_id
stringlengths
15
22
url
stringlengths
31
150
title
stringlengths
1
86
text
stringlengths
100
23.8k
20231101.sw_3313_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/Tsung-Dao%20Lee
Tsung-Dao Lee
Tsung-Dao Lee (amezaliwa 25 Novemba 1926) alikuwa mwanafizikia kutoka nchi ya China; baadaye alihamia Marekani. Hasa alichunguza vipande vya atomu na nadharia yake. Mwaka wa 1957, pamoja na Chen Ning Yang alikuwa mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Fizikia.
20231101.sw_3314_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/Chen%20Ning%20Yang
Chen Ning Yang
Chen Ning Yang (amezaliwa 22 Septemba 1922) alikuwa mwanafizikia kutoka nchi ya China; baadaye alihamia Marekani. Pia alijiita Frank Yang. Hasa alichunguza vipande vya atomu na nadharia yake. Mwaka wa 1957, pamoja na Tsung-Dao Lee alikuwa mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Fizikia.
20231101.sw_3317_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/John%20Steinbeck
John Steinbeck
John Ernst Steinbeck (27 Februari 1902 – 20 Desemba 1968) alikuwa mwandishi hodari kutoka nchi ya Marekani. Anajulikana hasa kwa riwaya yake “Zabibu za Hasira” (kwa Kiingereza: Grapes of Wrath) iliyotolewa mwaka wa 1939; akatuzwa Tuzo ya Pulitzer ya Bunilizi kwa riwaya hiyo mwaka wa 1940. Mwaka wa 1962 alikuwa mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Fasihi.
20231101.sw_3319_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/Herman%20Wouk
Herman Wouk
Herman Wouk (amezaliwa 27 Mei 1915) ni mwandishi kutoka nchi ya Marekani. Anajulikana hasa kwa riwaya zake zinazoeleza hali ya Vita Kuu ya Pili ya Dunia. Mwaka wa 1952 alikuwa mshindi wa Tuzo ya Pulitzer ya Bunilizi kwa riwaya yake The Caine Mutiny.
20231101.sw_3320_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/Allen%20Drury
Allen Drury
Allen Stuart Drury (2 Septemba 1918 – 2 Septemba 1998) alikuwa mwandishi wa habari kutoka nchi ya Marekani. Mwaka wa 1960 alikuwa mshindi wa Tuzo ya Pulitzer ya Bunilizi kwa ajili ya riwaya yake ya kwanza “Shauri ukakubali” (kwa Kiingereza: Advise and Consent).
20231101.sw_3322_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/Theodor%20Seuss%20Geisel
Theodor Seuss Geisel
Theodor Seuss Geisel (2 Machi 1904 – 24 Septemba 1991) alikuwa mwandishi na mchoraji vielezo kutoka nchi ya Marekani. Anajulikana hasa kwa vitabu vyake kwa watoto alivyoviandika chini ya jina la Dr. Seuss.
20231101.sw_3324_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/James%20Kirkwood
James Kirkwood
James Kirkwood (22 Agosti 1924 – 21 Aprili 1989) alikuwa mchezaji na mwandishi wa michezo ya kuigiza kutoka nchi ya Marekani. Anajulikana hasa kwa kuandika, pamoja na Nicholas Dante, igizo lenye muziki liitwalo kwa Kiingereza A Chorus Line lililotolewa 1975. Mwaka wa 1976 alikuwa mshindi wa Tuzo ya Pulitzer ya Tamthiliya kwa ajili ya igizo hilo.
20231101.sw_3325_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/Alice%20Walker
Alice Walker
Alice Malsenior Walker (amezaliwa 9 Februari 1944) ni mwandishi wa kike kutoka nchi ya Marekani. Aliandika hasa riwaya na mashairi yanayoonyesha hali ya Wamarekani-Waafrika. Anajulikana hasa kwa riwaya yake “Rangi ya Zambarau” (kwa Kiingereza: The Color Purple) iliyotolewa 1982. Mwaka wa 1983 alikuwa mshindi wa Tuzo ya Pulitzer ya Bunilizi kwa ajili ya riwaya hiyo.
20231101.sw_3327_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/Sam%20Shepard
Sam Shepard
Samuel Shepard Rogers (5 Novemba 1943 - 27 Julai 2017) alikuwa mchezaji na mwandishi wa michezo ya kuigiza kutoka nchi ya Marekani. Anajulikana hasa kwa jina la Sam Shepard.
20231101.sw_3327_1
https://sw.wikipedia.org/wiki/Sam%20Shepard
Sam Shepard
Mwaka wa 1979 alikuwa mshindi wa Tuzo ya Pulitzer ya Tamthiliya kwa ajili ya tamthiliya yake iitwayo kwa Kiingereza Burning Child.
20231101.sw_3329_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/William%20Inge
William Inge
William Motter Inge (3 Mei 1913 – 10 Juni 1973) alikuwa mwandishi wa michezo ya kuigiza kutoka nchi ya Marekani. Mwaka wa 1954 alikuwa mshindi wa Tuzo ya Pulitzer ya Tamthiliya kwa ajili ya tamthiliya yake iitwayo kwa Kiingereza Picnic.
20231101.sw_3331_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/Edward%20Albee
Edward Albee
| anajulikana kwa = ''Who's Afraid of Virginia Woolf?'The Zoo StoryThe American DreamThe Goat, or Who is Sylvia?
20231101.sw_3331_1
https://sw.wikipedia.org/wiki/Edward%20Albee
Edward Albee
}}Edward Franklin Albee (12 Machi, 1928 - 16 Septemba, 2016) alikuwa mwandishi wa tamthiliya kutoka nchi ya Marekani. Anajulikana hasa kwa tamthiliya yake “Nani Anaogopa Virginia Woolf?” (kwa Kiingereza: Who’s Afraid of Virginia Woolf?) iliyotolewa 1962. Kwa ajili ya tamthiliya zake za baadaye alikuwa mshindi wa Tuzo ya Pulitzer ya Tamthiliya''' miaka ya 1967, 1976 na 1992.
20231101.sw_3333_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/Robert%20Sherwood
Robert Sherwood
Robert Emmet Sherwood (4 Aprili 1896 – 14 Novemba 1955) alikuwa mwandishi wa michezo ya kuigiza kutoka nchi ya Marekani. Anajulikana hasa kwa tamthiliya zake zinazojishughulikia na shida za kijamii na za kisiasa. Alipokea Tuzo ya Pulitzer ya Tamthiliya mara tatu: 1936, 1939 na 1941. Tena alipokea Tuzo ya Pulitzer ya Wasifu mwaka wa 1949 kwa kitabu chake Roosevelt and Hopkins.
