_id
stringlengths 15
22
| url
stringlengths 31
150
| title
stringlengths 1
86
| text
stringlengths 100
23.8k
|
---|---|---|---|
20231101.sw_1783_82
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ghana
|
Ghana
|
Nchi ya Ghana ina mfumo wa elimu ya msingi wa miaka 6 kuanzia umri wa miaka sita, na, chini ya mageuzi ya elimu yaliyotekelezwa mnamo 1987 na kurekebishwa mnamo 2007, watoto huingia katika mfumo wa miaka mitatu wa elimu ya upili ya daraja la chini.
|
20231101.sw_1783_83
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ghana
|
Ghana
|
Mwishoni mwa mwaka wa tatu katika shule ya upili ya Junior High, kuna mtihani wa lazima unaojulikana kama Basic Education Certificate Examination (BECE).
|
20231101.sw_1783_84
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ghana
|
Ghana
|
Wale wanaoendelea na masomo ni lazima wamalize masomo ya miaka mitatu ya shule ya upili ya daraja ya juu (senior high school - SHS) na kufanya mtihani wa kukubaliwa kuingia katika masomo ya chuo kikuu au taasisi yoyote ile.
|
20231101.sw_1783_85
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ghana
|
Ghana
|
Kwa sasa, Ghana ina shule za msingi 21,530, shule za upili za daraja ya chini 8,850, shule za upili za daraja ya juu 900, vyuo vya mafunzo vya umma, 52, vyuo vya mafunzo vya kibinafsi, 5 vyuo vya elimu ya sanaa, 5 taasisi za umma ambazo si vyuo vikuu, 4 zisizo chuo kikuu Msingi umma taasisi, 8 vyuo vikuu 4 na zaidi ya taasisi za kibinafsi 45.
|
20231101.sw_1783_86
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ghana
|
Ghana
|
Wengi baina ya Waghana wanaweza kupata huduma za elimu ya msingi na ya upili kwa urahisi. Idadi hizi zinaweza kutofautishwa na zile za chuo kikuu kimoja tu na shule chache tu za upili na za msingi zilizokuwepo wakati wa kujinyakulia uhuru mnamo 1957.
|
20231101.sw_1783_87
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ghana
|
Ghana
|
Gharama ya nchi ya Ghana kwa elimu imekuwa kati ya asilimia 28 na 40 ya bajeti yake ya mwaka katika mwongo mmoja uliopita.
|
20231101.sw_1783_88
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ghana
|
Ghana
|
Mafunzo yote hufanywa kwa lugha ya Kingereza ambayo ndiyo lugha rasmi ya Ghana, na hufanywa na walimu Waghana waliohitimu.
|
20231101.sw_1783_89
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ghana
|
Ghana
|
Masomo yanayofunzwa katika Shule ya Msingi au ya Mwanzo ni pamoja na Kingereza, Lugha na Utamaduni wa Ghana, Hisabati, masomo ya masuala ya Mazingira, Masomo ya Kijamii na Kifaransa kama lugha ya tatu, yakiongezwa masomo ya Sayansi Jumuishi au ya Ujumla, masomo ya mwanzo ya Ustadi wa Ufundi (Pre-vocational Skills and Pre-technical skills) Elimu ya Dini na Maadili na shughuli za utendaji kama vile Muziki, Ngoma na Elimu ya Mazoezi ya Viungo.
|
20231101.sw_1783_90
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ghana
|
Ghana
|
Mtaala wa daraja la upili la Senior High una masomo ya Lazima na yale ya Kuchagua. Wanafunzi wanapaswa kuchukua masomo manne ya lazima ya Lugha ya Kingereza, Hisabati, Sayansi ya Ujumla (yakiwemo masomo ya Sayansi, Kilimo na Masomo ya maswala ya Mazingira) na Masomo ya Kijamii (uchumi, jiografia, historia na serikali). Wanafunzi wa shule ya upili vilevile hufanya masomo matatu ya kuchaguliwa kati ya matano yafuatayo: Mtaala wa Kilimo, Mtaala wa Kijumla (chaguo la Sanaa au Sayansi), Mtaala wa somo la Biashara, Mtaala wa Ufundi (Vocational Programme and Technical Programme).
|
20231101.sw_1783_91
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ghana
|
Ghana
|
Mbali na shule za msingi na za upili zinazofuata mfumo wa elimu wa Ghana, kunazo shule za kimataifa kama vile Ghana International school, Lincoln Community School na SOS-Hermann Gmeiner International College ambazo hufuata mfumo wa International Baccalaureat, Advanced Level General Certificate of Education na International General Certificate of Secondary Education (IGCSE).
|
20231101.sw_1783_92
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ghana
|
Ghana
|
Huku ikiwa na asilimia 83 ya watoto wake shuleni, kwa sasa nchi ya Ghana ni baina ya nchi zilizo na viwango vya juu zaidi vya uandikishaji shuleni katika eneo la Afrika Magharibi.
|
20231101.sw_1783_93
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ghana
|
Ghana
|
Uwiano wa wasichana na wavulana katika ujumla wa mfumo wa elimu ni 1:0.96, ambao kwa nchi ya Afrika Magahribi, ni mafanikio makubwa. Kadiri ya watoto 500,000 hawaendi shuleni kwa sababu ya ukosefu wa mapato ya kuwezesha ujenzi wa shule, kutoa vitabu vya kusoma vya kutosha na kutoa mafunzo kwa walimu wapya.
