_id
stringlengths
15
22
url
stringlengths
31
150
title
stringlengths
1
86
text
stringlengths
100
23.8k
20231101.sw_2682_10
https://sw.wikipedia.org/wiki/Johann%20Sebastian%20Bach
Johann Sebastian Bach
Explores cognition, formal methods, logic and mathematics—particularly Gödel's incompleteness theorem—in the music of Bach, the art of MC Escher and other sources.
20231101.sw_2682_11
https://sw.wikipedia.org/wiki/Johann%20Sebastian%20Bach
Johann Sebastian Bach
JSBach.org, by Jan Hanford - extensive information on Bach and his works; huge and growing database of user-contributed recordings and reviews
20231101.sw_2682_12
https://sw.wikipedia.org/wiki/Johann%20Sebastian%20Bach
Johann Sebastian Bach
J.S. Bach FAQ (from the Internet Archive), by Bernard Greenberg - answers many common questions about Bach
20231101.sw_2682_13
https://sw.wikipedia.org/wiki/Johann%20Sebastian%20Bach
Johann Sebastian Bach
JSBach.net, maintained by David J. Grossman - includes a catalog of works, images, MIDI files, and audio
20231101.sw_2682_14
https://sw.wikipedia.org/wiki/Johann%20Sebastian%20Bach
Johann Sebastian Bach
J.S. Bach on Radio 3 - extensive resources on Bach, on occasion of BBC Radio 3's complete airing of Bach's works in Dec 2005
20231101.sw_2682_15
https://sw.wikipedia.org/wiki/Johann%20Sebastian%20Bach
Johann Sebastian Bach
IMSLP's ongoing project to sort and make freely avalible all of Bach's works from the Bach Gesellschaft Ausgabe.
20231101.sw_2682_16
https://sw.wikipedia.org/wiki/Johann%20Sebastian%20Bach
Johann Sebastian Bach
james kibbie - bach organ works, Free downloads of the complete organ works of Johann Sebastian Bach, recorded by Dr. James Kibbie on original baroque organs in Germany
20231101.sw_2682_17
https://sw.wikipedia.org/wiki/Johann%20Sebastian%20Bach
Johann Sebastian Bach
Bach cylinder recordings , from the Cylinder Preservation and Digitization Project at the University of California, Santa Barbara Library.
20231101.sw_2682_18
https://sw.wikipedia.org/wiki/Johann%20Sebastian%20Bach
Johann Sebastian Bach
Bach manuscripts - video lectures by Christoph Wolff on the Bach family's hidden manuscripts archive
20231101.sw_2686_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/Dahomey
Dahomey
Dahomey ilikuwa jina la jamhuri ya Benin hadi mwaka 1975 lakini hasa jina la ufalme wa Afrika ya Magharibi katika eneo la Benin ya kusini ya leo.
20231101.sw_2686_1
https://sw.wikipedia.org/wiki/Dahomey
Dahomey
Dahomey ilianzishwa na Waaja baada ya uhamisho wao kutoka Togo kuja Benin ya leo. Jina la Dahomey linasemekana kuwa limetokana na neno la Kifon la "dan" lenye maana ya "nyoka" - dokezo la ibada ya nyoka kusini mwa nchi.
20231101.sw_2686_2
https://sw.wikipedia.org/wiki/Dahomey
Dahomey
Jina la mfalme wa kwanza ni Do Aklin aliyekuwa mmoja wa wana watatu wa mfalme wa Ardra waliogawanya ufalme kati yao mnamo 1625 BK. Do Aklin aliunda mji wa Abomey ukawa mji mkuu wa Dahomey.
20231101.sw_2686_3
https://sw.wikipedia.org/wiki/Dahomey
Dahomey
Waaja wa Abomey walichanganyikana na wenyeji wakawa kabila jipya la Wafon au Wadahomey. Waliratibu ufalme wao kwa kuupa serikali ya mfalme mwenye nguvu, wakaunda jeshi la kudumu.
20231101.sw_2686_4
https://sw.wikipedia.org/wiki/Dahomey
Dahomey
Hasa mfalme Wegbadja aliweka utaratibu kwa vizazi vilivyofuata: mfalme alikuwa mtawala mkuu, mkoani au majimboni hapana watawala wa kieneo bali watumishi wake tu.
20231101.sw_2686_5
https://sw.wikipedia.org/wiki/Dahomey
Dahomey
Ardhi yote ilitazamwa kuwa mali ya mfalme mwenyewe, mafundisho yaliyohakikisha malipo ya kodi kutoka kwa wakulima waliokubali ya kwamba nchi waliyoilima ni mali ya mfalme.
20231101.sw_2686_6
https://sw.wikipedia.org/wiki/Dahomey
Dahomey
Mamlaka ya mfalme yalihakikisha nguvu ya Dahomey katika mazingira yake. Jeshi la kudumu lilimpatia chombo muhimu. Ndani ya jeshi hilo kulikuwa na kikosi kimoja cha pekee ambacho kilikuwa kikosi cha wanawake.
20231101.sw_2686_7
https://sw.wikipedia.org/wiki/Dahomey
Dahomey
Wasafiri wa Ulaya walikiita kikosi hiki "Waamazoni" kutokana na askari wa kike katika masimulizi ya Wagiriki wa Kale.
20231101.sw_2686_8
https://sw.wikipedia.org/wiki/Dahomey
Dahomey
Wegbadja na wafuasi wake walikaza pia umuhimu wa ibada za pamoja. Wafalme wenyewe na mizimu yao walipewa nafasi muhimu. Sadaka zilienda na kila nafasi, hasa sadaka kwa mizimu ya wafalme.
20231101.sw_2686_9
https://sw.wikipedia.org/wiki/Dahomey
Dahomey
Ufalme uliongezeka nguvu ya kiuchumi kutokana na biashara ya watumwa. Kupaa kwa nguvu ya Dahomey kulikwenda sambamba na kuenea kwa wafanyabiashara Wazungu kwenye pwani za Afrika ya Magharibi walionunua watumwa kwa ajili ya safari ya Marekani, wakiuza silaha na bidhaa kutoka Ulaya.
