_id
stringlengths 15
22
| url
stringlengths 31
150
| title
stringlengths 1
86
| text
stringlengths 100
23.8k
|
---|---|---|---|
20231101.sw_2194_3
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Jibuti
|
Jibuti
|
Kwa kilomita 13 Jibuti inapakana na Eritrea, huku kukiwa na urefu wa kilomita 337 za mpaka kati ya Jibuti na Ethiopia, na mpaka wa km 58 na Somalia. Kwa jumla ina mpaka wa km 506. Pia ina pwani ya urefu wa km 314.
|
20231101.sw_2194_4
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Jibuti
|
Jibuti
|
Jibuti inakaa kaika eneo la kufana, ikiwa karibu na leni zenye shughuli nyingi zaidi duniani la meli na pia karibu na mahali pa uchimbaji mafuta nchini Saudi Arabia.
|
20231101.sw_2194_5
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Jibuti
|
Jibuti
|
Milima iliyopo katikati ya nchi hugawa tambarare za pwani kutoka plateau. Eneo la chini zaidi ni Ziwa Assal mita 155 chini ya usawa wa bahari na la juu zaidi ni volikano Moussa Ali yenye kimo cha mita 2028. Hakuna shamba la ukulima, unyunyizaji maji, mimea iliyojimeza huko (msitu upo tu katika milima ya Goda, hasa mbuga ya Day Forest). Takribani asilimia 9 ya nchi ni malisho yeliyojimeza (1993 mashariki). Kwa hiyo Jibuti inahesabiwa kuwa sehemu ya nyasi ya Ethiopia, isipokuwa kijisehemu kinachopakana na Bahari ya Shamu ambacho ni baadhi ya Jangwa la Pwani ya Eritrea ambayo inajulikana kuwa njia nzuri ya uhamiaji wa ndege ambao wanaweza kuwindwa.
|
20231101.sw_2194_6
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Jibuti
|
Jibuti
|
Matukio ya kimaumbile ni pamoja na Matetemeko ya ardhi, kiangazi, mawimbi kutoka Bahari ya Hindi ambayo husababisha mafuriko na mvua kubwa. Malighafi ni pamoja na umeme kutoka ardhini (geothermal energy). Eneo hili limekumbwa na uhaba wa maji salama ya kunywa na pia kugeuka kwa eneo hilo kuwa jangwa.
|
20231101.sw_2194_7
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Jibuti
|
Jibuti
|
Jibuti ni mwanachama wa makubaliano ya kimataifa kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa, ueneaji wa jangwa, viumbehai vilivyo hatarini, sheria ya bahari, kulinda ukanda wa ozoni na uharibifu wa mazingira na meli.
|
20231101.sw_2194_8
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Jibuti
|
Jibuti
|
Nchi ilikuwa koloni la Ufaransa kwa jina la Somalia ya Kifaransa, halafu (1967) Eneo la Kifaransa la Waafar na la Waisa, kutokana na majina ya makabila mawili makubwa zaidi ya eneo hilo.
|
20231101.sw_2194_9
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Jibuti
|
Jibuti
|
Sababu ya kuanzishwa kwa koloni ilikuwa nia ya Ufaransa ya kuwa na bandari ya mji wa Jibuti karibu na Bab el Mandeb inayotawala mawasiliano kati ya Bahari Hindi na Bahari ya Shamu kuelekea Mfereji wa Suez.
|
20231101.sw_2194_10
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Jibuti
|
Jibuti
|
Hadi leo umuhimu na uchumi wake unategemea bandari, ambapo zinapitia asilimia 95 za bidhaa zinazoingizwa Ethiopia. Nchi hiyo imeunganishwa na Jibuti kwa reli, moja ya zamani, na nyingine mpya iliyokamilika mwaka 2016.
|
20231101.sw_2194_11
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Jibuti
|
Jibuti
|
Siku hizi wakazi wengi (60%) ni Wasomali, hasa wa kabila la Waisa, halafu Waafar (35%). Asilimia 5 zilizobaki ni Waarabu, Waethiopia na Wazungu (hasa Wafaransa na Waitalia).
|
20231101.sw_2194_12
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Jibuti
|
Jibuti
|
Upande wa dini, Uislamu unafuatwa na 94% za wakazi na ndio dini rasmi pekee. Asilimia 6 wanafuata Ukristo katika madhehebu mbalimbali, hasa Waorthodoksi wa Mashariki kutoka Ethiopia (3.2%), halafu Wakatoliki (1.4%) na Waprotestanti (chini ya 1%).
|
20231101.sw_2201_0
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mbuni
|
Mbuni
|
Mbuni ni ndege wakubwa wa familia Struthionidae. Kuna spishi mbili katika jenasi moja, lakini wataalamu wengine wanafikiri ni spishi moja tu. Ndege hao ni wakubwa kuliko wengine wote. Wana miguu mirefu na shingo ndefu na wanaweza kukimbia sana, hata kwa mwendo wa km 65 kwa saa, lakini hawawezi kuruka hewani.
|
20231101.sw_2201_1
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mbuni
|
Mbuni
|
Rangi za manyoya ya dume ni nyeusi na nyeupe na rangi ya ngozi yake (shingo na miguu) ni nyekundu, pinki au buluu kufuatana na nususpishi. Manyoya ya jike ni kahawiakijivu na rangi ya ngozi ni sawa na dume. Mbuni wanaishi katika savana, nyika na majangwa ya Afrika, lakini wanafugwa ulimwenguni mwote.
|
20231101.sw_2201_2
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mbuni
|
Mbuni
|
Jina la kisayansi la spishi kuu, Struthio camelus, linatoka katika lugha ya Kiyunani: στρουθιον = jurawa na καμηλος = ngamia.
