_id
stringlengths
15
22
url
stringlengths
31
150
title
stringlengths
1
86
text
stringlengths
100
23.8k
20231101.sw_1208_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kiido
Kiido
Kiido ni lugha ya kupangwa. Inafanana sana na Kiesperanto, lakini haizungumzwi na watu wengi kama Kiesperanto.
20231101.sw_1208_1
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kiido
Kiido
Nomino (majina) zote zinahitimu kwa kiambishi tawali -o, kwa mfano "arbo" (mti). Wingi wa nomino unahitimu kwa -i (arbi = miti).
20231101.sw_1663_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mungu
Mungu
Mungu ni jina lenye asili ya Kibantu linalotumika kwa yeyote anayesadikiwa katika dini mbalimbali kuwa na uhai wa hali ya juu.
20231101.sw_1663_1
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mungu
Mungu
Kati ya wafuasi wa dini hizo, wengi wanaona kuwa Umungu, kwa jinsi ulivyo au unavyofirika, haukubali mgawanyiko. Hasa katika Uyahudi, Ukristo na Uislamu wanasisitiza umoja wa Mungu kuwa ndio msingi wa imani yao. Kwao Mungu ni wa milele, anafahamu yote na kutaka hasa uwepo wa viumbe. Tena kwa hiari yake alipenda kujifunua kwa binadamu; kielelezo ni Ibrahimu/Abrahamu aliyefanywa rafiki yake na baba wa waamini wote.
20231101.sw_1663_2
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mungu
Mungu
Kuna dini nyingine zinazokubali kuwepo kwa miungu mbalimbali (wawili au zaidi). Hasa dini nyingi za jadi zinaamini wingi wa miungu. Dini kubwa duniani inayosadiki miungu mingi ni Uhindu. Pia katika sehemu za Afrika ya Magharibi ibada za miungu mingi zinaendelea hadi leo.
20231101.sw_1663_3
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mungu
Mungu
Jamii za Afrika zilikuwa na dini zao ambamo tunaweza kuona imani katika nguvu za kiroho ambazo zinaitwa majina tofauti. Tunaweza kukuta imani ya Mungu Mkuu, pia ya miungu mbalimbali, pamoja na imani ya kuwepo kwa roho za wahenga, mizimu na pepo mbalimbali.
20231101.sw_1663_4
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mungu
Mungu
Tukijiuliza juu ya uhusiano kati ya mizimu, roho, miungu mbalimbali na Mungu Mkuu, ni lazima kwanza tujue imani za jadi hutofautiana kutoka jamii moja hadi jamii nyingine.
20231101.sw_1663_5
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mungu
Mungu
Mara ningi imani za Kiafrika humwona Mungu Mkuu mmoja kuwa wa juu na mwenye nguvu zaidi. Yuko kabla ya kila kitu kingine na asili yake haijulikani. Hivyo nguvu hutazamwa kwa ngazi tofauti; Mwenyezi Mungu yuko juu, chini yake kuna roho mbalimbali au hata miungu pamoja na nguvu za asili, na mwishoni binadamu wasio na nguvu nyingi.
20231101.sw_1663_6
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mungu
Mungu
Wakati mwingine hadithi za uumbaji za Kiafrika zinamwonyesha Mungu akiwa au akienda mbali na watu au hawasiliani nao tena moja kwa moja. Anaacha washughulikiwe na roho au miungu midogo aliyoumba pia. Mungu wa aina hiyo anaonekana mbali sana na mambo ya binadamu; kwa sababu hiyo, mara kwa mara miungu midogo huombwa badala yake ili kupata usaidizi. Katika jamii nyingine wanaamini kwamba mizimu inaweza kuleta mawasiliano baina ya Mungu na binadamu.
20231101.sw_1663_7
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mungu
Mungu
Vikundi vingine humwona Mungu Mkuu kuwa karibu sawa na miungu mingine, kama mwenyekiti wao au kama mfalme kati ya machifu. Wafon katika Afrika ya Magharibi humwaza Mungu mkuu kama mapacha mawili: Mavu, nguvu ya kike, na Lisa, nguvu ya kiume. Wakitazamwa kama nguvu moja huitwa Mavu pekee. Wameumba watoto ambao hutawala shughuli za dunia na viumbe vyake kama miungu.
20231101.sw_1663_8
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mungu
Mungu
Dhana za aina hiyo zimeleta majadiliano kati ya wataalamu kuhusu kuainisha dini za Kiafrika kuwa za Mungu mmoja (monotheistic) au za miungu mingi (polytheistic). Wengine huona uainishaji huo hauna maana kwa dini za Kiafrika.
20231101.sw_1663_9
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mungu
Mungu
Mtaalamu John Mbiti wa Kenya aliona kwamba kimsingi imani katika Mungu mmoja inapatikana kwa namna moja au nyingine katika dini zote za asili. Anaeleza nguvu nyingine za kiroho kama tabia au shughuli za Mungu yeye yule zinazotazamwa pekepeke.
20231101.sw_1663_10
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mungu
Mungu
Biblia inaanza kwa kukiri kwamba asili ya uhai wote ni Mwenyezi Mungu: “Hapo mwanzo Mungu aliziumba mbingu na nchi” (Mwa 1:1).
20231101.sw_1663_11
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mungu
Mungu
Tena, kwamba Mungu anazidi kushughulikia viumbe vyake, akividumisha na kuviongoza vyote vifikie lengo alilovipangia. “Ndani yake yeye tunaishi, tunakwenda na kuwa na uhai wetu” (Mdo 17:28). Tunamtegemea pande zote: angetuacha kidogo tungetoweka mara. Yesu alipolaumiwa kwa kuponya watu siku ya pumziko, alijitetea kwamba, “Baba yangu anatenda kazi hata sasa, nami ninatenda kazi” (Yoh 5:17). "Yeye hujishughulisha sana kwa mambo yenu" (1Pet 5:7).
20231101.sw_1663_12
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mungu
Mungu
Kutokana na imani hiyo, tunahimizwa kujiachilia mikononi mwake kwa moyo wa kitoto, tukiwajibika bila mahangaiko yanayowapata watu wasiomjua. “Waangalieni ndege wa angani, ya kwamba hawapandi, wala hawavuni, wala hawakusanyi ghalani; na Baba yenu wa mbinguni huwalisha hao. Ninyi je, si bora kupita hao?” (Math 6:26). “Nawe una nini usichokipokea?” (1Kor 4:7). “Nimrudishie Bwana nini kwa ukarimu wake wote alionitendea?” (Zab 116:12).
