_id
stringlengths 15
22
| url
stringlengths 31
150
| title
stringlengths 1
86
| text
stringlengths 100
23.8k
|
---|---|---|---|
20231101.sw_2128_10
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mkoa%20wa%20Lindi
|
Mkoa wa Lindi
|
Mkoa wa Lindi wakazi wake wengi ni wakulima, hasa maeneo ya vijijini wengi wanalima mazao mchanganyiko, yaani ya biashara na chakula. Mazao ya biashara hasa ni korosho, ambazo zinapatikana kwa wingi katika wilaya ya Ruangwa, Lindi Vijijini, na Nachingwea, pia kuna zao la ufuta na ndizi kama zao la biashara na chakula pia.
|
20231101.sw_2128_11
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mkoa%20wa%20Lindi
|
Mkoa wa Lindi
|
Mazao ya chakula kuna mahindi, mpunga, muhogo, nyanya, vitunguu: hizi pia hulimwa sana wakati wa masika kutegemea na mvua za vuli.
|
20231101.sw_2128_12
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mkoa%20wa%20Lindi
|
Mkoa wa Lindi
|
Biashara wakazi wengi wa mkoa wa Lindi wanafanya biashara, hasa biashara ndogondogo zijulikanazo kama "machinga trade": wanauza mazao wakati wa mavuno na huchukua bidhaa nyingi kutoka Dar es salaam na kupeleka vijijini hasa kwenye kata.
|
20231101.sw_2128_13
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mkoa%20wa%20Lindi
|
Mkoa wa Lindi
|
Mkoa wa Lindi huko nyuma kielimu kwani shule za sekondari mpaka sasa si nyingi sana na shule hizo hazina walimu wa kutosha kutokana na miundombinu ya barabara na shule zenye kidato cha tano na cha sita mpaka sasa ni Lindi sekondari - Lindi, Mahiwa na Namupa seminari - Lindi vijijini. Pia kuna chuo cha ualimu Nachingwea katika wilaya ya Nachingwea.
|
20231101.sw_2131_0
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kilwa
|
Kilwa
|
Kilwa Kisiwani ni kisiwa karibu na mwambao kinachotazama Kilwa Masoko. Hapo ndipo Kilwa ya kihistoria iliyojulikana kama mji mkubwa wa pwani ya Afrika ya Mashariki tangu nusu ya kwanza ya karne ya 14 BK kutokana na taarifa ya msafiri Ibn Battuta. Pamoja na mabaki ya mji wa Songo Mnara, magofu ya Kilwa Kisiwani yameandikishwa katika orodha ya UNESCO ya "Urithi wa Dunia" (World Heritage).
|
20231101.sw_2135_0
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Keremkerem
|
Keremkerem
|
Keremkerem ni ndege wa familia ya Meropidae. Wana mwili mwembamba wa rangi maridadi. Mdomo wao ni mrefu na mwembamba na mkia wa aina nyingi za keremkerem una mileli mirefu katikati.
|
20231101.sw_2135_1
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Keremkerem
|
Keremkerem
|
Ndege hao wanaishi uwandani kwa kanda ya tropiki na nusu-tropiki ya Afrika, Ulaya na Asia. Hula wadudu, nyuki, manyigu na mabunzi hasa, ambao wanakamatwa hewani. Kabla ya kula, ndege anatoa mshale wa mdudu akimgongea tawi la mti au kitu kigumu kingine.
|
20231101.sw_2135_2
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Keremkerem
|
Keremkerem
|
Keremkerem hupenda kuwa pamoja kwa makundi. Huchimba mashimo ndani ya kando za mchanga kwa kutaga mayai yao meupe.
|
20231101.sw_2135_3
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Keremkerem
|
Keremkerem
|
Familia ya Meropidae imegawika katika nusufamilia mbili: Nyctyornithinae (keremkerem wenye ndevu) na Meropinae (keremkerem wa kawaida).
|
20231101.sw_2137_0
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Pangani%20%28mto%29
|
Pangani (mto)
|
Mto Pangani ni kati ya mito mikubwa ya Tanzania. Unabeba maji ya Milima ya Meru, Kilimanjaro, Pare na Usambara kwenda Bahari ya Hindi. Mdomo wake uko mjini Pangani.
|
20231101.sw_2137_1
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Pangani%20%28mto%29
|
Pangani (mto)
|
Katika karne ya 19 kabla ya ukoloni mwendo hadi maporomoko karibu na Hale (Mnyuzi) ulijulikana zaidi kama "Ruvu", na sehemu ya mwisho kuanzia maporomoko hadi bahari kwa jina "Pangani" kutokana na mji ulipofikia baharini .
|
20231101.sw_2137_2
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Pangani%20%28mto%29
|
Pangani (mto)
|
Kwenye ramani za zamani za ukoloni majina yote mawili yalitumika kandokando: "Ruvu" na "Pangani". Ramani za zamani za uhuru wa Tanzania mara nyingi huwa na maandishi "Pangani or Ruvu River". .
|
20231101.sw_2137_3
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Pangani%20%28mto%29
|
Pangani (mto)
|
Beseni la Pangani ni eneo la km2 43,650. Karibu yote imo Tanzania isipokuwa kuna km2 3,914 huko Kenya katika mazingira ya Taveta. Jumla ya wakazi katika beseni la Pangani ni milioni 3.7.
|
20231101.sw_2137_4
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Pangani%20%28mto%29
|
Pangani (mto)
|
Chanzo cha mto Pangani ni maungano ya matawimto Kikuletwa na Ruvu inayokutana leo katika lambo la Nyumba ya Mungu kusini kwa Moshi. Mto Kikuletwa hupokea maji kutoka Mlima Meru na mitelemko ya Kilimanjaro upande wa kusini. Ruvu hupokea maji kutoka mitelemko ya Kilimanjaro upande wa mashariki pamoja na Ziwa la Jipe.
|
20231101.sw_2137_5
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Pangani%20%28mto%29
|
Pangani (mto)
|
Mto Pangani unaendelea km 432 hadi Pangani mjini unapoingia katika Bahari Hindi. Kwenye sehemu ya kwanza baada ya Nyumba ya Mungu mto unaitwa wakati mwingine bado "Ruvu".
|
20231101.sw_2137_6
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Pangani%20%28mto%29
|
Pangani (mto)
|
Mto Pangani unategemea misitu panapokusanywa maji yake. Misitu hii imepungua sana kutokana na uenezaji wa mashamba, kukatwa kwa miti kwa ajili ya makaa na matumizi ya ubao.
