_id
stringlengths 15
22
| url
stringlengths 31
150
| title
stringlengths 1
86
| text
stringlengths 100
23.8k
|
---|---|---|---|
20231101.sw_1843_40
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Eritrea
|
Eritrea
|
Mwaka 1998 kulitokea vita kati ya Eritrea na Ethiopia vilivyokwisha na ushindi wa Ethiopia. Wanajeshi la kulinda amani la UM wanajaribu kutunza hali ya kutopigana.
|
20231101.sw_1843_41
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Eritrea
|
Eritrea
|
Kiongozi wa EPLF, Isaias Afewerki, akawa Rais. Eritrea (EPLF or Shaebia), ikawa chama pekee kinachotawala Eritrea kwa sheria na kubadilisha jina People's Front for Democracy and Justice (PFDJ).
|
20231101.sw_1843_42
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Eritrea
|
Eritrea
|
Mwaka 1998, vita vya mpaka na Ethiopia vilileta kifo kwa wanajeshi wengi kwa nchi zote mbili, na Eritrea uchumi wake ukafifia na wananchi wakahangaika sana. Umma wa nchi ukanza kuhama na uchumi kukosa maendeleo. Eritrea ni nchi moja ya Afrika ambapo kuna shida ya mabomu ya ardhi. Serikali ya Ethiopia iliwafukuza WaEritrea ambao waiishi Ethiopia ama watu waliokuwa na utamaduni wa Eritrea baada ya vita na Eritrea. Hii iliwaletea Waeritrea shida na uhamaji.
|
20231101.sw_1843_43
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Eritrea
|
Eritrea
|
Hata baada ya kuonyesha maendeleo kidogo kwa uchumi na siasa, serikali ya Eritrea inanyanyasa magazeti na waandishi na pia watu kwa siasa. Serikali yenyewe hata haijaweza kuweka Katiba mpya na kuleta kura ya kidemokrasia.
|
20231101.sw_1843_44
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Eritrea
|
Eritrea
|
Baadaye, serikali ya Eritrea imeweza kusisitiza desturi ya ukoloni wa Waitalia ambayo inadai Kanisa na Dini kujiandikisha kwa serikali na kupewa ruhusa wa kuhubiri. Dini zilizopewa ruhusa na serikali ni Kanisa la Kiorthodoksi la Eritrea, Kanisa Katoliki, Kanisa la Mekane Yesus (Walutheri) na Uislamu. Nyingine zote, hasa zenye itikadi kali zimebanwa kote nchini.
|
20231101.sw_1843_45
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Eritrea
|
Eritrea
|
Vita vya Eritrea na Ethiopia viliisha mwaka 2000 kwa mashauriano yanayojulikana kama Mapatano ya Algiers. Mojawapo ya makubaliano lilikuwa kuanzisha Muungano wa kimataifa wa kuweka amani, ambao unajulikana kama Muungano wa Kimataifa wa misheni ya Eritrea na Ethiopia (UNMEE); Walinda amani 4,000 wa UM wamebaki kutoka mwezi Agosti 2004.
|
20231101.sw_1843_46
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Eritrea
|
Eritrea
|
Makubaliano mengine ya Algiers yalikuwa kuanzisha usawazisho wa mwisho wa mpaka uliyobishaniwa kati ya Eritrea na Ethiopia. Komisheni iliyokuwa na madaraka kutoka kwa UM, iliyoitwa Komisheni ya Mpaka wa Ethiopia na Eritrea (EEBC), baada ya mashauriano mrefu, ilikata maamuzi ya mwisho mnamo Aprili 2002, lakini maamuzi yao yakakataliwa na Ethiopia.
|
20231101.sw_1843_47
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Eritrea
|
Eritrea
|
Kutoka Oktoba 2005 bishano la mpaka bado lilibaki kuwa suala nyeti, na wanajeshi wa kulinda amani wa UM walijaribu kutunza hali ya kutopigana.
|
20231101.sw_1843_48
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Eritrea
|
Eritrea
|
Bunge la Taifa la viti 150, liliyotekezwa mwaka 1993 baada ya Uhuru, lilimchagua Rais wa sasa, Isaias Afewerki. Kura za nchi huwa zinapangwa na kupanguliwa.
|
20231101.sw_1843_49
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Eritrea
|
Eritrea
|
Shina za taarifa madaraka za kutangaza habari kwa siasa za nyumbani Eritrea haziko; na Septemba 2001 serikali ilifunga vyombo vya habari vya binafsi, na watu wanaopinga serikali hufungwa bila kushtakiwa. Hii yote ni kutoka taarifa ya washufu wa ulimwengu, kama Waangalizi wa haki za Kibinadamu (Human Rights Watch) na Wakombozi wa Kimataifa (Amnesty International).
|
20231101.sw_1843_50
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Eritrea
|
Eritrea
|
Mambo ya nje yanahusu vita na Ethiopia, Sudan na Jibuti. Baada ya wajumbe wa serikali ya Eritrea wa Idara ya mambo ya kigeni kuenda Sudan, ushirikiano umeanza kuwa wa kawaida. Bishano na Ethiopia bado ni wazo kubwa la chuki ambalo limemfanya Rais kuuambia Umoja wa Mataifa ichukue hatua. Uagizaji huu umeelezwa kwa barua kumi na moja za Rais.
|
20231101.sw_1843_51
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Eritrea
|
Eritrea
|
Makabila makubwa ni Watigrinya (55%) na Watigre (30%), ambao wote wawanazungumza lugha za Kiafrika-Kiasia.
|
20231101.sw_1843_52
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Eritrea
|
Eritrea
|
Nchi haina lugha rasmi ili kuheshimu sawasawa lugha zote. Hata hivyo Kitigrinya, Kiarabu na Kiingereza vina nafasi za pekee.
