_id
stringlengths 15
22
| url
stringlengths 31
150
| title
stringlengths 1
86
| text
stringlengths 100
23.8k
|
---|---|---|---|
20231101.sw_1899_137
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ukimwi
|
Ukimwi
|
Mgonjwa mashuhuri kutoka Uingereza mwaka huo alikuwa Nicholas Eden mwanasiasa shoga na mwana wa Waziri Mkuu, marehemu Anthony Eden.
|
20231101.sw_1899_138
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ukimwi
|
Ukimwi
|
Tarehe 24 Novemba 1991, virusi hivi vilipelekea kifo cha mwanamuziki wa aina ya muziki wa rock, Mwingereza Freddie Mercury. Mercury, aliyeongoza bendi iliyojulikana kama Queen alifariki kutokana na magonjwa yanayohusiana na UKIMWI baada ya kujulikana kuwa na ugonjwa huo siku iliyopita tu. Hata hivyo, Mercury alikuwa ametambuliwa kuwa na ugonjwa huo mwaka 1987.
|
20231101.sw_1899_139
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ukimwi
|
Ukimwi
|
Kimojawapo kati ya visa maarufu zaidi vilivyotokana na ngono kati ya watu wa jinsia tofauti ni kile cha Arthur Ashe, mchezaji tenisi Mmarekani. Ashe alitambuliwa kuwa na VVU tarehe 31 Agosti 1988; baada ya kuambukizwa alipokuwa akiongezewa damu akifanyiwa upasuaji wa moyo awali miaka ya 1980. Vipimo zaidi katika saa 24 baada ya utambuzi wa kwanza vilionyesha kuwa Ashe alikuwa na UKIMWI, lakini hakuwambia watu kuhusu utambuzi huu hadi Aprili 1992. Ashe alifariki kutokana na UKIMWI akiwa na umri wa miaka 49 tarehe 6 Februari 1993.
|
20231101.sw_1899_140
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ukimwi
|
Ukimwi
|
Picha ya Therese Frare ikionyesha mwanaharakati wa ushoga David Kirby akifariki kutokana na UKIMWI huku akizungukwa na familia yake, ilipigwa Aprili mwaka wa 1990. LIFE magazine ilisema kuwa picha hiyo ilikuja kufahamika kama picha maarufu zaidi kuwahi kuhusishwa na janga la UKIMWI/VVU.'' Picha hiyo iliyochapishwa na gazeti hilo ilishinda tuzo la World Press Photo, kisha kupata umaarufu ulimwenguni kote baada ya kutumiwa na United Colors of Benetton katika kampeni ya utangazaji ya mwaka 1992.
|
20231101.sw_1899_141
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ukimwi
|
Ukimwi
|
Kikundi kidogo cha watu kingali kinakana uhusiano wa VVU na UKIMWI, uwepo wa VVU au ubora wa vipimo vya VVU na njia za matibabu.
|
20231101.sw_1899_142
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ukimwi
|
Ukimwi
|
Madai hayo, yanayojulikana kama ukanaji UKIMWI, yamechunguzwa na kukataliwa na jamii ya kisayansi.Hata hivyo, madai hayo yana athari kuu kisiasa, hasa nchini Afrika Kusini. Hatua ya serikali ya nchi hiyo kukubali kirasmi ukanaji wa UKIMWI ilipelekea mwitikio usiofaa wa janga hili, na imelaumiwa kupelekea visa vingi vya maambukizi ya VVU na mamia ya maelfu ya vifo ambavyo vingeepukwa.
|
20231101.sw_1899_143
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ukimwi
|
Ukimwi
|
Urusi ulianzisha Operesheni INFEKTION, uhamasisho wa ulimwengu mzima kueneza habari kuwa VVU/UKIMWI ulitengenezwa na Marekani. Takwimu zinaonyesha kuwa idadi kubwa ya watu wanaamini na wanaendelea kuamini madai hayo.
|
20231101.sw_1899_144
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ukimwi
|
Ukimwi
|
Kuna aina nyingi za dhana potovu kuhusu VVU na UKIMWI. Dhana tatu kuu ni kwamba UKIMWI unaweza kusambazwa kwa kumgusa mtu, kuwa ngono na bikira itatibu UKIMWI na kuwa VVU vinaweza tu kuambukiza mashoga na watumiaji wa madawa. Dhana nyingine potovu ni kuwa tendo lolote la ngono ya kinyeo kati ya mashoga wasioambukizwa linaweza kupelekea maambukizi.
|
20231101.sw_1899_145
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ukimwi
|
Ukimwi
|
Utafiti wa kuboresha matibabu ya kisasa unajumuisha kupunguza madhara ya ziada ya dawa zilizopo, kurahisisha kanuni za kutumia dawa na kuboresha ubora na kuamua utaratibu bora wa kanuni ili kudhibiti ukinzani wa dawa. Hata hivyo, chanjo pekee ndiyo inayodhaniwa kuweza kusitisha janga hili. Hii ni kwa sababu chanjo ni ya bei nafuu, hivyo mataifa yanayostawi yanaweza kuimudu, na haitahitaji matibabu ya kila siku.
|
20231101.sw_1899_146
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ukimwi
|
Ukimwi
|
Hata hivyo, baada ya miaka 20 ya utafiti, imekuwa vigumu kupata chanjo dhidi ya VVU-1, hivyo tiba bado haijapatikana.
