_id
stringlengths 15
22
| url
stringlengths 31
150
| title
stringlengths 1
86
| text
stringlengths 100
23.8k
|
---|---|---|---|
20231101.sw_3026_21
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mbeya%20%28mji%29
|
Mbeya (mji)
|
Kiasili Mbeya ilikuwa eneo la Wasafwa. Siku hizi sehemu kubwa ya wakazi wanaweza kuwa mchanganyiko wa Wasafwa pamoja na makabila ya Wanyakyusa kutoka wilaya za Rungwe na Kyela, Wanyiha kutoka Mbozi, Wandali kutoka Ileje na Wakinga kutoka Makete.
|
20231101.sw_3026_22
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mbeya%20%28mji%29
|
Mbeya (mji)
|
Viwanda mbalimbali vilianzishwa, lakini havikufaulu sana. Kuna viwanda kwa mfano Zana za kilimo, Highland Soap, Mbeya Textiles. Mbeya Ceramics iliporomoka kitambo.
|
20231101.sw_3026_23
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mbeya%20%28mji%29
|
Mbeya (mji)
|
Chuo Kikuu Teofilo Kisanji ambacho ni chuo kikuu cha Kanisa la Moravian Tanzania kinachotoa kozi za ualimu na teolojia tangu mwaka 2005. Kilitanguliwa na chuo cha Motheco.
|
20231101.sw_3026_24
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mbeya%20%28mji%29
|
Mbeya (mji)
|
Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya (MUST) ambacho zamani kilijulikana kama Mbeya Technical College (MTC) kilichopo eneo la Iyunga, Mbeya
|
20231101.sw_3026_25
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mbeya%20%28mji%29
|
Mbeya (mji)
|
Chuo cha Kilimo Uyole (Agricultural Research Institute -ARI- Uyole) ambacho ni taasisi ya uchunguzi wa kisayansi pamoja na chuo.
|
20231101.sw_3026_26
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mbeya%20%28mji%29
|
Mbeya (mji)
|
Chuo Kikuu cha Mzumbe, Chuo cha Kampasi ya Mbeya ambacho ni tawi la Chuo Kikuu Mzumbe kilichopo Morogoro
|
20231101.sw_3027_0
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Tukuyu
|
Tukuyu
|
Tukuyu ilianzishwa mnamo 1901 wakati wa ukoloni wa Kijerumani. Wajerumani waliwahi kuunda kituo cha kwanza pale Lumbila ya leo, kando ya Ziwa Nyasa wakakiita "Langenburg" kwa heshima ya kabaila na mwanasiasa Mjerumani. Langenburg iliendelea kuwa makao makuu ya Mkoa wa Langenburg lakini ilikuwa na matatizo machoni pa Wajerumani walioona tabianchi haifai kwao kiafya. Mwaka 1900 waliamua kuhamisha makao makuu sehemu iliyokuwa baridi zaidi na kujulikana kwa jina Tukuyu wakaiita "Neu Langenburg" ("Langenburg mpya"). Boma jipya lilijengwa mwaka 1901. Hadi leo jina la hoteli "Langiboss" linakumbusha jina la zamani. Neu Langenburg iliendelea kuwa mji mdogo; mnamo 1913 ilikuwa na maduka 10 na kituo cha polisi chenye askari 66.
|
20231101.sw_3027_1
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Tukuyu
|
Tukuyu
|
Wakati wa Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia Waingereza walivamia Afrika ya Mashariki ya Kijerumani kutoka Nyasaland (Malawi) na Wajerumani waliondoka mjini mwaka 1916; Waingereza walianzisha serikali yao ya kimkoa. Mwaka 1919 iliamuliwa katika Mkataba wa Versailles kwamba koloni la Kijerumani litawekwa mikononi mwa Waingereza waliobadilisha jina rasmi kuwa Tukuyu kuanzia mwaka 1920.
|
20231101.sw_3027_2
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Tukuyu
|
Tukuyu
|
Pia ni kitovu cha kilimo cha ndizi za kuiva: takribani mkoa wote wa Mbeya hutegemea ndizi kutoka Tukuyu.
|
20231101.sw_3027_3
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Tukuyu
|
Tukuyu
|
Kwa miaka mingi Tukuyu ilikuwa na tatizo la mawasiliano mabaya kutokana na uharibifu wa barabara pamoja na matatizo ya kisiasa kati ya Malawi na Tanzania.
|
20231101.sw_3027_4
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Tukuyu
|
Tukuyu
|
Tukuyu ni eneo la Konde au Wanyakyusa. Mji wenyewe umekuwa kituo cha dayosisi ya Konde ya Walutheri pia dayosisi ya Wakatoliki. Makao makuu ya Moravian bado yako Rungwe misioni.
|
20231101.sw_3027_5
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Tukuyu
|
Tukuyu
|
Tukuyu ina shule za msingi na sekondari, chuo cha ualimu na taasisi ya utafiti wa tiba, pia kuna ofisi za serikali ambayo ndiyo makao makuu ya Wilaya ya Rungwe (halmashauri) au umma pamoja na mashirika binafsi au taasisi binafsi, pia kuna huduma za posta, smu, hospitali ya wilaya na huduma za benki mbalimbali.
