_id
stringlengths 15
22
| url
stringlengths 31
150
| title
stringlengths 1
86
| text
stringlengths 100
23.8k
|
---|---|---|---|
20231101.sw_2511_5
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mayotte
|
Mayotte
|
Mwaka 1974, wakati visiwa vingine vitatu vya Komoro walidai uhuru na kuunda Umoja wa Comoro, Mayotte iliomba kubaki na Ufaransa, na mwaka 2011 ilipewa hali ya eneo la ng'ambo la Ufaransa kwa kura ya maoni.
|
20231101.sw_2511_6
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mayotte
|
Mayotte
|
Kuna lugha tatu ambazo huzungumzwa kisiwani Mayotte, yaani Kifaransa (lugha rasmi), Kimaore ya Komori (55.1%), na Kibushi ya Madagaska.
|
20231101.sw_2511_7
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mayotte
|
Mayotte
|
Kisiwa cha Mayotte kina mchanga wa pwani ya rangi tofauti (nyeusi, kahawia, kijivu, nyekundu, beige, nyeupe). Rasi yake ni kubwa (km² 1500).
|
20231101.sw_2512_0
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Funguvisiwa
|
Funguvisiwa
|
Funguvisiwa ni kundi la visiwa vinavyokaa sehemu pamoja baharini. Mara nyingi kundi la namna hiyo lina asili moja, kama vile kuwa mabaki ya kisiwa kikubwa zaidi kilichogawika kutokana na mmomonyoko wa ardhi yake au kuwa na asili ya volkeno.
|
20231101.sw_2512_1
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Funguvisiwa
|
Funguvisiwa
|
Atolli inaweza kuonekana pia kama kundi la visiwa lakini huhesabiwa zaidi kama kisiwa kimoja hata kama sehemu kadhaa ziko chini ya maji. Katika Bahari ya Pasifiki na Bahari Hindi kuna mafunguvisiwa ya atolli.
|
20231101.sw_2512_2
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Funguvisiwa
|
Funguvisiwa
|
Funguvisiwa kubwa kabisa duniani ni lile la Indonesia pamoja na Ufilipino linaloitwa pia Funguvisiwa la Malay.
|
20231101.sw_2512_3
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Funguvisiwa
|
Funguvisiwa
|
Bahari ya Pasifiki ina mafunguvisiwa mengi, pia sehemu ya Karibi ya Bahari ya Atlantiki karibu na Amerika ya Kati.
|
20231101.sw_2512_4
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Funguvisiwa
|
Funguvisiwa
|
Mafunguvisiwa muhimu ya Afrika ni Zanzibar, Shelisheli na Komoro katika Bahari Hindi, halafu Visiwa vya Kanari na Visiwa vya Madeira katika Atlantiki.
|
20231101.sw_2513_0
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Lamu%20%28maana%29
|
Lamu (maana)
|
Lamu (mji) - ni kati ya miji ya kale sana ya Waswahili kwenye pwani ya Afrika ya Mashariki; uko kwenye orodha ya UNESCO ya "Urithi wa Dunia"
|
20231101.sw_2513_1
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Lamu%20%28maana%29
|
Lamu (maana)
|
Lamu (wilaya) ilikuwa wilaya ya kiutawala wa Jamhuri ya Kenya iliyounganisha funguvisiwa pamoja na sehemu za bara jirani nayo
|
20231101.sw_2516_0
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Wilaya
|
Wilaya
|
Wilaya ni mgawanyo wa kiutawala au eneo lililotengwa kwa ajili ya utawala. Mikoa ya Tanzania na Kenya imegawiwa kwa wilaya.
|
20231101.sw_2516_1
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Wilaya
|
Wilaya
|
Asili ya neno ni Kiarabu "ولاية" (wilaayatun - Kituruki: vilayet). Katika Dola la Osmani "vilayet" ilikuwa ngazi ya kwanza ya mgawanyo wa kiutawala ikimaanisha jimbo au mkoa. Mkuu wake au gavana alikuwa na cheo cha "Wali". Neno hili la "wilaya" limepatikana katika nchi nyingi zilizoathiriwa na utamaduni wa Uislamu au lugha ya Kiarabu kama vile Uturuki, Algeria, Tunisia, Oman, Mauritania, Sudan, Malaysia, Indonesia, Afghanistan, Tajikistan, Turkmenistan na Uzbekistan.
|
20231101.sw_2516_2
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Wilaya
|
Wilaya
|
Katika Kiarabu cha Kisasa "wilaayatun" inamaanisha pia dola ndani ya shirikisho - kwa mfano madola kama vile Texas ndani ya Marekani.