|
20231101.sw_1783_94
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ghana
|
Ghana
|
Chuo Kikuu cha zamani zaidi nchini Ghana, Chuo Kikuu cha Ghana, ambacho kilianzishwa mnamo mwaka wa 1948, kilikuwa na takriban jumla ya wanafunzi 29,754 katika mwaka wa 2008. Tangu unyakuzi wa uhuru wa Ghana, nchi hii imekuwa mojawapo ya vitovu vya elimu katika eneo la Afrika Kusini mwa Sahara na imekuwa mwenyeji wa watu maarufu kama vile Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe, Alhaji Sir Dauda Jawara wa The Gambia na Cyprian Ekwensi wa Nigeria baina ya wengine. Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia cha Kwame Nkrumah, ambacho ndicho chuo kikuu cha pili kuanzishwa nchini Ghana, ndicho chuo cha kwanza cha masomo ya sayansi na teknolojia nchini humo na katika ukanda wa Afrika Magharibi.
|
20231101.sw_1783_95
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ghana
|
Ghana
|
Ikiwa imejaliwa sana na maliasili, nchi ya Ghana ina mapato yanayokadiriwa kupata kila mtu (per capita output) yaliyo mara mbili yakilinganishwa na yale ya nchi zilizo maskini zaidi za Afrika Magharibi. Hata hivyo, Ghana imebakia kutegemea kwa kiwango fulani biashara na usaidizi wa kimataifa na vilevile shughuli za uwekezaji kutokana na Waghana wanaoishi nchi za ng’ambo. Karibu 28% ya wakazi wanaishi chini ya mstari wa kimataifa wa umaskini wa dola za kimarekani 1.25 kwa siku, na kwa mujibu wa wa Benki ya Dunia, kisio la mapato ya kila mtu (per capita income) ya Ghana yamekuwa mara dufu lakini kwa shida kwa miaka 45 iliyopita.
|
20231101.sw_1783_96
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ghana
|
Ghana
|
Nchi ya Ghana, ikijulikana kwa dhahabu yake katika enzi za ukoloni, bado ni kati ya wazalishaji wakuu ulimwenguni wa dhahabu. Mauzo yake mengine nje ya nchi kama vile kakao, mbao, umeme, almasi, bauxiti, na manganisi ni uzalishaji mkuu wa fedha za kigeni. Kiwanja cha mafuta kinachoripotiwa kuwa na hadi pipa bilioni 3 (480,000,000 m3 za mafuta mepesi kiligunduliwa mnamo mwaka wa 2007. Utafutaji wa mafuta bado unaendelea na kiasi cha mafuta kinaendelea kuongezeka.
|
20231101.sw_1783_97
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ghana
|
Ghana
|
Bwawa la Akosombo, ambalo lilijengwa juu ya Mto Volta mnamo mwaka wa 1965 linatoa umeme unaozalishwa na maji kwa nchi ya Ghana na nchi zinazoizunguka.
|
20231101.sw_1783_98
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ghana
|
Ghana
|
Nguvukazi ya Ghana katika mwaka wa 2008 ilikuwa jumla ya watu milioni 11.5. Uchumi unaendelea kutegemea sana kilimo ambacho huchangia 37% ya Pato la Taifa na kutoa ajira kwa kwa 56% ya watu wanaofanya kazi, hasa wenye ardhi ndogo. Sekta ya viwanda ni sehemu ndogo tu ya uchumi wa Ghana iliyochangia kwa ujumla 7.9% ya Pato la Taifa mnamo 2007.
|
20231101.sw_1783_99
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ghana
|
Ghana
|
Sera za kiuchumi zisizofaa za serikali za kijeshi zilizopita na masharti ya vikosi vya kulinda usalama katika maeneo ya kanda vimechangia mfumuko katika fedha za nakisi, kushuka thamani kwa Sidi, na kuongezeka kwa kutoridhika kwa umma katika maswala ya hatua za kupunguza ugumu wa maisha. Hata hivyo, Ghana inabakia kuwa mojawapo baina ya nchi za Afrika nzima ambazo zina ustawi wa kiuchumi.
|
20231101.sw_1783_100
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ghana
|
Ghana
|
Mnamo Julai 2007, Benki ya Ghana ilianzisha shughuli ya kugeuza sarafu, kutoka kwa Sidi (¢) hadi kwa sarafu mpya, Sidi ya Ghana (GH¢). Kiwango cha ubadilishanaji ni Sidi moja ya Ghana kwa kila Sidi 10,000. Benki ya Ghana ilizindua kampeni kabambe katika vyombo vya habari ili kuelimisha umma juu ya mageuzo haya.
|
20231101.sw_1783_101
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ghana
|
Ghana
|
Sarafu mpya ya Sidi ya Ghana iko imara kwa kiwango kikubwa na katika mwaka wa 2008 ilibadilishwa kwa ujumla kwa thamani ya dola moja ya marekani kwa Sidi 1.1 ya Ghana.
|
20231101.sw_1783_102
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ghana
|
Ghana
|
Kodi ya Ongezeko la Thamani ni kodi ya matumizi itozwayo nchini Ghana. Utaratibu huu wa kodi ambao ulianza mnamo 1998 ulikuwa wa kiwango kimoja lakini tangu Septemba 2007 utaratibu wa viwango kadhaa ulizinduliwa.
|
20231101.sw_1783_103
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ghana
|
Ghana
|
Mnamo 1998, kiwango cha kodi kilikuwa ni 10% na na kilirekebishwa mnamo mwaka wa 2000 na kuwa 12.5%. Hata hivyo baada ya kupitishwa kwa Sheria ya 734 (Act 734) ya mwaka 2007, kodi ya usawa ya 3% (a 3% VAT Flat Rate Scheme (VFRS) ) ilianza kufanya kazi kwa sekta ya usambazaji wa rejareja. Hii inawezesha wauzaji wa rejareja wa bidhaa zinazotozwa ushuru chini ya Sheria ya 546 (Act 546) kotoza ushuru wa pambizoni wa 3% kwa mauzo yao na kuhesabu ushuru huu pamoja na ule wa VAT. Hii inanuia kurahisisha utaratibu wa uchumi na kuongezeka kwa maafikiano.
