_id
stringlengths 15
22
| url
stringlengths 31
150
| title
stringlengths 1
86
| text
stringlengths 100
23.8k
|
---|---|---|---|
20231101.sw_2027_9
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Abu%20Nuwas
|
Abu Nuwas
|
Hadithi zote za "Riwaya" zinasimuliwa katika nchi nyingine kwa majina tofauti. Waturuki humwita "Nasreddin Hodja", Wauzbeki "Hodja" pekee, watu wa Algeria "Ben Sikran", Waarabu wengine "Juba (Guba)", Waitalia wa Kusini "Giufa".
|
20231101.sw_2027_10
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Abu%20Nuwas
|
Abu Nuwas
|
Huko Iraq kumbukumbu ya Abu Nuwas mshairi imechanganywa na hadithi za huyu mjinga mcheshi mwenye hekima anayejulikana katika nchi zote za Mediteraneo na Mashariki ya Kati. Hadithi katika "Riwaya za Abunuwasi“ zinatumia mapokeo ya urithi huo.
|
20231101.sw_2027_11
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Abu%20Nuwas
|
Abu Nuwas
|
Lakini kuna angalau hadithi moja ya Abu Nuwas mwenyewe inayolingana na Abunuwasi wa “Riwaya” – inasaidia kuelewa jinsi gani jina lake limeunganishwa na urithi wa Guba – Nasreddin:
|
20231101.sw_2027_12
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Abu%20Nuwas
|
Abu Nuwas
|
“Abu Nuwas alipenda divai mno. Siku moja alipatikana hali amelewa sana wakati Khalifa Harun ar-Rashid alipita barabarani pamoja na askari zake. Khalifa Harun alimpenda Abu Nuwas mshairi hata aliwahi kukaa naye na kunywa naye lakini aliona hawezi kumruhusu kulewa barabarani mbele ya watu wote asionekane mwenyewe Khalifa anayedharau sharia ya Allah.
|
20231101.sw_2027_13
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Abu%20Nuwas
|
Abu Nuwas
|
Hivyo ar-Rashid akamwendea Abu Nuwas alijeficha chupa nyuma yake akikishika kwa mkono wa kuume. “Unionyeshe mkono wako!” Khalifa alisema.
|
20231101.sw_2027_14
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Abu%20Nuwas
|
Abu Nuwas
|
Abu Nuwas alishika chupa kwa mkono wa kulia nyuma yake akionyesha mkono wa kiume. “Unionyeshe mkono mwingine!” alidai ar-Rashid.
|
20231101.sw_2027_15
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Abu%20Nuwas
|
Abu Nuwas
|
Tena mshairi alishika chupa kwa mkono wa kushoto akimwonyesha Khalifa mkono wa kulia. Akasema ar-Rashid: “Sasa unionyeshe mikono yote miwili!”
|
20231101.sw_2027_16
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Abu%20Nuwas
|
Abu Nuwas
|
Abu Nuwas akakanyaga hatua moja nyuma hadi ukuta wa nyumba akashika chupa kwa matako yake ukutani akimwonyesha Khalifa mikono yote mawili. Huyu alidai akanyage hatua moja mbele.
|
20231101.sw_2027_17
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Abu%20Nuwas
|
Abu Nuwas
|
“Ee amirulmuumina”, akajibu Abu Nuwas, “Wewe unajua ya kwamba chupa kitanguka chini nikitembea kitavunjika !”
|
20231101.sw_2027_18
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Abu%20Nuwas
|
Abu Nuwas
|
Khalifa na askari wote walicheka sana. Abu Nuwas alitegemea kupokea viboko 80 lakini Khalifa alitangaza: “Mwenye akili kama huyu hawezi kuwa mlevi wala siwezi kumwadhibu kwa tendo la kushika chupa tu. Basi aende!"
|
20231101.sw_2027_19
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Abu%20Nuwas
|
Abu Nuwas
|
Ewald Wagner: Abu Nuwas Al-Hasan B. Hani' Al-Hakam, makala katika The Encyclopaedia Of Islam New Edition I, Leiden 1986, uk. 143
|
20231101.sw_2027_20
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Abu%20Nuwas
|
Abu Nuwas
|
Sophia Smith Galer: The Arab poet who worshipped wine, tovuti ya BBC Culture, 14th November 2017, iliangaliwa Januari 2021
|
20231101.sw_2027_21
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Abu%20Nuwas
|
Abu Nuwas
|
Esat Ayyıldız. "Ebû Nuvâs’ın Şarap (Hamriyyât) Şiirleri". Bozok Üniversitesi İlahiyat Fakültesi Dergisi 18 / 18 (2020): 147-173.
|
20231101.sw_2032_0
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Bi%20Kidude
|
Bi Kidude
|
Bi Kidude (jina halisi: Fatuma binti Baraka; amefariki Bububu, Zanzibar, 17 Aprili 2013, akikisiwa kuwa na umri wa miaka 102) alikuwa gwiji wa muziki katika bara la Afrika. Bi Kidude alikuwa msanii mkongwe na mahiri sana katika fani ya muziki wa mwambao ambao hujulikana kwa jina la Taarabu. Muziki huo, ambao ni mchanganyiko wa muziki toka nchi za Kiarabu na vionjo vya muziki wa Kiafrika, umekita sana katika mwambao wa Afrika Mashariki yaani Zanzibar, Mombasa, Lamu na kwingineko.
