_id
stringlengths
15
22
url
stringlengths
31
150
title
stringlengths
1
86
text
stringlengths
100
23.8k
20231101.sw_2555_9
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mwezi
Mwezi
Muda wa mabadiliko kati ya mwezi mwandamo hadi kupotea na kuwa mwezi mwandamo tena ni kati ya siku 28 hadi 29. Kipindi hiki kinakumbukwa kirahisi kinaonekana kwa watu wote.Hivyo muda wa kurudi kwa Mwezi ulikuwa kati ya vipimo vya kwanza vya wakati kwa binadamu pamoja na kipindi cha siku.
20231101.sw_2555_10
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mwezi
Mwezi
Awamu za mwezi zilikuwa vipindi vya kuhesabu wakati tangu mwanzo wa kalenda. Hadi leo kuna kalenda ya mwezi ambayo ni kalenda ya Kiislamu. Inapanga wakati kutokana na hali halisi ya awamu za mwezi.
20231101.sw_2555_11
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mwezi
Mwezi
Mwezi wetu ni gimba la angani la kwanza ambako wanadamu wamefika. Tarehe 21 Julai 1969 mwanaanga Mmarekani Neil Armstrong alikuwa mtu wa kwanza wa kukanyaga uso wa mwezi. Wanaanga wengine 11 kutoka Marekani waliendelea kufika mwezini hadi mwaka 1972.Baadaye safari za kwenda mwezini hazikufanywa tena kutokana na gharama kubwa.
20231101.sw_2555_12
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mwezi
Mwezi
Hata kama Warusi na Wamarekani walifikisha bendera zao mwezini, hawadai kuwa na mali huko. Katika mkataba kuhusu anga-nje nchi 192 za Dunia zimekubaliana kuwa Mwezi utaangaliwa sawa na maeneo ya kimataifa ya bahari. Walikubaliana kuwa ni marufuku kupeleka silaha kali kama za nyuklia angani. Mataifa mengi ya Dunia yametia sahihi mkataba huo, isipokuwa nchi chache hususan za Afrika ikiwemo Tanzania.
20231101.sw_2555_13
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mwezi
Mwezi
Lakini kuna watu binafsi wanaodai kuwa na mali kwenye Mwezi. Tangu mwaka 1980 yupo Mwamerika mmoja aliyefaulu kuandikisha Mwezi kwa jina lake kwenye ofisi ya msajili wa viwanda mjini San Francisco akiendelea kuuza hati za kumiliki maeneo mwezini. Kuna pia familia moja pale Ujerumani iliyorithi hati ambako mfalme wa Prussia kwenye mwaka 1756 alitoa zawadi ya Mwezi kwa mzee wao. Taasisi ya Sheria ya Anga-Nje (International Institute of Space Law) ilitoa tamko kuwa madai haya hayana msingi wa kisheria .
20231101.sw_2557_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mwezi%20%28wakati%29
Mwezi (wakati)
Mwezi ni mojawapo wa vipindi kumi na mbili vya mwaka. Muda wa mwezi unategemea aina ya kalenda inayotumika.
20231101.sw_2557_1
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mwezi%20%28wakati%29
Mwezi (wakati)
Uso wa mwezi jinsi unavyoonekana duniani hubadilikabadilika. Mwezi mpevu unaonekana kama duara kamili la kung'aa lakini baada ya kuonekana hivi umbo lapungua kila siku hadi kutoonekana kabisa na hali hii huitwa mwezi mwandamo. Baadaye mwezi unaonekana tena kama hilali nyembamba na kuongezeka hadi kuwa duara tena. Muda wa mabadiliko yote kupita mara 1 ni siku 29 1/4.
20231101.sw_2557_2
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mwezi%20%28wakati%29
Mwezi (wakati)
Muda wa mabadiliko kati ya mwezi mwandamo hadi kupotea na kuwa mwezi mwandamo tena ni kati ya siku 28 - 29. Kipindi hiki kinakumbukwa kirahisi, kinatazamiwa na watu wote wakati uleule kwa hiyo pamoja na kipindi cha siku kilikuwa kati ya vipimo vya kwanza vya wakati kwa binadamu.
20231101.sw_2557_3
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mwezi%20%28wakati%29
Mwezi (wakati)
Awamu za mwezi zilikuwa vipindi vya kuhesabu wakati tangu mwanzo wa kalenda. Hadi leo kuna kalenda ya mwezi ndiyo kalenda ya Kiislamu inayopanga wakati kutokana na hali halisi ya awamu za mwezi.
20231101.sw_2557_4
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mwezi%20%28wakati%29
Mwezi (wakati)
Katika kalenda ya mwezi ni sawa na kipindi kutoka awamu ya mwezi mpya angani hadi mwezi mpya unaofuata ni 29.53 siku. Mwezi mpya unaanza sawa na kuonekana kwa mwezi mpya jinsi ilivyo katika kalenda ya Kiislamu.