|
20231101.sw_2201_3
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mbuni
|
Mbuni
|
Dume la mbuni ana harimi ya majike 2-7 lakini moja tu anatawala. Dume hupanda majike yote ya harimi yake na majike huyataga mayai yao yote katika tago moja ambalo dume amelitengeneza. Jike anayetawala hutaga kwanza na baadaye hutupa mayai ya majike wasio na nguvu sana. Kwa kawaida hubakisha mnamo mayai 20. Majike huyaatamia mayai mchana na dume hufanya usiku, kwa sababu rangi ya jike inafanana na mchanga na rangi nyeusi ya dume haionekani usiku.
|
20231101.sw_2201_4
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mbuni
|
Mbuni
|
Mbuni ni ndege wakubwa, huku asili yao ikiwa ni Afrika. Hawa ni ndege wasio na uwezo wa kuruka. Wanapatikana kwenye oda ya Struthioniformes, pamoja na ndugu aitwaye kiwi. Mbuni ni wa pekee sana sababu ya muonekane wake, wa shingo na miguu mirefu pamoja na uwezo wake mkubwa wa kukimbia, karibu ya maili 45 kwa saa. Huu ni mwendokasi mkubwa zaidi kwa ndege yeyote ardhini. Mbuni ndiyo ndege mkubwa kuliko wote wanaoishi duniani, wakiwa pia ndio watagaji wa mayai makubwa kuliko wote pia.
|
20231101.sw_2201_5
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mbuni
|
Mbuni
|
Mlo wa mbuni kwa kiasi kikubwa huwa ni mimea, ingawa pia hula wadudu. Mbuni huishi katika makundi ya kutansatanga kati ya ndege watano mpaka hamsini. Wanapotishwa, mbuni hujificha kwa kulala ardhini au kukimbia mbali kama wakizingirwa, hushambulia adui zao kwa miguu yao yenye nguvu. Tabia kujamiiana hutofautiana kutoka maeneo moja mpaka vingine, ambapo mbuni dume hupigaia mbani jike hupigania nafasi ya kuwapata mbuni jike kwa nguvu.
|
20231101.sw_2201_6
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mbuni
|
Mbuni
|
Mbuni hufugwa dunia nzima, hasa kutokana na manyoya yake, ambayo hunitia na kutumika kuondolea vumbi. Ngozi yake hutumika kutangenezea mtu mbali mbali huku nyama yake ikilizwa kibiashara.
|
20231101.sw_2201_7
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mbuni
|
Mbuni
|
Mbuni huwa na uzito wa kilogramu 63-130, luku mbuni dume wakifika mpaka uzito wa kg 155. Manyoya ya mbuni dumu wakubwa huwa kwa kiasi kikubwa meusi huku mkia ukiwa wakubwa huwa na rangi ya kahawia na nyeupe. Vichwa vya mbuni wote huwa havina manyoya. Ngozi za mbuni jike huwa na rangi ya pinki – kijini, huku dume wakiwa na ngozi ya bluu au kijini kutegemeana na nususpishi.
|
20231101.sw_2201_8
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mbuni
|
Mbuni
|
Shingo zao ndefu, hukiweka kichwa chao mita 1.8 mpaka 2.75 juu ya ardhi, na macho yao husemwa kuwa ndiyo makubwa kuliko wanyama wote wa ardhini, yakiwa na sm 5, hivyo huweza kuwaona adui zao hata wakiwa mbali sana. Macho yao yanakingwa na mwanga mkali wa jua kutoka juu.
|
20231101.sw_2201_9
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mbuni
|
Mbuni
|
Miguu ya mbuni, kama ilivyo kwa ndege wengine, haina manyoya isipokuwa magamba. Ndege hawa wawili huwa na vidole vikubwa viwili huku wengi wakiwa na vine, huku kucha moja ikiwa kubwa, ikifanana na kwato. Mbawa hutanuka kwa upana wa mita 2 hivyi, na hutumika sana kwenye tabia za kujamiiana na kujikinga na jua. Wana manyoya 50-60 hivi ya mkiani. Midomo yao huwa mipana na ncha ya duara kidogo. Tofauti na ndege wengine, mbuni hutoa mkoja tofauti na kinyesi, hivyo kuwa na kibofu. Pia tofauti na ndege wengine tena, huwa na ogani ya kutolea manii inayoweza kutoka nje ya mwili kwa urefu wa inchi 8.
|
20231101.sw_2201_10
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mbuni
|
Mbuni
|
Mbuni hukomaa na kuwa na uwezo wa kuzaa wakiwa na miaka miwili/minne watoto wa mbuni hukua kwa kiasi ya sm 25 kwa mwezi. Wakiwa na umri wa mwaka mmoja tu, mbuni huwa na uzito wa kg 45. Mbuni jike huweza kuyatambua mayai yake hata kwenye kiota cha jumuiya.
|
20231101.sw_2201_11
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mbuni
|
Mbuni
|
Kujamiiana huwa na misimu tofauti kutokana na maeneo. Mbuni dume hupigania nafasi ya kujamiiana na jike wengine, na akishinda basi huwa na uwezo wa kujamiiana na jike wote wa kundi lake lote japo atakuwa na jike wake atakayedumu naye kwa wakati husika.
|
20231101.sw_2201_12
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mbuni
|
Mbuni
|
Mbuni dume humvutia mbuni jike, kwa kumchezeachezea na kumpigia mbawa zake, ambaye humfuata na wao huenda faragha kwa ajili ya kujamiiana. Wakifika huko huwafukuza wanyama/mbuni wengine kama wapo na kisha dume kuweza tena, mbuni jike hukaa chini na kuwa tayari kwa kujamiiana.
