_id
stringlengths
15
22
url
stringlengths
31
150
title
stringlengths
1
86
text
stringlengths
100
23.8k
20231101.sw_2444_2
https://sw.wikipedia.org/wiki/Daniel%20Arap%20Moi
Daniel Arap Moi
Baada ya kumaliza masomo ya chuo cha upili cha Tambach, aliweza kujiunga na chuo cha ualimu mjini Kapsabet.
20231101.sw_2444_3
https://sw.wikipedia.org/wiki/Daniel%20Arap%20Moi
Daniel Arap Moi
Mwaka wa 1960, Moi na Ronald Ngala waliunda chama cha KADU ambayo kwa Kiswahili ni Muungano wa Demokrasia ya Waafrika wa Kenya kilichoshindana na KANU iliyoongozwa na Jomo Kenyatta. Lengo la KADU, lilikuwa kuhifadhi maslahi ya makabila madogo kama Wakalenjin dhidi ya makabila makubwa kama Waluo na Wakikuyu, makabila ambayo yalikuwa zaidi upande wa chama cha KANU, Kenyatta mwenyewe akiwa Mkikuyu.
20231101.sw_2444_4
https://sw.wikipedia.org/wiki/Daniel%20Arap%20Moi
Daniel Arap Moi
KADU ilipendelea katiba ya majimbo ambapo mamlaka nyingi zingebaki kwenye ngazi za chini, na KANU ilipendelea mfumo wa serikali ya umoja ambapo mamlaka zingeunganishwa mikononi mwa serikali ya kitaifa. KANU ilipata kura nyingi katika uchaguzi kabla ya uhuru, hivyo serikali ya kikoloni ya Waingereza iliachana na katiba ya majimbo.
20231101.sw_2444_5
https://sw.wikipedia.org/wiki/Daniel%20Arap%20Moi
Daniel Arap Moi
Mwaka wa 1957, Moi alichaguliwa kwa baraza la Bonde la Ufa tena, na mwaka wa 1961 kwa baraza la bunge kwa kiti cha Baringo ya Kaskazini.
20231101.sw_2444_6
https://sw.wikipedia.org/wiki/Daniel%20Arap%20Moi
Daniel Arap Moi
Baada ya Kenya kupata uhuru mnamo 12 Desemba 1963, Kenyatta alimsihi Moi ya kwamba KADU na KANU ziungane pamoja kumaliza ukoloni. Kwa hiyo Kenya ikawa nchi ya chama kimoja, ikiimarishwa na muungano wa wengi Wakĩkũyũ-Waluo.
20231101.sw_2444_7
https://sw.wikipedia.org/wiki/Daniel%20Arap%20Moi
Daniel Arap Moi
Moi, aliweza kupanda cheo na kuwa waziri wa mambo ya ndani mwaka 1964, hasa kwa umuhimu wake kuleta faraja za watu wa bonde la ufa na jumla KADU kwa serikali ya umoja wa Taifa.
20231101.sw_2444_8
https://sw.wikipedia.org/wiki/Daniel%20Arap%20Moi
Daniel Arap Moi
Baadaye aliweza kupanda cheo zaidi akawa Makamu wa Rais mnamo 1967. Kama kiongozi kutoka kabila dogo, alituliza makabila haya makubwa nchini Kenya.
20231101.sw_2444_9
https://sw.wikipedia.org/wiki/Daniel%20Arap%20Moi
Daniel Arap Moi
Lakini, Moi alipingwa na wanasiasa wa makabila makubwakubwa, hasa Wakikuyu na Waluo. Walijaribu kubadilisha katiba na kufuta kanuni iliyomfanya makamu wa rais kuchukua nafasi yake wakati rais anaaga dunia. Hata kwa uzee na afya yake Kenyatta kudhoofika, alipinga mipango hii; katiba ilibaki jinsi ilivyokuwa.
20231101.sw_2444_10
https://sw.wikipedia.org/wiki/Daniel%20Arap%20Moi
Daniel Arap Moi
Mzee Jomo Kenyatta alipoaga dunia tarehe 22 Agosti 1978, Moi alichukua kiapo na kuwa Rais wa Kenya. Alikuwa na sifa nchini, kona zote. Alisafiri sehemu na maeneo yote Kenya, na basi wananchi wakampa faraja na hongera. Alipochukua kiapo kuwa Rais wa Kenya, alinena kwamba atafuata "nyayo" za Mzee Kenyatta, kwa maana ataendelea na sera za Kenyatta na umoja wa Harambee. Ijapokua wapinzani wake wa kisiasa, hasa kutoka makabila makubwa, walimwona Moi kama rais wa mpito tu, asiyeweza kukaa muda mrefu kwa sababu ametoka katika kabila dogo.
20231101.sw_2444_11
https://sw.wikipedia.org/wiki/Daniel%20Arap%20Moi
Daniel Arap Moi
Mnamo 1 Agosti 1982, kundi la askari wa jeshi la anga la Kenya, wakiongozwa na Hezekiah Ochuka, lilijaribu kumpindua Moi, lakini walikuta upinzani wa mikono mingine ya jeshi na polisi waliosimama upande wa rais na kushinda uasi (Ona uasi wa wanahewa wa Kenya 1982).
20231101.sw_2444_12
https://sw.wikipedia.org/wiki/Daniel%20Arap%20Moi
Daniel Arap Moi
Moi alichukua fursa hiyo kuwafukuza wapinzani wa kisiasa na kuimarisha nguvu yake. Alipunguza ushawishi wa wafuasi wa Kenyatta kwenye baraza la mawaziri kupitia uchunguzi wa muda mrefu. Uchunguzi huo ulionyesha kwamba wanasiasa kadhaa walikuwa wakishiriki katika uasi. Moi aliwasamehe lakini alifaulu kuwaonyesha kama wasaliti mbele ya jamii ya Kenya. Viongozi wa uasi huo, pamoja na Ochuka walihukumiwa kufa, na hii ilikuwa mara ya mwisho hukumu za mauti zilitekelezwa Kenya . Moi alipandisha ngazi wafuasi wake waaminifu, akabadilisha katiba kuifanya KANU iwe chama cha kisiasa pekee kinachoruhusiwa kisheria nchini. Wasomi wengi hawakukubali mabadiliko hayo walimoona mwelekeo wa kidikteta. Vyuo vikuu vilikuwa chanzo cha harakati ambazo zilitaka kuanzisha mageuzi ya kidemokrasia. Walakini, polisi jasusi iliingilia vikundi hivyo na wanaharakati wengi wa demokrasia walikwenda uhamishoni. Serikali ilipiga marufuku kufundishwa kwa Umarx katika vyuo vikuu vya Kenya. Harakati za siri zilizaliwa, kama vile Mwakenya na Pambana.
