_id
stringlengths
15
22
url
stringlengths
31
150
title
stringlengths
1
86
text
stringlengths
100
23.8k
20231101.sw_2797_77
https://sw.wikipedia.org/wiki/Tarakilishi
Tarakilishi
Ni kawaida kwenye maduka ya Kiunzikuu kuhusika na kanzidata kubwa na mafaili. Mafaili yenye ukubwa wa Gigabyte mpaka terabyte si yasiyo ya kawaida. Ikilinganishwa na tarakilishi binafsi (PC), kwa kawaida Viunzikuu zina mara mia kwa maelfu ya vitunza data vitumikavyo, na vinaweza kufikiwa kwa kasi. Familia nyingine za seva pia zinapunguza kazi za I/O na kutilia mkazo mchakato wa kazi.
20231101.sw_2797_78
https://sw.wikipedia.org/wiki/Tarakilishi
Tarakilishi
Mainframe return on investment (ROI), kama jukwaa lingine lolote la mchakato, ni tegemezi katika uwezo wake wa kupima, kuhimili kazi michanganyiko, upunguzaji gharama za leba, ufikishaji huduma usiopingika kwa matumizi muhimu ya kibiashara, na vipengele vingine kadhaa vya gharama vilivyopunguzwa hatari.
20231101.sw_2797_79
https://sw.wikipedia.org/wiki/Tarakilishi
Tarakilishi
Aina hizi za kompyuta zilidhihiri katika kipindi cha miaka ya 1960. Ni kompyuta zenye umbile dogo kuliko zile zilizotangulia kutajwa, na ni bora kwa kuunganishia kompyuta nyingine zinazotumika viwandani na ndani ya nchi.
20231101.sw_2797_80
https://sw.wikipedia.org/wiki/Tarakilishi
Tarakilishi
Matumizi ya kompyuta yanatofautiana kutokana na malengo na makusudio ya mtumiaji mwenyewe. Yamegawanyika katika sehemu kuu mbili.
20231101.sw_2797_81
https://sw.wikipedia.org/wiki/Tarakilishi
Tarakilishi
Kuna kompyuta zilizoandaliwa kwa ajili ya matumizi yote ambayo mtumiaji anaweza kutumia kutegemea na malengo yake binafsi, kwa mfano mhasibu anaweza kutumia kompyuta kwa ajili ya kufanyia kazi zake za uhasibu (hesabu).
20231101.sw_2797_82
https://sw.wikipedia.org/wiki/Tarakilishi
Tarakilishi
pia mwanasayansi, fundi, mwalimu na mwanafunzi, wote hao wanaweza kutumia kompyuta kwa malengo yao tofauti.
20231101.sw_2797_83
https://sw.wikipedia.org/wiki/Tarakilishi
Tarakilishi
Kompyuta hizi zimeandaliwa kwa ajili ya malengo maalumu tu, kama zile kompyuta zilizoandaliwa kwa ajili ya kuchorea moyo na kupigia picha za X-ray, ambazo ni vigumu kwa mtu mwingine kuzitumia kwa ajili ya kufanyia kazi zake binafsi ambazo zinatofautiana na hizo za hospitalini.
20231101.sw_2797_84
https://sw.wikipedia.org/wiki/Tarakilishi
Tarakilishi
Kutokana na kuendelea kwa elimu ya teknolojia imetusaidia sana kujifunza mambo mbalimbali kupitia kompyuta, ambapo unaweza kuitumia kwa ajili ya kuuliza maswali na kujibiwa kwa haraka tena kwa njia tofauti, kwa ajili ya kufanya majadiliano ya kielimu, pia unaweza kuandaa vipindi mbalimbali vya masomo na kufundishia elimu tofauti.
20231101.sw_2797_85
https://sw.wikipedia.org/wiki/Tarakilishi
Tarakilishi
Pia unaweza kuonyeshea filamu zenye mafundisho mazuri, kama kuonyesha filamu zenye elimu ya jiografia na sayansi ya mifugo na kilimo, kuonyesha sehemu muhimu za nchi, kuonyesha athari za nchi ambazo ndiyo sehemu kuu zinazoleta fedha za kigeni katika nchi, na kuonyesha picha za maendeleo katika sekta mbali mbali za nchi yetu, pia kuonyeshea mila na tamaduni za taifa na mataifa mengine mbalimbali duniani na kadhalika.
20231101.sw_2797_86
https://sw.wikipedia.org/wiki/Tarakilishi
Tarakilishi
Kompyuta zimeandaliwa ndani yake programu mbalimbali zenye michezo tofauti, ambayo inaweza kutumika na watu kulingana na umri wao, na ambayo inajulikana kama moja ya kazi za kukuza kipaji na kuchangamsha akili, na ni sehemu mojawapo ya kuburudisha nafsi.
20231101.sw_2797_87
https://sw.wikipedia.org/wiki/Tarakilishi
Tarakilishi
Kompyuta zinaweza kutumika kwa ajili ya kufanyia kazi za ufundi, kama kuchora ramani ya nyumba na mazingira ya nje ya nyumba, kutengenezea picha kwa kuibadilisha na kuiremba na kuifanya ionekane katika sura nyengine ambayo ni tofauti na ile ya asili.
