_id
stringlengths
15
22
url
stringlengths
31
150
title
stringlengths
1
86
text
stringlengths
100
23.8k
20231101.sw_1782_8
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kwame%20Nkrumah
Kwame Nkrumah
Chuo kikampa nafasi ya mhadhiri msaidizi kwa masomo ya falsafa akaendelea kusoma teolojia akachukua BA mwaka 1942. Alisoma pia Chuo Kikuu cha Pennsylvania alipomaliza digrii za master katika falsafa na ualimu.. Wakati huohuo alishirikiana na mwanaisimu William Everett Welmers kutunga kitabu cha sarufi ya Fante iliyokuwa lugha yake ya kwanza.
20231101.sw_1782_9
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kwame%20Nkrumah
Kwame Nkrumah
Wakati wa likizo Nkrumah alipenda kwenda Harlem (New York) iliyokuwa kitovu cha kiutamaduni kwa Waamerika Weusi. Hapa alienda kuzunguka mitaani na kusikiliza wahubiri wa barabarani.
20231101.sw_1782_10
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kwame%20Nkrumah
Kwame Nkrumah
Chuoni Nkrumah alikusanya wanafunzi kutoka nchi za Afrika na kuanzisha "African Students Association of America and Canada" akichaguliwa kuwa mwenyekiti wake. Katika majadiliano ya kundi hili alisisitiza haja ya nchi zote za Afrika kushikamana baada ya uhuru, si kufuata shabaha za pekee kwa kila koloni. Nkrumah alishiriki pia katika Mkutano wa Umoja wa Afrika mjini New York wa mwaka 1944 uliosisitiza Marekani kusaidia nchi za Afrika kufikia uhuru baada ya Vita Kuu ya Pili ya Dunia.
20231101.sw_1782_11
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kwame%20Nkrumah
Kwame Nkrumah
Katika kipindi chake nchini Marekani Nkrumah alikutana pia na wafuasi wa Umarx, hasa wa mwelekeo wa Trotzki. Hasa C.L.R. James kutoka Trinidad alikuwa na athira juu yake. Nkrumah aliandika baadaye ni Johnson aliyemfundisha namna gani kufanya kazi ya kisasa kwa siri kama ni lazima..
20231101.sw_1782_12
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kwame%20Nkrumah
Kwame Nkrumah
Wakati Nkrumah alitaka kurudi Afrika baada ya vita kwenye mwaka 1945, James alitunga barua ya kumtambulisha kwa marafiki huko London akiandika: "Huyu kijana anakuja sasa kwenu. Si mtu mwelekevu mno, lakini fanyeni mnachoweza kumsaidia; anataka kuwafukuza Wazungu kutoka Afrika".
20231101.sw_1782_13
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kwame%20Nkrumah
Kwame Nkrumah
Nkrumah alfika London mwezi wa Mei 1945 akajiandikisha kwenye chuo cha London School of Economics kama mwanafunzi wa PhD katika anthropolojia. Aliacha baada ya mhula mmoja, akajiandikisha kwenye chuo kikuu kwa shabaha ya kufuata PhD ya falsafa lakini hakuendelea. Mwishoni alijaribu masomo ya sheria. Profesa wa falsafa Alfred Ayer hakumwona Nkrumah kuwa mwanafalsafa bora. Alisema juu yake: "Nilimpenda nikafurahi kujadili naye. Lakini kwangu hakuonekana kuwa na akili ya mchambuzi. Alitafuta majibu ya harakaharaka. Labda sehemu ya matatizo yake ilikuwa ya kwamba hajajikazia kuendeleza thesis yake. Kwake ilikuwa njia tu ya kupita muda hadi aliweza kurudi Ghana"
20231101.sw_1782_14
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kwame%20Nkrumah
Kwame Nkrumah
Nkrumah alitumia nguvu nyingi kupanga mikutano ya siasa. Alikuwa kati ya waratibu walioandaa mkutano wa Pan-African Congress mjini Manchester (15-19 Oktoba 1945). Wajumbe wa mkutano huu walipatana kuelekea kwa Shirikisho la Maungano ya Madola ya Afrika na kujenga utamaduni mpya kwa Afrika bila ukabila na siasa itakayounganisha usoshalisti au ukomunisti na demokrasia. Kati ya wajumbe waliohudhuria walikuwa mzee W.E.B. Dubois pamoja na Waafrika walioendelea kuwa viongozi wa nchi zao baada ya uhuru kama vile Hastings Banda wa Nyasaland (Malawi), Jomo Kenyatta wa Kenya, Obafemi Awolowo wa Nigeria na C.L. R. James.
20231101.sw_1782_15
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kwame%20Nkrumah
Kwame Nkrumah
Baada ya kurusi Gold Coast, Nkrumah kwenye mwaka 1947 alikuwa katibu mkuu wa chama cha United Gold Coast Convention (UGCC). Mwaka 1948 kulitokea ghasia ya "Accra Riots"; askari Waafrika wa jeshi la Kiingereza walioachishwa baada ya vita kuu walidai malipo waliyoahidiwa. Nkrumah alihutubia mkutano wao; baada ya maandamano yao kuvunjwa na polisi na watu kufa katika ghasia iliyofuata, polisi ilikamata viongozi wa chama cha UGCC.
20231101.sw_1782_16
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kwame%20Nkrumah
Kwame Nkrumah
Mwaka 1949 Nrumah alitoka katika UGCC akaunda Convention People’s Party (CPP) iliyokuwa na madai makali zaidi. Mwaka 1951 CPP ilipata kura nyingi katika uchaguzi baada ya kudai uhuru mara moja. Nkrumah aliyekuwa tena mbaroni aliruhusiwa kugombea, alipata asilimia 98,5 za kura mjini Accra akaachwa huru. Mwaka 1952 alichaguliwa na Halmashauri ya Kisheria kuwa waziri mkuu wa koloni.
20231101.sw_1782_17
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kwame%20Nkrumah
Kwame Nkrumah
Aliendelea kuongoza serikali na mwaka 1957 wakati wa uhuru alibadilisha jina la nchi kuwa Ghana. Hii ilikuwa koloni la kwanza kupata uhuru katika Afrika ya Magharibi, baada ya Liberia. Mwaka huohuo alifunga ndoa na Fathia Helen Ritzk, Mkristo wa Kikopti kutoka nchi ya Misri.