|
20231101.sw_1783_104
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ghana
|
Ghana
|
Tovuti ya African Activist Archive Project ina picha za mkutano wa All Africa People's Conference uliofanyika Accra, Ghana, 5-13 Desemba 1958 ikiwemo ile ya Kwame Nkrumah, Waziri Mkuu wa Ghana , akiuhutubia mkutano, ujumbe wa American Committee on Africa ukikutana na Nkrumah, na ya Patrick Duncan na Alfred Hutchinson wa Afrika Kusini katika mkutano huo.
|
20231101.sw_1788_0
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Carola%20Kinasha
|
Carola Kinasha
|
Carola Daniel Amri Kinasha (alizaliwa Longido, Mkoa wa Arusha, Tanzania, mnamo Machi mwaka 1962) ni mwanamuziki wa kike wa kitanzania.
|
20231101.sw_1788_1
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Carola%20Kinasha
|
Carola Kinasha
|
Baada ya kumaliza masomo ya elimu ya msingi huko Longido, alihamia jijini Dar Es Salaam ambako alipata elimu ya sekondari na ya chuo kikuu katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Carola amekuwa akijihusisha na masuala ya muziki tangu mwaka wa 1988.
|
20231101.sw_1788_2
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Carola%20Kinasha
|
Carola Kinasha
|
Ameshiriki katika miradi na matamasha mbalimbali ya kimuziki, ndani na nje ya Tanzania.Pia amekuwa mtetezi wa haki za binadamu kwa ujumla akiweka msisitizo zaidi kwenye haki za wasanii wa Tanzania. Anaamini kuwa ili tasnia ya sanaa ya Tanzania iweze kukua na kujulikana kimataifa ni muhimu kurejesha elimu ya sanaa kwenye shule zetu. Pia kuwa na sehemu za kufanyia shughuli za sanaa kwenye kila kitongoji.
|
20231101.sw_1789_0
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Wikipedia
|
Wikipedia
|
Wikipedia ni kamusi elezo huru ya lugha nyingi katika mtandao wa wavuti. Inalenga kukusanya elimu nyingi iwezekanavyo na kuisambaza kwa njia ya intaneti.
|
20231101.sw_1789_1
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Wikipedia
|
Wikipedia
|
Inatumia taratibu za wikiwiki. Ni bure kabisa, na inaweza kusomwa, kuandikwa, na kuhaririwa na mtu yeyote, popote pale. Yaani kila mtu anaweza kuchangia makala akiwa na uhuru wa kuboresha makala zilizopo kwa kuzihariri.
|
20231101.sw_1789_2
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Wikipedia
|
Wikipedia
|
Kamusi hii inajengwa kwa utaratibu huria ambao unategemea falsafa ya ushirikiano ambako watu wengi hushirikiana kwa kujitolea bila kupokea malipo yoyote.
|
20231101.sw_1789_3
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Wikipedia
|
Wikipedia
|
Falsafa hii inaonekana katika vuguvugu la programu huria ya tarakilishi, mikutano huria, demokrasia huria, n.k.
|
20231101.sw_1789_4
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Wikipedia
|
Wikipedia
|
Wikipedia imeshachukua nafasi za kamusi elezo mashuhuri kama Encyclopedia Britannica zilizotazamwa kuwa mkusanyo wa elimu ya Dunia kabla ya kutokea kwa intaneti. Kwa lugha za Kiafrika kama Kiswahili ni mara ya kwanza ya kwamba jaribio la kukusanya elimu za fani mbalimbali limeanzishwa.
|
20231101.sw_1789_5
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Wikipedia
|
Wikipedia
|
Hadi mwaka 2018 wachangiaji wa Wikipedia walishirikiana kuunda zaidi ya makala milioni 47 kwa lugha 300.
|
20231101.sw_1789_6
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Wikipedia
|
Wikipedia
|
Wikipedia kubwa zenye makala zaidi ya milioni mbili zilikuwa kwenye Novemba 2018: Wikipedia ya Kiingereza (makala 5,758,502), ya Kicebuano (makala 5,379,917), ya Kiswidi (makala 3,764,225), ya Kijerumani (2,243,097) na ya Kifaransa (makala 2,060,362). Kwa jumla kulikuwa na Wikipedia zenye zaidi ya makala milioni moja kwa lugha 15.
|
20231101.sw_1789_7
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Wikipedia
|
Wikipedia
|
Kisheria maudhui yote ya Wikipedia si mali ya mtu yeyote kwa kuwa ni maudhui huria. Seva za wikipedia na programu zake zinatunzwa na taasisi ya Wikimedia Foundation ambayo ni shirika lisilo la kiserikali lililoandikishwa chini ya sheria za jimbo la Kalifornia, Marekani. Taasisi hii inapokea mapato yote kutoka kwa wafadhili wa kujitolea kote duniani.
|
20231101.sw_1789_8
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Wikipedia
|
Wikipedia
|
Katika nchi mbalimbali kuna shirika za kitaifa zinazojumuisha wanawikipedia ama kwa umbo la taasisi au kwa umbo la makundi ya watumiaji (Wikimedia User Groups).
|
20231101.sw_1789_9
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Wikipedia
|
Wikipedia
|
Nchini Tanzania kuna kundi la Wikimedia Community User Group Tanzania. Kundi la Jenga Wikipedia ya Kiswahili ni jumuiya ya wachangiaji kutoka nchi mbalimbali wanaoangalia maendeleo ya Wikipedia ya Kiswahili.
