_id
stringlengths
15
22
url
stringlengths
31
150
title
stringlengths
1
86
text
stringlengths
100
23.8k
20231101.sw_3160_6
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ujerumani
Ujerumani
Tangu mwaka 1945 mpaka wa mashariki ni mto Oder dhidi ya Poland na vilele vya Milima ya Madini (jer. Erzgebirge) na Msitu wa Bohemia.
20231101.sw_3160_7
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ujerumani
Ujerumani
Upande wa magharibi mpaka na Ufaransa ni mto Rhein pamoja na vilima kati ya Alsasi na Rhine-Palatino na vilima dhidi ya Luxemburg na milima ya Eifel dhidi ya Ubelgiji. Mpaka na Uholanzi katika magharibi kaskazini inapita katika tambarare ikifuata mistari ya kihistoria.
20231101.sw_3160_8
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ujerumani
Ujerumani
uwanda wa kaskazini ambao ni sehemu ya Tambarare ya Ulaya Kaskazini ni takriban theluthi ya eneo lake
20231101.sw_3160_9
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ujerumani
Ujerumani
Tambarare ya pwani ya kaskazini ni eneo bapa; hakuna milima na nchi haipandi juu ya mita 200, sehemu kubwa ni kati ya uwiano wa bahari na mita 60 juu yake. Uso wa nchi ni tokeo la kupitiwa na barafuto kubwa za enzi ya barafu iliyopita iliyonyosha uso wa nchi ikiacha vilima vya mchanga, kokoto na ardhi ambavyo ni miinuko pekee inayofika hadi mita 200 juu ya uwiano wa bahari.
20231101.sw_3160_10
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ujerumani
Ujerumani
Nyanda za milima ya kati ni mabaki ya milima ya kale iliyotokea miaka milioni 350 iliyopita na kupungua sana tangu zamani zile kwa njia ya mmomonyoko. Kwa hiyo hakuna vilele vikali bali vyote vina umbo poa.
20231101.sw_3160_11
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ujerumani
Ujerumani
Alpi katika kusini ni milima mirefu Ujerumani ingawa sehemu kubwa na za juu zaidi ziko nje ya mipaka ya Ujerumani huko Ufaransa, Italia, Uswisi na Austria. Milima hiyo ilianza kutokea miaka 135-50 milioni iliyopita tu. Kilele cha juu katika Ujerumani ni mlima wa Zugspitze yenye urefu wa mita 2,962 juu ya UB.
20231101.sw_3160_12
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ujerumani
Ujerumani
Makabila mbalimbali ya Wagermanik yamekuwa yakiishi kaskazini mwa Ujerumani wa leo tangu zamani za Roma ya Kale. Eneo lililoitwa kwa Kilatini "Germania" linajulikana tangu mwaka 100 BK.
20231101.sw_3160_13
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ujerumani
Ujerumani
Kuanzia mwaka 400 hivi, wakati wa Dola la Roma kudhoofika, makabila hayo yalisambaa hasa kwenda kusini.
20231101.sw_3160_14
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ujerumani
Ujerumani
Mnamo mwaka 800 Karolo Mkuu, mtawala wa Wafaranki, aliunganisha maeneo ya Ujerumani na Ufaransa ya leo akaendelea kutwaa Italia ya Kaskazini na ya Kati hadi Roma. Mwaka 800 Papa alimpa cheo cha "Kaisari wa Roma". Baada ya kifo chake himaya iligawanyika, na upande wa mashariki hatimaye viongozi wa makabila walikutana mwaka 919 wakamchagua mfalme kati yao anayehesabiwa kuwa mfalme wa kwanza wa Wajerumani.
20231101.sw_3160_15
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ujerumani
Ujerumani
Kuanzia karne ya 10 wafalme wa Ujerumani walikuwa pia wadhamini wa Papa wa Roma aliyeendelea kuwapa cheo cha "Kaisari". Hivyo himaya yao iliitwa Dola Takatifu la Kiroma.
20231101.sw_3160_16
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ujerumani
Ujerumani
Katika karne ya 16 maeneo ya Ujerumani kaskazini yakawa kiini cha Matengenezo ya Kiprotestanti katika Ukristo.
20231101.sw_3160_17
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ujerumani
Ujerumani
Kisha kushindwa katika vita vikuu vya kwanza, hilo Dola la Ujerumani lilikoma na kuiachia nafasi Jamhuri ya Weimar.
20231101.sw_3160_18
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ujerumani
Ujerumani
Adolf Hitler aliposhika uongozi wa nchi mwaka 1933 aligeuza nchi kuwa ya kidikteta na kuingiza dunia katika vita vikuu vya pili ambapo hasa Wayahudi waliangamizwa kwa mamilioni katika makambi maalumu.
20231101.sw_3160_19
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ujerumani
Ujerumani
Baada ya kushindwa tena vitani, nchi iligawanyika pande mbili, magharibi chini ya Marekani, Uingereza na Ufaransa, na mashariki chini ya Muungano wa Kisovyeti.
20231101.sw_3160_20
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ujerumani
Ujerumani
Ukomunisti ulipopinduliwa mwaka 1989, tarehe 3 Oktoba 1990 Ujerumani mashariki ulijiunga na shirikisho la Ujerumani magharibi ambao ulikuwa tayari kati ya nchi waanzilishi wa Umoja wa Ulaya wa leo.
