_id
stringlengths
15
22
url
stringlengths
31
150
title
stringlengths
1
86
text
stringlengths
100
23.8k
20231101.sw_2849_6
https://sw.wikipedia.org/wiki/Leonard%20Mbotela
Leonard Mbotela
Katika maisha yake ya kazi alikuwa pia mhusika wa huduma ya "Presidential Press Service" chini ya Rais Moi kwa miaka saba.
20231101.sw_2849_7
https://sw.wikipedia.org/wiki/Leonard%20Mbotela
Leonard Mbotela
Hata baada ya kustaafu ameendelea kusikika redioni akisoma habari na kipindi chake "Je Huu ni Ungwana?".
20231101.sw_2851_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/William%20Booth
William Booth
William Booth (10 Aprili 1829 – 20 Agosti 1912) ni Mkristo aliyeanzisha Jeshi la Wokovu na kuwa mkurugenzi wake wa kwanza (1878 – 1912).
20231101.sw_2851_1
https://sw.wikipedia.org/wiki/William%20Booth
William Booth
Booth alizaliwa katika kijiji cha Sneiton, wilaya ya Nottingham, nchi ya Uingereza. Alikuwa mmoja wa watoto wanne, lakini mwana wa kiume wa pekee, wa Samuel Booth na Mary Moss. Baba yake alikuwa tajiri, lakini wakati wa utoto wa William, familia ilianza kuwa maskini.
20231101.sw_2851_2
https://sw.wikipedia.org/wiki/William%20Booth
William Booth
Mwaka 1842 Samuel, ambaye wakati huo alikuwa amefilisika, hakuweza kulipa ada za shule kwa William aliyekuwa na umri wa miaka 13. Hivyo William alianza kuwa mwanagenzi wa mweka rahani. Kabla mwaka huo haujaisha, baba yake alifariki.
20231101.sw_2851_3
https://sw.wikipedia.org/wiki/William%20Booth
William Booth
Wakati wa uanagenzi wake William aliingia Ukristo. Alianza kusoma vitabu vingi, kujifundisha kuandika na kutoa hotuba, na kuwa mhubiri mlei wa Kanisa la Metodisti.
20231101.sw_2851_4
https://sw.wikipedia.org/wiki/William%20Booth
William Booth
Alipomaliza uanagenzi wake mwaka 1848, alijaribu kupata kazi nyingine kwa vile hakupenda kazi ya mweka rahani. Mwaka 1849 aliacha familia yake na kuhamia jiji la London ambapo alipata kazi katika duka la mweka rahani tena. Pia aliendelea na huduma ya mhubiri mlei lakini hakuridhika na nafasi alizozipata. Kwa hiyo aliacha kazi ya mhubiri mlei na kuanza huduma ya uinjilisti mitaani.
20231101.sw_2851_5
https://sw.wikipedia.org/wiki/William%20Booth
William Booth
Mwaka 1851 alijiunga na Kanisa la Wesley, na tarehe 10 Aprili 1852, sikukuu yake ya kuzaliwa ya 23, aliacha kazi ya mweka rahani na kuwa mhubiri kwenye makao makuu yao kule Clapham. Baada ya wiki tano tu, alimchumbia Catherine Mumford.
20231101.sw_2851_6
https://sw.wikipedia.org/wiki/William%20Booth
William Booth
Mwezi wa Novemba 1852, Booth alialikwa kuwa mchungaji wa kanisa kule Spalding, wilaya ya Lincolnshire.
20231101.sw_2851_7
https://sw.wikipedia.org/wiki/William%20Booth
William Booth
William Booth na Catherine Mumford walifunga ndoa tarehe 16 Juni 1855 katika kanisa la Stockwell Green kule London. Walikuwa na watoto wanane wafuatao:
20231101.sw_2851_8
https://sw.wikipedia.org/wiki/William%20Booth
William Booth
Ingawa Booth alikuwa mwinjilisti hodari, hakufurahia uchungaji. Mkutano wa kila mwaka wa kanisa lake walipoendelea kumpa majukumu ya uchungaji na kumkatalia ombi lake la kufanya uinjilisti tu, alijiuzulu uchungaji wake mwaka 1861.
20231101.sw_2851_9
https://sw.wikipedia.org/wiki/William%20Booth
William Booth
Kwa vile madhehebu yake hayakumruhusu kufanya uinjilisti ndani ya makanisa baada ya kujiuzulu kwake, akawa mwinjilisti aliyejitegemea. Hata hivyo, teolojia yake haikubadilika. Aliendelea kuhubiri kwamba wasiookoka watateswa milele, kwamba kila mtu anahitaji kutubu, na kwamba Mungu anatuwezesha kuwa watakatifu, yaani tukiishi maisha ya upendo kwa Mungu na wenzetu. Hatimaye, hata watoto wa Booth walishirikisha katika huduma yake.