|
20231101.sw_2032_1
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Bi%20Kidude
|
Bi Kidude
|
Fatuma binti Baraka au Bi Kidude, alizaliwa katika kijiji cha Mfagimarigo Zanzibar katika familia ya watoto saba (7). Baba yake Mzee Baraka alikuwa ni mfanyabiashara wa nazi, zao ambalo ni la kutumainiwa sana Zanzibar. Bi Kidude anasema hafahamu tarehe halisi aliyozaliwa, isipokuwa anachojua ni kwamba alizaliwa wakati rupia ikitumika kama fedha, na vilevile ana hakika ni kabla ya Vita Kuu ya Kwanza ya Ulaya. Wataalamu wa mahesabu baada ya kupata taarifa hizo wakampigia mahesabu na kumkabidhi miaka yake kwamba ni zaidi ya miaka 90.
|
20231101.sw_2032_2
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Bi%20Kidude
|
Bi Kidude
|
Bi Kidude anasema uimbaji aliuanza tangu alipokuwa na umri wa miaka kumi na alijifunza kutoka kwa msanii mkongwe na aliyetamba sana enzi hizo Sitti binti Saad. Anasema wageni wengi kutoka sehemu mbalimbali walikuwa wakifika Zanzibar kuja kumwona Sitti, na kwa vile Bi Kidude na Sitti walikuwa wako karibu basi yeye alikuwa akiwapeleka wageni wale nyumbani kwa Bi Sitti, wakifika huko wageni walikuwa wakiingia ndani na yeye kubakia nje, kule ndani Bi Sitti alikuwa akiwaimbia wale wageni, na yeye huku nje alikuwa akimsikiliza kwa makini na kumfuatiza jinsi alivyokuwa akiimba. Aliendelea hivyo hadi akawa mahiri sana katika uimbaji.
|
20231101.sw_2032_3
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Bi%20Kidude
|
Bi Kidude
|
Alipokuwa na miaka 13, kwa mara ya kwanza alitoroka nyumbani kwao Zanzibar na kukimbilia Tanzania Bara, baada ya kulazimishwa kuolewa. Lakini alipokuwa kigoli wa kutosha kuolewa aliolewa ingawa ndoa hiyo nayo haikudumu kutokana na manyanyaso aliyokuwa akiyapata, hivyo aliamua kukimbilia kaskazini mwa Misri ikiwa ni katika miaka ya 1930, huko aling'ara sana katika fani yake ya uimbaji na uchezaji ngoma. Lakini ilipofika miaka ya 1940 aliamua kurudi nyumbani Zanzibar ambako aliendelea na shughuli zake uimbaji.
|
20231101.sw_2032_4
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Bi%20Kidude
|
Bi Kidude
|
Bi Kidude hategemei kazi moja tu ya kuimba, kwani pia ni mfanyabiashara ya 'wanja' na 'hina' ambavyo anavitengeneza yeye mwenyewe, pia ni mtaalamu wa matibabu kwa dawa za mitishamba na zaidi ya hayo ni mwalimu mzuri sana wa 'Unyago' na ameanzisha chuo chake mwenyewe na anasema katika wanafunzi wake wote hakuna aliyepata talaka kutoka kwa mumewe.
|
20231101.sw_2032_5
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Bi%20Kidude
|
Bi Kidude
|
Watu wanasema 'Utu uzima dawa' Bi Kidude ana upeo mkubwa sana wa akili kwani pamoja na kukulia katika mazingira yaliyogubikwa na tamaduni za kiarabu ambapo mwanamke anatakiwa wakati wote akiwa hadharani ajifunike, Bi Kidude aliliona hili katika upeo mwingine kwamba ni sheria tu ya kitamaduni toka Uarabuni, hivyo aliamua kuvunja sheria hiyo na kuondoa hijabu mwilini mwake, na sasa hivi anavaa kama Mtanzania na si kama Mwarabu. Lakini hakubakia hapo alivunja na miiko mingine zaidi ya kutokunywa na kuvuta, kwani Bi Kidude anakunywa pombe na kuvuta sigara jambo ambalo si kawaida kwa wanawake Zanzibar.
|
20231101.sw_2032_6
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Bi%20Kidude
|
Bi Kidude
|
Bi Kidude amekwisha tembelea nchi nyingi sana ikiwa ni pamoja na Oman, Ufaransa, Hispania, Ufini, Ujerumani na Uingereza.
|
20231101.sw_2032_7
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Bi%20Kidude
|
Bi Kidude
|
Amekwisha pata tuzo mbalimbali ikiwa ni pamoja na ile ya Tamasha la Filamu la Nchi za Jahazi (ZIFF) mwaka 1999 tuzo ni ya maisha. Pia mwaka jana tuzo ya WOMAX ilienda kwake.
