_id
stringlengths
15
22
url
stringlengths
31
150
title
stringlengths
1
86
text
stringlengths
100
23.8k
20231101.sw_2920_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/Hans%20Fischer
Hans Fischer
Hans Fischer (27 Julai 1881 – 31 Machi 1945) alikuwa mwanakemia kutoka nchi ya Ujerumani. Hasa alijihusisha na rangi, k.m. rangi za mimea (klorofili), za damu na za nyongo. Mwaka wa 1930 alikuwa mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Kemia.
20231101.sw_2921_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/Heinrich%20Otto%20Wieland
Heinrich Otto Wieland
Heinrich Otto Wieland (4 Juni 1877 – 5 Agosti 1957) alikuwa mwanakemia kutoka nchi ya Ujerumani. Alihariri kumbukumbu za kikemia za Justus von Liebig. Pia alichunguza mifumo ya kikemia ya sumu za uyoga na asidi ya nyongo. Mwaka wa 1927 alikuwa mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Kemia.
20231101.sw_2922_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/Irving%20Langmuir
Irving Langmuir
Irving Langmuir (31 Januari 1881 – 18 Agosti 1957) alikuwa mwanafizikia na mwanakemia kutoka nchi ya Marekani. Alifanya utafiti kuhusu taa za gesi, neli za elektroni na vivuta hewa. Mwaka wa 1932 alikuwa mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Kemia.
20231101.sw_2923_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/Jean%20Perrin
Jean Perrin
Jean Baptiste Perrin (30 Septemba 1870 – 17 Aprili 1942) alikuwa mwanafizikia kutoka nchi ya Ufaransa. Hasa alichunguza mada za fizikia ya kiini na kemia ya kifizikia. Mwaka wa 1926 alikuwa mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Fizikia.
20231101.sw_2924_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/Theodor%20Svedberg
Theodor Svedberg
Theodor Svedberg (30 Agosti 1884 – 26 Februari 1971) alikuwa mwanakemia kutoka nchi ya Sweden. Baadhi ya uchunguzi mwingi aliunda aina ya mashinepewa. Pia alitafiti mada za fizikia ya kiini. Mwaka wa 1926 alikuwa mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Kemia.
20231101.sw_2925_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/Artturi%20Ilmari%20Virtanen
Artturi Ilmari Virtanen
Artturi Ilmari Virtanen (15 Januari 1895 – 11 Novemba 1973) alikuwa mwanakemia kutoka nchi ya Finland. Baadhi ya utafiti mwingi alichunguza virusi vikaavyo kwenye udongo. Mwaka wa 1945 alikuwa mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Kemia.
20231101.sw_2926_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/Gerhard%20Domagk
Gerhard Domagk
Gerhard Johannes Paul Domagk (30 Oktoba 1895 – 24 Aprili 1964) alikuwa daktari kutoka nchi ya Ujerumani. Hasa alichunguza virusi visababishavyo magonjwa mbalimbali, na kuchapa kazi kwa ajili ya tiba ya kikemia kukomesha magonjwa kama kifua kikuu na kansa. Mwaka wa 1939 alikuwa mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Tiba.
20231101.sw_2927_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/Richard%20Kuhn
Richard Kuhn
Richard Kuhn (3 Desemba 1900 – 1 Agosti 1967) alikuwa mwanakemia kutoka nchi ya Ujerumani. Hasa alichunguza vitamini. Mwaka wa 1938 alikuwa mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Kemia.
20231101.sw_2928_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/Patrice%20Lumumba
Patrice Lumumba
Patrice Lumumba (2 Julai 1925 – 17 Januari 1961) alikuwa mwanasiasa na kiongozi wa uhuru wa nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
20231101.sw_2928_1
https://sw.wikipedia.org/wiki/Patrice%20Lumumba
Patrice Lumumba
Mwaka wa 1958 alikuwa miongoni mwa waanzishaji wa Chama cha Taifa la Kongo (kwa Kifaransa: Mouvement National Congolais).
20231101.sw_2928_2
https://sw.wikipedia.org/wiki/Patrice%20Lumumba
Patrice Lumumba
Mwaka wa 1960 alipata kuwa Waziri Mkuu wa kwanza wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo baada ya kuongoza harakati za kugombea uhuru toka kwa utawala wa kikoloni wa Wabelgiji.
20231101.sw_2928_3
https://sw.wikipedia.org/wiki/Patrice%20Lumumba
Patrice Lumumba
Baada ya miezi miwili tu ya kuwa Waziri Mkuu, Lumumba alipinduliwa na baadaye kutiwa ndani kabla ya kuuawa katika mazingira ya kutatanisha katika eneo la Katanga upande wa kusini wa Kongo.
20231101.sw_2928_4
https://sw.wikipedia.org/wiki/Patrice%20Lumumba
Patrice Lumumba
Patrice Lumumba alizaliwa katika familia ya Watetela, wazazi wake walikuwa François Tolenga Otetshima, na Julienne Wamato Lomendja, ambao walikuwa wafugaji katika eneo la Katakokombe kwenye Mkoa wa Kasai.
20231101.sw_2928_5
https://sw.wikipedia.org/wiki/Patrice%20Lumumba
Patrice Lumumba
Jina lake la kuzaliwa lilikuwa Élias Okit'Asombo alilobadilisha baadaye. na asombó ('cursed or bewitched people who will die quickly'). Alikuwa na kaka watatu ambao ni Charles Lokolonga, Émile Kalema, and Louis Onema Pene Lumumba.Alilelewa katika makuzi ya Kikatoliki, alisoma katika shule ya msingi ya Waprotestanti, halafu katika shule ambayo iliyomilikiwa na wamisionari wa Kanisa Katoliki, na baadaye alipata mafunzo katika chuo kimoja cha serikali, alijishindia kozi mbalimbali na kisha kuajiriwa, alipata kazi katika mji wa Stanleyville ambao kwa sasa unajulikana kwa jina la Kisangani ambapo alifanya kazi kama karani wa posta.
