_id
stringlengths
15
22
url
stringlengths
31
150
title
stringlengths
1
86
text
stringlengths
100
23.8k
20231101.sw_2621_3
https://sw.wikipedia.org/wiki/Historia%20ya%20Moroko
Historia ya Moroko
Mwanzoni Moroko ilikuwa sehemu ya milki ya khalifa ya Waomawiyya waliotawala Dameski (Siria). Baada ya kupinduliwa kwa Waomawiyya na Waabasiya wa Baghdad (Iraq) mkimbizi Mwarabu Idris ibn Abdallah (788-791) alikusanya makabila ya Waberber na kuunda milki ya kujitegemea. Hii ilikuwa mwanzo wa Moroko kuwa milki ya Kiislamu inayojitawala.
20231101.sw_2621_4
https://sw.wikipedia.org/wiki/Historia%20ya%20Moroko
Historia ya Moroko
Wafalme wa Wamurabitun (Almoravi) (1073-1147) na wa Wamuwahidun (Almohad) (1147-1269) walieneza utawala wao hadi Afrika ya Magharibi (Mauretania, Senegal na Mali ya leo) na sehemu kubwa ya Andalusia (Hispania ya Kiislamu), tena hadi mipaka ya Misri.
20231101.sw_2621_5
https://sw.wikipedia.org/wiki/Historia%20ya%20Moroko
Historia ya Moroko
Wamuwahidun waliendelea kupanuka kuelekea Misri lakini baadaye walidhoofika wakapaswa kuwaachia Wahispania Wakristo sehemu za Andalusia. Athira ya milki ya Moroko ilipungua baadaye hadi Hispania yote ikarudishwa kwa watawala Wakristo mwaka 1492; pia utawala kusini kwa Sahara haukuendelea.
20231101.sw_2621_6
https://sw.wikipedia.org/wiki/Historia%20ya%20Moroko
Historia ya Moroko
Wareno wa Wahispania waliendelea kuteka miji kwenye pwani za Moroko. Utawala wa Hispania juu ya Ceuta na Melilla leo ni mabaki ya nyakati zile.
20231101.sw_2621_7
https://sw.wikipedia.org/wiki/Historia%20ya%20Moroko
Historia ya Moroko
Sehemu za nchi zilianza kujitawala bila kukubali tena mamlaka wa juu, kwa mfano makabila ya Waberber milimani au miji ya Rabat na Sale iliyounda dola dogo la Jamhuri ya Bou Regreg katika karne ya 17 na kujishughulisha na uharamia.
20231101.sw_2621_8
https://sw.wikipedia.org/wiki/Historia%20ya%20Moroko
Historia ya Moroko
Katika karne ya 17 familia ya Waalawi walishika mamlaka wakaendelea nayo hadi leo. Waliweza kutunza uhuru wa nchi hadi mwanzo wa karne ya 20. Lakini mwanzo wa karne ya 20 Ufaransa na Hispania walimlazimisha mfalme Mulay Abdelaziz kukubali mkataba uliofanya Moroko kuwa kama koloni chini ya nchi hizo mbili.
20231101.sw_2621_9
https://sw.wikipedia.org/wiki/Historia%20ya%20Moroko
Historia ya Moroko
Vita Kuu ya Pili ya Dunia ilidhoofisha Ufaransa pamoja na kuingia kwa wanajeshi Waamerika na Waingereza na ahadi zao za kuleta uhuru tokeo lililohamasisha wazalendo wa Maroko kupigania upya uhuru wa nchi.
20231101.sw_2621_10
https://sw.wikipedia.org/wiki/Historia%20ya%20Moroko
Historia ya Moroko
Baada ya vita Wafaransa walijaribu kukandamiza mwendo huo wakamwondoa Sultani Mohammed V nchini 1953. Ghasia zikaongezeka, Sultani akarudi na nchi ikapewa uhuru mwaka 1956.
20231101.sw_2621_11
https://sw.wikipedia.org/wiki/Historia%20ya%20Moroko
Historia ya Moroko
Utawala wa mwanae Hassan II kuanzia mwaka 1961 uliitwa "miaka ya risasi" kwa sababu mfalme alikataa kukubali utaratibu wa kidemokrasia. Chaguzi zilikuwa za uwongo, wapinzani wakatupwa jela au kuuawa. Hassan II alishinda majaribio mbalimbali ya kumpindua. Siasa ya kushikamana na Marekani ilimsaidia mfalme kimataifa lakini baada ya mwisho wa "vita baridi" alilazimishwa na Wamarekani kulegeza utawala wake.
20231101.sw_2624_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/Changarawe
Changarawe
Changarawe ni mawe madogo. Kama ukubwa wa kila kijiwe ni chini ya 2 mm ndipo mchanga. Kama ni kubwa zaidi kuliko 60-75 mm (kawaida hutofautiana kati ya nchi na nchi) si changarawe tena ni jiwe.
20231101.sw_2624_1
https://sw.wikipedia.org/wiki/Changarawe
Changarawe
Changarawe imetokea kutokana na mmomonyoko wa mawe au mwamba. Idadi kubwa ya changarawe hutokana na mmomonyoko katika mito. Njia nyingine ni mmomonyoko wa barafuto.
20231101.sw_2624_2
https://sw.wikipedia.org/wiki/Changarawe
Changarawe
Changarawe ni jambo muhimu katika ujenzi. Kama kokoto inatumika chini ya barabara au kuchanganywa na simiti kwa ajili ya misingi ya majengo.
20231101.sw_2626_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/Tuta%20la%20mchanga
Tuta la mchanga
Tuta la mchanga ni kilima cha mchanga kilichojengwa na upepo kwa kupuliza na kusukuma punje za mchanga. Kama halishikwi na mimea inaweza kuhamahama.