|
20231101.sw_2201_13
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mbuni
|
Mbuni
|
Mbuni jike hutaga mayai yaliyorutubishwa kwenye kiota cha jumuiya, ambacho huwa ni shimo lenye upana wa mita tatu na kina cha sentimeta 30-60. Mbuni dume ndiyo huchimba kiota hiki mayai ya mbuni ndiyo mayai makubwa kuliko yote na huwa na uzito wa kg 1.4, zaidi ya mara 20 ya yai la kuku. Huwa na rangi ya maziwa na wakati mwingine pamoja na madoa madogo. Mayai hutumiwa na mbuni jike wakati wa mchana na kutamiwa na mbuni dume wakati wa usiku .
|
20231101.sw_2201_14
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mbuni
|
Mbuni
|
Mayai huanguliwa baada ya siku 35-45, na kisha hapo mbuni jike na dume wote hushirikiana kuwakuza watoto wao. Mbuni weusi huwindwa wakati huu, na mara nyingi mbuni mtoto mmoja tu ndiyo hufanikiwa kukua, huku wengine wakigeuzwa kitoweo na wanyama wengine wala nyama.
|
20231101.sw_2201_15
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mbuni
|
Mbuni
|
Mbuni wanaokuzwa na binadamu, huhamisha sana upendo wao, na kuanza kuwapenda sana binadamu wanaowatunza.
|
20231101.sw_2201_16
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mbuni
|
Mbuni
|
Struthio asiaticus (Asian Ostrich) (Asia ya kati mpaka China, mwanzo wa Pliocene - mwisho wa Pleistocene)
|
20231101.sw_2201_17
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mbuni
|
Mbuni
|
Struthio chersonensis (Ulaya wa kusini mashariki mpaka Asia ya magharibi ya kati, Pliocene) - spishi kutoka mayai
|
20231101.sw_2201_18
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mbuni
|
Mbuni
|
Struthio karingarabensis (Afrika ya kusini magharibi na kati, mwisho wa Miocene - mwanzo wa Pliocene) - spishi kutoka mayai(?)
|
20231101.sw_2205_0
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mfumo%20wa%20Jua
|
Mfumo wa Jua
|
Mfumo wa Jua (:en:solar system) ni mpangilio wa Jua letu, sayari na sayari kibete zinazolizunguka pamoja na miezi yao, asteroidi, meteoridi, kometi na vumbi la angani, vyote vikishikwa na graviti ya Jua.
|
20231101.sw_2205_1
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mfumo%20wa%20Jua
|
Mfumo wa Jua
|
Karibu masi yote ni ya Jua lenyewe, likiwa na asilimia 99.86 za masi ya mfumo wake. Kwa hiyo sayari zote kwa pamoja na asteroidi ni asilimia 0.14 tu ya masi ya mfumo kwa jumla.
|
20231101.sw_2205_2
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mfumo%20wa%20Jua
|
Mfumo wa Jua
|
Umbali kati ya Jua na Dunia yetu ni takriban kilomita milioni 150. Umbali huu unaitwa "kizio astronomia" (:en:astronomical unit AU). Sayari ya mbali zaidi ni Neptuni ambayo ipo katika umbali wa vizio astronomia 30 kutoka Jua yaani ipo mara 30 mbali zaidi kutoka Jua kuliko Dunia. Magimba ya nje sana yanazunguka Jua kwa umbali wa vizio astronomia 50 au zaidi.
|
20231101.sw_2205_3
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mfumo%20wa%20Jua
|
Mfumo wa Jua
|
Pamoja na sayari kuna idadi kubwa ya violwa vingine. Vingi ni vipande vidogo vya mwamba vinavyokusanyika katika kanda 3 zenye umbo la mwiringo ambazo ni ukanda wa asteroidi, ukanda wa Kuiper na wingu la Oort.
|
20231101.sw_2205_4
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mfumo%20wa%20Jua
|
Mfumo wa Jua
|
Sayari hupatikana katika vikundi viwili. Mara nyingi zinaitwa "Sayari za ndani" na "Sayari za nje".Sayari nne za ndani ni Utaridi, Zuhura, Dunia na Mirihi ambazo ni ndogo na ni sayari za mwamba kama Dunia.
|
20231101.sw_2205_5
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mfumo%20wa%20Jua
|
Mfumo wa Jua
|
Baada ya obiti ya Mirihi kuna pengo lenye upana wa vizio astronomia zaidi ya tatu na nusu hadi Mshtarii. Katika pengo hili upo ukanda wa asteroidi wenye violwa laki kadhaa pamoja na sayari kibete ya Ceres.
|
20231101.sw_2205_6
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mfumo%20wa%20Jua
|
Mfumo wa Jua
|
Nje ya ukanda wa asteroidi hufuata kundi la sayari za gesi ambazo ni kubwa kushinda sayari za ndani. Sehemu kubwa ya masi yao si mwamba bali ni elementi na kampaundi zinazopatikana duniani kama gesi hasa hidrojeni(H), heliamu(He), Amonia(NH3) na methani(CH4). Gesi hizi zimeganda na kuwa imara kutokana na shinikizo kubwa na baridi kali.
|
20231101.sw_2205_7
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mfumo%20wa%20Jua
|
Mfumo wa Jua
|
Kuna magimba 8 yanayozunguka Jua letu yanayoitwa sayari. Sayari za kwanza kuanzia Utaridi(ing. Mercury) hadi Zohali (ing. Saturn) zinaonekana kwa macho. Tangu zamani zilipewa majina na watu. Sayari za mbali zaidi ziligunduliwa tu baada ya kupatikana kwa darubini.
|
20231101.sw_2205_8
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mfumo%20wa%20Jua
|
Mfumo wa Jua
|
(Namba zinazotaja sifa mbalimbali za sayari zinarejelea kipimo kulingana na tabia za Dunia yetu ambayo ni "1". Kuhusu majina ya sayari kadhaa kuna mkanganyiko katika kamusi na vitabu. Kama huna jina mbadala au umbo tofauti, limewekwa katika mabano kama (jina).)
