_id
stringlengths 15
22
| url
stringlengths 31
150
| title
stringlengths 1
86
| text
stringlengths 100
23.8k
|
---|---|---|---|
20231101.sw_2391_12
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Nyasa%20%28ziwa%29
|
Nyasa (ziwa)
|
Mzozo ulifufuka tena tangu mwaka 2012 baada ya Malawi kutoa vibali vya upelelezi wa gesi na mafuta chini ya ziwa, tendo linalopingwa na Tanzania.
|
20231101.sw_2395_0
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Malawi%20%28maana%29
|
Malawi (maana)
|
Malawi kama matamshi ya ufalme wa Marawi uliokuwa na nguvu katika kusini ya nchi kati ya karne 16. - 19. BK
|
20231101.sw_2396_0
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mafia
|
Mafia
|
Wilaya ya Mafia katika Tanzania inayojumuisha kisiwa cha Mafia pamoja na visiwa vidogovidogo karibu nacho
|
20231101.sw_2398_0
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kisiwa%20cha%20Mafia
|
Kisiwa cha Mafia
|
Mafia ni funguvisiwa la Tanzania, pamoja na jina la kisiwa kikubwa ndani yake, linalotazama mwambao wa Afrika ya Mashariki km 130 kusini kwa Dar es Salaam karibu na mdomo wa Mto Rufiji.
|
20231101.sw_2398_1
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kisiwa%20cha%20Mafia
|
Kisiwa cha Mafia
|
Kisiwa kikuu kina urefu wa km 49 na upana wa km 16; eneo lake ni takriban km² 400. Inajulikana pia kwa jina "Chole shamba" kutokana na mji wa kale wa Chole uliokuwepo kwenye kisiwa kidogo cha Chole kilichopo karibu na kisiwa kikuu kwa umbali wa mita 900.
|
20231101.sw_2398_2
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kisiwa%20cha%20Mafia
|
Kisiwa cha Mafia
|
Wilaya ya Mafia ni kati ya wilaya 6 za mkoa wa Pwani ikiwa na wakazi 40,801 (2002). Mji mkubwa na makao makuu ya wilaya ni Kilindoni.
|
20231101.sw_2398_3
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kisiwa%20cha%20Mafia
|
Kisiwa cha Mafia
|
Wakazi walio wengi ni wavuvi wanaolima pia mashamba madogo. Bidhaa za sokoni ni pamoja na nazi, chokaa na samaki.
|
20231101.sw_2398_4
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kisiwa%20cha%20Mafia
|
Kisiwa cha Mafia
|
Kuna utalii unaosifiwa sana lakini idadi ya wageni bado ni ndogo. Hasa Waitalia wamependa kutembelea Mafia pia kwa sababu ya jina la kisiwa ambalo kwa Kiitalia linamaanisha shirika la kigaidi lenye historia ndefu katika Italia ya kusini hadi siku ya leo.
|
20231101.sw_2398_5
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kisiwa%20cha%20Mafia
|
Kisiwa cha Mafia
|
Mafia ilikuwa mahali pa miji ya kale ya utamaduni wa Waswahili kama vile miji ya Chole na Kua. Baada ya kuondoka kwa Wareno ilikuwa chini ya Sultani wa Omani (baadaye wa Zanzibar).
|
20231101.sw_2398_6
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kisiwa%20cha%20Mafia
|
Kisiwa cha Mafia
|
Mwaka 1892 Wajerumani walinunua Mafia kutoka kwa Sultani wa Zanzibar ikawa sehemu ya Afrika ya Mashariki ya Kijerumani.
|
20231101.sw_2398_7
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kisiwa%20cha%20Mafia
|
Kisiwa cha Mafia
|
Mwaka 1915, wakati wa Vita Kuu ya Kwanza, Waingereza waliteka kisiwa wakishambulia kutoka hapa manowari ya Kijerumani ya SMS Königsberg mdomoni mwa mto Rufiji kutoka Mafia.
|
20231101.sw_2398_8
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kisiwa%20cha%20Mafia
|
Kisiwa cha Mafia
|
Mnamo 1922, baada ya mwisho wa Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia Mafia imekuwa sehemu ya Tanganyika, si tena Zanzibar.
|
20231101.sw_2398_9
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kisiwa%20cha%20Mafia
|
Kisiwa cha Mafia
|
Asili ya Kua , kuhusu historia ya mji wa Kua kisiwani Chole, ilivyokusanywa na Pat Caplan mnamo mwaka 1966
|
20231101.sw_2399_0
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Wilaya%20ya%20Mafia
|
Wilaya ya Mafia
|
Mafia ni moja kati ya wilaya 6 za mkoa wa Pwani katika Tanzania yenye postikodi namba 61700. Eneo lake ni hasa Kisiwa cha Mafia na visiwa vidogo karibu nacho. Mji mkuu na makao makuu ya wilaya ni Kilindoni. Wakati wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, wilaya ilikuwa na wakazi wapatao 46,438 walioishi humo.
|
20231101.sw_2399_1
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Wilaya%20ya%20Mafia
|
Wilaya ya Mafia
|
Wilaya hii inajumuisha funguvisiwa pamoja na kisiwa cha Mafia ndani yake inayotazama mwambao wa Afrika ya Mashariki 130 km kusini ya Daressalaam karibu na mdomo wa Mto Rufiji. Umbali wake na bara ni 16 km.
