_id
stringlengths 15
22
| url
stringlengths 31
150
| title
stringlengths 1
86
| text
stringlengths 100
23.8k
|
---|---|---|---|
20231101.sw_1870_3
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Togwa
|
Togwa
|
chukua mtama mwingine uloweke kwa siku moja alafu uusage,unga wake pika uji wa saizi ya kati si mzito si mwepesi.Uache ule uji upowe,ukisha poa
|
20231101.sw_1870_4
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Togwa
|
Togwa
|
chukua kile kimea(mtama ulioanza kuota) usage kidogo ili kubakia na chenga chenga.Alafu mimina zile chenga chenga za kimea kwenye ule uji.Tia sukari
|
20231101.sw_1871_0
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Liberia
|
Liberia
|
Liberia (yaani Nchi ya watu huru kwa Kilatini) ni nchi iliyoko Afrika ya Magharibi. Imepakana na nchi za Ivory Coast, Guinea, na Sierra Leone.
|
20231101.sw_1871_1
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Liberia
|
Liberia
|
Ni mojawapo ya nchi za Afrika ambazo hazikutawaliwa na Wazungu. Hata hivyo watu wa Liberia huongea Kiingereza sana.
|
20231101.sw_1871_2
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Liberia
|
Liberia
|
Liberia ni nchi iliyoundwa na makabila 16 ya asili nchini humo na wahamiaji Weusi toka Marekani na Karibi (5%), mbali na machotara wa aina mbalimbali.
|
20231101.sw_1871_3
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Liberia
|
Liberia
|
Wamarekani Weusi hao walikuwa watumwa waliopata uhuru ambao kwa kushirikiana na chama cha American Colonization Society waliunda taifa hili na kutangaza uhuru wa nchi hiyo tarehe 26 Julai 1847.
|
20231101.sw_1871_4
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Liberia
|
Liberia
|
Wamarekani Weusi hao waliichukulia nchi hiyo kama nchi ya ahadi kutokana na asili yao kuwa Afrika, ambako ndiko mababu zao walikotokea kabla ya kupelekwa utumwani Marekani.
|
20231101.sw_1871_5
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Liberia
|
Liberia
|
Hata hivyo, wahamiaji hao waliendelea kujitambulisha kama Wamarekani na hawakujenga mahusiano ya karibu na wenyeji.
|
20231101.sw_1871_6
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Liberia
|
Liberia
|
Alama za taifa hili (bendera, kauli mbiu, na nembo) na hata muundo wa serikali vilikuwa vikionyesha mahusiano ya karibu kati ya nchi hizo mbili.
|
20231101.sw_1871_7
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Liberia
|
Liberia
|
Hivi karibuni umefanywa kwa mara ya pili uchaguzi kwa amani na kuweza kumchagua George Weah kushika nafasi ya mwanamke wa kwanza kuwa Rais barani Afrika, Ellen Johnson-Sirleaf.
|
20231101.sw_1871_8
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Liberia
|
Liberia
|
Lugha rasmi ni Kiingereza, ambacho kinatumiwa na asilimia 15 za wakazi. Lugha za taifa ni 4: Kiingereza cha Kiliberia, Kikpelle, Kimeriko na Krioli.
|
20231101.sw_1871_9
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Liberia
|
Liberia
|
Upande wa dini, wakazi kwa asilimia 85.5 ni Wakristo, hasa Waprotestanti, halafu Wakatoliki (5.8%). Waislamu ni 12.2%. Wanaoendelea kufuata dini asilia za Kiafrika ni 0.5% tu.
|
20231101.sw_1871_10
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Liberia
|
Liberia
|
Wilton Sankawulo, Great Tales of Liberia. Dr. Sankawulo is the compiler of these tales from Liberia and about Liberian culture. Published by Editura Universitatii "Lucian Blaga"; din Sibiu, Romania, 2004. ISBN 973–651–838–8.
|
20231101.sw_1871_11
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Liberia
|
Liberia
|
Sundown at Dawn: A Liberian Odyssey by Wilton Sankawulo. Recommended by the Cultural Resource Center, Center for Applied Linguistics for its content concerning Liberian culture. ISBN 0-9763565-0-3
|
20231101.sw_1871_12
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Liberia
|
Liberia
|
Victoria Lang, To Liberia: Destiny's Timing (Publish America, Baltimore, 2004, ISBN 1-4137-1829-9). A fast-paced gripping novel of the journey of a young Black couple fleeing America to settle in the African motherland of Liberia.
|
20231101.sw_1871_13
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Liberia
|
Liberia
|
Godfrey Mwakikagile, Military Coups in West Africa Since The Sixties, Chapter Eight: Liberia: 'The Love of Liberty Brought Us Here,' pp. 85–110, Nova Science Publishers, Inc., Huntington, New York, 2001; Godfrey Mwakikagile, The Modern African State: Quest for Transformation, Chapter One: The Collapse of A Modern African State: Death and Rebirth of Liberia, pp. 1–18, Nova Science Publishers, Inc., 2001.
|
20231101.sw_1871_14
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Liberia
|
Liberia
|
Elma Shaw, Redemption Road: The Quest for Peace and Justice in Liberia (a novel), with a Foreword by President Ellen Johnson Sirleaf (Cotton Tree Press, 2008, ISBN 978-0-9800774-0-7)
|
20231101.sw_1871_15
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Liberia
|
Liberia
|
Helene Cooper, House at Sugar Beach: In Search of a Lost African Childhood (Simon & Schuster, 2008, ISBN 0-7432-6624-2)
|
20231101.sw_1873_0
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ruth%20Perry
|
Ruth Perry
|
Ruth Fahnbulleh Perry (16 Julai 1939 - 8 Januari 2017) alikuwa kiongozi wa Liberia toka 3 Septemba 1996 hadi 2 Agosti 1997. Aliongoza nchi hiyo kama mwenyekiti wa Baraza la Taifa ambalo liliongoza nchi hiyo kufuatia kuangushwa kwa Sajenti Samuel Doe na mwisho wa urais wa Amos Sawyer. Perry alikuwa mwanachama wa chama cha National Democratic Party cha Liberia.
