_id
stringlengths
15
22
url
stringlengths
31
150
title
stringlengths
1
86
text
stringlengths
100
23.8k
20231101.sw_2561_1
https://sw.wikipedia.org/wiki/Zimbabwe
Zimbabwe
Imepakana na Afrika ya Kusini upande wa kusini, Botswana upande wa magharibi, Zambia upande wa kaskazini-mashariki, na Msumbiji upande wa mashariki.
20231101.sw_2561_2
https://sw.wikipedia.org/wiki/Zimbabwe
Zimbabwe
Jina Zimbabwe linatokana na neno "dzimba dzamabwe" linalomaanisha "nyumba ya mawe" kwa lugha ya Kishona. Nyumba hiyo ya mawe, ambayo imehifadhiwa kama eneo la kihistoria, ilikuwa makao ya Ufalme wa Mutapa ambaye mfalme wake aliongoza eneo hilo miaka ya kale.
20231101.sw_2561_3
https://sw.wikipedia.org/wiki/Zimbabwe
Zimbabwe
Zimbabwe imegawiwa katika mikoa 8 na miji 2 yenye hadhi ya mikoa. Imegawiwa zaidi katika wilaya 59 na kata 1,200.
20231101.sw_2561_4
https://sw.wikipedia.org/wiki/Zimbabwe
Zimbabwe
Tangu karne ya 11, Zimbabwe ya leo imekuwa na falme imara kwenye njia muhimu ya biashara, hasa ufalme wa Mutapa.
20231101.sw_2561_5
https://sw.wikipedia.org/wiki/Zimbabwe
Zimbabwe
Baada ya miaka 14 ya kutengwa kimataifa na kupigana na raia Waafrika katika miaka ya 1970, mapatano ya mwaka 1979 yalikubali wakazi wote wawe na haki ya kupiga kura na nchi ikawa huru kweli kwa jina la Zimbabwe mwaka 1980.
20231101.sw_2561_6
https://sw.wikipedia.org/wiki/Zimbabwe
Zimbabwe
Rais Robert Mugabe alipata umaarufu katika siasa kama mpiganaji dhidi ya ukoloni lakini pia kama aina ya dikteta aliyerudisha nyuma uchumi wa nchi.
20231101.sw_2561_7
https://sw.wikipedia.org/wiki/Zimbabwe
Zimbabwe
Baada ya yeye kulazimishwa na wanajeshi kujiuzulu, tarehe 24 Novemba 2017 Emmerson Mnangagwa amekuwa rais mpya wa Zimbabwe.
20231101.sw_2561_8
https://sw.wikipedia.org/wiki/Zimbabwe
Zimbabwe
Wakazi wengi (82%) ni wa kabila la Washona, 14% ni Wandebele, 2% ni wa makabila mengine ya Kiafrika, 1% ni machotara, Wahindi, Wazungu n.k.
20231101.sw_2561_9
https://sw.wikipedia.org/wiki/Zimbabwe
Zimbabwe
Kwa sasa lugha rasmi ni 16. Lugha kubwa ni Kishona (70%) na Kindebele (20%). Kiingereza ni lugha ya kwanza ya chini ya asilimia 2.5% za wakazi.
20231101.sw_2561_10
https://sw.wikipedia.org/wiki/Zimbabwe
Zimbabwe
Upande wa dini, 84.1% ni Wakristo (hasa Waanglikana, Wakatoliki 8%, Wasabato na Wamethodisti). Waliobaki ni wafuasi wa dini asilia za Kiafrika (4.5%), ni Waislamu (0.7%), au hawana dini (10.2%) .
20231101.sw_2561_11
https://sw.wikipedia.org/wiki/Zimbabwe
Zimbabwe
Zimbabwe Situation A comprehensive collection of news stories concerning Zimbabwe from different sources
20231101.sw_2561_12
https://sw.wikipedia.org/wiki/Zimbabwe
Zimbabwe
Economic Development Bulletin (Maelezo ya maedeleo ya uchumi) kupoteza haki ya mali Zimbabwe na udhoofu wa uchumi.
20231101.sw_2561_13
https://sw.wikipedia.org/wiki/Zimbabwe
Zimbabwe
Center for Global Development (senta ya maedeleo ya dunia) garama na mwanzo wa misukosuko Zimbabwe.
20231101.sw_2563_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kilindi
Kilindi
Kilindi (Unguja Kaskazini), kata ya Wilaya ya Unguja Kaskazini 'A' katika Mkoa wa Kaskazini Unguja, Tanzania
20231101.sw_2565_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/Wilaya%20ya%20Handeni
Wilaya ya Handeni
Handeni ilikuwa wilaya ya Mkoa wa Tanga katika Tanzania hadi kugawiwa katika Wilaya ya Handeni Mjini na Wilaya ya Handeni Vijijini mnamo mwaka 2012.