|
20231101.sw_2032_8
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Bi%20Kidude
|
Bi Kidude
|
Nyimbo alizowahi kuimba ni pamoja na Muhogo wa jang'ombe, na aliimba kwa Kiswahili na Kiarabu. Hakuwahi kupata elimu nyingine zaidi ya Kurani.
|
20231101.sw_2033_0
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Binyavanga%20Wainaina
|
Binyavanga Wainaina
|
Alizaliwa Nakuru, nchini Kenya. Alihudhuria masomo ya msingi na sekondari nchini Kenya kabla ya kujiunga na Chuo Kikuu cha Transkei, Afrika Kusini.
|
20231101.sw_2033_1
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Binyavanga%20Wainaina
|
Binyavanga Wainaina
|
Baada ya kumaliza masomo yake alihamia katika jiji la Cape Town ambapo alifanya kazi kama mwandishi wa kujitegemea wa masuala ya chakula na utalii.
|
20231101.sw_2033_2
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Binyavanga%20Wainaina
|
Binyavanga Wainaina
|
Mwezi Julai 2002 Binyavanga alishinda Tuzo ya Caine kwa Uandishi wa Kiafrika. Yeye ndiye mwanzilishi wa jarida la fasihi la Kwani?, ambalo linachukuliwa kuwa ndio gazeti kuu la masuala ya fasihi toka Afrika Mashariki.
|
20231101.sw_2033_3
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Binyavanga%20Wainaina
|
Binyavanga Wainaina
|
Aliaandika riwaya yake ya kwanza iitwayo The Fallen World of Appearances. Mwaka 2003 alipata tuzo toka Chama cha Wachapishaji wa Kenya (Kenya Publishers Association) kutokana na juhudi zake za kuendeleza fasihi ya Kenya.
|
20231101.sw_2033_4
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Binyavanga%20Wainaina
|
Binyavanga Wainaina
|
Alisomea shahada ya pili ya Uandishi wa Ubunifu katika Chuo Kikuu cha East Anglia. Kazi zake zimetoka katika magazeti na majarida mbalimbali kama vile National Geographic, The East African, The Sunday Times (ya Afrika Kusini), The Guardian (ya Uingereza).
|
20231101.sw_2033_5
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Binyavanga%20Wainaina
|
Binyavanga Wainaina
|
Beyond the River Yei: Life in the Land Where Sleeping is a Disease (Riwaya ya picha pamoja na Steven Torfinn, Kwani Trust).
|
20231101.sw_2033_6
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Binyavanga%20Wainaina
|
Binyavanga Wainaina
|
Tarehe 1 Disemba 2016, katika siku ya UKIMWI Duniani, Wainaina alitangaza kupitia akaunti yake ya Twitter kwamba amethibitika kuwa na UKIMWI.
|
20231101.sw_2033_7
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Binyavanga%20Wainaina
|
Binyavanga Wainaina
|
Wainaina amefariki dunia baada ya kupata ugonjwa majira ya saa nne usiku ya tarehe 21 Mei, 2019, katika Hospitali ya Aga Khan jijini Nairobi, hiyo ni kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa wanandugu.
|
20231101.sw_2035_0
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mkutano%20huria
|
Mkutano huria
|
Mkutano huria ni mkutano ambao unaendeshwa na wahudhuriaji au wajumbe badala ya mwandaaji au waandaaji wa mkutano. Katika mkutano wa aina hii hakuna watoa mada na wapokea mada, hakuna watoa hotuba na wasikilizaji. Wahudhuriaji wote ndio watoa mada na wapokea mada. Dhana hii imepewa umaarufu na wataalamu wawili wa programu ya tarakilishi, Lenn Pryyor na Dave Winer.
|
20231101.sw_2036_0
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Podikasiti
|
Podikasiti
|
Podikasiti ni neno lililoanza kutumiwa mwaka 2004 pale matumizi ya programu ya RSS ilipoanza kutumiwa kusambaza matangazo kwa ajili ya kusikiliza kupitia tarakilishi au zana nyingine za mkononi kama vile aipodi.
|
20231101.sw_2036_1
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Podikasiti
|
Podikasiti
|
Podikasiti ni mafaili ya video au sauti ambayo yako kwenye mtandao wa tarakilishi kwa ajili ya yeyote yule anayetaka kutazama au kusikiliza. Wana podikasiti wanasambaza kazi zao kwenye tovuti au blogu zao kwa taratibu mbalimbali. Wako wanaoweka mafaili ambayo mtu yeyote anaweza kuyapakua bure au kwa kulipia, lakini kitu kinachofanya podikasiti kuwa tofauti na mafaili, kwa mfano, ya muziki ambayo unaweza kuyapakua na kusikiliza ni kwamba podikasiti inatumia teknolojia ambayo matangazo mapya yanaletwa kwako bila kukuhitahi wewe kwenda kwenye tovuti au blogu ya mwana podikasiti.
|
20231101.sw_2036_2
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Podikasiti
|
Podikasiti
|
Redio nyingi kama vile BBC, NPR (Marekani), hivi sasa zinatuma matangazo yao kwa wasikilizaji kwa kwa kutumia teknolojia ya podikasiti.
