_id
stringlengths
15
22
url
stringlengths
31
150
title
stringlengths
1
86
text
stringlengths
100
23.8k
20231101.sw_2239_17
https://sw.wikipedia.org/wiki/Historia%20ya%20Kiswahili
Historia ya Kiswahili
Wajerumani waliamua kutumia Kiswahili kama lugha ya utawala katika Afrika ya Mashariki ya Kijerumani. Hapo walitumia kazi ya utafiti iliyofanywa na wamisionari.
20231101.sw_2239_18
https://sw.wikipedia.org/wiki/Historia%20ya%20Kiswahili
Historia ya Kiswahili
Utawala wa kikoloni ulirahisisha mawasiliano kati ya wenyeji. Reli zilijengwa na wafanyakazi kutoka makabila mbalimbali walishirikiana. Waafrika walilazimishwa kulipa kodi kwa wakoloni, hivyo walitafuta kazi ya ajira. Hasa katika mashamba makubwa yaliyolima mazao ya biashara pia katika migodi ya Kongo watu wa makabila mengi walichanganyikana wakitumia hasa Kiswahili kati yao. Kwa namna hiyo lugha ilienea zaidi.
20231101.sw_2239_19
https://sw.wikipedia.org/wiki/Historia%20ya%20Kiswahili
Historia ya Kiswahili
Waingereza baada ya kuchukua Tanganyika kutoka kwa Wajerumani waliendela kutumia Kiswahili kama lugha ya utawala. Kuanzia mwaka 1930 waliunda kamati yenye shabaha ya kuunganisha lahaja mbalimbali na kuunda Kiswahili cha pamoja kwa ajili ya Afrika ya Mashariki (Inter-territorial Language (Swahili) committee for the East African Dependencies). Mwenyekiti alikuwa Frederick Johnson, makatibu R. K. Watts, P. Mzaba na Seyyid Majid Khalid Barghash. Kamati hiyo iliamua kutumia lahaja ya Kiunguja kuwa msingi wa Kiswahili cha pamoja kilichoendela kufundishwa shuleni. Leo hii ni Kiswahili rasmi kinachofunzwa na wanafunzi na kuandikwa magazetini na vitabuni.
20231101.sw_2239_20
https://sw.wikipedia.org/wiki/Historia%20ya%20Kiswahili
Historia ya Kiswahili
Miaka ya ukoloni ilisababisha pia kupokelewa kwa maneno mapya katika Kiswahili. Kijerumani kiliacha maneno machache kama "shule" (Kijerumani Schule) na "hela" (Heller) lakini maneno mengi sana ya asili ya Kiingereza yalipokelewa.
20231101.sw_2239_21
https://sw.wikipedia.org/wiki/Historia%20ya%20Kiswahili
Historia ya Kiswahili
Kiswahili kimeonyesha uwezo mkubwa wa kupokea maneno kutoka lugha tofauti sana, kikitumia maneno haya kufuatana na sarufi ya Kibantu ya Kiswahili.
20231101.sw_2239_22
https://sw.wikipedia.org/wiki/Historia%20ya%20Kiswahili
Historia ya Kiswahili
Tofauti na lugha nyingi za Afrika, Kiswahili kiliandikwa tangu karne kadhaa kwa herufi za Kiarabu. Mwandiko wa Kiarabu huwa na herufi kadhaa kwa sauti ambazo haziko katika lugha za Kibantu, vilevile kuna sauti kama "p" au "g" ambazo hazina herufi kwa Kiarabu. Ilhali miji ya Waswahili kwenye eneo kubwa kutoka Somalia hadi Msumbiji ilijitegemea, hapakuwa na tahajia sanifu.
20231101.sw_2239_23
https://sw.wikipedia.org/wiki/Historia%20ya%20Kiswahili
Historia ya Kiswahili
Katika Tanzania Kiswahili kimekuwa lugha rasmi ya serikali na taifa. Shule za msingi hutumia Kiswahili lakini shule za sekondari na vyuo bado zinaendelea kufundisha kwa Kiingereza. Tarehe 15 Februari 2015 rais Jakaya Kikwete alitangaza mpango wa kubadilisha lugha ya elimu nchini kwa kutumia Kiswahili kwenye ngazi zote hadi shule za sekondari na chuo kikuu.
20231101.sw_2239_24
https://sw.wikipedia.org/wiki/Historia%20ya%20Kiswahili
Historia ya Kiswahili
Kenya imetangaza Kiswahili kuwa lugha ya taifa lakini inaendelea kutumia Kiingereza katika shughuli za serikali. Watu wa matabaka ya juu mara nyingi hupendelea kutumia Kiingereza wakiona ni lugha bora. Lakini tangu 1986 wanafunzi wote wanatakiwa kujifunza Kiswahili katika shule za sekondari. Tatizo mojawapo ni kuwepo wa makabila makubwa kama Wakikuyu au Waluo wenye wasemaji wengi sana katika eneo moja, hali isiyosaidia kujifunza lugha tofauti. Pia kaskazini na magharibi mwa Kenya wenyeji wengi si wasemaji wa lugha za Kibantu nao hawaoni Kiswahili ni lugha rahisi.
20231101.sw_2239_25
https://sw.wikipedia.org/wiki/Historia%20ya%20Kiswahili
Historia ya Kiswahili
Uganda inatumia Kiswahili kama lugha ya polisi na jeshi, hali ambayo haikuongeza upendo wa Waganda kwa lugha kutokana na historia ya Uganda ya kuwa na vita na serikali za kijeshi. Lakini kinasikika pia kama lugha ya biashara masokoni. Pamoja na kwamba Waganda walikichukulia Kiswahili kama lugha ya kitumwa lakini pia lugha hii ilionekana kuwa na ustaarabu wa Kiarabu zaidi, yaani Uislamu. Lugha ya Kiswahili ilitumika katika kueneza dini hiyo.
