_id
stringlengths 15
22
| url
stringlengths 31
150
| title
stringlengths 1
86
| text
stringlengths 100
23.8k
|
---|---|---|---|
20231101.sw_2759_2
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mohamed%20Abdelaziz
|
Mohamed Abdelaziz
|
Mohammed Abdelaziz kama kiongozi alikubali njia ya mazungumzo na diplomasia. Alihakikisha ya kwamba vita ya Polisario ilikuwa "vita" safi bila kutumia mbinu za ugaidi. Ana wapinzani wake wanaopendelea kurudi vitani dhidi ya Moroko. Amehakikisha
|
20231101.sw_2762_0
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Namibia
|
Namibia
|
Sehemu kubwa ya nchi ni kavu sana na jangwa za Namib na Kalahari zinafunika asilimia kubwa ya uso wa nchi.
|
20231101.sw_2762_1
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Namibia
|
Namibia
|
Jangwa la Namib liko upande wa magharibi likifuata pwani ya Atlantiki kuanzia Afrika Kusini hadi Angola. Upande wa mashariki kuna jangwa la Kalahari linalovuka mpaka wa Botswana.
|
20231101.sw_2762_2
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Namibia
|
Namibia
|
Katika karne ya 14 hivi BK walifika wahamiaji Wabantu wenye ujuzi wa kilimo na uhunzi walioshika utawala na hatimaye kuwa wengi kuliko wenyeji.
|
20231101.sw_2762_3
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Namibia
|
Namibia
|
Namibia katika mipaka ya sasa ilianzishwa katika karne ya 19 kama koloni la Ujerumani kwa jina la Afrika ya Kusini-Magharibi ya Kijerumani. Maeneo yake yaliunganishwa mara ya kwanza kwenye mwaka 1884.
|
20231101.sw_2762_4
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Namibia
|
Namibia
|
Wakati wa Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia ilivamiwa na Uingereza na Afrika Kusini. Pamoja na makoloni mengine ya Ujerumani iliwekwa chini ya mamlaka ya Shirikisho la Mataifa. Tangu mwaka 1919 ilikuwa eneo la kudhaminiwa kwa niaba ya Shirikisho la Mataifa chini ya serikali ya Afrika Kusini.
|
20231101.sw_2762_5
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Namibia
|
Namibia
|
Afrika ya Kusini-Magharibi (kwa Kiingereza South-West Africa) ilikuwa jina la eneo hilo kuanzia mwaka 1922 hadi uhuru wa nchi ya Namibia mwaka 1990.
|
20231101.sw_2762_6
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Namibia
|
Namibia
|
Baada ya Vita Kuu ya Pili ya Dunia, wakati wa kuvunjwa kwa Shirikisho la Mataifa mwaka 1946, Umoja wa Mataifa ulichukua jukumu la kuratibu maeneo ya kudhaminiwa.
|
20231101.sw_2762_7
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Namibia
|
Namibia
|
Afrika Kusini haikutambua badiliko hilo ikitangaza ya kwamba hali ya udhamini ilikuwa ya Afrika ya Kusini-Magharibi tangu kuvunjwa kwa Shirikisho la Mataifa.
|
20231101.sw_2762_8
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Namibia
|
Namibia
|
Mwaka 1949 bunge la Afrika Kusini lilitangaza sheria ya kufanya eneo kuwa jimbo la tano la Afrika Kusini na kueneza siasa ya apartheid (ubaguzi wa rangi) hadi hukoikijaribu kulitendea eneo hilo kama sehemu kamili ya Afrika Kusini. Hii haikukubaliwa na Umoja wa Mataifa na nchi nyingi za dunia.
|
20231101.sw_2762_9
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Namibia
|
Namibia
|
Baadaye mfumo wa bantustans sawa na Afrika Kusini ulianzishwa pia huko ambako maeneo makubwa yenye rutuba yalitengwa kwa ajili ya Wazungu ilhali Waafrika walitakiwa kuwa na maeneo kadhaa tu kama "homeland" walipokuwa na haki ya kukaa, lakini katika maeneo mengine waliruhusiwa kukaa kama wafanyakazi kwa muda tu. Mfumo huo haukutekelezwa kwa ukali, tofauti na Afrika Kusini yenyewe.
|
20231101.sw_2762_10
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Namibia
|
Namibia
|
Hii haikukubaliwa na Umoja wa Mataifa ulioendelea kudai ya kwamba Afrika Kusini ilipaswa kuandaa eneo kwa uhuru.
|
20231101.sw_2762_11
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Namibia
|
Namibia
|
Mwaka 1966 Mkutano Mkuu wa UM uliamua kuondoa mamlaka ya Afrika Kusini na kuweka eneo moja kwa moja chini ya Umoja wa Mataifa. Azimio hilO halikuweza kutekelezwa kwa sababu Afrika Kusini ilikataa.
|
20231101.sw_2762_12
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Namibia
|
Namibia
|
Mwaka 1971 Mahakama ya Kimataifa ya Haki ikaamua ya kwamba utawala wa Afrika Kusini si wa haki. Mwaka 1978 Umoja wa Mataifa uliamua ya kwamba Afrika ya Kusini-Magharibi unapaswa kupewa uhuru. Hapo serikali ya Afrika Kusini ikaanza kuchukua hatua za kuandaa uhuru wa eneo hili, lakini vita kati ya jeshi lake, SWAPO na wanajeshi wa Angola na Kuba iliendelea.