20231101.sw_2565_1
https://sw.wikipedia.org/wiki/Wilaya%20ya%20Handeni
Wilaya ya Handeni
Imepakana na wilaya ya Kilindi upande wa magharibi, wilaya ya Korogwe na Mkoa wa Kilimanjaro upande wa kaskazini, wilaya ya Pangani upande wa mashariki na Mkoa wa Pwani kwa kusini.
20231101.sw_2565_2
https://sw.wikipedia.org/wiki/Wilaya%20ya%20Handeni
Wilaya ya Handeni
Wilaya ya Handeni ilikuwa na tarafa 7 kata 19 na vijiji 112. Tarafa zilizopo ni Chanika, Sindeni, Mkumburu, Magamba, Kwamsisi, Mzundu na Mazingara. Kata zilizopo nia kama zifuatazo:
20231101.sw_2569_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/Rungwe%20%28wilaya%29
Rungwe (wilaya)
Wilaya ya Rungwe ni kati ya wilaya 8 za Mkoa wa Mbeya katika Tanzania yenye Postikodi namba 53500. Imepakana na Wilaya ya Mbeya vijijini upande wa kaskazini, Mkoa wa Iringa upande wa mashariki, Wilaya ya Kyela upande wa kusini-mashariki, Wilaya ya Ileje kwa kusini-magharibi na Mbeya Mjini kwa magharibi. Makao makuu ya wilaya yako Tukuyu.
20231101.sw_2569_1
https://sw.wikipedia.org/wiki/Rungwe%20%28wilaya%29
Rungwe (wilaya)
Jina la wilaya limetokana na kituo cha misioni ya Moravian cha Rungwe kilichopo kwenye mitelemko ya mlima wa Rungwe takriban km 20 kutoka Tukuyu.
20231101.sw_2569_2
https://sw.wikipedia.org/wiki/Rungwe%20%28wilaya%29
Rungwe (wilaya)
Rungwe ni hasa eneo la Wanyakyusa ikishika sehemu kubwa ya eneo la Unyakyusa lililoitwa kihistoria pia "Konde".
20231101.sw_2579_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kur%C3%B3w
Kurów
Kurów ni kijiji katika Poland ya Kusini-Mashariki kwenye mto wa Kurowka. Iko katikati ya miji ya Pulawy na Lublin katika wilaya ya Lublin. Ina wakazi 2811 (2005).
20231101.sw_2579_1
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kur%C3%B3w
Kurów
Katika karne ya 15 BK kijiji kilipewa cheo cha mji chini ya sheria ya mji ya Magdeburg. Katika karne ya 16 BK ikawa kati ya miji ya Poland iliyopokea Uprotestanti.
20231101.sw_2579_2
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kur%C3%B3w
Kurów
Wakati wa migawanyiko ya Poland ikawa mwanzoni chini ya Austria, baadaye chini ya Urusi. Tangu 1918 imekuwa tena sehemu ya dola la Poland iliyoanzishwa upya.
20231101.sw_2579_3
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kur%C3%B3w
Kurów
Wojciech Jaruzelski aliyekuwa kwanza waziri mkuu, halafu rais wa Poland kati ya 1981 hadi 1990 alizaliwa Kurow.
20231101.sw_2580_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/Angola
Angola
Angola ni nchi kubwa iliyopo upande wa kusini magharibi wa bara la Afrika ikipakana na Namibia, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Zambia. Upande wa magharibi kuna pwani ndefu ya Bahari Atlantiki. Mkoa wa Kabinda umetenganika na sehemu nyingine za nchi na unapakana na Jamhuri ya Kongo pia.
20231101.sw_2580_1
https://sw.wikipedia.org/wiki/Angola
Angola
Angola ni nchi tajiri kwa mafuta na madini: almasi ndiyo muhimu zaidi. Lakini nchi ni maskini kutokana na vita vya miaka 29; kwanza vita vya kupigania uhuru dhidi ya Ureno iliyofuatwa na vita ya wenyewe kwa wenyewe hadi mwaka 2002.
20231101.sw_2580_2
https://sw.wikipedia.org/wiki/Angola
Angola
Nchi yenyewe hasa ni ya kidemokrasia na inajulikana kama Jamhuri ya Angola (kwa Kireno: República de Angola, kwa matamshi ya IPA: //; kwa lugha za wenyeji: Repubilika ya Ngola).