20231101.sw_2239_26
https://sw.wikipedia.org/wiki/Historia%20ya%20Kiswahili
Historia ya Kiswahili
Mashariki mwa Kongo Kiswahili kimeenea sana: ni moja kati ya lugha nne za kitaifa katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
20231101.sw_2239_27
https://sw.wikipedia.org/wiki/Historia%20ya%20Kiswahili
Historia ya Kiswahili
Nurse, D. and Hinnebusch, T. J. 1993. Swahili and Sabaki: A Linguistic History. Berkeley and Los Angeles: University of California Press.
20231101.sw_2240_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/Lahaja%20za%20Kiswahili
Lahaja za Kiswahili
Wakati wa ukoloni wa Uingereza azimio lilitolewa kutumia Kiswahili cha Unguja kuwa Kiswahili rasmi katika Tanganyika, Kenya na Zanzibar. Waingereza walikitumia pia kama lugha ya polisi na jeshi katika Uganda.
20231101.sw_2240_1
https://sw.wikipedia.org/wiki/Lahaja%20za%20Kiswahili
Lahaja za Kiswahili
Kimvita: eneo la Mvita au Mombasa (Kenya). Zamani ilikuwa lahaja kubwa ya kisomi ikitungiwa mashairi kuliko Kiunguja.
20231101.sw_2240_2
https://sw.wikipedia.org/wiki/Lahaja%20za%20Kiswahili
Lahaja za Kiswahili
Chichifundi: kusini mwa PWANI Kwale,Kenya (kando ya fuo za bahari. hususan Gazi, Munje, Funzi, Bodo, Shimoni, Wasini, Mkwiro na Vanga)
20231101.sw_2242_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kidachi
Kidachi
Kidachi ni neno la Kiswahili cha zamani linalosikika hadi leo katika sehemu za Tanzania kwa ajili ya lugha ya Kijerumani au tabia za Wajerumani. Neno limetokana na "Deutsch" (tamka: doitsh) ambalo ni jinsi Wajerumani wenyewe wanavyojiita.
20231101.sw_2242_1
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kidachi
Kidachi
Kidachi, Mdachi/Wadachi na Udachi yalikuwa maneno ya Kiswahili cha kawaida kutokana na utawala wa Kijerumani katika Afrika ya Mashariki ya Kijerumani.
20231101.sw_2242_2
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kidachi
Kidachi
Tangu mwisho wa ukoloni wa Wajerumani mwaka 1918 na kuja kwa Waingereza wasemaji wa Kiswahili wamezoea zaidi kuwataja "Wadachi" kwa kutumia jina lenye asili ya Kiingereza, yaani Kijerumani, Mjerumani/Wajerumani na Ujerumani.
20231101.sw_2242_3
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kidachi
Kidachi
Mara nyingi maneno yenye "-dachi" huchanganywa na neno la Kiingereza "Dutch" linalomaanisha Waholanzi.
20231101.sw_2242_4
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kidachi
Kidachi
Kidachi kimeathiri kwa kiasi fulani lugha ya Kiswahili cha Tanzania bara kama vile kukikopesha maneno mbalimbali, kwa mfano: shule, hela n.k.
20231101.sw_2248_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mkoa%20wa%20Rukwa
Mkoa wa Rukwa
Unapakana na mikoa ya Kigoma, Tabora na Katavi upande wa kaskazini, mkoa wa Mbeya upande wa mashariki, Zambia kusini na upande wa magharibi Ziwa Tanganyika lililo mpaka na Kongo pia.
20231101.sw_2248_1
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mkoa%20wa%20Rukwa
Mkoa wa Rukwa
Kabla ya kumegwa mwaka 2012 eneo la mkoa lilikuwa takriban km² 70,000. Kwa sasa lina kilomita ya mraba 22,792.
20231101.sw_2248_2
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mkoa%20wa%20Rukwa
Mkoa wa Rukwa
Wilaya ya Mpanda ilikuwa sehemu ya Rukwa ikaendelea kuwa kiini cha mkoa mpya wa Katavi kuanzia mwaka 2012.
20231101.sw_2248_3
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mkoa%20wa%20Rukwa
Mkoa wa Rukwa
Kabila kubwa zaidi mkoani ndio Wafipa walioko hasa katika wilaya za Sumbawanga na Nkansi. Kati ya makabila mengine kuna Wamambwe-Lungu, Wawanda na Wanyamwanga katika wilaya ya Sumbawanga; kuna pia Wasukuma, Wanyamwezi na Wamasai.
20231101.sw_2250_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mkoa%20wa%20Shinyanga
Mkoa wa Shinyanga
Mkoa wa Shinyanga ni kati ya mikoa 31 ya Tanzania wenye msimbo wa posta 37000. Mkoa umepakana upande wa kaskazini na mikoa ya Mwanza, Geita na Kagera, upande wa kusini na Mkoa wa Tabora. Mkoa wa Kigoma uko upande wa magharibi, na mkoa wa Simiyu upande wa mashariki.
20231101.sw_2250_1
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mkoa%20wa%20Shinyanga
Mkoa wa Shinyanga
Baada ya kumegwa upande wa mashariki na kuzaa mkoa wa Simiyu, Shinyanga ina wakazi 2,241,299 kufuatana na sensa ya mwaka 2002 kutoka wakazi 1,534,808 wa sensa ya mwaka 2012.