|
20231101.sw_2399_2
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Wilaya%20ya%20Mafia
|
Wilaya ya Mafia
|
Mafia kisiwa kikuu ina urefu wa 50 km na upana wa 8 km; eneo lake ni takriban 400 km². Inajulikana pia kwa jina "Chole shamba" kutokana na mji wa kale wa Chole iliyokuwepo kwenye kisiwa kidogo cha Chole mjini karibu na kisiwa kikuu.
|
20231101.sw_2400_0
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Tanganyika%20%28ziwa%29
|
Tanganyika (ziwa)
|
Ziwa Tanganyika ni moja ya maziwa makubwa ya Afrika ya Kati likienea mpakani mwa Tanzania, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Burundi na Zambia.
|
20231101.sw_2400_1
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Tanganyika%20%28ziwa%29
|
Tanganyika (ziwa)
|
Ni ziwa kubwa la pili duniani kwa wingi wa maji matamu baada ya Ziwa Baikal (Siberia) kwa kuzingatia kiasi cha maji ndani yake na kina (hadi mita 1,470).
|
20231101.sw_2400_2
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Tanganyika%20%28ziwa%29
|
Tanganyika (ziwa)
|
Hatuna uhakika jinsi gani wenyeji walioishi kando ya ziwa hilo waliliita kwa lugha zao mbalimbali. Kutokana na taarifa za wapelelezi Wazungu waliofika huko kwenye karne ya 19 na kushika yale waliyoelewa kutoka kwa wenyeji, kuna ushuhuda fulani kuhusu majina manne ambayo ni "Tanganika", "Liemba", "Kimana" na "Nsaga".
|
20231101.sw_2400_3
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Tanganyika%20%28ziwa%29
|
Tanganyika (ziwa)
|
Jina la Tanganika limepokewa na Wazungu wa kwanza kutoka kwa wenyeji wa Ujiji. Henry Morton Stanley aliyetembelea ziwa mnamo mwaka 1876 aliandika ya kwamba watu wa Ujiji hawakuwa na uhakika kuhusu maana ya jina, ila tu kwamba lilimaanisha "ziwa kubwa". Maana waliita maziwa madogo "Kitanga", na waliita pia "ziwa la Usukuma" yaani Viktoria Nyanza kwa jina hilo "Tanganika". Wajiji walimwambia Stanley ya kwamba labda neno "nika" ilitokana na aina ya samaki walioitwa vile. Baadaye Stanley alikumbuka neno "nika" katika lugha nyingine za Kiafrika kwa maana ya "tambarare, eneo kubwa bapa" akahisi ya kwamba waliita ziwa kama "tambarare kubwa iliyotanda" .
|
20231101.sw_2400_4
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Tanganyika%20%28ziwa%29
|
Tanganyika (ziwa)
|
Stanley alishika pia majina ya ziwa kwa makabila mengine: watu wa Marungu walisema "Kimana", wale wa Urungu "Iemba" na Wakawendi "Nsaga" kwa maana "ziwa lenye dhoruba". Alichoshika na watu wa Urungu, yaani "Iemba", inalingana na taarifa ya David Livingstone aliyekuta jina "Liemba" kuwa jina la sehemu ya kusini ya ziwa na jina hili linaendelea kutumiwa kwa meli ya MV Liemba inayosafirisha watu na bidhaa ziwani tangu mwaka 1914.
|
20231101.sw_2400_5
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Tanganyika%20%28ziwa%29
|
Tanganyika (ziwa)
|
Jina la ziwa limekuwa pia jina la eneo lililokabidhiwa kwa Uingereza kama Tanganyika baada ya Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia tangu 1919.
|
20231101.sw_2400_6
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Tanganyika%20%28ziwa%29
|
Tanganyika (ziwa)
|
Maji ya Ziwa Tanganyika yanajaza ufa kubwa kwenye ganda la dunia ambalo ni sehemu ya bonde la ufa la Afrika ya Mashariki. Ni ziwa lenye kina kikubwa katika Afrika.
|
20231101.sw_2400_7
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Tanganyika%20%28ziwa%29
|
Tanganyika (ziwa)
|
Kina cha wastani ni m 570, ni kubwa zaidi katika sehemu ya kaskazini ambako vilindi vyake hufikia kina cha mita 1470. Kutokana na kina kikubwa kinashika kiwango kikubwa cha maji matamu kati ya maziwa yote ya Afrika (18,900 km³) na asilimia 16 ya maji matamu yote duniani.
|
20231101.sw_2400_8
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Tanganyika%20%28ziwa%29
|
Tanganyika (ziwa)
|
Urefu wa ziwa ni kilomita 676 kutoka kaskazini hadi kusini na upana wake ni km 50 kwa wastani. Uso wa maji huwa na eneo la km2 32,900 na urefu wa pwani yake ni km 1,828.
|
20231101.sw_2400_9
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Tanganyika%20%28ziwa%29
|
Tanganyika (ziwa)
|
Kina kikubwa cha ziwa kimesababisha kuwepo kwa safu za maji zisizochanganya maana maji ya chini hayakorogwi kwa upepo au mikondo na maji ya juu, hivyo maji ya chini hayapokei oksijeni na kuwa na uhai kidogo. Samaki na viumbehai wengi hawawezi kuishi katika maji bila oksijeni.
|
20231101.sw_2400_10
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Tanganyika%20%28ziwa%29
|
Tanganyika (ziwa)
|
Ziwa linapokea maji yake kutoka mito ya mazingira inayoishia humo. Beseni lake huwa na eneo la km2 231,000 (sq mi 89,000).
