_id
stringlengths
15
22
url
stringlengths
31
150
title
stringlengths
1
86
text
stringlengths
100
23.8k
20231101.sw_1800_3
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ukoloni
Ukoloni
Ukoloni ni hasa ule wa kipindi tangu karne ya 15 ambako Ureno na Hispania zilianza kueneza himaya zao Afrika na Amerika ya Kusini na kudumu pengine hadi baada ya Vita Kuu ya Pili ya Dunia.
20231101.sw_1800_4
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ukoloni
Ukoloni
Lakini kulikuwa na vipindi vya ukoloni pia zamani katika historia kama vile ukoloni wa Roma ya Kale, ukoloni wa Waarabu na wengine. Ukoloni kwa maana hii unaweza kuwa tofauti na kuundwa kwa koloni katika vipindi mbalimbali vya historia ambapo maeneo bila wakazi au yenye wakazi wachache sana yaliingiliwa na watu kutoka sehemu nyingine.
20231101.sw_1800_5
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ukoloni
Ukoloni
Ukoloni mamboleo ni aina ya nchi au kundi la nchi fulani kutawala nchi nyingine kinyemela kwa kuweka vikwazo na masharti yatakayowafanya watawaliwa waendelee kuwa na uchumi tegemezi ili watajirishe zaidi hao wanaowatawala kinyemela.
20231101.sw_1800_6
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ukoloni
Ukoloni
Utawala wa kikoloni ni utawala ulioanzishwa hasa na Wazungu kwa lengo la kunyonya na pengine kuwabagua Waafrika na watu wengine wenyeji wa Asia, Oseania na Amerika.
20231101.sw_1800_7
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ukoloni
Ukoloni
Baada ya kuanzisha utawala huo wakoloni walibadilisha utawala wa jadi na kuufanya utawale kwa masilahi ya wakoloni; pia utawala huo uliharibu hadhi ya utawala wa jadi na misingi ya jadi.
20231101.sw_1800_8
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ukoloni
Ukoloni
(b) Kazi katika ngazi za chini zilifanywa na wenyeji kama vile ukarani, utarishi, ufagizi na ukorokoroni.
20231101.sw_1800_9
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ukoloni
Ukoloni
Nchi za Afrika ziliwekwa rasmi chini ya ukoloni wa nchi za Ulaya mara baada ya Mkutano wa Berlin wa 1885 ulioitishwa na chansella wa Ujerumani Bismarck mwaka 1884-1885.
20231101.sw_1800_10
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ukoloni
Ukoloni
Nchi zilizojenga ukoloni huo Afrika zilikuwa Uingereza, Ufaransa, Ureno, Ujerumani, Uhispania, Italia na Ubelgiji. Uholanzi karne za nyuma ilikuwa na Afrika Kusini.
20231101.sw_1800_11
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ukoloni
Ukoloni
2. Uingereza ilikuwa na Afrika Kusini, Botswana, Cameroon ya Kiingereza, Gambia, Ghana, Kenya, Lesotho, Malawi, Mauritius, Misri, Nigeria, Shelisheli, Sierra Leone, Somaliland, Sudan, Swaziland, Tanganyika, Uganda, Zanzibar, Zambia, Zimbabwe na sehemu nyingine kwa muda.
20231101.sw_1800_12
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ukoloni
Ukoloni
3. Ufaransa ilikuwa na Algeria, Benin, Cameroon, Chad, Cote d'Ivoire, Jamhuri ya Afrika ya Kati, Jibuti, Komoro, Gabon, Guinea, Madagaska, Mali, Mauritania, Moroko, Niger, Senegal, Togo, Tunisia na sehemu nyingine kwa muda.
20231101.sw_1800_13
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ukoloni
Ukoloni
3. Ujerumani ilikuwa na Afrika ya Kusini-Magharibi ya Kijerumani (leo Namibia), Afrika ya Mashariki ya Kijerumani (tangu 1922 Burundi, Rwanda na Tanganyika), Kamerun na Togo, lakini baada ya vita vikuu vya kwanza ilinyang'anywa kila mojawapo; zilikuwa maeneo ya kudhaminiwa kwa niaba ya Shirikisho la Mataifa na kuweka chini ya Uingereza, Ufaransa, Ubelgiji na Afrika Kusini.
20231101.sw_1800_14
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ukoloni
Ukoloni
4. Italia ilikuwa na Eritrea, Libya na Somalia ya Kiitalia; pia Ethiopia kwa miaka mitano tu (1936-1941).
20231101.sw_1841_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/Burundi
Burundi
{| border="1" cellpadding="2" cellspacing="0" align="right" width="330px" style="margin-left:15px; border-collapse:collapse; border-color:#f2f2f4"
20231101.sw_1841_1
https://sw.wikipedia.org/wiki/Burundi
Burundi
|}Jamhuri ya Burundi (iliyojulikana zamani kama Urundi') ni nchi ndogo ambayo iko katika eneo la Maziwa Makubwa ya Afrika. Burundi imepakana na Rwanda upande wa kaskazini, Tanzania upande wa mashariki, na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo upande wa magharibi.