20231101.sw_2250_2
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mkoa%20wa%20Shinyanga
Mkoa wa Shinyanga
Mkoa wa Shinyanga una wilaya 5: Kahama Mjini, Kahama Vijijini, Kishapu, wilaya ya Shinyanga Vijijini na wilaya ya Shinyanga Mjini.
20231101.sw_2250_3
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mkoa%20wa%20Shinyanga
Mkoa wa Shinyanga
Wakazi wa Mkoa wa Shinyanga hujishughulisha na uchimbaji mdogo wa madini ya dhahabu na almasi. Kuna migodi mikubwa ya uchimbaji wa madini ya almasi katika mgodi wa Mwadui na dhahabu katika migodi ya Bulyanhulu na Buzwagi.
20231101.sw_2250_4
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mkoa%20wa%20Shinyanga
Mkoa wa Shinyanga
Mgodi wa Williamson Diamond, ulioko katika Mkoa wa Shinyanga kilomita 160 kusini mwa jiji la Mwanza, ni moja ya mabomu saba yanayoendeshwa na Petra Diamonds. Mgodi huo kwa 75% inamilikiwa na almasi ya Petra na 25% na Serikali ya Tanzania. Williamson ni mgodi wazi wa shimo ulioenea juu ya eneo la hekta 146. Mgodi huo umekuwa ukifanya kazi kwa miaka 70. Bado ina rasilimali muhimu ya almasi bado inapaswa kuchimbwa. Mpango wa sasa wa mgodi kwa Williamson ni kwa miaka 18. Maisha yanayowezekana ya mgodi ni zaidi ya miaka 50.
20231101.sw_2250_5
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mkoa%20wa%20Shinyanga
Mkoa wa Shinyanga
Mgodi huo umetajwa kwa jina la Dk John Williamson, mtaalamu wa jiolojia wa Canada, ambaye aligundua mnamo 1940 kama amana ya msingi ya kiuchumi ya almasi. Dk Williamson alisimamia mgodi huo hadi kifo chake mnamo 1958.
20231101.sw_2251_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/Idhaa%20ya%20Kiswahili%20ya%20Radio%20Tehran
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Tehran
Idhaa ya Kiswahili Sauti ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ni huduma ya matangazo ya "Islamic Republic of Iran Broadcasting" (IRIB) ambayo ni redio ya taifa ya Iran (Uajemi) kwa lugha ya Kiswahili.
20231101.sw_2251_1
https://sw.wikipedia.org/wiki/Idhaa%20ya%20Kiswahili%20ya%20Radio%20Tehran
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Tehran
IRIB inarusha matangazo kwa lugha mbalimbali kama vile Kirusi, Kiarabu, Kiingereza, Kifaransa Kichina na mengine.
20231101.sw_2251_2
https://sw.wikipedia.org/wiki/Idhaa%20ya%20Kiswahili%20ya%20Radio%20Tehran
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Tehran
Kwa lugha ya Kiswahili ilianza kurusha matangazo yake kwa mara ya kwanza siku ya Ijumaa usiku ya tarehe 30 Desemba mwaka 1994.
20231101.sw_2251_3
https://sw.wikipedia.org/wiki/Idhaa%20ya%20Kiswahili%20ya%20Radio%20Tehran
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Tehran
Kwa wakati huo matangazo ya Radio Tehran yaliyokuwa yakirushwa kwa ajili ya nchi za mashariki na katikati mwa Afrika, yalianza yakiwa na wafanyakazi wachache ambao ni Sayyid Muhammad Ridha Shushtari, Sayyid Hashim Shushtari ambaye kwa sasa ni marehemu, Muhammad Baraza, Leyla Kimani, Abdul Fatah Mussa, Ahmed Rashid, Nargis Jalalakhan na Said Kambi. Watangazaji wengine wa idhaa hii ni Asmahan Ghanima Mohammad, Salum Bendera, Mubarak Henia, Sudi Ja'afar Shaban na Hussein Hassan Kamau. Lengo la kuasisiwa Idhaa ya Kiswahili Sauti ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ni kufikisha sauti ya Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran kwa wananchi waliodhulumiwa wa bara la Afrika, kuelimisha na kufichua njama za ubeberu wa kimataifa dhidi ya bara hilo.
20231101.sw_2251_4
https://sw.wikipedia.org/wiki/Idhaa%20ya%20Kiswahili%20ya%20Radio%20Tehran
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Tehran
Kuanzia tarehe 26 Aprili mwaka 1997 Radio Tehran ilianza kutangaza kwa muda wa saa moja kuanzia saa mbili na nusu usiku kwa saa za Afrika Mashariki, na matangazo hayo kurejewa siku ya pili yake kuanzia saa 12:30 asubuhi kwa majira ya Afrika Mashariki sawa na saa 11:30 asubuhi kwa majira ya Afrika ya Kati.
20231101.sw_2251_5
https://sw.wikipedia.org/wiki/Idhaa%20ya%20Kiswahili%20ya%20Radio%20Tehran
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Tehran
Mnamo tarehe 23 Mfunguo Tatu (Dhulhijja) 1418 Hijria iliyosadifiana na tarehe 21 Aprili 1998 Milaadia, matangazo ya Radio Tehran yalianza kurushwa hewani kwa muda wa masaa matatu katika nyakati za usiku, asubuhi na machana. Saa moja ilikuwa ni marudio ya matangazo ya asubuhi, ambayo yalikuwa yakisikika kuanzia saa saba kamili hadi saa nane kamili mchana kila siku kwa majira ya Afrika Mashariki.
