_id
stringlengths 15
22
| url
stringlengths 31
150
| title
stringlengths 1
86
| text
stringlengths 100
23.8k
|
---|---|---|---|
20231101.sw_1970_8
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Jakaya%20Kikwete
|
Jakaya Kikwete
|
Mwaka 1995 alijaribu kuchaguliwa kuwa mgombea wa urais upande wa CCM. Inasemekana ya kwamba Mwalimu Julius Nyerere alimwomba wakati ule kumwachia nafasi Benjamin Mkapa aliyeteuliwa na Halmashauri Kuu ya CCM. Kikwete akawa Waziri wa Mambo ya Nje katika serikali zote mbili za Mkapa.
|
20231101.sw_1970_9
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Jakaya%20Kikwete
|
Jakaya Kikwete
|
Mwaka 2005 alifaulu kuteuliwa mgombea wa CCM kwa nafasi ya rais akashinda uchaguzi wa Desemba 2005 akizoa 80% za kura zote.
|
20231101.sw_1970_10
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Jakaya%20Kikwete
|
Jakaya Kikwete
|
Katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 alitangazwa tena mshindi ingawa kwa asilimia ndogo zaidi na kwa wasiwasi kuhusu uwezekano wa matokeo kuchakachuliwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi aliyoiteua mwenyewe. Katiba ya nchi hairuhusu kukata rufaa dhidi ya tangazo la tume hiyo.
|
20231101.sw_1970_11
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Jakaya%20Kikwete
|
Jakaya Kikwete
|
Kuapishwa kwa mara ya kwanza kwa Jakaya Kikwete kama Rais wa 4 wa Tanzania kulifanyika Jumatano, tarehe 21 Desemba 2005. Ilikuwa ni mwanzo wa muhula wa kwanza wa miaka mitano wa Jakaya Kikwete kama Rais na Ali Mohamed Shein kama Makamu wa Rais.
|
20231101.sw_1970_12
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Jakaya%20Kikwete
|
Jakaya Kikwete
|
Katika miaka mitano iliyofuata, rais aliendelea kusafiri sana nje ya nchi, kiasi kwamba alikaa ughaibuni siku nyingi kuliko zile alizokaa nchini Tanzania.
|
20231101.sw_1970_13
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Jakaya%20Kikwete
|
Jakaya Kikwete
|
Hali ya mwisho ya nchi ilifananishwa na mwandamizi wake John Magufuli kuwa kama "shamba la bibi", ambamo kila mtu anaweza kuchuma anavyotaka. Pia rais mpya alilalamika kwa kukuta hazina haina fedha, mbali na madeni ya kimataifa kufikia kiasi cha karibu Shilingi za Tanzania milioni 1 kwa kila mwananchi.
|
20231101.sw_1985_0
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Jens%20Fink-Jensen
|
Jens Fink-Jensen
|
Jens Fink-Jensen (alizaliwa Copenhagen, Denmark, 19 Desemba 1956) ni mwandishi katika lugha ya Kidenishi katika nyanja mbalimbali kama vile semi za kawaida na mashairi. Vile vile yeye ni mpigapicha na mwandishi wa vitabu hasa vya muziki na nyimbo.
|
20231101.sw_1985_1
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Jens%20Fink-Jensen
|
Jens Fink-Jensen
|
Alianza maisha yake kama mwandishi wa vitabu vya hadithi 4 Juni 1975 wakati alipoandika hadithi fupi ijulikanayo kama Juni 1995. Kitabu hicho kilichapishwa kwenye gazeti la kila siku kwa lugha ya Kidenish lijulikanalo kama "Nipashe Habari'". Hatimaye kwenye mwezi wa Mei katika mwaka wa Elfu Moja na Mia Tisa na Sabini na Sita, akawa mwandishi wa mashairi kwanza kwa kuandika tunzi nne za mashairi zilizo chapishwa kwenye jarida nambari sabini na sita mkwaju moja, na ambalo hujulikana kama “Mbegu ya Ngano” (Hvedekorn).
|
20231101.sw_1985_2
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Jens%20Fink-Jensen
|
Jens Fink-Jensen
|
Tunzi zake za mwanzo kwenye nyanja ya mashairi zilichapishwa kwa mara ya kwanza kunako Mwaka wa Elfu Moja Mia Nane na Dhemaanini na Moja na zikajulikana kwa kupewa kicwa cha maneno Dunia Kwenye Jicho. Alianza kukusanya mashairi yalio kua yameandikwa na washairi wengine na kuyaweka katika hali ya vitabu kwenye mwaka wa Elfu Moja Mia Tisa na Dhemanini na Sita. Vitabu vyenyewe vilichapishwa vikiwa katika hali ya mkusanyiko wa hadidhi fupi-fupi na vikatambulika kwa jina la Wanyama mwitu. Hatimae kunako mwaka wa Elfu Moja Mia Tisa na Tisini na Nne, akaanza kuandika vitabu kwa watoto, baadhi yavyo kikiwa ni kile kiitwacho Jonas na Konokono.