20231101.sw_2444_13
https://sw.wikipedia.org/wiki/Daniel%20Arap%20Moi
Daniel Arap Moi
Moi, alijulikana ng'ambo kama kiongozi anayeunga mkono Ulaya ya magharibi, kwa vita baridi kati ya Ukomunisti na Ukapitalisti. Kenya ilikuwa kwa Muandamano wa kutojiunga. Lakini serikali za Ulaya ya magharibi ziliona Kenya kama nchi inayopinga Ukomunisti na hivyo kambi ya nguvu kwao kushinda ukomunisti. Kwa hiyo Kenya ilipokea misaada kutoka nchi za kibepari zaidi ili kuzuia ujamaa uliotambakaa, Ethiopia, Somalia, Tanzania na pia Vita za Uganda. Kwa hiyo siasa za uhuru na haki za kibinadamu, hazikuwazisha Ulaya ya magharibi hata kidogo.
20231101.sw_2444_14
https://sw.wikipedia.org/wiki/Daniel%20Arap%20Moi
Daniel Arap Moi
Lakini, vita baridi vilipokwisha kwa kuanguka kwa Umoja wa Kisovyeti, mambo hayo mapya yakatokea, mwandamano wa watu na wanasiasa kuitisha demokrasia ya vyama nyingi, wakiongozwa na Matiba na Oginga Odinga. Moi alianza kuonekana kama mdhalimu kwa sababu alianza kuwafunga jela wanamgambo wa kidemokrasia, na pia jela nyingine za kisiri ambazo watu waliteswa kwa kunanuliwa na swali. Ulaya ya Magharibi ikaacha kuipa Kenya usaidizi wa kigeni na kwa kazo pande zote ndani ya Kenya na ng'ambo, Moi kakubali kuruhusu Demokrasia ya vyama nyingi, ambapo Moi mwenyewe kaunga uchaguzi na kukampaini kwa nguvu zaidi kwa kupinga upinzani Kasarani mnamo Desemba 1991.
20231101.sw_2444_15
https://sw.wikipedia.org/wiki/Daniel%20Arap%20Moi
Daniel Arap Moi
Moi alishinda uchaguzi wa miaka 1992 na 1997, ambapo ulizidi kwa vita vya ukabila mkoa wa bonde la ufa. Moi aliweza kuwagawa watu wa upinzani kwa kukema ukabila, na vyama vya upinzani kupasuka kwa kambi za faraja za kabila. Pia inasemekana wizi wa kura, hasa mkoa wa bonde la ufa na Ukambani.
20231101.sw_2444_16
https://sw.wikipedia.org/wiki/Daniel%20Arap%20Moi
Daniel Arap Moi
Mwaka wa 1999 Intidhamu zisizohusika na serikali kama Amnesty na uchunguzi wa Umoja wa Mataifa zilichapishwa kuonyesha haki za kibinadamu kwa wapizani wa siasa hazikutetewa Kenya Moi akiwa Rais.
20231101.sw_2444_17
https://sw.wikipedia.org/wiki/Daniel%20Arap%20Moi
Daniel Arap Moi
Jina la Moi lilitajwa kwa Ufisadi wa 'migodi' na uzuiaji wa ufisadi huo, ambapo serikali kwa sahihi za watu wachache ilisemekana imetoa pesa ya kununua na kuuza migodi ng'ambo kwa jina la kampuni bandia Goldenbarg ambapo Kamlesh Pattni, mfanyabiashara wa Kenya, alisemekana kuwa fisadi halisi kwa oparesheni za Goldenbarg na wanasiasa waliohusika. Ilisemekana kwamba Moi aliiona Goldenberg kama njia ya kupata pesa za kigeni nchini Kenya ambapo uchumi, utalii na usaidizi wa kigeni ulipokoma mwaka wa 1992. Hivyo goldenberg ilinunua na kuuza migodi iliyochomolewa Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo. Aibu hii ya Goldenbarg ni gharama ya asilimia 10 ya utolezi wa uchumi mwaka mmoja.
20231101.sw_2444_18
https://sw.wikipedia.org/wiki/Daniel%20Arap%20Moi
Daniel Arap Moi
Pesa zilizolipwa Goldenbarg, zilikuwa zitolee kenya pesa za kigeni lakini kwa sababu ni mambo fisadi, basi waliopewa pesa hizo wakurudisha na basi serikali ya Mwai Kibaki ilijaribu kuchunguza kesi yenyewe zaidi.
20231101.sw_2444_19
https://sw.wikipedia.org/wiki/Daniel%20Arap%20Moi
Daniel Arap Moi
Rais Moi, kazuiwa na katiba kwa Uchaguzi wa mwaka 2002. Wengi kwa faraja za Moi walisema katiba itekelezwe ili achaguliwe mara ya tatu, lakini Moi mwenyewe kawapinga na kutawa, na kumchagua Uhuru Kenyatta, mwana wa Rais wa kwanza, kama mwenyekiti kwa chama cha KANU. Raila Amollo Odinga kwa bidii, alikampainia Mwai Kibaki, ambaye alishinda urais kwa muungano wa NARC na Kukiriwa 29 Desemba 2002.
20231101.sw_2444_20
https://sw.wikipedia.org/wiki/Daniel%20Arap%20Moi
Daniel Arap Moi
Moi aliishi kwa utawa mjini Kapsabet, ambapo huduma zake za amani na usaidizi azifanyia kwa Chuo cha Moi Afrika. Wakenya wengi wamtambua Moi kwa hoja na vigelegele mahali popote aliposimama. Moi aliunga nchi ya umoja, ambayo inaunganisha makabila yote, juzi siku ya uchaguzi wa maono wa katiba mpya, Moi kaipinga katiba ambayo itagawa watu. Katiba mpya ilipokataliwa na watu, Kibaki kwa hadhara, yasemekana na magazeti kwamba kapanga mkutano na Moi kujadili njia ya kusonga mbele.