|
20231101.sw_1899_147
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ukimwi
|
Ukimwi
|
Mwaka wa 2007, Timothy Ray Brown, mwanaume wa umri wa miaka 40 aliyekuwa na VVU, pia anayejulikana kama "the Berlin Patient" alipewa huduma ya pandikizo la seli kuu kama mojawapo ya matibabu ya lukemia sugu ya mieloidi (LSM).Pandikizo la pili lilifanyika mwaka uliofuata baada ya kuugua tena. Mfadhili alichanguliwa sio tu kwa kuwa ana upatanifu wa kijeni lakini pia kwa kuwa alikuwa na utangamano wa kubadilika kwa CCR5-Δ32 ambayo huwezesha ukinzani dhidi ya maambukizi ya VVU. Baada ya miezi 20 bila matibabu ya dawa za kudhibiti VVU, iliripotiwa kuwa viwango vya VVU kwenye damu ya Brown uboho na matumbo vilikuwa chini ya kiwango cha kutambulika.Virusi hivi vilibakia katika kiwango hicho kwa miaka mitatu baada ya upandikizo wa kwanza.Ingawa watafiti na baadhi ya wachambuzi wanasema kuwa matokeo haya ni tiba, wengine wao wanadokeza kuwa virusi hivi vinaweza kuwa vimejificha ndani ya tishukama vile ubongo (unaotumika kama hifadhi). Matibabu ya seli kuu yamebakia chini ya kuchunguzwa kwa sababu ya asili yake ya kinadharia, ugonjwa wenywe na hatari ya kufa inayohusishwa na upandikizaji wa seli kuu na ugumu wa kupata wafadhili mwafaka.
|
20231101.sw_1899_148
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ukimwi
|
Ukimwi
|
Matibabu saidizi za kudhibiti uigaji wa virusi, matibabu ya kingamwili zinazoweza kusaidia kuboresha mfumo wa kingamwili zilizochunguzwa awali, na juhudi zinazoendelea ni pamoja na IL-2 na IL-7.
|
20231101.sw_1899_149
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ukimwi
|
Ukimwi
|
Kutofaulu kwa chanjo kadhaa kukinga dhidi ya maambukizi ya VVU na kuendelea kwa UKIMWI kumepelekea mwelekeo mpya wa kuzingatia taratibu za kibayolojia zinazosababisha ufiche wa VVU. Kipindi kifupi cha matibabu ya kuunganisha dawa za kudhibiti VVU na dawa zinazolenga hifadhi fiche siku moja kinaweza kutokomeza maambukizi ya VVU.Watafiti wamegundua abusaimu inayoweza kuharibu eneo la kufungia protini ya gp120 CD4. Protini hii hupatikana katika aina zote za VVU kwa sababu ndiyo ncha ambapo limfosaiti za B hujishikisha kisha kuafikiana kwa mfumo wa kingamwili.
|
20231101.sw_1899_150
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ukimwi
|
Ukimwi
|
New England Journal of Medicine Ibara "Ruhusu dhidi ya Wagonjwa? Kurefusha maisha Tiba katika India"
|
20231101.sw_1901_0
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Desemba
|
Desemba
|
Desemba ni mwezi wa kumi na mbili katika kalenda ya Gregori na ni kati ya miezi saba katika kalenda hiyo yenye siku 31.
|
20231101.sw_1901_1
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Desemba
|
Desemba
|
Tarehe 21 ya mwezi huo wa Desemba (katika miaka mingine inawezekana kuwa tarehe 20 au 22) ni siku ya solistasi ya Kusini (kutoka Kiingereza solstice), yaani wakati Jua linapokuwa kusini kabisa mwa Ikweta.
|
20231101.sw_1901_2
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Desemba
|
Desemba
|
Neno Desemba limetokana na neno la Kilatini "decem" linalomaanisha "kumi." Desemba ulikuwa ni mwezi wa kumi katika kalenda ya Kirumi.
|
20231101.sw_1904_0
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mmea
|
Mmea
|
Mimea (kwa Kiingereza: "plants", kutoka Kilatini "Plantae") ni moja kati ya makundi ya viumbe hai duniani likijumuisha miti, maua, mitishamba na kadhalika. Kuna zaidi ya aina 300,000 ya mimea.
|
20231101.sw_1904_1
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mmea
|
Mmea
|
Sayansi inayochunguza mimea huitwa botania ambayo ni kitengo cha biolojia. Kwenye uainishaji wa kisayansi mimea hujumlishwa katika himaya ya plantae kwenye milki ya Eukaryota (viumbehai vyenye kiini cha seli na utando wa seli).
|
20231101.sw_1904_2
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mmea
|
Mmea
|
Kwa hiyo mimea huwa na utando wa seli wenye selulosi. Mmea unapata sehemu kubwa ya nishati kutoka nuru ya jua kwa njia ya usanisinuru, yaani hujilisha kwa msaada wa nuru. Ndani ya majani ya mimea kuna klorofili, dutu ya rangi ya kijani, inayofanya kazi ya kupokea nuru na kupitisha nishati yake kwa sehemu nyingine ya mmea ambamo inatumiwa kujenga molekuli zinazotunza nishati kwa njia ya kikemia na kutumiwa katika metaboli ya mwili.
