_id
stringlengths 15
22
| url
stringlengths 31
150
| title
stringlengths 1
86
| text
stringlengths 100
23.8k
|
---|---|---|---|
20231101.sw_1773_9
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Jua
|
Jua
|
Wataalamu wanatofautiana katika makadirio yao kama upanuzi huu utasababisha pia kupotea kabisa kwa sayari za Utaridi, Mirihi na Dunia zikimezwa na kuingia ndani ya Jua.
|
20231101.sw_1773_10
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Jua
|
Jua
|
Baada ya miaka bilioni kadhaa ya kuwaka kama jitu jekundu, masi yake itakuwa imepungua itajikaza na kuendelea kwa muda usio mrefu kama nyota ndogo na hafifu. Kuna uwezekano mkubwa wa kwamba Jua litaendelea baadaye kama nyota kibete nyeupe (White Dwarf) itakayoendelea kuzimika polepole.
|
20231101.sw_1773_11
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Jua
|
Jua
|
Jua linatoa mwanga, joto na mnururisho mwingine wa aina mbalimbali. Sehemu ya mnururisho huu unatoka kwa umbo la chembe kama protoni na elektroni ambazo kwa jumla hujulikana pia kama upepo wa Jua. Masi ya upepo wa Jua ni takriban tani moja kwa kila sekunde. Asili ya nishati hii ni mchakato wa myeyungano wa kinyuklia ndani yake. Katika myeyungano huo hidrojeni inabadilishwa kuwa heliamu. Elementi nyingine zinatokea pia kwa kiasi kidogo. Badiliko kutoka hidrojeni kwenda heliamu inaachisha nishati inayotoka kwenye Jua kwa njia ya mnururisho.
|
20231101.sw_1773_12
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Jua
|
Jua
|
Nishati ya mnururisho huu ni msingi wa maisha ya mimea na viumbe hai katika dunia. Nuru ya Jua inabadilishwa na mimea kwa njia ya usanisinuru kuwa nishati ya kikemia inayojenga miili yao itakayokuwa lishe tena ya mimea na wanyama.
|
20231101.sw_1773_13
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Jua
|
Jua
|
Jua la utosi,upepo,mwinuko,mvua,uoto,bahari na maziwa ni mambo yanayoathiri tabia ya nchi ya Afrika Mashariki.
|
20231101.sw_1773_14
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Jua
|
Jua
|
Dunia yetu ina mistari ya kubuni inayowezesha kutambua maeneo mbalimbali kwa urahisi,mistari hiyo ni pamoja na mstari wa Ikweta,tropiki ya kansa na tropiki ya Kaprikoni
|
20231101.sw_1773_15
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Jua
|
Jua
|
Mstari wa Ikweta unaigawa dunia katika sehemu nbili za kaskazini na kusini,mstari huu una nyuzi 0 na unapita eneo la Afrika mashariki katika nchi za Kenya na Uganda.Mstari wa Tropiki ya kansa upo upande wa kaskazini mwa Ikweta.
|
20231101.sw_1773_16
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Jua
|
Jua
|
Kipindi ambacho jua la Utosi lipo Tropiki ya kansa ,eneo La Kizio cha Kaskazini Huwa na joto,kwa kuwa hewa ikipata joto hutanuka hivyo huwa na mgandamizo mdogo wa hewa.Pepo huvuma kuelekea huko.
|
20231101.sw_1773_17
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Jua
|
Jua
|
Pepo hizi huvuma kutoka kusini-mashariki kuanzia mwezi desemba wakati jua la utosi linapokuwa tropiki ya kaprikoni kipindi hiki kizio cha kusini huwa na joto na Pepo huvuma kutoka kusini-mashariki.Pia hali hiyo husababisha mabadiliko ya upatikanaji wa mvua na hali ya joto katika eneo la Afrika Mashariki.
|
20231101.sw_1773_18
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Jua
|
Jua
|
Maeneo ya Ikweta yana tabia ya Kiikweta ya kuwa na mvua nyingi na joto jingi.Kusini na Kaskazini mwa eneo lenye tabia ya Kiikweta kuna tabia ya kitropiki yenye majira mawili makuu ya mwaka.Majira hayo ya mwaka ni masika na kiangazi.Lakini katika maeneo ya pwani majira ya mwaka hugawanyika katika sehemu nne ambazo ni vuli,kipupwe,masika na kiangazi.
|
20231101.sw_1773_19
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Jua
|
Jua
|
Afrika Mashariki ina mwinuko wa meta 0 kutoka usawa wa bahari hadi kufika meta 4600.Maeneo ya pwani mwinuko wake ni kuanzia meta 0 hadi meta 500 kutoka usawa wa bahari.
|
20231101.sw_1773_20
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Jua
|
Jua
|
Wastani wa jotoridi ni nyuzi za sentigredi 26.Joto hupungua kadiri unavyoelekea bara.Meta 1500 Kutoka usawa wa bahari ni nyuzi za sentigredi 22 ambapo ni wastani wa joto linalopatikana katika maeneo ya Tabora.Maeneo ya mlima mrefu kama kilimanjaro wenye urefu wa meta 5895 huwa na jotoridi la chini ya nyuzi za sentigredi 0
|
20231101.sw_1773_21
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Jua
|
Jua
|
Maeneo yaliyo kandokando ya maziwa na bahari huwa na unyevunyevu na mvua nyingi.Mara nyingi maeneo yanayozunguka bahari na maziwa mfano Ziwa Viktoria na Bahari ya Hindi yana tabia ya nchi ya aina moja.Maeneo hayo kwa kawaida hupata mvua nyingi.