|
20231101.sw_1985_3
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Jens%20Fink-Jensen
|
Jens Fink-Jensen
|
Alihitimu masomo yake kwenye shule ya upili kidato cha sita na kupita vizuri katika masomo ya lugha mbali-mbale akiwa katika shule ya bweni ya Herlufsholm kunako mwaka wa Elfu Moja mia Tisa na Sabini na Sita. Baadae alifanya mafunzo ya kijeshi na kuhitimu kwa kutunukiwa cheo cha Kamanda kwenye kikosi kiitwacho Walinzi Hai wa Kifalme (Royal Life Guards). Hatimae kwenye mwaka wa Elfu-moja na Mia Tisa na Dhemaanini na Sita, akajiunga na chuo kitoacho masomo kwenye fani ya ujenzi kilichoko mjini Conpenhagen amboko alitunukiwa shahada ya Mastas katika uchoraji na ujenzi. Katika mwaka wa Elfu moja Mia Tisa na Tisini na Saba, akiwa bado angali kwenye chuo hicho-hicho, aliyaendeleza masomo yake kwa kushiriki kwenye masomo ya ukusanyaji na utoaji wa habari katika misingi inayo husisha matumizu ya mbinu mbali-mbali.
|
20231101.sw_1985_4
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Jens%20Fink-Jensen
|
Jens Fink-Jensen
|
Na akiwa kama mojawapo wa waandishi wakongwe walio vuma katika miaka ya Dhemaanini na ambao walipenda kua na uhusiano wa karibu sana na bwana Poul Borum, (mhariri wa Hvedekorn), yeye pamoja na wenzake wengine kama vile Michael Strunge, walichangia katika kubuni onyesho la kusisimua ambalo lilijulikana kama “Kizazi Kipya” na ambalo liliandaliwa katika ukumbi wa Huset ulioko mjini Copenhagen. Hii ilikua ni kwenye mwaka wa Elfu Moja mia Tisa na Dhemaanini.
|
20231101.sw_1985_5
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Jens%20Fink-Jensen
|
Jens Fink-Jensen
|
Vile-vile, alijishirikisha kwenye maonyesho ya tunzi mbali-mbali na alishikilia nafasi maalum ya kusoma mashairi yenye kuelezea hali ya furaha na huzuni, huku akionyesha picha zinazo onyeshwa kwenye kuta kwa kutumia miale ya mwangaza. Mengine alio jihusisha nayo yalikua ni Kuleta hali ya uuwiyano katika tunzi mbali-mbali zilizo tungwa na shule mbali-mbali za upili, na kwenye sherehe zingine mbali-mbali zilizo wahi kufanyika wakati huo; Hii ikiwa ni baadhi ya matukio mengine alio jihusisha nayo. Wengine walio shiriki nae ni mwana mziki Fredrik Mellqvist ambae ana uhodari wa kucheza chombo kiitwacho Keyboard. Wengine alio shiriki nao ni pamoja na yule mchezaji wa chombo kiitwacho Saksafoni aitwae Jens Severin.
|
20231101.sw_1985_6
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Jens%20Fink-Jensen
|
Jens Fink-Jensen
|
Mwana sanaa huyu Jens Fink-Jensen amewahi vile-vile kuandaa maonyesho ya picha, kwamfano yale yaliyo julikana kama “Meli za Kusini” pamoja na Uso wa Beijing. Mengine yalikua ni pamoja na maonyesho yalio julikana kama Picha za Neno ambazo ziliandamana na picha ambazo huonyeshwa kwa kutumia miyale ya mwangaza na ambazo hushirikisha sauti. Mfano ukiwa ni ile ijulikanayo kama Jicho limulikalo Ulimwengu likiwa ni onyesho lililokua linasimulia kuhusu malighafi inayo tumika ndani ya vitabu.
|
20231101.sw_1985_7
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Jens%20Fink-Jensen
|
Jens Fink-Jensen
|
1994 Vitabu kwa Watoto Jonas og konkylien (Jonas na konokono) (ambamo picha za tafsiri zimechorwa na msanii Mads Stage)
|
20231101.sw_1985_8
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Jens%20Fink-Jensen
|
Jens Fink-Jensen
|
1998 Kitabu Kwa Watoto Jonas og himmelteltet (Jonas na hema ipepeayo kwenye mawingu) (ambamo picha za tafsiri zimechorwa na msanii Mads Stage)
|
20231101.sw_1989_0
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Krismasi
|
Krismasi
|
Krismasi (pia Noeli) ni sikukuu ambayo Wakristo wengi husheherekea kuzaliwa kwake Yesu Kristo zaidi ya miaka 2000 iliyopita.
|
20231101.sw_1989_1
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Krismasi
|
Krismasi
|
Kwa kawaida husheherekewa tarehe 25 Desemba katika Ukristo wa magharibi na tarehe 6 Januari katika ule wa mashariki.
|
20231101.sw_1989_2
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Krismasi
|
Krismasi
|
Krismasi kutokana na neno la Kiingereza lenye maana ya "Christ`s Mass" yaani misa au ibada ya Kristo.
|
20231101.sw_1989_3
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Krismasi
|
Krismasi
|
Noeli kutokana na neno la Kiingereza "Noel" (au "Nowell") ambalo limepokewa kutoka lugha ya Kifaransa "Noël". Hilo ni ufupisho wa neno la Kilatini "Natalis (dies)", "(siku ya) kuzaliwa".
|
20231101.sw_1989_4
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Krismasi
|
Krismasi
|
Hakuna uhakika kamili ni lini Krismasi ilianza kusheherekewa. Ni sikukuu ya kale katika Ukristo lakini haikuwepo tangu mwanzoni. Tarehe halisi ya kuzaliwa kwake Yesu haijulikani kwa sababu utamaduni wa Wayahudi wa wakati ule haukuwa na sherehe au kumbukumbu ya siku ya kuzaliwa.
