_id
stringlengths 15
22
| url
stringlengths 31
150
| title
stringlengths 1
86
| text
stringlengths 100
23.8k
|
---|---|---|---|
20231101.sw_2695_1
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Hekaya%20za%20Abunuwasi
|
Hekaya za Abunuwasi
|
Abunuwasi wa hekaya ni mjanja anayeshindana mara kwa mara na tabia mbaya za watu wenzake kama vile walafi, matajiri wasio na huruma, akiwadanganya kwa kutumia mbinu zao wenyewe. Mara nyingi hadithi zilezile zinasimuliwa pia katika nchi nyingine za Waislamu kwa majina kama hekaya za Nasreddin, Guha au "hekaya za Mullah".
|
20231101.sw_2695_2
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Hekaya%20za%20Abunuwasi
|
Hekaya za Abunuwasi
|
Mchoraji Mtanzania Godfrey Mwampembwa (anayejulikana kwa jina la Gado) alitunga kitabu cha vibonzo kwa jina la Abunuwasi kinachosimulia tatu za hekaya zake. Kitabu hiki kilitolewa na Sasa Sema Publications mwaka 1996.
|
20231101.sw_2695_3
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Hekaya%20za%20Abunuwasi
|
Hekaya za Abunuwasi
|
Kuna wakati, Abunuwasi aliamua kuwa mfuga mbuzi. Alinunua mbuzi wa kufuga huku akiwa na lengo la kujiongezea kipato chake pindi mbuzi huyo atapoanza kuzaa, ili awafuge ndama wawe wengi na kumuwezesha kuwa tajiri kuliko wote waliokuwepo katika mji ule..
|
20231101.sw_2695_4
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Hekaya%20za%20Abunuwasi
|
Hekaya za Abunuwasi
|
Siku moja Abunuwasi akipokuwa anampeleka mbuzi wake malishoni, alikuta kiatu kimoja kizuri sana katikati ya njia. Alisimama na kukiangalia. Kiatu kilipendeza machoni mwake ila akasema "kiatu hiki ni kizuri lakini mbona kipo kimoja tu?" Alitafuta kiatu cha pili pembezoni mwa njia ila hakukiona. Alipoona hawezi kuvaa kiatu kimoja, aliamua kukiacha palepale. .
|
20231101.sw_2695_5
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Hekaya%20za%20Abunuwasi
|
Hekaya za Abunuwasi
|
Abunuasi akachukuwa mbuzi wake na mbele kidogo akaona kile kiatu cha mguu wa pili. Abunuwas alishangaa na akaona bora angelikichukua kile cha mwanzo kwa sababu cha pili kimepatikana.
|
20231101.sw_2695_6
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Hekaya%20za%20Abunuwasi
|
Hekaya za Abunuwasi
|
Aliporudi pale mwanzo kukitafuta alichokiacha awali lakini hakukikuta tena, alijaribu kukitafuta lakini hakukiona. Basi akadhani kuna mtu amekiokota. Akarudi haraka alipomfunga mbuzi wake nako pia hakumkuta mbuzi wala kile kiatu kimoja. Mwisho akawa amemkosa mbuzi na viatu, Ndoto zote za Abunuwasi kupata utajiri zikaruka na akabaki na umasikini wake kwa sababu ya tamaa yake.
|
20231101.sw_2697_0
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Bunge%20la%20Umoja%20wa%20Afrika
|
Bunge la Umoja wa Afrika
|
Wabunge wake 265 hawapigwi kura na raia wa nchi wanachama bali wanateuliwa na bunge za nchi wanachama. Kwa sasa kazi ya bunge ni kutoa ushauri tu kwani haina mamlaka ya kutunga sheria.
|
20231101.sw_2697_1
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Bunge%20la%20Umoja%20wa%20Afrika
|
Bunge la Umoja wa Afrika
|
Makao makuu ya bunge yapo mjini Midrand (Afrika Kusini, sasa kwa muda katika jengo la Gallagher Estate katikati ya Johannesburg na Pretoria. Afrika Kusini inalipa gharama za makao na za ofisi ya bunge.
|
20231101.sw_2697_2
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Bunge%20la%20Umoja%20wa%20Afrika
|
Bunge la Umoja wa Afrika
|
Mkutano wa kwanza ulifanyika Machi 2004. Mwenyekiti wa kwanza wa bunge hilo alikuwa Gertrude Mongella kutoka Tanzania.
|
20231101.sw_2700_0
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Christopher%20Mtikila
|
Christopher Mtikila
|
Christopher Mtikila (1950-2015) alikuwa mchungaji wa Kikristo na mwanasiasa nchini Tanzania kama kiongozi wa chama cha upinzani cha Democratic Party (DP).
|
20231101.sw_2700_1
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Christopher%20Mtikila
|
Christopher Mtikila
|
Mwanzoni mwa miaka ya 1990, mchungaji Mtikila alijipatia umaarufu mkubwa katika siasa za Tanzania kutokana na uwezo wake mkubwa wa kuongea, upinzani wake dhidi ya muundo wa muungano kati ya Tanganyika na Zanzibar, madai yake kuhusu hujuma za uchumi zinazofanywa na Wahindi (ambao aliwaita Magabacholi), na kesi mbalimbali za kikatiba alizokuwa akizifungua katika mahakama za Tanzania.
