_id
stringlengths 15
22
| url
stringlengths 31
150
| title
stringlengths 1
86
| text
stringlengths 100
23.8k
|
---|---|---|---|
20231101.sw_2353_0
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Culture
|
Culture
|
Culture ni kundi la muziki ya reggae kutoka nchi ya Jamaika lililoanzishwa mwaka wa 1976. Jina la mwanzoni la kundi hilo lilikuwa ni "African Disciples". Kundi la Culture linaaminika kuwa ni kati ya makundi wanaopiga muziki halisi ya reggae yenye mafunzo na busara. Waanzilishi wa kundi hilo ni Joseph Hill, mwimbaji mwongozaji, Kenneth Dayes, mwitikiaji, na Albert Walker, mwitikiaji. Wimbo wao wa "Two Sevens Clash" uliorekodiwa mwaka wa 1977 katika studio ya Joe Gibbs, na uliwapatia umaarufu mkubwa na kuwaweka kwenye ramani ya muziki ya reggae duniani.
|
20231101.sw_2355_0
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/True%20Jesus%20Church
|
True Jesus Church
|
True Jesus Church ni kanisa la kujitegemea la Ukristo wa Kiprotestanti lililo na asili huko Beijing, Uchina, mwaka 1917.
|
20231101.sw_2355_1
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/True%20Jesus%20Church
|
True Jesus Church
|
Idadi kubwa wako ndani ya Uchina ambako si rahisi kuhakikisha idadi kamili kwa sababu TSC ni kati ya makanisa na vikundi vya Kikristo vilivyopigwa marufuku na serikali ya nchi hiyo.
|
20231101.sw_2355_2
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/True%20Jesus%20Church
|
True Jesus Church
|
Tovuti za TJC katika nchi mbalimbali zinataja Wakristo 70,000 hadi 80,000 katika "nchi huru", wengi wao wakiwa na asili ya Kichina.
|
20231101.sw_2355_3
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/True%20Jesus%20Church
|
True Jesus Church
|
Kanisa lilianzishwa wakati wa kustawishwa kwa harakati za Kipentekoste nchini Uchina mwanzo wa karne ya 20. Harakati hizi zilianzia Marekani wakati wa mkutano wa kwanza wa Kipentekoste katika Azusa Street Revival huko Los Angeles iliyoongozwa na William J. Seymour miaka [1906]]-1908.
|
20231101.sw_2355_4
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/True%20Jesus%20Church
|
True Jesus Church
|
Kulikuwepo moja ya nyumba tatu za Kichina zilizotengenezwa kabla ya Chama cha Kikomunisti cha Uchina kuchukua mamlaka mwaka 1949.
|
20231101.sw_2355_5
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/True%20Jesus%20Church
|
True Jesus Church
|
Tangu mwaka 2002 lilianza kuwasiliana na kikundi cha kikristo huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kilichojiunga nalo mnamo mwaka 2004.
|
20231101.sw_2355_6
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/True%20Jesus%20Church
|
True Jesus Church
|
Wanajieleza kwamba Yesu Kristo alianzisha Kanisa moja la kimitume lililopeleka Injili katika nchi mbalimbali.
|
20231101.sw_2355_7
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/True%20Jesus%20Church
|
True Jesus Church
|
Lakini Kanisa hilo likavurugika na kupatwa na imani potovu na uzushi hadi mwaka 1917 Mungu alipoamua kulifufua kwa nguvu ya Roho Mtakatifu na ndio mwanzo wa TJC.
|
20231101.sw_2355_8
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/True%20Jesus%20Church
|
True Jesus Church
|
Wanakataza ibada za Jumapili wakidai siku ya Jumamosi ndiyo siku takatifu ya Sabato iliyoamriwa na Mungu.
|
20231101.sw_2355_9
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/True%20Jesus%20Church
|
True Jesus Church
|
Hawasheherekei sikukuu za Krismasi na Pasaka kwa sababu wanaamini zina asili za kipagani na ni mifano ya imani ya Kikristo ya asili kuingiliwa na uzushi.
|
20231101.sw_2355_10
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/True%20Jesus%20Church
|
True Jesus Church
|
Mafundisho mengine yanafanana na yale ya Wapentekoste, kama vile kusema kwa lugha za roho au kubatizwa kwa jina la Yesu kwa kuzamishwa chini ya maji, tena maji ya kutiririka.