|
20231101.sw_2400_11
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Tanganyika%20%28ziwa%29
|
Tanganyika (ziwa)
|
Mito miwili mikubwa na mito mingi midogo inaishia ziwani. Mto Lukuga hutoka ziwani na kupeleka maji yake kwenda beseni la Kongo.
|
20231101.sw_2400_12
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Tanganyika%20%28ziwa%29
|
Tanganyika (ziwa)
|
Mto mkubwa zaidi unaoingia ni Ruzizi unaofika upande wa kaskazini kutoka Ziwa Kivu. Malagarasi, ambao ni mto mrefu wa pili nchini Tanzania, inaingia upande wa mashariki.
|
20231101.sw_2400_13
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Tanganyika%20%28ziwa%29
|
Tanganyika (ziwa)
|
Kutokana na mahali pake katika tropiki kwenye jua kali, Ziwa Tanganyika linapotewa na maji mengi kwa njia ya uvukizaji. Kwa hiyo kiasi cha maji ndani yake inategemeana na kiasi cha maji yanayoingia. Kwa sasa chanzo kikubwa ni maji ya Ziwa Kivu. Imegunduliwa ya kwamba uwiano wa ziwa ulibadilika sana katika historia.
|
20231101.sw_2400_14
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Tanganyika%20%28ziwa%29
|
Tanganyika (ziwa)
|
Mnamo miaka 200,000 iliyopita uso wa ziwa ulikuwa mita 600 chini ya uwiano wa leo. Wakati wa vipindi vya tabianchi yenye mvua nyingi zaidi uwiano ulipanda juu, na kupungua tena kwenye vipindi vya ukame. Vipindi hivi vya mabadiliko vilidumu mara kwa mara miaka elfu kadhaa.
|
20231101.sw_2400_15
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Tanganyika%20%28ziwa%29
|
Tanganyika (ziwa)
|
Hali ya sasa imepatikana tangu miaka 12,000. Wakati ule volkeno za Virunga vililipuka na kuziba mto uliowahi kubeba maji ya Ziwa Kivu kuelekea mto Naili na baada ya kufikia uwiano wa leo maji ya Kivu yalianza kutoka upande wa Tanganyika kupitia njia ya Ruzizi.
|
20231101.sw_2400_16
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Tanganyika%20%28ziwa%29
|
Tanganyika (ziwa)
|
Mabadiliko ya uwiano wa maji kwenye ziwa yalitazamwa pia katika historia ya miaka 200 iliyopita kwa kulinganisha kumbukumbu ya wakazi na taarifa za wapelelezi Wazungu walioandika taarifa juu ya safari zao. Baada ya mwaka 1800 maji yalikuwa chini sana, kabla ya 1900 yalikuwa juu sana, tangu 1900 yalishuka tena. Katika miaka ya 1960 ziwa lilijaa tena likabaki hivi hadi sasa.
|
20231101.sw_2400_17
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Tanganyika%20%28ziwa%29
|
Tanganyika (ziwa)
|
Miji mikubwa ziwani ni bandari za Kigoma kwa upande wa Tanzania na Kalemie kwa upande wa Kongo. Kila bandari ni pamoja na mwanzo wa njia ya reli. Mji mkubwa kabisa ni Bujumbura, mji mkuu wa Burundi.
|
20231101.sw_2400_18
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Tanganyika%20%28ziwa%29
|
Tanganyika (ziwa)
|
Eneo lote la ziwa limegawiwa baina ya nchi jirani yaani Tanzania, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Burundi na Zambia. Sehemu kubwa iko chini ya Tanzania (46%) na Kongo (40%).
|
20231101.sw_2400_19
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Tanganyika%20%28ziwa%29
|
Tanganyika (ziwa)
|
Kuna spishi nyingi za samaki aina ya cichlidae zinazokadiriwa kuwa 250 na angalau spishi 75 za samaki wengine. Spishi nyingi wanaishi karibu na mwambao na hadi kina cha mita 180; chini yake kiwango cha oksijeni kinapungua mno. Lakini kiasi kikubwa cha samaki kinapatikana katikati ya ziwa, ila ni spishi chache tu, hasa spishi mbili za kapenta (inayoitwa pia dagaa) na spishi nne za sangala.
|
20231101.sw_2400_20
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Tanganyika%20%28ziwa%29
|
Tanganyika (ziwa)
|
Cichlidae karibu spishi zote ni wenyeji wa ziwa yaani wametokea hapa. Pia sangala ni wenyeji wa Tanganyika, kwa hiyo hakuna matatizo kama huko Viktoria Nyanza ambako spishi ya sangala iliingizwa miaka 50 iliyopita na kuvuruga ekolojia ya ziwa.
|
20231101.sw_2400_21
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Tanganyika%20%28ziwa%29
|
Tanganyika (ziwa)
|
Cichlidae wa ziwa Tanganyika wanapendwa kama samaki wa mapambo wakinunuliwa na kufugwa na wenye tangisamaki kote duniani.
|
20231101.sw_2400_22
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Tanganyika%20%28ziwa%29
|
Tanganyika (ziwa)
|
Tasnia muhimu katika eneo la ziwa ni uvuvi. Inakadiriwa ya kwamba baina ya 25–40% za protini katika chakula cha milioni 1 ya watu wanaoishi kule ni kutoka samaki wa ziwani.