|
20231101.sw_1989_5
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Krismasi
|
Krismasi
|
Lakini baadaye Ukristo ulienea katika Dola la Roma kati ya mataifa yaliyokuwa na kawaida ya kuzingatia siku ya kuzaliwa. Hivyo ilijitokeza hamu ya kusheherekea pia sikukuu ya kuzaliwa kwake Kristo. Ndiyo asili ya sikukuu ya Krismasi.
|
20231101.sw_1989_6
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Krismasi
|
Krismasi
|
Tangu mwanzo wa karne ya 3 BK kuna kumbukumbu ya waandishi mbalimbali waliojadili tarehe ya kuzaliwa kwake Yesu Kristo.
|
20231101.sw_1989_7
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Krismasi
|
Krismasi
|
Habari za kwanza kabisa za makadirio ya tarehe ya kuzaliwa kwake Yesu zinapatikana kutoka Misri mnamo mwaka 200 BK. Mwandishi Mkristo Klemens wa Alexandria alilalamikia udadisi wa wataalamu kadhaa wa Misri waliodai kwamba wamekadiria tarehe hiyo katika mwezi Mei, wengine katika Aprili. Alisema pia kuwa kikundi cha Kikristo cha wafuasi wa Basilides huko Misri walisheherekea Epifania pamoja na kuzaliwa kwake Yesu tarehe 6 Januari.
|
20231101.sw_1989_8
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Krismasi
|
Krismasi
|
Lakini kadirio la tarehe 25 Desemba lina asili katika Misri pia. Kuanzia mwaka 200 (kwa mara ya kwanza katika maandishi ya Sixtus Julius Africanus) wataalamu nchini Misri waliona tarehe 14 Nisan ya kalenda ya Kiyahudi ambayo ni sawa na 25 Machi ilikuwa tarehe ya kufa kwake Kristo na pia siku ya utungaji mimba wake. Kwa kuongeza miezi tisa ya mimba inajitokeza 25 Desemba kama tarehe ya kuzaliwa.
|
20231101.sw_1989_9
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Krismasi
|
Krismasi
|
Inaonekana tarehe 25 Desemba ilijitokeza wakati huo. Kuna taarifa ya mwaka 204 kutoka Ipolito wa Roma kwamba tarehe 25 Desemba ilikuwa sikukuu ya kuzaliwa kwake Yesu Kristo.
|
20231101.sw_1989_10
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Krismasi
|
Krismasi
|
Mjini Roma wakati wa karne ya 4 tarehe ya Krismasi katika Desemba ilitokea pamoja na sikukuu ya Kipagani iliyoitwa "Siku ya Sol Invictus". Hii ilikuwa sherehe ya Jua kama mungu "Sol invictus" (yaani "Jua lisiloshindika"). Hii ilikuwa ibada iliyoingia Roma kutoka Uajemi ambako mungu Mithra aliabudiwa kama mungu wa nuru.
|
20231101.sw_1989_11
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Krismasi
|
Krismasi
|
Waumini wa dini ya Jua waliona wakati wa Desemba kama kipindi cha pekee kutokana na solistasi ya mwezi huo; katika nusutufe ya kaskazini ya Dunia urefu wa mchana unapungua na usiku unakuwa mrefu tangu sikusare ya 21/22 Septemba hadi tarehe 21/22 Desemba; kuanzia siku za 21/22 Desemba mchana huwa mrefu na nuru inaongezeka. Mwendo huo ulitazamwa kama ushindi wa nuru = Jua juu ya giza.
|
20231101.sw_1989_12
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Krismasi
|
Krismasi
|
Pale Roma Kaisari Eliogabalus (aliyezaliwa Syria, alitawala Roma 218 hadi 222) alianzisha sherehe ya sikukuu ya "Kuzaliwa Jua" huko Roma. Baadaye Kaisari Aurelianus akaithibitisha rasmi mwaka 273.
|
20231101.sw_1989_13
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Krismasi
|
Krismasi
|
Wakati wa Kaisari Licinius (308-324) sikukuu hiyo ilikuwa ikiadhimishwa bado tarehe 19 Desemba. . Hatimaye ikahamishiwa tarehe 25 Desemba.
|
20231101.sw_1989_14
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Krismasi
|
Krismasi
|
Wataalamu mbalimbali walidai kwamba Kanisa lilipachika sikukuu ya Kristo kwenye tarehe hiyo kwa nia ya kufanya ichukue nafasi ya sikukuu ya jua kama mungu "Sol invictus" (yaani "Jua lisiloshindika"). Kwa namna yoyote hata katika Ukristo Jua linatazamwa kama ishara ya Kristo; katika sehemu mbalimbali za Biblia Kristo alifananishwa tayari na Jua na maneno haya yaliandikwa muda mrefu kabla ya kutokea kwa siku ya Sol Invictus. Mifano ni Injili ya Luka 1,78 Ufunuo 21, 23 , Malaki 4,2 (, hivyo katika mashindano na dini ya kuabudu Jua Wakristo walitumia lugha ya Biblia kwa kudokeza Kristo ndiye Jua la kweli.
|
20231101.sw_1989_15
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Krismasi
|
Krismasi
|
Wakristo wengi husheherekea tarehe 25 Desemba (Wakatoliki na sehemu ya Waprotestanti na Waorthodoksi). Kati ya Waorthodoksi kuna tarehe nyingine, hasa 6 Januari kutokana na tofauti katika kalenda.
|
20231101.sw_1989_16
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Krismasi
|
Krismasi
|
Habari za Krismasi kama sherehe hazipatikani katika Biblia kwa sababu zilizotajwa hapa juu na kwa sababu mwanzoni mwa Kanisa mkazo ulikuwa juu ya kifo na ufufuko wa Yesu, tunavyoona hasa katika barua za Mtume Paulo.