20231101.sw_2686_10
https://sw.wikipedia.org/wiki/Dahomey
Dahomey
Katika karne tatu za historia yake Dahomey ilikuwa kati ya wafanyabiashara wakuu wa watumwa. Jeshi la Dahomey lilikuwa na bunduki zilizonunuliwa kwa Wazungu wakiwauzia watumwa; silaha hizo zilitumika kwa ajili ya kupiga vita dhidi ya majirani na kujipatia wafungwa waliouzwa kama watumwa. Mapato kutoka biashara hiyo yaliwezesha wafalme wa Dahomey kununua silaha mpya.
20231101.sw_2687_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/Bibi%20Titi%20Mohammed
Bibi Titi Mohammed
Bibi Titi Mohammed (1926 - 5 Novemba 2000) alikuwa mmoja wa wanawake wa kwanza mzalendo kushika nafasi za ubunge na uwaziri nchini Tanzania. Pia alikuwa kati ya wanawake wa kwanza kujiunga na harakati za kupigania uhuru wa Tanganyika.
20231101.sw_2687_1
https://sw.wikipedia.org/wiki/Bibi%20Titi%20Mohammed
Bibi Titi Mohammed
Mwaka 1969 Bibi Titi Mohammed alikamatwa na mwaka uliofuata alifikishwa mahakamani kwa kosa la kula njama ya kutaka kupindua serikali. Katika kesi hiyo, Bibi Titi alikuwa ni mwanamke pekee katika washtakiwa 7. Baada ya kesi hiyo kusikilizwa alipatikana na hatia na kuhukumiwa kifungo cha maisha. Hata hivyo, mwaka 1972 alisamehewa na rais Julius Nyerere.
20231101.sw_2687_2
https://sw.wikipedia.org/wiki/Bibi%20Titi%20Mohammed
Bibi Titi Mohammed
Juu ya kutolewa kwake, Mohammed aliongoza maisha yake akiwa mpweke. Mume wake alimtelekeza wakati wa kesi, ushirika wake wa kisiasa ukanyang'anywa, na marafiki zake wengi wakamlaani.
20231101.sw_2687_3
https://sw.wikipedia.org/wiki/Bibi%20Titi%20Mohammed
Bibi Titi Mohammed
Mnamo mwaka wa 1991, wakati Tanzania ikisherekea miaka 30 ya uhuru, Bibi Titi ameonekana kwenye maandishi ya chama tawala kama "Shujaa wa Kike Aliyepigania Uhuru".
20231101.sw_2687_4
https://sw.wikipedia.org/wiki/Bibi%20Titi%20Mohammed
Bibi Titi Mohammed
Tarehe 5 Novemba 2000 Mohammed alifariki kwenye hospitali ya Net Care Hospital mjini Johannesburg ambapo alikuwa akitibiwa.
20231101.sw_2687_5
https://sw.wikipedia.org/wiki/Bibi%20Titi%20Mohammed
Bibi Titi Mohammed
Moja kati ya mabarabara makubwa ya jijini Dar es Salaam limepewa jina la Mohammed kwa heshima ya mafaniko makubwa aliyoyafanya wakati wa mbio za kutafuta uhuru wa Mtanzania.
20231101.sw_2687_6
https://sw.wikipedia.org/wiki/Bibi%20Titi%20Mohammed
Bibi Titi Mohammed
Mfahamu Bibi Titi Mohamedi mwanaharakati mwanamke asiyeogopa chochote/Waziri wa kwanza wa wanawamke (YouTube)
20231101.sw_2693_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/Theluji
Theluji
Theluji (kutoka Kiarabu ثلج, thalj) ni aina ya pekee ya barafu ya maji. Inapatikana kama usimbishaji unaotelemka kwa maumbile ya barafu ya fuwelia. Fuwele za theluji ni ndogo; muundo wa fuwele unaonekana kwa macho matupu kama fuwele ni kubwa. Vipande vyake ni vyembamba sana, hivyo theluji hutelemka nyepesi si kama vipande vizito vya mvua ya mawe.
20231101.sw_2693_1
https://sw.wikipedia.org/wiki/Theluji
Theluji
Theluji haipatikani kwa halijoto juu ya 0 C°. Katika Afrika inaweza kutokea tu kwenye milima mirefu kama mlima Kilimanjaro na
20231101.sw_2693_2
https://sw.wikipedia.org/wiki/Theluji
Theluji
Theluji hutokea kama mvuke wa maji mawinguni unafikia halijoto chini ya -10 C°. Maji mawinguni yanaweza kukaa kiowevu (majimaji) hata chini ya 0 C° kwa muda. Matone yake madogo sana yanaanza kushikana na punje ndogo za vumbi hewani na kuganda. Fuweli ndogo (chini ya mm 0,1) hutokea. Kadiri zinavyokua na kuwa nzito zinaanza kushuka. Njiani mvuke baridi inashikana na fuweli zinazoendelea kukua. Maumbile yanatokea ya kufanana na picha ya nyota.
20231101.sw_2693_3
https://sw.wikipedia.org/wiki/Theluji
Theluji
Watu katika nchi baridi wamezoea kutofautisha aina mbalimbali za theluji. Lugha nyingi zina maneno ya pekee kwa ajili ya aina tofauti za theluji, kama ni nyepesi au nzito, chepechepe au kavu, mpya au kama imeshakaa muda fulani.
20231101.sw_2693_4
https://sw.wikipedia.org/wiki/Theluji
Theluji
kama mchanganyiko wa theluji na mvua ikiwa theluji imeanza kuyeyuka wakati wa kunyesha kutokana na kupitia kanda la hewa isiyo baridi
20231101.sw_2693_5
https://sw.wikipedia.org/wiki/Theluji
Theluji
kufunikwa na ganda la barafu kama imeshakaa chini kwa siku kadhaa na jua liliwaka na kuyeyusha theluji ya juu kidogo. Theluji hii inaganda tena na kuwa barafu juu ya theluji ya chini.
20231101.sw_2694_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/Elimu
Elimu
Elimu kwa maana pana ni tendo au uzoefu wenye athari ya kujenga akili, tabia ama uwezo wa kimaumbile wa mtu binafsi. Katika dhana ya kiufundi, elimu ni njia ambayo hutumiwa makusudi na jamii kupitisha maarifa, ujuzi na maadili kutoka kwa kizazi kimoja hadi kingine.