|
20231101.sw_1904_3
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mmea
|
Mmea
|
Mimea kadhaa imepoteza uwezo wa kutengeneza klorofili ya kutosha, hivyo inajipatia nishati kama vimelea kutoka kwa mimea au viumbehai wengine.
|
20231101.sw_1904_4
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mmea
|
Mmea
|
Mimea mingi inazaa kwa njia ya jinsia, yaani kwa kuunganisha seli za kiume na kike; mara nyingi viungo vya kiume na vya kike vinapatikana ndani ya mmea mmoja. Kuna pia mimea inayozaa kwa njia isiyo ya kijinsia, kwa mfano kwa kuotesha mzizi wa hewani ambao unaingia ardhini na kuendelea kama mmea wa pekee.
|
20231101.sw_1904_5
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mmea
|
Mmea
|
Mimea ni msingi muhimu kwa viumbehai wengine duniani kwa sababu sehemu kubwa ya oksijeni katika angahewa ya dunia inatengenezwa na mimea..
|
20231101.sw_1904_6
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mmea
|
Mmea
|
Mimea inatoa chakula kwa binadamu kama vile nafaka, matunda na mboga za majani, pia lishe kwa wanyama wa kufugwa.
|
20231101.sw_1907_0
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Usanifu%20majengo
|
Usanifu majengo
|
Usanifu majengo ni sanaa na sayansi ya kubuni muundo na sura ya majengo. Sanaa na sayansi hii inajumuisha pia mambo kama mipango miji, usanifu wa eneo la kujenga, na hata ubunifu wa samani zitakazotumika ndani ya jengo.
|
20231101.sw_1907_1
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Usanifu%20majengo
|
Usanifu majengo
|
Watu wanaojihusisha na haya huitwa "wasanifu majengo". Wanahitaji elimu ya ujenzi, hesabu, sanaa, teknolojia, elimu jamii na historia. Msanifu wa kwanza anayejulikana kwa jina ni Imhotep wa Misri ya Kale.
|
20231101.sw_1907_2
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Usanifu%20majengo
|
Usanifu majengo
|
Mbinu za usanifu hutegemea teknolojia inayopatikana, hali ya hewa, hali ya jamii, utaratibu wa siasa yake, hali ya uchumi na mengine mengine.
|
20231101.sw_1908_0
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mipango%20miji
|
Mipango miji
|
Mipango miji ni sayansi na sera kuhusu maendeleo ya kijamii, kiuchumi, kimazingira katika miji na vitongoji vyake. Mgiriki Hippodamus anasemekana kuwa ndiye baba wa mipango miji kutokana na ubunifu wake wa mji wa Miletus ingawa kumekuwa na miji iliyopangwa kabla yake.
|
20231101.sw_1910_0
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/IRC
|
IRC
|
Internet Relay Chat (IRC) ni aina ya mawasiliano ya papo kwa hapo kupitia mtandao wa Intaneti. Teknolojia hii imeundwa hususan kwa ajili ya mawasiliano ya watu wengi kwa wakati mmoja, lakini pia mawasiliano ya mtu mmoja kwa mmoja yanawezekana.
|
20231101.sw_1910_1
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/IRC
|
IRC
|
Teknolojia hii ilitengenezwa na Jarkko Oikarinen Agosti 1998 ili kuchukua nafasi ya teknolojia nyingine kama hii iliyokuwa ikiitwa MUT huko Ufini.
|
20231101.sw_1910_2
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/IRC
|
IRC
|
IRC ilipata umaarufu pale ilipotumika kuripoti jaribio la kuipindua serikali ya Urusi mwaka 1991. Teknolojia hii ilitumiwa pia kuripoti uvamizi wa Kuwait na nchi ya Iraki.
|
20231101.sw_1911_0
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Blogu%20za%20mkononi
|
Blogu za mkononi
|
Blogu za mkononi ni aina ya blogu zinazotumia zana zinazoshikika mkononi kama vile simu za mkononi. Kwahiyo, habari, maoni, au visa vinatolewa katika mtandao wa kompyuta kwa kutumia zana hizi. Teknolojia hii ilianza huko Japan ambapo simu za mkono zenye kamera zilianza kupatikana kwa urahisi.
|
20231101.sw_1911_1
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Blogu%20za%20mkononi
|
Blogu za mkononi
|
Inasemekana utumaji wa habari kwenye mtandao wa kompyuta toka katika zana za mkononi ulifanywa na Steven Mann hapo mwaka 1955 alipotumia kompyuta inayovalika. Mwaka 2000 ndipo utumaji wa habari katika mtandao wa kompyuta toka katika simu ya mkono ulifanywa na Tom Paamand nchini Udeni.
|
20231101.sw_1911_2
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Blogu%20za%20mkononi
|
Blogu za mkononi
|
Adam Greenfield ndiye aliyeanzisha matumizi ya neno "blogu za mkononi." Aliandaa Mkutano wa Kwanza wa Kimataifa wa Blogu za Mkononi jijini Tokyo, Japani mwaka 2003.
|
20231101.sw_1912_0
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Paul%20Simon
|
Paul Simon
|
Paul Simon ni mwanamuziki wa country, anaimba na kupiga gitaa. Amewahi kushirikiana na wanamuziki wengi; moja ya makundi hayo ni Ladysmith Black Mambazo. Nyimbo alizowahi kuimba ni "Homeless", "Mother and child reunion" na "Diamond in the sole of her shoes".