|
20231101.sw_2700_2
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Christopher%20Mtikila
|
Christopher Mtikila
|
Kesi za kikatiba ambazo aliwahi kuzifungua ni pamoja na kesi ya kutaka wagombea binafsi kuruhusiwa katika uchaguzi Tanzania, wananchi wa Tanzania Bara kuruhusiwa kwenda Zanzibar bila pasipoti, na vyama vya siasa kuruhusiwa kufanya mikutano bila kuomba kibali toka kwa Mkuu wa Wilaya na polisi.
|
20231101.sw_2700_3
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Christopher%20Mtikila
|
Christopher Mtikila
|
Mtikila alifungwa kwa mwaka mmoja mnamo 1999 baada ya kupatikana na hatia ya kutoa maneno ya kashfa dhidi ya aliyekuwa katibu mkuu wa CCM, marehemu Horace Kolimba.
|
20231101.sw_2700_4
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Christopher%20Mtikila
|
Christopher Mtikila
|
Mwaka 2004 alihukumiwa kifungo kilichosimamishwa cha miezi sita kwa kutoa maneno ya kashfa dhidi ya mkuu wa polisi wa wilaya ya Ilala.
|
20231101.sw_2700_5
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Christopher%20Mtikila
|
Christopher Mtikila
|
Kwa muda mrefu chama chake cha DP hakikuweza kupata usajili wa kudumu kutokana na kukataa kwake kutambua Zanzibar. Alikuwa akisisitiza kuwa chama chake ni cha Tanganyika na si Tanzania. Hata hivyo Mtikila alibadili msimamo wake katika miaka iliyofuata kwa kukubali kutafuta wanachama toka Zanzibar (kama sheria ya uchaguzi inavyotaka) na hivyo chama chake kuweza kupata usajili wa kudumu.
|
20231101.sw_2700_6
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Christopher%20Mtikila
|
Christopher Mtikila
|
Mtikila alikuwa ni kati ya wagombea 10 wa nafasi ya urais katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2005. Katika uchaguzi huo alipata kura asilimia 0.27.
|
20231101.sw_2700_7
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Christopher%20Mtikila
|
Christopher Mtikila
|
Pamoja na shughuli za siasa, Mchungaji Mtikila alikuwa mwanzilishi na mkuu wa kanisa la Kipentekoste la Full Salvation Church.
|
20231101.sw_2700_8
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Christopher%20Mtikila
|
Christopher Mtikila
|
Mchungaji Mtikila alijihusisha pia na harakati za haki za binadamu kwa kupitia kitengo cha haki za binadamu cha kanisa hilo kiitwacho Liberty Desk.
|
20231101.sw_2700_9
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Christopher%20Mtikila
|
Christopher Mtikila
|
Mchungaji Mtikali amefariki alfajiri ya Jumapili 4 Oktoba 2015 kwa ajali ya gari kwenye kijiji cha Msolwa karibu na Chalinze.
|
20231101.sw_2704_0
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Barafu
|
Barafu
|
Barafu inaeleweka ni maji ya mgando. Hata kiowevu kingine kinaweza kushika baridi na kuganda kuwa barafu, ila kama maziwa yanaganda tunayaita "barafu ya maziwa". Pia hewa ya kaboni inaweza kugandishwa na kuwa barafu kavu.
|
20231101.sw_2704_1
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Barafu
|
Barafu
|
Inapatikana katika hali na ukubwa mbalimbali. Kama ni ndogo ni fuweli kadhaa tu; kubwa zaidi ni vipande vya mvua ya mawe. Barafu inaweza kuwa ganda kubwa kama bapa nene sana kama lile linalofunika bara la Antaktiki.
|
20231101.sw_2704_2
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Barafu
|
Barafu
|
Barafu ina kazi muhimu katika hali ya hewa duniani. Hasa maganda ya barafu kwenye ncha za dunia yanatunza sehemu kubwa ya maji matamu yaliyopo.
|
20231101.sw_2704_3
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Barafu
|
Barafu
|
Maji yakiganda hupanuka. Hivyo barafu yake inahitaji nafasi kubwa kuliko maji ya kiowevu kiasi cha 9%. Mfano wake ni: chupa ya soda katika friji inaweza kupasuka. Sababu yake ni: maji ndani ya soda inahitaji nafasi kubwa kuliko soda ya majimaji, hivyo kupasua chupa yenyewe.
|
20231101.sw_2704_4
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Barafu
|
Barafu
|
Kutokana na hali hiyohiyo, barafu ni nyepesi kuliko maji, hivyo hubaki juu ya maji. Vipande vikubwa vya barafu vikiyeyuka na barafu ya Antaktiki au Aktiki vinaelea baharini kama siwa barafu vinaweza kuharibu hata meli kubwa, jinsi ilivyoonyesha mfano wa meli Titanic.
|
20231101.sw_2711_0
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Botswana
|
Botswana
|
Botswana (yaani: Utswana) ni nchi huru iliyoko Kusini mwa Afrika. Jina rasmi ni Jamhuri ya Botswana.