20231101.sw_2557_5
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mwezi%20%28wakati%29
Mwezi (wakati)
Kwa kalenda ya jua muda wa mwezi unakaribia tu muda kati ya awamu za mwezi. Katika kalenda ya Gregori miezi ina kati ya siku 28 hadi 31. Lakini vipindi hivi havina uhusiano tena na hali halisi ya awamu za mwezi wa angani mwenyewe. "Mwezi" ni lugha tu haimaanishi gimba la angani tena.
20231101.sw_2557_6
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mwezi%20%28wakati%29
Mwezi (wakati)
Kwa Kiswahili nchini Tanzania miezi inatofautishwa kwa namba; mwezi wa kwanza, wa pili, wa tatu ... hadi mwezi wa kumi na mbili.
20231101.sw_2557_7
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mwezi%20%28wakati%29
Mwezi (wakati)
Pamoja na njia hiyo, kuna majina ya Kilatini iliyofika kwenye Kiswahili kupitia lugha za wakoloni, yaani Kijerumani na Kiingereza. Ndiyo yanayotumika zaidi nchini Kenya.
20231101.sw_2557_8
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mwezi%20%28wakati%29
Mwezi (wakati)
Februari huongezeka siku moja kufikia 29 katika miaka mirefu kufuatana na utaratibu wa kalenda ya Gregori.
20231101.sw_2557_9
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mwezi%20%28wakati%29
Mwezi (wakati)
Miezi hii haina wakati maalumu katika kalenda ya jua yenye miezi Januari - Desemba, bali inabadilika kila mwaka.
20231101.sw_2559_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kalenda
Kalenda
Kalenda ni utaratibu wa kupanga wakati. Hupatikana kama orodha ya vipindi vya wakati kama vile siku, juma, mwezi na mwaka. Kalenda mbalimbali zimejua pia vipindi vya miaka kadhaa.
20231101.sw_2559_1
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kalenda
Kalenda
Kalenda inayotumika zaidi leo kimataifa ni kalenda ya Gregori iliyo muhimu kwa uchumi na biashara. Kuna pia nchi zinazotumia hasa kalenda zao za kitaifa au kalenda mbalimbali sambamba.
20231101.sw_2559_2
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kalenda
Kalenda
Hasa maisha ya kidini hupangwa kufuatana na kalenda maalumu. Kihistoria palikuwako na kalenda nyingi.
20231101.sw_2559_3
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kalenda
Kalenda
Kwa watu wengi duniani mabadiliko ya mchana na usiku ni utaratibu wa kwanza unaogawa wakati. Mchana na usiku pamoja inahesabiwa kama siku moja. Lakini kuna njia tofauti jinsi gani kuanza hesabu hiyo: asubuhi (mwanzo wa mchana) au jioni (mwanzo wa usiku) zilikuwa njia za kawaida za kuhesabu siku mpya. Tangu kupatikana kwa saa zinazoonyesha masaa hata gizani ni saa sita usiku (katikati ya usiku) inayoangaliwa kuwa mwanzo wa siku mpya.
20231101.sw_2559_4
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kalenda
Kalenda
Awamu za mwezi huonekana vizuri kwa kila mtu. Kwa sababu hii awamu hizi zilikuwa mbinu unaoeleweka rahisi kupanga siku kwa vipindi. Kipindi kutoka mwezi mpya hadi mwezi mpya ni kipimo kinachopatikana katika kila nchi ni siku 29 1/2.
20231101.sw_2559_5
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kalenda
Kalenda
Majira au badiliko la vipindi vinavyorudi vya joto na baridi au vya ukame na mvua vilikuwa utaratibu mwingine ulioonekana kwa watu. Ila tu hesabu hii ilitegemea na mazingira na hali ya hewa katika eneo fulani.
20231101.sw_2559_6
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kalenda
Kalenda
Hasa katika nchi ambako majira yanatofautiana vikali na kufuata utaratibu wa kurudia hata mimea na wanyama hufuata mwendo wa majira. Katika mazingira kama hii imewezekana kutofautisha matokeo katika maisha kufuatana na idadi ya vipindi vya baridi au vya joto au vya mvua vilivyopita tangu tokeo fulani.
20231101.sw_2559_7
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kalenda
Kalenda
Mabadiliko ya mimea hutegemea mwendo wa jua na idadi ya mwanga pamoja na joto linalopatikana katika sehemu mbalimbali za dunia.
20231101.sw_2559_8
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kalenda
Kalenda
Katika nchi karibu na ikweta tofauti hizi mara nyingi si kali sana na majira hazionekani vizuri isipokuwa majira ya mvua na ukame. Katika nchi hizi kalenda za kale mara nyingi zilitegemea nyota hasa Zuhura (Ng'andu) na mahali angani inapoonekana asubuhi au jioni kwa wakati fulani.