20231101.sw_2251_6
https://sw.wikipedia.org/wiki/Idhaa%20ya%20Kiswahili%20ya%20Radio%20Tehran
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Tehran
Kwa hivi sasa Idhaa imeongeza wafanyakazi wake ambapo matangazo ya mchana nayo sasa yanasikika kwa njia ya moja kwa moja kuanzia saa 5:30 hadi 6:30 mchana kwa saa za Afrika Mashariki. Inarusha matangazo yake kwa ajili ya nchi za Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, Congo, mashariki mwa Zambia, kaskazini mwa Malawi na Msumbiji pamoja na Afrika Kusini. Inarusha pia matangazo yake kwa ajili ya nchi za Mashariki ya Kati hususan za Ghuba ya Uajemi na ina waandishi wake katika maeneo ya Afrika Mashariki na Kati kama vile Kenya, Tanzania, Uganda, Burundi na Kongo.
20231101.sw_2251_7
https://sw.wikipedia.org/wiki/Idhaa%20ya%20Kiswahili%20ya%20Radio%20Tehran
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Tehran
Matangazo ya IRIB yanalenga kusambaza habari juu ya Iran na utamaduni wake. Yanalenga kusambaza mitazamo ya Kiislamu na mafundisho ya Ahlul Baiti (as) inayolingana na siasa ya Iran. Matangazo ya IRIB pia yananawabaishia Walimwengu ubeberu wa Marekani na madola ya Kimagharibi dhidi ya mataifa mengine na ukandamizaji wa utawala haramu wa Israel dhidi ya wananchi madhulumu wa Palestina.
20231101.sw_2253_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mkoa%20wa%20Pwani
Mkoa wa Pwani
Mkoa umepakana upande wa Kaskazini na Tanga, upande wa mashariki na Dar-es-Salaam na Bahari Hindi, upande wa kusini na mkoa wa Lindi na upande wa magharibi na mkoa wa Morogoro.
20231101.sw_2253_1
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mkoa%20wa%20Pwani
Mkoa wa Pwani
Mkoa huu unalo eneo la km² 32,407, ukiwa na idadi ya wakazi wapatao 2,024,947 kadiri ya sensa ya mwaka 2022 kutoka 1,098,668 (2012).
20231101.sw_2253_2
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mkoa%20wa%20Pwani
Mkoa wa Pwani
Wilaya ya Rufiji imegawanyika sehemu mbili, visiwani na bara: wenyeji wa visiwani ni wa kabila la Wanyagatwa na walio bara ndio Wandengereko. Wenyeji wa visiwani wanajishughulisha sana na uvuvi, kilimo cha mnazi na kupika chumvi, Wandengereko wanajishughulisha sana na mazao ya vyakula kama vile mpunga, mahindi n.k.
20231101.sw_2253_3
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mkoa%20wa%20Pwani
Mkoa wa Pwani
Mkoa huu una jumla ya majimbo ya uchaguzi yanayofikia (9) ambayo yanajumuisha Bagamoyo, Chalinze, Kibaha, Kibaha Vijijini, Kibiti, Kisarawe, Mafia, Mkuranga na Rufiji
20231101.sw_2255_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mkoa%20wa%20Manyara
Mkoa wa Manyara
Mkoa wa Manyara ni kati ya mikoa 31 ya Tanzania wenye postikodi namba 27000. Umepakana na mikoa ya Arusha na Kilimanjaro upande wa kaskazini, Mkoa wa Tanga upande wa mashariki, Mkoa wa Dodoma upande wa kusini na mikoa ya Singida na Shinyanga upande wa magharibi.
20231101.sw_2255_1
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mkoa%20wa%20Manyara
Mkoa wa Manyara
Mkoa wa Manyara umetengwa na Mkoa wa Arusha mwaka 2002 kwa azimio la rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ukiwa na eneo la km² 46,359.
20231101.sw_2255_2
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mkoa%20wa%20Manyara
Mkoa wa Manyara
Idadi hiyo imepatikana katika wilaya zifuatazo (idadi ya wakazi katika mabano mwaka 2002): Babati (303,013), Hanang (205,133), Mbulu (237,882), Simanjiro (141,676) na Kiteto (152,757).
20231101.sw_2255_3
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mkoa%20wa%20Manyara
Mkoa wa Manyara
Sensa zinaonyesha kwamba ni kati ya mikoa ya Tanzania yenye ongezeko kubwa la wakazi. Pia ni kati ya mikoa yenye maambukizi machache zaidi ya Ukimwi.
20231101.sw_2255_4
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mkoa%20wa%20Manyara
Mkoa wa Manyara
Wenyeji wa mkoa huu ni pamoja na Wairaqw, Wamasai, Wambugwe, Wafyomi na Wabarbaig wakijihusisha na shughuli za kilimo na ufugaji kama njia ya kuingiza kipato chao cha kila siku.
20231101.sw_2257_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/Korongo%20%28Gruidae%29
Korongo (Gruidae)
Korongo hawa (pia mana) ni ndege wa familia ya Gruidae wenye domo fupi na jembamba kuliko lile la korongo wa familia ya Ciconiidae. Spishi nyingi hufanya mikogo ya kubembeleza jike wakitoa sauti kubwa. Huugana kwa maishi yao yote. Spishi za nchi za halijoto wastani huhama kila mwaka kabla ya wakati wa baridi. Korongo hawa hupenda kuwa pamoja na huhama kwa makundi makubwa. Hula kila kitu kinachopatikana, kama panya, watambaazi, amfibia au samaki, hata nafaka na matunda madogo. Spishi za korongo zinatokea mabara yote ghairi ya Amerika ya Kusini.
20231101.sw_2259_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mkoa%20wa%20Mwanza
Mkoa wa Mwanza
Mkoa wa Mwanza ni kati ya mikoa 31 ya Tanzania, wenye postikodi namba 33000. Umepakana na Geita upande wa magharibi, Shinyanga na Simiyu upande wa kusini na Mara upande wa mashariki. Ziwa la Viktoria Nyanza liko kaskazini.