20231101.sw_2851_10
https://sw.wikipedia.org/wiki/William%20Booth
William Booth
Mwaka wa 1865, Booth pamoja na mke wake walianzisha Shirika la Uamshaji la Kikristo (β€˜β€™Christian Revival Society’’)) katika eneo la East End la London. Waliendesha mikutano kila jioni na siku nzima ya Jumapili wakitoa huduma za toba, wokovu na maadili ya kikristo kwa fukara, pamoja na walevi, wahalifu na malaya. Jina la shirika lilibadilishwa baadaye kuwa Misheni ya Kikristo (β€˜β€™Christian Mission’’).
20231101.sw_2851_11
https://sw.wikipedia.org/wiki/William%20Booth
William Booth
Booth na wanashirika wake walitenda walichohubiri, yaani waliishi maisha ya kikristo wakijitolea mhanga katika huduma kwa wengine. Kwa mfano, waligawa chakula kwa maskini bila kujali wakidharauliwa kwa ajili ya huduma zao za kikristo.
20231101.sw_2851_12
https://sw.wikipedia.org/wiki/William%20Booth
William Booth
Mwaka wa 1878, jina la shirika lilibadilishwa tena kuwa Jeshi la Wokovu. Kama majeshi mengine, lilipata bendera yake na nyimbo zake ambazo hufuata sauti za watu wa kawaida zikiunganishwa na maneno ya kikristo. Booth na wanajeshi wengine huvaa sare za jeshi la Mungu kwenye mikutano. Booth alianza kuitwa Jenerali, na watumishi wengine walipewa vyeo vya afisa vilivyofaa.
20231101.sw_2851_13
https://sw.wikipedia.org/wiki/William%20Booth
William Booth
Ingawa walibanwa kifedha, Jeshi la Wokovu na huduma zake zilienea haraka na kuzalia matawi katika nchi nyingine, baadhi yao Marekani, Ufaransa, Uswisi, Sweden, Australia, Kanada, Uhindi, Afrika ya Kusini, New Zealand, Jamaika, na kadhalika.
20231101.sw_2851_14
https://sw.wikipedia.org/wiki/William%20Booth
William Booth
Wakati wa maisha yake, William Booth alianzisha huduma za Jeshi la Wokovu katika nchi 58 akisafiri sana na kuendesha mikutano. Booth alitoa jarida na kuandika vitabu kadhaa. Pia alitunga nyimbo nyingi. Kitabu chake maarufu kabisa ni In Darkest England and the Way Out kilichotolewa mwaka wa 1890.
20231101.sw_2851_15
https://sw.wikipedia.org/wiki/William%20Booth
William Booth
Ili kumheshimu Booth, mshairi Vachel Lindsay aliandika shairi liitwalo General William Booth Enters Into Heaven, na Charles Ives aliyekuwa jirani wa Booth alitunga sauti kwa shairi hilo.
20231101.sw_2852_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/Aidani%20wa%20Lindisfarne
Aidani wa Lindisfarne
Aidani wa Lindisfarne (Ireland, 590 hivi - Northumberland, Uingereza, 31 Agosti 651) ndiye aliyeanzisha kituo cha utawa na kuwa askofu wake wa kwanza kwenye kisiwa cha Lindisfarne. Kabla hajafika Northumbria alikuwa mtawa katika kwenye kisiwa cha Iona katika nchi ya Uskoti.
20231101.sw_2852_1
https://sw.wikipedia.org/wiki/Aidani%20wa%20Lindisfarne
Aidani wa Lindisfarne
Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki, Waorthodoksi na Waanglikana kama mtakatifu kwa kufufua Ukristo katika eneo la Northumbria hata akaitwa Mtume wa Northumbria.
20231101.sw_2852_2
https://sw.wikipedia.org/wiki/Aidani%20wa%20Lindisfarne
Aidani wa Lindisfarne
Wakati wa enzi ya Warumi, Ukristo ulikuwa umeenea mpaka Uingereza, lakini kwa sababu ya kushindwa kwa Warumi, Upagani ukaanza kurudi upande wa kaskazini wa Uingereza.
20231101.sw_2852_3
https://sw.wikipedia.org/wiki/Aidani%20wa%20Lindisfarne
Aidani wa Lindisfarne
Oswald, mfalme wa Northumbria, mwaka 616 alilazimishwa kwenda uhamishoni katika kisiwa cha Iona ambako akabadilika kuwa Mkristo na kubatizwa.
20231101.sw_2852_4
https://sw.wikipedia.org/wiki/Aidani%20wa%20Lindisfarne
Aidani wa Lindisfarne
Mwaka 634 Oswald alirudishiwa ufalme wa Northumbria akaamua kuwaingiza katika Ukristo wananchi wake ambao wengi wao walikuwa Wapagani. Ili kutekeleza lengo hilo aliwaomba watawa wa Iona wamtumie wamisionari, naye Aidani akafika mwaka 635.
20231101.sw_2852_5
https://sw.wikipedia.org/wiki/Aidani%20wa%20Lindisfarne
Aidani wa Lindisfarne
Aidani alichagua kisiwa cha Lindisfarne kiwe makao makuu ya dayosisi yake kwa vile kilikuwa karibu na ngome ya kifalme kule Bamburgh.