20231101.sw_2559_9
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kalenda
Kalenda
Inaaminika ya kwamba tangu kuanza kilimo watu wameanza pia kushika kumbukumbu ya wakati. Katika nchi nyingi kupanda na kuvuna kunategemea mwendo wa majira yanayorudia. Kazi ya pamoja inahitaji mpangilio na lugha ya pamoja. Hapa ni mwanzo wa kalenda.
20231101.sw_2559_10
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kalenda
Kalenda
Kutokana na migawanyo asilia ya wakati zilitokea njia mbalimbali jinsi ya kupanga wakati katika kalenda. Kutokana na hapo kuna hasa kalenda ya mwezi, kalenda ya jua na kalenda ya lunisolar (=kalenda jua-mwezi) inayounganisha mwaka kufuatana na mwendo wa jua na vipindi halisi vya mwezi.
20231101.sw_2559_11
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kalenda
Kalenda
Kalenda hizi hufuata awamu za mwezi. Kutoka mwezi mwandamu (=mwezi mpya) hadi mwezi mwandamu unaofuata ni muda wa siku 29 na nusu. 12 za vipindi hivi ni takriban sawa na mwaka 1 yaani kipindi hadi kurudia kwa majira kama joto au baridi. Lakini kuna tofauti kati ya mwaka wa jua unaotawala kurudi kwa majira baada ya siku 365 ¼ na muda wa miezi halisi 12 mwenye siku 354 pekee.
20231101.sw_2559_12
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kalenda
Kalenda
Hii ni hasara ya kalenda ya mwezi ya kwamba baada ya miaka kadhaa hailingani tena na majira kwa hiyo ni vigumu kupanga kilimo kufuatana na kalenda hii. Lakini katika maeneo ya dunia ambako majira si muhimu vile kalenda za mwezi zinaendelea kutumiwa.
20231101.sw_2559_13
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kalenda
Kalenda
Mfano maarufu wa kalenda ya mwezi ni kalenda ya Kiislamu; hapo kipindi cha „mwezi kinalingana kabisa na awamu za mwezi angani na baada ya miezi 12 ya aina hii mwaka mpya mwenye muda wa siku 354.3 unaanza tena. Ilhali mwaka huu una upungufu ya siku 11-12 kulingana na mwaka wa jua sikuu zake „zinatembea“ kutoka majira hadi majira; katika mazingira ya jangwa ya Uarabuni ulikotokea kilimo na majira hayakuwa muhimu vile.
20231101.sw_2559_14
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kalenda
Kalenda
Nchi nyingi za dunia zinategemea kilimo. Kilimo hufuata majira ya hali ya hewa. Majira haya hutawaliwa na jua yaani na kiasi cha mwanga na nishati zinazofika dunianikutoka kwa jua na hii inabadilika kutokana na umbali wa jua unaobadilika katika mwendo wa dunia kuzunguka jua letu. Mwendo huu wa dunia kuzunguka jua unachukua siku 365 ¼ kwa hiyo watu katika tamaduni mbalimbali baada ya kugundua muda huu walitunga kalenda zilizoshika mwendo huo.
20231101.sw_2559_15
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kalenda
Kalenda
Kalenda hizi zinaweza kugawiwa kwa namna mbalimbali lakini mara nyingi zinatumia vipindi 12. Vpindi hivi vinaweza kuitwa „mwezi“ lakini havina uhusiano tena na awamu halisi za mwezi.
20231101.sw_2559_16
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kalenda
Kalenda
Kalenda jua-mwezi zinalenga kuunganisha mwaka wa jua na mwendo wa majira kwa pande mmoja na awamu halisi za mwezi kwa upande mwingine.
20231101.sw_2559_17
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kalenda
Kalenda
Kwa hiyo kalenda hizi zinatumia vipindi vya mwaka vya mwezi yaani miezi halisi 12. Kila baada ya miaka 2 – 3 kuna mwaka mrefu mwenye miezi 13. Kwa njia hii upungufu wa mwaka wa mwezi kulingana na mwaka wa jua unasawazishwa.
20231101.sw_2559_18
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kalenda
Kalenda
Kalenda ya kimataifa (=Kalenda ya Gregori) huanza hesabu yake katika mwaka ulioaminiwa kuwa mwaka wa kuzaliwa kwa Yesu Kristo na hesabu hii huitwa baada ya Kristo. Hesabu hii imefikia baada ya mwaka 2010.
20231101.sw_2559_19
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kalenda
Kalenda
Kalenda ya Kiislamu huanza hesabu yake katika mwaka wa hijra yaani kuondoka kwa Muhamad kutoka Maka kwenda Madina. Hesabu hii imefika zaidi ya miaka 1430.
20231101.sw_2559_20
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kalenda
Kalenda
Kalenda ya Kiyahudi inaanza hesabu katika mwaka ulioaminiwa kuwa uumbaji wa dunia na leo imefikia hesabu ya zaidi ya miaka 5770.
20231101.sw_2559_21
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kalenda
Kalenda
Hata leo hii kuna kalenda mbalimbali zinazotumiwa duniani. Kalenda inayotumiwa zaidi kimataifa ni kalenda ya Gregori inayohesabu miaka tangu Kristo kuzaliwa. Kalenda hii imepokea muundo wake kutoka kalenda ya Roma ya Kale hasa miezi na idadi ya siku zao.