|
20231101.sw_2205_9
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mfumo%20wa%20Jua
|
Mfumo wa Jua
|
{| class="toccolours" border=1 cellspacing=0 cellpadding=2 style="text-align:center; border-collapse:collapse;"
|
20231101.sw_2205_10
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mfumo%20wa%20Jua
|
Mfumo wa Jua
|
* Utaridi ni jina la sayari ya kwanza kutokana na lugha ya Kiarabu na pia katika mapokeo ya Kiswahili tangu kale. Vitabu vingine hutumia neno "Zebaki" ambalo pia lina asili ya Kiarabu likimaanisha metali mojawapo; inaonekana limepatikana kama tafsiri ya jina la Kiingereza la sayari ya kwanza "Mercury" bila kujua historia ya majina ya sayari sita ya kwanza yaliyoingia katika Kiswahili kutoka katika lugha ya Kiarabu. ** Zuhura - Ng'andu ni sayari ambayo hutambulika kwa jina la Kibantu(Ng'andu) pamoja na jina lenye asili ya Kiarabu (Zuhura)
|
20231101.sw_2205_11
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mfumo%20wa%20Jua
|
Mfumo wa Jua
|
*** Tazama makala ya Dunia kwa ajili ya namba halisi. Neno "ardhi" hutumika na waandishi kadhaa badala ya "dunia" wakitaka kutaja sayari ya tatu.
|
20231101.sw_2205_12
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mfumo%20wa%20Jua
|
Mfumo wa Jua
|
Hadi mwaka 2006 Pluto iliyopo nje ya mzingo wa Neptuni ilihesabiwa kuwa sayari, lakini baada ya azimio la Umoja wa Kimataifa wa Astronomia, Pluto inaitwa sasa "sayari kibete“, si sayari kamili tena. Kwa sasa kuna magimba 5 yanayotambuliwa kama sayari kibete:
|
20231101.sw_2205_13
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mfumo%20wa%20Jua
|
Mfumo wa Jua
|
Katika miaka iliyopita wanaastronomia wamejadili uwezekano wa kuwepo kwa sayari za ziada katika umbali mkubwa. Imetambuliwa ya kwamba muundo wa mfumo wa jua ni mkubwa kuliko wataalamu wa kale walivyofikiri.
|
20231101.sw_2205_14
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mfumo%20wa%20Jua
|
Mfumo wa Jua
|
Tangu kutambuliwa wa ukanda wa Kuiper ambamo Pluto ni sehemu tu inajulikana ya kwamba kuna magimba ya angani mengi yasiyoonekana kwa kirahisi kwa sababu yanapokea na kuakisi nuru kidogo sana kutoka kwenye Jua.
|
20231101.sw_2205_15
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mfumo%20wa%20Jua
|
Mfumo wa Jua
|
Kuhusu magimba ya angani yaliyo mbali zaidi kuliko ukanda wa Kuiper hakuna uhakika bado, lakini tangu mwaka 2012 vipimo vipya vilisababisha kutokea kwa nadharia tete kuhusu sayari ya tisa katika umbali mkubwa sana ambayo haikutazamiwa bado.
|
20231101.sw_2205_16
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mfumo%20wa%20Jua
|
Mfumo wa Jua
|
Mwaka 2017 kilitokea kiolwa cha anga kutoka nje ya mfumo wa Jua letu. Kiolwa hiki kilichoitwa ʻOumuamua kilifika kwa njia isiyolingana na bapa la sayari za mfumo wa Jua, tena kwa kasi kubwa mno hivyo kilionekana si sehemu ya mfumo wetu.
|
20231101.sw_2205_17
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mfumo%20wa%20Jua
|
Mfumo wa Jua
|
Mfumo wa Jua ulianza kutokea zamani sana na wataalamu wanaendelea kujadili nadharia zinazoeleza tabia zake kulingana na kanuni za fizikia.
|
20231101.sw_2205_18
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mfumo%20wa%20Jua
|
Mfumo wa Jua
|
Takriban miaka bilioni 4.5 iliyopita kulikuwa na wingu kubwa la molekuli lililozunguka kitovu cha galaksi yetu yaani Njia Nyeupe. Wingu hilo lilifanywa hasa na hidrojeni na heliamu (zaidi ya asilimia 99), pamoja na viwango vidogo vya elementi nzito zaidi. Hidrojeni na heli zilitokea katika mlipuko mkuu ulioanzisha ulimwengu wetu. Elementi nzito zilitokea katika nyota zilizowahi kutangulia na kulipuka kabla ya kuzaliwa kwa Jua letu na kusambaza mata zao kama vumbi ya angani. Ndani ya wingu kubwa kulikuwa na sehemu ambamo molekuli ziliongezeka na hivyo kuunda uga wa graviti iliyoendelea kuvuta mata nyingine, kuongeza tena graviti ya sehemu hizi kadiri zilivyopokea mata zaidi. Miendo ndani ya wingu labda ilianzishwa na mishtuko ya supanova ya karibu. Lakini hii ni nadharia tete tu hadi sasa.
|
20231101.sw_2205_19
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mfumo%20wa%20Jua
|
Mfumo wa Jua
|
Sasa sehemu moja ya wingu kubwa ambako molekuli zinaendelea kukusanyika inaanza kuzunguka kwenye mhimili wake na kuongeza mzunguko huo pamoja na ongezeko la graviti. Graviti hiyo inaendelea kuvuta molekuli za eneo kubwa zaidi hadi diski ya uongezekaji (ing. accretion disk) inatokea. Hapo masi kubwa inaelekea kukusanyika katika kitovu cha diski ambako shinikizo na jotoridi zinaanza kupanda. Kadiri atomi zinavyokazwa na graviti na jotoridi kuwa juu, mchakato wa myeyungano wa kinyuklia unaanza katika kitovu na hapo nyota changa inatokea.
