_id
stringlengths
15
22
url
stringlengths
31
150
title
stringlengths
1
86
text
stringlengths
100
23.8k
20231101.sw_2326_3
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mkoa%20wa%20Unguja%20Kaskazini
Mkoa wa Unguja Kaskazini
Upande wa magharibi utalii umeanza kuwa muhimu. Eneo la Ras Nungwi ni sehemu moja yenye mahoteli ya watalii wa nje.
20231101.sw_2327_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/Tikisa
Tikisa
Wana mkia mrefu ambao wanautikisa mara kwa mara. Ndege hao ni wadogo na wembamba na spishi kadhaa zina rangi nzuri.
20231101.sw_2328_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mkoa%20wa%20Unguja%20Kusini
Mkoa wa Unguja Kusini
Mkoa wa Unguja Kusini ni mmojawapo kati ya mikoa 31 ya Tanzania wenye postikodi namba 72000 na uko kwenye kisiwa cha Unguja.
20231101.sw_2328_1
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mkoa%20wa%20Unguja%20Kusini
Mkoa wa Unguja Kusini
Mwaka 2012 walikuwa 115,588 katika wilaya mbili ikiwa Wilaya ya Kati ina wakazi 73,346 na Wilaya ya Kusini ina wakazi 39,242.
20231101.sw_2328_2
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mkoa%20wa%20Unguja%20Kusini
Mkoa wa Unguja Kusini
Wakazi wa eneo hili la kisiwa cha Unguja, mbali na kujishughulisha na uvuvi kwenye Bahari ya Hindi, ni maarufu pia kwa kilimo cha zao la karafuu, zao linalokifanya Kisiwa cha Zanzibar kujulikana zaidi kama kisiwa cha viungo.
20231101.sw_2336_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/Joseph%20Hill
Joseph Hill
Joseph Hill (22 Januari 1949 – 19 Agosti 2006) alikuwa mtunzi na mwimbaji wa Reggae toka nchini Jamaika. Alianza muziki katika kundi lijulikanalo kama The Soul Defender lililokuwa na makazi yake kitongoji cha St Catherine. Baadaye akaanzisha kundi la Culture akiwa na Telford Nelson na Albert Walker. Mwaka 1977 walitoa wimbo uliovuma sana uitwao Two Sevens Clash ambao ulizungumzia herufi mbili za 7 katika mwaka 1977. Hadi sasa Joseph Hill na wenzake wametoa album 22. Falsafa ya nyimbo za Joseph Hill ni ya kimapinduzi na kiroho inayopinga utumwa na ukosefu wa maadili na ucha mungu. Joseph Hill ni muumini wa imani na utamaduni wa Kirastafari. Katika wimbo wake wa wa PAY DAY anauliza ni lini watu walioumizwa na utumwa watalipwa. Pia amepinga aina zote za ukoloni na kumzumgumzia Chistopher Columbas kama muongo kwa kusema kwamba amegundua visiwa vya Jamaika ambavyo vilikuwapo tayari na watu. Joseph Hill pia anaenzi kitabu Bibilia anachoamini kuwa ni kitakatifu na amekuwa akitumia mistari na manabii toka kwenye Biblia kwenye nyimbo zake, kwa mfano wimbo wake kuhusu nabii Eliya.
20231101.sw_2338_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mkoa%20wa%20Kaskazini-Mashariki%20%28Kenya%29
Mkoa wa Kaskazini-Mashariki (Kenya)
Kaskazini-Mashariki ulikuwa mmoja kati ya mikoa 9 ya Kenya. Eneo lake lilikuwa km² 127 000 na wakazi 962,143 (sensa ya 1999).
20231101.sw_2338_1
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mkoa%20wa%20Kaskazini-Mashariki%20%28Kenya%29
Mkoa wa Kaskazini-Mashariki (Kenya)
Wakati wa ukoloni eneo hilo liliitwa "Northern Frontier District" (Eneo la mpakani wa kaskazini) likitawaliwa pekee na sehemu kubwa ya Kenya.
20231101.sw_2338_2
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mkoa%20wa%20Kaskazini-Mashariki%20%28Kenya%29
Mkoa wa Kaskazini-Mashariki (Kenya)
Wakazi walio wengi ni Wasomalia kwa lugha na utamaduni; kuwepo kwao ndani ya Kenya badala ya Somalia ni urithi wa mipaka ya kikoloni. Wengine ni Waborana, Warendille na Waturkana.
20231101.sw_2338_3
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mkoa%20wa%20Kaskazini-Mashariki%20%28Kenya%29
Mkoa wa Kaskazini-Mashariki (Kenya)
Eneo hili ni kavu sana. Mbali na bonde la mto Tana na maeneo mengine madogo, mkoa haufai kwa kilimo. Wakazi walio wengi hujipatia riziki kutokana na ufugaji.
20231101.sw_2339_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ali%20Farka%20Toure
Ali Farka Toure
Ali Farka Touré ni mmoja wa wanamuziki mahiri barani Afrika. Alizaliwa jijini Bamako nchini Mali mwaka 1939. Jina lake hasa ni Ali Ibrahim Touré. Muziki wa Ali Farka Touré ni mchanganyiko wa muziki wa asili wa Mali na muziki wa Amerika ya Kaskazini hasa blues.