20231101.sw_2580_3
https://sw.wikipedia.org/wiki/Angola
Angola
Jina Angola linatokana na neno la lugha ya Kibantu "N’gola", ambalo lilikuwa jina la kiongozi wa ufalme wa Kwimbundo karne ya 16, ambapo Wareno walianza ukoloni katika eneo hili.
20231101.sw_2580_4
https://sw.wikipedia.org/wiki/Angola
Angola
Katika karne za kwanza BK kutoka kaskazini walifika wahamiaji Wabantu wenye ujuzi wa kilimo na uhunzi.
20231101.sw_2580_5
https://sw.wikipedia.org/wiki/Angola
Angola
Kuanzia karne ya 14, falme mbalimbali zilienea sehemu za Angola, kwa mfano Dola la Kongo, Dola la Lunda na Dola la Kasanje.
20231101.sw_2580_6
https://sw.wikipedia.org/wiki/Angola
Angola
Dola la Kongo lilikuwa ufalme ulioenea ndani ya nchi za leo za Angola, Kongo (Kinshasa) na Kongo (Brazzaville).
20231101.sw_2580_7
https://sw.wikipedia.org/wiki/Angola
Angola
Ufalme huo umejulikana zaidi kihistoria kwa sababu ya mawasiliano yake ya kimataifa. Katika karne ya 15 meli za Wareno zilifika mwambaoni mwake.
20231101.sw_2580_8
https://sw.wikipedia.org/wiki/Angola
Angola
Wakati wa kukutana na Wareno Ufalme wa Kongo labda ulikuwa na eneo la km² 300,000 ukaunganisha robo ya magharibi ya Kongo (Kinshasa) pamoja na sehemu za Angola na Kongo (Brazzaville).
20231101.sw_2580_9
https://sw.wikipedia.org/wiki/Angola
Angola
Manikongo mbalimbali walijenga uhusiano na Ureno na Kongo ilikuwa taifa la kushikamana na Ureno hadi kuharibika kwa uhusiano huo. Katika kipindi kile taarifa mbalimbali ziliandikwa zinazotupa leo picha nzuri ya ufalme huo.
20231101.sw_2580_10
https://sw.wikipedia.org/wiki/Angola
Angola
Baada ya wafalme kuwa Wakristo Wakatoliki na kujengwa kwa kanisa kuu, jina la "São Salvador do Congo" (kwa Kireno: "Mwokozi Mtakatifu wa Kongo") lilikuwa kawaida kwa mji mkuu wa milki.
20231101.sw_2580_11
https://sw.wikipedia.org/wiki/Angola
Angola
Ufalme ukawa na majimbo, wilaya na vijiji. Majimbo yalikuwa saba ya Mpemba, Nsundi, Mpangu, Mbata, Mbamba na Soyo.
20231101.sw_2580_12
https://sw.wikipedia.org/wiki/Angola
Angola
Dola la Lunda lilikuwa ufalme wa Kibantu katika miaka 1600 hadi 1850 hivi kandoni kwa mto Kasai, mpakani kwa nchi za kisasa za Angola na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
20231101.sw_2580_13
https://sw.wikipedia.org/wiki/Angola
Angola
Dola la Kasanje lilikuwa ufalme wa Kibantu katika miaka 1620 hadi 1910 hivi kandoni kwa mto Kwango, upande wa kaskazini wa nchi ya kisasa ya Angola. Lilianzishwa na viongozi kutoka Dola la Lunda.
20231101.sw_2580_14
https://sw.wikipedia.org/wiki/Angola
Angola
Dola lingine la kusini lilikuwa lile la Ndongo, lililopambana na Wareno miaka 30 chini ya malkia Njinga katika karne ya 17.
20231101.sw_2580_15
https://sw.wikipedia.org/wiki/Angola
Angola
Mwaka 1966 Jonas Savimbi alianzisha tapo la UNITA (kwa Kireno: União Nacional para a Independência Total de Angola) kama harakati ya kukomboa Angola kutoka ukoloni wa Ureno. UNITA ilikuwa moja kati ya harakati tatu zilizoshindana.
20231101.sw_2580_16
https://sw.wikipedia.org/wiki/Angola
Angola
UNITA ilianza kama kikundi cha kikomunisti kufuatana na itikadi ya Mao Zedong. Uadui kati ya Wakomunisti wa Uchina na Urusi ulionekana katika mashindano ya UNITA dhidi ya MPLA (kwa Kireno: Movimento Popular de Libertação de Angola - Partido do Trabalho) iliyosaidiwa na Urusi.