20231101.sw_2852_6
https://sw.wikipedia.org/wiki/Aidani%20wa%20Lindisfarne
Aidani wa Lindisfarne
Mwanzoni alikuwa mfalme Oswald mwenyewe aliyewatafsiria Aidan na watawa wake kwa vile walikuwa hawajajifunza lugha ya kale ya Kiingereza. Baada ya kifo cha Oswald mwaka 642, Aidan alisaidiwa na mfalme Oswine wa Deira, nao wakawa marafiki wa karibu sana.
20231101.sw_2852_7
https://sw.wikipedia.org/wiki/Aidani%20wa%20Lindisfarne
Aidani wa Lindisfarne
Aidani alikuwa huwatembelea watu kijiji hadi kijiji, na kuongea nao kwa adabu na kujaribu katika maongezi hayo wavutwe na Ukristo.
20231101.sw_2852_8
https://sw.wikipedia.org/wiki/Aidani%20wa%20Lindisfarne
Aidani wa Lindisfarne
Kufuatana na hadithi moja, mfalme alimpa Aidani farasi ili asihitaji kutembea kwa miguu lakini Aidan akatoa farasi kama zawadi kwa mtu maskini.
20231101.sw_2852_9
https://sw.wikipedia.org/wiki/Aidani%20wa%20Lindisfarne
Aidani wa Lindisfarne
Aidani aliweza kuongea na watu na hivyo alifaulu kuwasaidia wananchi wengi wa Northumbria wawe Wakristo. Pia katika kituo chake cha utawa aliwafundisha wavulana kumi na wawili, wenyeji wa Northumbria, ili kuhakikisha kwamba Kanisa la Uingereza liongozwe na Waingereza wenyewe.
20231101.sw_2852_10
https://sw.wikipedia.org/wiki/Aidani%20wa%20Lindisfarne
Aidani wa Lindisfarne
Aidani alifuata tawi la Kiselti la Ukristo, si mapokeo ya Kiroma. Hata hivyo tabia yake na bidii katika umisionari zilisababisha Papa Honorius I amheshimu.
20231101.sw_2852_11
https://sw.wikipedia.org/wiki/Aidani%20wa%20Lindisfarne
Aidani wa Lindisfarne
Kituo cha utawa cha Lindisfarne kiliendelea kukua na kuanzisha makanisa na vituo vingine. Pia kilikuwa kama hazina ya ujuzi wa kitaalamu.
20231101.sw_2852_12
https://sw.wikipedia.org/wiki/Aidani%20wa%20Lindisfarne
Aidani wa Lindisfarne
Attwater, Donald and Catherine Rachel John. The Penguin Dictionary of Saints. 3rd edition. New York: Penguin Books, 1993. ISBN 0-14-051312-4.
20231101.sw_2852_13
https://sw.wikipedia.org/wiki/Aidani%20wa%20Lindisfarne
Aidani wa Lindisfarne
Powicke, F. Maurice and E. B. Fryde Handbook of British Chronology 2nd. ed. London:Royal Historical Society 1961
20231101.sw_2856_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/Alfred%20Nobel
Alfred Nobel
Alfred Nobel (21 Oktoba 1833 – 10 Desemba 1896) alikuwa mhandisi na mwenye viwanda wa nchi ya Sweden.
20231101.sw_2856_1
https://sw.wikipedia.org/wiki/Alfred%20Nobel
Alfred Nobel
Mwaka wa 1867 aligundua jinsi ya kutengeneza baruti kali. Pia aliboresha utoneshaji wa mafuta. Akafaulu kiuchumi akawa tajiri na wakati uleule mwenye wasiwasi kuhusu matumizi ya baruti aliyogundua kwa sababu aliona matumizi mabaya kwa ajili ya silaha. Hivyo katika hati yake ya wasia alianzisha Tuzo ya Nobel kwa ajili ya mafanikio ya kisayansi lakini pia kwa ajili ya amani duniani.
20231101.sw_2856_2
https://sw.wikipedia.org/wiki/Alfred%20Nobel
Alfred Nobel
Kuanzia ilipoanzishwa tuzo ya Nobel watu mbalimbali wametunukiwa tuzo hiyo kama vile Albert Einstein, Niels Bohr, Max Planck, Mama Teresa, Nelson Mandela n.k.
20231101.sw_2858_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/Henri%20Dunant
Henri Dunant
Henri Dunant (8 Mei 1828 - 30 Oktoba 1910) alikuwa mwandishi na mfadhili wa nchi ya Uswisi. Mwaka wa 1859 alianzisha Chama cha Kimataifa cha Msalaba Mwekundu. Pia alisababisha Mapatano ya Geneva. Mwaka wa 1901, pamoja na Frederic Passy, alikuwa mshindi wa Tuzo ya Nobel kwa Amani.