20231101.sw_3160_21
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ujerumani
Ujerumani
Wakazi ni Wajerumani asilia (76.4%), Wazungu wengine (11%), Waturuki (3.4%), Waasia wengine (3.5%, hasa kutoka Mashariki ya Kati), Waafrika (0.8%) n.k. Kati yao, 12% si raia wa nchi.
20231101.sw_3160_22
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ujerumani
Ujerumani
Lugha asilia ni Kijerumani kinachojadiliwa kwa lahaja mbalimbali, lakini wenyeji wote wanasikilizana. Katika maeneo mawili kuna wasemaji asilia wa Kideni na Kisorbia.
20231101.sw_3160_23
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ujerumani
Ujerumani
Upande wa dini, kadiri ya sensa ya mwaka 2011, Wakristo ni 66.8% (Wakatoliki 30.8%, Walutheri 30.3%, Waprotestanti wengine 5.7%), huku Waislamu wakiwa 1.9%. Thuluthi moja ya wakazi haina dini yoyote. Kadirio la mwaka 2021 linasema Wakristo ni 52.7% (Wakatoliki 26%, Waprotestanti 23.7%, Waorthodoksi 1.9%, wengineo 1.1%), Waislamu walau 3.6%, Wabudha 0.3%, Wahindu 0.1%, Wayahudi 0.1%, Wayazidi 0.1%. Wasio na dini yoyote ni 41.9%.
20231101.sw_3161_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/Okapi
Okapi
Okapi (jina la kisayansi: Okapia johnstoni) ni mamalia wa familia ya twiga. Umbo lake hufanana na farasi ina michoro miguuni kama punda milia lakini haina uhusiano naye, ni aina ya twiga.
20231101.sw_3161_1
https://sw.wikipedia.org/wiki/Okapi
Okapi
Okapi ni mnyama aliyejulikana na wenyeji wa maeneo yake tu hadi mwaka 1901. Hapo zamani ilikuwa inaaminika kuwa mnyama huyu hupatikana tu katika misitu ya Ituri lakini mwaka 2006 zilipatikana dalili zilizoonyesha kwamba mnyama huyu yuko pia kwenye misitu ya hifadhi ya taifa ya Kongo ya Virunga. Kwenye misitu ya Ituri kuna hifadhi ya Okapi yenye eneo la km² 14,000.
20231101.sw_3161_2
https://sw.wikipedia.org/wiki/Okapi
Okapi
Shingo yake ni fupi kuliko twiga lakini ina ulimi mrefu sana wa kujipatia majani unaomwezesha kusafisha masikio yake yeye mwenyewe. Dume ina pembe mbili fupi kichwani.
20231101.sw_3161_3
https://sw.wikipedia.org/wiki/Okapi
Okapi
Kimo cha okapi ni hadi mita 2.5 kichwani na hadi mita 2 mabegani. Anafikia uzito kati ya kg 200 hadi 250. Anakula majani ya miti pamoja na nyasi, matunda na nyoga.
20231101.sw_3162_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/Limpopo%20%28mto%29
Limpopo (mto)
Chanzo kipo katika milima ya Witwatersrand, kati ya Pretoria na Johannesburg, nchini Afrika Kusini. Sehemu ya kwanza inaitwa "Krokodil" (Kiafrikaans kwa mamba). Baada ya kupokea mto wa Marico jina linabadilika na kuwa Limpopo. Hapo unapita mwendo wa upinde mkubwa ukielekea kwanza kaskazini-magharibi halafu mashariki hadi Bahari Hindi. unafuata mpaka kati ya Afrika Kusini na Botswana, halafu mpaka wa Afrika Kusini na Zimbabwe.
20231101.sw_3162_1
https://sw.wikipedia.org/wiki/Limpopo%20%28mto%29
Limpopo (mto)
Tawimto mkubwa ni mto Olifants (Limpopo) (Kiafrikaans kwa tembo) unaojiunga na Limpopo katika Msumbiji km 200 kabla ya mdomo wake. Mto unafikia Bahari Hindi kwenye mji wa Xai-Xai (Msumbiji).
20231101.sw_3168_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/Msumbiji%20%28kisiwa%29
Msumbiji (kisiwa)
Kisiwa cha Msumbiji (kwa lugha ya Kireno: "Ilha de Moçambique") ni kisiwa kidogo (na pia mji) kilichopo km 3 mbele ya mwambao wa Msumbiji ya kaskazini. Urefu ni km 3 na upana kati ya m 500 hadi 200. Kisiwa ni sehemu ya mkoa wa Nampula.
20231101.sw_3168_1
https://sw.wikipedia.org/wiki/Msumbiji%20%28kisiwa%29
Msumbiji (kisiwa)
Kisiwa kilikuwa chanzo cha koloni la Kireno la Msumbiji na mji ulikuwa mji mkuu wa nchi kwa karne kadhaa hadi mwaka 1898 BK. Leo hii mji umepanuka kote kisiwani. Kuna wakazi 60,000 wanaoishi katika mji wenye sehemu mbili: mji wa mawe upande wa kaskazini na mji wa makuti upande wa kusini.
20231101.sw_3168_2
https://sw.wikipedia.org/wiki/Msumbiji%20%28kisiwa%29
Msumbiji (kisiwa)
Habari za kwanza za Kisiwa cha Msubiji zimetokana na Wareno. Alipofika Vasco da Gama mwaka mwaka 1498 BK kisiwa kilikuwa na mji wa Waswahili na Waarabu kikiwa kituo muhimu cha biashara ya kimataifa katika Bahari Hindi.