|
20231101.sw_2137_7
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Pangani%20%28mto%29
|
Pangani (mto)
|
Vilevile machafuko yamekuwa hatari kwa ajili ya afya ya mto na watu wanaotegemea maji yake. Asili ya machafuko ni hasa kilimo, mvua hupeleka mbolea mtoni na kusababisha kukua kwa wingi wa majani yasiyotakika.
|
20231101.sw_2138_0
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Rhapta
|
Rhapta
|
Rhapta ni jina la soko na mji wa kale katika pwani la Afrika ya Mashariki. Habari zake zilipatikana tangu karne ya kwanza katika mwongozo wa kigiriki kwa ajili ya mabaharia. Jina la Rhapta lilitajwa tena katika vitabu vingine hadi karne ya 6 BK lakini baadaye lilipotea au kubadilishwa.
|
20231101.sw_2138_1
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Rhapta
|
Rhapta
|
Wataalamu walio wengi hukubaliana ilikuwepo ufukoni wa Tanzania lakini hakuna uhakika kuhusu mahali pake kamili. Kuna kisio la kuwa Rhapta ni jina la kale la Pangani lakini hiyo ni kisio tu kutokana na bandari nzuri ya kiasili inayopatikana pale Pangani. Wengine wanaona Tanga au mdomo wa mto Rufiji ilikuwa mahali pa Rhapta.
|
20231101.sw_2138_2
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Rhapta
|
Rhapta
|
Kitabu cha Periplus ya Bahari ya Eritrea kilichoandikwa mnamo mwaka 70 BK kinataja Rhapta kuwa soko kuu la Azania barani pia kituo cha mwisho kati ya miji na vituo vilivyofanya biashara na dunia ya Kiroma. Mnamo mwaka 200 mwandishi Mmisri Claudius Ptolemaius anataja Rhapta kuwa mji mkuu wa Barbaria (Afrika ya Mashariki barani). Rhapta ilikuwa mdomoni wa mto mwenye jina la Rhapta pia ambao uliaminika kuwa na asili yake katika "Milima ya Mwezi". Mdomo wa mto ulikuwa karibu na kisiwa cha Menouthis. Hakuna uhakika kama kisiwa hiki ni Pemba au Mafia.
|
20231101.sw_2138_3
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Rhapta
|
Rhapta
|
Sarafu za kiroma za karne za kwanza BK zimepatikana mahali mbalimbali za pwani; zinathebitisha kuwepo kwa biashara kati ya dunia ya Kiroma na Azania wakati ule.
|
20231101.sw_2140_0
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Pangani%20%28mji%29
|
Pangani (mji)
|
Pangani ni mji wa Mkoa wa Tanga, nchini Tanzania, uliopo ufukoni mwa Bahari Hindi kati ya Dar es Salaam na Tanga ukielekea pande zote mbili za mdomo wa mto Pangani.
|
20231101.sw_2140_1
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Pangani%20%28mji%29
|
Pangani (mji)
|
Leo hii ni mji mdogo mwenye wakazi karibu 8n000 na makao makuu ya Wilaya ya Pangani. Lakini ina historia ndefu, hasa kwa sababu kuna bandari nzuri ya kiasili mdomoni wa mto wa Pangani inayofaa kwa jahazi ndogo.
|
20231101.sw_2140_2
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Pangani%20%28mji%29
|
Pangani (mji)
|
Majengo mbalimbali ya kale ni ishara ya historia ndefu ya mji huu. Pamoja na Boma, lililojengwa na Waarabu wa Unguja na kutumiwa na wakoloni wa Kijerumani na wa Kiingereza, kuna nyumba za Waswahili.
|
20231101.sw_2140_3
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Pangani%20%28mji%29
|
Pangani (mji)
|
Eneo la mji limegawiwa kwa kata mbili ambazo ni Pangani Mashariki (pamoja na mji wa kihistoria) na Pangani Magharibi.
|
20231101.sw_2140_4
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Pangani%20%28mji%29
|
Pangani (mji)
|
Mji wa Pangani uliundwa kando la hori ya Bahari Hindi mahali ambako mto Pangani unakwisha. Hori ina upana wa kilomita 5 ikiingia barani kilomita 2.5. Mdomo wa mto Pagani una upana wa mita 300 - 500 kwa kilomita kadhaa ndani ya nchi kavu na hivyo ni bandari salama kwa jahazi ndogo. Mji wa Pangani ulianzishwa upande wa kaskazini wa mdomo huo uko kwenye pwani katikati ya visiwa vya Unguja na Pemba.
|
20231101.sw_2140_5
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Pangani%20%28mji%29
|
Pangani (mji)
|
Bandari ya Pangani inafikiwa na jahazi ndogo jinsi zilivyokuwa kawaida kwenye pwani la bahari Hindi. Ndani ya mdomo wa mto merikebu zilikuwa salama hata wakati wa dhoruba baharini. Uzuri wa bandari hii ulikuwa msingi kwa kustawi kwa mji kama kituo cha safari kwenye pwani na mahali pa biashara kati ya bara na visiswa vya karibu vya Unguja (50 km) na Pemba (75 km). Sehemu hii ya pwani ilifaa kama chanzo cha njia ya misafara kufuata bonde la mto Pangani kuelekea Kilimanjaro (290 km) na ndani zaidi.
|
20231101.sw_2140_6
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Pangani%20%28mji%29
|
Pangani (mji)
|
Mazingira ya Pangani inapokea milimita 100 - 1100 kwa mwaka , inayotosha kwa kilimo kwenye kanda la pwani. Kwenye mpangilio wa tabianchi wa Koeppen hii inatazamiwa kama "Aw", yaani tabianchi ya kitropiki ya savana.
|
20231101.sw_2140_7
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Pangani%20%28mji%29
|
Pangani (mji)
|
Wataalamu kadhaa waliochungulia habari za kale walipendekeza ya kwamba mji wa Rhapta ulikuwa sawa na au karibu na Pangani ya leo. Mji huu wa Rhapta unajulikana kutokana na kitabu cha Periplus ya Bahari ya Eritrea kilichoandikwa mnamo mwaka 70 B.K. Lakini Pangani ni mahali pamoja kati ya patano palipotajwa kuwa mahali pa Rhapta ya kale, hakuna uhakika.