20231101.sw_2928_6
https://sw.wikipedia.org/wiki/Patrice%20Lumumba
Patrice Lumumba
Baadaye alihamia Léopoldville ambao kwa sasa unajulikana kwa jina la Kinshasa alipofanya kazi ya uuzaji wa bia kwa wasafiri. Mnamo mwaka 1951 alimuoa Pauline Opangu. Mwaka 1955 Lumumba alijiunga na Cercles des évolués ambazo zilikuwa klabu za Waafrika wenye elimu ya kibelgiji na kutazamwa kuwa "wameendelea" mjini Stanleyville na baadaye alijiunga na chama cha Liberal Party of Belgium, ambapo alifanya kazi ya uhariri na usambazaji wa kijarida cha Chama cha Kiliberali cha Ubeljiji. Baadaye alifanya ziara ya mafunzo ya wiki tatu nchini Ubeljiji, mwaka 1956 alikamatwa na kushitakiwa kwa kosa la ubadhirifu na kuhukumiwa kifungo cha mwaka mmoja jela kwa kifungo cha nje na, kisha wakili wa Kibelgiji kuthibitisha kwamba Lumumba amesharejesha zile fedha, aliachiliwa huru mapema mwaka uleule.
20231101.sw_2928_7
https://sw.wikipedia.org/wiki/Patrice%20Lumumba
Patrice Lumumba
Baada ya kuachiliwa kwake alisaidiwa na kuanzisha chama cha w:Mouvement national congolais (MNC). Mwaka 1958, alichaguliwa kuwa Rais wa chama hicho. Mnamo Desemba 1958 Lumumba na wenzake walikiwakilisha chama chao katika mkutano wa Baraza la watu wote wa Afrika mjini Accra, Ghana, katika mkutano huo wa Desemba wa muungano wa Afrika uliokuwa chini ya Rais wa Ghana Kwame Nkrumah, Lumumba ambaye alionekana kuongea lugha nyingi, zikiwemo za Kitetela, Kifaransa, Lingala, Kiswahili, na Kiluba, alijitambulisha kwa imani yake kwa bara la Afrika.
20231101.sw_2928_8
https://sw.wikipedia.org/wiki/Patrice%20Lumumba
Patrice Lumumba
Mnamo mwezi wa Oktoba, mwaka 1959, Lumumba, kama kiongozi wa chama cha MNC, alikamatwa kwa kosa la kuchochea vurugu za kupinga serikali ya kikoloni katika mji wa Stanleyville ambapo watu takriban 30 waliuawa na yeye alihukumiwa kwenda jela kwa muda wa miezi sita. Mnamo tarehe 18 Januari 1960 ambayo ilikuwa siku ya majaribio na hapohapo katika siku ya kwanza ya mkutano wa kuzungumzia hatma ya nchi ya Kongo itakumbukwa kwamba, licha ya Lumumba kuwa jela katika kipindi hicho, chama chake cha MNC kilifanikiwa kuwashawishi wananchi kwenye uchaguzi uliofanyika mwezi Desemba na kushinda katika jamhuri ya Kongo. Kutokana na nguvu ya umma iliyokuwa ikifanywa na wananchi wa Kongo dhidi ya kuachiliwa kwa Lumumba kutoka kila kona, aliachiliwa na kuruhusiwa kuhudhuria katika mkutano wa Brussels. Mkutano huo ulifikia kilele tarehe 27 June 1960 kwa azimio la uhuru wa nchi ya Kongo na kupanga uchaguzi kwa mwaka huohuo wa 1960 (Uchaguzi Mkuu wa Kongo 11–25 Mei 1960.
20231101.sw_2928_9
https://sw.wikipedia.org/wiki/Patrice%20Lumumba
Patrice Lumumba
Lumumba na chama chake cha MNC walipata ushindi uliowawezesha kuunda serikali kwa tangazo la tarehe 23 June 1960 na Patrice Lumumba anapata cheo cha uwaziri mkuu akiwa na umri wa miaka 34 na Joseph Kasa-Vubu akiwa ndie Rais wake wa kwanza. Kwa mujibu wa katiba ya Congo mnamo tarehe 24 June serikali ilipitisha kura ya kijasiri ambayo iliamuliwa na baraza la maseneta kwamba tarehe 24 iwe ni siku ya ya kuadhimisha uhuru wa Congo.