20231101.sw_1782_18
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kwame%20Nkrumah
Kwame Nkrumah
Nkrumah alianzisha mipango mingi ya kuendeleza Ghana kiutamaduni, kielimu na kiuchumi. Pamoja na Haile Selassie wa Ethiopia aliunda Umoja wa Muungano wa Afrika (kwa Kiingereza: Organisation of African Union - OAU). Alikaribia nchi za kikomunisti na kuajiri washauri na wahandisi kutoka Urusi na China.
20231101.sw_1782_19
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kwame%20Nkrumah
Kwame Nkrumah
Alijipatia maadui kati ya machifu waliokuwa na mamlaka kubwa wakati wa ukoloni lakini sasa wengi waliachishwa au kupinduliwa na serikali kama hawakufuata maagizo yote kutoka juu. Alipata pia maadui kati ya wakulima tajiri wa kakao kwa sababu aliongeza sana kodi wakati bei ya zao hili kwenye soko la dunia ilipanda juu. Mnamo mwaka 1960 bei za kakao zilishuka sana na hapo alikosa pesa kwa miradi mingi aliyoanzisha wakati mapato ya kakao yalikuwa juu.
20231101.sw_1782_20
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kwame%20Nkrumah
Kwame Nkrumah
Gharama za miradi kubwa zililipiwa kwa kukopa pesa nje ya nchi. Deni la taifa lilikua haraka. Baada ya bidhaa kadhaa kuwa haba, serikali ilijaribu kuongoza uchumi kwa mfano wa nchi za kikomunisti. Upinzani kati ya wananchi ulitazamwa kama uasi na watu wengi walikamatwa. Kodi zilipandishwa.
20231101.sw_1782_21
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kwame%20Nkrumah
Kwame Nkrumah
Inasemekana ya kwamba pia huduma za siri za CIA (Marekani) na MI5 (Uingereza) zilichochea wapinzani wa Nkrumah waliopanga kumpindua. Mwaka 1966 alipokwenda safari ya kutembelea China na Korea ya Kaskazini kamati ya siri ya upinzani pamoja na jeshi la ulinzi na polisi ya kitaifa ilipindua serikali.
20231101.sw_1782_22
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kwame%20Nkrumah
Kwame Nkrumah
Nkrumah alishindwa kurudi. Kwa miaka kadhaa alikaa Guinea. Baada ya kugonjeka alihamia kwa tiba huko Romania alipoaga dunia mwaka 1972.
20231101.sw_1782_23
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kwame%20Nkrumah
Kwame Nkrumah
"Negro History: European Government in Africa", The Lincolnian, 12 April 1938, p. 2 (Lincoln University, Pennsylvania) - see Special Collections and Archives, Lincoln University
20231101.sw_1782_24
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kwame%20Nkrumah
Kwame Nkrumah
"The essence of neo-colonialism is that the State which is subject to it is, in theory, independent and has all the outward trappings of international sovereignty. In reality its economic system and thus its political policy is directed from outside." (Introduction)
20231101.sw_1782_25
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kwame%20Nkrumah
Kwame Nkrumah
Handbook of Revolutionary Warfare (1968) - first introduction of Pan-African pellet compass. ISBN 0-7178-0226-4
20231101.sw_1783_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ghana
Ghana
Jamhuri ya Ghana ni nchi ya Afrika Magharibi inayopakana na Côte d'Ivoire (Ivory Coast) upande wa magharibi, Burkina Faso upande wa kaskazini, Togo upande wa mashariki, na Ghuba ya Guinea upande wa kusini.
20231101.sw_1783_1
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ghana
Ghana
Kabla ya ukoloni Ghana ilikaliwa na idadi ya watu wa kale, hasa wa Falme za Akan, wakiwemo Waakwamu upande wa mashariki, Ufalme wa Ashanti ya bara na falme kadha wa kadha za Kifante, pia falme zisizo za Kiakan kama Waga na Waewe waliokuwa pwani na bara.
20231101.sw_1783_2
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ghana
Ghana
Biashara na nchi za Ulaya ilistawi baada ya kukutana kwao na Wareno katika karne ya 15, na Waingereza walianzisha nchi ya Gold Coast, chini ya himaya ya Uingereza mwaka wa 1874.
20231101.sw_1783_3
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ghana
Ghana
Nchi ya Gold Coast ilijinyakulia uhuru kutoka kwa Uingereza mwaka wa 1957, ikawa taifa la kwanza la Afrika Kusini mwa Sahara (Sub-Saharan Africa) kufanya hivyo
20231101.sw_1783_4
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ghana
Ghana
Ghana ni mwanachama wa mashirika mbalimbali ya kimataifa yakiwemo Jumuiya ya Madola, Jumuiya ya Kiuchumi ya Afrika Magharibi, Umoja wa Afrika, na Umoja wa Mataifa.
20231101.sw_1783_5
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ghana
Ghana
Ghana ni nchi ya pili baina ya nchi zinazozalisha mmea wa kakao ulimwenguni kote, pia ni kiambo cha Ziwa Volta, ambalo ndilo ziwa kubwa zaidi ulimwenguni kuundwa na binadamu.
20231101.sw_1783_6
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ghana
Ghana
Vilevile, Ghana ni nchi inayojulikana sana katika ulimwengu wa soka. Tarehe 16 Oktoba 2009, Ghana lilikuwa taifa la kwanza la Kiafrika kushinda Kombe la Dunia la FIFA kwa walio chini ya umri wa miaka 20 (FIFA U-20 World Cup) kwa kushinda nchi ya Brazil kwa mabao 4 kwa 3 kupitia mikwaju ya penalti.
20231101.sw_1783_7
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ghana
Ghana
Neno Ghana lina maana ya "Shujaa Mfalme", na lilikuwa jina la heshima walilopewa wafalme wa Himaya ya Ghana nyakati za kale za Afrika Magharibi.. Limekuwa chimbuko la jina “Guinea” (kupitia kwa Kifaransa Guinoye), ambalo limetumika kurejelea pwani ya Afrika Magharibi (na ambalo linatumika katika Ghuba ya Guinea).
20231101.sw_1783_8
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ghana
Ghana
Jina hilo lilichaguliwa kwa taifa jipya ili kuashiria himaya ya kale ya Ghana, ambayo kwa wakati mmoja ilienea katika sehemu kubwa ya Afrika Magharibi, ingawa kijiografia, Himaya ya Ghana inakadiriwa ilikuwa kilomita 800 kaskazini na magharibi mwa Ghana ya kisasa, na ilitawala majimbo katika eneo la Mto Sénégal na mashariki kuelekea Mto wa Niger, katika maeneo ya sasa ya Senegal, Mauritania na Mali.