|
20231101.sw_1843_53
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Eritrea
|
Eritrea
|
Serikali inatambua rasmi Kanisa la Kiorthodoksi la Eritrea, Kanisa Katoliki na Kanisa la Kiinjili la Kilutheri pamoja na Uislamu. Makadirio yanatofautiana: Wakristo kwa jumla ni 50-68%, Waislamu 36-48%.
|
20231101.sw_1843_54
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Eritrea
|
Eritrea
|
Mwaka 2004 Idara ya taifa ya Marekani (U.S. State Department) iliamua kwamba Eritrea ni Nchi mahsusi ya kufuatiliwa (Country of Particular Concern, au CPC) kwa kufinya uhuru wa dini.
|
20231101.sw_1848_0
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Umoja%20wa%20Mataifa
|
Umoja wa Mataifa
|
Umoja wa Mataifa (UM) (Kiingereza: United Nations, UN) ni shirika la kiserikali ambalo malengo yake ni kudumisha amani na usalama wa kimataifa, kuendeleza uhusiano wa kirafiki kati ya mataifa, kufikia ushirikiano wa kimataifa, na kuwa kituo cha kuoanisha matendo ya mataifa. Ni umoja wa nchi zote duniani isipokuwa zile zisizotambuliwa kuwa dola huru.
|
20231101.sw_1848_1
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Umoja%20wa%20Mataifa
|
Umoja wa Mataifa
|
Umoja huo ulianzishwa na nchi washindi wa Vita Kuu ya Pili ya Dunia kuchukua nafasi ya Shirikisho la Mataifa (1919 - 1946). Makubaliano yalifikiwa tarehe 24 Oktoba 1945 huko San Francisco, California.
|
20231101.sw_1848_2
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Umoja%20wa%20Mataifa
|
Umoja wa Mataifa
|
Mwanzoni nchi zilikuwa 51 lakini kufikia mwaka 2017 kulikuwa na nchi wanachama 193, mbali ya Ukulu mtakatifu (Vatikani) na Palestina ambazo zinashiriki kama watazamaji wa kudumu, zikiwa na haki karibu zote isipokuwa kupiga kura.
|
20231101.sw_1848_3
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Umoja%20wa%20Mataifa
|
Umoja wa Mataifa
|
Dhumuni la umoja huu ni kuratibu mahusiano ya kimataifa kupitia sheria na mikataba ya kimataifa kwenye maeneo kama usalama, amani, maendeleo ya jamii na ya uchumi, haki za binadamu, uhuru, demokrasia n.k.
|
20231101.sw_1848_4
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Umoja%20wa%20Mataifa
|
Umoja wa Mataifa
|
Toka mwanzo makao makuu ya Umoja wa Mataifa yako Manhattan, New York City, New York nchini Marekani na hayako chini ya mamlaka ya nchi hiyo. Ofisi nyingine ziko Geneva (Uswisi), Nairobi (Kenya) na Vienna (Austria).
|
20231101.sw_1848_5
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Umoja%20wa%20Mataifa
|
Umoja wa Mataifa
|
Katibu Mkuu wa UM anachaguliwa kwa miaka mitano; kwa sasa ni António Guterres kutoka Ureno, aliyechaguliwa kuwa Katibu Mkuu mwaka 2016 akichukua nafasi ya Ban Ki-moon.
|
20231101.sw_1848_6
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Umoja%20wa%20Mataifa
|
Umoja wa Mataifa
|
UNESCO (United Nations Educational, Scientific and Cultural Organization) - Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi, na Utamaduni
|
20231101.sw_1848_7
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Umoja%20wa%20Mataifa
|
Umoja wa Mataifa
|
UNCTAD (United Nations Conference on Trade and Development) - Mkutano wa Kimataifa kuhusu Biashara na Maendeleo
|
20231101.sw_1848_8
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Umoja%20wa%20Mataifa
|
Umoja wa Mataifa
|
IAEA (Shirika la Kimataifa la Nishati ya Nyuklia) inashirikiana na UM na kutoa taarifa kwa Baraza la Usalama hata kama si chini ya katiba ya UM
|
20231101.sw_1855_0
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Marijani%20Rajab
|
Marijani Rajab
|
Marijani Rajabu (3 Machi 1955 - 23 Machi 1995) alikuwa mwanamuziki maarufu katika miondoko ya muziki wa dansi kutoka nchini Tanzania.
|
20231101.sw_1855_1
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Marijani%20Rajab
|
Marijani Rajab
|
Historia ya gwiji huyu ilianzia siku alipozaliw,a tarehe 23 Machi mwaka 1955, katika eneo la Kariakoo. Mama yake alikuwa mama wa nyumbani wakati baba yake alikuwa anafanya shughuli za uchapishaji. Maisha yake ya utoto yalikuwa ya kawaida ila alikuwa akipenda sana uimbaji wa Tabu Ley na mwimbaji mmoja wa Guinea Sorry Kandia. Alisoma shule ya Msingi ikiambatana na elimu ya Madrasa. Mwaka 1970 Akiwa bado shuleni, utaona umri wake ulikuwa miaka 15 tu, alijiunga na STC Jazz, ikiwa chini ya mpiga gitaa maarufu wakati huo Raphael Sabuni, kabla ya hapo bendi hii ilikuwa ikijulikana kama The Jets.
|
20231101.sw_1855_2
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Marijani%20Rajab
|
Marijani Rajab
|
Katika bendi hii Marijani aliweza kutoka nje ya Tanzania kwa mara ya kwanza ambapo alikwenda Nairobi na kurekodi nyimbo zilizotoka katika label ya Phillips. Hili jambo la mwanafunzi kusafiri na bendi likaleta shida na kwa vile (STC) ilikuwa mali ya umma akaachishwa kazi na mwaka1972 alijiunga na The Trippers ya David Mussa ambayo kwa wakati huo ilikuwa inapiga zaidi nyimbo za hoteli na za kukopi na muimbaji wao kiongozi wakati huo alikuwa Ali Rajabu.