|
20231101.sw_1773_22
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Jua
|
Jua
|
Maeneo yenye misitu hupata mvua nyingi kwani mawingu huweza kufanyika kwa urahisi.Misitu hiyo pia huifadhi unyevu usipotee ardhini kwa urahisi kwa njia ya mvukizo.
|
20231101.sw_1773_23
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Jua
|
Jua
|
Pepo za msimu za Kaskazini-mashariki Huleta Mvua kidogo katika eneo kubwa la kenya na kaskazini mwa Tanzania. Pepo huvuma sambamba na pwani.Pepo hizi pia huvuma kutoka sehemu kubwa ya nchi kavu katika nchi ya Ethiopia na Sudani kabla ya kufika eneo la Afrika Mashariki.
|
20231101.sw_1774_0
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Wachagga
|
Wachagga
|
Wachagga ni kabila la watu wenye asili ya Kibantu (lakini pia mchanganyiko wa damu, hasa ya Kikushi) wanaoishi kaskazini mwa Tanzania chini ya mlima Kilimanjaro, mkoani Kilimanjaro.
|
20231101.sw_1774_1
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Wachagga
|
Wachagga
|
Wachagga ni kabila la tatu kwa ukubwa nchini Tanzania. Takwimu za mwaka 2003 zinaonyesha kuwa idadi yao ni watu 2,000,000.
|
20231101.sw_1774_2
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Wachagga
|
Wachagga
|
Wachagga wana historia ndefu ya asili yao na ya maingiliano yao na makabila mengine. Kabila la Kichagga ni mkusanyiko wa makabila madogomadogo (ya Kichagga) yaliyosambaa kijiografia kuzunguka mlima Kilimanjaro kuanzia mashariki (Tarakea, Rombo) hadi magharibi kwa Kilimanjaro (Siha, Machame).
|
20231101.sw_1774_3
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Wachagga
|
Wachagga
|
Wachaga ni kama vile Wa-Vunjo ambao wanajumuisha watu wa Mwika, Mamba, Marangu, Kilema na Kirua ambayo ndiyo inajulikana na wengi kama Kirua Vunjo. Ukipenda unaweza kuwagawa watu hawa wa Vunjo kufuatana na vijiji hivyo. Wengine ni Wa-Old Moshi, Wa-Kibosho, Wa-Machame, Wa-Uru, na Wa-Siha.
|
20231101.sw_1774_4
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Wachagga
|
Wachagga
|
Lugha ya Kichagga inabadilika kuanzia unapotoka Tarakea mpaka unapofika Siha magharibi mlima Kilimanjaro.
|
20231101.sw_1774_5
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Wachagga
|
Wachagga
|
Kutokana na tofauti hizo Kichagga kimegawanyika katika Kirombo (ambacho nacho kinatofautiana kadiri unavyotoka eneo moja hadi jingine; mfano Kiseri, Kimashati, Kimkuu, Kimengwe, Kimahida), Kimachame, Kivunjo, Kimarangu, Kioldimoshi, Kingassa, Kiuru, Kikibosho, na Kisiha.
|
20231101.sw_1774_6
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Wachagga
|
Wachagga
|
Lugha hizo zinakaribia kufanana kadiri makundi hayo yalivyopakana. Kwa mfano, Kivunjo kinafanana na Kioldimoshi. Vile vile Kisiha kinafanana sana na Kimachame ambacho pia kinafanana kidogo na Kikibosho.
|
20231101.sw_1774_7
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Wachagga
|
Wachagga
|
Baadhi ya Wamachame walihamia sehemu za Meru, Arusha, na kuchanganyikana na Waarusha, hivyo lugha yao ikabadilika kidogo na kuwa Kimeru. Kwa sababu hiyo Wameru wanasikilizana sana na Wamachame ingawa lafudhi zao zinatofautiana kidogo.
|
20231101.sw_1774_8
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Wachagga
|
Wachagga
|
Majina ya kiukoo ya Kichagga pia huashiria wanatoka sehemu gani ya Uchaga, japo si lazima kuwa hivyo: kwa mfano, familia maarufu za Kichagga nchini Tanzania ni kama ukoo wa akina Mushi au Moshi, Mmasy, Kimaro, Swai, Massawe, Lema, Urassa, Nkya, Ndosi, Meena n.k.
|
20231101.sw_1774_9
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Wachagga
|
Wachagga
|
Akina Temu, Mlaki, Mlay, Lyimo, Moshiro, Mselle, Kamnde, Kileo, Kimambo, Tesha, Msaki, Assey, Kyara, Kessy, Ndanu, Macha, Mbishi, Moshi, Kombe, Njau wanatoka Old Moshi na Vunjo.
|
20231101.sw_1774_10
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Wachagga
|
Wachagga
|
Majina mengine ya Old Moshi ni kama yafuatayo: Saria, Mmari, Macha, Machange, Mshiu, Kyara, Moshi, Massamu, Kimambo, Mboro, Mlngu, Saule, Tenga, Njau, Malisa, Maro, Maeda, Ringo,Olomi, Ngowi, Lyatuu na mengine mengi.