|
20231101.sw_2355_11
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/True%20Jesus%20Church
|
True Jesus Church
|
Roho Mtakatifu: "kupatwa na Roho Mtakatifu ambayo huthibitishwa na uwezo wa kuongea pepo, ni hakikisho yetu ya kurithi ufalme mbinguni."
|
20231101.sw_2355_12
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/True%20Jesus%20Church
|
True Jesus Church
|
Ubatizo: "Kubatizwa kwa maji ni sakramenti ya kutubu dhambi na kuzaliwa tena. Ubatizo unafaa kufanywa kwenye maji ya kawaida kama vile kwenye mto, kisima au ziwa. Mbatizaji, ambaye pia amebatizwa vilevile na kwa Roho Mtakatifu, hutimiliza ubatizaji kwa jina la Mwana Yesu Kristu. Kichwa cha Mbatizwaji hutumbUkizwa kwenya maji kukamilisha ubatizo."
|
20231101.sw_2355_13
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/True%20Jesus%20Church
|
True Jesus Church
|
Kutakaswa: "Sakramenti ya kunawa miguu huwezesha binafsi kuwa na shirika na Bwana Yesu. Pia hutukumbusha mara kwa mara ni lazima tuwe na upendo, utakatifu, unyeyekevu, msamaha na utumishi. Yeyote aliyepata ubatizo wa maji ni lazima aoshwe miguu kwa jina la Yesu Kristo. Kunawishwa miguu yaweza kufanywa inapohitajika."
|
20231101.sw_2355_14
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/True%20Jesus%20Church
|
True Jesus Church
|
Komunio Takatifu: "Komunio Takatifu ni sakramenti ya kusheherekea kifo cha Mola Yesu Kristu. Inatueneza kupata mwili na damu ya mwokozi wetu na kuwa na umoja naye ili tuweze kupata uzima wa milele na kufufuliwa siku ya mwisho. Sakramenti hii ina haja ya kufanywa kila iwezekanapo. Katika sakramenti hii hutumiwa mkate na divai."
|
20231101.sw_2355_15
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/True%20Jesus%20Church
|
True Jesus Church
|
Sabato: "Siku ya sabato, ambayo ni siku ya saba kwenye wiki (Jumamosi), ni siku takatifu, iliyobarikiwa na kusahihishwa na Mungu Baba. Siku hii hubudiwa kwa ajili ya ukumbusho wa maumbo na pia ukombozi na Mungu Baba, na tarajio la pumziko la milele daima kwenye maisha yatakayokuja."
|
20231101.sw_2355_16
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/True%20Jesus%20Church
|
True Jesus Church
|
Yesu Kristo: "Yesu Kristo, Neno aliyefanyika mwili, akafa msalabani kwa msamaha wa wenye dhambi, akafufuka siku ya tatu akapaa juu mbinguni. Yeye ndiye mwokozi wa binadamu, Muumba wa mbingu na nchi na ndiye Mungu wa kweli."
|
20231101.sw_2355_17
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/True%20Jesus%20Church
|
True Jesus Church
|
Biblia Takatifu (Maandiko Matakatifu): "Biblia Takatifu, ina Agano la Kale na Agano Jipya ambayo imewezeshwa na Mungu na yenye Maandiko Matakatifu ya kweli kwa maisha ya Mkristo."
|
20231101.sw_2355_18
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/True%20Jesus%20Church
|
True Jesus Church
|
Wokovu: "Wokovu unatolewa kwa neema ya Mungu kupitia imani. Waaminio lazima wamwamini Roho Mtakatifu ili kupata utakatifu, kwa kumheshimu Mungu, na kwa upendo wa watu"
|
20231101.sw_2355_19
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/True%20Jesus%20Church
|
True Jesus Church
|
Kanisa: "Kanisa, lililetwa na Bwana Yesu Kristo, kupitia Roho Mtakatifu kipindi cha 'nyakati za mwisho', ni kanisa la kweli lililorejeshwa nyakati za ki'Apostoliki."
|
20231101.sw_2355_20
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/True%20Jesus%20Church
|
True Jesus Church
|
Hukumu ya mwisho: "Kuja kwa Yesu kwa mara ya pili itakuwa siku ya mwisho wakati akishuka kutoka mbinguni kuhukumu: walio na haki watapokea uzima wa milele wasio na haki watahukumiwa milele"
|
20231101.sw_2355_21
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/True%20Jesus%20Church
|
True Jesus Church
|
Ingefaa ueleweke ukweli wa msimamo wa TJC kulingana na Biblia wanapodai kwa miaka mia kadhaa duniani halikuwepo tena Kanisa la kweli, wakati Yesu aliahidi, "Nipo pamoja nanyi siku zote hata ukamilifu wa dahari" (Mathayo 28:20). Tena "Wewe ndiwe Petro, na juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa langu, wala milango ya kuzimu haitalishinda" (Mathayo 16:18).