|
20231101.sw_1855_3
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Marijani%20Rajab
|
Marijani Rajab
|
Hapa ndipo ubora wake ulifunguka haswa na kuweza kuinyanyua Trippers, ambayo sasa ilibadili jina na kuwa Safari Trippers kutokana na msimamo wa serikali wakati huo wa kutaka majina ya nyumbani yatumike bala ya yale ya kigeni na kuwa moja ya bendi maarufu za wakati huo. Waliweza kutoa vibao vilivyopendwa mfululizo na kuweza kuzunguka nchi nzima. Vibao kama Rosa Nenda Shule, Georgina, Mkuki Moyoni, viliweza kuuza zaidi ya nakala 10,000 za santuri na hivyo kuwezesha bendi kuwa na vyombo vyake vizuri.
|
20231101.sw_1855_4
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Marijani%20Rajab
|
Marijani Rajab
|
Bendi wakati huo ikiwa na wanahisa wanne, ambao kwa bahati mbaya wakati bendi ndio iko juu, wakakosa kuelewana na ukawa ndio mwisho wa bendi hiyo. Marijani alishiriki kutunga, kuimba nyimbo karibu zote za Trippers sanjari na kupiga gitaa kwa baadhi ya nyimbo. Mfano wimbo Olila ambao alipiga rhythm na kuimba.
|
20231101.sw_1855_5
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Marijani%20Rajab
|
Marijani Rajab
|
Mwaka 1976, Marijani na baadhi ya wanamuziki wa Trippers waliamua kuihama bendi na kwenda baadaye kuasisi Dar es salaam International chini ya umiliki wa Mzee Zakaria Ndabemeye. Baadhi ya wanamuziki hao ni pamoja na Abel Baltazar kutoka Msondo, Kassimu Mponda kutoka Trippers, Abdallah Gama, Joseph Mulenga, Haruna Lwali na George Kessy Omojo waliokuwa wanapiga muziki Magot pale, Said Mohamed kutoka Polisi Jazz, Cosmas Chidumule kutoka Urafiki, Belesa Kakere kutoka Biashara Jazz, Joseph Bernard kutoka Trippers, Ali Rajabu kutoka Trippers, na King Michael Enock kutoka Dar es Salaam Jazz.
|
20231101.sw_1855_6
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Marijani%20Rajab
|
Marijani Rajab
|
Akiwa Dar Inter alishiriki kutunga nyimbo mbili, Betty na Sikitiko. Hata hivyo kama waswahili wanavyosema mafahari wawili hawakai zizi moja ndivyo ilivyotokea kati yake na Abel Balthazal kiasi cha hatimaye Marijani kufukuzwa ndani ya bendi kutokana na ubishi kuhusu wimbo aliotunga Marijani, kuna maelezo kuwa wimbo ulionekana unafanana na wimbo fulani toka Kongo na hivyo Marijani akatakiwa aubadilishe na ndipo ugomvi ukaanza.
|
20231101.sw_1855_7
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Marijani%20Rajab
|
Marijani Rajab
|
Hata hivyo mwishoni mwa mwaka 1978, Marijani alirejeshwa tena kundini kutokana na rundo la wanamuziki wa Dar Inter kuihama bendi kwa kishindo kikubwa na kwenda kuifungua bendi mpya kabisa ya Orchestra Mlimani Park. Aliporejeshwa Marijani alikuja na wanamuziki wengi wapya wakati huo kama akina Christopher Kasongo, Mohamed Tungwa, Mafumu Bilal, Hamis Milambo, Athuman Momba, Mzee Alex Kanyimbo na wengine na kuja na mtindo wa Super Bomboka.
|
20231101.sw_1855_8
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Marijani%20Rajab
|
Marijani Rajab
|
Katika kudhihirisha hasira zake kwa Abel, Marijani alimtungia Abel wimbo wa kumnanga ukiitwa Kidudu Mtu ambao hata hivyo RTD waliukataa kuurekodi, jambo lililokuwa kawaida enzi hizo kwa redio kukataa wimbo. Sifa nyingine ambayo Marijani alikuwa nayo ni kuibua wanamuziki chipukizi kama alivyofanya mwaka 1983 alipomuibua kutoka Tanga kijana Mkuu Waziri Kungugu Kitanda Milima almaaruf Fresh Jumbe ambaye kwa hakika kabisa Marijani hakujutia kumchukua kijana huyo.
|
20231101.sw_1855_9
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Marijani%20Rajab
|
Marijani Rajab
|
Alimuamini kupita maelezo kiasi kwamba wakati mwingine alikuwa akimuachia bendi aongoze na yeye anapumzika nyumbani. Mbali na Fresh, wanamuziki wengine ni kama vile Tino Masinge, Mohamed Mwinyikondo, Juma Choka na wengine kibao. Baada ya kurekodi Zuena na Mwanameka na nyimbo nyingine katika album hiyo alichoambulia ni malipo ya nauli toka RTD ya sh 2500/- tu. Kilichosikitisha zaidi ni kuwa nyimbo zao tisa ziliuzwa kwa kampuni ya Polygram bila ridhaa yao.
|
20231101.sw_1855_10
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Marijani%20Rajab
|
Marijani Rajab
|
Hata hivyo safari ya Dar International ilikoma mwaka 1987 kutokana na sababu za kawaida za kufa kwa bendi lakini kubwa ni uchakavu wa vyombo. Hata hivyo Marijani aliendelea kufanya muziki na kwa kipindi kifupi amewahi kucheza na Kurugenzi ya Arusha na Mwenge Jazz ambayo alirekodi nayo wimbo mmoja wa Ukimwi na hata kupitia bendi ya Watafiti ambayo hatimaye ilikuja kuwa 38..
|
20231101.sw_1855_11
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Marijani%20Rajab
|
Marijani Rajab
|
Mwaka huohuo wa 1987 Marijani na Muhidin Maalim Gurumo waliliongoza kundi la wanamuziki zaidi ya 50 kutunga nyimbo maalum hasa kwa maadhimisho ya miaka 10 ya CCM na 20 ya Azimio la Arusha. Kundi hilo lilijulikana kwa jina la Tanzania All Stars. Aidha mwaka 1994 aliwahi kurekodi zong zing na marehemu Eddy Sheggy.