|
20231101.sw_2205_20
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mfumo%20wa%20Jua
|
Mfumo wa Jua
|
Myeyungano wa kinyuklia unasababisha mnururisho unaoelekea nje. Mnururisho huu ni kani yenye mwelekeo kinyume cha graviti. Hapo nyota haikazwi zaidi. Hivyo nyota inaingia katika hali thabiti ya uwiano baina ya graviti inayotaka kukaza mata yake kwenye kitovu na shinikizo la mnururisho linaloelekea kinyume.
|
20231101.sw_2205_21
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mfumo%20wa%20Jua
|
Mfumo wa Jua
|
Ndani ya mata iliyobaki kwenye diski nje ya kiini cha nyota changa kuna sehemu ambapo molekuli zinakazana na kuunda vianzio sayari (ing. planetesimal)''. Viini vikubwa zaidi vinavuta tena viini vidogo na kufanya idadi ya viini kupungua ilhali viini vinaungana. Vinavyobaki hukua na kuongeza masi zake na ndipo chanzo cha sayari zetu.
|
20231101.sw_2205_22
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mfumo%20wa%20Jua
|
Mfumo wa Jua
|
Tabia za sayari zinatokea tofauti kutegemeana na umbali wa Jua. Elementi nzito zaidi zinakusanyika karibu na Jua. Kinyume chake, elementi nyepesi zinasukumwa na upepo wa Jua zinaanza kukusanyika kwa umbali mkubwa zaidi. Kwa hiyo sayari zilizo karibu na Jua kama Utaridi, Zuhura, Dunia na Mirihi ni sayari za miamba, zinafanywa na elementi nzito. Sayari zilizo mbali na Jua kama Mshtarii, Zohali, Uranusi na Neptuni ni sayari za gesi, zinafanywa na elementi nyepesi.
|
20231101.sw_2206_0
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Zuhura
|
Zuhura
|
Zuhura (alama: ; pia: Ng'andu; kwa Kiingereza Venus) ni sayari ya pili katika mfumo wa jua na sayari zake. Kati ya sayari zote za jua ndiyo inayofanana zaidi na dunia yetu.
|
20231101.sw_2206_1
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Zuhura
|
Zuhura
|
Sayari hii ina majina mawili kwa Kiswahili: Zuhura, kwa matamshi mengine pia "Zuhra", ni jina leye asili ya Kiarabu زُهَرَة zuhara lenye maana asilia ya "mwenye kung'aa".
|
20231101.sw_2206_2
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Zuhura
|
Zuhura
|
Kwenye anga la usiku inang'aa kushinda nyota zote isipokuwa mwezi. Kutokana na nguvu ya mwanga wake inaonekana mapema kati ya nyota za kwanza zinazoonekana jioni; vilevile huwa inaonekana kama nyota ya mwisho wakati wa pambazuko.
|
20231101.sw_2206_3
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Zuhura
|
Zuhura
|
Zuhura ina umbali wa kati ya kilomita milioni 107.5-108.9 kutoka jua. Umbali kutoka dunia yetu hutegemea na mahali pa dunia na Zuhura kwenye mizingo yao ya kuzunguka jua: uko kati ya kilomita milioni 38.3-260.9.
|
20231101.sw_2206_4
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Zuhura
|
Zuhura
|
Ukubwa wake na pia kemia yake zinafanana sana na dunia ikiwa kipenyo chake ni km 12,103.6 kwenye ikweta.
|
20231101.sw_2206_5
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Zuhura
|
Zuhura
|
Mwaka wa Zuhura (ambao ni muda wa kutimiza obiti moja wa kuzunguka dunia) una siku 224.7 za kidunia.
|
20231101.sw_2206_6
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Zuhura
|
Zuhura
|
Hali ya hewa ni ya joto sana, kwa wastani sentigredi 500. Hewa yake ni hasa ya kabonidaioksaidi inayosababisha mawingu mengi yanayozuia sura yake isionekane kwa darubini. Kutokana na halijoto kali hakuna maji.
|
20231101.sw_2206_7
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Zuhura
|
Zuhura
|
Warusi na Wamarekani walifaulu kupeleka vipimaanga mbalimbali hadi Zuhura, vingine vilipita na kupima hewa, vingine vilifika kwenye sura ya sayari na kutuma picha za mazingira hadi kuharibika kutokana na joto kali.
|
20231101.sw_2206_8
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Zuhura
|
Zuhura
|
Uso wa sayari umefanyiwa utafiti kwa msaada wa rada kutoka vipimaanga Magellan na Pioneer-Venus. Kutokana na matokeo yake ramani ya kwanza ilitokea. Sehemu kubwa ya sayari ni tambarare yenye vilima na mabonde yasiyo marefu. Kutokana na joto kubwa (mnamo 500°C) hakuna maji wala bahari.
|
20231101.sw_2206_9
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Zuhura
|
Zuhura
|
Kuna sehemu mbili ambako nyanda za juu zinapanda juu ya uwiano wa kawaida na hizi zilifananishwa na kontinenti za Dunia. Karibu na ikweta ya Zuhura iko sehemu inayoitwa "Aphrodite Terra" yenye ukubwa kama Amerika Kusini. Kwenye upande wa mashariki kuna safu za milima na mabonde makubwa pamoja na volkeno. Sehemu ya pili huitwa "Ishtar Terra" yenye ukubwa sawa na Australia kwenye Dunia. Hapa kuna milima ya Maxwell yenye urefu wa mita 10.800 juu ya uwiano wa wastani.
|
20231101.sw_2214_0
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ungo
|
Ungo
|
Ungo ni chombo cha kupepetea vitu hasa nafaka kilichotengenezwa kwa chane za miwale au mimea mingine ya jamii hiyo.
|
20231101.sw_2215_0
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mchuzi
|
Mchuzi
|
Mchuzi ni kitoweo cha majimaji kinachopikwa kwa kuchanganya nyama au samaki n.k. pamoja na viungo kama vile binzari, vitunguu, mafuta, chumvi na nyanya.