20231101.sw_2928_10
https://sw.wikipedia.org/wiki/Patrice%20Lumumba
Patrice Lumumba
Maadhimisho ya uhuru wa Congo kwa mara ya kwanza yalifanyika mnamo tarehe 30 June 1960 ambapo maadhimisho hayo yalihudhuriwa pia na Mfalme Baudouin wa Ubelgiji pamoja na vyombo mbalimbali vya habari kutoka nchi za nje. Lumumba alitoa hotuba yake kama Waziri mkuu katika nchi huru japo yeye alikuwa ameenguliwa katika ratiba ya shughuli hiyo. Mfalme wa Ubeljiji alihutubia kwa kutukuza utawala wa kikoloni, huku akilingania fikra za mjomba wake ambaye alikuwa mfalme wa Ubelgiji akiitwa Leopold II wa Ubelgiji bila kutaja maangamizi ya Dola huru la Kongo. Mfalme aliendelea kutoa masharti, "aliwataka kutokufanya mabadiliko yoyote mpaka wao watakapoona kwamba wanaweza kufanya vyema, na kwamba wataendelea kutoa ushauri. " Lumumba aliufahamisha umma kwamba uhuru uliotolewa na Wabeljiji haukuja hivihivi:
20231101.sw_2928_11
https://sw.wikipedia.org/wiki/Patrice%20Lumumba
Patrice Lumumba
kwa uhuru huu wa Congo hata kama tunasherehekea leo na Wabeljiji, nchi rafiki ambayo tupo sawa kwa sawa, hakuna Mkongo hata mmoja ambaye atasahau kwamba vita waliyipigana hatimaye wakashinda wamaeshinda, kwa mapambano yaliyokuwa yakiendelea, mapambano ambayo watu tulijitoa ambayo kwayo watu walikuwa tayari kwa lolote hata kumwaga damu, kwa namna kwa hakika yalikuwa mapambano matukufu na yalikuwa na mwelekeo wa kukomesha utumwa ambao ulikuwa ukiendeshwa dhidi yetu kwa nguvu.
20231101.sw_2929_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/George%20Gershwin
George Gershwin
George Gershwin (26 Septemba 1898 – 11 Julai 1937) alikuwa mtungaji wa muziki na mpiga kinanda kutoka nchi ya Marekani. Alitunga nyimbo nyingi zilizoathiriwa na mitindo ya Jazz. Pia alitunga opera moja iitwayo Porgy na Bess. Aliaga dunia mapema baada ya kupatwa na kansa ya ubongo. Mwaka wa 1998 alituzwa tuzo maalumu ya Tuzo ya Pulitzer ya Muziki kwa kazi ya maisha yake, yaani baada ya kifo chake.
20231101.sw_2930_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/William%20Murdock
William Murdock
William Murdock (25 Agosti 1754 – 15 Novemba 1839) alikuwa mhandisi kutoka nchi ya Uingereza. Alivumbua na kubuni taa ya gesi.
20231101.sw_2933_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/Florini
Florini
Florini ni dutu sahili na halojeni simetali. Namba atomia yake ni 9. Katika mazingira yetu kawaida iko katika hali ya gesi yenye rangi njanokijani. Alama yake ya kikemia ni F.
20231101.sw_2933_1
https://sw.wikipedia.org/wiki/Florini
Florini
Kwa kawaida hupatikana kama molekuli ya F2. Kati ya elementi zote mmenyuko wake wa oksidisho ni kali sana. Tabia hii inasababisha Florini kuwa sumu kali. Inamenyuka vikali na karibu elementi zote.
20231101.sw_2940_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/Tuzo%20ya%20Nobel%20ya%20Fizikia
Tuzo ya Nobel ya Fizikia
Tuzo ya Nobel ya Fizikia hutolewa kila mwaka kufuatana na wasia ya Alfred Nobel na kamati ya Taasisi ya Taaluma ya Sayansi ya Sweden.
20231101.sw_2940_1
https://sw.wikipedia.org/wiki/Tuzo%20ya%20Nobel%20ya%20Fizikia
Tuzo ya Nobel ya Fizikia
2016 David James Thouless, Frederick Duncan Michael Haldane na John Michael Kosterlitz "for theoretical discoveries of topological phase transitions and topological phases of matter"
20231101.sw_2941_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/Tuzo%20ya%20Nobel%20ya%20Kemia
Tuzo ya Nobel ya Kemia
Tuzo ya Nobeli ya Kemia hutolewa kila mwaka kufuatana na wasia wa Alfred Nobel na Kamati ya Taasisi ya Taaluma ya Sayansi ya Sweden.
20231101.sw_2942_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/Tuzo%20ya%20Nobel%20ya%20Tiba
Tuzo ya Nobel ya Tiba
Tuzo ya Nobel ya Tiba au Fiziolojia hutolewa kila mwaka kufuatana na wasia ya Alfred Nobel na kamati ya Taasisi ya Taaluma ya Sayansi ya Sweden.
20231101.sw_2944_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/Tuzo%20ya%20Nobel%20ya%20Amani
Tuzo ya Nobel ya Amani
Tuzo ya Nobel ya Amani inatolewa na kamati ya Nobel ya Norway iliyochaguliwa na Bunge ya Norway kufuatana na wasia ya Alfred Nobel.
20231101.sw_2946_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/Lilongwe
Lilongwe
Lilongwe ni mji mkuu wa Malawi wenye wakazi 597,619 (sensa ya mwaka 2003). Yenyewe iko kusini magharibi mwa nchi, magharibi mwa Mto Malawi karibu na mpaka wa Malawi na Msumbiji na Zambia. Lilongwe mahali pake ni (-13.98333, 33.78333).
20231101.sw_2946_1
https://sw.wikipedia.org/wiki/Lilongwe
Lilongwe
Mji huo ulianza kama kijiji kwa ufuo wa Mto Malawi na kuwa Kituo cha amri ya wakoloni Waingereza kwa mwanzo wa karne 1900. Yasemekana kwamba, Lilongwe ilisaidia sana kama kituo cha serikali ya wakoloni kwa sababu Lilongwe ilikuwa kwa ruti ya kusini na kaskazini ambayo iliwezesha utawala wa Rhodesia ya kaskazini inayojulikana sasa kama Zambia. Mji wa Lilongwe baadaye ukawa mji wa pili kwa ukubwa Malawi. Mwaka wa 1974, Mji mkuu wa nchi ulihamishwa kutoka Zomba (mji ambao sasa ni wa tatu kwa ukubwa nchini Malawi), hadi kwa mji namba mbili kwa ukubwa, Lilongwe.