20231101.sw_2797_88
https://sw.wikipedia.org/wiki/Tarakilishi
Tarakilishi
Kompyuta inaweza kutumika kwa ajili ya kufanyia mawasiliano kupitia mtandao wa (Internet) ambao leo hii ndiyo umeshika nafasi kubwa sana ya mawasiliano kuliko kitu chengine ulimwenguni, kama kuwasiliana kwa kutumiana ujumbe wa barua pepe (E-mail) ambayo ni rahisi na inafika haraka kuliko barua za kupitia posta, pia kwa kutumia barua pepe hakuna haja ya kufikiria sehemu aliko mtu America au bara hindi au sehemu nyingine duniani, kuwasiliana kwa maneno ya maandishi (chat), pia kuwasiliana kwa maneno ya sauti na kuonekana picha (video chat).
20231101.sw_2797_89
https://sw.wikipedia.org/wiki/Tarakilishi
Tarakilishi
Kwa kutumia kompyuta unaweza kuendeshea kazi za usafirishaji katika vituo vikuu vya usafirishaji, kama usafiri wa ardhini (mabasi, metro na treni), usafiri wa majini (meli), na usafiri wa angani (ndege).
20231101.sw_2797_90
https://sw.wikipedia.org/wiki/Tarakilishi
Tarakilishi
Kama kuendeshea mashine viwandani kwa ajili ya kuzalisha bidhaa mbali mbali, kama kutengenezea magari, kuzalishia umeme na kutengenezea bidhaa nyengine za kawaida kama nguo mazulia na kadhalika.
20231101.sw_2797_91
https://sw.wikipedia.org/wiki/Tarakilishi
Tarakilishi
Kompyuta hizi zina utofauti kidogo na zile nyingine hasa kwa sababu huwazimebuniwa na kuundwa kufanya operesheni fulani kulingana na kiwanda na zina uwezo wa kufanya kazi kwa mazingira magumu kuliko kompyuta ya kawaida kama vile mazingira yenye joto, vumbi, kemikali, mvuke, au baridi zaidi.
20231101.sw_2797_92
https://sw.wikipedia.org/wiki/Tarakilishi
Tarakilishi
Kama ilivyokuwa ada na kawaida hivi sasa kutumia kompyuta kwa ajili ya kuendeshea kazi za benki,kwa ajili kurahisisha kazi za mahesabu.
20231101.sw_2797_93
https://sw.wikipedia.org/wiki/Tarakilishi
Tarakilishi
Kompyuta zimekuwa na matumizi makubwa na muhimu sana katika kufanyia uchunguzi na matibabu hospitalini, kama kuchunguza na kuelekeza dawa ya kutibu ugonjwa uliyoonekana, pia kupimia na kujaribia mimba na kutoa maelekezo kuhusiana na siku na tarehe ya kujifungua.
20231101.sw_2797_94
https://sw.wikipedia.org/wiki/Tarakilishi
Tarakilishi
Sehemu zinazoshikika (Hardware), ni aina zote za vifaa vya kompyuta, navyo vimegawanyika katika sehemu kuu tatu.
20231101.sw_2797_95
https://sw.wikipedia.org/wiki/Tarakilishi
Tarakilishi
Kibodi inatumika kwa ajili ya kuingizia herufi, namba, alama na michoro, nayo imegawanyika katika sehemu kuu nne, nazo ni kama ifuatavyo: Funguo za kuandikia (Typewriter keys), funguo za kuhama (Movement keys), funguo za namba pamoja na michoro mingine (Numeric keys) na funguo za kazi Function keys).
20231101.sw_2797_96
https://sw.wikipedia.org/wiki/Tarakilishi
Tarakilishi
Kibonyezo (cha) mahesabu ‘numeral key’ Inatumika kwa ajili ya kufunga na kufungulia namba na michoro.
20231101.sw_2797_97
https://sw.wikipedia.org/wiki/Tarakilishi
Tarakilishi
Kibonyezo (cha) kuendelea ‘enter key’ Inatumika kwa ajili ya kutekeleza amri, au kuanzisha fungu la maneno kwenye ukurasa..
20231101.sw_2797_98
https://sw.wikipedia.org/wiki/Tarakilishi
Tarakilishi
Kibonyezo (cha) mpangilio ‘tab key’ Inatumika kwa ajili ya kuwacha masafa maalumu tofauti na ya kawaida (Normal).
20231101.sw_2797_99
https://sw.wikipedia.org/wiki/Tarakilishi
Tarakilishi
Kibonyezo (cha) kudhibiti ‘control key’ inatumika daima pamoja na ufunguo mwengine kwa ajili ya kutekeleza amri maalumu.
20231101.sw_2797_100
https://sw.wikipedia.org/wiki/Tarakilishi
Tarakilishi
Kibonyezo (cha) kibadalishi ‘alt(ernate) key’ inatumika daima pamoja na ufunguo mwengine kwa ajili ya kutekeleza amri maalumu.