|
20231101.sw_2360_0
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Umoja%20wa%20Afrika
|
Umoja wa Afrika
|
Umoja wa Afrika (UA) (kwa Kiingereza: African Union (AU); Kifaransa: Union Africaine (UA); Kihispania: Unión Africana (UA) ; Kireno: União Africana (UA) ) ni muungano wa nchi 55 za Afrika ulioanzishwa mnamo Julai 2002.
|
20231101.sw_2360_1
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Umoja%20wa%20Afrika
|
Umoja wa Afrika
|
Umoja huu unaendeleza kazi za Umoja wa Muungano wa Afrika (kwa Kiingereza: Organisation of African Union - OAU) uliokuwepo 1963 hadi 2002.
|
20231101.sw_2360_2
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Umoja%20wa%20Afrika
|
Umoja wa Afrika
|
Nia ya umoja huu ni kujenga muundo na mfumo wa kisiasa, wa kiuchumi, na wa kijamii ili kufikia wakati ambapo bara la Afrika litakuwa na bunge moja, benki moja, jeshi moja, rais mmoja, sarafu moja, n.k.
|
20231101.sw_2360_3
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Umoja%20wa%20Afrika
|
Umoja wa Afrika
|
Dhumuni kubwa la umoja huu ni kuunganisha nguvu za mataifa ya Afrika ili kuweza kutatua matatizo yanayokabili bara hili kama vile vita, njaa, Ukimwi, n.k.
|
20231101.sw_2360_4
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Umoja%20wa%20Afrika
|
Umoja wa Afrika
|
Umoja wa Afrika ina nchi wanachama 55, yaani nchi zote za bara la Afrika (baada ya kurudi kwa Moroko, iliyokuwa imejiondoa mwaka 1985 kwa sababu UA ilitambua Sahara ya Magharibi kuwa nchi huru wakati Moroko inadai ni eneo la majimbo yake ya kusini).
|
20231101.sw_2364_0
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Shelisheli
|
Shelisheli
|
Shelisheli ni funguvisiwa na jamhuri katika Bahari Hindi, mashariki kwa mwambao wa Afrika Mashariki na kaskazini kwa Madagaska.
|
20231101.sw_2364_1
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Shelisheli
|
Shelisheli
|
Shelisheli ina visiwa 115; 32 kati ya hivyo ni visiwa vikubwa kidogo vyenye milima, vingine ni vidogo na huitwa "Visiwa vya nje".
|
20231101.sw_2364_2
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Shelisheli
|
Shelisheli
|
Kisiwa kikubwa zaidi ni Mahé na mji mkuu Victoria uko huko. Wakazi wengi huishi Mahe pamoja na visiwa vya karibu, hasa Praslin na La Digue.
|
20231101.sw_2364_3
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Shelisheli
|
Shelisheli
|
Visiwa hivyo vina milima inayofikia hadi mita 900 juu ya UB. Mkubwa ni Morne Seychellois wenye mita 905 juu ya UB.
|
20231101.sw_2364_4
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Shelisheli
|
Shelisheli
|
Hali ya hewa ni ya kitropiki ikiwa halijoto iko kati ya 24 °C na 30 °C. Kiasi cha mvua ni kati ya mm 2.880 huko Victoria na mm 3.550 mlimani.
|
20231101.sw_2364_5
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Shelisheli
|
Shelisheli
|
Hakuna hakika kuhusu wakazi wa kwanza. Inaaminika ya kwamba ndio mabaharia na wafanyabiashara Waarabu.
|
20231101.sw_2364_6
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Shelisheli
|
Shelisheli
|
Kwa karne moja na nusu meli au jahazi zilipitia Shelisheli tu kwa kusudi la kuchota maji ya kunywa au kukusanya matunda bila ya kuanzisha makao ya kudumu. Majambazi wa baharini walipenda kujificha Shelisheli.
|
20231101.sw_2364_7
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Shelisheli
|
Shelisheli
|
Ndio Ufaransa uliojenga vituo vya kwanza vya kudumu mwaka 1756. Wafaransa waliita visiva "Seychelles" kwa heshima ya waziri wao wa siku zile Jean Moreau de Sechelles.