20231101.sw_2860_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/Antoine%20Henri%20Becquerel
Antoine Henri Becquerel
Antoine Henri Becquerel (15 Desemba 1852 – 25 Agosti 1908) alikuwa mwanafizikia kutoka nchi ya Ufaransa.
20231101.sw_2860_1
https://sw.wikipedia.org/wiki/Antoine%20Henri%20Becquerel
Antoine Henri Becquerel
Mwaka wa 1896 aligundua mionzi nururishi. Mwaka wa 1903, pamoja na Pierre Curie na Marie Curie alikuwa mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Fizikia.
20231101.sw_2861_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/Robert%20Koch
Robert Koch
Heinrich Hermann Robert Koch (11 Desemba 1843 – 27 Mei 1910) alikuwa daktari kutoka nchi ya Ujerumani. Hasa alichunguza virusi visababishavyo magonjwa mbalimbali. Mwaka wa 1882 aligundua kirusi kinachosababisha kifua kikuu, na mwaka wa 1883 kirusi kinachosababisha kipindupindu. Mwaka wa 1905 alikuwa mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Tiba.
20231101.sw_2862_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/Rudyard%20Kipling
Rudyard Kipling
Rudyard Kipling (30 Desemba 1865 – 18 Januari 1936) alikuwa mwandishi kutoka nchi ya Uingereza. Hasa aliandika riwaya fupi kwa ajili ya kutetea ukoloni. Mwaka wa 1907 alikuwa mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Fasihi.
20231101.sw_2863_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/Gabriel%20Lippmann
Gabriel Lippmann
Gabriel Lippmann (16 Agosti 1845 – 13 Julai 1921) alikuwa mwanafizikia kutoka nchi ya Ufaransa. Hasa alichunguza taalamu ya kupiga picha kwa rangi. Mwaka wa 1908 alikuwa mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Fizikia.
20231101.sw_2864_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/Albrecht%20Kossel
Albrecht Kossel
Ludwig Karl Martin Leonhard Albrecht Kossel (16 Septemba 1853 – 5 Julai 1927) alikuwa daktari kutoka nchi ya Ujerumani. Hasa alichunguza protini. Mwaka wa 1910 alikuwa mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Tiba.
20231101.sw_2865_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/Maurice%20Maeterlinck
Maurice Maeterlinck
Maurice Polydore Marie Bernard Maeterlinck (29 Agosti 1862 – 5 Mei 1949) alikuwa mwandishi na mshairi kutoka nchi ya Ubelgiji. Mwaka wa 1911 alikuwa mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Fasihi.
20231101.sw_2866_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/Alexis%20Carrel
Alexis Carrel
Alexis Carrel (28 Juni 1873 – 5 Novemba 1944) alikuwa daktari mpasuaji kutoka nchi ya Marekani. Hasa alichunguza mkusanyiko wa vyembe mwilini (tishu) na mbinu za kuuhamisha. Mwaka wa 1912 alikuwa mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Tiba.
20231101.sw_2867_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/Elihu%20Root
Elihu Root
Elihu Root (15 Februari 1845 – 7 Februari 1937) alikuwa mwanasiasa kutoka nchi ya Marekani. Alikuwa mwanachama wa Chama cha Jamhuri cha Marekani. Kutoka 1905 hadi 1909 alikuwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani. Mwaka wa 1912 alikuwa mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Amani.
20231101.sw_2868_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/Rabindranath%20Tagore
Rabindranath Tagore
Rabindranath Tagore (7 Mei 1861 – 7 Agosti 1941) alikuwa mwandishi na mwanafalsafa kutoka nchi ya Uhindi. Tagore ni mwakilishi mkuu wa fasihi ya Kihindi ya kisasa. Pia alitafuta mawasiliano ya kitamaduni na Ulaya na Marekani ambako amesafari mara kadhaa. Mwaka wa 1913 alikuwa mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Fasihi.
20231101.sw_2869_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/Romain%20Rolland
Romain Rolland
Romain Rolland (29 Januari 1866 – 30 Desemba 1944) alikuwa mwandishi kutoka nchi ya Ufaransa. Baadhi ya maandiko yake aliandika wasifu ya maisha ya Ludwig van Beethoven. Baada ya Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia alifuata mawazo ya Gandhi na ya kikomunisti. Mwaka wa 1915 alikuwa mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Fasihi.
20231101.sw_2870_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/Johannes%20Stark
Johannes Stark
Johannes Stark (15 Aprili 1874 – 21 Juni 1957) alikuwa mwanafizikia kutoka nchi ya Ujerumani. Hasa alichunguza maswali ya umeme. Mwaka wa 1905 aligundua athari ya Doppler katika mionzi maalumu. Mwaka wa 1919 alikuwa mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Fizikia.
20231101.sw_2871_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/Jules%20Bordet
Jules Bordet
Jules Bordet (13 Juni 1870 – 6 Aprili 1961) alikuwa daktari kutoka nchi ya Ubelgiji. Hasa alichunguza virusi visababishavyo magonjwa mbalimbali. Mwaka wa 1919 alikuwa mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Tiba.
