_id
stringlengths 15
22
| url
stringlengths 31
150
| title
stringlengths 1
86
| text
stringlengths 100
23.8k
|
---|---|---|---|
20231101.sw_2375_0
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Chuo%20Kikuu%20cha%20Makerere
|
Chuo Kikuu cha Makerere
|
Chuo Kikuu cha Makerere ni chuo kikuu cha kwanza cha Afrika ya Mashariki na chuo kikuu kikubwa cha Uganda.
|
20231101.sw_2375_1
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Chuo%20Kikuu%20cha%20Makerere
|
Chuo Kikuu cha Makerere
|
Kimeanzishwa wakati wa ukoloni mwaka 1922 kama shule ya ufundi kwa wanafunzi 14. Kozi za kwanza zilikuwa pamoja na useremala, ujenzi na umekanika.
|
20231101.sw_2375_2
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Chuo%20Kikuu%20cha%20Makerere
|
Chuo Kikuu cha Makerere
|
Mwaka 1949 Makerere ikawa chuo kishiriki cha Chuo Kikuu cha London kikitoa shahada ya kwanza ya ngazi ya chuo kikuu.
|
20231101.sw_2375_3
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Chuo%20Kikuu%20cha%20Makerere
|
Chuo Kikuu cha Makerere
|
Mwaka 1963 ikawa sehemu ya Chuo Kikuu cha Afrika ya Mashariki pamoja na kampasi za Dar es Salaam na Nairobi.
|
20231101.sw_2375_4
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Chuo%20Kikuu%20cha%20Makerere
|
Chuo Kikuu cha Makerere
|
Chuo Kikuu cha Afrika ya Mashariki kimegawiwa mwaka 1970 kutokana na kufifia kwa Jumuiya ya Afrika ya Mashariki. Makerere ikawa Chuo Kikuu cha kitaifa cha Uganda.
|
20231101.sw_2375_5
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Chuo%20Kikuu%20cha%20Makerere
|
Chuo Kikuu cha Makerere
|
Makerere ilikuwa chuo waliposoma viongozi wengi wa Afrika, wakiwa pamoja na marais wa zamani Milton Obote (Uganda), Julius Nyerere na Benjamin Mkapa (Tanzania) na Mwai Kibaki (Kenya).
|
20231101.sw_2375_6
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Chuo%20Kikuu%20cha%20Makerere
|
Chuo Kikuu cha Makerere
|
Baada ya uhuru Makerere ilikuwa pia mahali pa majadiliano na mafunzo ya utamaduni wa Kiafrika. Waandishi na walimu muhimu wa Kiafrika walianzisha mafunzo yao au walifundisha kwa muda fulani Makerere kama vile Nuruddin Farrah, Ali Mazrui, David Rubadiri, Okello Oculi, Ngugi wa Thiongo, John Ruganda, Paul Theroux na Peter Nazareth.
|
20231101.sw_2375_7
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Chuo%20Kikuu%20cha%20Makerere
|
Chuo Kikuu cha Makerere
|
Makerere ina idara 22 zinazohudumia wanafunzi 30,000 hivi, wakiwemo 3,000 wa kozi za shahada za ngazi ya juu.
|
20231101.sw_2377_0
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ngugi%20wa%20Thiongo
|
Ngugi wa Thiongo
|
Ngũgĩ wa Thiong'o (amezaliwa 5 Januari 1938) ni mwandishi Mkenya aliyeandika kwa Kiingereza lakini siku hizi anatumia lugha ya Gikuyu.
|
20231101.sw_2377_1
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ngugi%20wa%20Thiongo
|
Ngugi wa Thiongo
|
Maandishi yake ni pamoja na riwaya, tamthilia, hekaya, insha na uhakiki. Ameanzisha gazeti la lugha ya Gikuyu Mũtiiri.
|
20231101.sw_2377_2
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ngugi%20wa%20Thiongo
|
Ngugi wa Thiongo
|
Tangu mwaka 1982 ameishi nje ya Kenya akifundisha kwenye vyuo vikuu mbalimbali kama Yale, New York na Irvine/California.
|
20231101.sw_2377_3
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ngugi%20wa%20Thiongo
|
Ngugi wa Thiongo
|
Ngugi amezaliwa Kenya katika kijiji cha Kamiriithu karibu na Limuru, wilaya ya Kiambu katika jamii ya Wagikuyu akabatizwa James Ngugi. Alikuwa mtoto wa tano wa mke wa tatu wa baba yake Thiong'o wa Nducu. Baba alikuwa mkulima aliyepotea shamba lake kutokana na Waingereza kuteka na kutwaa Nyanda za Juu za Kenya. James alisoma shule za wamisionari za Kamaandura (Limuru), Karinga (Mangu) na Alliance High School (Kikuyu). Katika miaka ile akawa Mkristo. Wakati alikisoma shule familia yake iliathiriwa na vita ya Maumau ikawa kaka yake aliuawa na mama yake aliteswa.
|
20231101.sw_2377_4
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ngugi%20wa%20Thiongo
|
Ngugi wa Thiongo
|
Baada ya kumaliza Alliance High akasoma Makerere akahitimu kupata digrii ya Kiingereza mwaka 1963. Akafunga ndoa na Nyambura mwaka 1961 akazaa naye watoto sita katika miaka iliyofuata. Mwaka 1962 aliandika tamthilia yake ya kwanza "The Black Hermit". Baada ya digrii alirudi Nairobi alipofanya kazi ya uandishi wa gazeti.
|
20231101.sw_2377_5
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ngugi%20wa%20Thiongo
|
Ngugi wa Thiongo
|
1964 akachukua nafasi ya masomo huko Chuo Kikuu cha Leeds. Hapo Uingereza alitunga riwaya ya "WEEP NOT, CHILD" (1964) akiwa mwandishi wa kwanza kutoka Afrika ya Mashariki aliyetunga riwaya kwa Kiingereza. Alisimulia hadithi ya kijana Njoroge mwenye ndoto ya kuendeleza elimu yake lakini anakwama kati ya ndoto zake na hali halisi ya maisha ya Kiafrika chini ya ukoloni.
|
20231101.sw_2377_6
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ngugi%20wa%20Thiongo
|
Ngugi wa Thiongo
|
Aliendelea kwa "THE RIVER BETWEEN" (1965) akichora picha ya kijiji kilichopasuliwa kati ya wakristo na wafuasi wa dini ya asili.