20231101.sw_2259_1
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mkoa%20wa%20Mwanza
Mkoa wa Mwanza
Kabla ya kumegwa na kuzaa mkoa mpya wa Geita, mkoa wa Mwanza ulikuwa na wakazi 2,942,148 (sensa ya mwaka 2002) katika wilaya 8 ukiwa na eneo la 19,592 km2.
20231101.sw_2259_2
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mkoa%20wa%20Mwanza
Mkoa wa Mwanza
Wilaya ndizo Ukerewe, Magu, Sengerema, Geita, Misungwi, Kwimba, Nyamaganga na Ilemela. Jiji la Mwanza ndani yake lina wilaya za Nyamagana na Ilemela.
20231101.sw_2259_3
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mkoa%20wa%20Mwanza
Mkoa wa Mwanza
Makabila makubwa ya Mwanza ndio Wasukuma na Wazinza upande wa bara, halafu Wakerewe na Wakara visiwani.
20231101.sw_2266_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/Heroe
Heroe
Heroe ni ndege wa jenasi Phoenicopterus, jenasi pekee ya familia ya Phoenicopteridae. Ndege hawa hukaa kwa maji ya chumvi kwa makundi makubwa. Wana miguu mirefu na shingo ndefu na nyembamba. Wakiruka angani hunyosha shingo. Urefu wao ni kati ya futi 3 na 5. Hula vijimea (algae) na nduvi ndogo ambazo huzikamata na domo lao zungu linalotumika kama chujio. Tago lao ni kifungu cha matope kwa tundu fupi ambalo ndani lake yai moja linatagwa.
20231101.sw_2269_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mkoa%20wa%20Kilimanjaro
Mkoa wa Kilimanjaro
Mlima Kilimanjaro, mlima mrefu kupita yote barani Afrika, umo ndani ya mkoa wa Kilimanjaro. Jina la mlima huu ndilo limeupatia mkoa jina lake.
20231101.sw_2269_1
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mkoa%20wa%20Kilimanjaro
Mkoa wa Kilimanjaro
Mkoa wa Kilimanjaro umepakana na Kenya upande wa kaskazini, Mkoa wa Tanga upande wa kusini na mikoa ya Manyara na Arusha upande wa magharibi.
20231101.sw_2269_2
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mkoa%20wa%20Kilimanjaro
Mkoa wa Kilimanjaro
Makabila makubwa mkoani humo ni Wachagga, Wagweno na Wapare, ambapo pia kuna makabila mengine madogomadogo kama Wamasai na Wakamba.
20231101.sw_2269_3
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mkoa%20wa%20Kilimanjaro
Mkoa wa Kilimanjaro
Katika sekta ya elimu wakazi wameendelea kidogo kwa maeneo ya mjini, lakini katika sehemu za vijijini elimu bado inatetereka kwa kiasi kikubwa, maana teknolojia ya utandawazi katika eneo kubwa haijashamiri.
20231101.sw_2269_4
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mkoa%20wa%20Kilimanjaro
Mkoa wa Kilimanjaro
Mkoa wa Kilimanjaro una wilaya 7 ambazo ni: Hai, Mwanga, Moshi mjini, Moshi vijijini, Rombo na Same na ile mpya ya Siha.
20231101.sw_2270_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/Unguja
Unguja
Unguja ni kisiwa kikubwa katika Bahari Hindi mkabala wa mwambao wa Afrika ya Mashariki karibu na Dar es Salaam.
20231101.sw_2270_1
https://sw.wikipedia.org/wiki/Unguja
Unguja
Unguja ndicho kisiwa kikuu cha funguvisiwa la Zanzibar ambavyo ni sehemu ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania.
20231101.sw_2270_2
https://sw.wikipedia.org/wiki/Unguja
Unguja
Kisiwani Unguja kuna mitatu kati ya mikoa 31 ya Tanzania ambayo ni Unguja Kaskazini, Unguja Kusini na Unguja Mjini Magharibi.
20231101.sw_2271_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/Zanzibar%20%28maana%29
Zanzibar (maana)
Kijiografia Funguvisiwa la Zanzibar kwenye mwambao wa Afrika ya Mashariki hasa visiwa vikubwa vya Unguja na Pemba pamoja na visiwa vidogo vidogo
20231101.sw_2271_1
https://sw.wikipedia.org/wiki/Zanzibar%20%28maana%29
Zanzibar (maana)
Kihistoria Usultani wa Zanzibar iliyoanzishwa baada ya kifo cha Sultani Sayyid Said na kugawiwa kwa Usultani ya Omani mwaka 1856 wakati mwanaye Sayyid Majid alipokuwa sultani wa kwanza wa Zanzibar akitawala funguvisiwa ya Zanzibar pamoja na pwani la Afrika ya Mashariki kati ya Mogadishu (leo mji mkuu wa Somalia) na Rasi ya Delgado (leo Msumbiji ya Kaskazini karibu na mto wa Ruvuma).
20231101.sw_2271_2
https://sw.wikipedia.org/wiki/Zanzibar%20%28maana%29
Zanzibar (maana)
Kisiasa Jamhuri ya Watu wa Zanzibar ambayo ni sehemu ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania. Zanzibar ilipata uhuru kwa njia ya mapinduzi mwaka 1963 na iliungana na Tanganyika mwaka 1964 hivyo kuunda Jamhuri ya Muungano ya Tanzania na waasisi walikuwa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Sheikh Abeid Amani Karume. Zanzibar ina jumla ya mikoa mitano ambayo ni: Mjini Magharibi, Kaskazini Unguja, Kusini Unguja, Kaskazini Pemba na Kusini Pemba
20231101.sw_2271_3
https://sw.wikipedia.org/wiki/Zanzibar%20%28maana%29
Zanzibar (maana)
Jina la filamu, vitabu, hoteli n.k. zilizotajwa kufuatana na neno lenyewe kama vile Jamhuri ya Zanzibar, funguvisiwa la Zanzibar, jiji la Zanzibar n.k.
