_id
stringlengths
15
22
url
stringlengths
31
150
title
stringlengths
1
86
text
stringlengths
100
23.8k
20231101.sw_2404_56
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ethiopia
Ethiopia
Uislamu nchini Ethiopia unapatikana kutoka mwanzo wa dini hiyo; ambapo nabii Muhammad aliwaambia Waislamu waepuke kuuliwa Maka kwa kukimbilia Uhabeshi, ambayo ilitawaliwa na Mfalme Mkristu.
20231101.sw_2404_57
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ethiopia
Ethiopia
Wayahudi, ambao wanaitwa Beta Israeli a Wafalasha, walioishi Ethiopia tangu karne nyingi, wengi wao wamehamia Israeli hasa katika karne ya 20.
20231101.sw_2404_58
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ethiopia
Ethiopia
Mnamo Aprili 2005, Mnara wa Aksum, mojawapo ya dafina za kidini Ethiopia, ulirudishwa na Waitalia ambao waliunyakua mwaka 1937 na kuupeleka Roma. Italia ikakubali kuurudisha mnamo 1947 kulingana na mkataba wa Umoja wa Mataifa.
20231101.sw_2404_59
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ethiopia
Ethiopia
Ethiopia ndiyo Nyumba ya kiroho ya Mwendo wa Rastafari, ambao wanaamini Ethiopia ni Zion. Warastafari wamuona mfalme Haile Selassie I kama Yesu.
20231101.sw_2404_60
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ethiopia
Ethiopia
Baada ya mapinduzi ya mwaka 1974, uchumi wa Ethiopia ulikuwa uchumi wa kijamaa: amri ya uchumi iliwekwa na jimbo, na upande mkubwa wa uchumi uliwekwa kwa jamii, kutoka viwanda vyote vya kisasa, kilimo cha biashara, taasisi za kukopesha na mashamba yote na mali yote ya kukomboa.
20231101.sw_2404_61
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ethiopia
Ethiopia
Kutoka kati ya 1991, uchumi ulianza kutolewa katika ujamaa na kuendekeza uchumi wa soko huria, serikali inasisitiza uchumi wa rasilimali ili kuzuia uvivu wa uchumi uliojitokeza wakati wa amri ya ujamaa. Mwaka 1993, Ubinafsishaji wa kampuni kaanza, viwanda, mabenki, ukulima, biashara za ndani na biashara za kimataifa.
20231101.sw_2404_62
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ethiopia
Ethiopia
Kilimo ni karibu asilimia 41% ya mapato ya uchumi (GDP), ambayo ni asilimia 80 ya biashara ya kimataifa, na asilimia 80 ya wananchi wanategemea kilimo.
20231101.sw_2404_63
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ethiopia
Ethiopia
Mambo mengi ya biashara hutegemea ukulima, wauzaji, viwanda vya kufunganya na kuuza nje mavuno ya ukulima. Mavuno yanayouzwa nje mengi yanatolewa na wakulima wa kiasi binafsi. Wanazalisha kahawa, nafaka (hasa maharagwe), mbegu za mafuta, viazi, miwa, na mboga.
20231101.sw_2404_64
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ethiopia
Ethiopia
Mifugo ya Ethiopia inaaminika kuwa ndiyo wengi zaidi Afrika. Mnamo 1987 ilihesabika kuwa asilimia 15 ya mapato ya uchumi yanatokana na mifugo.
20231101.sw_2404_65
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ethiopia
Ethiopia
Ethiopia ni nchi mojawapo inayotoa wanariadha wazuri zaidi duniani, hasa kama wa mbio wa masafa ya kati na masafa marefu. Kenya na Morocco ni wapinzani wa Ethiopia kwa Michezo ya mabingwa wa Dunia na Olimpiki kwa masafa ya kati na marefu.
20231101.sw_2404_66
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ethiopia
Ethiopia
Machi 2006, Waethiopia wawili walitamalaki mbio za masafa marefu, kwa jina wakiwa: Haile Gebreselassie (Bingwa wa Dunia na Olimpiki) aliyevunja rekodi ya kilometa 10 na sasa pia kilomita 20, NusuMarathoni, na rekodi ya kilomita 25, na kijana Kenenisa Bekele (bingwa wa dunia, mbio za majira (bara), na pia bingwa wa olimpiki), anayeshikilia Rekodi za Dunia za mita 5,000 na 10,000.
20231101.sw_2404_67
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ethiopia
Ethiopia
Deguefé, Taffara (2006). Minutes of an Ethiopian Century, Shama Books, Addis Ababa, ISBN 99944-0-003-7.
20231101.sw_2404_68
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ethiopia
Ethiopia
Hugues Fontaine, Un Train en Afrique. African Train, Centre Français des Études Éthiopiennes / Shama Books. Édition bilingue français / anglais. Traduction : Yves-Marie Stranger. Postface : Jean-Christophe Belliard. Avec des photographies de Matthieu Germain Lambert et Pierre Javelot. Addis Abeba, 2012, ISBN 978-99944-867-1-7. English and French.
20231101.sw_2404_69
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ethiopia
Ethiopia
Mauri, Arnaldo (2010). Monetary developments and decolonization in Ethiopia, Acta Universitatis Danubius Œconomica, VI, n. 1/2010, pp. 5–16. and WP
20231101.sw_2404_70
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ethiopia
Ethiopia
Murphy, Dervla (1968). In Ethiopia with a Mule. London: Century, 1984, cop. 1968. N.B.: An account of the author's travels in Ethiopia. 280 p., ill. with a b&w map. ISBN 0-7126-3044-9
20231101.sw_2404_71
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ethiopia
Ethiopia
Siegbert Uhlig, et al. (eds.) (2003). Encyclopaedia aethiopica, Vol. 1: A-C. Wiesbaden: Harrassowitz Verlag.