20231101.sw_2559_22
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kalenda
Kalenda
Kalenda nyingine inayotumiwa katika nchi kadhaa ni kalenda ya Kiislamu inayohesabu miaka tangu hijra ya Muhamad; kalenda hii hutumiwa na Waislamu wote kwa kukadiria sikukuu zao hata wakitumia menginevyo kalenda ya Gregori.
20231101.sw_2559_23
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kalenda
Kalenda
Kalenda nyingine ni kalenda kama ile ya Kichina, ya Kihindi na kadhalika zinazotumiwa kwa makadirio ya sikukuu katika dini au utamaduni wao lakini kwa maisha ya kawaida watu wengi wanatumia kalenda ya Gregori.
20231101.sw_2559_24
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kalenda
Kalenda
Nchi kadhaa huwa pia na namna ya pekee za kalenda kwa mfano Ethiopia hufuata kalenda yake inayohesabu tangu kuzaliwa kwake Kristo lakini kwa tofauti ya hesabu ya miaka 7 na miezi 3; ina miezi 13. Kalenda ya Uajemi huhesabu miaka tangu hijra lakini tofauti na Waislamu wengi hutumia mwaka wa jua si mwaka wa mwezi kwa hiyo kuna tofauti ya takriban miaka 40 hivi.
20231101.sw_2559_25
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kalenda
Kalenda
Hesabu ya wiki haifuati kalenda ni kipindi cha siku 7 kinachorudia mfululizo bila kujali mwisho au mwanzo wa mwaka. Asili yake iko katika Mashariki ya Kati hasa Babeli ikasambazwa kupitia imani ya Uyahudi na Ukristo. Inaanza kwa siku ya Jumapili inayotazamiwa kidini kama siku ya kwanza ya uumbaji wa dunia na kwa wakristo pia siku ya ufufuo wa Yesu unaotazamiwa kama uumbaji wa pili. Kwa kusudi la kupanga maisha na hasa kazi wiki za mwaka zinahesabiwa kuanzia 1 - 52; hapo wiki ya kwanza na wiki ya mwisho kwa kawaida si kamili kwa sababu siku kadhaa zimo katika mwaka uliotangulia au kufuata.
20231101.sw_2559_26
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kalenda
Kalenda
Tangu kuenea desturi ya wikendi yaani mapumziko ambako wengi hawafanyi kazi siku za Jumapili na Jumamosi kalenda nyingi huonyesha siku ya kwanza ya wiki ambayo ni Jumatatu kama chanzo cha wiki ya kazi.
20231101.sw_2559_27
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kalenda
Kalenda
Mpangilio wa wiki kama hesabu ya siku ya kupumzika na siku za kazi umeenea kote duniani hasa kwa ofisi za serikali ingawa katika nchi nyingi watu maskini hawana nafasi za kupumzika mara kwa mara.
20231101.sw_2560_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/Sudan
Sudan
Sudan (jina rasmi: Jamhuri ya Sudan) ni nchi ya tatu kwa ukubwa katika bara la Afrika na ya kumi na sita duniani
20231101.sw_2560_1
https://sw.wikipedia.org/wiki/Sudan
Sudan
Imepakana na Misri kaskazini, Bahari ya Shamu kaskazini-mashariki, Eritrea na Ethiopia mashariki, Sudan Kusini kusini-mashariki, Afrika ya Kati na Chadi magharibi, na Libya kaskazini-magharibi.
20231101.sw_2560_2
https://sw.wikipedia.org/wiki/Sudan
Sudan
Majimbo ya Sudan Kusini yalikuwa sehemu ya nchi hiyo lakini yalipiga kura ya kujitenga yakapata kuwa nchi huru kuanzia tarehe 9 Julai 2011.
20231101.sw_2560_3
https://sw.wikipedia.org/wiki/Sudan
Sudan
Sudan iko upande wa Afrika ya kaskazini, ina pwani kwenye bahari ya Shamu kati ya Misri na Eritrea. Imetamalikiwa zaidi na mto Nile na mikono yake.
20231101.sw_2560_4
https://sw.wikipedia.org/wiki/Sudan
Sudan
Katika milenia ya 5 KK watu walizidi kuhama Sahara ikigeuka jangwa wakasogea katika eneo la Sudan ya sasa (bonde la mto Nile).
20231101.sw_2560_5
https://sw.wikipedia.org/wiki/Sudan
Sudan
Katika karne ya 8 KK watu wa ufalme huo waliteka Misri na kuitawala kwa karne moja hadi waliposhindwa na Waashuru.
20231101.sw_2560_6
https://sw.wikipedia.org/wiki/Sudan
Sudan
Baadaye makao makuu yalikuwa Meroe, ambapo ufalme uliendelea hadi karne ya 4 BK ukiwa maarufu kwa uhunzi kwa jina la Ethiopia.