20231101.sw_3335_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/William%20Saroyan
William Saroyan
William Saroyan (31 Agosti 1908 – 18 Mei 1981) alikuwa mwandishi kutoka nchi ya Marekani. Aliandika hasa mikusanyiko ya hadithi, tamthiliya na riwaya. Mwaka wa 1940 aliteuliwa kuwa mshindi wa Tuzo ya Pulitzer ya Tamthiliya kwa ajili ya tamthiliya yake “Wakati wa Maisha Yako” (kwa Kiingereza: The Time of Your Life). Lakini alikataa kupokea tuzo hiyo.
20231101.sw_3336_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/Thornton%20Wilder
Thornton Wilder
Thornton Niven Wilder (17 Aprili 1897 – 7 Desemba 1975) alikuwa mwandishi kutoka nchi ya Marekani. Aliandika riwaya na tamthiliya. Mwaka wa 1928 alituzwa Tuzo ya Pulitzer ya Bunilizi kwa riwaya yake The Bridge of San Luis Rey. Tena alituzwa Tuzo ya Pulitzer ya Tamthiliya mara mbili, 1938 na 1943. Anajulikana hasa kwa tamthiliya yake iitwayo kwa Kiingereza The Matchmaker. Ilitolewa mwaka wa 1954, na 1964 ilibadilishwa kuwa igizo la muziki chini ya jina Hello, Dolly!.
20231101.sw_3338_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/James%20Michener
James Michener
James Albert Michener (3 Februari 1907 – 16 Oktoba 1997) alikuwa mwandishi kutoka nchi ya Marekani. Aliandika hasa riwaya zinazoeleza historia ya nchi au eneo la dunia. Mwaka wa 1948 alikuwa mshindi wa Tuzo ya Pulitzer ya Bunilizi kwa ajili ya mkusanyiko wake “Hadithi za Pasifiki ya Kusini” (kwa Kiingereza: Tales of the South Pacific) iliyoandikwa mwaka wa 1947.
20231101.sw_3341_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/William%20Carlos%20Williams
William Carlos Williams
William Carlos Williams (17 Septemba 1883 – 4 Machi 1963) alikuwa mwandishi na mshairi kutoka nchi ya Marekani. Pamoja na kufanya kazi kama daktari, aliandika mashairi, insha za historia na riwaya fupi. Mwaka wa 1963 wakati alipokuwa ameshafariki aliteuliwa kuwa mshindi wa Tuzo ya Pulitzer ya Ushairi kwa ajili ya mkusanyiko wake “Picha za Brueghel, na Mashairi Mengine” (kwa Kiingereza: Pictures from Brueghel, and Other Poems) iliyotolewa mwaka wa 1962.
20231101.sw_3342_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/Joseph%20Pulitzer
Joseph Pulitzer
Joseph Pulitzer (10 Aprili 1847 – 29 Oktoba 1911) alikuwa mhariri wa magazeti nchini Marekani; lakini alizaliwa nchi ya Hungaria. Alinunua magazeti mbalimbali na kusimamia uhariri wao.
20231101.sw_3342_1
https://sw.wikipedia.org/wiki/Joseph%20Pulitzer
Joseph Pulitzer
Katika hati ya wasia yake alisaidia kuanzisha Idara ya Uandikaji Habari ndani ya Chuo Kikuu cha Columbia iliyofunguliwa mwaka wa 1912.
20231101.sw_3343_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/Tuzo%20ya%20Pulitzer
Tuzo ya Pulitzer
Tuzo ya Pulitzer ni tuzo iliyoanzishwa na Joseph Pulitzer katika hati ya wasia yake. Tangu mwaka wa 1917 imetolewa kila mwaka na Chuo Kikuu cha Columbia katika mji wa New York kwa ajili ya maandishi hodari yanayoendeleza uandikaji habari na fasihi ya Marekani kwa jumla.
20231101.sw_3346_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/Maputo
Maputo
Maputo ni mji mkuu wa Msumbiji. Hadi 1976 ilijulikana kwa jina la Kireno la Lourenço-Marquès. Serikali mpya ya Msumbiji huru chini ya rais Samora Machel iliipa jina jipya la Maputo.
20231101.sw_3346_1
https://sw.wikipedia.org/wiki/Maputo
Maputo
Mji una wakazi 1,200,000 (pamoja na mitaa ya nje: 1,800,000). Uchumi wake unategemea sana bandari yake kwenye hori ya Maputo ya Bahari Hindi.
20231101.sw_3348_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/Randal%20Cremer
Randal Cremer
Randal Cremer (18 Machi 1838 – 22 Julai 1908) alikuwa kiongozi wa chama cha wafanyakazi kutoka nchi ya Uingereza.
20231101.sw_3348_1
https://sw.wikipedia.org/wiki/Randal%20Cremer
Randal Cremer
Anajulikana pia kwa maandishi yake yaliyojaribu kuzuia vita. Mwaka wa 1903 alikuwa mshindi wa Tuzo ya Nobel kwa Amani. Mwaka wa 1907 alipewa cheo cha “Sir” cha Uingereza.
20231101.sw_3350_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/Fr%C3%A9d%C3%A9ric%20Passy
Frédéric Passy
Frédéric Passy (20 Mei 1822 – 12 Juni 1912) alikuwa mtaalamu wa uchumi kutoka nchi ya Ufaransa. Anajulikana hasa kwa maandishi yake yaliyojaribu kuzuia vita. Mwaka wa 1901, pamoja na Henri Dunant, alikuwa mshindi wa Tuzo ya Nobel kwa Amani.
20231101.sw_3352_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/Auguste%20Beernaert
Auguste Beernaert
Auguste Marie Francois Beernaert (26 Julai 1829 – 6 Oktoba 1912) alikuwa mwanasheria na mwanasiasa kutoka nchi ya Ubelgiji. Kuanzia 1884 hadi 1894 alikuwa Waziri Mkuu na Waziri wa Fedha. Baadaye alikuwa mwakilishi wa Ubelgiji kwenye mikutano ya amani iliyofanyika katika mji wa The Hague mwaka wa 1899 na wa 1907. Mwaka wa 1909, pamoja na Paul d’Estournelles alikuwa mshindi wa Tuzo ya Nobel kwa Amani.
