_id
stringlengths 15
22
| url
stringlengths 31
150
| title
stringlengths 1
86
| text
stringlengths 100
23.8k
|
---|---|---|---|
20231101.sw_3108_1
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kismayu
|
Kismayu
|
Mji ulianzishwa na Wabajuni waliokuwa Waswahili Wabantu. Wasomali wenyewe walichelewa kufika eneo hili.
|
20231101.sw_3108_2
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kismayu
|
Kismayu
|
Katika karne za kati, Kismayu ilikuwa chini ya serikali ya Ajuuraan iliyokuwa ikutawala eneo kadhaa za Somalia.
|
20231101.sw_3108_3
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kismayu
|
Kismayu
|
Kismayu pamoja na pwani ilikuwa chini ya masultani wa Zanzibar tangu 1835 BK. Kati ya 1875 na 1876 Kismayu ilitawaliwa na Misri.
|
20231101.sw_3108_4
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kismayu
|
Kismayu
|
Tangu 1895 ilikuwa chini ya utawala wa Uingereza pamoja na Kenya lakini mwaka 1924 ilikabidhiwa kwa utawala wa Italia. Ikawa mji mkuu wa jimbo la Oltre Giuba (ng'ambo ya Juba).
|
20231101.sw_3108_5
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kismayu
|
Kismayu
|
Kismayu iliharibika sana kutokana na mapigano katika vita vya wenyewe kwa wenyewe vya Somalia tangu 1991.
|
20231101.sw_3110_0
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Okavango
|
Okavango
|
Okavango (pia: Okovango; katika Angola: Kubango au Cubango) ni mto wa Afrika ya kusini-magharibi. Unaanza nchini Angola katika milima ya Bié inapojulikana kwa jina la Kubango. Mwendo wake wa km 1600 ni kusini tu hadi jangwa la Kalahari unapoishia kwenye delta ya barani. Katika kusini ya Angola ni mpaka na Namibia. Unapita nchi ya Namibia mwanzoni wa kishoroba ya Caprivi na kuendelea Botswana Unapoishia jangwani katika delta yake.
|
20231101.sw_3110_1
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Okavango
|
Okavango
|
Chanzo cha mto ni kusini KWa mji wa Vila Nova (Angola) katika milima ya Bié kwenye kimo cha mita 1,780. Mwanzoni mwendo wake ni wa haraka kuna maporomoko madogo. Halafu mto ni mpaka kati ya Angola na Namibia. Baada ya kupokea tawimto la Kwito unaingia Namibia unapopita kanda nyembamba ya kishoroba ya Caprivi kwa kilomita chache. Kabla ya kuvuka mpaka wa Botswana mto unashuka mita 4 kwenye maporomoko ya Popa.
|
20231101.sw_3110_2
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Okavango
|
Okavango
|
Takriban km 70 ndani ya Botswana mwendo wa mto unapanuka na kugawanyika kuwa delta ya barani yenye zaidi ya km² 16,000.
|
20231101.sw_3111_0
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kubango
|
Kubango
|
Chanzo cha mto ni kwenye kimo cha m 1780 juu ya UB katika nyanda za juu za Bie mashariki kwa Huambo, kilomita chache kusini kwa Nova Vila.
|
20231101.sw_3111_1
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kubango
|
Kubango
|
Haielekei baharini bali kusini inapoishia katika jangwa la Botswana. Njiani inapita Namibia kwenye kishoroba ya Caprivi. Kuanzia Namibia mto huitwa kwa jina la Okavango.
|
20231101.sw_3112_0
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kishoroba%20cha%20Caprivi
|
Kishoroba cha Caprivi
|
Kishoroba cha Caprivi ni kanda nyembamba ya eneo la Namibia inayoelekea mashariki kwenye pembe la kaskazini-mashariki kabisa ya nchi Namibia kati ya Botswana upande wa kusini na Angola pamoja na Zambia upande wa kaskazini. Kishoroba hicho kina urefu wa km 450, upana ni mara nyingi km 30 pekee.
|
20231101.sw_3112_1
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kishoroba%20cha%20Caprivi
|
Kishoroba cha Caprivi
|
Kiutawala kishoroba imegawanyika kati ya mikoa ya Caprivi and Okavango ya Jamhuri ya Namibia. Mji mkubwa ni Katima Mulilo ambao ni makao makuu ya mkoa wa Caprivi.
|
20231101.sw_3112_2
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kishoroba%20cha%20Caprivi
|
Kishoroba cha Caprivi
|
Jina la Caprivi limetokana na Chansella wa Ujerumani Leo von Caprivi aliyekuwa mkuu wa serikali ya Dola la Ujerumani wakati wa Mkataba wa Ujerumani na Uingereza wa 1890 unaoitwa "Mkataba wa Helgoland-Zanzibar". Ilikubaliwa ya kwamba Ujerumani inapata kishoroba cha nchi hadi mto Zambezi chenye upana "usiopungua maili 20".
|
20231101.sw_3112_3
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kishoroba%20cha%20Caprivi
|
Kishoroba cha Caprivi
|
Wakati ule Ujerumani ulitaka njia ya mawasiliano kati ya Namibia na mto Zambezi. Ilidhaniwa ya kwamba kuna uwezekano wa kutumia mto Zambezi kwa ajili ya usafiri na kupata njia ya maji kati ya Namibia na Bahari Hindi. Dhana hiyo ilikuwa kosa na kwa muda mrefu eneo la Caprivi lilikuwa na mawasiliano tu kupitia Zambia. Siku hizi kuna barabara ya lami hadi Katima Mulilo.