20231101.sw_2339_1
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ali%20Farka%20Toure
Ali Farka Toure
Touré alizaliwa katika kijiji cha Kanau katika ukingo wa mto Niger, kaskazini magharibi mwa nchi ya Mali. Mama yake alikuwa na watoto kumi ambapo ndugu zake wote walifariki wakiwa wachanga. Jina la "Farka" ni jina la utani ambalo alipewa na wazazi wake likimaanisha mnyama punda kutokana na kuwa na msimamo mkali na kiburi.
20231101.sw_2339_2
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ali%20Farka%20Toure
Ali Farka Toure
Muziki wa Touré una nguvu kama za miujiza. Wapenzi wake dunia nzima wamelogwa na upigaji wake wa gitaa. Mara nyingi nyimbo zake amekuwa akiimba kwa lugha za Kisonghai, Kifula, na Kitamasheck. Albamu yake iitwayo Talking Timbukuta, ambayo aliitoa kwa kushirikiana na mwanamuziki Ry Cooder, iliuzwa na kumpatia umaarufu mkubwa hasa katika soko la muziki la nchi za Magharibi. Mwaka 2005 alitoa albamu ya In the Heart of the Moon akishirikiana na mwanamuziki Toumani Diabaté. Albamu hii ilimpatia tuzo ya Grammy.
20231101.sw_2339_3
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ali%20Farka%20Toure
Ali Farka Toure
Pamoja na muziki, Ali Farka Touré alikuwa akijihusisha na masuala ya kisiasa. Mwaka 2004 alichaguliwa kuwa meya wa mji wa Niafunké.
20231101.sw_2340_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/Rupia
Rupia
Neno "rupia" limetokana na lugha ya Kihindi cha kale "rūp" au "rūpā" linalomaanisha "fedha". Katika lugha ya Sanskrit "rupyakam" (रूप्यकम्) inamaanisha sarafu ya fedha. Hii ni asili ya "Rūpaya" iliyotumika katika India kama sarafu yenye gramu 11.66 za fedha tangu mwaka 1540. Rupia moja ilikuwa na Anna 16, Paisa 64 au Pai 192.
20231101.sw_2340_1
https://sw.wikipedia.org/wiki/Rupia
Rupia
Kwenye eneo la India ya leo katika makoloni ya nchi zifuatazo: Denmark, Ufaransa na Ureno, pia katika madola mbalimbali ya Kihindi kabla ya ukoloni na kabla ya uhuru kama vile Hyderabad.
20231101.sw_2341_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/Afrika%20ya%20Mashariki%20ya%20Kiingereza
Afrika ya Mashariki ya Kiingereza
Afrika ya Mashariki ya Kiingereza (kwa Kiingereza British East Africa Protectorate) lilikuwa jina la eneo la Kenya lililowekwa chini ya utawala wa ulinzi wa Uingereza kuanzia mwaka 1895 hadi 1920 BK kama mtangulizi wa koloni la Kiingereza la Kenya.
20231101.sw_2341_1
https://sw.wikipedia.org/wiki/Afrika%20ya%20Mashariki%20ya%20Kiingereza
Afrika ya Mashariki ya Kiingereza
Wakati wa mashindano ya kugawa Afrika kati ya madola ya Ulaya, Kampuni ya Kifalme ya Kiingereza kwa Afrika ya Mashariki ilianza shughuli zake katika eneo hili kwa kibali cha sultani wa Zanzibar kuanzia mwaka 1888.
20231101.sw_2341_2
https://sw.wikipedia.org/wiki/Afrika%20ya%20Mashariki%20ya%20Kiingereza
Afrika ya Mashariki ya Kiingereza
Kampuni hiyo ilitakiwa kuwa na mamlaka juu ya eneo hili kwa kusudi la kufanya biashara, lakini uwezo wake haukutosha kutimiza shughuli, hasa maandalizi ya kujenga reli ya Uganda kati ya Mombasa na Kampala.
20231101.sw_2341_3
https://sw.wikipedia.org/wiki/Afrika%20ya%20Mashariki%20ya%20Kiingereza
Afrika ya Mashariki ya Kiingereza
Baada ya kuazimia kujenga reli, Uingereza iliona haja ya kulinda eneo la reli hiyo: ndipo ikatangaza eneo lote kati ya Mombasa na Uganda kuwa chini ya ulinzi wake kuanzia tarehe 1 Julai 1895. Huo ndio mwanzo wa Afrika ya Mashariki ya Kiingereza ambaye baadaye iliitwa Kenya.
20231101.sw_2341_4
https://sw.wikipedia.org/wiki/Afrika%20ya%20Mashariki%20ya%20Kiingereza
Afrika ya Mashariki ya Kiingereza
Eneo hilo baadaye lilipanuliwa zaidi hadi kukutana na maeneo yaliyokuwa chini ya utawala wa Italia (Somalia) na Ethiopia upande wa Kaskazini, utawala wa ushirikiano wa Misri na Uingereza (Sudan). Upande wa kusini mpaka ulifuata mapatano na Afrika ya Mashariki ya Kijerumani.
20231101.sw_2341_5
https://sw.wikipedia.org/wiki/Afrika%20ya%20Mashariki%20ya%20Kiingereza
Afrika ya Mashariki ya Kiingereza
Mpaka na eneo chini ya utawala wa ulinzi wa Uganda ulisahihishwa mwaka 1905; hadi wakati ule sehemu kubwa ya eneo la Kenya ya Magharibi ya leo ilihesabiwa kuwa upande wa Uganda.