|
20231101.sw_2762_13
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Namibia
|
Namibia
|
Baada ya miaka ya vita vya kupigania uhuru, mchakato wa kimataifa wa kuelekea uhuru ulianza na kufikia mapatano ya kumpumzisha silaha mwaka 1988. Hatimaye mwaka 1990 nchi ilipata uhuru wake kwa jina la Namibia.
|
20231101.sw_2762_14
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Namibia
|
Namibia
|
Wakazi wengi ni wa makabila ya Wabantu, hasa Waovambo (49.5%). Pia wako wengi wa jamii ya Wakhoisan, ambao wametokana na wenyeji wa nchi. Asilimia 4 - 7 wana asili ya Ulaya, hasa Makaburu na Wajerumani, na asilimia 8 ni machotara.
|
20231101.sw_2762_15
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Namibia
|
Namibia
|
Upande wa lugha, Oshiwambo ni lugha ya kwanza ya karibu nusu ya wakazi, lakini Kiingereza ndicho lugha rasmi ingawa ni lugha ya kwanza ya 3% pekee za wakazi. (Angalia Orodha ya lugha za Namibia.)
|
20231101.sw_2762_16
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Namibia
|
Namibia
|
Kijerumani na Kiafrikaans zilikuwa lugha rasmi pamoja na Kiingereza hadi uhuru. Wakazi wengi hutumia Kiafrikaans kama lugha ya pili, na 10.4% kama lugha ya kwanza.
|
20231101.sw_2762_17
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Namibia
|
Namibia
|
Wakazi wenye asili ya Ulaya huongea kama lugha ya kwanza Kiafrikaans (60%), lakini pia Kijerumani (32%) na Kireno (4-5%), hasa wenye asili ya Angola.
|
20231101.sw_2762_18
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Namibia
|
Namibia
|
Upande wa dini, 87.9% za wakazi ni Wakristo (hasa Walutheri ambao ni 43.7%; Wakatoliki ni 22.8%, Waanglikana ni 17%). Waliobaki kwa kawaida wanafuata dini asilia za Kiafrika (10.2%).
|
20231101.sw_2764_0
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mauritania
|
Mauritania
|
Mauritania ni nchi ya Afrika kaskazini-magharibi. Upande wa magharibi kuna pwani ya bahari ya Atlantiki, upande wa kusini imepakana na Senegal, upande wa mashariki na Mali na Algeria, upande wa kaskazini na Sahara ya Magharibi inayotawaliwa na Moroko.
|
20231101.sw_2764_1
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mauritania
|
Mauritania
|
Jina limeteuliwa kutokana na Mauritania ya kale iliyokuwa ufalme wa Waberber kusini kwa Mediteranea katika eneo la Algeria na Moroko ya leo.
|
20231101.sw_2764_2
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mauritania
|
Mauritania
|
Mji mkuu ni Nouakchott. Mji wa pili na kitovu cha uchumi ni bandari ya Nouadhibou karibu na mpaka wa Sahara Magharibi.
|
20231101.sw_2764_3
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mauritania
|
Mauritania
|
Mnamo Machi 2007 wananchi walipata nafasi ya kumchagua rais mara ya kwanza katika historia ya nchi tangu uhuru. Sidi Ould Cheikh Abdallahi alishinda katika duru ya pili kwa 53% za kura zote akaapishwa tarehe 20 Aprili 2007.
|
20231101.sw_2764_4
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mauritania
|
Mauritania
|
Wakazi wengi (70%) ni Wamori, mchanganyiko wa Waarabu, Waberber na Waafrika waliotokana na watumwa kutoka kusini kwa Sahara. Asilimia 30 zilizobaki ni makabila ya Kiafrika yasiyoongea Kiarabu, ambacho ndicho lugha rasmi.
|
20231101.sw_2764_5
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mauritania
|
Mauritania
|
Upande wa dini, karibu wote ni Waislamu (hasa Wasuni). Uhuru wa dini unabanwa sana kwa nyingine zote.
|
20231101.sw_2764_6
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mauritania
|
Mauritania
|
Pamoja na hayo, hadi leo asilimia 4 za wakazi ni watumwa, ingawa mwaka 2007 ilifutwa haki ya kuwamiliki.
|
20231101.sw_2772_0
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mlima%20Kenya
|
Mlima Kenya
|
Mlima Kenya (Kikuyu: Kĩrĩnyaga; Kiembu: Kirenia; Kimaasai: Ol Donyo Keri; Kimeru: Kirimara) ndio mrefu zaidi nchini Kenya. Mlima huu una urefu wa mita 5,199. Mlima huu unatokana na volkeno zimwe ikikadiriwa ya kwamba mlipuko wake wa mwisho ulitokea mnamo miaka milioni 2.6 hadi 3.1 iliyopita.
|
20231101.sw_2772_1
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mlima%20Kenya
|
Mlima Kenya
|
Vilele vyake vya juu vinaitwa Batian (m 5,199), Nelion (m 5,188) na Lenana (m 4,985). Kuna barafuto nane mlimani lakini zinapungua kila mwaka kutokana na kupanda kwa halijoto duniani na kupungua kwa usimbishaji kwa sababu ya kukatwa kwa miti mingi.
|
20231101.sw_2772_2
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mlima%20Kenya
|
Mlima Kenya
|
Mlima Kenya ni volkeno rusu iliyoumbwa takriban miaka milioni 3 baada ya kuumbika wa Bonde la Ufa. Umekuwa na theluji kwa maelfu ya miaka. Theluji hiyo hufanya kuwe na mmomonyoko unaosababishwa na barafuto na kutengeneza mabonde. Barafuto zimepungua kutoka 18 hadi 10. Mlima huu ni chanzo muhimu cha maji kwa Kenya.
