_id
stringlengths 15
22
| url
stringlengths 31
150
| title
stringlengths 1
86
| text
stringlengths 100
23.8k
|
---|---|---|---|
20231101.sw_1751_0
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kilimanjaro%20%28Volkeno%29
|
Kilimanjaro (Volkeno)
|
Kilimanjaro ni jina la mlima mrefu kuliko yote barani Afrika. Mlima huo uko nchini Tanzania katika Mkoa wa Kilimanjaro. Una urefu wa mita 5,895 (futi 19,340).
|
20231101.sw_1751_1
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kilimanjaro%20%28Volkeno%29
|
Kilimanjaro (Volkeno)
|
Hali halisi Kilimanjaro ni zaidi ya mlima tu, ni kama safu ndogo ya milima mitatu: Kibo, Mawenzi na Shira. Hiyo mitatu inaonekana kama vilele vitatu vya mlima mmoja, hivyo si vibaya kusema Kilimanjaro ni mlima.
|
20231101.sw_1751_2
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kilimanjaro%20%28Volkeno%29
|
Kilimanjaro (Volkeno)
|
Kijiolojia Kilimanjaro ni volkeno iliyolala kwa sasa. Kwenye kilele cha Kibo gesi bado inatoka. Kumbukumbu ya wenyeji ina habari ya mlipuko mnamo mwaka 1730.
|
20231101.sw_1751_3
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kilimanjaro%20%28Volkeno%29
|
Kilimanjaro (Volkeno)
|
Kilele cha juu cha Kibo kinaitwa Uhuru. Mtu wa kwanza kufika kileleni hapo alikuwa Johannes Kinyala Lauwo kutoka Marangu aliyewaongoza Wajerumani Hans Meyer na Ludwig Purtscheller tarehe 6 Oktoba 1889 wakati wa ukoloni wa Ujerumani. Wakati ule waliita ncha ya juu "Kaiser-Wilhelm-Spitze" (kwa Kijerumani: Kilele cha Kaisari Wilhelm) kwa heshima ya Kaisari wa Ujerumani.
|
20231101.sw_1751_4
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kilimanjaro%20%28Volkeno%29
|
Kilimanjaro (Volkeno)
|
Asili ya jina "Kilimanjaro" haijulikani kikamilifu. Vyanzo vya kimaandishi vinajulikana tangu takriban mwaka 1860 ambapo wapelelezi Wazungu walitumia jina hilo katika taarifa zao wakidai "Kilimanjaro" ni jina la Kiswahili. Pamoja na umbo hili kulikuwa pia na tahajia ya sehemu mbili ama "Kilima-Njaro" au kwa namna ya Kijerumani “Kilima-Ndscharo”.
|
20231101.sw_1751_5
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kilimanjaro%20%28Volkeno%29
|
Kilimanjaro (Volkeno)
|
Johann Ludwig Krapf aliandika mnamo 1860 kuwa Waswahili kwenye pwani waliita mlima huo "Kilimanjaro". Alisema pia ya kwamba hao Waswahili walieleza maana yake kuwa ama “mlima mkubwa” au “mlima wa misafara” ingawa mwenyewe hakukubali maelezo hayo. Kwa elezo la mwisho "Kilima" kilimaanisha "mlima" na "Jaro" labda "misafara".
|
20231101.sw_1751_6
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kilimanjaro%20%28Volkeno%29
|
Kilimanjaro (Volkeno)
|
Jim Thompson aliandika mnamo 1885 kuwa jina Kilima-Njaro lilichukuliwa mara nyingi kuwa na maana ya "mlima mkubwa" lakini mwenyewe alipendelea maelezo tofauti yaliyosema "mlima mweupe". "Njaro" ni Kiswahili cha Zamani kwa "ng’ara".
|
20231101.sw_1751_7
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kilimanjaro%20%28Volkeno%29
|
Kilimanjaro (Volkeno)
|
Vivyo hivyo Krapf aliandika ya kwamba aliwahi kuwatembela Wakamba mnamo 1849 walioita mlima “Kima jaJeu” yaani mlima mweupe Leo hii Wakamba wangesema “Kiima Kyeu” na elezo hili limekubaliwa na watafiti mbalimbali.
|
20231101.sw_1751_8
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kilimanjaro%20%28Volkeno%29
|
Kilimanjaro (Volkeno)
|
Wengine wamejaribu kuona msingi wa jina katika lugha ya Kichagga. Hapo wanadai uwezekano kuwa "Kileman" limetokana na neno la Kichagga "kileme" linalomaanisha “kinachoshinda” au neno "kilelema" linalomaanisha "kilichokuwa vigumu, kilichoshindikana". Katika hoja hiyo "Jaro" imetokana na Kichagga “njaare” (aina ya ndege, au kufuatana na wengine chui) au kutoka neno “jyaro” (msafara). Elezo lingine ni kwamba Wachagga walisema mlima huo hauwezi kupandwa "kilemanjaare" au "kilemajyaro" na wapagazi au wafasiri kutoka pwani waliichukua kuwa jina la mlima na kutafsiri vile kwa Wazungu.
|
20231101.sw_1751_9
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kilimanjaro%20%28Volkeno%29
|
Kilimanjaro (Volkeno)
|
Tangu miaka ya 1880 mlima umekuwa sehemu ya Afrika ya Mashariki ya Kijerumani ukaitwa "Kilima-Ndscharo" kwa Kijerumani.
|
20231101.sw_1751_10
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kilimanjaro%20%28Volkeno%29
|
Kilimanjaro (Volkeno)
|
Tarehe 6 Oktoba 1889 Hans Meyer alikuwa mtu wa kwanza anayejulikana kupanda mlima na kufika hadi kilele cha Kibo. Alichagua jina la "Kaiser-Wilhelm-Spitze" ("Ncha ya Kaisari Wilhelm").