|
20231101.sw_2377_7
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ngugi%20wa%20Thiongo
|
Ngugi wa Thiongo
|
1967 alitumia historia ya vita ya Maumau na maarifa ya familia yake kwa ajili ya riwaya ya "A GRAIN OF WHEAT".
|
20231101.sw_2377_8
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ngugi%20wa%20Thiongo
|
Ngugi wa Thiongo
|
Mwaka uleule baada ya kuchukua digrii ya pili alirudi Kenya akifundisha Chuo Kikuu cha Nairobi 1967-1969. Aliondoka kwa sababu alipinga kuingia kwa siasa ya serikali katika mambo ya chuo. Baada ya mwaka moja huko Makerere alipata nafasi ya kufundisha Marekani kwenye Chuo Kikuu cha Evanston (1970-71).
|
20231101.sw_2377_9
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ngugi%20wa%20Thiongo
|
Ngugi wa Thiongo
|
Mwaka 2013 akatunukiwa Shahada ya Heshima ya Uzamivu na Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam (UDSM) nchini Tanzania.
|
20231101.sw_2377_10
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ngugi%20wa%20Thiongo
|
Ngugi wa Thiongo
|
1973 alirudi Nairobi kama Profesa wa Kiingereza na mwenyekiti wa idara ya fasihi. Idara hii ilianzishwa kutokana na upinzani wa Ngugi na wenzake dhidi ya hali ya Kiingereza kuwa nguzo kuu ya elimu katika Afrika. Katika makala 'On the Abolition of the English Department' aliyoandika 1968 pamoja na Taban lo Liyong na Henry Owuor-Anyumba, aliwahi kuuliza "Tukihitaji kutazama historia ya utamaduni mmoja kwa undani kwa ajili ya masomo yetu, kwa nini tusichague utamaduni mmoja wa Kiafrika na kuupa kipaumbele ili tulinganishe tamaduni mbalimbali nao?" Kutokana na msimamo huo aliendelea kutafiti fasihi ya simulizi ya makabila ya Kenya, hasa ya Wagikuyu na fasihi ya Kiswahili.
|
20231101.sw_2377_11
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ngugi%20wa%20Thiongo
|
Ngugi wa Thiongo
|
Katika miaka hii huko Nairobi Ngugi aliamua hawezi kuwa tena mkristo. Mwaka 1976 akabadilisha jina lake kutoka James Ngugi kuwa Ngugi wa Thiong'o.
|
20231101.sw_2377_12
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ngugi%20wa%20Thiongo
|
Ngugi wa Thiongo
|
Kazi yake ya kifasihi ilimpeleka katika mzozo na serikali. Kuanzia mwaka 1976 Ngugi alishirikiana na wanakijiji Wagikuyu karibu na Limuru kuanzisha maagizo ya tamthilia katika lugha yao. 1976 riwaya yake ya "PETALS OF BLOOD" ilichora picha ya watawala wapya Waafrika jinsi walivyochukua nafasi ya wakoloni wa awali wakidharau na kukandamiza wananchi. Mwaka uleule aliandika tamthilia ya "Ngaahika Ndeenda" (Nitaolewa nitakapopenda). Wakubwa katika serikali walikuwa na wasiwasi wakiogopa mwelekeo wa kimarxist wa Ngugi hasa alipotoka katika Chuo Kikuu na kuingia kati ya wananchi wa kawaida kwa njia ya maigizo yake katika lugha ya Gikuyu. Makamu wa Rais wa Kenya Moi aliamua kumkamata Ngugi kwa misingi ya sheria ya usalama wa kitaifa wakati Rais Jomo Kenyatta mwenyewe tayari alikuwa amedhoofika kutokana na uzee na ugonjwa.
|
20231101.sw_2377_13
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ngugi%20wa%20Thiongo
|
Ngugi wa Thiongo
|
Ngugi alikaa mwaka mmoja katika gereza la Kamiti akaandika riwaya ya kwanza kwa Gikuyu "Caitaani mũtharaba-Inĩ" (Shetani msalabani) akitumia karatasi ya choo. Baada ya kuachichwa huru hakuruhusiwa kurudi kazini kwenye Chuo Kikuu. Mwaka 1982 aliondoka Kenya kwenda London.
|
20231101.sw_2377_14
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ngugi%20wa%20Thiongo
|
Ngugi wa Thiongo
|
Ngugi ameendelea kutumia Gikuyu pekee kwa ajili ya riwaya lakini amefundisha na kutunga insha kwa Kiingereza. Kati ya maandiko yaliyofuata ni "Detained" (Daiari ya gerezani - 1981); "Decolonizing the Mind: The Politics of Language in African Literature" (Kuondoa ukoloni rohoni - siasa ya lugha katika fasihi ya Afrika 1986) alimodai waandishi Waafrika watumie lugha zao za kienyeji badala la lugha za Kiulaya; Matigari (1987) alimotumia hadithi ya kiutamaduni wa Gikuyu.
|
20231101.sw_2377_15
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ngugi%20wa%20Thiongo
|
Ngugi wa Thiongo
|
Mwaka 2004 Ngugi alirudi mara ya kwanza Kenya lakini alipata maarifa mabaya akishambuliwa na wahuni na kuibiwa mali mke wake akibakiwa. Shabaha muhmu wa ziara yake ilikuwa kutangaza riwaya yake mpya kwa Gikuyu "Muroogi wa Kigogo".
|
20231101.sw_2377_16
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ngugi%20wa%20Thiongo
|
Ngugi wa Thiongo
|
Kiini cha imani ya Ngugi ni ya kwamba kwa kutumia lugha za kienyeji pekee waandishi waafrika watafikia wanachi wa kawaida na kushinda ukoloni mamboleo rohoni. Tatizo alilo nalo hapo ni ya kwamba lugha za kienyeji zinarudi nyuma haraka katika mazingira ya kisasa hata zikiendelea kuzungumzwa na kusikilizwa kwa redio si lazima zinasomwa pia.