20231101.sw_3168_3
https://sw.wikipedia.org/wiki/Msumbiji%20%28kisiwa%29
Msumbiji (kisiwa)
Mwaka 1507 Wareno walijenga kituo cha kijeshi. Jengo la kale kisiwani ni kanisa dogo la Nossa Senhora de Baluarte lililojengwa mwaka 1522 BK.
20231101.sw_3168_4
https://sw.wikipedia.org/wiki/Msumbiji%20%28kisiwa%29
Msumbiji (kisiwa)
Tangu mwaka 1558 hadi 1620 Wareno walijenga boma kubwa la Mtakatifu Sebastiano kwa gharama kubwa. Mawe yote yalichukuliwa kwa meli kutoka Ureno, Goa (Uhindi) na pia pwani ya Msumbiji yenyewe. Umuhimu wa Msumbiji machoni pa Wareno ulikuwa nafasi ya kituo chenye usalama cha safari ndefu kati ya Ureno na Bara Hindi.
20231101.sw_3168_5
https://sw.wikipedia.org/wiki/Msumbiji%20%28kisiwa%29
Msumbiji (kisiwa)
Kisiwa kilikua kituo kikuu cha Wareno katika Afrika ya mashariki hasa baada ya kupotea Boma la Yesu huko Mombasa. Waholanzi na Wafaransa walishambulia kisiwa lakini walishindwa kuteka boma lenyewe.
20231101.sw_3168_6
https://sw.wikipedia.org/wiki/Msumbiji%20%28kisiwa%29
Msumbiji (kisiwa)
Mwanzoni Msumbiji ilitawaliwa kama sehemu ya Uhindi ya Kireno kutoka mji mkuu wa Goa. Mwaka 1720 Msumbiji ilipata kuwa kama jimbo la pekee na kisiwa cha Msumbiji kikawa mji mkuu. Kisiwa kilikuwa bandari muhimu katika biashara ya watumwa kwa visiwa vya Bahari Hindi na pia hadi Brazil ya Kireno.
20231101.sw_3168_7
https://sw.wikipedia.org/wiki/Msumbiji%20%28kisiwa%29
Msumbiji (kisiwa)
Katika miaka ya 1960 daraja lilijengwa kati ya kisiwa na bara. Idadi ya watu kisiwani imezidi kukua. Walio wengi wanaishi bila maji wala choo. Nafasi ya kila mtu ni m² 27,6 pekee.
20231101.sw_3168_8
https://sw.wikipedia.org/wiki/Msumbiji%20%28kisiwa%29
Msumbiji (kisiwa)
Kabla ya kuhamishwa kwa mji mkuu kisiwa kilikuwa makao ya Gavana Mkuu wa Msumbiji, wa askofu, wa balozi za nchi kadhaa na wafanyabiashara kutoka India, Ujerumani, Uswisi, Ufaransa na Uingereza. Mabaki yao ni majengo ya kihistoria ambayo ni mfano wa pekee wa mji wa kikoloni hasa kwa sababu ujenzi mpya haukutokea baada ya kuondoka kwa makao ya serikali.
20231101.sw_3170_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kasubi
Kasubi
Kasubi ni jina la kilima ndani ya mji wa Kampala mji mkuu wa Uganda. Kasubi imejulikana hasa kama mahali pa Makaburi ya Kasubi ya wafalme wa Buganda.
20231101.sw_3170_1
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kasubi
Kasubi
Mwaka 1882 ikulu ya Kabaka Mutesa I. ilijengwa kwenye kilima cha Kasubi. Alipokufa ikulu ikawa kaburi lake jinsi iliyvokuwa kawaida kati ya makabaka wa Buganda. Kuna desturi kwa makabila mbalimbali ya Afrika ya Mashariki ya kuwa mtu atazikwa nyumbani kwake hakuna atakeyeikalia tena.
20231101.sw_3170_2
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kasubi
Kasubi
Kutokana na kuja kwa ukoloni hapakuwa tena na nafasi ya kumjengea kila Kabaka ikulu mpya hivyo Kasubi ikawa mahali pa kaburi wa makabaka waliomfuata Mutesa I. yaani Mwanga II., Daudi Chwa II. na Mutesa II..
20231101.sw_3170_3
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kasubi
Kasubi
Jengo kuu ni Muzibu Azaala Mpanga ambalo ni kuba kubwa lililojengwa kwa ubao na matete lenye ujuu wa 12 m na kipenyo cha 31m. Ujenzi huu ni namna ya kiutamaduni kwa ajili ya majengo ya kifalme katika Afrika ya Mashariki na Kati.
20231101.sw_3170_4
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kasubi
Kasubi
Majengo mengine hukaliwa na wanawake hasa wajane wa familia ya kifalme wenye wajibu wa kuyatunza makaburi.
20231101.sw_3170_5
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kasubi
Kasubi
Majengo yamo ndani ya eneo pana la hektari 30 ambalo sehemu kubwa hulimwa na wakina mama wanaotunza makaburi.
20231101.sw_3170_6
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kasubi
Kasubi
Kwa Waganda wengi makaburi ni kitovu cha kiroho. Tangu mwaka 2001 yameingizwa katika orodha la UNESCO la Urithi wa Dunia.
20231101.sw_3170_7
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kasubi
Kasubi
Mwaka 2010 jengo kuu lenye makaburi yenyewe lilichomwa motoni lililowaka kwa sababu zisizojulikana. Mabaki ya wafalme hayakuharibiwa. Kuna mipango ya kulijenga upya jinsi ilivyokuwa.