20231101.sw_2797_101
https://sw.wikipedia.org/wiki/Tarakilishi
Tarakilishi
Kibonyezo (cha) kuhama ‘shift key’ inatumika daima pamoja na ufunguo mwengine kwa ajili ya kutekeleza amri maalumu.
20231101.sw_2797_102
https://sw.wikipedia.org/wiki/Tarakilishi
Tarakilishi
Kuna vitufe viwili kwenye kila mausi, kitufe cha upande wa kushoto (Left click) kinatumika kufungulia windozi, programu na kuchagulia maandishi, maneno na picha, na kitufe cha upande wa kulia (Right click) kinatumika kufungulia orodha ya mapendekezo ya kazi.
20231101.sw_2797_103
https://sw.wikipedia.org/wiki/Tarakilishi
Tarakilishi
Printa inatumika kwa ajili ya kutolea vitu vya maandishi au picha kwenye kompyuta kwa njia ya karatasi (kuchapisha).
20231101.sw_2797_104
https://sw.wikipedia.org/wiki/Tarakilishi
Tarakilishi
Plota ni chombo kinachotumika kwa ajili ya kutolea vitu, ambacho kinafanana na printa katika ufanisi wake wa kazi, lakini umbile lake ni kubwa kuliko printa, na kinatumika kwa ajili ya kuchapishia picha na michoro ya kiufundi, pia kinaweza kutumika kwa ajili ya kuchapisha maandishi kama herufi namba na alama.
20231101.sw_2797_105
https://sw.wikipedia.org/wiki/Tarakilishi
Tarakilishi
Kompyuta haiwezi kufanya kazi mpaka kipatikane kitu kinachoitwa software, ambacho kinawakilisha programu zinazoendesha kompyuta. Programu hizo zimegawanyika katika sehemu kuu mbili:
20231101.sw_2797_106
https://sw.wikipedia.org/wiki/Tarakilishi
Tarakilishi
1. Programu za kuendeshea kompyuta (operating systems): programu hizo zinaitwa Windows, na kuna aina nyingi za Windows kulingana na toleo lake na ubora wake, kwani siku zinavyozidi kwenda mbele ndipo tunapozidi kupokea programu nyingine za Windows zenye ubora zaidi kuliko zile za awali.
20231101.sw_2797_107
https://sw.wikipedia.org/wiki/Tarakilishi
Tarakilishi
2. Programu za kufanyia kazi (application systems), nazo ni: Microsoft Office na Graphics design; programu hizo daima zinafanya kazi ndani ya windows, ambazo zinatumika kwa ajili ya kazi mbalimbali za uandishi na hesabu, na kazi nyinginezo za kuunda na kutengeneza picha n.k.
20231101.sw_2797_108
https://sw.wikipedia.org/wiki/Tarakilishi
Tarakilishi
Vifaa hivi vipo ndani ya chombo kiitwacho C.P.U. (kifupi cha Central Processing Unit), ambacho ni kiini cha kompyuta na ndicho kinachofanya kazi ya kuviendesha vifaa vyote vya kompyuta na kutoa maelekezo yote.
20231101.sw_2797_109
https://sw.wikipedia.org/wiki/Tarakilishi
Tarakilishi
Ndani ya madhabodi (Motherboard) kinapatikana kifaa kinachoitwa Bios (kifupi cha Basic Input Output System), ambacho ndicho kinachofanya kazi ya kuviendesha vifaa vya kuingizia na kutolea vitu.
20231101.sw_2797_110
https://sw.wikipedia.org/wiki/Tarakilishi
Tarakilishi
Ni vigumu kufuta au kurekebisha vitu vilivyomo ndani ya kifaa hicho kwani vinazingatiwa ni vitu vya kusomea tu na si kwa kazi nyingine.
20231101.sw_2797_111
https://sw.wikipedia.org/wiki/Tarakilishi
Tarakilishi
Kazi za mahesabu ni kazi zote zinazofanywa na hesabu, kama vile kutoa, kujumlisha, kuzidisha na kugawanya.
20231101.sw_2797_112
https://sw.wikipedia.org/wiki/Tarakilishi
Tarakilishi
Hakuna bei haswa ya tarakilishi. Bei huenda ikawa juu au chini kulingana na aina (model), uwezo wa kuhifadhi data, ukubwa wa diski, ukubwa wa RAM, spidi ya procesa na programu ambayo kompyuta yaweza kuzitumia.
20231101.sw_2800_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/Tripoli%20%28Libya%29
Tripoli (Libya)
Jina la Kiarabu ni طرابلس (tarāblus) au طرابلس الغربية (tarābulus al-gharbiyya - Tripoli ya Magharibi kwa sababu ya Tripoli ya mashariki huko Lebanon) lina asili ya lugha ya Kigiriki (Τρίπολη) likimaanisha "miji mitatu".
20231101.sw_2800_1
https://sw.wikipedia.org/wiki/Tripoli%20%28Libya%29
Tripoli (Libya)
Tripoli ina wakazi 1,150,990 ambayo ni zaidi ya robo moja ya wakazi wote wa Libya na inaendelea kukua haraka.