|
20231101.sw_2377_17
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ngugi%20wa%20Thiongo
|
Ngugi wa Thiongo
|
2012: National Book Critics Circle Award (finalist Autobiography) for In the House of the Interpreter
|
20231101.sw_2377_18
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ngugi%20wa%20Thiongo
|
Ngugi wa Thiongo
|
This Time Tomorrow (three plays, including the title play, "The Rebels", and "The Wound in the Heart") (c. 1970)
|
20231101.sw_2377_19
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ngugi%20wa%20Thiongo
|
Ngugi wa Thiongo
|
Ngaahika Ndeenda: Ithaako ria ngerekano (I Will Marry When I Want) (1977, 1982) (with Ngugi wa Mirii)
|
20231101.sw_2377_20
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ngugi%20wa%20Thiongo
|
Ngugi wa Thiongo
|
Penpoints, Gunpoints and Dreams: The Performance of Literature and Power in Post-Colonial Africa (The Clarendon Lectures in English Literature 1996), Oxford University Press, 1998.
|
20231101.sw_2377_21
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ngugi%20wa%20Thiongo
|
Ngugi wa Thiongo
|
Something Torn and New: An African Renaissance (2009) "Queries over Ngugi's appeal to save African languages, culture", Daily Nation, Lifestyle Magazine, 13 June 2009.
|
20231101.sw_2379_0
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kilwa%20Kivinje
|
Kilwa Kivinje
|
Kilwa Kivinje ni mji mdogo katika Wilaya ya Kilwa ufukoni wa Bahari Hindi. Kiutawala ni sehemu ya kata ya Kivinje Singino.
|
20231101.sw_2379_1
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kilwa%20Kivinje
|
Kilwa Kivinje
|
Wakati wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, mji ulilikuwa na wakazi wapatao 15,061. Msimbo wa posta ni 65402.
|
20231101.sw_2379_2
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kilwa%20Kivinje
|
Kilwa Kivinje
|
Wakati wa utawala wa Zanzibar ilikuwa makao ya liwali ya Sultani kwa ajili ya pwani la kusini la Tanganyika ikichukua nafasi ya Kilwa Kisiwani kama bandari muhimu katika sehemu hii ya pwani la kusini. Kivinje ilikuwa lengo la misafara ya watumwa katika kusini ya Tanzania. the mainland port of Kilwa Kivinje supplanted Kisiwani as the terminus of the southern slave caravan. Bandari yake ya mchanga ilifaa kwa maboti madogo ya ubao waliobeba watumwa Zanzibar. Kuna makadirio ya kwamba watumwa 20,000 walipita Kivinje kila mwaka. Mnamo mwaka 1850 Kivinje ilikuwa mji wa wakazi 12-15,000 pamoja na wanfanyabiashara wenye asili ya Uhindini. Baada ya Sultani wa zanzibar kupiga biashara ya watumwa marufuku Kivinje ilijulikana kwa kuendelea na biashara hii kwa siri. Zanzibar ilimkamata sulatani wa mwisho wa Kivinje na kumtuma nje ya mji.
|
20231101.sw_2379_3
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kilwa%20Kivinje
|
Kilwa Kivinje
|
Ilikuwa makao makuu ya wilaya tangu zamani ya ukoloni wa Kijerumani. Wakati wa vita ya Abushiri iliona mapigano dhidi ya Wajerumani na wawakilishi wa Kampuni ya Kijerumani kwa Afrika ya Mashariki waliuawa tar. 22 Septemba 1888. Mei 1890 Wajerumani walirudi chini ya meja Hermann von Wissmann wakateka mji bila upinzani.
|
20231101.sw_2379_4
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kilwa%20Kivinje
|
Kilwa Kivinje
|
Wakati wa Afrika ya Mashariki ya Kijerumani Kilwa Kivinje ilikuwa makao makuu ya mkoa wa nane iliyoenea kati ya Rufiji na Lindi. Utawala wa Kijerumani kilikwisha tar. 7 Septemba 1916 siku ambako Wajerumani waliobaki mjini walijisalimisha mbele ya kikosi cha wanamaji Waingereza.
|
20231101.sw_2379_5
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kilwa%20Kivinje
|
Kilwa Kivinje
|
Tangu kuondoka kwa makao makuu ya wilaya mji umerudi nyuma. Nyumba za ghorofa za wafanyabiashara hazitumiki tena zimeanza kuporomoka. Boma la Kale la Wajerumani bado linatumika.
|
20231101.sw_2379_6
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kilwa%20Kivinje
|
Kilwa Kivinje
|
Eneo la kihistoria lina magofu ya majengo ya Waswahili ya enzi za kati na baadhi ya majengo ya kiswahili yaliyosalia kutoka mwishoni mwa karne ya 19. Makazi haya yanachukuliwa kama kimbilio la wenyeji wa awali kutoka Kilwa Kisiwani ambao walikuwa wakimbizi kutoka kwa Vasco da Gama ambae alikuwa akiwafukuza mji huo mnamo 1505 na pia kuwachukua kama wakimbizi waliokimbia maharamia wa Madagaska mnamo 1822.
|
20231101.sw_2379_7
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kilwa%20Kivinje
|
Kilwa Kivinje
|
Picha za kilwa Kivinje wakati wa Wajerumani, pamoja na Boma (Kaiserliches Bezirksamt), Boma na Hospitali (Gruppe von Menschen vor der Boma und dem Hospital von Kilwa-Kivinje), Kikosi cha askari(Station Kilwa), Posta (Kais. Post, Akazienstrasse), Nyumba ya wanfanyabiashara de Souza (Haus der Firma de Souza jr. Dias & Co;)
|
20231101.sw_2380_0
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Wilaya%20ya%20Kilwa
|
Wilaya ya Kilwa
|
Wilaya ya Kilwa iko katika Mkoa wa Lindi, takriban kilometa 220 kusini mwa Dar es Salaam. Kilwa imepakana na Mkoa wa Pwani upande wa kaskazini, Bahari ya Hindi upande wa mashariki, wilaya ya Lindi Vijijini upande wa kusini na wilaya ya Liwale upande wa magharibi. Wakati wa sensa ya nwaka 2012, wilaya hii ilikuwa na wakazi 190,744 (mwaka 2002 waliohesbiwa 171,850 ).