|
20231101.sw_1751_11
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kilimanjaro%20%28Volkeno%29
|
Kilimanjaro (Volkeno)
|
Jina hilo lilitumika hadi Tanzania ilipoundwa mwaka 1964, na kilele kubadilishiwa jina kuwa "Uhuru", likiwa na maana ya "Kilele cha Uhuru"
|
20231101.sw_1751_12
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kilimanjaro%20%28Volkeno%29
|
Kilimanjaro (Volkeno)
|
Kilimanjaro inapanda hadi mita 4877 juu ya tambarare karibu na mji wa Moshi uliopo miguuni pake. Hii inafanya kilele chake kuwa mita 5895 juu ya uwiano wa bahari.
|
20231101.sw_1751_13
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kilimanjaro%20%28Volkeno%29
|
Kilimanjaro (Volkeno)
|
Kilimanjaro ni volkeno ya rusu iliyojengwa na rusu za majivu, zaha na mata nyingine. Ni volkeno ndefu kuliko zote duniani nje ya Amerika Kusini.
|
20231101.sw_1751_14
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kilimanjaro%20%28Volkeno%29
|
Kilimanjaro (Volkeno)
|
Uhuru ni sehemu ya juu kwenye ukingo wa kasoko ya Kibo. Taasisi ya Tanzania National Parks Authority na UNESCO zinataja kimo cha Uhuru Peak kuwa mita 5895. Kimo hicho kimetokana na upimaji uliofanyika wakati wa ukoloni wa Uingereza mwaka 1952. Tangu upimaji ule kimo cha mlima kimepimwa tena: kinaonyesha kuwa mlima unapungua polepole. Kipimo kilikuwa mita 5892 mwaka 1999 na mita 5891 mwaka 2014.
|
20231101.sw_1751_15
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kilimanjaro%20%28Volkeno%29
|
Kilimanjaro (Volkeno)
|
Muundo wa ndani wa Kilimanjaro haujulikani sana kwa sababu hadi sasa haujatokea mmomonyoko mkubwa unaoweza kufunua ndani yake.
|
20231101.sw_1751_16
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kilimanjaro%20%28Volkeno%29
|
Kilimanjaro (Volkeno)
|
Kilele cha kale zaidi ni Shira iliyoanza kutema moto takriban miaka milioni 2.5 iliyopita ikaacha miaka milioni 1.9 iliyopita. Wakati ule upande wa kaskazini wa mzingo wa kasoko ulipinduka. Leo hii Shira ina tambarare pana kwenye kilele chake kwenye kimo cha mita 3800; inawezekana hii kiasili ilikuwa kaldera iliyojaa lava. Mabaki ya mzingo wa kaldera yamepungua sana kutokana na mmomonyoko. Kabla ya kutoa moto na kutokea kwa mmomonyoko kimo cha Shira kilikuwa kati ya mita 4,900 na 5,200. Mata yake ni hasa lava pamoja na kiasi cha piroklasti.
|
20231101.sw_1751_17
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kilimanjaro%20%28Volkeno%29
|
Kilimanjaro (Volkeno)
|
Mawenzi na Kibo zilianza kulipuka (kutoa moto) takriban miaka milioni iliyopita. Zimetengwa na tambarare ( "Saddle Plateau") kwenye kimo cha mita 4400.
|
20231101.sw_1751_18
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kilimanjaro%20%28Volkeno%29
|
Kilimanjaro (Volkeno)
|
Miamba ya kijana kwenye Mawenzi ilitokea miaka 448,000 iliyopita. Mawenzi huwa na mgongo wenye umbo la kiatu cha farasi mwenye ncha kali na kufunguka upande wa kaskazini-magharibi. Mgongo unakatwa na mabonde kadhaa na upande wa mashariki wa mlima umepungua kutokana na mmomonyoko. Mawenzi huwa na kilele cha pili kinachojulikana kwa jina la “Neumann Tower” chenye mita 4425.
|
20231101.sw_1751_19
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kilimanjaro%20%28Volkeno%29
|
Kilimanjaro (Volkeno)
|
Kibo ni pia ya kivolkeno yenye kimo kirefu ikiwa na upana wa kilomita 15 kwenye "Saddle Plateau". Ililipuka mara ya mwisho miaka 150,000 na 200,000 iliyopita na mlipuko huo ulifanya kasoko kwenye kilele cha Kibo cha sasa. Hadi leo gesi inatoka kwenye mashimo ardhini. Kibo huwa na pia kwenye kilele chake chenye umbo kamili. Kuna kaldera yenye upana wa kilomita 2.5 na ndani yake pia iko kasoko ya Reusch. Jina hilo lilitolewa na serikali ya Tanganyika mwaka 1954 kwa heshima ya Mjerumani Gustav Otto Richard Reusch alipopanda mlima mara ya 25. Ndani ya kasoko ya Reusch kuna shimo refu linalojulikana kwa jina la “ash pit” (shimo la majivu). Wakati wa mlipuko wa mwisho uliotokea miaka 100,000 iliyopita sehemu za mzingo wa kasoko ziliporomoka na kuacha pengo kubwa.
|
20231101.sw_1751_20
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kilimanjaro%20%28Volkeno%29
|
Kilimanjaro (Volkeno)
|
Kibo huwa na pia za kando zaidi ya 250 ambazo ni mashimo ambako gesi, zaha na piroklasti zilitoka kwenye pande za mlima wakati wa kuwa volkeno hai. Zilitokea miaka 150,000 hadi 200,000 iliyopita . Zinapatikana hadi Ziwa Chala na Taveta upande wa kusini-mashariki na hadi Lengurumani upande wa kaskazini-magharibi. Zaha iliyotoka katika pia hizo za kando ilifunika sehemu kubwa ya pande za mlima.