|
20231101.sw_1774_11
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Wachagga
|
Wachagga
|
Kavishe, Mrosso, Bongole, Mariki, Moshi, Tarimo, Laswai, Mallya, Mrema, Mkenda, Mushi, Massawe, Silayo, Lyaruu, Makyao, Mowo, Lamtey, Tairo, Masue, Maleto, Mramba, Kauki, Kiwango na Kyauke wanatoka Rombo.
|
20231101.sw_1774_12
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Wachagga
|
Wachagga
|
Mchaki, Masawe, Sawe, Usiri, Shayo, Kiwelu, Makundi, Urasa, Mtui, Moshi, Meela, Minja, Njau, Saria, Mtei wanatoka Marangu na Kilema.
|
20231101.sw_1774_13
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Wachagga
|
Wachagga
|
Rite, Makule, Minja, Mashayo, Chao, Shao, Makawia, Ndesano, Kimario, Tilla, Mariale, Tarimo, Mafole, Kituo, Mrosso, Lyakundia, Kessy, Mmbando, Matemba, Ndenshau, Morio, Akaro, Matowo, Towo, Mkony, Temba, Foya, Munishi, Kilawe, na kadhalika hutoka Kibosho.
|
20231101.sw_1774_14
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Wachagga
|
Wachagga
|
Ukoo wa akina Teri wako Mamba, Chami, Chuwa, Kiria Owoya na wachache Sango, Old Moshi na wengine walihamia Maji ya Chai, Mkoa wa Arusha.
|
20231101.sw_1774_15
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Wachagga
|
Wachagga
|
Watawala wa Kichagga waliitwa "Mangi". Akina mangi walihodhi mashamba, ng'ombe na waliheshimiwa kama viongozi wa jadi. Walikuwa na nguvu za kisiasa na utajiri. Baadhi ya Ma-mangi mashuhuri katika historia ni kama Mangi Shangali (wa ukoo wa Mushi) kutoka Machame, Mangi Rindi aliyeingia mikataba na wakoloni (Wajerumani), Mangi Sina wa Kibosho na Mangi Horombo wa Keni - waliojulikana kwa uhodari wao wa vita katika kupigana na Wamachame na kupora ng'ombe na mazao yao, na Mangi Marealle wa Marangu na Vunjo. Mangi Meli alikuwa mangi wa Waoldmoshi ambaye alipigana na Wajerumani na aliishia kukatwa kichwa; mpaka sasa fuvu lake lipo Ujerumani, alizikwa kiwiliwili tu baada ya kunyongwa; mti aliyonyongewa upo mpaka sasa sehemu ya Oldmoshi bomani karibu na Kolila Sekondari. Alinyongwa kwa sababu alikataa kuwa kibaraka wa kutumika na Wajerumani.
|
20231101.sw_1774_16
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Wachagga
|
Wachagga
|
Wakoloni walipokuja Kilimanjaro waliingia mikataba na viongozi hao wa kikabila ili kuweza kuweka misingi yao ya kikoloni. Pia ndugu na watoto wa Ma-mangi walikuwa wa kwanza kupata elimu ya kikoloni, kwa hiyo waliweza kushirikishwa katika serikali za kwanza. Hao pia wanaaminika walikuwa kama mabepari wa kwanza wa kijadi, maana walifanyiwa kazi na watu wengine wakati wao wamekaa kuhesabu mali zao. Hii ni desturi ya watawala, hasa wafalme kote ulimwenguni.
|
20231101.sw_1774_17
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Wachagga
|
Wachagga
|
Wachagga wanajulikana kwa uwezo wao mkubwa katika uwanja wa elimu, hususani katika masomo ya sayansi na hisabati. Moshi ni maeneo ya mwanzo ambayo wamisionari wa Ukristo walijenga makanisa na shule.
|
20231101.sw_1774_18
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Wachagga
|
Wachagga
|
Sababu hii imefanya Wachagga kuwa kabila namba moja lenye watu wengi zaidi walio na elimu ya kisasa (elimu ya juu) na mkoa wa Kilimanjaro unaongoza kwa idadi ya shule za sekondari nchini Tanzania. Kulingana na takwimu za elimu mkoa huo una shule za sekondari zaidi ya 320. Pia mkoa una shule za msingi zipatazo 950. Idadi hii ya shule ni kubwa zaidi ya idadi ya shule katika mikoa mingine Tanzania.
|
20231101.sw_1774_19
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Wachagga
|
Wachagga
|
Hali ya hewa na vivutio vya kitalii katika mkoa huu viliwavutia zaidi walowezi na wakoloni na kuweka makazi yao hapo. Hivyo wamisionari walijenga shule za kwanza wakifuatiliwa na serikali za wakoloni
|
20231101.sw_1774_20
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Wachagga
|
Wachagga
|
Wachagga waliobahatika kupata fedha binafsi baadaye waliwekeza kwenye ujenzi wa shule binafsi kama kitega-uchumi, wakati wakazi wa mikoa mingine kadhaa walisubiri serikali iwajengee shule.
|
20231101.sw_1774_21
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Wachagga
|
Wachagga
|
Ukichanganya sababu 1, 2 & 3 utagundua shule katika mkoa Kilimanjaro zimezidi sana idadi ya shule katika mikoa mingine yote.
|
20231101.sw_1774_22
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Wachagga
|
Wachagga
|
Ni vema pia kusema kuwa shule hizo huvutia wanafunzi kutoka Tanzania nzima, haziwasomeshi Wachagga tu.