20231101.sw_1663_13
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mungu
Mungu
Tunaanza kumjua Mungu kwa kuzingatia viumbe vyake, hasa dhamiri yetu. “Kwa sababu mambo yake yasiyoonekana tangu kuumbwa ulimwengu yanaonekana, na kufahamika kwa kazi zake; yaani, uweza wake wa milele na Uungu wake” (Rom 1:20).
20231101.sw_1663_14
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mungu
Mungu
Hivyo tunaweza pia kusema juu ya Mungu kuanzia wema, ukweli na uzuri wa viumbe vyake na kumsifu kiasi chetu kwamba ndiye wema, ukweli na uzuri wenyewe. Lakini tukiri pia kuwa maneno yetu duni hayawezi kutosha kamwe kufafanua fumbo lake. “Kwa maana, nimesema maneno nisiyoyafahamu, mambo ya ajabu ya kunishinda mimi, nisiyoyajua” (Ayu 42:3). Tungemuelewa, asingekuwa Mungu.
20231101.sw_1663_15
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mungu
Mungu
Mwenyezi Mungu ni ukamilifu mtupu usio na mipaka kwa milele yote. “Tazama, Mungu ni mkuu, nasi hatumjui; hesabu ya miaka yake haitafutiki” (Ayu 36:26). “Mungu ni Roho, nao wamwabuduo yeye imewapasa kumwabudu katika roho na kweli” (Yoh 4:24).
20231101.sw_1663_16
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mungu
Mungu
Akiwa Roho, viungo ambavyo pengine anapewa vinamaanisha tu sifa fulani: k.mf. macho ujuzi wake, mikono uwezo wake, mabawa ulinzi wake, n.k. “Roho haina mwili na mifupa” (Lk 24:39).
20231101.sw_1663_17
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mungu
Mungu
Hasa Mungu amejifunua kuwa upendo wenyewe. “Bwana, Bwana, Mungu mwingi wa huruma, mwenye fadhili, si mwepesi wa hasira, mwingi wa rehema na kweli” (Kut 34:6). “Mungu ni upendo, naye akaaye katika pendo, hukaa ndani ya Mungu, na Mungu hukaa ndani yake” (1Yoh 4:16). “Yeye asiyependa, hakumjua Mungu, kwa maana Mungu ni upendo” (1Yoh 4:8).
20231101.sw_1663_18
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mungu
Mungu
Pickover, Cliff, The Paradox of God and the Science of Omniscience, Palgrave/St Martin's Press, 2001. ISBN 1-4039-6457-2
20231101.sw_1663_19
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mungu
Mungu
Collins, Francis, The Language of God: A Scientist Presents Evidence for Belief, Free Press, 2006. ISBN 0-7432-8639-1
20231101.sw_1663_20
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mungu
Mungu
Armstrong, Karen, A History of God: The 4,000-Year Quest of Judaism, Christianity and Islam, Ballantine Books, 1994. ISBN 0-434-02456-2
20231101.sw_1663_21
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mungu
Mungu
Paul Tillich, Systematic Theology, Vol. 1 (Chicago: University of Chicago Press, 1951). ISBN 0-226-80337-6
20231101.sw_1664_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/Volkeno
Volkeno
Volkeno (pia: volkano au volikano) ni mahali ambako zaha inatoka nje ya uso wa ardhi. Mara nyingi - lakini si kila mahali - volkeno imekuwa mlima. Volkeno huwa na kasoko yaani shimo ambako zaha na gesi zinatoka nje.
20231101.sw_1664_1
https://sw.wikipedia.org/wiki/Volkeno
Volkeno
Asili ya jina ni mungu wa dini ya Roma ya Kale aliyeitwa "Vulcanus". Kati ya miungu ya Kiroma alihusika na moto, radi na uhunzi; kwa hiyo aliheshimiwa hasa na wote waliotumia moto kwa kuyeyusha metali kama chuma au shaba.
20231101.sw_1664_2
https://sw.wikipedia.org/wiki/Volkeno
Volkeno
Volkeno ni dalili ya kwamba mahali pake ganda la dunia si nene sana, hivyo joto la ndani linapata njia ya kutoka nje. Volkeno huanza katika tambarare. Zaha hutoka katika hali ya kiowevu; ikipoa haraka inaganda kuwa mwamba na hujenga mlima wa kuzunguka shimo la kasoko yake. Milima ya aina hiyo inaweza kukua sana. Mfano wa volkeno kubwa ni Kilimanjaro. Miamba yake yote ilijengwa na zaha iliyotoka ndani ya dunia.
20231101.sw_1664_3
https://sw.wikipedia.org/wiki/Volkeno
Volkeno
Volkeno nyingi hutokea pale ambako mabamba ya ganda la dunia yanaachana au kusukumana. Hivyo volkeno hutokea hasa kwenye mistari ya kukutana kwa mabamba hayo.
20231101.sw_1664_4
https://sw.wikipedia.org/wiki/Volkeno
Volkeno
Volkeno inaweza kupatikana kama volkeno hai inayoendelea kutema moto, gesi na majivu. Inaweza pia kuonekana kama volkeno bwete inayokaa kama milima mingine bila kuonyesha dalili za moto. Lakini kutokana na umbo na tabia za miamba yake inaonekana mlima huu ulijengwa kwa njia ya kivolkeno.
20231101.sw_1664_5
https://sw.wikipedia.org/wiki/Volkeno
Volkeno
Volkeno bwete inaweza kuamka tena. Mara nyingi kuwepo kwa chemchemi za maji ya moto au kutokea kwa gesi kwenye sehemu fulani ni dalili ya kwamba bado kuna njia kati ya mlima na magma ya chini. Kipindi kati ya milipuko kinaweza kuwa cha miaka mingi.
20231101.sw_1664_6
https://sw.wikipedia.org/wiki/Volkeno
Volkeno
Mlipuko wa volkeno ni hatari kwa ajili ya wanadamu na mazingira. Mlipuko unaweza kurusha idadi kubwa ya gesi sumu na mawe ya moto hewani na kumwaga lava nje inayosambaa kama mto wa moto kwa umbali wa kilomita kadhaa.