20231101.sw_2343_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/Siti%20Binti%20Saad
Siti Binti Saad
Siti binti Saad (alizaliwa Fumba, Zanzibari, 1880 akapewa jina la 'Mtumwa' kwa vile alizaliwa kipindi cha utumwa wa Kiarabu. Jina la Siti alipewa na kabaila mmoja wa Kiarabu) alikuwa mwimbaji wa Zanzibar.
20231101.sw_2343_1
https://sw.wikipedia.org/wiki/Siti%20Binti%20Saad
Siti Binti Saad
Baba yake bwana Saadi alikuwa ni Mnyamwezi kutoka Tabora na mama yake alikuwa Mzigua toka Tanga, lakini wote wawili walizaliwa Zanzibar. Hali ya maisha ya familia yao ilikuwa ni duni sana na walijishughulisha zaidi katika shughuli za kilimo na ufinyanzi kazi ambazo Siti alijifunza na kuzimudu vizuri pia.
20231101.sw_2343_2
https://sw.wikipedia.org/wiki/Siti%20Binti%20Saad
Siti Binti Saad
Kama Waswahili wasemavyo "kuzaliwa masikini si kufa masikini", Siti alibarikiwa kuwa na kipaji cha pekee cha uimbaji. Kipaji hiki kilimsaidia sana tangu siku za awali ya maisha yake kwani alitumia uimbaji wake kuuza vyungu vya mama yake alivyokuwa akimsaidia kuvitembeza. Siti alipoimba sauti yake iliweza kupaa na kusafiri kwa umbali wa maili nyingi na hii ndio ilikuwa ishara ya watu kujua kwamba vyungu vya kina Mtumwa vinapita leo. Alifananishwa kuwa na mapafu yenye nguvu kama ya simba kutokana na alivyoweza kupaza sauti yake mbali na bila kuachia pumzi.
20231101.sw_2343_3
https://sw.wikipedia.org/wiki/Siti%20Binti%20Saad
Siti Binti Saad
Kutokana na wakati huo elimu kwa watoto wa kike kutotiliwa mkazo, Siti hakuwahi kwenda shule wala kuhudhuria mafunzo ya Kurani. Hivyo mnamo mwaka 1911 aliona ni bora ahamie mjini ili kuboresha maisha yake zaidi. Ujio wake wa mjini ulikuwa wa neema kwani alikutana na bwana mmoja wa kundi la muziki wa Taarabu la "Nadi Ikhwani Safaa" aliyeitwa Muhsin Ali. Katika kipindi hicho, hilo ndilo lilikuwa kundi pekee la muziki wa taarabu lililoanzishwa na Sultani mpenda starehe na anasa bwana Seyyid Barghash Said. Kundi hili lilikuwa ni la wanaume peke yao, wanawake hawakuruhusiwa kujiunga na vikundi vya muziki kwa vile ilikuwa ikichukuliwa kama ni uhuni. Bwana Muhsin alikiona kipaji cha pekee cha Siti na hivyo akajitolea kumfundisha kuimba kwa kufuata vyombo vya muziki na lugha ya kiarabu. Baada ya hapo alikwenda kumtambulisha kwa wanamuziki wenzie wa "Nadi Ikhwani Safaa" ambao bila kusita wakaanza kufanya naye maonyesho mbalimbali katika jamii. Walipata mialiko mingi hasa kutoka kwa Sultani na matajiri wengine wa Kiarabu, pia katika harusi na sherehe zingine mbalimbali, inasemekana ulifika wakati ambapo sherehe ilishindwa kufana kama Siti binti Saadi hakuwepo kutumbuiza. Siti alikuwa ni moto wa kuotea mbali na jina lake lilivuma kwa haraka sana hadi nje ya mipaka ya nchi na bara la Afrika. Na punde Siti alianza kufananishwa na 'Umm Kulthum', mwimbaji mahiri wa kike aliyetamba wakati huo kutoka Misri.
20231101.sw_2343_4
https://sw.wikipedia.org/wiki/Siti%20Binti%20Saad
Siti Binti Saad
Kama nilivyosema moto wa Siti ulikuwa si wa kuusogelea karibu, mwaka 1928 kampuni ya kurekodi muziki ya Columbia and His Master's voice yenye makazi yake Mumbai India ilisikia umaarufu wa Siti binti Saadi na hivyo ikamwalika yeye pamoja na kundi lake kwenda kurekodi kwa lugha ya Kiswahili ili kujaribu kama muziki wake utauzika. Kampuni ile haikuweza kuamini jinsi muziki ule ulivyouzika kwa kasi kubwa kwani wastani wa santuri 900 ziliweza kuuzika katika kipindi cha miaka miwili ya mwanzo, na hadi kufikia 1931 santuri 72,000 zilikuwa zimeuzwa. Kutokana na kusambaa kwa santuri hizi, umaarufu wa Siti ulizidi mara dufu na watu kutoka sehemu mbalimbali za dunia walizuru Zanzibari kumwona. Mambo yalizidi kuwa mazuri kwa Siti hadi ikafikia hatua kampuni ya kurekodi ya Columbia kuamua kujenga studio ya kurekodi muziki palepale Zanzibar maalumu kwa ajili ya Siti binti Saadi.