|
20231101.sw_2364_8
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Shelisheli
|
Shelisheli
|
Walowezi wao walianzisha mashamba makubwa ya mazao ya biashara wakitumia watumwa kutoka Madagaska na Afrika bara kwa ajili ya kazi yenyewe.
|
20231101.sw_2364_9
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Shelisheli
|
Shelisheli
|
Tangu mwaka 1814 visiwa vilikuwa chini ya Uingereza. Waingereza walivumilia walowezi na utamaduni wa Kifaransa visiwani.
|
20231101.sw_2364_10
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Shelisheli
|
Shelisheli
|
Kwanza Shelisheli zilikuwa zikitawaliwa pamoja na Mauritius, lakini mwaka 1903 visiwa vilipewa cheo cha koloni mbali na Mauritius.
|
20231101.sw_2364_11
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Shelisheli
|
Shelisheli
|
Mwaka 1970 Shelisheli walipata uhuru. Katiba ya kwanza ilifuata mfano wa Uingerezeza lakini mwaka 1979 katiba mpya ilileta mfumo wa chama kimoja.
|
20231101.sw_2364_12
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Shelisheli
|
Shelisheli
|
Wakazi kwa jumla (93.2%) ni machotara wenye mchanganyiko wa damu ya Afrika bara, Ulaya na Asia. Licha ya hao kuna vikundi vidogo vya Wahindi (6%), Wazungu (5%) na Wachina (0.5%) halisi.
|
20231101.sw_2364_13
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Shelisheli
|
Shelisheli
|
Lugha rasmi ni tatu: Kiingereza (5.1%), Kifaransa (0.7%) na Kiseselwa, aina ya Krioli ambayo imetokana na Kifaransa na ndiyo lugha ya kawaida (91%).
|
20231101.sw_2364_14
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Shelisheli
|
Shelisheli
|
Upande wa dini, wakazi wengi ni Wakristo, hasa Wakatoliki (76.2%), halafu Waprotestanti (13.0%), wengine wachache ni Wahindu (2.4%), Waislamu (1.6%) n.k.
|
20231101.sw_2364_15
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Shelisheli
|
Shelisheli
|
Biashara ya Shelisheli inategemea hasa utalii unaoingiza 70% ya pato la taifa. Asilimia 30 hivi za wafanyakazi wote wamo katika utalii.
|
20231101.sw_2364_16
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Shelisheli
|
Shelisheli
|
National Bureau of Statistics, government agency responsible for collecting, compiling, analysing and publishing statistical information
|
20231101.sw_2364_17
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Shelisheli
|
Shelisheli
|
Island Conservation Society, a non-profit nature conservation and educational non-governmental organisation
|
20231101.sw_2365_0
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Haile%20Selassie
|
Haile Selassie
|
Haile Selassie (kwa Kige'ez: ቀዳማዊ ኃይለ ሥላሴ, qädamawi haylä səllasé, [ˈhaɪlə sɨlˈlase]; 23 Julai 1892 – 27 Agosti 1975) alikuwa Kaisari au Negus Negeste wa Ethiopia. Kabla ya kuwa mfalme aliitwa Ras Tafari Makonnen. Jina lake la kifalme lina maana ya "Utukufu wa Utatu (Mtakatifu)". Pia anafahamika kwa jina la Simba wa Yuda, Mfalme wa wafalme.
|
20231101.sw_2365_1
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Haile%20Selassie
|
Haile Selassie
|
Alizaliwa katika kijiji kiitwacho Ejersa. Baba yake alikuwa kabaila Mwethiopia aliyeitwa Ras Makonnen akawa gavana wa Harar, familia yake ikiwa na watoto 11.
|
20231101.sw_2365_2
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Haile%20Selassie
|
Haile Selassie
|
Ras Tafari Makonnen alikuwa bado kijana alipopewa cheo cha gavana wa Sidamo mwaka 1907. Mwaka 1911 akarithi nafasi ya gavana wa Harar.
|
20231101.sw_2365_3
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Haile%20Selassie
|
Haile Selassie
|
Wakati wa ugomvi kuhusu Negus Mwislamu Lij Iyasu (1913-1916) alisimama awali upande wa mfalme lakini alifaidika zaidi na uasi uliompindua Negus. Makabaila waliomwondoa Iyasu mwaka 1916 walimteua shangazi yake Zauditu, aliyekuwa binti wa Negus Negesti marehemu Menelik II, kuwa malkia, wakaamua pia Ras Tafari awe mwangalizi wake.