20231101.sw_3174_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/Bustani%20ya%20wanyama
Bustani ya wanyama
Bustani ya wanyama ni mahali ambapo wanyama, hasa wanyamapori wa aina mbalimbali, wanatunzwa ili watu wapate kuwatazama. Siku hizi bustani Za wanyama zimekuwa pia mahali pa kutunza spishi au aina za wanyama walioko hatarini kutokomea. Vile vile bustani za wanyama zimewekwa kwa ajili ya maonyesho.
20231101.sw_3174_1
https://sw.wikipedia.org/wiki/Bustani%20ya%20wanyama
Bustani ya wanyama
Miji mingi mikubwa duniani ina bustani za wanyama. Katika baadhi ya bustani hizo watu hulipa kiingilio wakitaka kuingia. Hata hivyo bustani hizo hazipokei mapato ya kutosha, hivyo hazina budi kupokea pia misaada kutoka serikali.
20231101.sw_3177_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kabaka
Kabaka
Kabaka ni cheo cha mfalme wa Buganda ambayo ni ufalme ndani ya jamhuri ya Uganda. Cheo kingine pamoja na Kabaka ni Ssebataka.
20231101.sw_3177_1
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kabaka
Kabaka
Tangu mwisho wa karne ya 19 Makabaka wamekuwa Wakristo Waanglikana wakipokea taji katika kanisa kuu la Kianglikana la Kampala. Makabaka wa mwisho wamezikwa katika makaburi ya Kasubi mjini Kampala.
20231101.sw_3177_2
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kabaka
Kabaka
Serikali ya kwanza ya Milton Obote ilifuta falme zote nne za Uganda na kumlazimisha Kabaka Mutesa II kuondoka Uganda akipata kimbilio lake Uingereza.
20231101.sw_3177_3
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kabaka
Kabaka
Kati ya 1967 hadi 1993 cheo cha Kabaka hakikuwepo kisheria nchini Uganda lakini Waganda wengine walisikitikia. Serikali ya Yoweri Museveni ilirudisha falme za kale kama enzi za kiutamaduni.
20231101.sw_3177_4
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kabaka
Kabaka
Tarehe 24 Julai 1993 Ronald Muwenda Mutebi II aliruhusiwa kurudi Uganda kutoka Uingereza alikokuwa amemfuata baba yake akapokea rasmi taji la Kabaka mjini Kampala.
20231101.sw_3177_5
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kabaka
Kabaka
Mwanga II (mara ya pili) 1889 - 1897 – aliporudi kutoka nje baada ya kuuawa kwa Kiweewa Mutebi na Kalema na wafuasi wake
20231101.sw_3179_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/Chansela%20%28kiongozi%29
Chansela (kiongozi)
Chansela (kwa Kijerumani: "Kanzler"), pia kansela, ni cheo cha mkuu wa serikali, lakini si mkuu wa dola, katika Ujerumani na Austria. Kinafanana na cheo cha waziri mkuu.
20231101.sw_3180_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/Lomami%20%28mto%29
Lomami (mto)
Lomami ni tawimto kubwa la mto Kongo katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wenye mwendo wa takriban km 1500.
20231101.sw_3180_1
https://sw.wikipedia.org/wiki/Lomami%20%28mto%29
Lomami (mto)
Lomami inajiunga na mto Kongo karibu na Isengi, takriban km 150 baada ya mji wa Kisangani kuelekea mdomo wa Kongo. Sehemu ya mwisho kabla ya mdomo wa Lomami inapitika kwa meli.
20231101.sw_3183_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/UNESCO
UNESCO
UNESCO ni kifupisho cha United Nations Educational, Scientific and Cultural Organization yaani Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa.
20231101.sw_3183_1
https://sw.wikipedia.org/wiki/UNESCO
UNESCO
Ni kitengo cha Umoja wa Mataifa ambacho kinashughulika habari za elimu, sayansi na utamaduni duniani.
20231101.sw_3183_2
https://sw.wikipedia.org/wiki/UNESCO
UNESCO
Kati ya shughuli muhimu za UNESCO mojawapo ni Orodha la Urithi wa Dunia linalojumlisha mahali penye umuhimu wa pekee kihistoria, kisayansi au kiutamaduni.
20231101.sw_3185_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kofi%20Annan
Kofi Annan
Kofi Atta Annan (8 Aprili 1938 - 18 Agosti 2018) alikuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa 1996 - 2006. Annan na Umoja wa Mataifa walipata Tuzo ya Amani ya Nobeli mwaka 2001. Alikuwa mwanzilishi na mwenyekiti wa Kofi Annan Foundation na pia mwenyekiti wa Elders, shirika la kimataifa lililoanzishwa na Nelson Mandela.
20231101.sw_3185_1
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kofi%20Annan
Kofi Annan
Alizaliwa huko Kumasi, Ghana. Alipewa jina Kofi kuonyesha kuwa alizaliwa siku ya Ijumaa kuendana na utamaduni wa Ashanti. Jina Annan linamaanisha kuwa alikuwa ni mtoto wa nne kuzaliwa.
20231101.sw_3185_2
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kofi%20Annan
Kofi Annan
Annan alienda shule ya Mfantsipim katika mji wa Cape Coast, Ghana (1954-1957). Baadaye, alienda Kumasi shule ya sayansi na teknolojia (sasa ni Kwame Nkruma Shule ya sayansi na teknolojia) kwa mwaka mmoja. Msaada kutoka Taasisi ya Ford ulimwezesha kusoma uchumi katika chuo kikuu cha Macalester, Saint Paul, Minnesota. Alipomaliza shahada ya kwanza mwaka 1961, alisoma mahusiano ya kimataifa katika chuo kikuu cha kimataifa masomo katika Geneva, Switzerland (1961-62). Alisoma katika chuo kikuu cha MIT, shule ya Sloan, na alipata shahada ya M.S.