20231101.sw_1664_7
https://sw.wikipedia.org/wiki/Volkeno
Volkeno
Hiyo hatari ni kubwa zaidi pale ambako volkeno ililala kama volkeno bwete kwa miaka mingi, labda elfu kadhaa. Hapo mara nyingi watu wamevutwa na udongo wenye rutuba kutokana na majivu ya volkeno wajenge makazi na kulima. Kama hapo volkeni inageuka kuwa hai tena hatari ni kubwa. Kuna mifano ya vifo vingi vilivyosababishwa na volkeno. Hasara inategema kama miji iko karibu na volkeno au la, na kama serikali zina huduma za kutazama volkeno na kuonya watu watoke mapema wakati dalili za kwanza zinatokea.
20231101.sw_1664_8
https://sw.wikipedia.org/wiki/Volkeno
Volkeno
mlipuko wa volkeno ya Krakatau, Indonesia mwaka 1883. Ilirusha mavumbi mengi angani kiasi kilichoonekana kote duniani
20231101.sw_1664_9
https://sw.wikipedia.org/wiki/Volkeno
Volkeno
mlipuko wa volkeno Nevado del Ruiz, Kolombia mwaka 1985 uliua watu 25.000 kutokana na kuyeyusha theluji na barafu mlimani na kusababisha mafuriko ya ghafla
20231101.sw_1664_10
https://sw.wikipedia.org/wiki/Volkeno
Volkeno
Katika karne ya 21 volkeno ya Nyiragongo katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ililipuka mara mara mbili mwaka 2002 na mwaka 2021 na kusababisha vifo katia miji jirani ya Gisenyi na Goma.
20231101.sw_1665_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/Tofaa
Tofaa
Tofaa (pia: tufaha; kutoka kar. تفاح tofah; kwa Kiingereza: apple) ni tunda la mtofaa. Ni kati ya matunda yanayovunwa sana duniani. Maua nyeupe hutoa tunda lenye umbo mviringo na kipenyo cha sentimita 5 - 9.
20231101.sw_1665_1
https://sw.wikipedia.org/wiki/Tofaa
Tofaa
Asili ya mimea iko Asia. Leo kuna takriban aina 7,500 za matofaa. Mavuno ya kila mwaka hufikia tani milioni 55.
20231101.sw_1665_2
https://sw.wikipedia.org/wiki/Tofaa
Tofaa
Tufaa ni tunda la mtufaa (Malus pumila), mti wa familia Rosaceae. Ni miongoni ya miti inayokuzwa kwa wingi sana. Mti ni mdogo na wenye kupukutisha majani yake, wenye kufikia urefu wa mita 3 mpaka 12 za kimo, na kushona kwa majani mengi kwelikweli. majani yake yamejipanga kwa namna tofauti tofauti, yakiwa na urefu wa sm 5 – 12 na upana wa sm 3 – 6 kwa upana. Maua mengi huchanua majira ya kuchipua sambamba na kufunguka kwa vichipukizi. Maua ni meupe na alama kidogo za rangi ya waridi ambayo hufifia taratibu. Mfaua hayo huwa na petali tano, na yana upana wa sm 2.5 mpaka 3.5. kwa kipenyo. Matunda hukomaa msimu wa kuchipua, na huwa yamefikia kipenyo cha sm 5 – 9. Katikati mwa tunda huwa na kapeli tano zilizojipanga muundo kama wa nyota tano, huku kila kapeli moja ikiwa na mbegu moja mpaka tatu hivi.
20231101.sw_1665_3
https://sw.wikipedia.org/wiki/Tofaa
Tofaa
Mti huu asili yake ni Asia ya Kati, ambako miti pori ya kale ya tufaa bado inapatikana mpaka leo. Sasa hivi kuna zaidi ya aina ya miti ya tufaa 7,500 inayofahamika inayopelekea kuwa na kila aina ya tabia ya miti ianyotakiwa kwa eneo husika. Aina hizo zinatofautiana kwa mazao yao na ukubwa wa miti yenyewe, hata kama yakipandwa katika shina moja.
20231101.sw_1665_4
https://sw.wikipedia.org/wiki/Tofaa
Tofaa
Zaidi ya tani milioni 55 za matufaa zilizalishwa duniani kote ndani ya mwaka 2005, kwa thamani ya takribani dola za kimarekani bilioni 10. China pekee ilizalisha karibu 35% ya jumla hii. Marekani ni ya pili kwa uzalishajji, kwa zaidi ya 7.5% uzalishaji duniani. Uturuki, ufaransa, Italia na Irani pia wazalishaji wazuri wa tufaa.
20231101.sw_1665_5
https://sw.wikipedia.org/wiki/Tofaa
Tofaa
Aina inayoongoza ni ile ya pori ya "Malus sieverii", inayopatikana huko kati mwa Asia, kusini mwa Kazakstani, Krygyzstani, Tajikistani na Xinjiang, China, na awkati mwingine Malus sylvestris.
20231101.sw_1665_6
https://sw.wikipedia.org/wiki/Tofaa
Tofaa
Mwanzo wa kuchipua kwa jenasi ya Malus ni huko Uturuki Mashariki. Mtufaa pengine ndio ukawa mti wa kwanza kuanza kulimwa na binadamu, na matunda yake yamekuwa yakiboreshwa kwa uchaguzi maalumu kwa miaka maelfu. Mfalme, "Alexander the Great", huonwa ndiye mgunduzi wa miti mifupi ya tufaa huko Asia Ndogo mnamo 300 KK, ambayo baadae ilipelekwa Macedonia. Tufaa za kipupwe, ambazo huchumwa mwishoni mwa msimu wa kuchipua na kuhifadhiwa katika baridi kali, kimekuwa chakula mihimu kwa Asia na Ulaya kwa miaka mingi , hali kadhalika na kwa Marekani na hata huko Argentina. tufaa zilipelekwa Amerika ya kaskazini na wakoloni miaka ya 1600, na mti wa tufaa wa kwanaza huko Amerika ya Akskazini wasemekana kuwa huko Boston, mwaka 1625.mwaka 1900, miradi ya kilimo cha umwagiliaji ilianza kuruhusu kilimo cha matunda kilichogharimu mabilioni, huku tufaa zikiwa ndiyo spishi zinazoongoza.
20231101.sw_1665_7
https://sw.wikipedia.org/wiki/Tofaa
Tofaa
Kwa kawaida huko msituni tufaa huzaliana kwa mbegu. Hata hivyo, kama yalivyo matunda mengi yanayokua zaidi ya mwaka mmoja, huweza kupanda kwa vichipukizi. Hii ni kwasababu matunda mengi yanayokuzwa kwa mbegu, huweza kuzalisha mmea wenye tabia tofauti kabisa baina yamimea – wazazi, na zinaweza kuwa zenye hasara kubwa. spishi nyingi imara huzalishwa kwa kuchanaganya vizalia vya mimea mbalimbali.