20231101.sw_2447_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kasi%20ya%20nuru
Kasi ya nuru
Kasi ya nuru (pia: kasi ya mwanga, kwa Kiingereza speed of light) ni kasi yake iliyopimwa hata imekubaliwa kuwa nuru inakwenda karibu kilomita laki tatu kwa sekunde moja katika ombwe. Kama nuru inapitia katika hewa kasi yake inapungua.
20231101.sw_2447_1
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kasi%20ya%20nuru
Kasi ya nuru
Katika nadharia ya uhusianifu ya Albert Einstein kasi ya nuru inadhaniwa kuwa ileile wakati wowote, pia katika hali yoyote. Yaani kasi inabaki ileile hata kama nuru inatoka katika chombo chenye kasi yenyewe au kama mtazamaji ana mwendo wake mwenyewe. Katika nadharia hiyo hakuna mwendo wenye kasi kushinda nuru. Kasi ya nuru imekuwa kipimo cha msingi katika sayansi za fizikia na unajimu.
20231101.sw_2447_2
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kasi%20ya%20nuru
Kasi ya nuru
Kasi hiyo haihusu nuru pekee inayoonekana na macho ya binadamu lakini pia kwa aina mbalimbali ya mnururisho kama mawimbi ya redio n.k.
20231101.sw_2447_3
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kasi%20ya%20nuru
Kasi ya nuru
Tangu safari ya kwanza ya watu kufika juu ya mwezi chini ya Mradi wa Apollo wa NASA tabia ya nuru kuwa na kasi ilionekana kwa watazamaji wote. Kila safari kituo cha NASA katika mji wa Houston iliwaita wanaanga kwa redio: jibu lilichukua sekunde kadhaa hadi kufika kutokana na umbali wa kilomita lakhi tatu kati ya dunia na mwezi, hivyo mazungumzo yaliendelea kwa vituo vya kusubiri hadi sauti ilipofika na kurudi.
20231101.sw_2447_4
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kasi%20ya%20nuru
Kasi ya nuru
Kama siku moja wanaanga watasafiri mbali zaidi, hadi Mirihi au Zohali ,muda huu utaongezeka kutokana na umbali na kasi ya nuru inayobaki ileile.
20231101.sw_2449_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/Galaksi
Galaksi
Galaksi (ing. galaxy) ni kundi la nyota nyingi zinazoshikamana pamoja katika anga ya ulimwengu kutokana na graviti yao. Nyota hupatikana angani katika makundi kama mawingu makubwa sana.
20231101.sw_2449_1
https://sw.wikipedia.org/wiki/Galaksi
Galaksi
Kuna galaksi nyingi sana ulimwenguni. Kwa wastani kila galaksi imekadiriwa kuwa na nyota kama bilioni 100 lakini kuna galaksi kubwa na ndogo.
20231101.sw_2449_2
https://sw.wikipedia.org/wiki/Galaksi
Galaksi
Galaksi yetu, ikiwemo mfumo wetu wa jua, imekadiriwa kuwa na nyota zaidi ya bilioni 300 (3·1011). Sehemu ya nyota hizi zinaonekana kama kanda la kung'aa kwenye anga la usiku linalojulikana kwa rangi yake kama njia nyeupe au "njia ya maziwa". Umbo lake linafanana na kisahani kikiwa na kipenyo cha miakanuru 100,000 na kikiwa na unene wa miakanuru 3,000.
20231101.sw_2449_3
https://sw.wikipedia.org/wiki/Galaksi
Galaksi
Kwenye kitovu cha galaksi graviti ni kubwa sana kiasa cha kwamba galaksi nyingi huaminiwa kuwa na shimo jeusi kituvoni.
20231101.sw_2449_4
https://sw.wikipedia.org/wiki/Galaksi
Galaksi
Galaksi zilizo karibu angani zinaitwa Mawingu ya Magellan ambayo ni galaksi mbili ndogo zilizopo kwenye umbali wa miakanuru 170,000 na 200,000. Galaksi kubwa ya jirani ni Andromeda na ina umbali wa miakanuru milioni 2.5.
20231101.sw_2449_5
https://sw.wikipedia.org/wiki/Galaksi
Galaksi
Idadi kamili ya galaksi zote angani haijulikani. Kuna makadirio ya kwamba idadi ya galaksi zinazoweza kuangaliwa kwa vyombo vinavyopatikana ni mabilioni. Hadi sasa sehemu ndogo tu imehesabiwa lakini mara kwa mara galaksi mpya zinatambuliwa kwa njia ya darubini au vyombo vya angani.
20231101.sw_2449_6
https://sw.wikipedia.org/wiki/Galaksi
Galaksi
Galaksi kati yao hujumuika pia zikiathiriana kwa njia ya graviti yao na kuzunguka kitovu cha graviti cha pamoja. Galaksi hadi 50 zinazoshikamana katika kipenyo cha miakanuru milioni 10 huitwa kundi la galaksi (ing. galaxy group). Kuna pia galaksi mamia hadi maelfu kadhaa zinazoshikamana na hii huitwa fundo la galaksi (ing. galaxy cluster) linaweza kuwa na kipenyo cha miakanuru milioni 10 - 20.
20231101.sw_2450_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/Moshi%20William
Moshi William
TX Moshi William (jina halisi: Shaban Ally Mhoja Kishiwa) alikuwa mmoja wa wanamuziki mahiri wa muziki wa dansi nchini Tanzania aliyeweza kurekodi albamu 13.
20231101.sw_2450_1
https://sw.wikipedia.org/wiki/Moshi%20William
Moshi William
Kwa miaka mitatu mfululizo (2003, 2004, 2005) Moshi William alitunukiwa tuzo ya kitaifa ya utunzi bora.
20231101.sw_2450_2
https://sw.wikipedia.org/wiki/Moshi%20William
Moshi William
Moshi William alijiunga na bendi kongwe nchini Tanzania Juwata Jazz Band mwaka 1982 akitokea Bendi ya Polisi Jazz.
20231101.sw_2450_3
https://sw.wikipedia.org/wiki/Moshi%20William
Moshi William
Mwanamuziki huyo alijipatia umarufu mkubwa kwa kutunga nyimbo zilizokuWa na mafunzo katika jamii: mfano wa nyimbo kama Ashibae, Mwaka wa Watoto, Msafiri Kakiri, Asha Mwanaseifu, Kaza Moyo, Ajuza, Ndoa Ndoano, Mwanamkiwa, AjaLi, Nyongo Mkaa na Ini, Isihaka Kibene, Harusi ya Kibene, Piga Ua Talaka Utatoa na nyimbo nyingine nyingi.