20231101.sw_1841_2
https://sw.wikipedia.org/wiki/Burundi
Burundi
Jina lenyewe la nchi hii, limetokana kwa msingi na kutanuka kwa lugha ya Kirundi ambacho ni lugha ya Kibantu kama vile Kiswahili ambacho pia kinatumika sana.
20231101.sw_1841_3
https://sw.wikipedia.org/wiki/Burundi
Burundi
Burundi ni kati ya nchi ndogo zaidi zilizomo barani Afrika. Eneo lote ni km² 27,834 pekee. Wakazi milioni 10 ni wengi kulingana na eneo dogo la nchi, msongamano wa watu ni wakazi 314.3 kwenye kila kilomita ya mraba.
20231101.sw_1841_4
https://sw.wikipedia.org/wiki/Burundi
Burundi
Ingawa Burundi haina bahari, sehemu ya mpaka wake eneo la mashariki unaishia kwenye mwambao wa Ziwa Tanganyika.
20231101.sw_1841_5
https://sw.wikipedia.org/wiki/Burundi
Burundi
Eneo lote ni nyanda za juu zenye kimo cha mita 1700 juu ya UB kwa wastani. Sehemu ya juu zaidi ni kilele cha mlima Heha chenye mita 2685 juu ya uwiano wa bahari uliopo katika safu ya milima inayopakana na bonde la ufa la Afrika ya Mashariki.
20231101.sw_1841_6
https://sw.wikipedia.org/wiki/Burundi
Burundi
Sehemu ya magharibi ya nchi ni sehemu ya bonde la ufa yenye kimo cha mita 760-850 juu ya uwiano wa bahari. Sehemu ya kusini ya bonde la ufa katika Burundi imejaa maji ya Ziwa Tanganyika.
20231101.sw_1841_7
https://sw.wikipedia.org/wiki/Burundi
Burundi
Upande wa mashariki wa safu ya milima inayopakana na bonde la ufa kuna chanzo cha mto Ruvyironza (pia: Luvironza) unaoishia katika mto Kagera na hivyo huhesabiwa kati ya vyanzo vya mto Naili.
20231101.sw_1841_8
https://sw.wikipedia.org/wiki/Burundi
Burundi
Hali ya hewa ni ya kitropiki: kuna vipindi viwili vya mvua. Joto linapungua kutokana na kimo cha nchi. Kuna mvua kwa wastani wa milimita 1,000 kwa mwaka.
20231101.sw_1841_9
https://sw.wikipedia.org/wiki/Burundi
Burundi
Matumizi ya ardhi ni kwa ajili ya kilimo au mifugo. Msongamano wa watu umesababisha kuenea kwa ukataji wa misitu, mmomonyoko wa ardhi na kupotea kwa ardhi yenye rutuba. Eneo la misitu lililobaki ni kilomita cha mraba 600 pekee linalopungua kwa kasi ya asilimia 9 kwa mwaka.
20231101.sw_1841_10
https://sw.wikipedia.org/wiki/Burundi
Burundi
Kuna hifadhi mbili za taifa ambazo ni Hifadhi ya Taifa ya Kibira kwenye kaskazini-magharibi (inapakana na Msitu wa Nyungwe huko Rwanda), na Hifadhi ya Taifa ya Ruvubu upande wa kaskazni-mashariki karibu na mto Rurubu (pia Ruvubu au Ruvuvu). Hifadhi zote mbili zilianzishwa mwaka 1982 kwa shabaha ya kuhifadhi wanyamapori.
20231101.sw_1841_11
https://sw.wikipedia.org/wiki/Burundi
Burundi
Idadi ya watu ni takriban milioni 10 na nusu. Asilimia 46 kati yao hawajamaliza miaka 15. Umri wa wastani ni miaka 16.7 hivi.
20231101.sw_1841_12
https://sw.wikipedia.org/wiki/Burundi
Burundi
Idadi ya watoto wanaoaga dunia mapema, ni 62 kati ya 1000 wanaozaliwa (mwaka 2007). Kwa umri wa kifo kwa wastani ni miaka 54 tu. Takriban 1.2% za wananchi wana UKIMWI.
20231101.sw_1841_13
https://sw.wikipedia.org/wiki/Burundi
Burundi
Vikundi kati ya wakazi ni hasa Wahutu (~80%), Watutsi (~14%) na Watwaa (mbilikimo) (chini ya 1%). Wote wanatumia lugha ya Kirundi.
20231101.sw_1841_14
https://sw.wikipedia.org/wiki/Burundi
Burundi
Pamoja na hayo, kuna Warundi wachache wanaojinasibu kuwa wao si Watutsi wala Wahutu bali ni Waswahili (~5%). Hilo kabila lilikuwepo toka enzi za tawala za kifalme nchini humo, na ndio wenyeji wa jiji la Bujumbura, waliomsaidia Mwanamfalme Louis Rwagasore katika harakati za kutafuta uhuru wa Burundi.