|
20231101.sw_1751_21
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kilimanjaro%20%28Volkeno%29
|
Kilimanjaro (Volkeno)
|
Wamaasai wana kumbukumbu ya kuwa Ziwa Chala upande wa mashariki wa Kibo lilikuwa mahali pa kijiji kimoja kilichoharibika na mlipuko wa volkeno.
|
20231101.sw_1751_22
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kilimanjaro%20%28Volkeno%29
|
Kilimanjaro (Volkeno)
|
Maji yatoka mlimani kwa njia ya mito na vijito hasa upande wa kusini unaopokea mvua zaidi hasa juu ya mita 1200. Chini ya kimo hicho maji kwenye mito inapungua kutokana na mvukizo na matumizi ya binadamu. Mito ya Lumi na Pangani inabeba maji ya Kilimanjaro kuelekea mashariki na kusini.
|
20231101.sw_1751_23
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kilimanjaro%20%28Volkeno%29
|
Kilimanjaro (Volkeno)
|
Tabianchi ya Kilimanjaro inaathiriwa na kimo cha mlima kinachoruhusu kufika kwa upepo kutoka bahari wenye unyevu mwingi na wakati mmoja pia upepo za juu sana. Tabia nyingine ni hali yake ya kuwa mlima wa juu sana peke yake bila jirani ya karibu sana. Mlima huwa na mfumo wa upepo ambako mchana upepo unaelekea juu na wakati wa usiku kuna upepo unaotelemka kutoka juu. Hii inatokea zaidi upande wa kusini kuliko upande wa kaskazini kwa sababu tako la mlima ni pana zaidi upande wa kusini na mitelemko yake inaelekea zaidi hivyo kuathiri tabianchi zaidi. .
|
20231101.sw_1751_24
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kilimanjaro%20%28Volkeno%29
|
Kilimanjaro (Volkeno)
|
Kilimanjaro huwa na majira mawili ya mvua, moja ya Machi hadi Mei na nyingine mnamo mwezi wa Novemba. Mitelemko ya kaskazini hupokea mvua chache kulingana na mitelemko ya kusini.
|
20231101.sw_1751_25
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kilimanjaro%20%28Volkeno%29
|
Kilimanjaro (Volkeno)
|
Sehemu za chini za mtelemko wa kusini hupokea milimita za mvua 800 – 900 kwa mwaka. Kiwango hiki kinaongezeka kwa milimita 1,500 hadi 2,000 kwenye kimo cha mita 1,500 na hadi juu ya milimita 3,000 kwenye ukanda wa msitu kwa mita 2,000 hadi 2,300. Juu zaidi usimbishaji unapungua tena hadi milimita 200.
|
20231101.sw_1751_26
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kilimanjaro%20%28Volkeno%29
|
Kilimanjaro (Volkeno)
|
Halijoto kwenye kilele ina wastani ya sentigredi -7 yaani jalidi. Halijoto juu ya ngao ya barafu upande wa kaskazini wakati wa usiku huwa na wastani wa sentigredi -9 na wakati wa mchana -4. Viwango vya chini vya -15 hadi -27 vimepimiwa pia.
|
20231101.sw_1751_27
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kilimanjaro%20%28Volkeno%29
|
Kilimanjaro (Volkeno)
|
Usimbishaji wa theluji unaweza kutokea wakati wowote lakini kwa kawaida hutokea Zaidi wakati wa majira ya mvua. (Novemba–Desemba na Machi–Mei). Usimbishaji wote kwenye kilele ni hasa theluji au mchnganyiko wa tehluji na mvua kwenye kiwango cha milimita 250 hadi 500 kwa mwaka na kuvukiza haraka.
|
20231101.sw_1751_28
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kilimanjaro%20%28Volkeno%29
|
Kilimanjaro (Volkeno)
|
Mlima Kilimanjaro hujulikana kuwa kuwa ni mlima wa Afrika mwenye kofia ya barafu ya kudumu. Pamoja na Kilimanjaro kuna sehemu mbili nyingine tu barani Afrika, ni Ruwenzori na Mlima Kenya. Lakini kiasi cha barafu imepungua kwa kipindi cha zaidi ya miaka 100. Mwingereza P.C. Spink aliona mwaka 1944 ya kwamba barafu ilipungua sana kulingana na taarifa aliyojua kutoka mpandaji wa kwanza Hans Meyer. Baina 1912 eneo la ngao ya barafu limepungua kutoka kilomita za mraba 12 hadi 1.85 km² kwenye mwaka 2009. Hii inalingana na kupunguzwa asilimia 85%. Sababu kuu ya mabadiliko haya ni kupungukiwa kwa kiwango cha usimbishaji katika mazingira ya mlima tangu mwisho wa karne ya 19.
|
20231101.sw_1751_29
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kilimanjaro%20%28Volkeno%29
|
Kilimanjaro (Volkeno)
|
Maana Kilimanjaro ni mlima wa juu vile ya kwamba mvua wote (pamoja na ukungu na usimbishaji mwingine) unaofika kwenye kilele chake utaganda na kuwa theluji. Theluji inayokaa muda mrefu tena katika ganda nene itakuwa barafu. Lakini wakati uleule mishale ya jua zinasababisha kupotea kwa theluji na barafu kwa njia ya uvukizaji. Kwa jumla kuongezeka au kupungukiwa kwa barafu kwenye kimo hiki ni swali la kiasi cha mvua na usimbishaji mwingine zinazofika hapa.