|
20231101.sw_3112_4
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kishoroba%20cha%20Caprivi
|
Kishoroba cha Caprivi
|
Miaka mingi wa vita ya kupigania uhuru wa Namibia na baadaye vita katika Angola eneo la kishoroba lilikuwa eneo lililofungwa kwa mawasiliano yasiyo ya kijeshi. Tangu mwisho wa vita ya wenyewe kwa wenyewe nchini Angola na kujengwa kwa barabara watu wa Caprivi wanaweza kusafiri kwa urahisi na wageni wanaweza kufika bila matatizo.
|
20231101.sw_3112_5
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kishoroba%20cha%20Caprivi
|
Kishoroba cha Caprivi
|
Tangu 1994 kuna "Harakati ya Ukombozi wa Caprivi", kundi kati ya Walozi wa Caprivi wanaopendelea umoja na Walozi wenzao huko Zambia wakitafuta hali ya kujitawala kwa eneo lao. Mwaka 1999 ilitokea ghasia katika mashariki ya Caprivi na mapigano kati ya wanamgambo Walozi na jeshi la serikali.
|
20231101.sw_3114_0
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mkataba%20wa%20Helgoland-Zanzibar
|
Mkataba wa Helgoland-Zanzibar
|
Mapatano baina Uingereza na Ujerumani kuhusu Afrika na Helgoland (kifupi mkataba wa Helgoland-Zanzibar) yalifanywa kati ya Ujerumani na Uingereza tarehe 1 Julai 1890. Pande zote mbili zilielewana juu ya mipaka ya makoloni yao au maeneo walimotaka kuwa na athira kuu katika Afrika.
|
20231101.sw_3114_1
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mkataba%20wa%20Helgoland-Zanzibar
|
Mkataba wa Helgoland-Zanzibar
|
Mkataba ulihusu maeneo katika Afrika ya Mashariki, Afrika ya Kusini-Magharibi (leo Namibia) na Afrika ya Magharibi (Togo ya leo) pamoja na kisiwa cha Helgoland mbele ya pwani ya Ujerumani katika Bahari ya Kaskazini.
|
20231101.sw_3114_2
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mkataba%20wa%20Helgoland-Zanzibar
|
Mkataba wa Helgoland-Zanzibar
|
Shabaha kuu ya mkataba wa 1890 ilikuwa kuondoa hatari za migongano kati ya Ujerumani na Uingereza na kutunza uhusiano mzuri.
|
20231101.sw_3114_3
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mkataba%20wa%20Helgoland-Zanzibar
|
Mkataba wa Helgoland-Zanzibar
|
Tangu kufika kwa Ujerumani kama mkoloni kwenye bara la Afrika mwaka 1884 Uingereza ulitafuta mapatano ya amani na nchi hii. Serikali ya Ujerumani chini ya chansella Bismarck ilijitahidi pia kutovurugisha uhusiano na Uingereza. Baada ya kuanzishwa kwa koloni ya Kampuni ya Kijerumani kwa Afrika ya Mashariki kwenye sehemu za Tanganyika, kulikotokea kiasili dhidi ya nia ya Bismarck, serikali hizi mbili zilikubaliana mapatano ya 1886 kati ya Ujerumani na Uingereza juu ya Afrika ya Mashariki kuhusu maeneo walipotaka kuwa na kipaumbele na maeneo waliyokubali kuwa ya Zanzibar.
|
20231101.sw_3114_4
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mkataba%20wa%20Helgoland-Zanzibar
|
Mkataba wa Helgoland-Zanzibar
|
Udhaifu wa Zanzibar ulizidi kuonekana katika miaka iliyofuata ambako Sultani alikodi haki zake kwenye pwani la Afrika Mashariki kwanza kwa kampuni ya Kiingereza mwaka 1887 upande wa kaskazini halafu kwa kampuni ya Kijerumani upande wa kusini mwaka 1888. Katika vita ya upinzani wa wenyeji dhidi ya kampuni ya Kijerumani, Sultani alishindwa kufanya lolote. Hivyo Ujerumani na Uingereza waliendelea kugawana maeneo yake. Ujerumani walikubali ulinzi wa Uingereza juu ya maeneo yote yaliyobaki rasmi chini ya Sultani pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba. Sultani aliambiwa kukubali kuza maeneo yake ya pwani (yaliyokuwa baadaye Tanganyika) kwa Ujerumani na kukubali ulinzi wa Uingereza juu ya maeneo yake yaliyobaki.
|
20231101.sw_3114_5
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mkataba%20wa%20Helgoland-Zanzibar
|
Mkataba wa Helgoland-Zanzibar
|
Leo von Caprivi alikuwa chansella mpya wa Ujerumani tangu Machi 1890 akimfuata Otto von Bismarck. Caprivi alitaka kujenga uhusiano mwema hasa na Uingereza.
|
20231101.sw_3114_6
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mkataba%20wa%20Helgoland-Zanzibar
|
Mkataba wa Helgoland-Zanzibar
|
Wakati huohuo uhusiano ule ulikuwa mashakani kidogo kutokana na matendo ya Karl Peters aliyejaribu kupanua eneo la Shirika la Kijerumani kwa Afrika ya Mashariki hadi Uganda, kinyume cha mapatano ya 1886 kati ya Ujerumani na Uingereza juu ya Afrika ya Mashariki.
