Funguvisiwa la Karolini
Tangu kufika kwa Wahispania katika karne ya 16 visiwa vilikuwa chini ya ubwana wa nje lakini maisha ya kawaida yaliendelea bila mabadiliko makubwa kwa muda mrefu.
20231101.sw_174629_3
https://sw.wikipedia.org/wiki/Funguvisiwa%20la%20Karolini
Funguvisiwa la Karolini
Mwisho wa karne ya 19 Hispania iliuza koloni hilo kwa Ujerumani; utawala wa Kijerumani ulikwisha katika Vita vikuu vya kwanza ukachukuliwa na Japani hadi mwisho wa Vita vikuu vya pili.
20231101.sw_174629_4
https://sw.wikipedia.org/wiki/Funguvisiwa%20la%20Karolini
Funguvisiwa la Karolini
Japani ilifuatwa na Marekani iliyoendelea kutawala kwa niaba ya UM hadi uhuru (mwaka 1986 kwa shirikisho na 1994 kwa Palau).
20231101.sw_174630_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kisiwa%20cha%20Iona
Kisiwa cha Iona
Kisiwa cha Iona ni kisiwa kidogo magharibi kwa Uskoti Kaskazini kilicho maarufu kutokana na monasteri iliyoanzishwa huko na Kolumba mwaka 563.
20231101.sw_174630_1
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kisiwa%20cha%20Iona
Kisiwa cha Iona
Kwa karne tatu monasteri hiyo ya Ukristo wa Kikelti ilipata kuwa kituo muhimu cha uinjilishaji kwa Uskoti mzima (Wapikti na Waskoti wa kale) na hata mbali zaidi.
20231101.sw_174630_2
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kisiwa%20cha%20Iona
Kisiwa cha Iona
Christian, J & Stiller, C (2000), Iona Portrayed – The Island through Artists' Eyes 1760–1960, The New Iona Press, Inverness, 96pp, numerous illustrations in B&W and colour, with list of artists.
20231101.sw_174630_3
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kisiwa%20cha%20Iona
Kisiwa cha Iona
Dwelly, Edward (1911). Faclair Gàidhlig gu Beurla le Dealbhan/The Illustrated [Scottish] Gaelic- English Dictionary. Edinburgh. Birlinn. .
20231101.sw_174630_4
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kisiwa%20cha%20Iona
Kisiwa cha Iona
Gregory, Donald (1881) The History of the Western Highlands and Isles of Scotland 1493–1625. Edinburgh. Birlinn. 2008 reprint – originally published by Thomas D. Morrison. .
20231101.sw_174630_5
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kisiwa%20cha%20Iona
Kisiwa cha Iona
Hunter, James (2000). Last of the Free: A History of the Highlands and Islands of Scotland. Edinburgh. Mainstream.
20231101.sw_174630_6
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kisiwa%20cha%20Iona
Kisiwa cha Iona
Johnson, Samuel (1775). A Journey to the Western Islands of Scotland. London: Chapman & Dodd. (1924 edition).
20231101.sw_174630_7
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kisiwa%20cha%20Iona
Kisiwa cha Iona
Watson, W. J., The History of the Celtic Place-names of Scotland. Reprinted with an introduction by Simon Taylor, Birlinn, Edinburgh, 2004. .
20231101.sw_174630_8
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kisiwa%20cha%20Iona
Kisiwa cha Iona
Campbell, George F. (2006). The First and Lost Iona. Glasgow: Candlemas Hill Publishing. (and on Kindle).
20231101.sw_174630_9
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kisiwa%20cha%20Iona
Kisiwa cha Iona
Herbert, Maire (1996). Iona, Kells and Derry: The History and Hagiography of the Monastic familia of Columba. Dublin: Four Courts Press.
20231101.sw_174630_10
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kisiwa%20cha%20Iona
Kisiwa cha Iona
MacArthur, E Mairi, Iona, Colin Baxter Island Guide (1997) Colin Baxter Photography, Grantown-on-Spey, 128pp.
20231101.sw_174631_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mitume%20kumi%20na%20wawili%20wa%20Ireland
Mitume kumi na wawili wa Ireland
Mitume kumi na wawili wa Ireland walikuwa wachache bora kati ya maelfu ya wanafunzi wa Finiani wa Clonard (470-549) katika monasteri ya Clonard, Ireland, kituo muhimu sana cha Ukristo wa Kikelti.