|
20231101.sw_2042_0
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mkoa%20wa%20Singida
|
Mkoa wa Singida
|
Mkoa wa Singida ni kati ya mikoa 31 ya Tanzania: mkoa huu upo kanda ya kati, ukipakana na mikoa ya Manyara upande wa kaskazini , Dodoma mashariki, Iringa, Mbeya kusini, Tabora upande wa magharibi na Shinyanga. msimbo wa posta ni 43000.
|
20231101.sw_2042_1
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mkoa%20wa%20Singida
|
Mkoa wa Singida
|
Wakazi wa wilaya za Singida mjini na kijijini ni hasa Wanyaturu. Walio wengi Iramba ndio Wanyiramba na wakiwa Wagogo wengi huko Manyoni. Pia kati ya wenyeji kuna Wanyisanzu na makabila mengine madogo. Makabila hayo wanaishi kwa amani na upendo.
|
20231101.sw_2042_2
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mkoa%20wa%20Singida
|
Mkoa wa Singida
|
Singida ni kati ya maeneo maskini zaidi ya Tanzania. Uchumi wake ni hasa ufugaji: idadi ya ng'ombe hukadiriwa kuwa takribani milioni 1.4. mbali na punda, kondoo, kuku. Masoko hayako karibu na barabara si nzuri.
|
20231101.sw_2042_3
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mkoa%20wa%20Singida
|
Mkoa wa Singida
|
Kilimo si kizuri kwa sababu ya hali ya mvua. Ukame huleta njaa. Singida ni kati ya mikoa inayotegemea misaada ya chakula. Kati ya mazao yapo ya chakula na ya biashara. Mazao yanayolimwa mkoani hapo ni mtama, alzeti, vitunguu, uweli, viazi, mahindi, karanga, maharage n.k.
|
20231101.sw_2042_4
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mkoa%20wa%20Singida
|
Mkoa wa Singida
|
Pamoja na kuwa mkoa wa Singida umekuwa ukikumbwa na njaa kwa sababu ya ukame, na hata pale mvua inaponyesha ni duni sana, una shughuli mbalimbali ambazo zinaingiza kipato kwa watu wa mkoa huo.
|
20231101.sw_2042_5
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mkoa%20wa%20Singida
|
Mkoa wa Singida
|
Ikiwa kuanzia miaka ya 1990 na kuendelea mpaka sasa imekuwa madini ya dhahabu yakigunduliwa katika sehemu mbalimbali mkoani Singida japo kumekuwa aidha hakufanyiwi uchunguzi wa kina kuhakiki kiwango cha hifadhi ya madini iliyopo katika eneo husika au huwa kiwako kilichopo ni kidogo, hivyo kutokuvutia wawekezaji wakubwa katika maeneo hayo. Kati ya madini ambayo yamewahi kugunduliwa katika mkoa wa Singida ni dhahabu ambayo imewahi kugunduliwa huko Londoni na Iruma wilayani Manyoni.
|
20231101.sw_2042_6
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mkoa%20wa%20Singida
|
Mkoa wa Singida
|
Mkoani Singida kuna mapori mengi ya akiba ambayo yamejaa wanyama wa aina nyingi ambao kama mapori hayo yatafanywa kuwa hifadhi kamili za taifa yangesaidia sana kuvutia utalii na kuufanya mkoa wa Singida uongeze pato lake na kupunguza umaskini miongoni mwa wanajamii kwani utatoa ajira kwa jamii inayozunguka hifadhi hizo.
|
20231101.sw_2044_0
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kigermanik
|
Kigermanik
|
Lugha za Kigermanik zenye wasemaji wengi ni Kiingereza (milioni 380) na Kijerumani (milioni 120). Lugha nyingine za Kigermanik ni lugha za Skandinavia, halafu Kiholanzi na Kiafrikaans wa Afrika Kusini.
|
20231101.sw_2044_1
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kigermanik
|
Kigermanik
|
Mwanzo wa lugha hizi uko gizani. Wataalamu wamejaribu kutambua sifa za lugha asilia kwa kulinganisha lugha mbalimbalimbali zilizo karibukaribu ikiwa habari zao zimejulikana.
|
20231101.sw_2044_2
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kigermanik
|
Kigermanik
|
Kutokana na makisio hayo Kigermanik kilianza Ulaya ya Kaskazini, labda Sweden ya Kusini katika miaka elfu ya kwanza K.K..
|
20231101.sw_2044_3
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kigermanik
|
Kigermanik
|
Wasemaji wa Kigermanik walianza kuhamahama wakati wa Dola la Roma na ndipo habari za kwanza za kihistoria zimepatikana.