|
20231101.sw_2140_8
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Pangani%20%28mji%29
|
Pangani (mji)
|
Pangani ilikuwa mji muhimu katika utamaduni wa Waswahili. Katika karne ya 19 BK biashara ya misafara kati ya eneo la maziwa makubwa na Zanzibar ilipita mara nyingi hapa; Bidhaa kutoka zanzibar zilipelekwa Pangani na kugawiwa kwa wapagazi wa misafara. Makundi ya watumwa waliobeba ndovu wakati wa kurudi walihamishwa hapa kwenye boti ziizowapeleka hadi soko la watumwa Zanzibar.
|
20231101.sw_2140_9
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Pangani%20%28mji%29
|
Pangani (mji)
|
Tangu uhamisho wa ikulu wa Waarabu wa Omani kuja Zanzibar Pangani iliona maendeleo ya kiuchumi. Makabaila walijipatia mashamba makubwa wakalima miwa wakitumia kazi ya watumwa.
|
20231101.sw_2140_10
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Pangani%20%28mji%29
|
Pangani (mji)
|
Hata kwa wapelelzi wazungu waliofika Zanzibar kwa meli kubwa Pangani ilikuwa mara nyingi mlango wa kungia Afrika bara.
|
20231101.sw_2140_11
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Pangani%20%28mji%29
|
Pangani (mji)
|
Pangani ilikuwa sehemu ya kanda ya pwani iliyokabidhiwa na Sultan Bargash kwa kampuni ya Kampuni ya Kijerumani kwa Afrika ya Mashariki ya Karl Peters. Mwaka 1889 Pangani ilikuwa mahali palipoanzia vita vya Bushiri dhidi ya utawala wa Wajerumani. Mwakilishi wa Kampuni ya Kijerumani kwa Afrika ya Mashariki Emil von Zelewski alimtendea liwali wa Sultani kwa ukali uliosababisha ghasia ya watu wa Pangani na kuanzisha Vita ya Abushiri.
|
20231101.sw_2140_12
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Pangani%20%28mji%29
|
Pangani (mji)
|
Baada ya kukomeshwa kwa vita hii umuhimu wa Pangani ulipungua sana kwa sababu meli kubwa kutoka Ulaya hazikuweza kuinghia katika mdomo wa mto Pangani, mizigo na abiria walipaswa kuhamishwa kwa boti ndogo kutoka meli hadi mjini. Hivyo Wajerumani walikazia maendeleo ya Tanga penye bandari ya kina kirefu.
|
20231101.sw_2140_13
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Pangani%20%28mji%29
|
Pangani (mji)
|
Polepole Pangani imerudi nyuma. Uhaba wa mawasiliano na barabara uliongeza mwendo huu. Hadi leo hakuna barabara ya lami kabisa katika wilaya yake.
|
20231101.sw_2140_14
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Pangani%20%28mji%29
|
Pangani (mji)
|
Miaka ya nyumba mahoteli mbalimbali katika mazingira ya Pangani yameanza kutumia nafasi nzuri kwa utalii mwambaoni.
|
20231101.sw_2141_0
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/William%20Tyndale
|
William Tyndale
|
William Tyndale alikuwa mwanatheolojia Mwingereza, kasisi ya kanisa na mtaalamu aliyetafsiri Biblia mara ya kwanza katika Kiingereza cha kisasa. Alizaliwa huko Gloucestershire mnamo mwaka 1494 - aliuawa Vilvoorde (Brabant - Ubelgiji ya leo) tarehe 6.9.1536. Tafsiri yake ya Biblia ilikuwa toleo la kwanza lililochapishwa kwa kutumia mitambo mapya ya uchapaji vitabu.
|
20231101.sw_2141_1
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/William%20Tyndale
|
William Tyndale
|
Mawazo yake yalipingwa kwa nguvu zote na watawala na watu wa dini yalionekana kama upinzani wa kidini hivyo aliamua kukimbilia Ujerumani kwa usalama wake, huko alitafuta mchapishaji aliyetoa nakala ya kwanza ya Agano Jipya kwa lugha ya kingereza nakufuatiwa baadaye na agano la kale.
|
20231101.sw_2141_2
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/William%20Tyndale
|
William Tyndale
|
Askofu Kardinali Wolsey alimtangaza kuwa mzushi. Lakini ilikuwa tendo la kupinga ndoa na talaka za mfalme wa Uingereza Henry VIII ilikuwa sababu ya kifo chake. Henry VIII alikasirika juu ya Tyndale akamwomba Kaisari Karl V wa Ujerumani kumkamata. Tyndale alishikwa huko Brussels (mji chini ya Kaisari wakati ule) akasoimamishwa mbele ya mahakama iliyotoa hukumu ya mauti kwa sababu ya uzushi dhidi ya kanisa katoliki. Katika mji wa Vilvoorde penye gereza lake alifungwa mtini akachongwa na mwili wake kuchomwa motoni.
|
20231101.sw_2142_0
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Pel%C3%A9
|
Pelé
|
Pelé (jina lake halisi ni Edison Arantes do Nascimento; 23 Oktoba 1940- 29 Desemba 2022) alikuwa mchezaji wa mpira wa miguu kutoka Brazili. Anahesabiwa na wengi, kama waandishi wa habari na mashabiki, kuwa mchezaji mzuri zaidi wa wakati wote.
|
20231101.sw_2142_1
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Pel%C3%A9
|
Pelé
|
Alicheza kama mshambuliaji wa kati. Aliisaidia Brazili kutwaa kombe la dunia 1958, 1962 na baadaye tena mwaka 1970. Aliweka rekodi mwaka 1958 ya kuwa mchezaji mdogo kuliko wote duniani kucheza katika fainali ya kombe la dunia alipocheza akiwa na umri wa miaka 17. Alivuma sana katika miaka ya 1970 duniani kote.
|
20231101.sw_2142_2
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Pel%C3%A9
|
Pelé
|
Mwaka 1999 alichaguliwa na shirikisho la mpira wa miguu duniani kuwa mchezaji bora wa karne. Kwa mujibu wa shirikisho la mpira wa miguu alikuwa mfungaji bora wa muda wote kwa kufunga magoli 1281 kati ya mechi 1363. Ana wastani wa goli moja kwa kila mechi katika uchezaji wake wote. Katika kipindi cha uchezaji wake alikuwa mchezaji anayelipwa pesa nyingi duniani.