20231101.sw_1841_15
https://sw.wikipedia.org/wiki/Burundi
Burundi
Upande wa dini, Wakristo ni 80-90% kati ya wakazi wote, hasa Wakatoliki (65%), halafu Waprotestanti (26%). Asilimia 5 wanafuata dini za jadi na 3 Uislamu.
20231101.sw_1841_16
https://sw.wikipedia.org/wiki/Burundi
Burundi
Dola la kwanza katika eneo hili lilikuwa Ufalme wa Burundi. Katika mapokeo ya wenyeji ulianzishwa katika karne ya 17 na mtu kwa jina la Cambarantama aliyefika ama kutoka Rwanda ama kutoka Buha katika Mkoa wa Kigoma, Tanzania ya leo.
20231101.sw_1841_17
https://sw.wikipedia.org/wiki/Burundi
Burundi
Ufalme huo ulitawaliwa na kundi la Watutsi waliokuwa wafugaji wa ng'ombe na kutawala wenyeji waliokuwa wakulima Wabantu. Watutsi walikuwa tabaka la kikabaila. Mfalme au mwami alikuwa mkuu wa makabaila hao ambao walitazamiwa kama mabwana wa ardhi iliyolimwa na watu wa kawaida. Hao wakulima waliruhusiwa kulima nchi wakipaswa kutoa huduma na sehemu ya mavuno kwa mabwana waliopaswa kuwatetea dhidi ya maadui.
20231101.sw_1841_18
https://sw.wikipedia.org/wiki/Burundi
Burundi
Ufalme huo ulienea katika karne zilizofuata. Mwami Ntare IV Rutaganzwa Rugamba aliyetawala tangu mwaka 1796 hadi 1850 aliweza kupanua mipaka ya ufalme wake hadi kushika sehemu kubwa ya eneo la leo.
20231101.sw_1841_19
https://sw.wikipedia.org/wiki/Burundi
Burundi
Wazungu wa kwanza waliofika walikuwa wapelelezi Waingereza Richard Burton na John Hanning Speke mnamo mwaka 1854. Lakini habari za falme kwenye eneo kati ya maziwa makubwa hazikuenea sana. Wakati wa Mkutano wa Berlin 1885 Wajerumani hawakujua ya kwamba falme za Burundi na Rwanda zilikuwepo ndani ya eneo waliotegemea kutwaa. Waliitambua baadaye tu.
20231101.sw_1841_20
https://sw.wikipedia.org/wiki/Burundi
Burundi
Mwaka 1894 Mjerumani wa kwanza alipita Burundi aliyekuwa Oskar Baumann. Wakati ule Ujerumani uliwahi tayari kuanzisha koloni ya Afrika ya Mashariki ya Kijerumani lakini Wajerumani walichelewa kufika kaskazini-magharibi mwa maeneo waliyotazama kuwa sehemu yao.
20231101.sw_1841_21
https://sw.wikipedia.org/wiki/Burundi
Burundi
Katika Burundi kikosi cha kwanza cha Kijerumani kilifika mnamo 1896 wakakuta ufalme wa mwami wakaridhika kumwacha mwakilishi mkazi (resident) katika mji mkuu Gitega ambaye hakuhusika na mambo ya utawala wa ndani. Wakati ule eneo lilijulikana kwa jina "Urundi". Hapa sawa na Rwanda na Bukoba Wajerumani walitumia mbinu ya eneo lindwa ingawa walikuwa pia na majadiliano kuingiza falme hizi za kienyeji moja kwa moja ndani ya koloni lao.
20231101.sw_1841_22
https://sw.wikipedia.org/wiki/Burundi
Burundi
Baada ya Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia Burundi pamoja na Rwanda ilikabidhiwa kwa Ubelgiji kwa niaba ya Shirikisho la Mataifa kama eneo la kudhaminiwa lililoitwa Ruanda-Urundi. Kimsingi Wabelgiji waliendelea na mfumo wa Wajerumani uliomwachia mtemi mamlaka kubwa. Waliweka Ruanda-Urundi chini ya serikali ya Kongo ya Kibelgiji.
20231101.sw_1841_23
https://sw.wikipedia.org/wiki/Burundi
Burundi
Lakini baadaye walianza kuingilia zaidi, na ilhali wakati ule walipendelea Watutsi, karibu machifu wote walikuwa Watutsi, na Wahutu walipotea katika nafasi za uongozi kimahali.
20231101.sw_1841_24
https://sw.wikipedia.org/wiki/Burundi
Burundi
Tangu mwaka 1946 Shirikisho la Mataifa lilikwisha na Ubelgiji ilipokea wito wa kutawala Ruanda-Urundi na Umoja wa Mataifa.