20231101.sw_3354_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/Tobias%20Asser
Tobias Asser
Tobias Michael Carel Asser (28 Aprili 1838 – 29 Julai 1913) alikuwa mwanasheria kutoka nchi ya Uholanzi. Alikuwa profesa wa sheria kwenye Chuo Kikuu cha Amsterdam. Mwaka wa 1899 na tena 1907 alikuwa mwakilishi wa Uholanzi kwenye mikutano ya amani iliyofanyika katika mji wa The Hague. Mwaka wa 1911, pamoja na Alfred Fried alikuwa mshindi wa Tuzo ya Nobel kwa Amani.
20231101.sw_3356_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/Leo%20Sowerby
Leo Sowerby
Leo Sowerby (1 Mei 1895 – 7 Julai 1968) alikuwa mtungaji muziki, mpiga kinanda na mwalimu wa muziki kutoka nchi ya Marekani. Alifundisha na kupiga kinanda hasa katika mji wa Chicago. Mwaka wa 1946 alikuwa mshindi wa Tuzo ya Pulitzer ya Muziki ya muziki kwa utungaji wake wa “Wimbo ya Jua” (kwa Kiingereza Canticle of the Sun).
20231101.sw_3357_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/Thomas%20Aquinas%20Mtakatifu
Thomas Aquinas Mtakatifu
Mtakatifu Thomas Aquinas (Roccasecca, katika eneo la watawala wa Aquino, leo katika wilaya ya Frosinone, Italia, 1224 au 1225 - Fossanova, wilaya ya Latina, Italia, 7 Machi 1274) alikuwa mtawa wa Shirika la Wahubiri na padri wa Kanisa Katoliki.
20231101.sw_3357_1
https://sw.wikipedia.org/wiki/Thomas%20Aquinas%20Mtakatifu
Thomas Aquinas Mtakatifu
Mnyofu, mkimya, aliyekuwa tayari kutumikia, kiutu alipendwa na wote, naye alipendelea watu wa chini, akihubiria mafukara kwa usahili na wema hata zaidi ya mara moja kwa siku.
20231101.sw_3357_2
https://sw.wikipedia.org/wiki/Thomas%20Aquinas%20Mtakatifu
Thomas Aquinas Mtakatifu
Kuliko wengine wote, Thoma aliona elimu na masomo kama njia ya kufikia utakatifu; ni kati ya watu bora upande wa nadharia, hasa wa teolojia ya shule, iliyofikia kilele chake katikati ya karne XIII.
20231101.sw_3357_3
https://sw.wikipedia.org/wiki/Thomas%20Aquinas%20Mtakatifu
Thomas Aquinas Mtakatifu
Mwanafunzi wa Alberto Mkuu, alitumia hasa mawazo ya mwanafalsafa wa Ugiriki Aristoteli na ya Waarabu waliomtafsiri, lakini pia ya Plato: ili kufafanua imani, alikubali ukweli ulioweza kutolewa na yeyote, kwa sababu kweli zote zinatoka kwa Mungu; kinyume chake alikanusha udanganyifu wowote.
20231101.sw_3357_4
https://sw.wikipedia.org/wiki/Thomas%20Aquinas%20Mtakatifu
Thomas Aquinas Mtakatifu
Hivyo aliweza kufanya usanisi mpana ambao mpaka leo Kanisa Katoliki linautambua kama tokeo bora la mafundisho yake lenyewe na kama kielelezo cha namna ya kufikiri na ya kufanya teolojia.
20231101.sw_3357_5
https://sw.wikipedia.org/wiki/Thomas%20Aquinas%20Mtakatifu
Thomas Aquinas Mtakatifu
Anajulikana hasa kwa vitabu vyake “Jumla ya Teolojia” (kwa Kilatini Summa theologiae) na “Jumla dhidi ya Wapagani” (kwa Kilatini Summa contra gentiles).
20231101.sw_3357_6
https://sw.wikipedia.org/wiki/Thomas%20Aquinas%20Mtakatifu
Thomas Aquinas Mtakatifu
Alitangazwa na Papa Yohane XXII kuwa mtakatifu tarehe 18 Julai 1323, halafu na Papa Pius V kuwa mwalimu wa Kanisa mwaka 1568. Kwa Kilatini anaitwa Doctor Angelicus (Mwalimu wa Kimalaika) au Doctor Communis (Mwalimu wa wote).
20231101.sw_3357_7
https://sw.wikipedia.org/wiki/Thomas%20Aquinas%20Mtakatifu
Thomas Aquinas Mtakatifu
Alizaliwa na Landolfo, sharifu mwenye asili ya Kilombardi, na mke wake, Teodora, katika ngome ya familia yao.
20231101.sw_3357_8
https://sw.wikipedia.org/wiki/Thomas%20Aquinas%20Mtakatifu
Thomas Aquinas Mtakatifu
Akiwa mtoto wa miaka 5 tu, alitumwa kuishi na Wabenedikto katika abasia jirani ya Monte Cassino ili apate malezi ya msingi kwa watawa.
20231101.sw_3357_9
https://sw.wikipedia.org/wiki/Thomas%20Aquinas%20Mtakatifu
Thomas Aquinas Mtakatifu
Alipofikia umri wa miaka 14 alihamia Napoli, mji mkuu wa Ufalme wa Sicilia, aliposoma katika chuo kikuu maarufu kilichoanzishwa na Kaisari Federiko II. Humo mawazo mbalimbali kama yale ya Aristotle yalifundishwa bila vizuio vilivyokuwepo sehemu nyingine.
20231101.sw_3357_10
https://sw.wikipedia.org/wiki/Thomas%20Aquinas%20Mtakatifu
Thomas Aquinas Mtakatifu
Basi, Thoma alianza kutambua thamani ya falsafa ya Mgiriki huyo iliyokuwa imesahaulika kwa muda mrefu lakini wakati huo ilikuja kujulikana upya kupitia wafafanuzi wake wa Kiarabu, Avisena na Averoe.
20231101.sw_3357_11
https://sw.wikipedia.org/wiki/Thomas%20Aquinas%20Mtakatifu
Thomas Aquinas Mtakatifu
Ilikuwa na mpango mzima wa mawazo kuhusu ulimwengu, roho na maadili ambao ulikamilika kabla ya Kristo kwa kutumia akili tu, na ambao ulionekana kujitosheleza na kuridhisha kama mtazamo sahihi.
20231101.sw_3357_12
https://sw.wikipedia.org/wiki/Thomas%20Aquinas%20Mtakatifu
Thomas Aquinas Mtakatifu
Jambo lingine muhimu la miaka hiyo ni kwamba alikuwa karibu na konventi ya Mt. Dominiko akavutiwa na karama ya shirika lililoanzishwa na mtakatifu huyo. Ingawa alipingwa sana na familia, mwaka 1244 aliamua kujiunga na Wadominiko.