|
20231101.sw_3033_0
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mto
|
Mto
|
Chanzo cha mto mara nyingi ni chemchemi au ziwa au maungano ya vijito vidogo. Mto hufuata mwendo wake kwa mtelemko hadi mwisho wake baharini au ziwani au kwa mto mwingine. Kama mto ni mdogo huitwa kijito. Mto mkubwa sana kama Kongo au Nile unaweza kuitwa mto mkubwa au jito.
|
20231101.sw_3033_1
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mto
|
Mto
|
Njiani mwake mto huwa umechimba lalio linalofanana na mfereji kati ya udongo au mawe ya kingo zake. Nguvu ya kusogeza maji mtoni ni uvutano wa dunia.
|
20231101.sw_3033_2
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mto
|
Mto
|
Mwisho wa mto huitwa mdomo. Mdomoni kwa kawaida mto huishia katika gimba kubwa zaidi ya maji, ama mto mkubwa au ziwa au bahari.
|
20231101.sw_3033_3
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mto
|
Mto
|
Mdomo huo unaweza kuwa mpana kama kijazio hasa baharini ambako bahari inapanuka wakati wa maji kujaa.
|
20231101.sw_3033_4
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mto
|
Mto
|
Mito mingine inaonyesha mdomo wa delta kama imegawanyika mdomoni kuwa na mikono mingi inayoelekea bahari kwa umbo la pembetatu.
|
20231101.sw_3033_5
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mto
|
Mto
|
Njiani mito mingi inaunganika kuwa mito mikubwa zaidi. Ni desturi kutumia jina la mto ulio mkubwa zaidi mahali pa kuungana kwa ajili ya sehemu inayofuata ya mto uliopanuka.
|
20231101.sw_3033_6
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mto
|
Mto
|
Kwa mfano mito ya Ubangi na Kongo inakutana kwenye mji wa Mbandaka. Huko Kongo ni mto mkubwa kushinda Ubangi; hivyo baada ya Mbandaka kuelekea bahari mto unaendelea kuitwa "Kongo".
|
20231101.sw_3033_7
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mto
|
Mto
|
Wakati mwingine ni swali la uzoefu tu jinsi ya kutaja mto; Kongo inaitwa Lualaba hadi mji wa Kisangani. Wataalamu wengine wanasema ya kwamba mto Kagera ingestahili kuitwa "Nile" kwa sababu ni mto uleule unaopita tu kwenye ziwa Viktoria Nyanza.
|
20231101.sw_3033_8
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mto
|
Mto
|
Kuna pia uzoefu ambako jina la mto mdogo linaendelea kutumika. Mto Ruvuma unatoka Songea na kufuata mpaka wa Tanzania na Msumbiji. Unakutana na mto Lujenda ambao ni mkubwa zaidi; inawezekana kusema ya kwamba Ruvuma inaingia Lujenda lakini jina la Ruvuma linatumika hadi mdomoni.
|
20231101.sw_3033_9
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mto
|
Mto
|
Jumla ya eneo ambako matawimito yote hadi vijito asilia kabisa vinaanza na kupokea maji yake huitwa beseni. Sehemu kubwa ya Tanzania ya kaskazini-magharibi pamoja na Kenya magharibi ni sehemu ya beseni la Nile kwa sababu matone ya mvua kama yanafika mtoni yote huelekea ziwa Viktoria Nyanza na kuingia mto Nile kwenda bahari ya Mediteranea.
|
20231101.sw_3033_10
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mto
|
Mto
|
Sehemu kubwa zaidi ya Afrika ya Mashariki inapeleka maji kwenda mabeseni ya Rufiji, Ruvuma, Ruaha Mkuu au mto Tana ambayo yote inaishia katika Bahari Hindi.
|
20231101.sw_3033_11
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mto
|
Mto
|
Mipaka kati ya beseni huitwa tengamaji. Tengamaji kwa kawaida ni eneo la juu ambako upande mmoja maji hutelemka kuelekea beseni moja na upande mwingine kwenda beseni tofauti. Kwa mfano tengamaji kati ya mabeseni ya Ruaha Mkuu na Mto Zambezi (kupitia Ziwa Nyasa) inafuata milima ya Uporoto na milima ya Kipengere.
|
20231101.sw_3033_12
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mto
|
Mto
|
Maji ya mtoni ni maji matamu, tofauti na maji ya chumvi ya baharini. Hii ni sababu ya kwamba mimea, wanyama na watu hupenda kukaa karibu na mito.
|
20231101.sw_3033_13
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mto
|
Mto
|
Watu huona faida zaidi kwa sababu mito mikubwa na majito inafaa pia kwa usafiri. Kihistoria mito ilikuwa kati ya njia za kwanza kabisa za mawasiliano kati ya maeneo ya mbali.
|
20231101.sw_3033_14
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mto
|
Mto
|
Kadirio ya urefu wa mto hutegemea jinsi ya kuhesabu matawimito yake. Orodha inayofuata ina tofauti na orodha inayokadiria kwa namna nyingine.
|
20231101.sw_3033_15
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mto
|
Mto
|
Mito inaweza kupatikana pia kwenye sayari nyingine zenye kiowevu. Maziwa na mito imegunduliwa kwenye mwezi Titan wa sayari Zohali. Angahewa ya Titan haina maji, ni karibu yote nitrojeni. Kiowevu ya maziwa na mito yake inaaminiwa kuwa methani na hidrokaboni nyingine zinazotokea duniani kama gesi lakini kwenye baridi ya Titan hupatikana kama kiowevu.