|
20231101.sw_1855_12
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Marijani%20Rajab
|
Marijani Rajab
|
Bendi yake ya mwisho ilikuwa ni Africulture ama Mahepe Ngoma ya Wajanja, iliyokuwa mali ya Rogers Malila, alikokuwa na wanamuziki kadhaa kama akina Hassan Kunyata, Mgosi na wengine. Bado Marijani ataendelea kukumbukwa na wapenda muziki kote nchini na hata Afrika kwa ujumla kwa nyimbo zake zenye mafundisho na tamu huku akienzi utamaduni na ngoma za kwao Kigoma.
|
20231101.sw_1856_0
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Uchoraji
|
Uchoraji
|
Uchoraji ni sanaa ya kuweka alama au picha kwa kutumia vifaa mbalimbali vya kuchorea, kama vile kalamu ya wino au ya risasi, burashi, penseli za rangi ya nta, crayoni, makaa, choko, pastels, aina mbalimbali za erasers, markers, styluses, metali mbalimbali (kama silverpoint) na siku hizi hata elektroniki au kitu kingine cha kuandikia au kupaka rangi katika karatasi, kitambaa, ubao, metali, mwamba, kadi, plastiki, ngozi, canvas, na bodi au penginepo.
|
20231101.sw_1856_1
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Uchoraji
|
Uchoraji
|
Upatikanaji mpana wa vyombo vya kuchora hufanya uchoraji kuwa moja ya shughuli za kawaida za kisanii. Ni sanaa wakilishi maana inaweza kutumika kuwasilisha ujumbe kwa jamii, hivyo imekuwa njia maarufu na ya msingi ya kujieleza kwa umma katika historia ya binadamu. Ni njia rahisi na yenye ufanisi zaidi ya kuwasiliana mawazo ya kuona.
|
20231101.sw_1856_2
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Uchoraji
|
Uchoraji
|
Mbali na namna zake zaidi za kisanii, kuchora mara nyingi hutumiwa katika biashara, usanifu, uhandisi na ufundi. Msanii anayeshughulikia au anafanya kazi katika kuchora kiufundi anaweza kuitwa pia mchoraji.
|
20231101.sw_1856_3
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Uchoraji
|
Uchoraji
|
Hata hivyo kuna aina tofauti za uchoraji. Hii inategemea mchoraji mwenyewe anapenda aina gani ya uchoraji: wakati mwingine sanaa hii ya uchoraji si ya kuwakilisha ujumbe tu, bali pia kumvutia mtazamaji kwa rangi za kupendeza bila kujali ujumbe uliobebwa na picha hiyo. Wakati mwingine inawezekana picha isiwe na ujumbe kabisa, lakini ikawa imechorwa kwa ustadi mkubwa na kupakwa rangi za kuvutia sana, mpaka mtazamaji kumvutia na kumfanya apende kuendelea kuitazama picha husika.
|
20231101.sw_1856_4
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Uchoraji
|
Uchoraji
|
Kuchora ni moja ya aina kuu za kujieleza ndani ya sanaa za kuona. Kwa ujumla ni wasiwasi na kuashiria mistari na maeneo ya toni kwenye karatasi / vifaa vingine, ambapo uwakilishi sahihi wa ulimwengu wa kuona unaonyeshwa juu ya uso wa ndege. Mchoro wa jadi ulikuwa monochrome, au angalau alikuwa na rangi kidogo, wakati michoro za kisasa za rangi za penseli zinaweza kufikia au kuvuka mipaka kati ya kuchora na uchoraji. Katika istilahi ya Magharibi, kuchora ni tofauti na uchoraji, ingawa mara nyingi vyombo vya habari vinavyoajiriwa katika kazi zote mbili. Vyombo vya kavu, vinavyohusishwa na kuchora, kama vile choko, vinaweza kutumika katika uchoraji wa pastel. Kuchora kunaweza kufanywa kwa kati ya kioevu, hutumiwa na maburusi au kalamu. Msaada sawa pia unaweza kutumika: uchoraji kwa ujumla unahusisha matumizi ya rangi ya kioevu kwenye tani iliyopangwa tayari au wakati mwingine, lakini wakati mwingine kutengeneza chini hutolewa kwanza kwa msaada huo huo. Kuchora mara nyingi huchunguza, kwa msisitizo mkubwa juu ya uchunguzi, kutatua matatizo na utungaji. Kuchora pia hutumiwa mara kwa mara katika maandalizi kwa ajili ya uchoraji, na kuendelea kuifanya tofauti yao. Michoro iliyoundwa kwa madhumuni haya inaitwa masomo.
|
20231101.sw_1856_5
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Uchoraji
|
Uchoraji
|
Kuna makundi kadhaa ya kuchora, ikiwa ni pamoja na kuchora takwimu, kuchora, kuchora, mkono wa bure na shading. Pia kuna mbinu nyingi za kuchora, kama vile kuchora mstari, kusonga, shading, njia ya surrealist ya entopic graphomania (ambayo dots hufanywa kwenye maeneo ya uchafu katika karatasi tupu, na mistari hufanyika kati ya dots), Na kufuatilia (kuchora kwenye karatasi inayojitokeza, kama vile kufuatilia karatasi, karibu na muhtasari wa maumbo yaliyomo ambayo yanaonyesha kupitia karatasi).
|
20231101.sw_1856_6
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Uchoraji
|
Uchoraji
|
Picha za kale kabisa zinaonyesha uchoraji kwenye miamba katika mapango. Katika Afrika ni Wasan au watu waliokuwa karibu nao waliochora wanyama kwenye kuta za mipango walipopumzika. Picha zao zinapatikana kote katika Afrika ya Kusini hadi Tanzania ambako kuna mifano mbalimbali karibu na Kondoa. Mifano ya uchoraji wa aina hii imepatikana pia Ulaya, Asia na Australia.
