_id
stringlengths 15
22
| url
stringlengths 31
150
| title
stringlengths 1
86
| text
stringlengths 100
23.8k
|
---|---|---|---|
20231101.sw_2994_0
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Eduard%20Buchner
|
Eduard Buchner
|
Eduard Buchner (20 Mei 1860 – 13 Agosti 1917) alikuwa mwanakemia kutoka nchi ya Ujerumani. Hasa alichunguza kimeng'enya cha hamira. Mwaka wa 1907 alikuwa mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Kemia.
|
20231101.sw_2995_0
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Hans%20Buchner
|
Hans Buchner
|
Hans Ernst August Buchner (16 Desemba 1850 – 5 Aprili 1902) alikuwa daktari kutoka nchi ya Ujerumani. Hasa alichunguza virusi visababishavyo magonjwa na damu ya binadamu. Alikuwa kaka ya Eduard Buchner aliyepokea Tuzo ya Nobel ya Kemia mwaka wa 1907.
|
20231101.sw_2997_0
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Hans%20Buchner%20%28Mtunzi%29
|
Hans Buchner (Mtunzi)
|
Hans Buchner (26 Oktoba 1483 – Machi 1538) alikuwa mtungaji muziki na mpigakinanda kutoka nchi ya Ujerumani. Aliandika "Kitabu cha Msingi" (kwa Kijerumani: Fundamentbuch). Humo kitabuni alikusanya muziki kwa kinanda pamoja na maelezo ya upigakinanda.
|
20231101.sw_2998_0
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ernest%20Rutherford
|
Ernest Rutherford
|
Ernest Rutherford (30 Agosti 1871 – 19 Oktoba 1937) alikuwa mwanafizikia kutoka nchi ya Uingereza. Utafiti wake hasa uliweka msingi kwa fizikia ya kiini. Mwaka wa 1908 alikuwa mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Kemia.
|
20231101.sw_2999_0
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Vesuvio
|
Vesuvio
|
Ni volkeno hai iliyoendelea kuwa na milipuko mara kwa mara tangu mlipuko wake wa kwanza iliyojulikana mwaka 79 BK.
|
20231101.sw_2999_1
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Vesuvio
|
Vesuvio
|
Leo hii inaonekana kuwa ni volkeno yenye hatari sana kwa sababu baada ya muda bila milipuko mikubwa mazingira yake yamejaa watu katika eneo la jiji la Napoli, takriban milioni tatu.
|
20231101.sw_2999_2
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Vesuvio
|
Vesuvio
|
Ilipolipuka mwaka 79 BK iliharibu miji ya Pompei na Herkulaneo ikaua watu maelfu. Mlipuko huu una maarufu kwa sababu mwandishi Mroma Plinio aliutazama akaandika taarifa juu yake. Miji miwili iliyofunikwa na majivu ya Vesuvio ilifunuliwa tena katika karne ya 20 imetupa picha nzuri ya maisha ya Kiroma ya kale.
|
20231101.sw_3000_0
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Hifadhi%20ya%20Taifa%20ya%20Nyerere
|
Hifadhi ya Taifa ya Nyerere
|
Hifadhi ya Taifa ya Nyerere (awali: Selous, matamshi: "saluu") ni hifadhi ya taifa kubwa kuliko yote nchini Tanzania, pia ni kati ya hifadhi ya wanyama kubwa kabisa duniani. Hifadhi imeanzishwa mwaka wa 2019; kabla ya kupandishwa hadhi na kuwa hifadhi, ilikuwa pori tengefu lililojulikana kwa jina la Selous.
|
20231101.sw_3000_1
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Hifadhi%20ya%20Taifa%20ya%20Nyerere
|
Hifadhi ya Taifa ya Nyerere
|
Eneo lake ni la km² 54,600 katika mikoa ya Pwani, Morogoro, Lindi, Mtwara na Ruvuma. Eneo hilo ni kubwa kushinda nchi 70 duniani ikikadiriwa kuwa na eneo sawa na nchi ya Kostarika (Amerika ya Kati) na takribani mara mbili kuliko nchi ya Ubelgiji (Ulaya).
|
20231101.sw_3000_2
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Hifadhi%20ya%20Taifa%20ya%20Nyerere
|
Hifadhi ya Taifa ya Nyerere
|
Sehemu kubwa ya eneo iko katika hali ya asili bila kuvurugwa na shughuli za binadamu. Tangu mwaka 1982 imeingizwa katika orodha ya UNESCO ya Urithi wa Dunia. Tena mwezi Juni 2014 imeingizwa kwenye orodha ya UNESCO ya hifadhi zenye hatari ya kupotewa na uhai wake.
|
20231101.sw_3000_3
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Hifadhi%20ya%20Taifa%20ya%20Nyerere
|
Hifadhi ya Taifa ya Nyerere
|
Jina la Hifadhi ya Taifa ya Nyerere limechaguliwa kwa heshima ya mwanzilishi wa Taifa na Rais wa kwanza wa Tanzania, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
|
20231101.sw_3000_4
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Hifadhi%20ya%20Taifa%20ya%20Nyerere
|
Hifadhi ya Taifa ya Nyerere
|
Jina la awali lilitokana na Mwingereza Frederick Selous aliyekuwa mwindaji wakati wa kuanzishwa kwa ukoloni katika Afrika ya Kusini na Mashariki na ambaye aliuawa katika Tanzania ya leo akiwa mwanajeshi wakati wa Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia.