|
20231101.sw_3034_0
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mito%20mirefu%20ya%20Afrika
|
Mito mirefu ya Afrika
|
Mara nyingi mto wa Nile unahesabiwa kuwa mtu mrefu kuliko yote ya Afrika tena duniani. Kadirio la urefu wa mto hutegemea jinsi ya kuhesabu matawimto yake. Orodha inayofuata ina tofauti na orodha inayokadiria kwa namna nyingine.
|
20231101.sw_3036_0
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kongo%20%28mto%29
|
Kongo (mto)
|
Mto wa Kongo (kati ya miaka 1971 na 1997 uliitwa zaidi "Zaire") ni mto mkubwa wa Afrika ya kati. Ni mto mrefu wa pili katika Afrika baada ya Nile. Pia ni mto wenye kina kirefu zaidi duniani.
|
20231101.sw_3036_1
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kongo%20%28mto%29
|
Kongo (mto)
|
Beseni la Kongo pamoja na matawimto yake ni eneo kubwa la pili duniani la msitu wa mvua. Kwa kiasi cha mshuko wa maji mdomoni ni mto mkubwa wa pili duniani baada ya Amazonas (Amerika ya Kusini).
|
20231101.sw_3036_2
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kongo%20%28mto%29
|
Kongo (mto)
|
Urefu wake ni kilomita 4,700 ukipimwa kuanzia chanzo cha tawimto la mbali zaidi ambalo ni mto Chambeshi wenye chanzo nchini Zambia. Mara nyingi urefu hutajwa kuanzia chanzo cha Lualaba halafu ni kilomita 4,374.
|
20231101.sw_3036_3
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kongo%20%28mto%29
|
Kongo (mto)
|
Jina la mto limetokana na Ufalme wa Kongo uliokuwa dola kubwa katika Angola ya Kaskazini na Kongo ya Magharibi wakati wa karne ya 14-17 BK. Jamhuri zote mbili za Kongo za leo zimepata majina yao kutoka mto huo.
|
20231101.sw_3036_4
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kongo%20%28mto%29
|
Kongo (mto)
|
Kuna taarifa ya mwaka 1535 kuhusu ufalme mdogo wa pili ulioitwa Kakongo kingdom. Ramani ya dunia iliyochorwa na Abraham Ortelius mnamo 1564 inaonyesha mji wa "Manicongo" kwenye mdomo wa mto kando ya bahari.
|
20231101.sw_3036_5
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kongo%20%28mto%29
|
Kongo (mto)
|
Jina la Bakongo kwa ajili ya jumla ya wasemaji wa lugha ya Kikongo ni jina la kisasa lililotumiwa tangu karne ya 20 tu.
|
20231101.sw_3036_6
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kongo%20%28mto%29
|
Kongo (mto)
|
Jina la pili linalotumiwa wakati mwingine ni "Zaire"; dikteta Mobutu Sese Seko alilifanya kuwa jina rasmi la mto pamoja na la taifa kati ya miaka 1971 - 1997. Jina hilo linatokana na neno la Kikongo "nzere" ("mto").
|
20231101.sw_3036_7
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kongo%20%28mto%29
|
Kongo (mto)
|
Katika karne za 16 na 17 mto ulijulikana kwa majina yote mawili jinsi inavyoonekana katika maandishi ya siku zile, kwa mfano Mwingereza James Barbot aliandika mwaka 1746 juu ya safari kwenda mto "Kongo au Zaire" ("Voyage to Congo River, Or the Zair") <ref>James Barbot, An Abstract of a Voyage to Congo River, Or the Zair and to Cabinde in the Year 1700 (1746). Mifano mingine inayotaja majina yote mawili: James Hingston Tuckey, Narrative of an Expedition to Explore the River Zaire, Usually Called the Congo, in South Africa, in 1816 (1818), (via google books, imetazamiwa May 2016). "Congo River, called Zahir or Zaire by the natives" John Purdy, Memoir, Descriptive and Explanatory, to Accompany the New Chart of the Ethiopic Or Southern Atlantic Ocean, 1822, p. 112.</ref>
|
20231101.sw_3036_8
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kongo%20%28mto%29
|
Kongo (mto)
|
Beseni la Kongo linalokusanya utiririshaji wa maji lina eneo la kilomita za mraba 4,014,500 . Kongo inashusha (kutegemeana na majira na kiasi cha mvua) kila sekunde kati ya m³ 23,000 hadi 75,000 za maji kwenye Atlantiki (wastani umekadiria kuwa mita za ujazo 41,000 kwa sekunde).
|
20231101.sw_3036_9
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kongo%20%28mto%29
|
Kongo (mto)
|
Kongo na matawimto yake inapita katika eneo kubwa la misitu ya mvua duniani (Amazonas pekee inapita katika msitu wa mvua mkubwa zaidi). Kwa kuwa ikipita pande zote mbili za ikweta, yaani kaskazini na kusini, sehemu fulani ya beseni lake huwa na majira ya mvua muda wowote.