20231101.sw_3185_3
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kofi%20Annan
Kofi Annan
Baada ya masomo ya uchumi alijiunga na huduma ya Umoja wa Mataifa mwaka 1962 katika WHO. 1974-1976 alifanya kazi Ghana halafu akarudi tena huduma ya UM. Akapanda ngazi kuwa Makamu wa Katibu Mkuu mhusika wa usalama aliwajibika kusimamia shughuli za wanajeshi walio chini ya UM.
20231101.sw_3185_4
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kofi%20Annan
Kofi Annan
Alihusika na vita ya Rwanda pia ya Yugoslavia ambako wanajeshi chini ya bendera ya UM walishirikiana.
20231101.sw_3185_5
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kofi%20Annan
Kofi Annan
Mwaka 1996 alichaguliwa kuwa Katibu Mkuu wa UM, akarudishwa cheo mwaka 2001. Tangu 1 Januari alifuatwa ofisini na Ban Ki-moon.
20231101.sw_3185_6
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kofi%20Annan
Kofi Annan
Mwaka 2008 Annan alirudi katika habari za kimataifa alipofika Kenya kwa shabaha ya kupatanisha viongozi wa kisiasa waliopigana juu ya matokeo ya uchaguzi wa rais wa Kenya 2007. Akisaidiana na Grace Machel na rais mstaafu wa Tanzania Benjamin Mkapa aliendesha majadiliano kati ya wawakilishi wa ODM na PNU kwa muda wa wiki 5. Akafaulu kuleta mapatano ya ushirikiano kati ya pande zote mbili.
20231101.sw_3188_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/Shaka%20Zulu
Shaka Zulu
Shaka (pia: Tshaka, Tchaka au Chaka; halafu: Shaka Zulu, Shaka ka Senzangakhona) (* takriban 1781 - 1828 BK) alikuwa kiongozi wa Wazulu aliyebadilisha ukoo mdogo wa Kinguni kuwa kabila au taifa kubwa lililotawala maeneo mapana ya Afrika Kusini hasa Natal ya leo.
20231101.sw_3188_1
https://sw.wikipedia.org/wiki/Shaka%20Zulu
Shaka Zulu
Sifa zake zimetokana na uwezo wa kupanusha utawala wake kutoka eneo ndogo la 260 km² kuwa 28.500 km², kuvunja nguvu ya makabila mengine na kuyaunganisha na taifa lake. Katika historia ya kijeshi ya Afrika alianzisha mbinu mpya zilizopanusha uwezo na enzi yake. Sifa hizi, jinsi ilivyo mara nyingi na viongozi wanaotegemea nguvu ya kijeshi, zimeenda pamoja na vita na uharibufu mwingi. Miaka ya Shaka ilianzisha kipindi cha mfecane yaani "uharibifu" kinachokumbukwa na mataifa mengi ya Afrika Kusini.
20231101.sw_3188_2
https://sw.wikipedia.org/wiki/Shaka%20Zulu
Shaka Zulu
Shaka alikuwa mtoto wa chifu Senzangakhona ka Jama na Nandi binti wa chifu wa Langeni. Jina lake ni kutokana na neno la kizulu "iShaka" linalomtaja mdudu ambaye katika imani ya utamaduni wa Kizulu anasemekana kuvuruga hedhi ya wakinamama. Jina hili ni dalili ya kuzaliwa nje ya utaratibu. Hivyo miaka ya kwanza ya Shaka ilikuwa miaka migumu bila baba anayejulikana rasmi akisikia kudharauliwa na watu wengine. Utoto huu ulisababisha hasira ndani yake akalipiza kisasi baadaye.
20231101.sw_3188_3
https://sw.wikipedia.org/wiki/Shaka%20Zulu
Shaka Zulu
Alipo kuwa kijana Shaka alikaa kwenye kabila kubwa zaidi la Mthethwa alikoingia pamoja na hirima yake katika jeshi. Wakati ule ukoo wa Wazulu walikubali Wamthehtwa kuwa mabwana wao. Chifu wa Mthethwa alikuwa Dingiswayo aliyeanzisha utaratibu mpya wa impi yaani kupanga watu wake vitani katika vikundi na kuwa na ngazi mbalimbali za mamlaka. Shaka alihudumia miaka sita katika vita za Dingiswayo akawa hodari sana na kujifunza uongozi aliouboresha baadaye.
20231101.sw_3188_4
https://sw.wikipedia.org/wiki/Shaka%20Zulu
Shaka Zulu
Baada ya kifo cha baba yake, Shaka alirudi kwa Wazulu kwa msaada wa Dingiswayo akachukua uongozi mnamo mwaka 1812. Baada ya kuwa kiongozi akalipiza kisasi kwa maadui zake wa utotoni na kuwaua kwa njia mbalimbali.