|
20231101.sw_3000_5
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Hifadhi%20ya%20Taifa%20ya%20Nyerere
|
Hifadhi ya Taifa ya Nyerere
|
Hifadhi ya Taifa ya Nyerere ina aina kadhaa za wanyamapori wanaopatikana ndani yake: kati yao ni: simba, nyumbu, twiga, pundamilia, kiboko, kifaru, swala, fisi, mbwa mwitu wa Afrika, na idadi kubwa ya mamba wanaopatikana katika mto Rufiji. Hao wote wanaweza kuonekana wakati wa kutembelea hifadhi hii. Hapo awali hifadhi ya Taifa ya Nyerere (Selous) ilikuwa nyumbani kwa tembo wengi sana lakini kwa sababu ya ujangili uliokithiri idadi imepungua sana.
|
20231101.sw_3000_6
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Hifadhi%20ya%20Taifa%20ya%20Nyerere
|
Hifadhi ya Taifa ya Nyerere
|
Safari kwa kutumia ndege: Hifadhi ya kitaifa ya Nyerere inaweza kufikika kwa urahisi kwa usafiri wa anga na ndege yoyote inayounganisha kutoka Ruaha na Dar es Salaam. Ni takriban dakika 90 kutoka Hifadhi ya Taifa ya Ruaha na dakika 45 kutoka kwa jiji la Dar es Salaam.
|
20231101.sw_3000_7
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Hifadhi%20ya%20Taifa%20ya%20Nyerere
|
Hifadhi ya Taifa ya Nyerere
|
Safari kwa kutumia barabara; unaweza pia kufika kwa barabara na safari inayounganisha kutoka Dar es salaam ambayo au kupitia Hifadhi ya taifa ya Mikumi na kisha ambapo unaweza kuingilia geti la matambwe. Safari hii ambayo inaweza kuchukua kama masaa 4 kufika umbali wa kilomita 220 ni chaguo jingine.
|
20231101.sw_3000_8
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Hifadhi%20ya%20Taifa%20ya%20Nyerere
|
Hifadhi ya Taifa ya Nyerere
|
Safari kwa kutumia njia ya reli; unaweza kutumia usafiri wa reli, kwa reli ya Tanzania na Zambia TAZARA huanza kutoka Dar Es Salaam na kukuchukua hadi Matambwe, ambapo unaweza kupata gari kwa safari yako ya utalii. .
|
20231101.sw_3002_0
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Nagib%20Mahfuz
|
Nagib Mahfuz
|
Nagib Mahfuz (1911 - 2006) (kwa Kiarabu: نجيب محفوظ) alikuwa mwandishi nchini Misri aliyepokea Tuzo ya Nobel mwaka 1988 akiwa mshindi wa pili kutoka Afrika aliyepokea tuzo hiyo. Katika muda wa miaka 70 ya kazi alitunga riwaya 34, hadithi fupi zaidi ya 350, makumi ya mswada andishi ya filamu na tamthiliya 5. Nyingi za kazi zake zimechukuliwa kuwa filamu nchini Misri na nje ya Misri.
|
20231101.sw_3002_1
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Nagib%20Mahfuz
|
Nagib Mahfuz
|
Mahfuz alizaliwa 11 Desemba 1911 katika familia ya wastani ya Waislamu kwenye eneo la Gamaliya mjini Kairo. Wazazi walimpa jina kulingana na profesa Naguib Pasha Mahfouz (1882–1974) tabibu mashuhuri Mkopti aliyesimamia kuzaliwa kwake. Katika familia yake alikuwa mtoto wa saba na mdogo kati ya akina kaka wanne na akina dada wawili.
|
20231101.sw_3002_2
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Nagib%20Mahfuz
|
Nagib Mahfuz
|
Familia iliishi kwanza katika mtaa wa Bayt al-Qadi wa eneo la Gamaliya kwenye mji wa kale wa Kairo. 1924 walihamia Abbaseya iliyokuwa mtaa mpya upande wa kaskazini ya mji wa kale. Maeneo yote mawili yalirudia baadaye katika masimulizi na riwaya zake.
|
20231101.sw_3002_3
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Nagib%20Mahfuz
|
Nagib Mahfuz
|
Babake Abdel-Aziz Ibrahim alikuwa mtumishi wa serikali na Mahfouz hatimaye alifuata mfano wake baada ya kumaliza shule na chuo. Mamake Fatimah alikuwa binti wa shehe kwenye chuo kikuu cha Al-Azhar. Hata kama yeye mwenyewe hakuweza kusoma wala kuandika alienda mara kwa mara pamoja na mtoto Mahfouz kutembelea na kuona mahali pa utamaduni kama Makumbusho ya Misri na Piramidi za Giza.