|
20231101.sw_1751_30
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kilimanjaro%20%28Volkeno%29
|
Kilimanjaro (Volkeno)
|
Leo hii kuna barafuto kwenye Kibo pekee pamoja na mabaki ya ngao ya barafu kwenye tambarare ya kilele na kwenye mitelemko ya Kibo.
|
20231101.sw_1751_31
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kilimanjaro%20%28Volkeno%29
|
Kilimanjaro (Volkeno)
|
Hii ngao ya barafu bado iko kwa sababu Kilimanjaro ni mlima usio na vilele vikali unaofika juu ya kimo cha mstari wa jeledi. Kasoko ya Kibo imepita na kukata ngao hiyo.
|
20231101.sw_1751_32
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kilimanjaro%20%28Volkeno%29
|
Kilimanjaro (Volkeno)
|
Siku hizi hakuna miendo ya maana inayoonekana kwenye barafuto za kilele kwa sababu unene wao imepungua mno..
|
20231101.sw_1751_33
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kilimanjaro%20%28Volkeno%29
|
Kilimanjaro (Volkeno)
|
Utafiti wa kijiolojia umeonyesha ya kwamba kulikuwa na vipindi vitano vya upanuzi wa barafuto katika miaka 500,000 iliyopita vilivyofuatwa na vipindi vya kupungua.
|
20231101.sw_1751_34
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kilimanjaro%20%28Volkeno%29
|
Kilimanjaro (Volkeno)
|
Ngao ya barafu mfululizo ilifunika mlima wote hadi kimo cha mita 3,200 miaka 24,000 – 25,000 iliyopita wakati barafuto kote duniani zilienea sana. Kuna dalili ya kwamba barafu yote mlimani iliwahi kupotea kabisa takriban miaka 11,500 iliyopita kutokana na ukame dunaini wakati ule.
|
20231101.sw_1751_35
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kilimanjaro%20%28Volkeno%29
|
Kilimanjaro (Volkeno)
|
Kuongezeka kwa usimbishaji wakati wa Holoseni (miaka 11,500 iliyopita) kumeruhusu kurudi kwa barafu mlimani. barafuto ziliweza kudumisha kipindi cha ukame miaka 4,000 iliyopita.
|
20231101.sw_1751_36
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kilimanjaro%20%28Volkeno%29
|
Kilimanjaro (Volkeno)
|
Wakati wa kutembelewa mara ya kwanza katika miaka ya 1880, kilele cha Kibo kilifunikwa kabisa kwa ngao ya barafu yenye eneo la kilomita za mraba 20 hivi na mikondo ya barafuto iliendelea wenye mitelemko ya kando. Isipokuwa pia ya kati, kaldera yote ilifunikwa na barafu.
|
20231101.sw_1751_37
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kilimanjaro%20%28Volkeno%29
|
Kilimanjaro (Volkeno)
|
Imetazamiwa ya kwamba barafuto kwenye mitelemko ilirudi nyuma haraka kuanzia 1912 hadi 1953, na polepole zaidi tangu wakati ule. Inaendelea kupungua nah ii inaonyesha ya kwamba bado hakuna uwiano kati ya kiasi cha mvua kinachofika kwenye kilele na uvukizaji nah ii inaonyesha mabadiliko ya tabianachi yanayoendelea.
|
20231101.sw_1751_38
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kilimanjaro%20%28Volkeno%29
|
Kilimanjaro (Volkeno)
|
Pamoja na kufunika eneo dogo zaidi, yaani kujikaza, barafuto pia zimepungua unene kutokana na kuyeyuka na uvukizaji. Mabadiliko haya kwenye barafuto za Kilimanjaro zinalingana na mabadiliko yanayoonekana kwenye barafuto kote duniani. At the current rate, most of the ice on Kilimanjaro will disappear by 2040 and "it is highly unlikely that any ice body will remain after 2060".
|
20231101.sw_1751_39
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kilimanjaro%20%28Volkeno%29
|
Kilimanjaro (Volkeno)
|
Kama barafu juu ya Kilimanjaro ingepotea kabisa hii isingekuwa tatizo kubwa kwa maji yanayopatikana katika maeneo yanayozunguka mlima. Kiasi cha barafu juu ya mlima ni kidogo sana kuliko kiasi cha maji yanayohifadhiwa na misitu kwenye mitelemko ya mlima chini zaidi. Misitu hii ni chanzo cha maji yanayotiririke chini katika mito na vijito vya mlima mkubwa.
|
20231101.sw_1751_40
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kilimanjaro%20%28Volkeno%29
|
Kilimanjaro (Volkeno)
|
Sehemu ya chini hulimwa kwa kupanda mahindi, maharagwe na alizeti, pia ngano upande wa magharibi. Kuna mabaki ya uoto wa savana ya awali yenye miti kama Acacia, Combretum, Terminalia na Grewia.
|
20231101.sw_1751_41
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kilimanjaro%20%28Volkeno%29
|
Kilimanjaro (Volkeno)
|
Kuanzia kimo cha mita 1000 hadi mita 1800 kuna kilimo cha kahawa kwa namna ya kidesturi ya "Wachaga inayopanda miti na mazao kwa pamoja. Uoto asilia umebaki pekee katika mabonde majkali yasiyoweza kutumiwa kwa kilimo na hapa ni tofauti na uoto kwenye maeneo ya juu zaidi.