|
20231101.sw_3036_10
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kongo%20%28mto%29
|
Kongo (mto)
|
Vyanzo vya Kongo viko katika nyanda za juu na kwenye milima inayopakana na Bonde la Ufa la Afrika ya Mashariki, pamoja na Ziwa Tanganyika na Ziwa Mweru ambayo yanamwaga maji kwenda mto Lualaba ulio tawimto kubwa zaidi la Kongo. Kwa kawaida chanzo cha mto Chambeshi huko Zambia, ambao unaishia katika Lualaba, huhesabiwa kama chanzo cha Kongo.
|
20231101.sw_3036_11
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kongo%20%28mto%29
|
Kongo (mto)
|
Lualaba inabadilisha jina lake mjini Kisangani ambako mto umepita maporomoko ya Bayoma na baada ya hapo huitwa Kongo. Mto unaelekea kaskazini, halafu mwendo wake unapinda kuelekea kusini magharibi, unapita mji wa Mbandaka unapopokea mto Ubangi halafu unaingia katika Bwawa la Malebo (kwa Kiingereza: Stanley Pool). Miji ya Kinshasa na Brazzaville inatazamana ikiwa pande mbili za bwawa hilo. Baada ya bwawa mto unakuwa mwembamba ukipita katika mabonde ya korongo kwenye idadi ya maporomoko inayojulikana kama maporomoko ya Livingstone Falls). Unapita miji ya Matadi na Boma (Kongo) na kuufikia baharini kwenye mji mdogo wa Muanda.
|
20231101.sw_3036_12
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kongo%20%28mto%29
|
Kongo (mto)
|
Matawimto yanaorodheshwa kuanzia mdomo kulekea chanzo. Kma namba zinatajwa zinaeleza urefu wa mwendo kwa kilomita (=km), eneo la beseni la tawimto kwa kilomita za mraba (=km²) na mshuko wa maji yaani kiasi cha maji kinachotoka mdomoni kwa mita za ujazo kwa sekunde (=m3/s)
|
20231101.sw_3036_13
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kongo%20%28mto%29
|
Kongo (mto)
|
Mto Kongo ni njia muhimu ya mawasiliano na biashara kwa meli zinazoweza kusafiri mle kwa kushirikiana na njia za reli penye maporomoko mahali patatu.
|
20231101.sw_3036_14
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kongo%20%28mto%29
|
Kongo (mto)
|
Maporomoko ya Livingstone yanazuia meli kupita kutoka baharini. Kuanzia Kisangani hadi Kinshasa mto ni njia ya maji inayopitiwa na meli za mtoni. Upande wa Lualaba kuna sehemu kadhaa zinazofaa kwa meli lakini njia ya maji inakatwa mara kadhaa na maporomoko.
|
20231101.sw_3036_15
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kongo%20%28mto%29
|
Kongo (mto)
|
Mto Kongo ni mto wenye maji mengi katika Afrika yote. Hivyo kuna nafasi kubwa ya kuzalisha umememaji. Kama nafasi zote zingetumika ingewezekana kutosheleza mahitaji yote ya umeme kwa Afrika kusini kwa Sahara.
|
20231101.sw_3036_16
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kongo%20%28mto%29
|
Kongo (mto)
|
Hadi sasa kuna takriban vituo 49 vinavyozalisha umememaji katika beseni la Kongo. Kituo kikubwa kiko kwenye Lambo la Inga takriban kilomita 200 upande wa kusini magharibi wa Kinshasa. Mradi ulianzishwa katika miaka ya 1970. Wakati ule mfululizo wa malambo 5 ulipangwa. Hadi sasa 2 yamejengwa, lambo la kwanza (Inga I) lilikuwa tayari mwaka 1972, Inga II ikafuata mwaka 1982 na yote miwili ina rafadha 14 zinazoweza kuzalisha megawati 1,775 kwa jumla, lakini kutokana na uhaba wa matengenezo na usimamzi yanafikia si zaidi ya nusu yake.
|
20231101.sw_3036_17
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kongo%20%28mto%29
|
Kongo (mto)
|
Shirika la Eskom kutoka Afrika Kusini imependekeza kuongeza lambo la tatu na - pamoja na matengenezo kwenye malambo mengine - kuongeza uwezo wa majiumeme hadi kiwango cha gigawati 40.
|
20231101.sw_3036_18
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kongo%20%28mto%29
|
Kongo (mto)
|
Lakini kuna wataalamu walioonyesha mashaka kuwa malambo mapya yatakuwa hatari kwa ekolojia ya mto na hasa maisha ya spishi nyingi za mtoni.
|
20231101.sw_3036_19
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kongo%20%28mto%29
|
Kongo (mto)
|
1837: Silence – A Fable is a short story by Edgar Allan Poe, written in 1837. "The region of which I speak is a dreary region in Libya, by the borders of the river Zaire."
|
20231101.sw_3036_20
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kongo%20%28mto%29
|
Kongo (mto)
|
1878: Henry Morton Stanley documented his journey down the Congo River in Through the Dark Continent, first published in 1878.Through the Dark continent. Open Library. Retrieved on 2011-11-29.