20231101.sw_1665_8
https://sw.wikipedia.org/wiki/Tofaa
Tofaa
Tufaa lazima zipate uchavushaji kila mwaka ili kuzalisha matunda. Kila msimu wa maua, wakulima wa tufaa lazima waandae wachavushaji kwaajili ya kubeba poleni. Nyuki wa asali hutumika kwa kazi hii, hasa wale wa aina ya Orchard mason bee, na hutumika kwma msaada wa uchavushaji kwenye mashmba ya biashara. Pia wakati mwingine nyuki aina ya "Bumble bee queens" huwepo mashambani kwa kazi hiyo hiyo.
20231101.sw_1665_9
https://sw.wikipedia.org/wiki/Tofaa
Tofaa
Aina mbalimbali za tufaa hutofautiana kwa mazao na ukubwa wa miti, hata kama yakikuzwa kwenye shina moja. Kama baadhi ya miti isipopunguzwa hukua na kuwa miti mikubwa kwelikweli, lakini hufanya uvunaji uwe mgumu. Miti ya kawaida iliyokomaa huzalisha kg 40 – 200 za tufaa kila mwaka, japo uzalishaji unaweza kukarubia hata sifuri kwene misimu mibaya. Tufaa huvunwa kwa ngazi tatu zinazofungwa kwenye miti. Miti midogo hutoa karibu kg 10 – 80 za tufa kwa mwaka.
20231101.sw_1665_10
https://sw.wikipedia.org/wiki/Tofaa
Tofaa
Kibiashara, tufaa huhifadhiwa kwa miezi kadhaa kwenye joto maalumu ili kuratibu kiwango cha kuiva kwa nyakati maalumu kwa kutumia kemikali maalumu. Hutunzwa kwenye chemba zenye kiwango kikubwa cha gesi ya ukaa (kaboni daioksaidi) na hewa iliyochujwa vizuri. Hii huzuia ili kemikali maalumu, ethylene, inayotumika kuivisha matunda isiongezeke na hivyo kuivisha matunda hovyo. Yakiwa nyumbani kwajili ya matamizi, tufaa huweza kuhifadhiwa kwenye jokofu za kawaida kwa majuma mawili hivi, kwenye sehemu zenye baridi hasa chini ya 5 °C.
20231101.sw_1665_11
https://sw.wikipedia.org/wiki/Tofaa
Tofaa
Ule msemo “tufaa moja kwa siku, humweka dokta mbali,” huonesha faida za tufaa tangu karne ya 19. Tafiti zinaonesha tufaa hupunguza uwezekano wa mtu kupata kansa ya utumbo mkubwa, tezi ya uzazi (prostate) na hata kansa ya mapafu. ukilinganisha na matunda mengine, tufaa zina kiwangio kidigo cha vitamin C, lakini zina kiwango kikubwa cha kampaundi za antioxidant.Kiwango cha makapi, ambacho ni kidogo kuliko kwenye matunda mw=engine husaidia kuratibu mizunguko ya tumbo na hivyo kupunguza uwezakano wa kansa ya utumbo mkubwa. Husaidia pia kupunguza magonjwa ya moyo, kupunguza uzito, na kiwango cha mafuta kwenye mishipa ya damu na moyo, kwa kuwa na kiasi kikubwa cha kalori kama ilivyo kwa matunda mengi na mbogamboga.
20231101.sw_1667_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kiazi%20cha%20kizungu
Kiazi cha kizungu
Kiazi cha kizungu, kiazi ulaya, kiazi mviringo au mbatata ni mmea wa chakula uliomo katika familia ya Solanaceae. Chakula ni sehemu nene za mizizi yake (kiazi) yenye wanga, vitamini na madini. Sehemu bichi zinazoonekana juu ya ardhi haziliwi ni sumu.
20231101.sw_1667_1
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kiazi%20cha%20kizungu
Kiazi cha kizungu
Viazi hivi ni chakula muhimu kimataifa ni chakula kikuu katika nyingi. Asili ya mmea iko Amerika ya Kusini ilipoteuliwa na kukuzwa na Maindio. Wahispania walikikuta Amerika na kuisambaza Ulaya. Hata hivyo wakati mwingine huitwa "kiazi ulaya" au "kiazi kizungu" kwa sababu imefika Afrika kupitia Ulaya.
20231101.sw_1675_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/Seattle%2C%20Washington
Seattle, Washington
Seattle ni mji wa jimbo la Washington (ncha ya kaskazini magharibi ya Marekani). Kwa mujibu wa sensa iliyofanyika mnamo mwaka wa 2018, mji una wakazi wapatao milioni 3.87 wanaoishi katika mji huu.
20231101.sw_1675_1
https://sw.wikipedia.org/wiki/Seattle%2C%20Washington
Seattle, Washington
Seattle ni njia kuu ya biashara kati ya Marekani na Asia, ukiwa na bandari ya nne kwa ukubwa katika Marekani Kaskazini kwa kontena, tangu mwaka 2015. Seattle na Mombasa (Kenya) ni miji-ndugu.
20231101.sw_1675_2
https://sw.wikipedia.org/wiki/Seattle%2C%20Washington
Seattle, Washington
Seattle ni mji mkubwa zaidi ya yote katika jimbo la Washington na mkoa wa Pacific Northwest katika Marekani Kaskazini na ni mkubwa wa kumi na tano katika Marekani. Katika Julai 2013, Seattle iliongeza haraka zaidi katika miji mikuu ya Marekani.
20231101.sw_1675_3
https://sw.wikipedia.org/wiki/Seattle%2C%20Washington
Seattle, Washington
Mji upo ismus kati ya Puget Sound (njia ya Bahari ya Pasifiki) na Ziwa Washington, kilometa 160 (maili 100) kusini mwa mpaka wa Marekani na Kanada.
20231101.sw_1675_4
https://sw.wikipedia.org/wiki/Seattle%2C%20Washington
Seattle, Washington
Wamarekani wa asili walikaa eneo la Seattle si chini ya miaka 4,000 kabla ya wakoloni Wazungu kuja kwa mara ya kwanza. Arthur A. Denny na kundi la Wazungu, ambalo liliitwa “Denny Party,” walifika Alki Point tarehe 13 Novemba 1851 katika meli inayoitwa Exact. Walitoka Illinois na walipitia Portland, Oregon kabla ya kufika eneo la Seattle. Walianzisha koloni katika pwani ya mashariki ya Elliott Bay ambayo waliita “Seattle” mwaka 1852 kuheshimu Mtemi Si’ahl wa makabila ya huko yaliyoitwa Duwamish na Suquamish. Sasa, Seattle ina idadi kubwa ya watu kama Wamarekani wa asili, Waafrika na Waasia. Pia, ni mji wa sita kwa kuwa na idadi ya watu wa jamii ya LGBT katika Marekani kwa asilimia.