20231101.sw_2343_5
https://sw.wikipedia.org/wiki/Siti%20Binti%20Saad
Siti Binti Saad
Hatua hiyo ya hadi kujengewa studio iliwaumiza wengi wenye wivu, hivyo wakaanza kumtungia nyimbo za kumkejeli ili kumshusha na hasa walitumia kigezo kwamba hana uzuri wa sura, nyimbo nyingi ziliimbwa lakini huu ndio uliovuma sana:
20231101.sw_2343_6
https://sw.wikipedia.org/wiki/Siti%20Binti%20Saad
Siti Binti Saad
Kwa kujibu shambulio hilo kwa namna yake aliwafunga midomo wale wote waliokuwa wakimkejeli. Siti pia alikuwa ni mwanamke wa kwanza mwanaharakati katika kipindi chake kwa kuwatetea wanawake na wanyonge kwa ujumla, kwani katika kipindi chake watu matajiri walikuwa wakiwaonea masikini na walipofikishwa mbele ya haki waliweza kutoa hongo na kuachiwa huru halafu wewe uliyeshitaki ndiye unayefungwa.
20231101.sw_2343_7
https://sw.wikipedia.org/wiki/Siti%20Binti%20Saad
Siti Binti Saad
Utunzi wake wa wimbo wa Kijiti ulimpatia sifa kubwa kwani ulikuwa ukielezea kisa cha kweli kilichomkuta mwanamke mmoja mgeni kutoka bara, mwanamke huyu alipofika alikutana na Tajiri mmoja ambaye alijifanya amempenda, hivyo akamchukua na kulala naye halafu baadaye akamuua. Tajiri yule alishitakiwa na bahati nzuri walikuwepo mashahidi wawili walioshuhudia tukio lile, lakini kwa vile ni Tajiri alitoa pesa na kesi ikawageukia wale mashahidi na kufungwa.
20231101.sw_2343_8
https://sw.wikipedia.org/wiki/Siti%20Binti%20Saad
Siti Binti Saad
Siti aliendelea kumwambia katika nyimbo zake kwamba asijethubutu kwenda Dar es Salaam kwa maana watu wenye hasira wanamsubiri na wameapa kwa ajili yake.
20231101.sw_2343_9
https://sw.wikipedia.org/wiki/Siti%20Binti%20Saad
Siti Binti Saad
Siti aliendelea na shughuli yake ya muziki hadi uzeeni, muda mfupi kabla ya kifo chake alikutana na mwandishi maarufu na mwanamashairi Shaaban Robert ambaye alimhoji na kuweza kuandika wasifu wake katika kitabu alichokiita " Wasifu wa Siti binti Saadi." Wasifu huu unaonekana kuwa ndio bora zaidi uliowahi kuandikwa katika fasihi ya Tanzania. Kitabu hiki kinatumika kufundishia shule za sekondari za Tanzania.
20231101.sw_2343_10
https://sw.wikipedia.org/wiki/Siti%20Binti%20Saad
Siti Binti Saad
Tarehe 8 Julai 1950 Siti binti Saadi alifariki dunia na kuacha pengo kubwa katika fani ya Taarabu. Ingawa pengo hilo haliwezi kuzibika lakini kuna watu wengi walioweza kuibuka na umaarufu wa kuimba taarabu kupitia kwake, mfano hai ni Bi Kidude.
20231101.sw_2343_11
https://sw.wikipedia.org/wiki/Siti%20Binti%20Saad
Siti Binti Saad
Hata baada ya kifo chake jina lake bado linatumika sana kama kielelezo cha ushujaa wake, Chama cha waandishi wa habari wanawake Tanzania (TAMWA), kimetumia jina lake kulipa jina gazeti la chama chao "Sauti ya Siti". Hadi leo hii Siti hutumika kama kipimo cha kufundishia uimbaji wa Taarabu. Na anakumbukwa katika historia yake ya kuwa mwanamke wa kwanza Afrika mashariki kurekodi muziki katika santuri.
20231101.sw_2345_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/Rwanda
Rwanda
Rwanda huitwa nchi ya vilima elfu (kwa Kinyarwanda: Igihugu cy'Imisozi Igihumbi; kwa Kifaransa: Pays de Mille Collines): ndivyo sehemu kubwa ya eneo lake inavyoonekana, hasa magharibi.
20231101.sw_2345_1
https://sw.wikipedia.org/wiki/Rwanda
Rwanda
Ni nyanda za juu na milima; sehemu kubwa ni mita 1500 juu ya UB. Milima kaskazini mwa nchi inapanda hadi mita 4507 juu ya UB. Kutokana na urefu huo hali ya hewa haina joto kali.
20231101.sw_2345_2
https://sw.wikipedia.org/wiki/Rwanda
Rwanda
Mpaka na Kongo ni hasa Ziwa Kivu ambalo ni mojawapo kati ya maziwa ya bonde la ufa la Afrika ya Mashariki.
20231101.sw_2345_3
https://sw.wikipedia.org/wiki/Rwanda
Rwanda
Huko kuna mazingira ya pekee duniani yenye sokwe wa milimani. Wako hatarini kuangamizwa kutokana na uwindaji na upanuzi wa mashamba unaopunguza mazingira wanamoishi.