|
20231101.sw_2142_3
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Pel%C3%A9
|
Pelé
|
Pelé alianza kuichezea Santos akiwa na umri wa miaka 15 na timu ya taifa ya Brazil akiwa na miaka 16.Katika ngazi za kimataifa alishinda kombe la dunia mara tatu 1958,1962 na 1970,akiwa ni mchezaji wa pekee kufanya hivyo.Ni mchezaji wa kibrazili anayeongoza kwa magoli mengi zaidi kwa kufunga magoli 77 kwenye mechi 92.Kwenye ngazi ya klabu ni mfungaji bora wa muda wote katika klabu ya Santos, na aliisaidia kubeba taji la Copa Libertadores kwa miaka ya 1962 na 1963.Kwa mchezo wake wa haraka ,chenga zake na magoli yake ya ajabu yalimpa umaarufu duniani kote.Tangu alipostaafu mwaka 1977,Pelé amekuwa balozi wa mpira wa miguu duniani.
|
20231101.sw_2142_4
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Pel%C3%A9
|
Pelé
|
Pelé alikuwa na uwezo wa kuupiga mpira kwa mguu wowote ili kuwazidi ujanja wapinzani wake uwanjani.Akiwa bila mpira kwa muda mrefu hurudi nyuma na kufanya kazi ya kukabana kusambaza mipira na kutumia uwezo wake wa kupiga pasi kwa kutoa pasi za zinazozaa mabao na kutumia uwezo wake wa kukokota mpira kuwapita wapinzani.Brazil wanamuheshimu kama shujaa wa taifa kwa mchango wake wa kisoka na sera zilizosaidia katika kupunguza umaskini katika nchi hiyo.Katika uchezaji wake na mpaka kustaafu amepokea tuzo nyingi za timu na za binafsi kwa uwezo wake anapokuwa uwanjani na uvunjaji rekodi wake.
|
20231101.sw_2142_5
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Pel%C3%A9
|
Pelé
|
Pelé alizaliwa mjini Três Corações, Minas Gerais, Brazil, na ni mtoto wa mchezaji wa zamani wa Fluminense Dondinho (mtoto wa João Ramos do Nascimento) na Celeste Arantes.Ni mkubwa kati ya watoto wawili. Alipewa jina la shujaa wa Kimarekani Thomas Edison. Wazazi wake waliamua kuitoa herufi "i" na kumuita "Edson",lakini kulikuwa na makosa kwenye cheti chake cha kuzaliwa kusababisha litumike jina la "Edison" badala ya "Edson".F amilia yake walimpa jina la "Dico". Alipewa jina la "Pelé" alipokuwa shule inaposemekana kuwa alishindwa kutamka jina la golikipa wa timu ya Vasco Da Gama anayeitwa Bilé,alivyozidi kulitamka ndivyo alivyozidi kuchapia. Pelé aliwahi kusema hakujua maana ya jina hilo wala marafiki zake waliompa jina hilo.Lakini jina hilo lilitokana na jina la Bilé lakini kwa Kiebrania maana yake ni maajabu (פֶּ֫לֶא),lakini jina halina maana yoyote kwa KIreno.
|
20231101.sw_2142_6
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Pel%C3%A9
|
Pelé
|
Pelé alikulia katika hali ya umaskini huko Bauru kwenye mji wa Paulo.Alijikusanyia fedha kidogo alipofanya kazi kwenye duka la chai.Alfundishwa kucheza mpira wa miguu na baba yake lakini hakuweza mara acheze na soksi iliyojazwa na magazeti au magada ya mapera huku akifunga na kamba.Amechezea klabu nyingi za vijana kama Sete de Setembro, Canto do Rio, São Paulinho, na Amériquinha. Pelé aliisaidia Bauru Athletic Club klabu ya vijana (ikifundishwa na Waldemar de Brito) kushinda mataji mawili ya mashindano ya klabu za vijana za São Paulo.Pelé alishindana mashindano ya mpira wa miguu ya ndani ya chumba ambapo aliisaidia timu yake ya Bauru.
|
20231101.sw_2142_7
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Pel%C3%A9
|
Pelé
|
Pelé aliwahi kukiri kuwa mashindiano hayo yana changamoto kubwa,alisema kuwa kuwa mchezo huo ulikuwa wa haraka kidogo kuliko mpira wa miguu wa kwenye nyasi na kwamba mchezo huo ulihitaji uwezo mkubwa wa kufikiri haraka kwa kuwa kila watu wanakuwa karibukaribu ndani ya uwanja.Pelé anauheshimu sana mchezo huo kwa kuwa ulimpa uwezo mkubwa wa kufikiri papo kwa papo anapokuwa uwanjani.Licha ya hivyo mchezo huo ulimpa uwezo wa kuchezaccredits indoor football for helpin na wakubwa zaidi rika lake alipokuwa na umri wa miaka 14.Katika kila mashindano aliyowahi kucheza alikuwa akichukuliwa kama mdogo asingeweza kucheza lakini kila mashindano yanapoisha yeye ndiye anayekuwa mfungaji bora akiwa na magoli kumi na nne au kumi na tano."Hicho kilinipa kujiamini zaidi", Pelé alisema"Hapo nilijua kuwa nisiwe mwoga kwa chochote kile".
|
20231101.sw_2142_8
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Pel%C3%A9
|
Pelé
|
Mwaka 1956, de Brito alimpeleka Pelé Santos,mji wa viwanda na bandari karibu na São Paulo,alienda kwa majaribio kwenye klabu ya Santos FC,akiwaambia mabosi kuwa kijana wa miaka 15 atakuwa mchezaji mkubwa duniani.Pelé alimshangaza kocha Lula wakati majaribio kwenye uwanja wa Estádio Vila Belmiro, na akasaini mkataba na klabu hiyo Juni 1956.Pelé alitangazwa sana kwenye vyombo vya habari kuwa nyota wa baadae.Alianza vizuri Septemba 7 1956 akiwa na umri wa miaka 15 kwenye ushindi wa 7-1 dhidi ya Corinthians Santo Andre akishinda goli la kwanza.
|
20231101.sw_2142_9
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Pel%C3%A9
|
Pelé
|
Wakati msimu wa 1957 ulipoanza, Pelé alipewa nafasi katika kikosi cha kwanza akiwa na umri wa miaka 16 akawa mfungaji bora wa ligi.Miezi kumi baadaye aliitwa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Brazil.Baada ya kombe la dunia la 1958 na 1962,klabu tajiri za Ulaya kama Real Madrid, Juventus and Manchester United, walijaribu kutaka kumsajili.Mwaka 1958 Iner Milan walimsajili lakini Angelo Moratti ilimbidi akatishe mkataba huo baada ya mwenyekiti wa klabu ya Santos kushambuliwa na shabiki wa Kibrazili.Lakini mwaka 1961 serikali ya Brazil chini ya rais Jânio Quadros ilisema kuwa Pelé ni mchezaji kivutio kwa nchi hivyo haruhusiwi kuhamishwa kwenda nje ya nchi.