|
20231101.sw_1790_0
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Dar%20es%20Salaam
|
Dar es Salaam
|
Dar es Salaam ni jiji kubwa kuliko yote nchini Tanzania. Pia ni jina la mkoa wake. Dar es Salaam ni mji mkongwe na wenye watu wengi zaidi katika Jumuia ya Afrika Mashariki. Katika Tanzania ndio mji wenye vitega uchumi vingi na ndio mji unaoangaliwa na watu wengi.
|
20231101.sw_1790_1
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Dar%20es%20Salaam
|
Dar es Salaam
|
Ni mji mkuu wa kibiashara wa Tanzania wakati Dodoma ni mji mkuu wa Tanzania (kinadharia tangu mwaka 1973). Mpango wa kuhamishia serikali mjini Dodoma unaendelea kwa kasi chini ya rais John Magufuli, japokuwa bado ofisi kadhaa za serikali, ikiwa ni pamoja na Ikulu, zipo Dar es Salaam.
|
20231101.sw_1790_2
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Dar%20es%20Salaam
|
Dar es Salaam
|
Surah Al-Anam (Korani 6:127) ina maneno لَهُمْ دَارُ السَّلَامِ عِندَ رَبِّهِمْ lahum dāru as-salāmi `inda rabbihim yanayomaanisha "Hao watapata nyumba ya salama kwa Mola Mlezi wao." . Jina linafanywa na maneno mawili ya Kiarabu; دار dar inayomaanisha "nyumba, jengo, makazi, eneo", "es" ni silabi ya kuunganisha sehemu za jina linalounganishwa na maneno mawili, سلام salaam inamaanisha "amani, raha, usalama".
|
20231101.sw_1790_3
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Dar%20es%20Salaam
|
Dar es Salaam
|
Mara nyingi jina limetafsiriwa kama "Bandari ya Amani" lakini hii ni kosa kutokana na kuchanganya maneno ya Kiarabu دار "dar" (nyumba) na بندر "bandar" (bandari) maana kwa matamshi ya Kiswahili tofauti ya tahajia katika Kiarabu haitambuliki.
|
20231101.sw_1790_4
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Dar%20es%20Salaam
|
Dar es Salaam
|
Jina la Daressalaam limetumiwa kwa maumbo tofauti kwa mahali mbalimbali katika mazingira ya Kiislamu, kwa mfano huko Brunei Darussalaam, Dar El Salam (Misri), Dar os Salam (Iran), pia kama majina ya taasisi mbalimbali.
|
20231101.sw_1790_5
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Dar%20es%20Salaam
|
Dar es Salaam
|
Jiji hili zamani lilikuwa kijiji na kuitwa Mzizima. Sultani Seyyid Majid wa Zanzibar aliamua kujenga ikulu ya pili barani kando la Mzizima akachagua jina "Dar es Salaam". Hadi leo kuna majengo mawili yaliyobaki ya vyanzo hivi ambayo ni Boma la Kale na Nyumba ya Atiman House.
|
20231101.sw_1790_6
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Dar%20es%20Salaam
|
Dar es Salaam
|
Dar es Salaam ilichaguliwa na wakoloni Wajerumani kuwa mji mkuu wa Afrika ya Mashariki ya Kijerumani kwa sababu ya bandari asilia yenye mdomo mpana wa mto Kurasini. Hivyo kuanzia mwaka 1891 Dar es Salaam ilichukua nafasi ya Bagamoyo kama makao makuu ya utawala.
|
20231101.sw_1790_7
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Dar%20es%20Salaam
|
Dar es Salaam
|
Bandari pamoja na ujenzi wa reli ya kati kwenda Kigoma tangu mwaka 1904 viliimarisha nafasi ya mji ulioendelea kama mji mkuu baada ya Tanzania bara ya leo kuwa eneo lindwa la Tanganyika chini ya Uingereza.
|
20231101.sw_1790_8
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Dar%20es%20Salaam
|
Dar es Salaam
|
Utawala wa Dar es Salaam uliona mabadiliko kadhaa ambapo mwanzoni mji ulitawaliwa na halmashauri yake na baadaye serikali ya kitaifa ilichukua utawala mikononi mwake au kuukabidhi kwa tume ya serikali.
|
20231101.sw_1790_9
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Dar%20es%20Salaam
|
Dar es Salaam
|
Mwaka 2000 eneo la jiji liligawanywa kwa mamlaka tofauti ambazo mwanzoni zilikuwa nne, ambazo zilikuwa manisipaa za Ilala, Temeke na Kinondoni. Baadaye Ubungo na Kigamboni zilikuwa manisipaa za pekee, kila moja na halmashauri yake. Kwa jiji lote Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam iliundwa. Kwa hiyo hadi 2021 Dar es Salaam ilikuwa na Halmashauri 6.
|
20231101.sw_1790_10
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Dar%20es%20Salaam
|
Dar es Salaam
|
Kwenye Februari 2021 Halmashauri ya Dar es Salaam ilivunjwa na serikali, na Ilala ilibadilishwa jina kuwa Dar es Salaam.
|
20231101.sw_1790_11
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Dar%20es%20Salaam
|
Dar es Salaam
|
Dar es Salaam inakadiriwa kuwa na wakazi wapatao milioni tatu. Ingawa Dodoma inafahamika kama ndio mji mkuu wa Tanzania, Dar es Salaam ndiko ziliko ikulu, mabalozi, mashirika ya kimataifa, n.k.
|
20231101.sw_1790_12
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Dar%20es%20Salaam
|
Dar es Salaam
|
Uwanja wa ndege mkuu wa Tanzania uko pia mjini hii ni Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere.