|
20231101.sw_2380_1
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Wilaya%20ya%20Kilwa
|
Wilaya ya Kilwa
|
Kilwa Kisiwani - ambayo ni mfano bora wa miji ya Waswahili wa kale uliojulikana kimataifa tangu karne ya 13 BK
|
20231101.sw_2380_2
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Wilaya%20ya%20Kilwa
|
Wilaya ya Kilwa
|
Wakazi wengi hutegemea kilimo na uvuwi. Mazao yanayolimwa hasa ni pamoja na muhogo, mahindi, mtama na mpunga. Hata hivyo uzalishaji wa chakula hautoshelezi mahitaji ya wakazi. Sababu za upungufu ni kuongezeka kwa watu pamoja mitindo ya kilimo cha kimila ambako mashamba ni madogo, kwa wastani ekari 2, yakilimwa kwa mkono tu. Sehemu kubwa za wilaya kuna ardhi isiyo na rutba kubwa ambayo haushiki maji vizuri. Penye udongo mweusi mzuri karibu na Makangaga, Liwiti, Matandu, na Mbwemkuru inawezekana kulima mpunga. Kuna maeneo katika Milima ya Matumbi ambako miti ya matunda kutunzwa, hasa minazi na michungwa. Karibu na Likawage, Nanjirinji, Nainokwe, Njinjo na Singino Hill watu wanavuna pia korosho. Upatikanaji wa inzi za tsetse ni kizuizi kwa ufugaji.
|
20231101.sw_2380_3
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Wilaya%20ya%20Kilwa
|
Wilaya ya Kilwa
|
Gesi asilia huzalishwa kwenye Kisiwa cha Songosongo. Gesi hii inapelekwa hasa Dar es Salaam kwa uzalishaji wa umeme; lakini kuna pia kituo cha umeme kinachoendedhwa na gesi ya Songosongo kilichopo kwenye kata ya Somanga kikihudumia wilaya hii.
|
20231101.sw_2381_0
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kilwa%20Masoko
|
Kilwa Masoko
|
Iko barani ikitazama Kilwa Kisiwani. Mji ni wa kisasa. Kuna uwanja mdogo wa ndege pia bandari ndogo yenye kituo cha forodha.
|
20231101.sw_2381_1
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kilwa%20Masoko
|
Kilwa Masoko
|
Wakati wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 13,601 Msimbo wa posta ni 65408 walioishi humo.
|
20231101.sw_2382_0
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Wilaya%20ya%20Pangani
|
Wilaya ya Pangani
|
Imepakana na wilaya ya Muheza upande wa Kaskazini, Wilaya ya Handeni upande wa magharibi, wilaya ya Bagamoyo (Mkoa wa Pwani) upande wa kusini na Bahari Hindi upande wa mashariki. Makao makuu ya wilaya yako Pangani mjini.
|
20231101.sw_2382_1
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Wilaya%20ya%20Pangani
|
Wilaya ya Pangani
|
Wilaya ina wakazi 54,025 (2012) katika tarafa 4, kata 14 na vijiji 33. Ina shule za msingi 35, shule za sekondari 10 na zahanati 16.
|
20231101.sw_2382_2
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Wilaya%20ya%20Pangani
|
Wilaya ya Pangani
|
Eneo la wilaya ni kama kanda linalofuata ufuko wa Bahari Hindi. Mji wa Pangani upo mdomoni mwa mto Pangani unaoingia ndani ya nchi kavu kwa umbo la mlango mpana. Maeneo yaliyo karibu zaidi na bahari yenye ardhi ya rutuba kuna kilimo cha korosho, nazi, mihogo, mahindi, viazi vitamu na ndizi. Maeneo ya ndani zaidi pasipo rutuba sana kuna mashamba ya katani na mahindi.
|
20231101.sw_2382_3
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Wilaya%20ya%20Pangani
|
Wilaya ya Pangani
|
Kihistoria mazingira ya Pangani ni kati ya maeneo ya utamaduni wa Uswahilini; kabla ya ukoloni kulikuwa na mashamba ya Waarabu waliotumia watumwa na tangu kufika kwa ukoloni wa Kijerumani mashamba makubwa ya katani yalianzishwa.
|
20231101.sw_2382_4
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Wilaya%20ya%20Pangani
|
Wilaya ya Pangani
|
Wilaya hii ilikuwa pia nyumbani ya Abushiri ibn Salim al-Harthi na chanzo cha vita ya Abushiri dhidi ya utawala wa Kampuni ya Kijerumani kwa Afrika ya Mashariki.
|
20231101.sw_2383_0
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Historia%20ya%20Rwanda
|
Historia ya Rwanda
|
Historia ya Rwanda inahusu eneo la Afrika Mashariki ambalo wakazi wake leo wanaunda Jamhuri ya Rwanda.
|
20231101.sw_2383_1
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Historia%20ya%20Rwanda
|
Historia ya Rwanda
|
Rwanda ilikuwa eneo penye utawala wa kifalme tangu karne nyingi kabla ya kufika kwa ukoloni. Mwanzo wake ni katika eneo la Ziwa la Muhazi. Watawala wenye cheo cha "mwami" kutoka kikundi cha wafugaji (Watutsi) walisambaza eneo lao tangu miaka ya karne ya 16 BK hadi kufika eneo la leo. Wafugaji wa ng'ombe Watutsi walikalia nchi pamoja na wakulima wa Kihutu na wavindaji Watwaa.
|
20231101.sw_2383_2
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Historia%20ya%20Rwanda
|
Historia ya Rwanda
|
Ukoloni ulichelewa kufika Rwanda; mwaka 1890 Ujerumani na Uingereza walipatana ya kuwa Rwanda na Burundi ni sehemu ya Afrika ya Mashariki ya Kijerumani. Lakini ilikuwa mwaka 1908 tu ya kwamba Wajerumani walimtuma afisa wa kudumu aliyekaa Rwanda kama mwakilishi wa serikali ya Ujerumani. Mwaka 1916 Ubelgiji na Uingereza walivamia Rwanda katika Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia. Baadaye ikawa chini ya Ubelgiji pamoja na Burundi kama "Rwanda-Urundi" katika hali ya eneo la kudhaminiwa kutokana na azimio la Shirikisho la Mataifa.