20231101.sw_2872_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/Carl%20Spitteler
Carl Spitteler
Carl Friedrich Georg Spitteler (24 Aprili 1845 – 29 Desemba 1924) alikuwa mshairi kutoka nchi ya Uswisi. Hasa aliandika mashairi, riwaya fupi na insha. Mwaka wa 1919 alikuwa mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Fasihi.
20231101.sw_2873_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/August%20Krogh
August Krogh
August Krogh (15 Novemba 1874 – 13 Septemba 1949) alikuwa daktari na mwanafiziolojia kutoka nchi ya Denmark. Hasa alichunguza maswali ya uvutaji pumzi. Mwaka wa 1920 alikuwa mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Tiba.
20231101.sw_2874_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/Knut%20Hamsun
Knut Hamsun
Knut Hamsun (4 Agosti 1859 – 19 Februari 1952) alikuwa mwandishi kutoka nchi ya Norway. Hasa aliandika mashairi na riwaya. Mwaka wa 1920 alikuwa mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Fasihi.
20231101.sw_2875_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/Jacinto%20Benavente
Jacinto Benavente
Jacinto Benavente (12 Agosti 1866 – 14 Julai 1954) alikuwa mwandishi kutoka nchi ya Hispania. Hasa aliandika tamthiliya. Mwaka wa 1922 alikuwa mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Fasihi.
20231101.sw_2876_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/Fridtjof%20Nansen
Fridtjof Nansen
Fridtjof Nansen (10 Oktoba 1861 – 13 Mei 1930) alikuwa mpelelezi wa maeneo ya ncha ya Kaskazini, mwanazuolojia na mwanasiasa kutoka nchi ya Norwei. Katika safari yake ya miaka 1888-89 alikuwa mpelelezi wa kwanza kuvuka kisiwa cha Greenland kutoka Mashariki kwenda Magharibi. Miaka ya 1893-96 alisafiri na meli yake iliyoitwa Fram ndani ya barafu ya Bahari ya Ncha ya Kaskazini. Miaka ya 1906-08 alikuwa balozi ya Norwei kule London, Uingereza. Mwaka wa 1922 alikuwa mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Amani.
20231101.sw_2877_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/Willem%20Einthoven
Willem Einthoven
Willem Einthoven (21 Mei 1860 – 29 Septemba 1927) alikuwa daktari na mwanafiziolojia kutoka nchi ya Uholanzi. Hasa alichunguza maswali ya umeme wa moyo na kuunda mbinu za kuupima. Mwaka wa 1924 alikuwa mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Tiba.
20231101.sw_2878_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/Johannes%20Fibiger
Johannes Fibiger
Johannes Fibiger (23 Aprili 1867 – 30 Januari 1928) alikuwa daktari na mwanapatholojia kutoka nchi ya Denmark. Hasa alichunguza ugonjwa wa kansa. Mwaka wa 1926 alikuwa mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Tiba.
20231101.sw_2879_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/Grazia%20Deledda
Grazia Deledda
Grazia Deledda (30 Septemba 1871 – 15 Agosti 1936) alikuwa mwandishi wa kike kutoka nchi ya Italia. Hasa aliandika riwaya ambazo wahusika wake wametoka kisiwa chake cha Sardinia. Mwaka wa 1926 alikuwa mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Fasihi.
20231101.sw_2880_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/Henri%20Bergson
Henri Bergson
Henri Bergson (18 Oktoba 1859 – 4 Januari 1941) alikuwa mwanafalsafa na mwandishi kutoka nchi ya Ufaransa. Mwaka wa 1927 alikuwa mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Fasihi.
20231101.sw_2881_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/Charles%20Nicolle
Charles Nicolle
Charles Jules Henri Nicolle (21 Septemba 1866 – 28 Februari 1936) alikuwa daktari kutoka nchi ya Ufaransa. Hasa alichunguza virusi visababishavyo magonjwa mbalimbali. Alikuwa wa kwanza kueleza jinsi ya kuenea kwa homa ya madoa madoa. Mwaka wa 1928 alikuwa mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Tiba.
20231101.sw_2882_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/Sigrid%20Undset
Sigrid Undset
Sigrid Undset (20 Mei 1882 – 10 Juni 1949) alikuwa mwandishi wa kike kutoka nchi ya Norwei. Hasa aliandika riwaya ambazo ndani yake alijishughulikia na matatizo ya wanawake wa kisasa. Mwaka wa 1928 alikuwa mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Fasihi.
20231101.sw_2883_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/Karl%20Landsteiner
Karl Landsteiner
Karl Landsteiner (14 Juni 1868 – 26 Juni 1943) alikuwa daktari kutoka nchi ya Austria. Baadhi ya utafiti mwingi alichunguza virusi visababishavyo magonjwa mbalimbali. Aligundua aina nne za damu ya mwanadamu. Mwaka wa 1930 alikuwa mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Tiba.