|
20231101.sw_1790_13
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Dar%20es%20Salaam
|
Dar es Salaam
|
Bandari ya Dar es Salaam katika bahari ya Hindi, ndio bandari kubwa nchini Tanzania inayojihusisha na usafirishaji na uingizaji wa bidhaa mbalimbali za kilimo, ufugaji, ujenzi, magari, madawa, n.k.
|
20231101.sw_1790_14
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Dar%20es%20Salaam
|
Dar es Salaam
|
Kiutawala, Dar es Salaam imegawanywa katika manisipaa za Temeke, Ilala, Kinondoni, Kigamboni na Ubungo.
|
20231101.sw_1790_15
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Dar%20es%20Salaam
|
Dar es Salaam
|
Dar es Salaam ni mji unaosemekana kuwa mkubwa kuliko yote kwa sababu ya maendeleo mbalimbali ya viwanda, uwepo wa bahari, uwepo wa sehemu mbalimbali za kihistoria n.k.
|
20231101.sw_1790_16
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Dar%20es%20Salaam
|
Dar es Salaam
|
Huduma ya maji Dar es Salaam imekuwa na tatizo kubwa katika kudhibiti mfumo wa maji taka katika mkoa wa Dar es Salaam kwa muda mrefu. Tangu shirika la maji DAWASCO (Dar es Salaam Water Supply Company) lilipowekwa rasmi kama shirika husika katika kuratibu utaratibu mzima wa mfumo wa maji safi na maji taka, kumekuwa na nafuu kidogo tu, lakini baada ya muda, liliibuka tatizo la kuibiwa kwa mabomba na uharibifu wa vyanzo mbalimbali vya maji.
|
20231101.sw_1790_17
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Dar%20es%20Salaam
|
Dar es Salaam
|
Kwenye suala hili la elimu vijana wanatakiwa kupewa elimu; hasa vijana wa mitaani wasioingiza kipato inabidi wapewe elimu kwa kazi fulani ili waweze kuajiriwa na kulipa faida taifa kwa kuingizia kipato na kukuza uchumi wa taifa. Mfano wa kazi hizo ni kama ujenzi wa nyumba n.k.
|
20231101.sw_1790_18
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Dar%20es%20Salaam
|
Dar es Salaam
|
Mohamed Said: Mwalimu in 1950s Dar (East African October 12 2008 - inasimulia maisha ya Nyerere Dar es Salaam pamoja na habari nyingi za jiji wakati wa miaka ya 1950)
|
20231101.sw_1791_0
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Bahari%20ya%20Hindi
|
Bahari ya Hindi
|
Bahari ya Hindi ni bahari ya tatu kwa ukubwa duniani ikiwa imechukua asilimia 20 ya uso wa dunia na kuzungukwa na mabara manne.
|
20231101.sw_1791_1
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Bahari%20ya%20Hindi
|
Bahari ya Hindi
|
Upande wa kaskazini imepakana na Asia ya Kusini; magharibi imepakana na Ghuba ya Uajemi, Bahari ya Shamu na Afrika; mashariki imepakana na Ghuba ya Malay, visiwa vya Sunda (Indonesia), na Australia; na upande wa kusini imepakana na Bahari ya Kusini.
|
20231101.sw_1791_2
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Bahari%20ya%20Hindi
|
Bahari ya Hindi
|
upande wa magharibi (Atlantiki) ni mstari unaoelekea kusini kutoka Rasi Agulhas (Afrika Kusini) kwenye longitudo ya 20° mashariki
|
20231101.sw_1791_3
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Bahari%20ya%20Hindi
|
Bahari ya Hindi
|
upande wa mashariki ni mstari unaoelekea kusini kutoka sehemu ya kusini zaidi cha Tasmania (Australia) kwenye longitudo ya 146°55'E
|
20231101.sw_1791_4
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Bahari%20ya%20Hindi
|
Bahari ya Hindi
|
upande wa kusini imeamuliwa kutumia latitudo ya 60°S kama mpaka wa Bahari Hindi na Bahari ya Kusini inayozunguka bara la Antaktiki.
|
20231101.sw_1791_5
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Bahari%20ya%20Hindi
|
Bahari ya Hindi
|
Kwa hiyo eneo lote la uso wa bahari hii ni kilomita za mraba 70,560,000 km²; kina cha wastani ni mita 3,741 ilhali kina kikubwa kinafikia mita 7,906. Mjao wake ni kilomita za ujazo 264,000,000 km³ inayolingana na asilimia 19.8% ya mjao wa bahari zote duniani.
|
20231101.sw_1791_6
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Bahari%20ya%20Hindi
|
Bahari ya Hindi
|
Kama kawaida, pale ambako mabamba yanaachana kuna nafasi inayoruhusu kupanda juu kwa joto na magma kutoka kiini cha dunia na kutokea kwa volkeno pamoja na safu za milima chini ya maji.
|
20231101.sw_1791_7
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Bahari%20ya%20Hindi
|
Bahari ya Hindi
|
Tetemeko la ardhi na tsunami ya 2004, iliyosababisha uharibifu na vifo katika sehemu za kaskazini za Bahari Hindi, ilisababishwa na mwendo wa ghafla la bamba la Australia juu ya bamba la Uhindi.
|
20231101.sw_1791_8
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Bahari%20ya%20Hindi
|
Bahari ya Hindi
|
Kwa jumla Bahari Hindi ina halijoto ya juu kulingana na bahari kubwa nyingine za dunia. Tofauti na Atlantiki na Pasifiki haina maeneo makubwa kwenye nusutufe ya kaskazini ya dunia hivyo haipokei baridi kutoka Aktiki.