|
20231101.sw_2516_3
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Wilaya
|
Wilaya
|
Katika matumizi ya Kiswahili huko Kenya na Tanzania "wilaya" imekuwa mgawanyo wa ngazi ya pili yaani ni kitengo chini ya ngazi ya kwanza ya mikoa. Vitengo vya wilaya ni tarafa. Na vitengo vya tarafa ni kata zinazoitwa shehia katika Zanzibar na chini yake vijiji au mitaa.
|
20231101.sw_2517_0
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mmomonyoko
|
Mmomonyoko
|
Mmomonyoko (kwa Kiingereza erosion) ni hali ya kuvunjika au kumegekamegeka kwa udongo au mwamba kutokana na athira ya upepo, maji, barafu, joto au mwendo wa ardhi. Kazi za binadamu zimekuwa pia sababu muhimu ya mmomonyoko.
|
20231101.sw_2517_1
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mmomonyoko
|
Mmomonyoko
|
Mmomonyoko ni kati ya nguvu muhimu zinazofinyanga uso wa dunia. Uso wa mabonde na milima ya dunia ni matokeo ya mmomonyoko.
|
20231101.sw_2517_2
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mmomonyoko
|
Mmomonyoko
|
Maji ni kati ya nguvu kuu za mmomonyoko. Mwendo wa maji unasukuma sehemu ndogo za ardhi na kuzipeleka mbali kabisa. Hata vipande vya mwamba vinaweza kukatwa hasa kwa mawe madogo yanayorushwa na maji dhidi ya miamba mikubwa.
|
20231101.sw_2517_3
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mmomonyoko
|
Mmomonyoko
|
Mwendo wa maji ya mito unaweza kuchimba mabonde makubwa. Ukali wake unategemea na kiasi cha maji, kasi yake na aina ya ardhi, kama ina mtelemko mkubwa au kama maji yamepita kwenye ardhi au juu ya miamba. Kama mtelemko ni mkubwa na ardhi ni laini ni rahisi kwa maji kukata bonde refu na kubwa.
|
20231101.sw_2517_4
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mmomonyoko
|
Mmomonyoko
|
Hata mtelemko wa mvua unaleta mmomonyoko. Matone yenyewe hugongagonga sehemu ndogo za ardhi na kuzibeba kidogo jinsi inavyoonekana vizuri baada ya mvua kwenye eneo penye mchanga.
|
20231101.sw_2517_5
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mmomonyoko
|
Mmomonyoko
|
Udongo wote pamoja na mawe madogo unaobebwa na maji hutuamishwa mahali fulani kama mashapo. Kwa njia hiyo maji yanaweza kutenganisha aina mbalimbali za mashapo. Kwa kawaida sehemu nzito hutelemka kwanza na kukaa kama mwendo wa maji unaanza kupungua wakati mto umetoka kwenye mtelemko na kuingia eneo la tambarare. Kwa njia hii aina za mashapo kama vile changarawe, mchanga, matamahuluku na udongo kabisa zinapatikana.
|
20231101.sw_2517_6
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mmomonyoko
|
Mmomonyoko
|
Mmomonyoko kwenye mwambao wa bahari au ziwa ni aina ya pekee ya mmomonyoko wa maji. Unatokea hasa kutokana na nguvu ya mawimbi na mikondo. Mikondo ya baharini hubeba muda wote mashapo kwa kuyachukua hapa na kuyatuamisha pale. Kama kiasi kilichochukuliwa kinazidi kiasi kilichotuamishwa mmomonyoko unatokea. Pale panapotuamishwa zaidi kuliko kuchukuliwa fungu linatokea.
|
20231101.sw_2517_7
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mmomonyoko
|
Mmomonyoko
|
Watu wakijenga karibu mno na bahari -kwa mfano mahoteli ya kitalii- wataona mara nyingi ya kwamba nyumba zinachukuliwa na bahari baada ya miaka kadhaa kwa sababu ya mmomonyoko wa pwani wa kawaida.
|
20231101.sw_2517_8
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mmomonyoko
|
Mmomonyoko
|
Upepo unaweza kupuliza chembe ndogo za udongo kama udongo huu ni laini na kavu. Aina hii ya mmomonyoko hutokea hasa pasipo na mimea inayofunika udongo wa juu. Jangwani kiasi kikubwa cha udongo au mchanga huhamishwa na dhoruba.
|
20231101.sw_2517_9
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mmomonyoko
|
Mmomonyoko
|
Upepo ukibeba machanga unaweza kusababisha hata mmomonyoko kwa miamba. Mchanga unarushwa na upepo kwa kasi kubwa dhidi ya mwamba na kuisagasaga.