20231101.sw_3188_5
https://sw.wikipedia.org/wiki/Shaka%20Zulu
Shaka Zulu
Shaka aliendelea kukubali ubwana wa Mthethwa na Dingiswayo alipouawa vitani na kabila la Ndwandwe mwaka 1817. Lakini pamoja na hayo alipigana vita na koo au makabila madogo jirani. Mbinu yake ilikuwa kuwashambulia waliompinga au kuwa hatari kwake; wanawake na watoto waliingizwa katika ukoo wake, pamoja na wanajeshi wa kiadui walio salimika kufa vitani lakini waliokubali kumfuata baada ya kushindwa. Kwa njia hiyo ukoo mdogo wa Wazulu uliendelea kukua.
20231101.sw_3188_6
https://sw.wikipedia.org/wiki/Shaka%20Zulu
Shaka Zulu
Baada ya kifo cha Dingiswayo mw. 1817 Shaka alishambulia kabila kubwa la Ndwandwe akawashinda kwenye mapigano ya kilima cha Gqokli kwa sababu ya mbinu zake za kijeshi ingawa idadi ya watu wake ilikuwa nusu tu ya adui.
20231101.sw_3188_7
https://sw.wikipedia.org/wiki/Shaka%20Zulu
Shaka Zulu
Katika miaka iliyofuata Shaka aliendelea kushambulia vikundi vya jirani na kuwaingiza katika utawala wake. Makabila mengine walimfuata bila vita wakikubali uongozi wake na kuingiza vijana wao katika impi au vikosi vya kijeshi vya Shaka. Alituma viongozi au majenerali zake pamoja na impi pande mbalimbali hadi Msumbiji na Zimbabwe. Vikundi kama Ndebele huko Zimbabwe au hata Wangoni katika Tanzania ni matokeo ya matembezi ya impi za kizulu zilizoenda mbali na kupoteza mawasiliano na nyumbani.
20231101.sw_3188_8
https://sw.wikipedia.org/wiki/Shaka%20Zulu
Shaka Zulu
Vita hizi zilisababisha makabila mengine kukimbia na kuhamahama wakishambulia majirani zao iliyopelekea kupanua eneo la vita katika nchi mbali na Wazulu wenyewe. Kipindi hiki kinakumbukwa kwa majina kama "mfecane" (Kizulu) au "difaqane" (Kisotho) kuwa miaka 30 ya vita na kifo.
20231101.sw_3188_9
https://sw.wikipedia.org/wiki/Shaka%20Zulu
Shaka Zulu
Katika mawazo ya wataalamu Shaka aliandaa upanuzi wa Makaburu kwa uharibifu wa vita zake. Makaburu walipoanza kuenea ndani ya Afrika Kusini walikuta maeneo mazuri bila watu lakini maghofu ya kuonyesha watu waliwahi kuishi hapa. Pamoja na hayo makabila mengine kama Wasotho, Waswazi, Wandebele au Wagaza walioshambuliwa walijifunza mbinu za kijeshi, wakaweza kujitetea na kuanzisha mataifa makubwa yaliyounganisha koo na makabila madogo zaidi.
20231101.sw_3188_10
https://sw.wikipedia.org/wiki/Shaka%20Zulu
Shaka Zulu
Utawala wa Shaka ulikuwa na tabia za kinyama zilizosababisha chuki nyingi dhidi yake. Baada ya kifo cha mamake Nandi alikuwa na hasira kiasi cha kuua watu 7000 kati ya wanajeshi wake kwa kosa la kutoonyesha huzuni ya kutosha na kuamuru kipindi cha kufunga miezi mitatu. Aliamuru mashamba yasilimwe kwa mwaka mmoja na kila mwanamke aliyeonekana kuwa na mimba katika kipindi hiki aliuawa pamoja na mumewe. Wataalamu wengine huona ya kwamba wakati ule Shaka alionekana kuwa na kichaa. Maadui walifanya mipango dhidi yake mwishowe aliuawa na ndugu zake. Mwaka 1828 impi nyingi zilikuwa mbali vitani ikulu ikawa bila ulinzi wa kutosha. Kaka zake Dingane na Mhlangana walimwua na kutupa maiti shimoni.
20231101.sw_3188_11
https://sw.wikipedia.org/wiki/Shaka%20Zulu
Shaka Zulu
Shaka aliboresha utaratibu alioukuta katika utumishi wa Dingiswayo. Wataalamu hutofautiana ni kwa kiasi gani ya kwamba Shaka alianzisha mbinu kadhaa au kiasi gani ndiye Shaka aliyeunganisha mbinu mbalimbali zilizowahi kujulikana lakini yeye alifuata utaratibu kuzitumia kushinda viongozi wote wengine. Kati ya mbinu alizotumia ni zifuatazo:
20231101.sw_3188_12
https://sw.wikipedia.org/wiki/Shaka%20Zulu
Shaka Zulu
Utamaduni wa Wanguni ulikuwa mikuki ya assegai na kila mtu alibeba tatu. Shaka aliona silaha za kutupwa ni hasara. Aliongea mwenyewe na wahunzi akawapa wanajeshi silaha katikati ya mkuki na upanga - "Iklwa". Haikufaa kutupwa bali kushikwa hivyo kuwalazimisha watu wake kushambulia na kuwa karibu na adui. Aliwapatia pia vigao vizito vya ngozi ya ng'ombe.
20231101.sw_3188_13
https://sw.wikipedia.org/wiki/Shaka%20Zulu
Shaka Zulu
Alilazimisha watu wake kuacha kuvaa viatu au kukinga miguu yao na kutembea pekupeku. Hii iliongeza kasi ya impi zake na uwezo wao wa kushambulia haraka. Inasemekana ya kwamba Shaka aliua wote waliolalamika walipoamriwa kuacha viatu vyao.