20231101.sw_2694_1
https://sw.wikipedia.org/wiki/Elimu
Elimu
Walimu katika taasisi za elimu huratibisha elimu ya wanafunzi wao kupitia masomo kama vile ya kuandika, kusoma, kuhesabu (hisabati), sayansi na historia. Mbinu hii wakati mwingine huitwa masomo haswa tunaporejelea somo la aina fulani, kwa kawaida mbinu hii hutumiwa na maprofesa katika taasisi za masomo ya juu.
20231101.sw_2694_2
https://sw.wikipedia.org/wiki/Elimu
Elimu
Kuna elimu maalumu kwa wale wanaohitaji ujuzi wa kitaaluma, kama vile wanaohitaji kuwa marubani. Juu ya hayo, kuna nafasi nyingi za elimu katika viwango vingine visivyo rasmi kama vile majumba ya ukumbusho, maktaba pamoja na mtandao na tajriba za maisha.
20231101.sw_2694_3
https://sw.wikipedia.org/wiki/Elimu
Elimu
Haki ya kusoma imeweza kuelezwa kuwa haki ya msingi ya binadamu katika kifungu cha pili cha itifaki ya kwanza ya maagano ya haki za binadamu barani Ulaya kuanzia mwaka wa 1952 ambapo wanachama wote wanashurutishwa kuhakikisha elimu kwa wote. Katika kiwango cha kimataifa, Mapatano ya Umoja wa Mataifa ya haki za kiuchumi, za kijamii na za kiutamaduni katika mwaka wa 1966 yanahakikisha haki hii katika kifungu cha 13.
20231101.sw_2694_4
https://sw.wikipedia.org/wiki/Elimu
Elimu
Mwongozo hurejelea urahisishaji wa somo na hulenga kutambua shabaha zilizobuniwa na mwalimu au mbinu zingine za kufunza.
20231101.sw_2694_5
https://sw.wikipedia.org/wiki/Elimu
Elimu
Kujifunza hurejelea masomo yenye mtazamo unaolenga kuwapa wanafunzi elimu, ujuzi na uwezo unaoweza kutumika punde tu wakamilishapo kipindi cha masomo.
20231101.sw_2694_6
https://sw.wikipedia.org/wiki/Elimu
Elimu
Masomo ya msingi huchukua kati ya miaka 5-7 ya kwanza ya elimu rasmi. Kwa jumla elimu ya juu hujumulisha miaka 6-8 ya masomo kuanzia mwaka wa tano au sita, lakini hutofautiana baina na kati ya nchi. Asilimia 70 ya watoto waliotimu umri wa kujiunga na shule hujiandikisha katika masomo ya msingi kote ulimwenguni na viwango hivi vinaongezeka. Chini ya Elimu kwa mipango yote inaendeshwa na UNESCO, nchi nyingi wana nia ya kufanikisha zima uandikishaji katika elimu ya msingi ifikapo mwaka 2015, na katika nchi nyingi, ni lazima kwa watoto kupata elimu ya msingi.Chini ya mpango wa elimu kwa wote ulioanzishwa na Shirika la Elimu, Sayansi na utamaduni la Umoja Wa Mataifa (UNESCO), nchi nyingi zimejitolea.
20231101.sw_2694_7
https://sw.wikipedia.org/wiki/Elimu
Elimu
Katika mifumo ya kisasa ya elimu ulimwenguni, elimu ya shule za upili au sekondari huchukua kipindi cha pili cha elimu rasmi ambayo hutokea wakati wa ujana wa wanafunzi. Mfumo huu hutofautian na masomo ya msingi ambayo ni ya lazima, ni ya jumla na yanayofanana.
20231101.sw_2694_8
https://sw.wikipedia.org/wiki/Elimu
Elimu
Yale ya shule za upili ni teule na ya hiari. Shule hizi hujulikana kama sekondari, shule za upili, shule za kati, vyuo au shule za ujuzi wa kitaalamu kulingana na kipindi au mfumo unaofuatwa. Maana ya dhana hizi hutofautiana kutoka mfumo mmoja hadi mwingine. Mpaka kamili kati ya elimu ya msingi na ya upili hutofautiana kutoka nchi moja hadi nyingine. Tofauti hizi zipo hata katika nchi lakini kwa kijumla hutokea kati ya mwaka wa saba na wa kumi wa kusoma.
20231101.sw_2694_9
https://sw.wikipedia.org/wiki/Elimu
Elimu
Elimu ya sekondari hutokea katika umri wa ujana. Nchini Marekani na Kanada elimu ya msingi na sekondari kwa pamoja hurejelewa kama elimu ya K-12 na katika nchini ya Nyuzilandi, elimu hii hurejelewa kama elimu ya miaka 1-13. Azma ya elimu ya sekondari ni kutoa maarifa ya kawaida, kutayarisha wanafunzi kwa elimu ya juu au kuwafunza watu kazi moja kwa moja.
20231101.sw_2694_10
https://sw.wikipedia.org/wiki/Elimu
Elimu
Elimu ya sekondari iliibuka nchini Marekani mwaka wa 1910 na ilisababishwa na kuwepo kwa biashara kubwa na maendeleo ya kiteknolojia viwandani. Ili kuafikia mahitaji ya kazi, shule za upili zilijengwa na mtaala uliolenga maarifa ya kazi za ofisi na za sulubu ukazinduliwa. Hii ilibainika kuwa njia ya manufaa kwa mwajiri kwani uimarishaji wa huduma za kibinadamu uliwafanya waajiriwa kuwa madhubuti kazini na kushusha gharama kwa waajiri huku waajiriwa wakinufaika na mishahara minono ikilinganishwa na waliokuwa na elimu ya msingi pekee.
20231101.sw_2694_11
https://sw.wikipedia.org/wiki/Elimu
Elimu
Barani Ulaya, shule za sarufi au akademia zilikuwepo hata katika miaka ya 1500. Shule za umma au zile za kulipa karo au hata shule za ufadhili na wakfu zina historia ndefu zaidi.