20231101.sw_2345_4
https://sw.wikipedia.org/wiki/Rwanda
Rwanda
Miji mikubwa zaidi ndiyo: Kigali wakazi 745.261, Butare wakazi 89.800, Gitarama wakazi 87.613, Ruhengeri wakazi 86.685 na Gisenyi wakazi 83.623.(namba za Januari 2005)
20231101.sw_2345_5
https://sw.wikipedia.org/wiki/Rwanda
Rwanda
Gisenyi ni mji kwenye ncha ya kaskazini ya Ziwa la Kivu mpakani kwa Kongo ukiwa jirani na mji wa Goma. Kuna usafiri wa mashua kwenda Kibuye na Cyangugu.
20231101.sw_2345_6
https://sw.wikipedia.org/wiki/Rwanda
Rwanda
Kibuye ni mji mdogo ufukoni mwa Ziwa la Kivu. Una wavuvi wengi, kituo cha watalii na nyumba za kihistoria za wamisionari. Hadi mwaka 1994 Watutsi 250,000 waliishi katika wilaya ya Kibuye, lakini tangu uangamizaji wa Watutsi katika vita vya wenyewe kwa wenyewe wamebaki 8000 pekee.
20231101.sw_2345_7
https://sw.wikipedia.org/wiki/Rwanda
Rwanda
Wakazi wa Rwanda ni zaidi ya milioni 11. Banyarwanda milioni 2 wako Uganda na wengi zaidi Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
20231101.sw_2345_8
https://sw.wikipedia.org/wiki/Rwanda
Rwanda
Kwa kawaida vikundi vitatu hutajwa kuwa wakazi wa Rwanda ndio Wahutu, Watutsi, Watwa. Lakini kuna tofauti kali kati ya mawazo kama vikundi hivyo ni makabila, mataifa ya pekee au matabaka ya kijamii. Hali halisi wanatumia lugha ileile ya Kinyarwanda na wanafuata utamaduni uleule.
20231101.sw_2345_9
https://sw.wikipedia.org/wiki/Rwanda
Rwanda
Wanahistoria wengi wanasema ya kuwa Watwa walikuwa wakazi wa kwanza wakiwa wawindaji, Wahutu ndio wakulima wa Kibantu waliopatikana kwa uenezi wa Wabantu katika Afrika ya Kati na mababu wa Watutsi waliingia kama wafugaji kutoka kaskazini.
20231101.sw_2345_10
https://sw.wikipedia.org/wiki/Rwanda
Rwanda
Watutsi walikuwa tabaka la kikabaila, pia mfalme alikuwa Mtutsi. Lakini wengine wanaamini ya kwamba vikundi vyote vitatu vilijitokeza nchini si kama tokeo la uhamiaji mbalimbali lakini zaidi kama matabaka yaliyotofautiana kikazi: wakulima, wavindaji na wafugaji waliokuwa pia askari wa mfalme.
20231101.sw_2345_11
https://sw.wikipedia.org/wiki/Rwanda
Rwanda
Wakati wa ukoloni Wabelgiji walihesabu mwaka 1931 wakazi wa nchi kama ifuatavyo: 84 % Wahutu, 15 % Watutsi na 1 % Watwa.
20231101.sw_2345_12
https://sw.wikipedia.org/wiki/Rwanda
Rwanda
Kabla ya uhuru vilitokea kwa mara ya kwanza vita vya wenyewe kwa wenyewe kati ya makabila mawili makubwa viliyosababisha kupungua kwa Watutsi kutokana na mauaji na zaidi kwa Watutsi kukimbilia nchi jirani. Mnamo 1990 asilimia ya Watutsi ilikadiriwa kuwa 9 - 10 %.
20231101.sw_2345_13
https://sw.wikipedia.org/wiki/Rwanda
Rwanda
Vita vya wenyewe kwa wenyewe vya miaka ya 1990 vilileta uangamizaji mkubwa wa Watutsi. Kati ya asilimia 75 hadi 90 za wakazi Watutsi waliuawa katika wiki chache za mwaka 1994. Baada ya mwisho wa vita Watutsi wengi ambao wenyewe au wazazi wao walikuwa wamekimbilia Uganda na Tanzania walirudi tena Rwanda.
20231101.sw_2345_14
https://sw.wikipedia.org/wiki/Rwanda
Rwanda
Kwa wastani kuna wakazi 300 kwa kilomita ya mraba ambayo ni msongamano mkubwa kabisa katika Afrika. Karibu nusu ya wakazi ni watoto hadi umri wa miaka 14.
20231101.sw_2345_15
https://sw.wikipedia.org/wiki/Rwanda
Rwanda
Lugha ya taifa, lugha rasmi na lugha ya mama kwa Wanyarwanda wote ni Kinyarwanda ambayo ni lugha ya Kibantu, mojawapo ya Niger-Kongo.
20231101.sw_2345_16
https://sw.wikipedia.org/wiki/Rwanda
Rwanda
Lugha rasmi tangu enzi za ukoloni ni Kifaransa. Tangu mwaka 1994 serikali mpya, iliyoongozwa na Watutsi walioishi miaka mingi Uganda, imetumia pia Kiingereza kama lugha rasmi ya tatu.
20231101.sw_2345_17
https://sw.wikipedia.org/wiki/Rwanda
Rwanda
Kadiri ya sensa ya mwaka 2012 wakazi wengi ni Wakristo, hasa Waprotestanti (49.5%) na Wakatoliki (43.7%). Waislamu ni 2%.