20231101.sw_2626_1
https://sw.wikipedia.org/wiki/Tuta%20la%20mchanga
Tuta la mchanga
Kando la bahari: mahali pengi ufukoni ni kawaida kuwa na mstari mmoja au miwili ya matuta ya mchanga kando la maji.
20231101.sw_2626_2
https://sw.wikipedia.org/wiki/Tuta%20la%20mchanga
Tuta la mchanga
Matuta ya mchanga ni hatari kwa ajili ya binadamu kwa sababu yanaweza kufunika mashamba, nyumba hata kijiji kizima. Kama upepo ni mkali yanaweza kuhama mita makumi kila nafasi ya dhoruba.
20231101.sw_2626_3
https://sw.wikipedia.org/wiki/Tuta%20la%20mchanga
Tuta la mchanga
Kuna majaribio mengi ya kusimamisha matuta yasihame. Njia mojawapo ni kupanda manyasi katika maeneo penye mvua wa kutosha. Hii ni kazi inayohitaji uangilifu. Lazima kurudia kupanda pale ambako majani yamekufa. Lazima kuzuia wanyama na watu wasikanyage kati ya manyasi haya.
20231101.sw_2627_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/Sahara
Sahara
Sahara ni jangwa kubwa kaskazini mwa Afrika. Ni jangwa kubwa kabisa barani, ni la kwanza duniani kati ya majangwa joto na jangwa la tatu kwa ukubwa ulimwenguni baada Bara la Antaktiki na Aktiki.
20231101.sw_2627_1
https://sw.wikipedia.org/wiki/Sahara
Sahara
Ina eneo la kilometa za mraba 9,200,000, sawa na eneo la Marekani au karibu sawa na eneo lote ya Ulaya.
20231101.sw_2627_2
https://sw.wikipedia.org/wiki/Sahara
Sahara
Sahara inafunika sehemu kubwa ya Afrika Kaskazini isipokuwa kanda lenye rutuba kwenye ufuko wa Bahari Mediteranea, milima ya Atlas kwenye Maghreb na bonde la mto Naili huko Misri na Sudan. Inaenea kuanzia Bahari ya Shamu upande wa mashariki hadi Atlantiki upande wa magharibi, na kutoka Mediteranea upande wa kaskazini hadi kanda la Sahel upande wa kusini.
20231101.sw_2627_3
https://sw.wikipedia.org/wiki/Sahara
Sahara
Wataalamu wa jiografia husema Sahara haikuwa hivyo wakati wote. Kutokana na utafiti wa dalili katika udongo na mawe yake eneo la Sahara katika milenia zilizopita lilikuwa na vipindi vya ukame vikifuatana na vipindi vya mvua.
20231101.sw_2627_4
https://sw.wikipedia.org/wiki/Sahara
Sahara
Sahara iko kaskazini mwa Afrika. Ina nchi za Moroko, Algeria, Tunisia na Libya upande wa kaskazini. Upande wa kusini kuna nchi za kanda la Sahel kama Chad, Mali, Mauritania na Niger. Sahara ya Magharibi ina sehemu ufukoni mwa Atlantiki, na upande wa mashariki ni Sudani na Misri ambako oasisi ya mto Nile inakata eneo lake.
20231101.sw_2627_5
https://sw.wikipedia.org/wiki/Sahara
Sahara
Upande wa magharibi Sahara inaanza kwenye pwani ya Atlantiki ikielekea hadi pwani ya Bahari ya Shamu kwa umbali wa km 5000. Kwa jumla maeneo ya Sahara ni takriban asilimia 30 za bara lote la Afrika.
20231101.sw_2627_6
https://sw.wikipedia.org/wiki/Sahara
Sahara
Uso wa Sahara ni takriban asilimia 80 mawemawe na miamba. Takriban asilimia 20 umefunikwa na mchanga unaosukumwa na upepo kuwa na umbo la matuta ya mchanga ambao yanaweza kuwa na kimo cha mita 180 au zaidi. Kama kila jangwa uso wake unafanyizwa na upepo na maji kutokana na mvua inayonyesha mara chache.
20231101.sw_2627_7
https://sw.wikipedia.org/wiki/Sahara
Sahara
Kuna milima ambayo mara nyingi ina asili ya kivolkeno kama vile Aïr, Ahaggar, Tibesti, Adrar des Iforas na milima ya Bahari ya Shamu. Mlima mrefu ni volkeno ya Emi Koussi iliyo sehemu ya safu ya Tibesti kaskazini mwa Chadi.
20231101.sw_2627_8
https://sw.wikipedia.org/wiki/Sahara
Sahara
Mito ya Sahara haiendelei mwaka wote ikiwa na maji kwa majira tu au hata kila baada ya miaka kadhaa kama mvua imenyesha. Mfano pekee wa kinyume ni mto Naili unaovuka jangwa lote kutoka vyanzo vyake katika Afrika ya Kati hadi kuishia katika Bahari Mediteranea.
20231101.sw_2627_9
https://sw.wikipedia.org/wiki/Sahara
Sahara
Tabianchi ni ya joto na yabisi. Halijoto ni kati ya +58 °C wakati wa mchana ikishuka usiku hadi +13 °C (mlimani hadi -10 °C). Wastani wa mvua katika Sahara ni mm 45.5 kwa mwaka lakini kuna miaka bila mvua yoyote.
