_id
stringlengths
15
22
url
stringlengths
31
150
title
stringlengths
1
86
text
stringlengths
100
23.8k
20231101.sw_2007_18
https://sw.wikipedia.org/wiki/Tsunami
Tsunami
Pitisha hewa safi (ondoa hewa) kwenye magari au vyumba unaposafirisha, kuhifadhi au kutumia barafu kavu. Bila kupita kwa hewa safi, gesi inayotoka kwenye barafu inayoyeyuka inaweza kuongezeka polepole na kusababisha madhara, yakiwemo kupoteza fahamu na kifo.
20231101.sw_2007_19
https://sw.wikipedia.org/wiki/Tsunami
Tsunami
Tsunami inaweza kutengeneza mbingiriko wa maji ya bahari ambayo inaweza kutapakaa sehemu kubwa ya kijiografia. Maji ya bahari yakiendelea kusongea ufuoni, maji ya kunywa ya visima yanaweza kuzamishwa na kuweza kuchafuliwa na vidubini (bakteria, virusi, parasiti) na kemikali ambazo zinaweza kuathiri afya ya binadamu. Chumvi ya baharini inayohusishwa na maji ya chumvi inayofurika maji ya kunywa ya pwani si tishio la haraka kwa afya.
20231101.sw_2007_20
https://sw.wikipedia.org/wiki/Tsunami
Tsunami
Kwa sababu ya ladha mbaya ya maji ya chumvi, watu wengi hawawezi kumeza (kunywa) maji mengi: hiyo itasababisha shida za afya mara moja. Hata hivyo, ugonjwa unaosababisha vidubini husambaa kupitia mafuriko kwa kawaida huwa haitoi ladha nzito. Ikiwa maji yaliyona ugonjwa-yanayosababisha vidubini yatanyiwa, hata kwa kiwango kidogo, inaweza kusababisha shida za afya kwa maisha kama vile uharishaji ulio sugu, kipindupindu, na maambukizi hatari. Matumizi ya maji chafu kusafisha vidonda yanaweza kuleta maambukizi hatari.
20231101.sw_2007_21
https://sw.wikipedia.org/wiki/Tsunami
Tsunami
Zaidi ya hayo, uchafu wa kemikali unaopatikana katika mafuriko ya maji unaweza kuchafua visima kwa urahisi. Uchafu wa kemikali unaweza kujumuisha bidhaa za fueli kutoka kwa tangi za fueli zilizoanguka, au dawa za kuua wadudu ambazo zimehifadhiwa katika meneo ya mafuriko. Ukinywa maji yaliyo na aina hii ya uchafu wa kemikali inaweza kuwa hatari kwa afya na maisha.
20231101.sw_2007_22
https://sw.wikipedia.org/wiki/Tsunami
Tsunami
Baada ya visima kusafishwa vizuri na kuanza kujaza maji kutoka kwa mpenyo wa mwamba, kiwango kikubwa cha chumvi (kuwa na chumvi nyingi) unapaswa kupungua. Visiwa vifupi vinaweza kuathiriwa zaidi kuliko visima vyenye kina ndefu kwa sababu ya kuwepo kwa maji ya chumvi katika eneo la juu ya udongo. Ingawa kuanza upya kwa visima vinaweza kuwa pole pole kuliko ile ya visima vyenye kina ndefu, kuwepo kwa chumvi kwa visima vinapaswa kuwa kidogo kwa muda.
20231101.sw_2007_23
https://sw.wikipedia.org/wiki/Tsunami
Tsunami
Baada ya tsunami, watu katika sehemu zilizoathirika wanapaswa kusikiza matangazo ya umma kuhusu usalama wa kupeana maji. Visima vya kibinafsi vilivyofurika vinapaswa kuchunguzwa na kusafishwa baada ya maji ya mafuriko kupungua. Ikiwa harufu mbaya, ladha na rangi isiyo kuwa ya kawaida, au matokeo ya awali ya uchunguzi wa maji yatafanya watu washuku kuwa visima vya eneo hilo vimechafuliwa na fueli, dawa ya kuua wadudu, au hata kemikali zingine, uchunguzi wa kemikali ya maji ya kunywa unahitaji sana. Maswali kuhusu uchunguzi yanapaswa kutolewa kwa viongozi wa eneo hilo.
20231101.sw_2007_24
https://sw.wikipedia.org/wiki/Tsunami
Tsunami
Maji mazuri ya kunywa, kupikia, na usafi wa kibinafsi inajumuisha maji yaliyowekwa kwa chupa, chemshwa, au kutibiwa. Baada ya tsunami, asili ya maji yanaweza kuchafuliwa na maji ya chumvi. Ukitumia maji ya chumvi (mchanganyiko wa maji ya chumvi na maji isiyotiwa chumvi) kwa kunywa na kupika kwa muda mrefu yanaweza kusababisha shida za afya kutoka kwa viwango vya juu ya chumvi yanayoweza kunyiwa. Viongozi wa eneo lako wanaweza kupanga mapendekezo maalum kwa uchemshaji na uwekaji wa kemikali maji katika eneo lako. Ukipata maji kutoka kwa tangi la maji au kisima, tafadhali rejelea ujumbe wa kusafisha matangi ya maji au visima. Usipopata maji kutoka kwa tangi la maji au kisima, fuata sheria hizi kuhusiana na maji ya kunywa, kupikia, na usafi wa kibanfsi.
20231101.sw_2007_25
https://sw.wikipedia.org/wiki/Tsunami
Tsunami
Usitumie maji yaliyochafuliwa kuosha vyomba, kusugua meno, kuosha na kutayarisha chakula, kuosha mikono, kutengeneza barafu au kutayarisha fomyula ya mtoto. Ikiwezekana, tumia fomyula ya mtoto isiyohitaji kuongezwa maji. Unaweza kutumia kisafisha mikono chenye alkoholi ili kuosha mikono.
20231101.sw_2007_26
https://sw.wikipedia.org/wiki/Tsunami
Tsunami
Ikiwa utatumia maji ya chupa, hakikisha kuwa yametolewa katika chanzo salama. Ikiwa hujui iwapo maji hayo yalitolewa kwenye chanzo salama, unapaswa kuyachemsha au kuyatibu kabla ya kutumia. Tumia maji ya chupa, yaliyochemshwa au yaliyotibiwa tu hadi maji ya chanzo chako yatakavyochunguzwa na kupatikana kuwa salama.