|
20231101.sw_2383_3
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Historia%20ya%20Rwanda
|
Historia ya Rwanda
|
Utawala wa Wabelgiji ilikuwa ya moja-kwa moja na kali zaidi kuliko Wajerumani. Wabelgiji walijaribu kutoa faida ya kiuchumi wakilazimisha wenyeji kupanda mikahawa na kutekeleza kazi za serikali ya kikoloni. Katika utawala wao Wabelgiji walitumia zaidi Watutsi wakiwapa nafasi za elimu na kuwatumia katika shughuli za serikali. Wataalamu wengine huamini ya kwamba siasa hii ilisababisha kukua kwa chuki dhidi ya Watutsi kwa upande wa wakulima Wahutu iliyoleta kumwaga kwa damu baadaye.
|
20231101.sw_2383_4
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Historia%20ya%20Rwanda
|
Historia ya Rwanda
|
Katika miaka ya 1950 ilionekana ya kwamba ukoloni unaelekea mwisho wake. Uhusiano kati ya Wahutu na Watutsi ukawa vigumu kwa sababu Wabelgiji walibadilisha siasa yao yakupendelea Watutsi wakidai haki zaidi kwa ajili ya Wahutu wliokuwa wengi. Ni hasa wamisionari wa katoliki Mapadre Weupe waliosimama upande wa Wahutu wakiona ndio wagandamizwa.
|
20231101.sw_2383_5
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Historia%20ya%20Rwanda
|
Historia ya Rwanda
|
Mwami Mutara Rudahigwa aliyejiita pia Charles alijaribu kuleta upatanishi kati ya vikundi katika nchi. Mwaka 1954 aligawa nchi ya kifalme kati ya Wahutu na Watutsi. Lakini alikuwa na wapinzani Watutsi waliomwua mwaka 1959.
|
20231101.sw_2383_6
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Historia%20ya%20Rwanda
|
Historia ya Rwanda
|
Mtoto wake Mwami Kigeri V aliwekwa kwenye kiti chake. Tendo hili lilisababisha ghasia na vurugu nchini kwa sababu Wahutu walidai kuwa na neno katika mabadiliko ya serikali. Mwezi wa Novemba 1959 Mwami Kigeri V. alilazimishwa kuondoka nchini akikimbilia Uganda. Watutsi wenye siasa kali walijaribu kumwua kiongozi wa Mouvement Democratique Republicain (MDR) chama kikubwa cha Wahutu. Wahutu walijibu kwa kuwashambulia na kuua Watutsi. Wabelgiji walitumia wanajeshi wao kupoza hali nchini. Katika uchaguzi wa kwanza wa halmashauri ya tarafa na miji kabla ya uhuru ndicho chama cha Parmehutu kilichopata kura nyingi. Viongozi wa Parmehutu walitangaza serikali mpya mwaka 1961. Uchaguzi wa Bunge ulileta kura ya 77% kwa ajili ya chama cha Parmehutu kilichomchagua kiongozi wake Grégoire Kayibanda kuwa Rais.
|
20231101.sw_2383_7
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Historia%20ya%20Rwanda
|
Historia ya Rwanda
|
Tarehe 1 Julai 1962 Rwanda ilipata uhuru wake wa kisiasa. Wakati huu zaidi ya Watutsi 350,000 wameshakuwa wakikimbilia nchi jirani. Mwaka uliofuata vikundi vya Watutsi kutoka nchi hizi za jirani walijaribu kushambulia utaratibu mpya. Iliyofuata ilikuwa uangamizaji wa kwanza wa Watutsi; zaidi ya 100,000 waliuawa na Wahutu. Hata katika miaka iliyofuata mauaji dhidi ya Watutsi yaliendelea. Wanasiasa Wahutu walizoea kuwaita Watusi ndio "Wadudu". Kila kitu kilichokuwa si sawa kilielezwa ni kosa la Watutsi waliokuwa raia bila haki. Idadi kubwa ya Watutsi walikimbilia Burundi, Uganda na Tanzania.
|
20231101.sw_2383_8
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Historia%20ya%20Rwanda
|
Historia ya Rwanda
|
Mwaka 1973 Generali Habariyama alimpindua rais Kayibanda na kuanzisha serikali ya kijeshi akijaribu kupatanisha vikundi ndani ya taifa. Lakini hata mwaka uliofuata 1974 mauaji ya Watutsi yalitokea tena.
|
20231101.sw_2383_9
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Historia%20ya%20Rwanda
|
Historia ya Rwanda
|
Mnamo 1990 ilikuwa wazi ya kwamba Rwanda ilikuwa na hali ngumu. Kwa upande moja nchi za nje zilisukuma serikali za Afrika kuruhusu kura huru za kisiasa; katika Rwanda ongezeko la wakazi lilileta msongamano mkubwa na uhaba wa ardhi ya kilimo. Uchumi ilikuwa duni. Wakati huohuo wapinzani Wahutu walikusanyika nje ya nchi ny kudai demokrasia. Na kati ya watoto wa Watutsi waliokuwa walitoka nchini sauti zikasikika zilizodai warudi tena.
|
20231101.sw_2383_10
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Historia%20ya%20Rwanda
|
Historia ya Rwanda
|
Habyarimana alijaribu kutafuta suluhisho akanza kujadiliana na Watutsi wa nje lakini alikuta pia upinzani kwa upande wa Wahutu wakali waliochukia uelewano wa Watutsi.
|
20231101.sw_2383_11
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Historia%20ya%20Rwanda
|
Historia ya Rwanda
|
Mnamo Oktoba 1990 Watutsi waliokaa Uganda walianzisha chama cha RPF (Rwanda Patriotic Front) wakiwa na wafuasi wahutu wachache wakavamia Rwanda kwa silaha. Kiongozi wao alikuwa Paul Kagame aliyeondoka Rwanda akiwa mtoto wa miaka minne. Alikuwa amejiunga na jeshi la Yoweri Museveni na kupanda ngazi katika jeshi la Uganda hadi kuwa mkuu wa huduma ya usalama ya kijeshi ya Uganda. Walitaka kulazimisha serikali ibadilishe hali ya Watutsi kuwa raia bila haki. Lakini uvamizi huu ulisababisha kuongezeka kwa ukali dhidi ya Watutsi ndani ya Rwanda na siasa kali kwa upande wa viongozi Wahutu. Kikundi cha kihutu cha Interahamwe na kupewa silaha. Maelfu ya Watutsi Warwanda waliuawa.