20231101.sw_2580_17
https://sw.wikipedia.org/wiki/Angola
Angola
Baada ya uhuru mwaka 1975 MPLA ilitawala mji mkuu na kuunda serikali rasmi lakini Savimbi aliendelea kuipinga.
20231101.sw_2580_18
https://sw.wikipedia.org/wiki/Angola
Angola
Savimbi alipata kupokea baadaye usaidizi kutoka maadui wote wa MPLA bila kujali itikadi. UNITA ilipata misaada toka serikali mbalimbali duniani ili kuiondoa madarakani serikali ya MPLA. Savimbi alikuwa akipata misaada ya fedha na silaha toka serikali za Marekani, China, Afrika Kusini, Ivory Coast, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (wakati huo ikijulikana kama Zaire), Moroko, n.k. Serikali ya Angola ilikuwa ikipata misaada toka Urusi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kijerumani, Kuba, na Nicaragua.
20231101.sw_2580_19
https://sw.wikipedia.org/wiki/Angola
Angola
Tarehe 22 Machi 2002, Jonas Savimbi aliuawa vitani. Muda mfupi baadaye UNITA na MPLA zilikubaliana kusimamisha mapigano. UNITA ilichukua nafasi ya chama cha upinzani. Hata hivyo taratibu za kidemokrasia zilichelewa hadi chaguzi za miaka 2008 na 2012 na toleo la katiba mpya la mwaka 2010.
20231101.sw_2580_20
https://sw.wikipedia.org/wiki/Angola
Angola
Sensa ya mwaka 2014 ilihesabu watu 24,383,301 na kufikia mwaka 2016 walikuwa 25,789,024. Wakazi wengi ni Waafrika, hasa wa makabila ya Waovimbundu (37%), Waambundu (23%) na Wakongo (13%). Machotara ni 2%, Wachina 1,6% na Wazungu 1%.
20231101.sw_2580_21
https://sw.wikipedia.org/wiki/Angola
Angola
Ingawa lugha za Kibantu zinaongoza, na 6 kati yake zina hadhi ya lugha ya taifa, lugha rasmi ni Kireno.
20231101.sw_2580_22
https://sw.wikipedia.org/wiki/Angola
Angola
Upande wa dini, inakadiriwa kuwa zaidi ya nusu ni Wakatoliki na robo ni Waprotestanti wa madhehebu mia tofauti.
20231101.sw_2581_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/Shilingi%20ya%20Kenya
Shilingi ya Kenya
Shilingi ya Kenya ilianzishwa mwaka 1966 baada ya kuvunjwa kwa bodi ya fedha ya Afrika ya Mashariki iliyosimamia fedha ya pamoja ya Kenya, Tanzania na Uganda iliyoitwa East African Shilling iliyotumiwa katika maeneo yote yaliyokuwa chini ya Uingereza katika Afrika ya Mashariki.
20231101.sw_2581_1
https://sw.wikipedia.org/wiki/Shilingi%20ya%20Kenya
Shilingi ya Kenya
Noti zilitolewa za shilingi 5, 10, 20, 50, 100, 200, 500 na 1000 ingawaje noti za shilingi 5, 10 na 20 ni nadra sana kuonekana.
20231101.sw_2582_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ikweta
Ikweta
Ikweta ni mstari unaogawa dunia katika sehemu mbili (kaskazini na kusini) kwenye umbali sawa kati ya ncha ya kaskazini na ya kusini.
20231101.sw_2582_1
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ikweta
Ikweta
Baina ya nchi za Afrika ni Somalia, Kenya, Uganda, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Jamhuri ya Kongo, Gaboni na Sao Tome na Principe ambazo ziko kwenye mstari wa ikweta.
20231101.sw_2582_2
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ikweta
Ikweta
Katika Amerika ikweta inapita Ekwado (jina limetokana na neno la ikweta kwa Kihispania), Kolombia na Brazili. Katika Asia ikweta inapita funguvisiwa ya Indonesia.
20231101.sw_2587_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kamerun
Kamerun
Imepakana na Nigeria, Chadi, Jamhuri ya Afrika ya Kati, Jamhuri ya Kongo, Gabon, Guinea ya Ikweta na Ghuba ya Guinea.
20231101.sw_2587_1
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kamerun
Kamerun
Katika karne za BK Wabantu wenye ujuzi wa kilimo na uhunzi walianza uenezi wao kutoka huko kwenda kutawala maeneo mengi ya Afrika ya Kati, Kusini mwa Afrika na Afrika Mashariki.