20231101.sw_174632_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/Landeriko
Landeriko
Landeriko (kwa Kifaransa: Landry; alifariki Paris, Ufaransa, 656 hivi) alikuwa askofu wa ishirini na nane wa mji huo kuanzia mwaka 650 hadi kifo chake.
20231101.sw_174632_1
https://sw.wikipedia.org/wiki/Landeriko
Landeriko
Ili kusaidia fukara wakati wa njaa aliuza hata vyombo vya ibada na kujenga hospitali karibu na kanisa kuu.
20231101.sw_174632_2
https://sw.wikipedia.org/wiki/Landeriko
Landeriko
François De Vriendt, Saint Landry, évêque de Paris, dans Dictionnaire d'histoire et de géographie ecclésiastiques, t. 30, Paris, 2008, col. 289-292.
20231101.sw_174633_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/Itamari%20wa%20Rochester
Itamari wa Rochester
Itamari wa Rochester (kwa Kiingereza: Ithamar, Ythamar; alifariki Rochester, 656/664 ) alikuwa askofu wa Kanisa Katoliki katika mji huo wa Uingereza, wa kwanza mwenye asili ya Kigermanik.
20231101.sw_174634_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/Bogumili
Bogumili
Bogumili (alifariki Dobrowo, Polandi, 10 Juni 1192) alikuwa askofu mkuu wa Gniezno, miaka 1170-1182, lakini miaka yake ya mwisho aliishi kama mkaapweke mwenye maisha magumu .
20231101.sw_174634_1
https://sw.wikipedia.org/wiki/Bogumili
Bogumili
Tangu kale anaheshimiwa na Kanisa Katoliki kama mtakatifu. Heshima hiyo ilithibitishwa na Papa Pio XI tarehe 27 Mei 1925.
20231101.sw_174635_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/Alida%20Mkoma
Alida Mkoma
Alida Mkoma (pia: Aleydis, Alix, Alice, Adelaide; Schaerbeek, leo nchini Ubelgiji 1120 hivi - Ixelles, Ubelgiji, 11 Juni 1150), alikuwa bikira wa shirika la Wasitoo ambaye akiwa na umri wa miaka 22 alipatwa na ukoma, hivyo akalazimika kuishi upwekeni. Polepole alipotewa na uwezo wa kuona na kutumia viungo vyake vyote isipokuwa kinywa ili aweze kuimba sifa za Mwenyezi Mungu.
20231101.sw_174635_1
https://sw.wikipedia.org/wiki/Alida%20Mkoma
Alida Mkoma
Tarehe 14 Machi 1907 Papa Pius X alithibitisha heshima ya mtakatifu ambayo Wakatoliki walimpa tangu zamani.
20231101.sw_174635_2
https://sw.wikipedia.org/wiki/Alida%20Mkoma
Alida Mkoma
Latin Critical edition: "De B. Aleyde Scharembekana, Sanctimoniali Ordinis Cisterciensis, Camerae Iuxta Bruxellam", in Acta Sanctorum, edited by Godfrey Henschen, 477–83. Paris: Société des Bollandistes, 1688; repr. 1969.
20231101.sw_174635_3
https://sw.wikipedia.org/wiki/Alida%20Mkoma
Alida Mkoma
Modern English translation: Life of St Alice of Schaerbeek. Translated by Martinus Cawley, O.C.S.O. Lafayette, OR: Our Lady of Gaudalupe Abbey, 2000. Excerpts of the translation are available to read online:
20231101.sw_174635_4
https://sw.wikipedia.org/wiki/Alida%20Mkoma
Alida Mkoma
Campion, Eleanor, O.C.S.O. "Bernard and Alice the Leper: An Odor of Life for Some." Cistercian Studies Quarterly 39, no. 2 (2004): 127–39.
20231101.sw_174635_5
https://sw.wikipedia.org/wiki/Alida%20Mkoma
Alida Mkoma
Cawley, Martinus. "Introduction." In Life of St Alice of Schaerbeek, edited by Martinus Cawley, v-xxx. Lafayette, OR: Our Lady of Gaudalupe Abbey, 2000.