20231101.sw_2627_10
https://sw.wikipedia.org/wiki/Sahara
Sahara
Katikati yake Sahara ni yabisi sana, uoto ni haba mno. Katika sehemu za kaskazini na kusini kuna maeneo yenye kiwango cha nyasi na vichaka vidogo kadhaa. Kama unyevu unaweza kudumu kwa muda katika mabonde, vichaka vinakuwa vikubwa zaidi na huko na huko kuna pia miti. Sehemu za milima ya juu ambako joto si kama vile kuna kiwango kidogo cha usimbishaji na hapo mabaki ya misitu ya zamani yapo.
20231101.sw_2627_11
https://sw.wikipedia.org/wiki/Sahara
Sahara
Upande wa kaskazini katika Misri na sehemu za Libya jangwa la Sahara linafika moja kwa moja hadi ufuko wa Mediteranea. Lakini katika nchi za Maghreb jangwa linaishia mguuni pa milima ya Atlas ambayo ina tabianchi ya Kimediteranea yenye majira ya joto na ya baridi pamoja na mvua. Halihewa hiyo inaruhusu uoto wa miti na misitu pamoja na kilimo. Mpaka wa kaskazini wa Sahara unalingana na mpaka wa kaskazini wa kilimo cha mitende na pia mpaka wa kusini wa uoto wa manyasi ya esparto ambayo ni nyasi ya Maghreb na rasi ya Iberia. Mpaka wa kaskazini unalingana pia na mwisho wa maeneo yanayopokea angalau milimita 100 za mvua kwa mwaka.
20231101.sw_2627_12
https://sw.wikipedia.org/wiki/Sahara
Sahara
Upande wa kusini Sahara inapakana na Sahel ambayo ni kanda la savana kavu yenye majira ya mvua na kanda hili laenea upana wote wa Afrika kutoka magharibi hadi mashariki. Mpaka wa kusini wa Sahara unalingana na mstari wa mwisho wa maeneo yanayopokea angalau milimita 150 za mvua kwa mwaka.
20231101.sw_2627_13
https://sw.wikipedia.org/wiki/Sahara
Sahara
Sahara haikuwa jangwa wakati wote. Michoro ya watu wa zamani katika milima ya Tibesti na Air inaonesha wawindaji na wanyama kama viboko na mamba wanaohitaji maji mengi. Wataalamu wamegundua kutokana na utafiti wa mawe na udongo ya kwamba eneo la Sahara lilikuwa na vipindi vikavu na vipindi vya mvua nyingi.
20231101.sw_2627_14
https://sw.wikipedia.org/wiki/Sahara
Sahara
Mnamo miaka 7000 iliyopita Sahara ilikuwa eneo nusu yabisi lenye maji katika mito mirefu. Inawezekana kuilinganisha na Kenya Kaskazini ya leo. Watu waliwinda na kufuga wanyama.
20231101.sw_2627_15
https://sw.wikipedia.org/wiki/Sahara
Sahara
Mnamo miaka 5000 iliyopita Sahara ilikauka hadi kufikia hali yabisi kama leo. Lakini maji ya mvua ya nyakati zile bado yapo chini ya ardhi. Misri na Libya ina miradi mikubwa ya kutumia maji yale kwa pampu na kuanza kilimo jangwani kabisa.
20231101.sw_2627_16
https://sw.wikipedia.org/wiki/Sahara
Sahara
Flora ya Sahara ina mimea tofauti sana kulingana na mazingira mbalimbali ndani yake. Kuna kanda tatu za flora ambazo ni kaskazini, kati na kusini. Zinatofautiana kwa kiwango cha mvua inayonyesha. Wataalamu hutofautisha pia kanda mbili za mpito - mpito wa Mediteranea-Sahara na mpito wa Sahel.
20231101.sw_2627_17
https://sw.wikipedia.org/wiki/Sahara
Sahara
Kuna spishi 2800 za mimea ya juu, na robo ya spishi hizi inapatikana katika Sahara pekee. Nusu ya spishi ni za kawaida katika jangwa kuanzia huko hadi Uarabuni.
20231101.sw_2627_18
https://sw.wikipedia.org/wiki/Sahara
Sahara
Sahara ya Kati, ambayo ni kanda yabisi zaidi, ina spishi 500 za mimea pekee. Hii ni idadi ndogo kulingana na ukubwa wa eneo. Mimea kama miti, mitende, vichaka na manyasi imerekebisha kwa ajili ya mazingira haya kwa kuwa ndogo zaidi, kuhifadhi maji katika shina, na kukuza mizizi ya mlalo kwa kusudi la kukusanya maji na unyevu na pia kuwa na majani yenye ngozi nene (au umbo la sindano) ili kutopoteza maji mengi kwa njia ya uvukizaji. Mimea ina uwezo wa kukauka kabisa halafu kurudi baada ya miaka wakati mvua inanyesha.
20231101.sw_2627_19
https://sw.wikipedia.org/wiki/Sahara
Sahara
Fauna ya Sahara pia ina spishi zilizorekebisha maumbile au maisha kulingana na mazingira. Kuna spishi za bweha na spishi za paa na swala. Paa anayeitwa addax anaweza kuishi mwaka mzima bila kunywa.
20231101.sw_2627_20
https://sw.wikipedia.org/wiki/Sahara
Sahara
Duma ya Sahara imepungua sana kutokana na uwindaji lakini bado yuko Algeria, Togo, Niger, Mali, Benin na Burkina Faso. Lakini idadi ni chini ya duma 250 kwa jumla. Paka huyu anaepukana na jua kuanzia Aprili hadi Oktoba akipumzika wakati wa mchana mahali pa kivuli.
20231101.sw_2627_21
https://sw.wikipedia.org/wiki/Sahara
Sahara
Richard W. Bulliet. The Camel and the Wheel. Harvard University Press, 1975. Republished with a new preface Columbia University Press, 1990.