20231101.sw_1841_25
https://sw.wikipedia.org/wiki/Burundi
Burundi
Mwaka moja kabla ya uhuru kulikuwa na uchaguzi wa kwanza chini ya usimamizi ya UM na chama mshindi kilikuwa UPRONA kilichoongozwa na mwanamfalme Mtutsi Louis Rwagasore aliyemwoa mwanamke wa Kihutu na chama kiliunganisha pande zote mbili. Lakini miezi michache baadaye Rwagasore aliuawa na chama chake kilitengana kufuatana na ukabila.
20231101.sw_1841_26
https://sw.wikipedia.org/wiki/Burundi
Burundi
Baada ya uchaguzi wa 1965 mapigano yalitokea kwa silaha, na kikundi cha Watutsi wakali kilichukua serikali.
20231101.sw_1841_27
https://sw.wikipedia.org/wiki/Burundi
Burundi
Mwaka 1966 mwami alipinduliwa na mwanasiasa Michel Micombero aliyejitangaza kuwa rais na nchi kuwa jamhuri. Kuanzia hapo wanasiasa na watumishi wakubwa walio Wahutu walifukuzwa, kukamatwa au kuuawa.
20231101.sw_1841_28
https://sw.wikipedia.org/wiki/Burundi
Burundi
Burundi ilundwa kama ufalme ulioongozwa na Watutsi waliotawala Wahutu. Lakini kabla ya ukoloni mipaka kati ya makundi hayo haikuwa imara mno; Wahutu matajiri katika utumishi wa mwami waliweza kupanda ngazi na kuwa Watutsi na pia Watutsi maskini waliweza kushuka ngazi na kuhesabiwa kati ya Wahutu, hasa baada ya kuoa au kuolewa na mtu wa upande mwingine. Uhusiano wa makundi hayo ulifanana zaidi na ule wa matabaka si wa makabila tofauti, pia kwa sababu lugha ilikuwa moja kwa wote.
20231101.sw_1841_29
https://sw.wikipedia.org/wiki/Burundi
Burundi
Utawala wa kikoloni uliimarisha mipaka kati ya makundi hayo mawili maana kila mtu aliandikishwa na kupangwa katika moja kati ya makundi hayo. Pia Wabelgiji walipendelea Watutsi na kuangalia wapate nafasi zote za uchifu ambako walipaswa kutoa kibali. Kuhamia katika kundi lingine kulikwisha. Uhusiano kati ya makundi ulianza kufanana zaidi na ukabila.
20231101.sw_1841_30
https://sw.wikipedia.org/wiki/Burundi
Burundi
Katika hali hiyo Burundi ilikaribia uhuru. Vyama vya siasa viliundwa vilivyofuata ugawaji wa kimbari kati ya Watutsi na Wahutu. Mapigano ya kwanza kati ya Wahutu na Watutsi yalitokea mwaka 1959 kabla ya uhuru yakakomeshwa na Wabelgiji.
20231101.sw_1841_31
https://sw.wikipedia.org/wiki/Burundi
Burundi
Baada ya uhuru katika Burundi, kinyume na Rwanda, utawala ulibaki upande wa Watutsi kwa sababu jeshi lilikuwa mikononi mwao. Vipindi vya mashambulio kati ya vikundi vilifuata.
20231101.sw_1841_32
https://sw.wikipedia.org/wiki/Burundi
Burundi
Mwaka 1993 uongozi wa Kitutsi ulikubali tena uchaguzi huru ambako Mhutu Melchior Ndadaye alichaguliwa kuwa rais. Alipouawa na wanajeshi Watutsi malaki ya Watutsi waliuawa na Wahutu wakali.
20231101.sw_1841_33
https://sw.wikipedia.org/wiki/Burundi
Burundi
Tangu mwaka 1995 Umoja wa Afrika na Umoja wa Mataifa zilijitahidi kujenga mapatano kati ya vikundi. Marais na wanasiasa walioshiriki katika jitihada hizo walikuwa pamoja na Julius Nyerere, Boutros Boutros-Ghali, Nelson Mandela, Thabo Mbeki na rais wa Marekani Bill Clinton.
20231101.sw_1841_34
https://sw.wikipedia.org/wiki/Burundi
Burundi
Mapatano yalifikiwa na kusainiwa mwaka 2000 na washiriki karibu wote huko Arusha. Majadiliano yaliendelea hadi mwaka 2003 hatimaye vita ilisimamishwa. Mapatano yaliyofikiwa yanasema ya kwamba Watutsi pamoja na Watwa, ambao ni asilimia 15 za wananchi, watakuwa na asilimia 40 ya nafasi kwenye bunge na ya kwamba jeshini kila upande utashika asilimia 50 za nafasi. Pia kwenye senati ya bunge kila upande utakuwa na asilimia 50.