|
20231101.sw_2215_1
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mchuzi
|
Mchuzi
|
Kuna aina nyingi za mchuzi. Mchuzi wa bata na kuku ni mtamu sana; wachanganywa na viungo na mafuta: ladha yake ni ya pekee.
|
20231101.sw_2216_0
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kande
|
Kande
|
Kande ni chakula kinachopikwa kwa kuchanganya punje za mahindi na maharagwe au kunde, lakini pia maboga n.k.
|
20231101.sw_2219_0
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/NASA
|
NASA
|
NASA ni kifupi cha Kiingereza cha "National Aeronautics and Space Administration" (Mamlaka ya Marekani ya Usafiri wa Anga). Mamlaka hii ilianzishwa 1958. Wajibu wake ni kusimamia miradi ya serikali ya Marekani ya kuendesha utafiti na uchunguzi wa anga. NASA inasimamia utengenezaji wa roketi za kurusha vyombo vya angani na utengenezaji wa vyombo vya angani vyenyewe.
|
20231101.sw_2219_1
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/NASA
|
NASA
|
Miradi ya NASA ilianzishwa kutokana na Mshtuko wa Sputnik yaani baada ya Warusi kushtusha dunia kwa kupeleka vyombo vya angani vya kwanza katika mradi wao wa Sputnik. Uliofuatiwa na mradi wa "Vostok" ambao tarehe 12 Aprili 1961 ulimfikisha Yuri Gagarin angani akiwa mtu wa kwanza kwenda angani.
|
20231101.sw_2219_2
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/NASA
|
NASA
|
Mradi wa kwanza wa NASA ulikuwa Mradi wa Mercury uliotakiwa kuonyesha ya kwamba wanaanga wanaweza kukaa angani kwa muda fulani. Alan B. Shepard Jr. alikuwa Mmarekani wa kwanza angani kwa muda wa dakika 15; John Glenn alikuwa Mmarekani wa kwanza wa kuzunguka dunia tarehe 20 Februari 1962 kwa chombo cha angani "Friendship 7".
|
20231101.sw_2219_3
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/NASA
|
NASA
|
Mradi huo ulifuatiwa na Mradi wa Gemini kuanzia mwaka 1965 ulionyesha ya kwamba watu wanaweza kukaa angani kwa muda wa siku kadhaa hata kutekeleza shughuli fulani. Gemini iliandaa Mradi wa Apollo uliopeleka watu wa kwanza mwezini. Chombo cha angani "Apollo 11" kilifikisha wanaanga Neil Armstrong na Buzz Aldrin kwenye uso wa mwezi tarehe 20 Julai 1969 na kuwarudisha dunia tena.
|
20231101.sw_2221_0
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Korongo
|
Korongo
|
Korongo ni ndege wenye shingo ndefu na miguu mirefu na hunyoosha shingo na miguu wakiruka angani. Yangeyange na makoikoi hupinda shingo yao wakiruka angani.
|
20231101.sw_2222_0
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Waarabu
|
Waarabu
|
Waarabu (kwa Kiarabu عَرَبِ, matamshi ya Kiarabu: [ʕarabi]) ni watu ambao lugha mama yao ni Kiarabu wakijitambua vile.
|
20231101.sw_2222_1
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Waarabu
|
Waarabu
|
Kiasili walikuwa watu wa Bara Arabu na maeneo jirani katika Syria na Iraki, lakini tangu kuja kwa Uislamu walienea nje ya eneo asilia hasa katika Afrika ya Kaskazini na nchi za Mashariki ya Kati ambako walijichangaya na wenyeji ambao wengi wao wamepokea lugha ya Kiarabu tangu karne nyingi na kujitazama kama Waarabu pia.
|
20231101.sw_2222_2
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Waarabu
|
Waarabu
|
Kutokana na uhamiaji wako pia katika Afrika ya Mashariki, Visiwa vya Komoro na visiwa vingine vya Bahari Hindi, Amerika, Ulaya Magharibi, Indonesia, Uhindi na Iran.
|
20231101.sw_2222_3
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Waarabu
|
Waarabu
|
Dini ya Uislamu ilianzia kati ya Waarabu na hivyo Kiarabu ndiyo lugha ya Qurani na maandiko ya Kiislamu, na Waarabu wengi ni Waislamu. Walakini kati ya Waislamu wote Waarabu ni kama asilimia 20 tu.
|
20231101.sw_2222_4
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Waarabu
|
Waarabu
|
Kihistoria Waarabu walitajwa mara ya kwanza wakati wa karne ya 9 KK kama makabila ya mashariki na kusini mwa Syria na kaskazini mwa Bara Arabu. Waarabu wanaonekana walikuwa chini ya wafalme wa Milki ya Ashuru (911-612 KK), na baadaye chini ya Milki ya Babeli iliyofuata (626-539 KK), Waakhemi (539-332 KK), Waseleukidi na Waparthi.
|
20231101.sw_2222_5
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Waarabu
|
Waarabu
|
Katika karne ya 3 KK Waarabu wa Nabatea waliunda ufalme wao karibu na Petra katika Yordani ya leo. Makabila ya Kiarabu kama Waghassanidi na Walakhmidi huanza kuonekana katika jangwa la Syria Kusini kuanzia katikati ya karne ya 3 BK wakiunda milki zao zilizoshirikiana na Dola la Roma na Wasasani. Hadi karne ya 7 sehemu ya Waarabu hasa wa magharibi mwa eneo lao walikuwa Wakristo, wengine pia Wayahudi.