20231101.sw_2404_72
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ethiopia
Ethiopia
Siegbert Uhlig, et al. (eds.) (2005). Encyclopaedia aethiopica, Vol. 2: D-Ha. Wiesbaden: Harrassowitz Verlag.
20231101.sw_2404_73
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ethiopia
Ethiopia
Siegbert Uhlig, et al. (eds.) (2007). Encyclopaedia aethiopica, Vol. 3: He-N. Wiesbaden: Harrassowitz Verlag.
20231101.sw_2404_74
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ethiopia
Ethiopia
Siegbert Uhlig & Alessandro Bausi, et al. (eds.) (2010). Encyclopaedia aethiopica, Vol. 4: O-X. Wiesbaden: Harrassowitz Verlag.
20231101.sw_2404_75
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ethiopia
Ethiopia
Alessandro Bausi & S. Uhlig, et al. (eds.) (2014). Encyclopaedia aethiopica'', Vol. 5: Y-Z and addenda, corrigenda, overview tables, maps and general index. Wiesbaden: Harrassowitz Verlag.
20231101.sw_2404_76
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ethiopia
Ethiopia
meetethiopia.com Portal that introduces and celebrates the rich history, culture and diversity of Ethiopia through the use of a repository that contains Ethiopia-related websites ranging from Arts, Society and Religion to Entertainment, Shopping and Technology
20231101.sw_2406_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/Yoweri%20Kaguta%20Museveni
Yoweri Kaguta Museveni
Yoweri Kaguta Museveni (* 1944 Ntungamo, Wilaya ya Ntungamo, Uganda) ni Rais wa Uganda tangu 29 Januari 1986. Alichukua madaraka baada ya kushinda vita vya msituni chini ya kundi la National Resistance Movement na kushinda katika chaguzi za urais za mwaka 1996, 2001 na 2006.
20231101.sw_2406_1
https://sw.wikipedia.org/wiki/Yoweri%20Kaguta%20Museveni
Yoweri Kaguta Museveni
Kwa muda mrefu, kabla ya kuwa rais wa Uganda, Museveni aliongoza vita vya msituni dhidi ya serikali za Idd Amin aliyetawala toka mwaka 1971-79, na serikali ya Milton Obote aliyekuwa madarakani mwaka 1980-85.
20231101.sw_2406_2
https://sw.wikipedia.org/wiki/Yoweri%20Kaguta%20Museveni
Yoweri Kaguta Museveni
Kutokana na mafanikio ya mapambano dhidi ya ugonjwa wa Ukimwi na kukubali kwake kufuata sera za Benki ya Dunia na Shirika la Fedha Duniani, Museveni alipata sifa kubwa toka kwa viongozi wa mataifa ya Magharibi. Mwishoni mwa miaka ya 1990, Museveni alikuwa akielezewa kuwa ni mfano bora wa kizazi kipya cha viongozi wa Afrika.
20231101.sw_2406_3
https://sw.wikipedia.org/wiki/Yoweri%20Kaguta%20Museveni
Yoweri Kaguta Museveni
Hata hivyo uongozi wake umetiwa dosari na mambo kadhaa ikiwa ni pamoja na ushiriki wake katika vita vya wenyewe kwa wenyewe katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Rwanda. Mambo mengine ni pamoja na ukiukwaji wa haki za kisiasa unaofanywa na serikali yake dhidi ya wapinzani kama vile Kizza Besigye na kitendo cha kubadili katiba ya nchi hiyo ili aweze kugombea urais mwaka 2006.
20231101.sw_2439_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/Jeshi
Jeshi
Jeshi ni jumla ya watu wanaopewa mamlaka ya kutumia nguvu ya silaha kutetea nchi kwa niaba ya dola au kutekeleza maagizo ya serikali dhidi ya maadui wa nje.
20231101.sw_2439_1
https://sw.wikipedia.org/wiki/Jeshi
Jeshi
Kusudi hilo dhidi ya hatari ya nje ndiyo tofauti kuu na kazi ya polisi ambayo ni mkono mwingine wa serikali ya taifa wenye silaha. Hata hivyo kuna nchi ambako tofauti kati ya jeshi na polisi si wazi vile, hasa kuna nchi nyingi ambako jeshi limepewa wajibu wa ndani ya taifa au ambako wanajeshi walichukua mamlaka mikononi mwao kwa nguvu ya silaha.
20231101.sw_2439_2
https://sw.wikipedia.org/wiki/Jeshi
Jeshi
Katika nchi mbalimbali kuna vikosi vinavyotekeleza shughuli ndani ya taifa lakini vina silaha sawa na sehemu za jeshi na wakati mwingine vinahesabiwa kama sehemu ya jeshi. Kwa mfano vikosi vinavyolingana na FFU ya Tanzania vinaitwa gendarmerie huko Ufaransa na nchi nyingi za Afrika Magharibi au carabinieri huko Italia na kule vinahesabiwa kama mkono wa jeshi ingawa kazi yao ni ya ndani ya nchi.
20231101.sw_2439_3
https://sw.wikipedia.org/wiki/Jeshi
Jeshi
Hali ya jeshi vitani husimamiwa na sheria ya kimataifa ya vita jinsi ilivyoundwa katika mikataba mbalimbali ya kimataifa. Sheria hiyo inalenga kulinda raia wakati wa vita na pia haki za wanajeshi wakikamatwa na adui. Sheria inadai ya kwamba wanajeshi wote wanahitaji
20231101.sw_2439_4
https://sw.wikipedia.org/wiki/Jeshi
Jeshi
Wanajeshi wanafuata utaratibu huo wanalindwa na sheria inayokataza pia raia kubeba na kutumia silaha na kushiriki katika mapigano. Katika vita nyingi sheria ilipuuzwa lakini kuna mifano kadhaa katika karne ya 20 ambapo jinai za vitani zilifuatiliwa kwa mfano kwenye Kesi za Nuremberg kuhusu jinai za vitani upande wa Ujerumani na kesi zilizofikishwa mbele ya Mahakama ya Kimataifa ya Jinai tangu mwaka 2000.