|
20231101.sw_3002_4
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Nagib%20Mahfuz
|
Nagib Mahfuz
|
Familia ya Mahfouz walikuwa Waislamu waaminifu na ulezi wa Mahfouz ulifuata kanuni za dini hii. Baadaye aliona ya kwamba msimamo katika familia yake ulikuwa kali kiasi akashangaa alipokuwa mzee: Usingefikiri ya kwamba siku moja msanii atatoka katika familia hii".
|
20231101.sw_3002_5
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Nagib%20Mahfuz
|
Nagib Mahfuz
|
Mahfouz alipokuwa na miaka 7 alishuhudia mapinduzi ya Misri ya 1919 akitazama kutoka dirisha ya nyumba jinsi gani wanajeshi walivyofyatulia risasi dhidi ya wanaume na wanawake walioandamana. Alisema baadaye "tukio moja lililonishtusha na kuvunja hisia ya usalama katika utoto wangu lilikuwa mapinduzi ya 1919".
|
20231101.sw_3002_6
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Nagib%20Mahfuz
|
Nagib Mahfuz
|
Mahfouz alianza kusoma mapema akiathiriwa na Hafiz Najib, Taha Hussein na Salama Moussa aliyekuwa mfuasi wa shirika la kisoshalisti la Fabian Society.
|
20231101.sw_3002_7
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Nagib%20Mahfuz
|
Nagib Mahfuz
|
Baada ya kumaliza shule ya sekondari Mahfouz alisoma falsafa kwenye chuo kikuu cha Kairo alipomaliza kwa cheti ya BA mwaka 1934. Alianza tasnifa ya MA lakini aliiacha baada ya mwaka mmoja akaamua kufuata uandishi kama wito wake.
|
20231101.sw_3002_8
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Nagib%20Mahfuz
|
Nagib Mahfuz
|
Alitafuta ajira katika utumishi wa serikali akifuata nyayo za babake lakini wakati huohuo alianza pia kuchangia taarifa na hadithi fupi katika magazeti mbalimbali kama vile Al-Risala, Al-Hilal na Al-Ahram.
|
20231101.sw_3002_9
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Nagib%20Mahfuz
|
Nagib Mahfuz
|
Ajira yake ya kwanza ilikuwa kama karani kwenye chuo kikuu, tangu 1938 katika wizara ya waqf. 1945 aliomba kuhamishwa kwenda maktaba ya makumbusho ya Sultan Al-Ghuri. Hapa alichukua nafasi ya kufanya mahojiano na wakazi wa mtaa penye maktaba. Aliendelea na wajibu mbalimbali katika wizara ya utamaduni.
|
20231101.sw_3002_10
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Nagib%20Mahfuz
|
Nagib Mahfuz
|
Katika muda wa miaka 70 ya kazi Mahfouz alitunga riwaya 34, hadithi fupi zaidi ya 350, makumi ya mswada andishi ya filamu na tamthiliya 5. Nyingi za kazi zake zimechukuliwa kuwa filamu nchini Misri na nje ya Misri.
|
20231101.sw_3002_11
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Nagib%20Mahfuz
|
Nagib Mahfuz
|
Katika miaka ya 1940 alianza kusimulia habari za Misri ya kisasa. Riwaya yake ya 1959 "Watoto wa mtaa wetu" ilisababisha ugomvi na wataalamu waislamu waliodai inakashifu imani. Riwaya inatoa mfano wa historia ya binadamu wakiwemo watu wanaofanana na Adamu, Musa, Isa na Mohamad. Kitabu kilitolewa kimilango katika gazeti, lakini upinzani wa wataalamu Waislamu uliwalazimisha wahariri kusimamisha riwaya. Hadi leo haikuchapishwa kwa lugha ya Kiarabu katika nchi ya Misri ingawa inapatikana kwa Kiingereza pia toleo la Kiarabu kutoka Lebanon inapatikana kwa siri.
|
20231101.sw_3002_12
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Nagib%20Mahfuz
|
Nagib Mahfuz
|
Riwaya yake mashuhuri zaidi ni "Thelathiya Alqahira" (Riwaya ya Kairo kwa sehemu tatu, ing. Cairo trilogy) anamosimulia maisha ya vizazi vitatu vya familia mbalimbali mjini Kairo kuanzia Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia hadi mapinduzi ya 1952 iliyomfukuza Mfalme Farouk.
|
20231101.sw_3002_13
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Nagib%20Mahfuz
|
Nagib Mahfuz
|
sehemu za riwaya zake zilitolewa mlango kwa mlango katika gazeti Al-Ahram na kufikia wasomaji wengi sana. Alipopokea Tuzo ya Nobel ya Fasiki kulikuwa na riwaya chache tu zilizotafsiriwa hadi wakati ule kwa lugha za Ulaya.
|
20231101.sw_3002_14
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Nagib%20Mahfuz
|
Nagib Mahfuz
|
Mwaka 1989 shehe Mmisri Omar Abdul-Rahman alitamka mbele ya wanahabari ya kwamba heri Mahfuz angeadhibiwa wakati ule. Tamko hili lilisababisha jaribio la Waislamu wakali la kumwua Mahfuz. Hadi kifo chake aliishi chini ya ulinzi wa Polisi.
|
20231101.sw_3002_15
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Nagib%20Mahfuz
|
Nagib Mahfuz
|
Mockery of the Fates (1939) عبث الأقدار. His first full-length novel, translated title in English Khufu's Wisdom.