|
20231101.sw_2222_6
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Waarabu
|
Waarabu
|
Baada ya Muhamad, makhalifa wa kwanza (632-661 BK) waliunganisha Waarabu wote chini ya utawala wao wakaendelea kuvamia milki jirani za Dola la Roma na Uajemi ya Wasasani. ote walianza kutumia lugha ya Kiarabu kama lugha ya utawala. Makabila mengi kutoka Bara Arabu yalianza kuhamia nchi zilizovamiwa katika hiyo milki kubwa ya Kiislamu iliyoenea kutoka Moroko na Hispania upande wa magharibi hadi mipaka ya China na Uhindi upande wa mashariki. Katika karne zilofuata, wakazi wengi wa maeneo hayo walianza kuwa Waislamu na kutumia Kiarabu kama lugha ya kidini na ya kielimu; hasa katika sehemu kubwa ya Afrika Kaskazini pamoja na Misri na katika nchi za Asia Magharibi (hasa nchi za leo Syria, Lebanoni, Iraki) wenyeji wengi walianza kutumia Kiarabu kama lugha yao na hivyo kuitwa Waarabu.
|
20231101.sw_2222_7
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Waarabu
|
Waarabu
|
Kwa karne nyingi Waarabu hao walitawaliwa na Milki ya Osmani. Baada ya Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia (1914-1918) milki hiyo ilivunjwa na kugawiwa kwa maeneo ya nchi za Kiarabu za leo ambazo kwa muda mfupi zilitawaliwa bado kama makoloni au nchi lindwa chini ya Uingereza na Ufaransa.
|
20231101.sw_2222_8
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Waarabu
|
Waarabu
|
Leo hii Waarabu kimsingi hukalia nchi 22 wanachama wa Jumuiya ya Nchi za Kiarabu. Nchi hizo zinaenea kwa kilomita za mraba milioni 13 kutoka bahari ya Atlantiki upande wa magharibi hadi Bahari ya Kiarabu katika mashariki na kutoka Bahari ya Mediterranean katika kaskazini hadi Pembe ya Afrika na Bahari ya Hindi katika kusini. Watu wasio Waarabu wakitumia lugha zao za pekee huishi pia katika nchi hizo, wakati mwingine wakiwa wengi. Hawa ni pamoja na Wasomali, Wakurdi, Waberberi, Waafar, Wanubi na wengineo .
|
20231101.sw_2222_9
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Waarabu
|
Waarabu
|
Wakati wa kuzaliwa kwa Mtume Muhamad lugha ya Kiarabu ilitumika Uarabuni tu, nchi ya jangwa na oasisi. Kutoka hapa makabila ya Waarabu Waislamu walivamia nchi jirani ambako wenyeji walitumia lugha mbalimbali. Lugha kadhaa zimeendelea kwa viwango vidogo, vingine vimebaki na nguvu zaidi. Lugha ya Kiaramu iliyowahi kutamalaki katika siasa na uchumi kuanzia Syria hadi Uajemi na zaidi, imebaki kati watu wa vijiji katika maeneo ya kaskazini ya Syria na Iraki, pia kama lugha ya liturgia kanisani. Kikopti iliyokuwa lugha ya Misri imebaki pekee katika liturgia ya kanisa ilhali Wakristo Wakopti wanaongea Kiarabu tu. Kiberber bado inazungumzwa na milioni kadhaa katika Moroko na Algeria. Kikurdi ina nguvu katika milima ya Syria na Iraki kaskazini. Kiajemi (lugha ya Iran) kimefaulu kurudi kama lugha ya kitaifa lakini imepokea karibu asilimia 40 za msamiati wake kutoka Kiarabu; atahri kubwa ya lugha ya Kiarabu inaonekana pia katika lugha nyingine nyingi hadi Kiswahili.
|
20231101.sw_2222_10
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Waarabu
|
Waarabu
|
Katika nchi zinazoitwa Kiarabu, lugha ya Kiarabu imekuwa lugha ya kila siku ya kuongea na pia ya serikali, biashara na utamaduni hata kwa hao ambao bado wmetunza lugha nyingine kama lugha yao ya kwanza.
|
20231101.sw_2222_11
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Waarabu
|
Waarabu
|
Katika zama za kabla ya Uislamu, Waarabu wengi walifuata dini za kuabudu miungu mingi. Makabila kadhaa yalikuwa yamekubali Ukristo au Uyahudi na watu wachache waliotwa hanif walisemekana kuwa na imani kwa Mungu mmoja.
|
20231101.sw_2222_12
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Waarabu
|
Waarabu
|
Leo, karibu asilimia 93 za Waarabu ni wafuasi wa Uislamu . Kuna pia Wakristo kama jumuiya ndogo zaidi. Waislamu Waarabu kimsingi ni wa madhehebu ya Wasunni, Washiia, Waibadi na Waalawi.
|
20231101.sw_2222_13
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Waarabu
|
Waarabu
|
Wakristo wa Kiarabu kwa ujumla hufuata moja ya Makanisa ya Kikristo ya Mashariki, kama yale yaliyo ndani ya makanisa ya Orthodox ya Mashariki, makanisa Katoliki ya Mashariki, au makanisa ya Kiprotestanti ya Mashariki. Kuna pia idadi ndogo ya Wayahudi wa Kiarabu ambao bado wanaishi katika nchi za Kiarabu lakini wengi wao waliondoka kwao wakihamia Israeli au nchi nyingine za Ulaya na Amerika. Sehemu ya Wakristo katika nchi za Kiarabu hawajitambui kuwa Waarabu kwa mfano Wakopti au Waashuri.
|
20231101.sw_2223_0
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Korongo%20%28Ciconiidae%29
|
Korongo (Ciconiidae)
|
Korongo hawa ni ndege wa familia ya Ciconiidae wenye domo refu na nene (korongo wa familia ya Gruidae wana domo fupi na jembamba zaidi). Wanaitwa kongoti pia, hususa korongo mfuko-shingo. Mabawa yao ni marefu sana, yale ya korongo mfuko-shingo yana m 3.2: marefu kuliko yale ya ndege wote ghairi ya tumbusi wa Andes (Andean condor).