|
20231101.sw_2142_10
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Pel%C3%A9
|
Pelé
|
Pelé alishinda taji kubwa kwa mara ya kwanza akiwa na Santos mwaka 1958 ambapo timu ailishinda taji la Campeonato Paulista; Pelé alimaliza mashindano akiwa mfungaji bora wa magoli 58, rekodi inayoshikiliwa hadi sasa.Mwaka mmoja baaadaye aliisaidia nchi yake kushinda mabao 3-0 dhidi ya Vasco Da Gama kwenye michuano ya Torneio Rio-São Paulo Santos hawakuwa na uwezo wa kushindana kwenye michuano hiyo.Mwaka 1960, Pelé alifunga magoli 33 akiisaidia timu yake kurudi tena kwenye michuano ya Campeonato Paulista na kubeba taji hilo lakini walifungwa kwenye michuano ya Rio-São Paulo baada ya kumaliza wakiwa nafasi ya nane.Kwenye msimu wa 1960, Pelé alifunga magoli 47 na kuisaidia Santos kubeba taji la Campeonato Paulista.Walisonga mbele na kubeba taji la Taça Brasil mwaka huohuo kwa kuwafunga Bahia kwenye fainali.Kwenye fainali,Pelé aliibuka mfungaji bora akiwa na magoli 9.
|
20231101.sw_2142_11
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Pel%C3%A9
|
Pelé
|
Mechi ya kwanza ya Pelé kimataifa ilikuwa dhidi ya Argentina waliposhinda 2-1 Julai 7 1957 uwanja wa Maracanã.Kwenye mechi hiyo alifunga goli lake la kwanza akiwa na timu yake ya taifa akiwa na miaka 16 na miezi tisa na anabaki kuwa mchezaji mdogo wa Brazili kuwahi kufinga goli kwenye timu yake ya taifa.
|
20231101.sw_2142_12
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Pel%C3%A9
|
Pelé
|
Pelé alienda nchini Sweden akiwa na jeraha la goti lakini wenzake walimtetea ili aitwe kwenye kikosi.Mechi yake ya kwanza ilikuwa dhidi ya USSR kwenye mechi ya tatu kwenye mzunguko wa kwanza wa kombe la dunia la mwaka 1958,ambapo alimpa pasi Vavá iliyozaa goli la pili.Alikuwa mchezaji mdogo kuliko wote kwenye michuano na mchezaji mdogo kuwahi kucheza kombe la dunia.Dhidi ya Ufaransa kwenye nusu fainali,Brazili walikuwa wakiongoza 2-1.
|
20231101.sw_2142_13
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Pel%C3%A9
|
Pelé
|
Mnamo Desemba 29, 2022, Pelé alifariki akiwa na umri wa miaka 82 katika hospitali ya Israeli ya Albert Einstein huko São Paulo, Brazil. Wakala wake Joe Fraga alithibitisha kifo chake. Pelé alikuwa akitibiwa kansa ya utumbo mkubwa tangu mwaka 2021 na alikuwa amelazwa hospitalini kwa mwezi mmoja uliopita.
|
20231101.sw_2145_0
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Eastleigh
|
Eastleigh
|
Eastleigh (Uingereza) ni mji wa Uingereza wa kusini karibu na Southampton katika wilaya ya Hampshire
|
20231101.sw_2145_1
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Eastleigh
|
Eastleigh
|
Kutokana na mji huu ni jina la maeneo yaliyowahi kutawaliwa na Uingereza katika sehemu mbalimbali ya dunia:
|
20231101.sw_2145_2
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Eastleigh
|
Eastleigh
|
Eastleigh (Nairobi) ni mtaa au eneo la mji mkuu wa Kenya inayopakana na mitaa ya Pangani pia Mathare Valley
|
20231101.sw_2145_3
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Eastleigh
|
Eastleigh
|
Jina limetokana na maneno "east" = mashariki na "leigh" kutokana na Kiingereza ya Kale "leah" / "legh" yaani aina ya mti.
|
20231101.sw_2150_0
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mkoa%20wa%20Tanga
|
Mkoa wa Tanga
|
Mkoa wa Tanga ni kati ya mikoa 31 ya Tanzania na uko Kaskazini Mashariki mwa nchi, ukipakana na Kenya upande wa Kaskazini, Bahari Hindi upande wa mashariki na mikoa ya Morogoro, Manyara na Kilimanjaro wenye Postikodi namba 21000. Mpaka upande wa kusini unafuata mto Mligaji kuutenganisha na mkoa wa Pwani.
|
20231101.sw_2150_1
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mkoa%20wa%20Tanga
|
Mkoa wa Tanga
|
Tanga ni kati ya mikoa midogo ya Tanzania ikiwa na msongamano mkubwa wa wakazi ndani ya eneo lake. Msongamano ni mkubwa hasa wilaya ya Lushoto kwenye ardhi yenye rutuba nzuri.
|
20231101.sw_2150_2
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mkoa%20wa%20Tanga
|
Mkoa wa Tanga
|
Mkoa una eneo la km² 27,348 ambalo linaunganisha sehemu za pwani pamoja na milima ya ndani kama Usambara.
|
20231101.sw_2150_3
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mkoa%20wa%20Tanga
|
Mkoa wa Tanga
|
Kuna wilaya 10 ambazo ni Handeni Vijijini, Handeni Mjini, Kilindi, Korogwe Vijijini, Korogwe Mjini, Lushoto, Mkinga, Muheza, Pangani na Tanga Mjini.
|
20231101.sw_2150_4
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mkoa%20wa%20Tanga
|
Mkoa wa Tanga
|
Kwa jumla hali ya hewa ni joto lenye unyevu. Handeni kuna joto kavu zaidi. Milima ya Usambara hakuna joto sana.
|
20231101.sw_2150_5
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mkoa%20wa%20Tanga
|
Mkoa wa Tanga
|
Miezi ya Desemba - Machi halijoto huko Tanga inafikia sentigredi 30-32 mchana na 26-29 usiku. Wakati wa Mei hadi Oktoba halijota inapoa: ni sentigredi 23-28 mchana na 20-24 usiku. Unyevu iko juu kati ya asilimia 100 na asilimia 65.