20231101.sw_2450_4
https://sw.wikipedia.org/wiki/Moshi%20William
Moshi William
Ukipita mitaa ya Keko Machungwa jijini Dar es Salaam sehemu alikokuwa anaishi mwanamuziki huyu lazima utasikia moja ya nyimbo zake zikipigwa katika klabu mbalimbali au kwenye majumba ya wenyeji. Pia katika miji mbalimbali ya Afrika Mashariki na kati mwanamuziki huyu alifananishwa sana na mwanamuziki Madilu System wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kutokana na staili yake ya uimbaji katika Bendi ya Msondo Ngoma na mtoto wake Hassan Moshi William.
20231101.sw_2452_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/Nyotamkia
Nyotamkia
Nyotamkia (kometi, pia nyota msafiri, shihabu, Kiing. comet) ni gimba dogo la angani linalozunguka Jua kwa njia ya duaradufu yenye sehemu kubwa mbali na Jua na sehemu ndogo karibu na Jua. Pale inapokaribia Jua inaotesha "mkia" unaoipa jina lake la "nyota yenye mkia". Mkia huu ni hasa mvuke unaong'aa kutokana na nuru inayoakisiwa.
20231101.sw_2452_1
https://sw.wikipedia.org/wiki/Nyotamkia
Nyotamkia
Mwili wa nyotamkia ni mchanganyiko wa mawe, vumbi na barafu. Nyotamkia hutokea katika sehemu za mbali za mfumo wa Jua, ng'ambo ya obiti ya Uranus, katika Wingu la Oort. Ukubwa hauzidi kipenyo cha kilomita kadhaa zikiwa na maumbo tofauti tofauti. Muda mwingi nyotamkia iko mbali na Jua pengine haionekani kwa darubini. Ikifuata njia ya mzunguko na kukaribia Jua kiasi cha kutosha inaanza kuonekana kama nyota ikiakisi nuru ya Jua. Ikikaribia Jua zaidi sehemu ya barafu yake inaanza kuyeyuka kuwa mvuke na mvuke huu ni kama angahewa ya muda. Sehemu nyingine ya mvuke huachana na nyotamkia yenyewe na kuonekana kama "mkia". Mkia huu unaelekea kila wakati upande usio wa Jua kwa sababu upepo wa Jua unasukuma mvuke upande ule.
20231101.sw_2452_2
https://sw.wikipedia.org/wiki/Nyotamkia
Nyotamkia
Kati ya nyotamkia ni chache tu zinazokaribia kiasi cha kutosha hadi zinaonekana kuwa na mkia kwa macho tu kwa muda wa wiki hadi miezi kadhaa. Zamani ziliaminiwa kuwa ishara kutoka mbinguni au kutoka kwa Mungu zikisababisha wasiwasi na hofu.
20231101.sw_2452_3
https://sw.wikipedia.org/wiki/Nyotamkia
Nyotamkia
Kataka tamaduni nyingi za dunia Nyotamkia zilitazamiwa kama tukio nje ya utaratibu wa kawaida na hivyo kama ishara ya balaa fulani inayokaribia. Tangu karne ya 16 Nyotamkia zimetambuliwa kuwa magimba yanayorudi baada ya muda fulani. Mara ya kwanza nyotamkia ya Halley ilitambuliwa na Mwingereza Edmond Halley mwaka 1705 ya kuwa inarudi. Halley alitambua ya kwamba nyotamkia aliyoiona mwaka 1705 ilikuwa ileile iliyowahi kuonekana mwaka 1682. Alitabiri ya kwamba nyotamkia hii itaonekana tena mwaka 1759 ikawa hivyo. Nyotamkia hii iliyopewa jina la "Halley" imeendelea kurudi kila baada ya miaka 76. Wanahistoria waliweza kuthibitisha ya kwamba taarifa mbalimbali katika historia kuhusu nyotamkia tangu mwaka 240 BK ziliihusu "Halley". Ilipoonekana mwaka 1985/1986 nuru yake ilikuwa imepungua kulingana na ziara za awali kutokana na kupungua kwa maada yake iliyopotea katika "mkia".
20231101.sw_2452_4
https://sw.wikipedia.org/wiki/Nyotamkia
Nyotamkia
Leo kuna nyotamkia takriban 170 zilizothibitishwa ya kuwa zimerudi. Kuna pia nyotamkia chache zilizoonekana kwa darubini jinsi zilivyopasuka na kuisha wakati wa kupita karibu na Jua.
20231101.sw_2452_5
https://sw.wikipedia.org/wiki/Nyotamkia
Nyotamkia
Kutokana na habari hizo zote wataalamu hufikiri ya kwamba kuna nyotamkia nyingi katika mfumo wa Jua letu lakini idadi inaendelea kupungua polepole zikikwisha kutokana na kupungua kwa maada au kukaribia mno Jua au hata kugongana na magimba mengine. Haiwezekani kujua idadi kwa sababu muda wa kuzunguka Jua ambao ni sawa na muda wa kuonekana tena unaweza kuwa miaka mamia, hivyo nyingine hazikuonekana bado tangu mwanzo wa astronomia ya kisayansi.
20231101.sw_2452_6
https://sw.wikipedia.org/wiki/Nyotamkia
Nyotamkia
Tarehe 11 Novemba 2014 kifaa cha kutua(lander) ya chomboanga Rosetta ilitua juu ya nyotamkia Churyumov–Gerasimenko baada ya safari ya miaka 10 (zaidi ya kilometa bilioni 6). Ndiyo mara ya kwanza ya chombo kilichotengenezwa na binadamu kutua juu ya nyotamkia yoyote.
20231101.sw_2455_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/Dedan%20Kimathi
Dedan Kimathi
Dedan Kimathi (Thenge, tarafa ya Tetu, kaunti ya Nyeri, 31 Oktoba 1920 - 18 Februari 1957) alikuwa Mkenya aliyeongoza harakati za kundi la Mau Mau za kutwaa ardhi iliyokuwa iko mikononi mwa wakoloni toka Uingereza.
20231101.sw_2455_1
https://sw.wikipedia.org/wiki/Dedan%20Kimathi
Dedan Kimathi
Kimathi alihukumiwa na kunyongwa kutokana na harakati zake za kuikomboa nchi ya Kenya. Serikali ya wakoloni Waingereza ilimchukua Kimathi kama gaidi, lakini wananchi wengi wa kabila la Gikuyu walimchukua kama mpigania uhuru.