20231101.sw_1783_9
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ghana
Ghana
Ghana lilichaguliwa kuwa jina rasmi la nchi ya Gold Coast nchi hii iliponyakua uhuru mnamo tarehe 6 Machi 1957; hata hivyo, Ghana haikuweza kutangaza uhuru wake kamili kutoka kwa Uingereza hadi tarehe 1 Julai 1960 ambapo nchi ilianza kujulikana kama Jamhuri ya Ghana.
20231101.sw_1783_10
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ghana
Ghana
Nchi hii ina eneo la kilomita mraba 238,500 (maili mraba 92,085). Eneo hili limezungukwa na Togo kwa upande wa mashariki, Cote d’Ivoire upande wa magharibi, Burkina Faso upande wa kaskazini na Ghuba ya Guinea (Bahari ya Atlantiki) upande wa kusini.
20231101.sw_1783_11
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ghana
Ghana
Ghana ni nchi ambayo inapatikana katika Ghuba ya Guinea, nyuzi chache kaskazini mwa Ikweta, jambo ambalo linaipa nchi hii hali ya joto. Vilevile mstari wa Greenwich Meridian hupita ndani ya Ghana, katika jiji la viwanda la Tema. Hivyo kijiografia Ghana iko karibu zaidi ya sehemu ya “katikati” mwa ulimwengu kuliko nchi yoyote ile, ingawa sehemu halisi ya katikati, (0°, 0°) inapatikana katika Ghuba ya Guinea, katika Bahari ya Atlantiki, kwa makadirio kilomita 614 (maili 382) kusini mwa Accra, Ghana.
20231101.sw_1783_12
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ghana
Ghana
Nchi hii ina maeneo tambarare, vilima vya chini na mito michache. Nchi ya Ghana inaweza kugawanywa katika maeneo matano tofauti ya kijiografia. Eneo la pwani ni sehemu ambayo ni ya chini na iliyo na ufuo wa mchanga huku ikipakana na koko na kukingamana na mito na vijito kadha wa kadha huku sehemu ya kaskazini ikiwa na maeneo ya juu yaliyo tambarare. Eneo la kusini magharibi na kusini ya kati mwa Ghana ni sehemu iliyoinuka sawa na pana yenye misitu ikiwa na vilima vya Ashanti na eneo sawa na pana (plateau) la Kwahu na safu ya vilima vya Akuapim-Togo vinapatikana kwenye mpaka wa mashariki mwa nchi. Bonde la Volta linachukua eneo la kati mwa Ghana. Sehemu ya juu zaidi nchini Ghana ni Mlima Afadjato ulio na urefu wa mita 855 (futi 2,904) na unaopatikana kwenye safu ya vilima vya Akwapim-Togo.
20231101.sw_1783_13
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ghana
Ghana
Hali ya hewa ni ya hari. Kanda ya pwani ya mashariki ni ya joto na iliyokauka (angalia Dahomey Gap); pembe ya kusini magharibi, huwa na joto jingi na unyevu hewani; huku sehemu ya kaskazini ikiwa yenye joto jingi na iliyokauka. Ziwa Volta, ziwa lisilo la asili kubwa zaidi ulimwenguni, linaenea kupitia katika mafungu makubwa mashariki mwa Ghana na ndicho chanzo kikuu cha vijito vingi kama vile vya Oti na Afram.
20231101.sw_1783_14
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ghana
Ghana
Kuna misimu miwili mikuu nchini Ghana, masika na kiangazi. Kaskazini mwa Ghana huwa na msimu wa masika kutoka Machi hadi Novemba huku sehemu ya kusini, ukiwemo mji mkuu wa Accra, ikiwa na masika kutoka Aprili hadi Novemba katikati.
20231101.sw_1783_15
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ghana
Ghana
Kusini mwa Ghana kuna misitu ambayo daima ni ya kijani kibichi na ile ambayo hupoteza majani yake wakati fulani wa mwaka ikiwa na miti kama mikangazi, odumu na mipingo. Sehemu hii inayo pia mingi ya mitende ya mafuta na mikoko. Miti ya Shea, mibuyu na mikakaya hupatikana kwa kawaida katika maeneo ya Volta na kaskazini mwa nchi.
20231101.sw_1783_16
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ghana
Ghana
Ghana imegawiwa katika mikoa 16, ambayo yamegawiwa zaidi katika wilaya 275, kila moja ikiwa na Bunge la Wilaya (District Assembly). Chini ya wilaya kuna aina kadhaa za mabaraza, yakiwemo mabaraza 58 ya miji au maeneo, mabaraza 108 ya kanda na mabaraza 626 ya maeneo. Kamati za vitengo 16,000 huwa katika daraja ya chini zaidi.
20231101.sw_1783_17
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ghana
Ghana
Kuna ushahidi kutoka kwa maarifa ya mambo ya kale ambao unaonyesha kwamba watu wameishi katika eneo linalojulikana siku hizi kama Ghana kutoka karibu miaka ya 1500 KK (Kabla ya Kristo).
20231101.sw_1783_18
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ghana
Ghana
Licha ya hayo, hakuna ushahidi wa kuonyesha kuwa wakazi hao wana uhusiano na wale wa eneo hili kwa sasa. Kwa mujibu wa mapokeo simulizi, mengi kati ya makabila ya Ghana, leo kama vile watu wa chimbuko la makabila kadhaa kama Waakan, Waga na Waewe, walifika Ghana mnamo karne ya 13.
20231101.sw_1783_19
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ghana
Ghana
Mengi ya maeneo ya Ghana yanajumuisha eneo lililokuwa la Himaya ya Ashanti, mojawapo ya falme zilizokuwa na ushawishi mkubwa katika eneo la Afrika Kusini mwa Sahara kabla ya enzi za ukoloni.
20231101.sw_1783_20
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ghana
Ghana
Wahamiaji Waakan walihama kuelekea kusini na kuanzisha mataifa kadhaa, likiwemo lile la kwanza la himaya kuu ya Akan ya Wabono, ambayo kwa sasa inajulikana kama eneo la Brong Ahafo nchini Ghana.
20231101.sw_1783_21
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ghana
Ghana
Sehemu kubwa ya eneo la sasa la kusini na kati mwa Ghana ilikuwa imeungana chini ya Himaya ya Ashanti ya Waashanti, tawi la Waakan wa karne ya 16.