|
20231101.sw_1774_23
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Wachagga
|
Wachagga
|
Ingawa ardhi ni msingi wa maendeleo kwa watu wote, kwa Wachagga, ardhi ni mali sana kwa sababu kilimo chao ni cha mazao ya kudumu kama kahawa na ndizi hukaa shambani kwa muda wa miaka mingi.
|
20231101.sw_1774_24
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Wachagga
|
Wachagga
|
Mojawapo ya urithi wapewayo watoto ni "kihamba". Hii ni sehemu ya ardhi ambayo mtoto anategemewa atajenga na kuanzisha familia yake. Bahati mbaya watoto wa kike walikuwa hawapewi kipaumbele katika ugawanaji wa vihamba. Uhaba wa ardhi huko Uchaga ulipelekea Wachagga wengi kuhamia mikoa mingine. Hivi leo utakuta Wachagga wakiishi Dodoma, Morogoro, Iringa, Mbeya n.k. wakiwa wamepanda migomba yao na kuendesha biashara za maduka ya vyakula, pamoja na biashara nyingine.
|
20231101.sw_1774_25
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Wachagga
|
Wachagga
|
Ukienda kwenye mikoa hiyo utakuta wamejenga jamii zao na vyama vyao vya kusaidiana wakati wa sherehe au matatizo. Aidha hata pombe ya mbege utaweza kuikuta kwenye makusanyiko ya Wachagga katika mikoa mbalimbali.
|
20231101.sw_1774_26
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Wachagga
|
Wachagga
|
Wachagga hulima mazao ya chakula kama vile mahindi, maharagwe, viazi, ndizi, ulezi na mboga mbalimbali. Pia mazao ya biashara kama vile kahawa, nyanya na vitunguu.
|
20231101.sw_1774_27
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Wachagga
|
Wachagga
|
Ingawa Wachagga wa leo wanakula vyakula mbalimbali kama vile ugali, wali na viazi, chakula kikuu cha Wachagga ni ndizi.
|
20231101.sw_1774_28
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Wachagga
|
Wachagga
|
Kuna ndizi za aina mbalimbali na kwa matumizi tofauti. Mfano ndizi sukari ni fupi na huachwa hadi ziive na huliwa mbivu kama tunda.
|
20231101.sw_1774_29
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Wachagga
|
Wachagga
|
Ndizi mshale hukatwa zikiwa mbichi na kupikiwa vyakula mbalimbali pamoja na nyama ya ng'ombe, kondoo au mbuzi. Mara nyingine hupikwa na maharage, choroko, kunde au hata maziwa ya mtindi. Vyakula vya ndizi huja kwa ladha tofauti kama vile ndizi nyama, mtori, machalari, kiburu na kadhalika.
|
20231101.sw_1774_30
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Wachagga
|
Wachagga
|
Aina nyingine ni ndizi ng'ombe ambazo huachwa ziive halafu humenywa na kutumiwa kutengenezea kinywaji maarufu kiitwacho mbege. Mbege hutengenezwa kwa kutumia ndizi mbivu, maji, na ulezi.
|
20231101.sw_1774_31
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Wachagga
|
Wachagga
|
Aina nyingine ni ndizi mzuzu. Hizi zikikomaa huachwa zianze kuiva kidogo halafu huchomwa na kuliwa kama kitafunwa pamoja na chai au kinywaji kingine. Ukipita mitaa ya Dar es Salaam utaona ndizi mzuzu zikichomwa sambamba na muhogo au kuku vumbi au kiti moto.
|
20231101.sw_1774_32
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Wachagga
|
Wachagga
|
Inasemekana kuwa "Mchagga halisi hali muhogo - akila muhogo atakufa". Usemi huu umetokana na historia ya mababu kuwa Wachagga waliopanda mihogo Kilimanjaro enzi za kale walikufa baada ya kuila. Historia hiyo yaweza kuwa ya ukweli kwa sababu aina nyingi za mihogo zinajenga sumu ya sianidi ndani yake; watu waliozoea kutumia mihogo huwa na njia za kuondoa sumu kwa kuiloweka mihogo katika maji kwa muda. Lakini kama Wachagga wale wa zamani, hasa wa Machame, walifanya jaribio bila kujua mbinu ya kuondoa sumu, ajali iliweza kutokea. Cha kushangaza ni kwamba hukohuko Kilimanjaro, majirani na watani wa Wachagga, yaani Wapare, walikuwa wameshazoea mihogo na ilikuja kuwa moja ya chakula chao kikuu.
|
20231101.sw_1774_33
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Wachagga
|
Wachagga
|
Pamoja na kilimo cha mazao, Wachagga hupendelea sana kufuga nguruwe kwa ajili ya biashara kwani nyama ya nguruwe hupendwa sana na watu na huuzwa sana kwenye baa na hoteli mbalimbali mijini hasa katika jiji la Dar es Salaam. Tabia ya kula nyama ya nguruwe ijulikanayo leo kwa jina la "kiti moto" ni moja ya mambo yaliyoenezwa na Wachagga. Ulaji wa "kiti moto" haukuwapendeza baadhi ya wenyeji wa Pwani na Dar es Salaam ambapo Wachagga walihamia, kwani wengi wao ni Waislamu, kwa hiyo nguruwe kwao ni haramu. Wakazi wa Dar es Salaam watokao makabila mengine na wasio Waislamu kwao kula nguruwe ilikuwa "ruksa".