|
20231101.sw_2772_3
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mlima%20Kenya
|
Mlima Kenya
|
Habari kuhusu mlima zilifikishwa Ulaya mwaka 1849 na Ludwig Krapf, lakini jamii ya wanasayansi walibaki na wasiwasi kuhusu ripoti kuwa kulikuwa na theluji karibu na ikweta. Uwepo wa Mlima Kenya ulithibitishwa mwaka 1883 na 1887. Ulipandwa na timu iliyoongozwa na Halford John Mackinder, mwaka 1899. Leo Mlima Kenya hupandwa na watalii na wanaopenda kupanda milima na miamba.
|
20231101.sw_2772_4
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mlima%20Kenya
|
Mlima Kenya
|
Mfumo wa ekolojia wa Mlima Kenya una aina tofauti za mimea na wanyama. Mteremko hufunikwa na aina tofauti ya misitu. Spishi asilia ni kama vile mianzi, tai na pimbi. Kwa sababu hii, eneo la km2 715 linalozunguka mlima ni hifadhi ya taifa na liliorodheshwa na UNESCO kama urithi wa dunia mwaka 1997. Hifadhi hupokea wageni zaidi ya 15,000 kwa mwaka.
|
20231101.sw_2772_5
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mlima%20Kenya
|
Mlima Kenya
|
Neno Kenya linaweza kuwa lilitokana na majina ambayo makabila wenyeji waliupatia Mlima Kenya. Wakikuyu; Kirinyaga, Waembu; Kirenyaa na Wakamba; Kiinyaa. Ludwig Krapf aliliandika jina kama Kenia na Kegnia, maneno ambayo yanaaminika kutoholewa kutoka neno la Kikamba.
|
20231101.sw_2772_6
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mlima%20Kenya
|
Mlima Kenya
|
Vilele vya Batian, Nelion na Lenana vimepewa majina ya Laibon Mbatian na wanawe ambao walikuwa Wamasai.. Kilele cha Terere pia kilipatiwa jina la kiongozi Mmasai. Majina mengine yalitoka kwa majina ya wazungu wapelelezi, k.v. Shipton, Sommerfelt, Tilman, Dutton na Arthur. Kuna majina yaliyotoka kwa wakenya na walowezi maarufu. Majina ya watume John na Peter yalitolewa na Arthur, aliyekuwa mmishonari.
|
20231101.sw_2772_7
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mlima%20Kenya
|
Mlima Kenya
|
Mlima Kenya ni volkeno rusu iliyokuwa hai kati ya miaka milioni 2.6 na 3.1 iliyopita. Kasoko ya awali ilikuwa pengine katika urefu wa m 6,000; juu kuliko Kilimanjaro. Tangu izimike, kumekuwa na vipindi viwili vya barafu. Barafuto za leo hazipiti m 4,650 .
|
20231101.sw_2772_8
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mlima%20Kenya
|
Mlima Kenya
|
Miteremko ya kitako cha mlima haijawahi kuwa na barafuto. Ni misitu na baadhi ya sehemu zikalimwa. Miteremko hiyo ina mabonde yenye umbo la V na vijito vingi. Juu mlimani, katika eneo ambalo ni nyika, mabonde yenye umbo la U na vina vifupi. Mabonde hayo yaliumbwa na barafuto.
|
20231101.sw_2772_9
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mlima%20Kenya
|
Mlima Kenya
|
Wakati Mlima Kenya ulikuwa hai, shughuli za kivolkeno mbali kiasi na mlima. Kaskazini mashariki, kando ya mlima kuna vizibo vingi vya volkeno na kreta. Kreta ya Ithanguni ndio kubwa zaidi. Inadhaniwa kuwa ilikuwa na theluji wakati huo. Hii inaweza kuonekana kwa kuwa kilele kimelainika. Vilima vidogo huonekana hapo kama ishara kuwa vilikuwa vizibo.
|
20231101.sw_2772_10
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mlima%20Kenya
|
Mlima Kenya
|
Miamba inayounda Mlima kenya ni pamoja na basalt, rhomb porphyrite, phonolite, kenyte na trachyte. Kenyte iliripotiwa kuonekana mara ya kwanza mwaka 1900 na Gregory katika utafiti wake wa jiolojia ya Mlima Kenya.
|
20231101.sw_2772_11
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mlima%20Kenya
|
Mlima Kenya
|
Joseph Thompson alipendekeza utafiti ufanyiwe Mlima Kenya mara ya kwanza mwaka 1883. Aliona mlima kutoka Tambarare ya Laikipia na akaandika kuwa ilikuwa volkeno zimwe, kizibo kikionekana. Hata hivyo, maoni yake hayakuaminika na wanasayansi wa magharibi, hasa baada ya mwaka 1887 wakati Teleki na von Höhnel walikwea mlima na kueleza walichokatia kauli kuwa kreta. Mwaka 1893 msafara wa Gregory ulifika Barafuto ya Lewis, m 5,000. Alithibitisha kuwa volkeno ilikuwa imezimwa na kuwa kulikuwa na barafuto.
|
20231101.sw_2772_12
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mlima%20Kenya
|
Mlima Kenya
|
Asili ya vilele vingi ni shughuli za volkeno. Vilele vingi vimekaribia kati mwa mlima. Vinafanana na vilele vya Alpi kwa sababu ya mikunjo. Kuvu, kuvumwani na mimea midogo ya milimani humea katika vilele vya kati. Vizibo vya volkeno vimefunikwa kwa majivu ya volkeno na udongo.