20231101.sw_2800_2
https://sw.wikipedia.org/wiki/Tripoli%20%28Libya%29
Tripoli (Libya)
Jiji hilo liko ufukoni mwa bahari ya Mediteranea likiwa na hali ya hewa ya wastani. Mwezi Agosti inafika halijoto ya sentigredi 28,1°, Januari sentigredi 12,1°. Miezi ya baridi kuna mvua, Juni hadi Agosti ni majira ya kiangazi.
20231101.sw_2800_3
https://sw.wikipedia.org/wiki/Tripoli%20%28Libya%29
Tripoli (Libya)
Tripoli ni mji wa kale ambao bado historia yake imetunzwa ikionyesha mabaki ya historia yake ndefu tangu enzi za Wafinisia, Waroma, Waarabu, Wahispania, Waturuki na Waitalia.
20231101.sw_2803_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/Niger
Niger
Niger (pia Nijeri) ni nchi kubwa zaidi ya Afrika ya Magharibi kwa eneo, lakini 80% ni katika jangwa la Sahara.
20231101.sw_2803_1
https://sw.wikipedia.org/wiki/Niger
Niger
Imepakana na Algeria na Libya upande wa kaskazini, Mali na Burkina Faso upande wa magharibi, Chad upande wa mashariki na Nigeria pamoja na Benin upande wa kusini.
20231101.sw_2803_2
https://sw.wikipedia.org/wiki/Niger
Niger
Ni sehemu ya kanda la Sahel, yaani sehemu kubwa ya nchi ni yabisi, kaskazini mwake ni yabisi sana ikiwa jangwa la Sahara.
20231101.sw_2803_3
https://sw.wikipedia.org/wiki/Niger
Niger
Jaribio la mapinduzi lilifanyika usiku wa kuamkia Machi 31, 2021, siku chache kabla ya kuapishwa kwa Mohamed Bazoum, rais mteule.
20231101.sw_2803_4
https://sw.wikipedia.org/wiki/Niger
Niger
Mipaka ilichorwa wakati wa ukoloni wa Ufaransa, ikiunganisha watu wenye utamaduni tofautitofauti, kama vile Watuareg (9.3% za wakazi wote) wa Sahara, wahamaji Wafula (8.5%) na Wakanuri (4.7%) wa eneo la Sahel na wakulima wa kusini kama Wasonghai (21%) na Wahausa: hawa wa mwisho ni 55.4% .
20231101.sw_2803_5
https://sw.wikipedia.org/wiki/Niger
Niger
Tofauti hizo kubwa zilileta kipindi cha ugomvi kati ya makabila uliopoa tena baada ya mwaka 2000. Tatizo kubwa la nchi ni vipindi vya ukame na njaa vinavyorudiarudia mara kwa mara.
20231101.sw_2803_6
https://sw.wikipedia.org/wiki/Niger
Niger
Wakazi walikuwa zaidi ya milioni 17 katika sensa ya mwaka 2012. Kwa sasa ni 22.4 kutokana na ongezeko la haraka. Idadi kubwa wako kusini.
20231101.sw_2803_7
https://sw.wikipedia.org/wiki/Niger
Niger
Tangu wakati wa ukoloni, lugha rasmi ni Kifaransa. Lakini kuna lugha 10 za taifa kati ya lugha kuu za makabila asili. Muhimu zaidi ni Kihausa na Kizarma-Sonrai.
20231101.sw_2803_8
https://sw.wikipedia.org/wiki/Niger
Niger
Walio wengi kabisa (99.3%) ni wafuasi wa Uislamu; baadhi yao wanasemekana kuchanganya Uislamu na dini asilia za Kiafrika. Wakristo ni 0.3% tu. Hata hivyo Niger ni nchi isiyo na dini rasmi.
20231101.sw_2804_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mogadishu
Mogadishu
Mogadishu (kwa Kisomali Muqdisho; kwa Kiitalia Mogadiscio) ni mji mkuu wa Somalia. Iko ufukoni wa Bahari Hindi ikiwa na wakazi milioni 2.590 (2017).
20231101.sw_2804_1
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mogadishu
Mogadishu
Mogadishu imeundwa mnamo mwaka 900 BK ikawa mji wa kaskazini kabisa wa utamaduni wa Waswahili kwenye pwani ya Afrika ya Mashariki. Ilikuwa sehemu ya biashara ya kimataifa ya Waswahili jinsi inavyonekana kutokana na sarafu za kale za Uchina, Sri Lanka na Vietnam zilizokutwa na wanaakiolojia katika ardhi yake.
20231101.sw_2804_2
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mogadishu
Mogadishu
Msafiri Mwarabu Ibn Battuta alitembelea Mogadishu mnamo mwaka 1300 akaona matajiri akataja "watu wanene wengi".
20231101.sw_2804_3
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mogadishu
Mogadishu
Mji ulikuwa na vipindi vya kujitegemea na vipindi vya kutawaliwa na nchi za nje katika historia yake. Mnamo mwaka 1500 Wareno walikuwa mabwana wake. Tangu katikati ya karne ya 19 Mogadishu ilikuwa chini ya sultani wa Zanzibar.