20231101.sw_3188_14
https://sw.wikipedia.org/wiki/Shaka%20Zulu
Shaka Zulu
Shaka alijenga nidhamu ya watu wake kwa kuwa na utaratibu wa mamlaka kati yake mwenyewe na vikosi vidogo zaidi. Sehemu nyingine ilikuwa adhabu kali: askari asiyeweza kuonyesha damu kwenye silaha yake aliweza kuuawa baada ya kurudi vitani. Impi ambao walipata sifa machoni pa Shaka waliruhusiwa kuoa baada ya ushindi.
20231101.sw_3188_15
https://sw.wikipedia.org/wiki/Shaka%20Zulu
Shaka Zulu
Shaka alitumia wavulana wadogo kuanzia umri wa miaka sita waliongozana na impi wakibeba mizigo au kuwafuata wanajeshi kwa ng'ombe kama chakula cha baadae. Hata hii iliharakisha mwendo wa impi zake.
20231101.sw_3188_16
https://sw.wikipedia.org/wiki/Shaka%20Zulu
Shaka Zulu
Hirima au vikundi vya kujumuisha watu wa umri mmoja ni tabia ya utamaduni kwa Wabantu wengi. Shaka alipoanzisha impi zake -badala ya kushambulia na watu wake wote mara moja jinsi ilivyokuwa kawaida awali- alitumia vikundi vilivyokuwepo tayari kiutamaduni kama msingi wa impi zake.
20231101.sw_3188_17
https://sw.wikipedia.org/wiki/Shaka%20Zulu
Shaka Zulu
3. vikosi vya ziada au vya wazee vilikuwa "viuno" vilivyotumika ama kuongeza uzito wa mashambulio panapohitajika au kuimarisha utetezi pale ambako adui alisogea mbele.
20231101.sw_3189_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/Afrika%20Kusini
Afrika Kusini
Imepakana na Namibia, Botswana, Zimbabwe, Msumbiji na Uswazi. Nchi nzima ya Lesotho iko ndani ya eneo la Afrika Kusini.
20231101.sw_3189_1
https://sw.wikipedia.org/wiki/Afrika%20Kusini
Afrika Kusini
Mji mkubwa ni Johannesburg. Majukumu ya mji mkuu yamegawiwa kati ya miji mitatu: Cape Town ni makao ya Bunge, Pretoria ni makao ya Serikali na Bloemfontein ni makao ya Mahakama Kuu.
20231101.sw_3189_2
https://sw.wikipedia.org/wiki/Afrika%20Kusini
Afrika Kusini
Nchi ina majina rasmi 11 kutokana na lugha rasmi 11, nazo ni: Kiafrikaans, Kiingereza, Kizulu, Kixhosa, Kiswati, Kindebele, Kisotho cha Kusini, Kisotho cha Kaskazini, Kitsonga, Kitswana na Kivenda.
20231101.sw_3189_3
https://sw.wikipedia.org/wiki/Afrika%20Kusini
Afrika Kusini
Zamadamu waliishi katika eneo la Afrika Kusini tangu miaka milioni 3 iliyopita, inavyoshuhudiwa na akiolojia.
20231101.sw_3189_4
https://sw.wikipedia.org/wiki/Afrika%20Kusini
Afrika Kusini
Binadamu wameishi huko kwa miaka 170,000 mfululizo. Wakazi wa muda mrefu zaidi ni Wakhoikhoi na Wasani, ambao wazagumzumza lugha ya jamii ya Khoi-San.
20231101.sw_3189_5
https://sw.wikipedia.org/wiki/Afrika%20Kusini
Afrika Kusini
Chanzo cha Afrika Kusini kama nchi ni Koloni la Rasi iliyoundwa na Waholanzi katika eneo la Cape Town kuanzia mwaka 1652. Huko kabila jipya la Makaburu lilijitokeza kati ya walowezi Wazungu kutoka Uholanzi, Ufaransa na Ujerumani. Lugha yao ilikuwa Kiholanzi iliyoanza kuchukua maneno ya Kifaransa, Kiafrika na Kiingereza na kuendelea kuwa lugha ya pekee Kiafrikaans.
20231101.sw_3189_6
https://sw.wikipedia.org/wiki/Afrika%20Kusini
Afrika Kusini
Karne za kwanza za koloni la Kiholanzi ziliona pia kufika kwa watumwa kutoka Indonesia walioletwa kama wafanyakazi wa Waholanzi na Makaburu. Hao Waindonesia walikuwa chanzo cha jumuiya ya Uislamu kwenye rasi.
20231101.sw_3189_7
https://sw.wikipedia.org/wiki/Afrika%20Kusini
Afrika Kusini
Pia machotara walitokea kutokana na kuzaliana kati ya Makaburu na wanawake Waafrika na Waindonesia. Sehemu ya machotara hao wameingia katika jumuiya ya Makaburu na wengi wao wanapimwa kuwa na mababu Waafrika.
20231101.sw_3189_8
https://sw.wikipedia.org/wiki/Afrika%20Kusini
Afrika Kusini
Katika miaka ya baadaye ubaguzi wa rangi uliongezeka na watoto machotara wa Wazungu na Waafrika mara nyingi hawakukubalika; walianza kuishi kama kundi la pekee kati ya Waafrika na Wazungu, nao ni chanzo cha hao walioitwa baadaye "Cape Coloreds".