20231101.sw_2007_27
https://sw.wikipedia.org/wiki/Tsunami
Tsunami
Kuchemsha maji, kunapowezekana, ndiyo njia bora zaidi ya kuua bakteria na parasiti. Kuchemsha maji kwa dakika 1 kutaua vimelea vingi. Hata hivyo, kuchemsha maji ya chumvi kwa zaidi ya dakika 5 kunaweza kuongeza kukolea kwa chumvi za bahari na vichafuzi vingine.
20231101.sw_2007_28
https://sw.wikipedia.org/wiki/Tsunami
Tsunami
Iwapo hautaweza kuchemsha maji, unaweza kuyatibu kutumia tembe za klorini, aidini au dawa ya klorini ya nyumbani isiyo na harufu (asilimia 5.25 ya sodium hypochlorite):
20231101.sw_2007_29
https://sw.wikipedia.org/wiki/Tsunami
Tsunami
Ukitumia dawa ya klorini ya nyumbani, ongeza 1/8 ya kijiko cha chai (takriban mililita 0.75) ya klorini kwa kila galoni ya maji ikiwa maji haya ni safi. Kwa maji yasiyo safi, ongeza 1/4 ya kijiko cha chai (takriban mililita 1.50) ya klorini kwa kila galoni. Changanya mmumunyo huu kikamilifu kisha uuache kwa dakika 30 kabla ya kutumia.
20231101.sw_2007_30
https://sw.wikipedia.org/wiki/Tsunami
Tsunami
Tumia mmumunyo wa dawa ya klorini kukamua vyombo vya maji kabla ya kuvitumia tena. Tahadhari unapotumia tangi za kuhifadhi maji na aina zingine za vyombo. Kwa mfano, tangi za maji za zimamoto na makopo au chupa zilizotumika awali huenda zimechafuliwa na mikrobu au kemikali. Usitegemee matumizi ya vyombo ambavyo havijajaribiwa vya kusafisha maji.
20231101.sw_2007_31
https://sw.wikipedia.org/wiki/Tsunami
Tsunami
Kuua viini vya maradhi kwenye Matangi ya Maji na Mifumo Mingine ya Kunasa Maji ya Mvua Baada ya Mafuriko
20231101.sw_2007_32
https://sw.wikipedia.org/wiki/Tsunami
Tsunami
Katika maeneo mengi ulimwenguni, watu hupata maji ya kunywa kwenye mifumo ya kunasa (kukusanya) maji ya mvua na kuyahifadhi. Hata inapotengenezwa na kutumika inavyofaa, mifumo hii huchafuliwa kwa urahisi na viinitete vinavyoweza kusababisha magonjwa. Baadhi ya mifumo ya kusambaza maji hutumia sehemu kama vile paa ili kukusanya maji na kuyaelekeza kwenye tangi la maji (tangi la kuhifadhi). Ikiwa hupati maji yako kutoka kwa tangi au kisima, rejelea Maji ya Kunywa, Kupika na Usafi wa Kibinafsi kwa habari kuhusu kuua viini kwenye maji yako.
20231101.sw_2007_33
https://sw.wikipedia.org/wiki/Tsunami
Tsunami
Maji ya matangi ya maji na mifumo sawa yanapotangamana na maji ya mafuriko, watu wanapaswa kuchukulia kuwa maji yao ya kunywa yamechafuliwa. Ikiwa unasikitika kuhusu kuchafuliwa kwa chanzo cha maji yako ya kunywa, tafadhali rejelea Maji ya Kunywa, Kupika, na Usafi wa Kibinafsi kuhusu uchafuzi wa maji chumvi, uchafuzi wa kemikali na athari za kiafya.
20231101.sw_2007_34
https://sw.wikipedia.org/wiki/Tsunami
Tsunami
Moja ya mbinu zifuatazo inaweza kutumika kuua viini kwenye matangi ya maji na mifumo mingine ya kunasa maji ya mvua katika hali za mikasa kwa kuzingatia iwapo chanzo cha maji ya kunywa kinapatikana tangi la maji au mfumo wa kunasa maji unasafishwa (Mbinu ya 1) au iwapo tangi la maji au mfumo wa kunasa maji unahitaji kutumika kwa haraka zaidi kama chanzo cha maji ya kunywa (Mbinu ya 2). Iwapo bidhaa za fueli au vichafuzi vingine vya kemikali vimetangamana na tangi la maji au mfumo wa kunasa maji ya mvua, au iwapo kuna harufu ya fueli au kemikali zingine katika mazingira karibu na mfumo huo, tumia tu Mbinu ya 1 kwa uuaji viini.
20231101.sw_2007_35
https://sw.wikipedia.org/wiki/Tsunami
Tsunami
Mbinu ya 1—Tumia mbinu hii ikiwa maji safi ya kunywa yanapatikana kutoka kwenye chanzo kingine tangi la maji au mfumo wa kunasa maji unaposafihshwa. Mbinu hii ni bora, lakini huchukua muda mrefu zaidi, kwani tangi la maji/mfumo ni lazima utolewe maji yote na kujazwa tena mara mbili.
20231101.sw_2007_36
https://sw.wikipedia.org/wiki/Tsunami
Tsunami
Bila kuingia kwenye tangi, sugua sehemu ya ndani vizuri iwezekanavyo kwa brashi dhabiti au ufagio na mmumunyo wa kikombe 1 (aunsi 8; takriban lita 0.25) wa asilimia 5.25 ya dawa ya klorini isiyo na harufu (sodium hypochlorite) katika galoni 10 (takriban lita 38) za maji.
20231101.sw_2007_37
https://sw.wikipedia.org/wiki/Tsunami
Tsunami
Iwapo hufahamu kiasi cha tangi, tumia fomyula ifuatayo kutambua kiasi cha maji linachoweza kuhifadhi: Kwa tangi la umbo la mstatili, zidisha kina cha tangi (katika futi) kwa urefu (katika futi) na kwa upana (katika futi), kisha uzidishe matokeo kwa 7.5 ili kupata idadi ya galoni zitakazojaza tangi hilo. Kwa tangi la mviringo, zidisha urefu (katika futi) kwa matokeo ya kuzidisha nusu kipenyo cha tangi kwa chenyewe, zidisha matokeo kwa 3.14, na kisha uzidishe matokeo hayo kwa 7.5 ili kupata galoni. Ikiwa hakuna mbinu kati ya hizi inayoweza kutumika, unaweza kukadiria kiasi kwa galoni kwa kufanya "kisio la kidhahania," kisha uzidishe kiasi cha dawa itakayotumika mara mbili katika mmumunyo wa kuua viini.