|
20231101.sw_1912_1
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Paul%20Simon
|
Paul Simon
|
Paul Simon alizaliwa tarehe 13 Oktoba 1941 katika mji wa Newark Height, New Jersey. Huko alifahamika kama muimbaji na mtunzi mwenye asili ya kiyahudi. Aliwahi kufunga ndoa mara tatu, ana watoto wanne. Mmojawapo ni mpigaji gitaa kama baba yake.
|
20231101.sw_1928_0
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Shaaban%20Robert
|
Shaaban Robert
|
Shaaban Robert (1 Januari 1909 - 22 Juni 1962) alikuwa mshairi na mwandishi wa riwaya. Mchango wake katika lugha ya Kiswahili ni mkubwa kwani kazi zake zinaheshimika katika fasihi ya Kiswahili na pia zinatumika shuleni.
|
20231101.sw_1928_1
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Shaaban%20Robert
|
Shaaban Robert
|
Shaaban Robert alizaliwa tarehe 1 Januari 1909 katika kijiji cha Vibambani, jirani na Machui, kilomita 10 kusini mwa mji wa Tanga.
|
20231101.sw_1928_2
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Shaaban%20Robert
|
Shaaban Robert
|
Wazazi wake wote wawili walikuwa wa ukoo wa Mganga wa kabila la Wayao, lakini hakujiita Myao kabisa, bali alikuwa mmojawapo wa wachache ambao daima walijiita Waswahili.
|
20231101.sw_1928_3
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Shaaban%20Robert
|
Shaaban Robert
|
Kabla ya baba yake kuitwa Roberto , mwanzo alifahamika kwa jina la Ufukwe na jina hili lilitokana na Mzee Robert kuzaliwa karibu na ufukwe . Jina la Roberto lilitokana na tajiri mmoja aliyekuwa amemuajiri baba yake (babu yake Shaabani Robert). Baada tu ya Shaaban Robert kuingia katika shule za Wazungu alibadili jina kutoka Roberto na kuwa Robert.
|
20231101.sw_1928_4
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Shaaban%20Robert
|
Shaaban Robert
|
Alipata elimu yake katika shule ya Msimbazi, jijini Dar-es-Salaam kati ya miaka 1922 na 1926, akawa mtu wa pili katika wanafunzi kumi na mmoja waliofaulu mitihani yao na kupewa shahada ya kutoka chuoni, yaani School Leaving Certificate.
|
20231101.sw_1928_5
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Shaaban%20Robert
|
Shaaban Robert
|
Akaajiriwa na serikali ya kikoloni akawa karani katika idara ya forodha huko Pangani miaka 1926 – 1944. Bila shaka kukaa kwake miaka mingi hivi katika mji wa kihistoria uliokuwa mahali pa utamaduni wa Waswahili tena mahali patulivu kulisaidia maendeleo yake Shaaban kama mwandishi wa Kiswahili.
|
20231101.sw_1928_6
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Shaaban%20Robert
|
Shaaban Robert
|
Tangu mwaka 1944 hata 1946 alihamia ofisi nyingine ya Hifadhi ya Wanyama, baadaye ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tanga (tokea mwaka 1952 hata 1960).
|
20231101.sw_1928_7
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Shaaban%20Robert
|
Shaaban Robert
|
Alipandishwa cheo kuwa Grade III Higher Division mwaka 1929, na katika mwaka wa 1944 akapandishwa tena kuwa Grade II Local Service.
|
20231101.sw_1928_8
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Shaaban%20Robert
|
Shaaban Robert
|
Kwa ujumla Shaaban Robert aliandika vitabu ishirini na mbili. Baadhi ya vitabu hivi ni: Adili na Nduguze, Kusadikika, Kufikirika, Wasifu wa Siti Binti Saad, Maisha Yangu Baada ya Miaka Hamsini, Utubora Mkulima.
|
20231101.sw_1928_9
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Shaaban%20Robert
|
Shaaban Robert
|
Mbali na maandiko yake alikuwa na athari kubwa katika maendeleo ya lugha ya Kiswahili akiwa mjumbe wa kamati za East Africa Swahili Committee, East Africa Literature Bureau na Tanganyika Languages Board. Alikuwa pia mwanachama wa Tanga Township Authority.
|
20231101.sw_1928_10
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Shaaban%20Robert
|
Shaaban Robert
|
Alifariki dunia huko Tanga tarehe 22 Juni 1962 akazikwa Machui. Aliacha wake watatu na watoto watano, ingawa aliwazaa kumi. Mke wa kwanza alikuwa Mdigo. Pia aliacha dada yake (wa baba mmoja) Mwana Saumu, na mama yake.
|
20231101.sw_1928_11
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Shaaban%20Robert
|
Shaaban Robert
|
Alitunza kwa zawadi ya waandishi inayoitwa ‘Margaret Wrong Memorial Prize’; pia alikuwa ametunzwa nishani ya M.B.E.
|
20231101.sw_1950_0
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mkoa%20wa%20Mbeya
|
Mkoa wa Mbeya
|
Mkoa wa Mbeya ni kati ya mikoa 31 ya Tanzania, ukipakana na Zambia na Malawi, halafu na mikoa ya Rukwa, Tabora, Singida na Iringa, mbali na mkoa mpya wa Songwe uliomegwa kutoka ule wa Mbeya upande wa magharibi mwaka 2016. Una Postikodi namba 53000.