|
20231101.sw_3036_21
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kongo%20%28mto%29
|
Kongo (mto)
|
1899: Joseph Conrad's Heart of Darkness is a short novel about Charles Marlow's life as an ivory transporter down the Congo River in Central Africa. The river is "a mighty big river, that you could see on the map, resembling an immense snake uncoiled, with its head in the sea, its body at rest curving afar over a vast country, and its tail lost in the depths of the land".
|
20231101.sw_3036_22
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kongo%20%28mto%29
|
Kongo (mto)
|
1914: American poet Vachel Lindsay portrays a dark and savage society around the Congo River in his 1914 poem The Congo: A Study of the Negro Race.
|
20231101.sw_3036_23
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kongo%20%28mto%29
|
Kongo (mto)
|
1930: Both Congo River and basin form the setting of Hoity Toity, the Soviet science fiction novel by Alexander Belyayev.
|
20231101.sw_3036_24
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kongo%20%28mto%29
|
Kongo (mto)
|
1980: The Congo River is featured in a chapter of Michael Crichton's novel Congo (published in 1980), as well as in the 1995 film based on the book.
|
20231101.sw_3036_25
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kongo%20%28mto%29
|
Kongo (mto)
|
1995: The Congo River is featured in the action film Congo, by director Frank Marshall, although it is not mentioned by name in the film. The film is based on the 1980 novel of the same name by Michael Crichton.
|
20231101.sw_3036_26
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kongo%20%28mto%29
|
Kongo (mto)
|
1996: British author Redmond O'Hanlon has a travelogue published by Penguin Books under the title of Congo Journey (1996).
|
20231101.sw_3036_27
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kongo%20%28mto%29
|
Kongo (mto)
|
2006: The river's history is discussed in the book Brazza, A Life for Africa (by Maria Petringa, Bloomington, IN: AuthorHouse, 2006).
|
20231101.sw_3036_28
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kongo%20%28mto%29
|
Kongo (mto)
|
2007: The Congo River and the Democratic Republic of Congo are the scenario for the 2007 book Blood River by journalist Tim Butcher, based on his intrepid travels up and down Africa's second longest river. Blood River was an attempt to retrace Henry Morton Stanley's trip down the Congo River, documented in Through the Dark Continent (first published, 1878), and was shortlisted for the 2008 British Book Awards.
|
20231101.sw_3036_29
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kongo%20%28mto%29
|
Kongo (mto)
|
2010: The Congo River is a central element in the 2010 novel by Mario Vargas Llosa, El sueño del celta (The Dream of the Celt), a fictionalisation of episodes in the life of the Irishman Roger Casement. The book is to be published in English in 2012.
|
20231101.sw_3036_30
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kongo%20%28mto%29
|
Kongo (mto)
|
2012: Phil Harwood's book "Canoeing the Congo" , Harwood, P. (2012). Canoeing the Congo: First Source to Sea Descent of the Congo River. Matador. ISBN 978-1780880075,
|
20231101.sw_3048_0
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Niger%20%28mto%29
|
Niger (mto)
|
Niger ni mto mkubwa kabisa wa Afrika ya Magharibi na mto mrefu wa tatu barani Afrika ukiwa na mwendo wa km 4.374. Njia yake ni kama upinde ikianza Guinea katika nyanda za juu za Futa Djallon kuelekea kaskazini-mashariki kupitia Mali hadi Niger. Karibu na mji wa Timbuktu inageukia kuelekea mashariki, halafu mashariki-kusini kupitia Benin na Nigeria hadi kufika mdomo wa delta yake kwenye Ghuba ya Guinea ya bahari ya Atlantiki.
|
20231101.sw_3048_1
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Niger%20%28mto%29
|
Niger (mto)
|
Kabla ya kufikia Timbuktu (Niger) mto unapanuka kuwa na delta ya barani pia mdomo wake baharini una delta kubwa sana.
|
20231101.sw_3048_2
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Niger%20%28mto%29
|
Niger (mto)
|
Jina linatokana na lugha ya Watuareg "ghir n-igheren" (yaani "Mto wa mito"). Jina hili lilichukuliwa na waandishi wa Ulaya ya karne za kati na kusomwa kwa namna ya Kilatini kama "Niger" yaani "cheusi", "mto mweusi" au "mto wa nchi ya Weusi". Jina hili la Kilatini lilionekana mara ya kwanza kwenye ramani ya Klaudio Ptolemaio kwa ajili ya mto mmoja upande wa kusini wa milima ya Atlas.
|
20231101.sw_3048_3
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Niger%20%28mto%29
|
Niger (mto)
|
Nchi za kisasa za Niger na Nigeria zimepata majina yake kutoka kwa jina la mto huo. Wenyeji wa huko wana majina mbalimbali kwa ajili ya mto huu: Joliba katika lugha za Kimandinga na Isa Ber kwa Kisonghai. Majina yote humaanisha "mto mkubwa". Katika maeneo karibu na mdomo wake ulijulikana pia kama "Kworra" (au Quorra).
|
20231101.sw_3048_4
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Niger%20%28mto%29
|
Niger (mto)
|
Wataalamu wa Ulaya waliokusanya habari zake walifikiri mwanzoni ya kwamba unaishia kwenye Ziwa Chad au katika mto Naili. Walitambua baadaye ya kwamba ni mto uleule uliojulikana kwao tayari kwa jina la "Quorra".