20231101.sw_2007_38
https://sw.wikipedia.org/wiki/Tsunami
Tsunami
Kipimo kwa mita: Katika vipimo vya mita, zidisha urefu (mita) X upana (mita) X kina (mita) X 1,000 = kiasi katika lita. Kwa matangi ya mviringo, zidisha kina X matokeo ya kuzidisha nusu kipenyo cha tangi kwa chenyewe (mita) X 3,140 = kiasi katika lita.
20231101.sw_2007_39
https://sw.wikipedia.org/wiki/Tsunami
Tsunami
Ongeza vikombe 4 (aunsi 32; takribani lita 1) vya asilimia 5.25 ya dawa ya klorini isiyo na harufu kwa kila galoni 100 (takribani lita 380) za maji katika tangi. Hii inapaswa kukupa ukolezi wa klorini wa takribani sehemu 100 kwa kila milioni.
20231101.sw_2007_40
https://sw.wikipedia.org/wiki/Tsunami
Tsunami
Fungua maji kwenye paipu zote zinazotumika kwa maji ya kunywa nyumbani kwako hadi utakapotambua harufu kali ya klorini.
20231101.sw_2007_41
https://sw.wikipedia.org/wiki/Tsunami
Tsunami
Foka paipu zote za nyumbani kwako hadi harufu ya klorini itakapoisha kabisa kabla ya kuanza kutumia mfumo huu tena.
20231101.sw_2007_42
https://sw.wikipedia.org/wiki/Tsunami
Tsunami
Mbinu ya 2— Tumia mbinu hii ikiwa maji safi ya kunywa yanapatikana kutoka kwa asili nyingine wakati tangi/mfumo unaambukuliwa. Mbinu hii si bora kama ilivyo Mbinu ya 1, lakini huchukua muda mfupi kwani tangi/mfumo unahitaji kutolewa maji na kujazwa tena mara moja tu.
20231101.sw_2007_43
https://sw.wikipedia.org/wiki/Tsunami
Tsunami
Iwapo haufahamu kiasi cha tangi, tumia fomyula ifuatayo kutambua kiasi cha maji kinachoweza kuwekwa ndani ya tangi: Kwa tangi la mstatili, zidisha kina cha tangi (katika futi) kwa urefu (katika futi) na kwa upana (katika futi), kisha uzidishe matokeo na 7.5 ili kupata idadi ya galoni. Kwa tangi la mviringo, zidisha urefu (futi) kwa matokeo ya kuzidisha nusu kipenyo kwa chenyewe, zidisha matokeo kwa 3.14, kisha uzidishe matokeo hayo kwa 7.5 ili kupata idadi ya galoni zinazoweza kulijaza. Ikiwa hakuna mbinu kati ya hizi inayoweza kutumika, unaweza kukadiria kiasi kwa galoni kwa kufanya "kisio la kidhahania," kisha uzidishe kiasi cha dawa itakayotumika mara mbili katika mmumunyo wa kuua viini. Kipimo kwa mita: Katika vipimo vya mita, zidisha urefu (mita) X upana (mita) X kina (mita) X 1,000 = kiasi katika lita. Kwa matangi ya mviringo, zidisha kina X matokeo ya kuzidisha nusu kipenyo cha tangi kwa chenyewe (mita) X 3,140 = kiasi katika lita.
20231101.sw_2007_44
https://sw.wikipedia.org/wiki/Tsunami
Tsunami
Ongeza vikombe 4 (aunsi 32; takribani lita 1) vya asilimia 5.25 ya dawa ya klorini isiyo na harufu kwa kila galoni 100 (takribani lita 380) za maji katika tangi. Hii inapaswa kukupa ukolezi wa klorini wa takribani sehemu 100 kwa kila milioni.
20231101.sw_2007_45
https://sw.wikipedia.org/wiki/Tsunami
Tsunami
Fungua maji kwenye paipu zote zinazotumika kwa maji ya kunywa nyumbani kwako hadi utakapotambua harufu kali ya klorini.
20231101.sw_2007_46
https://sw.wikipedia.org/wiki/Tsunami
Tsunami
Bila kuingia kwenye tangi, sugua vizuri sehemu ya ndani ya tangi kwa brashi dhabiti au ufagio na mmumunyo wa kikombe 1 (aunsi 8; takriban lita 0.25) wenye asilimia 5.25 ya dawa ya klorini isiyo na harufu (sodium hypochlorite) katika galoni 10 (takribani lita 380) za maji.
20231101.sw_2007_47
https://sw.wikipedia.org/wiki/Tsunami
Tsunami
Foka paipu zote za nyumbani kwako hadi harufu ya klorini itakapoisha kabisa kabla ya kuanza kutumia mfumo huu tena.
20231101.sw_2007_48
https://sw.wikipedia.org/wiki/Tsunami
Tsunami
Baada ya tsunami, huenda visima katika maeneo yaliyoathiriwa vikawa vimechafuliwa. Tafadhali rejelea Maji ya Kunywa, Kupika na ya Usafi wa Kibinafsi kuhusu uchafuzi wa maji chumvi, uchafuzi wa kemikali na athari za afya. Iwapo unashuku kuwa kisima chako kimechafuliwa, wasiliana na mamlaka za eneo lako kwa ushauri mahususi zaidi. Iwapo haupati maji yako kutoka kwa tangi au kisima, rejelea Maji ya Kunywa, Kupika na ya Usafi wa Kibinafsi kwa habari kuhusu kuua viini kwenye maji yako. Yafuatayo ni baadhi ya maagizo ya jumla ya kuua viini kwenye visima.
20231101.sw_2007_49
https://sw.wikipedia.org/wiki/Tsunami
Tsunami
Vuta maji yote kutoka kwa kisima. (Fahamu: Katika sehemu zisizo na nguvu za umeme, jenereta ya kubeba inaweza kuhitajika kuendesha pampu.) Tumia mifereji ya nje kuondoa maji kwenye kisima iwapo inapatikana.
20231101.sw_2007_50
https://sw.wikipedia.org/wiki/Tsunami
Tsunami
Ili kubainisha kiasi kamili cha kutumia, zidisha kiasi cha kiua viini kinachohitajika (kulingana na kipenyo cha kisima) na kina cha maji kwenye kisima hicho. Kwa mfano, kisima chenye kipenyo cha futi 5 huhitaji vikombe 4½ vya dawa ya klorini kwa kila futi ya maji. Iwapo maji katika kisima hicho ni futi 30 kwenda chini, zidisha vikombe 4½ na futi 30 ili kubainisha idadi kamili ya vikombe vya dawa ya klorini vinavyohitajika (4½ X 30 = vikombe 135).