|
20231101.sw_1989_17
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Krismasi
|
Krismasi
|
Hasa vitabu viwili vya Agano Jipya vina habari za kuzaliwa kwake Yesu, yaani Injili za Mathayo na Luka.
|
20231101.sw_1989_18
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Krismasi
|
Krismasi
|
Bikira Maria, Mama wa Yesu, alipata mimba wakati alipokuwa mchumba wa Yosefu. Yosefu alitaka kumwacha lakini aliambiwa na malaika aanze kuishi naye na kumkubali mtoto kama wake kwa kumpa jina "Yesu".
|
20231101.sw_1989_19
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Krismasi
|
Krismasi
|
Mamajusi kutoka mashariki waliwatembelea kijijini Bethlehemu na kuwaletea zawadi kwa sababu waliona nyota ya pekee iliyokuwa kwao alama ya kuzaliwa kwa mfalme mpya katika Uyahudi ikawaongoza hadi mjini Yerusalemu. Lakini walipompitia mfalme Herode Mkuu, huyo alikasirika akimwogopa mfalme mpya. Hata hivyo aliwaelekeza Bethlehemu kadiri ya utabiri wa nabii Mika.
|
20231101.sw_1989_20
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Krismasi
|
Krismasi
|
Yosefu alipata tena ujumbe kutoka kwa malaika akaondoka na mtoto na Maria kukimbilia Misri kabla ya askari wa Herode hawajaweza kumuua Yesu.
|
20231101.sw_1989_21
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Krismasi
|
Krismasi
|
Baada ya kifo cha Herode walirudi kutoka Misri lakini hawakuenda tena Bethlehemu bali walihamia Nazareti katika mkoa wa Galilaya.
|
20231101.sw_1989_22
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Krismasi
|
Krismasi
|
Katika taarifa ya Luka (mlango wa 1 na 2) Maria alipokea huko Nazareti ujumbe wa malaika mkuu Gabrieli kwamba atapata mimba halafu mtoto wa pekee.
|
20231101.sw_1989_23
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Krismasi
|
Krismasi
|
Yosefu na Maria walikwenda Bethlehemu kwa sababu ya sensa iliyowataka kwenda katika mji asili wa ukoo wa Yosefu, mjukuu wa mfalme Daudi. Hapo Yesu alizaliwa katika hori la kulishia wanyama; wachungaji mabondeni walitangaziwa na malaika habari hiyo wakaja kumwona mtoto.
|
20231101.sw_1989_24
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Krismasi
|
Krismasi
|
Baada ya kuzaliwa wazazi walimpeleka Yesu Yerusalemu katika hekalu kufuatana na sheria ya Agano la Kale (Kitabu cha Kutoka 13,2; 13,15) halafu wakarudi kwao Nazareti.
|
20231101.sw_1989_25
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Krismasi
|
Krismasi
|
Sura ya tatu (Al Imran, 42-47) ina habari za tangazo la malaika kwa Bikira Mariamu zinazofanana na Luka 1.
|
20231101.sw_1989_26
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Krismasi
|
Krismasi
|
Sura ya 19 (Mariamu, 16-34) inarudia tangazo la malaika kwa Mariamu na inasimulia kuzaliwa kwake Yesu chini ya mti wa mtende, halafu majadiliano kati ya Mariamu na ndugu zake. Mtoto mchanga Yesu akaanza kusema wakati wa kuzaliwa akimtetea mama yake dhidi ya ndugu zake.
|
20231101.sw_1989_27
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Krismasi
|
Krismasi
|
Kipindi cha Noeli kinatimiza haja hiyo, kwa kuwa kinaadhimisha kuzaliwa kwa mtu mpya kabisa ambaye anatuvutia kwa wema wake na ambaye tukimuona tumemuona Mungu, tena tukimpokea tunazaliwa upya kama wana wa Mungu.
|
20231101.sw_1989_28
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Krismasi
|
Krismasi
|
“Leo amezaliwa kwa ajili yenu Mwokozi, ndiye Kristo Bwana”. Tunapoadhimisha Noeli tangazo hilo la malaika kwa wachungaji linatufikia sisi. Si kujidanganya, kana kwamba Yesu angezaliwa leo, wala hatukumbuki tu tukio la zamani, bali fumbo la kuzaliwa Bwana linatufikia leo katika liturujia na kutuletea neema zake. Hivyo tunaweza tukazaliwa upya kwa kushiriki kuzaliwa kwa kichwa chetu.
|
20231101.sw_1989_29
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Krismasi
|
Krismasi
|
Liturujia inashangilia hivi, “Lo! Mabadilishano ya ajabu! Mwana wa Mungu anakuwa mtu kusudi mtu awe mwana wa Mungu!”. Tena si binadamu tu, bali viumbe vyote vinapata heshima mpya kwa Neno wa milele kujifanya kiumbe.
|
20231101.sw_1989_30
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Krismasi
|
Krismasi
|
Sherehe ya Krismasi imekuwa sikukuu muhimu sana katika tamaduni za mataifa yaliyoathiriwa na Ukristo. Kuna desturi nyingi zilizojitokeza katika karne zote za kusheherekea Krismasi. Sehemu ya desturi hizi zimeenea pia nje ya nchi za asili na hata kutumiwa na watu wasiofuata imani ya Kikristo.