|
20231101.sw_2711_1
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Botswana
|
Botswana
|
Botswana haina pwani kwenye bahari yoyote. Imepakana na Zambia, Zimbabwe, Afrika Kusini na Namibia. Mpaka baina ya taifa la Botswana na Zambia ni meta 700 tu na ndio mfupi kuliko mipaka yote ulimwenguni.
|
20231101.sw_2711_2
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Botswana
|
Botswana
|
Moja ya maeneo muhimu nchini Botswana ni delta ya mto Okavango. Ndiyo delta kubwa kabisa duniani, maana yake mdomo wa mto si baharini bali kwenye nchi kavu, maji yakiishia jangwani.
|
20231101.sw_2711_3
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Botswana
|
Botswana
|
Botswana imekuwa na mfumo wa demokrasia kwa miaka mingi, ikiwa na viongozi ambao huchaguliwa kwa kura ya wananchi wote.
|
20231101.sw_2711_4
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Botswana
|
Botswana
|
Watu wa Botswana hujiita Batswana kutokana na jina la kabila kubwa kabisa nchini (79%). Kuna wakazi takriban milioni 2.3. Kwa sababu nchi ni kubwa msongamano wa watu kwa kilometa za mraba ni 3.7 pekee. Idadi hiyo ndogo imetokana na sehemu kubwa ya nchi hiyo kuwa jangwa.
|
20231101.sw_2711_5
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Botswana
|
Botswana
|
Upande wa dini, wakazi wengi (73%) ni Wakristo, wakiwemo Waprotestanti (66%) na Wakatoliki (7%). Wafuasi wa dini asilia ya Kiafrika ni 6%. Asilimia 20 haina dini yoyote.
|
20231101.sw_2711_6
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Botswana
|
Botswana
|
Uchumi wa Botswana umekuwa imara kwa miaka mingi na hali ya maisha imeendelea kuwa bora kila mwaka tangu uhuru.
|
20231101.sw_2711_7
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Botswana
|
Botswana
|
Utajiri wa nchi unatokana hasa na migodi ya almasi, pamoja na machimbo ya shaba na minerali kama vile chumvi.
|
20231101.sw_2713_0
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Bendera
|
Bendera
|
Bendera ni kitambaa chenye rangi mbalimbali. Mara nyingi ina umbo la pembenne, pia la mraba au pembetatu. Ina kazi ya kitambulisho au alama ya mawasiliano.
|
20231101.sw_2713_1
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Bendera
|
Bendera
|
Nchi inweka bendera yake kwa kuonyesha: hapa eneo letu linaanza; au: leo tunaonyesha bendera kwa sababu ni sikukuu ya taifa. Serikali zinaweza kuweka bendera mbele ya majengo rasmi ikonyesha: hapa ndipo jengo rasmi kama kituo cha polisi, shule, nyumba ya wizara na kadhalika.
|
20231101.sw_2713_2
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Bendera
|
Bendera
|
Klabu ya soka inaweza kuwa na bendera. Bendera ya klabu inaonyeshwa na wafuasi wake uwanjani kwa kusidi la kuwaonyesha wachezaji kuwa wenzao wako.
|
20231101.sw_2713_3
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Bendera
|
Bendera
|
Bendera zilikuwa kati ya alama muhimu vitani. Vikosi mbalimbali vilikuwa na bendera zao zilizowasaidia wanajeshi kutambua jeshi lao liko sehemu gani kama walitengwa na wenzao wengine katika mapigano ya watu maelfu.
|
20231101.sw_2713_4
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Bendera
|
Bendera
|
Matumizi ya kale kabisa ya mabendera ni kuwasilisha habari. Matumizi haya yanahitaji uelewano kuhusu maana ya rangi zinazoonyeshwa. Rangi mbalimbali pamoja zinaweza kumaanisha maneno, herufi au amri. Bendera zenye rangi hizi zinaonekana kwa umbali wa wastani unaotegemea ukubwa wa bendera. Utaratibu huu uliwahi kutumika kati ya meli baharini tangu karne nyingi.
|
20231101.sw_2713_5
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Bendera
|
Bendera
|
Hadi leo meli zinatumia mawasiliano ya bendera hata siku hizi za simu na redio. Lakini bendera zinasaidia kama mitambo imeharibika au kama meli mbili zinakutana zisizojua marudio ya redio ya meli nyingine.
|
20231101.sw_2713_6
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Bendera
|
Bendera
|
Matumizi haya ni kawaida pia katika michezo fulani, kwa mfano mshika bendera kwenye soka au alama ya mwanzo mbioni.
|
20231101.sw_2714_0
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Lesotho
|
Lesotho
|
Ufalme wa Lesotho, au Lesotho, ni nchi ndogo inayozungukwa na Afrika Kusini pande zote. Haina pwani kwenye bahari yoyote.
|
20231101.sw_2714_1
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Lesotho
|
Lesotho
|
Jina Lesotho lamaanisha eneo la Basotho (wakazi 99.7%), watu ambao wanaongea lugha ya Kisotho, ambayo ni lugha rasmi pamoja na Kiingereza. Wakati wa ukoloni ilijulikana kama Basutoland.