|
20231101.sw_1875_0
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mwai%20Kibaki
|
Mwai Kibaki
|
Mwai Kibaki (1931-2022) alikuwa rais wa tatu wa Jamhuri ya Kenya kuanzia mwaka 2002 hadi 2013 akiwa ametanguliwa na Rais wa Kwanza wa Kenya, Mzee Jomo Kenyatta na rais wa pili Daniel Arap Moi. Jina lake la kubatizwa ni Emilio Stanley .
|
20231101.sw_1875_1
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mwai%20Kibaki
|
Mwai Kibaki
|
Kibaki alisoma uchumi, historia na sayansi ya siasa katika chuo kikuu cha Makerere, Kampala, Uganda. Akiwa mwanafunzi Makerere, Kibaki alikuwa ni mwenyekiti wa chama cha wanafunzi toka Kenya, Kenya Students' Association. Alipomaliza masomo yake mwaka 1955 alipewa tuzo kutokana na kufanya vyema katika mitihani. Tuzo hiyo ilimwezesha kwenda kusoma katika chuo cha London School of Economics. Alipomaliza masomo alikwenda kufundisha katika chuo kikuu cha Makerere. Baadaye aliacha kazi ya kufundisha na kuwa mtendaji mkuu wa chama cha Kenya African National Union.
|
20231101.sw_1875_2
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mwai%20Kibaki
|
Mwai Kibaki
|
Kibaki, licha ya kuwa mbunge, amewahi kuwa Naibu Waziri wa Fedha, Mwenyekiti wa Tume ya Mipango, Waziri wa Biashara na Viwanda, na Waziri wa Fedha. Moi alipoingia madarakani baada ya kifo cha Jomo Kenyatta, Kibaki aliteuliwa kuwa Makamu wa Rais.
|
20231101.sw_1875_3
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mwai%20Kibaki
|
Mwai Kibaki
|
Mwaka 1988 Kibaki alianza kuwa na mgongano na Rais Moi. Mwaka huo alivuliwa Umakamu wa Rais na kupelekwa Wizara ya Afya.
|
20231101.sw_1875_4
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mwai%20Kibaki
|
Mwai Kibaki
|
Mwaka 1991 Kibaki aliondoka chama cha KANU na kuanzisha chama cha Democratic Party. Katika uchaguzi wa Urais wa mwaka 1991, Kibaki alikuwa wa tatu na mwaka 1997 alikuwa wa pili.
|
20231101.sw_1875_5
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mwai%20Kibaki
|
Mwai Kibaki
|
Katika uchaguzi wa 2002 Kibaki alishinda na kutangazwa kuwa Rais wa Kenya. Alikuwa mgombea wa maungano wa vikundi vingi vya upinzani vilivyoshirikiana kwa jina la "NARC".
|
20231101.sw_1875_6
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mwai%20Kibaki
|
Mwai Kibaki
|
Kibaki ameweka historia mwezi Novemba 2005 baada ya kuwa Rais wa kwanza nchini Kenya kuondoa baraza lote la mawaziri kufuatia kura ya maoni ambayo ilikuwa inahusu katiba mpya ya Kenya. Kibaki alikuwa upande wa kundi lililokuwa likiunga mkono katiba hiyo kambi ya ndizi. Kundi lililokuwa likiipinga katiba hiyo kambi ya machungwa lilipata ushindi.
|
20231101.sw_1875_7
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mwai%20Kibaki
|
Mwai Kibaki
|
Uchaguzi wa 28 Desemba 2007 ulimrudisha Kibaki kwa kipindi cha pili kama rais. Uchaguzi huu ulipingwa na chama cha upinzani,ODM , na watazamaji wa kimataifa kuwa matokeo hayo hayakuwakilisha matakwa ya Wakenya. Mpinzani wake mkuu, Raila Odinga alikuwa mbele katika hesabu za kura hadi Kamati ya Uchaguzi iliposimamisha kuhesabu; baada ya kuendelea na matanganzo Kibaki alionekana kuwa mbele. Kulikuwa na hofu ya kwamba matokeo ya majimbo ya uchaguzi kadhaa yalibadilishwa yakiegemea upande wake kwa kumwongezea kura. Hisia hizi zilisababisha ghasia kuibuka Nairobi, Kisumu, Eldoret, Kericho, Mombasa na sehemu zinginezo nchini. Kibaki aliapishwa upya kuwa rais wa Kenya masaa machache tu baada ya kutangazwa kuwa mshindi; hafla ilifanywa katika Bustani ya Ikulu ya Nairobi mbele ya waalikwa wachache walioruhusiwa kushuhudia.
|
20231101.sw_1875_8
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mwai%20Kibaki
|
Mwai Kibaki
|
Kamati iliyobuniwa tutathmini ukweli wa mambo katika uchaguzi huo wa urais, iliyoongozwa na jaji mstaafu kutoka Afrika Kusini Johann Kriegler, iliripoti kwamba mshindi katika uchaguzi huo wa urais wa 2007 hangeweza kujulikana. Hii ni kwa sababu wizi wa kura ulifanyika katika sehemu nyingi nchini na ulitekelezwa kule mashinani na wafuasi wa wapinzani wote katika kinyang'anyiro cha Urais. Kriegler pia alielekeza lawama kwa Tume ya Uchaguzi ya Kenya kwa kutowajibika katika utendakazi, na ripoti hiyo ya Krieger ilipendekeza tume hiyo ivunjwe na ibadilishwe na ingine iliyo huru.