|
20231101.sw_1950_1
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mkoa%20wa%20Mbeya
|
Mkoa wa Mbeya
|
Kabla ya kugawiwa kulikuwa na wilaya 9 zifuatazo: Mbeya Mjini, Mbeya Vijijini, Rungwe, Kyela, Ileje, Mbozi, Chunya, Momba na Mbarali.
|
20231101.sw_1950_2
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mkoa%20wa%20Mbeya
|
Mkoa wa Mbeya
|
Tangu 2016 mkoa umekuwa na wilaya za Busekelo, Chunya, Kyela, Mbarali, Mbeya Mjini, Mbeya Vijijini na Rungwe.
|
20231101.sw_1950_3
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mkoa%20wa%20Mbeya
|
Mkoa wa Mbeya
|
Kijiolojia mkoa wa Mbeya ni eneo la kukutana kwa mikono miwili ya Bonde la Ufa la Afrika ya Mashariki inayoendelea hapa katika ziwa Nyasa. Mkoa wa Mbeya inapakana pia na Ziwa Rukwa. Hasa milima yenye asili ya volkeno ya wilaya ya Rungwe imejaa maziwa ya kasoko.
|
20231101.sw_1950_4
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mkoa%20wa%20Mbeya
|
Mkoa wa Mbeya
|
Wilaya ya Rungwe ni eneo lenye mvua nyingi katika Tanzania, ila maeneo makubwa ya Wilaya ya Chunya ni makavu..
|
20231101.sw_1950_5
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mkoa%20wa%20Mbeya
|
Mkoa wa Mbeya
|
Mkoa kwa ujumla ni mmojawapo kati ya mikoa yenye kilimo kizuri inayotoa mazao ya kulisha taifa Mbeya na Mbozi kahawa hupandwa. Rungwe pana chai nyingi, pamoja na Rungwe na Chimala hulimwa mpunga. Nyanda za juu kuna nafaka na viazi.
|
20231101.sw_1950_6
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mkoa%20wa%20Mbeya
|
Mkoa wa Mbeya
|
Wilaya ya Chunya ina madini mbalimbali hasa dhahabu. Wenyeji wa wilaya ya Chunya ni Wabungu na waishio huko zaidi ni Wanyiha.
|
20231101.sw_1950_7
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mkoa%20wa%20Mbeya
|
Mkoa wa Mbeya
|
Mbeya ni kati ya maeneo yanayopendeza kabisa ndani ya Tanzania ikiwa na sehemu za ziwa Nyasa, Mlima ya Mbeya, Mlima ya Rungwe, Uwanda wa juu wa Uporoto, Uwanda wa Usangu ingawa haukufikiwa bado na utalii. Mkoa wa Mbeya una idadi ya vivutio vya kitalii ambavyo ni pamoja na:
|
20231101.sw_1951_0
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ladysmith%20Black%20Mambazo
|
Ladysmith Black Mambazo
|
Ladysmith Black Mambazo ni kundi la muziki ambalo linaimba bila kutumia ala za muziki. Kundi hili lipo Afrika ya Kusini. Neno "Mambazo" linamaanisha "shoka" kwa Kizulu. Na "Ladysmith" ni kitongoji katika jimbo la Natal alichotoka Joseph Shabalala kiongozi na mwanzilishi wa kundi hili.
|
20231101.sw_1951_1
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ladysmith%20Black%20Mambazo
|
Ladysmith Black Mambazo
|
Ladysmith Black Mambazo lina albamu zaidi ya 40. Kundi hili lilipata umaarufu mkubwa liliposhirikiana na mwanamuziki wa Marekani Paul Simon kutoa albamu ya Graceland ambayo iliwashirikisha pia wanamuziki maarufu duniani kama Miriam Makeba na Hugh Masekela.
|
20231101.sw_1953_0
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mkoa%20wa%20Arusha
|
Mkoa wa Arusha
|
Mkoa wa Arusha ni mmojawapo kati ya mikoa 31 ya Tanzania wenye postikodi namba 23000, na ni wa pili kwa utajiri nchini.
|
20231101.sw_1953_1
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mkoa%20wa%20Arusha
|
Mkoa wa Arusha
|
Umepakana na Kenya upande wa kaskazini. Mikoa ya jirani, kufuatana na mwendo wa saa, ni: Kilimanjaro, Manyara, Shinyanga na Mara.
|
20231101.sw_1953_2
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mkoa%20wa%20Arusha
|
Mkoa wa Arusha
|
Kati ya milima yake Oldoinyo Lengai (m 2,878) ni volkeno hai bado, na mlima Meru ni volkeno iliyolala tangu mwaka 1910.
|
20231101.sw_1953_3
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mkoa%20wa%20Arusha
|
Mkoa wa Arusha
|
Mvua hunyesha kati ya milimita 1,800 kwa mwaka mlimani Arusha hadi mm 508 kwa mwaka katika maeneo makavu.
|
20231101.sw_1953_4
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mkoa%20wa%20Arusha
|
Mkoa wa Arusha
|
Mkoa wa Arusha ndio kitovu cha utalii Tanzania Bara. Kuna mbuga za taifa na hifadhi za wanyamapori Ngorongoro, Serengeti, Olduvai, Arusha, na Ziwa Manyara. Hifadhi ya Mlima Kilimanjaro na Hifadhi ya Tarangire ziko karibu.