20231101.sw_2439_5
https://sw.wikipedia.org/wiki/Jeshi
Jeshi
Jeshi la ardhi lina kituo ama kambi ambayo kambi hii yaweza kulinda makundi ya Jeshi, divisheni ama umma wa jeshi. Kukitokea vita, Jeshi huwa wakipeleka divisheni na makundi ya kijeshi kwa vipimo kulingana na vita na mbinu za kusukuma ama kushinda adui kwa vita. Na pia ratili ya vita ikiwapendukia, Jeshi hupeleka wanajeshi pulikiza ili kusukuma adui kabisa ama kumshinda.
20231101.sw_2439_6
https://sw.wikipedia.org/wiki/Jeshi
Jeshi
Jeshi la Taifa ni chombo kilichoanzishwa kisheria chenye silaha na askari wenye mafunzo ya kivita amabao kazi yao ni kupambana kivita kulinda ardhi ya nchi husika dhidi ya uvamizi kutoka nje. Nchi huwa na jeshi moja la kulinda mipaka yake dhidi ya uchokozi kutoka nje, lakini pia huwa na majeshi 'Usu' kadhaaa kwaajili ya kulinda usalaama wa ndani. kwa mfano; majeshi ya nchi ni kama Jeshi la Uganda (UPDF), Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (TPDF). Majeshi Usu ni kama Polisi, Magereza, Uhamiaji, Zimamoto na TANAPA.
20231101.sw_2439_7
https://sw.wikipedia.org/wiki/Jeshi
Jeshi
Shughuli nyingi za majeshi hutofautiana kulingana na kitengo husika cha jeshi, kwa mfano jeshi la nchi kavu,Jeshi la Anga na Jeshi la Majini, haya ndiyo matawi makuu matatu ya jeshi . Kwa historia, Jeshi la anga lilikuwa pamoja na Jeshi la ardhini, hasa kwa historia ya Uchina ama Jeshi la ukombozi wa umma wa Uchina ilichanganya (jeshi la ardhi, jeshi la majini, jeshi la anga, divisheni za makombora na usayari) kwa tawi moja.
20231101.sw_2439_8
https://sw.wikipedia.org/wiki/Jeshi
Jeshi
Majeshi ya kisasa yaitwa pia huduma, ama askari watawala). Hii inaweza kuhusu pia matawi ya Vita: jeshi la nchi kavu, vifaru, makombora, na mhandisi wa jeshi, na pia Wasafirishaji wa matawi kama: mawasiliano, watambuzi, daktari, wapeleka vifaa, na Jeshi la ndege (tofauti na jeshi la anga).
20231101.sw_2439_9
https://sw.wikipedia.org/wiki/Jeshi
Jeshi
Jeshi laweza kuwa kubwa kama chama, chama cha Jeshi (Shurutisho) ambalo lina makundi mengi zaidi ya askari. Jeshi tofauti hujigawa kulingana na utamaduni wao — hasa Marekani (Jeshi la kwanza la Marekani). Kwa Jeshi la Uingereza Jeshi kwa shurutisho ni "Jeshi la kwanza", na Marekani ni "divisheni ya kwanza".
20231101.sw_2439_10
https://sw.wikipedia.org/wiki/Jeshi
Jeshi
Jeshi la Urusi wakati wa Muungano wa Sovieti lilikuwa limegawanywa kwa kundi za askari ambazo zilikuwa chini ya Jeshi shurutisho vitani. Lakini wakati wa amani kundi hizi zilikuwa chini ya tarafa ya Jeshi.
20231101.sw_2440_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/Elimuanga
Elimuanga
Elimuanga (pia: astronomia, kutoka maneno ya Kigiriki ἄστρον astron "nyota" na νόμος nomos "sheria") ni elimu juu ya magimba ya ulimwengu kama vile nyota, sayari, miezi, vimondo, nyotamkia, galaksi kuhusu nyendo zao, nafasi, umbali, ukubwa na sheria zinazotawala tabia zake.
20231101.sw_2440_1
https://sw.wikipedia.org/wiki/Elimuanga
Elimuanga
Elimuanga ni tofauti na unajimu ambayo si sayansi bali jaribio la kuona uhusiano kati ya nyota na tabia za wanadamu na pia kutabiri mambo yajayo. Hata hivyo vyanzo vya fani zote mbili zilikuwa karibu sana katika historia ya binadamu hadi kutokea kwa elimuanga ya kisayansi.
20231101.sw_2440_2
https://sw.wikipedia.org/wiki/Elimuanga
Elimuanga
Tangu zamani watu waliangalia nyota wakajifunza kuzitofautisha. Mabaharia na wasafiri wakati wa usiku waliweza kutumia nyota kama vielekezi safarini. Walitazama pia mabadiliko ya kurudia kati ya nyota zinazoonekana angani wakati wa usiku. Wakaona mabadiliko haya ya jinsi nyota zinavyoonekana yaweza kuwa uhusiano na nyakati za mvua, baridi na joto, mavuno na ustawi wa mimea katika mwendo wa mwaka. Kutazama nyota vile kulikuwa msaada wa kupanga vipindi vya mwaka na kuunda kalenda.
20231101.sw_2440_3
https://sw.wikipedia.org/wiki/Elimuanga
Elimuanga
Watazamaji wa nyota walianza kutambua pia tofauti kati ya nyota mbalimbali, kwa mfano nyota zenye mahali palepale kila wakati na nyota chache za pekee zilizobadilisha mahali angani kwa utaratibu wa kurudia na hizi ziliitwa sayari, tena nyota nyingine zilizoonekana kwa muda tu zikibadilisha mahali pake angani zikaitwa vimondo.