20231101.sw_1841_35
https://sw.wikipedia.org/wiki/Burundi
Burundi
Mwaka 2005 uchaguzi wa kwanza wa bunge baada ya vita ya wenyewe kwa wenyewe ulifanyika. Chama cha CNDD-FDD kilipata kura nyingi na kiongozi chake Pierre Nkurunziza alichaguliwa na bunge kuwa rais wa taifa. Vyama vya UPRONA na FRODEBU vilivyotangulia kuongoza serikali ya mpito vilipata kura chache kwa sababu vilishtakiwa kuwa na rushwa na upendeleo wa kindugu.
20231101.sw_1841_36
https://sw.wikipedia.org/wiki/Burundi
Burundi
Chama tawala kinajaribu kufuata siasa ya mapatano ya ndani, lakini ina uvumilivu mdogo tu kwa upinzani na mawazo yanayopinga siasa yake.
20231101.sw_1841_37
https://sw.wikipedia.org/wiki/Burundi
Burundi
Mwezi Aprili 2009 chama cha Palipehutu FNL hatimaye kilisimamisha upinzani kwa silaha kikakubaliwa kama chama cha kisiasa cha FNL.
20231101.sw_1841_38
https://sw.wikipedia.org/wiki/Burundi
Burundi
Nkurunziza alichaguliwa tena kwa kura ya wananchi wote mwaka 2010. Chama cha upinzani FNL kilikataa kukubali ushindi wa CNDD-FDD.
20231101.sw_1841_39
https://sw.wikipedia.org/wiki/Burundi
Burundi
Mwaka 2015 rais Nkurunziza alipendekezwa kugombea tena urais katika uchaguzi akakubali. Hatua hiyo ilisababisha upinzani mkali wa wananchi walioandamana wakiona hii inavunja mapatano ya amani ya Arusha.
20231101.sw_1841_40
https://sw.wikipedia.org/wiki/Burundi
Burundi
Tarehe 13 Mei jenerali Godefroid Niyombare alitangaza kufukuzwa kwa Nkurunziza kutoka urais wakati huyo alikuwa safarini Tanzania, lakini uasi huu wa kijeshi ulikandamizwa.
20231101.sw_1841_41
https://sw.wikipedia.org/wiki/Burundi
Burundi
Nkurunziza alirudi na kutangaza ya kwamba kura inatakiwa kufanyika jinsi ilivyopangwa tarehe 26 Mei 2015 kwa bunge na tarehe 26 Juni kwa urais.
20231101.sw_1841_42
https://sw.wikipedia.org/wiki/Burundi
Burundi
Taasisi ya kimataifa na nchi jirani walitamka wasiwasi kuhusu mwelekeo wa hali ya kisiasa katika Burundi. Nkosazana Dlamini-Zuma, mwenyekiti wa kamati tendaji ya Umoja wa Afrika, aliomba kuahirishwa kwa kura nchini Burundi hadi hali iwe imetulia.
20231101.sw_1841_43
https://sw.wikipedia.org/wiki/Burundi
Burundi
Tarehe 24 Julai 2015 Tume ya Uchaguzi ilimtangaza Nkurunziza mshindi wa uchaguzi kwa 69.41% za kura. Agathon Rwasa alishika nafasi ya pili kwa 18.99% ingawa alikuwa amehimiza wananchi wasipige kura.
20231101.sw_1841_44
https://sw.wikipedia.org/wiki/Burundi
Burundi
Kilichofuata kimesababisha wananchi 200,000 wakimbie, huko rais akikataza Umoja wa Afrika usitume askari kulinda amani na haki nchini, wakati wanajeshi wanaendelea kuua na kunyanyasa Watutsi wakielekea mauaji ya kimbari.
20231101.sw_1841_45
https://sw.wikipedia.org/wiki/Burundi
Burundi
Burundi imegawiwa katika mikoa 17 (kwa Kifaransa province, kwa Kirundi: IProvense) inayoitwa kufuatana na miji yenye makao makuu ya utawala.
20231101.sw_1841_46
https://sw.wikipedia.org/wiki/Burundi
Burundi
Mambo mengi ya Burundi yamepatikana kutoka CIA World Factbook 2000 na 2003 U.S. Department of State website.
20231101.sw_1841_47
https://sw.wikipedia.org/wiki/Burundi
Burundi
Updated humanitarian news from the United Nations Office for the Coordination of Humanitarian Affairs
20231101.sw_1843_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/Eritrea
Eritrea
Eritrea ni nchi ya Afrika ya Mashariki. Mashariki na Kusini-Mashariki Eritrea ina pwani ndefu katika Bahari ya Shamu.
20231101.sw_1843_1
https://sw.wikipedia.org/wiki/Eritrea
Eritrea
Upande wa Magharibi imepakana na Sudan, upande wa Kusini imepakana na Ethiopia, na Kusini-Mashariki kuna nchi ya Djibouti. Eneo hili lote hujulikana pia kama Pembe ya Afrika.