20231101.sw_1783_22
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ghana
Ghana
Utawala wa Waashanti ilihudumu mwanzoni kama mtandao mlegevu kabla ya kuwa ufalme ulioungana huku ukiwa na urasimu ulioendelea na wenye uchanganuzi mkubwa uliokuwa na makao yake Kumasi. Inasemekana kuwa katika kilele chake, Waasantehene wangeweza kutuma askari 500,000 vitani na kuwa na ushawishi wa kijeshi wa kiwango fulani juu ya majirani wake wote.
20231101.sw_1783_23
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ghana
Ghana
Waga walianzisha muungano wenye ufanisi mnamo 1500 na Wagonja, Wadagomba na Wamamprusi, pia walipigania uwezo wa kisiasa katika miaka ya 1620.
20231101.sw_1783_24
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ghana
Ghana
Mawasiliano ya awali na Ulaya kutoka kwa Wareno, walioingia Ghana mnamo 1419, yalizingatia upatikanaji wa dhahabu. Wareno walitua kwanza katika jiji la pwani lililokuwa makazi ya ufalme wa Wafante na kuliita eneo hili Elmina, jina ambalo linamaanisha “mgodi” kwa Kireno.
20231101.sw_1783_25
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ghana
Ghana
Mwaka wa 1481, Mfalme John II wa Ureno aliagiza Diogo de Azambuja kujenga Kasri ya Elmina, ambayo ilikamilishwa mwaka uliofuata. Lengo lao lilikuwa kufanya ubadilishanaji wa dhahabu, pembe za ndovu na watumwa, ili kuimarisha mamlaka yao yaliyokuwa yanakua kwa kasi katika eneo hilo.
20231101.sw_1783_26
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ghana
Ghana
Kufikia mwaka wa 1598 Waholanzi walikuwa wameungana nao, na kujenga ngome katika maeneo ya Komenda na Kormantsi. Mwaka wa 1637, waliiteka Kasri ya Elmina kutoka kwa Wareno na vilevile Axim mwaka wa 1642 (Ngome ya Mtakatifu Antoni).
20231101.sw_1783_27
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ghana
Ghana
Wafanyabiashara wengine kutoka Ulaya walijiunga nao kufikia miaka ya kati ya karne ya 17, hasa Waingereza, Wadenmarki na Waswidi. Wafanyabiashara Waingereza, waliovutiwa na rasilimali katika eneo hilo, waliliita Gold Coast, (Pwani ya Dhahabu), huku nao wafanyabiashara Wafaransa, wakivutiwa na mapambo waliyokuwa wakivaa watu wa pwani, wakiliita eneo la sehemu ya magharibi “Côte d'Ivoire", au Ivory Coast (pwani ya pembe za ndovu).
20231101.sw_1783_28
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ghana
Ghana
Zaidi ya ngome na kasri thelathini zilijengwa na wafanyabiashara Wareno, Waholanzi, Waingereza na Wadenmarki.
20231101.sw_1783_29
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ghana
Ghana
Eneo la Gold Coast lilijulikana kwa karne nyingi kama ‘Kaburi la Mtu Mweupe’ kwa sababu wengi kati ya Wazungu walioenda huko kutoka Ulaya walikufa kutokana na malaria na magonjwa mengine ya eneo la hari.
20231101.sw_1783_30
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ghana
Ghana
Baada ya Waholanzi kuondoka mwaka wa 1874, Uingereza iliiweka Gold Coast chini ya himaya yake. Kufuatia ushindi wa Uingereza mwaka wa 1896, hadi unyakuzi wa uhuru mnamo Machi 1957, eneo la Ghana ya sasa ghairi ya sehemu ya Volta Region (British Togoland), lilikuwa likijulikana kama Gold Coast.
20231101.sw_1783_31
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ghana
Ghana
Vita vingi vilitokea baina ya utawala wa kikoloni na baadhi ya mataifa ya eneo hilo vikiwemo Vita vya 1806 vya Ashanti-Fante na mapambano ya kudumu ya Waashanti dhidi ya Waingereza, ambayo yalikoma baada ya Vita vya Tatu baina ya Waashanti na Waingereza (the third Ashanti-British War) (1900-1901).. ]
20231101.sw_1783_32
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ghana
Ghana
Hata chini ya utawala wa kikoloni machifu na watu wao walipinga mara kwa mara sera za Waingereza; hata hivyo, ushawishi wa kupinga ukoloni ulikolea baada ya Vita vya Pili vya Dunia. Mwaka wa 1947 chama kipya cha United Gold Coast Convention (UGCC) kilitoa wito wa “utawala wa kujitegemea katika wakati mfupi iwezekanavyo.”
20231101.sw_1783_33
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ghana
Ghana
Baada ya kuongezeka kwa maandamano mnamo 1948, wanachama wa chama cha United Gold Coast Convention walikamatwa, akiwemo Waziri Mkuu na Rais wa baadaye, Kwame Nkrumah. Baadaye, Nkrumah aliunda chama chake mwenyewe, the Convention People's Party (CPP) ambacho kiliongozwa na usemi ‘serikali ya kujitegemea sasa’ (self government now). Alianzisha kampeni ya ‘Vitendo Chanya’ na kupata ufuasi wa watu wa sehemu za mashambani na wa daraja la wafanyakazi.
20231101.sw_1783_34
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ghana
Ghana
Kwa mara nyingine Nkrumah alishikwa na kuzuiliwa kwa kuwa msimamizi wa chama ambacho kilisababisha ususiaji, migomo na vitendo vingine vya uasi wa raia.
20231101.sw_1783_35
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ghana
Ghana
Hata hivyo, baada ya kushinda wingi wa viti katika Bunge ya Kuunda Sheria mnamo 1952, Kwame Nkrumah aliachiliwa na kuchaguliwa kuwa Kiongozi wa Masuala ya Serikali.
20231101.sw_1783_36
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ghana
Ghana
Baada ya mazungumzo na Uingereza, hatimaye tarehe 6 Machi 1957 saa sita usiku, Kwame Nkrumah alitangaza Ghana kuwa “huru milele”.
20231101.sw_1783_37
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ghana
Ghana
Bendera iliyokuwa na rangi nyekundu, dhahabu, kijani kibichi na nyota nyeusi ilikuwa bendera mpya mnamo 1957. Bendera hiyo iliundwa na Theodosia Salome Okoh, na rangi nyekundu inawakilisha damu iliyomwagwa ili kupata uhuru, rangi ya dhahabu inawakilisha ukwasi wa madini wa Ghana, ile ya kijani kibichi inaashiria utajiri wa kilimo na ile nyeusi ni ishara ya Uhuru wa Waafrika.