20231101.sw_2804_4
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mogadishu
Mogadishu
Mwaka 1892 sultani alikodisha mji kwa Italia iliyoinunua kutoka kwake mwaka 1905 ukawa mji mkuu wa koloni la Somalia ya Kiitalia.
20231101.sw_2804_5
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mogadishu
Mogadishu
Wakati wa Vita Kuu ya Pili ya Dunia mji ulivamiwa na Waingereza mwaka 1941 waliourudisha kwa Italia mwaka 1954.
20231101.sw_2804_6
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mogadishu
Mogadishu
Mwaka 1990 dikteta Siad Barre alipinduliwa halafu Mogadishu pamoja na nchi yote iliingia katika vita vya wenyewe kwa wenyewe. Wanajeshi wa Marekani walijaribu mwaka 1993 kurudisha hali ya usalama kwa niaba ya Umoja wa Mataifa lakini walikuta upinzani mkali kutoka kwa vikundi vya wanamgambo Wasomalia. Baada ya kupoteza askari Marekani iliondoka tena.
20231101.sw_2804_7
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mogadishu
Mogadishu
Hali ya vita imeendelea hadi mwaka 2012, na kwa muda mrefu nchi ikiwa haina serikali wala bunge na uharamia ulishamiri.
20231101.sw_2806_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kitenduli
Kitenduli
Vitenduli ni ndege wadogo wa jenasi Uraeginthus katika familia ya Estrildidae ambao wana rangi buluu. Kuna spishi mbili zingine kwa jenasi hii ambazo zinaitwa tunguhina na zina rangi kahawianyekundu, lakini wataalamu wengine wanaziweka katika jenasi Granatina. Vitenduli wanatokea Afrika chini ya Sahara tu. Hupenda kuwa karibu na makazi ya watu. Tago lao hutengenezwa na manyasi juu ya mti au ndani ya paa; limefunikika juu na mwingilio kando.
20231101.sw_2806_1
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kitenduli
Kitenduli
Uraeginthus angolensis, Kitenduli Mashavu-buluu (Southern au Blue-breasted Cordon-bleu au Blue Waxbill)
20231101.sw_2807_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/Tunguhina
Tunguhina
Tunguhina ni ndege wadogo wa jenasi Uraeginthus katika familia ya Estrildidae ambao wana rangi kahawianyekundu na viraka buluu au zambarau. Kuna spishi tatu zingine kwa jenasi hii ambazo zinaitwa vitenduli na zina rangi buluu. Wataalamu wengine wanaweka spishi mbili za tunguhina ndani ya jenasi Granatina. Spishi hizi zinatokea Afrika chini ya Sahara tu. Tunguhina ni ndege waoga, lakini kwa bustani ya hoteli na nyumba wanazoea watu. Tago lao hutengenezwa na manyasi ndani ya magugu; limefunikika juu na lina mwingilio kando.
20231101.sw_2810_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/Morisi
Morisi
Morisi ni kisiwa karibu na Afrika, pia ni nchi inayoitwa rasmi Jamhuri ya Morisi (kwa Kiingereza: Republic of Mauritius, kwa Kifaransa: République de Maurice). Ni nchi ya visiwa katika Bahari Hindi takriban Km 900 mashariki kwa Madagaska na km 4000 kusini-magharibi kwa Bara Hindi.
20231101.sw_2810_1
https://sw.wikipedia.org/wiki/Morisi
Morisi
Eneo la jamhuri ni pamoja na kisiwa cha Morisi yenyewe, kisiwa cha Rodrigues, visiwa vidogo vya Cargados Carajos na Agalega.
20231101.sw_2810_2
https://sw.wikipedia.org/wiki/Morisi
Morisi
Kisiwa kikuu cha Mauritius ni km² 1,865 au 91% za ardhi yote ya jamhuri. Karibu wakazi wote (1,261,208) huishi huko.
20231101.sw_2810_3
https://sw.wikipedia.org/wiki/Morisi
Morisi
Kisiwa cha Rodrigues kipo km 560 mashariki kwa Morisi yenyewe. Eneo lake ni km² 109; kuna wakazi 41,000.
20231101.sw_2810_4
https://sw.wikipedia.org/wiki/Morisi
Morisi
Visiwa vya Cargados Carajos (vinaitwa pia Saint Brandon) ni visiwa 16 vidogo sana, vyenye eneo la km² 1.3 pekee. Viko km 300 kaskazini kwa Morisi. Kuna wakazi mia chache wavuvi.
20231101.sw_2810_5
https://sw.wikipedia.org/wiki/Morisi
Morisi
Agalega ni visiwa viwili, yaani Kisiwa cha Kaskazini na Kisiwa cha Kusini, takriban km 1,122 kaskazini kwa Morisi yenyewe. Visiwa hivyo vina eneo la km² 70. Kuna vijiji vya Vingt Cinq na La Fourche kwenye kisiwa cha kaskazini na kijiji cha Ste Rita kwenye kisiwa cha kusini. Wenyeji wanalima mazao ya mnazi pamoja na mboga kwa matumizi yao wenyewe.