|
20231101.sw_1989_31
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Krismasi
|
Krismasi
|
Pango la Noeli lililoanzishwa na Fransisko wa Asizi mwaka 1223 kijijini Greccio (Italia ya Kati) na kuenea kila mahali kama sanaa inayoonyesha kwa njia mbalimbali jinsi Yesu alivyozaliwa.
|
20231101.sw_1989_32
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Krismasi
|
Krismasi
|
Mapambo ya Krismasi: ni hasa nuru na taa za pekee. Alama za nyota kwa kukumbuka nyota iliyopeleka mamajusi hadi Bethlehemu inawekwa ndani na nje ya nyumba na maduka.
|
20231101.sw_1989_33
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Krismasi
|
Krismasi
|
Mti wa Krismasi - ni ishara ya pekee ya Krismasi yenye asili katika Ujerumani kusini-magharibi ya karne ya 16 hivi. Asili yake iko katika maigizo yaliyosimulia hadithi za Biblia na mti wa Paradiso unaohusiana na masimulizi ya dhambi la kwanza na ujumbe wa Kristo kama mwokozi anayekuja kuondoa dhambi hilo. Kutoka maigizo ya kanisani ishara ya mti uliopambwa matunda uliingia katika nyumba za Wakristo ambako ulipambwa zaidi kwa matunda, keki tamu na pipi kwa watoto. Umekuwa mapambo ya nyumbani kwa majira ya Krismasi. Tangu Krismasi kuwa nafasi muhimu kwa uchumi kuna pia maduka mengi yanayoweka miti hii na katika mazingira ya kibiashara uhusiano wake na mti wa Paradiso umesahauliwa mara nyingi.
|
20231101.sw_1989_34
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Krismasi
|
Krismasi
|
Zawadi za Krismasi - Martin Luther alitaka kuongeza umuhimu wa Krismasi kwa Wakristo ambao wakati wake walikuwa na desturi ya kuwazawadia watoto kwenye siku ya Mtakatifu Nikolasi tarehe 6 Desemba, wiki 2 kabla ya sikukuu. Hapo Luther alipendekeza kuhamisha zawadi kwa watoto kwenda siku ya kuzaliwa kwake Yesu ili wamkumbuke zaidi Yesu kuliko mtakatifu huyo. Hapo alirejea zawadi zilizopelekwa kwa Yesu na mamajusi kutoka mashariki kufuatana na taarifa ya Injili ya Mathayo mlango 2. Desturi ya kuwazawadia watoto kwenye sikukuu hii ilienea hadi kuwa desturi ya kupeana zawadi kati ya watu wa kila umri. Katika karne ya 20 desturi ilienea kiasi cha kuwa nafasi muhimu ya biashara. Katika nchi nyingi mwezi Desemba umekuwa mwezi wa mapato makubwa kushinda miezi mingine. Hata katika miji mikubwa ya nchi kama Dubai au Japani ambako Wakristo ni wachache desturi ya kupeana zawadi imeenea na mapambo ya Krismasi katika maduka yanataka kuwahamasisha wateja kununua zawadi za majira.
|
20231101.sw_1989_35
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Krismasi
|
Krismasi
|
The Battle for Christmas, by Stephen Nissenbaum (1996; New York: Vintage Books, 1997). ISBN 0-679-74038-4
|
20231101.sw_1989_36
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Krismasi
|
Krismasi
|
Christmas Customs and Traditions, by Clement A. Miles (1976: Dover Publications) ISBN 978-0-486-23354-3
|
20231101.sw_1989_37
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Krismasi
|
Krismasi
|
The World Encyclopedia of Christmas, by Gerry Bowler (October 2004: McClelland & Stewart) ISBN 978-0-7710-1535-9
|
20231101.sw_1989_38
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Krismasi
|
Krismasi
|
Santa Claus: A Biography, by Gerry Bowler (November 2007: McClelland & Stewart) ISBN 978-0-7710-1668-4
|
20231101.sw_1989_39
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Krismasi
|
Krismasi
|
There Really Is a Santa Claus: The History of St. Nicholas & Christmas Holiday Traditions, by William J. Federer (December 2002: Amerisearch) ISBN 978-0-9653557-4-2
|
20231101.sw_1989_40
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Krismasi
|
Krismasi
|
St. Nicholas: A Closer Look at Christmas, by Jim Rosenthal (July 2006: Nelson Reference) ISBN 1-4185-0407-6
|
20231101.sw_1989_41
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Krismasi
|
Krismasi
|
Just say Noel: A History of Christmas from the Nativity to the Nineties, by David Comfort (November 1995: Fireside) ISBN 978-0-684-80057-8
|
20231101.sw_1989_42
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Krismasi
|
Krismasi
|
4000 Years of Christmas: A Gift from the Ages, by Earl W. Count (November 1997: Ulysses Press) ISBN 978-1-56975-087-2
|
20231101.sw_1991_0
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mto%20Kagera
|
Mto Kagera
|
Mto Kagera (kwa Kinyarwanda: Akagera) ni kati ya mito inayounda mto Nile, pia ni mto mkubwa kabisa wa kuingia ziwa la Viktoria Nyanza.
|
20231101.sw_1991_1
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mto%20Kagera
|
Mto Kagera
|
Unaanzia Burundi inapounganika mito ya Nyawarongo na Ruvuvu ikiendela km 400 hadi kuingia ziwa Viktoria.
|
20231101.sw_1991_2
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mto%20Kagera
|
Mto Kagera
|
Mto Kagera ukielekea kaskazini ni mpaka kati ya Tanzania na Rwanda; pale unapogeuka kuelekea mashariki karibu na mji wa Kikagati ni mpaka kati ya Tanzania na Uganda. Sehemu ya mwisho ya njia yake inaingia kabisa ndani ya eneo la Tanzania hadi kufika Viktoria Nyanza km kama 40 kaskazini kwa Bukoba.