20231101.sw_3357_13
https://sw.wikipedia.org/wiki/Thomas%20Aquinas%20Mtakatifu
Thomas Aquinas Mtakatifu
Wakubwa wa shirika, kisha kuhisi ukuu wa akili yake, walimtuma Paris aweze kukamilisha masomo yake, lakini kabla hajafika huko alikamatwa na wanafamilia na kufungwa katika ngome ya baba yake huko Monte San Giovanni Campano alipokaa mwaka mzima, akishinikizwa aoe.
20231101.sw_3357_14
https://sw.wikipedia.org/wiki/Thomas%20Aquinas%20Mtakatifu
Thomas Aquinas Mtakatifu
Hatimaye, akiwa amefikia umri wa kujiamulia maisha, alitoroka au alifunguliwa kwa ombi la Papa Inosenti IV.
20231101.sw_3357_15
https://sw.wikipedia.org/wiki/Thomas%20Aquinas%20Mtakatifu
Thomas Aquinas Mtakatifu
Baada ya kukaa kidogo Napoli na Roma, alifika Paris (Ufaransa) ili kufundishwa na Alberto Mkuu, mwanasayansi, mwanafalsafa na mwanateolojia wa shirika lake.
20231101.sw_3357_16
https://sw.wikipedia.org/wiki/Thomas%20Aquinas%20Mtakatifu
Thomas Aquinas Mtakatifu
Mapema walianza kuheshimiana na kupendana, hivyo mwaka 1248 Thoma alimfuata Alberto Cologne (Ujerumani) alipokuwa ametumwa na viongozi wa shirika aanzishe kituo cha teolojia.
20231101.sw_3357_17
https://sw.wikipedia.org/wiki/Thomas%20Aquinas%20Mtakatifu
Thomas Aquinas Mtakatifu
Baadaye, Thoma aliamua kutekeleza mpango wa mwalimu wake wa kulinganisha Ukristo na falsafa ya Aristotle iliyokuwa inazidi kuathiri Ulaya Magharibi na ustaarabu wake uliotegemea imani, ingawa wengine waliipinga falsafa hiyo, hasa kwa sababu wafafanuzi wake wa Kiarabu walikuwa wameipendekeza tofauti, wakisema, k.mf. kwamba ulimwengu ni wa milele kama Mungu.
20231101.sw_3357_18
https://sw.wikipedia.org/wiki/Thomas%20Aquinas%20Mtakatifu
Thomas Aquinas Mtakatifu
Hapo Thoma alifanya jambo la maana sana kwa historia yote ya falsafa, teolojia na elimu kwa jumla: kusoma kikamilifu vitabu vya Aristotle na vya wafafanuzi wake, kisha kujipatia tafsiri mpya kutoka Kigiriki ili asitegemee tu walivyoelewa Waarabu hao.
20231101.sw_3357_19
https://sw.wikipedia.org/wiki/Thomas%20Aquinas%20Mtakatifu
Thomas Aquinas Mtakatifu
Hapo alifafanua mwenyewe sehemu kubwa ya maandishi ya Aristotle, akitofautisha kweli za kudumu zilizomo, mambo yanayotia shaka na yale yasiyo sahihi kabisa, akionyesha yanavyolingana na Ufunuo wa Kimungu na jinsi yanavyoweza kutumika katika teolojia ya Kikristo.
20231101.sw_3357_20
https://sw.wikipedia.org/wiki/Thomas%20Aquinas%20Mtakatifu
Thomas Aquinas Mtakatifu
Kifupi, Thoma alithibitisha hivyo ulinganifu wa imani na hoja za akili, wakati ambapo hizo mbili zilionekana kupingana moja kwa moja, hata kusababisha watu wajione ni lazima waachane na imani na kufuata akili.
20231101.sw_3357_21
https://sw.wikipedia.org/wiki/Thomas%20Aquinas%20Mtakatifu
Thomas Aquinas Mtakatifu
Kwa usanisi huo, Thoma aliunda msimamo wa karne zijazo, kwamba kweli haziwezi kupingana kamwe; ikionekana hivyo maana yake ama akili imekosea katika hoja zake, ama kinachodaiwa kuwa ukweli wa imani hakifundishwi nayo.
20231101.sw_3357_22
https://sw.wikipedia.org/wiki/Thomas%20Aquinas%20Mtakatifu
Thomas Aquinas Mtakatifu
Kutokana na vipawa vyake kuanzia mwaka 1252 aliitwa kufundisha teolojia kwenye Chuo kikuu cha Paris, akianza kama baccalarius biblis, na baada ya miaka 4 aliweza kufundisha kama profesa.
20231101.sw_3357_23
https://sw.wikipedia.org/wiki/Thomas%20Aquinas%20Mtakatifu
Thomas Aquinas Mtakatifu
Wakati huo Thoma alianza kazi ya kutunga vitabu ambayo aliendelea nayo hadi karibu na kifo na ambayo ni ya ajabu hata tukizingatia kwamba alisaidiwa na karani kadhaa, kati yao akiwemo hasa rafiki yake Rejinaldo wa Piperno.
20231101.sw_3357_24
https://sw.wikipedia.org/wiki/Thomas%20Aquinas%20Mtakatifu
Thomas Aquinas Mtakatifu
Alipinga falsafa ya wafuasi wa Mwarabu Averroe waliosema imani haiwezi kupatana na akili: "Imani ni kwa watu wanyofu, falsafa ni kwa wasomi".
20231101.sw_3357_25
https://sw.wikipedia.org/wiki/Thomas%20Aquinas%20Mtakatifu
Thomas Aquinas Mtakatifu
Thoma alipambana pia na Waagustino ambao walifuata falsafa ya Plato hata kusema ile ya Aristoteli haipatani na imani.
20231101.sw_3357_26
https://sw.wikipedia.org/wiki/Thomas%20Aquinas%20Mtakatifu
Thomas Aquinas Mtakatifu
Mwaka 1259 alihiriki mkutano mkuu wa shirika huko Valenciennes, akaingizwa katika jopo la kupanga masomo ya Wadominiko wote.
20231101.sw_3357_27
https://sw.wikipedia.org/wiki/Thomas%20Aquinas%20Mtakatifu
Thomas Aquinas Mtakatifu
Baadaye alirudi Italia na kushirikiana na Papa Urbano IV, akiishi kwenye konventi ya Orvieto (1261-1265).