|
20231101.sw_2772_13
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mlima%20Kenya
|
Mlima Kenya
|
Vilele na vizibo vingine ni pamoja na Piggot (m 4,957), Dutton (m 4,885), John (m 4,883), John Minor (m 4,875), Krapf Rognon (m 4,800), Peter (m 4,757), Slade (m 4,750) na Midget (m 4,700). Vyote vina miinuko inayotengeneza umbo kama la piramidi.
|
20231101.sw_2772_14
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mlima%20Kenya
|
Mlima Kenya
|
Barafuto zinazidi kudidimia kila mwaka. Kila mwaka, theluji inayolimbikika katika majira ya baridi ni kidogo kuliko inayoyeyuka katika majira ya joto. Inabashiriwa kuwa hali ikiendelea hivyo, Mlima Kenya hautakuwa na theluji miaka 30 itakayokuja. Kupungua kwa barafuto kunasababishwa na kuongezeka kwa halijoto au kubadilika kwa tabia ya usimbishaji. Eneo la barafuto lilipimwa rasmi mara ya kwanza mwaka 1980 na kubainika kuwa ni 0.7 km2 .
|
20231101.sw_2772_15
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mlima%20Kenya
|
Mlima Kenya
|
Jalidi usiku hufanya kuwe na miundo ya kingo za kingo za barafuto. Kuna sentimita chache ardhi jalidi chini ya uso wa ardhi. Kupanuka na kupunguka kwa ardhi kwa sababu ya halijoto, hufanya mimea isiweze kumea katika kingo.
|
20231101.sw_2772_16
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mlima%20Kenya
|
Mlima Kenya
|
Mlima Kenya ni eneo kuu la vyanzo vya maji vya mito miwili mikubwa nchini Kenya; Mto Tana na Mto Ewaso Ngiro Kaskazini. Mfumo wa ekolojia wa Mlima Kenya hupatia watu zaidi ya milioni 2 maji. Wiani wa vijito ni kubwa hasa katika miteremko ambayo haijawahi kuwa na barafuto. Vijito na mito inayoanza Mlima Kenya humwaga maji ndani ya Mto Sagana, Mto Tana na Mto Ewaso Ngiso Kaskazini moja kwa moja au kupitia mito mingine.
|
20231101.sw_2772_17
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mlima%20Kenya
|
Mlima Kenya
|
Eneo la Mlima Kenya lina kanda tofauti za kiekolojia. Kila ukanda una sifa zake na spishi kuu ya mimea. Spishi nyingi zinazopatikana katika sehemu zilizo juu ya mlima zinapatikana pia katika maeneo mengine ya mlima na Afrika Mashariki.
|
20231101.sw_2772_18
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mlima%20Kenya
|
Mlima Kenya
|
Pia kuna tofauti kati ya kanda, kutegemea upande wa mlima na ukali wa mteremko. Kusini mashariki pa mlima ni sehemu nyevu kuliko kaskazini kwa hivyo, spishi nyingi za sehemu hiyo hutegemea unyevu kukua. Baadhi ya spishi, k.v. mianzi, haziwezi kukua katika pande zote za mlima kwa sababu za tofauti za unyevu.
|
20231101.sw_2772_19
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mlima%20Kenya
|
Mlima Kenya
|
Tabianchi hubadilika kulingana na mwinuko. Katika kitako cha mlima, udongo una rutuba na hivyo ni mzuri kwa ukulima. Ukulima ulikuwa ukifanyika hapo kwa miaka.
|
20231101.sw_2772_20
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mlima%20Kenya
|
Mlima Kenya
|
Mlima Kenya umezungukwa na misitu. Uoto katika misitu unategemea kiwango cha mvua, na spishi hutofautiana zaidi kusini na kaskazini mwa mteremko. Misitu katika kitako cha mlima hutishiwa na binadamu wanaokata miti ili watengeneze mbao na wanyakuzi ardhi.
|
20231101.sw_2772_21
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mlima%20Kenya
|
Mlima Kenya
|
Juu ya misitu ni ukanda wa mianzi asilia. Ukanda huu huzunguka mlima isipokuwa sehemu ya kaskazini ambapo kuna upungufu wa mvua. Ni vigumu kupata spishi nyingine za mimea hapo kwa sababu uoto wa mianzi ni mzito na huzuia mimea mingine kumea.
|
20231101.sw_2772_22
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mlima%20Kenya
|
Mlima Kenya
|
Juu ya ukanda wa mianzi ni ukanda wa mpaka wa miti. Miti hapa mara nyingi ni midogo kuliko miti katika misitu ya kitako cha mlima.
|
20231101.sw_2772_23
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mlima%20Kenya
|
Mlima Kenya
|
Mahali miti haiwezi kuota ni nyika ya mlima, m 3,000. Mimea ya jenasi Erica hupatikana katika sehemu ya magharibi ambayo huwa nyevu. Vichaka na nyasi hupatikana katika sehemu kame ambayo hushuhudia moto wa pori.
|
20231101.sw_2772_24
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mlima%20Kenya
|
Mlima Kenya
|
Kimo kinapoongezeka, halijoto hupungua zaidi na hewa hupungua, katika ukanda unaojulikana kama Alpi ya Kiafrika. Mazingira ya ukanda huo yanafanana tu na yale ya Safu ya Aberdare. Mimea mingi ya ukanda huo imejirekebisha ili kuweza kukabili halihewa.
