_id
stringlengths
15
22
url
stringlengths
31
150
title
stringlengths
1
86
text
stringlengths
100
23.8k
20231101.sw_2640_8
https://sw.wikipedia.org/wiki/Lugha%20za%20Kibantu
Lugha za Kibantu
Kiswahili na lahaja zake (wasemaji milioni 150): Tanzania, Kenya, Uganda, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Rwanda, Burundi, Komori, Mayotte, Msumbiji, Somalia.
20231101.sw_2640_9
https://sw.wikipedia.org/wiki/Lugha%20za%20Kibantu
Lugha za Kibantu
Lingala (wasemaji milioni 10): Angola, Jamhuri ya Afrika ya Kati, Jamhuri ya Kongo, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Gabon
20231101.sw_2644_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/Abuja
Abuja
Abuja ni mji mkuu wa Nigeria. Idadi ya wakazi wake imekadiriwa kuwa watu 178,462 . Mwaka wa 1976, serikali ya Nigeria iliamua kuanzisha mji mkuu mpya badala ya Lagos. Wakachagua katikati ya nchi, na mipango ya ujenzi ikaundwa chini ya makampuni matatu ya Marekani: PRC Corporation; Wallace, McHarg, Roberts na Todd; na Archisystems. Mipango hiyo ikabadilishwa baadaye na Kenzo Tange, msanifu majengo maarufu wa Japani. Abuja ikatangazwa rasmi kuwa mji mkuu wa Nigeria tarehe 12 Desemba 1991. Iko mahali pa 9, 10, Kaskazini na 7, 10, Mashariki.
20231101.sw_2644_1
https://sw.wikipedia.org/wiki/Abuja
Abuja
Sifa muhimu ya Abuja ni Mlima wa Aso ambao ni mwamba ulio na urefu wa mita 400. Upande wa kusini wa mlima huo, kuna Ikulu ya Rais, Bunge la Nigeria, Mahakama Kuu na sehemu nyingi za mji.
20231101.sw_2644_2
https://sw.wikipedia.org/wiki/Abuja
Abuja
Majengo maarufu mengine ni Msikiti wa Taifa (Nigerian National Mosque) na Kanisa Kuu la Madhehebu (National Ecumenical Centre Cathedral). Kuna kiwanja cha ndege cha kimataifa (Nnamdi Azikiwe International Airport), karibu na Mlima wa Zuma. Sehemu nyingine za mji hazijajengwa ilivyopangwa, na majengo mengi yanaendelea kujengwa.
20231101.sw_2644_3
https://sw.wikipedia.org/wiki/Abuja
Abuja
Mji wa Abuja unagombea kuwa mahali pa Michezo ya Jumuiya ya Madola kwa mwaka wa 2014 (2014 Commonwealth Games).
20231101.sw_2645_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/Jakarta
Jakarta
Jakarta (zamani iliitwa Batavia) ni mji mkuu wa Indonesia. Iko kwenye kisiwa cha Java, na mahali pake ni 6, 11, Kusini, na 106, 50, Mashariki. Ukubwa wa eneo lake ni 661.52 km². Idadi ya wakazi wake imekadiriwa kuwa 8,792,000 (mwaka wa 2004).
20231101.sw_2647_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/Windhoek
Windhoek
Windhoek ni mji mkuu wa Namibia, na uko mahali pa 22.56 S 17.09 E. Idadi ya wakazi wake ni takriban 230,000. Mji huu ni kituo muhimu kwa biashara ya ngozi za kondoo. Zamani ulikuwa makao makuu ya mtemi wa kabila la Nama aliyewashinda kabila la Waherero wakati wa karne ya 19. Mwaka wa 1885, nchi ilivamiwa na wakoloni kutoka Ujerumani, na mji wa Windhoek ukawa makao makuu ya serikali ya ukoloni mwaka wa 1892. Wakati wa Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia nchi ilivamiwa na majeshi ya Makaburu kutoka Afrika ya Kusini ambao wametawala nchi ya Namibia hadi mwaka wa 1990. Namibia ilipopata uhuru, mji wa Windhoek ukawa mji mkuu wa Jamhuri ya Namibia.
20231101.sw_2648_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/Koigi%20Wamwere
Koigi Wamwere
Koigi Wamwere ni mwanasiasa, mwanaharakati, na mwandishi kutoka nchi ya Kenya. Koigi alizaliwa mwaka wa 1949 huko Bahati, wilaya ya Nakuru. Koigi anajulikana kwa kujaribu kupindua serikali za Jomo Kenyatta na Daniel arap Moi. Koigi aliwekwa kizuizini na watawala hawa, na baadaye alikimbilia uhamishoni nchini Norway miaka ya 80. Baada ya kurudi Kenya miaka ya 90, Koigi alikamatwa na kushtakiwa kwa madai ya kuhusika na uhaini na uporaji kwa kutumia silaha. Kutokana na kampeni kubwa ya kimataifa dhidi ya kesi hiyo ambayo ilichukuliwa kuwa na nia ya kumnyamazisha, serikali ya Kenya ilimwachia huru.
20231101.sw_2648_1
https://sw.wikipedia.org/wiki/Koigi%20Wamwere
Koigi Wamwere
Koigi ni mwandishi wa vitabu na makala kadhaa. Vitabu vyake ni "A Woman Reborn", "Justice on Trial", na "I Refuse to Die".
20231101.sw_2648_2
https://sw.wikipedia.org/wiki/Koigi%20Wamwere
Koigi Wamwere
Hivi sasa Koigi ni mbunge wa jimbo la Subukia na waziri msaidizi wa Habari katika serikali ya Mwai Kibaki. Koigi, ambaye huko nyuma alikuwa na nywele msokoto (dreadlocks), alinyoa nywele zake baada ya kuangushwa kwa serikali ya chama cha KANU kutimiza ahadi yake kuwa atanyoa nywele baada ya ushindi dhidi ya chama hicho kupatikana.