|
20231101.sw_1875_9
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mwai%20Kibaki
|
Mwai Kibaki
|
Baada ya kutangazwa kuwa rais mpya Kibaki aliteua mawaziri 17 kama awamu ya kwanza ya serikali akiacha nafasi nyingine serikalini kando kwa muda.
|
20231101.sw_1875_10
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mwai%20Kibaki
|
Mwai Kibaki
|
Rais Kibaki alifariki tarehe 21 Aprili 2022 akiwa na umri wa miaka 90 na kifo chake kutangazwa na rais wa nne wa Kenya, Uhuru Kenyatta, kupitia televisheni za taifa.
|
20231101.sw_1875_11
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mwai%20Kibaki
|
Mwai Kibaki
|
Mnamo tarehe 25 Aprili 2022, mwili wake ulipelekwa katika majengo ya bunge kwa mazishi ya kitaifa. Rais Uhuru Kenyatta na mkewe Margaret Kenyatta waliongoza Wakenya kuuona mwili wake.
|
20231101.sw_1875_12
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mwai%20Kibaki
|
Mwai Kibaki
|
Ibada ya mazishi ilifanyika tarehe 29 Aprili 2022 katika uwanja wa Nyayo na ilihudhuriwa na wageni mashuhuri pamoja na baadhi ya ma rais wa sasa.
|
20231101.sw_1875_13
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mwai%20Kibaki
|
Mwai Kibaki
|
Hatimaye alizikwa nyumbani kwake Othaya, iliyopo katika Kaunti ya Nyeri tarehe 30 Aprili 2022 huku Kanisa Katoliki likiadhimisha misa.
|
20231101.sw_1876_0
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kura%20ya%20maoni
|
Kura ya maoni
|
Kura ya maoni zinatumika katika demokrasia ili kuchagua viongozi wa nchi au kuamua kama sheria fulani itumike. Kawaida kura ya maoni hupigwa na wale wote wenye umri halali wa kupiga kura ili kukubali au kukataa pendekezo, sera, sheria, mabadiliko ya katiba, katiba mpya, kukataa au kumuunga mkono kiongozi fulani. Kura ya maoni huchukuliwa kuwa ni aina mojawapo ya demokrasia ya moja kwa moja.
|
20231101.sw_1877_0
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kura%20juu%20ya%20katiba%20mpya%20ya%20Kenya%20%282005%29
|
Kura juu ya katiba mpya ya Kenya (2005)
|
Kura ya maoni juu ya katiba mpya ya Kenya ilipigwa tarehe 21 Novemba 2005. Asilimia 58 ya Wakenya waliopiga kura waliikataa.
|
20231101.sw_1877_1
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kura%20juu%20ya%20katiba%20mpya%20ya%20Kenya%20%282005%29
|
Kura juu ya katiba mpya ya Kenya (2005)
|
Rais wa Kenya na baadhi ya mawaziri walipiga kampeni kutaka Wakenya waiunge mkono katiba hiyo. Kundi lililokuwa likiiunga mkono katiba mpya lilikuwa likiwakilishwa na alama ya ndizi na kundi lililokuwa likiipinga lilitumia alama ya machungwa.
|
20231101.sw_1877_2
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kura%20juu%20ya%20katiba%20mpya%20ya%20Kenya%20%282005%29
|
Kura juu ya katiba mpya ya Kenya (2005)
|
Ingawa watu wanane walikufa katika fujo zilizohusiana na kura hiyo, kwa ujumla zoezi hili lilifanyika kwa amani. Suala ambalo lilikuwa likijadiliwa sana ni kiasi cha madaraka ambacho rais anapaswa kupewa. Katiba mpya ilikuwa impe madakaraka makubwa sana rais wa Kenya wakati ambapo wanaoipinga katiba hiyo walitaka kuwe na Waziri Mkuu ambaye atagawana madaraka na Rais.
|
20231101.sw_1877_3
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kura%20juu%20ya%20katiba%20mpya%20ya%20Kenya%20%282005%29
|
Kura juu ya katiba mpya ya Kenya (2005)
|
Suala la umiliki wa ardhi nalo lilipewa kipaumbele kwenye mjadala wa kufaa au kutofaa kwa katiba hiyo. Katiba mpya ilikuwa ikiweka vikwazo kwa watu wasio Wakenya kumiliki ardhi, ilikuwa iruhusu wanawake kumiliki ardhi (kwa kurithi), na ilitaka iundwe tume ya ardhi ambayo ingekuwa na wajibu wa kugawa ardhi na kuondoa uwezekano wa viongozi wa serikali kupeana ardhi. Tume hii pia ingekuwa ndio msikilizaji mkuu wa kesi za ardhi na ingekuwa na jukumu la kurudisha ardhi kwa makundi na watu binafsi ambao waliipoteza miaka iliyopita.
|
20231101.sw_1878_0
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Demokrasia%20ya%20moja%20kwa%20moja
|
Demokrasia ya moja kwa moja
|
Demokrasia ya moja kwa moja ni aina ya demokrasia ambayo wananchi wote wanaweza kushiriki katika kuamua masuala ya kisiasa, kijamii, kisheria, na kiuchumi bila kutumia chombo cha uwakilishi kama vile bunge.
|
20231101.sw_1878_1
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Demokrasia%20ya%20moja%20kwa%20moja
|
Demokrasia ya moja kwa moja
|
Uwezo huu wa wananchi kutoa maamuzi unaweza kuwapa wananchi hata uwezo wa kimahakama ingawa mara nyingi wananchi hupewa uwezo wa kutunga au kupitisha sheria tu.