|
20231101.sw_2365_4
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Haile%20Selassie
|
Haile Selassie
|
Kwa njia hiyo Ras Tafari akawa kiongozi muhimu zaidi nchini. Mwaka 1928 Zauditu akampa cheo cha negus chini yake mwenyewe. Baada ya kifo cha Zauditu (1930) Ras Tafari akapokea taji na cheo cha Negus Negeste (au mfalme wa wafalme) wa Ethiopia akajiita Haile Selassie.
|
20231101.sw_2365_5
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Haile%20Selassie
|
Haile Selassie
|
Habari zake zikaenea kote duniani zikasababisha kutokea kwa dini mpya ya Rastafari iliyopokea jina kutoka kwake, ingawa mwenyewe alibaki mwamini wa Kanisa la Orthodoksi, akiwa na daraja ya ushemasi. Watu weusi kisiwani Jamaika, waliokuwa wajukuu wa watumwa wenye asili ya Afrika, walisikia kwa mara ya kwanza ya kwamba Mwafrika anaheshimiwa na wafalme wa Ulaya, wakaona yeye ni mwokozi wa Mungu aliyerudi duniani kwa ajili ya watu weusi.
|
20231101.sw_2365_6
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Haile%20Selassie
|
Haile Selassie
|
Haile Selassie alifukuzwa katika Ethiopia mwaka 1936 Italia ilipovamia Ethiopia, akarudi 1941 kwa msaada wa Uingereza iliyoondoa Waiitalia nchini katika Vita Kuu ya Pili ya Dunia.
|
20231101.sw_2365_7
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Haile%20Selassie
|
Haile Selassie
|
Utawala wa Haile Selassie uliingiza Ethiopia katika Chama cha Mataifa ikiwa nchi ya kwanza ya Afrika kujiunga nacho. Baadaye ulimpa nafasi kubwa katika harakati ya uhuru wa Afrika na makao makuu ya Umoja wa Afrika yalijengwa Addis Ababa, mji mkuu wa Ethiopia.
|
20231101.sw_2365_8
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Haile%20Selassie
|
Haile Selassie
|
Katika siasa ya ndani alishindwa kuendeleza nchi yake. Alikosa nguvu na nia ya kumaliza utawala wa kikabaila nchini uliosababisha umaskini mkali kati ya wakulima waliopaswa kuwaachia wakabaila sehemu ya mazao.
|
20231101.sw_2365_9
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Haile%20Selassie
|
Haile Selassie
|
Hivyo kimataifa Haile Selassie aliheshimiwa sana lakini ndani ya nchi maendeleo yalikwama, wanafunzi na wasomi wakikasirikia na wakulima maskini wakifa njaa mara kwa mara.
|
20231101.sw_2365_10
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Haile%20Selassie
|
Haile Selassie
|
Njaa kubwa ya miaka 1972–1973 katika majimbo ya Wollo na Tigray ikafuatwa na mapinduzi ya kijeshi ya mwaka 1974. Kamati ya kijeshi ya Derg ikamkamata tarehe 12 Septemba 1974.
|
20231101.sw_2365_11
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Haile%20Selassie
|
Haile Selassie
|
Kifo chake kikatangazwa tarehe 28 Agosti 1975 na haieleweki kama aliuawa au alikufa kutokana na ugonjwa.
|
20231101.sw_2365_12
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Haile%20Selassie
|
Haile Selassie
|
Baada ya kuondolewa kwa Derg mabaki ya maiti ya Kaisari yalipatikana mwaka 1992 chini ya sakafu ya choo cha jumba la kifalme alikokamatwa. Tarehe 5 Novemba 2000 mabaki hayo yalipewa mazishi ya kifalme katika kanisa kuu la Kiorthodoksi la Addis Ababa.
|
20231101.sw_2368_0
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kampala
|
Kampala
|
Kampala ni mji mkuu wa Uganda, pia mojawapo ya wilaya za nchi. Iko karibu na ziwa kubwa la Nyanza Viktoria, mita kama 1,189 juu ya UB.
|
20231101.sw_2368_1
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kampala
|
Kampala
|
Jina la Kampala limetokana na msemo wa Kiganda "Kasozi K'Empala" wenye maana ya "kilima cha swala" kwa sababu wafalme wa Buganda walipenda kuwinda katika eneo hili.