|
20231101.sw_1856_7
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Uchoraji
|
Uchoraji
|
Hatujui mengi kuhusu namna nyingine za uchoraji wa kale kwa sababu vifaa vingine vilivyotumiwa havikudumu.
|
20231101.sw_1856_8
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Uchoraji
|
Uchoraji
|
Kutoka ustaarabu wa juu kama wa Misri, bonde la Indus au China tunajua mifano mingine ya uchoraji inayoonyesha hali ya juu zaidi. Katika ustaarabu wa madola ya kwanza wachoraji walikuwa tayari watu waliokuwa na nafasi ya kufuata sanaa yao bila haja ya kuwinda au kulima wenyewe, kwa sababu mtu mkubwa kama mfalme au kuhani aliwapatia riziki ya maisha.
|
20231101.sw_1856_9
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Uchoraji
|
Uchoraji
|
Katika makaburi ya Nubia, Ufalme wa Kush kuna picha zilizohifadhiwa ukutani. Makaburi ya Wamisri yalijengwa mara nyingi kwenye jangwa, kando ya bonde la Naili. Ukavu wa mazingira pamoja na giza vilitunza rangi vema.
|
20231101.sw_1856_10
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Uchoraji
|
Uchoraji
|
Wamisri wa Kale walichora watu bila kutofautisha mandharimbele au mandharinyuma. Wati muhimu waliochorwa wakubwa kuliko wale waliokuwa na cheo kidogo. Mwili ulionyeshwa mara nyingi kwa mbele lakini kichwa na uso kwa kando.
|
20231101.sw_1856_11
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Uchoraji
|
Uchoraji
|
Katika Ugiriki wa Kale uchoraji na wasanii wake waliheshimiwa sana. Philostrates aliandika mnamo mwaka 300 KK ya kwamba uchoraji ulibuniwa na miungu. Kuna taarifa juu ya picha lakini ni machache tu yaliyohifadhiwa kwa sababu ya hali ya hewa na kwa sababu picha nyingi zilichorwa juu ya ubao au matofali.
|
20231101.sw_1856_12
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Uchoraji
|
Uchoraji
|
Waroma wa Kale walituachia mifano mingi ya uchoraji wa ukutani; nje ya makaburi ni hasa nyumba za miji ya Pompei na Herkulaneo zilizofunikwa na majivu ya volkeno Vesuvio ambako picha nzuri zimehifadhiwa tangu mwaka 79 BK. Wakati ule wasanii walitofautisha tayari kati ya mandharimbele na mandharinyuma.
|
20231101.sw_1856_13
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Uchoraji
|
Uchoraji
|
Uchoraji wa China uliendelea sana kufuatana na utamaduni wake; mnamo mwaka 600 kuna picha za mandhari zinazoonyesha nchi na milima; msanii wa kwanza anayejulikana alitumia mbinu hii alikuwa Zhan Ziqian.
|
20231101.sw_1856_14
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Uchoraji
|
Uchoraji
|
On Drawing, an essay about the craft of drawing, by artist Norman Nason. Archived from the original on April 25, 2012.
|
20231101.sw_1856_15
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Uchoraji
|
Uchoraji
|
Leonardo da Vinci: anatomical drawings from the Royal Library, Windsor Castle, exhibition catalog fully online as PDF from The Metropolitan Museum of Art (a great drawing resource).
|
20231101.sw_1856_16
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Uchoraji
|
Uchoraji
|
Leonardo da Vinci, Master Draftsman, exhibition catalog fully online as PDF from The Metropolitan Museum of Art (a great drawing resource).
|
20231101.sw_1856_17
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Uchoraji
|
Uchoraji
|
Drawing in the Middle Ages A summary of how drawing was used as part of the artistic process in the Middle Ages.
|
20231101.sw_1857_0
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kamusi%20elezo
|
Kamusi elezo
|
Kamusi elezo (pia: ensaiklopidia kutoka Kiingereza: encyclopedia) ni kitabu kinachokusudiwa kukusanya ujuzi wa binadamu kadiri iwezekanavyo kulingana na wingi wa kurasa zake.
|
20231101.sw_1857_1
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kamusi%20elezo
|
Kamusi elezo
|
Siku hizi, Wikipedia ni kamusi elezo kubwa zaidi duniani lakini si kitabu cha karatasi, ni mkusanyo wa habari kwa umbo dijitali katika intaneti. Zamani (kabla ya kuja kwa Wikipedia) Encyclopedia Britannica ilikuwa kati ya kamusi elezo kubwa zaidi iliyokuwa ikitolewa kama vitabu vilivyochapishwa.
|
20231101.sw_1857_2
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kamusi%20elezo
|
Kamusi elezo
|
Katika historia yalikuwepo majaribio mbalimbali ya kukusanya ujuzi wote wa dunia. Mfano bora wa kale ni kamusi ya Yongle kutoka China iliyotungwa na wataalamu 2000 katika karne ya 14 na kuandikwa kwa mkono katika vitabu 1100.
|
20231101.sw_1857_3
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kamusi%20elezo
|
Kamusi elezo
|
Lakini kamusi elezo au ensaiklopedia zimekuwa na athari kubwa sana tangu Johannes Gutenberg na kupatikana kwa uchapaji wa vitabu ulioshusha kabisa bei ya vitabu kwa watu wengi.
|
20231101.sw_1857_4
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kamusi%20elezo
|
Kamusi elezo
|
Ensaiklopedia ya kwanza ya kisasa iliyokuwa na athira kubwa sana ilikuwa "Encyclopédie ou Dictionnaire raisonné des sciences, des arts et des métiers" iliyokusanywa na Denis Diderot pamoja na Jean Baptiste le Rond d’Alembert pamoja na waandishi zaidi ya 130 katika karne ya 18 huko Ufaransa. Kamusi elezo hii ikawa moja kati ya vyanzo vya harakati ya Zama za Mwangaza.