20231101.sw_2627_22
https://sw.wikipedia.org/wiki/Sahara
Sahara
Eamonn Gearon. The Sahara: A Cultural History. Signal Books, UK, 2011. Oxford University Press, USA, 2011.
20231101.sw_2627_23
https://sw.wikipedia.org/wiki/Sahara
Sahara
János Besenyő. Western Sahara (2009), free online PDF book, Publikon Publishers, Pécs, ISBN 978-963-88332-0-4, 2009
20231101.sw_2627_24
https://sw.wikipedia.org/wiki/Sahara
Sahara
Lizzie Wade. Drones and satellites spot lost civilizations in unlikely places, Science (American Association for the Advancement of Science), DOI: 10.1126/science.aaa7864, 2015
20231101.sw_2628_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kituo%20cha%20Nishi%20Isahaya
Kituo cha Nishi Isahaya
Nishi-Isahaya (kwa Kijapani: 西諫早駅,にしいさはやえき) ni kituo cha treni katika mji wa Nagasaki, nchini Ujapani. Kilifunguliwa mwaka wa 1985.
20231101.sw_2633_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/Gabon
Gabon
Nchi hii ina umma mdogo, madini na mali kwa wingi, na wafanyabiashara kutoka nchi za kigeni wameweza kufanya Gabon iwe nchi yenye maendeleo makubwa.
20231101.sw_2633_1
https://sw.wikipedia.org/wiki/Gabon
Gabon
Jamhuri ya Gabon, tangu kupata uhuru kutoka Ufaransa tarehe 17 Agosti 1960, imeongozwa na Rais watatu, Léon M'ba, El Hadj Omar Bongo ambaye amekuwa kiongozi kutoka mwaka wa 1967 hadi kifo chake (2009: ndiye aliyekuwa kiongozi barani Afrika aliyeshikilia uongozi kwa muda mrefu zaidi), halafu mwanae Ali aliyepinduliwa na wanajeshi tarehe 30 Agosti 2023.
20231101.sw_2633_2
https://sw.wikipedia.org/wiki/Gabon
Gabon
Mwaka wa 1990 Gabon ilianza demokrasia ya vyama vingi na katiba ya kidemokrasia ili ruhusu ukweli wa uchaguzi na uwajibikaji wa idara za serikali, lakini hali iliendelea kuwa karibu ileile.
20231101.sw_2633_3
https://sw.wikipedia.org/wiki/Gabon
Gabon
Gabon ni nchi yenye neema sana kuliko nchi jirani. Uchumi wake, hasa chumo cha umma, ni mara nne ya nchi za Afrika kusini kwa Sahara. Hii hasa ni kwa sababu ya uzalishaji wa mafuta ambao umeleta utajiri na mali, lakini usambazaji wa mali hii ya mafuta bado umedhoofika.
20231101.sw_2633_4
https://sw.wikipedia.org/wiki/Gabon
Gabon
Gabon ilikuwa mwanachama wa Muungano wa Nchi Zinazouza Mafuta (OPEC) kutoka mwaka wa 1975 mbaka 1995.
20231101.sw_2633_5
https://sw.wikipedia.org/wiki/Gabon
Gabon
Mwaka 1990, udhaifu wa pesa CFA frank uliacha Gabon katika shida ya kulipa deni za kimataifa; Ufaransa na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) wameipa Gabon mkopo na usaidizi kwa uelewano kwamba Gabon itageuza uchumi wake barabara.
20231101.sw_2633_6
https://sw.wikipedia.org/wiki/Gabon
Gabon
Yasemekana mambo ya mazingira yalifanya umma wa Gabon kutopanda kwa sensa kati ya miaka 1900 na 1940.
20231101.sw_2633_7
https://sw.wikipedia.org/wiki/Gabon
Gabon
Ni nchi ambayo ina umma mdogo zaidi katika Afrika bara, na upungufu wa wafanyakazi ni mojawapo ya mambo yanayofanya hasa uchumi kutovuma zaidi.
20231101.sw_2633_8
https://sw.wikipedia.org/wiki/Gabon
Gabon
Gabon hasa ina makabila zaidi ya 40 ambayo yana utamaduni na lugha tofauti lakini karibu wote (95%) ni wa jamii ya Bantu. Wafang ndio kabila kubwa zaidi nchini Gabon, wengine ni Wamyene, Wabandjabi, Waeshira, Wabapounou na Waokande.
20231101.sw_2633_9
https://sw.wikipedia.org/wiki/Gabon
Gabon
Lugha ya Kifaransa ndiyo lugha rasmi ya taifa ambayo hutumika kwa mawasiliano (wakazi wanaoimudu ni 80%). Wafaransa 10,000 wanaishi Gabon, na Ufaransa unaathiri mambo ya kigeni, utamaduni na biashara nchini Gabon.
20231101.sw_2633_10
https://sw.wikipedia.org/wiki/Gabon
Gabon
Upande wa dini, imekadiriwa kwamba 75.6% za wakazi ni Wakristo (hasa Wakatoliki), 12.2% ni Waislamu (hasa wageni), na 5.7% wanafuata dini asilia za Kiafrika (Bwiti).
20231101.sw_2633_11
https://sw.wikipedia.org/wiki/Gabon
Gabon
David E. Gardinier and Douglas A. Yates, Historia elekezo ya Gabon, tolezi ya 3. (The Scarecrow Press, Inc., 2006)
20231101.sw_2633_12
https://sw.wikipedia.org/wiki/Gabon
Gabon
David E. Gardinier, Kamusi ya Historia ya Gabon, tolezi ya 2. (The Scarecrow Press, Inc., 1994) – kazi inayohusu maelezo biografia ya vifaa 1,453
20231101.sw_2634_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/Utendi
Utendi
Utendi (pia: utenzi; kutoka kitenzi "kutenda") ni aina ya ushairi na tanzu mojawapo ya fasihi simulizi. Kwa kawaida, utendi husimulia maisha na matendo ya mhusika shujaa au wa visasili.