20231101.sw_2650_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/Lusaka
Lusaka
Lusaka ni mji mkuu wa Zambia. Jiji la Lusaka liko Kusini ya Kati ya Zambia, na mahali pake ni 15°25' Kusini, 28°17' Mashariki . Iko futi 4200 (au mita 1400) juu ya UB. Idadi ya wakazi wake imekadiriwa kuwa watu 1,391,000 (mwaka wa 2000).
20231101.sw_2650_1
https://sw.wikipedia.org/wiki/Lusaka
Lusaka
Mji wa Lusaka ulianzishwa mwaka wa 1905 na wakoloni Wazungu kwenye mahali pa kijiji ambacho mwenyekiti wake aliitwa Lusaaka. Kwa vile Lusaka iko katikati ya nchi, mwaka wa 1935 wakoloni Waingereza walihamishia mji mkuu wao wa Rhodesia ya Kaskazini huko kutoka mji wa Livingstone. Baada ya kupata uhuru, Lusaka ikaendelea kama mji mkuu wa Zambia hadi hivi sasa.
20231101.sw_2650_2
https://sw.wikipedia.org/wiki/Lusaka
Lusaka
Lusaka hufikika kupitia kiwanja cha ndege cha kimataifa (Lusaka International Airport), au kupitia garimoshi kwenye njia ya reli inayoelekea kutoka mji wa Livingstone kwenda mji wa Kitwe.
20231101.sw_2655_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kunguru
Kunguru
Kunguru ni ndege wakubwa kiasi wa familia Corvidae. Spishi nyingine huitwa vinubi. Wanatokea mabara yote isipokuwa Antakitiki. Spishi nyingi ni nyeusi au nyeusi pamoja na rangi ya nyeupe, kijivu au kahawa; nyingine zina rangi mbalimbali kama buluu, pinki n.k. Hula nusra kila kitu: wanyama na ndege wadogo, wadudu, mizoga, matunda, nafaka n.k. Hulijenga tago lao kwa vijiti juu ya mti au jabali. Spishi nyingine huyajenga matago kwa makundi. Jike huyataga mayai 3-10.
20231101.sw_2655_1
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kunguru
Kunguru
Baadhi ya kunguru huonwa kuwa ni waharibifu na inajulikana kwamba kunguru mkubwa kaskazi (Corvus corax), kunguru mkubwa wa Australia (Corvus coronoides) na kunguru mlamizoga (Corvus corone) wanaweza kuua wanakondoo dhaifu. Lakini mara nyingi hula mizoga iliyouawa karibuni kwa namna nyingine, ugonjwa k.m. Wengine wanaweza kuiga sauti ya binadamu, lakini hawawezi kuongea kama kasuku. Kunguru waliofundishwa kuongea, huonwa kama sehemu muhimu ya Asia ya Mashariki, kwa sababu kunguru huonwa kama alama ya bahati. Baadhi ya watu wanafuga kunguru kama wanyama wa nyumbani. Japo binadamu hawawezi kuwatambua kunguru, kunguru wanaweza kuwatambua watu na kuelewa kwamba hawa ni watu wabaya au la.
20231101.sw_2655_2
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kunguru
Kunguru
Kwa tamaduni nyingi za kienyeji za kaskazi ya mbali sana kunguru, spishi kubwa hasa, wamekuchwa kama viumbe vya kirobo au miungu. Katika Afrika Waxhosa wa Afrika Kusini waliwachukulia kunguru kuwa ni ndege wa Mungu. Hadithi ya kixhosa kuhusu shujaa aitwaye Gxam inasimulia kwamba kunguru walirudishia shujaa aliyefanywa upofu uwezo wake wa kuona. Hadithi nyingine ya Wasara wa Chadi na Sudani inasimulia kwamba Mungu mkuu, Wantu Su, alimpa mpwa wake wa kiume Wantu ngoma iliyokuwa ndani yake na mifano ya kila kitu kilichokuwamo mbinguni. Wantu alitarajiwa kuwapatia binadamu vitu hivi, lakini alikuwa akishuka kamba iliyounga mbingu na dunia, kunguru alipiga ngoma. Ngoma akaanguka duniani, akavunjika na akatawanya wanyama, samaki na mimea duniani kote.
20231101.sw_2655_3
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kunguru
Kunguru
Huko Marekani kunguru huwindwa kwa kibali cha serikali. Isipokuwa kwanzia Agosti mpaka Machi, msimu wa uwindaji kunguru sababu huwa wengi na hapo watu huruhusiwa kuwinda kunguru. Huko Uingereza ni marufuku mpaka pale mtu atakapopewa kibali.
20231101.sw_2655_4
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kunguru
Kunguru
Kunguru anamaamuzi ya haraka sana, na anamacho yenye uwezo mkubwa wa kuona, pia kunguru anaonekana kuwa na ujasiri mkubwa hamwogopi binadam wa kike (mwanamke)
20231101.sw_2655_5
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kunguru
Kunguru
Kunguru hutoa milio mbalimbali. Suala kwamba kuna mawasiliano ya kunguru ni aina ya lugha ni mjadala mkubwa mpaka leo. Kunguru pia wamejifunza kuitika milio ya wanyama wengine na tabia hii hubadilika kwa misimu kadhaa. Milio ya kunguru ni tata na migumu kuelewa, na milio yao hutofautiana kwa spishi tofauti na hasa ugumu wa kujifunza milio huja pale ambapo inafahamika kuwa kunguru wanauwezo wa kusikia sauti ndogo sana ambazo binadamu hawezi kuzisikia.
20231101.sw_2655_6
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kunguru
Kunguru
Kama kundi, kunguru wameonekana kuwa na akili sana na majaribio mbalimbali yamethibitisha hili. Kunguru wamepata alama za juu sana kwenye tafiti za awali. Kunguru wa huko Israeli wamejifunza kutumia vipande vya mkate kama chombo cha kuvulia samaki. Spishi moja, New Caledonian Crow, wamefanyiwa tafiti sana kutokana na uwezo wao wa kutengeneza zana za matumizi ya kila siku. . Ujuzi mwingine ni ule wa kuangusha mbegu ngumu kwenye barabara inayopitisha magari makubwa ili yapasue, na kisha kusubiri taa za barabarani kuruhusu watu wapitie watawanye mbegu hizo. Na tafiti hivi karibuni zinaonesha kuwa kunguru wana uwezo wa nyuso za watu.