|
20231101.sw_3114_7
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mkataba%20wa%20Helgoland-Zanzibar
|
Mkataba wa Helgoland-Zanzibar
|
Uingereza ulikubali koloni la Afrika ya Mashariki ya Kijerumani (Tanganyika, Rwanda, Burundi za leo). Waingereza waliahidi kumshawishi Sultani wa Zanzibar ili awaachie Wajerumani haki za Zanzibar huko Tanganyika.
|
20231101.sw_3114_8
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mkataba%20wa%20Helgoland-Zanzibar
|
Mkataba wa Helgoland-Zanzibar
|
Ujerumani ulifuta mipango yake katika Uganda na Zanzibar ambako Mjerumani Karl Peters aliwahi kusaini mapatano ya ushirikiano na Kabaka na Sultani.
|
20231101.sw_3114_9
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mkataba%20wa%20Helgoland-Zanzibar
|
Mkataba wa Helgoland-Zanzibar
|
Pia uliwaachia Waingereza Usultani wa Witu uliokuwa tayari chini ya ulinzi wa Ujerumani tangu mwaka 1885 na madai yake kwenye pwani ya Kenya katika eneo la funguvisiwa ya Lamu na pwani ya Somalia hadi Kismayu.
|
20231101.sw_3114_10
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mkataba%20wa%20Helgoland-Zanzibar
|
Mkataba wa Helgoland-Zanzibar
|
Mengineyo ni kwamba mkataba ulieleza mipaka baina ya maeneo chini ya athari ya Uingereza na athari ya Ujerumani. Hapa kuna pia kipengele kuhusu mipaka kwenye Ziwa Nyasa kilichounda msingi kwa kutoelewana baina ya Malawi na Tanzania kuhusu mipaka kwenye ziwa hili tangu uhuru.
|
20231101.sw_3114_11
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mkataba%20wa%20Helgoland-Zanzibar
|
Mkataba wa Helgoland-Zanzibar
|
Pande zote mbili zilipatana kuhusu utawala wa Kijerumani katika eneo ambalo likawa Namibia baadaye. Wajerumani walikubali kutovuka mstari wa mto Oranje upande wa kusini na kukubali utawala wa Waingerezea juu ya Botswana.
|
20231101.sw_3114_12
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mkataba%20wa%20Helgoland-Zanzibar
|
Mkataba wa Helgoland-Zanzibar
|
Wajerumani walipewa pia njia ya kufikia Mto Zambezi katika kanda lililoitwa baadaye Kishoroba cha Caprivi.
|
20231101.sw_3114_13
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mkataba%20wa%20Helgoland-Zanzibar
|
Mkataba wa Helgoland-Zanzibar
|
Pande zote mbili zilipatana kuhusu mipaka kati ya makoloni yao ya Togo ya Kijerumani na "Pwani ya dhahabu ya Kiingereza" (leo Ghana) halafu kati ya Kamerun na "eneo la Kiingereza linalopakana" (leo Nigeria).
|
20231101.sw_3114_14
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mkataba%20wa%20Helgoland-Zanzibar
|
Mkataba wa Helgoland-Zanzibar
|
Uingereza uliachia Ujerumani kisiwa cha Helgoland katika Bahari ya Kaskazini. Kisiwa hicho kiliwahi kuchukuliwa na Uingereza wakati wa vita dhidi ya Napoleon Bonaparte mwaka 1807 ikawa koloni la Kiingereza. Kisiwa kilidaiwa na Ujerumani kwa sababu kihistoria ni sehemu ya jimbo la Frisia ya Kaskazini lililokuwa sehemu ya Ujerumani baada ya kuhamishwa mara kadhaa kati ya Ujerumani na Denmark.
|
20231101.sw_3114_15
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mkataba%20wa%20Helgoland-Zanzibar
|
Mkataba wa Helgoland-Zanzibar
|
The Anglo-German Treaty (Heligoland–Zanzibar Treaty) 1 July 1890, Translation of the German version of the contract
|
20231101.sw_3114_16
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mkataba%20wa%20Helgoland-Zanzibar
|
Mkataba wa Helgoland-Zanzibar
|
Vertrag zwischen dem Deutschen Reich und dem Vereinigten Königreich über die Kolonien und Helgoland vom 1. Juli 1890, Deutsche Geschichte in Dokumenten und Bildern (DGDB), Transcription of: Das Staatsarchiv. Sammlung der offiziellen Aktenstücke zur Geschichte der Gegenwart, Bd. 51, Duncker & Humblot, Leipzig 1891, S. 151.
|
20231101.sw_3114_17
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mkataba%20wa%20Helgoland-Zanzibar
|
Mkataba wa Helgoland-Zanzibar
|
Yokell, Marshall A.: "The treaty of Helgoland-Zanzibar : the beginning of the end for the Anglo-German friendship?" (2010), Master's Theses, University of Richmond, Paper 694, includes the citation of the English version of the contract
|
20231101.sw_3115_0
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Funguvisiwa%20la%20Lamu
|
Funguvisiwa la Lamu
|
Funguvisiwa la Lamu ni kundi la visiwa katika Bahari Hindi mbele ya pwani ya Kenya kaskazini ambavyo ni sehemu ya Kaunti ya Lamu, Kenya.
|
20231101.sw_3115_1
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Funguvisiwa%20la%20Lamu
|
Funguvisiwa la Lamu
|
Mji mkubwa zaidi ni Lamu kwenye Kisiwa cha Lamu. Mji huu uko katika orodha ya Urithi wa dunia ya UNESCO.