20231101.sw_2634_1
https://sw.wikipedia.org/wiki/Utendi
Utendi
Maarufu katika fasihi ya Ulaya, kuna tendi kama wimbo wa Troya, wimbo wa Odisei na wimbo wa kabila la Nibelungi; India kuna wimbo wa Mahabharata; Afrika kuna utendi wa Sundiata na wimbo wa Oduduwa. Hizo zote mara nyingi hudondolewa kama mifano ya utendi.
20231101.sw_2634_2
https://sw.wikipedia.org/wiki/Utendi
Utendi
Siku hizi hata riwaya au filamu, hasa kama ni ndefu sana pamoja na wahusika wengi au nyakati nyingi, huitwa utendi.
20231101.sw_2634_3
https://sw.wikipedia.org/wiki/Utendi
Utendi
Chum, Haji & H.E. Lambert (1962). Utenzi wa vita vya Uhud (The epic of the battle of Uhud), collected and compiled by Haji Chum, edited with a translation and notes by H. E. Lambert. (Johari za Kiswahili, vol. 3). Nairobi.
20231101.sw_2634_4
https://sw.wikipedia.org/wiki/Utendi
Utendi
Gérard, S. (1976) "Structure and values in three Swahili epics", Research in African Literatures, 7, 1, 7-22.
20231101.sw_2634_5
https://sw.wikipedia.org/wiki/Utendi
Utendi
Knappert, Jan (1967). Traditional Swahili poetry: an investigation into the concepts of East African Islam as reflected in the Utenzi literature. Leiden: Brill.
20231101.sw_2634_6
https://sw.wikipedia.org/wiki/Utendi
Utendi
Knappert, Jan (1977). Het Epos van Heraklios. Uit het Swahili vertaald in het oorspronkelijke metrum. Amsterdam: Meulenhoff. (Dutch translation in the original meter).
20231101.sw_2634_7
https://sw.wikipedia.org/wiki/Utendi
Utendi
Wamitila, K. W. (1999). "A Rhetorical Study of Kiswahili Classical Poetry: An Investigation into the Nature and Role of Repetition", Research in African Literatures, 30, 1, Spring 1999, 58-73.
20231101.sw_2635_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ali%20Hassan%20Mwinyi
Ali Hassan Mwinyi
Ali Hassan Mwinyi (amezaliwa 8 Mei 1925) alikuwa Rais wa pili wa Tanzania kuanzia mwaka 1985 hadi 1995. Aliyemtangulia ni Mwalimu Julius Nyerere, na aliyemfuata ni Benjamin Mkapa. Pia alikuwa mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuanzia mwaka 1990 hadi 1996.
20231101.sw_2635_1
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ali%20Hassan%20Mwinyi
Ali Hassan Mwinyi
Kabla ya hapo alikuwa Rais wa tatu wa Zanzibar baada ya kujiuzulu kwa mtangulizi wake Aboud Jumbe Mwinyi kwenye Januari 1984. Urais wa Zanzibar ulimfanya kuwa makamu wa rais wa Tanzania; hivyo aliteuliwa kugombea urais wa kitaifa wakati Julius Nyerere alipoamua kutogombea tena kwenye mwaka 1985. Mwinyi alichaguliwa akaacha cheo chake cha Zanzibar akawa rais wa Tanzania. Visiwani alifuatwa na Idris Abdul Wakil.
20231101.sw_2635_2
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ali%20Hassan%20Mwinyi
Ali Hassan Mwinyi
Mwinyi alizaliwa Kivure kwenye Mkoa wa Pwani wa Tanzania bara lakini wazazi wake walihamia Unguja alipokuwa mdogo. Kuanzia mwaka 1933 alipokea elimu ya msingi na sekondari kwenye shule za Mangapwani na Dole Secondary School alikohitimu mwaka 1942. Baada ya masomo ya ualimu aliendelea kwenye Chuo Kikuu cha Durham nchini Uingereza . .
20231101.sw_2635_3
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ali%20Hassan%20Mwinyi
Ali Hassan Mwinyi
Alianza kufundisha shuleni akaendelea kuwa mkuu wa chuo cha ualimu Unguja hadi kuteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa wizara ya elimu ya Zanzibar baada ya mapinduzi kwenye mwaka 1963. Mnamo 1970 alipewa uwaziri wa nchi katika ofisi ya rais akaendelea na vyeo mbalimbali katika serikali ya Zanzibar, pamoja na waziri wa afya, wa mambo ya ndani na wa utalii. Alihudumia pia miaka mitano kama balozi wa Tanzania nchini Misri. Kwenye Januari 1984 aliteuliwa kuwa rais wa Zanzibar baada ya mtangulizi wake Aboud Jumbe Mwinyi alilazimishwa kujiuzulu. Katika nafasi kama rais wa Zanzibar alikuwa pia makamu wa rais wa maungano; katika uchaguzi wa 1985 aliteuliwa na CCM kuwa mgombea kwa nafasi ya raisi wa taifa akachaguliwa bila mpinzani katika mfumo wa chama kimoja.