|
20231101.sw_1751_42
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kilimanjaro%20%28Volkeno%29
|
Kilimanjaro (Volkeno)
|
Kuanzia kimo cha mita 1000 hadi mita 1800 kuna kilimo cha kahawa kwa namna ya kidesturi ya "Wachaga inayopanda miti na mazao kwa pamoja. Uoto asilia umebaki pekee katika mabonde majkali yasiyoweza kutumiwa kwa kilimo na hapa ni tofauti na uoto kwenye maeneo ya juu Zaidi.
|
20231101.sw_1751_43
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kilimanjaro%20%28Volkeno%29
|
Kilimanjaro (Volkeno)
|
Kwenye mitelemko ya kusini penye mvua nyingi kuna misitu ya mvua yenye miti aina ya Ocotea usambarensis pamoja na kangaga na epipythi.
|
20231101.sw_1751_44
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kilimanjaro%20%28Volkeno%29
|
Kilimanjaro (Volkeno)
|
Juu zaidi penye ukungu wa kudumu kuna Podocarpus latifolius, Hagenia abyssinica na Erica excelsa pamoja na kuvumwani.
|
20231101.sw_1751_45
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kilimanjaro%20%28Volkeno%29
|
Kilimanjaro (Volkeno)
|
Upande wa kaskazini ulio kavu zaidi pana misitu ya mizeituni, Croton-Mlungu-mbago (Calodendrum), Cassipourea (Mugome na Msikundazi) na Juniperus (Mtarakwa) kadri kimo kinaongezeka.
|
20231101.sw_1751_46
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kilimanjaro%20%28Volkeno%29
|
Kilimanjaro (Volkeno)
|
Juu zaidi kati ya mita 3,100 na 3,900 hufuata kanda la vichaka vya Erica (mdamba) na juu yake kunamajanimajani tu kama Helichrysum hadi mita 4500.
|
20231101.sw_1751_47
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kilimanjaro%20%28Volkeno%29
|
Kilimanjaro (Volkeno)
|
Utafiti kwenye kasoko ya Maundi kwenye kimo cha mita 2780 umeonyesha ya kwamba uoto wa Kilimanjaro ulibadilika katika mwendo wa karne na milenia. Wakati wa baridi kwenye enzi ya barafu miaka 42,000 – 30,000 iliyopita misitu ilishuka chini na kanda la mdamba lilitokea takriban mita 1,500 chini ya hali yake ya sasa..
|
20231101.sw_1751_48
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kilimanjaro%20%28Volkeno%29
|
Kilimanjaro (Volkeno)
|
Hakuna wanyama wakubwa wengi waliobaki mlimani. Wanapatikana hasa kwenye misitu na sehemu za chini mlimani. Tembo na nyati wanaweza kuwa na hatari kwa watalii wanaopanda mlima na pia kwa wakulima. Pongo, vinyonga, digidigi, paa, Nguchiro, nyani mbalimbali kama mbega, komba, chui, chozi na ngiri wametazamiwa pia. Punda milia na fisi wanapatikana mara chache kweye tambarare juu ya Shira.
|
20231101.sw_1751_49
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kilimanjaro%20%28Volkeno%29
|
Kilimanjaro (Volkeno)
|
Kuna spishi chache zinazopatikana Kilimanjaro pekee hizi ni pamoja na “kirukanjia wa Kilimanjaro” na spishi ya kinyonga kinachoitwa Kinyongia tavetana.
|
20231101.sw_1751_50
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kilimanjaro%20%28Volkeno%29
|
Kilimanjaro (Volkeno)
|
Field Guide to the Moist Forest Trees of Tanzania Jon C. Lovett, Chris K. Ruffo & Roy E. Gereau, Miti ya milima ya Tanzania
|
20231101.sw_1752_0
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Julius%20Nyerere
|
Julius Nyerere
|
Mwalimu Julius Kambarage Nyerere (Butiama, Mkoa wa Mara, pembezoni mwa Ziwa Nyanza, 13 Aprili 1922 - London, Uingereza, 14 Oktoba 1999) alikuwa rais wa kwanza wa Tanzania, na mara nyingi anatajwa kama "Baba wa Taifa" kwa jinsi alivyoathiri nchi hiyo.
|
20231101.sw_1752_1
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Julius%20Nyerere
|
Julius Nyerere
|
Kabla ya kuingia kwenye siasa alikuwa ni mwalimu. Kazi hiyo ndiyo iliyompatia jina ambalo lilimkaa maisha yake yote la "Mwalimu."
|
20231101.sw_1752_2
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Julius%20Nyerere
|
Julius Nyerere
|
Kwanza aliongoza Tanganyika toka mwaka 1961 hadi 1964 kama waziri mkuu, halafu kama rais; baada ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar, aliongoza Tanzania kuanzia mwaka 1964 hadi mwaka 1985 kama rais.
|
20231101.sw_1752_3
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Julius%20Nyerere
|
Julius Nyerere
|
Mwalimu Nyerere ni kati ya viongozi wachache wa Afrika ambao wameacha madaraka kwa hiari baada ya kutawala kwa muda mrefu, akiwa bado anapendwa na wananchi walio wengi katika nchi.
|
20231101.sw_1752_4
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Julius%20Nyerere
|
Julius Nyerere
|
Alipostaafu urais mwaka 1985 alirudi kijijini kwake Butiama ambako aliendesha shughuli za kilimo. Hata hivyo aliendelea kuwa na athari kubwa katika siasa ya Tanzania hadi kifo chake.
|
20231101.sw_1752_5
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Julius%20Nyerere
|
Julius Nyerere
|
Kwa ruhusa ya makao makuu ya Kanisa Katoliki duniani, Jimbo Katoliki la Musoma lilianza kushughulikia kesi ya kumtangaza mwenye heri na hatimaye mtakatifu. Kwa sababu hiyo anaitwa pia "mtumishi wa Mungu". Baada ya hapo Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania limepokea jukumu la kuratibu mchakato huo pamoja na kesi kuhamishiwa Jimbo Kuu la Dar es Salaam kutokana na Nyerere kuishi muda mrefu jijini humo.