|
20231101.sw_1858_0
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ngoma
|
Ngoma
|
Katika lugha ya mitaani, ngoma inaweza kumaanisha virusi vya UKIMWI au Ukimwi wenyewe. Neno hili limetokana na methali ya Kiswahili isemayo, Ngoma ikivuma sana, mwishowe hupasuka.
|
20231101.sw_1859_0
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ellen%20Johnson-Sirleaf
|
Ellen Johnson-Sirleaf
|
Ellen Johnson-Sirleaf (alizaliwa 29 Oktoba 1938 nchini Liberia) amekuwa rais wa kwanza mwanamke barani Afrika baada ya kushinda katika uchaguzi wa mwaka 2005. Johnson-Sirleaf ameshika nyadhifa mbalimbali serikalini na katika mashirika ya kimataifa. Baada ya kumaliza masomo katika chuo kikuu cha Harvard, alifanya kazi katika serikali ya Rais William Tolbert mwaka wa 1970 akiwa ni Waziri wa Fedha.
|
20231101.sw_1859_1
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ellen%20Johnson-Sirleaf
|
Ellen Johnson-Sirleaf
|
Johnson amekuwa Rais wa kwanza mwanamke barani Afrika. Hata hivyo yeye sio mwanamke wa kwanza kuongoza nchi barani Afrika. Malikia Zauditu wa Ethiopia aliongoza nchi yake kwa miaka 13 toka mwaka 1917 hadi 1930. Ruth Perry ni mwanamke wa kwanza Afrika kuwa mkuu wa nchi pale alipokuwa mwenyekiti wa urais wa pamoja wa jamhuri ya Liberia toka mwaka 1996 hadi 1997.
|
20231101.sw_1859_2
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ellen%20Johnson-Sirleaf
|
Ellen Johnson-Sirleaf
|
Johnson-Sirleaf alihukumiwa kifungo cha miaka kumi jela mwaka 1985 baada ya kushutumu utawala wa kijeshi nchini humo katika kampeni zake za kugombea ubunge. Alitumia kifungo hicho kwa muda mfupi kabla ya kuachiliwa na baadaye kukimbilia uhamishoni hadi aliporudi mwaka 1997 akiwa anafanyia kazi Benki ya Dunia na Citibank.
|
20231101.sw_1859_3
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ellen%20Johnson-Sirleaf
|
Ellen Johnson-Sirleaf
|
Johnson-Sirleaf alimuunga mkono Charles Taylor wakati wa mapinduzi yake dhidi ya Jenerali Samuel Doe lakini baadaye alikuja kuwa mpinzani wake mkubwa na hata kugombea urais dhidi yake mwaka 1997. Taylor alimwandana na hata kumpeleka mahakamani kwa madai ya kuhusika na hujuma za kihaini.
|
20231101.sw_1859_4
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ellen%20Johnson-Sirleaf
|
Ellen Johnson-Sirleaf
|
Uchaguzi wa urais mwaka 2005 ulirudiwa baada wagombea urais kutopata kura za kutosha. Katika raundi ya kwanza Johnson-Sirleaf alikuwa wa pili, wa kwanza alikuwa ni mpinzani wake mkubwa George Weah. Katika raundi ya pili ya uchaguzi, Johnson-Sirleaf alitangazwa kuwa mshindi. Hata hivyo, George Weah amepeleka mashtaka mahakama kuu akidai kuwa uchaguzi haukuwa wa haki.
|
20231101.sw_1859_5
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ellen%20Johnson-Sirleaf
|
Ellen Johnson-Sirleaf
|
Mnamo Desemba 2021, James Sirleaf mmoja wa wana wa Ellen Sirleaf alikufa katika makazi yake huko Liberia chini ya hali isiyojulikana.
|
20231101.sw_1859_6
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ellen%20Johnson-Sirleaf
|
Ellen Johnson-Sirleaf
|
Ellen Johnson Sirleaf alizaliwa mjini Monrovia, mji mkuu wa Liberia, na elimu ya wazazi. Kabila lake ni nusu Gola kutoka upande wa baba yake, na robo Kru na robo Kijerumani kutoka upande wa mama yake.
|
20231101.sw_1859_7
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ellen%20Johnson-Sirleaf
|
Ellen Johnson-Sirleaf
|
Babake Sirleaf Jahmale Carney Johnson, alikuwa mzaliwa wa Liberia wa kwanza kuweza kukaa katika mbunge la taifa.
|
20231101.sw_1859_8
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ellen%20Johnson-Sirleaf
|
Ellen Johnson-Sirleaf
|
Sirleaf alisoma maswala ya uchumi na akaunti katika Chuo Afrika Magharibi mjini Monrovia. Aliolewa na James Sirleaf akiwa na miaka 17 tu na kuhamia Marekani katika mwaka wa 1961 ambapo aliendelea na masomo yake katika chuo kikuu cha Colorado na kuhitimu na shahada ya digri. Alisomea maswala ya uchumi na sera za umma katika chuo Chuo Cha Maswala Ya Serikali ya John F. Kennedy, mjini Harvard katika miaka ya 1969 na 1971 na kupata shahada ya maswala ya serikali. Kisha alirudi Liberia na kufanya kazi chini ya rais William Tolbert.
|
20231101.sw_1859_9
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ellen%20Johnson-Sirleaf
|
Ellen Johnson-Sirleaf
|
Alikuwa naibu waziri wa fedha kati ya mwaka wa 1972 na 1973. Alikuwa waziri wa fedha toka mwaka wa 1979 hadi Aprili 1980.
|
20231101.sw_1859_10
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ellen%20Johnson-Sirleaf
|
Ellen Johnson-Sirleaf
|
Aliweza kuwa naibu mwenyekiti wa benki ya CitiBank mjini Nairobi, Kenya kutoka mwaka wa 1983-1985. Aliwahi kufungwa mafungo ya nyumbani na Samule Doe aliyepindua serikali kwa kutangaza nia ya kugombea urais.