20231101.sw_2455_2
https://sw.wikipedia.org/wiki/Dedan%20Kimathi
Dedan Kimathi
Alipofika miaka kumi na mitano, Kimathi alijiunga na shule ya msingi, Karuna-ini, ambapo aliweza kujifunza kiingereza halisi. Hii baadaye ilimsaidia kuandika kwa kiingereza kabla ya mnyanyuko na wakati wa mnyanyuko wa Mau mau. Akiwa shuleni alijiunga kwa chama cha ushauri. Alikua muumini wa dini na alibeba Bibilia kila wakati. Alifanyia kazi idara ya misitu kuokota begu za miti, ili aweze kujilipia gharama ya shule. Baadaye akajiunga na shule ya upili ya Tumutumu CSM, lakini akaacha shule kwa sababu ya kutolipa gharama ya shule.
20231101.sw_2455_3
https://sw.wikipedia.org/wiki/Dedan%20Kimathi
Dedan Kimathi
Kimathi alifanya kazi kadhaa lakini hakupata msimamo. Mojawapo ya kazi hizo alijiunga na jeshi na kutumwa kwa Vita Kuu ya Pili ya Dunia mwaka wa 1941. Lakini, mwaka wa 1944, alifukuzwa jeshi kwa sababu ya makosa kadhaa. Mnamo 1946, alijiandikisha kwa chama cha Muungano wa Waafrika Wakenya. Mnamo 1949, alianza kufunza shule alikosomea, lakini wakamfukuza kazi kwa sababu ya kulaumiwa amefanya ubakaji. La kuaminika ni kwamba alipigwa kalamu kwa makosa ya uchochezi.
20231101.sw_2455_4
https://sw.wikipedia.org/wiki/Dedan%20Kimathi
Dedan Kimathi
Kimathi aliweza kuvutia watu kwa kuonyesha bidii kwa kazi aina zote, alizoweza kufanya. Kimathi alianza siasa za upinduzi mwaka wa 1950. Alianza kuwa mfuasi wa Mau Mau, na baadaye kupanda cheo na kuweza kuwapa wajiunga wapya kiapo cha Mau Mau na kwa hivyo akawa gaidi kulingana na Waingereza. Alijiunga tena na Kikundi ya Arubaini, wakombozi wa Chama cha Kati cha Wakikuyu mwaka wa 1951. Alichaguliwa kama karani kwa chama cha KAU eneo la Ol' Kalou na eneo la Thomson Falls mwaka wa 1952. Alishikwa kwa mmda mwaka huo, lakini akatoroka kwa usaidizi wa polisi wa kijiji. Hii ilileta mwanzo wa Vita vya ukereketwa halisi. Kimathi aliunda baraza la ulinzi wa Kenya, ambayo ilitoa amri kwa wapiganaji wote msituni mwaka wa 1953.
20231101.sw_2455_5
https://sw.wikipedia.org/wiki/Dedan%20Kimathi
Dedan Kimathi
Mwaka wa 1956, alishikwa pamoja na bibi yake mmoja, Wambui. (hadithi nyingi za Kimathi zaeleza vile alivyopigwa risasi.) Alihukumiwa kifo na mahakama, na Jaji wa sheria Chifu Kenneth O'Connor, akiwa bado kitandani katika hospitali kuu ya Nyeri. Asubuhi na mapema mnamo 18 Februari 1957 alinyogwa na serikali ya wakoloni Waingereza.
20231101.sw_2455_6
https://sw.wikipedia.org/wiki/Dedan%20Kimathi
Dedan Kimathi
Kimathi alizikwa kwenye kaburi la umma mahali pasipojulikana katika gereza la Kamiti. Serikali ya Uingereza mpaka sasa inapinga maiti ya Kimathi ifukuliwe ili azikwe tena kirasmi, kwasababu wanasema alikuwa gaidi. Lakini Wakenya wengi wamchukulia kuwa Shujaa wa Taifa. Jina la Kimathi linakumbukwa nchini Kenya hasa kutokana na mitaa ya miji, majengo mengi na pia barabara ambazo zimeitwa kwa jina lake.
20231101.sw_2455_7
https://sw.wikipedia.org/wiki/Dedan%20Kimathi
Dedan Kimathi
Mchezo wa Kuigiza wa "Mzalendo Kimathi" ama kwa kiingereza The Trial of Dedan Kimathi umeandikwa na Ngugi wa Thiong'o (ndugu wa shujaa wa Mau Mau) akishirikiana na Micere Mugo na mchezo huo unaeleza kisa cha Kimathi.
20231101.sw_2456_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/Fasihi%20simulizi
Fasihi simulizi
Fasihi simulizi ni kazi ya sanaa inayotumia mdomo (tofauti na maandishi kama kwenye fasihi andishi) kama njia kuu ya kufikisha ujumbe. Ni sehemu ya msingi ya utamaduni na vipengele vyake vingi vinafanya kazi kama katika fasihi kwa jumla.
20231101.sw_2456_1
https://sw.wikipedia.org/wiki/Fasihi%20simulizi
Fasihi simulizi
Katika jamii isiyo na uandishi ni wazi kuwa hakuna fasihi andishi. Hata hivyo kila jamii ina hazina ya mapokeo yapokelewayo Kwa mdomo na kihifadhiwa katika maandishi kwa mfano: utenzi, ngano au nyimbo za jadi. Hivyo vyote ni sehemu za fasihi simulizi.
20231101.sw_2456_2
https://sw.wikipedia.org/wiki/Fasihi%20simulizi
Fasihi simulizi
Hata jamii ijuayo kusoma na kuandika inaendelea kuwa na fasihi simulizi, hasa nyumbani, k.m. katika kuwasimulia watoto hadithi. Lakini mara nyingi fasihi simulizi ya jamii ijuayo kusoma na kuandika ni tofauti sana na fasihi simulizi ya jamii isiyo na uandishi, kwa vile imeathiriwa na ujuzi wa kusoma na kuandika, na mitindo ya masimulizi yake hayaendi sambamba na mitindo ya masimulizi yasiyoathiriwa na uandishi.