20231101.sw_1783_38
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ghana
Ghana
Huku ikiundwa kutoka kwa muungano wa maeneo ya Gold Coast na British Togoland kufuatia matokeo ya kura ya maoni ya watu yaliyodhaminiwa na Umoja wa Mataifa mnamo 1956, Ghana ilikuwa nchi ya kwanza ya Afrika Kusini mwa Sahara kunyakua uhuru mnamo 1957.
20231101.sw_1783_39
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ghana
Ghana
Kwame Nkrumah, Waziri Mkuu wa kwanza na baadaye Rais wa nchi ya sasa ya Ghana, hakuwa tu kiongozi wa Kiafrika wa kupigana dhidi ya ukoloni ila alikuwa pia mtu aliyekuwa na ndoto ya muungano wa Afrika ambayo haingejipata katika ukoloni mamboleo. Alikuwa kiongozi wa serikali ya kwanza Afrika kukuza Muungano wa Waafrika (Pan-Africanism), wazo ambalo alilipata wakati wa masomo yake katika Chuo Kikuu Cha Lincoln lililoko Pennsylvania (Marekani), wakati ambapo Marcus Garvey alikuwa anapata umaarufu kwa harakati zake za “Back to Africa Movement." Aliunganisha ndoto za Macus Garvey na zile za mwanachuo mashuhuri Mmarekani Mweusi W.E.B. Du Bois ili kuandaa Ghana kisasa.
20231101.sw_1783_40
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ghana
Ghana
Kanuni za Ghana za uhuru na haki, usawa na elimu ya bure kwa wote, bila kujali kabila, dini au mila, zinatokana na utekelezaji wa wazo la Pan-Africanism.
20231101.sw_1783_41
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ghana
Ghana
Ingawa lengo lake la muungano wa Afrika halikuwahi kuafikiwa, Osagyefo Dr. Kwame Nkrumah, kama ajulikanavyo sasa, alishiriki kwa kiwango kikubwa katika kuzinduliwa kwa Shirika la Umoja wa Afrika, ambalo lilifuatwa mnamo 2002 na Umoja wa Afrika (African Union). Ingawa Nkrumah aliheshimika sana ng’ambo, hakuwa akipendwa katika masuala ya ndani ya nchi.
20231101.sw_1783_42
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ghana
Ghana
Hakufeli tu kuanzisha uchumi wa viwanda, ila hata sera zake hukusu uchumi ziliishia kuifanya nchi ya Ghana kuwa maskini kuliko ilivyokuwa wakati wa kupata uhuru. Mafanikio yake yalikuwa kutambuliwa na raia wa Ghana wakati wa maadhimisho ya kuzaliwa Centenary wake na siku aliliweka kama likizo umma nchini Ghana.
20231101.sw_1783_43
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ghana
Ghana
Hatimaye Nkrumah aliondolewa madarakani na jeshi alipokuwa ng’ambo mnamo Februari 1966, na mabadiliko hayo yalikaribishwa na wengi wa wakazi wa Ghana. Inaaminika na wengi wa wachanganuzi wa masuala ya kisiasa kwamba shirika la Marekani la Central Intelligence Agency (CIA) lilihusika na mapinduzi hayo, lakini wazo hilo halijawahi kuthibitishwa.
20231101.sw_1783_44
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ghana
Ghana
Mfululizo wa baadaye wa mapinduzi kati ya 1966 na 1981 uliishia kwa kuingia madarakani kwa Liuteni wa Jeshi la Wanahewa (Flight Lieutenant) Jerry Rawlings mwaka wa 1981.
20231101.sw_1783_45
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ghana
Ghana
Mabadiliko hayo yalisababisha kusimamishwa kwa katiba ya nchi mnamo 1981 na kupigwa marufuku kwa vyama vya kisiasa. Uchumi ulishuka sana punde baadaye, na Waghana wengi walihamia nchi zingine. Ingawa wengi wa Waghana waliohama walienda Nigeria, serikali ya Nigeria iliwarudisha Ghana karibu Waghana milioni moja mwaka wa 1983.
20231101.sw_1783_46
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ghana
Ghana
Punde baadaye, Rawlings aliafikiana na shirika la International Monetary Fund juu ya mkataba wa mpango wa maendeleo (structural development plan) na kubadili sera nyingi za awali za uchumi na hivyo uchumi ukaanza kukua.
20231101.sw_1783_47
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ghana
Ghana
Katiba mpya iliyorudisha mfumo wa siasa za vyama vingi ilitangazwa mwaka wa 1992, na Rawlings alichaguliwa kuwa Rais na tena mwaka wa 1996. Katiba ya mwaka wa 1992 ilimzuia kuwania kiti hicho kwa muhula wa tatu, kwa hivyo chama chake, National Democratic Congress, kilimchagua Makamu wake wa Rais, John Atta Mills, kuwania urais dhidi ya vyama vya upinzani.
20231101.sw_1783_48
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ghana
Ghana
Huku akishinda uchaguzi wa mwaka 2000, John Kufuor wa chama pinzani cha New Patriotic aliapishwa kama Rais mnamo Januari 2001, na kumshinda tena Mills mwaka wa 2004; hivyo kuhudumia kama Rais kwa mihula miwili.
20231101.sw_1783_49
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ghana
Ghana
Mwaka wa 2009, John Atta Mills alichukua mamlaka huku kukiwa na tofauti ndogo sana ya kura 40,000 ambazo ni 0.46% kati ya chama chake, National Democratic Congress, na kile cha New Patriotic Party, tukio hili likiwa la pili la ubadilishanaji wa mamlaka kutoka kwa kiongozi mmoja aliyechaguliwa kihalali kwa mwingine, na hivyo kuimarisha hadhi ya Ghana kama demokrasia iliyo imara.
20231101.sw_1783_50
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ghana
Ghana
Kwa mujibu wa Fahirisi ya Mataifa Yaliyoanguka (Failed States Index), Ghana inaorodheshwa katika nambari ya 53 baina ya mataifa ambayo hayajaanguka huku likiorodheshwa kwa nafasi ya pili baina ya mataifa ya Afrika baada ya Mauritius. Taifa la Ghana liliorodheshwa katika nafasi ya 124 baina ya nchi 177 katika fahirisi hii na liliainishwa kama taifa la wastani. Vilevile, nchi ya Ghana imo katika nafasi ya 7 baina ya nchi 48 za Afrika zilizo Kusini mwa Sahara katika fahirisi ya mwaka wa 2008 ya Ibrahim Index of African Governance ambayo ilitokana na hakiki za mwaka wa 2006. Fahirisi ya Ibrahim ni kipimo chenye uchanganuzi mwingi kuhusu maswala ya utawala barani Afrika, kinachotokana na maswala ya mabadiliko tofautitofauti ambayo huashiria kufuzu kwa serikali wakati wa kutoa huduma muhimu za kisiasa kwa wananchi wao.