|
20231101.sw_2044_4
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kigermanik
|
Kigermanik
|
b) Kigermanik ya Magharibi: Kiingereza, Kijerumani (Kidachi), Kiholanzi, Kiafrikaans, Kijerumani ya Kaskazini, Kifrisia, Kiyiddish (Kiyahudi cha Ulaya)
|
20231101.sw_2044_5
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kigermanik
|
Kigermanik
|
c) Kigermanik ya Mashariki: lugha hizi kama Kivandali au Kigoti zimekufa zote zinajulikana kama lugha za kihistoria tu
|
20231101.sw_2048_0
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Uganda
|
Uganda
|
Uganda ni nchi ya Afrika ya Mashariki. Imepakana na Kenya upande wa mashariki, Sudan Kusini upande wa kaskazini, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo upande wa magharibi, Rwanda na Tanzania upande wa kusini.
|
20231101.sw_2048_1
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Uganda
|
Uganda
|
Uganda ni nchi mwanachama wa Jumuiya ya Afrika ya Mashariki na wa miundo mingine mbalimbali ya kimataifa.
|
20231101.sw_2048_2
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Uganda
|
Uganda
|
Jina Uganda lina asili yake katika ufalme wa Buganda ulioko kusini mwa nchi pamoja na mji mkuu, Kampala.
|
20231101.sw_2048_3
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Uganda
|
Uganda
|
Tazama piaː Orodha ya milima ya Uganda; Orodha ya maziwa ya Uganda; Orodha ya visiwa vya Uganda; Wilaya za Uganda
|
20231101.sw_2048_4
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Uganda
|
Uganda
|
Upande wa kusini nchi imepakana na Ziwa Nyanza Viktoria ambalo kwa eneo ndilo ziwa kubwa kuliko yote ya Afrika. Maziwa makubwa mengine upande wa magharibi ni Ziwa Albert na Ziwa Edward.
|
20231101.sw_2048_5
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Uganda
|
Uganda
|
Mto mkubwa ni Nile inayopita nchi yote kati ya Ziwa Viktoria hadi Ziwa Albert na kuendelea hadi mpaka wa Sudani ikiitwa mwanzoni Nile ya Viktoria na baadaye Nile ya Albert.
|
20231101.sw_2048_6
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Uganda
|
Uganda
|
Eneo la Uganda limeona uhamiaji wa vikundi vingi waliowazidi wenyeji asili (walioishi huko tangu miaka 50,000 kama si 100,000 KK).
|
20231101.sw_2048_7
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Uganda
|
Uganda
|
Kusini liliingiliwa hasa na wakulima Wabantu. Kaskazini iliona kufika kwa Waniloti kwa mfano Waluo na baadaye Karimojong.
|
20231101.sw_2048_8
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Uganda
|
Uganda
|
Tangu karne ya 15 himaya mbalimbali zilianza kujengwa na kati ya hizo ni hasa falme za Buganda, Ankole, Bunyoro Toro zilizoendelea kuwa muhimu hadi kuja kwa ukoloni na kwa kiasi fulani kama urithi wa kiutamaduni hata katika Uganda ya kisasa.
|
20231101.sw_2048_9
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Uganda
|
Uganda
|
Karne ya 19 iliona kufika kwanza kwa Waarabu na baadaye kwa Wazungu. Kila mmoja alileta dini yake yaani Uislamu na Ukristo wa Kikatoliki na wa Kianglikana.
|
20231101.sw_2048_10
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Uganda
|
Uganda
|
Katika mashindano juu ya Afrika ya Kati Waingereza walifaulu katika kushindana na Waarabu, Wafaransa na Wajerumani. Walienea kwa mapatano na Buganda wakisaidiana kukomesha upinzani kutoka falme za jirani.
|
20231101.sw_2048_11
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Uganda
|
Uganda
|
Baadaye Waingereza walikuwa na nguvu ya kutosha kuamua hata mambo ya ndani ya Buganda wakatangaza Uganda wote kuwa nchi lindwa tangu mwaka 1894.
|
20231101.sw_2048_12
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Uganda
|
Uganda
|
Serikali ya Obote ilipinduliwa na mkuu wa jeshi Idi Amini mwaka 1971. Utawala wake ulikuwa kipindi cha udikteta ulioharibu uchumi wa nchi na misingi ya dola. Takriban watu 300,000 waliuawa chini ya Amin ama wapinzani wa siasa yake ama watu wa makabila yaliyotazamwa kuwa maadui wa serikali. Raia wenye asili ya Asia walifukuzwa katika nchi na mali yao yote kutwaliwa na serikali.
|
20231101.sw_2048_13
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Uganda
|
Uganda
|
Mwaka 1978 vikosi vya jeshi la Uganda viliingia Tanzania na kuvamia maeneo ya mpakani kaskazini kwa mto Kagera. Mwaka 1979 Tanzania ilijibu kwa njia ya vita na jeshi lake pamoja na wapinzani wa Uganda walishinda jeshi la Amin na kumfukuza dikteta nchini. Rais wa baadaye Yoweri Museveni alikuwako kati ya wanamgambo waliosaidiana na Watanzania.
|
20231101.sw_2048_14
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Uganda
|
Uganda
|
Uchaguzi wa mwaka 1980 ulimrudisha madarakani Milton Obote aliyeanzisha upya udikteta na kuua watu ovyo. Wapinzani wake wakiongozwa na Museveni walirudi porini wakashika silaha. Katika vita vya wenyewe kwa wenyewe kundi la Museveni likashinda na kutwaa serikali tangu mwaka 1986.