20231101.sw_2456_3
https://sw.wikipedia.org/wiki/Fasihi%20simulizi
Fasihi simulizi
Fasihi simulizi ina sifa za kipekee ambazo huipambanua na fasihi andishi. Sifa hizo ndizo huipa uhai fasihi hii. Miongoni mwa sifa hizo ni pamoja na:
20231101.sw_2456_4
https://sw.wikipedia.org/wiki/Fasihi%20simulizi
Fasihi simulizi
Fanani kuwepo kwa fanani ambaye husimulia, huimba, hupiga makofi na kubadilisha miondoko na mitindo ya usimuliaji.
20231101.sw_2456_5
https://sw.wikipedia.org/wiki/Fasihi%20simulizi
Fasihi simulizi
Hadhira kuwepo kwa hadhira ambayo hushiriki kwa kuuliza maswali, kupiga makofi, kushangilia, kuimba, kuiga na kadhalika - kutegemea jinsi ambavyo fanani atawashirikisha.
20231101.sw_2456_6
https://sw.wikipedia.org/wiki/Fasihi%20simulizi
Fasihi simulizi
Fasihi simulizi huingiliana na mabadiliko ya kiwakati na kimazingira; baadhi ya tanzu au vipera vya fasihi simulizi vinaweza kuwa vimepitwa na wakati lakini bado vinaweza kubadilishwa na vikaafikiana na wakati mahususi.
20231101.sw_2456_7
https://sw.wikipedia.org/wiki/Fasihi%20simulizi
Fasihi simulizi
Fasihi simulizi ni mali ya jamii nzima, humilikiwa na kila mtu katika jamii. Sifa hii ndiyo huipa uwezo wa kurithishwa kutoka kizazi kimoja hadi kingine.
20231101.sw_2456_8
https://sw.wikipedia.org/wiki/Fasihi%20simulizi
Fasihi simulizi
Fasihi simulizi huzaliwa, hukua na hata hufa. Kuzaliwa: fasihi simulizi huzaliwa kutokana na mambo yanayotokea katika jamii. Kukua: fasihi simulizi hukua kadri inavyojadili matatizo yanayojitokeza. Kufa: fasihi simulizi hufa kwa namna mbili. Hii ni kutokana na maendeleo ya mazingira ambayo hufuata mfumo wa jamii husika. Kwa mfano kutokana na maendeleo ya sayansi na teknolojia fasihi inaweza kuhifadhiwa kwenye maandishi na kwenye kanda mbalimbali za kurekodi.
20231101.sw_2456_9
https://sw.wikipedia.org/wiki/Fasihi%20simulizi
Fasihi simulizi
Fasihi simulizi ina mandhari maalumu ya kutendea; ni sehemu ambayo imetengwa rasmi kwa ajili ya aina/kipera fulani cha fasihi simulizi. Mandhari hayo yanaweza kuwa porini, misituni, mtoni, pangoni, nyumbani na kadhalika.
20231101.sw_2456_10
https://sw.wikipedia.org/wiki/Fasihi%20simulizi
Fasihi simulizi
Fasihi simulizi ina sifa ya "kuwa na utegemezi".Utegemezi wa fasihi simulizi hutegemea zaidi sanaa za maonesho hasa sanaa za ghibu yaani muziki,kwa sababu,fasihi simulizi huchota uhai wake kutokana na vitendo na tabia za fanani,mahadhi na toni za kimuziki na vipengele vingine vya sanaa za maonesho.
20231101.sw_2456_11
https://sw.wikipedia.org/wiki/Fasihi%20simulizi
Fasihi simulizi
Masimulizi ni fasihi yenye kusimulia habari fulani. Ni masimulizi ambayo yanatumia lugha ya mjazo au nathari na mtiririko wake huwa mwepesi au sahili. Urefu wa hadithi hutofautiana kutoka kitanzu/kipera kimoja hadi kingine. Kwa jumla zipo hadithi ambazo ni za kubuni na zingine za kihistoria.
20231101.sw_2456_12
https://sw.wikipedia.org/wiki/Fasihi%20simulizi
Fasihi simulizi
Hizi ni hadithi za kimapokeo zitumiazo wahusika kama wanyama, miti na watu katika kuelezea au kuonya kuhusu maisha. Vijipera vya kipera hiki ni:
20231101.sw_2456_13
https://sw.wikipedia.org/wiki/Fasihi%20simulizi
Fasihi simulizi
Ni hadithi ndogo ndogo zinazohusisha utani na ucheshi kwa kiasi fulani. Hizi ni hadithi ambazo hutambwa katika mtiririko wa matukio ambao huzua kicheko. Soga hudhamiria kuchekesha na pia kukejeli.
20231101.sw_2456_14
https://sw.wikipedia.org/wiki/Fasihi%20simulizi
Fasihi simulizi
Masimulizi ya kimapokeo juu ya wahenga au mashujaa wa kabila au taifa yenye kuchanganya chuku na historia. Kwa mfano hadithi za Liyongo.
20231101.sw_2456_15
https://sw.wikipedia.org/wiki/Fasihi%20simulizi
Fasihi simulizi
Hizi ni hadithi ambazo husimulia au zimejengwa kwenye matukio ya kihistoria. Inawezekana matukio yanayosimuliwa yakawa ya kweli, yaani yalipata kutokea kihistoria. Hadithi hizi hutokea zaidi katika maandishi.
20231101.sw_2456_16
https://sw.wikipedia.org/wiki/Fasihi%20simulizi
Fasihi simulizi
Ni utanzu unaofungamana na imani za dini na mizungu ya jamii. Hizi ni hadithi za kale zenye kuwakilisha imani na mtazamo wa jamii inayohusika kuhusu asili ya ulimwengu na mwenendo wake, kuhusu asili yao wenyewe, na maana na shabaha ya maisha yao. Mara nyingi hadithi hizi huaminiwa kuwa ni kweli tupu, na hutumika kuelezea au kuhalalisha baadhi ya mila na madhehebu ya jamii inayohusika.
20231101.sw_2456_17
https://sw.wikipedia.org/wiki/Fasihi%20simulizi
Fasihi simulizi
Huu ni utanzu wa fasihi simulizi unaowasilishwa kwa hadhira kwa njia ya uimbaji au ughani badala ya usemaji wa kawaida. Katika utanzu huu kuna vipera viwili ambavyo ni nyimbo na maghani.