20231101.sw_174635_6
https://sw.wikipedia.org/wiki/Alida%20Mkoma
Alida Mkoma
Krahmer, Shawn Madison. "Redemptive Suffering: The Life of Alice of Schaerbeek in a Contemporary Context." In Maistresse of My Wit: Medieval Women, Modern Scholars, edited by Juanita Ruys and Louise d’Arcen, 267–93. Turnhout: Brepols, 2004.
20231101.sw_174635_7
https://sw.wikipedia.org/wiki/Alida%20Mkoma
Alida Mkoma
Madison, Shawn. "Suffering, Sacrifice, and Stability: "The Life of Aleydis of Schaerbeek" in a Contemporary Context ". Magistra 8, no. 2 (2002): 25-44.
20231101.sw_174635_8
https://sw.wikipedia.org/wiki/Alida%20Mkoma
Alida Mkoma
Mikkers, Edmund. O.C.S.O. "Meditations on the "Life" of Alice of Schaerbeek ". In Hidden Springs: Cistercian Monastic Women, edited by John A. Nichols and Lillian Thomas. O.C.S.O. Shank. Medieval Religious Women, 395-413. Kentucky: Cistercian Publications, 1995.
20231101.sw_174635_9
https://sw.wikipedia.org/wiki/Alida%20Mkoma
Alida Mkoma
Scholl , Edith, O.C.S.O. "The Golden Cross: Aleydis of Schaerbeek." In Hidden Springs: Cistercian Monastic Women, edited by John A. Nichols and Lillian Thomas. O.C.S.O. Shank. Medieval Religious Women, 377–93. Kentucky: Cistercian Publications, 1995.
20231101.sw_174635_10
https://sw.wikipedia.org/wiki/Alida%20Mkoma
Alida Mkoma
Spencer-Hall, Alicia. "Christ’s Suppurating Wounds: Leprosy in the Vita of Alice of Schaerbeek († 1250)." In ‘His Brest Tobrosten’: Wounds and Wound Repair in Medieval Culture, edited by Kelly DeVries and Larissa Tracy, 389–416. Leiden: Brill, 2015.
20231101.sw_174635_11
https://sw.wikipedia.org/wiki/Alida%20Mkoma
Alida Mkoma
Saint Lydwine of Schiedam, by J.K. Huysmans (translated from the French by Agnes Hastings), 1923, Kegan Paul, Trench, Trubner & Co., London. Reprinted 1979, TAN Books and Publishers, Rockford, Illinois, ISBN 0-89555-087-3
20231101.sw_174691_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/Eskil%20wa%20Tuna
Eskil wa Tuna
Eskil wa Tuna (Uingereza, karne ya 10 - Uswidi, karne ya 11) alikuwa askofu mmisionari huko Uswidi hadi alipouawa kwa kupigwa mawe mwaka 1038 au 1080.
20231101.sw_174692_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/Odulfi
Odulfi
Odulfi (pia: Odwulf, Odulf, Odulph, Odulfo, Odulphus ; alifariki Utrecht, Uholanzi, 865 hivi) alikuwa padri wa shirika la Waaugustino kutoka Brabant Kaskazini aliyeinjilisha kwa mafanikio Wafrisia.
20231101.sw_174693_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/Rambati
Rambati
(pia: Rambert, Ragnebert, Ragnebertus; alifariki karibu na Lyon, Ufaransa, 13 Juni 680) alikuwa mkabaila mwenye maadili ya hali ya juu ambaye alichukiwa na mkuu wa ikulu hata akafungwa na hatimae kuuawa.
20231101.sw_174733_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/Salmodi
Salmodi
Salmodi (pia: Psalmodius, Psalmet, Sauman, Saumay; aliishi karne ya 7) alikuwa mkaapweke karibu na Limoges, Akwitania, leo nchini Ufaransa.
20231101.sw_174734_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/Aventino%20wa%20Larboust
Aventino wa Larboust
Aventino wa Larboust (Bagnères-de-Luchon, 780 hivi - Saint-Aventin, 13 Juni karne ya 8) alikuwa mkaapweke katika bonde la Larboust, kwenye milima ya Pirenei, kusini mwa Ufaransa, hadi alipouawa na Waislamu.