|
20231101.sw_1791_9
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Bahari%20ya%20Hindi
|
Bahari ya Hindi
|
Upande wa kazkazini wa ikweta kuna monsuni; upepo kutoka kazkazini-mashariki uko kuanzia Oktoba hadi Aprili, kinyume chake upepo kutoka kusini unaendelea kuanzia Mei hadi Oktoba. Badiliko hili linafuata utaratibu wa kila mwaka na lilikuwa msingi kwa usafiri na biashara katika bahari hii maana iliwezekana kutumia upepo kwa jahazi tangu kale.
|
20231101.sw_1791_10
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Bahari%20ya%20Hindi
|
Bahari ya Hindi
|
Wakati wa badiliko la monsuni dhoruba kali zinaweza kutokeas hasa katika Bahari ya Uarabuni na Hori ya Bengali.
|
20231101.sw_1791_11
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Bahari%20ya%20Hindi
|
Bahari ya Hindi
|
Israel na Jordani (kupitia Ghuba ya Akaba na Bahari ya Shamu), Ufalme wa Uarabuni wa Saudia, Yemen, Omani, Falme za Kiarabu, Qatar, Kuwait, Iraq, Iran, Pakistan, India, Bangladesh, Myanmar, Uthai, Malaysia, Indonesia na Timor ya Mashariki.
|
20231101.sw_1791_12
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Bahari%20ya%20Hindi
|
Bahari ya Hindi
|
Afrika Kusini, Msumbiji, Tanzania, Kenya, Somalia, Jibuti, Eritrea, Sudani na Misri (kupitia Bahari ya Shamu).
|
20231101.sw_1791_13
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Bahari%20ya%20Hindi
|
Bahari ya Hindi
|
Ndani ya Bahari Hindi kuna mataifa huru ambayo ni nchi za visiwani pamoja na Bahrain (Ghuba ya Uajemi), Komori, Madagaska, Maldivi, Morisi, Shelisheli na Sri Lanka.
|
20231101.sw_1791_14
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Bahari%20ya%20Hindi
|
Bahari ya Hindi
|
Agalega, Anjouan, Bahrain, Cargados Carajos, Visiwa vya Cocos (Keeling), Diego Garcia, Kilwa Kisiwani, Kirimba (visiwa), Kisiwa cha Mafia, Komori, Kisiwa cha Krismasi, Lamu (kisiwa), Morisi, Madagaska, Mahore, Mahé, Maskarena, Mayotte, Moheli, Msumbiji (kisiwa), Mwali, Ngazija, Pamanzi, Pate, Pemba (kisiwa), Rodrigues (kisiwa), Réunion, Shelisheli, Sokotra, Unguja, Îles Éparses,
|
20231101.sw_1792_0
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Nairobi
|
Nairobi
|
Jina Nairobi limetokana na neno la Kimaasai, Enkarenairobi, linalomaanisha "mahali penye maji baridi."
|
20231101.sw_1792_1
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Nairobi
|
Nairobi
|
Nairobi yenyewe iko ndani ya eneo la jiji la Nairobi (kwa Kiingereza: Greater Nairobi Metropolitan region) lililoundwa na kaunti 4 kati ya jumla ya 47 za Kenya.
|
20231101.sw_1792_2
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Nairobi
|
Nairobi
|
Nairobi iko kilomita 150 upande wa kusini ya ikweta kwenye nyanda za juu za Kenya kando la mto Nairobi. Nairobi imeanzishwa mahali ambako nchi tambarare ya mto Athi inaanza kupanda juu hadi milima ya Ngong na vilima vingina vinyvyofanya ukuta wa mashariki wa Bonde la Ufa.
|
20231101.sw_1792_3
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Nairobi
|
Nairobi
|
Kitovu cha Nairobi kiko zipatao m 1624 juu ya UB. Sehemu za mashariki za jiji ziko bado kwenye tambarare, na sehemu za magharibi ziko kwenye mtelemko unaopanda hadi mita 1800 kwenye mpaka wa jiji na mita 2000 juu ya UB kwenye nje ya jiji huko Limuru.
|
20231101.sw_1792_4
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Nairobi
|
Nairobi
|
Hali ya hewa haina joto kali. Halijoto ya wastani ni 20,5°C mwezi wa Machi, na 16,8°C mwezi wa Julai. Wakati wa Juni na Julai usiku unaweza kuwa baridi halijoto ikishuka chini ya sentigredi 10.
|
20231101.sw_1792_5
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Nairobi
|
Nairobi
|
Nairobi ilianzishwa na Waingereza mwaka 1899 kama kambi ya kujenga Reli ya Uganda. Njia ya reli ilikuwa imefika kutoka Mombasa ikaonekana ya kwamba kuanzia hapa kasi ya ujenzi itachelewa kutokana na ugumo na eneo la Bonde la Ufa na mitelemko yake mikali. Mahali palikuwa karibu katikati ya Mombasa na Kampala, palikuwa na maji pakaonekana panafaa kwa kituo njiani. Hasahasa ilionekana tabianchi ya nyanda za juu ilifaa kiafya kwa Waingereza walioteswa na joto la pwani na kwenye nyanda za chini.
|
20231101.sw_1792_6
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Nairobi
|
Nairobi
|
Kitangulizi cha Nairobi kilikuwa kituo kidogo kilichoanzishwa mwaka 1896 kando ya mto Nairobi na wakala Mwingereza wa reli kwa kusudi la kuajiri wafanyakazi wazalendo kwa ujenzi wa reli. Mwaka uliofuata 1897 wakaguzi walioandaa njia ya reli walipiga kambi karibu naye. .