|
20231101.sw_1774_34
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Wachagga
|
Wachagga
|
Wanawake wa Kichagga (hasa kutoka Machame) hujulikana kama wafanyakazi hodari. Huchangia sana katika mapato ya nyumbani na chakula. Mama wa Kichagga anaweza kushinda shambani kutwa na hana desturi ya kubeba watoto mgongoni kwenda nao shambani, hivyo wanakuwa nyumbani na mayaya au peke yao. Mfano ulio dhahiri ni nyakati za asubuhi na mapema kwenye vyombo vya usafiri karibu robo tatu ya abiria ni wanawake wakienda katika shuguli za biashara na kilimo na vivyo hivyo nyakati za jioni wakirudi majumbani. Hao ni nje ya wale wanaotumia usafiri wa miguu ambao ni wengi zaidi.
|
20231101.sw_1774_35
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Wachagga
|
Wachagga
|
Ingawa wanaume wa Kichagga hupendelea kufanya kazi mbali na kwao, wake zao hukaa nyumbani (Kilimanjaro) kufuga ng'ombe na kufanya kazi za shambani. Kwa sasa kutokana na ugonjwa wa ukimwi tabia hii imepungua miongoni mwao.
|
20231101.sw_1774_36
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Wachagga
|
Wachagga
|
Pia baadhi ya kina mama wa Kichaga wanawajali waume zao zaidi kwani nyama nzuri ni ya baba. Ili kuepuka gharama baba ataandaliwa chakula kizuri, tofauti na chakula walichoandaliwa watoto, japo ni chakula kilekile.
|
20231101.sw_1774_37
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Wachagga
|
Wachagga
|
Pia Wachagga wamekuwa na desturi ya kuwaenzi wazee wao waliotangulia mbele za haki kwa kuwatambikia kwa pombe na nyama za mbuzi pale tu wanaporudi nyumbani mwezi Desemba. Hilo limekuwa suala la kawaida sana. Wengi wao huwa wanarudi na magari, ndiyo sababu utaona ya kwamba kila mwaka ufikapo mwezi Desemba foleni za magari zimekuwa zikiongezeka katika mji wa Moshi kutokana na Wachagga kurudi nyumbani msimu wa sikukuu. Wengi wao wamekuwa wakitoka sehemu mbalimbali za nchi na hata nje ya nchi.
|
20231101.sw_1774_38
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Wachagga
|
Wachagga
|
Wachagga wengi hupenda kurudi nyumbani kipindi cha Krismasi, ikiwa ni kuwatembelea wazazi wao, rafiki, au ndugu. Pia imekuwa kama desturi wanaukoo kukaa pamoja na kujadiliana mambo jinsi yalivyokwenda katika kipindi kizima cha mwaka na wakati mwingine inakuwa sehemu ya kwenda kuwatambulisha watoto kwa bibi na babu zao, hasa wale waliozaliwa mijini. Ni kipindi chenye shangwe na furaha sana: hakuna kaya utakayokuta haina furaha kwa sababu hata kama huna sherehe kuna mialiko mbalimbali ambao haihitaji kadi au michango.
|
20231101.sw_1774_39
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Wachagga
|
Wachagga
|
Ingawa wengi hudhani kwamba Wachagga wamepokea sana dini (imani) ya Ukristo kwa kuwa wengi wao ni Wakristo na hiki huwa kipindi cha likizo kwao, inaaminika pia kuwa kurudi kwao wakati wa Krismasi ni pamoja na kutembelea ndugu zao na kujumuika pamoja katika kuumaliza mwaka baada ya kazi nyingi za kutafuta pesa mwaka mzima.
|
20231101.sw_1774_40
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Wachagga
|
Wachagga
|
Kupumzika, hii ni baada ya kufanya kazi kwa mwaka mzima bila kwenda, biashara asubuhi, jioni mahesabu, kwao Desemba ni mwezi wa kutulia tu na familia ndugu na jamaa
|
20231101.sw_1774_41
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Wachagga
|
Wachagga
|
Kuchinja mbuzi, hapa kuna za matambiko na za kula na kufurahia tu. Matambiko hayo ni kushukuru wazee wao waliokufa mapema kwa baraka walizopata kwa kipindi chote cha mwaka mzima
|
20231101.sw_1774_42
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Wachagga
|
Wachagga
|
Sherehe mbalimbali: sherehe za wafu, maadhimisho ya ndoa mbalimbali, Krismasi, Ubatizo, Kipaimara, Komunyo, kutoa watoto jandoni na Mwaka mpya wenyewe. Kila inayoitwa sherehe hufanyika kipindi hiki, kuanzia tarehe 25 Desemba kufika tarehe 1 Januari ni shughuli tu, kula kunywa kusaza.
|
20231101.sw_1774_43
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Wachagga
|
Wachagga
|
Utambulisho mbalimbali kwa wazee, jamaa wa nyumbani kama vile mke, mchumba, mume, gari jipya, nyumba mpya, watoto n.k.
|
20231101.sw_1774_44
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Wachagga
|
Wachagga
|
Kukutana na watu mbalimbali ambao hamuonani baada ya kipindi hicho kama, marafiki, majirani, ndugu na jamaa. Hii ni kwa wale wanaofanya kazi mikoa tofauti (huyu Morogoro yule Mwanza mwingine katoka Dar es Salaam)
|
20231101.sw_1774_45
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Wachagga
|
Wachagga
|
Utekelezaji wa miradi mbalimbali hapo nyumbani kama ujenzi au ukarabati wa nyumba, njia pana za magari na kukagua mashamba n.k.