|
20231101.sw_2383_12
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Historia%20ya%20Rwanda
|
Historia ya Rwanda
|
Vita kati ya wapinzani kutoka Uganda na jeshi la serikali iliendelea mpakani hadi pande zote mbili zilikutana huko Arusha na kupatana koma kwa vita 1992 chini ya uangalizi wa Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika.
|
20231101.sw_2383_13
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Historia%20ya%20Rwanda
|
Historia ya Rwanda
|
Sehemu ya viongozi Warwanda walijiandaa kutafuta utaratibu mpya lakini wengine walifanya mipango ya kumaliza swali la Watutsi kabisa wakipanga kuua Watutsi wote nchini.
|
20231101.sw_2383_14
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Historia%20ya%20Rwanda
|
Historia ya Rwanda
|
Tarehe 6 Aprili 1994 rais Habariyama alirudi nchini kutoka safari ya Tanzania. Ndege yake ilipigwa risasi kabla ya kutelemka ikaanguka chini akafa. Haipingiki kwamba Watutsi wakali (RPF) ndio waliomwua.
|
20231101.sw_2383_15
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Historia%20ya%20Rwanda
|
Historia ya Rwanda
|
Tendo hili lilikuwa mwanzo wa mauaji ambayo hayakuwahi kutokea Afrika. Viongozi wa Interahamwe, wa jeshi la kitaifa na vikundi vikali vya Kihutu walitekeleza mipango ya kukusanya Watutsi kila mahali na kuwaua. Haiwezekani kuwa na idadi kamili lakini makadirio ya chini yanataja Watutsi 750.000 na Wahutu wasio wakali zaidi ya 600000 waliuawa na Interahamwe na wanajeshi wa serikali ya Kihutu. Watu walikimbilia na kutafuta hifadhi makanisani lakini hata huko walichinjwa bila huruma. Wahutu waliokataa kushiriki katika mauaji waliuawa pia.
|
20231101.sw_2383_16
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Historia%20ya%20Rwanda
|
Historia ya Rwanda
|
RPF chini ya uongozi wa Paul Kagame iliamua kutumia nguvu zote kwa kulipiza kisasi kwa kuwaua Wahutu wenye msimamo mkali na wengine wengi kufungwa maisha katika jela zenye hali mbaya sana, akilenga kulipiza kisasi cha mauaji. Kwa miezi miwili mauaji na vita vilikwenda sambamba hadi RPF iliposhinda mnamo Julai 1994 na kuchukua madaraka ya serikali.
|
20231101.sw_2383_17
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Historia%20ya%20Rwanda
|
Historia ya Rwanda
|
Jeshi, Waparmehutu na serikali ya kihutu walikimbilia Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wakiwalazimisha wakazi wengi kuongozana nao hali iliyosababisha kutokea kwa makambi ya wakimbizi makubwa sana katika Kongo ya mashariki yaliyokuwa na idadi ya wahutu milioni mbili. Walio wengi wamerudi baada ya kuimarika kwa serikali mpya.
|
20231101.sw_2383_18
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Historia%20ya%20Rwanda
|
Historia ya Rwanda
|
Tangu ushindi wa kijeshi mwaka 1994 RPF walianzisha serikali ya umoja wa kitaifa. Rais alikuwa Pasteur Bizimungu mwanasiasa Mhutu aliyeshikamana na RPF, Kagame akiwa makamu wake. Baada ya kupinduliwa kwa Bizimungu mwaka 2000 Kagame akawa Rais.
|
20231101.sw_2383_19
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Historia%20ya%20Rwanda
|
Historia ya Rwanda
|
Jeshi la Rwanda limeendelea kuwa na vita ndani ya Kongo ikipigana na mabaki ya Interahamwe walioshambulia Rwanda mara kwa mara kutoka Kongo.
|
20231101.sw_2383_20
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Historia%20ya%20Rwanda
|
Historia ya Rwanda
|
Ndani ya Rwanda mahakama za vijijini zinazoitwa "gachacha" zimejaribu kutoa hukumu juu ya wauaji wa mwaka 1994.
|
20231101.sw_2383_21
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Historia%20ya%20Rwanda
|
Historia ya Rwanda
|
Rais D. Gasangwa wa Eacu alisisitiza kwamba ilikuwa "Ethnic cleansing", si Holocaust kama ilivyoandikwa na Wazungu wa magazeti ya Ulaya. Watu karibu 600,000 waliuawa Rwanda, na Mkoa wa Kivu, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
|
20231101.sw_2384_0
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ceuta
|
Ceuta
|
Ceuta (tamka: the-uta; kwa Kiarabu: سبتة sabta) ni mji wa Kihispania kwenye pwani ya Mediteranea ambao upande wa bara unazungukwa na eneo la Moroko. Ceuta iko karibu na mji wa Tetouan upande wa Moroko. Umbali na Hispania ni km 21 kuvuka mlango wa bahari wa Gibraltar.
|
20231101.sw_2384_1
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ceuta
|
Ceuta
|
Pamoja na mji wa Melilla ni sehemu ya Hispania na Umoja wa Ulaya kisiasa , lakini kijiografia ni sehemu ya Afrika. Moroko inadai ni sehemu ya eneo lake la kitaifa.
|
20231101.sw_2384_2
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ceuta
|
Ceuta
|
Ceuta ina wakazi 75.276 katika eneo la km² 18.5. Karibu nusu ni Wazungu/Wakristo na nusu ya pili ni Waberber-Waarabu/Waislamu.
|
20231101.sw_2384_3
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ceuta
|
Ceuta
|
Ceuta inaaminika iliundwa na Karthago katika karne ya 5 KK. Jina la Kigiriki la mji imekuwa "Επτά Αδελφοί" (hepta adelphoí - ndugu saba).
|
20231101.sw_2384_4
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ceuta
|
Ceuta
|
Tangu Waroma walipochukua utawala wa Afrika ya Kaskazini mji ulijulikana kwa jina la "Septem Fratres" (ndugu saba). Jina hili limeendelea hadi leo, mji ukiitwa "sabta" kwa Kiarabu au kwa matamshi ya Kihispania "Ceuta".