|
20231101.sw_3048_5
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Niger%20%28mto%29
|
Niger (mto)
|
Njia ya upinde ya mto Niger ilichanganya wataalamu wa Ulaya pamoja na Waarabu kwa karne nyingi. Waroma wa kale walifahamu mto ule mkubwa karibu na Timbuktu wakafikiri ya kwamba unaendelea kujiunga na mto Nile. Mtaalamu Mwarabu Ibn Battuta alifikiri hivyo pia.
|
20231101.sw_3048_6
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Niger%20%28mto%29
|
Niger (mto)
|
Wengine waliona utaishia kwenye mto Senegal au mto Kongo. Kuchanganyikiwa huku kulisababisha kwa karne nyingi ramani zisizoonyesha mwendo halisi wa mto. Wasafiri na wataalamu wa nje hawakuelewa ya kwamba mto mkubwa ulio karibu na Timbuktu na mto mkubwa unaoingia Atlantiki kwenye Ghuba ya Guinea huko Nigeria ni mto uleule.
|
20231101.sw_3048_7
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Niger%20%28mto%29
|
Niger (mto)
|
Ni tangu mwaka 1830 tu ya kwamba msafara wa mpelelezi Mungo Park ulileta taarifa ya kutambua hali halisi.
|
20231101.sw_3048_8
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Niger%20%28mto%29
|
Niger (mto)
|
Mto Niger una chanzo chake katika milima ya Futa Djalon nchini Guinea, umbali wa kilomita 240 kutoka bahari Atlantiki. Lakini haufiki baharini moja kwa moja, bali unaelekea kaskazini mashariki kwa Sahara kupitia Bamako na kuunda delta ya barani inayoitwa "Massina" ambako mji mkubwa ni Mopti. Unaendelea hadi Timbuktu unapopita kwenye Sahara ya kusini na kubadilisha mweleko kwenda kusini mashariki. Karibu na mji wa Gao unapita kwa matuta ya mchanga ya Koyma na kuingia tena katika kanda la Sahel. Halafu unapita nchi ya Niger na mji mkuu wake, Niamey. Kutoka hapa njia yake ni mpaka wa Benin hadi "hifadhi ya W" mpakani mwa Niger, Burkina Faso na Benin. Kutoka hapa mto Niger unaendelea hadi Nigeria. Karibu na Lokoja unapokea tawimto wa Benue na kuingia katika kanda la msitu wa mvua wa Nigeria. Karibu na mji wa Onitsha mto unaanza kujigawa na kuwa delta ya Niger. Mikono yake mikubwa inaitwa Forcados, Nun na Escravos.
|
20231101.sw_3048_9
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Niger%20%28mto%29
|
Niger (mto)
|
Mto Niger unabeba matope kidogo kulingana na mto Naili kwa sababu chanzo chake kipo katika eneo la miamba.}} Sawa na Naili ina mafuriko ya kila mwaka yanayoanza mwezi wa Septemba, kufikia jii kwenye Novemba na kuishi mwezi wa Mei
|
20231101.sw_3048_10
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Niger%20%28mto%29
|
Niger (mto)
|
Tabia isiyo ya kawaida ni delta ya barani inayotokea pale ambako mtelemko wa mto unakwisha. Tokeo lake ni eneo lenye ukubwa wa Ubelgji ambako mto unagawiwa katika mikono mingi na vinamasi. Hili ni eneo zuri kwa uvuvi na kilimo. }}
|
20231101.sw_3048_11
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Niger%20%28mto%29
|
Niger (mto)
|
Kati ya delta ya barani na Timbuktu mto unapotewa na angalau theluthi mbili za maji yake katika ardhi kavu pamoja na uvukizaji. Upotevu huu umekadiriwa kulingana na km3 31 kwa mwaka lakini kiasi kinabadilika mwaka kwa mwaka.
|
20231101.sw_3048_12
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Niger%20%28mto%29
|
Niger (mto)
|
Baadaye matawimto mengi yanaingia na kuongeza kiwango cha maji, hata hivyo kiasi kikubwa kinapotea kwa sababu ya uvukizaji.
|
20231101.sw_3048_13
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Niger%20%28mto%29
|
Niger (mto)
|
Kiwango cha maji kwenye mto kinategemea majira: kuna tofauti kubwa kati ya majira ya mvua na ukame. Kiasi kilipimwa kwa muda wa miaka 40 kwenye mji wa Malanville nchini Benin uliopo kilomita 1100 kutoka mdomo wa mto. Katika kipindi hicho wastani wa maji katika miaka hii 49 ilikuwa m³/s 1053; kiasi kidogo kilikuwa m³/s 18, inayomaanisha mto karibu kukauka. Kiasi cha juu kilikuwa m³/s 2726. Kwa wastani ni m³/s 6000 zinazofikia Atlantiki.
|
20231101.sw_3050_0
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Binadamu
|
Binadamu
|
Binadamu (pia mwanadamu) ni neno lenye asili ya Kiarabu linalomaanisha "Mwana wa Adamu", anayeaminiwa na dini za Uyahudi, Ukristo na Uislamu kuwa ndiye mtu wa kwanza.
|
20231101.sw_3050_1
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Binadamu
|
Binadamu
|
Kisayansi jina hilo linaweza kutumika kwa maana ya Homo sapiens ili kumtofautisha na viumbehai wengine wa jenasi Homo ambao wote walitoweka walau miaka 12,000 hivi iliyopita.