|
20231101.sw_3115_2
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Funguvisiwa%20la%20Lamu
|
Funguvisiwa la Lamu
|
Funguvisiwa la Lamu lina sehemu mbalimbali zenye mabaki muhimu ya kiakiolojia kutoka vyanzo vya utamaduni wa Waswahili kama vile Takwa na mji wa Manda halafu Shanga, Pate.
|
20231101.sw_3115_3
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Funguvisiwa%20la%20Lamu
|
Funguvisiwa la Lamu
|
Kuna taarifa ya kwamba jahazi za kundi la meli la Zheng He zilizama karibu na Lamu mnamo mwaka 1415. Mabaharia wa jahazi hizi walibaki kwenye visiwa na kuoa wanawake wa huko. Uchunguzi wa DNA wa wenyeji umethibitisha kuwepo kwa damu ya Kichina.
|
20231101.sw_3115_4
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Funguvisiwa%20la%20Lamu
|
Funguvisiwa la Lamu
|
Allen, James de Vere: Lamu, with an appendix on Archaeological finds from the region of Lamu by H. Neville Chittick. Nairobi: Kenya National Museums.
|
20231101.sw_3115_5
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Funguvisiwa%20la%20Lamu
|
Funguvisiwa la Lamu
|
Martin, Chryssee MacCasler Perry; Martin, Esmond Bradley: "Quest for the Past: An Historical Guide to the Lamu Archipelago" Marketing and Publishing Ltd., 1973.
|
20231101.sw_3118_0
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Witu
|
Witu
|
Witu ni mji mdogo, kata na tarafa katika kaunti ya Lamu, eneo bunge la Lamu Magharibi, mashariki mwa Kenya.
|
20231101.sw_3118_1
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Witu
|
Witu
|
Mji huu upo kilomita 5 (maili 3) magharibi mwa msitu wa Witu, barabarani kutoka Malindi kwenda Lamu, takriban katikati ya mto Tana na Lamu.
|
20231101.sw_3118_2
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Witu
|
Witu
|
Katika karne ya 19 ilikuwa mji mkuu wa Usultani wa Witu. Kwa muda mfupi, kati ya mwaka 1885 hadi 1890, usultani wa Witu ulikuwa nchi lindwa chini ya Ujerumani na sehemu ndogo katika delta ya mto Tana ilikuwa koloni la moja kwa moja.
|
20231101.sw_3118_3
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Witu
|
Witu
|
Historia ya Witu ilianza mwaka 1858 BK. Sultani wa Pate Ahmad ibn Fumo Bakari, aliyezaliwa katika familia ya watawala wa Nabahani, alijenga makao mapya barani kwa sababu alitaka kujiokoa na Usultani wa Zanzibar uliotafuta utawala juu ya funguvisiwa la Lamu wakati ule.
|
20231101.sw_3118_4
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Witu
|
Witu
|
Mashambulio ya Wazanzibari yaliendelea na kumsababisha sultani kuomba msaada wa ulinzi wa Ujerumani mara ya kwanza mwaka 1867. Mwaka 1885 Sultani alifunga mkataba na ndugu Wajerumani Clemens na Gustav Denhardt akaweka nchi yake chini ya ulinzi wa Dola la Ujerumani kuanzia tarehe 27 Mei 1885. Kama shukrani kwa ndugu Denhardt aliwapa eneo la maili za mraba 25 akawafanya kuwa mawaziri wake.
|
20231101.sw_3118_5
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Witu
|
Witu
|
Sultani wa Zanzibar hakufurahia habari hizi wala balozi wa Uingereza Zanzibar mjini. Lakini mipango yao dhidi ya Witu ilishindikana kwa sababu serikali ya Ujerumani ilituma manowari SMS Gneisenau Afrika ya Mashariki na wanajeshi 30 Wajerumani walipiga kambi Witu. Mwaka 1888 Ujerumani ilifungua ofisi ya posta Lamu mjini kwa ajili ya mawasiliano kati ya Witu na Ujerumani kwa sababu meli zilipita mara kwa mara Lamu ilhali Witu haikuwa na bandari kamili.
|
20231101.sw_3118_6
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Witu
|
Witu
|
Serikali ya Ujerumani haikuonyesha nia ya kuimarisha utawala wake kwenye pwani ya Kenya; iliona Witu kama bidhaa kwa ajili ya biashara na Waingereza. Katika mkataba wa Helgoland-Zanzibar Witu iliachiliwa Uingereza na ulinzi wa Ujerumani ulikwisha tarehe 1 Julai 1890.
|
20231101.sw_3118_7
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Witu
|
Witu
|
Wenyeji wa Witu hawakupendezwa na mabadiliko hayo kwa sababu waliogopa ya kwamba watafikishwa chini ya Zanzibar, angalau waliwajua Waaingereza kuwa karibu sana na Sultani wa Zanzibar. Walihisi kuwa Wajerumani waliwasaliti. Katika Septemba 1890 ilitokea ugomvi mkali. Mfanyabiashara Mjerumani Andreas Küntzel alitegemea kuanzisha biashara katika eneo la Sultani lakini alikataliwa kwa sababu ya hasira iliyosababishwa na mkataba wa Julai 1890. Wenzake Küntzel walijaribu kulazimisha maafisa wa Sultani kwa kuonyesha silaha lakini walikamatwa, na silaha zao kuchukuliwa. Küntzel alijaribu kuwaweka huru akamtukana sultani mbele ya watu wake. Wenyeji wenye hasira waliwaua Wajerumani wale na kushambulia Wazungu wengine. Jumla Wajerumani 9 waliuawa, wengine wakakimbia.