|
20231101.sw_2368_2
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kampala
|
Kampala
|
Kitovu cha kwanza kilikuwa nyumba ya kifalme kwenye kilima cha Kasubi iliyojengwa na Kabaka Mutesa I wa Buganda mnamo mwaka 1882. Baada ya kifo chake Mutesa ikawa kaburi la kifalme. Ikulu mpya ya Kabaka Mwanga II ikajengwa karibu kwenye kilima cha Mengo.
|
20231101.sw_2368_3
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kampala
|
Kampala
|
Mwaka 1890 mwakilishi wa Kampuni ya Kifalme ya Uingereza kwa Afrika ya Mashariki (IBEA, kifupi kwa Imperial British East Africa Company), Frederick Lugard aliingilia vita vya wenyewe kwa wenyewe kati ya Waganda Waprotestanti, Wakatoliki na Waislamu, akajenga boma juu ya kilima kilichoitwa "Kampala" kikawa kitovu cha makao ya Wazungu katika mji mpya.
|
20231101.sw_2368_4
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kampala
|
Kampala
|
Wamisionari wakapewa na Kabaka nafasi ya kujenga makanisa na nyumba zao kwenye vilima mbalimbali: Namirembe ikawa kilima cha Waanglikana, Rubaga kilima cha Wakatoliki. Waislamu walikuwa na eneo lao hasa kwenye kilima cha Kibuli.
|
20231101.sw_2368_5
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kampala
|
Kampala
|
Kati ya 1900 hadi 1905 Kampala ikawa makao makuu ya utawala wa kikoloni wa Uingereza uliohamishwa baadaye kwenda Entebbe.
|
20231101.sw_2368_6
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kampala
|
Kampala
|
Utawala wa Idi Amin na vita vya kumpindua 1979 uliharibu mengi, kwanza tabaka la wafanyabiashara Wahindi pamoja na nguvu ya kiuchumi, baadaye pia majengo.
|
20231101.sw_2368_7
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kampala
|
Kampala
|
Kampala ina Chuo Kikuu katika mtaa wa Makerere kilichokuwa chuo kikuu cha kwanza katika Afrika ya Mashariki na mahali pa mafunzo kwa viongozi wengi wa Kiafrika upande wa siasa, utamaduni na uchumi.
|
20231101.sw_2369_0
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Italia
|
Italia
|
Jamhuri ya Italia (kwa Kiitalia: Repubblica Italiana) ni nchi ya Ulaya Kusini inayoenea katika sehemu kubwa ya Rasi ya Italia na baadhi ya visiwa vya jirani kwenye Bahari ya Kati.
|
20231101.sw_2369_1
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Italia
|
Italia
|
Eneo lake ni km² 302,072.84 ambalo lina wakazi 59,236,213 (31-12-2020): ni nchi ya 23 duniani kwa wingi wa watu, lakini ya 8 au 9 kwa uchumi. Mtu anayetokea katika nchi hii ya Italia kwa Kiswahili huitwa Mwitalia.
|
20231101.sw_2369_2
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Italia
|
Italia
|
Imepakana na Ufaransa, Uswisi, Austria na Slovenia. Nchi huru mbili ndogo zinazozungukwa na eneo la Italia pande zote ni San Marino na Vatikano.
|
20231101.sw_2369_3
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Italia
|
Italia
|
Umbo la jamhuri, kama lile la rasi yake, linafanana na mguu linalozungukwa na maji ya Mediteraneo pande tatu.
|
20231101.sw_2369_4
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Italia
|
Italia
|
Milima ya Appennini inaunda uti wa mgongo wake, wakati ile ya Alpi, ambayo ni mirefu zaidi, inaunda kwa kiasi kikubwa mpaka kati ya Italia na nchi nyingine za Ulaya.
|
20231101.sw_2369_5
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Italia
|
Italia
|
Mlima mrefu zaidi, ukiwa na mita 4,810 juu ya usawa wa bahari, unaitwa Monte Bianco (Mlima Mweupe) na uko mpakani kwa Ufaransa.
|
20231101.sw_2369_6
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Italia
|
Italia
|
Visiwa viwili vikubwa vya Sisilia na Sardinia ni sehemu za Italia pamoja na visiwa vingi vidogovidogo, vile vya Pelagie vikiwa upande wa Afrika.
|
20231101.sw_2369_7
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Italia
|
Italia
|
Italia ina volkeno 14, ambazo 4 kati yake ziko hai: ile ndefu zaidi kuliko zote za Ulaya (mita 3,329) inaitwa Etna na iko mashariki mwa Sisilia. Italia inaongoza Ulaya kwa wingi wa matetemeko ya ardhi.