|
20231101.sw_3050_2
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Binadamu
|
Binadamu
|
Watu wote walioko leo hii ni spishi ileile na tofauti zinazoonekana kati ya maumbile yao katika sehemu mbalimbali za dunia ni ndogondogo tu.
|
20231101.sw_3050_3
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Binadamu
|
Binadamu
|
Utafiti juu ya DNA umethibitisha kwamba binadamu wote wametokana na watu waliokuwepo Afrika walau miaka 300,000 hivi iliyopita.
|
20231101.sw_3050_4
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Binadamu
|
Binadamu
|
Kwa namna ya pekee, upimaji wa DNA ya mviringo, ambayo kila mmoja anarithi kwa mama tu, umeonyesha kuwa binadamu wote waliopo duniani wanachanga mama mmoja aliyewahi kuishi miaka 160,000 hivi iliyopita.
|
20231101.sw_3050_5
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Binadamu
|
Binadamu
|
Halafu upimaji wa kromosomu Y, ambayo kila mwanamume anarithi kwa baba tu, umeonyesha kuwa wanaume wote waliopo duniani wanachanga baba mmoja aliyewahi kuishi walau miaka 120,000 hivi iliyopita, kidogo tu kabla ya watu kuanza kuenea katika bara la Asia labda kufuatia pwani za Bahari ya Hindi.
|
20231101.sw_3050_6
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Binadamu
|
Binadamu
|
Hata hivyo, miaka hii ya mwisho imegundulika katika baadhi ya wanaume wenye asili ya makabila ya Wabangwa na Wambo (Camerun, Afrika ya Kati) aina ya kromosomu Y tofauti sana na ile ya wanaume wengine wote waliowahi kupimwa, kiasi cha kukadiria zimetofautiana miaka 350,000 hivi iliyopita.
|
20231101.sw_3050_7
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Binadamu
|
Binadamu
|
Vilevile, upimaji wa DNA ya mstari kwa jumla umeonyesha uwezekano wa kwamba baadhi ya binadamu wa leo, wale wasio wa Kusini kwa Sahara, wana asilimia 1-6 ya urithi wa kibiolojia kutoka kwa aina nyingine za Homo, hususan Homo neanderthalensis, ile ya pango la Denisova na ile iliyorithiwa na baadhi ya watu wa visiwa vya Andaman (India).
|
20231101.sw_3050_8
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Binadamu
|
Binadamu
|
Kama hao waliweza kweli kuzaliana na Homo sapiens na kuacha uzao uliojiendeleza maana yake walikuwa spishi moja na yeye. Hapo asili ya binadamu inatakiwa kuhesabiwa ya zamani zaidi sana kuliko miaka 200,000 iliyofikiriwa kwanza.
|
20231101.sw_3050_9
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Binadamu
|
Binadamu
|
Kutoka bara la Africa watu walienea kwanza Asia , Australia na Ulaya, halafu Amerika toka kaskazini hadi kusini.
|
20231101.sw_3050_10
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Binadamu
|
Binadamu
|
Hatimaye, katika karne ya 20 watu walikwenda kukaa kwa muda katika bara la Antaktika kwa ajili ya utafiti.
|
20231101.sw_3050_11
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Binadamu
|
Binadamu
|
Ingawa binadamu ana undugu mkubwa wa kibiolojia na sokwe na viumbe vingine, ustawi wake hauna mfano, kiasi cha kufanya wengi waamini kwamba tofauti iliyopo inadai kuelezwa kwa uwemo wa roho ndani ya mwili wake; roho ambayo dini hizo zinasadiki imetiwa na Mungu moja kwa moja.
|
20231101.sw_3050_12
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Binadamu
|
Binadamu
|
Kadiri ya Biblia, binadamu ameumbwa “kwa mfano wa Mungu” (Mwa 1:27), mwenye roho isiyokufa. Hivyo, Mungu amependa kuwasiliana na watu, akijitambulisha na kujitoa kwetu, tuweze kuishi katika urafiki naye na hatimaye tushiriki heri yake.
|
20231101.sw_3050_13
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Binadamu
|
Binadamu
|
Ameshirikishwa naye ukuu juu ya viumbe vyote vinavyoonekana. “Nikiziangalia mbingu zako, kazi ya vidole vyako, mwezi na nyota ulizoziratibisha; mtu ni kitu gani hata umkumbuke, na binadamu hata umwangalie? Umemfanya mdogo punde kuliko Mungu; umemvika taji ya utukufu na heshima” (Zab 8:3-5). “Siwaiti tena watumwa; kwa maana mtumwa hajui atendalo bwana wake; lakini ninyi nimewaita rafiki, kwa kuwa yote niliyoyasikia kwa Baba yangu nimewaarifu” (Yoh 15:15). Amefanya hivyo kwa maneno na matendo yanayoshikamana sana kwa kuwa maneno yanafafanua matendo, nayo matendo yanathibitisha maneno.