20231101.sw_1783_51
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ghana
Ghana
Taifa la Ghana lilianzishwa kama demokrasia ya bunge wakati wa kupata uhuru mnamo mwaka wa 1957, ikifuatiwa na ubadilishanaji wa serikali za kijeshi na za kiraia. Mnamo Januari 1993, serikali ya kijeshi iliondoka na kuipisha Jamhuri ya Nne baada ya uchaguzi wa urais na ubunge mnamo mwisho wa mwaka wa 1992. Katiba ya 1992 inagawa mamlaka kati ya Rais, Bunge, Baraza la Mawaziri, Baraza la Taifa na mahakama huru. Serikali huchaguliwa na upigaji kura wa haki kwa wote; ingawa bunge halina uwiano kabisa kwani wilaya zilizo na watu wachache hupata wawakilishi wengi kwa kila mtu zikilinganishwa na wilaya ambazo zina idadi ya juu ya wakazi.
20231101.sw_1783_52
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ghana
Ghana
Mfumo wa kisheria unatokana na ule wa Uingereza yaani British common law, sheria za kimila (kitamaduni), na katiba ya mwaka wa 1992. Daraja za mahakama hujumuisha Mahakama Kuu ya Ghana (mahakama ya juu zaidi), Mahakama za Rufaa na Mahakama Kuu za Kisheria. Chini ya mahakama hizi kuna mahakama za kuzunguka, mahakama za hakimu, na mahakama za kitamaduni. Taasisi zingine zisizo chini ya sheria ni pamoja na mahakama za umma. Tangu unyakuzi wa uhuru, mahakama zimekuwa huru kwa kiwango fulani; uhuru huu unaendelea chini ya Jamhuri ya Nne. Mahakama za chini zinadhahirishwa na kupangwa upya chini ya utawala wa Jamhuri ya Nne.
20231101.sw_1783_53
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ghana
Ghana
Vyama vya kisiasa vilihalalishwa katikati mwa mwaka wa 1992 baada ya kupigwa marufuku kwa miaka kumi. Kuna vyama vingi vya kiasisa chini ya Jamhuri ya Nne; hata hivyo vile vikubwa ni National Democratic Congress kilichoshinda uchaguzi wa urais na ubunge mnamo 1992, 1996 na 2008; New Patriotic Party, chama kikubwa cha upinzani kilichoshinda uchaguzi wa mwaka wa 2000 na ule wa 2004; People’s National Convention, na Convention People’s Party, ambacho kilichukua mahali pa chama cha awali cha Kwame Nkrumah kilichokuwa na jina lilo hilo.
20231101.sw_1783_54
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ghana
Ghana
Tangu unyakuzi wa uhuru, Ghana imefuata kwa dhati mwelekeo wa kutojiunga na upande wa kibepari au ule wa kikomunisti (nonalignment) na pia siasa zinazopendelea siasa za umoja wa Afrika (Pan-Africanism); mawazo ambayo yanahusishwa na rais wa kwanza, Osagyefo Dr. Kwame Nkrumah. Nchi ya Ghana inapendele31ushirikiano wa kimataifa na wa kikanda wa kisiasa na wa kiuchumi, na ni mwanachama mwenye mashuhuri wa Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika.
20231101.sw_1783_55
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ghana
Ghana
Wanadiplomasia na wanasiasa wengi Waghana wana vyeo katika mashirika ya kimataifa. Hawa ni pamoja na mwanadiplomasia Mghana na Katibu Mkuu wa zamani wa Umoja wa Mataifa, Kofi Annan, Jaji wa Mahakama ya Kimataifa ya Jinai Akua Kuenyehia, na rais wa zamani Jerry Rawlings, ambaye alichaguliwa kuwa mwenyekiti wa Jumuiya ya Kiuchumi ya Mataifa ya Afrika Magharibi (Economic Community of West African States).
20231101.sw_1783_56
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ghana
Ghana
Ingawa Ghana ni kiambo cha zaidi ya makabila 70 tofauti, haijashuhudia migogoro ya kikabila kama ile ambayo imesababisha vita vya wenyewe kwa wenyewe katika nchi nyingi za Afrika.
20231101.sw_1783_57
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ghana
Ghana
Makabila nchini Ghana ni ya Waakan (ambalo linajumuisha Fante, Akyem, Ashanti, Kwahu, Akuapem, Nzema, Bono, Akwamu, Ahanta na makabila mengine) 47.5%, Wamole-Dagbon 16.6%, Waewe 13.9%, Waga-Adangbe (likijumuisha Ga, Adangbe, Ada, Krobo na makabila mengine) 7.4%, Wabassare 5.9%, Wakonkomba 5.7%, Waguan 3.7%, Wagurunsi 2.5%, Wakusasi 2.2%, Wabissa 1.1%, mengine (Wahausa, Wazabarema, Wafula) 1.4% (sensa ya 2010).
20231101.sw_1783_58
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ghana
Ghana
Lugha rasmi ni Kiingereza; hutumika sana katika masuala ya serikali na biashara. Lugha hiyo vilevile ndiyo inayotumika katika mafundisho ya elimu. Kifaransa pia kinajulikana sana na kiko mbioni kufanywa lugha rasmi ya pili.
20231101.sw_1783_59
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ghana
Ghana
Ingawa wataalamu wengine wanasema nchini Ghana huzungumzwa zaidi ya lugha na lugha ndogo 250, Ethnologue inaziorodhesha 79 tu (angalia pia orodha ya lugha za Ghana). Lugha za asili za Ghana zimegawanywa katika jamii mbili ndogo kutokana na jamii ya lugha za Kiniger-Kongo.
20231101.sw_1783_60
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ghana
Ghana
Lugha za jamii ndogo ya Kwa zinapatikana zaidi katika maeneo ya kusini mwa Mto Volta, huku zile za jamii ya Gur zikipatikana katika eneo la kaskazini. Kikundi cha Kwa, lugha ambayo huzungumzwa na takribani 75% ya wakazi wa nchi, kinajumuisha lugha za Akan, Ga-Dangme na Ewe. Kikundi cha Gur kinajumuisha lugha za Gurma, Grusi, na Dagbani.