20231101.sw_1843_2
https://sw.wikipedia.org/wiki/Eritrea
Eritrea
Jina la nchi limetungwa mnamo mwaka 1890 na wakoloni wa Italia kutokana na neno la Kigiriki "erythraîa" linalomaanisha “bahari nyekundu” – kwa Kiingereza “Red Sea”. Hii ni kwa sababu Bahari ya Shamu iliitwa "Sinus Erythraeus" na mabaharia Wagiriki au “Mare Erythraeum” kwa Kilatini na Waroma wa kale – maana yake ni "bahari nyekundu".
20231101.sw_1843_3
https://sw.wikipedia.org/wiki/Eritrea
Eritrea
Eritrea iko katika eneo la Pembe la Afrika na ina Bahari ya Shamu upande wa kaskazini mashariki. Kwa mchanga wa pwani ulio eneo kame pahali pa kutega samaki ni Funguvisiwa la Dahlak.
20231101.sw_1843_4
https://sw.wikipedia.org/wiki/Eritrea
Eritrea
Eneo ambalo liko kwa milima kusini si kame vile, lakini hali ya hewa ni poa. Mlima wa juu zaidi ni Soira, ambao uko kati ya nchi, mita 3018 juu ya bahari.
20231101.sw_1843_5
https://sw.wikipedia.org/wiki/Eritrea
Eritrea
Mji mkuu wa Eritrea ni Asmara na miji mingine ni kama vile mji wa bandari Assab kusini mashariki, na pia miji kama Massawa na Keren.
20231101.sw_1843_6
https://sw.wikipedia.org/wiki/Eritrea
Eritrea
Pwani ilikaa karne nyingi chini ya utawala wa Uturuki au baadaye Misri kama nchi zenye nguvu kwenye Bahari ya Shamu.
20231101.sw_1843_7
https://sw.wikipedia.org/wiki/Eritrea
Eritrea
Historia ya Eritrea kama eneo la pekee jinsi ilivyopata uhuru mwisho wa karne ya 20 ilianza na ukoloni wa Italia.
20231101.sw_1843_8
https://sw.wikipedia.org/wiki/Eritrea
Eritrea
Mnamo Novemba 1869 kampuni ya biashara ya Kiitalia ya Rubattino ilinunua bandari ya Assab kutoka kwa sultani wa Afar. Ilikuwa inatafuta kituo kwa meli zake zilizoanza kupita katika bahari ya Shamu baada ya kufunguliwa kwa Mfereji wa Suez mwaka uleule.
20231101.sw_1843_9
https://sw.wikipedia.org/wiki/Eritrea
Eritrea
Serikali ya Misri ilipinga mapatano hayo kwa sababu ilidai eneo lilikuwa chini ya amri yake. Makubaliano hayakufikiwa hadi 1882, serikali ya Italia ilipochukua moja kwa moja mali ya kampuni kama koloni lake la kwanza katika Afrika.
20231101.sw_1843_10
https://sw.wikipedia.org/wiki/Eritrea
Eritrea
Tangu kuporomoka kwa utawala wa Misri nchini Sudan, baada ya vita vya Al-Mahdi, Misri ilijiondoa pia katika pwani ya kusini mwa bahari ya Shamu. Italia ilitumia nafasi hiyo na tarehe 5 Februari 1885 ilipeleka wanajeshi mjini Massawa na kuitangaza kuwa koloni lake.
20231101.sw_1843_11
https://sw.wikipedia.org/wiki/Eritrea
Eritrea
Waitalia waliendelea kuunganisha maeneo yao ya Assab na Massawa. Baadaye walijaribu kupanua utawala wao kutoka tambarare za pwani hadi nyanda za juu zilizokuwa chini ya Dola la Ethiopia.
20231101.sw_1843_12
https://sw.wikipedia.org/wiki/Eritrea
Eritrea
Negus Yohanne IV hakufurahia kufika kwa Italia kwa sababu aliamini ya kwamba Massawa iliahidiwa kwake baada ya kuwasaidia Wamisri kujiokoa mbele ya jeshi la Al-Mahdi. Hivyo upanuzi wa Italia katika nyanda za juu ulikutana na upinzani.
20231101.sw_1843_13
https://sw.wikipedia.org/wiki/Eritrea
Eritrea
Tarehe 26 Januari 1887 jeshi la Waitalia 587 walioelekea kaskazini lilishambuliwa karibu na Massawa kwenye kijiji cha Dogali na kushindwa na Ras Alula aliyekuwa mtemi chini ya Negus ya Ethiopia. Waitalia walipaswa kuongeza wanajeshi 13,000 ili kuhakikisha utawala wao.
20231101.sw_1843_14
https://sw.wikipedia.org/wiki/Eritrea
Eritrea
Baada ya Yohanne IV kufariki katika mapigano na jeshi la Al-Mahdi, Waitalia walichukua nafasi hiyo ya kuziingia nyanda za juu za Tigray na kujenga vituo vyao huko.