20231101.sw_2655_7
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kunguru
Kunguru
Kunguru wa Amerika wanaathirika sana na virusi vya Naili Magharibi ugonjwa ulioanza hivi punde tu huko Amerika kunguru hufa ndani ya wiki moja tu tangu waupate ugonjwa huu na wachache sana hufanikiwa kupona. Kunguru wa huko huathirika sana na, kiasi cha kwamba kifo chao sasa kinaonesha athari ya virusi hao kwenye maeneo yao.
20231101.sw_2655_8
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kunguru
Kunguru
Tangu miaka mingi wataalamu hawakubali kuhusu undugu wa familia Corvidae na jamaa yake. Mwishowe ilionekana kwamba kunguru wametokana na wahenga wa kiaustralasia na walitawanyika duniani kote. Majamaa yao ya karibu sana ni ndege wa peponi (birds of paradise), mbwigu na Australian mudnesters.
20231101.sw_2655_9
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kunguru
Kunguru
Kumbukumbu ya visukuku vya kunguru (mifupa yao) inaonyesha kwamba walikuwa wengi sana Ulaya lakini husiano baina ya kunguru wa kabla ya historia hazieleweki vizuri. Kunguru wa makubwa ya jackdaw, kunguru rangi-mbili na kunguru domo-nene wanaonekana kuwa walikuwepo tangu zamani sana. Kunguru waliwindwa na binadamu hadi enzi ya chuma, kitu ambacho kinaonyesha mabadiliko ya spishi za kisasa. Kunguru wa Marekani hawana historia sahihi inayoaminika. Chakushangaza spishi nyingi zimekwisha hivi sasa baada ya uvamizi wa binadamu, katika visiwa kama Nyuzilandi, Hawaii na Grinlandi hasa.
20231101.sw_2656_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mali
Mali
Imepakana na Algeria, Mauritania, Niger, Burkina Faso, Cote d'Ivoire na Senegal. Mali haina pwani kwenye bahari yoyote.
20231101.sw_2656_1
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mali
Mali
Theluthi mbili za eneo la Niger ni jangwa. Maeneo mengine ni ya Sahel na kanda la Sudan. Sehemu za kusini ni hasa tambarare za bonde la mto Niger.
20231101.sw_2656_2
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mali
Mali
Kanda la jangwani kaskazini - usimbishaji chini ya mm 100 kwa mwaka, yabisi na yabisi sana. Hapa wanaishi wafugaji pekee.
20231101.sw_2656_3
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mali
Mali
Kanda la Sahel: mbuga nusu yabisi inayobadilika kuwa savana kusini kwenye mvua zaidi. Kuna kilimo kando ya mto Niger.
20231101.sw_2656_4
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mali
Mali
Kanda la Sudan lina usimbishaji wa mm 1400 . Lina savana ilhali miti inaongezeka hadi kufika hali ya misitu kabisa kusini.
20231101.sw_2656_5
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mali
Mali
Baada ya uhuru Mali ilikuwa na mikoa 8. Tangu mwaka 2016 Mali imegawanywa katika mikoa kumi na eneo la pekee la mji mkuu.
20231101.sw_2656_6
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mali
Mali
Sheria ya mwaka 2012 ililenga kuwa na mikoa 19, lakini hadi mwaka 2023 kuna mikoa miwili mipya pekee iliyoanzishwa.
20231101.sw_2656_7
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mali
Mali
Kila mkoa unaitwa jina la mji mkuu wake. Mikoa imegawanywa katika wilaya (cercles) 56. Wilaya zote zimegawanywa katika manispaa (communes) 703 .
20231101.sw_2656_8
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mali
Mali
Zamani za Wafinisia na za Waroma palikuwa na mawasiliano ya biashara na nchi za Mediteranea kupitia wanafayabiashara Waberberi walioelewa njia za Sahara.
20231101.sw_2656_9
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mali
Mali
Baada ya uvamizi wa Waarabu na uenezaji wa Uislamu biashara ilianza upya. Ndio Waberberi Waislamu walioingiza dini mpya hata kusini ya Sahara.
20231101.sw_2656_10
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mali
Mali
Katika eneo la Mali ya leo pamoja na nchi jirani ni hasa madola matatu makubwa yaliyotawala upande wa kusini wa njia za biashara iliyovuka Sahara.
20231101.sw_2656_11
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mali
Mali
Dola la kwanza lilikuwa Dola la Ghana. Kuanzia karne ya 8 BK hadi mwaka 1076 lilitawala biashara ya dhahabu, pembe za ndovu na chumvi. Mji mkuu ulikuwa Kumbi Sale wenye wakazi 30,000 katika Mauretania ya leo.
20231101.sw_2656_12
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mali
Mali
Taarifa za wanahistoria Waarabu zimeonyesha ufalme tajiri. Utamaduni wake haukuwa wa Kiislamu bali wa Kiafrika asilia.
20231101.sw_2656_13
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mali
Mali
Mwisho wake ulianza wakati jeshi la Wamurabitun kutoka Moroko lilivuka jangwa na kuvamia Kumbi Sale.
20231101.sw_2656_14
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mali
Mali
Milki ya Mali ilianza kama ufalme mdogo wa Wamalinke kando ya Ghana. Wakati wa karne ya 13 ilianza kupanuka chini ya mfalme Sundiata Keita. Sundiata mwenyewe alipokea Uislamu mnamo 1240 BK na wafalme baada yake waliendela kuwa Waislamu.
20231101.sw_2656_15
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mali
Mali
Mfalme wa Mali aliyejulikana zaidi ndiye Mansa Kankan Musa I (1312–1337). Miaka 1324-1325 alihiji kwenda Makka. Alisafiri na dhahabu nyingi sana. Huku Misri alitoa zawadi kiasi cha kuharibu thamani ya dhahabu kwa miaka 12 iliyofuata.