|
20231101.sw_2517_10
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mmomonyoko
|
Mmomonyoko
|
Barafu ikipatikana kama barafuto (ganda nene la barafu inayoanza kutiririka polepole na kujisukuma mbele)ina uwezo wa kuvunja mawe na miamba mikubwa kabisa na kuzisukuma mbali. Barafuto isipoishia baharini inatoa mito inayoendeleza kazi ya mmomonyoko wa maji.
|
20231101.sw_2517_11
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mmomonyoko
|
Mmomonyoko
|
Njia nyingine ya barafu kufinyanga uso wa dunia hutokea pale ambako maji yanaingia kwa mashimo au safu ndogo katika mwamba. Hali ya hewa ikishuka chini ya 0° C majai haya yanaganda na kupanuka hivyo kuvunja mwamba.
|
20231101.sw_2517_12
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mmomonyoko
|
Mmomonyoko
|
Mabadiliko kutokana na kazi za kibinadamu yalisababisha mara nyingi mmomonyoko wa ghafla unaoshtusha na kuleta hasara. Mfano ni kukata miti hasa kwenye mitelemko ya milima au kulima milimani. Kazi hizi zinapunguza au kuondoa kabisa funiko la mimea na kuacha udongo bila hifadhi. Maji ya mvua na upepo hazina vizuizi tena.
|
20231101.sw_2517_13
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mmomonyoko
|
Mmomonyoko
|
Matokeo yake ni mafuriko ya ghafla kwa sababu wakati wa mvua maji huteremka haraka na mara moja yakichimba mifereji, kuharibu nyumba, kuua watu na kuondoa ardhi yenye rutuba kwenye mashamba.
|
20231101.sw_2517_14
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mmomonyoko
|
Mmomonyoko
|
Njia nyingine ni mmomonyoko kutokana na kuzidi kwa mifugo. Kazi ya kukanyaga kwa miguu mingi hasa kwenye njia zilezile zinazotumika kuzunguka kati ya boma, maji na sokoni kumeleta uharibifu mwingi. Kwato za mifugo kama ng'ombe, mbuzi, punda na wanyama wengine wafugwao huathiri udongo mara wanapokanyaga mara kwa mara na hivyo hufanya udongo huo kuwa rahisi kusombwa na wakala wa mmomonyoko, kama vile maji, barafu na upepo.
|
20231101.sw_2522_0
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Liwali
|
Liwali
|
Asili ni neno la Kiarabu "الوالي" al-wali linalomaanisha mtawala wa mahali au eneo asiyejitegemea bali aliyeteuliwa na serikali kushughulikia mambo ya utawala katika eneo fulani. Mara nyingi katika nchi za utamaduni wa Uislamu Wali alisimamia "wilaya". Kazi yake ililingana na "gavana".
|
20231101.sw_2522_1
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Liwali
|
Liwali
|
Katika eneo la Waswahili neno al-wali lilikuwa "liwali" na lilimtaja mkuu wa mahali au wa mji. Masultani wa Zanzibar waliteua maliwali kwa ajili ya miji ya pwani waliokuwa wawakilishi wa sultani mahali walipo.
|
20231101.sw_2522_2
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Liwali
|
Liwali
|
Mwaka 1886 kulikuwa na maliwali wafuatao wa Zanzibar kwenye pwani ya Afrika ya Mashariki: Tungi, Mikindani, Lindi, Kilwa Kivinje, Kikunye, Kisiju
|
20231101.sw_2522_3
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Liwali
|
Liwali
|
Katika mfumo wa utawala wa Kiingereza katika Afrika ya Mashariki liwali ilikuwa cheo cha afisa wa ngazi ya juu zaidi kilichopatikana kwa wazawa katika utawala wa miji.
|
20231101.sw_2522_4
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Liwali
|
Liwali
|
Cheo hiki kiliendelezwa kwenye pwani ya Kenya baada ya Uingereza kuchukua mamlaka juu ya pwani kutoka Sultani wa Zanzibar; liwali alipaswa kuwa Mwislamu. Alisimamia mahakama ya liwali iliyokuwa ngazi ya juu za mahakama za Kiislamu zilizoamua kesi za mali, ndoa na urithi baina ya Waislamu waliokuwa Waafrika wazalendo au kutoka nchi nyingine, Waarabu au Wahindi.
|
20231101.sw_2522_5
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Liwali
|
Liwali
|
Katika Afrika ya Mashariki ya Kijerumani Wajerumani waliendelea mwanzoni na maliwali waliorithi kutoka kwa Sultani lakini baadaye nafasi yao ilichukuliwa na afisa Mjerumani. Baada ya eneo kutekwa na Uingereza na kuitwa Tanganyika cheo cha liwali kilirudishwa mwaka 1921 kama cheo cha "native administration" ya miji. Kwa mfano mjini Dar es Salaam liwali alikuwa daima Mwislamu kutoka ukoo wa Kiarabu hadi uhuru. Aliwajibika na usimamizi wa mahakama yake alikoshika pia nafasi ya jaji akasimamia pia ukusanyaji wa kodi. Alikuwa na haki ya kuamulia adhabu ya kiboko "hadi viboko sita".