|
20231101.sw_2150_6
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mkoa%20wa%20Tanga
|
Mkoa wa Tanga
|
Maeneo mengi ya mkoa hupokea angalau milimita 750 za mvua kwa mwaka au zaidi. Pwani ni zaidi: takriban milimita 1,100 hadi 1,400 ikipungua sehemu za ndani isipokuwa milima ya Usambara ambako mvua inaweza kuzidi milimita 2000 kwa mwaka.
|
20231101.sw_2150_7
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mkoa%20wa%20Tanga
|
Mkoa wa Tanga
|
Makabila makubwa mkoani Tanga ni Wasambaa, Wazigua, Wabondei na Wadigo. Mengine ni Wapare, Wataita, Wambugu, Wasegeju na Wanago.
|
20231101.sw_2150_8
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mkoa%20wa%20Tanga
|
Mkoa wa Tanga
|
Wasambaa ndio kabila kubwa lililoko katika milima ya Usambara, Muheza, Korogwe na Lushoto. Kwa jumla ndio asilimia 40 ya wakazi wote wa mkoa.
|
20231101.sw_2150_9
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mkoa%20wa%20Tanga
|
Mkoa wa Tanga
|
Wazigua ni kabila kubwa huko Handeni na sehemu za Korogwe na Pangani. Wabondei wako hasa Muheza na sehemu za Pangani. Wadigo ndio wengi Tanga yenyewe na sehemu za pwani.
|
20231101.sw_2150_10
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mkoa%20wa%20Tanga
|
Mkoa wa Tanga
|
Katika mkoa huu elimu inahitaji kuboreshwa zaidi, hasa maeneo ya vijijini, maana watu wengi wa mkoa huu hufanya shughuli zao za kimila; hali hiyo huwafanya kushindwa kuendelea na shughuli za kimaendeleo katika taifa la Tanzania.
|
20231101.sw_2150_11
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mkoa%20wa%20Tanga
|
Mkoa wa Tanga
|
Wilaya ya Handeni kuna machimbo ya madini, ila kuhusu elimu ipo nyuma sana kwani mpaka sasa hakuna shule ya sekondari inayotoa huduma ya kidato cha tano na sita. Kama haitoshi shule za watu binafsi hakuna hata moja.
|
20231101.sw_2150_12
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mkoa%20wa%20Tanga
|
Mkoa wa Tanga
|
Katani ilikuwa zao la biashara hasa kwa ajili ya Tanga tangu kuingizwa kutoka Mexico zamani za Afrika ya Mashariki ya Kijerumani. Hulimwa kote mkoani isipokuwa Lushoto, hasa Muheza na Korogwe kwenye mashamba makubwa. Mashamba hayo yalikuwa ya walowezi, yakataifishwa baada ya uhuru. Tangu kuanguka kwa sekta ya umma yamebinafsishwa tena siku hizi. Zao la katani linategemea sana soko la dunia, umuhimu wake ulirudi nyuma tangu miaka ya 1960.
|
20231101.sw_2150_13
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mkoa%20wa%20Tanga
|
Mkoa wa Tanga
|
Tanga ilikuwa na viwanda vingi kiasi katika miaka ya 1960 na 1970 lakini karibu vyote vimekwama kutokana na siasa ya Ujamaa na uchumi wake ulioiga mfumo wa nchi za kisoshalisti. Viwanda vichache vilivyobaki havizalishi mali kulingana na uwezo wao. Kilichobaki hasa ni kiwanda cha saruji Tanga.
|
20231101.sw_2150_14
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mkoa%20wa%20Tanga
|
Mkoa wa Tanga
|
Utalii umeanza kupanuka kidogo, hasa katika eneo la Pangani, Mapango ya Amboni na kituo cha Makumbusho Urithi Tanga.
|
20231101.sw_2152_0
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Afrika%20ya%20Mashariki%20ya%20Kijerumani
|
Afrika ya Mashariki ya Kijerumani
|
Afrika ya Mashariki ya Kijerumani (au: ya Kidachi; kwa Kijerumani Deutsch-Ostafrika -DOA-; kwa Kiingereza German East Africa) ilikuwa jina la koloni la Ujerumani huko Afrika ya Mashariki kati ya miaka 1885 na 1918/1919.
|
20231101.sw_2152_1
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Afrika%20ya%20Mashariki%20ya%20Kijerumani
|
Afrika ya Mashariki ya Kijerumani
|
Eneo lake lilijumlisha nchi za kisasa za Tanzania bara (yaani bila Zanzibar), Burundi na Rwanda. Ilikuwa koloni kubwa kabisa la Dola la Ujerumani.
|
20231101.sw_2152_2
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Afrika%20ya%20Mashariki%20ya%20Kijerumani
|
Afrika ya Mashariki ya Kijerumani
|
Eneo la koloni lilikuwa na kilomita za mraba 997,000 pamoja na sehemu za maziwa makubwa kama Ziwa Tanganyika na Ziwa Viktoria. Eneo hili lilikuwa karibu mara mbili kuliko eneo la Ujerumani wenyewe kabla ya mwaka 1914.
|
20231101.sw_2152_3
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Afrika%20ya%20Mashariki%20ya%20Kijerumani
|
Afrika ya Mashariki ya Kijerumani
|
Mipaka iliamuliwa katika mapatano na Uingereza, Ubelgiji na Ureno zilizotawala makoloni ya jirani ya Afrika ya Mashariki ya Kiingereza (leo Kenya na Uganda), Kongo ya Kibelgiji (leo Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo), Rhodesia (leo Zambia na Zimbabwe), Nyasaland (leo Malawi) na Msumbiji. Mipaka hii ni pia mipaka ya Tanzania, Rwanda na Burundi hadi leo hii.
|
20231101.sw_2152_4
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Afrika%20ya%20Mashariki%20ya%20Kijerumani
|
Afrika ya Mashariki ya Kijerumani
|
Katika mapatano baina ya Uingereza na Ujerumani ya Novemba 1886 pande zote mbili ziliahidi kuheshimu utawala wa Sultani wa Zanzibar juu ya visiwa pamoja na kanda la maili 10 kwenye pwani baina ya mto Tana na Mto Minengani (Msumbiji). Pamoja na hayo walielewana kuhusu maeneo ya maslahi yao, wakipatana kuhusu mstari uliokuwa baadaye mpaka baina ya Tanzania na Kenya hadi leo.