|
20231101.sw_2048_15
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Uganda
|
Uganda
|
Mwaka 2005 ulikuwa na uchaguzi wa vyama vingi wa kwanza. Museveni alipata kibali cha bunge kwa badiliko la katiba lililomruhusu kugombea urais tena mwaka 2006 akachaguliwa mara ya tatu.
|
20231101.sw_2048_16
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Uganda
|
Uganda
|
Wakazi wa Uganda wameongezeka kutoka 9,500,000 (1969) hadi 34,634,650 (2014), hivyo wengi wao ni vijana kuliko nchi zote duniani. Umri wa wastani ni miaka 15 tu.
|
20231101.sw_2048_17
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Uganda
|
Uganda
|
Makabila makubwa ni Waganda (16.9%), Wanyankole (8.5%), Wanyoro (7.7%), Wasoga (7.4%), Walangi (7.1%), Wakiga (6.9%), Wateso (6.4%), Waacholi (5.7%), Wagisu (4.6%), Walugbara (4.2%). Wengineo ni 33.6%.
|
20231101.sw_2048_18
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Uganda
|
Uganda
|
Nchini kuna lugha asilia 40 hivi, ambazo zinagawanyika katika makundi makubwa mawili: lugha za Kibantu upande wa kusini na lugha za Kinilo-Sahara upande wa kaskazini. Pia kuna lugha za Kisudani na lugha za Kikuliak. Hata hivyo lugha rasmi ni Kiingereza na Kiswahili.
|
20231101.sw_2048_19
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Uganda
|
Uganda
|
Upande wa dini, kadiri ya sensa ya mwaka 2014, 84.5% za wakazi wanafuata Ukristo, hasa katika madhehebu ya Kikatoliki (39.3%) na ya Kianglikana (32%), halafu Wapentekoste (11.1%) na mengineyo. Waislamu ni 13.7%, wengi wao wakiwa Wasuni. Wanaoendelea kufuata dini asilia za Kiafrika ni 0.1% tu.
|
20231101.sw_2048_20
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Uganda
|
Uganda
|
Appiah, Anthony and Henry Louis Gates (ed). Encyclopaedia of Africa (2010). Oxford University Press.
|
20231101.sw_2048_21
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Uganda
|
Uganda
|
Chrétien, Jean-Pierre. The great lakes of Africa: two thousand years of history (2003). New York: Zone Books.
|
20231101.sw_2048_22
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Uganda
|
Uganda
|
Jagielski, Wojciech and Antonia Lloyd-Jones. The night wanderers: Uganda's children and the Lord's Resistance Army. (2012). New York: Seven Stories Press. ISBN 9781609803506
|
20231101.sw_2050_0
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mkoa%20wa%20Iringa
|
Mkoa wa Iringa
|
Mkoa wa Iringa ni mojawapo kati ya mikoa 31 ya Tanzania wenye Postikodi namba 51000. Upo katikati ya nchi, kidogo upande wa kusini. Umepakana na mikoa ya jirani ya Morogoro, Njombe, Mbeya, Singida na Dodoma.
|
20231101.sw_2050_1
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mkoa%20wa%20Iringa
|
Mkoa wa Iringa
|
Mkoa wa Iringa uko katika Nyanda za Juu za Kusini mwa Tanzania na kupakana na ukanda mkavu wa kati wa Tanzania upande wa kaskazini.
|
20231101.sw_2050_2
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mkoa%20wa%20Iringa
|
Mkoa wa Iringa
|
Hadi mwaka 2012 Mkoa wa Iringa ulikuwa na eneo lenye ukubwa wa jumla ya km² 58,936. Wastani wa asilimia 74 ya eneo hili linafaa kwa shughuli za kilimo ambalo ni sawa na km² 43,935. Eneo linalobakia la km² 15,001 ni eneo la maji, hifadhi ya mbuga za wanyama milima na misitu.
|
20231101.sw_2050_3
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mkoa%20wa%20Iringa
|
Mkoa wa Iringa
|
Tangu mwaka 2012 wilaya tatu za kusini zimetengwa na Iringa na kuwa mkoa mpya (Mkoa wa Njombe) kwa hiyo eneo la Iringa limepungua kilomita za mraba 21,347.
|
20231101.sw_2050_4
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mkoa%20wa%20Iringa
|
Mkoa wa Iringa
|
Mwaka 2022 kulikuwa na wakazi 1.192,728 katika wilaya zifuatazo: Iringa Vijijini (wakazi 254,032), Mufindi (wakazi 265,829), Kilolo (wakazi 218,130), Iringa Mjini (wakazi 151,345), na Mafinga Mjini (wakazi 51,902).
|
20231101.sw_2050_5
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mkoa%20wa%20Iringa
|
Mkoa wa Iringa
|
Wenyeji wa mkoa ni hasa Wahehe; wengine wanatokea makabila ya jirani kama Wabena, Wakinga, Wapangwa, Wasangu, Wawanji, Wagogo n.k.