|
20231101.sw_2772_25
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mlima%20Kenya
|
Mlima Kenya
|
Mimea ya mlima hutofautiana na mwinuko na mwelekeo wa mlima. Mwinuko unapoongezeka, mimea huwa na marekebisho spesheli ili kuhimili jalidi na miale ya urujuanimno. Kwa mfano, mimea ya jenasi Carduus, katika ukanda wa alpi ya kiafrika, hutumia majani kulinda jicho la ua kutokana na jalidi.
|
20231101.sw_2772_26
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mlima%20Kenya
|
Mlima Kenya
|
Wanyama wengi hukaa katika kitako cha mlima penye halianga nzuri kidogo. Spishi za nyani, pimbi wa mitini, ndovu, nungunungu, nyati, fisi, mbuni, duma na simba huishi hapo. Wanyama mamalia wachache, k.v. Sylvicapra grimmia na pimbi wa miamba wanaweza kuishi katika miinuko ya juu kidogo.
|
20231101.sw_2772_27
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mlima%20Kenya
|
Mlima Kenya
|
Spishi za ndege, k.v. chozi, kwenzi, tai na tumbusi hupatikana katika ukanda wa alpi ya kiafrika. Ndege ni muhimu katika mfumo wa ekolojia hiyo kwa kuwa wao husaidia katika mchavusho.
|
20231101.sw_2772_28
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mlima%20Kenya
|
Mlima Kenya
|
Tabianchi ya Mlima Kenya ni ya milima ya ikweta ambayo Hedberg alieleza kuwa ni 'majira ya baridi kila usiku, majira ya joto kila mchana'. Mlima Kenya mojawapo ya vituo vya uchunguzi wa angahewa vya Global Atmospheric Watch.
|
20231101.sw_2772_29
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mlima%20Kenya
|
Mlima Kenya
|
Mlima Kenya hushuhudia misimu miwili tofauti, misimu ya joto na misimu ya mvua, kama maeneo mengine ya Kenya. Miteremko ya mashariki kaskazini hupata mvua kubwa zaidi kwa kuwa uko katika upande wa pepo za kusi ambazo huleta mvua kutoka Bahari Hindi. Mvua hii huwezesha msitu uliosongamana katika upande huo. Katika miinuko ya juu, usimbishaji hufanyika kama theluji na kutengeneza barafuto.
|
20231101.sw_2772_30
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mlima%20Kenya
|
Mlima Kenya
|
Mlima Kenya ulikuwa kati ya vilele virefu Afrika kuonekana kwa mara ya kwanza na wapelelezi kutoka Ulaya. Wa kwanza kuuona alikuwa Johann Ludwig Krapf, mmisionari Mjerumani, tarehe 3 Desemba 1849, kutoka Kitui, mji ulio km 160 kutoka mlima, baada ya ugunduzi wa Mlima Kilimanjaro.
|
20231101.sw_2772_31
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mlima%20Kenya
|
Mlima Kenya
|
Krapf aliambiwa na watu wa kabila la Waembu kwamba walikuwa wakiuzunguka mlima lakini hawakuwa wamepaa juu kwa sababu ya baridi na theluji. Wakikuyu walithibitisha haya yametukia.
|
20231101.sw_2772_32
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mlima%20Kenya
|
Mlima Kenya
|
Krapf pia alibainisha kwamba mito inayotoka Mlima Kenya, na mingine katika eneo la milima, ilikuwa mito ya kudumu. Akagundua kuwa lazima kuna chanzo cha maji mlimani, katika umbo la barafuto. Aliamini ni chanzo cha Nili Nyeupe.
|
20231101.sw_2772_33
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mlima%20Kenya
|
Mlima Kenya
|
Mwaka 1851 Krapf akarudi Kitui. Yeye alisafiri km 65 karibu na mlima, lakini hakuweza kuuona tena. Mwaka 1877 Hildebrandt alikuwa katika eneo la Kitui na kusikia juu ya mlima, lakini pia hakuweza kuuona, hivyo watu walianza kumtuhumu Krapf.
|
20231101.sw_2772_34
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mlima%20Kenya
|
Mlima Kenya
|
Hatimaye, mwaka 1883, Joseph Thomson alipita upande wa magharibi wa mlima na Krapf alithibitisha madai yake. Hata hivyo, upelelezi rasmi wa kwanza ulifanyika mwaka 1887 na Samuel Teleki na Ludwig von Höhnel. Waliweza kufika mita 4,350 kwenye mteremko wa kusini magharibi. Katika safari ya upelelezi huo, waliamini kuwa walikuwa wamegundua volkeno.
|
20231101.sw_2772_35
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mlima%20Kenya
|
Mlima Kenya
|
Hatimaye, mwaka 1893 timu ilisafiri kutoka pwani hadi Ziwa Baringo katika Bonde la Ufa, ikiongozwa na John W. Gregory, mwanajiolojia Mwingereza. Walikwea mlima hadi mita 4,730 na wakakaa masaa kadhaa katika Barafuto ya Lewis. Aliporudi Uingereza, Gregory alichapisha majarida na hadithi ya mafanikio yake. George Kolb, daktari Mjerumani, alifanya safari mwaka 1894 na 1896 na alikuwa wa kwanza kufika nyika ya mlima upande wa mashariki.