20231101.sw_1675_5
https://sw.wikipedia.org/wiki/Seattle%2C%20Washington
Seattle, Washington
Kiwanda kikuu cha kwanza katika Seattle kilikuwa kukata mbao. Lakini, mwishoni mwa miaka 1800, mji ulibadilika na ulikuwa kituo kikubwa cha biashara na mahali pa kutengenezea meli. Seattle ilikuwa njia kwa watu waliosafiri Alaska wakati wa Klondike Gold Rush. Baada ya vita ya pili ya dunia, Seattle ilikuwa kituo cha kutengenezea ndege, kwa sababu shirika la Boeing lilianzishwa hapo. Tangu miaka ya 80, Seattle imekuwa kituo cha teknolojia na makampuni kama Microsoft na Amazon, ambayo yalianzishwa hapo. Kampuni ya ndege ya Alaska Airlines ilianzishwa katika SeaTac, Washington na ilihudumia uwanja wa ndege wa Seattle, Seattle-Tacoma International Airport. Mji umeona ukuaji wa uchumi kwa sababu makampuni mapya ya teknolojia na mtandao yalileta fedha na rasilimali. Idadi ya watu iliongezeka kwa 50,000 kati ya miaka 1990 na 2000.
20231101.sw_1675_6
https://sw.wikipedia.org/wiki/Seattle%2C%20Washington
Seattle, Washington
Seattle na jimbo la Washington lina baadhi ya mishahara mikuu zaidi katika nchi – $15 kwa saa kwa biashara ndogo ndogo na $16 kwa makampuni makuu – kwa sababu idadi ya watu wanaongezeka haraka sana.Seattle ina historia muhimu ya muziki pia. Kati ya miaka ya 1918 na 1951, kulikuwa na karibu  vilabu ishirini na nne vya klabu muziki wa jazz katika mtaa wa Jackson, kutoka wilaya ya Chinatown/International mpaka wilaya ya katikati. Seattle ni mahali pa kuzaliwa ya mwanamuziki maarufu, Jimi Hendrix, na pia makundi ya Nirvana, Pearl Jam, Foo Fighters na harakati za muziki wa mwamba mbadala.
20231101.sw_1675_7
https://sw.wikipedia.org/wiki/Seattle%2C%20Washington
Seattle, Washington
Mji umejulikana kimataifa hasa kwa sababu hadi 2001 ilikuwa makao makuu ya kampuni ya Boeing inayojenga ndege za abiria na mizigo.
20231101.sw_1676_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kenya
Kenya
Kenya imepakana na Ethiopia (kaskazini), Somalia (kaskazini mashariki), Tanzania (kusini), Uganda na Ziwa Victoria (magharibi), kisha Sudan Kusini (kaskazini magharibi).
20231101.sw_1676_1
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kenya
Kenya
Kenya ni nchi mwanachama wa Jumuiya ya Afrika ya Mashariki na wa miundo mingine mbalimbali ya kimataifa.
20231101.sw_1676_2
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kenya
Kenya
Kenya ni nchi ya 47 kwa ukubwa duniani ikifuata mara Madagaska ikiwa na eneo la kilomita mraba 580,367 (maili mraba 224,081).
20231101.sw_1676_3
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kenya
Kenya
Kutoka pwani ya Bahari ya Hindi, nyanda za chini zimeinuka hadi milima ya kati. Milima hii imetenganishwa na eneo la Bonde la Ufa; sehemu tambarare yenye rutuba upande wa mashariki. Milima ya Kenya ni kati ya iliyofaulu kwa kilimo barani Afrika.
20231101.sw_1676_4
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kenya
Kenya
Eneo hili la milima ndilo la juu zaidi nchini Kenya (na la pili kwa urefu barani Afrika): Mlima Kenya, unaofikia urefu wa mita 5,199 (futi 17,0570) na ni eneo lenye mito ya barafu.
20231101.sw_1676_5
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kenya
Kenya
Kusini mashariki milima ya Taita ndiyo mwanzo wa tao la Mashariki, safu za milima zenye miaka zaidi ya milioni 100 ambazo zinaenea hasa nchini Tanzania.
20231101.sw_1676_6
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kenya
Kenya
Upande huohuo wa kusini Mlima Kilimanjaro () huweza kuonekana ukiwa ng'ambo ya mpaka wa Kenya na Tanzania.
20231101.sw_1676_7
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kenya
Kenya
Kenya ni nchi yenye jua kali na nguo za majira ya joto huvaliwa mwaka mzima. Hata hivyo, huwa na baridi usiku na pia asubuhi na mapema.
20231101.sw_1676_8
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kenya
Kenya
Hali ya hewa ina joto na unyevu sehemu za pwani, joto kiasi sehemu za bara na ni kame katika sehemu za kaskazini na kaskazini-mashariki mwa nchi. Hata hivyo kuna mvua nyingi kati ya Machi na Aprili, na mvua ya kadiri kati ya Oktoba na Novemba. Halijoto huwa juu zaidi miezi hii yote.
20231101.sw_1676_9
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kenya
Kenya
Mvua ya masika hunyesha kuanzia Aprili hadi Juni. Mvua ya vuli nayo hunyesha kuanzia Oktoba hadi Desemba. Wakati mwingine mvua hii huwa nyingi na aghalabu hunyesha wakati wa alasiri na jioni. Majira ya joto jingi ni kuanzia Februari hadi Machi nayo ya baridi ni Julai hadi Agosti.
20231101.sw_1676_10
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kenya
Kenya
Kenya ina maeneo makubwa wanapoishi wanyamapori likiwemo Masai Mara, ambapo nyumbu na wanyama wengi walanyasi hushiriki katika uhamaji kila mwaka. Uhamaji huo, hasa uhamaji wa nyumbu, hutokea Juni hadi Septemba na hushirikisha mamilioni ya wanyama. Tukio hili huwavutia sana wapigaji picha za sinema. Takribani nyumbu 250,000 huangamia kila mwaka katika uhamaji huu wa kutafuta lishe wakati wa kiangazi.