|
20231101.sw_1991_3
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mto%20Kagera
|
Mto Kagera
|
Jina la mto wa Kagera umekuwa pia jina la mbuga ya wanyama ya Akagera National Park huko Rwanda na pia la Mkoa wa Kagera katika Tanzania.
|
20231101.sw_1992_0
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mkoa%20wa%20Kagera
|
Mkoa wa Kagera
|
Mkoa wa Kagera kati ya mikoa 31 ya Tanzania ndio mkoa wa kaskazini-magharibi kabisa wenye postikodi namba 35000. Jina lake linatokana na mto Kagera.
|
20231101.sw_1992_1
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mkoa%20wa%20Kagera
|
Mkoa wa Kagera
|
Mkoa wa Kagera umepakana na Burundi, Rwanda na Uganda upande wa Magharibi na Kaskazini. Upande wa Kusini umepakana na mikoa mingine ya Tanzania ya Kigoma, Shinyanga na Geita.
|
20231101.sw_1992_2
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mkoa%20wa%20Kagera
|
Mkoa wa Kagera
|
Eneo lake ni km² 28,953 za nchi kavu na km² 11,885 za maji ya ndani, hasa ya Viktoria Nyanza, jumla km² 40,838.
|
20231101.sw_1992_3
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mkoa%20wa%20Kagera
|
Mkoa wa Kagera
|
Kiutawala eneo la mkoa limegawiwa kwa wilaya saba: Bukoba, Misenyi, Muleba, Karagwe, Ngara, Biharamulo na Kyerwa pamoja na eneo la manisipaa ya Bukoba. Misenyi ni wilaya mpya iliyoanzishwa mwaka 2007 na Kyerwa ikafuata mwaka 2012.
|
20231101.sw_1992_4
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mkoa%20wa%20Kagera
|
Mkoa wa Kagera
|
Mkoa huu una makabila makubwa manne ambayo ni: Wanyambo, Wahangaza, Wahaya na Wasubi. Wanyambo huishi kwa wingi katika wilaya za Kyerwa na Karagwe, Wahangaza huishi kwa wingi katika wilaya ya Ngara, Wahaya huishi kwa wingi katika wilaya za Bukoba, Muleba na Misenyi na Wasubi huishi kwa wingi katika wilaya ya Biharamuro. Makabila ya Wanyambo na Wahaya hupenda kula ndizi kwa wingi na asilimia kubwa wanafuata mila na desturi za mababu: Zamani Wanyambo na Wahaya walikuwa hawawezi kuoana na hiyo bado sasa ipo kwa kiasi kidogo.
|
20231101.sw_1992_5
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mkoa%20wa%20Kagera
|
Mkoa wa Kagera
|
Pia mkoa huu una wakimbizi wengi, kwa asilimia kubwa wanatokea nchi za Rwanda na Burundi wakipitia wilaya ya Ngara.
|
20231101.sw_1992_6
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mkoa%20wa%20Kagera
|
Mkoa wa Kagera
|
Hali ya hewa ni nzuri kwa kuishi, kilimo, uvuvi. Mkoa huo ni maarufu kwa ulimaji wa kahawa, ndizi, miwa na chai.
|
20231101.sw_1992_7
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mkoa%20wa%20Kagera
|
Mkoa wa Kagera
|
Mkoa huu unapatikana ukanda wa ziwa Viktoria. Katika mkoa huu kuna mambo mengi ambayo yalitetemesha nchi ya Tanzania. Mambo hayo ni pamoja na vita ya Uganda na Tanzania, vita ambavyo vilihusishwa na mkoa huu; ilikuwa mwaka 1978.
|
20231101.sw_1992_8
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mkoa%20wa%20Kagera
|
Mkoa wa Kagera
|
Ndipo Idd Amin Dada aliyekuwa Rais wa Uganda alipoliamru jeshi lake kuvamia mkoa wa Kagera. Walianza kuvamia wilaya ya Missenyi. Hapo Julius K. Nyerere aliyekuwa rais wa Tanzania aliamuru jeshi lake kufukuza wavamizi hadi kuvamia nchi ya Uganda.
|
20231101.sw_1992_9
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mkoa%20wa%20Kagera
|
Mkoa wa Kagera
|
Agizo hilo lilikuwa zuri lakini vijana wa mkoa wa Kagera walipata shida kwa sababu walilazimishwa kufuzwa Uanamgambo mara moja na kupelekwa vitani. Walipoanza tu vita hivyo raia wa Uganda walishirikiana na jeshi la Tanzania kufichua maficho ya jeshi la Uganda. Jeshi la Tanzania liliwapiga na kuwapora mali zao, vifaa vya kivita na kuwateka wanajeshi wao.
|
20231101.sw_1992_10
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mkoa%20wa%20Kagera
|
Mkoa wa Kagera
|
Mwanzoni mwa mwaka wa 1979 Idd Amin Dada alikimbia na Tanzania kushinda vita hivyo. Mara baada ya vita hivyo Watanzania walichukua mali za Uganda, hasa mifugo, na walipofika nchini Tanzania walifurahia na kusherekea ushindi huo.