|
20231101.sw_1774_46
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Wachagga
|
Wachagga
|
Kutokana na sababu hizo wanaokwenda ni watu wote wa dini zote. Ukienda tofauti na kipindi hiki huwezi kukuta watu wengi sana. Kwanza baada ya kipindi hicho kupita kila mtu anashughulika na mambo yake (kutafuta pesa).
|
20231101.sw_1775_0
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Djibril%20Diallo
|
Djibril Diallo
|
Dakta Djibril Diallo ni mzaliwa wa Senegal. Amewahi kuwa mkurugenzi wa mawasiliano wa Shirika la Maendeleo ya Viwanda la Umoja wa Mataifa, mshauri maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusiana na mkutano wa kimataifa wa haki za binadamu. Tena alikuwa waziri nchini Mali.
|
20231101.sw_1775_1
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Djibril%20Diallo
|
Djibril Diallo
|
Hivi sasa anahudumia ofisi ya Umoja ya Mataifa inayojihusisha na miradi ya kuleta amani kwa kutumia michezo. Diallo pia ni msemaji wa Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa.
|
20231101.sw_1776_0
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Abedi%20Amani%20Karume
|
Abedi Amani Karume
|
Sheikh Abeid Amani Karume alikuwa Rais wa kwanza wa Zanzibar. Alizaliwa mwaka 1905 na kufariki tarehe 7 Aprili 1972 kwa kupigwa risasi.
|
20231101.sw_1776_1
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Abedi%20Amani%20Karume
|
Abedi Amani Karume
|
Karume aliongoza nchi baada ya mapinduzi yaliyomwangusha Sultani aliyekuwa akitawala Zanzibar hadi mwanzoni mwa mwaka 1964.
|
20231101.sw_1776_2
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Abedi%20Amani%20Karume
|
Abedi Amani Karume
|
Baada ya miezi mitatu Zanzibar iliungana na Tanganyika iliyokuwa ikiongozwa na Mwalimu Nyerere. Baada ya muungano wa nchi hizi mbili uliozaa Tanzania, Karume alikuwa makamu wa rais wa kwanza wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
|
20231101.sw_1776_3
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Abedi%20Amani%20Karume
|
Abedi Amani Karume
|
Amani Abeid Karume, ambaye ni mtoto wa Sheikh Karume, alikuwa rais wa Zanzibar tangu mwaka 2000 hadi 2010.
|
20231101.sw_1777_0
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Orodha%20ya%20vyama%20vya%20siasa%20Tanzania
|
Orodha ya vyama vya siasa Tanzania
|
Mfumo wa vyama vingi ni hali ya kuwa na chama zaidi ya kimoja,katika nchi moja.Madhumuni ya kuwa na vyama vingi vya siasa ni kuleta ushindani wa kisiasa,ili kuleta maendeleo ya nchi,upinzani wa kisiasa sio uadui kama watu wengi kwenye nchi zinazoendelea wanavyodhani,kuwa na vyama vingi ni kuongeza wigo wa demokrasia katika jamii huska.
|
20231101.sw_1777_1
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Orodha%20ya%20vyama%20vya%20siasa%20Tanzania
|
Orodha ya vyama vya siasa Tanzania
|
Tanzania ni nchi yenye mfumo wa vyama vingi vya siasa uliorejeshwa katika katiba ya Tanzania mwaka 1992.
|
20231101.sw_1778_0
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Nelson%20Mandela
|
Nelson Mandela
|
Nelson Rolihlahla Mandela (18 Julai 1918 - 5 Desemba 2013) alikuwa mwanasiasa nchini Afrika Kusini, kiongozi wa mapambano dhidi ya siasa ya ubaguzi wa rangi (Apartheid), mfungwa jela kwa miaka 27 halafu rais wa kwanza aliyechaguliwa kidemokrasia katika nchi yake.
|
20231101.sw_1778_1
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Nelson%20Mandela
|
Nelson Mandela
|
Alikuwa mwanasheria na mwanachama, baadaye kiongozi wa chama cha ANC kilichopigania haki za binadamu wote nchini Afrika Kusini.
|
20231101.sw_1778_2
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Nelson%20Mandela
|
Nelson Mandela
|
Mandela alizaliwa tarehe 18 Julai 1918 katika familia ya kabila la Waxhosa kwenye kijiji cha Mvezo karibu na Umtata iliyokuwa kwenye Jimbo la Rasi.
|
20231101.sw_1778_3
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Nelson%20Mandela
|
Nelson Mandela
|
Alipewa jina la Rolihlahla linalomaanisha "anayevuta tawi la mti" kwa maana ya "mwenye kuleta matata" katika lugha ya Kixhosa. Baadaye alijulikana kwa jina la ukoo wake "Madiba". Jina la Nelson alilipokea kutoka kwa mwalimu wake siku alipoanza kwenda shule.
|
20231101.sw_1778_4
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Nelson%20Mandela
|
Nelson Mandela
|
Alitoka katika familia ya kifalme. Baba wa babu yake Ngubengcuka alikuwa mfalme wa Wathembu katika maeneo ya Transkei wa jimbo la kisasa la Rasi Mashariki la Afrika Kusini.
|
20231101.sw_1778_5
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Nelson%20Mandela
|
Nelson Mandela
|
Baba yake Gadla Henry Mphakanyiswa alikuwa chifu na mshauri wa mfalme tangu mwaka 1915 hadi 1926. Mama yake Nelson, Nosekeni Fanny, alikuwa mke wa tatu.