20231101.sw_3357_28
https://sw.wikipedia.org/wiki/Thomas%20Aquinas%20Mtakatifu
Thomas Aquinas Mtakatifu
Kwa agizo lake, Thoma alitunga au kupanga matini ya liturujia yote ya sikukuu mpya ya Corpus Domini (Mwili na Damu ya Kristo) iliyoanzishwa tarehe 8 Septemba 1264. Kati ya matini hayo, ambamo zinajitokeza imani na hekima yake, maarufu zaidi kimataifa mpaka leo ni utenzi Pange Lingua, hasa sehemu ya mwisho inayoanzia na maneno Tantum Ergo (Sakramenti Kubwa Hiyo).
20231101.sw_3357_29
https://sw.wikipedia.org/wiki/Thomas%20Aquinas%20Mtakatifu
Thomas Aquinas Mtakatifu
Waliomfahamu walisisitiza heshima yake kwa fumbo la Ekaristi; pengine alikuwa akiegemeza kichwa chake penye tabenakulo, kama kwa kusikia mapigo ya Moyo wa Yesu na kupata majibu ya maswali magumu aliyojiuliza. Akiadhimisha Misa aliweza akalia machozi ya huruma, furaha na shukrani kwa Bwana aliyejitoa kafara kwa ajili ya binadamu. “Kwa kuwa hii ndiyo sakramenti ya Mateso ya Bwana wetu, ndani yake ina Yesu aliyeteseka kwa ajili yetu. Basi, tokeo lolote la Mateso ya Bwana wetu ni pia tokeo la sakramenti hii.”
20231101.sw_3357_30
https://sw.wikipedia.org/wiki/Thomas%20Aquinas%20Mtakatifu
Thomas Aquinas Mtakatifu
Halafu alihamia Roma (1265-1268) ili kuongoza chuo cha Mt. Sabina; ila katikati, mwaka 1267 Papa Clemens IV alimuita kwake Viterbo, alipohubiri mara nyingi katika kanisa la Santa Maria Nuova.
20231101.sw_3357_31
https://sw.wikipedia.org/wiki/Thomas%20Aquinas%20Mtakatifu
Thomas Aquinas Mtakatifu
Akiwa Italia ndipo alipoandika vitabu vingi kama vile Summa contra gentiles, De regimine principium, De unitate intellectus contra Averroistas na sehemu kubwa ya kazi yake bora, Summa Theologiae, inayotumika hadi leo katika teolojia kama ilivyoagizwa na Mtaguso II wa Vatikano katika hati mbili, Optatam Totius na Gravissimum Educationis.
20231101.sw_3357_32
https://sw.wikipedia.org/wiki/Thomas%20Aquinas%20Mtakatifu
Thomas Aquinas Mtakatifu
Mwaka 1269 alirudishwa Paris; huko wanafunzi wake walikuwa wengi hata kujaza kabisa ukumbi; mmojawao alishuhudia kwamba, “kumsikiliza kulimjaza heri ya dhati”. Hata waliompinga walikiri mafundisho yake ni bora na yanasahihisha yale ya walimu wengine.
20231101.sw_3357_33
https://sw.wikipedia.org/wiki/Thomas%20Aquinas%20Mtakatifu
Thomas Aquinas Mtakatifu
Mwaka 1272, akiitwa na mfalme Karolo I wa Angiò, alirudishwa Napoli na kupanga upya masomo ya teolojia kwenye chuo kikuu karibu na konventi yake asili. Huko alijitosa pia kuhubiria watu wa kawaida, nao walimiminika kumsikiliza. Mahubiri ya Kwaresima yake ya mwisho, aliyoyatoa katika kanisa la San Domenico Maggiore, yametunzwa kwa jina la “Opusculi” (yaani “Vijitabu”). Humo tunasoma alivyofafanua kwa usahili Kanuni ya Imani ya Mitume, [[sala++ ya Baba Yetu, Amri Kumi na sala ya Salamu Maria.
20231101.sw_3357_34
https://sw.wikipedia.org/wiki/Thomas%20Aquinas%20Mtakatifu
Thomas Aquinas Mtakatifu
Kwa mfano, kuhusu imani, alieleza thamani yake: kwa njia yake roho inaungana na Mungu na kuzaa uzima wa milele; maisha yanapata mwelekeo wa kufaa, nasi tunashinda vishawishi kwa urahisi.
20231101.sw_3357_35
https://sw.wikipedia.org/wiki/Thomas%20Aquinas%20Mtakatifu
Thomas Aquinas Mtakatifu
Dhidi ya hoja ya kwamba imani ni upumbavu kwa sababu inamfanya mtu asadiki kitu kisichofikiwa na hisi zake, Thoma alijibu kwamba akili yetu ina mipaka, haiwezi kujua yote. Ingeweza kufahamu kikamilifu mambo yote yanayoonekana na yasiyoonekana, hapo tu ingekuwa upumbavu kukubali ukweli fulani kwa imani. Kumbe hatuwezi kuishi bila kutegemea ushahidi wa wengine kila tunaposhindwa kujua kitu wenyewe. Kama ni hivyo, basi, inafaa tumsadiki Mungu anayejifunua na pia ushahidi wa Mitume wa Yesu. Ni kati ya maajabu ya historia kwamba mapema watu wengi wenye mali na hekima waliwasadiki hao watu wachache, fukara na wanyofu waliovunjwa moyo na kifodini cha mwalimu wao. Lisingetokea kama wasingekutana naye mfufuka.
20231101.sw_3357_36
https://sw.wikipedia.org/wiki/Thomas%20Aquinas%20Mtakatifu
Thomas Aquinas Mtakatifu
Thoma alieleza pia kwamba tafakuri juu ya umwilisho wa Mwana wa Mungu inaimarisha imani na tumaini kwa wazo la ujio wake kati yetu kama mmojawetu kwa lengo la kuwashirikisha watu umungu wake; pia inachochea upendo kwa sababu hakuna ishara wazi zaidi ya upendo wa Mungu kuliko kumuona Muumba wa ulimwengu kujifanya kiumbe kama sisi; hatimaye inawasha hamu ya kumfikia Kristo katika utukufu: “Kama ndugu wa mfalme angeishi mbali sana naye, bila shaka angetamani kuishi karibu naye. Basi, Kristo ni ndugu yetu; kwa hiyo tunapaswa kutamani tuwe naye na kuwa moyo mmoja naye”.
20231101.sw_3357_37
https://sw.wikipedia.org/wiki/Thomas%20Aquinas%20Mtakatifu
Thomas Aquinas Mtakatifu
Akifafanua Baba Yetu, alionyesha ni sala kamili kutokana na kuwa na sifa tano zinazohitajika: tumaini tulivu, maombi ya kufaa, mpangilio mzuri wa maombi, ari ya upendo na unyofu wa unyenyekevu.