|
20231101.sw_2055_0
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mkoa%20wa%20Dar%20es%20Salaam
|
Mkoa wa Dar es Salaam
|
Dar es Salaam ni kati ya mikoa 31 ya Tanzania. Umepakana na Mkoa wa Pwani pande zote barani na Bahari ya Hindi upande wa mashariki.
|
20231101.sw_2055_1
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mkoa%20wa%20Dar%20es%20Salaam
|
Mkoa wa Dar es Salaam
|
Eneo la mkoa ni jiji la Dar es Salaam ambalo ndilo kitovu cha shughuli za biashara (na za utawala, kwa kiasi fulani) nchini Tanzania, na ni kati ya majiji yanayokua haraka zaidi duniani.
|
20231101.sw_2055_2
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mkoa%20wa%20Dar%20es%20Salaam
|
Mkoa wa Dar es Salaam
|
Ni km² 1,800 pamoja na visiwa vidogo 8 na eneo la bahari kati ya pwani na visiwa hivi. Eneo la nchi kavu pekee ni km² 1,393.
|
20231101.sw_2055_3
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mkoa%20wa%20Dar%20es%20Salaam
|
Mkoa wa Dar es Salaam
|
Kuna wilaya tano: Kinondoni (wakazi 1,775,049), Ilala (wakazi 1,220,611) na Temeke (wakazi 1,368,881) ambazo zimeongezewa Kigamboni na Ubungo. Kila moja inaangaliwa kama mji. Takwimu hizi ni za mwaka 2012, kwa ujumla idadi ya wakazi ilikuwa 5,383,728.
|
20231101.sw_2055_4
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mkoa%20wa%20Dar%20es%20Salaam
|
Mkoa wa Dar es Salaam
|
Wakazi asili wa eneo la mkoa walikuwa Wazaramo pamoja na makabila madogo kama vile Wandengereko na Wakwere. Kutokana na kukua na kupanuka kwa jiji kuna makabila yote ya Tanzania.
|
20231101.sw_2059_0
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mkoa%20wa%20Dodoma
|
Mkoa wa Dodoma
|
Mkoa wa Dodoma ni kati ya mikoa 31 ya Tanzania wenye postikodi namba 41000. Uko katikati ya nchi na umepakana na mikoa ya Manyara, Morogoro, Iringa na Singida.
|
20231101.sw_2059_1
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mkoa%20wa%20Dodoma
|
Mkoa wa Dodoma
|
Eneo lote la mkoa lina km² 41,310. Sehemu kubwa ni nyanda za juu kati ya mita 830 hadi 2000 juu ya UB.
|
20231101.sw_2059_2
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mkoa%20wa%20Dodoma
|
Mkoa wa Dodoma
|
Kuna wilaya saba zifuatazo: Wilaya ya Bahi, Wilaya ya Chamwino, Wilaya ya Chemba, Wilaya ya Dodoma Mjini, Wilaya ya Kondoa, Wilaya ya Kongwa, Wilaya ya Mpwapwa. Wilaya ya awali ya Dodoma Vijijini imegawiwa kwa wilaya mpya za Chamwino na Bahi. Mnamo Machi 2012 ilianzishwa wilaya mpya ya Chemba.
|
20231101.sw_2059_3
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mkoa%20wa%20Dodoma
|
Mkoa wa Dodoma
|
Mawasiliano ni mazuri kwa barabara ya lami kuanzia mji wa Dodoma kwenda Morogoro - Daressalaam, barabara zingine ni za udongo to pamoja na njia kuu kuelekea Tanzania ya Magharibi - Rwanda - Kongo. Pia hali ya barabara ya kale ya "Cape - Cairo" inayovuka Dodoma kutoka kazkazini (Arusha - Kondoa ) kwenda kusini ni nzuri kwa kiwango cha lami. Kuna pia njia ya Reli ya Kati kutoka Daressalaam kwenda Kigoma yenye matatizo ya mara kwa mara. Dodoma mjini kuna uwanja wa kitaifa wa ndege.
|
20231101.sw_2059_4
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mkoa%20wa%20Dodoma
|
Mkoa wa Dodoma
|
Kwa jumla Dodoma haina mvua nyingi isipokuwa sehemu za wilaya za Mpwapwa na Kondoa. Hivyo hasa mazao yasiyotegemea sana mvua hulimwa kama vile mtama, wimbi, muhogo; kilimo cha mahindi hupatikana mara kwa mara na matatizo ya kukosa mvua. Mazao ya sokoni ni karanga alizeti na simsim. Dodoma ni pia mwanzo wa ustawishaji wa mizabibu na uzalishaji wa divai katika Tanzania.
|
20231101.sw_2059_5
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mkoa%20wa%20Dodoma
|
Mkoa wa Dodoma
|
Kutokana na hali ya hewa mifugo ni mingi (ng'ombe 1,600,000, mbuzi 954,000, kondoo 274,000, nguruwe 23,000, kuku takriban 1,400,000). Idadi ya mifugo imeongeza tatizo la mmomonyoko wa ardhi katika sehemu za mkoa.