20231101.sw_174734_1
https://sw.wikipedia.org/wiki/Aventino%20wa%20Larboust
Aventino wa Larboust
Paul Guérin et François Giry, « 13 juin : saint Aventin, apôtre de la Gascogne et martyr », dans Les petits Bollandistes Vies des saints de l'Ancien et du Nouveau Testament : Du 19 mai au 13 juin, t. 6, Bloud et Barral libraires-éditeurs, 1882, 654+VIII, p. 607-611
20231101.sw_174734_2
https://sw.wikipedia.org/wiki/Aventino%20wa%20Larboust
Aventino wa Larboust
Notice historique sur Saint-Aventin d'Aquitaine, martyr, par un prêtre du diocèse, Toulouse, Bon et Privat, 1850 ; rééd. Montréjeau, imp. Fabbro, 1988
20231101.sw_174747_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/Bungo%20mpenda-giza
Bungo mpenda-giza
Bungo wapenda-giza au madundu ni mbawakawa wa familia Tenebrionidae katika nusuoda Polyphaga ya oda Coleoptera. Kama bungo wote wanaweza kuwa wakubwa lakini wadogo pia. Baadhi ya spishi zinaweza kuwa haribifu, kama vile bungo wa unga (inayojulikana zaidi kama mnyoo wa unga). Kuna spishi zaidi ya 20,000 duniani kote; idadi ya spishi za Afrika ya Mashariki haijahesabiwa.
20231101.sw_174747_1
https://sw.wikipedia.org/wiki/Bungo%20mpenda-giza
Bungo mpenda-giza
Kwa ujumla, mbawakawa hawa wanafanana sana na mbawakawa wa wastani. Katika ukaguzi wa karibu, sifa zifuatazo zinaweza kutambuliwa:
20231101.sw_174747_2
https://sw.wikipedia.org/wiki/Bungo%20mpenda-giza
Bungo mpenda-giza
Tarsi zina pingili tano katika jozi ya kwanza na ya kati na nne katika jozi ya nyuma (5-5-4); kucha za tarsi ni rahisi.
20231101.sw_174747_3
https://sw.wikipedia.org/wiki/Bungo%20mpenda-giza
Bungo mpenda-giza
Lava ni ndefu, nyembamba na ya umbo la mcheduara na wana kutikulo yenye siklerotini nyingi. Kwa kawaida huwa na rangi ya manjano hadi rangi ya machungwa isiyoiva.
20231101.sw_174747_4
https://sw.wikipedia.org/wiki/Bungo%20mpenda-giza
Bungo mpenda-giza
Kama jina lao linavyoonyesha, wapevu hupenda kukaa mahali penye giza kama vile chini ya takataka au mawe, kwenye nyufa na mashimo. Wapevu na lava wa spishi nyingi ni wakulavyote wanaokula majani yanayooza, ubao unaooza, dutu bichi ya mimea, wadudu waliokufa na kuvu. [10] Wengine wamebobea katika kula nyoga. Spishi nyingi kubwa zaidi haziruki, mara nyingi kwa sababu mabawa yao mangumu ya mbele yameunganishwa pamoja, haswa katika maeneo makavu, ili kupunguza uvukizaji. Wapevu wa spishi nyingi huishi muda mrefu zaidi kuliko wadudu wengine wengi, kama miezi sita hadi miaka miwili.
20231101.sw_174747_5
https://sw.wikipedia.org/wiki/Bungo%20mpenda-giza
Bungo mpenda-giza
Lava wanaoishi ardhini huitwa nyunguwaya bandia (nyunguwaya wa kweli ni lava za bungo-fyatuo). Wanakula dutu za kikaboni zinazooza lakini pia wanaweza kusababisha hasara kwa kula mbegu zinazoota na kutafuna mizizi na machipukizi ya miche. Mara nyingi wao ni chanzo kinono cha chakula cha ndege na mamalia wadogo. Lava wengine hula nafaka iliyohifadhiwa na bidhaa zingine kama unga, nafaka za kiamshakinywa, tambi, biskuti, maharagwe na makokwa. Hawa huitwa minyoo ya unga, ikiwa ni pamoja na wale wa bungo mwekundu wa unga (Tribolium castaneum).