|
20231101.sw_3005_0
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kreta
|
Kreta
|
Kreta (pia kasoko, kwa Kiingereza: crater) ni uwazi kwenye ardhi uliotokana na mlipuko au mshtuko wa kugongwa na gimba.
|
20231101.sw_3005_1
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kreta
|
Kreta
|
Kreta ina umbo la duara; katikati ni kama shimo na ukingo wake unainuliwa juu ya uwiano wa mazingira yake. Duniani kreta zinapatikana mara nyingi kutokana na milipuko ya volkeno au milipuko mingine. Kwenye sayari au miezi yenye uso thabiti kuna kreat nyingi kama matokeo ya kugongwa na magimba kutoka anga-nje. Kwa mfano kwenye Mwezi wa Dunia kuna kreta nyingi zilizosababishwa na migongano ya asteroidi. Pigo la kitu kigumu linarusha mata iliyopo mahali pa mgongano ikae pembeni ya shimo hilo kwa umbo la ukingo wa mviringo.
|
20231101.sw_3005_2
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kreta
|
Kreta
|
Duniani kreta zilizosababishwa na mishtuko ya aina hiyo husawazishwa baada ya muda fulani kutokana na mmomonyoko unaosababishwa na mvua na upepo; kwenye magimba pasipo angahewa kama Mwezini zinabaki kwa muda mrefu.
|
20231101.sw_3005_3
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kreta
|
Kreta
|
kreta ya dharuba (mgongano) kutokana na kugongwa kwa uso la gimba na gimba nyingine, kwa mfano kama Dunia, sayari nyingine au Mwezi imegongwa na meteoridi au asteroidi
|
20231101.sw_3005_4
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kreta
|
Kreta
|
Kreta kubwa zaidi duniani zilisababishwa na asteroidi zilizogonga Dunia yetu. Kreta kubwa iliyojulikana hadi mwaka 2006 ilikuwa kreta ya Vredefort nchini (Afrika Kusini) yenye umbo la yai la urefu wa km 320 na upana wa km 180.
|
20231101.sw_3005_5
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kreta
|
Kreta
|
Mwaka 2006 wataalamu waligundua kreta kubwa zaidi yenye kipenyo cha km 500 huko Antarktika katika picha zilizopigwa kutoka angani. Iko chini ya barafu ya Antarktika katika eneo la Wilkes Land inatajwa kwa kifupi cha WLIC (ing.: Wilkes Land impact crater). Kasoko ya WLIC inaaminiwa imesababishwa na asteroidi yenye kipenyo cha takriban km 5.
|
20231101.sw_3006_0
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Chamko%20la%20volkeno
|
Chamko la volkeno
|
Chamko la volkeno hutokea kama lava (zaha) na gesi kutoka vilindi vya ganda la Dunia zinatoka nje ya ardhi. Kutegemeana na tabia ya magma (mwamba wa joto katika hali ya kiowevu) na mazingira chamko hilo linaweza kuwa kama mlipuko au kama kumwaga kwa lava ya moto inayosambaa kwa utaratibu zaidi.
|
20231101.sw_3006_1
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Chamko%20la%20volkeno
|
Chamko la volkeno
|
Volkeno hupatikana hasa pale ambapo vipande vya ganda la dunia vinaachana au kusukumana. Kuna pengo ambako magma joto kutoka ndani ya dunia inapanda juu kufika usoni mwake. Volkeno hutokea pia juu ya sehemu ya joto (hotspot) inayopanda juu kutoka kiini cha Dunia kupitia koti la Dunia.
|
20231101.sw_3006_2
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Chamko%20la%20volkeno
|
Chamko la volkeno
|
Pale ambapo lava inatoka ardhini inapoa na kuganda; hivyo inajenga ukuta kuviringisha shimo linapotoka; kwa njia hiyo kutoka kwa lava inaweza kujenga milima inayokua na kuwa mirefu yenye njia ya lava ndani yake.
|
20231101.sw_3006_3
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Chamko%20la%20volkeno
|
Chamko la volkeno
|
Volkeno nyingi hutoa zaha yake mara kwa mara. Hii inawezekana kama njia ya kasoko yake ni wazi. Aina hiyo ya volkeno inaweza kuachana na nguvu yake mara kwa mara. Haielekei kuwa na mlipuko mkali sana isipokuwa kama maji yameingia katika chumba cha magma (soma chini).
|
20231101.sw_3006_4
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Chamko%20la%20volkeno
|
Chamko la volkeno
|
Kama volkeno imelala kwa muda mrefu njia ya kasoko yake inafungwa kwa sababu zaha ndani yake imeganda kuwa mwamba imara. Ikitokea ya kwamba joto la chini linaongezeka tena magma inaanza kupanda juu lakini haiwezi kutoka nje. Inakwama chini ya volkeno na shindikizo ndani yake linaongezeka. Kama shindikizo linazidi husababisha mlipuko na kutoka ghafla kwa lava (zaha) na gesi nyingi mara moja. Ukali unaongezeka kama maji ya chini ya ardhi yanaingia katika chumba cha magma chini ya volkeno.