|
20231101.sw_2400_23
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Tanganyika%20%28ziwa%29
|
Tanganyika (ziwa)
|
Samaki wa ziwani wanauzwa kote Afrika ya Mashariki. Katika miaka ya 1950 uvuvi wa kibiashara ulianzishwa ziwani ukasabisha kupotea kwa samaki: kufikia mwaka 1995 mavuno ya samaki yalipungua hadi tani 180,000. Kampuni nyingi za uvuvi zilizostawi katika miaka ya 1980 ziliporomoka.
|
20231101.sw_2400_24
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Tanganyika%20%28ziwa%29
|
Tanganyika (ziwa)
|
Kigoma (Tanzania) kutoka Dar es Salaam, bado kwenye njia ya reli iliyojengwa zamani za ukoloni wa Kijerumani
|
20231101.sw_2400_25
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Tanganyika%20%28ziwa%29
|
Tanganyika (ziwa)
|
Mpulungu (Zambia) - hakuna reli bado, ila kuna mipango ya kujenga njia hadi hapa hadi njia kuu ya TAZARA
|
20231101.sw_2400_26
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Tanganyika%20%28ziwa%29
|
Tanganyika (ziwa)
|
Huduma iliyopo hadi sasa ni ngumu na hali za njia za reli si nzuri. Upande wa Tanzania treni zilichelewa mno, masaa hata siku, lakini hali ilianza kuwa afadhali kuanzia Julai 2016.
|
20231101.sw_2400_27
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Tanganyika%20%28ziwa%29
|
Tanganyika (ziwa)
|
Muhimu kwa ajili ya watu ziwani ni huduma ya feri. Kuna meli 2 zinazobeba abiria na mizigo ambazo ni MV Liemba baina ya Kigoma na Mpulungu halafu MV Mwongozo baina ya Kigoma na Bujumbura.
|
20231101.sw_2404_0
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ethiopia
|
Ethiopia
|
Ethiopia (kwa Kiamhara ኢትዮጵያ Ityopp'ya; kwa Kiswahili pia "Uhabeshi") ni nchi ya Afrika ya Mashariki iliyoko kwenye Pembe ya Afrika.
|
20231101.sw_2404_1
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ethiopia
|
Ethiopia
|
Nchi zinazopakana na Ethiopia ni Sudan na Sudan Kusini upande wa magharibi, Eritrea na Jibuti kaskazini, Somalia mashariki na Kenya upande wa kusini.
|
20231101.sw_2404_2
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ethiopia
|
Ethiopia
|
Ethiopia ni moja ya nchi mbili za Afrika ambazo hazikutawaliwa na wakoloni wakati walipong’ang’ania Afrika. Nchi nyingine ni Liberia. Kabla ya Vita Kuu ya Pili ya Dunia Ethiopia ilivamiwa na Waitalia (1936) lakini ilipata uhuru wake tena baada ya miaka michache.
|
20231101.sw_2404_3
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ethiopia
|
Ethiopia
|
Asili ya jina "Ethiopia" haijulikani. Kuna maelezo mbalimbali lakini yote yanakosa uhakika. Hilo ni sawa pia kwa jina la pili la kihistoria ambalo ni "Habasha" ilikuwa "Uhabeshi".
|
20231101.sw_2404_4
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ethiopia
|
Ethiopia
|
Ethiopia mara nyingi linaelezwa kuwa neno la Kigiriki cha Kale Αἰθιοπία Aithiopia lililotokana na Αἰθίοψ "Aithiops" ; maana yake "uso" (ὄψ) "kuwaka" (αιθw) hivyo labda "uso uliochomwa" ama sura nyeusi. Lakini jina hili halikumaanisha hasa nchi ya Ethiopia ya leo lakini nchi zote zenye watu wenye rangi nyeusinyeusi. Kwa muda mrefu watu wa Ulaya waliita Afrika yote kwa jina "Ethiopia". Pia si wazi kama neno la Kiafrika lenye maana tofauti limechukuliwa na Wagiriki kwa maana ya neno lao la "aithiops".
|
20231101.sw_2404_5
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ethiopia
|
Ethiopia
|
Nchi yenyewe ilijulikana kwa muda mrefu wa historia yake kwa jina la Habasha. Habasha ilikuwa jina la Kiarabu kwa ajili ya nchi ikaingia kama "Uhabeshi" katika Kiswahili au "Abisinia" katika lugha za Ulaya. Asili ya jina hilo haliko wazi; wengine husema ni katika lugha ya kale ya nchi yenyewe kumaanisha "nchi kwenye nyanda za juu"; tena wengine wanadai kwamba jina limetoka Uarabuni wa kusini lilipokuwa jina la kabila moja lililohamia na watu walioleta lugha za kisemiti Ethiopia.
|
20231101.sw_2404_6
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ethiopia
|
Ethiopia
|
Ethiopia ina eneo la kilometa mraba 1,127,127 (maili mraba 435,071). Nchi yenyewe ni mojawapo ya nchi za Pembe ya Afrika upande wa mashariki.
|
20231101.sw_2404_7
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ethiopia
|
Ethiopia
|
Nchini Ethiopia kuna milima mirefu; sehemu kubwa ya nchi inaundwa na Nyanda za juu za Ethiopia zilizotenganishwa na Bonde la Ufa la Afrika Mashariki, ambalo limepasua kutoka kusini - magharibi kwenda kaskazini – mashariki na kuzungukwa na mbuga maeneo yaliyo chini. Mabonde na milima hasa nchini Ethiopia yanaathiri hali ya hewa, udongo, mimea, na makazi ya watu.