|
20231101.sw_3118_8
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Witu
|
Witu
|
Waingereza walituma jeshi chini ya Admirali Sir E. Freemantle wakavamia Witu katika Septemba 1890. Tarehe 28 Oktoba 1890 mji mkuu wa Witu ulichomwa moto na Waingereza. Lakini mapigano yaliendelea. Kuna makadirio ya kwamba wenyeji 500 waliuawa, mji Witu ikaharibika na Sultani alitupwa jela alikokufa. Mapigano yaliendelea hadi mwaka 1894. Witu ikawa koloni la Uingereza. Katika mkataba wa Helgoland-Zanzibar Uingereza iliahidi ya kwamba itaheshimu mipaka ya eneo la Witu. Awali Waingereza walimteua sultani mpya Omar-bin-Hamed aliyetoka katika ukoo wa Nabahani vilevile.
|
20231101.sw_3118_9
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Witu
|
Witu
|
Lakini baadaye hawakuheshimu tena usultani wa Witu jinsi walivyowahi kuahidi katika mkataba wa 1890 wakaitendea kama sehemu ya mkoa wa Tana tu.
|
20231101.sw_3118_10
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Witu
|
Witu
|
Habari za uvamizi wa Waingereza katika Witu 1890 na 1893 kutokana na taarifa rasmi ya Admiral Freemantle
|
20231101.sw_3119_0
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Tana%20%28mto%29
|
Tana (mto)
|
Chanzo chake ni milima ya Aberdare magharibi kwa Nyeri. Mwanzoni unelekea mashariki, halafu inapinda kuzunguka Mlima Kenya upande wa kusini. Kisha huingia ndani ya mabwawa ya Masinga na Kiambere yaliyotokana na bwawa la Kindaruma. Chini ya bwawa mto huu hugeuka kuelekea kaskazini na kutiririka mpaka wa kaskazini-kusini kati ya kaunti za Meru na Kitui, Bisanadi, Kora na Hifadhi ya wanyama ya Rabole. Ndani ya hifadhi hugeuka kuelekea mashariki, na kisha kusini mashariki.
|
20231101.sw_3123_0
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Aruwimi
|
Aruwimi
|
Chanzo chake ni kwenye Mkoa wa Mashariki / Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo katika Milima ya Buluu, si mbali na mji wa Bunia na Ziwa Albert.
|
20231101.sw_3123_1
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Aruwimi
|
Aruwimi
|
Mwanzoni inaelekea kusini halafu inapinda kwenda magharibi hadi kufikia mto Kongo karibu na mji wa Basoko.
|
20231101.sw_3124_0
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Helgoland
|
Helgoland
|
Helgoland ni fungukisiwa ndogo cha Kijerumani katika Bahari ya Kaskazini takriban 70 km mbele ya Ujerumani bara. Ina visiwa viwili: Helgoland yenyewe ni kisiwa kinachokaliwa na watu halafu kisiwa kisicho na watu cha "Düne" (= tuta la mchanga). Kisiwa kikuu kina urefu wa 1700 m na wakazi 1,650.
|
20231101.sw_3124_1
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Helgoland
|
Helgoland
|
Kiutamaduni Helgoland ni sehemu ya Frisia; wenyeji wanasema Kifrisia na Kijerumani. Iliwahi kuwa sehemu za nchi za Denmark na Ujerumani na kwa muda wa karne ya 19 BK pia chini ya Uingereza.
|
20231101.sw_3124_2
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Helgoland
|
Helgoland
|
Zamani wakazi wa Helgoland walikuwa wavuwi na mabaharia. Tangu karne ya 19 utalii ilianza kuwa muhimu siku hizi wengi wanajipatia maisha kwa njia ya utalii.
|
20231101.sw_3124_3
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Helgoland
|
Helgoland
|
Helgoland ilivamiwa na Uingereza wakati wa vita kati ya Napoleon na Uingereza mw. 1807. Kisiwa cha Helgoland kikabaki kituo cha kijeshi cha Uingereza hadi 1890. Tangu kutokea kwa utaifa katika Ujerumani utawala wa kigeni ulisikitisha Wajerumani wengi.
|
20231101.sw_3124_4
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Helgoland
|
Helgoland
|
Serikali ya Dola la Ujerumani ilichukua nafasi ya majadiliano kuhusu mapatano ya mipaka ya kikoloni kati ya Uingereza na Ujerumani kuingiza swali la Helgoland katika mapatano haya.
|
20231101.sw_3124_5
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Helgoland
|
Helgoland
|
Mapatano kati ya Ujerumani na Uingereza ya tarehe 01. 07. 1890 yalisuluhisha maswali mbalimbali kuhusu mipaka ya maeneo yao katika Afrika ya Mashariki, ya Kusini-Magharibi na ya Magharibi. Maeneo mawili yaliyoangaliwa hasa na watu yalikuwa Zanzibar na Helgoland. Hivyo mapatano yamejulikana zaidi kwa jina la Mkataba wa Helgoland-Zanzibar ingawa jina rasmi lilikuwa "Mkataba kuhusu koloni na Helgoland" ikiwa visiwa viwili vilikuwa tu vipengele katika orodha ndefu ya maswali yaliyopata usulihisho.