|
20231101.sw_1752_6
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Julius%20Nyerere
|
Julius Nyerere
|
Julius Kambarage Nyerere alizaliwa mwaka 1922 katika kijiji cha Butiama, wilaya ya Musoma, mkoa wa Mara, Tanzania (wakati ule: Tanganyika).
|
20231101.sw_1752_7
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Julius%20Nyerere
|
Julius Nyerere
|
Alipokuwa mtoto Nyerere alichunga mifugo ya baba yake; katika umri wa miaka 12 aliingia shule akitembea kilomita 30 hadi Musoma.
|
20231101.sw_1752_8
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Julius%20Nyerere
|
Julius Nyerere
|
Mapadri wakiona akili yake kubwa walimsaidia kusomea ualimu huko Makerere, Kampala, Uganda kuanzia mwaka 1943 hadi 1945.
|
20231101.sw_1752_9
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Julius%20Nyerere
|
Julius Nyerere
|
Akiwa Makerere alianzisha tawi la Umoja wa Wanafunzi Watanganyika, pia alijihusisha na tawi la Tanganyika African Association (TAA).
|
20231101.sw_1752_10
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Julius%20Nyerere
|
Julius Nyerere
|
Mwaka 1949 alipata skolashipu ya kwenda kusoma kwenye Chuo Kikuu cha Edinburgh, Uskoti, Ufalme wa Muungano, akapata M.A. ya historia na uchumi (alikuwa Mtanganyika wa kwanza kusoma katika chuo kikuu cha Uingereza na wa pili kupata shahada ya elimu ya juu nje ya Tanganyika).
|
20231101.sw_1752_11
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Julius%20Nyerere
|
Julius Nyerere
|
Aliporejea kutoka masomoni, alifundisha Historia, Kiingereza na Kiswahili katika shule ya St. Francis iliyo karibu na Dar es Salaam.
|
20231101.sw_1752_12
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Julius%20Nyerere
|
Julius Nyerere
|
Mwaka 1953 alichaguliwa kuwa rais wa chama cha Tanganyika African Association (TAA), chama ambacho alikisaidia kukijenga alipokuwa mwanafunzi katika chuo kikuu cha Makerere.
|
20231101.sw_1752_13
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Julius%20Nyerere
|
Julius Nyerere
|
Mwaka 1954 alibadilisha jina la chama cha TAA kwenda chama cha Tanganyika African National Union (TANU), ambacho pia kilikuwa cha kisiasa zaidi kuliko TAA. Ndani ya mwaka mmoja chama cha TANU kikawa tayari chama cha siasa kinachoongoza nchini Tanganyika.
|
20231101.sw_1752_14
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Julius%20Nyerere
|
Julius Nyerere
|
Uwezo wa Nyerere uliwashtua viongozi wa kikoloni akalazimika kuchagua kati ya siasa na kazi ya ualimu. Nyerere alisikika akijisemea kuwa mwalimu kwa kuchagua na mwanasiasa kwa bahati mbaya.
|
20231101.sw_1752_15
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Julius%20Nyerere
|
Julius Nyerere
|
Alijiuzulu ualimu na kuzunguka nchi nzima ya Tanganyika kuzungumza na watu wa kawaida na machifu ili kuleta umoja katika kupigania uhuru. Pia alizungumza kwa niaba ya TANU katika Trusteeship Council na Fourth Committee ya Umoja wa Mataifa (UN) huko New York.
|
20231101.sw_1752_16
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Julius%20Nyerere
|
Julius Nyerere
|
Uwezo wake wa kuongea na wa kuunganisha watu ulimwezesha kufanikisha Tanganyika kupata uhuru bila umwagaji wa damu.
|
20231101.sw_1752_17
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Julius%20Nyerere
|
Julius Nyerere
|
Ushirikiano mzuri aliouonyesha aliyekuwa gavana wa wakati huo, Richard Turnbull, ulisaidia pia kuharakisha upatikanaji wa uhuru.
|
20231101.sw_1752_18
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Julius%20Nyerere
|
Julius Nyerere
|
Mwaka 1961 Tanganyika ilipata uhuru wake na tarehe 9 Desemba 1961 Nyerere alichaguliwa kuwa waziri mkuu wa Tanganyika huru; mwaka mmoja baadaye akawa rais wa kwanza wa Jamhuri ya Tanganyika.
|
20231101.sw_1752_19
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Julius%20Nyerere
|
Julius Nyerere
|
Nyerere alikuwa kiungo muhimu katika muungano wa Tanganyika na Zanzibar kutengeneza Tanzania mara baada ya mapinduzi ya Zanzibar mwaka 1964 yaliyomtoa madarakani sultani wa Zanzibar Jamshid bin Abdullah.
|
20231101.sw_1752_20
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Julius%20Nyerere
|
Julius Nyerere
|
Tarehe 5 Februari 1977 aliongoza chama cha TANU kuungana na chama tawala cha Zanzibar Afro Shirazi Party na kuanzisha chama kipya cha CCM (Chama cha Mapinduzi) akiwa mwenyekiti wake wa kwanza.
|
20231101.sw_1752_21
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Julius%20Nyerere
|
Julius Nyerere
|
Aliacha kuongoza Tanzania ikiwa ni mojawapo kati ya nchi maskini zaidi duniani, ingawa yenye huduma za elimu na afya zilizoenea kwa wananchi wengi.