20231101.sw_2656_16
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mali
Mali
Wakati ule mji wa Timbuktu ulikuwa kitovu cha biashara na elimu iliyojulikana kote katika umma wa Kiislamu hata Ulaya.
20231101.sw_2656_17
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mali
Mali
Asili ya Wasonghai ilikuwa Nigeria ya Kaskazini ya leo. Walipanua utawala wao kuelekea magharibi wakapokea Uislamu wakati wa uvamizi wa Almurabitun.
20231101.sw_2656_18
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mali
Mali
Mnamo mwaka 1250 walikuwa chini ya Mali lakini katika karne ya 14 walijipatia uhuru tena, wakaanza kushika maeneo ya Mali yenyewe.
20231101.sw_2656_19
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mali
Mali
Kilele cha nguvu yake ilikuwa wakati wa mfalme Askia Mohammad I katika karne ya 16 walipotawala eneo kubwa kutoka Kano (Nigeria) hadi pwani ya Atlantiki. Wakati wake mji wa Timbuktu ilitembelewa na msafiri Leo Africanus aliyeleta baadaye habari za nchi hadi Ulaya.
20231101.sw_2656_20
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mali
Mali
Utawala wao uliporomoka baada ya mashumbulizi kutoka Moroko mwaka 1591. Wakati ule mataifa ya Ulaya yameshaanza kufika kwenye mwambao wa Afrika ya Magharibi wakifungua biashara ya moja kwa moja na Ulaya. Umuhimu wa biashara ya kuvuka Sahara ulipungua vikali pamoja na faida iliyopatikana kwa watawala katika maeneo ya Sahel.
20231101.sw_2656_21
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mali
Mali
Kilichofuata kilikuwa kipindi cha madola madogo. Viongozi Waislamu walijaribu mara kadhaa kujenga utawala juu ya eneo lote.
20231101.sw_2656_22
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mali
Mali
Anayejulikana zaidi alikuwa Alhaj Omar aliyepiga vita kwa jina la dini ya Kiislamu dhidi ya Wabambara waliofuata utamaduni na dini asilia za Kiafrika.
20231101.sw_2656_23
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mali
Mali
Mtoto wa Alhaj Omar aliyeitwa Ahmadu alijaribu kuendeleza jihadi yake. Lakini wakati ule Wafaransa walianza kuenea katika Afrika ya Magharibi wakamshinda.
20231101.sw_2656_24
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mali
Mali
Mali ikawa koloni la Ufaransa kuanzia mwaka 1895. Ilikuwa sehemu ya Afrika ya Magharibi ya Kifaransa, na kuanzia 1920 ya Sudan ya Kifaransa.
20231101.sw_2656_25
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mali
Mali
Mwaka 1960 Mali pamoja na Senegal zilipata uhuru kama "Shirikisho la Mali". Baada ya Senegal kuacha umoja huo, Jamhuri ya Mali chini ya rais wa kwanza Modibo Keïta ikawa nchi ya kujitegemea.
20231101.sw_2656_26
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mali
Mali
Keita alipinduliwa mwaka 1968 na wanajeshi akishtakiwa kuwa ameharibu uchumi na kujitajirisha. Kiongozi mpya Moussa Traoré alitawala kama dikteta wa kijeshi, baadaye kwa msaada wa katiba ya chama kimoja.
20231101.sw_2656_27
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mali
Mali
Mabadiliko yaliyotokea kote Afrika tangu mwisho wa Ukomunisti kuanzia miaka ya 1990 yalisababisha kupinduliwa kwa Traoré katika Machi 1991 na kamati ya kijeshi iliyoongozwa na Amadou Toumani Touré.
20231101.sw_2656_28
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mali
Mali
Kaskazini mwa Mali kunakaliwa hasa na Watuareg na baadhi yao hawakupenda kuwa chini ya Mali. Hivyo mara kadhaa kulikuwa na mapigano kati yao na jeshi la nchi. Tangu mwaka 2012 mapigano yameanza upya. Mwaka huo wanamgambo na wanajeshi walikimbia vita kwenda Libya na kujiunga na wapiganaji Watuareg waliotangaza mnamo Aprili 2012 uhuru wa eneo la "Azawad" katika mikoa ya Timbuktu, Gao na Kidal. Lakini wanamgambo wa makundi yenye mwelekeo mkali wa Kiislamu kama Al-Qaeda waliwashinda Watuareg na kushika utawala wakianzisha mfumo wa sharia ya Kiislamu.
20231101.sw_2656_29
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mali
Mali
Serikali ya Mali iliomba usaidizi wa kijeshi wa Ufaransa uliokubaliwa na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kwa azimio na. 2085 ya tarehe 20 Desemba 2012. Jeshi la Kifaransa lilifaulu kuwaondoa wanamgambo Waislamu katika miji yote lakini hao waliendelea kujificha kwenye milima.
20231101.sw_2656_30
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mali
Mali
Baada ya mwisho wa kampeni ya Wafaransa nafasi yao ilichukuliwa na jeshi la Umoja wa Mataifa lililoingia kwa jina la "MINUSMA" lililokuwa na wanajeshi kutoka nchi 60. Kati ya nchi hizo, 19 ni za Kiafrika ambazo walileta idadi kubwa ya askari.
20231101.sw_2656_31
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mali
Mali
Mapigano yameendelea. Wananchi wengi vijijini walichukua silaha na kuunda vikundi vya wanamgambo kwa kujihami lakini vikundi hivyo vinashambuliana pia.
20231101.sw_2656_32
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mali
Mali
Miaka 2020 na 2021 jeshi la Mali liliasi mara mbili na kupindua serikali za kiraia. Kanali Assimi Goïta alitangazwa kuwa rais mtendaji. ECOWAS na Umoja wa Afrika vilisimamisha uanachama wa Mali. Ufaransa na nchi nyingine zilianza kuondoa wanajeshi katika ushirikiano na jeshi la kitaifa.