|
20231101.sw_2404_8
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ethiopia
|
Ethiopia
|
Ukweo wa milima na eneo la kijiografia vinasababisha aina mbili za hali ya hewa: eneo lililopoa liko zaidi ya ukweo wa mita 2,400 (futi 7,900) ambapo vipimo vya joto ni kati ya kuganda na 16°C (32°–61°F); vipimo vya joto kwa ukweo wa mita 1,500 na 2,400 (futi 4,900—7,900) joto ni 16°C hadi 30°C (61°–86°F); joto zaidi liko chini ya mita 1,500 (futi 4,900) ni hali ya hewa ya tropiki na hali ya hewa ya ukame na joto saa za mchana ni 27°C mpaka 50°C (81°–122°F).
|
20231101.sw_2404_9
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ethiopia
|
Ethiopia
|
Mvua ya kawaida ni kuanzia kati ya Juni mpaka kati ya Septemba lakini eneo la milima ya kusini mvua hunyesha zaidi ikianzia na mvua kidogo ya Februari ama Machi.
|
20231101.sw_2404_10
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ethiopia
|
Ethiopia
|
Ethiopia ni nchi ambayo ina ikolojia tambakazi. Ziwa Tana, ambalo liko kaskazini mwa nchi, ndilo chanzo cha Mto Naili ya Buluu (kwa Kiarabu: Bahr al Zraq). Eneo la mto huo lina aina za wanyama za pekee kama Gelada - nyani, Walia ibeka na pia Mbwa mwitu.
|
20231101.sw_2404_11
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ethiopia
|
Ethiopia
|
Historia ya binadamu katika Ethiopia ilianza mapema kabisa. Mifupa ya kale kabisa ya viumbe jamii ya watu imepatikana katika nchi hii kwa sababu zilihifadhiwa katika mazingira yabisi ya nchi.
|
20231101.sw_2404_12
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ethiopia
|
Ethiopia
|
Wataalamu wengi huamini ya kwamba Ethiopia (pamoja na Kenya na Tanzania) inaweza kuwa mahali ambako watu wa aina ya Homo Sapiens walianza kupatikana duniani.
|
20231101.sw_2404_13
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ethiopia
|
Ethiopia
|
Kuna mabaki mbalimbali ya kiutamaduni yanayochunguzwa na akiolojia, lakini sehemu kubwa ya nchi haijaangaliwa bado kitaalamu. Inaonekana kwamba katika karne za K.K. kulikuwa na uhusiano wa karibu na Uarabuni kwa sababu lugha za Kiethiopia ni karibu na lugha za upande mwingine wa Bahari ya Shamu. Inaaminiwa kwamba watu kutoka Uarabuni Kusini walihamia Ethiopia na kuleta lugha yao huko.
|
20231101.sw_2404_14
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ethiopia
|
Ethiopia
|
Biblia ina taarifa juu ya ziara ya malkia wa Sheba aliyemtembelea mfalme Suleimani wa Yerusalemu. Milki ya Sheba imedaiwa kuwepo ama Ethiopia au Yemen na wengine huamini ya kwamba ilikuwa dola la pande zote mbili za mlangobahari wa Bab el Mandeb unaotenganisha Eritrea ya leo na Uarabuni Kusini.
|
20231101.sw_2404_15
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ethiopia
|
Ethiopia
|
Milki ya kwanza ya Ethiopia inayoweza kutajwa kutokana na mabaki ya majengo na maandishi ilikuwa milki ya D'mt (pia: Da'amot) katika Ethiopia ya kaskazini pamoja na Eritrea ya leo. Kuna mabaki ya hekalu la Yeha pamoja na makaburi ambako majina ya wafalme kadhaa yamehifadhiwa kwa maandishi kwenye mawe. Lugha ilikuwa karibu sana na lugha za kale za Uarabuni. Ilikuwa na athira juu ya sehemu za kaskazini ya Ethiopia kwa kipindi kikubwa cha milenia ya 1 KK.
|
20231101.sw_2404_16
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ethiopia
|
Ethiopia
|
Ilifuata milki kubwa ya Aksum, iliyoanzishwa wakati wa kuzaliwa Yesu. Ufalme wa Aksum ulikuwa milki ya kwanza kutawala maeneo makubwa ya Ethiopia. Nabii Mwajemi Mani aliuweka Ufalme wa Aksum kwa utukufu sawa na Roma, Uajemi na Uchina kama nchi zilizokuwa na nguvu duniani karne ya 3 BK, wakati yeye alipoishi.
|
20231101.sw_2404_17
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ethiopia
|
Ethiopia
|
Ilikuwa karne ya 4 BK ambapo Frumentius, mtu Msiro-Mgiriki aliyekuwa amepotelea baharini kutokana na kuzama kwa jahazi, alishikwa na Wahabeshi na kupelekwa kortini na baadaye kumuongoa mfalme Ezana kuingia Ukristo. Kwa hiyo Wahabeshi wakampa jina Abba Selama. Kwa muda mfupi dini hiyo mpya ilienea kote.
|
20231101.sw_2404_18
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ethiopia
|
Ethiopia
|
Aksum ilistawi hasa kutokana na biashara kati ya Mediteranea na Bara Hindi iliyopita kwenye mlangobahari wa Bab el Mandeb ikatumia bandari ya Adulis (karibu na Massawa ya leo nchini Eritrea).