|
20231101.sw_2714_2
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Lesotho
|
Lesotho
|
Ukweli wa kijiografia ambao wajulikana zaidi kuhusu Lesotho ni kwamba ni nchi inayozungukwa na Afrika ya Kusini, na ni nchi huru pekee duniani ambayo yote iko juu ya mita 1,000 juu ya usawa wa bahari (UB) (ft 3,281). Eneo la chini zaidi liko mita 1,400 (futi 4,593), na zaidi ya asilimia 80 za nchi ziko juu ya mita 1,800 (futi 5,906).
|
20231101.sw_2714_3
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Lesotho
|
Lesotho
|
Lesotho ya sasa ilianza kupatikana mwaka 1822 chini ya chifu Moshoeshoe I aliyeungana na makabila mengine dhidi ya Shaka Zulu (1818-1828).
|
20231101.sw_2714_4
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Lesotho
|
Lesotho
|
Wamisionari walioalikwa na Mfalme Moshoeshoe I walianza kuandika na kuchapa kwa lugha ya Kisotho kati ya miaka 1837 na 1855.
|
20231101.sw_2714_5
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Lesotho
|
Lesotho
|
Mwaka 1867 nchi ikawa chini ya malkia wa Uingereza kwa jina la Basutoland lakini mwaka 1869, Waingereza waliwaachia Makaburu nusu ya eneo la Basutoland.
|
20231101.sw_2714_6
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Lesotho
|
Lesotho
|
Kwa usimamizi wa serikali, Lesotho imegawiwa katika wilaya 10, kila moja ikiongozwa na Karani wa wilaya.
|
20231101.sw_2714_7
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Lesotho
|
Lesotho
|
Wakazi kwa asilimia 90 ni Wakristo, wakigawanyika karibu sawa kati ya Wakatoliki na Waprotestanti wa madhehebu mbalimbali.
|
20231101.sw_2714_8
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Lesotho
|
Lesotho
|
US State Department - Lesotho (hii makala ya husu ustadi wa Lesotho na idara ya mabo ya kigeni ya Marekani)
|
20231101.sw_2719_0
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Shirikisho%20la%20Mataifa
|
Shirikisho la Mataifa
|
Shirikisho la Mataifa (kwa Kiingereza: League of Nations) lilikuwa umoja wa madola 63 ya dunia kati ya 1920 na 1946 BK.
|
20231101.sw_2719_1
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Shirikisho%20la%20Mataifa
|
Shirikisho la Mataifa
|
Umoja huo ulianzishwa na mataifa washindi wa Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia. Katika miaka 1920-1930 mataifa mengine yalijiunga nao.
|
20231101.sw_2719_2
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Shirikisho%20la%20Mataifa
|
Shirikisho la Mataifa
|
Wazo la kuwa na shirikisho la mataifa lilitolewa mara ya kwanza na mwanafalsafa Mjerumani Immanuel Kant mnamo mwaka 1795. Wazo la Kant lilirudiwa na wanafalsafa mbalimbali. Wakati wa vita kuu ya kwanza rais wa Marekani Woodrow Wilson alipendekeza hatua za kuanzisha shirikisho hili kwa kusudi la kuzuia vita kwa wakati ujao baada ya mwisho wa vita ile.
|
20231101.sw_2719_3
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Shirikisho%20la%20Mataifa
|
Shirikisho la Mataifa
|
Katiba ya shirikisho la mataifa ilikuwa sehemu ya mkataba wa Versailles mwaka 1919. Nchi washindi au mataifa ya ushirikiano zilijiunga na umoja huo mpya. Baada ya kukubaliwa na nchi za kutosha shirikisho lilianza rasmi tarehe 10 Januari 1920.
|
20231101.sw_2719_4
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Shirikisho%20la%20Mataifa
|
Shirikisho la Mataifa
|
fitina zote kati ya nchi zitasuluhishwa kwa njia ya amani kwa azimio ya kamati au mahakama ya kimataifa
|
20231101.sw_2719_5
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Shirikisho%20la%20Mataifa
|
Shirikisho la Mataifa
|
nchi wanachama zote zitaungana dhidi ya nchi yoyote itakayoanzisha vita mpya au kukataa azimio la mahakama ya kimataifa
|
20231101.sw_2719_6
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Shirikisho%20la%20Mataifa
|
Shirikisho la Mataifa
|
kamati kuu au halmashauri ya nchi wanachama nne (baadaye sita)na nafasi nne (baadaye 9) za nchi zinazobadilishana kwa zamu
|
20231101.sw_2719_7
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Shirikisho%20la%20Mataifa
|
Shirikisho la Mataifa
|
Mkataba wa Versailles ulianzisha aina mpya ya maeneo yaliyowahi kuwa ama koloni au majimbo ya nchi zilizoshindwa katika vita. Koloni zote za Ujerumani pamoja na sehemu kubwa ya majimbo ya Milki ya Osmani ya awali ziliwekwa chini ya mamlaka ya Shirikisho la Mataifa na kukabidhiwa kwa nchi washindi wa vita. Zilipewa hali ya pekee kama maeneo ya kudhaminiwa (League of Nations mandate territories). Tofauti na koloni za kawaida nchi wadhamini hazikupewa mamlaka yote jinsi iliyokuwa katika koloni zao za kawaida bali zilipokea maeneo ya kudhaminiwa chini ya masharti fulani pamoja na kulinda haki kadhaa za wenyeji na kuandaa nchi hizi kwa uhuru. Hapo mwanzoni tofauti kati ya koloni na eneo la kudhaminiwa haikuwa kubwa lakini baadaye masharti ya udhamini yalikuwa muhimu. Kwa mfano hali ya Tanganyika kuwa eneo ka kudhaminiwa ilisababisha Uingereza kutokubali walowezi wengi kuja hapa. Vivyo hivyo hali ya Afrika ya Kusini Magharibi kuwa eneo la kudhaminiwa ilizuia sehemu hii kuwa jimbo la Afrika Kusini na kuwa msingi kwa uhuru wake kama nchi ya Namibia.