20231101.sw_2440_4
https://sw.wikipedia.org/wiki/Elimuanga
Elimuanga
Kwa karne nyingi wataalamu katika sehemu mbalimbali za dunia walihisi ya kwamba nyota hizo zilikuwa miungu iliyoonekana kwa mbali sana. Katika vitabu vya dini vya kale kuna majadiliano juu ya tabia zao; wakati mitholojia ya mataifa mengi iliona nyota kuwa miungu, Biblia ilifundisha ni taa zilizowekwa angani na Mungu pekee aliye mwumbaji wa ulimwengu.
20231101.sw_2440_5
https://sw.wikipedia.org/wiki/Elimuanga
Elimuanga
Wataalamu wa kale katika nchi kama Uhindi au Ugiriki ya Kale walianza kutambua mwendo wa sayari na kuunda nadharia yuu ya uhusiano wa dunia, jua na sayari nyingine. Ndiyo chanzo cha imani ya kwamba nyota zinaweza kuwa na tabia fulani na athari juu ya maisha duniani na hasa kama mtu alizaliwa wakati nyota fulani ilionekana, basi tabia zilizoaminiwa kuwa za nyota ziliweza pia kuathiri maisha ya mtu huyo. Hapa kuna asili ya "kupiga falaki" na unajimu wa kisasa. Wakati uleule wataalamu hao walitazama nyota jinsi zilivyo, kuziorodhesha na kupiga hesabu za kalenda. Orodha ya kale iliyoendelea kutumiwa kwa zaidi ya miaka 1,000 ilikuwa ya Klaudio Ptolemaio kutoka Misri.
20231101.sw_2440_6
https://sw.wikipedia.org/wiki/Elimuanga
Elimuanga
Kwa macho matupu mtu mwenye afya ya macho anaweza kuona takriban nyota 6000 - 7000. Leo hii kuna zaidi za nyota 945,592,683 zilizoorodheshwa katika orodha za kimataifa.
20231101.sw_2440_7
https://sw.wikipedia.org/wiki/Elimuanga
Elimuanga
Katika karne ya 17 darubini za kwanza zilibuniwa Ulaya. Hivyo utazamaji wa nyota uliboreshwa na magimba ya angani mengi yalianza kuonekana. Galileo Galilei aliweza kuona miezi ya Mshtarii mwaka 1609 iliyokuwa haijajulikana hadi siku ile.
20231101.sw_2440_8
https://sw.wikipedia.org/wiki/Elimuanga
Elimuanga
Katika karne ya 19 kifaa cha kamera kilileta tena upanuzi wa elimu; upigaji picha uliwezesha uchunguzi wa picha za nyota wakati wowote. Kamera iliwezesha pia kuona nyota zisizoonekana kwa macho tu. Kuingiza mwanga kwenye kamera kwa masaa kunakusanya nuru hafifu na hivyo kuonyesha lakhi za nyota zisizoonekana kwa macho.
20231101.sw_2440_9
https://sw.wikipedia.org/wiki/Elimuanga
Elimuanga
Sehemu kubwa ya kazi ya wataalamu wa anga ilihama kutoka kwenye darubini kwenda deski ya mtafiti, siku hizi mbele ya kompyuta yenye data.
20231101.sw_2440_10
https://sw.wikipedia.org/wiki/Elimuanga
Elimuanga
Maendeleo ya tekinolojia yalileta mitambo mipya inayowezesha kupima mawimbi yasiyoonekana kwa macho kama vile
20231101.sw_2440_11
https://sw.wikipedia.org/wiki/Elimuanga
Elimuanga
Vipimo hivi vilipanusha tena elimu tuliyo nayo kuhusu muundo wa ulimwengu. Mnururisho wa mandharinyuma (ing. cosmic background radiation) ulitambuliwa uliothibitisha nadharia kuhusu umri wa ulimwengu tangu mlipuko mkuu.
20231101.sw_2440_12
https://sw.wikipedia.org/wiki/Elimuanga
Elimuanga
Tangu mwanzo wa usafiri wa anga-nje wataalamu wa anga walipata nafasi ya kuangalia na kupima nyota nje ya athira ya angahewa ya Dunia (inayopunguza kiasi cha nuru inayoonekana) na nje ya ugasumaku wake.
20231101.sw_2440_13
https://sw.wikipedia.org/wiki/Elimuanga
Elimuanga
Tangu miaka ya 1970 satelaiti mbalimbali zilirishwa zinazobeba darubini za anga-nje. Utafiti wa nyota umepanuka hadi kupima miale ya eksirei na ya gamma inayozuiliwa na ugasumaku na angahewa. Maendeleo yamekuwa makubwa isipokuwa gharama zimekuwa pia kubwa za kuunda vifaa, kuvipeleka kwenye anga-nje halafu kuvitunza , hadi gharama za kupeleka watu huko juu kwa matengenezo. Kati ya darubini za anga-nje zilizokuwa mdhhuri sana ni Darubini ya Hubble.
20231101.sw_2440_14
https://sw.wikipedia.org/wiki/Elimuanga
Elimuanga
Pamoja na uwezo wa kompyuta wa kushughulikia idadi kubwa za data darubini za anga-nje zmeleta vipimo na data za nyota mamilioni.
20231101.sw_2442_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/Sayari
Sayari
Sayari (kwa Kiingereza planet) ni kiolwa kikubwa cha angani kinachozunguka jua (au nyota nyingine) na kung'aa kutokana na nuru ya jua iliyoakisiwa, tofauti na nyota na jua zinazong'aa peke yake. Kwa macho inaonekana kama nyota, lakini baada ya kuitazama kwa muda wa mwaka inaonekana inabadilisha mahali pake angani, tofauti na nyota kwa jumla. Tofauti kubwa kati ya sayari na nyota ni kwamba, nyota ukiitazama inametameta ila sayari haiwezi.