|
20231101.sw_2404_19
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ethiopia
|
Ethiopia
|
Uenezi wa Uislamu ulivuruga biashara hiyo na Aksum ilipoteza utawala juu ya pwani. Kuporomoka kwa uwezo wa kibiashara kunaonekana katika kusimamishwa kwa uchapaji pesa ya wafalme wa Aksum katika karne ya 7. Nchi ilishambuliwa pia kutoka milki za barani.
|
20231101.sw_2404_20
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ethiopia
|
Ethiopia
|
Mabaki ya ufalme wa Aksum yaliharibiwa mnamo mwaka 900 wakati na malkia Gudit (au Judith) aliyekuwa ama Myahudi ama kiongozi wa makabila ya Kipagani kutoka nyanda za juu.
|
20231101.sw_2404_21
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ethiopia
|
Ethiopia
|
Kiongozi wa kabila la Agaw alimwoa binti wa mfalme wa mwisho wa Aksum akaanzisha nasaba ya Zagwe na kuunda upya ufalme wa Kikristo katika nyanda za juu. Kitovu cha ufalme huu kilipelekwa zaidi mbali na pwani.
|
20231101.sw_2404_22
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ethiopia
|
Ethiopia
|
Nasaba hii ilipinduliwa mnamo 1270 na Yekuno Amlak aliyetumia jina la kifalme Tasfa Iyasus. Alianzisha nasaba iliyojiita "Wa Suleimani" kwa kudai ilikuwa ukoo wa mwana wa mfalme Suleimani na malkia wa Sheba. Tasfa Iyasus alitumia cheo cha Negus Negesti ("Mfalme wa Wafalme").
|
20231101.sw_2404_23
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ethiopia
|
Ethiopia
|
Enzi ya Mfalme Lebna Dengel, Ethiopia iliweza kuwasiliana na nchi za Ulaya na kudumisha ubalozi na nchi kama Ureno. Lakini, Mfalme Susenyos alipojiunga na Kanisa Katoliki mwaka 1622, chakari na misukosuko ilifuata. Wamisionari Wajesuiti walichukiwa na waamini wa Kanisa la Ethiopia, na katika hiyo karne ya 17 Susenyos mwana wa Mfalme Basil aliwafukuza wanamisheni hao.
|
20231101.sw_2404_24
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ethiopia
|
Ethiopia
|
Baadaye Waoromo wakaanza kuasi amri ya Kanisa la Ethiopia na kutafuta njia za dini yao, eneo hili la Uhebeshi.
|
20231101.sw_2404_25
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ethiopia
|
Ethiopia
|
Mambo hayo yote yalifanya Ethiopia itengwe miaka ya 1700. Wafalme wakawa kama wakurugenzi, ambao waliamriwa na masharifu kama Ras Mikael Sehul wa Tigrinya. Ethiopia ilitoka kutoka utengo kwa kufuatia misheni ya Uingereza kufika Ethiopia na kukamilisha muungano kati ya nchi hizi mbili; lakini, hadi milki ya Tewodros II ndipo Ethiopia ilipoanza tena shauri za Duni.
|
20231101.sw_2404_26
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ethiopia
|
Ethiopia
|
Miaka ya 1880 ilikuwa miaka ya Ulaya kung’ang’ania ukoloni Afrika ambapo Waitalia na Waingereza walitafuta kutawala eneo la Assab, bandari iliyoko karibu na mdomo wa bahari ya Shamu. Bedari ya Kusini, karibu na kiingilio cha bahari ya Shamu, ilinunuliwa na Waitalia kutoka sultani mwenyeji Machi 1870 ambayo mwaka 1882 ilizaa koloni la Eritrea.
|
20231101.sw_2404_27
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ethiopia
|
Ethiopia
|
Haya yalizua magombano kati ya Waethiopia na Waitalia na Vita vya Adowa mwaka 1896, ambapo Waethiopia walishtua dunia kwa kupiga nguvu za wakoloni na kulinda madaraka yao kwa uongozi wa Menelik II. Italia na Ethiopia zilisaini mkataba wa amani tarehe 26 Oktoba 1896.
|
20231101.sw_2404_28
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ethiopia
|
Ethiopia
|
Karne ya 20 miaka ya kwanzakwanza ilimilikiwa na Mfalme Haile Selassie, aliyechukua nafasi ya kuendeleza Ethiopia mpaka uongozi wake ulipokatizwa kwa Vita ya pili ya Uhabeshi na Italia (1936).
|
20231101.sw_2404_29
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ethiopia
|
Ethiopia
|
Waingereza na wazalendo wa Jeshi la Ethiopia wakakomboa nchi mwaka 1941, na Waingereza kukiri madaraka ya Ethiopia kwa mkataba wa Uingereza na Ethiopia mnamo Desemba 1944.
|
20231101.sw_2404_30
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ethiopia
|
Ethiopia
|
Milki ya Haile Selassie ilikoma mwaka 1974, ambapo Wakomunisti wa "Derg" walimpindua na kuanzisha serikali ya kikomunisti chini ya Mengistu Haile Mariam.
|
20231101.sw_2404_31
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ethiopia
|
Ethiopia
|
Mwaka 1977 Somalia ilivamia eneo la Ogaden (Vita vya Ogaden), lakini Ethiopia iliweza kuwafukuza Wasomali kwa msaada wa vifaa vya kijeshi vya Urusi, na majeshi ya Kuba, Ujerumani Mashariki na Yemeni. Usaidizi mwingi kutoka Nchi za Kikomunisti uliwezesha Ethiopia kudumisha mojawapo ya majeshi kubwa Afrika.