20231101.sw_1783_61
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ghana
Ghana
Lugha kumi na moja zina hadhi ya kuwa lugha zinazodhaminiwa na serikali: Akuapem Twi, Ashanti Twi, Fante, Nzema, Dagaare/Wale, Dagbani, Dangme, Ewe, Ga, Gonja na Kasem.
20231101.sw_1783_62
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ghana
Ghana
Kwa mujibu wa sensa ya serikali ya 2010, mgawanyiko wa kidini ni: Wakristo 71.2% (hasa Waprotestanti 46.7% na Wakatoliki 13.1%), Waislamu 17.6%, dini asilia za Kiafrika 6.2%.
20231101.sw_1783_63
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ghana
Ghana
Kufikia mwaka wa 2009, matarajio ya urefu wa maisha (life expectancy) wakati wa kuzaliwa ni takriban miaka 59 kwa wanaume na 60 kwa wanawake huku makisio ya vifo vya watoto wachanga yakiwa 51 kwa watoto 1000 waliozaliwa hai .
20231101.sw_1783_64
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ghana
Ghana
Hesabu ya watoto wanaozaliwa pia ni takriban watoto wanne kwa kila mwanamke. Kuna takriban madaktari 15 na wauguzi 93 kwa watu 100,000.
20231101.sw_1783_65
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ghana
Ghana
Ghana ni nchi iliyo na makabila mbalimbali; kwa hivyo ni mchanganyiko wa tamaduni wa makabila yake yote, Ashanti, Fante, Akyem, Kwahu, Ga, Ewe, Mamprusi na Dagomba, baina ya mengine. Jambo hili linadhihirika katika upishi, sanaa na desturi ya mavazi ya Ghana.
20231101.sw_1783_66
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ghana
Ghana
Maadhimisho ya tamasha nchini Ghana ni sehemu muhimu ya utamaduni wa Ghana na kuna tamasha nyingi kama vile Homowo, Odwira, Aboakyer, Dodoleglime na Sandema baina ya zingine. Ibada na mila kadha wa kadha hufanywa wakati wote wa mwaka katika sehemu mbali mbali za nchi, zikiwemo zile za kuzaliwa, ibada za mpito maishani kama vile kubalehe, ndoa na kifo.
20231101.sw_1783_67
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ghana
Ghana
Timu za kitaifa za soka ya wanaume zinajulikana kama The Black Stars, the Black Satellites na the Black Starlets na timu hizi hushiriki katika michuano mingi ikiwemo ile ya Kombe la Mataifa ya Afrika, Kombe la Dunia la FIFA na Kombe la Dunia la FIFA kwa walio chini ya miaka 20. Timu ya the Black Satellites ilishinda Kombe la Dunia la FIFA kwa walio chini ya miaka 20 mnamo 2009 baada ya kushinda timu ya Brazili ya Seleção. Kuna timu za soka kadhaa nchini Ghana za kutajika zaidi zikiwa Accra Hearts ya Oak SC na Asante Kotoko baina ya zingine. Baadhi ya wachezaji wa soka wa Ghana wanaojulikana katika daraja ya kimataifa au waliopata ufanisi katika soka ya Ulaya ni Abedi Pele, Ibrahim Abdul Razak, Tony Yeboah, Anthony Annan, John Paintsil, Asamoah Gyan, Samuel Osei Kuffour, Richard Kingston, Sulley Muntari, Laryea Kingston, Stephen Appiah, Andre Ayew, Emmanuel Agyemang-Badu, Dominic Adiyiah na Michael Essien.
20231101.sw_1783_68
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ghana
Ghana
Kufumwa kwa vitambaa ni kitengo muhimu cha utamaduni wa Ghana. Vitambaa hivi hutumika kutengeneza mavazi ya kiasili na ya kisasa. Michoro na rangi tofauti humaanisha vitu tofauti. Pengine Kente ndicho kitambaa mashuhuri zaidi baina ya vitambaa vyote vya Ghana.
20231101.sw_1783_69
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ghana
Ghana
Kente ni kitambaa cha sherehe cha Waashanti ambacho kinatengenezwa kwa mkono kwenye kitanda cha mfumi. Vipande vya takribani inchi nne kwa upana hushonwa pamoja ili kuwa vitambaa vikubwa zaidi. Vitambaa hivi huwa katika rangi, ukubwa na namna tofautitofauti na huvaliwa wakati wa hafla muhimu sana za kijamii au kidini.
20231101.sw_1783_70
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ghana
Ghana
Katika muktadha wa kitamaduni, kitambaa cha kente kina umuhimu zaidi ya vazi tu. Ni uwakilishi wa kuonekana wa historia, na pia aina ya lugha iliyoandikwa kwa kufuma. Neno Kente lina mizizi yake katika neno la Kitwi kenten ambalo lina maana ya kikapu. Wasusi wa kwanza wa kente walitumia nyuzi za ukindu kufuma vitambaa vilivyoonekana kama kenten (kikapu); na hivyo vilikuwa vinaitwa kenten ntoma; kumanisha kitambaa cha kikapu. Jina la kiasili la Kiasante la kitambaa hiki lilikuwa nsaduaso au nwontoma, kumaanisha “kitambaa kilichotengenezwa kwa mkono kwenye kitanda cha mfumi”; hata hivyo neno kente ndilo hutumika zaidi na watu wengi siku hizi. Aina nyingi tofauti za vipande vyembamba vya vitambaa vinavyofanana na kente hufumwa na makabila mengi tofauti nchini Ghana kama Ewe, Ga na mengine ya Afrika. Kente pia hupendwa na Waafrika wanaoishi katika nchi za ng’ambo.
20231101.sw_1783_71
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ghana
Ghana
Nchi ya Ghana ina aina nyingi ya muziki wa kitamaduni na wa kisasa. Midundo hii hutofautiana kutoka kabila moja hadi jingine na eneo moja hadi lingine. Muziki wa Ghana unajumuisha aina nyingi tofauti za vyombo vya muziki kama vile ngoma za talking drum ensembles, zeze ya goje na kinubi cha koloko, muziki wa jumba la mfalme, ikiwemo miziki ya Waakan wa Atumpan, wa Waga wa mitindo ya Kpanlogo, na marimba ya gogo itumikayo katika muziki wa Waasonko. Aina za muziki ambazo zinajulikana zaidi kutoka Ghana ni Afro-jazz ambayo ilifumbuliwa na msanii Mghana Kofi Ghanaba.