20231101.sw_1843_15
https://sw.wikipedia.org/wiki/Eritrea
Eritrea
Mfalme mpya Menelik II tarehe 2 Mei 1889 aliutia sahihi mkataba wa Wuchale uliokubali utawala wa Italia juu ya kanda ya pwani pamoja na maeneo kadhaa ya nyanda za juu za Tigray.
20231101.sw_1843_16
https://sw.wikipedia.org/wiki/Eritrea
Eritrea
Waitalia walijaribu kumdanganya Negus katika mkataba huo kwa kuingiza maneno katika nakala ya Kiitalia yaliyosema "Ethiopia itakuwa chini ya ulinzi wa Italia". Menelik baada ya kuelewa haya alikana mkataba.
20231101.sw_1843_17
https://sw.wikipedia.org/wiki/Eritrea
Eritrea
Italia ilijibu kwa kuvamia Ethiopia kwa jeshi kubwa. Jeshi hilo lilishindwa na Waethiopia katika mapigano ya Adowa tarehe 1 Machi 1896. Italia ilipaswa kukubali uhuru wa Ethiopia katika mkataba wa amani tarehe 26 Oktoba 1896. Ethiopia ilikubali mamlaka ya Italia juu ya koloni lake katika kaskazini.
20231101.sw_1843_18
https://sw.wikipedia.org/wiki/Eritrea
Eritrea
Baada ya kumaliza mashindano na Ethiopia, Italia tarehe 1 Januari 1890 iliunganisha maeneo yake yote katika koloni lililoitwa Eritrea kufuatana na jina la kale "Bahari ya Eritrea".
20231101.sw_1843_19
https://sw.wikipedia.org/wiki/Eritrea
Eritrea
Katika kipindi hiki cha utawala wa kikoloni Eritrea ilitokea kama jamii na eneo la pekee. Koloni la Eritrea liliunganisha maeneo matatu yenye tabia za pekee:
20231101.sw_1843_20
https://sw.wikipedia.org/wiki/Eritrea
Eritrea
kanda la pwani lililokuwa na historia ndefu ya biashara na mawasiliano na Uarabuni ng'ambo ya Bahari ya Shamu
20231101.sw_1843_21
https://sw.wikipedia.org/wiki/Eritrea
Eritrea
Italia ilianzisha miradi ya kufanya Eritrea chanzo cha malighafi kwa ajili ya uchumi wa Italia. Kijiji cha Asmara katika nyanda za juu kilikuwa mji mkuu wa koloni na kupanuliwa kuwa mji kwa ajili ya walowezi Waitalia. Asmara ilipambwa na majengo mazuri ya kisasa.
20231101.sw_1843_22
https://sw.wikipedia.org/wiki/Eritrea
Eritrea
Katika miaka ya 1930 idadi ya motokaa zilizoendeshwa Asmara ilishinda idadi ya magari ya binafsi mjini Roma. Urithi huo wa majengo umekuwa sababu ya kuingiza Asmara katika orodha ya Urithi wa dunia ya UNESCO.
20231101.sw_1843_23
https://sw.wikipedia.org/wiki/Eritrea
Eritrea
Waitalia walipanga na kujenga miji mingine kama vitovu vya biashara, mabandari, vituo vya kijeshi au vya kiuchumi.
20231101.sw_1843_24
https://sw.wikipedia.org/wiki/Eritrea
Eritrea
Idadi ya wakazi wote ilikadiriwa kuwa takriban 200,000 mwaka 1890. Idadi hiyo iliongezeka haraka kufikia zaidi ya 600,000 mnamo 1939. Mabadiliko makubwa yalitokea hasa katika nyanda za juu ambako walowezi Waitalia walianzisha mashamba yao na miji mikubwa zaidi ilijengwa.
20231101.sw_1843_25
https://sw.wikipedia.org/wiki/Eritrea
Eritrea
Idadi ya wasemaji wa Kitigrinya iliongezeka kutoka asilimia 35 mwaka 1905 kuwa asilimia 54 mwaka 1939.
20231101.sw_1843_26
https://sw.wikipedia.org/wiki/Eritrea
Eritrea
Mwisho wa vita kati ya vikundi mbalimbali na kupatikana kwa huduma za kiafya pamoja na kuongezeka kwa upatikanaji wa chakula, vyote vilichangia katika kuongezeka kwa idadi ya watu.
20231101.sw_1843_27
https://sw.wikipedia.org/wiki/Eritrea
Eritrea
Kati ya mabadiliko makubwa ulikuwa ujenzi wa barabara na reli kati ya Massawa, Asmara, Keren na Agordat. Viwanda kadhaa vilianzishwa, pia migodi ya kuchimba mawe au madini.