20231101.sw_2560_7
https://sw.wikipedia.org/wiki/Sudan
Sudan
Ufalme huo uliposambaratika, zilitokea falme mbalimbali katika eneo lake, mmojawapo ukiwa ule wa Nubia.
20231101.sw_2560_8
https://sw.wikipedia.org/wiki/Sudan
Sudan
Huko Ukristo ulienea katika madhehebu tofauti: yale ya Kikopti kutoka Misri na yale ya Kibizanti kutoka Roma ya mashariki.
20231101.sw_2560_9
https://sw.wikipedia.org/wiki/Sudan
Sudan
Katika miaka ya 1870 juhudi za Wazungu za kukomesha biashara ya utumwa zilisababisha kutokea kwa Mahdi.
20231101.sw_2560_10
https://sw.wikipedia.org/wiki/Sudan
Sudan
Dola la Mahdi (kwa Kiarabu المهدية, "mahdiyya") lilianzishwa na Muhammad Ahmad Al-Mahdi mwaka 1881 alipojitangaza kuwa mahdi kufuatana na imani ya Kiislamu akaongoza uasi dhidi ya Misri iliyotawala Sudan ikisimamiwa yenyewe na Uingereza.
20231101.sw_2560_11
https://sw.wikipedia.org/wiki/Sudan
Sudan
Muhammad Ahmad Al-Mahdi alifaulu kukusanya wafuasi wengi na kushinda Wamisri. Tarehe 26 Januari 1885 jeshi lake lilitwaa mji mkuu Khartum na kumwua gavana Gordon Pasha.
20231101.sw_2560_12
https://sw.wikipedia.org/wiki/Sudan
Sudan
Al-Mahdi alianzisha mji mkuu mpya ng'ambo ya mto Nile kwa kuunda Omdurman. Wamisri na Waingereza wakatoka nje ya Sudan.
20231101.sw_2560_13
https://sw.wikipedia.org/wiki/Sudan
Sudan
Ugomvi ulitokea kati ya makamu wake hadi 1891 wakati Abdallahi ibn Muhammad mwenye sifa ya kuwa aliongoza jeshi la mahdi wakati wa mashambulio dhidi ya Khartum alikubaliwa wa viongozi wa mahdiyya akajiita "khalifa".
20231101.sw_2560_14
https://sw.wikipedia.org/wiki/Sudan
Sudan
Khalifa Abdullahi aliimarisha utawala wake wa kuwaua wapinzani bila neema, kati yao wanafunzi na ndugu za mahdi mwenyewe. Akajenga jumba mjini Omdurman linalosimama hadi leo.
20231101.sw_2560_15
https://sw.wikipedia.org/wiki/Sudan
Sudan
Khalifa Abdullahi alijaribu kutumia teknolojia mbalimbali. Akanunua meli za mvuke za mtoni alizoziona Waingereza walizitumia pia akajenga kiwanda cha kutengenezea bunduki. Akaanzisha nyaya za mawasilaino kwa simu. Lakini kwa ujumla vita na utawala wa mahdiyya zilikuwa ziliharubu uchumi iliyoendelea kuzorota.
20231101.sw_2560_16
https://sw.wikipedia.org/wiki/Sudan
Sudan
Khalifa alifaulu kupanua utawala wake juu ya maeneo karibu yote ya Sudan ya leo lakini alishindwa kufikia jimbo la Ikweta ambako Emin Pasha aliendelea kutetea mabaki ya Sudani ya Kimisri.
20231101.sw_2560_17
https://sw.wikipedia.org/wiki/Sudan
Sudan
Itikadi ya kupanua utawala wa mahdiyya kwa njia ya jihad ilimsababisha khalifa kushambulia nchi jirani ya Ethiopia iliyotawaliwa na kaisari wa Kikristo. Mwaka 1887 akaongoza jeshi la askari 60,000 hadi Gondar. Waethiopia wakajibu kwa kushambulia Sudan mwaka 1889. Kifo cha Kaisari Yohane IV katika mapigano ya Metemma tarehe 9 Machi 1889 ililazimisha Waethiopia kurudi kwao. Lakini jeshi la mahdiyya lilipoteza wanajeshi wengi pia likadhoofika.
20231101.sw_2560_18
https://sw.wikipedia.org/wiki/Sudan
Sudan
Wakati huohuo jemadari wa khalifa Abd ar-Raħmān an-Nujumī alishambulia Misri lakini alishindwa kwenye mapigano ya Tushkah. Hii ilikuwa mara ya kwanza ya jeshi la mahdiyya kushindwa.
20231101.sw_2560_19
https://sw.wikipedia.org/wiki/Sudan
Sudan
Majaribio ya vita za jihadi dhidi ya Wabelgiji katika jimbo la Ikweta na dhidi ya Waitalia katika Eritrea yalishindikana pia.