|
20231101.sw_1752_22
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Julius%20Nyerere
|
Julius Nyerere
|
Hata hivyo aliendelea kuongoza CCM hadi mwaka 1990 na kuwa na athari kubwa katika siasa ya Tanzania hadi kifo chake.
|
20231101.sw_1752_23
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Julius%20Nyerere
|
Julius Nyerere
|
Kwa mfano, inasadikika kuwa Nyerere alishawishi uteuzi wa Benjamin W. Mkapa kama mgombea wa urais mwaka 1995, ambaye alichaguliwa kuwa rais kwenye uchaguzi.
|
20231101.sw_1752_24
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Julius%20Nyerere
|
Julius Nyerere
|
Nyerere alikaa muda mwingi kwake Butiama akilima shamba lake. Pamoja na haya alianzisha taasisi yenye jina lake; mwaka 1996 alionekana akiwa mpatanishi wa pande mbalimbali za vita vya wenyewe kwa wenyewe huko Burundi.
|
20231101.sw_1752_25
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Julius%20Nyerere
|
Julius Nyerere
|
Tarehe 14 Oktoba 1999 aliaga dunia katika hospitali ya St Thomas mjini London baada ya kupambana na kansa ya damu.
|
20231101.sw_1752_26
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Julius%20Nyerere
|
Julius Nyerere
|
Kati ya mafanikio makubwa ya Nyerere kuna: kujenga umoja wa taifa kati ya watu wa makabila na dini tofauti, na hivyo kudumisha amani ya muda mrefu tofauti na hali ya nchi jirani, iliyofanya Tanzania iitwe "kisiwa cha amani".
|
20231101.sw_1752_27
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Julius%20Nyerere
|
Julius Nyerere
|
Pia kustawisha utamaduni wa Kiafrika pamoja na lugha ya Kiswahili, kushinda ubaguzi wa rangi, kutetea usalama wa taifa katika vita dhidi ya mvamizi Idi Amin wa Uganda.
|
20231101.sw_1752_28
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Julius%20Nyerere
|
Julius Nyerere
|
Kutoa mchango kwa vyama vya ukombozi vya nchi za Kusini mwa Afrika kama vile: Zimbabwe (ZANU), Afrika Kusini (ANC na PAC), Namibia (SWAPO), Angola (MPLA) na Msumbiji (Frelimo).
|
20231101.sw_1752_29
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Julius%20Nyerere
|
Julius Nyerere
|
Nyerere analaumiwa kwa siasa yake ya kiujamaa kuwa ilichelewesha maendeleo ya kiuchumi wa Tanzania. Siasa yake ya ujamaa ilishindikana kwa kiasi kikubwa baada ya mwaka 1976 kwa sababu mbalimbali za nje na za ndani ya nchi.
|
20231101.sw_1752_30
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Julius%20Nyerere
|
Julius Nyerere
|
Baada ya kuona kuwa uchumi wa Tanzania hautaweza kusimama kwa siasa ya kijamaa na kuwa hataweza kuvumilia kuendesha nchi kwa siasa nyingine ambazo yeye hakuwa na imani nazo, Nyerere kwa hiari yake mwenyewe aliamua kustaafu nafasi ya urais kuanzia uchaguzi wa mwaka 1985 na kumwachia usukani Ali Hassan Mwinyi, aliyetawala kwa siasa ya uchumi wa soko huria.
|
20231101.sw_1752_31
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Julius%20Nyerere
|
Julius Nyerere
|
Katika hali ya kukubali ukweli, Nyerere katika tafrija ya kumwaga alitamka juu ya siasa yake upande wa uchumi: “Nimefeli. Tukubali hivyo.”
|
20231101.sw_1752_32
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Julius%20Nyerere
|
Julius Nyerere
|
Kosa lingine ambalo wengine wanaona Nyerere alilifanya ni kumhadaa aliyekuwa Rais wa Zanzibar Mzee Abeid Amaan Karume kwa kuziunganisha Tanganyika na Zanzibar, na kuanza kupora mamlaka ya Zanzibar kidogokidogo. Kwa hivi sasa Wanzanzibari wengi wamechoka na Muungano huo, na wanataka uhuru wa nchi yao ili wapumue. Hata upande wa bara wananchi wengi wanalalamikia kutoweka kwa Tanganyika na serikali yake.
|
20231101.sw_1752_33
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Julius%20Nyerere
|
Julius Nyerere
|
Pia kuna makundi ya Waislamu wanaomtuhumu kwa kuendesha kwa siri vita dhidi ya dini yao na kupendelea Wakristo katika utoaji wa elimu na madaraka,japo wasomi wengi kwa kipindi cha utawala wake walikuwa Wakristo.
|
20231101.sw_1752_34
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Julius%20Nyerere
|
Julius Nyerere
|
Pamoja na hayo, Nyerere bado anakumbukwa na Watanzania hasa wa hali ya chini kutokana na sera zake za kujali utu. Pia ataendelea kukumbukwa na Waafrika barani kote hasa kwa mchango wake mkubwa wakati wa harakati za kupigania uhuru katika nchi mbali mbali barani Afrika.
|
20231101.sw_1752_35
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Julius%20Nyerere
|
Julius Nyerere
|
Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ni mmoja wa viongozi wachache waadilifu waliokwepa kujilimbikizia mali pamoja na kutawala kwa miaka zaidi ya 24.
|
20231101.sw_1752_36
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Julius%20Nyerere
|
Julius Nyerere
|
Mwishoni mwa maisha yake Nyerere aliishi kama mkulima wa kawaida kijijini kwake Butiama. Alipatwa na kansa ya damu (leukemia) akafariki Uingereza wakati wa kutibiwa katika mji wa London tarehe 14 Oktoba 1999.