20231101.sw_2273_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/Zanzibar%20%28Jiji%29
Zanzibar (Jiji)
Kitovu cha historia yake ni Mji Mkongwe (Stone Town) ulioandikishwa katika orodha ya UNESCO ya "Urithi wa Dunia" (World Heritage).
20231101.sw_2273_1
https://sw.wikipedia.org/wiki/Zanzibar%20%28Jiji%29
Zanzibar (Jiji)
Nyumba za Mji Mkongwe zilijengwa tangu mwaka 1830 wakati Sultani Sayyid Said alipohamisha mji mkuu wake kutoka Omani kuja Unguja.
20231101.sw_2273_2
https://sw.wikipedia.org/wiki/Zanzibar%20%28Jiji%29
Zanzibar (Jiji)
Kati ya majengo maarufu ni Beit al Ajaib (yaani Jumba la Maajabu lililobomoka tarehe 24 Desemba 2020), boma la kale, Kanisa Kuu la Kianglikana lililojengwa mahali pa soko la watumwa na hasa nyumba nyingi za kihistoria za ghorofa zilizojengwa na famila za tabaka la matajiri Waarabu zenye milango yenye mapambo mazuri.
20231101.sw_2273_3
https://sw.wikipedia.org/wiki/Zanzibar%20%28Jiji%29
Zanzibar (Jiji)
Stranger in Paradise: Searching for a Place to Call Home in Stone Town by Christopher Vourlias, World Hum, June 15, 2009
20231101.sw_2273_4
https://sw.wikipedia.org/wiki/Zanzibar%20%28Jiji%29
Zanzibar (Jiji)
Zanzibar Stone Town & Hotels A travel guide website containing pictures and information about Stone Town as well as a selection of Stone Town Hotels.
20231101.sw_2275_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mkoa%20wa%20Unguja%20Mjini%20Magharibi
Mkoa wa Unguja Mjini Magharibi
Mkoa wa Unguja Mjini Magharibi ni kati ya mikoa 31 ya Tanzania wenye Postikodi namba 71000. Mikoa mitatu kati yake iko katika kisiwa cha Unguja.
20231101.sw_2275_1
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mkoa%20wa%20Unguja%20Mjini%20Magharibi
Mkoa wa Unguja Mjini Magharibi
Mkoa una wakazi 893,169 kadiri ya sensa ya mwaka 2022 . Walikuwa 593,678; Mjini wako 223,033 na Magharibi 370,645 (sensa ya mwaka 2012).
20231101.sw_2276_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/Etimolojia%20ya%20neno%20Zanzibar
Etimolojia ya neno Zanzibar
Etimolojia ya neno "Zanzibar" inaonyesha ya kuwa ni jina la kale sana. Hakuna hakika kabisa kuhusu asili ya neno hilo. Etimolojia ni elimu ya asili ya maneno na uhusiano yake na maneno mengine.
20231101.sw_2276_1
https://sw.wikipedia.org/wiki/Etimolojia%20ya%20neno%20Zanzibar
Etimolojia ya neno Zanzibar
Zanzibar ina uhusiano na maneno mawili ya Kiarabu. Neno la kwanza ni "zanj- ﺯﻧﺞ" lililomaanisha watu weusi au nchi ya watu weusi. Katika historia kuna kipindi cha vita ya Wazanj waliokuwa watumwa Waafrika katika Irak karibu na mji wa Basra walioasi dhidi ya mabwana wao Waarabu kati ya 869 and 879 BK wakijaribu kujipatia uhuru. Neno "zanj" linaandikwa "zang زنگ" kwa Kiajemi na zamani taarifa nyingi za Wazungu zilitumia umbo la "Zanguebar" kwa matamshi ya Kiajemi wakitaja Zanzibar.
20231101.sw_2276_2
https://sw.wikipedia.org/wiki/Etimolojia%20ya%20neno%20Zanzibar
Etimolojia ya neno Zanzibar
Bila shaka wakazi asilia walikuwa na jina au majina yao kwa ajili ya mwambao wa Afrika ya Mashariki na visiwa. Lakini hatuna ushuhuda kuhusu majina yale yaliyotumiwa karne nyingi zilizopita. Katika taarifa ya wasafiri na wataalamu Wagiriki na Waarabu tunakuta majina yanayofanana na Zanzibar.
20231101.sw_2276_3
https://sw.wikipedia.org/wiki/Etimolojia%20ya%20neno%20Zanzibar
Etimolojia ya neno Zanzibar
Ptolemaio (aliishi mnamo mwaka 200 BK) alitaja rasi ya "Zingis" au "Zingisa" ((Ζίγγις ή Ζήγγισα) ambayo inaaminiwa kuwa Zanzibar; wasafiri wa baadaye walitumia jina tunalojua kutoka kwa Waarabu, kwa mfano Marco Polo aliyetaja "Zamzibar". Hatujui kama wale wageni walitumia jina walilopokea kutoka wenyeji.
20231101.sw_2276_4
https://sw.wikipedia.org/wiki/Etimolojia%20ya%20neno%20Zanzibar
Etimolojia ya neno Zanzibar
Kwa mahitaji yetu inatosha kusema ya kwamba kuna jina la kale kwa ajili ya mwambao wa Afrika ya Mashariki lililowahi kutajwa kwa umbo tofauti katika karne za kale kama vile Zingis, Zingium, Azania, au nchi (=bar) ya „Zanj“ (kiarabu) au ya „Zangi“ (kiajemi). Wajemi na Waarabu wote walitaja pia watu weusi kwa neno hili. „Zangibar“ au „zanjbar“ ni „nchi ya watu weusi“.