20231101.sw_2635_4
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ali%20Hassan%20Mwinyi
Ali Hassan Mwinyi
Wakati wa urais wa kitaifa wa Mwinyi, sera za Ujamaa zilianza kugeuzwa. Badala yake sera za soko huria zilianzishwa, masharti ya kuingiza bidhaa kutoka nchi za nje yalipunguzwa na uanzishaji wa biashara ya watu binafsi ulihamasishwa. Mwaka wa 1991, Mwinyi alianzisha Tume ya Nyalali iliyopendekeza kuanzisha mfumo wa vyama vingi nchini. Wakati wa awamu yake kwenye mwaka 1995 ulitokea uchaguzi wa kwanza wa vyama vingi vya kisiasa nchini Tanzania.
20231101.sw_2635_5
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ali%20Hassan%20Mwinyi
Ali Hassan Mwinyi
Sera za soko huria za Mwinyi zimeendelezwa chini ya Rais Benjamin Mkapa. Mwinyi mwenyewe, baada ya kustaafu, hakujiingiza katika mambo ya siasa tena. Anaendelea kuishi huko Dar es Salaam.
20231101.sw_2638_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/Hamed%20bin%20Mohammed%20el%20Murjebi
Hamed bin Mohammed el Murjebi
Hamad bin Muhammad bin Juma bin Rajab el Murjebi (amejulikana zaidi kwa jina la Tippu Tip; 1837 – 14 Juni 1905) alikuwa mfanyabiashara mashuhuri katika Afrika ya Mashariki na ya Kati wakati wa karne ya 19.
20231101.sw_2638_1
https://sw.wikipedia.org/wiki/Hamed%20bin%20Mohammed%20el%20Murjebi
Hamed bin Mohammed el Murjebi
Alikutana na wapelelezi mashuhuri kama David Livingstone, Henry Morton Stanley na Hermann von Wissmann.
20231101.sw_2638_2
https://sw.wikipedia.org/wiki/Hamed%20bin%20Mohammed%20el%20Murjebi
Hamed bin Mohammed el Murjebi
Baba yake alikuwa mfanyabiashara Mwarabu Muhammed bin Juma, mama yake Bint Habib bin Bushir, alikuwa Mwarabu wa tabaka la watawala toka Muscat.
20231101.sw_2638_3
https://sw.wikipedia.org/wiki/Hamed%20bin%20Mohammed%20el%20Murjebi
Hamed bin Mohammed el Murjebi
Hamed aliingia katika shughuli za biashara tangu umri wa miaka 12 akafaulu katika biashara ya misafara kati ya Zanzibar na Kongo.
20231101.sw_2638_4
https://sw.wikipedia.org/wiki/Hamed%20bin%20Mohammed%20el%20Murjebi
Hamed bin Mohammed el Murjebi
Akiwa na umri mdogo, Hamad aliongoza kundi la wanaume 100 kwenda Afrika ya Kati kutafuta watumwa na pembe za ndovu. Baada ya kuvamia maeneo mengi alirudi Zanzibar kuimarisha vyanzo vyake na kukusanya watu wa kumsaidia ili arudi bara. Hapa alipokea jina la Tippu Tip. Kwa mujibu wake mwenyewe, jina hilo lilitokana na mlio wa bunduki yake wa 'tiptip.
20231101.sw_2638_5
https://sw.wikipedia.org/wiki/Hamed%20bin%20Mohammed%20el%20Murjebi
Hamed bin Mohammed el Murjebi
Alipanga misafara ya mahamali waelfu akipeleka bidhaa kutoka Bagamoyo kupitia Tabora hadi Ujiji kwa Ziwa Tanganyika na ndani ya Kongo. Bidhaa alizobeba alizitumia kujipatia pembe za ndovu na watumwa; watumwa walisaidia kubeba pembe za ndovu njia ya kurudi hadi pwani. Hamed alitajirika sana. Athira yake ilipanuka katika Kongo ya Mashariki hadi alitawala eneo kubwa sana.
20231101.sw_2638_6
https://sw.wikipedia.org/wiki/Hamed%20bin%20Mohammed%20el%20Murjebi
Hamed bin Mohammed el Murjebi
Hamed akapata jina huko Ulaya kwa sababu alikutana na wasafiri na wapelelezi Wazungu kama David Livingstone, Veney Cameron, Henry Morton Stanley, Eduard Schnitzer (Emin Pascha), Hermann von Wissmann na Wilhelm Junker ambao mara nyingi walipata misaada muhimu kutoka kwake. Kati ya mwaka 1884 na 1887 alikuwa mtu mwenye mamlaka katika sehemu kubwa za Mashariki ya Kongo.
20231101.sw_2638_7
https://sw.wikipedia.org/wiki/Hamed%20bin%20Mohammed%20el%20Murjebi
Hamed bin Mohammed el Murjebi
Wabelgiji walipoanza kujenga ukoloni wao Kongo walimkuta kama mtawala wa Kongo ya Mashariki wakapatana naye na kumpa cheo cha gavana ya Mkoa wa Chutes Stanley ("maporomoko ya Stanley", leo Kisangani) mwaka 1887 alichoshika kwa miaka michache.
20231101.sw_2638_8
https://sw.wikipedia.org/wiki/Hamed%20bin%20Mohammed%20el%20Murjebi
Hamed bin Mohammed el Murjebi
Mwanzoni mwa 1887, Stanley aliwasili Zanzibar na kumtaka Hamad awe gavana wa Wilaya ya Stanley Falls kwenye Dola Huru la Kongo, iliyokuwa koloni binafsi la mfalme wa Ubelgiji. Mfalme Leopold II wa Ubelgiji na Sultani Barghash bin Said wa Zanzibar walikubaliana na tarehe 24 Februari 1887, Hamad alikubali. Wakati huohuo alikubali kuongoza safari za Stanley ili kwenda kumuokoa Mjerumani Emin Pasha (E. Schnitzer), gavana wa Kiosmani wa Equatoria (eneo la Misri ya Kiosmani, Sudan Kusini ya leo).