|
20231101.sw_2152_5
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Afrika%20ya%20Mashariki%20ya%20Kijerumani
|
Afrika ya Mashariki ya Kijerumani
|
Katika mkataba wa 1890 kuhusu mipaka katika Afrika Uingereza iliahidi kumshawishi Sultani wa Zanzibar kuuza maeneo yake kwenye pwani la bara pamoja na kisiwa cha Mafia kwa Ujerumani.
|
20231101.sw_2152_6
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Afrika%20ya%20Mashariki%20ya%20Kijerumani
|
Afrika ya Mashariki ya Kijerumani
|
Upande wa Kenya mstari ulichorwa kuanzia Bahari Hindi kwa mdomo wa mto Umba hadi Ziwa Jipe, halafu kufuata mitelemko ya kaskazini ya mlima Kilimanjaro na kutoka hapa hadi Ziwa Viktoria. Mipaka na Uganda ilifuata latitudo ya kwanza ya kusini ya ikweta hadi mpaka na Kongo. Upande wa Kongo mpaka ulifuata sehemu za chini za bonde la Ufa na katikati ya maziwa kama Kivu na Tanganyika.
|
20231101.sw_2152_7
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Afrika%20ya%20Mashariki%20ya%20Kijerumani
|
Afrika ya Mashariki ya Kijerumani
|
Upande wa kusini ulifuata mstari kati ya ncha ya kusini ya ziwa Tanganyika hadi mdomo wa Mto Songwe katika Ziwa Nyasa. Eneo lote la ziwa lenyewe lilibaki upande wa Nyasaland ya Kiingereza, halafu mstari kutoka Ziwa Nyasa kwa kufuata mto Ruvuma hadi Rasi ya Delgado kwenye Bahari Hindi.
|
20231101.sw_2152_8
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Afrika%20ya%20Mashariki%20ya%20Kijerumani
|
Afrika ya Mashariki ya Kijerumani
|
Mwaka 1913 takwimu ya Wajerumani ilihesabu wakazi Waafrika 7,645,000, Waasia (Wahindi na Waarabu) 14,898 na Wazungu 5,336, kati yao Wajerumani 4,107. Nusu ya wakazi wote waliishi katika eneo la maziwa makubwa ambako serikali ya kikoloni iliacha maeneo ya Rwanda (wakazi 2,000,000), Burundi (1,500,000) na Bukoba (275,000) kama maeneo lindwa chini ya watawala wa kienyeji waliosimamiwa na afisa mkazi Mjerumani.
|
20231101.sw_2152_9
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Afrika%20ya%20Mashariki%20ya%20Kijerumani
|
Afrika ya Mashariki ya Kijerumani
|
Koloni hilo halikuanzishwa kwa azimio la kisiasa upande wa serikali ya Ujerumani bali lilianzishwa kama mradi wa watu binafsi waliotafuta makoloni katika Afrika.
|
20231101.sw_2152_10
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Afrika%20ya%20Mashariki%20ya%20Kijerumani
|
Afrika ya Mashariki ya Kijerumani
|
mwanzo kama maeneo yaliyotawanyika ambako kampuni binafsi (Kampuni ya Kijerumani kwa Afrika ya Mashariki) ilifaulu kushawishi watawala wa kienyeji kutia sahihi kwenye mikataba; kipindi hiki kilianza 1885 hadi kuporomoka kwa utawala wa kampuni mnamo 1890
|
20231101.sw_2152_11
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Afrika%20ya%20Mashariki%20ya%20Kijerumani
|
Afrika ya Mashariki ya Kijerumani
|
koloni la Dola la Ujerumani (kwa Kijerumani Deutsches Reich) lililoamua kuchukua mamlaka mkononi mwake kuanzia 1891, ambako Ujerumani iliweza kupanusha utawala wake juu ya maeneo yote
|
20231101.sw_2152_12
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Afrika%20ya%20Mashariki%20ya%20Kijerumani
|
Afrika ya Mashariki ya Kijerumani
|
mwisho wa utawala wa Kijerumani wakati wa Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia kuanzia mwaka 1916 wakati jeshi kubwa la Uingereza na Afrika Kusini pamoja na Ubelgiji lilivamia, hadi kusalimu amri kwa jeshi la Schutztruppe kwenye Novemba 1918
|
20231101.sw_2152_13
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Afrika%20ya%20Mashariki%20ya%20Kijerumani
|
Afrika ya Mashariki ya Kijerumani
|
Katika mapatano baada ya vita koloni liligawiwa kati ya Uingereza (iliyopata Tanganyika) na Ubelgiji (iliyopata Rwanda na Burundi). Kwa historia ya baadaye ilikuwa na maana ya kwamba walikabidhiwa maeneo ya koloni la Kijerumani la awali si kama mali kamili lakini kama maeneo ya kudhaminiwa kwa niaba ya shirikisho la Mataifa (mtangulizi wa Umoja wa Mataifa (UN).
|
20231101.sw_2152_14
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Afrika%20ya%20Mashariki%20ya%20Kijerumani
|
Afrika ya Mashariki ya Kijerumani
|
Hadi mnamo mwaka 1880 serikali ya Ujerumani chini ya chansella Otto von Bismarck ilikataa kuanzisha makoloni. Sehemu ya wafanyabiashara Wajerumani walidai koloni. Walisikitika kuona faida za wenzao Waingereza waliopata mara nyingi msaada kutoka kwa wanajeshi na serikali za koloni za Uingereza hasa Asia. Waliona pia faida ya viwanda vya Uingereza vilivyokuwa na soko la kulindwa katika nchi kama Uhindi kwa sababu serikali ya kikoloni ilidai kodi kali kwa bidhaa zisizotoka Uingereza.
|
20231101.sw_2152_15
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Afrika%20ya%20Mashariki%20ya%20Kijerumani
|
Afrika ya Mashariki ya Kijerumani
|
Bismarck hakuamini ya kwamba koloni lingeleta faida kwa taifa kulingana na gharama kubwa kwa serikali. Lakini wapigania koloni walikuwa na wabunge muhimu kwa serikali na polepole Bismarck alianza kukubali hatua za kwanza.