|
20231101.sw_1878_2
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Demokrasia%20ya%20moja%20kwa%20moja
|
Demokrasia ya moja kwa moja
|
Muundo wa demokrasia ya asili uwezo huu wa kutunga au kupitisha sheria na kupitisha maamuzi ulikuwa uko mikononi mwa wananchi wenyewe na sio wawakilishi wao.
|
20231101.sw_1878_3
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Demokrasia%20ya%20moja%20kwa%20moja
|
Demokrasia ya moja kwa moja
|
Kutegemeana na mfumo wenyewe wa demokrasia ya moja kwa moja, wananchi huwa wana uwezo wa kutunga sheria, kupitisha sera, kuwaweka madarakani na pia kuwaondoa madarakani viongozi.
|
20231101.sw_1878_4
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Demokrasia%20ya%20moja%20kwa%20moja
|
Demokrasia ya moja kwa moja
|
Demokrasia ya moja kwa moja ni tofauti na demokrasia inayofuatwa katika nchi nyingi duniani hivi sasa ambapo wananchi huchagua wawakilishi wao katika uchaguzi.
|
20231101.sw_1879_0
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Bunge
|
Bunge
|
Bunge ni chombo cha kutunga sheria na pia ni mmoja wa mihimili mitatu inayounda mfumo wa utawala kulingana na mgawanyo wa madaraka katika dola. Mihimili mingine ni mahakama na serikali.
|
20231101.sw_1879_1
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Bunge
|
Bunge
|
Bunge ni chombo kinachotokana na mfumo wa utawala wa Westminster, ambao umerithiwa na nchi nyingi duniani kutoka Uingereza. Kutokana na mfumo huo kuenea, mara nyingi Bunge la Uingereza huitwa "Mama wa Bunge" duniani.
|
20231101.sw_1879_2
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Bunge
|
Bunge
|
Bunge la kwanza nchini Uingereza liliundwa wakati wa utawala wa Mfalme Henri III katika karne ya 13. Bunge hilo lina sehemu mbili, Bunge la Makabwela na Bunge la Mabwanyeye.
|
20231101.sw_1879_3
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Bunge
|
Bunge
|
Katika nchi nyingi zinazofuata mfumo wa Westminster, Waziri Mkuu huwa ndio kiongozi mkuu wa serikali bungeni.
|
20231101.sw_1879_4
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Bunge
|
Bunge
|
Bunge la "vyumba viwili" ambako kitengo kikubwa zaidi kina kazi ya kutunga sheria na wabunge wake huchaguliwa moja kwa moja na wananchi katika majimbo ya uchaguzi yanayotakiwa kuwa takriban na idadi ya wapiga kura sawa. Kitengo kingine mara nyingi huitwa "senati" au "chumba cha juu" kwa kawaida ni kidogo zaidi, wabunge wake huchaguliwa ama na wawakilishi wa mikoa au majimbo au wanateuliwa pia kufuatana na kanuni za katiba (k.m. kwa shabaha ya kuwakilisha makundi maalumu katika jamii) na madaraka yake kwa kawaida ni madogo lakini inathibitisha au kukataa sheria zilizoamuliwa na bunge la kwanza; lakini hapa kuna tofauti nyingi kati ya nchi na nchi.
|
20231101.sw_1890_0
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mahakama
|
Mahakama
|
Mahakama ni mfumo wa wataalamu na kamati maalumu ambao unatafsiri na kutumia sheria katika jina la wananchi, la jamhuri au la mfalme.
|
20231101.sw_1890_1
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mahakama
|
Mahakama
|
Mahakama pia inatoa mfumo wa kutatua migogoro. Chini ya mfumo wa mgawanyo wa madaraka mahakama kwa ujumla haitungi wala haiundi sheria (ambayo ni kazi ya bunge) wala kutekeleza sheria (ambayo ni wajibu wa serikali), bali inatafsiri sheria na kutumia na kutekeleza katika ukweli wa kila kesi.
|
20231101.sw_1890_2
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mahakama
|
Mahakama
|
Kwa kawaida kuna mahakama za ngazi mbalimbali; mahakama za juu zinapokea rufaa dhidi ya kesi za ngazi za chini hadi mahakama ya rufaa ya mwisho inayoitwa mahakama kuu au mahakama ya katiba. Tawi hili la mahakama lina uwezo wa kubatilisha sheria zisizolingana na katiba ya nchi.
|
20231101.sw_1890_3
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mahakama
|
Mahakama
|
Neno "mahakama" pia hutumika kumaanisha kwa pamoja maafisa ndani yake kama vile majaji, mahakimu na makarani wengine.
|
20231101.sw_1890_4
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mahakama
|
Mahakama
|
Kimsingi mahakama ina kazi ya kutumia sheria zilizopo na kuamua juu ya matumizi yao. Hali halisi sheria haziwezi kutaja kila kitu kinachoweza kutokea hivyo ni mahakama zinazoamua kwa njia ya kulinganisha kesi, sheria na maazimio ya mahakama yaliyotangulia.
|
20231101.sw_1890_5
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mahakama
|
Mahakama
|
Kwa hiyo mahakama zinashiriki kiasi katika kazi ya kutunga haki hasa pale ambako sheria za bunge zinaacha pengo.
|
20231101.sw_1890_6
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mahakama
|
Mahakama
|
Kidesturi muundo wa haki na sheria katika Uingereza na Marekani unaziachia mahakama nafasi kubwa zaidi kuendeleza taratibu za kisheria.
|
20231101.sw_1890_7
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mahakama
|
Mahakama
|
Cardozo, Benjamin N. (mwaka wa (1998). The Nature wa mchakato wa kimahakam. New Haven: Yale University Press.