|
20231101.sw_1859_11
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ellen%20Johnson-Sirleaf
|
Ellen Johnson-Sirleaf
|
Kati ya miaka ya 1986-1992 alikuwa makamu wa rais na mwanachama wa bodi ya benki ya Equator, Washington, DC. Kati ya miaka ya 1988-1999 alikuwa mbunge wa bodi ya wakurugenzi wa Taasisi ya Synergos. ALigombea urais kwa tiketi ya chama ya maungano(Unity Party) katika mwaka wa 1997 na kuwa
|
20231101.sw_1859_12
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ellen%20Johnson-Sirleaf
|
Ellen Johnson-Sirleaf
|
Ndiye rais wa sasa wa Liberia. Alimshinda alikuwa mwanasoka mashuhuri George Weah na zaidi ya asilimia ishirini katika uchaguzi wa mwaka wa 2005. Uzinduzi ulifanyika tarehe 16 Januari 2006 na ulihudhuriwa na wageni mashuhuri wakiwemo aliyekuwa waziri ya maswala ya kigeni wa Marekani, Condeleeza Rice, Laura Bush na Mitchelle Jean.
|
20231101.sw_1859_13
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ellen%20Johnson-Sirleaf
|
Ellen Johnson-Sirleaf
|
Katika mwaka wa 2005 alianzisha tume ya ukweli na maridhiano ambayo ilitoa ripoti yake katika mwaka wa 2009.
|
20231101.sw_1860_0
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/George%20Weah
|
George Weah
|
George Weah (alizaliwa Monrovia, 1 Oktoba 1966) ni rais wa Liberia kuanzia mwaka 2017. Kabla ya kuwa mwanasiasa aliwahi kuwa mwanakandanda mashuhuri duniani.
|
20231101.sw_1860_1
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/George%20Weah
|
George Weah
|
Weah ni wa kabila la Kru ambalo linatoka upande wa kusini-mashariki mwa Liberia kwenye Kaunti ya Grand Kru, ambayo ni moja ya maeneo maskini sana nchini humo.
|
20231101.sw_1860_2
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/George%20Weah
|
George Weah
|
Wazazi wake walikuwa William T. Weah, Sr. na Anna Quayeweah. Alilelewa zaidi na bibi yake upande wa baba, Emma Klonjlaleh Brown.
|
20231101.sw_1860_3
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/George%20Weah
|
George Weah
|
Alihudhuria shule ya msingi katika shule ya Muslim Congress and sekondari katika shule ya Wells Hairston High School.
|
20231101.sw_1860_4
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/George%20Weah
|
George Weah
|
Weah amemuoa Clar Weah, mwenye asili ya Visiwa vya Karibi. Wana watoto watatu: George Weah Jr, Tita na Timothy. Huyo, baada ya majaribio na timu ya Chelsea mwaka 2013, alijiunga na timu ya Paris Saint-Germain mwaka 2015. Timothy anaichezea pia timu ya taifa ya Marekani ya chini ya umri wa miaka 18. Binamu yake Weah, Christopher Wreh aliwahi pia kucheza soka la kulipwa kwenye timu ya Arsenal.
|
20231101.sw_1860_5
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/George%20Weah
|
George Weah
|
Weah aliwahi kubadili dini toka Ukristo kwenda Uislamu na baadaye akarudi tena kwenye Ukristo. Hivi sasa ni muumini wa Ukristo wa Kiprotestanti.
|
20231101.sw_1860_6
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/George%20Weah
|
George Weah
|
Kielimu, Weah ana Shahada ya Kwanza ya Uendeshaji Michezo toka Chuo Kikuu cha Parkwood, London, Uingereza. Hata hivyo baadhi ya watu wanatilia shaka shahada hii kwakuwa chuo hiki kinajulikana kwa kutoka shahada bila kusoma hapo. baadaye alipata shahada ya Usimamizi wa Biashara toa Chuo Kikuu cha DeVry, Miami nchini Marekani. Mwaka 1999 alipata shahada ya Udakitari ya Heshima toka Chuo Kikuu cha A.M.E Zion nchini Liberia.
|
20231101.sw_1860_7
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/George%20Weah
|
George Weah
|
Kabla ya kujiunga na soka la kulipwa, Weah alikuwa akifanya kazi katika Shirika la Mawasiliano la Liberia kama fundi simu.
|
20231101.sw_1860_8
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/George%20Weah
|
George Weah
|
Mwaka 1995 Weah alipewa na Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) tuzo ya kuwa Mwanasoka Bora Duniani. Yeye ni mwanasoka pekee toka Afrika aliyewahi kupewa tuzo hiyo. Mwaka huohuo alichaguliwa pia kuwa Mwanasoka Bora Ulaya na Mwanasoka Bora Afrika. Miaka 1989, 1994 na 1995 alichaguliwa kuwa Mwanasoka Bora wa Mwaka Afrika na mwaka 1996 alichaguliwa kuwa Mwanasoka Bora wa Karne wa Afrika. Mwaka 2004, Pelé alimchagua kwenye orodha ya FIFA ya wachezaji bora ambao wako hai.
|
20231101.sw_1860_9
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/George%20Weah
|
George Weah
|
Weah alianza safari yake ya soka katika timu Incincible Eleven ya Liberia na Tonnerre Yaounde ya Cameroon. Baada ya hapo alikwenda kucheza soka la kulipwa Ulaya mwaka 1988. Alijiunga na timu ya Monaco ambayo ilikuwa ikifundishwa na Arsène Wenger ambapo aliiongoza kushinda kombe la Ufaransa mwaka 1991. Baadaye alijiunga na Paris Saint Germain mwaka 1992-95. Aliiongoza timu hii kuchukua kombe la ligi ya Ufaransa mwaka 1994. Akiwa hapo aliweza kuwa mfungaji bora wa Ligi ya Mabingwa wa Ulaya (UEFA Champions League) mwaka 1994–95. Mwaka 1995-2000 alikuwa akiichezea timu ya AC Milan ambayo ilishinda ligi ya Italia mwaka 1996 na 1999. Mwaka 2000 aliondoka AC Milan na kujiunga na Chelsea, baada ya muda mfupi alijiunga na Manchester City na baadaye Marseille mwaka 2001. Alimaliza soka la kulipwa akiwa na timu ya Al JAzira ya Falme ya Nchi za Kiarabu. Kwa ujumla alicheza soka la kulipwa kwa miaka 14.