|
20231101.sw_2522_6
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Liwali
|
Liwali
|
James Norman Dalrymple Anderson, Islamic Law in Africa, reprint Routledge, 2008, ISBN 0415426006, 9780415426008
|
20231101.sw_2522_7
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Liwali
|
Liwali
|
James R. Brennan & alii, Dar es Salaam. Histories from an Emerging African Metropolis, African Books Collective, 2007, ISBN 9987449700, 9789987449705
|
20231101.sw_2522_8
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Liwali
|
Liwali
|
James R. Brennan, Taifa: Making Nation and Race in Urban Tanzania, Ohio University Press, 2012, ISBN 0821444174, 9780821444177
|
20231101.sw_2523_0
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Azimio%20la%20Dodoma
|
Azimio la Dodoma
|
Azimio la Dodoma ni makubaliano ya wanablogu wa Kiswahili wa Tanzania waliokutana jijini Dodoma kuhusu njia za kuendeleza blogu za wanablogu wa Tanzania kwa kuwa na maadili yanayoendana na utu, heshima, na kanuni za uandishi wa habari. Mkutano huo ulifanyika 7 Aprili 2006.
|
20231101.sw_2529_0
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Urithi%20wa%20Dunia
|
Urithi wa Dunia
|
Urithi wa Dunia ni maeneo yenye thamani kubwa ya kiutamaduni au kimazingira duniani yanayoangaliwa na shirika la UNESCO.
|
20231101.sw_2529_1
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Urithi%20wa%20Dunia
|
Urithi wa Dunia
|
Hadi Septemba 2023 sehemu 1,172 katika nchi 166 zimekubaliwa. Nchi zinazoongoza kwa wingi wa mahali ni Italia (59) na China (57) zikifuatwa na Ujerumani (52), Ufaransa (51) na Hispania (50).
|
20231101.sw_2529_2
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Urithi%20wa%20Dunia
|
Urithi wa Dunia
|
Afrika ina mahali 147 (8.56%) katika nchi 46, zikiongoza Afrika Kusini (10), Ethiopia na Moroko (9), Tunisia (8), Algeria, Misri, Senegal na Tanzania (7).
|
20231101.sw_2529_3
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Urithi%20wa%20Dunia
|
Urithi wa Dunia
|
Orodha rasmi ya UNESCO ina mahali 913 pa urithi wa dunia wa kiutamaduni na mahali 220 pa urithi wa dunia wa kimazingira, mbali ya 39 pa mseto.
|
20231101.sw_2529_4
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Urithi%20wa%20Dunia
|
Urithi wa Dunia
|
Mwanzo wa jitihada za kuhifadhi urithi wa dunia ulikuwa ujenzi wa bwawa la Assuan lililoelekea kuzamisha majengo mbalimbali ya utamaduni wa Misri na Nubia wa kale chini ya maji. Wakati ule UNESCO ilifaulu kukusanya pesa ili hekalu la Abu Simbel liweze kuhamishwa mlimani kabla ya kujaa kwa bwawa.
|
20231101.sw_2529_5
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Urithi%20wa%20Dunia
|
Urithi wa Dunia
|
Tangu 1972 kuna mkataba wa kimataifa wa Stockholm kuhusu hifadhi ya urithi wa dunia kiutamaduni na kimazingira.
|
20231101.sw_2529_6
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Urithi%20wa%20Dunia
|
Urithi wa Dunia
|
Kamati ya Urithi wa Dunia hukutana kila mwaka na kuangalia maombi ya kupokelewa katika orodha ya urithi wa dunia. Kamati inapokea taarifa kuhusu hifadhi na hali ya urithi uliopo tayari orodhani. Kila baada ya miaka miwili orodha inatolewa upya.
|
20231101.sw_2529_7
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Urithi%20wa%20Dunia
|
Urithi wa Dunia
|
KML file of the World Heritage List – Official KML version of the list for Google Earth and NASA Worldwind
|
20231101.sw_2529_8
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Urithi%20wa%20Dunia
|
Urithi wa Dunia
|
UNESCO Information System on the State of Conservation of World Heritage properties – Searchable online tool with over 3.400 reports on World Heritage sites
|
20231101.sw_2529_9
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Urithi%20wa%20Dunia
|
Urithi wa Dunia
|
Convention Concerning the Protection of the World Cultural and Natural Heritage – Official 1972 Convention Text in 7 languages
|
20231101.sw_2532_0
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Somalia
|
Somalia
|
Somalia (kwa Kisomali: Soomaaliya), ambayo inajulikana rasmi kama Jamhuri ya Shirikisho ya Somalia, ni nchi kwenye pwani ya Afrika ya Mashariki katika Pembe ya Afrika.