20231101.sw_2810_6
https://sw.wikipedia.org/wiki/Morisi
Morisi
Baada ya Waarabu na Wareno kuvumbua Morisi, wakazi wa kwanza (1638) walikuwa Waholanzi, lakini hawakuacha dalili isipokuwa majina ya mahali kwa sababu waliondoka mwaka 1710 baada ya kushindwa kiuchumi.
20231101.sw_2810_7
https://sw.wikipedia.org/wiki/Morisi
Morisi
Wafaransa walitawala visiwa kati ya 1715 hadi 1810. Walianzisha miji na mashamba ya miwa. Nje ya walowezi, Wafaransa walipeleka pia watumwa kutoka bara la Afrika. Mwaka 1767 walikuwepo Wafaransa 3,163 pamoja na watumwa Waafrika 15,000, pia Wahindi 587.
20231101.sw_2810_8
https://sw.wikipedia.org/wiki/Morisi
Morisi
Uingereza ulichukua utawala wa visiwa mwaka 1810 katika vita dhidi ya Napoleon. Tangu siku zile Kiingereza kilikuwa lugha rasmi ya serikali, lakini wakazi waliendelea kutumia lahaja za Kifaransa.
20231101.sw_2810_9
https://sw.wikipedia.org/wiki/Morisi
Morisi
Baada ya kuwapatia watumwa uhuru, Waingereza walileta Wahindi wengi, baadaye pia Wachina kama wafanyakazi kwenye mashamba ya sukari. Leo hii idadi kubwa ya wakazi ni wa asili ya Kihindi.
20231101.sw_2810_10
https://sw.wikipedia.org/wiki/Morisi
Morisi
Lakini 80% ya wananchi hutumia aina ya Kifaransa kama lugha ya kwanza (pamoja na krioli ya Kimorisyen. Asilimia 15 hutumia lugha za Kihindi kama vile Kibhojpuri, Kiurdu, Kitamil, na wengine Kichina na Kiingereza.
20231101.sw_2810_11
https://sw.wikipedia.org/wiki/Morisi
Morisi
Karibu nusu (48.5%) ya wakazi hufuata dini ya Uhindu, 32.7% Ukristo (hasa wa Kanisa Katoliki), 17.3% ni Waislamu (hasa Wasunni, lakini pia Washia), 0.4% Wabuddha.
20231101.sw_2810_12
https://sw.wikipedia.org/wiki/Morisi
Morisi
Nchi iliendelea kuwa na serikali zilizochaguliwa bila kupinduliwa: hali hii ya utulivu ilisaidia kukua kwa uchumi. Hali ya maisha ni ya juu kuliko nchi nyingi za Afrika.
20231101.sw_2811_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/Antananarivo
Antananarivo
Antanànarìvo (matamushi [An/ta/na/ri/vo], Umma 1,403,449 (2001 sensa), ni Mji Mkuu wa Madagaska, kwa Mkoa wa Antananarivo.
20231101.sw_2811_1
https://sw.wikipedia.org/wiki/Antananarivo
Antananarivo
Pia mji huu wajulikana kwa jina la Kifaransa kama Tananarive ama kwa kifupi ni Tana. Antanànarivo iko kati ya kisiwa kulingana na usabaa wa kisiwa, lakini ni maili 90 kutoka pwani ya magharibi. Mji mwenyewe una kituo cha amri, kinachojengwa juu ya milima na mabonde marefu yenye miamba na nyembamba. Hii milima na mabonde imesambaa kusini na kaskazini kama 2-½ maili, ikigawa kaskazini kwa njiapanda, na kukwea mahali juu zaidi pakiwa 690 ft. juu ya viwanja dhihirifu za mchele upande wa magharibi, ambazo zenyewe zimo 4060 ft. juu ya usawa wa bahari. Mji huu ni mji mkubwa nchini Madagaska na ni kituo cha amri ya serikali, mawasiliano, na kituo cha uchumi. Mahali Mji huu uko ni 18°55' Kusini, 47°31' Magharibi (-18.916667, 47.516667) , Maili 135 Magharibi-kusini magharibi ya Tamatave, ni bandari ya kisiwa hiki, ambayo imeungwa kwa reli, na kwa maili 60 kwa pwani kuna jahazi za kusafirisha. Viwanda vyahusu utolezi wa kuunda sigara, na nguo.
20231101.sw_2811_2
https://sw.wikipedia.org/wiki/Antananarivo
Antananarivo
Antananarivo ilianza pengine mwaka wa 1625. Kwa muda mrefu machifu wa kijiji cha Hova pekee, waliweza kujipa Uhuru kutoka sehemu nyingine za Madagaska, na kwa hivyo Antananarivo kuwa mji wa maana, na baadaye kuwa mji asili kwa kuongezeka wa wakazi 80,000. Mwaka wa 1793 mji huu ulifanywa uwe mji mkuu wa Wafalme wa Merina. Kushindwa kwa Mfalme Radama (wa kwanza) iliifanya Antananarivo iwe mji mkuu wa Madagaska yote. Mwaka wa 1869 majengo yote kwa mji asili, yalikuwa ya mbao ama nyazi, na hata hivyo mji wenyewe ulikuwa na Jumba za kifalme kubwa, kubwa zaidi ikiwa 120 ft. kwenda juu. Hili jumba lilataji sehemu ya bonde la kati; na jumba hili kubwa zaidi, dari na minara yake imepaa juu, na kwahivyo kuonekana kutoka sehemu zote.