20231101.sw_2276_5
https://sw.wikipedia.org/wiki/Etimolojia%20ya%20neno%20Zanzibar
Etimolojia ya neno Zanzibar
Wareno walianza baadaye kutofautisha kati ya bara na kisiwa wakiandika jina la kisiwa mbele ya pwani la „Zanguebar“ kama „Zanzibar“ yaani kwa namna inayolingana zaidi na matamshi ya Kiarabu lakini waliendelea kusema "Zanguebar" wakimaanisha bara.
20231101.sw_2306_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/Pemba
Pemba
Pemba (Msumbiji) (zamani: "Porto Amelia"), mji wa mwambao wa Msumbiji na makao makuu ya mkoa wa Cabo Delgado
20231101.sw_2307_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/Pemba%20%28kisiwa%29
Pemba (kisiwa)
Makala hii inahusu Kisiwa cha Pemba. Jina Pemba linatumika pia kwa ajili ya Pemba katika Msumbiji na Pemba wilaya pamoja na mji huko Zambia.
20231101.sw_2307_1
https://sw.wikipedia.org/wiki/Pemba%20%28kisiwa%29
Pemba (kisiwa)
Pemba ni kisiwa kilichopo takriban 50 km kaskazini ya Unguja katika Bahari Hindi. Visiwa vyote viwili ni sehemu za Jamhuri ya Watu wa Zanzibar katika Tanzania. Umbali na Tanganyika au Tanzania bara ni 50 km.
20231101.sw_2307_2
https://sw.wikipedia.org/wiki/Pemba%20%28kisiwa%29
Pemba (kisiwa)
Katika utamaduni wa Pemba kuna desturi ya kipekee katika Afrika ndiyo mchezo wa ng'ombe iliyorithiwa na Wareno walipokuwa na athari kisiwani karne zilizopita.
20231101.sw_2310_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mchezo%20wa%20ng%27ombe
Mchezo wa ng'ombe
Mchezo wa ng'ombe ni desturi inayojulikana hasa katika nchi za Hispania na Ureno, pia katika maeneo ya jirani ya Ufaransa kusini na katika koloni za zamani za Hispania huko Amerika ya Kilatini kama Meksiko. Imekuwa pia mila ya pekee kwenye Kisiwa cha Pemba, Tanzania. Kila mahali ni mashindano kati ya wanadamu na fahali wa ng'ombe lakini kuna taratibu tofautitofauti.
20231101.sw_2310_1
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mchezo%20wa%20ng%27ombe
Mchezo wa ng'ombe
Katika mchezo wa Hispania fahali anauawa uwanjani. Mchezo unafanywa katika uwanja wa pekee unaoitwa Plaza de Toros. Wale wanoshindana na ng'ombe dume wanaitwa "torero"; mkuu wao atakayemwua kwa pigo la upanga wake ni "matador". Matador anatangulia kucheza na fahali kwa kumkasirisha kwa kitambaa chekundu na kutoroka akishambuliwa. Wasaidizi wake wanapita kwa farasi na kumdunga fahali kwa mikuki midogo kwa kusudi la kumdhoofisha. Mwishoni ng'ombe anauawa na matador kwa upanga. Muda wa mchezo ni kama dakika 20 kwa kila mnyama.
20231101.sw_2310_2
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mchezo%20wa%20ng%27ombe
Mchezo wa ng'ombe
Historia ya desturi hii inarudi nyuma hadi zamani za Dola la Roma watu walipopenda kuwa na maonyesho ya mapambano ya wanyama pori, ama ya wenyewe kwa wenyewe au zaidi ya watu dhidi ya wanyama hawa. Maonyesho haya yalifanyika katika uwanja wa mji kwa mfano uwanja wa Koloseo huko Roma. Desturi hii imepotea kila sehemu ya eneo la kale la Dola la Roma kwa sababu ilipingwa na kanisa la kikristo isipokuwa Hispania na Ureno.
20231101.sw_2310_3
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mchezo%20wa%20ng%27ombe
Mchezo wa ng'ombe
Pemba ndipo mahali pa pekee katika Afrika penye desturi hii ya mchezo wa ng'ombe. Hii ni kutokana na athira ya Ureno kwenye mwambao wa Afrika ya Mashariki miaka 400 iliyopita. Mara Wareno walikuwa na kituo huko Chake Chake, mara walikuwa na mapatano ya usaidizi na Pemba, mara waliuachia utawala Sultani wa Mombasa. Haijulikani jinsi walivyoacha desturi hii Pemba.
20231101.sw_2310_4
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mchezo%20wa%20ng%27ombe
Mchezo wa ng'ombe
Kuhusu mchezo huu amesema Abdullah Amur Suleiman (http://groups.msn.com/SitiBintiSaad/mchezowangombebullfight.msnw ):
20231101.sw_2315_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/Lugha%20ya%20kupangwa
Lugha ya kupangwa
Lugha ya kupangwa ni aina ya lugha ya kuundwa. Kwa kawaida, msemo lugha ya kupangwa unatumika kwa lugha zile ambazo ziliundwa kwa ajili ya utumiaji wa kawaida baina ya watu.
20231101.sw_2315_1
https://sw.wikipedia.org/wiki/Lugha%20ya%20kupangwa
Lugha ya kupangwa
Kumbe kuna lugha iliyotengenezwa ambayo si lugha ya kupangwa, kama vile lugha za uzushi na lugha za siri.