|
20231101.sw_1890_8
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mahakama
|
Mahakama
|
Feinberg, Kenneth, Jack Kress, Gary McDowell, na Warren E. Burger (1986). The High Cost and Effect of Litigation, matoleo 3.
|
20231101.sw_1890_9
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mahakama
|
Mahakama
|
Marshall, Thurgood (2001). Thurgood Marshall: His Speeches, Writings, Arg, maoni na Reminiscences. Chicago: Lawrence Hill Books.
|
20231101.sw_1890_10
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mahakama
|
Mahakama
|
McCloskey, Robert G., na Sanford Levinson (2005). The American Supreme Court, toleo la 4. Chicago: University of Chicago Press.
|
20231101.sw_1890_11
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mahakama
|
Mahakama
|
Miller, Arthur S. (1985). Politics,Democracyand the Supreme Court:Essays on the Future of Constitutional Theory. Westport, CT: Greenwood Press.
|
20231101.sw_1890_12
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mahakama
|
Mahakama
|
Tribe, Laurence (1985). God Save This Honorable Court: How the Choice of Supreme Court Justices Shapes our History. New York: Random House.
|
20231101.sw_1891_0
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Katiba
|
Katiba
|
Katiba ni sheria au kanuni zinazoaInisha jinsi ambavyo nchi, chama, au shirika vitakavyoendesha shuguli zao.
|
20231101.sw_1891_1
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Katiba
|
Katiba
|
Kwa upande wa nchi, katiba ni sheria mama inayoainisha misingi mikuu ya kisiasa na kuonyesha madaraka na majukumu ya serikali. Katiba za nchi pia huainisha haki za msingi za wananchi.
|
20231101.sw_1899_0
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ukimwi
|
Ukimwi
|
Upungufu wa Kinga Mwilini (kwa kifupi UKIMWI; kifupisho cha Kiingereza AIDS) ni ugonjwa unaotokana na virusi ambavyo kwa Kiswahili vinaitwa kifupi VVU ("Virusi vya UKIMWI"; kwa Kiingereza: HIV, yaani "Human Immunodeficiency Virus") na vinashambulia mwili kwa kuondoa nguvu zake za kupambana na maambukizi nyemelezi yanayosababisha maradhi.
|
20231101.sw_1899_1
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ukimwi
|
Ukimwi
|
Ukimwi ni ugonjwa hatari sana katika maisha ya binadamu kwa kuwa husababisha vifo (yaani kupotea kwa uhai wa watu hao). Kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani, kufikia mwaka 2014 ugonjwa huu umeua watu milioni 39, hasa kati ya wanaoishi barani Afrika upande wa kusini kwa Sahara. Kwa mwaka 2015 pekee wamefariki watu milioni 1.2 na kati yao watoto wengi.
|
20231101.sw_1899_2
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ukimwi
|
Ukimwi
|
UKIMWI umekuwa na madhara makubwa katika jamii, kama ugonjwa wa mwili na kama chanzo cha ubaguzi. Kuna sintofahamu kuhusu UKIMWI kama vile kwamba eti, unaweza kusambazwa kwa kugusana tu bila ngono.
|
20231101.sw_1899_3
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ukimwi
|
Ukimwi
|
Hadi hivi sasa, UKIMWI hauna chanjo wala tiba, lakini ugonjwa huu unaweza kuepukika kwa kuachana na ngono, ambayo ndiyo husababisha sana ugonjwa huu. Pia, watu wanaweza kujikinga kutokana na ugonjwa huu kwa kuepuka kuchangia vifaa au vitu vyenye ncha kali.
|
20231101.sw_1899_4
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ukimwi
|
Ukimwi
|
Kimsingi zaidi ni kwamba ugonjwa huo umetokana na kuenezwa hasa na maadili mabovu. Dhidi yake watu wanahitaji kuelewa tangu utotoni na ujanani maana ya jinsia na maisha kwa jumla, kwamba vinadai upendo, nidhamu na uwajibikaji, si kufuata tamaa tofautitofauti daima.
|
20231101.sw_1899_5
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ukimwi
|
Ukimwi
|
Upungufu maana yake UKIMWI unaharibu uwezo wa mwili kupambana na magonjwa. Si UKIMWI moja kwa moja unaoweza kuua lakini mashambulio ya magonjwa ambayo kwa kawaida yasingekuwa tatizo kubwa.
|
20231101.sw_1899_6
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ukimwi
|
Ukimwi
|
Mwili usio na kinga unapatwa na matatizo mbalimbali kwa sababu mfumo wa kinga umeharibika, na hauwezi kupigana na ugonjwa wowote.
|
20231101.sw_1899_7
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ukimwi
|
Ukimwi
|
syndrome - ni mkusanyiko wa matatizo ya kiafya; ilhali kingamwili haufanyi kazi tena, mgonjwa anaathiriwa na magonjwa mbalimbali na kuonyesha dalili za magonjwa hayo yote.
|
20231101.sw_1899_8
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ukimwi
|
Ukimwi
|
Kila mtu huwa na mfumo wa kingamwili ndani yake. Seli za ulinzi zinazunguka mwilini na kutafuta vidubini vya nje vinavyoweza kuleta mvurugo na zinaviharibu. Kati ya seli hizi za ulinzi ni seli nyeupe za damu (lukosaiti) ambazo ni muhimu sana.
|
20231101.sw_1899_9
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ukimwi
|
Ukimwi
|
Ukimwi unasababishwa na VVU. Kama virusi vyote, VVU vinaingia katika mwili kwa kusudi la kuzaa. Virusi haviwezi kuzaa peke yake: vinahitaji seli vinapoweza kuingia ndani yake na kutumia mfumo wa seli kwa kunakili DNA yake.