20231101.sw_2884_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/Sinclair%20Lewis
Sinclair Lewis
Sinclair Lewis (7 Februari 1885 – 10 Januari 1951) alikuwa mwandishi kutoka nchi ya Marekani. Katika riwaya zake alikosoa jamii ya kimarekani. Mwaka wa 1926 alituzwa Tuzo ya Pulitzer ya Bunilizi lakini alikataa tuzo hiyo. Mwaka wa 1930 alikuwa mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Fasihi.
20231101.sw_2885_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/John%20Galsworthy
John Galsworthy
John Galsworthy (14 Agosti 1867 – 31 Januari 1933) alikuwa mwandishi kutoka nchi ya Uingereza. Aliandika hasa riwaya, tamthiliya na insha. Mwaka wa 1932 alikuwa mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Fasihi.
20231101.sw_2886_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/Luigi%20Pirandello
Luigi Pirandello
Luigi Pirandello (28 Juni 1867 – 10 Desemba 1936) alikuwa mwandishi kutoka nchi ya Italia. Alijihusisha hasa na tamthiliya na nadharia yake. Mwaka wa 1934 alikuwa mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Fasihi.
20231101.sw_2887_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/Arthur%20Henderson
Arthur Henderson
Arthur Henderson (20 Oktoba 1863 – 13 Septemba 1935) alikuwa mwanasiasa kutoka nchi ya Uingereza. Alikuwa kiongozi wa Chama cha Wafanyakazi (Labour Party) mara tatu: 1908-11, 1914-22, 1931-34. Pia alikuwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza kuanzia 1929 hadi 1931. Mwaka wa 1934 alikuwa mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Amani.
20231101.sw_2888_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/James%20Chadwick
James Chadwick
James Chadwick (20 Oktoba 1891 – 23 Julai 1974) alikuwa mwanafizikia kutoka nchi ya Uingereza. Aligundua na kuchunguza nutroni. Mwaka wa 1935 alikuwa mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Fizikia.
20231101.sw_2889_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/Hans%20Spemann
Hans Spemann
Hans Spemann (27 Juni 1869 – 12 Septemba 1941) alikuwa mwanazuolojia na mwanafiziolojia kutoka nchi ya Ujerumani. Kwa mfano alitafiti maendeleo ya miili ya aina ya chura. Mwaka wa 1935 alikuwa mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Tiba.
20231101.sw_2890_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/Carlos%20Saavedra%20Lamas
Carlos Saavedra Lamas
Carlos Saavedra Lamas (1 Novemba 1878 – 5 Mei 1959) alikuwa mwanasheria na mwanasiasa kutoka nchi ya Argentina. Alikuwa Waziri ya Mambo ya Nje kuanzia 1932 hadi 1938. Wakati ule alisaidia kukomesha Vita ya Chako. Mwaka wa 1936 alikuwa mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Amani.
20231101.sw_2891_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mikael%20Agricola
Mikael Agricola
Mikael Agricola (takriban 1509 – 9 Aprili 1557) alikuwa mwanateolojia katika nchi ya Ufini. Alikuwa mwanafunzi wa Martin Luther na Philipp Melanchthon na baadaye alileta mabadiliko ya kanisa kule Finland. Pia alianzisha fasihi katika lugha ya Kifini na kutafsiri Agano Jipya.
20231101.sw_2892_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/Otto%20Stern
Otto Stern
Otto Stern (17 Februari 1888 – 17 Agosti 1969) alikuwa mwanafizikia kutoka nchi ya Ujerumani. Wakati wa utawala wa Adolf Hitler alihamia Marekani. Hasa alichunguza usumaku wa atomu. Mwaka wa 1943 alikuwa mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Fizikia.
20231101.sw_2893_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/Herbert%20Spencer%20Gasser
Herbert Spencer Gasser
Herbert Spencer Gasser (5 Julai 1888 – 11 Mei 1963) alikuwa mwanafiziolojia kutoka nchi ya Marekani. Hasa alichunguza na kugundua kazi za neva mwilini. Mwaka wa 1944, pamoja na Joseph Erlanger alikuwa mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Tiba.
20231101.sw_2894_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/Joseph%20Erlanger
Joseph Erlanger
Joseph Erlanger (5 Januari 1874 – 5 Desemba 1965) alikuwa daktari na mwanafiziolojia kutoka nchi ya Marekani. Joseph alikuwa ni mtaalamu wa elimu ya neva. Mwaka wa 1944, pamoja na Herbert Spencer Gasser alikuwa mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Tiba.
20231101.sw_2895_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/Wolfgang%20Pauli
Wolfgang Pauli
Wolfgang Pauli (25 Aprili 1900 – 15 Desemba 1958) alikuwa mwanafizikia kutoka nchi ya Austria. Hasa alichunguza nadharia ya Albert Einstein (Relativity Theory) na nadharia ya kwanta. Mwaka wa 1925 alitangaza Kanuni ya Pauli. Mwaka wa 1945 alikuwa mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Fizikia.