20231101.sw_2456_18
https://sw.wikipedia.org/wiki/Fasihi%20simulizi
Fasihi simulizi
Nyimbo ni kila kinachoimbwa. Kipera hiki kimegawanyika katika vijipera vifuatavyo ambavyo ni, tumbuizo, bembea, kongozi, nyimbo za dini, wawe, tenzi, tendi, mbolezi, kimai, nyiso, nyimbo za vita, nyimbo za uwindaji, nyimbo za taifa.
20231101.sw_2456_19
https://sw.wikipedia.org/wiki/Fasihi%20simulizi
Fasihi simulizi
Maghani ni istilahi inayotumiwa kuelezea aina ya ushairi ambao hutolewa kwa kalima au maneno badala ya kuimbwa. Kipera hiki kina vijipera vitatu ambavyo ni maghani ya kawaida, sifo na maghani masimulizi.
20231101.sw_2456_20
https://sw.wikipedia.org/wiki/Fasihi%20simulizi
Fasihi simulizi
Hilo ni kundi ambalo tunaweza kuingiza fani mbalimbali za ushahiri simulizi kama vile ushairi wa mapenzi, siasa, maombolezo, kazi, dini ilimradi unaghanwa katika namna ya uwasilishwaji wake.
20231101.sw_2456_21
https://sw.wikipedia.org/wiki/Fasihi%20simulizi
Fasihi simulizi
Hizi ni tungo za kusifu ambazo husifu watu, wanyama na mimea. Baadhi ya sifo huwa zinakashifu au kukejeli. Sifo huwa na tanzu muhimu kama vile vivugo (majigambo), pembezi na tondozi.
20231101.sw_2456_22
https://sw.wikipedia.org/wiki/Fasihi%20simulizi
Fasihi simulizi
Semi ni tungo au kauli fupifupi za kisanaa zitumiazo picha na tamathali kuelezea maudhui yanayobeba maana au mafunzo muhimu kwa jamii. Kundi hili lina vipera au tanzu sita ambazo ni:
20231101.sw_2456_23
https://sw.wikipedia.org/wiki/Fasihi%20simulizi
Fasihi simulizi
Methali ni semi fupi fupi zenye mpangilio maalumu wa maneno ambazo huelezea kwa muhtasari mafunzo, mafumbo na mawazo mazito yaliyotokana na uzoefu wa kijamii. Mara nyingi mawazo hayo huelezwa kwa kutumia tamathali hasa sitiari na mafumbo.
20231101.sw_2456_24
https://sw.wikipedia.org/wiki/Fasihi%20simulizi
Fasihi simulizi
Methali nyingi huundwa na vipande viwili vya maneno vyenye fikra yurani. Kipande cha kwanza huashiria tendo au sharti na kipande cha pili huashiria matokeo ya tendo au sharti hilo. Au sehemu ya kwanza huanzisha wazo fulani, na sehemu ya pili hulikanusha au kulikamilisha wazo hilo. Kwa mfano; mwenda pole hajikwai, aliye juu mngoje chini.
20231101.sw_2456_25
https://sw.wikipedia.org/wiki/Fasihi%20simulizi
Fasihi simulizi
Ni semi zilizofumbwa ambazo hutolewa kwa hadhira ili izifumbue. Fumbo hilo kwa kawaida huwa linafahamika katika jamii hiyo, na mara nyingi lina mafunzo muhimu kwa washiriki, mbali na kuwachemsha bongo zao. Vitendawili ni sanaa inayotegemea uwezo wa mtu kutambua, kuhusisha na kulinganisha vitu vya aina mbalimbali vilivyomo katika maumbile.
20231101.sw_2456_26
https://sw.wikipedia.org/wiki/Fasihi%20simulizi
Fasihi simulizi
Ni semi za muda na mahali maalum ambazo huzuka na kutoweka kutegemea mazingira maalum. Msimu ukipata mashiko ya kutosha katika jamii huweza hatimaye kuingia katika kundi la methali za jamii hiyo.
20231101.sw_2456_27
https://sw.wikipedia.org/wiki/Fasihi%20simulizi
Fasihi simulizi
Ni semi za maonyo au mawaidha ambazo maana zake za ndani zimefichika. Fumbo hubuniwa na msemaji kwa shabaha na hadhira maalum, hivyo ni tofauti na methali au vitendawili ambavyo ni semi za kimapokeo.
20231101.sw_2456_28
https://sw.wikipedia.org/wiki/Fasihi%20simulizi
Fasihi simulizi
Haya ni majina ya kupanga ambayo baadhi ya watu hupewa au hujipatia kutokana na sifa zao za kimwili, kinasaba, kitabia au kimatendo. Majina haya huwa ni maneno au mafungu ya maneno yenye maana iliyofumbwa. Mara nyingi majina haya huwa ni sitiari. Baadhi ya majina haya humsifia mhusika, lakini mengine humkosoa au hata kumdhalilisha; Mifano: simba wa yuda- Hali Selassie, Baba wa taifa – Mwl Nyerere.
20231101.sw_2456_29
https://sw.wikipedia.org/wiki/Fasihi%20simulizi
Fasihi simulizi
Ni maonesho au maigizo ambayo hutumia watendaji na mazingira maalumu kwa kuiga tabia na matendo ya watu au viumbe wengine ili kuburudisha na kutoa ujumbe fulani kwa hadhira.
20231101.sw_2458_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/Bujumbura
Bujumbura
Bujumbura, ni mji mkuu wa Burundi unaokadiriwa kuwa na idadi ya wakazi 300,000. Mji upo kaskazini mashariki mwa Ziwa Tanganyika, na ni mji mkubwa zaidi Burundi, kitovu cha mawasiliano na uchumi nchini humo.
20231101.sw_2458_1
https://sw.wikipedia.org/wiki/Bujumbura
Bujumbura
Bujumbura ni mji pekee Burundi ambao una bandari ya kupakia mali na bidhaa mbalimbali za kuuza nje, kama vile kahawa, pamba, ngozi na madini ya stani.
20231101.sw_2458_2
https://sw.wikipedia.org/wiki/Bujumbura
Bujumbura
Bujumbura ilipanuka toka ilipokuwa kijiji kidogo kilichokuwa kambi ya Jeshi ya Wajerumani. Eneo hili lilikuwa sehemu ya Afrika ya Mashariki ya Kijerumani mwaka wa 1889.