|
20231101.sw_1899_10
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ukimwi
|
Ukimwi
|
Kwa kawaida virusi vinashambuliwa na mfumo wa kingamwili na kuharibika. Lakini VVU vina tabia mbili za pekee ambazo zinavifanya vvya hatari hasa:
|
20231101.sw_1899_11
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ukimwi
|
Ukimwi
|
vinaingia hasahasa katika seli nyeupe za damu za aina "seli za T". VVU vikianza kuongezeka katika seli nyeupe ya damu vinadhoofisha na hatimaye kuharibu seli hii.
|
20231101.sw_1899_12
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ukimwi
|
Ukimwi
|
Maana yake VVU vinashambulia moja kwa moja seli ambazo ni sehemu ya kingamwili na zinazohusika kukinga mwili. Kuenea kwa VVU mwilini kunapunguza idadi ya seli za ulinzi na hivyo kupunguza kiwango cha kingamwili.
|
20231101.sw_1899_13
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ukimwi
|
Ukimwi
|
Baada ya kupungua kwa kingamwili vidubini vingine vinaendelea kufika mwilini lakini sasa vinaenea zaidi kwa sababu seli za ulinzi zimekuwa chache. Kila ambukizo linaendelea kwa muda mrefu zaidi na hivyo mwili kwa jumla unateswa kwa muda mrefu zaidi.
|
20231101.sw_1899_14
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ukimwi
|
Ukimwi
|
Kadiri Ukimwi unavyoendelea vipindi vya magonjwa vinakuwa virefu zaidi na nguvu za mwili zinapunguapungua. Katika ngazi za mwisho idadi ya maambukizo inazidi uwezo wa mwili wa kupambana nayo na hapo mtu unakaribia kifo.
|
20231101.sw_1899_15
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ukimwi
|
Ukimwi
|
UKIMWI ni ugonjwa wa mfumo wa kingamwili wa binadamu unaosababishwa na virusi vya ukosefu wa kinga mwilini.Mwanzoni, baada ya kuambukizwa, mtu anaweza kukumbwa na kipindi kifupi cha maradhi ya aina ya mafua. Kwa kawaida, hali hii hufuatwa na kipindi kirefu kisicho na dalili. Ugonjwa huu huendelea kutatiza kingamwili jinsi unavyozidi, hivyo kumfanya mtu kuwa katika hatari zaidi ya kupata maambukizi, ikiwa ni pamoja na maambukizi nyemelezi, na kansa ambayo kwa kawaida hayawaathiri watu walio na kingamwili njema.
|
20231101.sw_1899_16
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ukimwi
|
Ukimwi
|
Kipindi cha kwanza kufuatia maambukizi ya VVU huitwa VVU vikali, VVU vya kimsingi au dalili kali za kudhibiti virusi. Watu wengi hupata maradhi ya mfano wa mafua au maambukizi ya mfano wa mononukleosi wiki 2 - 4 baada ya kuambukizwa ilhali wengine hawana dalili zozote kuu.Dalili hutokea katika asilimia 40-90 ya visa vyote na mara nyingi hujumuisha homa, tezi kubwa na chungu za limfu, inflamesheni ya koo, upele, maumivu ya kichwa, na/au vidonda vya kinywa na sehemu za uzazi.Upele huu, unaotokea katika asilimia 20 - 50 ya visa, hutokea katika kiwiliwili, na kwa kawaida huwa wa makiulopapula.
|
20231101.sw_1899_17
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ukimwi
|
Ukimwi
|
Baadhi ya watu pia hupata maambukizi nyemelezi katika awamu hii.Dalili za tumboni na utumboni kama vile kichefuchefu, kutapika au kuharisha zinaweza kutokea, sawa na dalili za kinuroni za niuropathia ya pembeni au sindromu ya Guillain-Barre. Muda ya dalili hutofautiana, ingawa kwa kawaida huwa wiki 1 - 2.
|
20231101.sw_1899_18
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ukimwi
|
Ukimwi
|
Kufuatia sifa zake za kutokuwa dalili maalum, hizi mara nyingi haziwezi kutambulika kama dalili za maambukizi ya VVU. Hata visa vinavyotambuliwa na daktari wa familia au katika hospitali mara nyingi hutambulika vibaya kama baadhi ya visababishi vingi vya magonjwa ambukizi yaliyo na dalili zinazoingiliana. Kwa hivyo, inapendekezwa kuchunguza VVU katika watu wanaoonyesha homa isiyoelezeka ambao wanaweza kuwa na vipengele hatari vya kuambukizwa.
|
20231101.sw_1899_19
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ukimwi
|
Ukimwi
|
Dalili za kwanza hufuatwa na awamu fiche (VVU visivyo na dalili au VVU vya muda mrefu).Bila ya matibabu, awamu hii ya pili ya historia asilia ya maambukizi ya VVU inaweza kudumu kutoka miaka 3 hadi zaidi ya miaka 20; (wastani wa miaka 8).Ingawa kwa kawaida mwanzoni kuna dalili chache, au hata zisiwemo, karibu mwishoni mwa awamu hii, watu wengi hupatwa na homa, kukonda, matatizo ya tumbo na utumbo, na maumivu ya misuli. Kati ya asilimia 50 na 70 ya wagonjwa pia hupata limfadenopathia ya mwili wote inayorejea, ambayo hudhihirika kwa uvimbe usio na kisababishi na usio chungu wa zaidi ya kikundi kimoja cha tezi za limfu (ila katika sehemu za uzazi) kwa zaidi ya miezi 3 hadi 6.