20231101.sw_2946_2
https://sw.wikipedia.org/wiki/Lilongwe
Lilongwe
Mji wenyewe una wilaya nyingi ambazo zajulikana kama eneo, mbila kati ya mji kuwa eneo iliopewa namba. Eneo zenyewe hazijapewa namba kulingana vile eneo zimepakana.
20231101.sw_2946_3
https://sw.wikipedia.org/wiki/Lilongwe
Lilongwe
Kuna mabasi na motokaa za abiria zinazosafirisha watu kwa miji ya kale, katikati ya Mji wenyewe na pia Kiwanja cha denge. Mataksi yapatikana rahisi kutoka kwa na taksi kwa jia inayoitwa Presidential Way, kaskazini mwa maduka za soko zilizokati ya Mji.
20231101.sw_2946_4
https://sw.wikipedia.org/wiki/Lilongwe
Lilongwe
Kuna chuo cha ukulima mjini Lilongwe. Wakati wa mvua hasa ni Oktoba na Aprili. Wakati wa ukame ni kuanzia Aprili hadi Oktoba. Kati ya muda huu wa ukame, Juni na Julai kuna baridi na Agosti kukizidi na upepo na vumbi.
20231101.sw_2946_5
https://sw.wikipedia.org/wiki/Lilongwe
Lilongwe
Ukulima ni kama wa tumbako, miwa, mipamba, chai, mahindi, viazi, mikota, mihogo, mituta, na pia kwa wanyama ni kama ng'ombe, mbuzi. Mashamba ya ukulima ni kama 34% za nchi.
20231101.sw_2946_6
https://sw.wikipedia.org/wiki/Lilongwe
Lilongwe
Vifaa vinavyonunuliwa kutoka nchi za kigeni ni vyakula, mafuta, vifaa vilivyoundwa, vifaa vya utumizi na vifaa vya usafirishaji.
20231101.sw_2946_7
https://sw.wikipedia.org/wiki/Lilongwe
Lilongwe
Madini na mali ni kama simiti, madini ya yuranimu ambayo hayajachimbwa, makaa ya miamba, madini ya shabu au alumini.
20231101.sw_2946_8
https://sw.wikipedia.org/wiki/Lilongwe
Lilongwe
Mambo ya mazingira; ukataji wa miti; mmomonyoko wa udongo; ujanaba wa maji, maji ya siwa (ya choo), takataka za viwanda; samaki kupunguka kwa kuaribu eneo za yai za samaki.
20231101.sw_2947_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/Hendrik%20Antoon%20Lorentz
Hendrik Antoon Lorentz
Hendrik Antoon Lorentz (18 Julai 1853 – 4 Februari 1928) alikuwa mwanafizikia kutoka nchi ya Uholanzi. Alitafiti nadharia ya elektroni. Pia alichunguza nadharia ya Albert Einstein (Relativity Theory) na ya kwanta. Mwaka wa 1902, pamoja na Pieter Zeeman alikuwa mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Fizikia.
20231101.sw_2948_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/Albert%20Abraham%20Michelson
Albert Abraham Michelson
Albert Abraham Michelson (19 Desemba 1852 – 9 Mei 1931) alikuwa mwanafizikia kutoka nchi ya Marekani. Tafiti zake ziliweka msingi kwa nadharia ya Albert Einstein (Relativity Theory). Pia aliboresha vipimo vya mwendo wa nuru. Mwaka wa 1907 alikuwa mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Fizikia.
20231101.sw_2949_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/Guglielmo%20Marconi
Guglielmo Marconi
Guglielmo Marconi (25 Aprili 1874 – 20 Julai 1937) alikuwa mwanafizikia kutoka nchi ya Italia. Baada ya uchunguzi mwingi, alivumbua njia ya mawasiliano bila waya.
20231101.sw_2949_1
https://sw.wikipedia.org/wiki/Guglielmo%20Marconi
Guglielmo Marconi
Mwaka wa 1909, pamoja na Ferdinand Braun alikuwa mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Fizikia. Marconi ametajwa mara nyingi kama mvumbuzi wa redio pamoja na Nikola Tesla na Alexander Popov.
20231101.sw_2950_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/Heike%20Kamerlingh%20Onnes
Heike Kamerlingh Onnes
Heike Kamerlingh Onnes (21 Septemba 1853 – 21 Februari 1926) alikuwa mwanafizikia kutoka nchi ya Uholanzi. Alichunguza elementi katika hali ya baridi sana. Pia alifaulu kuoesha elementi ya heliamu. Mwaka wa 1913 alikuwa mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Fizikia.
20231101.sw_2951_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/Max%20von%20Laue
Max von Laue
Max von Laue (9 Oktoba 1879 – 24 Aprili 1960) alikuwa mwanafizikia kutoka nchi ya Ujerumani. Pamoja na utafiti mwingine alichunguza mionzi ya eksirei. Mwaka wa 1914 alikuwa mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Fizikia. Tangu mwaka wa 1950 alikuwa mkurugenzi wa Taasisi ya Max Planck kwa kemia ya kifizikia kule Berlin.
20231101.sw_2955_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/Uholanzi
Uholanzi
Uholanzi ni nchi ya Ulaya ya Magharibi. Imepakana na Ujerumani upande wa mashariki, Ubelgiji upande wa kusini na Bahari ya Kaskazini (North Sea) upande wa magharibi na kaskazini.