20231101.sw_2442_1
https://sw.wikipedia.org/wiki/Sayari
Sayari
Jina la Kiswahili "sayari" lina asili yake katika neno la Kiarabu كوكب سيار kaukab sayar "nyota inayosogea" . Neno hilo la Kiarabu linalingana au ni tafsiri ya neno la Kigiriki πλανήτης planetes (lenye maana ya "yenye kusogea") ambalo ni asili ya jina "planet" kwa Kiingereza na lugha nyingine za Ulaya.
20231101.sw_2442_2
https://sw.wikipedia.org/wiki/Sayari
Sayari
Tangu zamani watazamaji wa anga katika tamaduni mbalimbali walitambua ya kwamba nyota kwa kawaida hukaa mahali pamoja lakini nyota chache zinabadilisha polepole mahali pake kati ya nyota nyingine zikifuata njia zinazorudia kila mwaka. Nyota hizo ziliitwa "nyota zinazosogea".
20231101.sw_2442_3
https://sw.wikipedia.org/wiki/Sayari
Sayari
Zamani kulikuwa na sayari 5 tu zilizoonekana angani kwa macho matupu kama nyota zinazobadilisha mahali. Tangu kupatikana kwa mitambo kama darubini miaka 400 iliyopita idadi ya violwa angani vyenye miendo ya pekee imeongezeka sana lakini imeonekana pia kuna tofauti kubwa sana kati ya violwa hivi.
20231101.sw_2442_4
https://sw.wikipedia.org/wiki/Sayari
Sayari
Hivyo wataalamu wa Umoja wa kimataifa wa astronomia (IAU) walikubaliana mwaka 2006 kuhusu ufafanuzi wa sayari. Kiolwa cha angani kinahesabiwa kuwa sayari kama kinatimiza masharti matatu:
20231101.sw_2442_5
https://sw.wikipedia.org/wiki/Sayari
Sayari
(c) kama ni kiolwa tawala cha obiti yake na hivyo limeondoa violwa vingine kwenye obiti kwa graviti yake.
20231101.sw_2442_6
https://sw.wikipedia.org/wiki/Sayari
Sayari
Ufafanuzi huo uliamuliwa kwa kura hata kama wanaastronomia wengine hawakukubali. Azimio hili liliondoa hadhi ya sayari kwa Pluto iliyowahi kutazamwa kuwa sayari katika miaka iliyopita.
20231101.sw_2442_7
https://sw.wikipedia.org/wiki/Sayari
Sayari
Wakati mwingine kuna violwa vingine ambavyo vinavyoitwa pia "sayari" ingawa havitoshelezi masharti yote matatu.
20231101.sw_2442_8
https://sw.wikipedia.org/wiki/Sayari
Sayari
Violwa vya angani katika mfumo wa jua letu yenye umbo la kufanana na tufe yasiyolingana na sharti c) huitwa "sayari kibete" - kwa mfano Pluto.
20231101.sw_2442_9
https://sw.wikipedia.org/wiki/Sayari
Sayari
Violwa vinavyozunguka nyota nyingine nje ya mfumo wa jua letu, kama yana masi ya kutosha, huitwa "sayari za nje" (ing. exoplanet). Hadi Mei 2016 kuna 2125 zilizotambuliwa .
20231101.sw_2442_10
https://sw.wikipedia.org/wiki/Sayari
Sayari
Violwa vyenye masi ya sayari ambazo si sehemu ya mfumo wa jua lolote lakini zinapita angani zinazoweza kuitwa sayari bila nyota (ing. wandering planets, starless planets, siku hizi zaitwa pia "planemo").
20231101.sw_2442_11
https://sw.wikipedia.org/wiki/Sayari
Sayari
sayari zinazoonekana kwa macho matupu ambazo ni Utaridi, Zuhura, Mirihi, Mshtarii na Zohali. Hizi zilijulikana tangu kale na mabaharia hasa walizitumia kwa kukadiria njia wakiwa baharini mbali na bara. Majina haya yamepokelewa na Waswahili wa Kale kutoka kwa lugha ya Kiarabu pamoja na majina mengi ya nyota. Ila sayari ya pili yaani Zuhura ambayo ni sayari inayong'aa kuliko zote pia ina jina la Kibantu ambayo ni Ng'andu ("mwenye kung'aa). Kwa lugha za Ulaya kama Kiingereza, Kifaransa, Kijerumani majina ya sayari za jua letu yanatokana na majina ya miungu ya Roma ya Kale au Ugiriki ya Kale.
20231101.sw_2442_12
https://sw.wikipedia.org/wiki/Sayari
Sayari
sayari zisizoonekana kwa macho kama Uranus na Neptun pamoja na sayari kibete (Pluto) zilitambuliwa tu bada ya kupatikana kwa mitambo ya darubini. Hatua hii ya kiteknolojia ilitokea Ulaya na hivyo wataalamu wa Ulaya waliendelea katika desturi ya kutumia majina yenye asili katika lugha za kale Kigiriki na Kilatini. Elimu ya sayari hizi za nje zilizokuwa geni kwa mataifa yote mengine ya dunia ilisambaa pamoja na majina ya Kiulaya na hivyo lugha nyingi zinatumia majina haya.
20231101.sw_2442_13
https://sw.wikipedia.org/wiki/Sayari
Sayari
Jua letu lina sayari nane ambazo ni Utaridi (Mercury), Zuhura (pia: Ng'andu; Venus), Dunia yetu (Earth), Mirihi (Mars), Mshtarii (Jupiter), Zohali (Saturn), Uranusi na Neptuni.
20231101.sw_2442_14
https://sw.wikipedia.org/wiki/Sayari
Sayari
Toka mwaka 1930 hadi Agosti 2006 Pluto ilikuwa ikitambulika kama sayari hivyo kufanya idadi ya sayari zinazojulikana kuwa tisa. Hata hivyo chama chenye mamlaka juu ya masuala ya sayari na nyota, Umoja wa Kimataifa wa Astronomia kimetangaza rasmi kuwa Pluto si sayari na kuiita sayari kibete. Vitabu vingi vya shule vimebadilishwa kulingana na uamuzi huo, japo bado kuna vitabu ambavyo bado vinaonyesha Pluto kuwa sayari kweli.