|
20231101.sw_3006_5
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Chamko%20la%20volkeno
|
Chamko la volkeno
|
Milipuko mikubwa ya aina hiyo iliwahi kurusha mlima wote hewani kwa mfano mlima wa Krakatau mwaka 1883 BK. Mlima wenye urefu wa mita 813 juu ya UB ulipotea kabisa pamoja na kisiwa chake.
|
20231101.sw_3006_6
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Chamko%20la%20volkeno
|
Chamko la volkeno
|
Hatari nyingine ya milipuko ni kiasi kikubwa cha gesi na majivu pamoja na tefra, yaani mawe na miamba ya moto. Gesi na majivu yenye halijoto hadi 800 °C zinaweza kusambaa haraka sana zikiteketeza kila kitu njiani. Pia gesi zinazotoka zinaweza kuwa za sumu. Wakati wa mlipuko wa Vesuvio watu wengi wa Pompei waliuawa na gesi pamoja na majivu.
|
20231101.sw_3008_0
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kamerun%20%28mlima%29
|
Kamerun (mlima)
|
Kamerun ni volkeno hai na mlima mkubwa nchini Kamerun wenye kimo cha m 4095 juu ya UB. Majina mengine ni Fako (jina la kilele cha juu) au Mongo ma Ndemi ("Mlima Mkubwa").
|
20231101.sw_3008_1
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kamerun%20%28mlima%29
|
Kamerun (mlima)
|
Milipuko imeripotiwa katika miaka 1650, 1807, 1825, 1838, 1852, 1865, 1866, 1871, 1909, 1922, 1925, 1954, 1959, 1982 na 1999 BK.
|
20231101.sw_3008_2
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kamerun%20%28mlima%29
|
Kamerun (mlima)
|
Kuna uwezekano ya kwamba tayari baharia Hanno wa Karthago alimaanisha mlima wa Kamerun alipoeleza habari za mlima wa "Gari la Miungu" uliotema moto kwa mwisho wa safari yake ya Afrika ya Magharibi mnamo mwaka 570 KK.
|
20231101.sw_3011_0
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Rungwe%20%28mlima%29
|
Rungwe (mlima)
|
Mlima Rungwe ni volkeno iliyozimika ya Tanzania kusini magharibi ikikadiriwa ya kwamba mlipuko wake wa mwisho ulitokea mnamo miaka 2000 hadi 5000 iliyopita.
|
20231101.sw_3011_1
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Rungwe%20%28mlima%29
|
Rungwe (mlima)
|
Mlima unasimama juu ya ncha ya kaskazini ya Ziwa Nyasa. Upande wa kusini-mashariki wa mlima hupokea usimbishaji wa mm 3,000 kwa mwaka ambao ni wa juu kabisa katika Tanzania.
|
20231101.sw_3012_0
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kaldera
|
Kaldera
|
Kaldera ni shimo kubwa ya mviringo iliyotokea wakati volkeno inaporomoka ndani yake baada ya mlipuko.
|
20231101.sw_3012_1
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kaldera
|
Kaldera
|
Kaldera hutokea kama chumba cha magma chini ya volkeno kimetoa nje yaliyomo yake yote na kuacha uwazi mkubwa (nafasi) ardhini. Mlima juu yake unaporomoka ndani ya nafasi hiyo na kuacha shimo juu yake: kaldera. Neno la kaldera lina asili ya Kihispania kumaanisha "sufuria" au "bakuli".
|
20231101.sw_3012_2
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kaldera
|
Kaldera
|
Kaldera inaweza kupatikana ndani ya kelele cha mlima. Kama kuporomoka kulitokea vikali sana mara nyingi mlima mwenyewe ulipotea ukaacha tu dalili za ukingo wake.
|
20231101.sw_3012_3
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kaldera
|
Kaldera
|
Kaldera kubwa kabisa duniani yenye ukingo usiovunjika au kukatika ni Ngorongoro (Tanzania) yenye kipenyo wa 27 km.
|
20231101.sw_3013_0
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kreta%20ya%20volkeno
|
Kreta ya volkeno
|
Zaha na gesi za joto zinapotoka ardhini kuwa volkeno husababisha kutokea kwa kreta. Milima ya volkeno huwa na kasoko kwenye kelele mara nyingi pia na kasoko kando.
|
20231101.sw_3013_1
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kreta%20ya%20volkeno
|
Kreta ya volkeno
|
Shimo linaweza kuonekana kubwa zaidi kama volkeno imeporomoka ndani yake yenyewe halafu huitwa "kaldera".
|
20231101.sw_3015_0
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kipenyo
|
Kipenyo
|
Kwa lugha nyingine kipenyo ni pia umbali kati ya nukta mbili kwenye mzingo wa duara zilizopo kwenye mstari ulionyooka unaopita kwenye kitovu cha duara.
|
20231101.sw_3017_0
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Selsiasi
|
Selsiasi
|
Selsiasi (sentigredi, Celsius) ni kipimo cha halijoto kinachotumika zaidi duniani. Alama yake ni °C.