20231101.sw_3189_9
https://sw.wikipedia.org/wiki/Afrika%20Kusini
Afrika Kusini
Mnamo mwaka 1800 falme na milki zilianza kutokea hapa. Mwanzo wa karne ya 19 ni hasa Wazulu chini ya Shaka Zulu walioanza kuenea na kuwashambulia majirani katika vita vya Mfecane. Vita hivyo vilileta uharibifu mkubwa lakini vilisababisha pia kutokea kwa milki za Wasotho na Watswana na wengine walioiga mitindo ya Wazulu na kujenga madola yenye uwezo wa kijeshi.
20231101.sw_3189_10
https://sw.wikipedia.org/wiki/Afrika%20Kusini
Afrika Kusini
Utawala wa Waingereza ulisababisha uhamisho wa nje wa sehemu ya Makaburu waliotokana na Wazungu kutoka Uholanzi, Ufaransa na Ujerumani; Makaburu hao walihama kwenda kaskazini wakaanzisha jamhuri ndogo kati ya maeneo ya Waafrika ama kwa njia ya mapatano au kwa njia ya vita.
20231101.sw_3189_11
https://sw.wikipedia.org/wiki/Afrika%20Kusini
Afrika Kusini
Kati ya miaka 1840 na 1850 Waingereza waliwafuata Makaburu kwa kueneza maeneo yao hadi mto Oranje; waliteka jamhuri ya Kikaburu ya Natalia na kuanzisha koloni jipya la Natal.
20231101.sw_3189_12
https://sw.wikipedia.org/wiki/Afrika%20Kusini
Afrika Kusini
Jamhuri mbili za Makaburu ziliweza kustawi kwa miaka kadhaa ambazo zilikuwa jamhuri ya Dola Huru la Oranje upande wa kaskazini wa mto Oranje na jamhuri ya Transvaal (ilijiita pia Jamhuri ya Kiafrika ya Kusini) upande wa kaskazini wa mto Vaal.
20231101.sw_3189_13
https://sw.wikipedia.org/wiki/Afrika%20Kusini
Afrika Kusini
Milki za Kiafrika zilitafuta njia zao kati ya himaya hizi za Wazungu ambao walikuwa na nguvu kutokana na silaha za kisasa. Wengine walitafuta uhusiano mzuri na Makaburu na kushikamana nao; wengine waliona Makaburu kama hatari wakatafuta uhusiano wa ulinzi na Waingereza.
20231101.sw_3189_14
https://sw.wikipedia.org/wiki/Afrika%20Kusini
Afrika Kusini
Mikataba kati ya Waingereza na milki za Kiafrika iliunda nchi lindwa zinazoendelea hadi leo kama nchi huru kama vile Botswana (Bechuanaland), Lesotho (Basutoland) na Uswazi (Swaziland).
20231101.sw_3189_15
https://sw.wikipedia.org/wiki/Afrika%20Kusini
Afrika Kusini
Katika miaka ya 1880 almasi na dhahabu zilipatikana kwa wingi katika jamhuri hizi na kusababisha kufika kwa wachimbamadini wengi, hasa Waingereza, waliotaka kutajirika; Makaburu walisita kuwapa haki za kiraia kwa sababu waliogopa wageni wengi. Tatizo hilo lilisababisha vita vya Makaburu dhidi ya Uingereza na jamhuri za Makaburu zilitwaliwa na jeshi la Kiingereza hadi mwaka 1902 zikawa makoloni.
20231101.sw_3189_16
https://sw.wikipedia.org/wiki/Afrika%20Kusini
Afrika Kusini
Jitihada za kupatanisha Wazungu wa Afrika Kusini (yaani Waingereza na Makaburu) zilisababisha kuundwa kwa Muungano wa Afrika Kusini kama nchi ya kujitawala ndani ya Milki ya Uingereza. Waafrika kwa jumla hawakuwa na haki za kiraia katika nchi hiyo isipokuwa katika Jimbo la Rasi kama walikuwa na elimu na mapato ya kulipa kodi za kutosha.
20231101.sw_3189_17
https://sw.wikipedia.org/wiki/Afrika%20Kusini
Afrika Kusini
Baada ya vita kuu ya pili ya dunia Chama cha National kilichofuata itikadi kali ilipata kura nyingi na kuchukua serikali ya Afrika Kusini. Hapo ilianzisha mfumo wa ubaguzi wa rangi kwa jina la apartheid.
20231101.sw_3189_18
https://sw.wikipedia.org/wiki/Afrika%20Kusini
Afrika Kusini
Haki za wasio Wazungu zilipunguzwa zaidi. Maeneo ya Kiafrika yalitangazwa kuwa nchi za pekee chini ya usimamizi wa serikali ya Kizungu ya Afrika Kusini; kwa hiyo wananchi kutoka maeneo hayo hawakuwa tena na haki za kukata rufaa mbele ya mahakama; walipewa vibali vya muda tu kukaa kwenye miji. Waafrika walipaswa kutembea muda wote na pasipoti na vibali; ndoa na mapenzi kati ya watu wa rangi tofauti zilipigwa marufuku. Shule na makazi zilitenganishwa.
20231101.sw_3189_19
https://sw.wikipedia.org/wiki/Afrika%20Kusini
Afrika Kusini
Siasa hiyo ilisababisha farakano kati ya nchi nyingi za dunia na Afrika Kusini. Upinzani kutoka Uingereza na Jumuiya ya Madola ulisababisha kuondoka kwa Afrika Kusini katika jumuiya hiyo na kutangazwa kwa Jamhuri ya Afrika Kusini.