|
20231101.sw_2369_8
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Italia
|
Italia
|
Mto mrefu zaidi unaitwa Po na una urefu wa kilomita 652. Mito mingine mirefu ni Adige, Tevere, Adda, Oglio, Tanaro, Ticino, Arno, Piave, Reno, Sarca-Mincio n.k.
|
20231101.sw_2369_9
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Italia
|
Italia
|
Maziwa makubwa zaidi ni: Garda (km2 367.94), Ziwa Maggiore (212.51, likiingia Uswisi), Ziwa la Como (145.9), Trasimeno (124.29) na Ziwa la Bolsena (113.55).
|
20231101.sw_2369_10
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Italia
|
Italia
|
Kutokana na urefu mkubwa wa Italia toka kaskazini hadi kusini, hali ya hewa ni tofauti sana, kuanzia baridi kali sana hadi joto kali sana.
|
20231101.sw_2369_11
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Italia
|
Italia
|
Akiolojia imethibitisha uwepo wa Homo neanderthaliensis miaka 128,000-187,000 hivi iliyopita. Homo sapiens sapiens alifika miaka 40,000 hivi iliyopita.
|
20231101.sw_2369_12
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Italia
|
Italia
|
Kufikia milenia ya 1 KK wakazi wengi walikuwa wa jamii ya Kizungu na kutumia lugha za Kihindi-Kiulaya.
|
20231101.sw_2369_13
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Italia
|
Italia
|
Peninsula ya Italia iliunganishwa mara ya kwanza na Jamhuri ya Roma (509-27 KK), lakini hiyo ilipoenea Ulaya kusini na magharibi, Afrika ya Kaskazini na Asia ya Magharibi ikawa na sura ya kimataifa kama Dola la Roma.
|
20231101.sw_2369_14
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Italia
|
Italia
|
Umoja ulipotea kuanzia uvamizi wa jiji la Roma uliofanywa na Wagermanik (476 BK) na hasa baada ya ufalme wa Karolo Mkuu aliyetawala sehemu ya kaskazini tu.
|
20231101.sw_2369_15
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Italia
|
Italia
|
Juhudi za kuurudisha umoja zilifanywa hasa katika karne ya 19, ambapo Ufalme wa Sardinia uliteka sehemu kubwa ya Italia (hasa miaka 1860, 1866 na 1870) na kubadilika kuwa Ufalme wa Italia wenye makao makuu Roma.
|
20231101.sw_2369_16
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Italia
|
Italia
|
Ni kati ya nchi sita zilizoanzisha Umoja wa Ulaya mwaka 1957 ikaendelea kuunga mkono ustawi wake hadi uanzishaji wa pesa ya pamoja (Euro).
|
20231101.sw_2369_17
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Italia
|
Italia
|
Italia ni kati ya nchi zilizoendelea, ikiwa na nafasi ya nane kwa nguvu ya uchumi duniani, hivyo ni mwanachama wa G7, G8 na G20.
|
20231101.sw_2369_18
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Italia
|
Italia
|
Italia ndiyo nchi inayongoza duniani kwa kuwa na mahali pengi (51) pa kimaumbile na pa kihistoria palipoingizwa katika orodha ya UNESCO ya "Urithi wa Dunia".
|
20231101.sw_2369_19
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Italia
|
Italia
|
Wananchi wana sifa za pekee kati ya Wazungu wote, hata upande wa DNA, kutokana na jiografia na historia ya rasi.
|
20231101.sw_2369_20
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Italia
|
Italia
|
Ni kati ya nchi ambamo watu wanatarajiwa kuishi miaka mingi zaidi, lakini pia ni kati ya nchi ambapo uzazi ni mdogo zaidi: wanaokufa ni wengi kuliko wanaozaliwa.
|
20231101.sw_2369_21
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Italia
|
Italia
|
Kutokana na umati wa Waitalia waliohama nchi hiyo karne za nyuma, sasa zaidi ya watu milioni 60 nje ya Italia wana asili ya nchi hiyo, mbali na raia zaidi ya milioni 4 wanaoishi nje.
|
20231101.sw_2369_22
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Italia
|
Italia
|
Lugha rasmi ni Kiitalia, inayotegemea zaidi lahaja za Italia ya Kati, lakini siku hizi inatumiwa na wananchi walio wengi hata katika mikoa mingine, ambayo kwa jumla ni 20.