20231101.sw_2694_12
https://sw.wikipedia.org/wiki/Elimu
Elimu
Elimu ya juu, yaani ile ya baada ya shule ya upili au elimu ya awamu ya tatu, si ya lazima. Elimu hii kwa kawaida hujumulisha viwango vya shahada pamoja na elimu ya ujuzi wa kitaalamu.
20231101.sw_2694_13
https://sw.wikipedia.org/wiki/Elimu
Elimu
Kwa jumla elimu ya juu hutolewa na vyuo na vyuo vikuu na huambatana na kutolewa kwa vyeti, stashahada za diploma na shahada za digrii kitaaluma.
20231101.sw_2694_14
https://sw.wikipedia.org/wiki/Elimu
Elimu
Masomo ya juu hujumuisha elimu, utafiti na huduma za jamii na katika uwanja wa elimu, hujumulisha viwango vya shahada ya kwanza na nyingine za juu. Elimu ya juu aghalabu huhusu kufuzu katika kiwango cha shahada ya kwanza, ya uzamili na ya uzamifu.
20231101.sw_2694_15
https://sw.wikipedia.org/wiki/Elimu
Elimu
Idadi kubwa ya watu katika nchi zilizoendelea (hadi kufikia asilimia 50) wameweza kupata elimu ya juu wakati fulani maishani mwao. Kwa hiyo, elimu ya juu ni muhimu kwa uchumi wa taifa, ni kiwanda cha pekee ambacho huzalisha wafanyakazi walioelimika.
20231101.sw_2694_16
https://sw.wikipedia.org/wiki/Elimu
Elimu
Katika nchi maskini serikali zinatakiwa kuongeza mikopo kwa wanafunzi wa vyuoni ili waweze kupata elimu hiyo na kusonga mbele, kwa kuwa elimu ni ufunguo wa maisha.
20231101.sw_2694_17
https://sw.wikipedia.org/wiki/Elimu
Elimu
Elimu ya ngumbaru au ya watu wazima imekuwa kawaida katika nchi nyingi. Elimu hii huchukua maumbo mengi yakiwemo elimu rasmi darasani, elimu ya binafsi na masomo ya mtandao. Idadi fulani ya kozi za kazi maalum kama vile elimu ya mifugo, masuala ya madawa, uwekezaji, uhasibu na kozi nyinginezo kwa sasa hupatikana mtandaoni.
20231101.sw_2694_18
https://sw.wikipedia.org/wiki/Elimu
Elimu
Elimu mbadala, ambayo pia hujulikana kama elimu isiyo rasmi, ni dhana yenye maana pana na inayoweza kutumiwa kurejelea aina zote za elimu zilizo nje ya elimu ya kawaida (kwa watu wote na viwango vyote vya elimu).
20231101.sw_2694_19
https://sw.wikipedia.org/wiki/Elimu
Elimu
Hujumuisha si tu mitindo ya elimu inayokusudiwa wanafunzi wenye mahitaji ya pekee lakini pia mitindo inayolenga hadhira ya jumla na kutumia mitindo na falsafa badala ya elimu.
20231101.sw_2694_20
https://sw.wikipedia.org/wiki/Elimu
Elimu
Elimu mbadala mara nyingi huwa matokeo ya mabadiliko katika elimu yaliyotokea katika misingi mbalimbali ya falsafa ambayo kwa kawaida ni tofauti na elimu ya jadi ya lazima. Mabadiliko mengine yana misingi ya kisasa, kiutafiti au kifalsafa, ilhali mengine ni miungano isiyo rasmi kati ya walimu na wanafunzi wasioridhika na masuala fulani ya elimu hiyo ya jadi.
20231101.sw_2694_21
https://sw.wikipedia.org/wiki/Elimu
Elimu
Elimu mbadala hii ambayo ni pamoja na shule za tabia, shule badala, shule zinazojitegemea na masomo ya nyumbani hutofautiana pakubwa, lakini zote hutilia maanani umuhimu wa idadi ndogo ya wanafunzi darasani na mahusiano ya karibu kati ya wanafunzi na walimu. Vilevile husababisha hali ya umoja.
20231101.sw_2694_22
https://sw.wikipedia.org/wiki/Elimu
Elimu
Kuongezwa kwa ruwaza za elimu ya asili (mbinu na maudhui yake) ndani ya elimu badala katika eneo la mfumo wa elimu rasmi na elimu isiyo rasmi kumewakilisha kipengele muhimu kilichochangia ufanisi wa mfumo wa elimu asili kwa wanajamii asili walioamua kufuata njia hii; hii ikiwa ni pamoja na wanafunzi na walimu.
20231101.sw_2694_23
https://sw.wikipedia.org/wiki/Elimu
Elimu
Kuingizwa kwa mbinu za asili kama vile kujua, kusoma, kuelekeza, kufunza na kusoma kama njia nzuri ya kuhakikisha kuwa wanafunzi/wanagenzi na walimu/waelekezi wanaweza kufaidika kutokana na elimu kwa njia ya kiasili iliyokuza, kutumia na kuendeleaza uhamasishaji wa tamaduni za kiasili.
20231101.sw_2694_24
https://sw.wikipedia.org/wiki/Elimu
Elimu
Kwa wanafunzi au wagenzi na walimu au waelekezi, kuwekwa pamoja kwa mbinu hizi mara nyingi huongeza fanaka, matarajio na matokeo ya elimu. Hili huafikiwa kwa kutoa elimu inayooana na taswira zao za asili, mazoea na mitiazamo yao ya ulimwengu. Kwa wanafunzi na walimu wasio wa asili, elimu ya aina hii ina athari ya kuongeza ufahamu wa tamaduni zao za kibinafsi na mazoea ya jumla ya umma na watu wanaowazunguka, hivyo basi kukuza heshima na kuthamini tamaduni za wanajamii hizo.