20231101.sw_2638_9
https://sw.wikipedia.org/wiki/Hamed%20bin%20Mohammed%20el%20Murjebi
Hamed bin Mohammed el Murjebi
Mabadiliko ya ukoloni yaliharibu biashara yake akarudi Zanzibar 1890/1891 alipobaki bila misafara mipya hadi kifo chake mwaka 1905.
20231101.sw_2638_10
https://sw.wikipedia.org/wiki/Hamed%20bin%20Mohammed%20el%20Murjebi
Hamed bin Mohammed el Murjebi
Hamed amejipatia nafasi katika historia ya Afrika ya Mashariki kwa kuandika yeye mwenyewe tawasifu au kumbukumbu ya maisha yake. Katika lugha ya Kiswahili ndio mfano wa kwanza wa tawasifu. Pia ni mfano wa pekee wa kumbukumbu ya kimaandishi ya matokeo ya siku zile zisizoandikwa na Mzungu lakini na mwenyeji. Aliandika kwa lugha ya Kiswahili akitumia mwandiko wa Kiarabu. Mfasiri katika Ukonsuli wa Ujerumani kwenye kisiwa, Heinrich Brode alinakili muswada wake kwa herufi za Kilatini na kuongeza tafsiri ya Kijerumani iliyochapishwa huko Berlin katika sehemu mbili mwaka 1902 na 1903 , .
20231101.sw_2638_11
https://sw.wikipedia.org/wiki/Hamed%20bin%20Mohammed%20el%20Murjebi
Hamed bin Mohammed el Murjebi
Brode alitumia kazi hiyo kutunga kitabu chake juu ya Hamed kilichochapishwa mwaka 1905 na kutafsiriwa kwa Kiingereza mwaka 1907.
20231101.sw_2638_12
https://sw.wikipedia.org/wiki/Hamed%20bin%20Mohammed%20el%20Murjebi
Hamed bin Mohammed el Murjebi
Baada ya kuondoka kwake Hemed katika Kongo, vita ya Waarabu katika Kongo ilianza. Waarabu na Waswahili wa Kongo Mashariki walipigana na serikali ya kikoloni ya Dola Huru la Kongo ilhali pande zote mbili zilitumia askari Waafrika wengi walioongozwa na viongozi wa nje, ama Waarabu /Waswahili au Wazungu.
20231101.sw_2638_13
https://sw.wikipedia.org/wiki/Hamed%20bin%20Mohammed%20el%20Murjebi
Hamed bin Mohammed el Murjebi
Tippu Tip alipoondoka Kongo, uwezo wa Dola Huru la kikoloni la Mfalme Leopold bado ulikuwa hafifu sana katika sehemu za mashariki. Mamlaka ilikuwa mkononi mwa Waarabu au Waswahili waliofanya biashara ya pembe za ndovu na watumwa kwenda Zanzibar. Kati yao walikuwa Sefu bin Hamed, mwana wa Tippu Tip, na mfanyabiashara aliyejulikana kwa jina la Rumaliza katika maeneo upande wa magharibi ya Ziwa Tanganyika.
20231101.sw_2638_14
https://sw.wikipedia.org/wiki/Hamed%20bin%20Mohammed%20el%20Murjebi
Hamed bin Mohammed el Murjebi
Mwaka 1892 Sefu bin Hamed alishambulia Wabelgiji waliofanya biashara ya pembe za ndovu iliyokuwa hatari kwa biashara ya Waswahili. Serikali ya koloni ya Dola Huru la Kongo ilituma kikosi chini ya kamanda Francis Dhanis kwenda sehemu za mashariki. Dhanis alifaulu mapema kushawishi kiongozi Mwafrika Ngongo Lutete aliyewahi kushirikiana na Sefu ahamie upande wake. Jeshi lake lilikuwa na silaha bora na nidhamu bora kati ya askari wake, likafaulu kumshinda Sefu mara kadhaa hadi ifo chake kwenye Oktoba 1893. Kutoka hapa Dhanis aliendelea kumshambulia Rumaliza na hatimaye kumlazimisha akimbie katika eneo la Afrika ya Mashariki ya Kijerumani.
20231101.sw_2638_15
https://sw.wikipedia.org/wiki/Hamed%20bin%20Mohammed%20el%20Murjebi
Hamed bin Mohammed el Murjebi
Kwa njia hii Wabelgiji walifaulu kuvunja nguvu ya Waarabu na Waswahili katika Kongo Mashariki. Kisiasa hakuna kitu kilichobaki na juhudi za Hemed bin Mohammed el Murjebi kujenga milki yake katika Kongo, ila tu kiutamaduni Hemed na wenzake walifaulu kueneza lugha ya Kiswahili katika sehemu zile.
20231101.sw_2638_16
https://sw.wikipedia.org/wiki/Hamed%20bin%20Mohammed%20el%20Murjebi
Hamed bin Mohammed el Murjebi
Hamad alifariki kutokana na ugonjwa wa malaria tarehe 13 Juni 1905 katika nyumba yake kwenye Mji Mkongwe wa Zanzibar.
20231101.sw_2638_17
https://sw.wikipedia.org/wiki/Hamed%20bin%20Mohammed%20el%20Murjebi
Hamed bin Mohammed el Murjebi
Jina lake linajulikana kama mfano wa mabaya ya biashara ya watumwa iliyoharibu maeneo makubwa huko Kongo kabla ya mwanzo wa ukoloni. Yeye mwenyewe aliona watumwa ni sehemu tu ya biashara yake akitajirika hasa na biashara ya pembe za ndovu.