20231101.sw_2587_2
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kamerun
Kamerun
Kamerun ilikuwa koloni la Ujerumani hadi Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia. Baada ya Ujerumani kushindwa vita, nchi ikagawiwa kati ya Uingereza na Ufaransa chini ya mamlaka ya Shirikisho la Mataifa kama eneo la kudhaminiwa.
20231101.sw_2587_3
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kamerun
Kamerun
Mwaka wa 1960, Wafaransa waliacha Kamerun ikawa nchi huru. Wananchi wa Kamerun ya Kiingereza walipiga kura kuamua kama walitaka kuwa sehemu ya Nigeria au ya Kamerun. Kaskazini wengi walipendelea kukaa Nigeria, hivyo maeneo hayo sasa ni sehemu ya Nigeria. Wananchi wengi wa kusini waliamua wajiunge na Kamerun. Kwa kusudi la kuheshimu tofauti za kiutamaduni kulikuwa na katiba mpya kwenye mwaka 1961 Shirikisho la Jamhuri ya Kamerun.
20231101.sw_2587_4
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kamerun
Kamerun
Tangu 1972 muundo wa nchi ulibadilishwa kuacha mfumo wa shirikisho na kuwa jamhuri ya muungano inayokazia zaidi matumizi ya lugha ya Kifaransa ingawa Kiingereza bado ni moja ya lugha rasmi. Jina la nchi pia likabadilishwa kuwa Jamhuri ya Muungano ya Kamerun mwaka wa 1972. Hapo sehemu ya Wakamerun wanaotumia lugha ya Kiingereza walijisikia kuwa wananyimwa haki zao. Baadaye, mwaka wa 1984 jina likabadilishwa tena kuwa Jamhuri ya Kamerun (kwa Kifaransa République du Cameroun'').
20231101.sw_2587_5
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kamerun
Kamerun
Tangu mwaka 2016 upinzani uliongezeka kati ya watu wa magharibi wanaotumia Kiingereza. Harakati hiyo ilijibiwa na serikali na polisi kwa ukali na hii umeleta kuanzishwa kwa wanamgambo wenye silaha wanaoshambulia polisi na jeshi la serikali kuu. Tangu mwaka 2017 wapinzani wamedai uhuru wa sehemu yenye lugha ya Kiingereza wakitangaza wameunda nchi mpya ya "Ambazonia". Serikali iliundwa inayokaa Nigeria; lakini kuna vikundi tofauti ambavyo wanapigana kati yao. Nchi hii haitambuliwi kimataifa. Mwaka 2021 kulikuwa na majadiliano kuhusu amani kati kundi linalojiita serikali ya Ambazonia na serikali ya Kamerun, lakini makundi mengine yaliendelea na mapigano ya silaha.
20231101.sw_2587_6
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kamerun
Kamerun
Wakazi walikuwa 22,534,532 mwaka 2013, ambao wamegawanyika sawasawa kati ya wanaoishi mijini na wale wa vijijini.
20231101.sw_2587_7
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kamerun
Kamerun
Lugha rasmi ni Kifaransa pamoja na Kiingereza. Hata hivyo wakazi wanaongea pia lugha za makabila yao mengi.
20231101.sw_2587_8
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kamerun
Kamerun
Upande wa dini, 70% ni Wakristo (40% Wakatoliki na 30% Waprotestanti), 18% ni Waislamu, 3% ni wafuasi wa dini asilia za Kiafrika. 6% hawana dini yoyote.
20231101.sw_2587_9
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kamerun
Kamerun
CMCLICK Online! Cameroon Portal - Cameroon Cameroon Internet Community. Cameroon Business Directory. Cameroon Information. Cameroon Culture.
20231101.sw_2587_10
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kamerun
Kamerun
Stanford University - Africa South of the Sahara: Cameroon Maelezo kuhusu Afrika, kusini kwa Sahara.
20231101.sw_2591_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/Sarafu
Sarafu
Sarafu (kar. صرافة badilisha) ni kipande cha metali iliyotolewa na serikali ya nchi kama namna ya pesa. Mara nyingi sarafu ina umbo la duara kama kisahani. Kuna pia sarafu za pembe tatu, pembe nne au pembe zaidi.
20231101.sw_2591_1
https://sw.wikipedia.org/wiki/Sarafu
Sarafu
Zamani sarafu ilikuwa umbo la kawaida ya pesa. Sarafu za kwanza zinazojulikana dunia zimepatikana kutoka Lydia katika Anatolia ya Magharibi iliyokuwa wakati ule sehemu ya utamaduni wa Wagiriki wa Kale. Sarafu zilitengenezwa hasa kwa kutumia metali ya thamani kama dhahabu na fedha, pia ya shaba na wakati mwingine ya chuma. Thamani ya sarafu ililingana na kiasi fulani cha metali hizi.