|
20231101.sw_3124_6
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Helgoland
|
Helgoland
|
Wafuasi wa hoja la kupanusha athira ya Ujerumani duniani walisikitika sana ya kwamba serikali ya Chansella Caprivi ilifuta madai ya Ujerumani juu ya Zanzibar na Uganda kwa ajili ya "mwamba mdogo" wa Helgoland. Lakini miaka 73 baada ya mkataba Uingereza haukuwa tena na neno kuhusu Zanzibar lakini Helgoland imeendelea kuwa sehemu ya Ujerumani.
|
20231101.sw_3129_0
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Chad%20%28ziwa%29
|
Chad (ziwa)
|
Ziwa Chad ni ziwa kubwa lisilo na njia ya kutoka lenye kina kidogo katika kanda la Sahel, kando ya jangwa kubwa la Sahara, kule ambako nchi za Chad, Kamerun, Niger na Nigeria zinapopakana, hivi kwamba eneo lake limegawanywa kati ya nchi hizo. Ziwa Chad lina umuhimu mkubwa kwa uchumi wa watu milioni 68 katika nchi hizo nne.
|
20231101.sw_3129_1
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Chad%20%28ziwa%29
|
Chad (ziwa)
|
Beseni lake ni beseni kubwa le bara la Afrika. Hata hivyo, eneo la uso wake limebadilika katika mwendo wa karne zilizopita kutegemeana na kiasi cha maji lilichopokea na kiwango cha uvukizaji na matumizi ya maji yake.
|
20231101.sw_3129_2
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Chad%20%28ziwa%29
|
Chad (ziwa)
|
Ziwa Chad lilipungua kwa asilimia 98 baina ya miaka 1963 na 1998 lakini picha za satelaiti za ESA zimeonyesha ya kwamba baada ya hapo limepanuka tena kiasi.
|
20231101.sw_3131_0
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Rukwa%20%28ziwa%29
|
Rukwa (ziwa)
|
Ziwa Rukwa ni ziwa kubwa la magadi nchini Tanzania. Liko upande wa kusini magharibi wa nchi, karibu na Zambia, kati ya Ziwa Tanganyika na Ziwa Nyasa..
|
20231101.sw_3131_1
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Rukwa%20%28ziwa%29
|
Rukwa (ziwa)
|
Ziwa liko kwenye kimo cha mita 800 juu ya UB katika bonde ambalo ni mkono wa Bonde la Ufa la Afrika ya Mashariki. Bonde hili ni sehemu ya kusini ya mkono wa magharibi wa bonde hili na mikono yote miwili inaungana huko Mbeya kabla ya kuendelea kwa pamoja katika Ziwa Nyasa.
|
20231101.sw_3131_2
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Rukwa%20%28ziwa%29
|
Rukwa (ziwa)
|
Beseni ya ziwa line eneo la takriban 80,000 km². Urefu na upana wake hubadilikabadilika kulingana na kiasi cha mvua inayonyesha. Kati ya mito inayoingia ni mto wa Songwe pekee ulio na maji muda wote. Kuna taarifa ya kwamba ziwa lilipotea wakati mwingine isipokuwa beseni ndogo upande wa kusini Songwe inapoingia hubaki na maji. Kama maji ni mengi ziwa lina urefu wa kilomita 180.
|
20231101.sw_3131_3
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Rukwa%20%28ziwa%29
|
Rukwa (ziwa)
|
Eneo la ziwa ni kavu sana na maji yake ni ya magadi. Kwa hiyo hakuna vijiji mbali na mito hasa upande wa kusini. Wakazi wa jirani ni hasa Wafipa, Wanyamwanga na Wasafwa.
|
20231101.sw_3134_0
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kwango
|
Kwango
|
Kwango (au Cuango) ni mto wa Angola na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ambao ni pia tawimto mrefu wa mto Kasai.
|
20231101.sw_3134_1
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kwango
|
Kwango
|
Chanzo chake kiko nyanda za juu za Bié katika Angola kikielekea kaskazini. Inakuwa mpaka kati ya Angola na Kongo halafu kuingia ndani ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Inaishia kwenye mto Kasai karibu na mji wa Bandudu.
|
20231101.sw_3136_0
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kwando
|
Kwando
|
Kwando (au: Cuando; kabla ya mdomo pia Linyanti halafu Chobe) ni mto wa Afrika ya Kusini na tawimto la Zambezi. Chanzo chake kiko nyanda za juu za Bié (Angola) inapoelekea kusini-mashariki. Inakuwa mpaka kati ya Angola na Zambia kwa km 140, halafu inapita Kishoroba cha Caprivi na kuwa mpaka kati ya Namibia na Botswana.
|
20231101.sw_3136_1
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kwando
|
Kwando
|
Inaingia katika mabwawa wa Linyanti yenye km² 1,425. Katika sehemu hizo mto huitwa Chobe au Liyanti.
|
20231101.sw_3136_2
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kwando
|
Kwando
|
Kwa jina la Chobe unaingia katika mto Zambezi kwenye mji wa Kazungula pale ambapo nchi nne za Botswana, Namibia, Zambia na Zimbabwe zinapokutana.
|
20231101.sw_3144_0
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Gambia%20%28mto%29
|
Gambia (mto)
|
Gambia ni mto unaoanza katika milima ya Futa Djalon huko Guinea. Unafuata njia ya kunyoka hadi Atlantiki. Mdomo wake ni pana sana.