|
20231101.sw_2719_8
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Shirikisho%20la%20Mataifa
|
Shirikisho la Mataifa
|
Shirikisho lilikuwa awali umoja wa mataifa washindi wa vita. Baadaye hata nchi zisizoshiriki katika vita na pia nchi zilizoshindwa kama Ujerumani zilipokelewa kama wanachama. Idadi ya wanachama ilipanda hadi kufikia 63.
|
20231101.sw_2719_9
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Shirikisho%20la%20Mataifa
|
Shirikisho la Mataifa
|
Mapatano ya kimataifa kuhusu wanawake kufanyiwa biashara ya umalaya, biashara ya madawa ya kulevya na kitambulisho cha wakimbizi
|
20231101.sw_2719_10
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Shirikisho%20la%20Mataifa
|
Shirikisho la Mataifa
|
Shirikisho la mataifa liliunda pia utaratibu wa utawala wa maeneo yaliyokuwa chini ya Uturuki na Ujerumani hadi 1919.
|
20231101.sw_2719_11
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Shirikisho%20la%20Mataifa
|
Shirikisho la Mataifa
|
Katika Afrika shirikisho liliunda utaratibu mpya kwa ajili ya koloni za Ujerumani yaani Tanganyika, Rwanda, Burundi, Togo, Kamerun na Namibia.
|
20231101.sw_2719_12
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Shirikisho%20la%20Mataifa
|
Shirikisho la Mataifa
|
Ujerumani haukubaliwa kuwa nazo tena kwa sababu ya kuwatendea wenyeji Waafrika vibaya. Hata kama sababu hiyo ilikuwa tamko la washindi wa vita waliotaka kujigawia wenyewe koloni hizi ilhali wenyewe waliwahi kuwatendea watu vibaya katika koloni zao msingi muhimu uliwekwa uliozaa matunda baadaye: yaani hata serikali ya kikoloni inatakiwa kuheshimu haki za binadamu.
|
20231101.sw_2719_13
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Shirikisho%20la%20Mataifa
|
Shirikisho la Mataifa
|
Halafu koloni za Ujerumani hazikukabidhiwa tu kwa Uingereza (Tanganyika, sehemu za Kamerun na Togo), Ufaransa (sehemu kubwa za Kamerun na Togo), Ubelgiji (Rwanda, Burundi) na Afrika Kusini (Namibia) hivi lakini kama maeneo ya kukabidhiwa chini ya uangalizi wa Shirikisho la Mataifa. Utaratibu huu ulikuwa muhimu baadaye wakati wa uhuru. Namibia ilikuwa sehemu ya Afrika Kusini chini ya sheria za nchi ile lakini jumuiya ya kimataifa haikukubali kwa sababu Namibia ilikuwa kati ya maeneo ya kukabidhiwa - mwishoni Afrika Kusini iliiacha Namibia iwe huru mwaka 1990 miaka 44 baada ya mwisho wa shirikisho lenyewe.
|
20231101.sw_2719_14
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Shirikisho%20la%20Mataifa
|
Shirikisho la Mataifa
|
Tatizo kubwa tangu mwanzo ilikuwa ya kwamba Marekani haukuthebitisha unachama wake. Rais Wilson aliyeandaa kuundwa kwa shirikisho alikuwa amekasirisha wabunge wake nyumbani hivyo Senati ya Marekani iliendelea kukataa uanachama ya Marekani.
|
20231101.sw_2719_15
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Shirikisho%20la%20Mataifa
|
Shirikisho la Mataifa
|
Matatizo mengine yaliyosababisha kushindwa kwa shirikisho la mataifa yalitokana hasa na udhaifu mkubwa wa kukosa jeshi lake. Tangu mwanzo shirikisho lilitegemea nguvu ya nchi wanachama kama nchi ilivunja mapatano na kukataa kuitikia maazimio ya shirikisho.
|
20231101.sw_2719_16
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Shirikisho%20la%20Mataifa
|
Shirikisho la Mataifa
|
Kuanzia mnamo mwaka 1930 mataifa wanachama makubwa yalianza kuvunja vibaya sheria za shirikisho lakini hatua kali hazikuchukuliwa dhidi yao. Shirikisho lilishindwa kuzuia vita na mashambulio dhidi ya nchi wanachama wake. Kati ya matukio muhimu yaliyoharibu sifa za shirikisho ni:
|
20231101.sw_2719_17
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Shirikisho%20la%20Mataifa
|
Shirikisho la Mataifa
|
Nchi mbalimbali zilitoka katika Shirikisho la Mataifa baada ya kupingwa mkutanoni kama vile Italia, Japan na Ujerumani.