|
20231101.sw_2772_36
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mlima%20Kenya
|
Mlima Kenya
|
Tarehe 28 Julai 1899, Halford John Mackinder aliongoza kundi la wapelelezi 6 kutoka Ulaya, 66 kutoka Uswahilini, Wamaasai 2 na Wakikuyu 96. Walipatana na matatizo mengi njiani. Mackinder aliendelea kupanda mlima. Alikita kambi m 3,142 katika Bonde la Höhnel. Alifanya jaribio la kwanza kufikia kilele tarehe 30 Agosti pamoja na Brocherel na Ollier kupitia upande wa mashariki, lakini wakabakisha kupanda m 100 kutoka Kilele cha Nelion. Tarehe 5 Septemba, Hausberg, Ollier na Brocherel walifanya mzunguko kutafuta njia rahisi ila hawakuweza kupata. Tarehe 11 Septemba Ollier na Brocherel walipanda Barafuto ya Darwin, lakini walilazimishwa kukatiza safari kutokana na dhoruba ya theluji.
|
20231101.sw_2772_37
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mlima%20Kenya
|
Mlima Kenya
|
Wakati Saunders alirudi kutoka Naivasha timu okozi, Mackinder, Ollier na Brocherel walijaribu kupanda kilele tena. Walifika kilele cha Batian saa sita mchana tarehe 13 Septemba, na walishuka kutumia njia ileile.
|
20231101.sw_2772_38
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mlima%20Kenya
|
Mlima Kenya
|
Baada ya ukweaji wa kwanza, hakukuwa na safari nyingi za kukwea mlima. Upelelezi kabla ya Vita ya Kwanza ya Dunia ulikuwa ukifanywa na walowezi nchini Kenya, ambao hawakufanya upelelezi wa kisayansi. Misheni ya Kanisa la Uskoti ilipofunguliwa ChogoriaChogoria,, wamishonari kadhaa walikwea mlima lakini hakuna aliyefanikiwa kufikia vilele vya Batian au Nelion.
|
20231101.sw_2772_39
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mlima%20Kenya
|
Mlima Kenya
|
Miti ya misitu ilikatwa ili kurahisisha safari ya kufikia vilele. Mwaka 1920, Arthur Fowell Buxton alijaribu kutengeneza njia kutoka kusini, na njia nyingine walikuja kutoka Nanyuki kaskazini, lakini njia iliyotumiwa zaidi ni ile ya Chogoria, kutoka mashariki, iliyotengenezwa na Ernest Carr.
|
20231101.sw_2772_40
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mlima%20Kenya
|
Mlima Kenya
|
Mwishoni mwa Julai 1930, Shipton na Bill Tilman walikwea vilele vyote. Katika safari hii, Shipton na Tilman walijaribu kukwea vilele vingine, ikiwa ni pamoja na Petro, Dutton, Midget , Pigott na aidha Terere au Sendeyo.
|
20231101.sw_2772_41
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mlima%20Kenya
|
Mlima Kenya
|
Katika miaka ya 1930 ziara zilifanyika zaidi katika nyika ya mlima. Raymond Hook na Humphrey Slade walikwea ili wachore ramani ya mlima na wakapeleka samaki. Februari mwaka 1938, C Carol na Mtu Muthara wakawa mwanamke wa kwanza na Mwafrika wa kwanza mtawalia kupaa Nelion, katika ziara na Noel Symington, mwandishi wa The Night Climbers of Cambridge, na tarehe 5 Machi Una Cameron akawa mwanamke wa kwanza kupaa Batian.
|
20231101.sw_2772_42
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mlima%20Kenya
|
Mlima Kenya
|
Wakati wa Vita Kuu ya Pili ya Dunia ziara za kukwea mlima zilididimia zaidi. Watu maarufu waliokwea katika wakati huo walikuwa wafungwa wa vitani Waitaliano, ambao walikuwa wamefungwa jela Nanyuki. Walitoroka na kupanda mlima kabla ya kurejea kambini.
|
20231101.sw_2772_43
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mlima%20Kenya
|
Mlima Kenya
|
Mwaka 1949 eneo kupita m 3,400 lilifanywa hifadhi ya kitaifa. Barabara ilijengwa kutoka Naro Moru ili kurahisisha safari ya kufikia nika ya mlima.
|
20231101.sw_2772_44
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mlima%20Kenya
|
Mlima Kenya
|
Mwaka 1963, katika siku ya uhuru wa Kenya, Kisoi Munayo alikita bendera ya Kenya juu ya mlima. Mwaka 1997, mlima Kenya uliteuliwa kuwa eneo la urithi wa dunia na UNESCO.
|
20231101.sw_2772_45
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mlima%20Kenya
|
Mlima Kenya
|
Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kenya, ilianzishwa mwaka 1949. Inahifadhi eneo linalozunguka mlima. Awali ilikuwa hifadhi ya misitu. Tangu Aprili 1978 eneo limeteuliwa kama Hifadhi ya Mazingira ya dunia UNESCO .
|
20231101.sw_2772_46
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mlima%20Kenya
|
Mlima Kenya
|
Serikali ya Kenya ilikuwa na sababu nne za kuanzisha Hifadhi ya Taifa inayozunguka Mlima Kenya: umuhimu wa utalii kwa uchumi, kuhifadhi eneo la uzuri, kuhifadhi viumbe hai ndani yake, na kuhifadhi vyanzo vya maji vinavyozunguka eneo.