20231101.sw_2955_1
https://sw.wikipedia.org/wiki/Uholanzi
Uholanzi
Uholanzi ni sehemu ya "Ufalme wa Nchi za Chini" (Kingdom of the Netherlands) pamoja na visiwa vya Aruba, Curaçao na Sint Maarten, mbali ya visiwa vingine vitatu vya Karibi vya Uholanzi.
20231101.sw_2955_2
https://sw.wikipedia.org/wiki/Uholanzi
Uholanzi
Jina la Uholanzi limetokana na “Holland”, eneo la magharibi la nchi hii. Watu wengi hutumia jina hilo, lakini wakazi wenyewe wanaiita nchi yao “Nederland” inayomaanisha "nchi ya chini". Kwa kweli, sehemu kubwa ya Uholanzi iko chini ya usawa wa bahari. Waholanzi wamejenga maboma kuzuia maji yasienee yakifurika.
20231101.sw_2955_3
https://sw.wikipedia.org/wiki/Uholanzi
Uholanzi
Akifika Uholanzi kwa uwanja wa ndege wa Schiphol, msafiri anastaajabu nchi ilivyo tambarare. Kwa kweli, kuna sehemu zenye vilima, lakini sehemu kubwa zaidi ya Uholanzi ni tambarare.
20231101.sw_2955_4
https://sw.wikipedia.org/wiki/Uholanzi
Uholanzi
Mahali pa juu kabisa nchini ni Kilima cha Vaals, upande wa kusini wa mkoa wa Limburg, kwa 322 m. Mahali pa chini kabisa ni karibu na Nieuwerkerk aan de IJssel, mkoa wa Zuid Holland, kwa -6.76 m (mita 6.76 chini ya usawa wa wastani wa bahari).
20231101.sw_2955_5
https://sw.wikipedia.org/wiki/Uholanzi
Uholanzi
Vipande vikubwa vya nchi vimepatikana kutoka ziwa au bahari. Ili kufanya hivyo boma linajengwa kuzunguka ziwa au sehemu ya bahari, kisha maji yanavutwa kwa bomba. Mahali kati ya boma huitwa “polder”. Mkoa mmoja mzima, Flevoland, umepatwa kwa maji ya “Zuiderzee” (Bahari ya Kusini). Kwa sababu hiyo watu husema: “Mungu aliumba dunia lakini Waholanzi waliumba Uholanzi.” Hata sasa sehemu muhimu ya Uholanzi ni maji: 18%.
20231101.sw_2955_6
https://sw.wikipedia.org/wiki/Uholanzi
Uholanzi
Maboma mengine makubwa yamejengwa upande wa kusini magharibi wa nchi ili ya kuzuia maji yasienee mikoa ya Zeeland na Zuid Holland. Mradi huu huitwa “Deltawerken” au Ujenzi wa Delta. “Oosterscheldekering” au boma la mto wa Oosterschelde ni jengo linaloshangaza. Urefu wake ni 9 km na katikati yake kuna malango makubwa 62 ambayo hujifunga wenyewe kila wakati ambapo maji ya bahari yakifura zaidi ya 3 m. Barabara kuu inapitia juu ya boma hili.
20231101.sw_2955_7
https://sw.wikipedia.org/wiki/Uholanzi
Uholanzi
Mito mikubwa kadhaa inaingia Uholanzi na kutiririka katika Bahari ya Kaskazini. Mto Rijn (Mto Rhine) unaingia kwa Tolkamer upande wa mashiriki, na karibu na Nijmegen Mto Waal unajitenga ambao unachukua 70% ya maji. Mto IJssel unajitenga karibu na Westervoort na kwenda upande wa kaskazini. Mto Maas (Mto Meuse) unaingia Uholanzi upande wa kusini wa Limburg, na karibu na Mook unageuka upande wa magharibi. Mto Schelde unaingia upande wa kusini wa Zeeland.
20231101.sw_2955_8
https://sw.wikipedia.org/wiki/Uholanzi
Uholanzi
Uholanzi umegawanyika katika mikoa 12. Kila mkoa unatawaliwa na gavana ambaye huitwa “Commissaris van de Koningin” isipokuwa yule wa Limburg ambaye huitwa “Gouverneur”. Mikoa na miji mikuu yao ni :
20231101.sw_2955_9
https://sw.wikipedia.org/wiki/Uholanzi
Uholanzi
Katika Uholanzi barabara daima zina msongamano wa magari. Hii ni kwa sababu watu wanakwenda kazini asubuhi hadi kurejea jioni, na wanaoishi Uholanzi ni wengi, na kufanya kazi nyingi sana.
20231101.sw_2955_10
https://sw.wikipedia.org/wiki/Uholanzi
Uholanzi
Kisha kutekwa na Julius Caesar katika karne ya 1 KK, kusini mwa nchi ikawa mpaka wa kaskazini wa Dola la Roma hadi lilipokoma (karne ya 5).
20231101.sw_2955_11
https://sw.wikipedia.org/wiki/Uholanzi
Uholanzi
Baadaye nchi ilivamiwa na makabila mbalimbali ya Wagermanik: Wasaksoni, Wabatavi, Wafrisi na Wafaranki.
20231101.sw_2955_12
https://sw.wikipedia.org/wiki/Uholanzi
Uholanzi
Katika karne ya 8 nchi ilikuwa sehemu ya dola la Karolo Mkuu, na katika karne ya 10 ya Dola Takatifu la Kiroma.