20231101.sw_2638_18
https://sw.wikipedia.org/wiki/Hamed%20bin%20Mohammed%20el%20Murjebi
Hamed bin Mohammed el Murjebi
Bennett, Norman Robert. Arab vs. European: Diplomacy and war in Nineteenth-Century East Central Africa. New York: Africana Publishing Company, 1986.
20231101.sw_2638_19
https://sw.wikipedia.org/wiki/Hamed%20bin%20Mohammed%20el%20Murjebi
Hamed bin Mohammed el Murjebi
Brode, Heinrich. Tippoo Tib: The Story of His Career in Zanzibar & Central Africa. Translated by H. Havelock with preface by Sir Charles Elliot. London: Arnold, 1907 (Online version).
20231101.sw_2638_20
https://sw.wikipedia.org/wiki/Hamed%20bin%20Mohammed%20el%20Murjebi
Hamed bin Mohammed el Murjebi
Edgerton, Robert B. (2002). The Troubled Heart of Africa: A History of the Congo. New York: St. Martin's Press. ISBN 0-312-30486-2.
20231101.sw_2638_21
https://sw.wikipedia.org/wiki/Hamed%20bin%20Mohammed%20el%20Murjebi
Hamed bin Mohammed el Murjebi
Maisha ya Hamed bin Mohammed el Murjebi yaani Tippu Tip kwa maneno yake mwenyewe, kimefasiriwa na W.H. Whitely (toleo la Kiswahili - Kiingereza), East Africa Literature Bureau 1974
20231101.sw_2638_22
https://sw.wikipedia.org/wiki/Hamed%20bin%20Mohammed%20el%20Murjebi
Hamed bin Mohammed el Murjebi
Sheriff, Abdul. Slaves, Spices & Ivory in Zanzibar: Integration of an East African Commercial Empire into the World Economy, 1770-1873. London, Nairobi, Tanzania, Athens,OH: James Currey, Heinemann Kenya, Tanzania Publishing House, Ohio University Press, 1987.
20231101.sw_2640_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/Lugha%20za%20Kibantu
Lugha za Kibantu
Lugha za Kibantu huzungumzwa hasa katika nchi za Nigeria, Kamerun, Guinea ya Ikweta, Gabon, Jamhuri ya Kongo, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Rwanda, Burundi, Uganda, Kenya, Tanzania, Komori, Msumbiji, Malawi, Zambia, Zimbabwe, Angola, Namibia, Botswana, Lesotho, Eswatini na Afrika ya Kusini.
20231101.sw_2640_1
https://sw.wikipedia.org/wiki/Lugha%20za%20Kibantu
Lugha za Kibantu
Uenezi huo unaonyesha kwamba kundi la lugha za Kibantu ni kubwa kabisa barani Afrika, na idadi ya wanaozitumia ni takriban watu milioni 310.
20231101.sw_2640_2
https://sw.wikipedia.org/wiki/Lugha%20za%20Kibantu
Lugha za Kibantu
Neno Bantu, maana yake ni watu katika lugha nyingi za kundi hilo. Shina lake ni -ntu, na kiambishi awali cha ba- kinaonyesha uwingi wa viumbehai. Kwa sababu hiyo, mtaalamu Wilhelm Heinrich Immanuel Bleek (aliyeishi tangu mwaka 1827 hadi 1875) alitumia neno hilo kwa kurejea kundi la lugha hizo. Bleek alilinganisha sarufi za lugha mbalimbali za Kibantu, na baadaye Carl Meinhof alimfuata katika utafiti huo.
20231101.sw_2640_3
https://sw.wikipedia.org/wiki/Lugha%20za%20Kibantu
Lugha za Kibantu
Kuna mamia ya lugha za Kibantu; wataalamu wengine wanahesabu 300, wengine wanahesabu 600. Mtaalamu Malcolm Guthrie aliziainisha kulingana na maeneo ya kijiografia. Kila eneo limepata herufi yake — A, B, C, D, E, F, G, H, K, L, M, N, P, R na S — na ndani ya kila eneo kuna tarakimu tena. Pia, Guthrie alichunguza lugha ya nasaba ambayo ni chanzo cha lugha zote za Kibantu.
20231101.sw_2640_4
https://sw.wikipedia.org/wiki/Lugha%20za%20Kibantu
Lugha za Kibantu
Lugha za Kibantu zina tabia mbalimbali za pamoja. Kati ya tabia hizo kuna viambishi awali na ngeli za nomino.
20231101.sw_2640_5
https://sw.wikipedia.org/wiki/Lugha%20za%20Kibantu
Lugha za Kibantu
Kutokana na sifa hizo wataalamu wamekadiria kwamba asili ya lugha za Kibantu ilikuwa katika maeneo ya Kamerun ya Kusini; kutoka huko wasemaji asilia wa Kibantu katika milenia ya pili KK walihamia Kongo hadi Zambia. Waliendelea kuhamahama na kupanuka hadi kufika maeneo yote walipo sasa.
20231101.sw_2640_6
https://sw.wikipedia.org/wiki/Lugha%20za%20Kibantu
Lugha za Kibantu
Sehemu kubwa ya maeneo ya wasemaji wa lugha za Kibantu zilikaliwa awali na wasemaji wa lugha za Khoisan. Wataalamu wamekisia kwamba Wabantu walifaulu kuenea kutokana na maarifa yao ya kilimo na hasa matumizi ya chuma katika zana za kilimo na pia silaha.
20231101.sw_2640_7
https://sw.wikipedia.org/wiki/Lugha%20za%20Kibantu
Lugha za Kibantu
Kati ya lugha za Kibantu zinazotumika zaidi kuna Kiswahili na Kilingala. Lugha zenye wasemaji wengi kama lugha ya kwanza ni Kizulu na Kishona.