20231101.sw_2007_51
https://sw.wikipedia.org/wiki/Tsunami
Tsunami
Mfumo wa mita: Katika mfumo wa mita, kisima chenye kipenyo cha takribani mita 1.5 huhitaji takribani lita 1.1 za dawa ya klorini kwa kila mita ya maji. Iwapo kisima ni takribani mita 9.1 kwenda chini, zidisha lita 1.1 na mita 9.1 ili kubainisha idadi kamili ya lita za dawa klorini itakayohitajika (1.1 X 9.1 = lita 10). Futi moja ya urefu wa maji = mita 0.305.
20231101.sw_2007_52
https://sw.wikipedia.org/wiki/Tsunami
Tsunami
Weka idadi hii kamili ya kiasi cha kiua viini katika galoni 10 za maji (lita 38). Rashia mchanganyiko huu kwenye ukuta au bitana ya kisima. Hakikisha kuwa kiua viini hicho kinagusa sehemu zote za kisima hicho.
20231101.sw_2007_53
https://sw.wikipedia.org/wiki/Tsunami
Tsunami
Fungua mifereji yote na uvute maji hadi utakapotambua harufu nzito ya dawa ya klorini kwenye kila mfereji. Kisha simamisha pampu na uwache mmumunyo huo kwenye kisima kwa saa 24 au, kwa kiwango cha chini, usiku kucha.
20231101.sw_2007_54
https://sw.wikipedia.org/wiki/Tsunami
Tsunami
Siku itakayofuata, endesha pampu kwa kufungua mifereji yote, kuendelea hadi harufu ya klorini itakavyoisha. Weka sawa mtiririko wa maji kwenye mifereji au vyombo vinavyopeleka maji kwenye mifumo ya maji chafu iweze kutiririka polepole ili kuepuka kujaza mno mfumo wa utupaji.
20231101.sw_2007_55
https://sw.wikipedia.org/wiki/Tsunami
Tsunami
Foka kisima hadi maji yawe safi. (Fahamu: Katika maeneo yasiyo na stima, genereta inayoweza kusogezwa kutoka mahali pamoja hadi pengine itahitajika ili kutumia pampu.) Tumia mifereji ya nje kutoa maji kutoka kwa kisima ikiwa inapatikana.
20231101.sw_2007_56
https://sw.wikipedia.org/wiki/Tsunami
Tsunami
Tambua kiasi cha maji katika kisima kwa kuzidisha galoni kwa kila futi ya kina cha kisima kwa futi (Jedwali 2). Kwa mfano, kisima kilicho na kipenyo cha inchi 6 ina galoni 1.5 ya maji kwa kila futi. Ikiwa kina cha kisima hiki ni futi 120, zidisha 1.5 kwa 120 (1.5 X 120 = galoni 180).
20231101.sw_2007_57
https://sw.wikipedia.org/wiki/Tsunami
Tsunami
Kipimo cha mita: Katika kipimo cha mita, tambua kiasi cha maji kwenye kisima kwa kuzidisha lita kwa kila mita kwa kina cha kisima kwa mita. Kwa mfano, kisima chenye kipenyo cha sentimita 15.2 kina lita 18.6 za maji kwa kila mita. Ikiwa kina cha kisima hiki ni mita 36.5, zidisha lita 18.6 kwa mita 36.5 ili kutambua idadi jumla ya lita za maji katika kisima (18.6 X 36.5 = lita 679).
20231101.sw_2007_58
https://sw.wikipedia.org/wiki/Tsunami
Tsunami
Kwa kila galoni 100 (lita 380) za maji kwenye kisima, tumia kiasi cha klorini (aina ya maji au chembechembe) kama ilivyoashiriwa katika Jedwali 3. Changanya kiasi chote cha klorini ya maji au chembechembe na takriban galoni 10 (lita 38) za maji.
20231101.sw_2007_59
https://sw.wikipedia.org/wiki/Tsunami
Tsunami
Unganisha mpira wa maji kutoka kwa mfereji ambapo maji hutokea kwa tangi kwa kifuniko cha kisima. Endesha pampu. Nyunyiza maji ndani ya kisima na uoshe pande za kifuniko kwa angalau dakika 15.
20231101.sw_2007_60
https://sw.wikipedia.org/wiki/Tsunami
Tsunami
Fungua mfereji yote katika mfumo na uache maji yapite hadi utakaponusa klorini. Kisha funga mifereji yote na uzibe sehemu ya juu ya kisima.
20231101.sw_2007_61
https://sw.wikipedia.org/wiki/Tsunami
Tsunami
Baada ya kuacha maji ndani ya kisima, endesha pampu kwa kufungulia mifereji yote na kuendelea hadi harufu ya klorini inapoisha. Sawazisha mwendo wa mifereji ya maji au chombo kinachotoa maji hadi kwa mifumo ya maji machafu hadi kufukia mwendo wa polepole ili kuepuka kuweka shinikizo katika mfumo wa maji machafu.
20231101.sw_2007_62
https://sw.wikipedia.org/wiki/Tsunami
Tsunami
Ni muhimu kukumbuka kutekeleza usafi wa kimsingi katika kipindi cha dharura. Osha mikono kila mara yako kwa sabuni na maji yaliyochemshwa au yaliyotiwa kiua viini. Maji yaliyochemshwa ndiyo bora zaidi.
20231101.sw_2007_63
https://sw.wikipedia.org/wiki/Tsunami
Tsunami
Maji safi yasipopatikana, unaweza kutumia bidhaa zenye spiriti zilizotengenezwa kwa ajili ya kuosha mikono.
20231101.sw_2007_64
https://sw.wikipedia.org/wiki/Tsunami
Tsunami
Maji ya mafuriko yanaweza kuwa na kinyesi kutoka kwa mifumo ya maji taka yanayoenea kwenye ardhi na mapato ya ziada ya kilimo na viwanda. Ingawa mgusano wa ngozi na maji ya mafuriko kwa wenyewe hauleti hatari kubwa ya afya, kuna hatari ya magonjwa kutokana na kula au kunywa chochote kilichochafuliwa na maji ya mafuriko. Ikiwa una vidonda wazi ambavyo vitatangamana na maji ya mafuriko, hakikisha umevisafisha vyema iwezekanavyo kwa kuviosha kwa sabuni ili kudhibiti maambukizi. Kidonda kikianza kuwa chekundu, kuvimba au kuwa na mtiririko, tafuta usaidizi wa kimatibabu mara moja.