|
20231101.sw_1953_5
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mkoa%20wa%20Arusha
|
Mkoa wa Arusha
|
Barabara ya lami Dar es Salaam-Nairobi inavuka eneo lake. Uwanja wa Kimataifa wa Ndege wa Kilimanjaro wahudumia miji ya Arusha na Moshi.
|
20231101.sw_1953_6
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mkoa%20wa%20Arusha
|
Mkoa wa Arusha
|
Fosfati inachimbuliwa Minjingu Mkoani Arusha, na takribani tani 48,000 kwa mwaka hutumiwa katika uzalishaji wa mbolea.
|
20231101.sw_1954_0
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Deutsche%20Welle
|
Deutsche Welle
|
Redio Deutsche Welle (DW), au Sauti ya Ujerumani ni kituo cha Shirikisho la Jamhuri ya Ujerumani kwa ajili ya matangazo ya nje.
|
20231101.sw_1954_1
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Deutsche%20Welle
|
Deutsche Welle
|
Kituo kimeanzishwa mw. 1953 kilitoa matangazo ya Kijerumani kwa ajili ya Wajerumani kote duniani kwa njia ya SW.
|
20231101.sw_1956_0
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kilomita%20ya%20mraba
|
Kilomita ya mraba
|
Msingi wake ni mita ya mraba (m²). Kilomita ya mraba hutumika kwa upimaji wa maeneo makubwa duniani kama mji, mkoa, nchi au dunia yote.
|
20231101.sw_1958_0
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Usawa%20bahari%20wastani
|
Usawa bahari wastani
|
Usawa wa wastani wa maji ya bahari hutumika kama kipimo cha kulinganisha kimo cha mahali duniani toka usawa wa bahari. Hali halisi usawa wa bahari hubadilika kati ya mahali na mahali na muda hadi muda. Kwa hiyo kuna kadirio la wastani wa vipimo hivyo inayotumika kuwa usawa bahari wastani.
|
20231101.sw_1959_0
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Alfu%20Lela%20U%20Lela
|
Alfu Lela U Lela
|
Kitabu cha Alfu Lela U Lela au Usiku Elfu na Moja (كتاب ألف ليلة وليلة kwa Kiarabu au هزار و یک شب kwa Kiajemi) ni mkusanyiko wa fasihi katika muundo wa visa kutoka Mashariki ya Kati.
|
20231101.sw_1959_1
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Alfu%20Lela%20U%20Lela
|
Alfu Lela U Lela
|
Visa hivi vinatokana na kitabu cha zamani cha Kiajemi kiitwacho Hazâr Afsâna (Visa vya Ngano Elfu Moja). Inaaminika kuwa mtu aliyekusanya visa hivi na kutafsiri kwa Kiarabu ni mtambaji hadithi maarufu Abu abd-Allah Muhammed el-Gahshigar katika karne ya 14. Tafsiri ya kwanza ya Kiarabu ya kisasa ilichapwa Cairo, Misri mwaka 1835.
|
20231101.sw_1959_2
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Alfu%20Lela%20U%20Lela
|
Alfu Lela U Lela
|
Inasadikika kuwa visa hivi vilianza kukusanywa wakati Baghdad ilipokuwa kitovu cha biashara na siasa Mashariki ya Kati. Wafanyabiashara toka Uajemi (Persia), China, India, Afrika, na Ulaya walikuwa wakitembelea Baghdad kwa ajili ya biashara.
|
20231101.sw_1959_3
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Alfu%20Lela%20U%20Lela
|
Alfu Lela U Lela
|
Mwanzo wa visa hivi ni kuudhiwa kwa mfalme Shahryar wa "kisiwa kilichoko kati ya India na China," na kitendo cha mke wake kuwa na mahusiano ya kimapenzi nje ya ndoa. Shahryar aliamua kumuua mke wake. Kwa kuamini kuwa wanawake wote wako kama mke wake aliyemuua (yaani sio waaminifu) anamwamuru mtumishi wake awe anampatia mke kila usiku. Baada ya kulala na mke wake mpya usiku, kunapokucha anaamuru mke huyo auawe.
|
20231101.sw_1959_4
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Alfu%20Lela%20U%20Lela
|
Alfu Lela U Lela
|
Hali hii inaendelea hadi pale binti wa huyo mtumishi wake anapounda mbinu maalum na kuamua kujitolea kuwa mke wa mfalme. Binti huyo jina lake ni Shahrazad (Scheherazade au Shahrastini katika vitabu vya Kiingereza). Kila usiku baada ya ndoa yao, binti huyo anatumia masaa na masaa kumsimulia mfalme visa vitamu na vya kusisimua ambapo utamu wake unakuwa umekolea inapofika alfajiri (ule wakati wa kuuawa kwa mke wa mfalme). Kwa nia ya kujua mwisho wa kisa, mfalme alikuwa akiahirisha mauaji ya Shahrazad. Aliendelea kuahirisha kuuawa kwa mke wake hadi akapata naye watoto watatu! Ulipofika wakati huo aliamini kuwa mke wake huyo ni mwaminifu hivyo akabadili uamuzi wa kuua wake zake.