|
20231101.sw_3017_1
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Selsiasi
|
Selsiasi
|
Kipimo hiki hutumia skeli ya vizio 100 kati ya 0 °C na 100 °C. 0 °C ni halijoto ya kuganda kwa maji kuwa barafu. 100 °C ni halijoto ya maji kuchemka, yote kwa shindikizo kawaida la hewa yaani takriban shindikizo la hewa linalopatikana kando la bahari.
|
20231101.sw_3017_2
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Selsiasi
|
Selsiasi
|
Kipimo hiki kilianzishwa na Msweden Anders Celsius (1701 - 1744). Yeye aliita halijoto ya kuchemka kwa maji kama 0 °C na halijoto ya kuganda kuwa 100 °C. Namna ya kuandika ilibadilishwa baadaye kinyume.
|
20231101.sw_3017_3
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Selsiasi
|
Selsiasi
|
Selsiasi ni kipimo kinachotumika zaidi kimataifa katika maisha ya kawaida. Kisayansi vipimo vya Kelvini vimekuwa kawaida. Siku hizi ufafanuzi wa kisayansi ya Selsiasi ni ya kuwa kizio kimoja cha Selsiasi ni sehemu ya 1/273.16 ya tofauti kati ya sifuri halisi (=0 K au Kelvini sifuri) na kiwango utatu cha maji (maji kubadilika kutoka barafu kuwa kiowevu (majimaji).
|
20231101.sw_3017_4
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Selsiasi
|
Selsiasi
|
Skeli ya Selsiasi imelinganishwa na skeli ya Kelvini yaani kizio kimoja cha Kelvini ni sawa na kizio kimoja cha Selsiasi.
|
20231101.sw_3018_0
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kiwango%20utatu
|
Kiwango utatu
|
Kiwango utatu ni kiwango cha maji au dutu nyingine inapoweza kutokea mahali pamoja katika hali mango, kiowevu na gesi (kwa mfano wa maji: barafu, majimaji na mvuke). Kiwango hiki kinategemea halijoto na shindikizo.
|
20231101.sw_3018_1
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kiwango%20utatu
|
Kiwango utatu
|
Kiwango utatu cha maji ni kiwango cha kukadiria skeli ya selsiasi au sentigredi (273.16 K au 0.01 °C).
|
20231101.sw_3019_0
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/K
|
K
|
K ni herufi ya 11 katika katika alfabeti ya Kilatini ambayo ni pia mwandiko wa Kiswahili cha kisasa. Asili yake ni Kappa ya alfabeti ya Kigiriki.
|
20231101.sw_3019_1
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/K
|
K
|
Asili ya herufi K ni katika miandiko iliyotangulia alfabeti ya Kilatini. Waroma walipokea mwandiko kutoka alfabeti ya Kigiriki kupitia alfabeti za Kiitalia za awali kama Kietruski. Wagiriki walipokea kutoka Wafinisia.
|
20231101.sw_3019_2
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/K
|
K
|
Wafinisia walikuwa na kaf iliyokuwa kiasili picha iliyorahisishwa ya kofi (au: uso wa mkono) wakitumia alama tu kwa sauti ya "k" na kuiita kwa neno lao kwa kofi "kaf". Wagiriki walichukua alama hiyo na kuiita "kapha" bila kujali maana asilia ya "kofi" ilikuwa sauti tu ya "k".
|
20231101.sw_3019_3
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/K
|
K
|
Waitalia ya kwanza wakaendelea kutumia alama kwa aina ya "k". Waroma mwanzoni hawakutumia alama hii kwa sababu hawakuwa na "k" jinsi Waetruski walivyoitamka. Kwa sauti ya "k" ya kawaida Waroma walitumia C. Lakini baadaye baada ya Roma kutwaa na kutawala Ugiriki walianza kutumia maneno mengi ya Kigiriki wakaingiza K ya Kigiriki katika alfabeti yao wakaitumia wka maneno ya kigeni tu.
|
20231101.sw_3021_0
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kelvini
|
Kelvini
|
Kiwango chake kinaanza kwenye sifuri halisi (= -273.15 °C) pasipo mwendo wowote wa molekuli. Kizio kimoja cha Kelvini ni sehemu ya 1/273.16 ya tofauti kati ya sifuri halisi (=0 K) na kiwango utatu cha maji (+0.01 °C).
|
20231101.sw_3021_1
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kelvini
|
Kelvini
|
Skeli ya Kelvini ililinganishwa na skeli ya selsiasi yaani kizio kimoja cha Kelvini ni sawa na kizio kimoja cha Selsiasi.
|
20231101.sw_3021_2
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kelvini
|
Kelvini
|
Jina limetokana na mwanafizikia Mwingereza William Thomson aliyekuwa na cheo cha Lord Kelvin (1824–1907).
|
20231101.sw_3022_0
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kirimba%20%28visiwa%29
|
Kirimba (visiwa)
|
Visiwa vya Kirimba (Kireno: Quirimbas, Ilhas de Querimba) ni funguvisiwa katika Bahari Hindi mbele ya mwambao wa Msumbiji wa kaskazini, kusini ya rasi ya Delgado. Inafuata mwendo wa pwani kwa umbali wa 180 km hadi mji wa Pemba. Umbali na pwani ni kati ya 12 na 20 km.