|
20231101.sw_2719_18
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Shirikisho%20la%20Mataifa
|
Shirikisho la Mataifa
|
Azimio la mwisho lenye maana kidogo yalikuwa kufukuza Urusi katika shirikisha baada ya uvamizi wake katika Finland mwaka 1939.
|
20231101.sw_2719_19
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Shirikisho%20la%20Mataifa
|
Shirikisho la Mataifa
|
Septemba 1939 Ujerumani ilivamia Poland. Baada ya siku chache ilionekana ya kwamba vita kuu ya pili imeanza - Shirikisho la Mataifa lilishindwa katika dhumuni lake la kuzuia marudio ya Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia.
|
20231101.sw_2719_20
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Shirikisho%20la%20Mataifa
|
Shirikisho la Mataifa
|
Washindi wa vita kuu ya pili waliamua kuanzisha chombo kipya. Umoja wa Mataifa uliundwa 1945 ukachukua nafasi yake. Vitengo kadhaa za shirikisho viliendela vikihamia kwa UM kwa mfano Shirika ya Kazi ya Kimataifa (ILO).
|
20231101.sw_2723_0
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Diego%20Garcia
|
Diego Garcia
|
Diego Garcia ni atolli ya Kiingereza katika Bahari Hindi, kati ya Tanzania na Indonesia. Ni sehemu ya funguvisiwa la Chagos na leo kisiwa pekee chenye wakazi ambao ni wanajeshi wa Marekani. Ni kituo kikubwa cha kijeshi cha Marekani katika Bahari Hindi.
|
20231101.sw_2723_1
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Diego%20Garcia
|
Diego Garcia
|
Kati ya miaka 1850 na 1965 kisiwa kilikuwa sehemu ya koloni la Morisi. Mwaka 1965 kilitengwa na Morisi pamoja na funguvisiwa lote. Mwaka 1971 Uingereza ilikodisha Diego Gracia kwa jeshi la Marekani ambao walitaka kuwa na kituo cha kijeshi kwenye Bahari Hindi katika mashindano yao na Umoja wa Kisovyeti.
|
20231101.sw_2723_2
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Diego%20Garcia
|
Diego Garcia
|
Katika miaka miwili iliyofuata wenyeji wote wa funguvisiwa waliondolewa visiwani, wakahamishiwa na watoto wao huko Mauritius, Shelisheli na Uingereza. Wengi wao wanapigania haki ya kurudi. Mahakama ya Uingereza iliwaruhusu mwaka 2000 warudi tena lakini serikali imekataa mwaka 2004.
|
20231101.sw_2723_3
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Diego%20Garcia
|
Diego Garcia
|
Diego Garcia ilikuwa kituo muhimu katika vita vya Marekani huko Afghanistan na Irak. Ndege za kijeshi za aina B-52 zinatoka hapa pamoja na ndege za kubeba petroli.
|
20231101.sw_2723_4
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Diego%20Garcia
|
Diego Garcia
|
The Chagos Conservation Trust – A non-political charity whose aims are to promote conservation, scientific and historical research, and to advance education concerning the archipelago.
|
20231101.sw_2723_5
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Diego%20Garcia
|
Diego Garcia
|
Christian Nauvel, "A Return from Exile in Sight? The Chagossians and their Struggle" (2006) 5 Northwestern Journal of International Human Rights 96–126 (retrieved 9 May 2011).
|
20231101.sw_2727_0
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ol%20Doinyo%20Lengai
|
Ol Doinyo Lengai
|
Ol Doinyo Lengai (maana kwa Kimaasai ni "Mlima wa Mungu") ni mlima wenye asili ya volkeno katika Tanzania ya Kaskazini. Iko takriban km 120 kaskazini-magharibi kwa Arusha na km 25 kusini kwa Ziwa Natron.
|
20231101.sw_2727_1
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ol%20Doinyo%20Lengai
|
Ol Doinyo Lengai
|
Ni volkeno ya pekee duniani kutokana na aina ya lava yake inayotoka hali ya kiowevu (majimaji) lakini si moto sana (mnamo 500° - 600 °C).
|
20231101.sw_2727_2
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ol%20Doinyo%20Lengai
|
Ol Doinyo Lengai
|
Ol Doinyo Lengai ililipuka tena kuanzia Machi 2006. Katika mwaka 2007 mlima umesababisha mitetemeko ya ardhi ya mara kwa mara kuanzia tarehe 12 Julai. Tetemeko la tarehe 18 Julai lilisikika hadi Nairobi.
|
20231101.sw_2727_3
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ol%20Doinyo%20Lengai
|
Ol Doinyo Lengai
|
Michael Greshko: 'Mountain of God' Volcano Preparing to Erupt, tovuti ya National geographic, 13 Julai 2017, iliangaliwa Julai 2017
|
20231101.sw_2729_0
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/M
|
M
|
M ni herufi ya 13 katika alfabeti ya Kilatini ambayo ni pia mwandiko wa Kiswahili cha kisasa. Asili yake ni Mi ya alfabeti ya Kigiriki.