|
20231101.sw_1959_5
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Alfu%20Lela%20U%20Lela
|
Alfu Lela U Lela
|
Visa vyenyewe ni mchanganyiko wa mapenzi, misiba, ucheshi, mashairi, na visa vya dini ya Kiislamu. Visa hivi vinajumuisha pia wanamazingaombwe na majini.Visa maarufu ni pamoja na Taa ya Alladin, Baharia Sindbad, Ali Baba na Wezi Arobaini. Kati ya majina mengi inayotajwa kuna pia majina ya Khalifa Harun ar-Rashid na mshairi Abu Nuwas. Inaaminika kuwa visa vya Alladin na Ali Baba viliingizwa katika mkusanyiko huo karne ya 18 na Antoine Galland ambaye alisikia visa hivyo toka kwa mtambaji hadithi wa Kimaroni tokea nchini Syria.
|
20231101.sw_1960_0
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Karne
|
Karne
|
Neno hili limetokana na Kiarabu "ﻗﺮﻥ" linamaanisha kipindi cha miaka mia moja. Kwa kawaida karne si miaka 100 yoyote inayofuatana lakini kipindi kati ya miaka kama vile 1901-2000 au 1801-1900.
|
20231101.sw_1960_1
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Karne
|
Karne
|
Karne inakwisha katika mwaka wenye "00" mwishoni yaani 1700, 1800, 1900, 2000. Sababu yake ni kwamba hakuna mwaka "0" ya kuanzisha hesabu, hivyo karne ya kwanza ya hesabu ilianza kwa mwaka 1. Hali hii huleta kila karne majadiliano kwa sababu watu wengi husikia karne mpya inaanza wakati tarakimu ya mbele waliyozoea muda mrefu inabadilika.
|
20231101.sw_1960_2
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Karne
|
Karne
|
Hivyo watu wengi walisheherekea karne mpya mwanzoni wa mwaka 2000 iliyokuwa mwaka wa mwisho wa karne ya 20, si mwaka wa kwanza wa karne ya 21. Ingawa maoni ya wataalamu hayakueleweka au hayakupokelewa, watu wengine walisema haidhuru.
|
20231101.sw_1961_0
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ubuntu
|
Ubuntu
|
Ubuntu ni falsafa ya Kiafrika inayosisitiza mahusiano na ushirikiano wa jamii kama msingi wa maisha bora na amani katika jamii.
|
20231101.sw_1961_1
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ubuntu
|
Ubuntu
|
Falsafa hii inaonesha nafasi ya mtu katika jamii iliyomzunguka. Ushirikiano ni njia bora ya kuishi kama jamii kuliko ubinafsi.
|
20231101.sw_1961_2
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ubuntu
|
Ubuntu
|
Neno Ubuntu limetoka kwenye lugha za Kizulu na Kixhosa za Afrika Kusini. Neno la Kihaya "Obuntu" au kwa Kiswahili "utu" linabeba, kwa kiasi fulani, maana ya neno Ubuntu.
|
20231101.sw_1961_3
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ubuntu
|
Ubuntu
|
Falsafa ya Ubuntu imetokana na mila na utamaduni wa Kiafrika ambao umejengwa juu ya maslahi ya jamii zaidi ya maslahi ya mtu binafsi.
|
20231101.sw_1961_4
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ubuntu
|
Ubuntu
|
Msingi wa falsafa hii ni, "mtu si mtu bila watu," kwa Kizulu, "Umuntu ngumuntu ngabantu." Kwa Kihaya "Omuntu ti muntu ka ataliho bantu" Baadhi ya watu wanaiona falsafa ya Ubuntu kuwa na maana nzito ya kiroho na ya kidini kwa kuwa imejengwa juu ya upendo wa watu wengine (kama unavyojipenda wewe) na hata mazingira.
|
20231101.sw_1962_0
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Malik%20Zulu%20Shabazz
|
Malik Zulu Shabazz
|
Malik Zulu Shabazz (amezaliwa mwaka wa 1968 kwa jina la Paris Lewis) ni mwanasheria nchini Marekani na kiongozi wa kundi la New Black Panther Party for Self Defence.
|
20231101.sw_1963_0
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/New%20Black%20Panther%20Party%20for%20Self%20Defence
|
New Black Panther Party for Self Defence
|
New Black Panther Party for Self-Defense ni kundi la wanaharakati weusi wenye siasa kali na mwamko wa kimapinduzi nchini Marekani. Kundi hili lilianzishwa mwaka 1989 na mtangazaji wa redio, Aaron Michaels, huko Dallas, Texas. Mwanzoni kundi hili lilichukua jina la "Black Panther Party" ambalo lilikuwa ni jina la kundi jingine lililokuwa na itikadi za kimapinduzi nchini Marekani. Wanachama wa kundi la mwanzo la Black Panther walipinga matumizi ya jina hilo yanayofanya na kundi jipya la Aaron Michaels. Michaels na wenzake walidai kuwa Black Panther haikuwa mali ya mtu binafsi bali jamii nzima ya watu weusi, hivyo hakuna ubaya jina hilo likatumika. Hata hivyo waliamua kuongeza neno "New" katika jina hilo.
|
20231101.sw_1963_1
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/New%20Black%20Panther%20Party%20for%20Self%20Defence
|
New Black Panther Party for Self Defence
|
Kundi hili linakua huku likifungua matawi sehemu mbalimbali nchini Marekani. Wafuasi wengi waliojitenga na kundi jingine la Nation of Islam walijiunga na kundi hili wakimfuata aliyekuwa kiongozi wa New Black Panther Party, marehemu Khalid Abdul Muhammad. Khalid Abdul Muhammad alikuwa ni mhubiri wa Nation of Islam kabla hajajiunga na New Black Panther Party.