20231101.sw_2591_2
https://sw.wikipedia.org/wiki/Sarafu
Sarafu
Karibu popote duniani sarafu hutumika kwa ajili ya pesa ndogo tu. Isipokuwa sarafu za dhahabu zinatolewa kwa idadi ndogo hasa kwa ajili ya watu wanaopenda kukusanya aina mbalimbali za sarafu zenye thamani ingawa hazitumiki kama pesa ya kulipia.
20231101.sw_2592_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kiolwa%20cha%20angani
Kiolwa cha angani
Kiolwa cha angani (pia: gimba la angani, kwa Kiingereza: astronomical object au celestial body) ni jina la jumla kwa ajili ya vitu vinayopatikana katika anga ya ulimwengu.
20231101.sw_2592_1
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kiolwa%20cha%20angani
Kiolwa cha angani
Kwa Kiingereza istilahi "object" (kiolwa) na "body" (gimba) mara nyingi hutumiwa kama visawe. Lakini ilhali kila gimba la anga-nje ni pia kiolwa cha anga-nje, kinyume chake si kweli. Gimba la anga-nje ni kitu kimoja cha pekee, kama vile sayari, mwezi, asteroidi. Kiolwa cha anga-nje ni wazo pana zaidi, likitaja pia mambo kama galaksi au nebula yenye sehemu nyingi ndani yake.
20231101.sw_2592_2
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kiolwa%20cha%20angani
Kiolwa cha angani
Hivyo vyote ni violwa asilia. Vitu vilivyoko kwenye anga-nje vilivyotengenezwa na binadamu ni vyombo vya anga-nje. Hapa kuna swali kama mabaki kutokana na vyombo vya anga-nje vilivyovunjika au takataka ya angani yanayotokana na safari za anga-nje yanastahili kuitwa kwa neno hili.
20231101.sw_2593_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/Nebula
Nebula
Nebula ni neno linalotumika kwa ajili ya kutaja eneo angavu na jeupejeupe linaloonekana angani ama kwa macho au kwa darubini.
20231101.sw_2593_1
https://sw.wikipedia.org/wiki/Nebula
Nebula
Zamani hata galaksi ziliweza kuitwa "nebula". Galaksi ya Andromeda iliyokuwa galaksi ya kwanza kutambuliwa angani ilikuwa inaitwa "Andromeda Nebula".
20231101.sw_2593_2
https://sw.wikipedia.org/wiki/Nebula
Nebula
Siku hizi neno linataja wingu kubwa linalong'aa. Maada yake inaweza kuwa gesi ya moto, vumbi na utegili.
20231101.sw_2593_3
https://sw.wikipedia.org/wiki/Nebula
Nebula
Mara nyingi nebula ni mahali pa kuzaliwa au kutokea kwa nyota mpya. Wakati mwingine wingu ni mabaki tu ya nyota aina ya nova, yaani nyota iliyokufa katika mlipuko mkubwa.
20231101.sw_2594_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/Utegili
Utegili
Utegili (damu) ni yale majimaji yanayobaki kwenye damu baada ya kuondolewa kwa seli za damu kwenye damu ya vetebrata
20231101.sw_2595_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/Utegili%20%28fizikia%29
Utegili (fizikia)
Utegili (pia: plasma) katika lugha ya fizikia, ni hali ya nne ya maada. Hali hiyo ni kama gesi ila ni ya kiioni. Nyinginezo ni hali mango (imara), kiowevu (majimaji) na gesi (kama hewa).
20231101.sw_2595_1
https://sw.wikipedia.org/wiki/Utegili%20%28fizikia%29
Utegili (fizikia)
Mfano wa maada mango ni jiwe la mwamba, maada kiowevu ni maji, na maada gesi ni hewa. Hivyo plasma ama utegili ni hali ya nne ambayo si ya asili katika maisha yetu ya kila siku. Huonekana katika mifumo ya kimaada iliyo katika joto kali.
20231101.sw_2595_2
https://sw.wikipedia.org/wiki/Utegili%20%28fizikia%29
Utegili (fizikia)
Plasma ni hali halisi ya jua. Lenyewe linafanyika na maada lakini si tena katika hali ya kawaida tunayoijua hapa duniani. Nayo ni kama gesi inayolipuka masaa yote na kufanya mnururiko wa nishati inayotufikia kama joto, mwanga na pia mawimbi ya plasma itufikiayo na kujidhihirisha kama aurora katika ncha ya kaskazini ya Dunia.