20231101.sw_2345_18
https://sw.wikipedia.org/wiki/Rwanda
Rwanda
Kwa sasa serikali inazidi kufungia maabadi. Miezi saba ya kwanza ya mwaka 2018, imefungia tayari makanisa 8,000.
20231101.sw_2345_19
https://sw.wikipedia.org/wiki/Rwanda
Rwanda
Mwanzo wa karne ya 20 ilikuwa sehemu ya Afrika ya Mashariki ya Kijerumani na sababu ya mzozo kati ya Ujerumani na Ubelgiji.
20231101.sw_2345_20
https://sw.wikipedia.org/wiki/Rwanda
Rwanda
Uhuru katika mwaka 1961 ulifika pamoja na vita vya wenyewe kwa wenyewe kati ya Wahutu na Watutsi. Uhusiano kati ya vikundi hivi viwili uliendelea kuwa vigumu.
20231101.sw_2345_21
https://sw.wikipedia.org/wiki/Rwanda
Rwanda
Kuuawa kwa rais Juvenal Habariyama mwaka 1994 kulisababisha mauaji ya watu karibu milioni moja (walau 600,000) kati ya Watutsi, Watwa pamoja na Wahutu wasio na msimamo mkali.
20231101.sw_2345_22
https://sw.wikipedia.org/wiki/Rwanda
Rwanda
Rwanda pamoja na Burundi zilijiunga na Kenya, Uganda na Tanzania kama wanashirika wa Jumuia ya Afrika Mashariki kwa maendeleo muhimu katika elimu, afya, uchumi na mambo mbalimbali. Mwaka 2017 bunge la Rwanda liliamua kufanya Kiswahili kuwa moja ya lugha rasmi nchini.
20231101.sw_2345_23
https://sw.wikipedia.org/wiki/Rwanda
Rwanda
Vita vya Kongo vilivyokuwa na majeshi ya mataifa mbalimbali (Kivu Conflict) vilimalizika mwaka 2012.
20231101.sw_2347_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/Malawi
Malawi
Malawi (wakati wa ukoloni iliitwa Unyasa au Nyasaland) ni nchi ya bara la Afrika iliyopo kusini-mashariki, ikipakana na Tanzania, Msumbiji na Zambia.
20231101.sw_2347_1
https://sw.wikipedia.org/wiki/Malawi
Malawi
Sehemu kubwa ya eneo lake ni ziwa linaloitwa na majirani "Ziwa Nyasa" au "Niassa", lakini "Ziwa Malawi" hapa nchini. Kati ya Malawi na Tanzania kuna mzozo kuhusu eneo la ziwa ambao unazidi kufanyiwa kazi.
20231101.sw_2347_2
https://sw.wikipedia.org/wiki/Malawi
Malawi
Katika karne ya 10 BK walifika Wabantu wenye ujuzi wa kilimo na uhunzi. Wengi walizidi kuelekea kusini, lakini wengine walihamia nchini.
20231101.sw_2347_3
https://sw.wikipedia.org/wiki/Malawi
Malawi
Hakuna habari za kimaandishi kabla ya kufika kwa Wazungu. Tangu karne ya 16 ufalme wa Wamaravi ulikuwepo upande wa kusini wa ziwa. Wamaravi walipanua utawala wao. Lakini katika karne ya 19 walishambuliwa sana na Wayao walioendesha biashara ya watumwa wakiwakamata katika eneo la ziwa na kuwapeleka hadi pwani ya Bahari Hindi kama vile Kilwa.
20231101.sw_2347_4
https://sw.wikipedia.org/wiki/Malawi
Malawi
Wamisionari walimfuata, hasa Wapresbiteri kutoka Uskoti, waliotafuta wafuasi wa Ukristo na kumpambana na wafanyabiashara ya utumwa.
20231101.sw_2347_5
https://sw.wikipedia.org/wiki/Malawi
Malawi
Mwaka 1891 serikali ya Uingereza iliweka nchi upande wa magharibi na kusini kwa ziwa chini ya ulinzi wake ikawa „Nyassaland Protectorate“, halafu tangu 1907 koloni la Unyasa.
20231101.sw_2347_6
https://sw.wikipedia.org/wiki/Malawi
Malawi
Wakati wa Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia Waingereza waliogopa kushambuliwa kutoka Afrika ya Mashariki ya Kijerumani wakachukua hatua za kudai huduma za nyongeza kutoka kwa wananchi. Hii ilisababisha ghasia ya John Chilembwe dhidi ya wakoloni.
20231101.sw_2347_7
https://sw.wikipedia.org/wiki/Malawi
Malawi
Baada ya Vita Kuu ya Pili ya Dunia Waingereza waliunganisha Unyasa na Rhodesia (leo Zambia na Zimbabwe) kuwa Shirikisho la Afrika ya Kati mwaka 1953. Shirikisho hilo halikudumu hadi mwisho wa ukoloni kutokana mielekeo tofautitofauti katika sehemu tatu za shirikisho.
20231101.sw_2347_8
https://sw.wikipedia.org/wiki/Malawi
Malawi
Katika Unyasa daktari Hastings Kamuzu Banda alijitokeza kuwa mwanasiasa aliyependelewa na wananchi wengi, akawa waziri mkuu wakati wa Unyasa kupata madaraka ya kujitawala katika mambo ya ndani na baadaye rais wa kwanza wa taifa.