20231101.sw_2560_20
https://sw.wikipedia.org/wiki/Sudan
Sudan
Mwaka 1895 mkuu wa jeshi la pamoja la Misri na Uingereza, jenerali Horatio Kitchener aliamua kulipiza kisasi kwa vita ya 1885 akaongoza jeshi kubwa dhidi ya Sudan. Kwa kutumia meli za mvuke kwenye mto Nile na kujenga reli akasongea mbele hadi Omdurman.
20231101.sw_2560_21
https://sw.wikipedia.org/wiki/Sudan
Sudan
Tarehe 2 Septemba 1898 jeshi la mahdiyya lilishindwa kabisa katika mapigano ya masaa matano. Safari hiyo Waingereza waliandaliwa vizuri zaidi, pia silaha mpya kama bunduki ya mtombo ziliwapa ushindi. Upande wa khalifa walikufa askari 11,000, upande wa Waingereza na Wamisri watu 400 pekee.
20231101.sw_2560_22
https://sw.wikipedia.org/wiki/Sudan
Sudan
Khalifa mwenyewe alitoroka akajenga jeshi upya na kutawala kusini mwa Sudan, lakini akauawa mwaka 1899 katika mapigano ya Umm Diwaykarat.
20231101.sw_2560_23
https://sw.wikipedia.org/wiki/Sudan
Sudan
Hivyo Waingereza walitawala Sudan pamoja na Misri hadi 1956, na Kitchener akawa gavana mkuu wa kwanza.
20231101.sw_2560_24
https://sw.wikipedia.org/wiki/Sudan
Sudan
Baada ya uhuru wa nchi (1956), makabila ya kusini, ambayo hayakukubali kusilimishwa, yalipigania vita ndefu hadi kupata uhuru wao.
20231101.sw_2560_25
https://sw.wikipedia.org/wiki/Sudan
Sudan
Kutokana na vita nyingi serikali hazikuwa imara na kulikuwa na mabadiliko ya mara kwa mara baada ya uhuru. Mapinduzi ya kijeshi ya kwanza yalitokea mwaka 1958, kisha jenerali Ibrahim Abboud alitawala hadi 1964 wakati alipopaswa kujiuzulu kutokana na upanuzi wa vita katika Sudan Kusini na upinzani wa wananchi kwenye mji mkuu.
20231101.sw_2560_26
https://sw.wikipedia.org/wiki/Sudan
Sudan
Kilichofuata kilikuwa kipindi cha serikali 3 za kiraia hadi 1969. Tarehe 25 Mei 1969 jeshi, chini ya kanali Gaafar Nimeiry, lilipindua tena serikali. Nimeiry alikuwa waziri mkuu, wakati bunge na vyama vyote vilipigwa marufuku. Nimeiry alitawala hadi 1985, na tangu 1971 alikuwa rais. Mwaka 1972 alifaulu kumaliza awamu ya kwanza ya vita ya wenyewe kwa wenyewe dhidi ya Sudan Kusini kwa mapatano ya Addis Ababa. Sudan Kusini ilipewa mamlaka ya kujitawala katika mambo ya ndani chini ya serikali ya kieneo.
20231101.sw_2560_27
https://sw.wikipedia.org/wiki/Sudan
Sudan
Mwanzoni Nimeiry alijaribu kuiga siasa ya Gamal Abdel Nasser nchini Misri na kutekeleza sera kadhaa za ujamaa. Utawala wake uliona upinzani kutoka kwa Wakomunisti na pia kutoka Waislamu wenye itikadi kali. Baada ya kupinduliwa kwa siku kadhaa na Wakomunisti alivunja ushirikiano na Urusi na kuanza kupokea wanasiasa wenye mwelekeo wa Uislamu mkali katika serikali yake.
20231101.sw_2560_28
https://sw.wikipedia.org/wiki/Sudan
Sudan
Tangu miaka ya 1980 alisogea zaidi upande wa Uislamu wa kisiasa. Mwaka 1983 alitangaza sharia kuwa msingi wa sheria zote na kubadilisha sheria za jinai ipasavyo. Hatua hii ilisababisha upinzani katika sehemu za nchi zisizokaliwa na Waislamu. Alivunja pia serikali ya kieneo kwa Sudan Kusini na hivyo vita ya wenyewe kwa wenywewe ilianza upya.
20231101.sw_2560_29
https://sw.wikipedia.org/wiki/Sudan
Sudan
Nimeiry alitangaza hali ya dharura iliyompa tena mamlaka za kidikteta. Mwaka 1985 aliruhusu kunyongwa kwa mwanafalsafa Mwislamu Mahmoud Mohammed Taha kwa kosa la "uasi dhidi ya Uislamu". Miezi minne baadaye Nimeiry alipinduliwa kwenye mwaka huohuo.