20231101.sw_2595_3
https://sw.wikipedia.org/wiki/Utegili%20%28fizikia%29
Utegili (fizikia)
Ikiwa gesi ni ya joto kali sana elektroni zake zinaanza kuachana na atomu zao. Tabia ya hali hii ni tofauti na hali ya gesi yenyewe. Elektroni zisizoshikwa na atomu pamoja na atomu hizo katika hali ya ioni zote zinajibu kwa uga wa sumakuumeme.
20231101.sw_2595_4
https://sw.wikipedia.org/wiki/Utegili%20%28fizikia%29
Utegili (fizikia)
Asilimia kubwa ya maada ulimwenguni iko katika hali ya utegili kwa sababu imo ndani ya nyota za angani.
20231101.sw_2595_5
https://sw.wikipedia.org/wiki/Utegili%20%28fizikia%29
Utegili (fizikia)
Kwa ajili ya matumizi ya mitambo hali ya utegili yaani ya kuionika husababishwa pia kwa leza au kwa uga wa sumakuumeme.
20231101.sw_2596_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ghuba
Ghuba
Mara nyingi ghuba hutokana na misogeo ya ganda la dunia inayosababisha maji kujaa nafasi iliyojitokeza.
20231101.sw_2596_1
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ghuba
Ghuba
Baadhi ya ghuba zinazojulikana ni kama vile Ghuba ya Guinea, Ghuba ya Uajemi, Ghuba ya Mexiko au Bahari ya Shamu.
20231101.sw_2597_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/Yuri%20Gagarin
Yuri Gagarin
Yuri Alexeyevich Gagarin (kwa Kirusi Юрий Алексеевич Гагарин; 9 Machi 1934 huko Klushino karibu na Smolensk, Urusi - 27 Machi 1968) alikuwa mwanaanga wa kwanza katika historia yaani mtu wa kwanza aliyefika kwenye Anga-nje.
20231101.sw_2597_1
https://sw.wikipedia.org/wiki/Yuri%20Gagarin
Yuri Gagarin
Alimwoa Valentina Goryachova akawa na mabinti wawili ambao ni Galina na Yelena. Akajiunga na Jeshi la Anga ya Urusi mwaka 1955.
20231101.sw_2597_2
https://sw.wikipedia.org/wiki/Yuri%20Gagarin
Yuri Gagarin
Mwaka 1960 aliteuliwa katika kikosi cha kwanza cha marubani walioandaliwa kurushwa kwa anga-nje akateuliwa kuwa mtu wa kwanza wa kutoka duniani.
20231101.sw_2597_3
https://sw.wikipedia.org/wiki/Yuri%20Gagarin
Yuri Gagarin
Tarehe 12 Aprili 1961 alirushwa na chombo cha angani Vostok 1 akizunguka dunia lote mara moja katika muda wa dakika 108.
20231101.sw_2597_4
https://sw.wikipedia.org/wiki/Yuri%20Gagarin
Yuri Gagarin
Alipandishwa cheo na kuwa mkuu wa kituo cha kuandaa wanaanga Warusi. Mwaka 1968 alikufa katika ajali ya ndege alipofanya mazoezi ya urubani akazikwa kwenye makaburi ya heshima huko Moscow.
20231101.sw_2597_5
https://sw.wikipedia.org/wiki/Yuri%20Gagarin
Yuri Gagarin
Kuhusiana na kifo Cha Gagarin, maombolezo ya kitaifa yalitangazwa katika Umoja wa Kisovyeti (kwa mara ya kwanza katika historia ya USSR kwa kumbukumbu ya mtu ambaye hakuwa mkuu wa nchi). Kwa heshima ya cosmonaut ya Kwanza Ya Dunia, idadi ya makazi yalipewa jina, barabara na njia zilipewa jina. Makaburi mengi ya Gagarin yamejengwa katika miji tofauti ya ulimwengu.
20231101.sw_2600_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/Jamhuri%20ya%20Afrika%20ya%20Kati
Jamhuri ya Afrika ya Kati
Jamhuri ya Afrika ya Kati (kwa Kisango Ködörösêse tî Bêafrîka) ni nchi ya bara bila pwani katika Afrika ya Kati.
20231101.sw_2600_1
https://sw.wikipedia.org/wiki/Jamhuri%20ya%20Afrika%20ya%20Kati
Jamhuri ya Afrika ya Kati
Imepakana na Chadi upande wa kaskazini, Sudan na Sudan Kusini upande wa mashariki, Jamhuri ya Kongo na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo upande wa kusini na Kamerun upande wa magharibi.