20231101.sw_2656_33
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mali
Mali
Katika maeneo makubwa ya kaskazini wanaishi makabila ya Waberberi, hasa Mauri na Watuareg ambao ni wahamaji. Ndio 10% ya wakazi wa nchi wakikalia asilimia kubwa za eneo.
20231101.sw_2656_34
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mali
Mali
Kikundi kikubwa ndio Wabambara (33.3%) katika eneo la mji mkuu Bamako, halafu wako Wafula, Wasoninke, Wasenufo/Wabwa, Wamandinka, Wadogon, Wasonghai, Watuareg na wengineo.
20231101.sw_2656_35
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mali
Mali
Kutokana na ukoloni, Kifaransa kilikuwa lugha rasmi, lakini sasa kimeshushwa cheo na kuwa lugha ya mawasiliano tu. Kibambara ndiyo lugha inayoeleweka na takriban 80% za wakazi, nacho kimefanywa lugha rasmi pamoja na nyingine 12 kati ya lugha asilia 56 zinazotumika nchini.
20231101.sw_2656_36
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mali
Mali
Uislamu ni dini kubwa nchini (95 % za wakazi). Wakristo wanafikia 2.3% (Wakatoliki 1.9% na Waprotestanti 0.4%). Wachache wanafuata bado dini asilia za Kiafrika (2.5%).
20231101.sw_2658_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/Aleksander%20Mashuhuri
Aleksander Mashuhuri
Aleksander Mashuhuri (au Aleksanda Mkuu, kwa Kigiriki Μέγας Αλέξανδρος, inayoandikwa kwa alfabeti yetu Megas Aleksandros) aliishi tangu Julai 356 KK hadi tarehe 11 Juni 323 KK.
20231101.sw_2658_1
https://sw.wikipedia.org/wiki/Aleksander%20Mashuhuri
Aleksander Mashuhuri
Mfalme wa Masedonia (336 – 323 KK), anajulikana kama mmoja kati ya amiri jeshi waliofanikiwa kupita wote wengine katika historia ya dunia. Kabla hajafariki kwa umri wa miaka 33 aliteka sehemu kubwa ya dunia iliyojulikana na Wagiriki wa zamani zake, kuanzia Ulaya hadi Bara Hindi na Misri.
20231101.sw_2658_2
https://sw.wikipedia.org/wiki/Aleksander%20Mashuhuri
Aleksander Mashuhuri
Aleksander alizaliwa mwaka 356 KK kama mwana wa mfalme Filippo II wa Masedonia na malkia Olympias. Masedonia ilikuwa nchi katika kaskazini ya Ugiriki ya Kale na Wagiriki wengi waliwatazama Wamasedonia kama washenzi walio nje ya ustaarabu wa Ugiriki. Tofauti na Ugiriki ya Kale iliyokuwa jamii ya madola-miji Masedonia iikuwa jamii ya miji michache na watu wengi walioishi vijijini. Ilitokea katika karne ya 5 KK tu ya kwamba wanamichezo kutoka Masedonia walikubaliwa kwenye Michezo ya Olimpiki..
20231101.sw_2658_3
https://sw.wikipedia.org/wiki/Aleksander%20Mashuhuri
Aleksander Mashuhuri
Filippo II alibadilisha hali ya Masedonia kwa kuimarisha jeshi lake hasa kuanzisha mbinu mpya za kupanga wanajeshi katika vikosi vya phalanx vyenye mikuku mirefu sana na kuunda vikosi vya askari farasi wazito wailokingwa kwa nguo za chuma kifuani na kofia kinga. Kwa kutumia jeshi hili alishinda madola mengine ya Ugiriki na majirani upande wa kaskazini na kuupatia ufalme wake kipaumbele katika Ugiriki. Baada ya kuunganisha Ugiriki chini ya uongozi wake kwa upanga alilenga kushinda pia mioyo yao kwa kuanza vita dhidi ya Milki ya Uajemi iliyowahi kupigana vita na Wagiriki mara kadhaa. Alianza kutuma sehemu ya jeshi kwenda Asia Ndogo iliyokuwa wakati ule sehemu ya Milki ya Uajemi.
20231101.sw_2658_4
https://sw.wikipedia.org/wiki/Aleksander%20Mashuhuri
Aleksander Mashuhuri
Kuna masimulizi mengi kuhusu utoto wa Aleksander ambayo mara nyingi ni hekaya zilizobuniwa baadaye. Hadithi moja inayokubaliwa na wanahistoria ni kuhusu Aleksader kijana wa miaka 10 aliyejipatia farasi iliyombeba baadaye hadi Uhindini. Katika simulizi hii mfalme alitembelewa na mtu aliyetaka kuuza farasi. Farasi moja aliyependeza hakuweza kupandwa na mtu yeyote na mfalme alimkataa. Hapo Aleksander aliomba ajaribu kumpanda akafaulu. Sababu yake ni Aleksander alitambua ya kwamba huyu farasi aligeuka ghafla akikiona kivuli chake wakati mtu alitaka kumpanda. Farasi alinunuliwa na Aleksander alimwita "Bukefalos" akamtumia katika miaka ijayo hadi Misri na Bara Hindi.
20231101.sw_2658_5
https://sw.wikipedia.org/wiki/Aleksander%20Mashuhuri
Aleksander Mashuhuri
Filippo alimwajiri mwanafalsafa Aristoteli kuwa mwalimu wa Aleksander katika falsafa, sanaa na hisabati. Aristoteli alimpa mwanafunzi wake wa kifalme nakala ya muswada ya Ilias na Aleksander aliibeba kwenye kampeni zake za kijeshi. Aristoteli alidai kama sehemu ya malipo yake ya kwamba mji wake wa nyumbani uliowahi kuharibika vitani na Filippo kujengwa upya na raia wake waliowahi kuuzwa kama watumwa wanunuliwe na mfalme na kupewa uhuru.
20231101.sw_2658_6
https://sw.wikipedia.org/wiki/Aleksander%20Mashuhuri
Aleksander Mashuhuri
Uhusiano baina ya kijana Alesander na babake ulikuwa baadaye na matatizo kutokana na husiano za kimapenzi za mfalme kando la mamake Aleksander.