20231101.sw_2955_13
https://sw.wikipedia.org/wiki/Uholanzi
Uholanzi
Katika karne ya 16 nchi ilikuwa chini ya familia ya makaisari (Absburg), lakini ilipokea Matengezo ya Kiprotestanti kinyume cha matakwa ya kaisari Karolo V.
20231101.sw_2955_14
https://sw.wikipedia.org/wiki/Uholanzi
Uholanzi
Mwanae Filipo II wa Hispania alipomrithi hakukubali jambo hilo na kusababisha uasi ulioenea kote (1566-1581) hadi wilaya saba zilipounda jamhuri iliyotambuliwa na Hispania mwaka 1648 tu, katika amani ya Westfalia.
20231101.sw_2955_15
https://sw.wikipedia.org/wiki/Uholanzi
Uholanzi
Karne ya 17 ndipo nchi ilipofikia kilele cha ustawi wake, ikiwa na makoloni mengi huko India, Indonesia, Afrika na Amerika, pamoja na biashara kubwa ya kimataifa duniani kote.
20231101.sw_2955_16
https://sw.wikipedia.org/wiki/Uholanzi
Uholanzi
Baada ya mapinduzi ya Kifaransa (1789) nchi ilitekwa na Wafaransa hadi Amani ya Vienna (1814-1815) iliyopanua Uholanzi huru tena, lakini kwa mfumo wa ufalme.
20231101.sw_2955_17
https://sw.wikipedia.org/wiki/Uholanzi
Uholanzi
Uholanzi haukutaka kushiriki Vita vikuu vya kwanza vya dunia, lakini katika vita vikuu vya pili ulivamiwa na Ujerumani (1940-1945).
20231101.sw_2955_18
https://sw.wikipedia.org/wiki/Uholanzi
Uholanzi
Baadaye Uholanzi umejitahidi sana kushiriki katika mahusiano ya kimataifa na ni kati ya nchi waanzilishi wa Umoja wa Ulaya.
20231101.sw_2955_19
https://sw.wikipedia.org/wiki/Uholanzi
Uholanzi
Wakazi wengi wana asili ya makabila ya Kijerumani, lakini kuna wahamiaji wengi pia kutoka nchi nyingi. 22% za wakazi wana walau mzazi mmoja kutoka nchi za nje.
20231101.sw_2955_20
https://sw.wikipedia.org/wiki/Uholanzi
Uholanzi
Upande wa dini, takwimu za serikali zinaonyesha kwamba mwaka 2015, 50.1% ya wakazi hawakuwa na dini yoyote, 43.8% walikuwa Wakristo (23.7% Wakatoliki, 21.1% Waprotestanti, hasa Wakalvini, 4.9% Waislamu, 1.1% Mabanyani, Wabuddha n.k.
20231101.sw_2957_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/Wole%20Soyinka
Wole Soyinka
Akinwande Oluwole (au "Wole" Soyinka) ni mwandishi Mnigeria na mshindi Mwafrika wa kwanza wa Tuzo ya Nobel ya fasihi (mwaka wa 1986). Wengi wanamwona ndiye mwandishi bora wa michezo ya kuigizwa Afrika.
20231101.sw_2957_1
https://sw.wikipedia.org/wiki/Wole%20Soyinka
Wole Soyinka
Alizaliwa tarehe 13 Julai 1934 kwa wazazi Wayoruba huko Abeokuta, Nigeria. Alisoma shule ya msingi kwao Abeokuta halafu shule ya sekondari ya Ibadan. Alifuata masomo ya fasihi Chuo Kikuu huko Ibadan (1952-1954) na Leeds (Uingereza) 1954-1957.
20231101.sw_2957_2
https://sw.wikipedia.org/wiki/Wole%20Soyinka
Wole Soyinka
Soyinka aligongana mara nyingi na serikali za kidikteta za nchi yake akipinga pia udikteta katika nchi mbalimbali kama vile utawala wa Mugabe huko Zimbabwe. Katika maandishi yake alilenga mara nyingi "buti linalokandamiza bila kujali rangi ya mguu ndani yake". Hasa wakati wa udikteta wa jenerali Sani Abacha (1993-1998) Soyinka alijikuta hatarini. Akaondoka Nigeria akaishi nje alipopata nafasi ya profesa ya fasihi kwenye Chuo Kikuu cha Emory (Atlanta - Marekani).
20231101.sw_2957_3
https://sw.wikipedia.org/wiki/Wole%20Soyinka
Wole Soyinka
Baada ya mwisho wa utawala wa kijeshi mwaka 1999 Soyinka alikubali nafasi kwenye chuo kikuu cha Ife kwa masharti ya kwamba mwanajeshi mstaafu hatakuwa kamwe chansela wa chuo kikuu kile.
20231101.sw_2957_4
https://sw.wikipedia.org/wiki/Wole%20Soyinka
Wole Soyinka
Wole Soyinka amemwoa mke wake Laide akazaa naye watoto wanne. Aliwahi kuwa na watoto wawili kabla ya kuoa.
20231101.sw_2963_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/Charles%20%C3%89douard%20Guillaume
Charles Édouard Guillaume
Charles Édouard Guillaume (15 Februari 1861 – 13 Juni 1938) alikuwa mwanafizikia kutoka nchi ya Uswisi aliyeishi Ufaransa.
20231101.sw_2965_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/Robert%20Millikan
Robert Millikan
Robert Andrews Millikan (22 Machi 1868 – 19 Desemba 1953) alikuwa mwanafizikia kutoka nchi ya Marekani. Baadhi ya uchunguzi mwingine alijishughulikia na vipimo vya umeme wa elementi. Mwaka wa 1923 alikuwa mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Fizikia.