|
20231101.sw_1992_11
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mkoa%20wa%20Kagera
|
Mkoa wa Kagera
|
Mwaka 1996 meli ya MV Bukoba ilizama ikisafirisha abiria kutoka mkoa wa Kagera kwenda Mwanza; watu wengi walikufa na lilikuwa pigo kwa serikali, kwa ndugu na majonzi makubwa kwa Watanzania kwa ujumla. meli hiyo ilikuwa ina mkoani mwanza katika ziwa la victoria
|
20231101.sw_1992_12
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mkoa%20wa%20Kagera
|
Mkoa wa Kagera
|
Katika mkoa huohuo mwaka 2016 lilitokea tetemeko la ardhi lililoleta maafa makubwa: watu walikufa, wengine walipoteza mali zao, hususani majumba yao. Uongozi wa mkoa wa Kagera uliomba kila Mtanzania kuchangia angalau shilingi 100 na kuwasaidia.
|
20231101.sw_1992_13
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mkoa%20wa%20Kagera
|
Mkoa wa Kagera
|
Katika mkoa huu elimu bado haijaenea kwa watu wote walioko vijijini. Elimu inakua kwa kasi ndogo na watu wengi wa mkoa huu hawajasoma: wengi wanafanya kazi ya kulima. Hali hiyo hufanya taifa kurudi nyuma kimaendeleo maana taifa kama taifa huongozwa na wasomi ili kukua kiuchumi.
|
20231101.sw_1996_0
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Yesu
|
Yesu
|
Yesu (kwa Kiebrania יֵשׁוּעַ, Yeshua, kifupisho cha יהושע, Yeoshua, yaani "Mungu anaokoa") alikuwa Myahudi mwanamume aliyeishi miaka 2000 hivi iliyopita (labda 6 KK - 30 BK).
|
20231101.sw_1996_1
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Yesu
|
Yesu
|
Alizaliwa na bikira Maria kwa uwezo wa Roho Mtakatifu, huko Bethlehemu ya Uyahudi. Maisha yake yalikuwa ya pekee kwa kuwa alifahamu vitu vingi kwa mfano: sheria hata kuwazidi walimu wa sheria japokuwa hakusomea sheria. Alifanya pia maajabu mengi.
|
20231101.sw_1996_2
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Yesu
|
Yesu
|
Ndiyo maana leo hii zaidi ya nusu ya wanadamu wote wanamuamini kuwa Mwana wa Mungu (ndio wanaoitwa Wakristo) au walau nabii (hasa Waislamu).
|
20231101.sw_1996_3
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Yesu
|
Yesu
|
Kutokana na umuhimu wake katika historia ya binadamu, kwa kawaida miaka yote inahesabiwa kuanzia ujio wake (ulivyokadiriwa na Denis Mdogo kimakosa katika karne ya 6).
|
20231101.sw_1996_4
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Yesu
|
Yesu
|
Yesu hakuacha maandiko yoyote. Habari zake zinapatikana hasa katika Biblia, kwa namna ya pekee katika Injili na vitabu vingine vya Agano Jipya.
|
20231101.sw_1996_5
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Yesu
|
Yesu
|
Nje ya Ukristo kuna habari fupi kuhusu Yesu katika maandiko ya waandishi wa Roma, Wagiriki na Wayahudi. Habari hizo zinaangaliwa sana kwa sababu zimetungwa na watu wasiomwamini Yesu kidini. Kwa ujumla zinathibitisha ya kwamba Yesu alikuwepo, na kwamba wakati hao walipoandika alikuwa na wafuasi huko Roma na ya kwamba awali Waroma hawakuelewa tofauti kati ya wafuasi wake na Wayahudi.
|
20231101.sw_1996_6
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Yesu
|
Yesu
|
1. Mtaalamu Myahudi Flavius Josephus: huyo aliandika mnamo 90 BK kitabu cha "Antiquitates Judaicae“ (Habari za historia ya Wayahudi) akitaja kifo cha "Yakobo ndugu wa Yesu“ (sura ya 20, 200).
|
20231101.sw_1996_7
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Yesu
|
Yesu
|
2. Mwandishi Mroma Tacitus: huyo aliandika mnamo mwaka 117 ya kwamba Kaisari Nero alishtaki kikundi cha “Chrestiani” ya kuwa wamechoma moto mji wa Roma. Aliongeza: “Mtu ambaye ni asili ya jina hilo ni Chrestus aliyeuawa wakati wa Tiberio kwa amri ya Pontio Pilato” (Annales XV,44).
|
20231101.sw_1996_8
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Yesu
|
Yesu
|
3. Mwandishi Mroma Svetonius: huyo alimtaja “Chrestos” katika kitabu chake juu ya maisha ya Kaisari Klaudio (25,4) ya kwamba huyu amesababisha fujo kati ya Wayahudi wa Roma hivyo Kaisari aliwafukuza wote mjini.
|
20231101.sw_1996_9
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Yesu
|
Yesu
|
4. Mwanasiasa Mroma Gaius Plinius Caecilius Secundus: huyo aliacha barua kadhaa zinazotaja Wakristo mnamo mwaka 100 BK. Alimwuliza Kaisari Traianus jinsi ya kushughulikia Wakristo waliokataa kutoa sadaka mbele ya sanamu za Kaisari.
|
20231101.sw_1996_10
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Yesu
|
Yesu
|
Nchi ambayo Yesu alizaliwa akafundisha ni nchi ileile ambayo Mungu aliwaahidia Waisraeli tangu zamani za Abrahamu, ni nchi ileile waliyoiteka chini ya Yoshua, ni nchi ileile waliyoirudia kutoka utumwani Babeli.