|
20231101.sw_3144_1
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Gambia%20%28mto%29
|
Gambia (mto)
|
Baada ya kutoka katika Futa Djallon mto unaelekea kaskazini-magharibi kupitia mkoa wa Tambakunda katika Senegal halafu mbuga wa wanyama wa Niokolo Koba. Hapa inapokea tawimiti ya Nieri Ko and Kuluntu na kuingia katika nchi ya Gambia karibu na mji wa Fatoto.
|
20231101.sw_3144_2
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Gambia%20%28mto%29
|
Gambia (mto)
|
Kuanzia hapa mto unaelekea magharibi tu isipokuwa kwa njia ya kunyokanyoka. Takriban km 100 kabla ya kufika mdomo unaanza kupanuka ukiwa na upana wa km 10 mdomoni penyewe.
|
20231101.sw_3144_3
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Gambia%20%28mto%29
|
Gambia (mto)
|
Mto una visiwa mbalimbali ndani yake, vikubwa zaidi ni kisiwa cha Tembo na kisiwa cha MacCarthy. Kisiwa cha James Island mdomoni kabisa kilikuwa kituo muhimu cha biashara ya watumwa na kimeandikishwa katika orodha ya UNESCO ya Urithi wa Dunia.
|
20231101.sw_3144_4
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Gambia%20%28mto%29
|
Gambia (mto)
|
Kutokana na upana na wingi wa maji Gambia inafaa kama njia ya maji; meli za baharini zinaingia ndani takriban km 280.
|
20231101.sw_3146_0
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Turkana%20%28ziwa%29
|
Turkana (ziwa)
|
Ziwa Turkana ni ziwa kubwa lililopo katika kaskazini yabisi ya Kenya. Halina mto unaotoka, hivyo maji yanayoingia yanapotea kwa njia ya uvukizaji. Kwa jumla ni ziwa la Kenya lakini ncha ya kaskazini iko ndani ya Ethiopia. Ni pia ziwa la jangwani liliko kubwa kuliko yote duniani.
|
20231101.sw_3146_1
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Turkana%20%28ziwa%29
|
Turkana (ziwa)
|
Umbo la ziwa ni kama kanda ndefu inayoelea kutoka kaskazini kwenda kusini. Urefu wa ziwa ni kilomita 290, upana wake hadi kilomita 32. Eneo la maji ni km² 6,405. Ndani ya ziwa kuna visiwa vitatu vidogo vinyavoitwa Kisiwa cha kusini, cha kati na cha kaskazini.
|
20231101.sw_3146_2
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Turkana%20%28ziwa%29
|
Turkana (ziwa)
|
Turkana ni ziwa la magadi lakini maji yake hunywewa na watu na wanyama na yanawezesha viumbehai wengi kuishi ndani yake.
|
20231101.sw_3146_3
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Turkana%20%28ziwa%29
|
Turkana (ziwa)
|
Hifadhi za wanyama kwenye ziwa Turkana zimeorodheshwa na UNESCO kama Urithi wa Dunia, zikiwemo Hifadhi ya Taifa ya Sibiloi (mashariki kwa ziwa), Hifadhi ya Taifa ya Kisiwa cha Kati na Hifadhi ya Taifa ya Kisiwa cha Kusini (visiwani).
|
20231101.sw_3146_4
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Turkana%20%28ziwa%29
|
Turkana (ziwa)
|
Mazingira hayo yote yanahatarishwa sasa na ujenzi wa lambo la Gilgel Gibe III kwenye mto Omo unaochangia ziwa kwa kiasi kikubwa.
|
20231101.sw_3146_5
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Turkana%20%28ziwa%29
|
Turkana (ziwa)
|
Wenyeji wametumia majina mbalimbali kufuatana na lugha zao. Waturkana hutumia "anam Ka'alakol" yaani "ziwa la samaki wengi". Wapelelezi Wazungu wa karne ya 19 walisikia jina la "Basso Narok" ingawa haieleweki hii ilikuwa lugha gani.
|
20231101.sw_3146_6
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Turkana%20%28ziwa%29
|
Turkana (ziwa)
|
Kimataifa ziwa lilijulikana zamani kwa jina la "Ziwa Rudolph" (Rudolfsee, Lake Rudolph) lililotolewa na mpelelezi Mhungaria Sámuel Teleki kwa heshima ya mtemi Rudolph, mtoto wa mfalme wa Austria-Hungaria.
|
20231101.sw_3146_7
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Turkana%20%28ziwa%29
|
Turkana (ziwa)
|
Mto wa kwanza kabisa katika kuchangia ziwa Turkana (90% hivi) uko upande wa Ethiopia: ni mto Omo (na matawimto yake na ya mito midogo zaidi inayoyachangia, kama Mto Usno, Mto Mago, Mto Neri, Mto Mui, Mto Mantsa, Mto Zigina, Mto Denchya, Mto Gojeb, Mto Gibe, Mto Gilgel Gibe, mto Amara, mto Alanga, Mto Maze na Mto Wabe. Miaka mingine Mto Kibish pia unafikia ziwa hilo.