20231101.sw_1676_11
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kenya
Kenya
Wale wanyama wakubwa watano wa Afrika wanapatikana Kenya: simba, chui, nyati, kifaru na ndovu. Wanyama wengine wengi wa pori na ndege hupatikana katika mbuga za taifa na hifadhi za wanyama hawa nchini.
20231101.sw_1676_12
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kenya
Kenya
Mabaki ya mamba mkubwa ajabu wa zamani za Mesozoic Era, ambayo ni miaka milioni 200 iliyopita, yaligunduliwa nchini Kenya katika chimbo zilizochimbwa na wataalamu kutoka Chuo Kikuu cha Utah na Makavazi ya Kitaifa nchini Kenya miezi ya Julai hadi Agosti 2004 katika bonde la Lokitaung, karibu na Ziwa Turkana.
20231101.sw_1676_13
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kenya
Kenya
Mabaki yaliyopatikana Afrika Mashariki yaonyesha kuwa miaka milioni 20 iliyopita viumbehai mfano wa sokwe waliishi eneo hili. Uchunguzi wa juzijuzi karibu na Ziwa Turkana waonyesha kuwa viumbe aina ya Homo habilis (walioishi miaka milioni 1.8 na 2.5 iliyopita) na Homo erectus (walioishi miaka milioni 1.8 na miaka 350,000 iliyopita) huenda ndio wazazi wa watu wa kisasa homo sapiens walioishi Kenya enzi za barafu kuu kuisha barani.
20231101.sw_1676_14
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kenya
Kenya
Katika mwaka wa 1984, uvumbuzi uliofanywa na mtafiti maarufu Richard Leakey na Kamoya Kimeu huko Ziwa Turkana ulikuwa wa mifupa ya mvulana iliyohusishwa na Homo erectus wa miaka milioni 1.6 iliyopita. Utafiti wa awali wa viumbe hawa unahusishwa na Mary Leakey na Louis Leakey, ambao ndio waliofanya uchunguzi wa mwanzo wa kiakiolojia huko Olorgesailie na Hyrax Hill. Baadaye utafiti wa Olorgesailie uliendelezwa na Glynn Isaac.
20231101.sw_1676_15
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kenya
Kenya
Wakazi wa kwanza wa eneo linaloitwa Kenya walikuwa wa jamii ya Wakhoisan: hadi leo kuna makabila matatu madogo yenye asili hiyo, ingawa yanatumia lugha za Kikushi: Waata, Waawer na Wadahalo.
20231101.sw_1676_16
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kenya
Kenya
Wakushi kutoka kaskazini waliingia Kenya kati ya miaka ya 3200 KK na 1300 KK. Mwaka 500 KK hivi wazungumzaji wa lugha za Kinilo-Sahara na katika milenia ya kwanza KK wale wa lugha za Kibantu waliingia katika eneo hili, na sasa Waniloti ni 30% ya Wakenya wote.
20231101.sw_1676_17
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kenya
Kenya
Wafanyabiashara Waarabu walianza kufika pwani ya Kenya karne ya 1 BK. Ukaribu wa Kenya na Uarabuni ulirahisisha ukoloni, hivyo Waarabu na Waajemi walianza kuishi eneo la pwani karne ya 8. Hata hivyo, baadhi ya walioitwa "Waarabu" katika eneo la Afrika Mashariki walikuwa machotara, Waafrika-Waarabu.
20231101.sw_1676_18
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kenya
Kenya
Pwani ya Kenya imekuwa makao ya jamii ya wahunzi na jamii ya wakulima wadogowadogo, wawindaji na wavuvi ambao walikuwa mhimili wa uchumi kwa kushiriki katika kilimo, uvuvi, utengenezaji chuma, na biashara na nchi za kigeni.
20231101.sw_1676_19
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kenya
Kenya
Kuanzia karne ya 6 au karne ya 9, Kenya ilijihusisha na shughuli za ubaharia kukuza uchumi ikaanza kutengeneza meli za kuabiria kusini hadi miji mingine yenye bandari kama Kilwa na Shanga iliyo katika pwani ya Afrika Mashariki.
20231101.sw_1676_20
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kenya
Kenya
Mombasa ulikuwa mji wenye bandari wa nchi ya Kenya katika karne za kati. Bandari hiyo ilitumika kuendeleza biashara na miji mingine yenye bandari Afrika, Uajemi, na wafanyabiashara Waarabu, Yemeni na hata Bara Hindi.
20231101.sw_1676_21
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kenya
Kenya
Baharia Mreno Duarte Barbosa wa karne ya 15 alidai kuwa "[Mombasa] ni bandari nzuri na yenye shughuli nyingi, mashua nyingi na hata meli kubwa ajabu, ambazo zote hutoka Sofala na nyingine kutoka Cambay, Melinde na nyingine zinazoabiri hadi kisiwani Unguja."
20231101.sw_1676_22
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kenya
Kenya
Karne kadhaa kabla ya ukoloni, upwa wa Kenya wanakoishi Waswahili ulikuwa sehemu ya eneo la mashariki mwa Afrika lililofanya biashara, hasa ya watumwa na pembe za ndovu na Waarabu na Wahindi. Inasemekana kwamba kabila la Wameru lilitokana na watumwa waliotoroka utumwa Uarabuni miaka ya 1700. Mwanzoni wafanyabiashara wengi walitokea milki za Uarabuni lakini baadaye wengine wakatokea Unguja (kama Tippu Tip).
20231101.sw_1676_23
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kenya
Kenya
Kiswahili, ambacho ni lugha ya Kibantu iliyokopa misamiati ya Kiarabu, Kiajemi na mingine kutoka Mashariki ya Kati na Asia Kusini, baadaye ilikua ikawa lingua franca ya biashara kwa jamii mbalimbali.
20231101.sw_1676_24
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kenya
Kenya
Kwa karne nyingi, upwa wa Kenya umekuwa mwenyeji wa wafanyabiashara na wasafiri. Kati ya miji iliyopo kwenye upwa wa Kenya , mji wa Malindi umebakia kuwa makazi muhimu ya Waswahili tangu karne ya 14 na wakati mmoja ulishindana na Mombasa kwa ukuu pande hizi za Afrika Mashariki. Kwa kawaida, Malindi umekuwa mji na bandari ya kirafiki kwa serikali nyingine. Mwaka wa 1414, Sultani Mwarabu wa Malindi alianzisha uhusiano wa kidiplomasia na utawala wa Uchina wa Ming, wakati wa safari za mchunguzi Zheng He. Katika mwaka wa 1498, utawala wa Malindi ulimkaribisha msafiri na mvumbuzi maarufu kutoka Ureno, Vasco da Gama.