20231101.sw_2442_15
https://sw.wikipedia.org/wiki/Sayari
Sayari
Sayari tano za Utaridi, Zuhura, Mirihi, Mshtarii na Zohari huonekana kwa macho kama nyota angani. Lakini tangu zamani zilitambuliwa kuwa tofauti kwa sababu hazikai mahali palepale kama nyota ya kawaida bali huhamahama angani. Kutokana na tabia hii zimetazamwa mara nyingi kuwa na nguvu za pekee au hata kuwa miungu. Unajimu umetumia mwendo wa sayari zinazoonekana kwa macho kama msingi muhimu wa makadirio yao.
20231101.sw_2442_16
https://sw.wikipedia.org/wiki/Sayari
Sayari
Sayari nyingine katika mfumo wa jua zimetambuliwa tangu kutokea kwa astronomia ya kisayansi kwa darubini. Hizi ni Uranus na Neptun. Katika lugha ya Kiswahili sayari zinazoonekana kwa macho huwa na majina ya asili ya Kiarabu isipokuwa Zuhura ina jina la Kibantu la Ng'andu pamoja na jina la asili ya Kiarabu. Majina mengine ni ya asili ya Kilatini.
20231101.sw_2442_17
https://sw.wikipedia.org/wiki/Sayari
Sayari
Jumla ya jua, sayari zote 8 pamoja na miezi yao, sayari kibete, vimondo, nyotamkia na asteroidi inaitwa mfumo wa jua.
20231101.sw_2442_18
https://sw.wikipedia.org/wiki/Sayari
Sayari
Sayari za jua letu hutofautiana kwa ukubwa na muundo. Mshtarii (Jupiter) ni sayari kubwa na masi yake ni mara 318 masi ya dunia yetu. Sayari ndogo ni Utaridi na masi yake ni takriban nusu ya dunia.
20231101.sw_2442_19
https://sw.wikipedia.org/wiki/Sayari
Sayari
Kutokana na umbali tunatofautisha "sayari za ndani" kuanzia Utaridi (Mercury) hadi ukanda wa asteroidi, halafu "sayari za nje" kuanzia Mshtarii (Jupiter) hadi Uranus.
20231101.sw_2442_20
https://sw.wikipedia.org/wiki/Sayari
Sayari
Sayari za mwamba: sayari hizi zina muundo unaofanana na dunia yetu; asilimia kubwa ya masi ni mwamba. Hizi ni sayari za ndani za mfumo wa jua letu. Zote ni ndogo kuliko sayari za nje.
20231101.sw_2442_21
https://sw.wikipedia.org/wiki/Sayari
Sayari
Sayari jitu za gesi: sayari hizi kama Mshtarii (Jupiter) na Zohali (Saturn) ni kubwa na zimefanywa na hidrojeni na heli. Masi ya Mshtarii ni mara 318 ile ya dunia, Zohali mara 95. Ilhali sayari hizi ni baridi kutokana na umbali mkubwa na jua, hidrojeni inapatikana kwa kiasi kikubwa katika hali mango na kwenye sehemu za ndani hidrojeni ina tabia kama metali kutokana na shinikizo kubwa.
20231101.sw_2442_22
https://sw.wikipedia.org/wiki/Sayari
Sayari
Sayari jitu za barafu: hizi ni Uranus na Neptun. Ni kubwa kuliko dunia, lakini si kama sayari jitu za gesi; Uranus huwa na masi 14 za dunia, Neptun na masi 17 za dunia. Ganda la nje ni mchanganyiko wa hidrojeni na methani, na sehemu za ndani ni barafu ya maji na methani.
20231101.sw_2442_23
https://sw.wikipedia.org/wiki/Sayari
Sayari
Wataalamu wa astronomia wamegundua sayari-nje (ing. exoplanets) yaani sayari zilizoko nje ya mfumo wa Jua letu zinazozunguka nyota mbalimbali. Kutokana na umbali mkubwa na matatizo ya utazamaji kwa muda mrefu hakukuwa na uhakika kama nyota kuwa na sayari ni jambo la kawaida angani au kama sayari ni chache tu.
20231101.sw_2442_24
https://sw.wikipedia.org/wiki/Sayari
Sayari
Tangu 1995 kuwepo kwa sayari-nje kuliweza kukadiriwa kutokana na mabadiliko ya mwendo wa nyota kadhaa yaliyoweza kuelezwa tu kutokana na masi ya karibu inayobadilisha mwendo wa kawaida. Baada ya kuboreshwa kwa vifaa vipimo vya mabadiliko ya mng'aro vimeonyesha mipito ya sayari, maana wakati wa kupita kwa sayari kati ya nyota fulani na mtazamaji duniani sayari inafunika sehemu ya nyota yake, hivyo mng'aro wake unapungua. Kiasi cha mabadiliko ya mng'aro kinaruhusu kukadiria umbali wa sayari na nyota yake na ukubwa wake. Sayari-nje nyingi zimetambuliwa kwa kutumia mbinu huu. Kutokana na maendeleo ya darubini imewezekana tangu mwaka 2004 kutambua sayari-nje kadhaa moja kwa moja lakini idadi yao hadi sasa ni ndogo wa sababu ugunduzi ni vigumu.
20231101.sw_2442_25
https://sw.wikipedia.org/wiki/Sayari
Sayari
Hadi Aprili 2019 kuwepo kwa sayari-nje 4,048 kumethibitishwa na kati ya hizi mifumo ya sayari 659 imetambuliwa ambako kuna zaidi ya sayari moja.