20231101.sw_2811_3
https://sw.wikipedia.org/wiki/Antananarivo
Antananarivo
Kutoka uwanzo wa mawe na tofali, mji wote umejengwa na sasa kuna majengo ya aina nyingi na ya kuhifadhi, Jumba la Kifalme, Nyumba ambazo zilikuwa za Waziri mkuu na masharifu, makazi ya kifaransa, Kathidro ya Aglikan na Katoliki wa Kiromathe, Kanisa kadhaa za mawe na nyingine za matofali, Chuo, Shule, hospitali, Mahakama ya Sheria na Majengo ya Serikali, na nyumba nyingine za kuishi.
20231101.sw_2811_4
https://sw.wikipedia.org/wiki/Antananarivo
Antananarivo
Mji huu ulitekwa na Wafaransa mwaka wa 1895 na kuwekwa kwa koloni ya eneo ya Madagaska. Kutoka ukoloni wa ufaransa barabara njema zilitengenezwa kwa mji, ngazi pana za kupaa kwa eneo ya mabonde zimeunganisha sehemu zile ziko kwa ukwea zaidi na ziwezi kuundwa barabara za kawaida, na sehemu ya kati inayoitwa Andohalo, ni sehemu nzuri sana, ambayo inajia za kutembea na daraja za ukwea ambazo ni shamba za maua na miti. Hifadhi zimewekwa karibu na makazi ya watu, na upandaji wa miti na mashamba ya uhifadhi eneo nyingi za mji zaipatia mji urembo na utulifu. Maji ya patikana kwa chemchem chini ya milima lakini maji mengi yatoka kwa mto Ikopa, ambao mto huo wapitia kando ya Mji kusini na magharibi. Mji wenyewe umelindwa na Vigome viwili ambazo zilijengwa kwa mlima mashariki na kusini-magharibi. Pia kathidro ya Anglikani na katoliki ya kiroma, kuna Kanisa zaidi ya hamsini mjini na eneo za mji, na hata Miskiti za kiislamu. Antananarivo ni nyumbani kwa Chuo Kikuu cha Madagascar na Chuo cha Ambatobe (Collège Rural d'Ambatobe).
20231101.sw_2811_5
https://sw.wikipedia.org/wiki/Antananarivo
Antananarivo
Antanànarìvo ya maanisha "Mji wa Maelfu" (arivo=Elfu). Miaka ya ukoloni na hata miaka iliyofuatia Uhuru wa Madagaska, Antananarivo iliitwa 'Tananarive.
20231101.sw_2812_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/Port%20Louis
Port Louis
Port Louis ni mji mkuu wa jamhuri ya Morisi. Ikiwa na wakazi 170,000 ni mji mkubwa wa taifa hili la visiwani katika Bahari Hindi.
20231101.sw_2812_1
https://sw.wikipedia.org/wiki/Port%20Louis
Port Louis
Kiwanja cha ndege cha kimataifacha Sir Seewoosagur Ramgoolam kipo 30 km kusini ya mji. Kutoka Port Louis kuna feri kwenda Saint Denis mji mkuu wa Réunion.
20231101.sw_2812_2
https://sw.wikipedia.org/wiki/Port%20Louis
Port Louis
Kuna viwanda vya nguo na vitambaa pia vya kemikali na madawa. Benki ziko nyingi. Kwa jumla Port Louis ni mji wa Afrika ambako wenyeji wana hali ya maisha iliyo juu kushinda miji mingine ya Afrika.
20231101.sw_2814_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/Maskarena
Maskarena
Maskarena ni funguvisiwa katika Bahari Hindi takriban 900 km mashariki ya Madagaska. Kwa jumla ni visiwa vya dola la Morisi pamoja na kisiwa cha Kifaransa cha Réunion.
20231101.sw_2814_1
https://sw.wikipedia.org/wiki/Maskarena
Maskarena
Asili ya jina ni nahodha Mreno Pedro Mascarenhas aliyekuwa Mzungu wa kwanza wa kuzitembelea. Havikuwa na wakazi lakini Mascarenhas alitoa taarifa ya kwamba alikuta mabaki ya meli iliyowahi kuharibika kitambo.
20231101.sw_2814_2
https://sw.wikipedia.org/wiki/Maskarena
Maskarena
Kwa hiyo inaaminika ya kwamba mabaharia Waarabu labda pia Wahindi waliwahi kufika mara kwa visiwani bila kuanzisha makao ya kudumu. Lakini visiwa vilisaidia wasafiri baharini kupata chakula na maji na kupumzika kabla ya kuendelea na safari zao.