20231101.sw_2007_65
https://sw.wikipedia.org/wiki/Tsunami
Tsunami
Isitoshe, wazazi wanahitaji kuwasaidia watoto kuepuka maradhi yanayoenezwa na maji. Usiwaruhusu watoto kucheza katika maeneo yenye maji ya mafuriko, osha mikono ya watoto mara nyingi (kila mara kabla ya kula) na usiwaruhusu kuchezea vinyago vilivyochafuliwa na maji ya mafuriko ambavyo havijatiwa kiua viini. Unaweza kutumia mmumunyo wa kikombe kimoja cha klorini katika galoni 5 za maji kwa kuua viini kwenye vinyago. Vinyago vingine kama vile wanyama waliojazwa nguo na vinyago vya watoto haviwezi kutiwa kiua viini; vinapaswa kutupwa.
20231101.sw_2008_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/Tanganyika%20African%20National%20Union
Tanganyika African National Union
Tanganyika African National Union (TANU) kilikuwa chama kilichotawala Tanganyika na Tanzania hadi muungano wa chama hiki na Chama cha Afro-Shirazi cha Zanzibar ulipounda Chama cha Mapinduzi (CCM) mwaka 1977.
20231101.sw_2008_1
https://sw.wikipedia.org/wiki/Tanganyika%20African%20National%20Union
Tanganyika African National Union
TANU ilianzishwa 7 Julai 1954 kutokana na Tanganyika African Association (TAA). TAA ilikuwa na mwelekeo wa kitamaduni zaidi ya siasa. Mwenyekiti wa kwanza wa TANU alikuwa Julius Kambarage Nyerere.
20231101.sw_2008_2
https://sw.wikipedia.org/wiki/Tanganyika%20African%20National%20Union
Tanganyika African National Union
TANU ilishinda kila uchaguzi chini ya utawala wa kikoloni ikawa chama cha kuongoza Tanganyika hadi ilipopata uhuru wake mwaka 1961. Katiba ya Taifa ya mwaka 1962 ilifanya TANU kuwa chama cha pekee nchini ikifuata mfano wa nchi za kijamaa zenye muundo wa siasa ya chama kimoja.
20231101.sw_2008_3
https://sw.wikipedia.org/wiki/Tanganyika%20African%20National%20Union
Tanganyika African National Union
1950: TAA yawasiliana na KAU; Abdulwahid alikwenda Nairobi kukutana na Jomo Kenyatta ili kujenga mawasiliano na chama cha Kenya African Union (KAU).
20231101.sw_2008_4
https://sw.wikipedia.org/wiki/Tanganyika%20African%20National%20Union
Tanganyika African National Union
1951: Kenyatta akutana tena na viongozi wa TAA. Safari hii mkutano huo ulifanyika Arusha. Wajumbe wa TAA walikuwa Abdulwahid Kleist Sykes, Dossa Aziz na Stephen Mhando.
20231101.sw_2008_5
https://sw.wikipedia.org/wiki/Tanganyika%20African%20National%20Union
Tanganyika African National Union
1952: Mwalimu Nyerere atambulishwa kwa Abdulwahid na Bwana Kasela Bantu. Baada ya utambulisho huo ikawa kila Jumamosi Mwalimu Nyerere akawa anakutana na akina Dossa Azizi, Bw. Ally Sykes, Abdulwahid Sykes, Dustan Omar na Mhando kujadili mustakbali wa nchi ya Tanganyika.
20231101.sw_2008_6
https://sw.wikipedia.org/wiki/Tanganyika%20African%20National%20Union
Tanganyika African National Union
Mikutano hiyo ama ilikuwa ikifanyika nyumbani kwa Dossa Azizi mtaa wa Congo au mtaa wa Stanley nyumbani kwa Abdulwahid.
20231101.sw_2008_7
https://sw.wikipedia.org/wiki/Tanganyika%20African%20National%20Union
Tanganyika African National Union
Alikuwa ni Dossa Azizi ambaye mara nyingi alikuwa akimrudisha Mwalimu Nyerere kwa gari lake Pugu (St. Francis College) baada ya mkutano.
20231101.sw_2008_8
https://sw.wikipedia.org/wiki/Tanganyika%20African%20National%20Union
Tanganyika African National Union
1953: Mwalimu achaguliwa kuwa Rais wa TAA. Wazee waliompa nguvu ya kisiasa Mwalimu mara baada ya kuingia katika TAA/TANU.
20231101.sw_2008_9
https://sw.wikipedia.org/wiki/Tanganyika%20African%20National%20Union
Tanganyika African National Union
Sheikh Hassan bin Amir, Sheikh Suleiman Takadir, Mzee Mohammed Jumbe Tambaza, Mshume Kiyate na Mwinjuma Mwinyikambi. Wengine walikuwa Rajab Diwani, Makisi Mbwana, Sheikh Haidar Mwinyimvua na Idd Faiz Mafongo. Aidha walikuwepo Idd Tosiri, Sheikh Mohamed Ramia na Mashado Ramadhani Plantan.
20231101.sw_2008_10
https://sw.wikipedia.org/wiki/Tanganyika%20African%20National%20Union
Tanganyika African National Union
Oktoba 10, 1953 Mwalimu Nyerere, Abdulwahid Sykes, Ally Sykes, Dossa Aziz na John Rupia walikutana kujadili namna ya kuibadili TAA kuwa chama kamili cha siasa.
20231101.sw_2008_11
https://sw.wikipedia.org/wiki/Tanganyika%20African%20National%20Union
Tanganyika African National Union
1954: TANU yaanzishwa. Wajumbe wa mkutano uliojadili kuibadili katiba ya TAA kuwa TANU walikuwa Abdulwahid Sykes, Julius Nyerere, Tewa Said Tewa, Dossa Aziz, Ally Sykes, Kasela Bantu, , Abubakar Ilanga na Saadan Abdu Kandoro. Wengine walikuwa S.M. Kitwana, C.O. Milinga, Patrick Kunambi, Gerimano Pacha, Japhet Kirilo na L.M. Makaranga. Walikuwa pia Joseph Kimalando na John Rupia.
20231101.sw_2008_12
https://sw.wikipedia.org/wiki/Tanganyika%20African%20National%20Union
Tanganyika African National Union
Mkutano wa kuizindua rasmi TANU ulihudhuriwa na wajumbe wafuatao: Julius Nyerere, Abdulwahid Sykes, Ally Sykes, Dossa Aziz, John Rupia na Mshume Kiyate. Wengine walikuwa Makisi Mbwana, Jumbe Tambaza, Juma Waziri, Clement Mtamila, Rajab Diwani, Schneider Plantan na Marsha Bilali. Walikuwepo pia Rashid Ally Meli, Frederick Njiliwa, Idd Faiz Mafongo, Idd Tulio, Denis Phombeah na wengine.