20231101.sw_2600_2
https://sw.wikipedia.org/wiki/Jamhuri%20ya%20Afrika%20ya%20Kati
Jamhuri ya Afrika ya Kati
Nchi hii, hasa inashikilia mbuga ya Sudani-Guinea, lakini pia jangwa la Sahara upande wa kaskazini na msitu wa ikweta kusini.
20231101.sw_2600_3
https://sw.wikipedia.org/wiki/Jamhuri%20ya%20Afrika%20ya%20Kati
Jamhuri ya Afrika ya Kati
Theluthi mbili za eneo la nchi zimetapakaa kwa mabia ya mto Ubangi unaotiririka kusini kwa Mto Kongo, na theluthi ya eneo katapakaa kwa mabia ya mto Shari, unaotiririka kusini kwa Ziwa Chadi.
20231101.sw_2600_4
https://sw.wikipedia.org/wiki/Jamhuri%20ya%20Afrika%20ya%20Kati
Jamhuri ya Afrika ya Kati
Kwa sababu ya utapakazi wa eneo kwa mabia ya mto Ubangi na mto Shari, Wafaransa wakati wa ukoloni waliita nchi hii Ubangi-Shari (Oubangui-Chari kwa Kifaransa).
20231101.sw_2600_5
https://sw.wikipedia.org/wiki/Jamhuri%20ya%20Afrika%20ya%20Kati
Jamhuri ya Afrika ya Kati
Ilipokuwa koloni la Ufaransa, Ubangi-Shari ziliwekewa mamlaka ya madaraka kama eneo la Jamii ya Wafaransa mwaka wa 1958, lakini baadaye ilipata uhuru tarehe 13 Agosti 1960.
20231101.sw_2600_6
https://sw.wikipedia.org/wiki/Jamhuri%20ya%20Afrika%20ya%20Kati
Jamhuri ya Afrika ya Kati
Kwa miongo mitatu kutoka uhuru, ‘Jamhuri ya Afrika ya Kati’ ilitawaliwa na serikali za mabavu zilizonyakua mamlaka bila kufuata taratibu za demokrasia.
20231101.sw_2600_7
https://sw.wikipedia.org/wiki/Jamhuri%20ya%20Afrika%20ya%20Kati
Jamhuri ya Afrika ya Kati
Kwa namna ya pekee Jean-Bédel Bokassa alitawala kuanzia tarehe 31 Desemba 1965 hadi Septemba 1979, akijifanya kaisari tarehe 4 Desemba 1976.
20231101.sw_2600_8
https://sw.wikipedia.org/wiki/Jamhuri%20ya%20Afrika%20ya%20Kati
Jamhuri ya Afrika ya Kati
Mwaka wa 1993, kura za kidemokrasia za kwanza zilifanywa na kumchagua Ange-Félix Patassé kuwa Rais. Lakini Rais Patassé alipinduliwa na Jenerali François Bozizé mwaka wa 2003. Baadaye huyo alishinda uchaguzi mnamo Mei 2005 na kuiongoza nchi mpaka Machi 2013 alipolazimika kukimbia.
20231101.sw_2600_9
https://sw.wikipedia.org/wiki/Jamhuri%20ya%20Afrika%20ya%20Kati
Jamhuri ya Afrika ya Kati
Kati ya Novemba 2012 na tarehe 23 Julai 2014 vita vya wenyewe kwa wenyewe vilipamba kwa ukatili na vinaendelea hadi mwaka 2020.
20231101.sw_2600_10
https://sw.wikipedia.org/wiki/Jamhuri%20ya%20Afrika%20ya%20Kati
Jamhuri ya Afrika ya Kati
Jamhuri ya Afrika ya Kati imegawiwa katika maeneo 14, yanayoitwa préfectures, na pia maeneo 2 ya uchumi (préfectures economique) na mji mmoja (commune).
20231101.sw_2600_11
https://sw.wikipedia.org/wiki/Jamhuri%20ya%20Afrika%20ya%20Kati
Jamhuri ya Afrika ya Kati
mikoa ni: Bamingui-Bangoran, Basse-Kotto, Haute-Kotto, Haut-Mbomou, Kémo, Lobaye, Mambéré-Kadéï, Mbomou, Nana-Mambéré, Ombella-M'Poko, Ouaka, Ouham, Ouham-Pendé, na Vakaga; maeneo ya uchumi ni Nana-Grébizi na Sangha-Mbaéré; na mji ni Bangui.