|
20231101.sw_2404_32
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ethiopia
|
Ethiopia
|
Lakini hii haikuzuia ukereketwa wa jimbo la Eritrea na Tigray, ambapo ukame wa mwaka 1985 na mapinduzi ya siasa hasa kwa Kambi za Ujamaa, zilileta uongozi wa Derg 1991 kukoma. Chama cha kukomboa Eritrea (EPLF) na Chama cha Mapinduzi cha Kidemokrasi Ethiopia (EPRDF), ziliungana kukomboa Ethiopia, wengi wa wanamgambo wakiwa wanaharakati wa Eritrea.
|
20231101.sw_2404_33
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ethiopia
|
Ethiopia
|
Mwaka 1993 jimbo la Eritrea likawa huru kutoka Ethiopia, kufuatia kura ya maoni iliyofanywa ili kumaliza vita hivyo vilivyodumu miaka 20, mmojawapo kati ya migogoro ya muda mrefu zaidi Afrika.
|
20231101.sw_2404_34
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ethiopia
|
Ethiopia
|
Mwaka 1998 magombano ya mipaka na Eritrea yalileta Vita vya Eritrea na Ethiopia ambayo vilidumu hadi Juni 2000. Vita hivyo vilileta uvivu wa uchumi na nguvu ya muungano unaongoza nchi.
|
20231101.sw_2404_35
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ethiopia
|
Ethiopia
|
Uchaguzi wa Ethiopia ulipitisha wanabaraza 547 Bungeni. Baraza hilo la bunge lilijumuika Juni 1994 na kupitisha katiba mpya ya Jimbo la Demokrasia ya Jamhuri ya Ethiopia mnamo Desemba 1994. Uchaguzi huu ulikuwa wa kwanza kuchagua wanabaraza wa kitaifa kwa sifa bungeni na wanabaraza wa majimbo mnamo Mei na Juni 1995. Vyama vingi vya upinzani viligoma kushiriki uchaguzi. Ushindi ulichukuliwa na Chama cha Mapinduzi cha Kidemokrasi cha Watu wa Ethiopia (EPRDF). Umoja wa Mataifa ukasema vyama vya upinzani vingeweza kushiriki uchaguzi kama zingetaka.
|
20231101.sw_2404_36
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ethiopia
|
Ethiopia
|
Serikali ya Majimbo ya Demokrasia ya Jamhuri ya Ethiopia ilichukua mamlaka mnamo Agosti 1995. Rais wa kwanza Negasso Gidada. EPRDF ikaongoza serikali na Waziri Mkuu Meles Zenawi ambaye aliunga mkono majimbo ya kikabila, na kuwapa madaraka viongozi wa kikabila. Ethiopia sasa ina majimbo 9 ambayo yana serikali ya madaraka ya shirika, na hata majimbo haya yanakubaliwa kutoza ushuru na kutumia akiba ya ushuru. Hata hivyo, uhuru wa habari na kisiasa bado umefinywa.
|
20231101.sw_2404_37
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ethiopia
|
Ethiopia
|
Serikali ya Zenawi ilichaguliwa tena mwaka 2000 kwa uchaguzi wa kwanza wa Kidemokrasia, Rais akiwa Girma Wolde-Giorgis.
|
20231101.sw_2404_38
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ethiopia
|
Ethiopia
|
Kutoka 1991, Ethiopia imetafuta urafiki zaidi na Marekani na Umoja wa Ulaya, ili kuweza kukopa fedha za kusaidia uchumi wake na pia kutoka Benki ya Dunia.
|
20231101.sw_2404_39
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ethiopia
|
Ethiopia
|
Uchaguzi mwingine wa Ethiopia ulikuwa tarehe 15 Mei 2005, ambao ulivutia wapigakura kiasi cha juu zaidi, asilimia 90% ya wananchi waliojiandikisha. Watazamaji wa Umoja wa Ulaya walidai uchaguzi haujafikia kiwango cha kimataifa, lakini Umoja wa Afrika ulitoa ripoti tarehe 14 Septemba kwamba Waethiopia walionyesha kujitokeza na kuheshimu demokrasia, halafu tarehe 15 Septemba, Carter Center, ikasema matokeo ya uchaguzi yaaminika na kuonyesha ushindani wa kisiasa. Uangalizi na ushuhuda wote ulimalizia kuranki Uchaguzi wa Ethiopia na kesi nyingine waipa, asilimia 64% ya matokeo mazuri, na vizuri zaidi kulingana na kesi nyingine 24%.
|
20231101.sw_2404_40
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ethiopia
|
Ethiopia
|
Tarehe za kwanza za Juni na tena Novemba, polisi kwa amri ya EPRDF wakafyatua risasi na kuua watu kwa maandamano yaliyokuwa yakipinga matokeo ya kura.
|
20231101.sw_2404_41
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ethiopia
|
Ethiopia
|
Ni kwamba vyama vya upinzani vililalamika kwamba EPRDF iliiba kura na kuwazisha wananchi na kusema baraza 299, wapata hitilafu ya wizi wa kura. Hayo yote yalichunguzwa na Watazamaji wa Uchaguzi wa kimataifa na pia Kamisheni ya Uchaguzi Ethiopia.