20231101.sw_1676_25
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kenya
Kenya
Wareno walikuwa Wazungu wa kwanza kuzuru eneo la Kenya ya sasa: Vasco da Gama alikuwa amezuru Mombasa mwaka wa 1498. Safari ya Vasco da Gama ilifaulu alipofikia huko India, na jambo hilo liliwawezesha Wareno kufanya biashara moja kwa moja na Mashariki ya Mbali kupitia bahari na hivyo kutatiza mitandao ya kibiashara ya awali ya nchi kavu na baharini kama njia za biashara ya viungo zilizotumia Ghuba la Uajemi, Bahari Nyekundu na misafara iliyofika hadi eneo la mashariki ya Mediterranea.
20231101.sw_1676_26
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kenya
Kenya
Jamhuri ya Venisi ndiyo iliyotawala maeneo ya biashara kati ta Uropa na Asia. Baada ya njia za kawaida za nchi kavu hadi India kufungwa na Waturuki wa Ottoman, Ureno ulitarajiwa kutumia njia ya baharini iliyotumiwa kwanza na Vasco da Ghama ili kuvunja ukiritimba wa Venice.
20231101.sw_1676_27
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kenya
Kenya
Utawala wa Wareno huko Afrika Mashariki ulijihusisha hasa na pwani iliyokaribia Mombasa. Kuwepo kwa Wareno Afrika Mashariki kulianza rasmi baada ya mwaka wa 1505, wakati manowari za Wareno, zikiongozwa na Don Francisco de Almeida, zilipokishinda Kilwa, kisiwa kilicho katika eneo ambalo sasa ni Tanzania kusini.
20231101.sw_1676_28
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kenya
Kenya
Kuwepo kwa Wareno Afrika Mashariki kuliwawezesha kudhibiti biashara katika Bahari ya Hindi, na kulinda njia za baharini zinazounganisha Uropa na Asia. Manowari zao za kivita zilikwamisha biashara za maadui wao magharibi mwa Bahari ya Hindi na walitoza kodi juu ya bidhaa zilizosafirishwa kupitia eneo hilo kwani walitawala bandari zote na njia kuu za meli.
20231101.sw_1676_29
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kenya
Kenya
Kujengwa kwa ngome iliyoitwa Fort Jesus Mombasa mwaka wa 1593 kulikusudiwa kuimarisha utawala wao katika eneo hilo, lakini ushawishi wao ulikatizwa na kuja kwa Waingereza, Waholanzi na Waarabu wa Omani katika eneo hilo karne ya 17.
20231101.sw_1676_30
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kenya
Kenya
Waarabu kutoka Omani ndio waliokuwa tishio kuu la utawala wa Wareno Afrika Mashariki na waliizingira ngome ya Wareno, wakazishambulia meli zao za kivita, kisha kuwafukuza Wareno waliobaki kutoka pwani ya Kenya na Tanzania mwaka wa 1730. Kufikia wakati huo, ufalme wa Ureno haukuwa na haja na njia ya bahari ya biashara ya viungo kwani faida yake ilikuwa imepungua sana. Utawala wa Wareno ulibakia tu katika bandari na maeneo ya kusini mwa Msumbiji hadi mwaka wa 1975.
20231101.sw_1676_31
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kenya
Kenya
Kutawaliwa kwa pwani ya Kenya na Tanzania na Waarabu kutoka Omani kuliifanya miji hii iliyojitawala hapo awali iwe chini ya uangalifu mkali wa wageni kuliko ilivyokuwa katika enzi za utawala wa Wareno. Waarabu wa Omani, kama Wareno waliowatangulia, waliweza kutawala eneo la pwani tu, si eneo la bara. Hata hivyo, kuanzishwa kwa mashamba makubwa ya mikarafuu, kuongezeka kwa biashara ya utumwa na kuhamishwa kwa makao makuu ya Waomani hadi Zanzibar mwaka wa 1839 na Seyyid Said kulisababisha Waomani kuimarisha utawala wao katika eneo hilo.
20231101.sw_1676_32
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kenya
Kenya
Utawala wa Waarabu katika bandari kuu zote za pwani ya Afrika Mashariki uliendelea hadi Uingereza ilipoamua kumaliza biashara ya utumwa na uanzishaji wa utaratibu wa kufanya kazi kwa malipo ukaanza kushinikiza utawala wa Waomani.
20231101.sw_1676_33
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kenya
Kenya
Kufikia mwisho wa karne ya 19, biashara ya watumwa katika bahari zote kuu ilikuwa imeharamishwa na Waingereza: Waarabu wa Omani hawakuwa na uwezo wa kupingana na jeshi la wanamaji la Uingereza lililokuwa likitekeleza amri hiyo. Waomani waliendelea kuwepo visiwani Unguja na Pemba hadi mapinduzi ya mwaka wa 1964, lakini kuwepo kwa Waarabu wa Omani nchini Kenya rasmi kulisitishwa wakati Wajerumani na Waingereza walipozidhibiti bandari zote kuu na kuanzisha mahusiano ya kibiashara na viongozi mashuhuri waliokuwa wenyeji miaka ya 1880. Hata hivyo, urithi waliouacha Afrika Mashariki ungali unaonekana kupitia kwa vizazi vyao vipatikanavyo pwani ya Kenya na ambavyo vinaona kuwa asili yao ni Oman. Vizazi hivi hata leo humiliki utajiri mwingi na ndio wenye ushawishi mkubwa wa kisiasa katika jamii za pwani ya Kenya.
20231101.sw_1676_34
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kenya
Kenya
Hata hivyo, wanahistoria wengi hushikilia kuwa historia ya ukoloni nchini Kenya ilianza wakati Wajerumani walipoanza kutawala mali ya Sultani wa Unguja iliyo pwani mwaka wa 1885, ikifuatwa na kuja kwa kampuni ya Imperial British East Africa Company mwaka wa 1888.
20231101.sw_1676_35
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kenya
Kenya
Uhasama wa kwanza baina ya mabepari ulikatizwa wakati Ujerumani ulipouachia Uingereza sehemu ya pwani iliyomiliki. Hii ilifuatia kujengwa kwa reli iliyounganisha Kenya na Uganda. Baadhi ya makabila ya Kenya yalipinga ujenzi huo, hasa Wanandi wakiongozwa na Orkoiyot Koitalel Arap Samoei kwa miaka kumi, kuanzia 1895 hadi 1905 – lakini hatimaye Waingereza waliijenga reli hii.