20231101.sw_2560_30
https://sw.wikipedia.org/wiki/Sudan
Sudan
Sudan ilirudi kwa miaka michache chini ya serikali ya kiraia. Mapinduzi yaliyofuata mwaka 1989 yalileta utawala wa jenerali Omar al-Bashir. Vita ya wenyewe kwa wenye iliendelea hadi mwaka 2005 ikamalizika kwa Mapatano ya Naivasha baina ya Sudan na SPLA. Sudan Kusini ilipewa miaka hadi 2011 kujitawala halafu kuwa na kura ya wananchi wa kusini kuhusu uhuru uliotangazwa mwaka uleule.
20231101.sw_2560_31
https://sw.wikipedia.org/wiki/Sudan
Sudan
Tangu mwaka 2003 Bashir alisimamia pia vita ya jeshi lake na wanamgambo dhidi ya wakazi wasio Waarabu wa Darfur waliopinga utawala wake.
20231101.sw_2560_32
https://sw.wikipedia.org/wiki/Sudan
Sudan
Tarehe 11 Aprili 2019 Bashir alipinduliwa na jeshi lake baada ya wiki kadhaa za maandamano ya wananchi wa Khartum na miji mingine dhidi yake. Kupinduliwa kwake pamoja na kipindi cha serikali ya mpito ya kijeshi vilitangazwa na waziri wa ulinzi, jenerali Awad Mohammed Ibn Auf. Ilhali waandamanaji waliendelea kupinga serikali ya kijeshi, Ibn Auf alijiuzulu tarehe 12 Aprili na siku iliyofuata, tarehe 13 Aprili, jenerali Abdel Fattah Burhan alitangaza wanajeshi wanatafuta ushirikiano wa karibu na wapinzani wa utawala wa awali<ref>[https://www.bbc.com/swahili/habari-47919489 Kiongozi wa baraza la kijeshi la mpito nchini Sudan ameapa kuung'oa utawala], BBC News Swahili 13-04-2019</ref>.
20231101.sw_2560_33
https://sw.wikipedia.org/wiki/Sudan
Sudan
Umma wa miji kama Khartoum (pamoja na Omdurman, na Khartoum ya kaskazini) waongezeka zaidi: umma wa miji hiyo yakadiriwa milioni 6-7 na wengine wahamiaji milioni 2 ambao wamekimbia vita vya kusini, magharibi, mashariki na pia wengine kwa sababu ya ukame.
20231101.sw_2560_34
https://sw.wikipedia.org/wiki/Sudan
Sudan
Sudan ina aina mbili za utamaduni — Waafrika walio na Uarabu na Waafrika wasio Waarabu — na maelfu ya makabila na migao ya kabila, lugha tofautitofauti kwa makundi au kabila – migawanyiko hii uleta siasa za utengo na ubaguzi.
20231101.sw_2560_35
https://sw.wikipedia.org/wiki/Sudan
Sudan
Majimbo ya Kaskazini hasa ndio makubwa nchini Sudan, na pia miji mikubwa iko katika majimbo haya. Zaidi ya milioni 22 wanaoishi katika majimbo haya ni Waislamu-Waarabu na wanaongea Kiarabu, lakini wengi pia huongea lugha 70 za kikabila hasa Kinubi, Kibeja, Kifur, Kinuban, Kiingessana, kwa kikundi hiki kuna wale wavutia zaidi kama: Wa-Kababish kutoka Kordofan kaskazini, watu hawa wanaofuga ngamia; Ga’alin (الجعلين), Rubatab (الرباطاب), Manasir (المناصير) and Shaiqiyah (الشايقيّة); makabila ambao makao yao ni karibu na mito ni kama Baggara wa Kurdufan na Darfur; Wakiham Beja eneo ya bahari ya Shamu na Wanubi wa Nile kaskazini, ambao wengine wamehamishwa karibu na mto Atbara. Eneo la Shokrya kwa Wabutana, Wabataheen wamepakana na Waga’alin na Washorya, upande wa kusini-magharibi eneo ya Butana. Pia kuna Warufaa, Wahalaween na makabila mengine mingi eneo la Gazeera na kwa ufuo wa Bluu Nile na eneo ya Dindir. Hata Wanubi kusini mwa eneo la Kurdufan na Wafur upande wa magharibi.
20231101.sw_2560_36
https://sw.wikipedia.org/wiki/Sudan
Sudan
Nchini Sudan kuna lugha zaidi ya 70. Kati yake, muhimu zaidi ni Kiarabu, ambacho ndicho lugha rasmi pamoja na Kiingereza. (Angalia Orodha ya lugha za Sudan.)
20231101.sw_2560_37
https://sw.wikipedia.org/wiki/Sudan
Sudan
Wakristo ni hasa Waorthodoksi wa Mashariki (Wakopti, Waethiopia na Waeritrea, lakini pia Waarmenia), halafu Waorthodoksi, Wakatoliki na Waprotestanti.
20231101.sw_2560_38
https://sw.wikipedia.org/wiki/Sudan
Sudan
Brown, Richard P.C. (1992) Public Debt and Private Wealth: debt, capital flight and the IMF in Sudan. Macmillan Publishers London ISBN 0-333-57543-1.