|
20231101.sw_2059_6
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mkoa%20wa%20Dodoma
|
Mkoa wa Dodoma
|
Kondoa kuna Warangi na pia Wasandawe wanaotumia lugha ya aina ya Khoikhoi. Babu zao wamewahi kukaa eneo la Tanzania kabla ya kuingia kwa Wabantu. Kondoa kuna pia sehemu penye michoro ya kale juu ya uso ya miamba ya aina ya Khoikhoi inayofanana na sanaa ya kale huko Zimbabwe au Afrika Kusini.
|
20231101.sw_2060_0
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kiyunani
|
Kiyunani
|
Kiyunani ni jina la Kiswahili cha zamani kwa "Kigiriki", ambayo ni lugha ya nchi ya Ugiriki ("Uyunani") au kwa tabia za Wagiriki ("Wayunani").
|
20231101.sw_2060_1
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kiyunani
|
Kiyunani
|
Neno la Kiswahili cha zamani limetokana na lugha ya Kiarabu ambapo يونان yunan linataja kiasili Wagiriki wa eneo la Ionia au wa kabila la Waioni walioishi kwenye pwani ya mashariki ya Bahari ya Aegeis.
|
20231101.sw_2060_2
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kiyunani
|
Kiyunani
|
Leo hii si la kawaida sana, lakini linapatikana bado, hasa katika matoleo mbalimbali ya Biblia. Kwa kuwa kitabu hicho kina miaka 2000-3000 hivi, ni wazi kwamba kinasimulia mambo ya zamani, hivyo pengine neno Kiyunani linatafsiriwa kuwa Kigiriki cha zamani, na Uyunani kuwa Ugiriki ya Kale.
|
20231101.sw_2060_3
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kiyunani
|
Kiyunani
|
Ni kwamba miaka ya nyuma neno "Kigiriki" limezidi kusambaa zaidi kati ya wanaoongea Kiswahili, kutokana na athira ya Kiingereza kinachotumia maneno "Greece, Greek" kutoka Kilatini "Graeci", ambayo ni kawaida katika lugha nyingi za Kiulaya.
|
20231101.sw_2062_0
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Roma%20%28maana%29
|
Roma (maana)
|
Roma (pia: Rumi) ni jina linalotumika kwa mji wa Roma (mji mkuu wa Italia), ama kwa dola la Roma lililokuwa kwa karne kadhaa kabla na baada ya Kristo dola kubwa kuliko zote duniani, tena kwa Kanisa la Roma ambalo ni kiini cha Kanisa Katoliki lote. Lilikuwa pia jina la mungu wa kike katika dini ya Roma ya Kale.
|
20231101.sw_2062_1
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Roma%20%28maana%29
|
Roma (maana)
|
Roma ni umbo asili la jina katika Kilatini na Kiitalia; limekuwa pia la kawaida katika Kiswahili cha kisasa.
|
20231101.sw_2062_2
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Roma%20%28maana%29
|
Roma (maana)
|
Kumbe "Rumi" ilikuwa kawaida katika Kiswahili cha zamani kutokana na kawaida ya lugha ya Kiarabu (الرُّومُ ar-Rūm).
|
20231101.sw_2062_3
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Roma%20%28maana%29
|
Roma (maana)
|
Matoleo ya Biblia ya "Union Version" iliyochapishwa tangu 1952 hutumia "Rumi", "Warumi". Kumbe tafsiri ya Biblia ya "Kiswahili cha Kisasa" hutumia "Roma", "Waroma".
|
20231101.sw_2062_4
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Roma%20%28maana%29
|
Roma (maana)
|
Dola la Roma, dola kubwa katika eneo lote kandokando ya Mediteraneo (Ulaya ya Kusini na magharibi, Asia ya Magharibi, Afrika ya Kaskazini) mnamo miaka 2400-1600 iliyopita. Liliendelea katika Dola ya Roma ya Mashariki au Bizanti hadi mwaka 1453 B.K..
|
20231101.sw_2062_5
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Roma%20%28maana%29
|
Roma (maana)
|
Miji mingine inayoitwa kwa jina la "Roma" iko Australia, Ecuador na Marekani; pia ni jina la eneo ndani ya mji wa Mexiko.
|
20231101.sw_2062_6
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Roma%20%28maana%29
|
Roma (maana)
|
Kanisa la Roma ni jina la jimbo ambalo majimbo yote ya Kanisa Katoliki yanalitegemea ili kudumisha umoja wa imani na upendo duniani kote. Kwa sababu hiyo jina hilo linatumika pia kumaanisha Kanisa Katoliki lote. Kwa mfano, mtu akisema, "Mimi nasali Roma", anamaanisha kuwa ni muumini wa Kanisa hilo.
|
20231101.sw_2062_7
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Roma%20%28maana%29
|
Roma (maana)
|
21 Aprili 753 KK ndiyo tarehe ya kimapokeo ambayo mji huo ulisemekana kuundwa na mapacha Romulo na Remo. Ukweli ni kwamba ulianzishwa mapema zaidi (1000 K.K. hivi).
|
Subsets and Splits
No community queries yet
The top public SQL queries from the community will appear here once available.