20231101.sw_2008_13
https://sw.wikipedia.org/wiki/Tanganyika%20African%20National%20Union
Tanganyika African National Union
Julius Nyerere alipewa kadi ya TANU Na. 1, kadi Na. 2 ikaenda kwa Ally Sykes na Abdulwahid akachukua kadi ya TANU Na. 3, Dossa Azizi alichukua kadi Na. 4, kadi Na. 5 ikaenda kwa Phombeah. Dome Okochi alipata kadi Na. 6, John Rupia Na. 7, Bibi Titi Mohamed kadi Na. 16 na Idd Tosiri kadi Na. 25.
20231101.sw_2009_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/Benjamin%20Mkapa
Benjamin Mkapa
Benjamini William Mkapa (12 Novemba 1938 - 24 Julai 2020) alikuwa Rais wa awamu ya tatu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (1995-2005) na mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi, CCM.
20231101.sw_2009_1
https://sw.wikipedia.org/wiki/Benjamin%20Mkapa
Benjamin Mkapa
Mkapa alizaliwa Lupaso karibu na Masasi katika kusini-mashariki ya Tanganyika. Kuanzia 1945 hadi 1951 alsoma shule za msingi pale Lupaso na Ndanda. 1952/53 alisoma shule ya seminari ya Kigonsera akaendelea kwenye shule ya sekondari ya watawa Wabenedikto pale Ndanda hadi kumaliza O-level. 1958/59 alimaliza A-levels pale St Farncis, Dar es Salaam (leo hii Pugu Secondary). Alipokelewa kwenye Chuo Kikuu cha Makerere alipohitimu 1962.
20231101.sw_2009_2
https://sw.wikipedia.org/wiki/Benjamin%20Mkapa
Benjamin Mkapa
Katika mwaka wa 1995, Mkapa alichaguliwa rais msingi wake ukiwa kampeni maarufu ya kupambana na ufisadi na kuuungwa mkono kwa nguvu na rais wa zamani Julius Nyerere . Juhudi za Mkapa za kupambana na ufisadi ni pamoja na kuumba jukwaa la wazi lililoitwa Tume ya Rais juu ya Ufisadi (Tume ya Warioba) na kuongeza msaada kwa Afisi ya Kuzuia Ufisadi.
20231101.sw_2009_3
https://sw.wikipedia.org/wiki/Benjamin%20Mkapa
Benjamin Mkapa
Muhula wa pili wa miaka 5 wa Mkapa kama Rais uliisha Desemba 2005. Katika wakati wake ofisini, Mkapa alibinafsisha kampuni zilizomilikiwa na serikali akaweka sera za soko huria. Wafuasi wake walimtetea kuwa kuvutia uwekezaji wa kigeni ungesaidia kukuza uchumi. Sera zake zilipata msaada wa Benki ya Dunia na IMF na kupelekea baadhi ya madeni ya nje ya Tanzania kufutiliwa mbali.
20231101.sw_2009_4
https://sw.wikipedia.org/wiki/Benjamin%20Mkapa
Benjamin Mkapa
Amekashifiwa kwa upungufu wa baadhi ya jitihada zake za kupambana na ufisadi vilevile matumizi mabaya ya fedha za umma. Utawala wake ulikuwa na matumizi sana na maposho bila kikomo. Alitumia £ 15 milioni kununua ndege ya binafsi ya kirais, vilevile karibu £ 30 milioni kwa vifaa vya angani vya kijeshi ambavyo wataalamu waliona yalizidi mahitaji machache ya majeshi ya nchi. Ilikuwa juu ya ununuzi huo wa mwisho ndipo katibu wa maendeleo ya kimataifa wa Uingereza wa wakati huo Clare Short alielezea hasira ya umma, na kusababisha yeye kujulikana kama 'Mama Radar' katika vyombo vya habari vya Tanzania.
20231101.sw_2009_5
https://sw.wikipedia.org/wiki/Benjamin%20Mkapa
Benjamin Mkapa
Baada ya kutoka ofisini kwa kukamilisha mihula miwili inayoruhusiwa, Mkapa alikumbwa na shutuma nyingi za ufisadi kati yao kujipa mwenyewe na Waziri wake wa zamani wa nishati na madini Daniel Yona "Mgodi wa Makaa ya Mawe wa Kiwira" yenye faida kubwa katika Nyanda za juu za kusini mwa Tanzania bila taratibu zifuatazo. Kwa kujibinafsishia mgodi wa makaa ya mawe wa Kiwira, alivunja katiba ya Tanzania ambayo haimruhusu rais kufanya biashara yoyote katika ikulu.
20231101.sw_2009_6
https://sw.wikipedia.org/wiki/Benjamin%20Mkapa
Benjamin Mkapa
Mnamo Desemba 7, 2019, alitunukiwa Nishani ya Heshima ikiwa ni kuthamini mchango wake katika kuanzisha vyuo vikuu binafsi, hivyo kukifanya Chuo Kikuu cha Iringa kuwa chuo kikuu cha kwanza binafsi nchini Tanzania wakati wa utawala wake.
20231101.sw_2009_7
https://sw.wikipedia.org/wiki/Benjamin%20Mkapa
Benjamin Mkapa
"Rais mstaafu Benjamin Mkapa Kutunukiwa Nishani ya Heshima kwa Kuanzisha Vyuo Vikuu Binafsi Nchini Wakati wa Utawala Wake.1661870/
20231101.sw_2010_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/Reli%20ya%20Kenya-Uganda
Reli ya Kenya-Uganda
''Makala hii yaeleza habari za njia ya reli ya kihistoria kati ya Mombasa na Uganda. Kwa habari za Shirika ya Reli ya Uganda ya kisasa tazama Uganda Railways Corporation.
20231101.sw_2010_1
https://sw.wikipedia.org/wiki/Reli%20ya%20Kenya-Uganda
Reli ya Kenya-Uganda
Reli ya Kenya-Uganda ni jina kwa reli kati ya Mombasa na Kampala iliyojengwa na Waingereza kuanzia mwaka 1896. Mwanzoni ilijulikana kwa jina la "Reliya Uganda" tu. Reli hii ilisababisha Uingereza kutafuta utawala juu ya eneo ambako njia ya reli ilipita. Eneo hili lilikuwa baadaye koloni na nchi ya Kenya. Hali halisi njia ya reli hii ilijengwa katika Kenya pekee hadi ziwa Viktoria Nyanza ambako usafiri uliendelea kwa njia ya meli hadi Uganda. Tangu 1931 kulikuwa na nyongeza ya njia ya reli hadi Uganda yenyewe.