|
20231101.sw_1899_20
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ukimwi
|
Ukimwi
|
Ingawa watu wengi walioambukizwa VVU-1 wana kiwango cha virusi kinachoweza kutambulika, na ambacho bila matibabu kitaendelea na kuwa UKIMWI, idadi ndogo (5%) huwa na kiwango kikubwa cha seli za CD4+(seli saidizi za T) bila matibabu ya kudhibiti virusi kwa zaidi ya miaka 5. Watu hao huainishwa kama wadhibiti wa VVU au watu wasioendeleza kwa muda mrefu, ilhali wale ambao pia hudumisha kiwango cha chini au kisichotambulika cha virusi bila matibabu hujulikana kama "wadhibiti hodari" au "wagandamizaji hodari" .
|
20231101.sw_1899_21
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ukimwi
|
Ukimwi
|
Ukosefu wa Kinga Mwilini (UKIMWI) hufasiliwa kwa msingi wa kiwango cha seli za CD4 + cha chini ya seli 200 kwa kila µL au kutokea kwa magonjwa maalumu yanayohusiana na maambukizi ya VVU. Bila matibabu maalum, takriban nusu ya watu walioambukizwa VVU hupata UKIMWI katika muda wa miaka 10.Hali zinazotokea mara nyingi zaidi kudhihirisha uwepo wa UKIMWI ni numonia ya numosistisi (40%), kakeksi kwa muundo wa dalili dhoofishi za VVU (20%) na kandidiasi ya umio.Dalili nyingine ni pamoja na maambukizi ya njia ya pumzi.
|
20231101.sw_1899_22
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ukimwi
|
Ukimwi
|
Maambukizi nyemelezi yanaweza kusababishwa na bakteria, virusi, kuvu na vimelea ambavyo kwa kawaida hudhibitiwa na mfumo wa kingamwili.Maambukizi yanayotokea hutegemea, kwa upande mmoja, aina ya viumbehai vinavyopatikana kwa wingi katika mazingira ya mtu.Maambukizi hayo yanaweza kudhuru karibu kila mfumo wa viungo.
|
20231101.sw_1899_23
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ukimwi
|
Ukimwi
|
Watu walio na UKIMWI wako katika hatari kuu zaidi ya kupata saratani nyingi zinazosababishwa na virusi, kama vile: Sakoma ya Kaposi, limfoma ya Burkitt, limfoma ya mfumo mkuu wa neva na saratani ya seviksi.Sakoma ya Kaposi ndiyo saratani inayotokea mara nyingi, yaani katika asilimia 10 hadi 20 ya watu wenye VVU.Saratani inayoifuata ni limfoma, ambayo imesababisha vifo vya karibu 16% ya watu wanaoishi na UKIMWI, na ndiyo dalili ya kwanza ya UKIMWI katika asilimia 3 - 4 ya watu.Saratani hizi mbili huhusishwa na virusi vya hepesi ya binadamu aina ya 8.Saratani ya seviksi hutokea mara nyingi zaidi katika watu walio na UKIMWI kwa sababu ya jinsi inavyohusiana na virusi vya papiloma ya binadamu.
|
20231101.sw_1899_24
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ukimwi
|
Ukimwi
|
Isitoshe, watu hao mara nyingi huwa na dalili za kimfumo, kama vile homa ya muda mrefu, jasho (hasa usiku), tezi za limfu zilizofura, ubaridi, udhaifu na kupoteza uzito.Kuharisha ni dalili nyingine inayotokea katika takriban 90% ya watu wenye UKIMWI.
|
20231101.sw_1899_25
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ukimwi
|
Ukimwi
|
UKIMWI huchukuliwa kama janga — yaani mlipuko wa ugonjwa katika eneo kubwa, na ambao ungali unaenea.
|
20231101.sw_1899_26
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ukimwi
|
Ukimwi
|
UKIMWI ulitambuliwa mara ya kwanza na Vituo vya Kuzuia na Kudhibiti Magonjwa huko Marekani mwaka 1981, ilhali kisababishi chake - VVU - kilitambuliwa mwanzoni mwa muongo huo nchini huko.
|
20231101.sw_1899_27
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ukimwi
|
Ukimwi
|
Matukio ya kwanza yalikuwa katika kikundi kidogo cha waraibu wa dawa za kudungia na wanaume shoga wasiokuwa na visababishi bayana vya udhaifu wa kingamwili na walioonyesha dalili za numonia ya Pneumocystis carinii, maambukizi nyemelezi yanayotokea kwa nadra na maarufu katika watu wenye kingamwili dhaifu sana.
|
20231101.sw_1899_28
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ukimwi
|
Ukimwi
|
Punde baadaye, idadi isiyotarajiwa ya mashoga wakapata Sakoma ya Kaposi (SK), saratani ya ngozi iliyokuwa nadra sana hapo awali.Visa vingine vingi vya NPC na SK vilitokea huku vikitahadharisha Vituo vya Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa nchini Marekani, hivyo kikosi cha kiutendaji kikaundwa ili kuudhibiti mzuko huu.
|
20231101.sw_1899_29
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ukimwi
|
Ukimwi
|
Katika siku za kwanza, kituo hicho hakikuwa na jina rasmi la ugonjwa huu, mara nyingi wakitumia majina ya magonjwa mengine yaliyohusishwa nao, kwa mfano, limfadenopathi, jina ambalo baadaye wavumbuzi wa VVU waliviita virusi hivi. Wavumbuzi pia walitumia “Sakoma ya Kaposi na Maambukizi nyemelezi”, jina lililokuwa la kikosi cha kiutendaji kilichoanzishwa mwaka wa 1981. Wakati mmoja, Kituo cha Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa kiliunda msemo "ugonjwa wa 4H", kwani sindromu hii ilionekana kuwaathiri watu wa Haiti, mashoga (homosexuals), wenye hemofilia na watumiaji wa heroini. Katika vyombo vikuu vya habari liliundwa neno "GRID" (lililosimamia "gay-related immune deficiency", yaani "ukosefu wa kinga uliohusishwa na mashoga". Hata hivyo, baada ya kutambua kuwa VVU havikuwaathiri jamii ya mashoga pekee, ilibainika kuwa neno GRID lilikuwa likipotosha, hivyo neno UKIMWI likaanzishwa kwenye mkutano mnamo Julai 1982. Kufikia Septemba 1982, Kituo cha Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa kilianza kuuita UKIMWI.