|
20231101.sw_2772_47
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mlima%20Kenya
|
Mlima Kenya
|
Makabila makuu wanaoishi kuzunguka Mlima Kenya ni Wakikuyu, Wameru, Waembu na Wamaasai. Hao wote huona mlima huo kama kipengele muhimu cha tamaduni zao.
|
20231101.sw_2772_48
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mlima%20Kenya
|
Mlima Kenya
|
Wakikuyu wanaishi kusini na magharibi mwa mlima. Wao ni wakulima na hulima katika udongo mwekundu wa volkeno. Wakikuyu waamini kwamba Mungu wao, Ngai aliishi juu ya Mlima Kenya aliposhuka kutoka mbinguni. Wao wanaamini kuwa mlima ni kiti cha enzi cha Ngai duniani. Ni mahali ambapo Gikuyu, baba wa kabila, alitumia kukutana na Mungu wao, Ngai. Jina kwa ajili ya Kikuyu Mlima Kenya ni Kĩrĩnyaga (Kirinyaga), tafsiri yake ikiwa ni mlima mweupe. Linatokana na weupe wa theluji.
|
20231101.sw_2772_49
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mlima%20Kenya
|
Mlima Kenya
|
Wazee wa Agikuyu husimulia kuwa Mlima Kenya uliundwa baada ya "Nyota" inayojulikana kama Riuki (kihalisi ikimaanisha -jiwe lililotoka angani) kugonga uso wa dunia. Athari hiyo ilizua mlipuko mkubwa na kufuatiwa na tetemeko la ardhi na mawimbi ya nje ya ulinganifu. Unyogovu ulioletwa na Riuki ulitoa ujiuji wa mawe (magma), majivu ya volkeno na uchafu wa riuki iliyosambaratika hadi juu. Riuki ikawa upachikaji wa miamba ya Mlima Kenya.
|
20231101.sw_2772_50
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mlima%20Kenya
|
Mlima Kenya
|
Masimuliyi haya yanaambatana sambamba na maoni yaliyotolewa na wanajografia na wanajiolojia, ambao wamebatiza mawe ya mlima Kenya kwa jina Kenyte. Kenyte inapatikana katika sehemu mbili tu duniani; kwenye Mlima Kenya na Antarctic katika Ncha ya Kusini. Kwa kupata Kenyte katika maeneo mawili tofauti, nadharia mpya ilisitawishwa, kwamba kimondo kikubwa kilipoingia kwenye angahewa ya dunia, kiligawanyika vipande viwili, kimoja kikigonga dunia kwenye ikweta katika Kenya ya kisasa na cha pili kilipiga Antaktika.
|
20231101.sw_2772_51
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mlima%20Kenya
|
Mlima Kenya
|
Waembu wanaishi kusini-mashariki mwa Mlima Kenya, na kuamini kuwa mlima ni nyumba ya Mungu wao, Ngai au Mwene Njeru. Mlima ni takatifu, na walikuwa wakijenga nyumba zikiwa na milango iliyokuwa ikitazama mlima. Waembu wanauita kiri Njeru, maana yake, mlima mweupe.
|
20231101.sw_2772_52
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mlima%20Kenya
|
Mlima Kenya
|
Wamasai ni wahamahamaji ambao walitumia ardhi kaskazini ya mlima kulisha mifugo wao. Wanaamini kuwa mababu zao walishuka kutoka mlima mwanzoni mwa wakati. Wamasai waliuita Ol Donyo Keri, ambalo linamaanisha 'mlima wa bakora au rangi nyingi' kudokeza theluji, misitu na mengineyo vinavyoonekana kutoka tambarare ya kandokando. Sala moja ya Wamasai kuhusu Mlima Kenya:
|
20231101.sw_2772_53
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mlima%20Kenya
|
Mlima Kenya
|
Wameru wanaishi Mashariki na Kaskazini mwa mlima. Walilima na kufuga katika sehemu yenye rutuba nyingi nchini Kenya. Jina la Mt. Kenya kwa Kimeru ni Kirimara (kutokana na weupe wa theluji).
|
20231101.sw_2772_54
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mlima%20Kenya
|
Mlima Kenya
|
Wazungu wa kwanza kutembelea Mlima Kenya mara nyingi walileta wajumbe wa makabila mengine kama marafiki na mabawabu. Wengi wao hawakuwa na uzoefu wa baridi, au kuwahi kuona theluji. Maitikio yao mara nyingi zilikuwa za woga na tuhuma.
|
20231101.sw_2772_55
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mlima%20Kenya
|
Mlima Kenya
|
Kuna njia nane za kutembea zinazoelekea kwenye kilele cha juu. Ni, kwa mzunguko wa akrabu, kutoka kaskazini, njia za Meru, Chogoria, Kamweti, Naro Moru, Burguret, Sirimon na Timau. Pia kuna njia inayozunguka vilele inayotumiwa kuunganisha njia tofauti. Kati ya hizi, Chogoria, Naro Moru na Sirimon ndio hutumika zaidi na zina malango. Njia nyingine zinahitaji idhini maalum kutoka kwa Huduma ya Wanyamapori Kenya ili kuzitumia.
|
20231101.sw_2772_56
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mlima%20Kenya
|
Mlima Kenya
|
Sir Halford Mackinder, The First ujio wa Mlima Kenya [KM Barbour, ed.], (London, 1991); hadithi ya ujio wa kwanza Batian, pamoja Mackinder's diary na baadhi ya Expedition's picha. Barbour discusses sababu Mackinder, ambaye aliandika na kuchapisha vitabu vingine, hawakuwa kuchapisha maelezo ya akaunti ya Expedition.