20231101.sw_2010_2
https://sw.wikipedia.org/wiki/Reli%20ya%20Kenya-Uganda
Reli ya Kenya-Uganda
Reli ilijengwa kwa sababu Kampuni ya Kifalme ya Uingereza kwa Afrika ya Mashariki IBEA (Imperial British East Africa Company) ilitaka kuboresha usafiri wa kwenda Uganda baada ya Uganda ilitangazwa nchi lindwa na Uingereza na kampuni ilitaka kuchukua nafasi hii ya kuanzisha mashamba ya kibiashara huko yasiyokuwa na faida bila usafiri wa kupeleka mazao kwenye masoko ya dunia.
20231101.sw_2010_3
https://sw.wikipedia.org/wiki/Reli%20ya%20Kenya-Uganda
Reli ya Kenya-Uganda
Mwenye kampuni ya IBEA William MacKinnon alianzisha biashara kati ya Mombasa na Uganda lakini safari hizi kwa magari ya maksai zilikuwa ngumu na ghali sana. MacKinnon alianza kushawishi Serikali ya Uingereza na kudai reli ijengwe. Awali serikali ya Uingereza ilisitasita kwa sababu faida ya kiuchumi haikuonekana pia Uingereza wakati ule haikupenda kuongeza idadi ya koloni zake ikipendelea kuwaachia watu binafsi na makampuni yao shughuli za kufungua masoko mapya katika nchi kama Uganda.
20231101.sw_2010_4
https://sw.wikipedia.org/wiki/Reli%20ya%20Kenya-Uganda
Reli ya Kenya-Uganda
Mipango hii ya kujenga biashara ya kampuni ilikuwa hatarini kutokana na uenezaji wa Ujerumani katika Afrika ya Mashariki. Mwaka 1890 mwakilishi wa kampuni kikoloni ya kijerumani Karl Peters alifaulu kusaini mapatano na Kabaka; wakati uleule Wajerumani walionekana kupanusha eneo la Witu kwenye pwani la Kenya na Somalia. Hapo serikali za nchi zote mbili ziliamua kumaliza mashindano kati ya makampuni haya kwa kuelewana juu ya mipaka ya maeneo katika Afrika kwa mapatano kati ya Uingereza na Ujerumani ya 1890.
20231101.sw_2010_5
https://sw.wikipedia.org/wiki/Reli%20ya%20Kenya-Uganda
Reli ya Kenya-Uganda
Mkataba huu ulifanya shughuli za Afrika ya Mashariki kuwa rasmi chini ya serikali ya Uingereza. Kutokana na azimio hili Uingereza iliamua 1894 kuitangaza Uganda kuwa chini ya ulinzi wake na pia kujenga reli kama njia ya kuhakikisha utawala wake na kuweka msingi wa uzalishaji mali huko Uganda kwa ajili ya soko la dunia.
20231101.sw_2010_6
https://sw.wikipedia.org/wiki/Reli%20ya%20Kenya-Uganda
Reli ya Kenya-Uganda
Baada ya azimio la kujenga reli Uingereza iliona haja ya kulinda njia ya reli yenyewe hivyo ikatangaza eneo lote kati ya Mombasa na Uganda kuwa chini ya ulinzi wake kuanzia tar. 01.07.1895. Kwa njia hii mipango ya kujenga reli ilikuwa mwanzo wa koloni ya Afrika ya Mashariki ya Kiingereza iliyokuwa Kenya baadaye.
20231101.sw_2010_7
https://sw.wikipedia.org/wiki/Reli%20ya%20Kenya-Uganda
Reli ya Kenya-Uganda
Mwezi wa Mei 1896 ujenzi ulianzishwa Mombasa chini ya uongozi wa mhandisi George Whitehouse. Alikuwa na bajeti ya BP 3,250,000. Kazi ilionekana ngumu sana kwa sababu ya maeneo magumu kama vile jangwa, kinamasi, milima, Bonde la Ufa na mtelemko wake, kwa ujumla zaidi ya 1000 km.
20231101.sw_2010_8
https://sw.wikipedia.org/wiki/Reli%20ya%20Kenya-Uganda
Reli ya Kenya-Uganda
Waingereza waliamua kuchukua wafanyakazi kutoka Bara Hindi kwa sababu katika majaribio ya kwanza Waingereza hawakuelewana na wenyeji wa pwani ambao waliajiria awali. Kwa ujumla zaidi ya Wahindi 13,000 walichukuliwa kufanya kazi ya reli. Kwa jumla walitoka hasa katika mikoa ya Gujarat na Panjab, na lugha hizi zinatumika hadileo katika Afrika ya Mashariki. Wengi walikuwa wafanyakazi wa mkono,lakini wengine pia mafundi na makarani. Wengi walikufa kwa sababu ya ugumu wa kazi, magonjwa, ajali na wanyama witu kama vile simba walioitwa wala-watu wa Tsavo walioua wafanyakazi 135.
20231101.sw_2010_9
https://sw.wikipedia.org/wiki/Reli%20ya%20Kenya-Uganda
Reli ya Kenya-Uganda
Mwaka 1899 reli ilifika eneo la Nairobi ya leo. Whitehouse aliamua kujenga hapa kambi kubwa kwa sababu mahali palikuwa na maji, tena takriban katikati ya Mombasa na Kampala, halafu kabla ya njia kupanda juu kwa milima inayoongozana na Bonde la Ufa. Kambi hii ilidumu ikawa mji wa Nairobi.
20231101.sw_2010_10
https://sw.wikipedia.org/wiki/Reli%20ya%20Kenya-Uganda
Reli ya Kenya-Uganda
Tar. 20.12.1901 reli imefika Port Florence (leo: Kisumu)ufukoni wa ziwa la Viktoria Nyanza. Kutoka hapa bidhaa zilipelekwa kwa meli hadi Port Bell / Kampala. Njia ya reli yenyewe ilifika Kampala mw. 1931 kutoka Nakuru.