20231101.sw_2560_39
https://sw.wikipedia.org/wiki/Sudan
Sudan
Churchill, Winston (1899; 2000). The River War — An Historical Account of the Reconquest of the Soudan. Carroll & Graf Publishers (New York City). ISBN 978-0-7867-0751-5.
20231101.sw_2560_40
https://sw.wikipedia.org/wiki/Sudan
Sudan
Clammer, Paul (2005). Sudan — The Bradt Travel Guide. Bradt Travel Guides (Chalfont St. Peter); Globe Pequot Press. (Guilford, Connecticut). ISBN 978-1-84162-114-2.
20231101.sw_2560_41
https://sw.wikipedia.org/wiki/Sudan
Sudan
Evans-Pritchard, Blake; Polese, Violetta (2008). Sudan — The City Trail Guide. City Trail Publishing. ISBN 978-0-9559274-0-9.
20231101.sw_2560_42
https://sw.wikipedia.org/wiki/Sudan
Sudan
El Mahdi, Mandour. (1965). A Short History of the Sudan. Oxford University Press. ISBN 0-19-913158-9.
20231101.sw_2560_43
https://sw.wikipedia.org/wiki/Sudan
Sudan
Fadlalla, Mohamed H. (2005). The Problem of Dar Fur, iUniverse (New York City). ISBN 978-0-595-36502-9.
20231101.sw_2560_44
https://sw.wikipedia.org/wiki/Sudan
Sudan
Fadlalla, Mohamed H. (2004). Short History Of Sudan. iUniverse (New York City). ISBN 978-0-595-31425-6.
20231101.sw_2560_45
https://sw.wikipedia.org/wiki/Sudan
Sudan
Fadlalla, Mohamed H. (2007). UN Intervention in Dar Fur, iUniverse (New York City). ISBN 978-0-595-42979-0.
20231101.sw_2560_46
https://sw.wikipedia.org/wiki/Sudan
Sudan
Jok, Jok Madut (2007). Sudan — Race, Religion and Violence. Oneworld Publications (Oxford). ISBN 978-1-85168-366-6.
20231101.sw_2560_47
https://sw.wikipedia.org/wiki/Sudan
Sudan
Mwakikagile, Godfrey (2001). Slavery in Mauritania and Sudan — The State Against Blacks, in The Modern African State — Quest for Transformation. Nova Science Publishers (Huntington, New York). ISBN 978-1-56072-936-5.
20231101.sw_2560_48
https://sw.wikipedia.org/wiki/Sudan
Sudan
O'Fahey, Rex Seán; Spauling, Jay Lloyd (1974). Kingdoms of the Sudan. Methuen Publishing (London). ISBN 978-0-416-77450-4. Covers Sennar and Darfur.
20231101.sw_2560_49
https://sw.wikipedia.org/wiki/Sudan
Sudan
Peterson, Scott (2001). Me Against My Brother — At War in Somalia, Sudan and Rwanda — A Journalist Reports from the Battlefields of Africa. Routledge (London; New York City). ISBN 978-0-203-90290-5.
20231101.sw_2560_50
https://sw.wikipedia.org/wiki/Sudan
Sudan
Prunier, Gérard (2005). Darfur — The Ambiguous Genocide. Cornell University Press (Ithaca, New York). ISBN 978-0-8014-4450-0.
20231101.sw_2560_51
https://sw.wikipedia.org/wiki/Sudan
Sudan
Welsby, Derek A. (2002). The Medieval Kingdoms of Nubia — Pagans, Christians and Muslims Along the Middle Nile. British Museum Press (London). ISBN 978-0-7141-1947-2.
20231101.sw_2560_52
https://sw.wikipedia.org/wiki/Sudan
Sudan
Zilfū, ʻIṣmat Ḥasan (translation: Clark, Peter) (1980). Karari — The Sudanese Account of the Battle of Omdurman. Frederick Warne & Co (London). ISBN 978-0-7232-2677-2.
20231101.sw_2560_53
https://sw.wikipedia.org/wiki/Sudan
Sudan
"Quo Vadis bilad as-Sudan? The Contemporary Framework for a National Interim Constitution". Law in Africa'' (Cologne; 2005). Vol. 8, pp.  63–82.
20231101.sw_2560_54
https://sw.wikipedia.org/wiki/Sudan
Sudan
Congressional Research Service (CRS) Reports regarding Sudan –(Kutoka taarifa za baraza ya Marekani)
20231101.sw_2560_55
https://sw.wikipedia.org/wiki/Sudan
Sudan
(Idara ya mambo ya kigeni ya Marekani- Sudan yahusu maandiko zingatizi juu ya usomi na habari kuu za nchi.
20231101.sw_2561_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/Zimbabwe
Zimbabwe
Jamhuri ya Zimbabwe (iliyojulikana wakati wa ukoloni kama Rhodesia ya Kusini) ni nchi isiyo na bahari iliyoko upande wa kusini wa Bara la Afrika, kati ya mto Zambezi na mto Limpopo.