|
20231101.sw_2532_1
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Somalia
|
Somalia
|
Kijiografia, imezungukwa upande wa kaskazini-mashariki na Ethiopia na Jibuti, na upande wa magharibi ya kati na Kenya; Ghuba ya Aden nayo iko mashariki.
|
20231101.sw_2532_2
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Somalia
|
Somalia
|
Kuanzia mwaka 1888 Italia ilijipatia mikataba ya ulinzi na masultani mbalimbali waliotawala maeneo madogo kwenye Pembe ya Afrika. Walitangulia 1889 na sultani ya bandari ya Hobyo na mtawala wa usultani wa Majerteen.
|
20231101.sw_2532_3
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Somalia
|
Somalia
|
Mwaka 1892 Usultani wa Zanzibar ulikodisha bandari ya Banadir kati ya Mogadishu hadi Brava kwa Italia. Mwaka 1905 Italia ilinunua eneo hili kutoka Zanzibar na kulitangaza kuwa koloni na Mogadishu kuwa mji mkuu.
|
20231101.sw_2532_4
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Somalia
|
Somalia
|
Baada ya Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia Waitalia walikabidhiwa na Uingereza eneo la Kismayu. Walilitawala kwa jina la "Oltre Giuba" (ng'ambo ya mto Juba) na kuliunganisha na Somalia ya Kiitalia tarehe 30 Juni 1926.
|
20231101.sw_2532_5
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Somalia
|
Somalia
|
Wakati uleule waliamua kumaliza hali ya sultani za Majarteen na Hobyo kuwa nchi lindwa na kuzifanya sehemu kamili za koloni. Mipango hiyo ilisababisha vita kali ya miaka miwili kwa sababu masultani waliona mikataba yao ya ulinzi ilivunjwa wakapinga jeshi la Italia.
|
20231101.sw_2532_6
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Somalia
|
Somalia
|
Wakati wa Vita Kuu ya Pili ya Dunia makoloni ya Italia yalivamiwa na Uingereza uliotawala Somalia tangu 1941.
|
20231101.sw_2532_7
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Somalia
|
Somalia
|
Uingereza uliingia katika eneo hili baada ya Misri kuondoka mwaka 1885 kwa kushindwa na jeshi la Mahdi huko Sudan. Uingereza uliingia kwa sababu iliona umuhimu wa kutawala pande zote mbili za Bab el Mandeb ikihofia uenezaji wa nchi nyingine za Ulaya, hasa Ufaransa iliyokuwa na koloni la kwanza ya Ubuk (Obok) katika Jibuti ya leo tangu 1862. Pamoja na hayo Waingereza walitegemea kununua nyama kwa ajili ya mji wa Aden na meli zilizopita hapo kati ya Uhindi na Ulaya.
|
20231101.sw_2532_8
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Somalia
|
Somalia
|
Somaliland ilitawaliwa awali kama mkoa wa Uhindi wa Kiingereza ikawa baadaye chini ya wizara ya makoloni huko London.
|
20231101.sw_2532_9
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Somalia
|
Somalia
|
Hata kama Uingereza haukuwa na nia ya kuingilia mno maisha ya wenyeji ulikutana na upinzani mkali kuanzia mwaka 1899 kutoka kwa kiongozi wa dini Diiriye Guure, aliyeitwa na Waingereza "Mullah majununi". Waingereza walijibu kwa ukatili katika vita vya miaka 20 iliyoua takriban theluthi moja ya wakazi wote wa eneo.
|
20231101.sw_2532_10
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Somalia
|
Somalia
|
Mwishowe Uingereza iliweza kumaliza upinzani kwa teknolojia mpya ya eropleni za kijeshi zilizotumia mabomu na bunduki za mtombo kutoka angani kwa mara ya kwanza katika Afrika.
|
20231101.sw_2532_11
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Somalia
|
Somalia
|
Wakati wa Vita Kuu ya Pili ya Dunia eneo likatwaliwa na Italia katika Agosti 1940 lakini lilichukuliwa tena na Uingereza katika Machi 1941.
|
20231101.sw_2532_12
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Somalia
|
Somalia
|
Mwaka 1960 utawala wa kikoloni ulikwisha na Somalia ikapata uhuru wake, ikiunganisha makoloni mawiliː la Waitalia (kusini) na la Waingereza (kaskazini).
|
20231101.sw_2532_13
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Somalia
|
Somalia
|
Baada ya mwaka 1991 nchi ya Somalia ilibaki haina serikali wala umoja wa taifa, bali iligawiwa na wakereketwa na wanamgambo wa ukoo na eneo, hasa Somaliland, Puntland na Galmudug upande wa kaskazini.