20231101.sw_2442_26
https://sw.wikipedia.org/wiki/Sayari
Sayari
Nyingi kati ya hizo zilikuwa na ukubwa kufanana na Mshtarii au kubwa zaidi. Lakini sayari ndogo zaidi zimetambuliwa pia.
20231101.sw_2443_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/Nyota
Nyota
Hali halisi nyota ni vitu sawa na Jua letu ambalo ni nyota mojawapo. Kwa kutumia darubini na vifaa vya kisayansi imegunduliwa ya kwamba ni magimba makubwa sana katika anga-nje yanayong'aa kwa sababu yanatoa mwanga, joto na aina mbalimbali za mnururisho kutokana na myeyungano wa kinyukilia ndani yake. Lakini ziko mbali sana na kwa hiyo tunaziona kama nukta ndogo za nuru. Kwa jumla nyota zinaonekana kwenye anga kwa mpangilio usiobadilika, na kila nyota huwa na mahali pake pasipobadilika kati ya nyota nyingine, hata kama nyota kwa jumla zinazunguka angani juu yetu kila siku.
20231101.sw_2443_1
https://sw.wikipedia.org/wiki/Nyota
Nyota
Leo tunajua ya kwamba nyota zote huwa na mwendo kwenye anga lakini mabadiliko haya hutokea polepole hayaonekani katika muda wa maisha ya binadamu. Lakini tunajua kutokana na habari za kihistoria ya kwamba mabadiliko yapo.
20231101.sw_2443_2
https://sw.wikipedia.org/wiki/Nyota
Nyota
Nyota nyingi ni magimba kama jua letu maana masi kubwa ya gesi na utegili wenye hali ya joto kali, ya sentigredi elfu kadhaa. Zinaonekana ndogo kwa sababu ya umbali wao.
20231101.sw_2443_3
https://sw.wikipedia.org/wiki/Nyota
Nyota
Galaksi: Nyota tatu zinaonekana kwa macho matupu si gimba moja tu bali kundi la nyota milioni au hata bilioni kadhaa; kutokana na umbali mkubwa zinaonekana kama nukta moja ya nuru. Hizi ni galaksi ya Andromeda na mawingu mawili ya Magellan. Makundi makubwa ya nyota yanaitwa fungunyota kama idadi ya nyota iko chini ya milioni au galaksi kama ni kundi kubwa zaidi linalojitegemea. Kwa darubini galaksi nyingi zimetambuliwa.
20231101.sw_2443_4
https://sw.wikipedia.org/wiki/Nyota
Nyota
Sayari: Kati ya nyota zinazoonekana kwa macho kuna chache zinazobadilisha polepole mahali angani kati ya nyota nyingine. Zikihama zinafuata mwendo maalumu unaorudia kila mwaka. Nyota hizi zinaitwa sayari. Tangu kupatikana kwa darubini tunajua ya kwamba sayari ni gimba mango kubwa kama dunia yetu lenye umbo la tufe linalozunguka jua kwenye anga ya ulimwengu. Kwa macho haiwezekani kutofautisha mara moja sayari na nyota nyingine. Kwa hiyo katika lugha ya kila siku sayari huitwa mara nyingi "nyota" ikionekana kwa macho. Lakini tangu milenia nyingi wataalamu waliotazama anga walijua kuna tofauti. Tangu miaka kadhaa inajulikana kuna sayari nyingi hata nje ya mfumo wa jua letu lakini hizi hazionekani kwa macho wala kwa darubini za kawaida. Zinaitwa sayari za nje (kwa Kiingereza exoplanets)
20231101.sw_2443_5
https://sw.wikipedia.org/wiki/Nyota
Nyota
Nyotamkia (comets): Mara kwa mara zinatokea nyota mpya ambazo hazikuonekana siku kadhaa zilizopita. Hazikai mahali palepale angani lakini zina mwendo wa kila siku kati ya nyota nyingine hadi kupotea tena. Zikionekana kubwa huonyesha nuru ya pembeni kama mkia, kwa hiyo huitwa nyotamkia au kometi. Hali halisi ni magimba mango yasiyo makubwa sana yanayozunguka jua letu.Sehemu ya mata yao ni barafu inayoyeyuka zikikaribia Jua na hii ni asili ya "mkia"
20231101.sw_2443_6
https://sw.wikipedia.org/wiki/Nyota
Nyota
Jua letu ni nyota iliyo karibu na dunia yetu tunapoishi ambayo ni sayari yake. Inaonekana kubwa kushinda nyota zote kwa sababu ni karibu. Wingi wa nuru yake unaficha nyota nyingine wakati wa mchana. Imegunduliwa ya kuwa ni tufe kubwa sana yenye joto kali na kwa hiyo mada yake ni katika hali ya utegili yaani kama gesi ya joto sana. Kipenyo chake ni zaidi ya kilomita milioni 1.3 na umbali wake nasi ni takribani kilomita milioni 150. Kwa jumla karibu nyota zote tunazoona ni jua kama letu yaani magimba kubwa sana ya utegili wa joto. Jua letu ni kitovu cha mfumo wa jua pamoja na sayari, miezi yao, kometi na vumbi nyingi ambazo zinaizunguka.
20231101.sw_2443_7
https://sw.wikipedia.org/wiki/Nyota
Nyota
Habari za nyota zinakusanywa na kufanyiwa utafiti na sayansi ya astronomia. Wanaastronomia wanatumia vifaa kama darubini kutazama nyota na kupima nuru yake. Kwa kutumia mbinu za sayansi ya fizikia inawezekana kutambua tabia nyingi za nyota ingawa ziko mbali sana.
20231101.sw_2443_8
https://sw.wikipedia.org/wiki/Nyota
Nyota
Tofauti na elimu ya unajimu ambao unatumia mbinu nyingi za kale, lakini haufuati utaratibu wa kisayansi, bali unajaribu kutabiri mambo yajayo kutokana na nyendo za nyota.