|
20231101.sw_2729_1
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/M
|
M
|
Katika astronomia majina ya nyota na magimba mengine ya angani hutajwa kwa M pamoja na namba ya Orodha ya Messier
|
20231101.sw_2729_2
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/M
|
M
|
Asili ya herufi M ni katika miandiko iliyotangulia alfabeti ya Kilatini. Waroma walipokea mwandiko kutoka alfabeti ya Kigiriki kupitia alfabeti za Kiitalia za awali kama Kietruski. Wagiriki waliipokea kutoka Wafinisia.
|
20231101.sw_2729_3
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/M
|
M
|
Wafinisia walikuwa na alama ya "Mem" iliyokuwa kiasili picha iliyorahisishwa ya maji wakitumia alama tu kwa sauti ya "m" na kuiita kwa neno lao kwa maji "mem". Kwa kurahisisha kazi ya kuandika waliongeza mstari mrefu upande walipoanza kuandika.
|
20231101.sw_2729_4
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/M
|
M
|
Wagiriki walichukua alama hiyo na kuiita "Mi" bila kujali maana asilia ya "maji", ilikuwa sauti tu ya "m". Waligeuza alama kulingana na mwendo wao wa kuandika kuanzia upande wa kushoto na kufikia umbo lililokaa hivyo.
|
20231101.sw_2731_0
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Herufi%20za%20Kiarabu
|
Herufi za Kiarabu
|
Herufi za Kiarabu ni maandishi maalumu ya lugha ya Kiarabu. Nje ya Kiarabu lugha mbalimbali zinaandikwa kwa herufi za Kiarabu, hasa lugha za nchi zenye Waislamu wengi, ingawa herufi hizo zilibuniwa kabla ya dini hiyo kuenea. Kati ya lugha hizo kuna Kiajemi, Kikurdi, Kimalay na Urdu. Pengine katika lugha hizo herufi kadhaa zinaongezwa au kupunguzwa, kulingana na lugha ilivyo.
|
20231101.sw_2731_1
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Herufi%20za%20Kiarabu
|
Herufi za Kiarabu
|
Kuna herufi 28 za Kiarabu zinazoandikwa kutoka kulia kwenda kushoto. Herufi zote isipokuwa sita zinaunganishwa wakati wa kuandika. Kutokana na tabia hiyo kila herufi inaweza kuonekana kwa maumbo tofautitofauti kiasi kutegemeana na mahali pake mwanzoni, katikati au mwishoni mwa neno.
|
20231101.sw_2731_2
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Herufi%20za%20Kiarabu
|
Herufi za Kiarabu
|
Kwa kawaida maandishi ya Kiarabu ni ya konsonanti tu bila vokali. Vokali zikiandikwa zinaonekana kama mstari au nukta chini au juu ya herufi zinazoanzisha silabi.
|
20231101.sw_2731_3
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Herufi%20za%20Kiarabu
|
Herufi za Kiarabu
|
Named Entity Recognition – for a discussion of inconsistencies and variations of Arabic written text.
|
20231101.sw_2737_0
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Bagamoyo%20%28mji%29
|
Bagamoyo (mji)
|
Bagamoyo ni mji mwambaoni mwa Bahari Hindi katika Tanzania takriban km 75 kaskazini kwa Dar es Salaam na km 45 magharibi kwa kisiwa cha Unguja.
|
20231101.sw_2737_1
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Bagamoyo%20%28mji%29
|
Bagamoyo (mji)
|
Bagamoyo iko kati ya miji ya kale kabisa ya Waswahili katika Tanzania ya leo. Magofu ya Kaole (msikiti na makaburi ya karne ya 13 BK) yako karibu na Bagamoyo yakionyesha umuhimu wa utamaduni wa Kiislamu katika eneo hili. Lakini hakuna uhakika kuhusu historia ya Bagamoyo ya kale isipokuwa ya kwamba mnamo karne ya 18 mji haukuwa muhimu. Wakazi walio wengi wakati ule walikuwa wavuvi na wakulima, ila palikuwa na biashara kiasi cha samaki na chumvi.
|
20231101.sw_2737_2
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Bagamoyo%20%28mji%29
|
Bagamoyo (mji)
|
Jina la Bagamoyo huelezwa kutokana na maneno "bwaga" na "moyo". Elezo la kawaida linarejea biashara ya watumwa kwa kudai eti watumwa waliona bahari ambako watasafarishwa hadi Unguja na mbali zaidi, hiyvo walikatishwa tamaa na "kumwaga moyo". Hayo husimuliwa mara nyingi kwa watalii wanaotembelea mji na kuangalia majengo ya kale.
|
20231101.sw_2737_3
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Bagamoyo%20%28mji%29
|
Bagamoyo (mji)
|
Lakini asili hiyo inapingwa na wataalamu wanaoonyesha kuwa biashara ya watumwa haikuwa muhimu sana hapa na asili ya jina inapatikana zaidi kutoka kwa wapagazi waliofika hapa kwa wingi kutoka bara baada ya safari ngumu ya miezi kadhaa walipoweza kushusha mizigo yao (wengi walibeba hadi kilogramu 70), kupokea mishahara na kuwa na starehe. Kwa hiyo maana si bwaga moyo kama kukataa tamaa, bali bwaga moyo kama kuachana na matatizo na wasiwasi wa safari ya hatari.