20231101.sw_2896_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kanuni%20ya%20Pauli
Kanuni ya Pauli
Kanuni ya Pauli ilitangazwa mwaka wa 1925 na Wolfgang Pauli. Inahusu elektroni za atomu. Kila elektroni ina tarakimu nne za kwanta. Kanuni ya Pauli inadai kwamba tarakimu hizo nne haziwezekani kuwa sawa kwa elektroni mbili ndani ya atomu moja.
20231101.sw_2897_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/Paulo%20Diakono
Paulo Diakono
Paulo Diakono (takriban 720 - 13 Aprili 799) alikuwa mmonaki Mbenedikto, shemasi na mwanahistoria aliyetoka kabila la Walongobardi.
20231101.sw_2897_1
https://sw.wikipedia.org/wiki/Paulo%20Diakono
Paulo Diakono
Aliandika historia ya maaskofu wa mji wa Metz, historia ya Walangobardi, na wasifu wa Papa Gregori I.
20231101.sw_2897_2
https://sw.wikipedia.org/wiki/Paulo%20Diakono
Paulo Diakono
Carlo Cipolla, Note bibliografiche circa l'odierna condizione degli studi critici sul testo delle opere di Paolo Diacono (Venice, 1901)
20231101.sw_2897_3
https://sw.wikipedia.org/wiki/Paulo%20Diakono
Paulo Diakono
Paul the Deacon, Liber de episcopis Mettensibus, ed. and trans. Damien Kempf, Dallas Medieval Texts and Translations 19 (Paris/Louvain/Walpole, MA: Peeters, 2013).
20231101.sw_2898_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/Adolphe%20Adam
Adolphe Adam
Adolphe Adam (24 Julai 1803 – 3 Mei 1856) alikuwa mtunzi wa nyimbo kutoka nchini Ufaransa. Adam alikuwa mtoto wa mtunzi na mpiga kinanda maarufu huko ufaransa, lakini baba yake hakupenda mtoto wake afuate kazi yake ya muziki.
20231101.sw_2898_1
https://sw.wikipedia.org/wiki/Adolphe%20Adam
Adolphe Adam
Adolphe alichaguliwa kama profesa katika Chuo cha Muziki cha Paris, Ufaransa. Na kupewa sifa na mwalimu wake wa zamani Daniel Auber na mwalimu wake Adrien Boieldieu kwa jitihada zake katika sanaa ya opera chuoni.
20231101.sw_2899_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/Daniel%20Auber
Daniel Auber
Daniel Auber (29 Januari 1782 – 12 Mei 1871) alikuwa mtungaji wa muziki kutoka nchi ya Ufaransa. Alikuwa mwanafunzi wa Luigi Cherubini. Hasa alitunga muziki ya opera.
20231101.sw_2900_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/Bela%20Bartok
Bela Bartok
Bela Bartok (25 Machi 1881 – 26 Septemba 1945) alikuwa mtunzi wa muziki kutoka nchi ya Hungaria. Alichunguza na kukusanya nyimbo za jadi kutoka maeneo yapakanayo na mto Danube.
20231101.sw_2902_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/Alexander%20Borodin
Alexander Borodin
Alexander Borodin (12 Novemba 1833 – 27 Februari 1887) alikuwa mtungaji wa muziki kutoka nchi ya Urusi. Baadhi ya muziki nyingi alitunga muziki ya simfoni.
20231101.sw_2903_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/William%20wa%20Ockham
William wa Ockham
William wa Ockham (takriban 1285 – 9 Aprili 1349 au 1350) alikuwa mtawa wa shirika la Ndugu Wadogo kutoka nchi ya Uingereza.
20231101.sw_2903_1
https://sw.wikipedia.org/wiki/William%20wa%20Ockham
William wa Ockham
Toleo bora la maandishi yake kuhusu falsafa na teolojia ni: William of Ockham: Opera philosophica et theologica, Gedeon GΓ‘l, et al., eds. 17 vols. St. Bonaventure, N. Y.: The Franciscan Institute, 1967–88.
20231101.sw_2903_2
https://sw.wikipedia.org/wiki/William%20wa%20Ockham
William wa Ockham
Karibu maandishi yake yote juu ya siasa yamo katika: William of Ockham, H. S. Offler, et al., eds. 4 vols., 1940–97, Manchester: Manchester University Press [vols. 1–3]; Oxford: Oxford University Press [vol. 4].
20231101.sw_2903_3
https://sw.wikipedia.org/wiki/William%20wa%20Ockham
William wa Ockham
Richard Utz and Terry Barakat, "Medieval Nominalism and the Literary Questions: Selected Studies." Perspicuitas
20231101.sw_2905_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/Valentin%20Weigel
Valentin Weigel
Valentin Weigel (7 Agosti 1533 – 10 Juni 1588) alikuwa mwanateolojia wa Kiprotestanti kutoka nchi ya Ujerumani. Jina lake pia liliandikwa Weichel. Alitunga maandiko mengi yaliyoathiriwa na uchaji wa kutafakari sana habari za Mungu.