20231101.sw_2968_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/Gustav%20Hertz
Gustav Hertz
Gustav Ludwig Hertz (22 Julai 1887 – 30 Oktoba 1975) alikuwa mwanafizikia kutoka nchi ya Ujerumani. Hasa alichunguza sifa za atomu. Pia alivumbua njia fulani ya kutenganisha isotopu. Mwaka wa 1925, pamoja na James Franck alikuwa mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Fizikia.
20231101.sw_2970_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/Werner%20Heisenberg
Werner Heisenberg
Werner Karl Heisenberg (5 Desemba 1901 – 1 Februari 1976) alikuwa mwanafizikia kutoka nchi ya Ujerumani. Alivumbua umekaniki wa kwanta na kutangaza Kanuni ya Heisenberg ya Utovu wa Hakika. Pia alifanya utafiti wa msingi kuhusu fizikia ya kiini. Mwaka wa 1932 alikuwa mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Fizikia. Mpaka mwaka wa 1970 alikuwa mkurugenzi wa Taasisi ya Max Planck kwa Fizikia ya Nyota.
20231101.sw_2971_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kanuni%20ya%20Heisenberg%20ya%20Utovu%20wa%20Hakika
Kanuni ya Heisenberg ya Utovu wa Hakika
Kanuni ya Heisenberg ya Utovu wa Hakika (kwa kifupi: Kanuni ya Utovu wa Hakika) ni kanuni muhimu katika fizikia ya kwanta. Inasema kwamba haiwezekani kupima sifa mbili zinazotegemeana za kipande kimoja cha elementi kwa uhakika kabisa. Baadhi ya sifa hizo kuna mahali na mwendo. Maana yake, kwa mfano, haiwezekani kupima kabisa mahali na mwendo wa elektroni moja wakati huohuo.
20231101.sw_2975_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/San%20Marino
San Marino
San Marino (kwa Kiitalia maana yake ni "Mtakatifu Marino") ni kati ya nchi ndogo kabisa duniani. Eneo lake lote limo ndani ya mipaka ya Italia, kati ya wilaya za Rimini na Pesaro-Urbino, karibu na mwambao wa bahari ya Adria.
20231101.sw_2975_1
https://sw.wikipedia.org/wiki/San%20Marino
San Marino
San Marino inatajwa kuwa jamhuri yenye umri mkubwa kuliko zote duniani. Ilianzishwa na Wakristo waliokimbia dhuluma ya Kaisari wa Roma Diokletiano wakitafuta kimbilio mlimani.
20231101.sw_2975_2
https://sw.wikipedia.org/wiki/San%20Marino
San Marino
Tangu hapo imefaulu kudumisha uhuru wake. Ndiyo sababu tangu mwaka 2008 imeorodheshwa na UNESCO kati ya mahali pa Urithi wa Dunia.
20231101.sw_2975_3
https://sw.wikipedia.org/wiki/San%20Marino
San Marino
San Marino ina wakazi 33,909 (2019) katika vijiji 9. Karibu wote (97.2%) ni waumini wa Kanisa Katoliki (jimbo la San Marino-Montefeltro) na wanaongea Kiitalia kwa lahaja ya Kiromagna.
20231101.sw_2975_4
https://sw.wikipedia.org/wiki/San%20Marino
San Marino
San Marino imetunza utaratibu wa serikali inayofanana na muundo wa jamhuri ya Roma ya kale. Serikali inaongozwa na watawala wawili ("Capitani Reggenti") wanaochaguliwa kwa muda wa miezi sita tu kama zamani konsuli wa Kiroma.
20231101.sw_2975_5
https://sw.wikipedia.org/wiki/San%20Marino
San Marino
Bunge linaitwa Halmashauri Kuu ("Consiglio Grande e Generale") likichaguliwa kila baada ya miaka mitano. Halmashauri inateua pia kamati ya watu 12 ("Consiglio dei XII") inayotekeleza kazi ya mahakama.
20231101.sw_2975_6
https://sw.wikipedia.org/wiki/San%20Marino
San Marino
Wananchi wote hukutana mara mbili kwa mwaka kama mkutano mkubwa wa "Arengo" wakiamua juu ya matamko na mapendekezo kwa serikali.
20231101.sw_2976_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/Sully%20Prudhomme
Sully Prudhomme
Sully Prudhomme (16 Machi 1839 – 7 Septemba 1907) alikuwa mwandishi na mshairi kutoka nchi ya Ufaransa. Jina lake la kuzaliwa lilikuwa René-François-Armand Prudhomme. Mashairi yake yanaonyesha sifa za ujumi. Mwaka wa 1901 alikuwa mshindi wa kwanza wa Tuzo ya Nobel kwa Fasihi.
20231101.sw_2979_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/Toni%20Morrison
Toni Morrison
Toni Morrison (18 Februari 1931 – 5 Agosti 2019) alikuwa mwandishi wa kike nchini Marekani na mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Fasihi ya mwaka 1993.
20231101.sw_2979_1
https://sw.wikipedia.org/wiki/Toni%20Morrison
Toni Morrison
Alizaliwa kwa jina la Chloe Anthony Wofford tarehe 18 Februari 1931 huko Lorain, Ohio - 2019 kama mtoto wa pili wa familia ya Waamerika weusi. Wazazi wake walikuwa wafanyakazi.