|
20231101.sw_1752_37
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Julius%20Nyerere
|
Julius Nyerere
|
Freedom and Unity (Uhuru na Umoja): Mkusanyiko wa maandiko na hotuba, 1952–1965 (Oxford University Press, 1967)Freedom and Socialism (Uhuru na Ujamaa). Mkusanyiko wa maandiko na hotuba, 1965-1967 (1968)
|
20231101.sw_1752_38
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Julius%20Nyerere
|
Julius Nyerere
|
Ndamo zimo: "The Arusha Declaration"; "Education for self-reliance"; "The varied paths to socialism"; "The purpose is man"; and "Socialism and development."Freedom & Development (Uhuru na Maendeleo). Mkusanyiko wa maandiko na hotuba, 1968-73 (Oxford University Press, 1974)
|
20231101.sw_1752_39
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Julius%20Nyerere
|
Julius Nyerere
|
Ujamaa - Essays on Socialism''' (1977)Crusade for Liberation (1979)Julius Kaisari, Tafsiri ya mchezo wa William Shakespeare unaoitwa Julius CaesarMabepari wa Venisi, Tafsiri ya mchezo mwingine wa William Shakespeare, The Merchant of VeniceUtenzi wa Enjili Kadiri ya Utungo wa Mathayo, Tafsiri ya kishairi ya Injili ya MathayoUtenzi wa Enjili Kadiri ya Utungo wa Marko, Tafsiri ya kishairi ya Injili ya MarkoUtenzi wa Enjili Kadiri ya Utungo wa Luka, Tafsiri ya kishairi ya Injili ya LukaUtenzi wa Enjili Kadiri ya Utungo wa Yohana, Tafsiri ya kishairi ya Injili ya YohaneUtenzi wa Matendo ya Mitume, Tafsiri ya kishairi ya Matendo ya Mitume
|
20231101.sw_1753_0
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mbege
|
Mbege
|
Mara nyingi mbege hutengenezwa na wanawake na hutumika katika sherehe na matukio mbalimbali kama vile harusi, misiba, kipaimara, kuzaliwa kwa mtoto, n.k. Mbege hutumiwa pia kama faini kwenye mahakama za jadi. Utengenezaji wa mbege hufanywa pia kwa biashara. Hapo huuzwa katika vilabu vya pombe na pia nyumbani.
|
20231101.sw_1753_1
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mbege
|
Mbege
|
Kinywaji hicho hutengenezwa kwa kuchemsha ndizi mbivu kama vile ndizi songea, ndizi uganda, kibungara, kisukari (kama zinapatikana sana) n.k. Ndizi hizo zikishachemshwa huachwa kwa kipindi cha kama tatu au zaidi ili zichache.
|
20231101.sw_1753_2
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mbege
|
Mbege
|
Baada ya hapo unga wa ulezi hupikwa na kuachwa upoe. Ndizi zilizochemshwa na kuchacha huchanganywa na maji, kisha kukamuliwa ili kupata juisi yake. Juisi hiyo huchanganywa na unga wa ulezi uliopikwa na tunapata (kivuo, kifue, togwa) na kuachwa usiku mzima. Kesho yake mbege huwa tayari kunywewa.
|
20231101.sw_1753_3
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mbege
|
Mbege
|
Kinywaji hicho kama haitanyewa na kumalizika siku hiyo basi ikilala tunapata kitu kinachooitwa ngera, ambayo ni chachu sana, ila ngera pia huweza kuzimuliwa na kuwa kinywaji kifaacho tena kwa kuchanganya na unga uliopikwa na unga kidogo usiopikwa, ila ngera ikilala tena humwagwa kwani haitafaa kunywea tena.
|
20231101.sw_1753_4
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mbege
|
Mbege
|
Watengenezaji wengi wa mbege huwa wanaweka gamba la mti wa msesewe (Rauvolfia Caffra), hasa maeneo ya Kibosho, Machame na Rombo ili kuongeza ladha ya uchachu na kupunguza kasi ya mbege kuchacha.
|
20231101.sw_1753_5
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mbege
|
Mbege
|
Chombo maalum kiitwacho kata hutumiwa kunywea mbege, ila mara nyingi sehemu za mijini hutumia vyombo vya plastiki, vikiwa na ujazo tofauti, navyo huitwa chubuku na kitochi. Katika maeneo ya vijijini mbege hunywewa kijamaa kwa kupokezana kata. Mtu mmoja anakunywa kisha anampatia mwingine anayekunywa na kumpa mwingine.
|
20231101.sw_1756_0
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kilimanjaro
|
Kilimanjaro
|
Jina la bidhaa mbalimbali zilizopewa jina la mlima kama vile bia ya aina ya Kilimanjaro Lager au maji ya kunywea katika Tanzania, karatasi za Kilimanjaro (Marekani), au keki ya Kilimandscharo (Ujerumani)
|
20231101.sw_1757_0
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Nchi%20za%20Maziwa%20Makuu
|
Nchi za Maziwa Makuu
|
Nchi za Maziwa Makuu ni nchi zinazopakana na maziwa makubwa ya Afrika ya Mashariki ambazo ni Tanzania, Rwanda, Burundi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Kenya na Uganda.
|
20231101.sw_1757_1
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Nchi%20za%20Maziwa%20Makuu
|
Nchi za Maziwa Makuu
|
Eneo hili ni muhimu kimataifa kutokana na bioanwai kubwa: asilimia 10 ya spishi za samaki wote duniani zinapatikana katika maziwa yake.
|
Subsets and Splits
No community queries yet
The top public SQL queries from the community will appear here once available.