|
20231101.sw_2404_42
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ethiopia
|
Ethiopia
|
Matokeo ya uchunguzi huo kama haijatokea mnamo Juni 2005, wanafunzi wa chuo kikuu walianza maandamano wakisaidiwa na wanamgambo wa Muungano wa Vyama vya Upinzani. Lakini serikali kwa kutoa amri ya kukomesha maaandamano, mnamo 8 Juni, watu 26 waliuliwa mjini Addis Ababa kwa msukosuko wa maandamano na wengine wengi kushikwa.
|
20231101.sw_2404_43
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ethiopia
|
Ethiopia
|
Mnamo 5 Septemba 2005, Kamisheni ya Uchaguzi Ethiopia, ilitoa matokeo na kusema kwamba (EPRDF) kashinda uchaguzi na kwa hiyo iongoze serikali. Lakini vyama vya upinzani viliongezea viti bungeni kutoka 12 mpaka 176. Muungano wa umoja na demokrasia ulishinda viti vyote vya Addis Ababa, kwa Bunge la Taifa na Baraza la mtaala.
|
20231101.sw_2404_44
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ethiopia
|
Ethiopia
|
Maandamano yalizuka tena mitaani 1 Novemba, ambapo vyama vya upinzani viliitisha mgomo kwa jumla na pia kwa Bunge mpya, wakatae matokeo ya uchaguzi. Polisi tena walijaribu kuzuia maandamano hayo na watu 42 wakafa kwa misukosuko mjini Addis Ababa. Polisi saba pia wakafa na mwingine pia kafa kutokana na majeruhi ya mlipuko wa bomu. Tope la watu walishikwa na kufungwa jela. Februari 2006 watu elfu sita bado walikuwa jela wakingoja hukumu Machi.
|
20231101.sw_2404_45
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ethiopia
|
Ethiopia
|
Mnamo 14 Novemba, Bunge la Ethiopia lilipitisha mkataba kuimarisha Kamisheni huru na kuchunguza visa vya 8 Juni na tarehe 1 na tarehe 2 Novemba. Februari 2006 Waziri mkuu wa Uingereza Tony Blair, alitamka kwamba, EPRDF kashinda kura, lakini angetaka kuona Ethipia ikitatua shida zake yenyewe na iendelee katika njia ya demokrasia. .
|
20231101.sw_2404_46
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ethiopia
|
Ethiopia
|
Zaidi ya hayo kuna maeneo ya miji miwili (astedader akababiwoch; umoja: astedader akababi): Addis Ababa na Dire Dawa.
|
20231101.sw_2404_47
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ethiopia
|
Ethiopia
|
Ethiopia ina makabila zaidi ya 80 yenye utamaduni tofautitofauti. Watu wengi huongea lugha za Kisemiti na lugha za Kikushi.
|
20231101.sw_2404_48
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ethiopia
|
Ethiopia
|
Waoromo (34.49%), Waamhara (26.89%), Wasomali (6.20%) na Watigrinya (6.07%) ni zaidi ya 73% ya wananchi wote. Kumbe kuna makabila mengine yenye watu wachache kiasi kama 10,000.
|
20231101.sw_2404_49
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ethiopia
|
Ethiopia
|
Ethiopia ina lugha 84 za kienyeji (angalia Orodha ya Lugha za Ethiopia). Mifano fulani ni kama ifuatavyo:
|
20231101.sw_2404_50
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ethiopia
|
Ethiopia
|
Kiamhara ilikuwa lugha ya ufundishaji katika shule ya msingi lakini sasa sehemu nyingi nafasi yake imeshikwa na Kioromo na Kitigrinya.
|
20231101.sw_2404_51
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ethiopia
|
Ethiopia
|
Wakristo, ambao ndio wengi (67.3%, kati yao Waorthodoksi wa mashariki 43.8%), wanaishi hasa kwenye milima, na Waislamu (31.3%) na Wapagani (0.6%) wengi wanaishi kwenye mabonde.
|
20231101.sw_2404_52
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ethiopia
|
Ethiopia
|
Ufalme wa Aksum ulikuwa milki na nchi ya kwanza kukubali Ukristo, ambapo askofu Frumentius wa Taya, aliyetumwa na Atanasi wa Aleksandria kuiinjilisha nchi, alimuongoa Ezana wa Aksum katika karne ya 4. Kwa hiyo Wahabeshi wakampa jina Abba Selama. Kwa muda mfupi dini hiyo mpya ilienea kote.
|
20231101.sw_2404_53
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ethiopia
|
Ethiopia
|
Labda Frumentius alifika tayari na wamonaki kama wamisionari. Lakini umonaki hasa ulianza mnamo mwaka 500 walipofika wamonaki tisa wenye asili ya Siria waliotokea Misri katika monasteri za Pakomi.
|
20231101.sw_2404_54
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ethiopia
|
Ethiopia
|
Hivyo mpaka leo mtindo huo ndio unaotawala kati ya umati wa wamonaki wa Ethiopia, wakati wakaapweke ni wachache, ingawa hawajawahi kukosekana. Athari za Siria na Misri zinajitokeza katika mambo mengi.
|
20231101.sw_2404_55
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ethiopia
|
Ethiopia
|
Wamonaki wanaishi katika vibanda vya binafsi wakikutana kwa sala tu. Wamonaki wanawake (kawaida ni wajane) wanaishi jirani na monasteri ya kiume wakiitegemea kiroho na kiuchumi.
|
Subsets and Splits
No community queries yet
The top public SQL queries from the community will appear here once available.