|
20231101.sw_2369_23
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Italia
|
Italia
|
Upande wa dini, wengi wao (81.2%) ni Wakristo wa Kanisa Katoliki, wakifuatwa na Waorthodoksi (2.8%, wengi wao wakiwa wahamiaji, hasa kutoka Romania) na Waprotestanti (1.1%, wengi wao wakiwa Wapentekoste). Uhamiaji mwingi wa miaka ya mwisho wa karne ya 20 umeleta pia Uislamu (3.7%) na dini nyingine.
|
20231101.sw_2369_24
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Italia
|
Italia
|
Dini zote zinaachiwa uhuru na, tofauti na nchi nyingi za Ulaya, waumini wake wanajitahidi kiasi kufuata ibada (29% kila wiki).
|
20231101.sw_2373_0
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Gideon%20Byamugisha
|
Gideon Byamugisha
|
Gideon Byamugisha ni kasisi Mwanglikana wa Uganda na mchungaji wa kwanza Mwafrika aliyetangaza wazi ya kwamba ameambukizwa UKIMWI.
|
20231101.sw_2373_1
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Gideon%20Byamugisha
|
Gideon Byamugisha
|
Alizaliwa Buranga Ndorwa, Wilaya ya Kabale, Uganda wa Magharibi tarehe 29 Agosti 1959 akasomea ualimu kwenye Chuo Kikuu cha Makerere akamaliza kwa digrii mwaka 1985.
|
20231101.sw_2373_2
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Gideon%20Byamugisha
|
Gideon Byamugisha
|
Akaendelea kusoma digrii ya theolojia huko Nairobi akapokelewa katika utumishi wa Kanisa la Kianglikana Uganda mwaka 1991. Mwaka uleule mke wake alikufa kutokana na UKIMWI.
|
20231101.sw_2373_3
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Gideon%20Byamugisha
|
Gideon Byamugisha
|
1992 alipokea baraka ngazi ya ukasisi akapewa jukumu la kufundisha chuo cha theolojia Mukono (sasa: Chuo Kikuu cha Kikristo cha Uganda). Wakati ule alifuata ushauri kutafuta upimaji wa damu yake ahakikishe hana UKIMWI. Alipopimwa akaonekana kuwa na viini vya HIV vilevile. Aliambiwa matokeo dakika chache tu kabla ya kuwa na somo chuoni. Aliamua kuwaambia wasikilizaji wake wakiwa na walimu wenzake ya kuwa amepatikana na HIV.
|
20231101.sw_2373_4
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Gideon%20Byamugisha
|
Gideon Byamugisha
|
Tangazo hili lilipokelewa kwa mshangao kwani katika utamaduni wa kiafrika na zaidi katika utamaduni wa kidini wa Afrika haikuwahi kutokea ya kwamba kiongozi wa kidini anasema waziwazi kuwa ameambukizwa UKIMWI. Kinyume chake mara nyingi wahubiri walitumia mfano wa UKIMWI kuonyesha ya kuwa ni adhabu kutoka Mungu na dalili ya dhambi.
|
20231101.sw_2373_5
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Gideon%20Byamugisha
|
Gideon Byamugisha
|
Gideoni Byamugisha aliitwa na kanisa lake kuanzia mwaka 1993 kusaidia katika mradi wa UKIMWI wa kanisa. 1995 - 2002 aliongoza idara wa HIV/UKIMWI ya dayosisi ya Kianglikana ya Namirembe.
|
20231101.sw_2373_6
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Gideon%20Byamugisha
|
Gideon Byamugisha
|
Mwaka 1995 alifunga ndoa mara ya pili akimwoa Pamela aliyekuwa mjane wakati ule kutokana na UKIMWI akipatikana mwenyewe na viini vya HIV. Wanalea watoto wao kutoka ndoa zote mbili za awali pia wakamzaa mtoto wa pamoja asiye na HIV kutokana na tibu la madawa ya ARV.
|
20231101.sw_2373_7
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Gideon%20Byamugisha
|
Gideon Byamugisha
|
Siku hizi (2005) Byamugisha anafanya kazi na shirika la Word Vision International pia pamoja na kasisi Jape Heath kutoka Afrika Kusini ameunda "Umoja wa viongozi wa kidini wa Afrika wanaoishi na UKIMWI" (ANERELA African Network of Religious Leaders living with HIV/AIDS).
|
Subsets and Splits
No community queries yet
The top public SQL queries from the community will appear here once available.