20231101.sw_1843_28
https://sw.wikipedia.org/wiki/Eritrea
Eritrea
Sehemu za Waeritrea waliingia katika maisha ya ajira ya kibepari. Hivyo maarifa ya wakazi wa Eritrea hasa katika nyanda za juu yalikuwa tofauti na wenzao katika Ethiopia yenyewe walioendelea kuishi chini ya utaratibu wa kikabaila. Waeritrea walisukumwa katika maisha ya kisasa na uchumi wa fedha.
20231101.sw_1843_29
https://sw.wikipedia.org/wiki/Eritrea
Eritrea
Hadi mwaka 1940 Eritrea ilikuwa tayari na tabaka la wafanyakazi wa viwandani na katika miji pia tabaka la wasomi wenye elimu ya kisasa.
20231101.sw_1843_30
https://sw.wikipedia.org/wiki/Eritrea
Eritrea
Baada ya Mussolini kushika serikali, siasa ya Italia ilibadilika. Wafashisti walidharau Waafrika na kuanzisha siasa ya ubaguzi wa rangi. Wenyeji walipewa tu shughuli duni kabisa katika utumishi wa serikali.
20231101.sw_1843_31
https://sw.wikipedia.org/wiki/Eritrea
Eritrea
Italia ya kifashisti ilifanya mipango ya kulipizia kisasi mapigano ya Adowa ikiandaa vita dhidi ya Ethiopia. Vita vilianza mwaka 1935 kutoka ardhi ya Eritrea. Silaha mpya za Italia (zikiwemo za kikemikali) zilishinda jeshi la Negus, hivyo Ethiopia yote ikawa koloni la Italia kwa miaka michache.
20231101.sw_1843_32
https://sw.wikipedia.org/wiki/Eritrea
Eritrea
Waitalia walishindwa katika Vita Vikuu vya Pili mwaka 1941, ambapo Waingereza waliteka Ethiopia pamoja na Eritrea.
20231101.sw_1843_33
https://sw.wikipedia.org/wiki/Eritrea
Eritrea
Mwaka huo Umoja wa Mataifa ulikabidhi Eritrea kwa Ethiopia kama eneo la pekee lenye serikali na bunge lake katika shirikisho.
20231101.sw_1843_34
https://sw.wikipedia.org/wiki/Eritrea
Eritrea
Mfalme wa Ethiopia, Haile Selassie hakupendezwa na utaratibu huoː alilenga kuunganisha tena Eritrea na Ethiopia na kwa mbinu mbalimbali alipata kura ya bunge la Eritrea ya kujivunja na kuwa jimbo la Ethiopia (1962).
20231101.sw_1843_35
https://sw.wikipedia.org/wiki/Eritrea
Eritrea
Vita vilitapakaa mwaka 1974 baada ya ufalme kupinduliwa na Umaksi kuingia na rundo la Jeshi lililoitwa Derg kuchukuwa mamlaka, na baadaye kuvamia Eritrea. Ukorofi wa serikali ya Mengistu Haile Mariam ulifanya mengi kuongeza waliotumaini uhuru wa Eritrea katika miaka ya 1980.
20231101.sw_1843_36
https://sw.wikipedia.org/wiki/Eritrea
Eritrea
Ukombozi wa Eritrea ulitegemea rundo la Eritrean Liberation Front (ELF), ambayo pia inaitwa "Jebha", na Eritrean People's Liberation Front (EPLF), ambaye pia inaitwa "Shaabia". ELF ilikuwa na Waislamu wengi wa pwani na wahifadhi wa tedo za wananchi, na EPLF wengi Wakristo kutoka nyanda za juu za Tigrayi waamini wa Umaksi-Ulenin. ELF ilisaidiwa na wafadhili Waarabu, na EPLF kutoka nchi za kikomunisti zilizokuwa upande wa Urusi, lakini baadaye nchi hizo zikapinduka na kusaidia Derg ya Mengistu Haile Mariam. ELF na EPLF hazikuweza kufanya kazi pamoja na kwa hiyo EPLF ikaimaliza ELF na kuendelea kutafuta uhuru.
20231101.sw_1843_37
https://sw.wikipedia.org/wiki/Eritrea
Eritrea
Vita vya uhuru vilikwisha mwaka 1991, ambapo Waeritrea na waasi Waethiopia kutoka Tigray walishinda jeshi la Ethiopia na kuteka Addis Ababa; serikali ya Derg ikaanguka miaka miwili baadaye.
20231101.sw_1843_38
https://sw.wikipedia.org/wiki/Eritrea
Eritrea
Baada ya kura ya wakazi wa Eritrea kukubali karibu kwa kauli moja, uhuru wa nchi ulitangazwa tarehe 24 Mei 1993 na kukubaliwa kimataifa.
20231101.sw_1843_39
https://sw.wikipedia.org/wiki/Eritrea
Eritrea
Awali uhusiano na serikali mpya ya Ethiopia ulikuwa mzuri, lakini baada ya miaka ya kwanza ulizorota.