|
20231101.sw_2384_5
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ceuta
|
Ceuta
|
Mwaka 710 Waarabu Waislamu walifika wakipita Ceuta kuvamia Hispania. Hadi karne ya 14 mji ulikuwa chini ya watawala Waislamu ama Waarabu au Waberberi. Kati ya Wakristo waliofia dini yao huko wanakumbukwa watakatifu Danieli mfiadini na wenzake (1226).
|
20231101.sw_2384_6
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ceuta
|
Ceuta
|
Mwaka 1415 Wareno waliteka Ceuta wakaitawala hadi mwaka 1668. Baada ya vita kati ya Ureno na Hispania mji ulikabidhiwa kwa mfalme wa Hispania.
|
20231101.sw_2384_7
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ceuta
|
Ceuta
|
Tangu mwaka 1668 Ceuta imekuwa sehemu ya Hispania. Ndani ya Hispania imekuwa Mji wa kujitawala (kwa Kihispania: ciudad autónoma) tangu 1995.
|
20231101.sw_2385_0
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kabla%20ya%20Kristo
|
Kabla ya Kristo
|
Kila mwaka huhesabiwa kuanzia ule uliodhaniwa kuwa mwaka wa kuzaliwa kwake Yesu Kristo. Miaka iliyofuata kuzaliwa kwake hutajwa kwa kuongeza Baada ya Kristo au kifupi: BK.
|
20231101.sw_2387_0
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ella%20Fitzgerald
|
Ella Fitzgerald
|
Ella Fitzgerald (25 Aprili 1917 – 15 Juni 1996) alifahamika kama muimbaji wa kike wa muziki wa Jazz (Lady of songs).
|
20231101.sw_2387_1
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ella%20Fitzgerald
|
Ella Fitzgerald
|
Ella Fitzgerald au mama Ella sauti yake ilikuwa ni muhimu sana kwenye muziki wa Jazz na hata mitindo mingine ya muziki katika karne ya ishirini.
|
20231101.sw_2387_2
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ella%20Fitzgerald
|
Ella Fitzgerald
|
Ella Fitzgerald alizaliwa 25 Aprili 1917 mjini Newport News (Va- Marekani). Ella ameshirikiana na wanamuziki wengi mojawapo ni Louis Armstrong "Satchimo" huyu alikuwa ni mpiga tarumpeta mashuhuri. Mama Ella alizama zaidi katika mtindo wa Swing Jazz.
|
20231101.sw_2387_3
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ella%20Fitzgerald
|
Ella Fitzgerald
|
Kati ya nyimbo alizowahi kuimba ni: That old black magic; Can't we be friends?; Love is the thing so they say; It's a blue wold;
|
20231101.sw_2388_0
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Simba%20Wanyika
|
Simba Wanyika
|
Simba Wanyika ilikuwa bendi nchini Kenya iliyoundwa mwaka wa 1971 na ndugu kutoka Tanzania, Wilson Kinyonga na George Kinyonga. Bendi hii ilivunjika mwaka wa 1994. Simba Wanyika na bendi zingine mbili zilizotoka kwayo, Les Wanyika na Super Wanyika Stars, zilikuwa bendi mashuhuri sana nchini Kenya. Muziki wao uliotokana na sauti ya gitaa, ikiongozwa na mpiga gitaa wa Soukous, Dr Nico,ikichanganywa na maneno matamu ya muziki wa rumba na kuimbwa kwa Kiswahili. Simba wa nyika tafsiri yake kwa Kiingereza ni "Lions of the Savannah".
|
20231101.sw_2388_1
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Simba%20Wanyika
|
Simba Wanyika
|
Wilson Kinyonga na George Kinyonga walianza muziki katika mji wao wa nyumbani wa Tanga nchini Tanzania walipojiunga na Jamhuri Jazz Band mwaka wa 1966. Walihamia Arusha mwaka wa 1970 na kuunda bendi ya Arusha Jazz na ndugu yao mwingine, William Kinyonga. Katika kipindi hiki, wanamuziki walikuwa wakisafiri watakavyo kati ya Kenya na Tanzania, na muziki wa Kenya ukashawishika sana na muziki wa rumba wa Tanzania. Mwaka wa 1971 ndugu hawa walihamia nchini Kenya na kuanzisha Simba Wanyika. Bendi ilitumbuiza katika vilabu vya usiku na baa mbalimbali katika jiji la Nairobi, nakupata wafuasi wengi mno, na katikati ya miaka ya 1970, walikuwa wanajulikana kote Kenya, kwa ajili ya nyimbo kama "Mwongele" na "Wana Wanyika".
|
20231101.sw_2388_2
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Simba%20Wanyika
|
Simba Wanyika
|
Kutekelezwa kwa vikwazo baina ya mpaka wa Kenya-Tanzania ilisababisha watu kukua kwa muziki na kuelekea katika mtindo wa uliokuwa unajitokeza wa benga nchini Kenya. Simba Wanyika waliendelea kucheza rumba, na walikuwa bado maarufu wakati bendi ilipogawanyika katika miaka ya 1970 wakati mpiga gitaa Omar Shabini alichukua baadhi ya wanamuziki wake na kutengeneza Les Wanyika. Mwaka wa 1980, George Kinyonga pia alijiondoa katika Simba Wanyika, akachukua wanamuziki zaidi na kuunda bendi ya Orchestra Jobiso. Lakini baadaye alirudi Simba Wanyika huku bado akifanya miradi za upande na Jobiso. Simba Wanyika baadaye walibadilisha jina lao hadi "Simba Wanyika Original" ili kuzuia mkanganyiko na Les Wanyika na kundi lilojigawa kutoka kwao la Super Wanyika Stars.
|
20231101.sw_2388_3
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Simba%20Wanyika
|
Simba Wanyika
|
Simba Wanyika ilirudia umaarufu wake katika katikati ya miaka ya 1980 wakitoa nyimbo zilizoptata umaarufu na baadaye kuzuru Ulaya mwaka wa 1989. Bendi ilivunjika mwaka wa 1994 lakini bendi kadhaa zilizotokana nayo bado ziko hai.
|
20231101.sw_2391_0
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Nyasa%20%28ziwa%29
|
Nyasa (ziwa)
|
Ziwa Nyasa (katika Malawi: Lake Malawi; katika Msumbiji: Niassa) ni kati ya maziwa makubwa ya Afrika ya Mashariki likiwa na nafasi ya tatu baada ya Viktoria Nyanza na Ziwa Tanganyika.