|
20231101.sw_2737_4
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Bagamoyo%20%28mji%29
|
Bagamoyo (mji)
|
Afisa Mjerumani August Leue aliandika mnamo mwaka 1900 kwamba wapagazi waliimba njiani wimbo ufuatao: "Tunakwenda Bagamoyo, roho yangu furahi, tumelia barani kuwa mbali nawe, Bagamoyo, Bagamoyo" akieleza kwamba wapagazi na pia wakazi wengine wa Mrima waliona Bagamoyo kama mji wa furaha na starehe.
|
20231101.sw_2737_5
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Bagamoyo%20%28mji%29
|
Bagamoyo (mji)
|
Hasa kuhamia kwa makao ya Sultani wa Oman kuja Zanzibar kuliongeza umuhimu wa mwambao wa Mrima karibu na Unguja. Bandari Zote zilizotazama Unguja zilianza kukua na kupokea mizigo kutoka na kwenda Unguja na kati ya hizo Bagamoyo ilikuwa muhimu zaidi kwa sababu ilikuwa karibu zaidi na mji wa Zanzibar.
|
20231101.sw_2737_6
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Bagamoyo%20%28mji%29
|
Bagamoyo (mji)
|
Tangu Zanzibar kuwa mji mkuu wa Omani familia za Waarabu pamoja na mawakala wa kampuni za Wahindi walihamia Bagamoyo wakipanua biashara yake. Mji ukawa kituo muhimu zaidi kwenye pwani; biashara ya misafara mikubwa ya karne ya 19 kwenda barani hadi Kongo ilianza na kurudi hapa kushinda bandari nyingine za Mrima.
|
20231101.sw_2737_7
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Bagamoyo%20%28mji%29
|
Bagamoyo (mji)
|
Kufikia mwaka 1860 hivi Bagamoyo ilikadiriwa kuwa na wakazi wa kudumu 3,000 walioongezeka kuwa 20,000 mnamo mwisho wa karne ya 19. Pamoja na wapagazi wa misafara waliokaa miezi kadhaa mjini baada ya kufika kutoka bara na kusubiri hadi kurudi, mara nyingi wakiajiriwa kubeba tena mizigo ya safari mpya, idadi yao ilifikia watu 30,000-40,000, hivyo jumla ya wakazi iliweza kufikia 50,000 hadi 60.000 kwa muda.
|
20231101.sw_2737_8
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Bagamoyo%20%28mji%29
|
Bagamoyo (mji)
|
Bagamoyo iliendelea kuwa mji mkubwa katika koloni la Afrika ya Mashariki ya Kijerumani hata baada ya serikali ya kikoloni kuhamia Dar es Salaam hadi kujengwa kwa reli ya kati iliyohamisha sehemu kubwa ya biashara kule ambako reli hiyo ilianza.
|
20231101.sw_2737_9
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Bagamoyo%20%28mji%29
|
Bagamoyo (mji)
|
Wafanyabiashara wa Zanzibar walikusanya bidhaa zao huko Unguja wakavuka bahari na kuajiri wapagazi waliozibeba hadi Tabora na Ujiji kwenye Ziwa Tanganyika; kutoka kule biashara iliendelea katika maeneo ya Kongo. Wapagazi wakarudi miezi au miaka kadhaa baadaye wakileta hasa pembe za ndovu zilizokuwa na soko kubwa katika Ulaya na Marekani. Wapagazi wengi walikuwa watu wa maeneo ya magharibi walioitwa kwa jumla "Wanyamwezi".
|
20231101.sw_2737_10
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Bagamoyo%20%28mji%29
|
Bagamoyo (mji)
|
Bagamoyo imepata pia sifa ya kuwa moja ya bandari kuu za biashara ya watumwa kwenye pwani ya Afrika ya Mashariki katika karne ya 19. Serikali ya Tanzania ilitumia tabia hiyo kama sababu muhimu ya kupendekeza mji huo kama sehemu ya urithi wa Dunia kwenye orodha ya UNESCO. Hata hivyo, wataalamu wengi wa historia hawakubali, wakiona Bagamoyo haikuwa muhimu sana katika biashara ya watumwa ya Afrika ya Mashariki, ikilinganishwa na Kilwa na Pangani. Hakika watumwa kadhaa walisafirishwa kutoka hapa kwa jahazi au dhau hadi Unguja wakiuzwa huko sokoni. Ila kundi la jeshi la maji la Uingereza lililotumwa Afrika Mashariki kwa kusudi la kuzuia biashara ya watumwa halikuwahi kulenga Bagamoyo bali hasa Kilwa na bandari za upande wa kaskazini wa Bagamoyo.
|
20231101.sw_2737_11
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Bagamoyo%20%28mji%29
|
Bagamoyo (mji)
|
Mapadre wa Roho Mtakatifu walijenga kituo chao cha kwanza cha barani katika Afrika ya Mashariki huko Bagamoyo wakiona umuhimu wa mji huo kama mlango wa bara. Kwenye eneo la misheni yao walianzisha kijiji kwa watumwa walionunuliwa nao ili kupewa uhuru, watumwa watoro waliokuta hapa mahali salama au watumwa waliopelekwa hapa na jeshi la majini la Uingereza wakikamatwa baharini wakati wa kusimamisha jahazi ambamo walibebwa,
|
Subsets and Splits
No community queries yet
The top public SQL queries from the community will appear here once available.