20231101.sw_3357_38
https://sw.wikipedia.org/wiki/Thomas%20Aquinas%20Mtakatifu
Thomas Aquinas Mtakatifu
Kuhusu Bikira Maria, alimuita “Triclinium totius Trinitatis”, yaani “mahali ambapo Utatu Mtakatifu unastarehe”, kwa maana Nafsi tatu za Mungu hazifurahii kukaa ndani ya mtu yeyote kuliko ndani ya roho yake iliyojaa neema.
20231101.sw_3357_39
https://sw.wikipedia.org/wiki/Thomas%20Aquinas%20Mtakatifu
Thomas Aquinas Mtakatifu
Miezi ya mwisho ya maisha yake iliathiriwa na tukio la pekee lililofanya azidi kuzama katika tafakuri. Ni kwamba tarehe 6 Desemba 1273, katika kanisa la Mt. Dominiko, alitoka nje ya nafsi yake na tangu siku hiyo aliacha kuandika, akimueleza kwa unyenyekevu ndugu Reginaldo wa Piperno, msaidizi na muungamishi wake: «Yale yote niliyoyandika naona ni fungu dogo la majani makavu kulingana na yale ambayo nimeyaona na kufunuliwa. Ndio mwisho wa kuandika kwangu na natumaini umekaribia pia mwisho wa maisha yangu».
20231101.sw_3357_40
https://sw.wikipedia.org/wiki/Thomas%20Aquinas%20Mtakatifu
Thomas Aquinas Mtakatifu
Ndiyo sababu Summa Theologiae haikukamilika (inaishia kwenye mada ya Kitubio) baada ya kukabili masuala 512 katika hoja 2,669 kwa kuchimba mafundisho ya Biblia na ya mababu wa Kanisa, hasa Augustino wa Hippo).
20231101.sw_3357_41
https://sw.wikipedia.org/wiki/Thomas%20Aquinas%20Mtakatifu
Thomas Aquinas Mtakatifu
Humo Thoma anazingatia kwanza kwamba Mungu yupo kwa namna tatu: 1) ndani mwake, akiwa asili na lengo la vyote, hivi kwamba viumbe vyote vinatokana naye na kumtegemea; 2) kwa njia ya neema katika uhai na utendaji wa watu anaowatakasa; 3) kwa namna ya pekee kabisa katika nafsi ya Kimungu ya Mwana iliyounganika kweli na ubinadamu wa Yesu na inayotenda katika sakramenti zinazotokana na kazi yake ya ukombozi.
20231101.sw_3357_42
https://sw.wikipedia.org/wiki/Thomas%20Aquinas%20Mtakatifu
Thomas Aquinas Mtakatifu
Ndiyo sababu kitabu hicho kikubwa kimegawanyika katika sehemu tatu: “Kwa kuwa lengo kuu la teolojia ni kufundisha ujuzi wa Mungu, si tu jinsi alivyo mwenyewe, bali pia kama asili na lengo kuu la vitu, na hasa la viumbe wenye akili, ilivyo wazi katika yale tuliyoyasema tayari, basi tutafafanua: 1) Mungu; 2) maendeleo ya kiumbe mwenye akili kumuelekea Mungu; 3) Kristo ambaye kama mtu ndiye njia yetu kwa Mungu”.
20231101.sw_3357_43
https://sw.wikipedia.org/wiki/Thomas%20Aquinas%20Mtakatifu
Thomas Aquinas Mtakatifu
Ni kama duara inayorudi ilipoanzia: Mungu alivyo anajitokeza kwa nje na kutushika mkono hivi kwamba pamoja na Kristo tumrudie yeye na kuungana naye awe yote katika wote.
20231101.sw_3357_44
https://sw.wikipedia.org/wiki/Thomas%20Aquinas%20Mtakatifu
Thomas Aquinas Mtakatifu
Sehemu ya kwanza ya Summa Theologiae inamchunguza Mungu mwenyewe, fumbo la Utatu na kazi yake ya kuumba. Humo tunakuta tafakuri ya dhati juu ya mtu pia, kama kiumbe aliye tunda la upendo wake. Uhai wetu unamtegemea Mungu, lakini ni wa kweli kwa sababu yeye ametaka kututia thamani.
20231101.sw_3357_45
https://sw.wikipedia.org/wiki/Thomas%20Aquinas%20Mtakatifu
Thomas Aquinas Mtakatifu
Sehemu ya pili inazidi kumzingatia mtu ambaye, akisukumwa na neema, anatamani kumjua na kumpenda Mungu ili awe na heri sasa na milele. Thoma anafafanua kiteolojia matendo maadilifu, ambayo yanachangiwa na akili, utashi na maono ya mtu, pamoja na uwezo wa neema ya Mungu kupitia maadili na vipaji vya Roho Mtakatifu, mbali ya msaada wa sheria yake. Kwa msingi huo, Thoma anamchora mtu ambaye anaongozwa na Roho Mtakatifu na hivyo kuwa mfano wa Mungu. Hapo anasimama kufafanua maadili matatu ya Kimungu na zaidi ya maadili hamsini ya kiutu, yanayotegemea maadili bawaba manne. Hatimaye anatakari juu ya miito mbalimbali yaliyopo ndani ya Kanisa.
20231101.sw_3357_46
https://sw.wikipedia.org/wiki/Thomas%20Aquinas%20Mtakatifu
Thomas Aquinas Mtakatifu
Sehemu ya tatu inachunguza fumbo la Kristo, aliye njia na ukweli, ambalo linatuwezesha kumfikia Mungu Baba. Humo Thoma anaeleza vizuri ajabu umwilisho na Mateso ya Yesu, akiongeza maelezo marefu kuhusu sakramenti ambazo Kristo anatushirikisha faida ya ukombozi. Akitumia vitu alivyochagua, anatugusa mpaka ndani.
20231101.sw_3357_47
https://sw.wikipedia.org/wiki/Thomas%20Aquinas%20Mtakatifu
Thomas Aquinas Mtakatifu
Asubuhi moja, Thoma alipokuwa anasali mbele ya msalaba wa kikanisa cha Mt. Nikola mjini Napoli, mtunzasakristia Dominiko wa Caserta alisikiliza maongezi yake na Yesu. Thoma alikuwa anauliza kwa fadhaiko kama aliyoyaandika kuhusu mafumbo ya imani ni sahihi au sivyo. Msulubiwa alimjibu: “Umeandika vema juu yangu, Thoma. Unataka tuzo gani?” Hapo Thoma alisema, “Si kitu kingine, ila wewe mwenyewe”.