20231101.sw_2458_3
https://sw.wikipedia.org/wiki/Bujumbura
Bujumbura
Lakini, baada ya Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia, Bujumbura ilichukuliwa na Ubeljiji ambapo Shirikisho la Mataifa ilisimamia Ruanda-Urundi. Jina la mji likabadilishwa kutoka Usumbura hadi Bujumbura. Burundi ilipopata uhuru, mwaka wa 1962.
20231101.sw_2458_4
https://sw.wikipedia.org/wiki/Bujumbura
Bujumbura
Bujumbura ni mji ambao umeshuhudia vita vya ukabila kati ya Wahutu na Watutsi kwa kung'ang'ania uongozi wa Burundi.
20231101.sw_2458_5
https://sw.wikipedia.org/wiki/Bujumbura
Bujumbura
Katika mji huo kuna majengo ni yale ya kikoloni na pia kuna soko, uwanja wa taifa, msikiti mkubwa na Kanisa kuu. Pia kuna Jumba la Makumbusho ambalo linaitwa jumba la makumbusho ya maisha na jumba la makumbusho ya jiologia.
20231101.sw_2458_6
https://sw.wikipedia.org/wiki/Bujumbura
Bujumbura
Mambo mengine ya kuchangamsha ni kama Hifadhi ya Rusizi, na Kiamba hapo Mugere, ambapo panasemekana kwamba David Livingstone na Henry Stanley walikutana. (Lakini watu wengi wasema walikutana Ujiji), Kigoma, nchini Tanzania ambapo panasemekana ni mwanzo wa mto unaosemekana kuwa ndio mwanzo wa Mto Nile).
20231101.sw_2459_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/Maumau
Maumau
Maumau lilikuwa kundi la wapiganaji wa Kenya waliokuwa wakipinga utawala wa kikoloni wa Waingereza toka mwaka 1952 hadi 1960.
20231101.sw_2459_1
https://sw.wikipedia.org/wiki/Maumau
Maumau
Kundi lilianzishwa mwaka wa 1946, na viongozi wa hao mashujaa walikuwa Jomo Kenyatta, Jaramogi Oginga Odinga, Paul Ngei, Ronald Ngala, Harry Thuku na wengineo.
20231101.sw_2459_2
https://sw.wikipedia.org/wiki/Maumau
Maumau
Walifanya kazi nzuri sana, kwanza juu ya kuonyesha vile watu wanavyoweza kufika mbali wakiwa kitu kimoja. Kama haingekuwa kwa maungano hawangeweza kufanya chochote.
20231101.sw_2459_3
https://sw.wikipedia.org/wiki/Maumau
Maumau
Ingawa vuguvugu la Maumau halikuwa na mafanikio makubwa kijeshi, upinzani wao ulichangia sana katika kuharakisha upatikanaji wa uhuru wa Kenya mwaka 1963.
20231101.sw_2459_4
https://sw.wikipedia.org/wiki/Maumau
Maumau
Chanzo cha jina la kundi hili, Maumau, hakieleweki vyema. Kuna hali ya kutokukubaliana juu ya chanzo na maana ya jina lenyewe. Baadhi wanadai kuwa ni jina la vilima fulani huko Kenya, wengine wanaamini kuwa jina hilo lilitoka kwa walowezi wa Kiingereza lililokuwa na nia ya kudhalilisha kundi hilo. Wako pia wanaosema kuwa jina hilo ni kifupi cha: Mzungu Aende Ulaya, Mwafrika Apate Uhuru.
20231101.sw_2459_5
https://sw.wikipedia.org/wiki/Maumau
Maumau
Sehemu kubwa ya kundi la Maumau iliundwa na watu wa kabila la Gikuyu huku kukiwa na baadhi ya wanachama toka Embu na Meru. Wagikuyu wenyewe hawakuwa wakiliita kundi hili Maumau bali "Muingi" (vuguvugu), "Muigwithania" (anayeunganisha), "Muma wa Uiguano" (kiapo cha umoja) au KCA (Kenya Central Association, chama kilichotangulia kupigania haki za Wakikuyu.
20231101.sw_2460_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/Bonde%20la%20Ufa
Bonde la Ufa
Bonde la Ufa kwenye fani ya jiolojia ni bonde ambalo limetokana na mwendo wa mabamba ya gandunia mahali yanapoachana.
20231101.sw_2460_1
https://sw.wikipedia.org/wiki/Bonde%20la%20Ufa
Bonde la Ufa
Mabonde ya ufa hutokana na mvutano wa tektoniki. Mwendo huu huleta utengano wa mabamba hayo. Bonde la ufa latokea kama mabamba ya gandunia huachana na kuacha nafasi.
20231101.sw_2462_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/Vita%20Kuu%20ya%20Dunia
Vita Kuu ya Dunia
Vita Kuu ya Dunia ni jina linalotumika kwa ajili ya vita inayohusu nchi nyingi katika sehemu mbalimbali za dunia badala ya eneo la nchi kadhaa pekee.
20231101.sw_2462_1
https://sw.wikipedia.org/wiki/Vita%20Kuu%20ya%20Dunia
Vita Kuu ya Dunia
Kwa kawaida vita mbili za karne ya 20 huitwa "Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia" (1914-1918) na "Vita Kuu ya Pili ya Dunia" (1939-1945).
20231101.sw_2462_2
https://sw.wikipedia.org/wiki/Vita%20Kuu%20ya%20Dunia
Vita Kuu ya Dunia
Jina hilo limepatikana tangu mwanzo wa karne ya 20 katika miaka kabla ya Vita Kuu ya Kwanza ilipoonekana ya kwamba vita ikianzishwa itahusu sehemu kubwa ya dunia kutokana na mapatano kati ya mataifa makubwa ya Ulaya yaliyotawala nchi nyingi duniani chini ya mfumo wa ukoloni.
20231101.sw_2462_3
https://sw.wikipedia.org/wiki/Vita%20Kuu%20ya%20Dunia
Vita Kuu ya Dunia
Wanahistoria wengine hudai ya kwamba hali halisi vita kuu ya kwanza ilizohusu dunia yote ilikuwa vita ya miaka saba (1756-1763) kati ya Uingereza na madola ya Kijerumani ya Uprusi na Hannover dhidi ya Ufaransa, Urusi, Austria, Uswidi, Saksonia na Hispania. Mapigano yalitokea Ulaya, Amerika ya Kaskazini, Visiwa vya Karibi, India, Asia ya Mashariki, Afrika na baharini kote duniani.