20231101.sw_174747_6
https://sw.wikipedia.org/wiki/Bungo%20mpenda-giza
Bungo mpenda-giza
Bungo wapenda-giza ni sehemu muhimu ya kina wadudu wa jangwani pamoja na bungo-mavi. Wale walio katika Jangwa la Namib wamebadilika kwa njia ambayo hukusanya matone ya ukungu yanayowekwa kwenye mabawa yao. Matone yanapokusanyika, maji hutiririka chini ya mgongo wa bungo hadi kwenye sehemu za kinywa, ambapo yanamezwa.[14]
20231101.sw_174759_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/Lotari%20wa%20Seez
Lotari wa Seez
(pia: Lother, Lotharie au Lohier; 685 - 15 Juni 756) alikuwa askofu wa 16 wa Seez, katika Ufaransa wa leo, hadi alipoamua kwenda kuishi upwekeni.
20231101.sw_174760_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/Isfridi
Isfridi
Isfridi, O.Prem. (1115 - Ratzeburg, Holstein, Ujerumani, 15 Juni 1204) alikuwa askofu wa 3 wa Ratzeburg kutoka shirika la Wapremontree, ambaye, huku akidumisha nidhamu ya kitawa, aliinjilisha Wavendi .
20231101.sw_174760_1
https://sw.wikipedia.org/wiki/Isfridi
Isfridi
Ndiyo sababu tangu kale anaheshimiwa kama mtakatifu. Papa Benedikto XIII alithibitisha heshima hiyo mwaka 1725.
20231101.sw_174766_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/Bobsledi
Bobsledi
Bobsledi (vilevile bobsleigh kutoka Kiingereza) ni aina ya mchezo wa Olimpiki unaohusisha timu ya watu wanaojitupa katika gari dogo la kusukuma lenye umbo la mstatili (bobsled). Maarufu sana nyakati za baridi. Ushindanishwaji wake huwa kwenye njia iliyotengenezwa katika barafu au utando wa baridi. Bobsledi inaweza kuwa mchezo wa kusisimua na unaohitaji ustadi mkubwa na ushirikiano kati ya wanariadha wa timu.
20231101.sw_174766_1
https://sw.wikipedia.org/wiki/Bobsledi
Bobsledi
Gari la Bobsled: Bobsledi ni gari la kushusha / kupoza baridi lenye muundo wa umbo la mstatili na lenye mawasiliano ya kushikilia baridi vizuri. Kuna aina tofauti za bobsledi, ikiwa ni pamoja na bobber-4 (kwa timu ya watu wanne) na bobber-2 (kwa timu ya watu wawili).
20231101.sw_174766_2
https://sw.wikipedia.org/wiki/Bobsledi
Bobsledi
Timu: Timu ya bobsledi ina jumla ya wanariadha wanaojumuisha dereva na wale wanaojipanga ndani ya bobsledi. Dereva anadhibiti mwelekeo na kasi ya bobsledi wakati wa kushuka kwenye njia.
20231101.sw_174766_3
https://sw.wikipedia.org/wiki/Bobsledi
Bobsledi
Njia: Njia ya bobsledi hutengenezwa kwenye barafu au utando wa baridi. Njia hizi zina vipengele, sehemu zenye mwinuko, haraka, pia zinaweza kuhusisha sehemu za kugeuza na changarawe ili kuongeza chachu ya mchezo.
20231101.sw_174766_4
https://sw.wikipedia.org/wiki/Bobsledi
Bobsledi
Shindano: Katika shindano la bobsledi, timu huanza kukimbiza mbio chombo kutoka juu ya mwinuko na kuingia kwenye bobsledi kwa kuchumpayao. Wanariadha hujaribu kushika nafasi za ndani ya gari ili kupunguza upinzani wa hewa. Dereva anatumia mbinu za kuendesha kubadilisha mwelekeo na kasi ya bobsledi wakati wa kushuka kwenye njia.
20231101.sw_174766_5
https://sw.wikipedia.org/wiki/Bobsledi
Bobsledi
Kasi na Usalama: Bobsledi inaweza kufikia kasi kubwa sana wakati wa kushuka, na kwa sababu hiyo, usalama ni jambo muhimu sana. Wanariadha wanavaa vifaa vya kinga, na kuna kanuni kali za usalama zinazosimamiwa katika mchezo huu.