20231101.sw_3357_48
https://sw.wikipedia.org/wiki/Thomas%20Aquinas%20Mtakatifu
Thomas Aquinas Mtakatifu
Mnamo Januari 1274 Papa Gregori X alimuagiza ashiriki Mtaguso wa pili wa Lyon, na Thoma akafunga safari ingawa hali yake haikuwa nzuri.
20231101.sw_3357_49
https://sw.wikipedia.org/wiki/Thomas%20Aquinas%20Mtakatifu
Thomas Aquinas Mtakatifu
Alilazimika kusimama kwenye ngome ya Maenza, lakini alipoona hali inazidi kuwa mbaya asiweze kufikia konventi ya shirika, akitaka kufia monasterini, aliagiza aletwe kwenye abasia ya Wasitoo ya Fossa Nuova (leo Fossanova, karibu na Priverno), ambapo alifariki baada ya wiki chache.
20231101.sw_3357_50
https://sw.wikipedia.org/wiki/Thomas%20Aquinas%20Mtakatifu
Thomas Aquinas Mtakatifu
Sababu si mafundisho yake tu, bali mbinu alizozitumia katika kusanisi falsafa na teolojia bila kuzichanganya kama ilivyotokea kabla yake. Falsafa kama ile ya Aristotle iliweza kujitegemea katika hoja zake, badala ya kumezwa na teolojia ambayo ilitegemea imani katika Ufunuo wa Mungu na kuja kukamilisha falsafa pale ambapo hiyo haiwezi kufika.
20231101.sw_3357_51
https://sw.wikipedia.org/wiki/Thomas%20Aquinas%20Mtakatifu
Thomas Aquinas Mtakatifu
Msingi wa hakika hiyo ya Thoma ni kwamba falsafa na teolojia vilevile zinatokana na chanzo cha kweli zote, ambacho ni Neno wa Mungu, aliyehusika na kazi ya uumbaji na ya ukombozi pia. Ingawa fani hizo zinafuata taratibu tofauti katika kulenga ujuzi sahihi, hazitakiwi kutengana, bali kushirikiana.
20231101.sw_3357_52
https://sw.wikipedia.org/wiki/Thomas%20Aquinas%20Mtakatifu
Thomas Aquinas Mtakatifu
Kadiri yake, kwa mfano, akili ya binadamu kwa njia ya hoja inaweza kufikia hakika kuhusu uwepo wa Mungu mmoja, ila imani tu, kwa kupokea Ufunuo kutoka juu, inaweza kuchota katika fumbo la Upendo wa Mungu Utatu.
20231101.sw_3357_53
https://sw.wikipedia.org/wiki/Thomas%20Aquinas%20Mtakatifu
Thomas Aquinas Mtakatifu
Wakati imani inakamilisha ujuzi wa akili, hoja pia inasaidia imani kwa namna tatu: “kwa kuthibitisha kweli zinazoandaa kusadiki; kwa kufafanua wazi zaidi kweli za imani kwa njia ya mifano kadhaa; kwa kupinga wale wanaosema dhidi ya imani, ama kwa kuonyesha kauli zao ni za uongo, ama kwa kuonyesha si hakika kuwa za kweli”.
20231101.sw_3357_54
https://sw.wikipedia.org/wiki/Thomas%20Aquinas%20Mtakatifu
Thomas Aquinas Mtakatifu
Ulinganifu huo wa msingi kati ya hoja za akili na imani ya Kikristo unajitokeza tena katika wazo lingine muhimu la Thoma: kwamba neema ya Mungu haibatilishi umbile la binadamu, bali inalitumia na kulikamilisha. Hiyo ni kwa sababu, hata baada ya kutenda dhambi, umbile hilo halijaharibika kabisa, ila limejeruhika na kudhoofika. Neema ambayo tunakirimiwa na Mungu na kushirikishwa kwa njia ya Neno aliyefanyika mwili, ni zawadi tu ya hiari yake ambayo umbile letu linaponywa, linatiwa nguvu na kusaidiwa lifikie heri ile linayotamani tu kwa dhati, hata bila kutambua na kuamua. Vipawa vyote vya mtu vinatakaswa, vinageuzwa na kuinuliwa na neema ya Mungu.
20231101.sw_3357_55
https://sw.wikipedia.org/wiki/Thomas%20Aquinas%20Mtakatifu
Thomas Aquinas Mtakatifu
Fundisho hilo juu ya uhusiano wa umbile na neema ndani mwetu linatumiwa hasa katika maadilidini ya Thoma. Kiini chake ni sheria mpya ya Injili, ambayo ni Roho Mtakatifu, yaani neema yake wanayopewa wale wanaomuamini Kristo. Mafundisho yote ya Kanisa kuhusu imani na maadili yameunganika na neema hiyo ambayo ni ya msingi katika kuishi kwa uadilifu: kutoka kwake yanapatikana maadili ya Kimungu na ya kiutu. Hivyo Wakristo wote wanaweza kufikia ukamilifu uliopendekezwa na Yesu katika hotuba ya mlimani, ikiwa wanaishi naye katika uhusiano wa imani na wako wazi kupokea kazi ya Roho Mtakatifu.
20231101.sw_3357_56
https://sw.wikipedia.org/wiki/Thomas%20Aquinas%20Mtakatifu
Thomas Aquinas Mtakatifu
Pamoja na hayo, “ingawa neema ina nguvu kuliko umbile, hata hivyo umbile linamhusu mtu zaidi, na kwa hiyo ni la kudumu zaidi”. Ndiyo maana kuna nafasi kwa hoja za akili katika kutambua maadili yanayodaiwa na utu kwa jinsi ulivyo. Akili inaweza kuyatambua kwa kutofautisha yanayofaa na yasiyofaa kufikia ile heri inayotamaniwa na mioyo yetu.
20231101.sw_3357_57
https://sw.wikipedia.org/wiki/Thomas%20Aquinas%20Mtakatifu
Thomas Aquinas Mtakatifu
Hayo yanahusika pia na majukumu kwa ajili ya wengine, mmojammoja na kwa jumla (ustawi wa jamii). Watungasheria wanapaswa kuzingatia hayo katika kazi yao ya kuratibu maisha ya jamii. Ndio msingi wa kuorodhesha na kutetea haki za binadamu. Si ajabu kwamba fundisho la hadhi ya nafsi ya mtu, inayomfanya kila mmoja awe na haki za msingi kwa sababu tu ni mtu, lilistawi kwanza kati ya waliozingatia urithi wa Thoma katika kuthamini umbile letu: “ndilo lililo kamili kuliko yote yanayopatikana ulimwenguni, yaani mmoja anayeishi akiwa na akili”.