|
20231101.sw_3022_1
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kirimba%20%28visiwa%29
|
Kirimba (visiwa)
|
Idadi ya visiwa ni takriban 50. Vingi ni vidogo havikaliwi na watu. Kisiwa kikuu ni Ibo penye makao ya utawala wa Wilaya ya Ibo inayotawala funguvisiwa yote. Visiwa ni sehemu ya jimbo la Cabo Delgado. Wilaya ina wakazi 7.061 na eneo la nchi kavu visiwani la 48 km². Kati ya visiwa ni Ibo, Kirimba (Quirimba), Matemo, Quilaluia, Quisiva na Rolas.
|
20231101.sw_3022_2
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kirimba%20%28visiwa%29
|
Kirimba (visiwa)
|
Sehemu ya kusini ya funguvisiwa pamoja na nchi ya bara karibu nayo imekuwa hifadhi ya taifa ya Kirimba.
|
20231101.sw_3022_3
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kirimba%20%28visiwa%29
|
Kirimba (visiwa)
|
Kihistoria kisiwa cha Kerimba (Quirimba) kilikuwa muhimu zaidi na kulipa jina lake kwa funguvisiwa. Funguvisiwa ilikuwa chini ya athira ya kisiasa ya Kilwa ikiwa na sultani yake ya pekee. Uislamu ulifika zamani visiwani lakini tarehe haijulikani.
|
20231101.sw_3022_4
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kirimba%20%28visiwa%29
|
Kirimba (visiwa)
|
Wareno walivamia visiwa mnamo mwaka 1522 kwa sababu ya biashara ya meno ya ndovu. Padre João dos Santos alifika kuhubiri Ukristo mwaka 1593 alikuta tabaka ya juu walikuwa Waislamu na watu wa kawaida wakifuata dini za jadi. Kuna taarifa ya mwaka 1769 juu ya malamiko ya Wareno dhidi ya Waarabu na Waswahili wa visiwa kuwa walifanya biashara ya watumwa na meno ya ndovu na Waswahili waislamu wa kaskazini badala ya Wareno wenyewe wa Msumbiji.
|
20231101.sw_3022_5
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kirimba%20%28visiwa%29
|
Kirimba (visiwa)
|
Hadi karne ya 19 visiwa vya Kirimba vilikuwa kituo muhimu cha biashara ya watumwa. Kuna kubukumbu ya mwaka 1860 kuhusu mzigo wa watumwa 846 waliofika Mauritius kutoka visiwa vya Kirimba.
|
20231101.sw_3022_6
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kirimba%20%28visiwa%29
|
Kirimba (visiwa)
|
Jina la visiwa liliwahi kuandikwa na Wareno kama: Queriba, Quiriba, Querimba, Quirimba, Carimba, Cerimba, Corimba, Querimbas au Quirimbas
|
20231101.sw_3022_7
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kirimba%20%28visiwa%29
|
Kirimba (visiwa)
|
en: Nunn, Slavery, Institutional Development,and Long-Run Growth in Africa, 1400–2000 p. 7 slavery appendix.pdf
|
20231101.sw_3026_0
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mbeya%20%28mji%29
|
Mbeya (mji)
|
Jiji la Mbeya ni mji mkubwa kusini-magharibi mwa Tanzania yenye hadhi ya jiji yenye Postikodi namba 53100.
|
20231101.sw_3026_1
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mbeya%20%28mji%29
|
Mbeya (mji)
|
Mji umeenea katika bonde kati ya safu za milima ya Mbeya na milima ya Uporoto. Mlima mkubwa unaoonekana kutoka mjini ni Mlima wa Mbeya (Mbeya Peak) wenye urefu wa m 2818.
|
20231101.sw_3026_2
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mbeya%20%28mji%29
|
Mbeya (mji)
|
Eneo la mji ni kati ya m 1600 kitovuni na m 1900 au zaidi juu ya UB kwenye mitelemko ya mlima Loleza.
|
20231101.sw_3026_3
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mbeya%20%28mji%29
|
Mbeya (mji)
|
Hali ya hewa haina joto kali kutokana na kimo. Wakati wa Juni-Julai halijoto wakati wa usiku inaweza kushuka chini hadi 0 °C, mlimani hata chini zaidi.
|
20231101.sw_3026_4
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mbeya%20%28mji%29
|
Mbeya (mji)
|
Mvua zinaanza mwezi Novemba hivyo ni wakati wa kupanda. Kwa kawaida mvua zinasimama tena Januari-Februari na kunyesha kwa wingi Machi-Aprili.
|
20231101.sw_3026_5
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mbeya%20%28mji%29
|
Mbeya (mji)
|
Uti wa mgongo wa mji ni barabara kuu ya TANZAM inayounganisha sehemu za nje kati ya Uyole na Mbalizi.
|
20231101.sw_3026_6
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mbeya%20%28mji%29
|
Mbeya (mji)
|
Jina la Mbeya limetokana na neno la Kisafwa "Ibheya" ambayo maana yake ni chumvi, kwani miaka mingi wafanyabiashara walikuwa wanafika mahali hapo kubadilishana mazao yao kwa chumvi.