|
20231101.sw_1963_2
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/New%20Black%20Panther%20Party%20for%20Self%20Defence
|
New Black Panther Party for Self Defence
|
Falsafa za kundi hili ni mchanganyiko wa mahubiri ya Malcolm X, Marcus Garvey, itikadi za uzalendo wa Kiafrika, na uanaharakati wa kimapinduzi.
|
20231101.sw_1968_0
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Bendera%20ya%20Tanzania
|
Bendera ya Tanzania
|
Bendera ya Tanzania ni ya mstatili unaokatwa pembe kwa pembe na kanda nyeusi yenye milia za njano kandokando.
|
20231101.sw_1968_1
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Bendera%20ya%20Tanzania
|
Bendera ya Tanzania
|
Matumizi ya bendera inahifadhiwa chini ya sheria ya "The National Flag and Coat of Arms Act, 15-1971".
|
20231101.sw_1968_2
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Bendera%20ya%20Tanzania
|
Bendera ya Tanzania
|
Bendera hii imepatikana tangu 30 Juni 1964 kutokana na muungano wa Tanganyika na Zanzibar. Bendera ya Tanganyika ilikuwa na rangi ya kijani ikiwa na kanda nyeusi katikati yenye milia za njano kando. Buluu imepatikana kutokana na bendera ya Zanzibar ya mwaka 1964 ikimaanisha bahari. Hata hivyo toka mwaka 2005, Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ilianza kutumia rasmi bendera ya Zanzibar. Hii ni mara ya kwanza toka kuungana kwa Tanganyika na Zanzibar kwa funguvisiwa la Zanzibar kuwa na bendera yake lenyewe.
|
20231101.sw_1968_3
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Bendera%20ya%20Tanzania
|
Bendera ya Tanzania
|
Kijani kwa ajili ya mashamba, kilimo na misitu. Kijani ni pia rangi ya bendera ya chama cha TANU kilichokuwa chama tawala tangu uhuru.
|
20231101.sw_1968_4
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Bendera%20ya%20Tanzania
|
Bendera ya Tanzania
|
Njano inakumbusha juu ya utajiri wa madini. Njano ya namna hiyo inaelezwa mara nyingine kuwa ni dhahabu , lakini maelezo rasmi mengine kwa Kiingereza yanataja rangi kuwa "Yellow Pantone 116c"
|
20231101.sw_1970_0
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Jakaya%20Kikwete
|
Jakaya Kikwete
|
Jakaya Mrisho Kikwete alikuwa rais wa nne wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tangu tarehe 21 Desemba 2005 hadi tarehe 5 Novemba 2015.
|
20231101.sw_1970_1
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Jakaya%20Kikwete
|
Jakaya Kikwete
|
Amezaliwa 7 Oktoba 1950 katika kijiji cha Msoga, kata ya Lugoba, tarafa ya Msoga, jimbo la uchaguzi la Chalinze, Wilaya ya Bagamoyo, mkoa wa Pwani.
|
20231101.sw_1970_2
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Jakaya%20Kikwete
|
Jakaya Kikwete
|
Alizaliwa katika familia ya wanasiasa. Babu yake Mzee Mrisho Kikwete alikuwa chifu wa Wakwere. Baba yake alikuwa Mkuu wa Wilaya Pangani, Same na Tanga.
|
20231101.sw_1970_3
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Jakaya%20Kikwete
|
Jakaya Kikwete
|
Jakaya Kikwete amesimulia hadithi ya kifamilia ya kuwa wakati mama yake alipokuwa mja mzito naye, babu alitamka kuwa ikiwa mtoto atakuwa wa kiume atampatia urithi wa cheo chake.
|
20231101.sw_1970_4
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Jakaya%20Kikwete
|
Jakaya Kikwete
|
Miaka 1958 – 1961 akasoma Shule ya Msingi Msoga, halafu 1962 – 1965 Shule ya Kati (Middle School) Lusonga, halafu Shule ya Sekondari Kibaha akiongeza A-level huko Shule ya Sekondari Tanga.
|
20231101.sw_1970_5
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Jakaya%20Kikwete
|
Jakaya Kikwete
|
Kuanzia mwaka 1972 alisoma uchumi katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam akimaliza kwa kupata digrii yake mwaka 1978.
|
20231101.sw_1970_6
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Jakaya%20Kikwete
|
Jakaya Kikwete
|
Jakaya aliposoma Shule ya Sekondari ya Kibaha alikuwa mwenyekiti wa wanafunzi na pia wa Vijana wa TANU. Katika Shule ya Sekondari Tanga alikuwa Kiranja Mkuu na pia kiongozi wa timu ya mpira. Katika UDS alichaguliwa kuwa mwenyekiti wa halmashauri ya wanafunzi.
|
20231101.sw_1970_7
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Jakaya%20Kikwete
|
Jakaya Kikwete
|
1mwaka huu alikuwa mkulima wa Msoga. Mwaka 1988 akateuliwa kuwa mbunge na waziri msaidizi. Mwaka 1990 alichaguliwa kuwa mbunge wa Bagamoyo/Chalinze akirudishwa kila uchaguzi hadi mwaka 2000. Akawa waziri akipita katika wizara za maji na fedha.
|
Subsets and Splits
No community queries yet
The top public SQL queries from the community will appear here once available.