|
20231101.sw_1792_7
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Nairobi
|
Nairobi
|
Njia ya reli ilifika kwenye kambi tarehe 30 Mei 1899. Hapo idadi ya wafanyakazi - hasa Wahindi - iliongezeka sana na kambi lilikuwa kubwa ya mahema na ghala za vifaa vya ujenzi. Mwezi wa Juni mizigo ya mabati ilifika kutoka Mombasa - tayari kwa reli - na majengo ya kudumu yalianza kutengenezwa katika mazingira ya eneo la kituo cha reli cha leo. Mwezi wa Agosti kamishna Mwingereza wa jimbo la Ukamba aliamuliwa kuhamisha makao makuu yake Nairobi kutoka Machakos akajenga boma lake kwenye eneo la Moi Avenue, mbali na reli jinsi inavyoonekana hadi leo kwenye majengo ya polisi ya kihistoria yanayotazama Bustani ya Jivanji.
|
20231101.sw_1792_8
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Nairobi
|
Nairobi
|
Barabara kuu ya kwanza ilikuwa "Station Road" kandokando ya Mtaa wa Tom Mboya wa leo iliyoitwa Victoria Street ikawa mahali pa maduka na hoteli za kwanza zilizoendeshwa na Wazungu na baadaye pia na Wahindi kadhaa. Soko la Wahindi maskini likuwa kando. Kwenye sehemu kati ya mitaa ya Haile Selassie na Harambee kulikuwa na makazi ya kwanza ya wafanyakazi. Mwaka uleule wa 1899 ofisi kuu ya reli ikapelekwa huko kutoka Mombasa kwa shabaha ya kurahisisha mawasiliano.
|
20231101.sw_1792_9
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Nairobi
|
Nairobi
|
Pale mwanzoni kulikuwa na wasiwasi kuhusu chaguo la mahali; baada ya mvua kali sehemu ya mahema na vibanda vilipatikana katikati ya ziwa la matope. Magonjwa yalisambaa na baada ya epidemia ya tauni soko la Wahindi Lilichomwa na kuhamishwa sehemu nyingine. Majaribio ya kukausha kinamasi yaliendelea kwa miaka kadhaa hadi kufaulu. Kutokana na usumbufu wa matope maafisa wa ngazi ya juu walijenga nyumba zao kwenye kilima cha karibu kilichojulikana kama Nairobi Hill.
|
20231101.sw_1792_10
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Nairobi
|
Nairobi
|
Mwaka 1905 Waingereza walihamisha ofisi kuu ya serikali yao ya kikoloni kutoka Mombasa kwenda Nairobi, ambayo ikawa hivyo makao makuu ya Afrika ya Mashariki ya Kiingereza (British East Africa, baadaye Kenya Colony).
|
20231101.sw_1792_11
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Nairobi
|
Nairobi
|
Uchumi wa mji ulitegemea pale mwanzoni hasahasa mahitaji ya utawala wa serikali na reli na utalii; matajiri wengi kutoka pande zote za dunia waliFIka kwa kusudi la kuwinda wanyama wakubwa wakivutwa na wingi wa wanyama kwenye nyanda za juu na usafiri rahisi kwa reli. Baadaye ardhi katika mazingira ya mji ilitolewa kwa walowezi Wazungu na kilimo cha biashara kilianza kuchangia.
|
20231101.sw_1792_12
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Nairobi
|
Nairobi
|
Kiasili Nairobi ilikuwa imepangwa kwa ajili ya Wazungu wa reli na serikali pamoja na Wahindi; Waafrika hawakupewa makazi isipokuwa mabweni ya wanfanyakazi wa reli na vibanda vya wafanyakazi wasaidizi kandokando ya nyumba za mabwana wao.
|
20231101.sw_1792_13
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Nairobi
|
Nairobi
|
Lakini Waingereza waliajiri askari kutoka Sudan na Somalia katika jeshi na polisi, na hao walifuatwa na wafanyabiashara kutoka kwao. Wapagazi na askari kutoka sehemu mbalimbali za Afrika ya Mashariki walifika Nairobi kikazi na wengine waliamua kubaki. Mitaa ya vibanda iliota haraka nje ya mji wenyewe, mingine ilibomolewa haraka, mingine iliweza kubaki. Mnamo 1921 kulikuwa na Waafrika 12,000 waliokaa katika mitaa ya Waafrika iliyoitwa Mombasa, Masikini, Kaburini, Kariokor, Kibera, Pumwani na Pangani.
|
20231101.sw_1792_14
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Nairobi
|
Nairobi
|
Nairobi imeibuka kuwa mmojawapo kati ya miji mikubwa katika bara la Afrika. Mashirika mengi makubwa duniani yamefungua ofisi zao zinazoshuhudia eneo la Afrika ya Mashariki na Afrika ya Kati. Mojawapo ya mashirika haya ni ofisi za tawi la Umoja wa Mataifa (United Nations), UNEP. Kunazo pia ofisi za mabalozi wa nchi mbalimbali duniani.
|
20231101.sw_1792_15
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Nairobi
|
Nairobi
|
Nairobi, kama miji mingi mikubwa, ina matatizo mengi yanayotokea kwa sababu ya ukubwa wake. Watamaduni walioupanga mji wa Nairobi hawakutegemea kuwa utatanuka hivyo. Wataalamu wengi wametoa maonyo mengi kuhusu ukubwa wa mji huu na uwezo wake wa kuwahudumia wakazi wote ambao wanazidi kuongezeka kila mwaka.
|
20231101.sw_1792_16
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Nairobi
|
Nairobi
|
Nairobi imewavutia wakazi wengi, wote wakiwa na hamu ya kujitafutia riziki yao. Ijapokuwa wapo wanaofanikiwa, wengi wao hujipata wameangulia patupu wakaachwa bila pesa au hali ya kujikimu. Jambo hili limepelekea kuwepo kwa wakazi wa maeneo yasiyotengwa wananchi, maarufu kama 'slums' kwa Kimombo. Eneo kubwa zaidi jijini Nairobi ni Kibera. Eneo hili lina ukubwa wa kilomita 2 kwa 2 na wakazi takribani milioni moja. Eneo hili halina mipango yoyote ya kuruhusu binadamu kuishi lakini umaskini umewavutia wengi kuishi kule.