20231101.sw_2694_25
https://sw.wikipedia.org/wiki/Elimu
Elimu
Katika elimu na mafunzo, kujumuishwa kwa maarifa ya kiasili, tamaduni, maono, mitazamo na dhana katika mitaala, vifaa vya kuelekeza na vitabu vya kozi vina athari kubwa kama ile ya kujumuisha mbinu za asili katika elimu ambayo hunufaisha walimu na wanafunzi katika usambamba wa masomo, kufaulu na matokeo ya masomo hayo. Ambayo hunufaisha walimu na wanafunzi katika usambamba wa masomo, kufaulu na matokeo ya masomo hayo. Walimu na wanafunzi wa kisasa wana heshima, hamasa na maridhio kwa jamii na watu wa kienyeji kutokana na elimu husishi wanayopata.
20231101.sw_2694_26
https://sw.wikipedia.org/wiki/Elimu
Elimu
Mfano mkuu unaoonyesha mbinu na maudhui ya asili yanaweza kukuza matokeo yaliyotajwa hapo juu undhihirika katika elimu ya juu nchini Kanada. Kwa sababu ya sheria fulani, dhamira ya kuongeza mafanikio kwa wanafunzi wa elimu asili na kukuza maadili ya jamii ya kitamanduni, kuingizwa kwa mbinu na maudhui ya asili katika elimu huonwa kuwa jukumu na wajibu wa serikali na taasisi za elimu zenye mamlaka.
20231101.sw_2694_27
https://sw.wikipedia.org/wiki/Elimu
Elimu
Somo la taaluma ni tawi la elimu ambalo hufunzwa kirasmi katika vyuo vikuu ama kupitia njia zingine kama hizo. Kwa kawaida, kila somo huwa na masomo mengine ama matawi na mipaka ya kuyabainisha mara nyingi huwa si dhahiri na na mara nyingine husababisha utata. Mifano ya masomo ya kitaaluma yenye upana ni kama vile sayansi asilia, hesabu, sayansi ya komputa, sayansi za jamii, sayansi za binadamu na sayansi za matumizi.
20231101.sw_2694_28
https://sw.wikipedia.org/wiki/Elimu
Elimu
Kuna utafiti uliofanywa kuhusu mitindo ya kusoma katika miongo miwili iliyopita. Dunn na Dunn walilenga kutambua vichangamshi husishi vinavyofanya masomo yavutie na namna ya kutawala mazingira ya shule. Baadaye Joseph RenzulLi alipendekeza mikAkati tofautitofauti ya kufunza. Howard Gardner alitambua talanta ama vipaji vya mtu binafsi katika nadharia zake za akili nyingi. Kwa misingi ya kazi za C. G. Jung “Kielezi Aina cha Myers Briggs” na “kitenga tabia cha Keisresy” vililenga kuelewa jinsi nafsi za watu huathiri uhusiano wa mtu binafsi na zinavyoathiri maelewano ya watu katika mazingira ya kujifunza. Kazi za David Kolib na Anthony Gregorc “jinsi ya kusawiri” ” hufuata mfano kama huu lakini uliorahisishwa.
20231101.sw_2694_29
https://sw.wikipedia.org/wiki/Elimu
Elimu
Kwa wakati huu, kugawika kwa elimu katika mitindo tofautitofauti hukubalika na wengi. Huenda ikawa kuwa mitindo ya kujifunza ndiyo ya kawaida:
20231101.sw_2694_30
https://sw.wikipedia.org/wiki/Elimu
Elimu
Imedaiwa kuwa kulingana na mtindo wa kujifunza unaopendelewa, mbinu tofautitofauti za kufunza huwa na matokeo ya viwango tofauti. Umuhimu wa nadharia hii ni kuwa kunakofaa, inapaswa kutumia mbinu mbalimbali za kufunza zinazojumulisha mitindo yote mitatu ya kufunza ili wanafunzi tofautitofauti wapate fursa ya kujifunza kwa njia inayowafaa. Guy Claxton ametilia shaka mitindo ya kujifunza kama vile VAK kwani kwa kiasi fulani mitindo hii ina mazoea ya kupachika watoto majina hivyo basi kuwazuia kujifunza.
20231101.sw_2694_31
https://sw.wikipedia.org/wiki/Elimu
Elimu
Kujifunza ni kutaka kujua juu ya jambo fulani ambalo hukulijua kabla. Hata jambo zuri kuhusu kujifunza ni kwamba hakuna mtu yeyote mwenye uwezo wa kukiweka mbali nawe kitu hicho ambacho umejifunza.
20231101.sw_2694_32
https://sw.wikipedia.org/wiki/Elimu
Elimu
Walimu wanapaswa kuelewa somo vilivyo ili kuwasilisha umuhimu wake kwa wanafunzi. Shabaha hapa ni kuunda misingi ya ujuzi kamili ambayo wanafunzi wanaweza kutumia kujijenga zaidi kwani wamewekwa wazi kwa matukio mbalimbali ya maisha. Walimu wazuri huweza kutafsiri habari kama hukadiria vizuri, hutumia mazoea na hekima hadi kwa elimu husika ambayo mwanafunzi anaweza kuelewa, kuhifadhi na kupititishia wengine.
20231101.sw_2694_33
https://sw.wikipedia.org/wiki/Elimu
Elimu
Utafiti kutoka Marekani unatoa maoni kuwa ubora wa walimu ndio kigezo kinachoathiri mafanikio ya wanafunzi, na kuwa nchi zinazopata alama za juu katika mtihani au majaribio ya kimataifa zimeweka sera chungu nzima zinazohakikisha kuwa walimu wanaoajiriwa ndio bora.
20231101.sw_2694_34
https://sw.wikipedia.org/wiki/Elimu
Elimu
Teknolojia ni kigezo muhimu katika elimu. Tarakilishi na simu za rununu zinatumiwa katika nchi zilizoendelea kuimarisha elimu iliyothibitishwa na kukuza njia mpya za elimu kama vile elimu ya mtandao (masomo ya mbali). Wanafunzi hupata fursa ya kuchagua wanachotaka kusoma.
20231101.sw_2694_35
https://sw.wikipedia.org/wiki/Elimu
Elimu
Kuenea kwa tarakilishi pia kunamaanisha kuongezeka kwa programu za kompyuta na kuongeza habari mtandaoni. Teknolojia hutoa vifaa muhimu vinavohitaji ujuzi mpya na uelewa wa wanafunzi zikiwemo njia nyingi za mawasiliano, na huleta njia mpya za kuhusisha wanafunzi kama vile mazingira ya kujifunza.