|
20231101.sw_2532_14
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Somalia
|
Somalia
|
Katika miaka 2008-2013 ilihesabika kama nchi filisika. Kwa sasa ni nchi dhaifu lakini inaanza kujengwa upya kama shirikisho na kujiandaa kujiunga na Jumuiya ya Afrika Mashariki.
|
20231101.sw_2532_15
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Somalia
|
Somalia
|
Kisomali ndiyo lugha ya kawaida ya wakazi wengi na lugha rasmi pamoja na Kiarabu. Kati ya lugha nyingine zinazotumika nchini, mojawapo ni Kiswahili (lahaja za Chimbalanzi na Kibajuni).
|
20231101.sw_2532_16
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Somalia
|
Somalia
|
Mawasiliano ya Jamhuri ya Somalia ilikaribia kuangamia kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe, lakini kwa sasa kampuni za binafsi za mawasiliano ya mitambo, zimetwaa karibu miji yote Somalia, na hata kutoa huduma njema kuliko nchi zilizo jirani.
|
20231101.sw_2532_17
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Somalia
|
Somalia
|
Somalia ni nchi mojawapo Afrika ambayo ina mawasiliano ya bei rahisi zaidi, pengine kwa kuwa Somalia haikuwa na serikali iliyotoza ushuru; (Telecoms thriving in lawless Somalia)
|
20231101.sw_2532_18
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Somalia
|
Somalia
|
Mauri, Arnaldo, Somalia, in G, Dell'Amore (ed.), "Banking Systems of Africa", Cariplo-Finafrica, Milan, 1971, pp. 209–217.
|
20231101.sw_2550_0
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Barafuto
|
Barafuto
|
Barafuto huitwa pia "mto wa barafu". Ni kanda kubwa la barafu iliyoanza kutambaa kutokana na uzito wake ikifuata graviti kwenye mtelemko. Kwa sababu hiyo barafuto zinapatikana hasa mlimani.
|
20231101.sw_2550_1
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Barafuto
|
Barafuto
|
Barafuto zimetokana na theluji inayokaa miaka mingi bila kuyeyuka katika mazingira baridi. Theluji mpya inakaa juu ya theluji ya miaka iliyotangulia. Uzito wa theluji ya baadaye inakandamiza ile ya chini. Kutokana na shindikizo hili theluji ya chini hubadilika kuwa barafu kabisa.
|
20231101.sw_2550_2
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Barafuto
|
Barafuto
|
Afrika ina barafuto ndogo kadhaa juu ya mlima Kilimanjaro na mlima Kenya lakini zinaelekea kupotea kutokana na uhaba wa mvua itakayobadilika kuwa theluji mpya.
|
20231101.sw_2550_3
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Barafuto
|
Barafuto
|
Zamani za enzi ya barafu kiwango cha barafu kwenye ncha ya kaskazini kilikuwa kikubwa kiasi cha kusababisha barafuto kutokea zilizosukuma barafu hadi Ulaya ya Kati.
|
20231101.sw_2551_0
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Utaridi
|
Utaridi
|
Utaridi (alama: ; kwa Kiingereza Mercury) ni sayari iliyo karibu zaidi na jua letu katika mfumo wa Jua.
|
20231101.sw_2551_1
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Utaridi
|
Utaridi
|
Jina lake limetokana na Kiarabu عطارد (soma ʿuṭaarid) inayomaanisha "mwendo wa haraka" kwa sababu kasi ya Utaridi inapita mwendo wa sayari nyingine kutokana na njia yake fupi ya kuzunguka Jua katika siku 88 pekee.
|
20231101.sw_2551_2
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Utaridi
|
Utaridi
|
Majina ya Wagiriki wa Kale "Hermes" na Waroma wa Kale "Mercurius" yalikuwa majina ya mungu wao aliyekuwa na kazi ya kuwasilisha habari za miungu wengine aliyeaminiwa kuwa na kasi kubwa kwa kazi hii: chaguo hili lilitokana na tabia ileile ya sayari. Jina hili la Kiroma Mercurius limeingia katika lugha nyingi za Ulaya.
|
20231101.sw_2551_3
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Utaridi
|
Utaridi
|
Umbo la Kiarabu limekuwa jina la watu katika nchi nyingi zilizoathiriwa na utamaduni wa Kiislamu, pia jina la sayari ya kwanza kwa mfano katika Kituruki na Kimalaysia.
|
20231101.sw_2551_4
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Utaridi
|
Utaridi
|
Katika vitabu kadhaa vya Kiswahili sayari inaitwa Zebaki lakini hii inaonekana ni kosa lililotokana na jina la Kiingereza "Mercury" kwa sayari hii. Mercury ni pia jina la metali inayoitwa zebaki kwa Kiswahili kutokana na Kiarabu زئبق (soma ziʾbaq).