20231101.sw_3357_58
https://sw.wikipedia.org/wiki/Thomas%20Aquinas%20Mtakatifu
Thomas Aquinas Mtakatifu
Basi, Thoma alipendekeza mtazamo mpana na lenye tumaini kuhusu akili ya binadamu. Mpana kwa sababu hauishii katika ujuzi wa sayansi zinazotegemea upimaji wa vitu vinavyoonekana, bali unakabili yote yaliyopo, kuanzia Mungu, na hivyo unahimizwa kutafuta maana ya maisha yetu. Lenye tumaini kwa sababu akili, hasa ikiangazwa na imani ya Kikristo, inapigania ustaarabu ambao unathamini hadhi ya kila mtu, unatetea haki zake pamoja na kumhimiza kuwajibika kwa wengine.
20231101.sw_3357_59
https://sw.wikipedia.org/wiki/Thomas%20Aquinas%20Mtakatifu
Thomas Aquinas Mtakatifu
Dhati ya mawazo ya Thoma ilitokana daima na maisha yake ya imani na sala yaliyojitokeza katika maneno kama haya: “Ee Bwana, Mungu wangu, unijalie akili ya kukufahamu, moyo wa kukutafuta, hekima ya kukupata, mwenendo wa kukupendeza, udumifu mwaminifu katika kukutarajia, na tumaini la kukukumbatia mwisho”.
20231101.sw_3357_60
https://sw.wikipedia.org/wiki/Thomas%20Aquinas%20Mtakatifu
Thomas Aquinas Mtakatifu
Mungu wa wema wote, utujalie tutamani motomoto, tutafute kwa busara, tujue kwa hakika na kutekeleza kikamilifu matakwa yako matakatifu kwa utukufu wa jina lako.
20231101.sw_3357_61
https://sw.wikipedia.org/wiki/Thomas%20Aquinas%20Mtakatifu
Thomas Aquinas Mtakatifu
Aquinas the Scholar from The Thirteenth, the Greatest of Centuries, ch. XVII. by James Joseph Walsh
20231101.sw_3357_62
https://sw.wikipedia.org/wiki/Thomas%20Aquinas%20Mtakatifu
Thomas Aquinas Mtakatifu
[http://www.nd.edu/Departments/Maritain/etext/gc.htm Summa contra Gentiles Summa Theologica The Principles of Nature On Being and Essence ()
20231101.sw_3357_63
https://sw.wikipedia.org/wiki/Thomas%20Aquinas%20Mtakatifu
Thomas Aquinas Mtakatifu
Online Galleries, History of Science Collections, University of Oklahoma Libraries High resolution images of works by Thomas Aquinas in .jpg and .tiff format.
20231101.sw_3359_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/Austen%20Chamberlain
Austen Chamberlain
Austen Chamberlain (16 Oktoba 1863 – 16 Machi 1937) alikuwa mwanasiasa kutoka nchi ya Uingereza. Kuanzia 1924 hadi 1929 alikuwa Waziri wa Mambo ya Nje. Mwaka wa 1925, pamoja na Charles Dawes alikuwa mshindi wa Tuzo ya Nobel kwa Amani kwa ajili ya kazi yake ya kupitisha Maafikiano ya Lokarno.
20231101.sw_3361_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/Charles%20Dawes
Charles Dawes
Charles Gates Dawes (27 Agosti 1865 – 23 Aprili 1951) alikuwa mwanasiasa kutoka nchi ya Marekani. Kuanzia 1925 hadi 1929 alikuwa Kaimu Rais chini ya Rais Calvin Coolidge. Mwaka wa 1925, pamoja na Austen Chamberlain alikuwa mshindi wa Tuzo ya Nobel kwa Amani.
20231101.sw_3364_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/Aristide%20Briand
Aristide Briand
Aristide Briand (28 Machi 1862 – 7 Machi 1932) alikuwa mwanasiasa kutoka nchi ya Ufaransa. Kati ya 1906 na 1932 alikuwa Waziri Mkuu mara 11. Mwaka wa 1926, pamoja na Gustav Stresemann alikuwa mshindi wa Tuzo ya Nobel kwa Amani.
20231101.sw_3365_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/Gustav%20Stresemann
Gustav Stresemann
Gustav Stresemann (10 Mei 1878 – 3 Oktoba 1929) alikuwa mwanasiasa kutoka nchi ya Ujerumani. Mwaka wa 1923 alikuwa Waziri Mkuu na kuanzia 1924 hadi 1929 alikuwa Waziri wa Mambo ya Nje. Mwaka wa 1926, pamoja na Aristide Briand alikuwa mshindi wa Tuzo ya Nobel kwa Amani.
20231101.sw_3366_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/Norman%20Angell
Norman Angell
Sir Ralph Norman Angell Lane (26 Desemba 1872 – 7 Oktoba 1967) alikuwa mtaalamu wa uchumi na mwandishi wa habari kutoka nchi ya Uingereza. Hasa alijitahidi kutekeleza amani ya kimataifa. Anajulikana sana kwa kitabu chake “Uwongo Mkubwa” (kwa Kiingereza Great Illusion) kilichotolewa mwaka wa 1910. Mwaka wa 1931 alipewa cheo cha "Sir" cha Uingereza. Mwaka wa 1933 alikuwa mshindi wa Tuzo ya Nobel kwa Amani.
20231101.sw_3368_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/Cordell%20Hull
Cordell Hull
Cordell Hull (2 Oktoba 1871 – 23 Julai 1955) alikuwa mwanasheria na mwanasiasa kutoka nchi ya Marekani. Kuanzia 1933 hadi 1944 alikuwa Waziri wa Mambo ya Nje. Mwaka wa 1945 alikuwa mshindi wa Tuzo ya Nobel kwa Amani kwa ajili ya kazi yake ya kuanzisha Umoja wa Mataifa.
20231101.sw_3369_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ralph%20Bunche
Ralph Bunche
Ralph Johnson Bunche (7 Agosti 1904 – 9 Desemba 1971) alikuwa mwanasiasa kutoka nchi ya Marekani. Mwaka wa 1950 alikuwa mshindi wa Tuzo ya Nobel kwa Amani kwa vile aliwasaidia Waarabu na Waisraeli kusimamisha vita yao kwa muda kule Palestina mwaka wa 1949.