|
20231101.sw_1778_6
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Nelson%20Mandela
|
Nelson Mandela
|
Miaka ya kwanza aliishi kijijini alipojifunza mila na desturi za Waxhosa na kutunza mifugo pamoja na wavulana wengine.
|
20231101.sw_1778_7
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Nelson%20Mandela
|
Nelson Mandela
|
Baba aliaga dunia Nelson alipokuwa na umri wa miaka tisa. Alibatizwa katika Kanisa la Kimethodisti akawa Mkristo wa kanisa hilo hadi kifo chake.
|
20231101.sw_1778_8
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Nelson%20Mandela
|
Nelson Mandela
|
Baada ya kifo cha baba, mama alimpeleka kwa chifu mkuu wa Wathembu aliyemlea kama mtoto wake. Pamoja na wazazi wake wapya alihudhuria ibada za kanisani kila Jumapili zilizoimarisha imani yake ya Kikristo.
|
20231101.sw_1778_9
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Nelson%20Mandela
|
Nelson Mandela
|
Akaendelea kusoma katika shule ya Kimethodisti aliposoma Kiingereza, Kixhosa, historia na jiografia. Katika ikulu ya chifu alisikia masimulizi mengi kuhusu historia ya Waafrika kutoka wageni waliokuja kumwaona baba wa kambo.
|
20231101.sw_1778_10
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Nelson%20Mandela
|
Nelson Mandela
|
Mwaka 1925 babake alimtuma kusoma shule ndogo ya Kimethodisti alipofanyikiwa vema. Baada ya kifo cha baba aliishi kwa chifu wa Watembo na hapo kwene umri wa miaka 16 alishiriki katika sherehe ya jando alipotahiriwa na kupokea jina Dalibunga.
|
20231101.sw_1778_11
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Nelson%20Mandela
|
Nelson Mandela
|
Baadaye aliendelea kusoma kwenye shule ya sekondari ya „Clarkebury Boarding Institute“ huko Engcobo iliyokuwa shule ya bweni kubwa kwa ajili ya vijana kutoka Wathembo.
|
20231101.sw_1778_12
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Nelson%20Mandela
|
Nelson Mandela
|
Hapa alianza mazoezi ya michezo na kupenda kazi ya bustani aliyoendelea kwa maisha yote. Baada ya miaka miwili alipokea cheti kidogo cha elimu ya sekondari.
|
20231101.sw_1778_13
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Nelson%20Mandela
|
Nelson Mandela
|
Mwaka 1937 kwenye umri wa miaka 19 aliendelea kwenye chuo cha Wamethodisti huko [[Fort Beaufort. Hapo alikuwa mara ya kwanza rafiki na kijana nje ya kabila lake aliyekuwa Msotho akaathiriwa na mwalimu mpendwa Mxhosa aliyevunja mwiko kwa kumwoa mke kutoka kwa Wasotho Mandela alitumia muda mwingi huko Healdtown kwa kufuata michezo ya kukimbia na bondia.
|
20231101.sw_1778_14
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Nelson%20Mandela
|
Nelson Mandela
|
Tangu 1939 alianza masomo kwa shahada ya kwanza kwenye Chuo Kikuu cha Fort Hare, chuo kwa ajili ya wanafunzi Waafrika katika jimbo la Rasi Mashariki. Masomo yake yalikuwa Kiingereza, anthropolojia, siasa na sheria. Wakati ule alitaka kuendelea kuwa mfasiri au afisa katika Idara ya Shughuli za Wazalendo (kitengo cha serikali ya Kizungu kwa maeneo ya Waafrika katika Afrika Kusini).
|
20231101.sw_1778_15
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Nelson%20Mandela
|
Nelson Mandela
|
Katika bweni lake alikuwa rafiki wa Kaiser Matanzima na Oliver Tambo aliyeendelea kuwa rafiki yake kwa miaka mingi ijayo.
|
20231101.sw_1778_16
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Nelson%20Mandela
|
Nelson Mandela
|
Pamoja na kupenda michezo Mandela alijifunza dansi ya Kizungu , alishiriki tamthiliya kuhusu about Abraham Lincoln, akatoa darasa la Biblia katika kanisa.
|
20231101.sw_1778_17
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Nelson%20Mandela
|
Nelson Mandela
|
Mandela alihukumiwa kifungo cha maisha kwa miaka 27 kutokana na harakati zake za kuupinga ubaguzi wa rangi. Alifungwa katika kisiwa cha Robben.
|
20231101.sw_1778_18
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Nelson%20Mandela
|
Nelson Mandela
|
Baada ya kuachiliwa huru mwaka 1990 alianzisha sera ya maridhiano au sera ya amani baina yake na watu weupe nchini Afrika Kusini, jambo ambalo watu wengi hawakulitegemea.
|
20231101.sw_1778_19
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Nelson%20Mandela
|
Nelson Mandela
|
Mwaka wa 1993, pamoja na Frederik Willem de Klerk alikuwa mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Amani ambayo ni tuzo ya nadra kutolewa duniani.
|
20231101.sw_1778_20
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Nelson%20Mandela
|
Nelson Mandela
|
Baada ya kutengana na mke wake, Winnie Madikizela, alimuoa Graca Machel aliyewahi kuwa mke wa rais wa Msumbiji, Samora Machel.