|
20231101.sw_2772_57
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mlima%20Kenya
|
Mlima Kenya
|
Dutton EAT, Kenya Mountain (London, 1929); akaunti ya Expedition Mlima Kenya mwaka 1926; illustreras.
|
20231101.sw_2772_58
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mlima%20Kenya
|
Mlima Kenya
|
Vivienne de Watteville, Mwambie Dunia - kuzunguka na Reflections kati Tembo na Milima (London & New York, 1935); akaunti ya mwandishi wa ugenini katika kibanda kidogo katika kanda ya Ziwa na Ellis explorations yake ya Gorges Valley; illustreras .
|
20231101.sw_2772_59
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mlima%20Kenya
|
Mlima Kenya
|
HW Tilman, theluji juu ya Ikweta (London, 1937); akaunti ya ujio wa kwanza (na Shipton) ya NW ridge na Nelion; illustreras.
|
20231101.sw_2772_60
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mlima%20Kenya
|
Mlima Kenya
|
Eric Shipton, juu ya kwamba Mlima, (London, 1943); akaunti ya ujio wa kwanza (na Tilman) ya NW ridge na Nelion; illustreras.
|
20231101.sw_2772_61
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mlima%20Kenya
|
Mlima Kenya
|
Felice Benuzzi, Fuga sul Kenya (Milano 1947) / No picnic juu ya Mlima Kenya (London, 1952); a mountaineering classic, kuhusu wafungwa wa kivita tatu ambao kutoroka kutoka gerezani kambi yao mwaka 1943, hupanda mlima na sparse mgawo, improvised vifaa na hakuna ramani, na kisha kuvunja kurejea katika kambi yao gerezani.
|
20231101.sw_2772_62
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mlima%20Kenya
|
Mlima Kenya
|
Roland Truffaut, Du Kenya au wa Kilimanjaro (Paris 1953) / Kutoka Kenya kwa Kilimanjaro (London, 1957); 1952 akaunti ya ujio wa Kifaransa N. uso wa Mt Kenya; illustreras.
|
20231101.sw_2772_63
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mlima%20Kenya
|
Mlima Kenya
|
Hamish MacInnes, bei ya Adventure, (London, 1987); inajumuisha hadithi ya wiki-mrefu uokozi wa Gerd Judmeier baada yake kuanguka karibu na kilele cha Batian mapema katika miaka ya 1970.
|
20231101.sw_2772_64
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mlima%20Kenya
|
Mlima Kenya
|
I. Allan, C. Kata, G. Boy, Snowcaps juu ya Ikweta (London, 1989); historia ya Afrika Mashariki milima na ascents yao, ikiwemo ya hivi karibuni zaidi pioneered njia; illustreras.
|
20231101.sw_2772_65
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mlima%20Kenya
|
Mlima Kenya
|
Yohana Msomaji, Mlima Kenya (London, 1989); akaunti ya ujio wa Nelion, pamoja na Iain Allan kama mwongozo; illustreras.
|
20231101.sw_2772_66
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mlima%20Kenya
|
Mlima Kenya
|
M. Amin, D. Willetts, B. Tetley, On Mungu Mountain: The Story wa Mlima Kenya (London, 1991). A photographic maadhimisho ya mlima.
|
20231101.sw_2772_67
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mlima%20Kenya
|
Mlima Kenya
|
Vizuka juu ya Mlima Kenya Kifungu kutoka National Geographic Adventure magazine (2007) Mathayo Power
|
20231101.sw_2778_0
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Visiwa%20vya%20Madeira
|
Visiwa vya Madeira
|
Visiwa vya Madeira ni funguvisiwa la Ureno katika bahari ya Atlantiki mbele ya pwani ya Afrika. Iko takriban km 1000 kusini kwa Lisbon na 600 magharibi kwa Moroko.
|
20231101.sw_2778_1
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Visiwa%20vya%20Madeira
|
Visiwa vya Madeira
|
Kisiwa kikubwa kinaitwa Madeira vilevile. Karibu nacho ni kisiwa kidogo cha Porto Santo na visiwa vidogo visivyo na wakazi vya Ilhas Desertas na Ilhas Selvagens.
|
20231101.sw_2785_0
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Addis%20Ababa
|
Addis Ababa
|
Addis Ababa (pia Addis Abeba; kwa Kiamhara አዲስ አበባ, "Ua Jipya"; kwa Kioromo Finfinne) ni mji mkuu wa Ethiopia na wa Umoja wa Afrika.
|
20231101.sw_2785_1
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Addis%20Ababa
|
Addis Ababa
|
Eneo hii lilichaguliwa na Malkia Taytu Betul na mji kuanzishwa mwaka wa 1886 na mume wake, Mfalme Menelik II, na sasa mji huu una umma milioni nne, na asilimia nane ya ukuzi wa uchumi.
|
20231101.sw_2785_2
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Addis%20Ababa
|
Addis Ababa
|
Mji huu uko kwenye Mlima Entoto na ni makazi maalum ya Chuo Kikuu cha Addis Ababa. Chuo Kikuu cha Addis Ababa kilijulikana kama Chuo Kikuu cha Haile Selassie I, kutokana na jina la Mfalme wa mwisho wa Ethiopia, ambaye alitoa jumba la mfalme (Jumba Guenete Leul) liwe makao maalum ya Chuo Kikuu cha Addis Ababa mwaka wa 1961.
|
Subsets and Splits
No community queries yet
The top public SQL queries from the community will appear here once available.