20231101.sw_2443_9
https://sw.wikipedia.org/wiki/Nyota
Nyota
Nyota zinazoonekana kwa macho wakati wa usiku ni kama 6,000 lakini idadi yake hali halisi ni kubwa mara nyingi zaidi. Hakuna aliyeweza kuhesabu nyota zote; kuna makadirio ya kuwa idadi inaweza kufika 70,000,000,000,000,000,000,000.
20231101.sw_2443_10
https://sw.wikipedia.org/wiki/Nyota
Nyota
Nyota hupatikana angani katika makundi kama mawingu makubwa sana. Kundi la namna hiyo huitwa galaksi. Galaksi yetu, ikiwemo mfumo wa jua letu, imekadiriwa kuwa na nyota zaidi ya 300,000,000,000. Tunaona sehemu za nyota zake angani zikionekana kama kanda ya kung'aa linalojulikana kwa jina "njia nyeupe".
20231101.sw_2443_11
https://sw.wikipedia.org/wiki/Nyota
Nyota
Kutokana na umbali mkubwa kati ya nyota na nyota umbali huo hautajwi kwa mita au kilomita jinsi ilivyo duniani. Wanaastronomia hutumia hapa vizio vya
20231101.sw_2443_12
https://sw.wikipedia.org/wiki/Nyota
Nyota
Nyota jirani kabisa na jua letu inaitwa Alpha Centauri: umbali wake ni mwakanuru 4.2, maana yake nuru yake inahitaji zaidi ya miaka minne hadi ifike kwetu. Kwa maana nyingine tunaiona nyota hii jinsi ilivyokuwa miaka minne iliyopita.
20231101.sw_2443_13
https://sw.wikipedia.org/wiki/Nyota
Nyota
Galaksi ya jirani inayoitwa Andromeda ina umbali wa mwakanuru milioni 2.5. Maana yake mwanga wake unahitaji miaka milioni mbili na nusu mpaka kuonekana kwetu au kwa lugha nyingine tunaona galaksi ya Andromeda jinsi ilivyokuwa miaka hiyo milioni mbili na nusu iliyopita.
20231101.sw_2443_14
https://sw.wikipedia.org/wiki/Nyota
Nyota
Fizikia na astronomia zimegundua ya kwamba nyota hazidumu milele bali zina mwanzo na pia mwisho. Kutokana na tabia hii wataalamu mara nyingi huongea juu ya "maisha", "kuzaliwa" na "kufa" kwa nyota ingawa si viumbehai.
20231101.sw_2443_15
https://sw.wikipedia.org/wiki/Nyota
Nyota
Nyota zinaanza katika nebula au katika mawingu makubwa ya gesi kwenye anga ya ulimwengu. Kama wingu, ambalo sehemu kubwa yake ni hidrojeni, ni kubwa sana inaanza kujikaza kutokana na graviti yake.
20231101.sw_2443_16
https://sw.wikipedia.org/wiki/Nyota
Nyota
Katika muda wa miaka milioni 10-15 mkusanyiko huu unazidi kuvuta mata kwake na kuongeza graviti yake tena na kujikaza. Katika kitovu cha masi hii shinikizo na halijoto zinapanda. Kadiri gesi inavyojikaza, nguvu ya graviti ndani yake inaongezeka, na atomi zake zinaanza kugusana. Halijoto inazidi hadi kufikia kiwango ambako myeyungano wa kinyuklia (nuclear fusion) unaanza ambako hidrojeni inabadilika kuwa heliamu.
20231101.sw_2443_17
https://sw.wikipedia.org/wiki/Nyota
Nyota
Kipindi cha mmeyungano nyuklia wa hidrojeni kinaendelea kwa miaka bilioni kadhaa hadi sehemu kubwa ya hidrojeni itakapokwisha. Hapo sehemu za nje za nyota hupoa na kupanuka; hali hii huitwa jitu jekundu (red giant) kwa sababu ya ukubwa na rangi yake. Majitu mekundu kadhaa huonekana kwa macho angani yaking'aa kwa nuru nyekundu. Kama masi ya nyota bado ni kubwa mmeyungano nyuklia unaendelea kuzaa elementi nzito zaidi kwa sababu sehemu ya heliamu inaendelea kujibadilisha kuwa elementi za juu zaidi. Inaaminiwa ya kwamba elementi zote ulimwenguni zilianzishwa ndani ya nyota.
20231101.sw_2443_18
https://sw.wikipedia.org/wiki/Nyota
Nyota
Mwishoni, kama masi haitoshi tena kuendeleza mmeyungano, mnururisho unapungua na masi inaweza kujikaza. Kutegemeana na ukubwa wa masi nyota inaweza kuingia upya katika mchakato wa myeyungano nyuklia kwa ghafla na kupasuka. Mabaki ya mlipuko huu yanakaa angani tu na mara nyingi huingia tena katika mwendo wa kuzaa nyota mpya; sehemu ndogo za masi hii huwa sayari.
20231101.sw_2443_19
https://sw.wikipedia.org/wiki/Nyota
Nyota
Kama masi imejikaza sana shimo jeusi (kwa Kiingereza: black hole) hutokea. Katika hali hii nguvu ya graviti ni kubwa mno: inashika hata nuru yenyewe ambayo haiwezi kutoka nje tena.
20231101.sw_2444_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/Daniel%20Arap%20Moi
Daniel Arap Moi
Daniel Toroitich arap Moi (2 Septemba 1924 - 4 Februari 2020) alikuwa Rais wa Kenya kutoka mwaka 1978 mpaka 2002.
20231101.sw_2444_1
https://sw.wikipedia.org/wiki/Daniel%20Arap%20Moi
Daniel Arap Moi
Moi alizaliwa Sacho, wilaya ya Baringo, Mkoa wa Bonde la Ufa, na alilelewa na mama yake Kimoi Chebii, kufuatia kuaga dunia mapema kwa baba yake.