20231101.sw_2347_9
https://sw.wikipedia.org/wiki/Malawi
Malawi
Mwaka 1964 Unyasa (Nyassaland) ilikuwa nchi huru kabisa lakini bado sehemu ya Jumuiya ya Madola chini ya malkia wa Uingereza kwa miaka miwili ya kwanza.
20231101.sw_2347_10
https://sw.wikipedia.org/wiki/Malawi
Malawi
Mwaka 1966 Banda alitangaza kura ya katiba mpya iliyopokewa na wananchi. Nchi ilipata jina la Malawi na chama cha Malawi Congress Party kikawa chama pekee.
20231101.sw_2347_11
https://sw.wikipedia.org/wiki/Malawi
Malawi
Mabadiliko ya kimataifa baada ya kuporomoka kwa Ukomunisti na ukuta wa Berlin miaka 1989/1990 yalileta shinikizo kote Afrika dhidi ya serikali zilizofuata mtindo wa chama kimoja. Shinikizo hilo lilimkuta Banda mzee na mgonjwa ilhali watu wa familia yake wakitawala kupitia yeye. Hali ya uchumi ilikuwa duni, rushwa na magendo juu.
20231101.sw_2347_12
https://sw.wikipedia.org/wiki/Malawi
Malawi
Mwaka 1993 serikali yake ililazimishwa kukubali kura ya wananchi wote walioamua kumaliza mfumo wa chama kimoja na kuanzisha kipindi kipya.
20231101.sw_2347_13
https://sw.wikipedia.org/wiki/Malawi
Malawi
Uchaguzi huru wa mwaka 1994 ulimaliza utawala wa MCP ukamfanya Bakili Muluzi wa United Democratic Front (UDF) ndiye rais aliyechaguliwa mara ya pili 1999.
20231101.sw_2347_14
https://sw.wikipedia.org/wiki/Malawi
Malawi
Katika uchaguzi wa mwaka 2004 alishinda tena mgombea wa UDF, ndiye Bingu Mutharika aliyeapishwa kuwa rais wa Malawi tarehe 24 Mei 2004 huko Blantyre.
20231101.sw_2347_15
https://sw.wikipedia.org/wiki/Malawi
Malawi
Malawi ilikuwa na siasa ya chama kimoja chini ya rais wa kwanza Hastings Kamuzu Banda tangu kupata uhuru mwaka 1964 na masahihisho ya katiba 1966.
20231101.sw_2347_16
https://sw.wikipedia.org/wiki/Malawi
Malawi
Kutokana na katiba ya 1995 rais wa taifa anayechaguliwa na wananchi ndiye mkuu wa dola pia mkuu wa serikali. Makamu wa rais anachaguliwa pamoja naye lakini rais ana haki ya kumteua makamu wa pili asiyetoka katika chama chake.
20231101.sw_2347_17
https://sw.wikipedia.org/wiki/Malawi
Malawi
Mahakama zinafuata mtindo wa Uingereza. Majaji huteuliwa kwa muda wa maisha; wanatakiwa kuwa huru na kutoathiriwa na siasa.
20231101.sw_2347_18
https://sw.wikipedia.org/wiki/Malawi
Malawi
Utawala hutekelezwa katika mikoa mitatu ya nchi zinazogawiwa katika wilaya 28. Wakuu wa mikoa na wilaya huteuliwa na serikali kuu.
20231101.sw_2347_19
https://sw.wikipedia.org/wiki/Malawi
Malawi
Serikali za mitaa zimeundwa na wilaya 28 katika maeneo matatu (Kaskazini, Kati na Kusini) yanayotawaliwa na Watawala wa Maeneo na Wakuu wa Wilaya ambao wanachaguliwa na serikali kuu.
20231101.sw_2347_20
https://sw.wikipedia.org/wiki/Malawi
Malawi
Uchaguzi wa kwanza wa Serikali za mitaa katika historia ya mfumo wa vyama vingi ulifanyika mnamo 21 Novemba 2000. UDF ilishinda asilimia 70 ya viti hivi katika uchaguzi huu.
20231101.sw_2347_21
https://sw.wikipedia.org/wiki/Malawi
Malawi
Wakazi wengi ni wa makabila ya Wabantu na wanatumia lugha za Kibantu, hasa Kichewa (zaidi ya 57%), lakini lugha rasmi ni Kiingereza.
20231101.sw_2347_22
https://sw.wikipedia.org/wiki/Malawi
Malawi
Upande wa dini, kadiri ya sensa ya mwaka 2018, wakazi wengi ni Wakristo (77.5%, kati yao Wakatoliki 17.2%), wakifuatwa na Waislamu (13.8%).
20231101.sw_2347_23
https://sw.wikipedia.org/wiki/Malawi
Malawi
Global Lives Project video recording of 24 hours of daily life of Edith Kaphuka in Ngwale Village, Malawi
20231101.sw_2351_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/Msumbiji
Msumbiji
Msumbiji iko ufukoni mwa Bahari Hindi ikipakana na Tanzania, Malawi, Zambia, Zimbabwe, Afrika Kusini na Eswatini.