|
20231101.sw_1792_17
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Nairobi
|
Nairobi
|
Kunayo pia matatizo ya ujambazi na utekaji nyara wa magari. Matatizo haya yamesababisha watu wengi kutoupendelea mji wa Nairobi.
|
20231101.sw_1792_18
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Nairobi
|
Nairobi
|
Red Strangers: The White Tribe of Kenya, by Christine Stephanie Nicholls, Timewell Press, 2005 (via google books, imetazamiwa Aprili 2
|
20231101.sw_1797_0
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Bara%20la%20Antaktiki
|
Bara la Antaktiki
|
Antaktiki ni bara lililopo kwenye ncha ya kusini ya dunia, kati ya bahari za Pasifiki, Atlantiki na Bahari Hindi.
|
20231101.sw_1797_1
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Bara%20la%20Antaktiki
|
Bara la Antaktiki
|
Jina "Antaktiki" linatokana na lugha ya Kigiriki likimaanisha "kinyume cha Aktiki", ambapo Aktiki ni eneo karibu na ncha ya kaskazini.
|
20231101.sw_1797_2
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Bara%20la%20Antaktiki
|
Bara la Antaktiki
|
Bara hili lina eneo la kilomita za mraba milioni 14 na eneo hili limefunikwa karibu kabisa, yaani kwa asilimia 98% za eneo na theluji na barafu. Eneo lake ni kubwa kushinda Ulaya lakini hakuna mti hata mmoja. Bara hili linajulikana kama jangwa baridi.
|
20231101.sw_1797_3
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Bara%20la%20Antaktiki
|
Bara la Antaktiki
|
Kwa sababu ya baridi kali katika bara hilo, ni bara pekee ambako binadamu hawaishi kwa namna ya kudumu, isipokuwa kuna watu 5,000, hasa wanasayansi, wanaokaa kwa muda katika vituo vyao.
|
20231101.sw_1797_4
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Bara%20la%20Antaktiki
|
Bara la Antaktiki
|
Bara la Antaktiki halikujulikana hadi karne ya 19, lakini wataalamu wa jiografia waliwahi kuhisi tangu zama za kale ya kwamba eneo kubwa la nchi kavu liko kwenye sehemu ya kusini ya dunia.
|
20231101.sw_1797_5
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Bara%20la%20Antaktiki
|
Bara la Antaktiki
|
Kuanzia Aristoteli wataalamu waliamini ya kwamba dunia ilipaswa kuwa na uwiano fulani, hivyo kuwepo kwa bara kubwa ingekuwa lazima kulingana na mabara ya nusutufe ya kaskazini. Nchi hii isiyojulikana kwa muda mrefu ikaitwa kwa jina la Kilatini "terra australis" yaani "nchi ya kusini" na pia kuchorwa kwenye ramani za dunia zilizoanza kutengenezwa tangu safari za wavumbuzi Wareno waliozunguka dunia nzima kwa mara ya kwanza. Ila tu ramani hizi za kwanza zilikuwa kama njozi tu.
|
20231101.sw_1797_6
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Bara%20la%20Antaktiki
|
Bara la Antaktiki
|
Kundi la kwanza la watu kufika kusini kwa kutosha na kuona kona ya barafu ya Antaktiki lilikuwa mwaka 1820 msafara wa kisayansi wa nahodha Fabian von Bellingshausen (Mjerumani Baltiki katika utumishi wa Tsar wa Urusi) akifuatwa mwaka uleule na nahodha Edward Bransfield wa Uingereza na tena Mmarekani Nathaniel Palmer.
|
20231101.sw_1797_7
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Bara%20la%20Antaktiki
|
Bara la Antaktiki
|
Pamoja na taarifa za mabaharia wengine waliopita kwenye pwani bado haikueleweka kama huko karibu na ncha ya kusini kulikuwa na visiwa mbalimbali au nchi kavu kubwa zaidi.
|
20231101.sw_1797_8
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Bara%20la%20Antaktiki
|
Bara la Antaktiki
|
Ni misafara ya Wafaransa na Wamarekani mnamo mwaka 1840 iliyoweza kuthibitisha ya kwamba ncha ya kusini ilipatikana ndani ya bara jipya. Sasa shauku ya upelelezi ilififia kwa sababu haikueleweka kuna nini katika bara jipya.
|
20231101.sw_1797_9
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Bara%20la%20Antaktiki
|
Bara la Antaktiki
|
Tangu mwaka 1890 Shirika la Kifalme la Jiografia (Royal Geographic Society) nchini Uingereza lilianza upya kusisitiza umuhimu wa utafiti wa Antaktiki iliyokuwa sehemu ya mwisho wa dunia isiyochunguliwa bado kabisa. Hapo misafara mbalimbali kutoka nchi tofauti ilifuatana na kupeleleza Antaktiki:
|
20231101.sw_1797_10
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Bara%20la%20Antaktiki
|
Bara la Antaktiki
|
Mwaka 1910 misafara miwili kutoka Norwei na Uingereza ilishindana kufika ncha ya kusini ya kijiografia. Mnorwei Roald Amundsen alikuwa wa kwanza kufika nchani tarehe 14 Disemba 1910 akarudi salama kwa meli yake. Kundi la Mwingereza Robert Scott likachelewa siku 33 likakuta bendera ya Norwei na hema la Amundsen. Kwenye njia ya kurudi Scott alikuta hali ya hewa mbaya akaishiwa chakula chote akafa pamoja na wenzake katika barafu.
|
Subsets and Splits
No community queries yet
The top public SQL queries from the community will appear here once available.