20231101.sw_174766_6
https://sw.wikipedia.org/wiki/Bobsledi
Bobsledi
Historia: Bobsled ulianza katika miaka ya 1870 huko Uswisi na baadaye ukawa mchezo maarufu wa barafu. Leo, bobsledi ni sehemu ya Michezo ya Olimpiki ya majira ya baridi na inashirikisha timu kutoka duniani kote.
20231101.sw_174767_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/Jon%20Turteltaub
Jon Turteltaub
Jon Turteltaub ni mwongozaji na mtayarishaji maarufu wa filamu kutoka Marekani. Alizaliwa mnamo Agosti 8, 1963, huko New York City, New York], Marekani. Akiwa na asili ya Italia katika familia ya wasanii, Jon alionyesha uwezo wa kuongoza na kuunda hadithi mapema katika maisha yake.
20231101.sw_174767_1
https://sw.wikipedia.org/wiki/Jon%20Turteltaub
Jon Turteltaub
Baada ya kumaliza masomo yake ya shule ya upili, Jon Turteltaub aliendelea na masomo yake ya chuo kikuu katika Chuo Kikuu cha Wesleyan, ambapo alisomea sanaa ya maigizo na uongozaji wa filamu. Elimu yake ya chuo kikuu ilimpa msingi imara wa uelewa wa sanaa na uigizaji, ambapo ulimsaidia kuendeleza kazi yake katika tasnia ya filamu.
20231101.sw_174767_2
https://sw.wikipedia.org/wiki/Jon%20Turteltaub
Jon Turteltaub
Kazi ya Jon Turteltaub katika tasnia ya filamu imejulikana kwa ubunifu wake na uwezo wa kuwafikishia watazamaji hadithi zenye kugusa mioyo na burudani. Baadhi ya filamu zake maarufu ni pamoja na "Cool Runnings" (1993), ambayo iliiangazia hadithi ya kweli ya timu ya mbio za sledi kutoka nchi ya Jamaica kushiriki katika Michezo ya Olimpiki ya majira ya baridi. Filamu hii ilikuwa kichekesho cha moyo na inayojenga ujasiri.
20231101.sw_174767_3
https://sw.wikipedia.org/wiki/Jon%20Turteltaub
Jon Turteltaub
"Phenomenon" (1996) ni nyingine iliyofanikiwa sana katika mkusanyiko wake, inaigiza John Travolta kama mwanaume wa kawaida ambaye anapata uwezo wa kipekee wa kujifunza na kufanya mambo ya ajabu baada ya tukio la kimya kimya. Filamu hii ilikuwa na ujumbe wa kusisimua kuhusu nguvu ya maarifa na uelewa.
20231101.sw_174767_4
https://sw.wikipedia.org/wiki/Jon%20Turteltaub
Jon Turteltaub
Jon Turteltaub pia alishiriki katika utengenezaji wa safu ya filamu za "National Treasure" (2004) na "National Treasure: Book of Secrets" (2007), ambazo zinajumuisha uchunguzi wa siri za kihistoria na hazina kubwa za taifa la Marekani. Filamu hizi zilileta pamoja historia, vitisho, na hadithi za uchunguzi kwa njia ya kufurahisha na kusisimua.
20231101.sw_174767_5
https://sw.wikipedia.org/wiki/Jon%20Turteltaub
Jon Turteltaub
Katika "The Sorcerer's Apprentice" (2010), Jon Turteltaub aliendelea kuonyesha ujuzi wake wa kuongoza filamu za vitisho na hatua. Filamu hii inaigiza Nicolas Cage na inategemea hadithi ya mwanafunzi wa uchawi ambaye anajifunza kutoka kwa mchawi mkongwe.
20231101.sw_174767_6
https://sw.wikipedia.org/wiki/Jon%20Turteltaub
Jon Turteltaub
Kupitia kazi yake ya kuigiza na kuongoza, Jon Turteltaub ameleta burudani na mafanikio kwa watazamaji ulimwenguni kote. Amekuwa mmoja wa waongozaji wa filamu wanaoheshimiwa sana katika tasnia ya burudani, na kazi zake zinaendelea kufurahisha na kuhamasisha watazamaji kote ulimwenguni.