|
20231101.sw_2152_16
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Afrika%20ya%20Mashariki%20ya%20Kijerumani
|
Afrika ya Mashariki ya Kijerumani
|
Mwenyewe aliamini mwanzoni ya kwamba itatosha kuwapa wafanyabiashara ulinzi kwa shughuli zao kwa kuwaruhusu matumizi ya bendera ya Ujerumani na kuwa na askari wao wa ulinzi kama wamepatana na viongozi wazalendo katika eneo fulani kuanzisha shughuli huko. Kwa njia hii alifungua mlango kwa harakati iliyoendelea kuwa mchango wa Ujerumani katika mbio wa kugawa dunia, hasa Afrika.
|
20231101.sw_2152_17
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Afrika%20ya%20Mashariki%20ya%20Kijerumani
|
Afrika ya Mashariki ya Kijerumani
|
Koloni hili lilianzishwa na kijana Mjerumani Karl Peters mwaka 1885 kwa niaba ya "Kampuni ya Kijerumani kwa Afrika ya Mashariki".
|
20231101.sw_2152_18
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Afrika%20ya%20Mashariki%20ya%20Kijerumani
|
Afrika ya Mashariki ya Kijerumani
|
Peters, aliyewahi kusoma chuo Uingereza, aliona wivu juu ya ukoloni wa Uingereza, akiamini ya kwamba Ujerumani ungestahili nafasi hiyo pia. Hivyo alianza kudai koloni katika mikutano, akaanzisha "Shirika kwa Ukoloni wa Kijerumani" mwaka 1884 iliyokuwa kitangulizi cha kampuni.
|
20231101.sw_2152_19
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Afrika%20ya%20Mashariki%20ya%20Kijerumani
|
Afrika ya Mashariki ya Kijerumani
|
Shirika hii ilimtuma pamoja na wenzake wawili kwenda Afrika na kutafuta nafasi ya kuanzisha koloni. Kiasili walilenga maeneo mpakani mwa Msumbiji na Zimbabwe ya leo lakini hatimaye waliamua kwenda Afrika ya Mashariki. Peters alifika Zanzibar alipoambiwa na konsuli ya Ujerumani ya kwamba hawezi kuendelea: serikali ya nyumbani iliogopa ugomvi na Uingereza ilikataa mipango yake. Aliamua kuvuka barani hata hivyo akafika Saadani tarehe 10 Novemba 1884 na kufuata njia kando ya mto Wami ili apite kanda la Kizanzibari kwenye pwani na kutembelea machifu na masultani ndani ya bara.
|
20231101.sw_2152_20
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Afrika%20ya%20Mashariki%20ya%20Kijerumani
|
Afrika ya Mashariki ya Kijerumani
|
Hapo alifaulu kushawishi watawala wa maeneo yaliyojulikana kama Usagara, Nguru, Useguha na Ukami kutia sahihi kwenye mikataba iliyoandikwa kwa Kijerumani ambayo hawakuielewa. Mikataba hii ilisema ya kwamba mtawala alikabidhi kwa kampuni nchi yake pamoja na haki juu ya ardhi na mali yote.
|
20231101.sw_2152_21
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Afrika%20ya%20Mashariki%20ya%20Kijerumani
|
Afrika ya Mashariki ya Kijerumani
|
Mwaka 1885 Peters alirudi Berlin na kuonyesha mikataba yake kwa magazeti na serikali. Chansela Bismarck alikataa, akacheka mikataba kama karatasi bila maana.
|
20231101.sw_2152_22
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Afrika%20ya%20Mashariki%20ya%20Kijerumani
|
Afrika ya Mashariki ya Kijerumani
|
Peters alitumia mbinu: akatisha kupeleka mikataba yake kwa mfalme Leopold II wa Ubelgiji aliyekuwa kununua haki zake. Hapa Bismarck aliogopa kilio cha wapenda koloni akakubali kumpa Peters hati ya ulinzi ya tarehe 27 Februari 1885 kwa maeneo yaliyokuwa ya kampuni kufuatana na mikataba.
|
20231101.sw_2152_23
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Afrika%20ya%20Mashariki%20ya%20Kijerumani
|
Afrika ya Mashariki ya Kijerumani
|
Peters na wawakilishi wake walirudi wakaendelea kutafuta machifu waliokuwa tayari kutia saini mikataba yake. Sultani wa Zanzibar alipinga juhudi hizi. Zanzibar ilisimamia pwani ya Afrika ya Mashariki na tangu karne watu wa miji ya pwani walikuwa na mawali wa Sultani.
|
20231101.sw_2152_24
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Afrika%20ya%20Mashariki%20ya%20Kijerumani
|
Afrika ya Mashariki ya Kijerumani
|
Zanzibar ilidai pia utawala ya bara hadi Ziwa Tanganyika na Kongo, ingawa hali halisi athira yake haikwenda mbali na njia za misafara ambako ndovu na watumwa walipelekwa pwani.
|
20231101.sw_2152_25
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Afrika%20ya%20Mashariki%20ya%20Kijerumani
|
Afrika ya Mashariki ya Kijerumani
|
Tarehe 27 Aprili 1885 serikali ya Zanzibar ilituma barua Berlin kupinga kazi na madai ya kampuni na kutangaza maeneo ya Tanzania ya leo kama milki yake. Iliongeza pia wanajeshi wake barani zilizokuwa chini ya amri ya mwanajeshi mstaafu Mwingereza Matthews. Hapo serikali ya Berlin ilituma kikosi cha manowari kwenda Bahari Hindi.
|
20231101.sw_2152_26
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Afrika%20ya%20Mashariki%20ya%20Kijerumani
|
Afrika ya Mashariki ya Kijerumani
|
Mwezi Agosti manowari za Kijerumani chini ya amri ya admirali Eduard von Knorr zilifika mbele ya Unguja zikalenga mizinga yao kwa ikulu ya sultani. Akishauriwa na balozi wa Uingereza, Sultani Bargash alipaswa kutoa tamko kuwa, "Kutokana na madai tunayopelekewa kwa matishio na Kaisari wa Ujerumani, tunatambua ulinzi wa Ujerumani juu ya nchi za Usagara, Nguru, Useguha, Ukami na juu ya wilaya ya Witu. Mipaka yake itaelezwa baadaye na sisi tunatambua ulinzi wa Kaisari juu ya mahali palipotajwa." .
|
20231101.sw_2152_27
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Afrika%20ya%20Mashariki%20ya%20Kijerumani
|
Afrika ya Mashariki ya Kijerumani
|
Sultani alipaswa pia kutia sahihi mkataba wa biashara na Ujerumani alipokubali haki nyingi kwa Wajerumani katika milki yake.
|
Subsets and Splits
No community queries yet
The top public SQL queries from the community will appear here once available.