|
20231101.sw_1996_11
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Yesu
|
Yesu
|
Lakini wakati wote wa Agano Jipya, yaani tangu Yesu alipozaliwa hadi mwisho wa maisha ya mitume wake, nchi hiyo haikuwa huru, bali chini ya himaya ya Warumi, ingawa pengine hao waliwakabidhi vibaraka, yaani watawala wenyeji waliowekwa na wakoloni.
|
20231101.sw_1996_12
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Yesu
|
Yesu
|
Vibaraka hao ni Herode Mkuu (37 KK-4 KK) na wazawa wake, ambao tena hawakuwa Waisraeli halisi bali Waedomu ingawa kabila lao lililazimishwa kuingia dini ya Uyahudi karne iliyotangulia. Ukoo huo unajulikana kwa ukatili, uchu wa madaraka na uzinifu wake.
|
20231101.sw_1996_13
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Yesu
|
Yesu
|
Vilevile maliwali wa Kirumi waliowekwa pengine kutawala nchi au sehemu fulani walionyesha mara nyingi ukatili na dharau kwa Waisraeli na dini yao, hata kusababisha chuki na mapigano kati ya jeshi na wananchi. Mfano mmojawapo ni Ponsyo Pilato aliyesimamia Uyahudi kuanzia mwaka 26 hadi 36 BK.
|
20231101.sw_1996_14
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Yesu
|
Yesu
|
Mbali na hayo, utawala wa Dola la Roma, ulioenea Ulaya Magharibi na Kusini, Afrika Kaskazini na nchi za Mashariki ya Kati kupakana na Iraq ya leo, kwa jumla ulihakikisha hali ya amani kwa muda wote wa Agano Jipya na karne za kwanza za Kanisa.
|
20231101.sw_1996_15
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Yesu
|
Yesu
|
Hali hiyo, pamoja na umoja wa dola hilo lote, na urahisi wa mawasiliano kwa njia ya barabara zilizotengenezwa na Warumi, na uenezi wa lugha ya kimataifa (Kiyunani, yaani Kigiriki cha zamani), ilichangia kasi ya uenezaji wa habari njema (Injili).
|
20231101.sw_1996_16
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Yesu
|
Yesu
|
Lugha hiyo ndiyo iliyotumiwa na waandishi wote wa Agano Jipya ili vitabu vyao viwafaidishe watu wengi zaidi, ingawa baadhi yao hawakuijua vizuri.
|
20231101.sw_1996_17
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Yesu
|
Yesu
|
Lugha mama ya Yesu na ya Mitume ilikuwa Kiaramu ambacho ni jamii ya Kiyahudi na ambacho polepole kilishika nafasi yake kati ya Wayahudi kuanzia karne ya 6 KK.
|
20231101.sw_1996_18
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Yesu
|
Yesu
|
Hao wote walitokea mkoa wa Galilaya, uliokuwa na mchanganyiko wa watu (Waisraeli na mataifa), kiasi kwamba huko Wayahudi wenyewe walifuata kwa urahisi desturi za Kiyunani hata wakadharauliwa na wenzao wa Kusini (Yerusalemu na mkoa wa Yudea).
|
20231101.sw_1996_19
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Yesu
|
Yesu
|
Kati ya mikoa hiyo miwili ulienea mkoa wa Samaria ambao wakazi wake walijenga uadui mkubwa na Wayahudi baada ya uhamisho wa Babeli, walipokataliwa kuchangia ujenzi wa hekalu la pili la Yerusalemu.
|
20231101.sw_1996_20
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Yesu
|
Yesu
|
Dionisi Mdogo, mmonaki aliyeanzisha (mwaka 533 hivi) mtindo wa kuhesabu miaka tangu kuzaliwa Yesu kurudi nyuma (K.K.) au kwenda mbele (B.K.), alikosea hesabu zake. Leo tunakisia Yesu alizaliwa mwaka 6 hivi K.K. kwa sababu alizaliwa Bethlehemu chini ya Herode Mkuu aliyefariki tayari mwaka 4 K.K.
|
20231101.sw_1996_21
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Yesu
|
Yesu
|
Huyo alipojaribu kumuua mtoto Yesu, familia takatifu ilikimbilia Misri mpaka baada ya kufa kwa Herode. Hapo ikarudi Galilaya hata Yesu akajulikana kwa jina la kijiji cha Nazareti kilichodharauliwa na Wagalilaya pia. Ndipo alipokulia na kuishi akifanya kazi ya ufundi.
|
20231101.sw_1996_22
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Yesu
|
Yesu
|
Hivyo Yesu alitumia sehemu kubwa ya maisha yake kijijini akiwatii wazee wake Maria na Yosefu na kufanya kazi za mikono. “Alishuka pamoja nao mpaka Nazareti, naye alikuwa akiwatii” (Lk 2:51). Kwa namna hiyo ametuachia kielelezo cha utakatifu katika maisha ya familia na ya kazi ambayo ndiyo njia ya kawaida ya kukomaa kiutu na kumtumikia Mungu. “Mnyenyekeane katika kicho cha Kristo” (Ef 5:21).
|
20231101.sw_1996_23
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Yesu
|
Yesu
|
Mwaka 26 hivi BK ndugu yake Yohane Mbatizaji aliacha maisha ya jangwani alikokulia na kuanza kuhubiri toba kandokando ya mto Yordani. Kwa kuwa Waisraeli walikosa manabii kwa muda mrefu, na walitamani sana ukombozi, walimuendea kwa wingi hata wakamtia hofu Herode Antipa.
|
Subsets and Splits
No community queries yet
The top public SQL queries from the community will appear here once available.