|
20231101.sw_1860_10
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/George%20Weah
|
George Weah
|
Weah aliichezea pia timu ya taifa ya Liberia na aliiwakilisha nchi yake katika Kombe la Mataifa ya Afrika mara mbili.
|
20231101.sw_1860_11
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/George%20Weah
|
George Weah
|
Weah amekuwa akitoa misaada kwa wananchi wa Liberia. Mwaka 2004 alipewa Tuzo ya Ujasiri ya Arthur Ashe kwa juhudi zake za kusaidia kujenga nchi yake.
|
20231101.sw_1860_12
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/George%20Weah
|
George Weah
|
Kwenye uchaguzi wa urais mwaka 2005, Weah alishindwa kwenye raundi ya pili na rais wa kwanza mwanamke Afrika, Ellen Johnson Sirleaf. Uchaguzi uliofuata mwa mwaka 2011, Weah alipigania kiti cha umakamu wa rais kama mgombea mwenza wa Winston Tubman. Mwaka 2014, Weah alishinda kiti cha useneti kupitia chama cha Congress for Democratic Change kwenye Kaunti ya Montserrado.
|
20231101.sw_1860_13
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/George%20Weah
|
George Weah
|
Mwaka 2017 alishinda uchaguzi wa urais wa Liberia. Aliongoza kwa kura nyingi katika uchaguzi uliofanyika Oktoba 10 2017. Hata hivyo, alishindwa kupata asilimia zaidi ya asilimia 50. Kwenye raundi ya pili ya uchaguzi hapo 25 Desemba 2017 alimshinda Joseph Boakai aliyekuwa makamu wa rais aliyetangulia Ellen Johnson Sirleaf. Weah alipata asilimia 61.5 za kura..
|
20231101.sw_1861_0
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Monrovia
|
Monrovia
|
Monrovia ni mji mkuu wa Liberia. Eneo uliko mji huu mwanzoni liliitwa Cape Mesurado na Wareno katika miaka ya 1560. Eneo hili lilianzwa kujenga mji mwaka 1822 na chama cha
|
20231101.sw_1861_1
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Monrovia
|
Monrovia
|
American Colonization Society ikiwa ni makazi ya watu waliokombolewa toka utumwani nchini Marekani. Jina Monrovia lilitokana na jina la Rais wa Marekani James Monroe. Kwa mujibu wa sensa ya mwaka 2003, Mji huu una wakazi wapatao 572,000.
|
20231101.sw_1861_2
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Monrovia
|
Monrovia
|
Uchumi wa Monrovia unategemea zaidi bandari yake na madini ya chuma. Bidhaa kama vile saruji, mafuta, matofali, vigae, samani, na kemikali zinatengenezwa Monrovia.
|
20231101.sw_1861_3
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Monrovia
|
Monrovia
|
Wakati mabaharia Wareno walipowasilia Monrovia na kuuita mji huu "Cape Mesurado" tayari kulikuwa na wakazi wakiishi hapo. Watu wa kwanza kuhamia Monrovia toka nchini Marekani waliwasili mwaka 1822 katika Kisiwa cha Sherboro nchini Sierra Leone. Wahamiaji wengi walifariki baada ya kuwasili Monrovia.
|
20231101.sw_1861_4
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Monrovia
|
Monrovia
|
Mkutano wa kutunga katiba ya Liberia wa American Colonization Society ulifanyikia Monrovia mwaka 1845.
|
20231101.sw_1864_0
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ngoma%20%28muziki%29
|
Ngoma (muziki)
|
Ngoma ni muziki na lugha ya pekee inayotumika kwa kuelezea utamaduni na historia ya nchi fulani, tunatumia lugha ya ngoma katika kuelezea hali mbalimbali za maisha yetu, kama vile huzuni, furaha, mapenzi, faraja, vitisho, shukurani na ushindi.
|
20231101.sw_1864_1
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ngoma%20%28muziki%29
|
Ngoma (muziki)
|
Ngoma pia ilitumika na jamii mbalimbali kama njia ya kuita watu kwenye kusanyiko muhimu, kama vile vita, mikutano n.k. na ilipigwa kwa milio tofauti kulingana na tukio.
|
20231101.sw_1869_0
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Bombwe%20%28sanaa%29
|
Bombwe (sanaa)
|
Bombwe ni sanaa ya urembo wa kuchora mwilini, kama kuchora kwa hina na kuchora kwa piko, sanaa hii hutumika zaidi na wanawake.
|
20231101.sw_1870_0
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Togwa
|
Togwa
|
Togwa ni kinywaji baridi kinachotengenezwa kwa nafaka au maji ya matunda. Namna ya kutengeneza ni sawa na pombe ya kawaida ila tu haikubadilika bado kuwa na alikoholi.
|
20231101.sw_1870_1
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Togwa
|
Togwa
|
Togwa ndiyo itakuwa pombe ikikaa. Kwa mfano, togwa ya ulanzi ni utomvu kutoka mianzi baada ya masaa kadhaa, na ulanzi wenye pombe ni utomvu uleule kutoka mianzi baada ya siku mbili hivi.
|
20231101.sw_1870_2
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Togwa
|
Togwa
|
Kwanza chukua mtama mkavu uoshe na uuweke kwenye chombo kikavu alafu uufunike kwa muda wa siku 2,ukifunua utakuta umeanza kuota(kimea)
|
Subsets and Splits
No community queries yet
The top public SQL queries from the community will appear here once available.