|
20231101.sw_3050_14
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Binadamu
|
Binadamu
|
Mungu ametufunulia pia ukweli juu yetu wenyewe akijibu kabisa maswali yanayotusumbua kuhusu maana na lengo la maisha yetu. “Mungu hutaka watu wote waokolewe, na kupata kujua yaliyo kweli” (1Tim 2:4). “Mungu si mtu, aseme uongo” (Hes 23:19). Yeye hadanganyiki wala hadanganyi.
|
20231101.sw_3050_15
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Binadamu
|
Binadamu
|
Kati ya viumbe vinavyoonekana, mtu tu ni nafsi, akiwa na uwezo wa kujifahamu, kujitawala, kujitolea na kupendana na wengine. Basi, anapaswa kulinda hadhi hiyo asitawaliwe na tamaa za kila aina. Akifanya hivyo anatimiza mpango wa Mungu juu yake na kupendana naye.
|
20231101.sw_3050_16
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Binadamu
|
Binadamu
|
Malaika na watu ndio viumbe pekee vyenye hiari ya kuchagua wenyewe wachangie mpango wa Mungu au la. “Nazishuhudiza mbingu na nchi juu yenu hivi leo, kuwa nimekuwekea mbele yako uzima na mauti, baraka na laana; basi, chagua uzima, ili uwe hai, wewe na uzao wako; kumpenda Bwana, Mungu wako, kuitii sauti yake, na kushikamana naye; kwani hiyo ndiyo uzima wako” (Kumb 30:19-20).
|
20231101.sw_3050_17
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Binadamu
|
Binadamu
|
Malaika na watu wanaweza kuchagua hata wawe wema au wabaya milele. “Kulikuwa na vita mbinguni: Mikaeli na malaika zake wakapigana na yule joka, yule joka naye akapigana nao pamoja na malaika zake; nao hawakushinda, wala mahali pao hapakuonekana tena mbinguni” (Ufu 12:7-8).
|
20231101.sw_3050_18
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Binadamu
|
Binadamu
|
Chaguo letu binadamu linafanyika siku kwa siku kwa kuchukua misimamo mizuri au mipotovu kuhusu dini na maadili. “Mwayachunguza Maandiko, kwa sababu mnadhani kwamba ninyi mna uzima wa milele ndani yake; na hayo ndiyo yanayonishuhudia. Wala hamtaki kuja kwangu mpate kuwa na uzima” (Yoh 5:39-40).
|
20231101.sw_3050_19
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Binadamu
|
Binadamu
|
Binadamu ni umoja wa mambo mawili: roho iliyoumbwa na Mungu moja kwa moja, na mwili ulioumbwa naye kwa njia ya wazazi. Maumbile hayo yanatakiwa kukamilika kwa kupokea na kutimiza upendo wa Mungu aliyesema, “’Na tufanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu; wakatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na wanyama, na nchi yote pia, na kila chenye kutambaa kitambaacho juu ya nchi’. Mungu akaumba mtu kwa mfano wake, kwa mfano wa Mungu alimwumba, mwanamume na mwanamke aliwaumba” (Mwa 1:26-27).
|
20231101.sw_3050_20
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Binadamu
|
Binadamu
|
Hivyo, mwili wetu ni muhimu, kwa sababu umeumbwa na Mungu, umetwaliwa na Mwanae ili atuokoe, umehuishwa na Roho Mtakatifu atakayeutukuza siku ya ufufuo kwa mfano wa Yesu. “Mwili si kwa zinaa, bali ni kwa Bwana, naye Bwana ni kwa mwili. Naye Mungu alimfufua Bwana, na tena atatufufua sisi kwa uweza wake. Je, hamjui ya kuwa miili yenu ni viungo vya Kristo? Basi nivitwae viungo vya Kristo na kuvifanya viungo vya kahaba? Hasha! Au hamjui ya kuwa yeye aliyeungwa na kahaba ni mwili mmoja naye?… Au hamjui ya kuwa mwili wenu ni hekalu la Roho Mtakatifu aliye ndani yenu, mliyepewa na Mungu?” (1Kor 6:13-16,19).
|
20231101.sw_3050_21
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Binadamu
|
Binadamu
|
Utotoni anasukumwa tu na haja za umbile lake, ambazo ni muhimu kwake na anazilenga bila ya kuhitaji juhudi.
|
20231101.sw_3050_22
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Binadamu
|
Binadamu
|
Lakini akikua anaanza kutambua tunu za maadili na dini, ambazo ni njema, ni muhimu kwa zenyewe na zinamdai azifuate kwa nia imara hadi afikie lengo.
|
20231101.sw_3050_23
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Binadamu
|
Binadamu
|
Anapopitia misukosuko ya ujana asikubali kushindwa na vionjo wala asikate tamaa, kwa kuwa Mungu amemuumba atawale hata nafsi yake na mwili wake.
|
20231101.sw_3050_24
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Binadamu
|
Binadamu
|
Mtu wa kwanza kuumbwa na Mungu kadiri ya Biblia alikuwa Adamu, akifuatwa na Eva mkewe. Hapo “Mungu aliona kila kitu alichokifanya, na tazama ni chema sana” (Mwa 1:31).
|
20231101.sw_3050_25
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Binadamu
|
Binadamu
|
Hata hivyo, baada ya dhambi ya asili anadaiwa bidii katika kutekeleza tunu ili wema alionao uzae matunda.
|
Subsets and Splits
No community queries yet
The top public SQL queries from the community will appear here once available.