|
20231101.sw_3026_7
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mbeya%20%28mji%29
|
Mbeya (mji)
|
Mlima mkubwa ulio karibu ulijulikana kwa jina la "Mbeya" wakati wa ukoloni wa Kijerumani, na mji ulipokea baadaye jina kutokana na mlima huu.
|
20231101.sw_3026_8
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mbeya%20%28mji%29
|
Mbeya (mji)
|
Mji wa kisasa wa Mbeya ulianzishwa na wakoloni Waingereza mnamo mwaka 1927. Wakati ule dhahabu ilianza kupatikana mlimani karibu na Mbeya hadi Chunya.
|
20231101.sw_3026_9
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mbeya%20%28mji%29
|
Mbeya (mji)
|
Mji ulianzishwa katika sehemu zinazoitwa bado Uhindini, Uzunguni na Majengo. Mji ulipangwa kufuatana na kawaida ya miji wa kikoloni ya Afrika ya Mashariki kuwa na sehemu tatu:
|
20231101.sw_3026_10
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mbeya%20%28mji%29
|
Mbeya (mji)
|
Uzunguni ni sehemu ya nyumba za Wazungu na karibu na ofisi za serikali (District Officer, polisi, mahakama)
|
20231101.sw_3026_11
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mbeya%20%28mji%29
|
Mbeya (mji)
|
Kanisa la Anglikana lililokuwa dhehebu rasmi la Uingereza lipo chini ya Uzunguni na karibu na ofisi za kiserikali (zinazoelekea siku hizi kuhamishwa kwenda Foresti) kama Mkuu wa Mkoa na mahakama. Kanisa hili ni jengo dogo kwa sababu lilipangwa kwa kundi dogo la maafisa na wafanyabiashara pamoja na wakulima Waingereza wa Mbeya.
|
20231101.sw_3026_12
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mbeya%20%28mji%29
|
Mbeya (mji)
|
Kanisa la mjini la Moravian, ambalo ni dhehebu la Kikristo asilia la Mbeya liko Majengo iliyokuwa sehemu kwa Waafrika. Kati ya Waingereza hawakuwepo Wamoravian.
|
20231101.sw_3026_13
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mbeya%20%28mji%29
|
Mbeya (mji)
|
Kanisa Kuu Katoliki lilihudumia Wazungu wachache, hasa Waeire, kati ya wakoloni pamoja na Wahindi kutoka Goa na pia Waafrika: kwa hiyo iko kati ya Uzunguni na Uhindini karibu na Majengo.
|
20231101.sw_3026_14
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mbeya%20%28mji%29
|
Mbeya (mji)
|
Mji uliendelea kupanuka pande zote. Barabara kuu ya TANZAM inaunganisha sehemu za nje kati ya Uyole na Mbalizi.
|
20231101.sw_3026_15
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mbeya%20%28mji%29
|
Mbeya (mji)
|
Siku hizi sehemu kubwa ya wakazi ni Wakristo, hasa wafuasi wa Kanisa Katoliki, Kanisa la Moravian na Kanisa la Kilutheri. Makundi makubwa mjini ni Wasafwa (wenyeji) na Wanyakyusa waliohamia kutoka Rungwe. Wanyakyusa ndio waliotangulia kuleta Ulutheri mjini.
|
20231101.sw_3026_16
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mbeya%20%28mji%29
|
Mbeya (mji)
|
Mbeya ni njiapanda ya njia mbalimbali muhimu: Barabara kuu ya lami kutoka Dar es Salaam (km 850) hugawanya hapa kwenda Malawi – Msumbiji kupitia Tukuyu/Rungwe, na kwenda Zambia – Afrika Kusini kupitia Tunduma/Mbozi.
|
20231101.sw_3026_17
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mbeya%20%28mji%29
|
Mbeya (mji)
|
Vilevile njia ya reli ya TAZARA hupita Mbeya kuelekea Zambia. Kuna ghala kubwa kwa ajili ya mizigo ya Malawi inayofikishwa kwa reli kutoka Dar es Salaam bandarini ikihamishwa kwa malori kwenda Malawi.
|
20231101.sw_3026_18
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mbeya%20%28mji%29
|
Mbeya (mji)
|
Mbeya imekuwa na uwanja wa ndege mdogo usiokuwa na huduma ya kawaida kwa muda mrefu. Lakini kuna mipango ya kujenga uwanja mpya huko Songwe zipatazo km 40 kufuata njia ya kwenda Zambia.
|
20231101.sw_3026_19
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mbeya%20%28mji%29
|
Mbeya (mji)
|
Tangu miaka ya 1990 kitovu cha mji kinahamishwa kutoka eneo la zamani kwenda karibu na barabara kuu ya Dar es Salaam – Zambia.
|
20231101.sw_3026_20
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mbeya%20%28mji%29
|
Mbeya (mji)
|
Mbeya ni mji wa nne kwa ukubwa nchini Tanzania. Idadi ya wakazi imehesabiwa kuwa 385,279 katika sensa ya mwaka 2012. Wengine 300,000 hivi wanaishi katika mazingira karibu na Mbeya mjini.
|
Subsets and Splits
No community queries yet
The top public SQL queries from the community will appear here once available.