|
20231101.sw_2551_5
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Utaridi
|
Utaridi
|
Mara chache neno "utaridi" limetumiwa kutaja sayari kibete ya "Pluto" lakini hii ni kwa kukosea pia.
|
20231101.sw_2551_6
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Utaridi
|
Utaridi
|
Utaridi ni sayari ndogo. Kipenyo chake kwa ikweta ni 4879.4 km. Kwa sababu iko karibu sana na jua ina mbio za haraka. Mwaka wa Utaridi ambayo ni muda wa kuzunguka jua ni siku 88 za dunia pekee.
|
20231101.sw_2551_7
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Utaridi
|
Utaridi
|
Inazunguka kwenye mhimili wake katika muda wa siku 58.6 za dunia. Kutokana na kuwa karibu na jua kuna joto kali upande unaotazama jua lakini upande wa usiku ni baridi kabisa kutokana na uhaba wa hewa inayoweza kutunza halijoto. Halijoto ya wastani ni +178.8 °C, (usiku -183.15 °C na mchana +426.85 °C).
|
20231101.sw_2551_8
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Utaridi
|
Utaridi
|
Mwaka 2012 barafu ya maji ilitambuliwa kwenye data kutoka chombo cha angani MESSENGER iliyochunguza sayari hii. Barafu inapatikana karibu na ncha ya kaskazini isiyofikiwa na miale ya jua.
|
20231101.sw_2551_9
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Utaridi
|
Utaridi
|
Uhaba wa hewa umesababisha uso wa sayari kujaa mashimo ya kasoko. Kasoko hizi zimesababishwa kwa kugongwa na meteoridi. Angahewa kama duniani ingeangamiza meteoridi ndogo na kusababisha kupasuka kwa kubwa lakini Utaridi zote zinafika usoni bila kizuizi. Alama za meteoridi ni mmomonyoko wa pekee unaoonekana hakuna dalili ya mmomonyoko kutokana na hewa au maji ya awali.
|
20231101.sw_2551_10
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Utaridi
|
Utaridi
|
Kutokana na kuwa karibu sana na jua Utaridi inaonekana kama nyota kwa macho katika masaa ya pambazuko na machweo pekee.
|
20231101.sw_2552_0
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mshtarii
|
Mshtarii
|
Mshtarii (alama: ; pia Mshiteri, Mushtarii au Mshatira, kutokana na Kiarabu المشتري al-mushtari; na hata Jupita kutokana na Kiingereza Jupiter) ni sayari ya tano toka kwenye jua katika Mfumo wa jua na sayari zake.
|
20231101.sw_2552_1
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mshtarii
|
Mshtarii
|
Mshtarii ni sayari kubwa kabisa ya jua letu. Masi yake inazidi mara mbili na nusu masi ya sayari zingine zote pamoja.
|
20231101.sw_2552_2
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mshtarii
|
Mshtarii
|
Mshtarii haina uso unaoonekana. Sehemu kubwa ya masi ya sayari ni elementi nyepesi kama hidrojeni na heli ambazo ni gesi katika mazingira ya duniani. Hii ndiyo sababu ya kwamba sayari kubwa za Mshtarii pamoja na Zohali huitwa "sayari jitu za gesi".
|
20231101.sw_2552_3
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mshtarii
|
Mshtarii
|
Kadiri gesi hizo zinavyopatikana chini zaidi (yaani kuelekea ndani) uzito wa matabaka ya juu unaongeza shinikizo katika vilindi vyake na kusababisha gesi za angahewa kuingia katika hali ya giligili (majimaji) inayobadilika kuwa mango (imara) ndani zaidi. Zamani iliaminika ya kwamba sayari yote ni ya gesi iliyoganda lakini siku hizi wataalamu wa astronomia huamini kwamba kuna kiini cha mwamba au metali.
|
20231101.sw_2552_4
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mshtarii
|
Mshtarii
|
Doa jekundu linaloonekana usoni mwa angahewa ni dhoruba ya tufani kubwa sana iliyotazamwa tangu darubini za kwanza zilipopatikana. Duniani tufani zinapotea kwa kawaida baada ya wiki kadhaa lakini doa jekundu limeendelea bila kusimama kwa miaka 300.
|
20231101.sw_2552_5
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mshtarii
|
Mshtarii
|
Miezi minne mikubwa ilitambuliwa mwaka 1610 na Galileo Galilei aliyekuwa kati ya wanaastronomia wa kwanza kutumia darubini. Ndiyo Io, Europa, Ganimedi na Kallisto. Ukubwa wa Ganimedi unakaribia kipenyo cha Utaridi ukipita kile cha Pluto. Miezi 63 huwa na kipenyo chini ya kilomita 10. Mwezi mdogo kabisa wa Mshtarii unajulikana kwa namba tu na una kipenyo cha km 1.