|
20231101.sw_2223_1
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Korongo%20%28Ciconiidae%29
|
Korongo (Ciconiidae)
|
Spishi nyingine huishi mahali pa majimaji nyingine mahali pakavu. Hula vyura, samaki, wadudu na nyungunyungu, hata ndege na wanyama wadogo. Korongo hawa hawawezi kutoa sauti. Lakini kwa tago hupiga kelele na domo yao.
|
20231101.sw_2225_0
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mkoa%20wa%20Ruvuma
|
Mkoa wa Ruvuma
|
Umepewa jina kutokana na mto Ruvuma ambao ni mpaka wake wa kusini na Msumbiji. Umepakana na Ziwa Nyasa na Mkoa wa Morogoro upande wa magharibi, mikoa ya Iringa na Lindi upande wa kaskazini na Mkoa wa Mtwara upande wa mashariki.
|
20231101.sw_2225_1
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mkoa%20wa%20Ruvuma
|
Mkoa wa Ruvuma
|
Makabila makubwa katika Ruvuma ni Wangoni, Wamatengo, Wayao, Wandendeule, Wamanda, Wanyasa, Wapoto, Wabena na Wandengereko.
|
20231101.sw_2225_2
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mkoa%20wa%20Ruvuma
|
Mkoa wa Ruvuma
|
Elimu bado inahitajika, hasa kwa maeneo ya vijijini, maana watu wengi katika mkoa huu hawajaelimika hivyo huleta changamoto katika maendeleo maana taifa huhitaji watu ambao ni wasomi.
|
20231101.sw_2225_3
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mkoa%20wa%20Ruvuma
|
Mkoa wa Ruvuma
|
Sehemu ya mashariki ya mkoa kuna barabara ya lami kutoka Dar es Salaam kupitia Makambako na Njombe hadi Songea. Barabara kuu kwenda [[Lindi] ni kiwango cha lami kuanzia Songea mjini kupitia Wilaya za Namtumbo, Tunduru, Nanyumbu, Masasi, Mnazimmoja-Lindi, hadi Dar es Salaam.
|
20231101.sw_2228_0
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/The%20Jackson%205
|
The Jackson 5
|
The Jackson 5 lilikuwa kundi la muziki wa roki la nchini Marekani lililoundwa na wanamuziki watano; mmojawapo ni Michael Jackson. Nyimbo zilizoimbwa na kundi hili ni kama "The Love You Save", "I Will Be There", "Mamas Pearl" na "Never Can Say Goodbye".
|
20231101.sw_2229_0
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Siku%20ya%20wapendanao
|
Siku ya wapendanao
|
Siku ya wapendanao (kwa Kiingereza: Valentine's Day) ni sikukuu ambayo huadhimishwa kila ifikapo tarehe 14 Februari ya kila mwaka.
|
20231101.sw_2229_1
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Siku%20ya%20wapendanao
|
Siku ya wapendanao
|
Historia yake imeanzia karne ya 3 huko Roma au Terni ambapo alikuwapo padri au askofu Valentinus ambaye akaja kuheshimiwa kama mtakatifu hasa tarehe hiyo.
|
20231101.sw_2229_2
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Siku%20ya%20wapendanao
|
Siku ya wapendanao
|
Inasemekana kwamba Kaisari wakati huo alikuwa Claudius II: yeye aliona kuwa askari mkakamavu na bora zaidi ni yule asiyeoa wala kuwa na familia (kapera). Hivyo alipiga marufuku ndoa kwa askari.
|
20231101.sw_2229_3
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Siku%20ya%20wapendanao
|
Siku ya wapendanao
|
Valentinus alipinga jambo hili na hivyo kuendelea kufungisha ndoa kwa siri. Mfalme Claudius alipopata habari hizi aliamuru Valentinus akamatwe na kuuawa.
|
20231101.sw_2229_4
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Siku%20ya%20wapendanao
|
Siku ya wapendanao
|
Kuna hadithi nyingine ya kuwa akiwa gerezani Valentinus aliandika barua ambayo ilikuwa na salamu za kwanza za Valentine kwa binti aliyekuja kumsalimia gerezani; mwisho wa barua alihitimisha kwa maneno haya: Kutoka kwa Valentinus wako.
|
20231101.sw_2229_5
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Siku%20ya%20wapendanao
|
Siku ya wapendanao
|
Mbali ya hadithi, askofu huyo alijulikana kwa miujiza yake. Huko Terni, mnamo 2011, ilipatikana mifupa ya Sabino e Serapia: mmoja alikuwa Mpagani akida wa jeshi la Roma, mwingine msichana Mkristo motomoto. Kwa ajili yake Sabino aliongokea Ukristo, lakini baada ya muda mfupi aligundua kwamba Serapia ni mgonjwa wa kifua kikuu. Ili asitengane naye, Sabino alimuomba Valentinus, naye alibariki ndoa yao na kuomba mapendo yao yadumu milele. Baadaye walifariki pamoja wamekumbatiana na ndivyo mifupa yao inavyopatikana hadi leo.
|
20231101.sw_2229_6
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Siku%20ya%20wapendanao
|
Siku ya wapendanao
|
Toka hapo Valentine anakumbukwa kama mtetezi wa wapendanao na sikukuu yake kuadhimishwa kote duniani.
|
20231101.sw_2229_7
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Siku%20ya%20wapendanao
|
Siku ya wapendanao
|
Kuna matukio kadha wa kadha kutokana na historia ya siku hiyo ikiwemo kufungwa jela kwa askofu Mt. Valentinus wa Roma kutokana na kuwatesa baadhi ya Wakristo katika Dola la Roma mnamo karne ya 3.
|
Subsets and Splits
No community queries yet
The top public SQL queries from the community will appear here once available.