20231101.sw_2658_7
https://sw.wikipedia.org/wiki/Aleksander%20Mashuhuri
Aleksander Mashuhuri
Mwaka 336 KK mfalme Filippo aliuawa na mlinzi wake. Aleksander kijana wa miaka 20 alitangaziwa mfalme mpya kwa msaada wa jemadari Antipater. Aliagiza kuuawa kwa maafisa wa babake waliosambaza uvumi kuwa Aleksander aliuwa ameshiriki jatika uuaji wa babake. Mwaka huohuo alikutana na mabalozi wa miji ya Ugiriki walioapa kumtii.
20231101.sw_2658_8
https://sw.wikipedia.org/wiki/Aleksander%20Mashuhuri
Aleksander Mashuhuri
Mwaka 335 alipaswa kufanya vita na makabila ya kaskazini walioingizwa katika ufalme na babake na sasa waliona nafasi ya kuasi, akawashinda.
20231101.sw_2658_9
https://sw.wikipedia.org/wiki/Aleksander%20Mashuhuri
Aleksander Mashuhuri
Wakati Aleksander alipigania vita katika kaskazini miji ya Wagiriki waliona nafasi ya kutafuta uhuru upya wakaasi. Wakazi wa Thebes waliwafukuza askari wa Kimakedinia katika mji wao. Aleksander alirudi Ugiriki moja kwa moja baada ya ushindi wake kwenye kaskazini akateka mji wa Thebes akaamuru nyumba zote zibomolewe isipokuwa hekalu na nyumba ya mshairi Pindar. Wakazi 6,000 walichinjwa na 30,000 kuuzwa kama watumwa.
20231101.sw_2658_10
https://sw.wikipedia.org/wiki/Aleksander%20Mashuhuri
Aleksander Mashuhuri
Sasa miji mingine ya Ugriki ilishikwa na hofu na kusalimu amri. Aleksander aliwasamehe Wagiriki kwa sababu aliwahitaji kwa mipango yake ya vita dhidi ya Uajemi. Alithebitishwa kama kiongozi na jemadari mkuu wa shirikisho la Wagiriki.
20231101.sw_2658_11
https://sw.wikipedia.org/wiki/Aleksander%20Mashuhuri
Aleksander Mashuhuri
Wakati wa Aleksander Milki ya Uajemi ilikuwa milki iliyotawala eneo kubwa duniani. Wakati wa karne mbili zilizotangulia watawala wa Uajemi waliwahi kuvamia na kuteka Mesopotamia, Shamu, Palestina, Misri, Asia Ndogo pamoja na sehemu za Asia ya Kati. Walijaribu mara kadhaa kuvamia Ugiriki pia lakini waliweza kushindwa kwa matatizo. Katika Asia Ndogo walitawala miji minghi ya Kigiriki iliyokaa ng'ambo ya Bahari ya Aegean. Hivyo Filippo II aliandaa vita dhidi ya Uajemi kwa sababu alitaka kutumia vita dhidi ya maadui wa miaka mingi kuimarisha nafasi yake kati ya Wagiriki. Uvamizi wa kwanza wa Masedonia katika Asia Ndogo ulirudishwa nyuma na Waajemi.
20231101.sw_2658_12
https://sw.wikipedia.org/wiki/Aleksander%20Mashuhuri
Aleksander Mashuhuri
Aleksander alivuka mlangobahari wa Dardaneli katika Mei 334 akiwa na jeshi la askari 35,000 Wamasedonia na Wagiriki. Alimwacha jemadari yake Antipater huko Ugiriki na askari 12,000. Mfalme wa Uajemi alikuwa Darios III aliyesita kumpa jemadari moja mamlaka ya vita akaacha kazi hii kwa makabaila Waajemi katika Asia ndogo. Upande wa Uajemi kulikuwa pia na jemadari Mgiriki Memnon aliyemhudumia mfalme wa Uajemi kama askari wa kukodiwa. Alishauri kutomshambulia Aleksander vikali badala yake kumvuta ndani ya Asia Ndogo na kuharibu akiba zote za chakula anakoenda. Lakini Wakubwa Waajemi walikataa wakatafuta mapigano.
20231101.sw_2658_13
https://sw.wikipedia.org/wiki/Aleksander%20Mashuhuri
Aleksander Mashuhuri
Mkutano wa kwanza wa Aleksander na jeshi la Uajemi ulitokea kwenye Mapigano ya Granikos. Viongozi Waajemi walipanga jeshi lao vibaya wakapigwa na Wamasedonia.
20231101.sw_2658_14
https://sw.wikipedia.org/wiki/Aleksander%20Mashuhuri
Aleksander Mashuhuri
Alesander aliendelea kupita kwenye miji ya pwani iliyokaliwa na Wagiriki na kumfungulia milango yao. Kwa njia hii alitaka kuondoa nafasi ya bandari kwa meli za nevi ya Waajemi zilizokuwa hatari kwa Ugiriki. Aleksander aliteua viongozi wenyeji kama maliwali wake katika majimbo ya Asia Ndogo na hivyo kuimarisha utawala wake.
20231101.sw_2658_15
https://sw.wikipedia.org/wiki/Aleksander%20Mashuhuri
Aleksander Mashuhuri
Baada ya kumaliza miji ya pwani akaingingia ndani ya Asia Ndogo hadi Frygia. Hapa katika mji mkuu wa kale wa Gordion alikata fundo mashihuri wa Gordion. Kwenye ikulu ya kale mjini Gordion ilitunzwa gari la farasi la kale sana. Lilifungwa kwa kamba zilizopigwa fundo imara kupita kiasa. Ilisemekana kuna utabiri kuwa kama mtu angeweza uondoa fundo hili atakuwa mtawala juu ya Asia. Kutokana na hekaya ya kale Aleksander alitazama fundo akaiona gumu akatoa upanga wake na kuikata.