20231101.sw_174768_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/Dawn%20Steel
Dawn Steel
Dawn Steel alikuwa mtendaji maarufu katika tasnia ya filamu ya Marekani. Alizaliwa mnamo Agosti 19, 1946, huko New York City, New York, USA, na alifariki mnamo Desemba 20, 1997. Alikuwa mmoja wa wanawake wachache waliopata mafanikio makubwa katika nafasi za uongozi katika tasnia ya filamu wakati wa kazi yake.
20231101.sw_174768_1
https://sw.wikipedia.org/wiki/Dawn%20Steel
Dawn Steel
Dawn Steel alipata elimu yake katika Chuo Kikuu cha West Virginia na baadaye alifanya kazi katika majarida ya burudani kabla ya kuanza kazi yake katika tasnia ya filamu. Alianza kama msimamizi wa utengenezaji na baadaye akafanya kazi na kampuni za filamu kama vile Paramount Pictures.
20231101.sw_174768_2
https://sw.wikipedia.org/wiki/Dawn%20Steel
Dawn Steel
Kazi ya Dawn Steel katika tasnia ya filamu imejulikana kwa uwezo wake wa kuchukua hatari na kuendeleza miradi ya kuvutia. Alihusika katika uzalishaji wa filamu nyingi maarufu, ikiwa ni pamoja na:
20231101.sw_174768_3
https://sw.wikipedia.org/wiki/Dawn%20Steel
Dawn Steel
"Top Gun" (1986) - Filamu hii ya vitisho na hatua ilikuwa moja wapo ya filamu za kubeba mapato zaidi za mwaka huo. Iliwasilisha maisha ya marubani wa kijeshi wa Navy na iliyoongozwa na Tony Scott.
20231101.sw_174768_4
https://sw.wikipedia.org/wiki/Dawn%20Steel
Dawn Steel
"Fatal Attraction" (1987) - Filamu hii ya kutisha iliyoiigiza Michael Douglas na Glenn Close ilitengeneza msisimko mkubwa na inaendelea kuchukuliwa kuwa moja ya sinema bora za kutisha za muda wote.
20231101.sw_174768_5
https://sw.wikipedia.org/wiki/Dawn%20Steel
Dawn Steel
"The Accused" (1988) - Filamu hii iliyoiigiza Jodie Foster ililenga suala la unyanyasaji wa kijinsia na ilipokea tuzo nyingi na sifa kwa uigizaji wa Foster.
20231101.sw_174768_6
https://sw.wikipedia.org/wiki/Dawn%20Steel
Dawn Steel
Dawn Steel alikuwa mtendaji wa kwanza wa kike kuchukua jukumu la uongozi katika kampuni kubwa ya filamu, Paramount Pictures, na aliendelea kufanya kazi kwa ufanisi katika majukumu ya utayarishaji na utendaji katika tasnia ya burudani. Alichangia sana katika mafanikio ya filamu za Hollywood na kuwa mfano wa mwanamke mwenye mafanikio katika tasnia hiyo. Kifo chake mnamo 1997 kilikuwa pigo kwa tasnia ya filamu na ulimwengu wa burudani.
20231101.sw_174776_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/Yustina%20wa%20Mainz
Yustina wa Mainz
Yustina wa Mainz (alifariki 451 hivi) alikuwa dada wa Aureus wa Mainz, askofu wa kwanza kujulikana wa Mainz, leo nchini Ujerumani, katika nusu ya kwanza ya karne ya 5.
20231101.sw_174781_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/Sekardo
Sekardo
Sekardo (kwa Kiitalia: Ceccardo; alifariki Carrara, Toscana, Italia, 860 au 892) alikuwa askofu wa Luni aliyeuawa na mafundi wa kukata miamba .
20231101.sw_174808_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/Vercetti%20Regular
Vercetti Regular
Vercetti Regular, ambayo pia inajulikana kama Vercetti, ni fonti isiyolipishwa ya sans serif ambayo inaweza kutumika kwa madhumuni ya kibiashara na kibinafsi. Ilianza kupatikana mnamo 2022 chini ya leseni ya Licence Amicale, ambayo inaruhusu watumiaji kushiriki faili za fonti na marafiki na wafanyikazi wenzako.