20231101.sw_2816_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/Shomoro
Shomoro
Shomoro ni ndege wadogo wa jenasi Passer katika familia ya Passeridae ambao wana rangi ya nyeusi, nyeupe, majivu na kahawia. Ndege hawa huitwa korobindo pia, lakini jina hili litumike afadhali kwa kuita ndege wa jenasi Petronia. Shomoro wenye kichwa kijivu huitwa jurawa. Ndege hawa wana domo fupi na nene lifaalo kula mbegu, lakini hula wadudu wadogo pia hasa wanapokuwa vifaranga. Kwa asili shomoro wanatokea Ulaya, Afrika na Asia, lakini watu wamewaletea Australia na Marekani.
20231101.sw_2818_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/Burkina%20Faso
Burkina Faso
Imepakana na nchi zifuatazo: Mali upande wa kaskazini, Niger upande wa mashariki, Benin, Togo, Ghana na Côte d'Ivoire upande wa kusini.
20231101.sw_2818_1
https://sw.wikipedia.org/wiki/Burkina%20Faso
Burkina Faso
Nchi ilianzishwa na Wafaransa kwa njia ya kugawa koloni la Cote d'Ivoire mwaka 1919. Jina la koloni jipya lilikuwa Volta ya Juu (kwa Kifaransa: Haute Volta). Jina limetokana na mto Volta unaoanzia hapa.
20231101.sw_2818_2
https://sw.wikipedia.org/wiki/Burkina%20Faso
Burkina Faso
Kiongozi wa nchi Thomas Sankara alibadilisha jina la nchi tarehe 4 Agosti 1984 kuwa Burkina Faso, yaani nchi ya watu waadilifu (kwa lugha ya Kimossi).
20231101.sw_2818_3
https://sw.wikipedia.org/wiki/Burkina%20Faso
Burkina Faso
Mlima wa juu ni Ténakourou (katika kusini) wenye m. 749. Sehemu ya chini ni bonde la mto Pendjari mpakani kwa Benin.
20231101.sw_2818_4
https://sw.wikipedia.org/wiki/Burkina%20Faso
Burkina Faso
Nchi imegawiwa kwa mikoa 13 (inaitwa region). Ndani ya mikoa kuna wilaya 45 (provinces) na tarafa 301 (departement). Kila mkoa husimamiwa na mkuu anayeitwa gouverneur.
20231101.sw_2818_5
https://sw.wikipedia.org/wiki/Burkina%20Faso
Burkina Faso
Burkina Faso ina chanzo cha matawimto ya mto Volta ambayo ni Mouhoun (pia Volta Nyeusi), Nakambé (pia Volta Nyeupe) na Nazinon (pia Volta Nyekundu). Mouhoun ni mto pekee wenye maji mwaka mzima.
20231101.sw_2818_6
https://sw.wikipedia.org/wiki/Burkina%20Faso
Burkina Faso
Sehemu za kaskazini na mashariki za nchi ambazo ni takriban robo ya eneo lake lote ni beseni yala mto Niger. Matawimto ya Niger (Béli, Gorouol, Goudébo na Dargol) yana maji kwa muda wa miezi 4-6 kila mwaka.
20231101.sw_2818_7
https://sw.wikipedia.org/wiki/Burkina%20Faso
Burkina Faso
Kuna kanda tatu ya hali ya hewa, kuanzia Sahel katika kaskazini hadi Sudan-Guinea katika kusini kwenye mvua zaidi.
20231101.sw_2818_8
https://sw.wikipedia.org/wiki/Burkina%20Faso
Burkina Faso
Katika maeneo yabisi ya kaskazini serikali mbalimbali zimejitahidi kupanda miti, jumla ya milioni 23 katika miaka 1996-2000.
20231101.sw_2818_9
https://sw.wikipedia.org/wiki/Burkina%20Faso
Burkina Faso
Miji mingine muhimu ni Bobo-Dioulasso (wakazi 366,383), Koudougou (wakazi 89,374), Ouahigouya (wakazi 62,325) na Banfora (wakazi 61,762). (takwimu za Januari 2006)
20231101.sw_2818_10
https://sw.wikipedia.org/wiki/Burkina%20Faso
Burkina Faso
Kabila kubwa nchini ni la Wamossi (karibu nusu ya wananchi wote) wakikaa karibu na Wagadugu. La pili ni la Wabobo hasa katika eneo la Bobo-Dioulasso. Kanda la Sahel katika kaskazini wako Wafula.
20231101.sw_2818_11
https://sw.wikipedia.org/wiki/Burkina%20Faso
Burkina Faso
Lugha ya Kifaransa ndiyo lugha rasmi. Lugha kuu za mawasiliano ni Kimossi na Kidiula. Kwa ujumla kuna lugha 68 nchini Burkina.
20231101.sw_2818_12
https://sw.wikipedia.org/wiki/Burkina%20Faso
Burkina Faso
Upande wa dini, wakazi Waislamu ni 60.5%, Wakristo ni 23.2% (Wakatoliki 19% na Waprotestanti 4.2%) na wafuasi wa dini asilia za Kiafrika ni 15.3%.
20231101.sw_2818_13
https://sw.wikipedia.org/wiki/Burkina%20Faso
Burkina Faso
Engberg-Perderson, Lars, Endangering Development: Politics, Projects, and Environment in Burkina Faso (Praeger Publishers, 2003).