20231101.sw_2979_2
https://sw.wikipedia.org/wiki/Toni%20Morrison
Toni Morrison
Alipenda kusoma vitabu tangu utoto. 1949 akajiunga na chuo kikuu cha Howard (chuo kwa Waamerika weusi katika mji mkuu Washington D.C.) akimaliza kwa digrii ya BA katika somo la Kiingereza. Wakati ule aliacha jina lake la Chloe akatumia "Toni" kama kifupi cha "Anthony". Mwaka 1955 alipata MA (shahada ya pili) kutoka chuo kikuu cha Cornell.
20231101.sw_2979_3
https://sw.wikipedia.org/wiki/Toni%20Morrison
Toni Morrison
Alianza kufundisha fasihi kwenye chuo kikuu cha Texas Kusini mjini Houston, tangu 1957 tena Howard. Aliolewa na Howard Morrison akazaa watoto wawili. Baada ya talaka mwaka 1964 alianza kazi ya uhariri wa vitabu kwa wachapishaji wa Random House. Alihariri vitabu vingi vya waandishi weusi.
20231101.sw_2979_4
https://sw.wikipedia.org/wiki/Toni%20Morrison
Toni Morrison
Mwaka 1970 alitoa kitabu chake cha kwanza "The Bluest Eye" (Jicho la buluu kabisa). Kitabu cha kwanza kilichofaulu kuuzwa vema kilikuwa "Song of Solomon" (Wimbo ya Suleimani) mwaka 1977. Mwaka wa 1988 alituzwa Tuzo ya Pulitzer ya Bunilizi kwa riwaya yake Beloved.
20231101.sw_2979_5
https://sw.wikipedia.org/wiki/Toni%20Morrison
Toni Morrison
Tangu 1989 amefundisha kama profesa katika chuo kikuu cha Princeton. 1993 alipokea Tuzo ya Nobel ya Fasihi.
20231101.sw_2980_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/Theodor%20Mommsen
Theodor Mommsen
Christian Matthias Theodor Mommsen (30 Novemba 1817 – 1 Novemba 1903) alikuwa mwanahistoria na mwandishi kutoka nchi ya Ujerumani. Anafahamika hasa kwa kitabu chake Historia ya Roma (kwa Kijerumani: Römische Geschichte). Mwaka wa 1902 alikuwa mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Fasihi.
20231101.sw_2981_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/Henryk%20Sienkiewicz
Henryk Sienkiewicz
Henryk Adam Aleksander Pius Sienkiewicz (5 Mei 1846 – 15 Novemba 1916) alikuwa mwandishi kutoka nchi ya Poland.
20231101.sw_2981_1
https://sw.wikipedia.org/wiki/Henryk%20Sienkiewicz
Henryk Sienkiewicz
Riwaya zake zilikuwa hupendwa sana na watu wengi. Mwaka wa 1905 alikuwa mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Fasihi.
20231101.sw_2983_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/Giosue%20Carducci
Giosue Carducci
Giosuè Carducci (27 Julai 1835 – 16 Februari 1907) alikuwa mwandishi na mshairi kutoka nchi ya Italia.
20231101.sw_2984_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/Rudolf%20Christoph%20Eucken
Rudolf Christoph Eucken
Rudolf Christoph Eucken (5 Januari 1846 – 14 Septemba 1926) alikuwa mwanafalsafa na mwandishi kutoka nchi ya Ujerumani. Alitafsiri vitabu vya Aristoteli na kuandika vitabu kuhusu maadili na dini. Mwaka wa 1908 alikuwa mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Fasihi.
20231101.sw_2987_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/Selma%20Lagerlof
Selma Lagerlof
Selma Lagerlöf (20 Novemba 1858 – 16 Machi 1940) alikuwa mwandishi wa kike kutoka nchi ya Sweden. Aliandika hasa riwaya. Mwaka wa 1909 alikuwa mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Fasihi akiwa mwanamke wa kwanza kupokea tuzo hiyo.
20231101.sw_2988_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/Svante%20Arrhenius
Svante Arrhenius
Svante Arrhenius (19 Februari 1859 – 2 Oktoba 1927) alikuwa mwanakemia kutoka nchi ya Sweden. Baadhi ya utafiti mwingine alichunguza uchanganuaji dutu kwa nguvu za umeme (elektrolisisi). Mwaka wa 1903 alikuwa mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Kemia.
20231101.sw_2990_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/William%20Ramsay
William Ramsay
William Ramsay (2 Oktoba 1852 – 23 Julai 1916) alikuwa mwanakemia kutoka nchi ya Uingereza. Hasa alivumbua na kuchunguza elementi za gesi, yaani neoni, agoni, kriptoni na xenoni. Mwaka wa 1904 alikuwa mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Kemia.
20231101.sw_2991_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/Adolf%20von%20Baeyer
Adolf von Baeyer
Adolf von Baeyer (31 Oktoba 1835 – 20 Agosti 1917) alikuwa mwanakemia kutoka nchi ya Ujerumani. Mwaka wa 1880 alifaulu kusanisi nili na kuendelea kuichunguza. Mwaka wa 1905 alikuwa mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Kemia.
20231101.sw_2993_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/Nili
Nili
Nili ni rangi ya buluu iliyoiva yaani kati ya buluu na zambarau. Katika lugha za magharibi huitwa "indigo" kwa sababu asili yake iko Uhindi.
20231101.sw_2993_1
https://sw.wikipedia.org/wiki/Nili
Nili
Hutumika hasa kwa kutia rangi nguo. Inatoka kwa mimea fulani kiasili hasa kwenye mnili (Indigofera tinctoria). Siku hizi, rangi ya nili hutengenezwa mara nyingi kwa usanisi.