20231101.sw_1783_72
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ghana
Ghana
na aina ya awali zaidi ya muziki wa kidunia inayoitwa Highlife. Highlife ni muziki uliochimbuka katika miaka ya mwisho ya 1800 na miaka ya mwanzo ya 1900 na kuenea kote Afrika Magharibi hasa Sierra Leone na Nigeria. Katika miaka ya 1900 aina mpya ya muziki ilizinduliwa na vijana huku ikiunganisha jinsi za Highlife, Afro-reggae, Dancehall na Hiphop. Mchanganyiko huu huitwa Hiplife. Wasanii wa Ghana kama vile mwimbaji wa R&B na Soul Rhian Benson, mwimbaji wa Highlife Kojo Antwi na msanii wa rap Tinchy Stryder (Kwasi Danquah) wamekuwa na ufanisi wa kimataifa.
20231101.sw_1783_73
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ghana
Ghana
Ngoma (densi) ya Ghana ina tofauti mithili ya muziki wake. Kila kabila lina ngoma zake za kitamaduni na kuna ngoma tofauti tofauti kwa hafla tofauti tofauti. Kuna ngoma za mazishi, sherehe za maadhimisho, usimulizi wa hadithi, sifa na kuabudu na kadhalika. Baadhi ya ngoma hizi ni:
20231101.sw_1783_74
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ghana
Ghana
Ngoma hii huchezwa na watu wa eneo la kaskazini mwa Ghana. Inasimulia hekaya ya wakati wa ukame mkubwa. Miungu iliwaambia watu kuwa ukame huo ulikuwa umeletwa na jinsi wanaume walikuwa wakiwakandamiza na kuwatweza wanawake. Ilisema pia kwamba ukame ungeondolewa tu pale wanaume wangejizusha na kuchukua majukumu waliyokuwa wamewatwika wanawake kwa kuvaa marinda na kushiriki katika ngoma hii. Wanaume walipofanya hivi, mvua ilianza kunyesha. Kwa sasa ngoma hii huchezwa wakati wa mavuno katika eneo la kaskazini magharibi mwa Ghana na wanaume pamoja na wanawake wa Dagbani.
20231101.sw_1783_75
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ghana
Ghana
Ngoma ya watu wa Ashanti wa Ghana. Ngoma hii inatajika hasa kwa madaha na weledi wa mzunguko wa wachezaji. Upigaji ngoma pia unasifika kwa weledi wa mfuatano wa sauti zinazochanganyika na ngoma mbili za atumpan ambazo zinatumika kama ngoma za kuongoza au ngoma simamizi. Ngoma hii ilikuwa awali ikichezwa katika mazishi, lakini kwa sasa inachezwa pia katika tamasha za kila mwaka na mikusanyiko ya kijamii.
20231101.sw_1783_76
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ghana
Ghana
huchezwa na watu wa Ga wa Ghana. Ngoma hii ya Kpanlongo ambayo mara nyingi huitwa “ngoma ya vijana,” ilianza kuchezwa punde tu baada ya unyakuzi wa Uhuru wa Ghana kama aina ya muziki wa burudani jijini Accra. Kpanlongo huchezwa kwa sasa kwa matukio yanayohusu maisha, tamasha na mikutano ya kisiasa.
20231101.sw_1783_77
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ghana
Ghana
Huu ni muziki na ngoma ambayo inahusishwa na ibada za kubalehe kati ya watu wa Krobo wa Ghana. Inasisitiza kusonga kwa madaha kwa mikono na miguu. Huku wakipiga hatua ndogo kuambatana na muziki na wakigeuza vichwa kwa utaratibu kuangalia chini, wacheza ngoma huwa mfano wa madahiro tulivu. Tofauti baina ya hatua za wachezaji zinanuiwa kuonyesha uzuri wa wacheza ngoma. Mara kwa mara, wachumba wanaotazama ngoma hii kutoka pembeni huzuru jamii ya msichana baada ya sherehe kwa madhumuni ya kumposa msichana huyo.
20231101.sw_1783_78
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ghana
Ghana
Vyombo vya habari vya Ghana ni mojawapo ya vile vilivyo na uhuru zaidi barani Afrika. Hapo awali, vilikuwa vimewekewa vizuizi vingi wakati wa mfululizo wa mapinduzi ya serikali na viongozi wa jeshi. Sura ya 12 ya katiba ya 1992 ya Ghana inatoa hakikisho la uhuru na kujisimamia kwa vyombo vya habari huku Sura ya 2 ikizuia uthibiti.
20231101.sw_1783_79
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ghana
Ghana
Baada ya kujinyakulia uhuru, serikali na vyombo vya habari vimekuwa mara kwa mara vikiwa na uhusiano ulio na mvutano, huku mashirika ya kibinafsi yakifungwa wakati wa mapinduzi ya kijeshi na sheria kali ili kuzuia ukosoaji wa serikali. Uhuru wa vyombo vya habari ulirejeshwa mnamo mwaka wa 1992, na baada ya uchaguzi wa 2000 wa John Kufuor mivutano kati ya vyombo vya habari vya kibinafsi na serikali ilipungua. Kufuor alikuwa mtetezi mkubwa wa uhuru wa vyombo vya habari na alifuta sheria ya masingizio, ingawa alisisitiza kuwa ni lazima vyombo vya habari vifanye kazi kwa uwajibikaji. Vyombo vya habari vya Ghana vimeelezwa kuwa “baadhi ya vile visivyo na uthibiti mkubwa na serikali mwingi” barani Afrika, huku vikifanya kazi vikiwa na masharti machache mno kwa vyombo vya habari vya kibinafsi. Vyombo vya habari vya kibinafsi mara kwa mara hukosoa sera za serikali.
20231101.sw_1783_80
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ghana
Ghana
Vyombo vya habari vilifanya kazi kwa bidii wakati wa uchaguzi wa rais wa Ghana wa mwaka wa 2008, na Chama cha Wanahabari wa Ghana (Ghanaian Journalists Association (GJA)) kilimpongeza John Atta Mills kwa ushindi wake, huku kikinuia kukuza uhusiano mwema baina ya vyombo vya habari na serikali.
20231101.sw_1783_81
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ghana
Ghana
Kiwango cha kujua kusoma na kuandika kwa watu wazima kilikuwa 65% mnamo 2007, huku wanaume wakiwa 71.7% na wanawake wakiwa 58.3%.