20231101.sw_2318_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/Taasisi%20ya%20Taaluma%20za%20Kiswahili
Taasisi ya Taaluma za Kiswahili
Taasisi ya Taaluma za Kiswahili (TATAKI) ni idara ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Tanzania. Taasisi hii ni miongoni mwa taasisi kongwe za lugha nchini Tanzania. Madhumuni yake yakiwa ni kusimamia usanifishaji na maendeleo ya lugha ya Kiswahili. Hadi mnamo mwaka 2009 taasisi hii ilijulikana zaidi kwa jina la TUKI au "Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili".
20231101.sw_2318_1
https://sw.wikipedia.org/wiki/Taasisi%20ya%20Taaluma%20za%20Kiswahili
Taasisi ya Taaluma za Kiswahili
Ilianzishwa mnamo mwaka 1930 kama Inter-territorial Language (Swahili) committee ya Nchi za Afrika ya Mashariki, baadaye ikaitwa Kamati ya Kiswahili ya Afrika Mashariki. Mnamo mwaka 1964 kamati ilifanywa kuwa Sehemu ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaamu. Baadaye ikaitwa Chuo cha Uchunguzi wa Lugha ya Kiswahili. Tangu 1970 kimepewa jina la Taasisi ya Uchunguzi wa Lugha ya Kiswahili. Mwaka 2009, TUKI iliungana na iliyokuwa Idara ya Kiswahili ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na kuunda Taasisi kubwa zaidi inayoitwa Taasisi ya Taaluma za Kiswahili - TATAKI
20231101.sw_2318_2
https://sw.wikipedia.org/wiki/Taasisi%20ya%20Taaluma%20za%20Kiswahili
Taasisi ya Taaluma za Kiswahili
Mwanzoni, Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili ni taasisi ya utafiti ilipewa jukumu la kutafiti nyanja zote za lugha ya Kiswahili, fasihi na utamaduni, na kuchapisha matokeo ya utafiti huo. Hivyo pamoja na BAKITA (Baraza la Kiswahili Tanzania) TUKI ndiye mlinzi wa usanifu wa lugha ya Kiswahili katika Tanzania.
20231101.sw_2318_3
https://sw.wikipedia.org/wiki/Taasisi%20ya%20Taaluma%20za%20Kiswahili
Taasisi ya Taaluma za Kiswahili
Baada ya kuungana na Idara ya Kiswahili, sasa TATAKI inafundisha Isimu, Fasihi na Historia ya Lugha ya Kiswahili katika Shahada za Awali, Mahiri na Uzamivu.
20231101.sw_2318_4
https://sw.wikipedia.org/wiki/Taasisi%20ya%20Taaluma%20za%20Kiswahili
Taasisi ya Taaluma za Kiswahili
Kutafiti na kuchapisha matokeo ya utafiti katika nyanja mbalimbali za Lugha, Isimu na Fasihi ya Kiswahili, TATAKI inasimamia Tafsiri na Ukalimani. Inafundisha Kiswahili kama lugha ya pili hasa kwa wageni kutoka nje ya ulimwengu wa Waswahili na kuendeleza utungaji wa Kamusi mbalimbali zinazohusiana na Kiswahili.
20231101.sw_2318_5
https://sw.wikipedia.org/wiki/Taasisi%20ya%20Taaluma%20za%20Kiswahili
Taasisi ya Taaluma za Kiswahili
TUKI imehariri toleo la Kiswahili la "Historia Kuu ya Afrika" iliyotungwa na kamati ya wataalamu ya UNESCO.
20231101.sw_2324_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mkoa%20wa%20Pemba%20Kusini
Mkoa wa Pemba Kusini
Mkoa wa Pemba Kusini mi mojawapo kati ya mikoa 31 ya Tanzania wenye postikodi namba 74000. Uko katika sehemu ya kusini ya Kisiwa cha Pemba ambacho ni sehemu ya Jamhuri ya Watu wa Zanzibar katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
20231101.sw_2324_1
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mkoa%20wa%20Pemba%20Kusini
Mkoa wa Pemba Kusini
Mkoa una wakazi 271,350 kadiri ya sensa ya mwaka 2022 . Katika sensa ya mwaka 2012 ulikuwa na wakazi wapatao 195,116.
20231101.sw_2325_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mkoa%20wa%20Pemba%20Kaskazini
Mkoa wa Pemba Kaskazini
Mkoa wa Pemba Kaskazini ni mmojawapo kati ya mikoa 31 ya Tanzania yenye postikodi namba 75000 . Uko katika sehemu ya kaskazini ya Kisiwa cha Pemba ambacho ni sehemu ya Zanzibar katika Muungano wa Tanzania.
20231101.sw_2326_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mkoa%20wa%20Unguja%20Kaskazini
Mkoa wa Unguja Kaskazini
Mkoa wa Unguja Kaskazini ni mmojawapo kati ya mikoa 31 ya Tanzania wenye Postikodi namba 73000. Uko Unguja ambayo ni kisiwa kikubwa cha Jamhuri ya Watu wa Zanzibar.
20231101.sw_2326_1
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mkoa%20wa%20Unguja%20Kaskazini
Mkoa wa Unguja Kaskazini
Kuna wilaya mbili ambazo ni Kaskazini Unguja 'A' (105,780 mwaka 2012) na Kaskazini Unguja 'B' (81,675 mwaka 2012).
20231101.sw_2326_2
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mkoa%20wa%20Unguja%20Kaskazini
Mkoa wa Unguja Kaskazini
Eneo la mkoa ni km² 470 ambako kuna jumla ya wakazi 257,290 kwa mujibu wa sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022.