20231101.sw_2658_16
https://sw.wikipedia.org/wiki/Aleksander%20Mashuhuri
Aleksander Mashuhuri
Kuelekea mwisho wa mwaka 333 Aleksander alipokwa habari kuwa mfalme wa Uajemi alikaribia Asia Ndogo kwa jeshi kubwa. Aleksander alipiga mbio kukutana naye. Kwenye mapigano ya Granikos mnamno 5 Novemba 333 majeshi ya Waajemi na Wagiriki yalikutana, tena ushindi ulikuwa upande wa Aleksander. Mfalme Dareios aliweza kukimbia kwa muda.
20231101.sw_2658_17
https://sw.wikipedia.org/wiki/Aleksander%20Mashuhuri
Aleksander Mashuhuri
Katika vitabu vya deuterokanoni vya Biblia anatajwa katika vitabu vya Wamakabayo kama mwanzilishi wa dola lililoeneza ustaarabu wa Kigiriki hata kuhatarisha imani ya Wayahudi na kuwadhulumu wakati wa mwandamizi wake Antioko Epifane wa Syria.
20231101.sw_2658_18
https://sw.wikipedia.org/wiki/Aleksander%20Mashuhuri
Aleksander Mashuhuri
Katika kitabu cha Kizoroastria cha kipindi cha kati ya Uajemi kilichoitwa Arda Wiraz Nāmag Aleksander anajulikana kama “Aleksander aliyelaaniwa” kwa sababu alishinda milki ya Uajemi na aliangamiza mji mkuu wake ulioitwa Persepolis. Lakini katika habari za baadaye za Uajemi, mpaka Irani ya siku hizi, anaitwa Eskandar na hata alishangiliwa wakati Ukuta Mkuu wa Sadd-e Eskandar ulijengwa wakati wa Ufalme wa Parthia.
20231101.sw_2658_19
https://sw.wikipedia.org/wiki/Aleksander%20Mashuhuri
Aleksander Mashuhuri
Pia anajulikana katika desturi za Mashariki ya Kati kama Dhul-Qarnayn kwa Kiarabu na Dul-Qarnayim kwa Kiyahudi na Kiaramu, yaani "mtu mwenye pembe mbili", huenda kwa sababu picha kwenye sarafu za wakati wa utawala wake ilimwonyesha kama anazo pembe mbili za kondoo dume za mungu Ammon wa Misri.
20231101.sw_2659_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/Wolfgang%20Amadeus%20Mozart
Wolfgang Amadeus Mozart
Wolfgang Amadeus Mozart (Salzburg, 27 Januari 1756 – Vienna, 5 Disemba 1791) alikuwa mtunzi mashuhuri wa opera na mpigaji wa ajabu sana wa piano kutoka nchini Austria.
20231101.sw_2659_1
https://sw.wikipedia.org/wiki/Wolfgang%20Amadeus%20Mozart
Wolfgang Amadeus Mozart
Licha ya kuwa na maisha mafupi (alifariki akiwa na umri wa miaka 35 tu), alitunga zaidi ya nyimbo 800 za kila aina, zikiwemo opera (muziki wenye hadithi) Don Giovanni na Die Zauberflöte (Filimbi ya Ajabu). Watu wanaamini kwamba Mozart ni moja kati ya watunzi bora wa muda wote wa nyimbo za Ulaya, ikimpelekea mtunzi mwenzake Joseph Haydn kuandika kuwa: "kizazi kingine hakitaona talanta kama yake tena kwa karne moja".
20231101.sw_2659_2
https://sw.wikipedia.org/wiki/Wolfgang%20Amadeus%20Mozart
Wolfgang Amadeus Mozart
Kazi zake alizianza na minuet (dansi) aliyoitunga akiwa na umri wa miaka minne, na alizimalizia kwa kipande chake cha mwisho, Requiem, ambacho alikiacha hajakimaliza.
20231101.sw_2659_3
https://sw.wikipedia.org/wiki/Wolfgang%20Amadeus%20Mozart
Wolfgang Amadeus Mozart
Mozart alizaliwa katika familia ya wanamuziki. Baba yake, Leopold Mozart, alikuwa mpiga zeze na mtunzi mashuhuri ambaye alifanya kazi na Askofu mkuu wa Salzburg. Alikuwa na dada mkubwa, Maria Anna, aliyeitwa kwa jina la utani "Nannerl" (kulikuwa na ndugu wengine ambao walifariki wakiwa watoto).
20231101.sw_2659_4
https://sw.wikipedia.org/wiki/Wolfgang%20Amadeus%20Mozart
Wolfgang Amadeus Mozart
Mozart alibatizwa asubuhi baada ya kuzaliwa kwake kwenye kanisa kuu la mjini Salzburg. Jina lake kamili kwa Kilatini lilikuwa “Joannes Chrysostomus Wolfgangus Theophilus Mozart”. Kwa kawaida alikuwa akifahamika kama “Wolfgang Amadeus Mozart”, na jina lake la utani lilikuwa “Wolfi”.
20231101.sw_2659_5
https://sw.wikipedia.org/wiki/Wolfgang%20Amadeus%20Mozart
Wolfgang Amadeus Mozart
Mozart alikuwa mtoto wa ajabu: tangu akiwa mdogo alikuwa na kipaji cha muziki ambacho si cha kawaida. Baba yake alimpa ala kadhaa ili amfundishe mwanawe kutunga muziki.
20231101.sw_2659_6
https://sw.wikipedia.org/wiki/Wolfgang%20Amadeus%20Mozart
Wolfgang Amadeus Mozart
Wolfgang alijifunza kupiga kinanda akiwa na umri wa miaka mitatu, na baada ya muda mfupi akajifunza pia kupiga zeze na organo vilevile.
20231101.sw_2659_7
https://sw.wikipedia.org/wiki/Wolfgang%20Amadeus%20Mozart
Wolfgang Amadeus Mozart
Kuna vipande viwili vifupi vya noti za piano alizotunga akiwa na umri wa miaka mitano, lakini ziliandikwa kwa mwandiko wa baba yake, hivyo si rahisi kusema kiasi cha msaada alioweza kuupata.