20231101.sw_2010_11
https://sw.wikipedia.org/wiki/Reli%20ya%20Kenya-Uganda
Reli ya Kenya-Uganda
Ni sawa kabisa kusema ya kwamba reli hii ilikuwa mwanzo na mbegu wa Kenya. Biashara ya Uganda haikuleta kabisa faida ya kiuchumi za kurudisha gharama za ujenzi lakini reli ilifungua sehemu kubwa za Kenya kwa ajili ya biashara ikawezesha kilimo ya kibiashara. Hivyo reli ilikuwa msingi kwa ajili ya mipango ya baadaye ya "White Highlands" ya kuunda koloni ya walowezi kama Afrika ya Kusini. Wahindi wengi walibaki wakawa mwanzo wa jumuiya ya Wakenya na Wauganda wenye asili ya kiasia.
20231101.sw_2010_12
https://sw.wikipedia.org/wiki/Reli%20ya%20Kenya-Uganda
Reli ya Kenya-Uganda
Gharama zilikuwa kubwa. Bajeti ya kifedha haikutosha kabisa iliongezeka mara mbili. Gharama za maisha zilikuwa nzito zaidi. Wafanyakazi wahindi walikuwa wa kwanza kulipa bei hiyo. Magonjwa yaliyokuja nao yalisababisha vifo vingi kati ya wenyeji hasa Wakikuyu; makabila kama Wanandi waliopinga ujenzi wa reli yalikandamizwa vikali na Waingereza.
20231101.sw_2011_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/Port%20Bell
Port Bell
Port Bell ni mji mdogo karibu na Kampala/ Uganda ufukoni wa ziwa la Viktoria Nyanza. Jina la mji limetokana na Sir Hesketh Bell aliyekuwa kamishna (gavana) Mwingereza huko Uganda kuanzia mwaka. 1905-1909.
20231101.sw_2011_1
https://sw.wikipedia.org/wiki/Port%20Bell
Port Bell
Kuna viwanda kadhaa kama vile Kiwanda cha Bia cha Uganda Breweries; bia ya Bell Lager inatengenezwa hapa. Kuna pia kiwanda cha pombe kali aina ya Waragi na kiwanda cha chai.
20231101.sw_2012_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/Chad
Chad
Chad (pia: Chadi) ni nchi huru iliyoko Afrika ya Kati. Imepakana na Libya, Sudan, Jamhuri ya Afrika ya Kati, Kamerun, Nigeria na Niger.
20231101.sw_2012_1
https://sw.wikipedia.org/wiki/Chad
Chad
Sehemu kubwa ya eneo lake ni jangwa na nchi yabisi. Kusini kuna kanda lenye hali ya hewa ya kitropiki, lakini ardhi yenye rutuba inayofaa kwa kilimo ni asilimia 3 tu za eneo lake lote .
20231101.sw_2012_2
https://sw.wikipedia.org/wiki/Chad
Chad
Katikati liko beseni la ziwa Chad lililokuwa kati ya maziwa makubwa kabisa duniani lakini limepungua sana, hasa mwishoni mwa karne ya 20.
20231101.sw_2012_3
https://sw.wikipedia.org/wiki/Chad
Chad
Katika historia kabla ya ukoloni watu wa kaskazini waliwafanyia vita watu wa kusini na kuteka wafungwa kama watumwa. Hivyo hadi leo uhusiano kati ya kusini na kaskazini ya nchi ni mgumu.
20231101.sw_2012_4
https://sw.wikipedia.org/wiki/Chad
Chad
Tangu mwaka 2003 petroli imekuwa inaongoza kati ya bidhaa zinazopelekwa nje ya nchi badala ya pamba.
20231101.sw_2012_5
https://sw.wikipedia.org/wiki/Chad
Chad
Tangu mwaka huo Mgogoro wa Darfur nchini Sudan umevuka mpaka na kuvuruga Chad pia. Ikiwa kati ya nchi zinazoongoza duniani kwa ufukara na ufisadi, ilipata shida kupokea wakimbizi kwa mamia elfu.
20231101.sw_2012_6
https://sw.wikipedia.org/wiki/Chad
Chad
Ingawa kulikuwa na vyama vingi vya siasa na mapigano ya kisiasa pamoja na majaribio ya mapinduzi, mamlaka ilibaki imara mikononi mwa Rais Déby na chama chake, Patriotic Salvation Movement, hadi alipouawa mwaka 2021.
20231101.sw_2012_7
https://sw.wikipedia.org/wiki/Chad
Chad
Kaskazini wako hasa watu walioathiriwa sana na utamaduni wa Uislamu (55% za wakazi wote, wengi wakiwa Wasuni). Mifano ni Waarabu (12.3%), Wafulbe, Wahaussa, Wazaghawa na wengineo. Wengi wao walikuwa wafugaji na sehemu ya makabila inaendelea hadi leo maisha ya kuhamahama.
20231101.sw_2012_8
https://sw.wikipedia.org/wiki/Chad
Chad
Kusini wako hasa watu wanaofuata Ukristo (41%, Wakatoliki wakiwa wengi kidogo kuliko Waprotestanti) au dini asilia za Kiafrika (1%) kama Wasara (27.7%). Wengi wao hulima.
20231101.sw_2012_9
https://sw.wikipedia.org/wiki/Chad
Chad
Kwa jumla leo kuna makabila zaidi ya 200 nchini, ambayo hutimia lugha na lahaja zaidi ya 100 (angalia orodha ya lugha hizo). Asili yao ni Afrika Mashariki, Afrika ya Kati, Afrika Magharibi na Afrika Kaskazini vilevile.
20231101.sw_2012_10
https://sw.wikipedia.org/wiki/Chad
Chad
Issa Serge Coelo, cinéaste tchadien: On a encore du travail à faire] [http://www.cefod.org/spip.php?article915
20231101.sw_2012_11
https://sw.wikipedia.org/wiki/Chad
Chad
Botha, D.J.J. (December 1992); "S.H. Frankel: Reminiscences of an Economist", The South African Journal of Economics 60 (4): 246–255.
20231101.sw_2012_12
https://sw.wikipedia.org/wiki/Chad
Chad
Boyd-Buggs, Debra & Joyce Hope Scott (1999); Camel Tracks: Critical Perspectives on Sahelian Literatures. Lawrenceville: Africa World Press. ISBN 0-86543-757-2
20231101.sw_2012_13
https://sw.wikipedia.org/wiki/Chad
Chad
"Chad". Country Reports on Human Rights Practices 2006, 6 March 2007. Bureau of Democracy, Human Rights, and Labor, U.S. Department of State.
20231101.sw_2012_14
https://sw.wikipedia.org/wiki/Chad
Chad
"Chad". Country Reports on Human Rights Practices 2004, 28 February 2005. Bureau of Democracy, Human Rights, and Labor, U.S. Department of State.