20231101.sw_2694_36
https://sw.wikipedia.org/wiki/Elimu
Elimu
Teknolojia inatumiwa si tu katika wajibu wa kutawala katika elimu bali pia katika kuwaelekeza wanafunzi. Matumizi ya teknolojia kama vile virusha maandishi (power point) na ubao mweupe hutumiwa kunasa akili za wanafunzi darasani. Teknolojia vilevile hutumiwa kuwatahini wanafunzi. Mfano mzuri ni mfumo wa kuvutia hadhira (ARS),ambao huruhusu majibu ya mitihani moja kwa moja pamoja na majadiliano darasani.
20231101.sw_2694_37
https://sw.wikipedia.org/wiki/Elimu
Elimu
Teknolojia pia imekuwa mojawapo wa maktaba katika elimu ambamo vitabu, ripoti za utafiti, tansifu n.k. huchapishwa. Tovuti zinazochapishwa vitabu, ripoti na tansifu zimekuwa za manufaa kwa wasomi. Zinawapa uwezo wa kupata vitabu maalum kwa ujumbe fulani tofauti na maktaba za kizama ambazo humlazimu mtu kusoma kwa urefu na upana kupata ule ujumbe. Tofuati hizi hufuata mpangilio, nyingine zikiruhusu watumizi kupakua vitabu bila malipo, nyingine zina malipo ya muda, ilhali nyingine hulazimu mtu kununua kile kitabu anachokihitaji.
20231101.sw_2694_38
https://sw.wikipedia.org/wiki/Elimu
Elimu
Teknolojia za habari na mawasiliano (ICT) ni "seti ya vifaa na rasilimali mbalimbali zinazotumiwa kuwasiliana, kuunda, kueneza na kuongoza habari." Teknolojia hizi ni pamoja na kompyuta, mtandao, teknolojia za kusambaza habari (redio na televisheni) na simu (kuongea na pia kwa ujumbe wa maandishi). Kuna mvuto unaoongezeka kuhusu namna tarakilishi na mtandao vinavyoweza kuimarisha elimu katika viwango vyote, yaani mseto wa elimu rasmi na ile isiyo rasmi.
20231101.sw_2694_39
https://sw.wikipedia.org/wiki/Elimu
Elimu
Teknolojia za habari na mawasiliano za awali, kama vile redio na televisheni, zimetumiwa kwa zaidi ya miaka 40 kwa elimu wazi na ile ya mbali, hata hivyo kupiga chapa ndiyo njia nafuu zaidi, inapatikana kwa urahisi, na hivyo basi ni mbinu iliyotawala katika nchi zilizoendelea na zile zinazoendelea.
20231101.sw_2694_40
https://sw.wikipedia.org/wiki/Elimu
Elimu
Matumizi ya tarakilishi na mtandao (ikiwa vinatumika) bado ni changa katika nchi zinazoendelea, na hii ni kwa sababu miundo msingi ni michache na ghali. Kwa kawaida teknolojia kadhaa hutumiwa kwa pamoja bali si mbinu pekee ya kupokelewa. Kwa mfano, Kothmel Community Radio Internet hutumia matangazo ya redio na kompyuta pamoja na teknolojia ya mtandao, na hivyo hurahisisha kugawa habari na kutoa nafasi za elimu katika kijiji fulani Sri Lanka.
20231101.sw_2694_41
https://sw.wikipedia.org/wiki/Elimu
Elimu
Chuo Kikuu cha Uingereza (UKOU) kilichoanzishwa mwaka wa 1969 kama taasisi ya elimu ya kwanza ulimwenguni kujitolea kutoa elimu ya wazi na ya mbali, bado hutegemea vifaa vilivyopigwa chapa na kuongezea redio, runinga na kompyuta. Vivyo hivyo, Chuo Kikuu cha Indira Gandhi nchini India huweka pamoja matumizi ya chapa, sauti zilizorekodiwa, video, redio, televisheni na teknolojia ya vielezo vya kusikiza mkutano.
20231101.sw_2694_42
https://sw.wikipedia.org/wiki/Elimu
Elimu
Dhana ya “masomo yanayosaidiwa na kompyuta” (CAL) limetumiwa kwa wingi kuelezea teknolojia katika masomo.
20231101.sw_2694_43
https://sw.wikipedia.org/wiki/Elimu
Elimu
Nadharia ya elimu ni nadharia ya azma, matumizi na ufafanuzi wa elimu na kusoma. Historia yake inatokana na wataalamu wa elimu kutoka Ugiriki kuanzia karne ya 18. Katika karne ya 20 mbinu za kusoma zimetumia nadharia katika kufunza, kutathmini na katika sheria za elimu ambazo hupatikana katika vitengo mbalimbali kama ifuatavyo:
20231101.sw_2694_44
https://sw.wikipedia.org/wiki/Elimu
Elimu
Sababu zimetolewa kuwa kiasi cha juu cha elimu ni muhimu kwa nchi ili kuwezesha ukuaji haraka wa uchumi. Uchunguzi unaotegemea nadharia huunga mkono nadharia za kutabiri kuwa nchi maskini zinapaswa kukua haraka kuliko nchi tajiri kwani nchi hizi zinaweza kutumia teknolojia mpya kabisa ambayo imeshajaribiwa na nchi tajiri.
20231101.sw_2694_45
https://sw.wikipedia.org/wiki/Elimu
Elimu
Hata hivyo, kuhamisha teknolojia kunahitaji viongozi wenye maarifa na wahandisi wenye uwezo wa kutumia mashine mpya ama mazoezi ya uzalishaji yaliyokopwa ili kuziba mpaka kwa miigo. Hivyo basi, uwezo wa nchi wa kujifunza kutoka kwa nchi kiongozi ni jukumu la wafanyakazi wa nchi hiyo.
20231101.sw_2694_46
https://sw.wikipedia.org/wiki/Elimu
Elimu
Utafiti wa hivi karibuni wa vitambulishi vya kujumuisha ukuaji wa kiuchumi umesisitiza umuhimu wa vyuo asili vya uchumi na majukumu ya ujuzi tambuzi.