|
20231101.sw_3146_8
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Turkana%20%28ziwa%29
|
Turkana (ziwa)
|
Mito mingine mingi inachangia pia ziwa Turkana upande wa Kenya, ingawa si kwa kiasi kile cha mto Omto; ni hii ifuatayo:
|
20231101.sw_3146_9
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Turkana%20%28ziwa%29
|
Turkana (ziwa)
|
Mito ifuatayo kutoka Uganda inachangia pia ziwa Turkana kupitia Kenya: Mto Arionomunyen, Mto Chosan, Mto Ekiringura, Mto Kacholese, Mto Kalodurr, Mto Kalopomongole, Mto Kanyagareng, Mto Komongim, Mto Koromoich, Mto Laburin, mto Lobuloyin, Mto Lochorakwangen, Mto Lodias, Mto Loitabela, Mto Lomapus, Mto Lopedot, Mto Naakot, Mto Nabunei, Mto Nakakerikeri, Mto Nakalale, Mto Nakatuman, Mto Namusio, Mto Nangolipia, Mto Natire, Mto Naunyet, Mto Nauyagum, Mto Onogin na Mto Otiko.
|
20231101.sw_3153_0
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Chari
|
Chari
|
Chari (Shari) ni mto mkubwa unaoishia katika Ziwa Chad. Unaanza katika Jamhuri ya Afrika ya Kati ukielekea kaskazini na kuingia nchi ya Chad. Baada ya kupita mji mkuu N'Djamena mto uunaunda mpaka na Kamerun halafu unaishia katika Ziwa Chad.
|
20231101.sw_3158_0
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Atbara%20%28mto%29
|
Atbara (mto)
|
Atbara (kwa Kiarabu: نهر عطبرة, Nahr ʿAṭbara) ni tawimto la Nile linalopatikana kaskazini magharibi mwa Ethiopia na katika Sudan.
|
20231101.sw_3158_1
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Atbara%20%28mto%29
|
Atbara (mto)
|
Chanzo chake ni katika milima ya Simien (Ethiopia) takriban km 50 kaskazini kwa Ziwa Tana au km 30 magharibi kwa mji wa Gondar.
|
20231101.sw_3158_2
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Atbara%20%28mto%29
|
Atbara (mto)
|
Tawimto lake ni hasa mto Tekeze (Setit) ambao una matawimto mengi. Kiasi cha maji ndani ya Atbara hubadilika sana. Miezi mingi ni mto mdogo sana unaopita katika nchi yabisi lakini wakati wa mvua katika nyanda za juu za Ethiopia unakuwa mpana wenye maji mengi.
|
20231101.sw_3158_3
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Atbara%20%28mto%29
|
Atbara (mto)
|
Kwenye mji wa Atbara nchini Sudan unaishia katika mto Nile, ukiwa tawimto lake la mwisho kabla ya kufikia Bahari ya Kati.
|
20231101.sw_3159_0
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mhozo
|
Mhozo
|
Mihozo ni ndege wa jenasi Oenanthe, Saxicola na Campicoloides. Zamani wataalamu waliwaweka katika familia ya mikesha (Turdidae), lakini siku hizi mihozo huainiwa baina ya shore (Muscicapidae). Mihozo wana mabaka maalum meusi na meupe au mekundu na meupe kwa kiuno na mkia wao mrefu. Ndume ni maridadi kuliko jike. Hukaa chini na hula wadudu. Wanatokea nyanda kavu katika Afrika, Ulaya na Asia. Spishi zinazozaa katika nchi za kaskazini huhamia Afrika wakati wa baridi. Hujenga matago yao ndani ya mianya ya miamba au vishimo visivyotumika.
|
20231101.sw_3160_0
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ujerumani
|
Ujerumani
|
Uchumi wa Ujerumani una uwezo mkubwa: ni nchi inayouza bidhaa nyingi nje kushinda mataifa yote duniani.
|
20231101.sw_3160_1
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ujerumani
|
Ujerumani
|
Muundo wake kiutawala ni shirikisho la jamhuri lenye majimbo 16 ndani yake na kila jimbo lina kiwango cha kujitawala.
|
20231101.sw_3160_2
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ujerumani
|
Ujerumani
|
Wenyeji wanaiita nchi "Deutschland" (, tamka: doich-land) na jina hilo limeingia katika Kiswahili kama "Udachi". Lilikuwa jina la kawaida katika karne ya 19 na mwanzoni mwa karne ya 20.
|
20231101.sw_3160_3
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ujerumani
|
Ujerumani
|
Siku hizi neno "Ujerumani" limechukua nafasi yake kutokana na Kiingereza kinachoiita "Germany". Watu wengine hulichukua "Udachi" kuwa na maana "Uholanzi" wakilichanganya na neno la Kiingereza "Dutch" (tamka datsh) linalomaanisha "Kiholanzi".
|
20231101.sw_3160_4
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ujerumani
|
Ujerumani
|
Ujerumani unaenea kati ya Bahari ya Kaskazini halafu ya Bahari Baltiki upande wa kaskazini na milima ya Alpi upande wa kusini. Mpaka na Denmark inakata sehemu ya kusini ya rasi ya Jutland. Mpaka wa kusini unafuata sehemu za chini za Alpi, Ziwa la Konstanz na mto Rhein dhidi ya Austria na Uswisi.
|
20231101.sw_3160_5
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ujerumani
|
Ujerumani
|
Mipaka yake upande wa magharibi na mashariki ilibadilika mara nyingi katika historia yake; baada ya vita kuu mbili za karne ya 20 maeneo makubwa yalitengwa na Ujerumani na kuwa sehemu za Poland, Urusi, Ucheki na Ufaransa. Wakazi Wajerumani kwa mamilioni walifukuzwa au kuwa raia wa nchi hizo.
|
Subsets and Splits
No community queries yet
The top public SQL queries from the community will appear here once available.