|
20231101.sw_1781_0
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Rosa%20Parks
|
Rosa Parks
|
Rosa Louise McCauley Parks (4 Februari 1913 – 24 Oktoba 2005) anakumbukwa kwa uamuzi wake wa kukataa kumpisha kiti Mmarekani Mweupe kama alivyodaiwa na dereva wa basi. Uamuzi wake huo hapo mwaka 1955 ulipelekea mzozo uliosababisha Mgomo wa Mabasi wa Montgomery na kuchangia katika Vuguvugu la Haki za Kiraia Marekani. Baada ya kitendo chake cha kukataa kumpa mtu mweupe kiti ndani ya basi na Mgomo wa Montgomery uliodumu kwa mwaka, Mahakama ya Marekani ilitamka kuwa sheria za ubaguzi ndani ya mabasi huko Alabama na Montgomery zilikiuka katiba.
|
20231101.sw_1782_0
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kwame%20Nkrumah
|
Kwame Nkrumah
|
Kwame Nkrumah (21 Septemba 1909 - 27 Aprili 1972) alikuwa Rais wa kwanza wa Ghana na mmoja wa viongozi wenye nia ya kujenga Muungano wa Afrika, tena mchochezi wa falsafa ya Umajinuni.
|
20231101.sw_1782_1
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kwame%20Nkrumah
|
Kwame Nkrumah
|
Kwame Nkrumah alizaliwa mnamo mwaka 1909 katika kijiji cha Nkroful kwenye koloni la Gold Coast (leo Ghana). Nkrumah mwenyewe aliandika ya kwamba tarehe ilikuwa 18 Septemba 1909 iliyokuwa siku ya Jumamosi. Hii inalingana na jina "Kwame" ambalo katika utamaduni wa Waakan ni jina la mwanamume aliyezaliwa siku hiyo. Ila tu aliposoma Marekani alijulikana kwa jina la Francis Nwia Kofi Nkrumah na "Kofi" ni jina la mwanamume aliyezaliwa siku ya Ijumaa.
|
20231101.sw_1782_2
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kwame%20Nkrumah
|
Kwame Nkrumah
|
Baba yake, ambaye jina lake halikuhifadhiwa, alikuwa na kazi ya fundi dhahabu. Mama yake aliitwa Nyanibah akaishi hadi kifo chake na kwa muda alitunza kaburi la mwanawe. .
|
20231101.sw_1782_3
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kwame%20Nkrumah
|
Kwame Nkrumah
|
Mtoto alilelewa kijijini pamoja na watoto wengine wa babake na ukoo. Mama alimsomesha katika shule ya msingi ya misioni ya Kanisa Katoliki. . Alipita madarasa kumi katika muda wa miaka minane.
|
20231101.sw_1782_4
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kwame%20Nkrumah
|
Kwame Nkrumah
|
Mnamo 1925 alikuwa Mkristo aliyebatizwa akafundisha katika shule yake kama mwalimu msaidizi. Kutoka hapo alikaribishwa na mchungaji Alec Garden Fraser, mkuu wa chuo cha ualimu cha serikali mjini Accra kujiunga na masomo huko. Huko makamu wa mkuu Kwegyir Aggrey aliyewahi kusoma Marekani alimweleza mafundisho ya Marcus Garvey na W. E. B. Du Bois. Aggrey, Fraser na walimu wengine wa chuo walifundisha ya kwamba ushirikiano wa watu wa rangi zote ni shabaha kwa maendeleo ya Gold Coast. Lakini Nkrumah alifuata mwelekeo wa Marcus Garvey akiamini ya kwamba ni lazima nchi yake itawaliwe na Waafrika wenyewe.
|
20231101.sw_1782_5
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kwame%20Nkrumah
|
Kwame Nkrumah
|
Baada ya kumaliza masomo yake mwaka 1930 Nkrumah aliajiriwa kama mwalimu wa shule ya msingi ya Kikatoliki huko Elmina na baada ya mwaka 1 alikuwa mwalimu mkuu wa shule ya Axim. Huko alianza kushiriki katika majadiliano ya kisiasa akaanzisha "Nzima Literary Society". Mwaka 1933 aliendelea na kuwa mwalimu kwenye seminari ya Kikatoliki mjini Amissa.
|
20231101.sw_1782_6
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kwame%20Nkrumah
|
Kwame Nkrumah
|
Alipokuwa mwanafunzi wa chuo Nkrumah alisikia hotuba ya mwandishi Nnamdi Azikiwe (baadaye alikuwa rais wa Nigeria). Alikutana naye, na Azikiwe alimpa ushauri kuendelea na masomo yake huko Marekani kwenye chuo cha Lincoln College alikowahi kusoma mwenyewe an kilichokuwa chuo kwa Waamerika Weusi. Nkrumah angependelea kusoma London (Uingereza) lakini alishindwa mitihani ya kuingia. Hivyo kwa msaada wa mjomba tajiri alisafiri Pennsylvania na kuanza masomo huko Lincoln kwenye Oktoba 1935..
|
20231101.sw_1782_7
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kwame%20Nkrumah
|
Kwame Nkrumah
|
Hakuwa na pesa nyingi, hivyo alifanya kazi ndogo kama kusafisha vyombo hotelini. Siku za Jumapili alisali katika makanisa ya Weusi mjini Philadelphia na New York. Mwaka 1939 alimaliza masomo akapokea digrii ya bachelor katika fani ya uchumi.
|
Subsets and Splits
No community queries yet
The top public SQL queries from the community will appear here once available.