|
20231101.sw_2553_0
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Laki
|
Laki
|
Laki (pia Lakhi) ni neno lenye asili ya Kihindi linalotumika kutaja namba 100,000, ambayo inafuata 99,999 na kufuatwa na 100,001. Inaweza kuandikwa pia 105.
|
20231101.sw_2553_1
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Laki
|
Laki
|
Neno limeingia katika Kiswahili kutokana na historia ndefu ya mawasiliano ya kibiashara kati ya Bara Hindi na pwani ya Afrika ya Mashariki.
|
20231101.sw_2555_0
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mwezi
|
Mwezi
|
Mwezi (alama: ) ni gimba la angani linalozunguka sayari, sayari kibete au asteroidi fulani. Kuna miezi mingi katika anga-nje. Vipindi vya kuonekana kwa mwezi wa Dunia vilisababisha matumizi ya "mwezi" kama majira ya wakati.
|
20231101.sw_2555_1
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mwezi
|
Mwezi
|
Mabadiliko ya kuonekana kwake yalisababisha katika Kiswahili neno "mwezi" litumike kama kipindi cha wakati. Awamu zake nne pengine ndizo chanzo cha majuma ya siku sabasaba.
|
20231101.sw_2555_2
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mwezi
|
Mwezi
|
Sayari inaweza kukosa mwezi au kuwa na miezi mingi. Mshtarii na Zohali ina miezi zaidi ya 80, mingine mikubwa kama sayari ndogo, mingine midogo yenye kipenyo cha km 1 tu. Dunia yetu ina mwezi mmoja tu. Utaridi haina mwezi.
|
20231101.sw_2555_3
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mwezi
|
Mwezi
|
Mwezi hauna nuru ya kwake yenyewe bali unang'aa kutokana na nuru ya jua inayoakisiwa usoni mwake kama kwenye kioo.
|
20231101.sw_2555_4
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mwezi
|
Mwezi
|
Mwezi wa dunia yetu ni kati ya miezi mikubwa kwenye mfumo wa Jua. Hakuna jina tofauti kuliko "Mwezi" isipokuwa watu wametumia pia jina la Kilatini "Luna" wakitaja Mwezi wetu ili kuutofautisha na miezi ya sayari nyingine. Katika Wikipedia hi tunajitahidi kuandika "Mwezi" kwa gimba linalozunguka Dunia na "mwezi" kama habari inahusu sayari nyingine.
|
20231101.sw_2555_5
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mwezi
|
Mwezi
|
Mwezi wetu huwa na umbo la tufe lakini si tufe kamili. Kipenyo cha wastani ni kilomita 3,476 ambacho ni takribani robo ya kipenyo cha Dunia. Mwezi unazunguka dunia yetu kwenye obiti chenye umbo la duaradufu. Umbali wake na Dunia ni baina ya kilomita 363,300 hadi 405,500 kutoka Dunia.
|
20231101.sw_2555_6
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mwezi
|
Mwezi
|
Huwa tunaangalia uso wake upande mmoja, tena uleule tu. Sababu yake ni ya kwamba mzunguko wa Mwezi kwenye mhimili wake ni sawa na kipindi cha obiti ya kuzunguka Dunia mara moja. Kipindi cha obiti yake ni siku 27 , masaa 7, dakika 43 na sekunde 11.5. Upande wa nyuma wa Mwezi uko gizani wakati sisi tunaona mwezi mpevu. Wakati wa mwezi mwandamo kwetu upande wa nyuma unapokea nuru ya Jua. .
|
20231101.sw_2555_7
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mwezi
|
Mwezi
|
Uso wa Mwezi unajaa mashimo ya kasoko yaliyosababishwa kwa kugongwa na meteoridi. Mwezi hauna angahewa inayozuia mapigo ya meteoridi ndogo au kupunguzu nguvu yao jinsi ilivyo duniani.
|
20231101.sw_2555_8
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mwezi
|
Mwezi
|
Uso wa mwezi jinsi unavyoonekana duniani hubadilikabadilika. Mwezi mpevu unaonekana kama duara kamili la kung'aa lakini baada ya kuonekana hivi umbo linapungua kila siku hadi kutoonekana kabisa na hali hii huitwa mwezi mwandamo. Baadaye mwezi unaonekana tena kama hilali nyembamba na kuongezeka hadi kuwa duara tena. Muda wa mabadiliko yote kupita mara moja ni siku 29 na robo.
|
Subsets and Splits
No community queries yet
The top public SQL queries from the community will appear here once available.