20231101.sw_2351_1
https://sw.wikipedia.org/wiki/Msumbiji
Msumbiji
Jina la nchi limetokana na Kisiwa cha Msumbiji (kwa Kireno: Ilha de Moçambique) kilichokuwa boma na makao makuu ya Ureno kwenye pwani ya Afrika ya Mashariki.
20231101.sw_2351_2
https://sw.wikipedia.org/wiki/Msumbiji
Msumbiji
Tambarare ya pwani ni sehemu kubwa ya kusini mwa nchi, lakini kwenda kaskazini upana wake unapungua.
20231101.sw_2351_3
https://sw.wikipedia.org/wiki/Msumbiji
Msumbiji
Milima mirefu zaidi inajulikana kama Inyanga yenye mita 2500 juu ya UB: iko katika jimbo la Tete inayopakana na Zimbabwe, Zambia na Malawi.
20231101.sw_2351_4
https://sw.wikipedia.org/wiki/Msumbiji
Msumbiji
Mito iko mingi, mkubwa zaidi ukiwa ndio Zambezi, halafu Ruvuma mpakani kwa Tanzania, Save na Limpopo.
20231101.sw_2351_5
https://sw.wikipedia.org/wiki/Msumbiji
Msumbiji
Umbo la eneo la nchi ni refu sana: ni kilomita 2000 kutoka mpaka wa Tanzania upande wa kaskazini hadi Maputo iliyoko karibu na Uswazi na Afrika Kusini.
20231101.sw_2351_6
https://sw.wikipedia.org/wiki/Msumbiji
Msumbiji
Katika karne za kwanza BK walifika wahamiaji Wabantu wenye ujuzi wa kilimo na uhunzi ambao walimeza wakazi wa kwanza inavyothibitishwa na DNA.
20231101.sw_2351_7
https://sw.wikipedia.org/wiki/Msumbiji
Msumbiji
Haijulikani ni lini ya kwamba wafanyabiashara Waarabu walianza kufika ufukoni na kujenga vituo na miji yao. Lakini utamaduni wa Waswahili ulifika hadi sehemu za mwambao wa Msumbiji. Hadi leo aina ya Kiswahili inazungumzwa kwenye visiwa vya Kirimba.
20231101.sw_2351_8
https://sw.wikipedia.org/wiki/Msumbiji
Msumbiji
Mto wa Zambezi ilitumika kama njia ya mawasiliano na biashara kati ya Ufalme wa Mwene Mtapa (Zimbabwe) na wafanyabiashara wa pwani.
20231101.sw_2351_9
https://sw.wikipedia.org/wiki/Msumbiji
Msumbiji
Taarifa za kimaandishi zinaanza na kufika kwa Wareno. Mwaka 1498 Vasco da Gama alifika akiwa njiani kuelekea Bara Hindi.
20231101.sw_2351_10
https://sw.wikipedia.org/wiki/Msumbiji
Msumbiji
Baadaye Msumbiji ikawa koloni la Wareno hadi mwaka 1975 vita vya ukombozi vya miaka 1964-1974 vilipomalizika kwa ushindi.
20231101.sw_2351_11
https://sw.wikipedia.org/wiki/Msumbiji
Msumbiji
Nchini Msumbiji kuna makabila mengi sana, kama vile Wamakua, Wanyungwe, Wayao, Wamakonde na Watsonga.
20231101.sw_2351_12
https://sw.wikipedia.org/wiki/Msumbiji
Msumbiji
Kila kabila lina lugha yake, lakini lugha rasmi ni Kireno, ambacho kinaweza kuzungumzwa na 50.3% za wakazi, ingawa ni lugha ya nyumbani kwa 16.6% tu.
20231101.sw_2351_13
https://sw.wikipedia.org/wiki/Msumbiji
Msumbiji
Upande wa dini, sensa ya mwaka 2017 ilikuta 59.2% ni Wakristo (hasa Waprotestanti na Wakatoliki, ambao ni 28.4%) na 18.9% ni Waislamu. 7.3% wanafuata dini asilia za Kiafrika au nyingine. Kumbe 13.9% hawana dini yoyote, kufuatana na kampeni ya Ukomunisti ya miaka 1979-1982.
20231101.sw_2351_14
https://sw.wikipedia.org/wiki/Msumbiji
Msumbiji
Abrahamsson, Hans Mozambique: The Troubled Transition, from Socialist Construction to Free Market Capitalism London: Zed Books, 1995
20231101.sw_2351_15
https://sw.wikipedia.org/wiki/Msumbiji
Msumbiji
Gengenbach, Heidi. Binding Memories: Women as Makers and Tellers of History in Magude, Mozambique. Columbia University Press, 2004. Entire Text Online
20231101.sw_2351_16
https://sw.wikipedia.org/wiki/Msumbiji
Msumbiji
Mwakikagile, Godfrey, Africa and America in The Sixties: A Decade That Changed The Nation and The Destiny of A Continent, First Edition, New Africa Press, 2006, ISBN 978-0-9802534-2-9
20231101.sw_2351_17
https://sw.wikipedia.org/wiki/Msumbiji
Msumbiji
Mwakikagile, Godfrey, Nyerere and Africa: End of an Era, Third Edition, New Africa Press, 2006, "Chapter Seven: "The Struggle for Mozambique: The Founding of FRELIMO in Tanzania," pp. 206–225, ISBN 978-0-9802534-1-2