|
20231101.sw_1899_30
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ukimwi
|
Ukimwi
|
Mnamo 1983, vikundi viwili tofauti vya watafiti vilivyoongozwa na Robert Gallo na Luc Montagnier bila kutegemeana vilitangaza kuwa retrovirusi mpya ilikuwa ikiwaambukiza wagonjwa wa UKIMWI, hivyo wakachapisha matokeo yao katika jarida la Science. Gallo alidai kuwa virusi vilivyokuwa vimetambuliwa kwa mara ya kwanza na kikundi chake kilikuwa sawa katika umbo na virusi vya binadamu vya limfotrophia-T. Kikundi cha Gallo kiliviita virusi hivi HTLV-III.
|
20231101.sw_1899_31
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ukimwi
|
Ukimwi
|
Wakati huohuo, kikundi cha Montagnier kilitambua virusi kutoka kwa mgonjwa aliyekuwa na uvimbe wa tezi za limfu kwenye shingo na udhaifu wa mwili ambazo ni dalili mbili bainifu za UKIMWI. Huku wakikanusha ripoti ya kikundi cha Gallo, Montagnier na wenzake walionyesha kuwa viini vya protini vya virusi hivyo vilikuwa tofauti na HTLV-I kiukingamwili. Kikundi cha Montagnier kiliviita virusi walivyovitambua virusi vinavyohusishwa na limfadenopathi. Virusi hivi vilibainika kuwa sawa mwaka wa 1986 na kubadilishwa na kuitwa VVU.
|
20231101.sw_1899_32
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ukimwi
|
Ukimwi
|
Leo wanasayansi wengi wanaamini VVU-1 na VVU-2 vimetokana na jamii ya sokwe huko Afrika Magharibi na ya Kati mwishoni mwa karne ya 19 au mwanzoni mwa karne ya 20, wakati virusi vya SIV kutoka kwa nyani au sokwe vilikwenda kwa binadamu. VVU-1 vinaaminika kutoka kusini mwa Cameroon kupitia kugeuka kwa VSVU(cpz), (virusi vya sokwe vinavyosababisha ukosefu wa kinga mwilini) vinavyoambukiza sokwe wa mwituni (VVU-1 hutokana na mzuko wa magonjwa ya VSVUcpz katika nususpishi ya sokwe iitwayo Pan troglodytes troglodytes).
|
20231101.sw_1899_33
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ukimwi
|
Ukimwi
|
Virusi vinavyohusiana kwa karibu na VVU-2 ni VSVU(smm) ambavyo ni virusi vya mangabi mwenye masizi (Cercocebus atys atys), tumbili wa kale anayeishi Afrika Magharibi (kutoka kusini mwa Senegali hadi magharibi mwa Côte d'Ivoire). Tumbili wa kisasa kama vile tumbili bundi wana ukinzani wa maambukizi ya VVU-1 kwa sababu ya uunganishaji wa jeni mbili zinazokinzana na virusi.
|
20231101.sw_1899_34
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ukimwi
|
Ukimwi
|
VVU-2 inadhaniwa kuruka kizuizi cha spishi katika angalau matukio matatu tofauti, hivyo kupelekea vikundi vitatu vya virusi hivi ambavyo ni M, N na O.
|
20231101.sw_1899_35
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ukimwi
|
Ukimwi
|
Kuna ushahidi kuwa wanadamu wanaoshughulikia nyama za mwituni kwa kuwinda au kuziuza, kwa kawaida hupata VSVU.Hata hivyo, virusi hivyo ni dhaifu na hukandamizwa na mfumo wa kingamwili baada ya wiki kadhaa za kuambukizwa. Inadhaniwa kuwa maambukizi kadhaa ya virusi hivyo kutoka kwa mtu hadi mwingine katika mfululizo wa haraka huhitajika ili vipate wakati unaotosha kubadilika na kuwa VVU. Zaidi ya hayo, kwa sababu ya kiwango chake kidogo cha kuambukiza kutoka kwa mtu hadi mwingine, virusi hivyo vinaweza tu kuenea katika wingi wa watu iwapo kuna njia moja au mbili za hatari ya kuambukizana ya kiwango cha juu. Njia hizi zinadhaniwa kutokuwepo barani Afrika kabla ya karne ya 20.
|
20231101.sw_1899_36
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ukimwi
|
Ukimwi
|
Njia maalumu za hatari kubwa ya maambukizi zinazoruhusu virusi hivi kubadilika ili kuweza kuishi katika wanadamu na kuenea katika jamii yote hutegemea wakati uliopendekezwa wa kuvuka kutoka kwa mnyama hadi mwanadamu. Tafiti za kijeni za virusi hivi zinadokeza kuwa chanzo cha hivi karibuni zaidi cha VVU-1 ya kikundi M kilitokea mnamo 1910. Wanaotaja kipindi hicho maalumu huhusisha mzuko wa janga la VVU na kuibuka kwa ukoloni na ukuaji wa miji mikubwa ya kikoloni ya Afrika, huku ukisababisha mabadiliko ya jamii pamoja na kiwango kikubwa cha uasherati, uenezi wa ukahaba na matukio mengi ya vidonda vya viungo vya uzazi (kama vile kaswende) katika miji iliyochipuka.
|
Subsets and Splits
No community queries yet
The top public SQL queries from the community will appear here once available.