|
20231101.sw_2391_1
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Nyasa%20%28ziwa%29
|
Nyasa (ziwa)
|
Lina urefu wa km 560 na upana wa km 50-80, likienea kutoka kaskazini kuelekea kusini. Vilindi vyake vinafikia hadi mita 704 chini ya uwiano wa maji yake.
|
20231101.sw_2391_2
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Nyasa%20%28ziwa%29
|
Nyasa (ziwa)
|
Katika ziwa hilo kuna mito mbalimbali inayoingiza maji yake humo kama vile mto Lufilyo, mto Mbaka, mto Kiwila, mto Songwe n.k.
|
20231101.sw_2391_3
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Nyasa%20%28ziwa%29
|
Nyasa (ziwa)
|
Ziwa Nyasa linajulikana kuwa na aina nyingi za samaki (zaidi ya 1500). Aina chache tu zinavuliwa kama chakula, lakini aina mbalimbali zinakamatwa na kuuzwa nje ya Afrika kwa wapenzi wa samaki wa rangi.
|
20231101.sw_2391_4
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Nyasa%20%28ziwa%29
|
Nyasa (ziwa)
|
Malawi lina ufuko mrefu ziwani upande wa magharibi na kusini, ilhali Tanzania inapakana na kaskazini mwa ziwa na kwenye ufuko wa mashariki, ikifuatwa na Msumbiji.
|
20231101.sw_2391_5
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Nyasa%20%28ziwa%29
|
Nyasa (ziwa)
|
Kuna ugomvi kati ya Malawi na Tanzania kuhusu mipaka ndani ya ziwa. Mpaka baina ya Malawi (zamani: Nyassaland) na Msumbiji ulipangwa wakati wa ukoloni. Lakini kuna mzozo kuhusu robo ya kaskazini-mashariki inayodaiwa na Tanzania kuwa ni eneo lake, ilhali Malawi inaidai pia.
|
20231101.sw_2391_6
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Nyasa%20%28ziwa%29
|
Nyasa (ziwa)
|
Malawi imedai ya kwamba maji yote hadi ufukoni upande wa Tanzania ni sehemu ya eneo lake la kitaifa. Tanzania imedai ya kwamba mpaka uwe katikati ya ziwa kufuatana na desturi za kimataifa.
|
20231101.sw_2391_7
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Nyasa%20%28ziwa%29
|
Nyasa (ziwa)
|
Sababu ya mzozo ni maelewano ya kikoloni. Wakati wa kuanzishwa kwa Afrika ya Mashariki ya Kijerumani lakini kabla ya serikali ya Ujerumani kuchukua koloni mkononi mwake, serikali za Uingereza na Ujerumani zilipatana kuhusu mipaka ya "eneo chini ya athira ya Ujerumani" ("German sphere of influence") kwa kutaja mpaka ulifuata ufuko wa Ziwa Nyasa. Leo inajadiliwa baina ya wanasharia wa kimataifa kama maneno haya yalitaja mipaka halisi ya kiutawala au kama yalikuwa tu mapatano ya awali kuhusu "maeneo chini ya athira" ya nchi husika.
|
20231101.sw_2391_8
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Nyasa%20%28ziwa%29
|
Nyasa (ziwa)
|
Baada ya mwaka 1919 Uingereza ilitawala Tanganyika pamoja na Malawi (Nyassaland), hivyo hakukuwa na shida.
|
20231101.sw_2391_9
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Nyasa%20%28ziwa%29
|
Nyasa (ziwa)
|
Kabla ya uhuru, wakati wawakilishi wa TANU walichaguliwa tayari kuwa wabunge katika bunge la kikoloni (legislative council) na Julius Nyerere alikuwa waziri mkuu wa Tanganyika tangu 1960, mbunge Chifu Mhaiki alitaka serikali iangalie upya haki za Tanganyika kwa maji ya ziwa. Tarehe 12 Oktoba 1960 waziri mkuu Nyerere alijibu: "Hakuna shaka lolote kuhusu mpaka huu. Tunajua kwamba hakuna tone la maji kwenye Ziwa Nyasa ni mali ya Tanganyika kufuatana na mapatano haya. Hali halisi tungedai serikali jirani ibadilishe mipaka kwa manufaa ya Tanganyika." . Chifu Mhaiki alirudia swali lake alipokuwa mbunge katika Bunge la Kitaifa baada ya uhuru wa Tanganyika mwaka 1962 na safari hii waziri mkuu Rashidi Kawawa alijibu tena kwamba hakuna sehemu ya Ziwa Nyasa iliyokuwa ndani ya Afrika ya Mashariki ya Kijerumani, kwamba Uingereza haikubadilisha mipaka hii na kwamba hata kama kuna hasara kwa Tanganyika serikali haiwezi kuanza majadiliano juu ya swali hili na Uingereza au serikali ya Nyasaland kabla ya uhuru wa nchi hii jirani.
|
20231101.sw_2391_10
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Nyasa%20%28ziwa%29
|
Nyasa (ziwa)
|
Tarehe 3 Januari 1967 serikali ya Tanzania iliandika mara ya kwanza kwa serikali ya Malawi na kuifahamisha kwamba iliona mpaka baina ya nhci hizi ilifuata mstari wa kati wa Ziwa Nyasa. Malawi ilithibitisha kupokelewa kwa barua hii bila kuijibu rasmi. Hata hivyo rais Banda wa Malawi alikataa madai ya tanzania mbele ya bunge lake. Polisi ya Malawi ilijaribu kutawala wavuvi na feri za Tanzania ziwani. Mzozo huu ulisababisha risasi kufyatuliwa hadi kutulia mwaka 1968.
|
20231101.sw_2391_11
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Nyasa%20%28ziwa%29
|
Nyasa (ziwa)
|
Hadi leo hakuna mapatano rasmi lakini nchi zote mbili zinaendelea kudai bila kutumia nguvu. Hali halisi Malawi imeheshimu dai la Tanzania, haijasumbua tena wavuvi wala feri za jirani ndani ya robo ya kaskazini-mashariki ya ziwa.
|
Subsets and Splits
No community queries yet
The top public SQL queries from the community will appear here once available.