20231101.sw_2906_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/Alphonse%20Laveran
Alphonse Laveran
Charles Louis Alphonse Laveran (18 Juni 1845 – 18 Mei 1922) alikuwa daktari kutoka nchi ya Ufaransa. Hasa alichunguza virusi visababishavyo magonjwa mbalimbali. Aligundua kirusi kinachosababisha malaria. Mwaka wa 1907 alikuwa mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Tiba.
20231101.sw_2907_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ernest%20Orlando%20Lawrence
Ernest Orlando Lawrence
Ernest Orlando Lawrence (8 Agosti 1901 – 27 Agosti 1958) alikuwa mwanafizikia kutoka nchi ya Marekani. Hasa alifanya utafiti wa fizikia ya kiini. Mwaka wa 1939 alikuwa mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Fizikia. Mwaka wa 1941 alifaulu kutenganisha isotopu za elementi ya urani.
20231101.sw_2909_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/Fr%C3%A9d%C3%A9ric%20Mistral
FrΓ©dΓ©ric Mistral
FrΓ©dΓ©ric Mistral (8 Septemba 1830 – 25 Machi 1914) alikuwa mwandishi kutoka nchi ya Ufaransa. Hasa alijishughulikia na kufufua lugha ya Provence inayozungumzwa sehemu za Kusini za Ufaransa. Aliandika mashairi mengi katika lugha hiyo na kutolea kamusi. Mwaka wa 1904 alikuwa mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Fasihi.
20231101.sw_2911_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/Gabriela%20Mistral
Gabriela Mistral
Gabriela Mistral (6 Aprili 1889 – 10 Januari 1957) alikuwa mwandishi na mshairi wa kike kutoka nchi ya Chile. Jina lake la kuzaliwa lilikuwa Lucila Godoy Alcayaga. Hasa aliuandikia upendo katika mashairi yake. Mwaka wa 1945 alikuwa mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Fasihi.
20231101.sw_2912_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/Camillo%20Golgi
Camillo Golgi
Camillo Golgi (7 Julai 1844 – 21 Januari 1926) alikuwa daktari kutoka nchi ya Italia. Hasa alichunguza mfumo wa neva. Mwaka wa 1906, pamoja na Santiago Ramon y Cajal alikuwa mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Tiba.
20231101.sw_2913_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/Philipp%20Lenard
Philipp Lenard
Philipp Eduard Anton Lenard (7 Juni 1862 – 20 Mei 1947) alikuwa mwanafizikia kutoka nchi ya Ujerumani. Alitayarisha misingi ya nadharia za elektroni. Pia aliipinga nadharia ya Albert Einstein (Relativity Theory). Mwaka wa 1905 alikuwa mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Fizikia.
20231101.sw_2914_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/Henri%20Moissan
Henri Moissan
Henri Moissan (28 Septemba 1852 – 20 Februari 1907) alikuwa mwanakemia kutoka nchi ya Ufaransa. Baadhi ya utafiti mwingi alichunguza elementi ya florini. Mwaka wa 1906 alikuwa mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Kemia.
20231101.sw_2915_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/Alfred%20Werner
Alfred Werner
Alfred Werner (12 Desemba 1866 – 15 Novemba 1919) alikuwa mwanakemia kutoka nchi ya Uswisi. Pamoja na utafiti mwingine alichunguza elementi ya naitrojeni. Mwaka wa 1913 alikuwa mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Kemia.
20231101.sw_2916_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/Frederick%20Soddy
Frederick Soddy
Frederick Soddy (2 Septemba 1877 – 22 Septemba 1956) alikuwa mwanakemia kutoka nchi ya Uingereza. Hasa alichunguza unururifu. Aliunda istilahi mpya ya isotopu. Mwaka wa 1921 alikuwa mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Kemia.
20231101.sw_2917_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/Fritz%20Haber
Fritz Haber
Fritz Haber (9 Desemba 1868 – 29 Januari 1934) alikuwa mwanakemia kutoka nchi ya Ujerumani. Pamoja na utafiti mwingine alichunguza maswali ya kemia ya umeme. Mwaka wa 1918 alikuwa mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Kemia.
20231101.sw_2918_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/Paul%20Ehrlich
Paul Ehrlich
Paul Ehrlich (14 Machi 1854 – 20 Agosti 1915) alikuwa daktari na mwanakemia kutoka nchi ya Ujerumani. Pamoja na Sahachiro Hata aligundua dawa ya kutibu kaswende. Mwaka wa 1908, pamoja na Ilya Mechnikov alikuwa mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Tiba.
20231101.sw_2919_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/Hermann%20Emil%20Fischer
Hermann Emil Fischer
Hermann Emil Fischer (9 Oktoba 1852 – 15 Julai 1919) alikuwa mwanakemia kutoka nchi ya Ujerumani. Baadhi ya utafiti mwingine aligundua usanisi wa glukosi (aina ya sukari). Mwaka wa 1902 alikuwa mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Kemia.