20231101.sw_2694_47
https://sw.wikipedia.org/wiki/Elimu
Elimu
Katika kiwango cha mtu binafsi, kuna maandishi yenye uhusiano na kazi ya Jacob Mincer, ya jinsi mapato yanahusiana na elimu na rasilimali ya mtu binafsi. Kazi hii imetia motisha idadi kubwa ya utafiti lakini pia inaelekea kuleta mabishano kwa kiasi fulani. Ubishi mkubwa unahusu jinsi ya kufasiri matokeo ya kusoma.
20231101.sw_2694_48
https://sw.wikipedia.org/wiki/Elimu
Elimu
Wataalamu wa uchumi Samwel Bowels na Herbert Ginits walitoa maoni kwamba kulikuwa na ubishi asili katika elimu nchini Marekani kati ya shabaha ya demokrasia shirikishi yenye usawa na faida ya mapato ya kibepari yaliyodokeza hali ya kutokuwa na usawa.
20231101.sw_2694_49
https://sw.wikipedia.org/wiki/Elimu
Elimu
Historia ya elimu ilianza miaka mingi iliyopita, kwa kuwa elimu kama sayansi haiwezi kutengwa na utamaduni wowote wa elimu iliyokuwepo awali. Wakubwa waliwafunza wadogo wao juu ya jamii kwa kutumia maarifa na ujuzi waliohitaji kufahamu na mwishowe kupitisha.
20231101.sw_2694_50
https://sw.wikipedia.org/wiki/Elimu
Elimu
Mabadiliko ya utamaduni na binadamu kama spishi yalitegemea mazoea ya kupitisha elimu. Katika jamii ambazo hazikujua kusoma, hili liliafikiwa kupitia mdomo na kuiga. Kusimuliana hadithi kuliendelezwa kutoka kizazi kimoja hadi kingine.
20231101.sw_2694_51
https://sw.wikipedia.org/wiki/Elimu
Elimu
Lugha ya mazungumzo iliendelea na kuwa ishara na herufi. Kina na upana wa elimu au maarifa ulioweza kuhifadhiwa na kupitishwa uliongezeka zaidi na zaidi. Wakati ambapo tamaduni zilianza kupanua elimu zaidi ya ujuzi wa kawaida wa mawasiliano, biashara, ukusanyaji chakula, tunu na desturi za kidini na kadhalika, mwishowe elimu rasmi na masomo vilifuatia. Kisomo kwa maana hii kilikuwa kimeshaanza nchini Misri kati ya 3000 na 500 KK.
20231101.sw_2694_52
https://sw.wikipedia.org/wiki/Elimu
Elimu
Siku hizi aina fulani ya elimu ni jambo la lazima kwa watu wote katika nchi nyingi. Kwa sababu ya ongezeko la watu na kuenea kwa elimu ya lazima, Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa (UNESCO) limepiga hesabu ya kwamba miaka 30 ijayo, watu wengi zaidi ulimwenguni watapata elimu rasmi katika historia ya binadamu.
20231101.sw_2694_53
https://sw.wikipedia.org/wiki/Elimu
Elimu
Falsafa ya elimu ni utafiti wa kifalsafa juu ya kusudi, utaratibu na ubora wa elimu kwa kuchunguza ufafanuzi, malengo na maana ya elimu kwa jumla au ya mtazamo mmojawapo juu yake.
20231101.sw_2694_54
https://sw.wikipedia.org/wiki/Elimu
Elimu
Falsafa ya elimu mara nyingi hubaki ndani ya falsafa na elimu, ilhali ni falsafa matumizi, iliyotokana na nyanja za zamani za falsafa (ontolojia, maadili, epistemolojia) na njia (kisia, taswira na tafiti), mbinu na mtaala, nadharia, kwa kutaja tu chache.
20231101.sw_2694_55
https://sw.wikipedia.org/wiki/Elimu
Elimu
Saikolojia ya elimu ni uchunguzi wa jinsi watu hujifunza katika mandhari ya elimu, ufaafu wa maingiliano ya elimu, saikolojia ya kufunza na saikolojia jamii za shule. Ingawa maneno “saikolojia ya kielimu” na “saikolojia ya shule“ mara nyingi hutumiwa kwa kubadilishana, watafiti na wananadharia wanaweza kutambuliwa kama wanasaikolojia wa elimu, ilhali weledi wanaopatikana shuleni au mandhari yanayoana na shule hujulikana kama wanasaikolojia wa shule. Saikolojia ya elimu inajishughulisha na utaratibu wa kutoa elimu kwa watu na umma kwa jumla na umma mdogo, kama vile watoto wenye vipaji na wale wenye ulemavu.
20231101.sw_2694_56
https://sw.wikipedia.org/wiki/Elimu
Elimu
Saikolojia ya elimu inaweza kueleweka kwa sehemu kupitia masomo mengine. Saikolojia ya elimu vilevile huarifiwa na saikolojia, ikileta uhusiano baina ya utabibu na biolojia. Saikolojia ya elimu pia huarifu masafa mapana ya masomo maalum yakiwemo mpango wa mafunzo. Teknolojia ya elimu, mtaala uliokuzwa, masomo yaliyopangwa, masomo maalumu, sayansi tambuzi na sayansi masomo. Katika vyuo vikuu, idara za elimu ya saikolojia zimehifadhiwa katika vitivo vya elimu. Hii ni kwa sababu ya uwezekano wa ukosefu wa uwakilishaji wa maudhui ya saikolojia ya elimu katika utangulizi wa vitabu vya saikolojia.
20231101.sw_2694_57
https://sw.wikipedia.org/wiki/Elimu
Elimu
Sosholojia ya elimu ni somo linalohusu jinsi taasisi za kijamii na kani huathiri michakato na matokeo ya elimu, na kinyume chake. Kwa wengi, elimu hueleweka kama mbinu ya kushinda vizuizi, kufanikisha usawa na kupata amani na hadhi kwa wote (Sargent 1994). Wanafunzi wanaweza kutiwa motisha na hamu ya maendeleo na uboreshaji. Elimu hutambuliwa kama mahali ambapo watoto huweza kujikuza kulingana na mahitaji yao ya pekee. Jukumu la elimu linaweza kuwa ni kukuza mtu binafsi hadi kilele. Uelewa wa shabaha na mbinu za michakato ya utangamano wa kielimu hutofautiana kulingana na dhana ya sosholojia iliyotumika.