20231101.sw_2659_8
https://sw.wikipedia.org/wiki/Wolfgang%20Amadeus%20Mozart
Wolfgang Amadeus Mozart
Baadaye baba yake akaanza kumruhusu mtoto wake, na kumfanya aanze kupiga kazi kwenye kumbi huku kukiwa na watu muhimu kibao mbele yake. Siku hizi hili linaweza kuitwa “ukandamizaji” wa watoto wenye vipaji, lakini miaka hiyo watu walikuwa hawaoni tatizo kumwachia mtoto atumike kwa namna hii. Inaonekana kwamba hili halikumwathiri kabisa, na hivyo akajikuta anakua akiwa mtunzi mkubwa kama vile alivyostahili kuwa.
20231101.sw_2659_9
https://sw.wikipedia.org/wiki/Wolfgang%20Amadeus%20Mozart
Wolfgang Amadeus Mozart
Mozart alianza kupiga kwenye umma mjini Salzburg alipokuwa na umri wa miaka mitano, halafu akachukuliwa na kuelekea jijini Vienna akiwa na umri wa miaka sita.
20231101.sw_2659_10
https://sw.wikipedia.org/wiki/Wolfgang%20Amadeus%20Mozart
Wolfgang Amadeus Mozart
Pia aliwahi kupiga mjini Linz na Pressburg (leo hii inaitwa Bratislava). Aliwahi kupiga mara mbili mbele ya malkia Maria Theresa wa Austria. Katika konseti hili alipiga nyimbo ambazo hata watu wazima wanaweza kuzicheza, na muziki ambao watu hawakuwahi kuusikia. Alikuwa akibuni mitindo na kuicheza huku akiwa amevaa kinanda, au akiwa hatazami mikono yake inapiga wapi na akipitisha mikono huku na huku. Pia alitengeneza miziki ambayo inafuata milio ya vitu vingine na alikuwa akiziweka mbeleni kwake.
20231101.sw_2659_11
https://sw.wikipedia.org/wiki/Wolfgang%20Amadeus%20Mozart
Wolfgang Amadeus Mozart
Watu wengi walimsikia kijana huyu mashuhuri na kuandika habari zake na ndiyo maana hadi leo hii tunajua mengi yaliyotokea. Pia inajulikana kwamba alikuwa anaweza kukumbuka noti za muziki aliotunga akizichungulia mara moja tu.
20231101.sw_2659_12
https://sw.wikipedia.org/wiki/Wolfgang%20Amadeus%20Mozart
Wolfgang Amadeus Mozart
Kwa muda mfupi Mozart akawa anasafiri nchi za nje kwa shughuli za kimuziki. Aliwahi kutumbuiza Munich, Prague, Paris, The Hague na London. Huko mjini London, alipiga mbele ya mfalme George III na kubahatika kukutana na mtunzi mmoja aitwaye Johann Christian Bach, mmoja kati ya watoto wa Johann Sebastian Bach. Alipenda sana muziki wa Christian Bach na hata akaamua kufanya pamoja naye kazi ya muziki.
20231101.sw_2659_13
https://sw.wikipedia.org/wiki/Wolfgang%20Amadeus%20Mozart
Wolfgang Amadeus Mozart
Mnamo mwaka 1767 alikuwa zake mjini Vienna tena ambapo alipata ugonjwa wa ndui, lakini alipona, na baba yake aliona hili kama ni dalili kutoka kwa Mungu kwamba mtoto wake atakuwa salama.
20231101.sw_2659_14
https://sw.wikipedia.org/wiki/Wolfgang%20Amadeus%20Mozart
Wolfgang Amadeus Mozart
Baada ya hapo akaenda nchini Italia ambapo alipata kusikia miziki ya watunzi wengine wengi wa Kiitalia. Watunzi hao ni pamoja na Gregorio Allegri ambaye aliandika wimbo Miserere ambao uliandikwa kwa ajili ya Papa na kwa kuimbiwa na kwaya nzima ya Basilika la Mt. Petro (Vatikani).
20231101.sw_2659_15
https://sw.wikipedia.org/wiki/Wolfgang%20Amadeus%20Mozart
Wolfgang Amadeus Mozart
Katika tungo hizo, hakuna mtu yeyote aliyeruhusiwa kuona kilichoandikwa kwenye muziki huo, hivyo hakukuwa na mtu mwingine aliyeweza kuziimba katika kwaya. Cha kushangaza Mozart alizisikia mara moja tu na kukaa chini na kuzichezea kwa kutumia kumbukumbu yake tu!
20231101.sw_2659_16
https://sw.wikipedia.org/wiki/Wolfgang%20Amadeus%20Mozart
Wolfgang Amadeus Mozart
Huko Mannheim akatokea kumpenda msichana mmoja aliyeitwa Aloysia Weber. Alikuwa na umri wa miaka 16 tu na alikuwa akisomea kuimba. Mozart akataka amchukue kisha aende naye Italia ili amfanye maarufu, lakini baba yake akamwandikia barua kali ya mkwara wa kumtaka aache kufikiria huo upuuzi.
20231101.sw_2659_17
https://sw.wikipedia.org/wiki/Wolfgang%20Amadeus%20Mozart
Wolfgang Amadeus Mozart
Mozart aliandika opera ndogondogo kadhaa akiwa bwana mdogo, lakini opera yake ya kwanza na muhimu ilikuwa Idomeneo, ambayo ilianza kutumbuizwa mjini Munich mnamo 1780.
20231101.sw_2659_18
https://sw.wikipedia.org/wiki/Wolfgang%20Amadeus%20Mozart
Wolfgang Amadeus Mozart
Mwaka uliofuatia akaenda zake Vienna. Lakini muda huo alikuwa akifanya kazi, kama baba yake, kwa Askofu Mkuu wa Salzburg. Aliporudi tena Salzburg akalumbana na Askofu Mkuu, kitendo ambacho kilipelekea kumfanya atimuliwe mbali. Mozart akarudi tena mjini Vienna ambapo alitumia maisha yake yote yaliyombakia.