20231101.sw_1676_36
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kenya
Kenya
Inaaminika kuwa Wanandi walikuwa kabila la kwanza kuwekwa kwenye maeneo yaliyotengewa Waafrika ili kuwazuia kutatiza ujenzi wa reli. Wakati huo Wahindi wengi wenye ujuzi waliingia nchini ili kuchangia ujenzi. Wakati wa ujenzi wa reli kupitia Hifadhi ya Taifa ya Tsavo Magharibi, Wahindi wengi na wenyeji Waafrika walivamiwa na simba wawili waliojulikana kama “wala watu wa Tsavo”. Wahindi hao na vizazi vyao baadaye walibakia nchini Kenya na kuunda kitovu cha jamii za Wahindi zijulikanayo kama Ismaili Muslim na Sikh.
20231101.sw_1676_37
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kenya
Kenya
Mnamo Agosti 1914, Vita vya Kwanza vya Dunia vilipoanza, magavana wa British East Africa (kama eneo hilo lilivyojulikana) na German East Africa walifikia makubaliano ili kuepusha makoloni yao machanga na uhasama. Hata hivyo, Luteni Kanali Paul von Lettow-Vorbeck alichukua mamlaka ya majeshi ya Ujerumani, akiwa na kusudi la kutwaa raslimali nyingi iwezekanavyo za Uingereza. Jeshi la Uingereza likiwa limemtenga na Ujerumani, von Lettow aliendesha kampeni iliyofaulu ya vita vya kuvizia, wakila walichopata, wakiteka bidhaa za matumizi za Uingereza, na kuepuka kushindwa. Mwishowe alisalimu amri na akajisalimisha nchini Zambia siku kumi na moja baada ya mapatano ya kusimamisha vita kutiwa sahihi mwaka wa 1918. Waingereza walitumia jeshi la Wahindi kumfukuza Lettow na walihitaji wachukuzi wengi ili kubeba vifaa vya matumizi hadi bara kwa miguu na hivyo kutatua shida kuu ya uchukuzi. Kundi la wanajeshi wachukuzi liliundwa na kuwajumuisha Waafrika 400,000, na kuchangia katika uhamasishaji wao wa muda mrefu kisiasa.
20231101.sw_1676_38
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kenya
Kenya
Hadi mwaka wa 1920, eneo linaloitwa Kenya lilijulikana kama Himaya ya Uingereza ya Afrika Mashariki. Mwaka huo, koloni la Kenya liliundwa na kupatiwa jina linalotokana na Mlima KenyaWaingereza walilitamka jina hilo kama ingawa matamshi ya wenyeji na yaliyokusudiwa katika maendelezo asili, Kenia yalikuwa ˈkɛnja. Enzi ya Jomo Kenyatta kuwa rais wa Kenya miaka ya 1960-1969, matamshi ya Kiingereza, yaani yalikubalika na kutumiwa sana kwa sababu jina lake lilidumisha matamshi asilia ya wenyeji. Kumbe saa ya uhuru, mwaka 1963, Jomo Kenyatta alichaguliwa kama rais wa kwanza. Awali alikuwa alishika jina hili kutafakari ahadi yake ya kuikomboa nchi yake na matamshi yake ya jina lake ulisababisha katika matamshi ya Kenya katika Kiingereza kubadilisha nyuma ya makadirio ya awali uliotokea matamshi,
20231101.sw_1676_39
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kenya
Kenya
Mwanzoni mwa karne ya 20, wakulima Waingereza na Wazungu wengine walituama katika nyanda za juu katika eneo la kati walikoondokea kuwa matajiri kwa kulima kahawa na chai. Kufikia mwaka 1930, takribani walowezi 30,000 waliishi katika maeneo hayo na walikuwa na ushawishi mkubwa wa kisiasa kwa sababu ya uwezo wao wa kiuchumi.
20231101.sw_1676_40
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kenya
Kenya
Maeneo hayo yalikuwa makao ya watu milioni moja wa kabila la Wakikuyu, na wengi wao hawakuwa na ithibati ya kumiliki mashamba kwa mujibu wa Waingereza (ingawa mashamba hayo yalimilikiwa na kabila hilo kabla ya Wazungu kufika), na waliishi kama wakulima wanaohamahama. Ili kuendeleza matakwa yao, walowezi waliwakataza kilimo cha kahawa na kuwalazimisha kulipa kodi ya nyumba, na maskwota walipewa mashamba madogo baada ya kuwafanyia kazi. Wakikuyu wengi walihamia mijini kwani mashamba yao hayangeweza kutosheleza mahitaji yao.
20231101.sw_1676_41
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kenya
Kenya
Mwaka wa 1951, Horace Hector Hearne akawa mkuu wa sheria nchini Kenya (alitoka Ceylon alikoshikilia wadhifa huohuo) na alifanya kazi katika Mahakama Kuu mjini Nairobi. Alihudumu katika wadhifa huo hadi mwaka 1954 alipoteuliwa kama Hakimu wa Rufaa katika Mahakama ya Rufaa ya Afrika Magharibi. Usiku wa tarehe 5 Februari 1952, wakati Mfalme George VI alipoaga dunia, Hearne alimsindikiza Malkia Elizabeth II na mumewe Filipo mwanamfalme wa Edinburgh, kwa dhifa ya kitaifa hotelini Treetops, ambayo sasa ni kivutio maarufu cha watalii. Hapa ndipo alipouanzia umalkia. Alirudi Uingereza mara moja akiandamana na Hearne.
20231101.sw_1676_42
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kenya
Kenya
Kuanzia Oktoba 1952 mpaka Desemba 1959, Kenya ilikuwa katika hali ya hatari kufuatia uasi wa Mau Mau dhidi ya utawala wa Uingereza. Gavana aliomba na kupata msaada wa wanajeshi Waingereza na Waafrika, pamoja na King's African Rifles. Mnamo Januari 1953, Meja Jenerali Hinde aliteuliwa kuwa mkuu wa oparesheni ya kuzima uasi. Hali hii haikuimarika kwa kukosa uchunguzi, kwa hivyo Jenerali George Erskine aliteuliwa kuwa kamanda msimamizi wa majeshi ya kikoloni mnamo Mei 1953, akiungwa mkono hasa na Winston Churchill.