20231101.sw_2694_58
https://sw.wikipedia.org/wiki/Elimu
Elimu
Katika nchi zinazoendelea idadi na uzito wa shida zilizoko kwa kawaida ni kubwa. Watu wa vijijini wakati mwingine huwa hawana habari kuhusu umuhimu wa elimu. Hata hivyo, nchi nyingine zina wizara ya elimu na katika masomo mengi, kama vile kujifunza lugha za kigeni, kiwango cha elimu kimo juu kuliko katika nchi zilizoendelea. Kwa mfano, katika nchi zinazoendelea ni kawaida kupata wanafunzi wakizungumza lugha nyingi za kigeni kwa usanifu mkubwa, ilhali jambo hili ni nadra katika nchi zilizoendelea ambapo idadi kubwa ya watu huzungumza lugha moja.
20231101.sw_2694_59
https://sw.wikipedia.org/wiki/Elimu
Elimu
Vilevile kuna shinikizo la kiuchumi kutoka kwa wazazi ambao hupendelea watoto wao wapate pesa kwa muda mfupi kuliko faida za elimu ya muda mrefu. Utafiti wa hivi karibuni kuhusu ajira ya watoto na umasikini zimependekeza kuwa familia zilizokumbwa na umasikini zinapofikia kiwango fulani cha kukidhi mahitaji yao ya kimsingi, wazazi huwarejesha watoto wao shuleni. Hii imethibitshwa kuwa kweli mara tu kizingiti kinapovukwa. Hata kama uwezekano wa thamani ya kiuchumi ya ajira ya watoto inaongezeka baada yao kurudishwa shuleni.
20231101.sw_2694_60
https://sw.wikipedia.org/wiki/Elimu
Elimu
Ukosefu wa vyuo vikuu bora na kiwango cha chini cha kukubalika katika vyuo hivi ni dhahiri katika nchi zilizo na idadi kubwa ya watu. Baadhi za nchi zina mitaala mikuu inayoweza kubadilika kwa urahisi, inayofanana na yenye miundo zaidi.
20231101.sw_2694_61
https://sw.wikipedia.org/wiki/Elimu
Elimu
Kuondolewa kwa asili mia fulani ya wanfunzi kwa ajili ya uboreshaji wa masomo (kwa kawaida hufanywa shuleni baada ya daraja la kumi)
20231101.sw_2694_62
https://sw.wikipedia.org/wiki/Elimu
Elimu
India inakuza teknolojia na mtandao. India ilizindua EDUSAT, elimu ya setilaiti ambayo inaweza kuwafikia wengi kwa gharama ya chini. Kuna pia mpango ulioanzishwa na shirika la OLPC, kundi lililotokana na maabara ya MIT lililoungwa mkono na mashirika makuu ili kukuza kompyuta ya kupakata ambayo ingeghalimu $100, ili kuwezesha kuwasilisha elimu ya programu ya kompyuta. Kompyuta hizi zimesambaa kote kufikia mwaka wa 2009. Kompyuta hizi zinauzwa au kutolewa kama msaada. Hii itawezesha nchi zinazoendelea kuwapa watoto wao elimu kwa kutumia mitambo.
20231101.sw_2694_63
https://sw.wikipedia.org/wiki/Elimu
Elimu
Barani Afrika, shirika la NEPAD limezindua programu ya masomo ya mtandao inayotoa vifaa vya kompyuta na masomo ya mtandao kwa shule zote za msingi na upili kwa kipindi cha miaka kumi. Vikundi vya binafsi kama vile Wamormoni, wanajikakamua kuwapa watu fursa ya kupokea elimu katika nchi zinazoendelea kupitia miradi kama vile Perpetual Educational Fund. Mradi wa maendeleo kimataifa inayofahamika kama nabuur.com, com iliyoanza kwa msaada wa rais wa Marekani Bill Clinton, hutumia mtandao kuwezesha ushirikiano wa watu binafsi kuzungumzia maswala ya maendeleo ya jamii.
20231101.sw_2694_64
https://sw.wikipedia.org/wiki/Elimu
Elimu
Elimu inaendelea kuwa jambo la kimataifa. Si vifaa vyake tu vinavyoendelea kuathiriwa na mazingira ya kimataifa yenye ukwasi bali pia mabadiliko ya wanafunzi katika viwango vyote yanayochangia kuendesha jukumu hili muhimu. Kwa mfano kule Uropa, programu ya Socratis Erusmus imechechemua mabadilishano kati ya vyuo vikuu vya Uropa. Vile vile, Shirika la Soros hutoa fursa nyingi kwa wanafunzi kutoka Asia ya kati na Uropa mashariki. Wasomi wengi hudai kwamba ingawa mfumo fulani unaweza kuzingatiwa kuwa bora au mbaya kuliko mwingine, kuzoea aina tofauti ya elimu mara nyingi huonwa kuwa elementi muhimu ya kuzoea masomo ya kimataifa.
20231101.sw_2694_65
https://sw.wikipedia.org/wiki/Elimu
Elimu
Elimu katika dini ya Uislamu ni muhimu kwa wake na waume, haswa kwa watoto wadogo. Kinyume na dhana ya kawaida, kutafuta aina zote za maarifa, yawe ya kitaaluma, ya kidini au ya kidunia yanaruhusiwa kwa watu wa umri wowote. Hata hivyo, masomo ya umri mdogo huonwa kuipa akili fursa ya kumakinika bila kuathiriwa na shida na majukumu ya maisha ya utu uzima.
20231101.sw_2695_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/Hekaya%20za%20Abunuwasi
Hekaya za Abunuwasi
Hekaya za Abunuwasi ni mkusanyo wa hadithi fupi zinazosimulia habari za Abunuwas. Hadithi hizi hazina uhusiano halisi na Abu Nuwas, mshairi Mwarabu aliyeishi Baghdad mnamo mwaka 800 BK.